Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Mzee Majuto: Siku Zangu za Kuishi Zimebaki Chache

$
0
0
Mzee Majuto: Siku Zangu za Kuishi Zimebaki Chache
KOMEDIANI mwenye jina kubwa Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, amevunja ukimya kuwa, katika umri alionao kwa sasa wa zaidi ya miaka sitini, hataki kulumbana na mtu maana siku zake za kuishi zimebaki chache asije akafa na mtu.

Akizungumza na Ijumaa  Wikienda, Mzee Majuto alisema kuwa, kitu ambacho anakiepuka kwa sasa ni kugombana na mtu na ndiyo maana hata akisemwa vibaya kwenye mitandao ananyamaza kwani umri umemtupa mkono.

“Siku zangu za kuishi zimebaki chache na huu uzee, ninatafuta nini kuanza kugombana na vijana wadogo? Hata watu wazima wezangu? Siku zangu za kuishi zimebaki chache, nisije nikafa na mtu bure,” alisema Mzee Majuto

Maneno Matamu Aloambiwa Roma na Mkewe baada ya Kuwa na Views Wengi

$
0
0
Maneno Matamu Aloambiwa Roma na Mkewe baada ya Kuwa na Views Wengi
Mke wa msanii wa Roma, Nancy ametoa ahadi yenye utata kidogo kwa mumewe mara baada ya video yake ‘Zimbabwe’ kufikisha views milioni moja.

Siku ya jana August 20, 2017 video ya Roma ilifikisha idadi hiyo ya views katika mtandao wa YouTube tangu ilipoweka katika mtandao huo August 10 mwaka huu. Kitendo hicho kilimchanganya Baby Mama huyo na kukimbilia katika mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe mfupi;

Ameandika hivi mke wa roma kwa mumewe"Finally You Made It #1Milion_Views Ndani ya Week 1 Na siku 3!!!😘😘 Walahi Mume wangu @roma_zimbabwe#LEO_NITAKUPA_STYLE_ZOTE Kwa Furaha Niliyonayo!!! Hongera Mno!! Much Congrat kwa shemela @nicklassm Nakuona Mbali Saaana!!'

Video hiyo hadi sasa ina views 1,040,849, hata hivyo imetoa katika trending baada ya kukaa katika number one trending kwa wiki moja. Lakini video mpya ya Rostam (Roma & Stamina) ‘Hivi Ama Vile’ ameanza kufanya vizuri ambapo kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika trending.

Msechu Atoboa Siri ya Kuwahi Kushika Nafasi ya Mwisho Darasani

$
0
0
Msechu Atoboa Siri ya Kuwahi Kushika Nafasi ya Mwisho Darasani
Msanii wa Bongo Flava, Peter Msechu ametoboa siri ya kuwahi kushika nafasi ya mwisho darasani katika mtihani wa hesabu kipindi akisoma kidato cha tano na sita (advance level) kitu kilichopelekea kuchapwa fimbo 6 hadharani .

kupitia ukurasa wake wa Instagram amebainisha hayo na kueleza kuwa kitendo hicho kilimfedhehesha sana kwa kuwa kilitokea mbele ya wadogo zake (O Level).

Mchana wa leo Tanga Nilipotembelea shule niliyosomea advance level GALANOS SEC SCHOOL.

Hapa niliposimama ndio sehemu ya assembly Kuu Kila jumatatu Hii ndio sehemu jumatatu moja hivi mbele ya wanafunzi wote wa O level na A level nilitangazwa wa mwisho katika mtihani wa darasani wa hesabu(pure mathematics) kuwa Mimi ndiye nimeshika nafasi ya mwisho, nilitangazwa baada ya headmaster kusikia wanatangazwa walioongoza katika mtuhani huo wakipewa Zawadi. Baada ya yeye kusikia hivyo kwa lengo la kutaka kuonyesha hataki Watu wafeli Shuleni kwake akaagiza aliyeshika mkia katika mtihani huo aje mbele naye apewa Zawadi yake (KUCHAPWA FIMBO 6 HADHARANI).

Siku hii niliumia Sana sana kwani niliona Kama nimedhalilishwa Sana pale Shuleni kitendo cha mm kutambulishwa wadogo zangu O level na shule nzima kiujumla kuwa nimekuwa wa mwisho.

Siwezi laumu kwani huwenda wao walihisi ni njia sahihi kwa Kipindi kile kunisaidia. Ila ninachokumbuka matokeo yake baada ya ile hali kutokea wanafunzi wa O level hawakuniheshimu tena hata walipokuja Kwenye Darasa letu la A level(EGM) kuja kuuliza maswali hakuna aliyeniuliza kwani waliona SINA AKILI na siwezi msaidia.

