Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live

Maghorofa ya Lugumi Hatarini Kupigwa Mnada

0
0
Maghorofa ya Lugumi Hatarini Kupigwa Mnada
Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd iliyotajwa katika sakata la zabuni ya Sh34 bilioni ya kuweka mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole ya Jeshi la Polisi, iko hatarini kupoteza mali zake kutokana na kudaiwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mnada wa maghorofa hayo utafanywa na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, kwa niaba ya TRA Mkoa wa Ilala. Maghorofa hayo yapo maeneo tofauti jijini Dar es Salaam; moja Mtaa wa Mazengo, Upanga na mawili yako Mbweni JKT wilayani Kinondoni.

Kuuzwa kwa maghorofa hayo kumetangazwa jana katika gazeti la Serikali la Sunday News, tangazo hilo likieleza kwamba ghorofa la Upanga linafaa kwa ofisi wakati yale ya Mbweni JKT yanafaa kwa makazi.

Mkurugenzi mtendaji wa Yono, Scolastica Kevela alisema mnada huo utafanyika Septemba 9, kuanzia saa 4:30 asubuhi kwenye maeneo yalipo maghorofa hayo.

Kevela alisema Lugumi Enterprises imeshindwa kulipa kodi ya TRA kwa wakati ndiyo maana wakapewa kazi ya kuuza majengo hayo.

Mkurugenzi huyo alikataa kutaja kiasi ambacho Lugumi anadaiwa na TRA pamoja na thamani ya maghorofa hayo.

Kevela alitoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, masharti ya mnada ni kulipa asilimia 25 ya thamani ya bei kwa atakayefanikiwa kuyanunua maghorofa hayo.

Kiasi kilichobaki kitatakiwa kulipwa ndani ya siku 14, tangu siku ya mnada na kwamba atakayeshindwa kulipa katika kipindi hicho hatarudishiwa fedha alizotoa na mnada utafanyika kwa mara nyingine.

Ukaguzi wa nyumba hizo unatakiwa kufanywa siku 10 kabla ya siku ya mnada.

Akizungumzia hilo, mkurugenzi wa huduma na elimu ya mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema Lugumi inadaiwa kodi za aina mbalimbali zinazotokana na mapato yake.

Lugumi ilikuwa gumzo mwaka jana baada ya taarifa ya CAG kuonyesha kuwa ililipwa zaidi ya ssilimia 90 ya fedha za zabuni kwa ajili ya kuweka vifaa hivyo katika vituo 138, lakini hadi wakati wa ukaguzi ilikuwa imeweka katika vituo 14 tu.

Taarifa hiyo ilifika bungeni na kuundwa kamati ndogo ambayo ilichunguza na kuwasilisha taarifa.    


Manowari ya Marekani Yagongana na Meli ya Mafuta Pwani mwa Singapore

0
0
Manowari ya Marekani Yagongana na Meli ya Mafuta Pwani mwa Singapore
Wanajeshi 10 hawajulikani waliko na wengine watano wamejeruhiwa baada ya manowari ya jeshi la Marekani kugongana na meli ya kubeba mafuta pwani mwa Singapore, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji la Marekani.

Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini wakati iligongana na meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Liberia.
Shughuli kubwa ya kuwatafuta na kuwaokoa wanajeshi inaendelea
Ndicho kisa cha pili kikubwa kinachoikumba meli ya jeshi la wanamaji wa Marekani miezi ya hivi karibuni.
Ripoti zinasema kuwa manowari hiyo ilikumbwa na uharibifu upande wake mmoja, lakini jeshi la Marekani lilsema kwa inaelea peke yake kwenda bandari ya Singapore.
Map shows the location of Singapore and the Strait of Malacca
Helikopta za jeshi la Marekani na jeshi la Singapore pamoja na walinzi wa pwani, wanafanya shughuli za uokoaji. Malaysia nayo imejiunga katika shughuli hiyo.

Kura taarifa kidogo kuhusu hali ya meli ya mafuta ya Alnic MC na wahudumu wake.
Meli hiyo ya mafuta inaripotiwa kuwa na uzito mara tatu wa manowari ya jeshi ya USS John McCain, na taarifa zinasema kuwa haikuwa imebeba mafuta wakati ya ajali hiyo.
Seneta John McCain ambaye jina lake limepewa manowari hiyo, aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa yeye na mke wake wanawaombea mabaharia hao.
Mwezi Juni mabaharia saba wa Marekani waliuawa wakati manowari ya USS Fitzgerald iligongana na meli ya mizigo kwenye bahari ya Japan karibu na bandari ya Yokosuka.

Serikali Yashikwa Kooni Sakata la Ndege ya Bombardier Kuzuiwa Canada

0
0
Serikali Yashikwa Kooni Sakata la Ndege ya Bombardier Kuzuiwa Canada
Serikali inazidi kubanwa kuhusu ndege aina ya Bombardier Q400 Dash 8, ambayo imezuiwa nchini Canada kutokana na kushindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kimataifa ya kulipa fidia.

Hukumu ya Mahakama ya Kimataifra ya Usuluhishi (ICSD) iliyotolewa mwaka 2010 iliitaka Serikali kuilipa kampuni ya ujenzi ya Stirling Civil Engineering Ltd dola 25 milioni za Kimarekani na riba ya asilimia nane, lakini hadi sasa haijalipwa na hivyo deni kufikia dola 38.7 milioni (sawa na Sh87 bilioni).

Fidia hiyo inatokana na Serikali ya Awamu ya Nne kuvunja mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Tegeta Wazo-Bagamoyo bila ya kufuata mkataba.

Habari za kuzuiwa kwa ndege hiyo ziliwekwa bayana na Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu na baadaye Serikali kuzithibitisha, huku ikitupia lawama wanasiasa.

Jana, kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ambaye alihoji kuhusu kutowasili kwa ndege hiyo siku chache kabla ya Lissu kuibuka, alionekana kuchukukizwa na majibu ya Serikali, akitaka iache kugeuza suala hilo kuwa la kisiasa au ushabiki wa mpira.