Ilinisumbuaga Sana kwa muda mrefu Ila kwa sababu nilikuwaga waruwaru nilikuja kuzoea baadae ila tokea Siku hiyo kwangu naamini ilikuwa Siku ya mwisho kutamani kuipenda shule. Nilirudi nyuma Sana Sana na nikawa kilaza Namba moja darasani nisiyejiweza.

LEO HII NINAJIFUNZA JAMBO KUWA MUNGU NDIO HUPANGA HATIMA YA MTU NA SI MWANADAMU. LEO HII NAKUJA HAPA NATAFAKARI SANA KWANINI MUNGU ASIITWE MUNGU?? #KAZANAnaUNACHOKIAMINI

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake itwayo Yakawa baada ya kubamba na ngoma ‘Nasema Nawe’ aliyoshirikishwa na Tabla.


Rais Magufuli Akutana na Rais wa JICA

$
0
0
Rais Magufuli Akutana na Rais wa JICA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akutana na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Shinichi Kitaoka Ikulu Dar es saalam. Ambapo Rais huyo wa JICA amempongeza Rais Magufuli kwa kupambana na rushwa na msukumo mkubwa anaouleta wa kupambana kuleta maendeleo hususani kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Nisher: Adam Juma Anaweza Kufanya video Kali Hakuna Aliyechukua Crown Yake.

$
0
0
Nisher: Adam Juma Anaweza Kufanya video Kali Hakuna Aliyechukua Crown Yake.
Director Nisher amesema bado anashangazwa na watu ambao hadi leo wanadai yeye alikuja kuchukua taji (crown) ya Adam Juma katika music video industry Bongo kwani hakuna anayeweza kufanya hivyo.

Nisher amesema hayo alipokuwa akijibu maswali ya mashabiki wake waliyouliza kupitia mitandao ya kijamii, ambapo ameeleza kuwa hata sasa hivi Adam Juma anaweza kufanya video kali kwani hakuna aliyechukua crown yake.

“Mpaka leo kuna ambao wanasema mimi nilimfukuza Adam Juma kwenye music video industry, siwezi kumfukuza Adam Juma, nimekuta ana C.V yake ndefu inatisha, am respect him forever. Siwezi nikakaa nisema nimekuja kuichua crown Adam Juma na the game is big enough for the both side, industry ni kubwa kiasi kwamba inatutosha watu wote kila mtu anaweza kuwa na crown.

“Mimi na uwezo wa kunyamaza mwaka mmoja au miezi kadhaa nisitoe video lakini nikitoa video imetua, ni Nisher kwa sababu nishajenga hilo jina, nimelijenga zaidi ya miaka saba sasa, ipo nobody can take my crown, nobody can take Adam Juma crown,” amesema Nisher.

Pia ameongeza kuwa, “Adam Juma sasa hivi akiamua kupiga video inatoka kali, amerudi, so hakuna kukosea, hakuna kufeli. Biashara tu inakupanda na kushuka, kuna wakati ni high season na kuna wakati ni low season, its business,” amesisitiza

Ester Bulaya Ahamishiwa Hospitali ya Bugando

$
0
0
Ester Bulaya Ahamishiwa Hospitali ya Bugando
Mbunge wa  jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime alikokimbizwa Jana Jumapili baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu  ya polisi mjini Tarime,  amehamishiwa  Hospitali ya Rufaa ya Bugando jjijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche amesema kuhamishiwa Bugando kwa mbunge huyo kumewezekana baada ya kupata dhamana ya polisi  aliyowekewa  na watu watatu akiwemo wakili wake, Alex Masaba.

Wengine waliomdhamini kwa kusaini hati ya Sh20 milioni ni Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko  na Mwenyekiti wa Mtaa wa Songambele ‘B’, Pamba Chacha.

Heche amesema kabla ya kuachiwa kwa dhamana Mkuu wa Wilaya ya Kipolisi (OCD), wa Tarime, Thomas Mapuli alimtembelea mbunge huyo hospitalini kuona hali yake kiafya.




Simba Watua Dar Tayari kwa Mechi na Watani Wao

$
0
0
Simba Watua Dar Tayari kwa Mechi na Watani Wao
Kikosi cha Klabu ya Simba kimemaliza kambi ambayo ilikuwa imewekwa kisiwani Unguja, Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga katika Ngao ya Jamii.