Wakati Zitto akisema hayo, wachambuzi wengine wamesema Serikali ina wajibu wa kutoa taarifa kuhusu mali za nchi na kuacha kulaumu wanasiasa wa upinzani.

Zitto, ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini, alisema suala la ndege hiyo linagusa nchi na mjadala wake ni lazima uwe na hadhi hiyo badala ya kuufanya wa kisiasa.

Jumatano iliyopita, Zitto alihoji katika akaunti yake ya Twitter sababu za ndege hiyo kutowasili Julai kama Serikali ilivyoahidi na mchangiaji mmoja mwenye jina la Mbarawa alijibu kuwa kulikuwa na matatizo kidogo na kuahidi kuwa yakiisha itakuja.

Juhudi za Mwananchi kuthibitisha kama mwenye jina lililotoa majibu hayo ni Waziri wa Ujenzi, Profesa Makame Mbarawa hazikufanikiwa, lakini juzi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Zamaradi Kawawa alithibitisha kuwapo kwa deni hilo na kusema matatizo yaliyojitokeza yamesababishwa na wanasiasa walioweka masilahi yao mbele kukwamisha jitihanda za maendeleo zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Akizungumza na Mwananchi jana, Zitto alisema majibu hayo yanataka kuligeuza suala hilo kuwa la kisiasa.

“Tusikubali kuingia kwenye huu ushabiki. Hili ni suala la kisheria, na ni suala la nchi ambayo sisi wote tuna maslahi ya kuona inakwenda mbele,” alisema Zitto.

Alisema si dhambi nchi kuwa na deni na kwamba mataifa makubwa duniani yanadaiwa.

“Mimi binafsi ninadaiwa madeni ya uchaguzi mpaka sasa na wengine kati ya wanaonidai wamenipeleka mahakamani. Si dhambi kudaiwa,” alisema.

Alisema ni muhimu wananchi kuelewa deni linatokana na nini kama ni uamuzi mbaya wa kisiasa au mikakati gani inawekwa ili kulilipa.

Zitto alisema maneno yanayosambazwa kuwa ameshiriki kuwezesha kukamatwa ndege ya Bombardier iliyonunuliwa na Serikali, ni propaganda na hazina ukweli.

“Serikali lazima ifahamu kuwa ni lazima ihojiwe na iwe tayari kutoa majibu, sisi kama vyama vilivyo nje ya Serikali ni wajibu wetu kuhoji jambo lolote,” alisema.

“Pia, ni haki yetu kupata taarifa zozote kutoka mahali popote zitakazosaidia kuisimamia Serikali. wajibu wa Serikali ni kujibu hoja zinazoibuliwa nasi.

“Suala la ndege yetu kuzuiwa nchini Canada lisifanywe la ushabiki kama wa mpira.

“Kitendo cha Kaimu Msemaji wa Serikali kulaumu wanasiasa kwa jambo la kisheria kama hili, ni utoto.”

Alisema historia inaonyesha kuwa hakuna mwanasiasa, hasa wa upinzani, anayeweza kushirikiana na kampuni za kigeni kuhujumu nchi.

“Falsafa ya chama ninachokiongoza, ACT Wazalendo, ni Taifa Kwanza, Leo na Kesho na filosofia yangu ni my country first, right or wrong (nchi yangu kwanza kwa usahihi au kwa makosa),” alisema.

Alisema Serikali ifahamu kuwa nchi ina madeni mengi na miongoni mwa madeni hayo yapo ambayo yameshaamuliwa na Mahakama.

“Kinachopaswa ni kuwa na maarifa ya kuzuia mali zetu nje ya nchi kuzuiwa kama ilivyo kwa ndege hii,” alisema.

“Hii ni nchi ni yetu sote, hakuna mwenye hatimiliki ya ukweli. Ukweli pia haupendi kupindwapindwa. Serikali itoke kueleza nini kimetokea mpaka ndege kuzuiwa.”

Maoni kama hayo alikuwa nayoProfesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu).

“Kazi za vyama vya upinzani ni kuikosoa Serikali. Wanapopata taarifa za Bombardier kuzuiwa Canada, unataka wakae kimya?” alihoji.

“Wakikaa kimya hawatakuwa wapinzani.”

Alisema Serikali itoe taarifa zinazojitosheleza kuhusu ndege hiyo badala ya kuwalaumu wanasiasa kuwa ndiyo wamesababisha mgogoro huo.

Alisema Serikali ilishaahidi kwamba ndege hiyo ingewasili Julai, hivyo kutowasili katika muda uliotangazwa kunasababisha wapinzani watafute taarifa.

Profesa Mpangala alisema sasa ni muhimu Serikali itoe taarifa kwa wananchi ni kwa nini ndege hiyo imezuiwa Canada badala ya kusubiri taarifa zitolewe na vyama vya upinzani.

“Vyama vya upinzani visilaumiwe kutoa taarifa hizo kwa kuwa wao pia ni sehemu ya jamii,” alisema.

“Tusiwalaumu wapinzani kuwa wanachochea migogoro. Kuikosoa Serikali ni moja ya kazi zao.”

Lakini, Profesa Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alikuwa na mawazo tofauti.

“Si kila jambo la Serikali linatakiwa liwekwe hadharani. Kuna mambo mengine hayawezi kuwekwa hadharani kwa sababu bado hajayaiva kuwaeleza wananchi,” alisema.

Hata hivyo, alisema si vibaya kwa Serikali kuweka bayana kilichotokea badala ya kuendelea kusikia taarifa hizo kutoka kwa wapinzani.

Alisema taarifa zilizotolewa na Msemaji wa Serikali haikujitosheleza na akashauri suala hilo lizungumzwe kwa kina na Waziri Mbarawa.    