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo timu zote zilikuwa nje ya jiji hilo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na maandalizi ya msimu wa 2017/18 kwa jumla.

Wachezaji wa Simba wamewasili Dar es Salaam majira ya saa tano wakiwa na benchi la ufundi baada ya timu hiyo kuwa Unguja kwa siku kadhaa.

Timu hiyo ilirejea Dar kwa ndege na kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kisha kuelekea kambini kujiandaa kwa mchezo huo wa Ngao ya Jamii.

Baadhi ya mastaa waliwasili ni Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Said Ndemla, Kotei, Salim Mbonde na wengine.

Wachezaji Hawa wa Yanga Kuikosa Mechi ya Ufunguzi wa Ligi Kuu Bara

$
0
0
Wachezaji Hawa wa Yanga Kuikosa Mechi ya Ufunguzi wa Ligi Kuu Bara
Zikiwa zimebaki siku mbili watani wa jadi Simba na Yanga kukutana katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara 2017/18 alimaarufu kama Ngao ya Jamii, klabu ya Yanga yatangaza wachezaji wake ambao hawataweza kucheza mchezo huo.

Klabu ya Yanga ambayo inatarajiwa kuingia nchini siku ya Jumanne ya tarehe 22 Agosti mwaka huu ikitokea visiwani Pemba Zanzibar ilipoweka kambi ya wiki nzima kujiandaa dhidi ya Simba imesema wachezaji wake watatu akiwepo Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zambia Obrey Chirwa , Benno Kakolanya na Mwasiuya kutokana na kuwa majeruhi.

Aidha klabu hiyo imesema kuwa imejipanga tayari kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya wapinzani wake wa jadi na kusema hali kikosini iko salama wanasubiri mchezo husika ambao utapigwa siku ya Jumatano tarehe 23 Agosti uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mitandao ya jamii bado tambo mbalimbali zimekuwa zikiendelea dhidi ya watani hao wajadi huku kila upande ukijigamba kuwa katika mchezo huo wao wataibuka na ushindi wa hali ya juu, huku wengine wakidai kuwa huenda Simba inaweza kurudi historia yake ya kuifunga Yanga kwa goli

Wizara ya Elimu Yakanusha Uvumi wa Kupata Degree Bila Kupita Kidato cha 6

$
0
0
Wizara ya Elimu Yakanusha Uvumi wa  Kupata Degree Bila Kupita Kidato cha 6
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia imeutaarifu umma kuwa taarifa zinazosambaa kwa kasi kwenye kichwa cha habari kuwa ” Serikali yapiga marufuku kusoma degree bila kupita kidato cha sita” sio za kweli na hazijatolewa na waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.

Wizara kupitia wizara yake imeutaarifu umma kuwa taarifa hizo ni taarifa za uongo ziliwahi kusambazwa pia kipindi cha udahili cha mwaka 2016.

Wizara hiyo imeendelea kusisitiza na kuufahamisha umma kuwa Waziri ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako hajatangaza chochote na popote na kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote.

Nchi 10 Zenye Watu Wenye IQ Mdogo zaidi Duniani......

$
0
0
Nchi 10 Zenye Watu Wenye IQ Mdogo zaidi Duniani......

IQ ni kifupi cha Intelligence Quotient,  IQ ni kipimo cha akili yako na imeelezwa kwa namba.

IQ ni kipimo kinachoonyesha uwezo wa akili katika nchi.


Nchi 10 zenye uwezo mgodo wa IQ Duniani.
1. Equatorial Guinea: IQ Wastani wa 59.
2. Saint Lucia: IQ Wastani wa 62.
3. Sierra Leone: IQ Wastani wa 64.
4. Mozambique: IQ Wastani wa 64.
5. Gabon: IQ Wastani wa 64.
6. Ethiopia: IQ Wastani wa 64.
7. Democratic Republic of the Congo: IQ Wastani wa 64.
8. Central African Republic: IQ Wastani wa 64.
9. Cameroon:  IQ Wastani wa 64.
10. Republic of the Congo:IQ Wastani wa 64.


IQ kwa nchi za East Africa
23 Uganda: IQ Wastani wa 84.
27 Kenya: IQ Wastani wa 80.
34 Tanzania: IQ Wastani wa 72.

Clouds FM Walianzisha Dude la Fiesta Kushirikiana na Tigo....Kutembelea Mikoa Hii

$
0
0
Tamasha la Fiesta ambalo huvutia umati mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali nchini, limezinduliwa rasmi Jumatatu hii jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta, Sebastian Maganga (kushoto), Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu (katikati) pamoja Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Tigo, William Mpinga.

Tamasha hilo ambalo huandaliwa kila mwaka na Kampuni ya Prime Time Promotions, mwaka huu linatimiza miaka 16 tangu kuanzishwa kwake. Linatarajiwa kufanyika katika mikoa 15 ambapo Watanzania watapata burudani na elimu jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika makao mkuu ya Kampuni ya Tigo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta, Sebastian Maganga alisema tamasha hilo safari hii litajulikana kwa jina la Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta, Sebastian Maganga na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Tigo, William Mpinga

Alisema safari hii Fiesta msimu wa 2017 wamejipanga vilivyo kuhakikisha Watanzania wananufaika na tamasha hilo katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na: kupata burudani na elimu ili kuhakikisha ubora wake wa miaka 15 iliyopita haupotei.

“Lakini pia baada ya uzinduzi huu, zoezi la usajili wa wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo unaanza mara moja na utachukua kama wiki mbili hivi, baada ya hapo ndipo itakapofahamika ni mkoa gani Tigo Fiesta 2017 Tumekosomaa itaanzia,” alisema Maganga.

Jenerali wa Jeshi Ateuliwa na Rais Magufuli Kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

$
0
0
Raisi John Magufuli leo August 21, 2017 amemteua Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Uteuzi wa Brigedia Jenerali John Julius Mbungo unaanza leo August 21, 2017.

Heche Awavaa Wanaomponda Tundu Lissu kwa Kuisema Serikali

$
0
0
Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), John Heche amefunguka na kuwachana baadhi ya wasomi wa nchi na serikali ambao awali waliibuka na kudai Tundu Lissu amehongwa na wazungu na kusema uzalendo wa nchi si kuiunga mkono serikali.

John Heche amesema hayo baada ya baadhi ya wasomi kuibuka na kuanza kumtuhumu Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu huku wakisema kuwa kiongozi huyo si mzalendo wa nchi hii huku wengine wakidai anatumiwa na wazungu kuhujumu nchi.

"Leo Benson Bana na wengine wachache wanahoji uzalendo wa Lissu, Bana amewahi kufanya nini cha kizalendo kwa nchi hii? Uzalendo siyo kuunga mkono serikali iliyopo madarakani uzalendo ni kupenda nchi yako" alisema John Heche

Mbali na hilo John Heche amesisitiza kuwa wasomi wa nchi hii wamekuwa wakilitia aibu taifa la Tanzania kutokana na maamuzi yao pamoja na kupotosha ukweli uliowazi kabisaa.

"Lissu alitoa tahadhari kwa serikali kuacha kuvunja mikataba bila kufuata utaratibu wa kisheria, serikali hii iliyotuingiza kwenye matope haya ikatoka na kusema Lissu amehongwa na wazungu kuwatetea.

"Leo mmeshindwa kesi mnatakiwa kulipa mabillion ya pesa za walipa kodi masikini kwa kuvunja mikataba bila utaratibu, Lissu kusema tena inaonekana siyo mzalendo! Hivi serikali hii inawaona Watanzania hawawezi kufikiri vizuri? na nyinyi wasomi wetu mnatia aibu sana" alisisitiza John Heche.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo wa Tarime Vijijini John Heche amemaliza ziara yake jimboni kwake huku akiwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi, lakini pia ametoa salamu kwa baadhi ya watawala wasio waadilifu na kuwaambia hawataweza kuwazuia katika kutimiza majukumu yao.

"Vitisho vya watawala wasiokuwa waadilifu kujaribu kutuzuia kufanya majukumu yetu havitafanikiwa. Asanteni Sirari kwa kujitokeza kwa wingi bila kuogopa vitisho. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu ametuwezesha kuhitimisha vizuri ziara ya majimbo yetu kuhakikisha tunasaidiana kusukuma mbele maendeleo ya watu wetu" alisema John Heche

JE Wajua Chanzo cha Fangasi Katika Mwili wa Binadamu? Soma Hapa

$
0
0
Fangasi ni nini
Watu wengi hawajisikii vizuri unapokuja wakati wa kuzungumza juu ya fangasi kutokana na namna ugonjwa wenyewe unavyochukuliwa na jamii. Hii inatokea sababu mara nyingi ugonjwa huu hutokea sehemu ambazo ni aibu kuzizungumzia au kuzionyesha hadharani.