Marekani na Korea Kusini Wafanya Mazoezi ya Pamoja ya Jeshi

0
0
Marekani na Korea Kusini Wafanya Mazoezi ya Pamoja ya Jeshi
Marekani na Korea Kusini wanafanya mazoezi ya kila mwaka ya jeshi, ambayo mara nyingi huighadhabisha Korea Kaskazini licha ya wito wa kutaka mazoezi hayo yasifanyike.
Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilionekana kulegeza kamba baada ya kutisha kuwa itarusha makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, lakini tena ikasema kuwa itafuatilia mienendo ya Marekani.

Korea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto.
China na Urusi mwezi Julai zilipendekeza kusitishwa mazoezi ya kijeshi ili nayo Korea Kaskazini iache kuyafanyia majaribio makombora.
Marekani inasema kuwa mazoezi hayo yatawahusisha wanajeshi 17,500 wa Marekani na yatadumu kwa kipindi cha siku kumi

Marekani na Korea Kusini hufanya mazoezi ya kijeshi mara mbili kwa mwaka yanayowashirikisha idadi kubwa ya wanajeshi na zana za kivita.
Mazoezi hayo hujumuisha ya ardhini , baharini na angani. Mazoezi hayo ambayo hufanyika Korea Kusini pia hujumuisha mafunzo jinsi ya kukabiliana na ugaidi na mashambulizi ya kemikali
Korea Kusini hutuma wanajeshi 50,000 huku Marekani nayo ikituma kati ya wanajeshi 25,000 na 30,000.

Mazoezi hayo pia wakati mwingine hushirikisha wanajeshi kutoka nchi washirika na mwaka uliopita nchi zingine tisa zilijiunga nayo.

Vita Kuu ya Mtoto wa Mobetto Yeendelea Huku ikimwacha Zari na Kilio Mobetto Kicheko

0
0
Vita Kuu ya Mtoto wa Mobetto Yeendelea Huku ikimwacha Zari na Kilio Mobetto Kicheko
HALI si shwari kati ya mwanamitindo matata wa Bongo, hamisa hassan Mobeto na mwanamama mjasiriamali wa Afrika Mashariki ambaye ni mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, Zarinah hassan ‘Zari The Boss Lady’, kisa kikielezwa kuwa ni mtoto.

Wakati mtoto huyo wa Mobeto aliyepewa jina la baba mzazi wa msanii huyo akitimiza siku 14 leo Jumatatu, uzao huo umesababisha Mobeto kuibuka na kicheko kwa kuungwa mkono na Wabongo huku Zari akidaiwa kuambulia kilio kutokana na kushambuliwa mitandaoni.

Mara tu baada ya Mobeto kujifungua mtoto huyo Agosti 8, mwaka huu, Zari alitokwa na povu ambalo siyo la nchi hii huku akipiga mkwara kuwa asihusishwe na mtoto huyo wa ‘bitch’ (malaya), kauli ambayo aliitoa kupitia ukurasa wake unaotambuliwa kwenye Mtandao wa Instagram. Kilichofuatia ni majibizano ya mashabiki wa Mobeto na wale wa Zari ambapo kila upande ulikuwa ukivutia upande wake, lakini pande zote zilichukizwa na neno ‘bitch’ ambalo ni tusi lililotumiwa na Zari kwenda kwa Mobeto ikielezwa kuwa lilitokana na hasira.

JINA LA BABA MkWE
Wakati mambo yakiwa hayajakaa sawa huku mtoto huyo wa pili wa Mobeto akiibua tafrani ya aina yake mitandaoni, mwanamitindo huyo aliibua lingine baada ya kumpa mtoto huyo jina lililodaiwa kuwa ni la baba mkwe wa Zari. Inasemekana kwamba, jambo hilo ndilo linalodaiwa kuthibitisha kuwa Mobeto amezaa na mwanaume huyo hivyo kuibua shangwe kwa Wabongo na kumuongezea machozi Zari.

Ilielezwa kuwa, jina hilo, ndilo lililomaliza maswali mengi ya mashabiki ambao walitaka kumjua baba wa mtoto huyo. Awali, Mobeto alifungua akaunti kwenye Mtandao wa Instagram kwa jina ‘Tanzania Baby’, lakini baadaye wiki iliyopita alibadilisha jina hilo ambapo hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, akaunti hiyo ilikuwa ikikaribia kuwa na wafuasi (followers) laki moja.

MAMA MZAZI NA DADA MTU
Tukio lingine lililoibua gumzo juu ya mtoto huyo ni kufuatia kitendo cha mama mzazi wa jamaa huyo na dada yake kuonekana kwa nyakati tofauti wakiwa kwenye hospitali ambayo Mobeto alijifungulia, ikidaiwa kuwa walifuata damu yao ambayo ni nzito kuliko maji.

Hata hivyo, jambo lingine lililozungumzwa zaidi ni kitendo cha jamaa huyo kumkana Mobeto ikidaiwa kuwa alilenga kumpooza Zari ambaye inasemekana jambo hilo lilimtibua mno na kumtaka jamaa huyo aliyezaa naye watoto wawili kukanusha kuzaa na Mobeto.
mobeto na zari
Mobeto.


MOBETO APIGWA STOP
Katika mazingira hayo, mtu wa ndani ya familia ya mwanaume huyo alilitonya Ijumaa Wikienda kuwa, kwa sasa Mobeto amepigwa ‘stop’ (marufuku) kufanya mahojiano na waandishi wa habari.

Hata hivyo, Ijumaa Wikienda lilifika nyumbani kwa Mobeto, maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar ambapo mara baada ya kujitambulisha lilifungiwa mlango wa geti kwa madai kwamba, waandishi hawahitajiki.

WAZAZI FULL RAHA
Kwa upande wao, wazazi wa mwanaume huyo anayedaiwa kuzaa na Mobeto, wamepokea baraka hiyo kwa mikono miwili huku babu mtu akifurahia zaidi mtoto huyo kupewa jina lake. 40 YA kiShiNDO Hata hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni zilieleza kwamba, familia ya Mobeto yaani mama yake ipo kwenye mipango kabambe ya kuandaa 40 ya mtoto huyo kwani itakuwa haijawahi kutokea Bongo. Tusubiri!