Fangasi mara nyingi inawapata zaidi watu wanaoishi kwenye maeneno ya joto kuliko wale wanaoishi maeneno ya baridi kutokana na vimelea vya ugonjwa wenyewe kushamiri zaidi sehemu za joto.

Pamoja na hayo yote fangasi ni ugonjwa wa kawaida ambao unaweza kumpata mtu yeyote, mimi mwenyewe nimewahi kupatwa na fangasi sehemu za siri na zilinisumbuwa sana. Takwimu zinadai katika kila watu watano mmoja kati yao anapatwa na maradhi haya katika safari yake ya kuishi kwa hapa Tanzania.

Hapo awali fangasi walikuwa wanahesabika kama ni aina mojawapo ya mimea lakini baadaye sayansi imekuja kugunduwa kuwa fangasi hawana sifa za kuwekwa katika kundi la mimea.

Kuna fangasi wa aina nyingi lakini tunaweza kuwaweka kwenye makundi makubwa mawili ambao ni fangasi wanaoleta madhara ya kwenye ngozi na fangasi ambao maisha yao yote wanaishi kwenye ngozi wakiitegemea hiyo tu ili waweze kuishi.

Vimelea hivi vya fangasi vinavyokaa kwenye ngozi vimegawanyika tena katika sehemu kuu mbili, kundi la kwanza ni wale wanaojulikana kwa kitaalamu kama dermatophytes au dematofaiti kwa kiswahili na hamira au yeast kwa kiingereza

Kwahiyo kama ulikuwa hufahamu, basi leo fahamu kuwa hamira yaani hamira ile inayotumika wakati wa kupika maandazi na hata mikate ni fangasi.  Fangasi huishi kwenye ngozi kwakuwa hutegemea protini inayopatikana kwenye ngozi ambayo huitwa keratini (keratin).

Keratini ni protini ya muhimu sana katika ngozi na inatengeneza asilimia kubwa ya ngozi, kucha na nywele ambako kama umeshagundua mpaka sasa ni sehemu ambazo fangasi hupenda sana kushambulia kuliko sehemu nyingine za mwili.

Kwahiyo utagundua kuwa sababu kubwa ya waTanzania wengi kuugua fangasi ni hii protini ya kwenye ngozi ijulikanayo kama keratini, joto na uwepo wa hali ya unyevu unyevu katika maeneno mengi hasa ukanda wa pwani.

Kwa hali ya kawaida, fangasi wa aina hii huwa hawana madhara makubwa, wao huweka makazi yao tu kwenye ngozi bila kusababisha hali yoyote ya madhara kwenye ngozi. Madhara ya vimelea hivi huonekana baada ya idadi kubwa ya vimelea hivi kuongezeka kwenye eneo dogo moja la ngozi.

Fangasi ni ugonjwa unaoambukiza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ikiwa watu hao watashirikiana mavazi na vifaa vingine vya usafi wa mwili.

Madhara ya Fangasi katika ngozi
Vimelea vya fangasi huathiri ngozi moja kwa moja kwa kuvamia na kutafuna keratini ambayo ni protini muhimu ya ngozi ikiwa inatengeneza sehemu kubwa ya ngozi, kucha na nywele.

Aina za maradhi ya ngozi yanayosababishwa na fangasi

Kuna aina nyingi za maradhi ya ngozi ambayo chanzo chake huwa ni fangasi na hayo yote yameganwanywa katika sehemu kuu mbili:

Download App ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu Yako Kupata Habari zetu Kwa Urahisi..Bonyeza Hapa

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Aliyevujisha Siri ya Bombardier Kwa Lissu Asakwa....Habari Zilizopo Katika Magazetibya Leo Jumanne ya August 22

$
0
0

Aliyevujisha Siri ya Bombardier Kwa Lissu Asakwa....Habari Zilizopo Katika Magazetibya Leo Jumanne ya August 22

Tarime: Kamanda wa Polisi Ashindwa Kueleza Sheria Aliyoivunjwa Esther Bulaya Kwenda Jimbo Lisilo lake

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya ashindwa kueleza kifungu cha sheria au kununi ya adhabu aliyovunja Esther Bulaya.

Wiki iliyoisha Esther Bulaya ambaye ni mbungewa Bunda mjini, aliwekwa Korokoroni kwa kile kilichodaiwa ni kufanya mkutano wa hadhara kwenye jimbo lisilo lake la Tarime Vijijini.