Soma Nafasi za Ajira zilizotangazwa Leo Jumatatu

0
0

Serikali Yakanusha Kumpa Tundu Lisu Siku 7

0
0
Serikali Ya kanusha Kumpa Tundu Lisu Siku 7
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kwamba imempa siku 7 Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu kuomba radhi kwa kupotosha umma.

Msemaji wa serikali ametoa taarifa akisema kuwa taarifa hizo si za kweli, kwani hata mtu aliyetumika kuandika hiyo taarifa yupo msibani



Madereva Daladala wa Kituo cha Mawasiliano Simu 2000 Wagoma

0
0
Madereva Daladala wa Kituo cha Mawasiliano Simu 2000 Wagoma
Baadhi ya madereva wa daladala zinazotumia kituo cha mabasi cha Simu-2000 Mawasiliano kuongezewa ushuru kutoka Sh 500 hadi 1000 wakati wa kutoka ndiyo sababu mojawapo iliyofanya wagome.

Mbali na hilo, wamesema ubovu wa barabara hiyo ya Mawasiliano ni sababu nyingi kwa madai ya kwamba magari yao yanaharibika kila kukicha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili walisema walianza mchakato huo tangu saa 11 alfajiri na kwamba wataendeleza hatua hiyo hadi mamlaka husika itakapotoa mwafaka w sinofahamu.

Mmoja wa madereva hao Abdulsalum Hamad amesema waliingia katika kituo kama kawaida lakini wakati wanataka kutoka wakaamriwa kulipa Sh 1000 jambo ambalo hawalukubaliana nalo.

"Baada ya kuamua kugoma kutolipa kiasi hiki walitushirikilia kwa nusu saa ndipo tukachukua uamuzi wa kugoma kabisa na gari itakayoingia hapa kituo haiwezi kutoka kabisa hadi kieleweke,"amesema Hamad

Kero nyingi ya muda mrefu waliaamua kuiunganisha na katika mgomo huo ni hatua ya wahusika wa kituo hicho cha kuwatoza faini ga Sh 50000 pindi wakatapobainika kunawa nyuso wakiwa msalani kwani hawaruhusiwa kufanya hivyo.

Hamad aliwataka wahusika wa kituo kuliangalia suala kwa jicho la tatu suala  la tozo ya Sh 1000  kwani huduma zinatolewa na kituo hicho haziendani na tozo hizo na badala yake waiache ya Sh 500.





Fid Q :Idadi ya Views Katika Mtandao wa YouTube si Kipimo cha Muziki wa Hip Hop Bongo

0
0
 Fid Q :Idadi ya Views Katika Mtandao wa YouTube si Kipimo cha  Muziki wa Hip Hop Bongo
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q amedai idadi ya views katika mtandao wa YouTube si kipimo katika muziki wa hip hop Bongo.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma zake mbili mpya ‘Fresh na Ulimi Mbili’, ameiambia FNL ya EATV kuwa idadi ya viewers mara myimgi huenda kinyume na uhalisia.

“Kwanza nafikiri nyingi hazipati (views) hizo kwa sababu wana hip hop ni watu ambao huwa tunatoa ngoma na zinakuwa zimefika. Unajua views na mambo ya YouTube sometimes hayamati sana katika uhalisia, huwa tunakutana na watu ambao wana-views milioni na kadhalika katika show na tunakuwa kama sisi ndio tuna hizi views milioni,” amesema na kuongeza.

“Kwa hiyo huwa nawaambia watu kila siku kwamba number do lie sometime, kwa sababu unaambia mbili jumlisha mbili ni nne na mbili mara mbili ni nne lakini mbili toa mbili ni sifuri,” amesisitiza.

Ngoma mpya Fid Q ‘Fresh’ ambayo aliitoa August 13 mwaka huu hadi sasa ina views 160,646 katika mtandao wa Youtube.


Joyce Sokombi: Maombi kwa Bulaya Yanahitajika

0
0
Joyce Sokombi:  Maombi kwa Bulaya Yanahitajika
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mara Joyce Sokombi (CHADEMA) amezungumzia hali ya Mbunge Mh. Ester Amos Bulaya, na kusema kwamba hali yake bado haijatengemaa kwani amepewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa, hivyo amewataka watanzania kumuombea.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Mh. Sokombi amesema presha ya Ester Bulaya ambaye ni Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini bado ipo chini, kiasi kwamba wameshindwa kumsafirisha kwenda hospitali kubwa, hivyo wanasubiri madaktari wamsaidie kurudisha hali ya presha yake, ndipo wamtoe hospitali.

Pia Mh. Sokombi amesema kwa sasa Bulaya ameshapatiwa dhamana akiwa hapo hospitalini, lakini hawajajua hatma ya kesi kwani mpaka sasa hawajapewa maelezo ya sababu iliyofanywa ashikiliwe na polisi.

Hamad Rashid Aingilia Ugomvi’ wa Lipumba, Seif

0
0
Hamad Rashid Aingilia Ugomvi’ wa Lipumba, Seif
Wakati mgogoro wa uongozi kati ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi ukishika kasi, Mwenyekiti wa Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed amesema mgogoro huo unakolezwa na Maalimu Seif kutokana na kung’ang’ania madaraka.

Akizungumza kwenye madhimisho ya miaka mitano ya ADC yaliyofanyika kwenye Makao Makuu yake Buguruni, Hamad alisema hatua hiyo inasababishwa na kutanguliza maslahi binafsi.

Hamad alisema kiongozi mzuri ni yule anayeendena na maneno yake kwa wanachama na wananchi, ili kuweza kujenga chama kama taasisi siyo chama cha mtu mmoja.

Hamad badala ya kuzungumzia maadhimisho ya chama chake, alijikita zaidi kwenye mgogoro wa CUF.