Bulaya ambaye ni CHADEMA, alienda kwenye jimbo la Heche la Tarime vijijini ambaye pia ni CHADEMA. Heche alikuwa na Ziara jimboni mwake ambapo kulifanyika mkutano Nyamongo, Walikuwa na mkutano wa hadhara, Polisi hawakufurahishwa na kitendo cha Bulaya kupanda jukwaani kusalimia na kuhutubia kwani sio jimboni kwake.

My Take;

Viongozi wetu wote wa Tanzania sasa ni wakati wao wa kupewa Semina Elekezi.

Sheikh Ponda Afunguka "Hali ni Mbaya Sana, Mauaji ya Kutisha Yanaendelea Nchini...Bahari Zimejaa Maiti Serikali ipo Kimya"

$
0
0

Sheikh ponda ametoa wito kwa jamii na kwa rais magufuli na kusema kuna mauaji ya kutisha yanaendelea nchi hii na kusema upo umuhimu wa mamlaka nyingine kama bunge kushughukikia suala hili na sio kuiachia serikali pekee

Amesema kwa sababu hali ni mbaya sana ipo haja ya kuunda tume huru ya bunge
Ameonyesha habari iliyoandikwa na gazeti la Nipashe ya miili ya watu 15 kukutwa kwenye viroba baharini na walioua hawajulikani hii ni ishara kuwa hali ni mbaya

Pia ameziasa taasisi za kutetea haki za binadamu kukemea hali hii

Amesema waliopotelewa na ndugu watoe taarifa polisi na kwa viongozi kama wao

TAZAMA VIDEO:

Je Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo, Kufika Kileleni Haraka na Kushindwa Kurudia Tendo au Maumbile Madogo ya Uume?

$
0
0
JE, UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO, KUFIKA KILELENI HARAKA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO AU MAUMBILE MADOGO YA UUME? Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume husababishwa na mambo mengi kama KISUKARI, UNENE ULIOPITILIZA, KUJICHUA (MASTER BLASHION), HOMONI kushindwa kufanya kazi ipasavyo n.k. Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.

 BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa ☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni ☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa. Kwa kutumia mimea na matunda @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250000@250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6 hadi 7 @150000@150,000/=
3.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150000@150,000/=
4.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130000@130,000/= BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA ZIMETHIBITISHWA KIAFYA. KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :- @markson_beauty_pr @markson_beauty_pr @markson_beauty_pr

Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa (+255) 0767447444 na 0714335378

NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

Mwili wa Aliyekuwa Mwanaharakati wa Kupiga Ujangili wa Tembo Kuagwa Leo Dar

$
0
0
Mwili wa Aliyekuwa Mwanaharakati wa Kupiga Ujangili wa Tembo Kuagwa Leo Dar
MWILI wa mwanaharakati wa kupinga ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo wa nchi za Afrika Wayne Lotter, aliyepigwa risasi na kuuawa jijini Dar es Salaam Jumatano iliyopita unatarajiwa kuagwa leo katika viwanja vya Baobao Villlge Masaki jijini Dar.

Wayne ambaye alikuwa mwanzilishi wa PAMS Foundation, taasisi ambayo imekuwa katika mstari wa mbele kusaidia kupambana na uwindaji haramu na biashara ya pembe za ndovu nchini Tanzania aliuawa na watu wasiofahamika Agosti 16 mwaka huu wakati anatoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akielekea nyumbani kwake Masaki.

Akizungumza na wana habari kwa niaba ya wana familia, jana Krissie Clark alisema wanatarajia kuuaga mwili wa mwanaharakati huyo leo kisha kuusafirisha kwenda nyumbani kwao Afrika Kusini kwa maziko.

Wayne Lotter.
Alisema kuuawa kwa Wayne hakutawafanya kurudisha nyuma mapambano dhidi ya ujangili na badala yake wameelekeza nguvu zao katika Afrika ili kutokomeza kabisa ujangili kama ilivyokuwa ndoto ya ndugu yao.

Kifo cha mwanaharakati huyo kimeacha maswali mengi yasiyokuwa na majibu hasa ikizingatiwa kuwa amesaidia kwa kiasi kikubwa kukamatwa kwa vinara wengi wa ujangili akiwemo Malkia wa Meno ya Tembo.
Kifo chake kimetikisa mataifa ya nje ya bara hili la Afrika kwani magazeti ya New York Times la Marekani na The Guardian na The Independent ya Uingereza yamekuwa yakimtaja kwamba enzi za uhai wake alitetea wanyama hasa tembo ambao wamekuwa wakiwindwa na majangili, hivyo kuwa mmoja wa waliosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujangili nchi mbalimbali Tanzania ikiwemo.

Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images