Pia, alisema hawataki viongozi wanaokipaka matope chama chake kwa kukiita CCM B. Alisema sera yao ni kuhakikisha wanadumisha amani na utulivu kwa wanachama wake, ili kupata muda wa kuendeleza demokrasia inayoleta mabadiliko.

“Katika chama chetu hatuna sera ya vurugu wala migogoro binafsi hatukubali hata kidogo, mtu kutuharibia chama chetu. Kiongozi huwezi kufanya kazi kwenye fitina,” alisema.

Alisema kiongozi yeyote hawezi kuongoza chama au wananchi iwapo kuna migogoro inayosababishwa na viongozi wachache.

“Chama chetu hatuwezi kumvumilia kiongozi muongo tunaamini uongozi unaweza kupatikana katika sehemu mbili za mabadiliko na uchanguzi, hatutaki kufanya mabaya yanayofanyika kwenye vyama vingine,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo alisema ADC siyo chama cha vurungu kutokana na wao kuamini maendeleo hayawezi kupatikana kwa maandamano,

Pia, Doyo alisema kitendo cha viongozi kushindwa kuelewana ndani ya chama, ni jambo ambalo linaleta picha mbaya na kurudisha nyuma maendeleo ya ujenzi wa demokrasia.

“Tuna uwezo wa kusameheana iwapo kumetokea mtafaruku, tunawataka wanachama wote kufanya hivyo katika matawi yao,” alisema Doyo.    

Lema Awapa Makavu Viongozi wa Dini

0
0
Lema Awapa Makavu Viongozi wa Dini
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema amewageukia viongozi wa dini nchini kwa kusema kwamba wanapaswa kukemea vitendo vya udhalilishwaji wanavyofanyiwa wabunge wa upinzani na siyo kukemea viroba na bia.

Lema aliitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari Mjini Arusha na kusema kuwa viongozi wa dini mbalimbali nchini wasifumbe macho yao na kujifanya hawayaoni mateso wanayopatiwa viongozi wa upinzani nchini.

"Viongozi wetu wa dini wasijifanye hili tunalofanyiwa upinzani hawayaoni. Kazi ya viongozi wa dini siyo kukemea bia na viroba bali wanatakiwa wapige kelele kwenye ukiukwaji wa misingi ya sheria inayoendelea hapa nchini dhidi ya upinzani", alisema Lema.

Pamoja na hayo, Mhe. Lema ameongeza kuwa viongozi wa dini endapo watasimama katika kukemea maovu yanayofanywa ndani ya nchi yakiwepo ya unyanyasaji watakuwa wamelikomboa taifa kwenye machafuko.

"Ipo siku  kuna watu watashindwa kuvumiliwa haya tunayofanyiwa, hapo ndipo vita vya wenyewe kwa wenyewe vitakapokuja hapo siku za mbeleni" alimaliza.

Ester Bulaya Apewa Dhamana Akiwa Hospitali

0
0
Ester Bulaya Apewa Dhamana Akiwa Hospitali
Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya amepewa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na Wadhamini watatu pamoja na fedha Tsh. Milioni 20 na amepata rufaa ya kwenda kutibiwa Muhimbili.

Taarifa zinasema kuwa Mbunge huyo ameweza kudhaminiwa baada ya kushikiliwa na Polisi kwa siku mbili baada ya kumkata akiwa Hotelini huku pia akiruhusiwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Hofu Yazudi Kutanda Bongo Maiti 15 Zakutwa Kwenye Viroba

0
0
Hofu Yazudi Kutanda Bongo Maiti 15 Zakutwa Kwenye Viroba
WAVUVI na wafanyabiashara katika masoko na minada ya samaki ya Kunduchi, Ununio na Feri jijini Dar es Salaam wanaishi kwa hofu baada ya kuwapo kwa taarifa za kuopolewa miili 15 ya watu baharini ikiwa imewekwa katika mifuko maalumu kama viroba, Bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kilichozungumza na Nipashe, miili hiyo iliokotwa kwa nyakati tofauti na wavuvi ambao waliwajulisha polisi, waliofika kuichukua.

Kuwapo kwa idadi kubwa ya miili inayoopolewa kutoka baharini au kukutwa fukweni ikiwa imefungwa kama mzigo kumefanya wavuvi na wafanyabiashara wa samaki kuingiwa na hofu ya kuja kutakiwa kuisadia polisi katika uchunguzi wa mauaji hayo, pindi wanapogundua na kutoa taarifa za maiti hizo.

Hofu hiyo imesababisha baadhi ya wavuvi kunyamaza wanapoona miili zaidi ikielea baharini.

“Polisi tunawajulisha, wanakuja, wanabeba maiti, lakini hakuna siku wametueleza ni za kina nani," alisema mvuvi mmoja wa Kunduchi aliyezungumza na Nipashe kwa sharti la kutotajwa jina gazetini akihofia usalama wake.

"Wavuvi tunafahamiana na ikitokea mwenzetu amekufa au chombo kimezama majini tunafahamu.

"Lakini tangu Agosti mwanzoni tunaokota miili ikiwa imeandaliwa (imefungwa) kabisa na siyo ya wenzetu.”

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu jana kuwa miili iliyookotwa ni mitatu na haikuwa kwenye viroba.

“Hadi sasa taarifa za miili mingi kama hiyo kuokotwa nazisikia kwako," alisema Kamanda Mkondya. "Hao watu watueleze nasi tutachukua hatua, hatuna taarifa za miili iliyofungwa kwenye viroba au sandarusi.

"Miili mitatu iliyookotwa Kunduchi iko Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na haijatambuliwa, wananchi wafike kuitambua.”

Lakini wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti kwenye maeneo ya uvuvi hayo jana, wavuvi walisema wamepokea taarifa kutoka wenzao wa eneo la Kizimkazi, Zanzibar, kwamba huko nako pia zimeokotwa maiti tano.

Mvuvi mmoja wa Kunduchi alisema siku mbili zilizopita ziliokotwa maiti tano katika eneo la Bongoyo na nne nyuma ya kisiwa cha Mbudya, jijini Dar es Salaam.

Alisema kati ya maiti tisa hizo, moja ilikuwa ya mwanamke na kwamba zilikuwa zimefungwa kamba miguuni, kichwani na tumboni.

"Zote zilikuwa zimeharibika na sura hazitambuliki," alisema na kueleza kuwa zilichukuliwa na polisi baada ya kutaarifiwa.

Alisema polisi waliochukua miili hiyo ni wa mkoa wa Kinondoni kutoka vituo vya Kawe ambayo ni wilaya ya kipolisi na Wazo Hill.

"Hawajawahi kusema mtu huyo alifia wapi na chanzo cha kifo, (hivyo) wengi tuna wasiwasi tu," alisema mvuvi mwingine ambaye pia aliomba jina lake lihifadhiwe.

“Ukiangalia umri ni miaka 25 hadi 50.

"Jamaa zetu wa Feli waliokota maiti sita wiki mbili zilizopita (na) kati yake mbili zimefungwa pamoja na katika hizo moja ni mwanamke.

"Tulichozoea wavuvi ni kuokota maiti za wavuvi wenzetu ambaye alizama au kupotea, na zinakuwa na nguo zake za kawaida, lakini hizi ni za kuandaliwa.”

KICHWA CHINI
Kwa mujibu wa wavuvi hao, wanakutana na maiti nyingi zikiwa ndani ya viroba, ambapo marehemu wanakuwa waliingizwa humo kwa kutanguliza kichwa.

"Yaani mtu kaingizwa kichwa kichwa, akafungwa kwenye miguu, tumboni na shingoni,” alisema mvuvi huyo na kueleza zaidi:
“Nyingine utazikuta zipo tatu zimefuatana na nyingine mbili ndani ya kiroba kimoja.

"Na kuna wakati zimepangana nyingi kwa pamoja na kila kiroba na maiti yake.”

Mvuvi huyo alisema wanaogopa kuziopoa kwa sasa na kwamba nyingi ni za wanaume.

Chanzo hicho kilieleza kuwa maiti nyingi zinakutwa nyuma ya kisiwa cha Mbudya, kwenye mkondo mkuu (bahari kuu).
Alisema baadhi ya wavuvi walizifungua maiti hizo na kukuta zimeharibika vibaya.

"Walishindwa kula kutwa nzima," alisema na kueleza kuwa baadhi ya maiti zina majeraha ya kukatwa miguuni.

“Maiti tunazoona na kutoa taarifa ni zile zinazokuja kwenye maeneo yetu, lakini tunapokwenda kuvua eneo la bahari kuu huko tunazikuta nyingi na tunashindwa kutoa taarifa,” alisema.

“Kipindi hiki ni Kusi, kawaida yake asubuhi unavuma umande, ukifika saa sita au saba kama sasa hivi unavuma matalahi yanaingiza ndani kutoka bahari kuu kuleta huku (Kunduchi)."

Kwa mujibu wa wavuvi hao, maiti hizo zinatoka maeneo ya ama Dar es Salaam, Pwani, Lindi au Mtwara.

Walipoulizwa wamejuaje kama maiti hizo zinatokea maeneo hayo, wavuvi hao walisema bahari ina pepo kuu mbili ambazo ni za Kaskazini na Kusini na kwamba kila mmoja unavyopiga ndivyo vitu au maiti inaweza kusafiri na kukutwa katika eneo fulani.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, upepo wa sasa hivi unavuma kutoka kusini kwenda kaskazini, hivyo maiti hizo zisingeweza kuwa zinatokea Tanga ama Kenya, kwa mfano.

“Hakuna kinachotoka kaskazini kuja kusini, ukiona kimekuja huko kimevushwa na upepo kutoka kusini kuja huku,” alisema mmoja wa wavuvi.

Aidha, alisema kwa kawaida kama ni maiti ambayo haijaandaliwa huokotwa moja au mbili na ikiwa kwenye mavazi ya kawaida kama suruali au kaptula, lakini zinazookotwa kwa sasa zipo ndani ya viroba.

“Tuna shaka kubwa sana na hii miili, hatuna shaka kuwa siyo wavuvi wenzetu, tuna mtandao mkubwa kutoka Mtwara hadi Tanga tunafahamiana na tunahabarishana.

"Hata maiti ikiokotwa eneo jingine tunajua, lakini hizi hatujui kwa kuwa tumewasiliana na wenzetu hakuna vifo vingi vya wavuvi.”
Nipashe iliwatafuta viongozi wa serikali ya mitaa kwenye maeneo husika, ambao walisema wamelisikia suala hilo kutoka kwa wavuvi, lakini waulizwe polisi.

Wasomi Waanza Kuhoji Uzalendo wa Mwanasiasa Tundu Lissu....

0
0
BAADHI ya wasomi nchini wamehoji uzalendo wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wa kushabikia matatizo ya nchi yake badala ya kuwa sehemu ya kutafuta ufumbuzi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa Benson Bana ameelezea kitendo cha Lissu kujitokeza mbele yalezea kwa mbwembwe suala la kuzuiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada, ni kitendo kinachozua maswali mengi juu ya uzalendo wake kwa Tanzania.

“Nilipomuona amejitokeza katika vyombo vya habari ilinishtua kwa sababu tangu mwanzo Lissu na wenzake walikuwa wanapinga ujio wa hata zile ndege mbili za mwanzo,” alieleza Profesa Bana. Alieleza kuwa mwenendo ambao Lissu ameendelea kuuonesha, unaashiria kuna walakini mkubwa katika suala la uzalendo na pia kujenga hisia kwamba inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia, linalomsukuma kufanya mambo yanayoharibu maslahi ya Taifa.

Msomi huyo alisema hivi sasa kumekuwa na minong’ono mingi juu ya uzalendo wa Lissu na namna anavyosemekana kushirikiana na watu wa nje katika kuiumiza nchi. “Tuliosoma somo la Uraia tulifundishwa namna ya kuipenda nchi yako na kutumia uwezo wako kuisaidia nchi yako badala ya kuivua nguo,” alisitiza Profesa Bana huku akimfananisha mwanasiasa huyo na askari aliyoko vitani, anayeuza siri za jeshi badala ya kupambana kulisaidia jeshi lake kushinda vita.

Aidha, alieleza pia kutokufurahishwa na kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACTWazalendo) cha kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kupitia akaunti ya tweeter kuhusu kutokuwasili kwa ndege ya Bombardier Q400-Dash 8, ambapo Profesa Bana ameielezea njia hiyo ya mawasiliano kama si sahihi na badala yake angeweza njia ambayo si ya kila mtu kujua.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Wakili Dk Damas Ndumbaro amemuelezea Lissu kama mtu anayetafuta umaarufu kwa njia yoyote ile hata kama njia anayoitumia itakuwa na madhara kwa maslahi ya nchi.

“Haya tunayoyaona kwa Lissu inatuonesha jinsi gani upeo wake upo kiuanaharakati zaidi kuliko uongozi na katika hili ni kama bomu linalosubiri kulipuka ambalo hata viongozi wa chama chake na hata wafuasi wake wanashindwa kuling’amua,” alieleza Dk Ndumbaro. Maneno ya Dk Ndumbaro yaliungwa mkono ya Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja ambaye alisema tatizo kubwa la Lissu ni kukosa maarifa ya uongozi.

“Lissu hajui uongozi na hii ndiyo shida kubwa inayomkabili. Hajui suala la maslahi ya nchi katika siku zijazo na siku zote amekuwa akiona mabaya,” alieleza Profesa Semboja. Kwa upande wake, mtaalamu wa sheria za kodi ya madini, Dk Hellen Kihunsi alisema hata kama kuzuiwa kwa ndege ni suala la kisheria lakini Tundu Lissu alipaswa kutumia njia bora zaidi ya kuwasilisha kwa mamlaka husika badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

“Masuala kama haya yana maslahi kwa Taifa mbapo hata yeye (Lissu) ni sehemu ya Taifa hili, lakini kwa mwenendo ambao siku zote amekuwa akiuonesha unatilia shaka uadilifu na uzalendo wake kwa Taifa,” alieleza Dk Kihunsi. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze kuchukua juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kumekuwa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wakipinga juhudi hizo, ambapo ndege mbili za awali aina ya Bombardier zilipigiwa kelele na wapinzani wakidai hazifai licha ya kwamba zimekuwa msaada mkubwa katika sekta ya usafirishaji

Godzilla: Mimi si wa Kwanza Kushindwa Kufika Mbali na Mpenzi Wangu

0
0

Godzilla: Mimi si wa Kwanza Kushindwa Kufika Mbali na Mpenzi Wangu
Rapa Godzilla ambaye kwa sasa anasumbua na ngoma ya  'X ' amekanusha kuchanganyikiwa kutokana na kuachana na mpenzi wake na kudai kuwa yeye siyo wa kwanza kushindwa kufika mbali na mpenzi wake na kwamba maneno yanaletwa na umaarufu wake.

Akizungumza na mwandishi wetu Godzilla amesema kwamba watu walikuwa wanamuona kama kachanganyikiwa kutokana na kutokujua ni nini kilichokuwa kinaendelea kwenye maisha yake hivyo wengi walikuwa wakimchokonoa ili kuweza kumfahamu zaidi kutokana tu tayari yeye ni msanii lakini pia siyo mtu wa kuonyesha maisha yake binafsi hadharani.

"Nashangaa hata hayo maneno yalipokuwa yanatoka, lakini kwa vile mimi ni maarufu lazima mishale inayorushwa kwangu mingine inipate hivyo kwa kuwa hilo nimeshalifahamu ndiyo maana nimekuwa kimya kwa sababu sipendi maisha yangu kuwa wazi kwa kila mtu. Unajua kuna mtu anaishi Temeke lakini ukimkuta anasimulia maisha yangu ya Salasala utadhani ananijua sana lakini siwezi kuwajibu tayari mimi ni msanii hivyo napokea mishale yao" Zilla

"Ni kweli nilikuwa kimya watu wakaanza kuni attack pasipokujua mimi nafanya nini. Nilikuwa nashughulika na studio yangu kukamilika na tayari tumeshamaliza hilo. Kila kinachohitajika ndani ya studio tumeshanunua na kazi zitaanza kusikika na vitu vingi ambavyo tutakuwa tunatengeneza hapo vitaanza kusikika na kuonekana hivi karibuni".

Akizungumzia kuhusu wimbo wa 'X' Zillah amesema kuwa hakumlenga mtu yeyote kwenye wimbo huo na badala yake ni kama kutoa ujumbe kwa mtu anayetaka mafanikio lazima kufuta baadhi ya watu wanaokufanya wewe usifanikiwe.

"Sijamlenga aliyekuwa mpenzi wangu kwenye wimbo huu. Mimi ni msanii natakiwa kuburudisha watu. Kwenye wimbo huu maisha yangu sijayaweka lakini ni ujumbe ambao nimeufikisha mtaani kuwasaidia watu wanaohitaji kufanikiwa katika maisha na ndiyo maana ya 'X',  " Zilla aliongeza
Zilla ameahidi kuachia kichupa cha wimbo huu haraka baada ya kuitambulisha 'Audio' mapema wiki iliyopita.

Maskini Nuhu Mziwanda Mapenzi Bado Yamchanganya Aomba Ushauri Huu kwa Mashabiki Zake

0
0
Maskini Nuhu Mziwanda Mapenzi Bado Yamchanganya Aomba Ushauri Huu kwa Mashabiki Zake
Staa wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda aliyewahi kupata umaarufu mkubwa akiwa kwenye mahusiano na Shilole ametoa malalamiko yake Instagram kuhusu kuumizwa kila anapokuwa kwenye mahusiano….

Kwenye IG Yake Nuh Mziwanda ameandika ” Nimejifunza mengi sana kwenye life style yangu ya kimapenzi na najitoaga sana ila siku ya mwisho naumizwa ‘je unahisi Mwanamke wa aina gani atanifaa na nitaweza kudumu nae?Leo Nawaachieni mashabiki wangu mmalize hili “

Hivi karibuni Ndoa ya Nuh Mziwanda na Nawal ilivunjika ikiwa ni mwaka mmoja tu umepita, Nuh na Nawal wana mtoto mmoja wa kike anaitwa Anya.

Kesi ya Lema Yapigwa Kalenda

0
0
Kesi ya Lema Yapigwa Kalenda
Kesi iliyokuwa ikimkabiri Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Godbless Lema imehairishwa hadi Septemba 20 mwaka huu ambapo itasikilizwa tena.

Hayo yamebainishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha, Devota Msofe, Mwanasheria wa serikali Agnes Hiera ambapo alieleza kuwa kesi ya Lema ilikuwa inatakiwa kusomewa maelezo ya awali ya mashtaka yanayomkabiri lakini kwa bahati mbaya majalada yake yameitwa kwa Mkurugenzi wa mashtaka nchini.

Baada ya maelezo hayo, Wakili wa utetezi Sheck Mfinaga ameiomba Mahakama leo ndiyo iwe kuweka aihirisho la mwisho kwa kesi zinazomkabiri Lema kwani zimekuwa zikiahirishwa mara kwa mara.

Awali, Mei 29 mwaka huu, Hakimu Mkazi Desdery Kamugisha ambaye alikuwa akisikiliza kesi hizo alijitoa kuendelea kusikiliza kesi namba 441/2016, ambapo Lema anadaiwa kutoa matamshi yenye chuki na kuibua nia ovu kwa jamii.

Mhe. Godbless Lema alikaa Mahabusu ya gereza kuu la Kisongo kwa zaidi ya miezi minne, kutokana na kukosa dhamana katika kesi iliyokuwa inamkabiri na kuja kuachiwa kwa dhamana Marchi 3 mwaka huu na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Amshukuru Kardinali Pengo

0
0
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Amshukuru Kardinali Pengo
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema  msaada wa uchimbaji wa kisima cha huduma ya maji safi na salama kilichochimbwa kwenye Kituo cha Mahabusu ya Watoto Upanga, kimeipunguzia Serikali gharama ya Sh4,800,000 zilizokuwa zinatolewa kila mwaka.

Kutokana na hatua hiyo Waziri Mwalimu amemshukuru , Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam,  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kwa kuhamasisha vikundi vya uinjilishaji na umisionari kuguswa na kujitolea kugharamia uchimbaji wa kisima hicho.

"Msaada huu ni mkubwa kwetu tulikuwa tunalazimika kutumia shilingi 400,000 kwa mwezi kwa ajili ya maji, ambazo sasa tunaweza kuzihamishia kwenye gharama za matibabu kwa kuwakatia bima ya afya watoto,anasema.

Kadinali Pengo kwa upande wake amesema katika misaada yao ambayo wamekuwa wakiitoa kwa jamii wanaepuka kuitoa kwa ubaguzi wa aina yoyote.

"Tunaweza kufanya hayo japo yanaweza kuonekana ni madogo lakini sisi tunasukumwa na upendo, hivyo tukifika mahali hatuulizi wewe ni dini gani au dhehebu gani tunapenda amani na upendo udumu kwenye jamii,"alisema.

Chanzo cha kuchimbwa kisima hicho ni kutokana na ziara waliyoifanya watoto wa Shirika la Utoto Kurasini kituoni hapo na kubaini changamoto inayowakabili watoto wenzao, hivyo wakaguswa na kuomba ushirikiano na vikundi  vingine vilivyowezesha kujengwa kwa gharama ya Sh 11,780,000

Meya wa Ubungo Afunguka Kuhusu Bomoabomoa ya Kimara Kuwa ni Uonevu na Unabebwa Kisiasa

0
0
Meya wa Ubungo Afunguka Kuhusu Bomoabomoa ya Kimara Kuwa ni Uonevu na Linabebwa Kisiasa
Meya wa Manispaa ya Ubungo Mh. Boniface Jacob, amelezea tukio la bomoa bomoa linaloendelea katika maeneo ya Kimara na kuathiri wakazi wake kuwa ni la uonevu na lenye kubebwa kisiasa.

Akizungumza na East Africa Radio, Boniface Jacob amesema kitendo hicho kimekuwa cha uonevu kwa sababu kesi bado iko mahakamani, lakini serikali imetoa amri nyumba hizo zibomolewe, bila kusubiria hatma ya kesi.

Boniface Jacob pia ameelezea tukio hilo limebebwa na sura ya kisiasa na kusema kuwa kitendo cha wakazi wa maeneo hayo kuwa upande wa vyama vya upinzani ndiyo umewagharimu, na kufanyiwa vitendo vya uonevu wa hali ya juu.

Eneo la Kimara kumefanyika zoezi la kubomoa nyumba na ambalo limeonekana kuathiri kiasi kikubwa cha wakazi wa maeneo hayo, na kuibua malalamiko mengi kwa watanzania ambao hata siyo wakazi wa maeneo haya.

East Africa Radio ilifanya jitihada za kumtafuta Mkurugenzi Mkuu TANROADS Patrick Mfugale ili iweze kuweka bayana suala hilo, na kusema kuwa kitu ambacho yeye anafahamu kesi ya mahakamani iliisha tangu mwaka 1993 na serikali ilishinda, hivyo walikuwa na amri napo, lakini kabla ya kuanza zoezi la ubomoaji walishatoa 'notice' kwa wakazi hao ili waweze kutoka maeneo hayo.
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live


Latest Images