Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

R.O.M.A Kuleta Hamsha Hamsha Mechi ya Simba na Yanga Taifa Kesho

0
0
R.O.M.A Kuleta Hamsha Hamsha Mechi ya Simba na Yanga Taifa Kesho
Ikiwa imebakia siku kuelekea mtanange kwa mechi ya Ngao ya Jamii, rapa Roma Mkatoliki ambaye ni mshabiki namba moja wa klabu ya Simba amefunguka akidai siku hiyo atakuwepo uwanja wa Taifa kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji na mashabiki wa Simba.


Roma amebainisha hayo muda mchache alipotoka katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema siku hiyo timu ya Yanga ijiandae kwa kupokea kichapo kitakatifu.
"Wanangu wote mashabiki wa timu ya Simba tukutane Taifa kwa ajili ya kumng'oa huyu jamaa wa rangi ya njano (Yanga), tutamkalisha Stamina na wanae wote wanaoshabikia timu hiyo. Najua mashabiki wa Yanga hawataamini kitakachotokea sisi hatuongei sana",alisema Roma.

Katika hatua nyingine, msanii Stamina ambaye ni shabiki wa Yanga amedai timu hiyo haina upinzani na klabu yoyote kwa kuwa timu ya Yanga ndiyo imeshikilia rekodi ya ushindi mpaka sasa.


Waziri Mkuu Awataka Watanzania Kuwa Wazalendo

0
0
Waziri Mkuu Awataka Watanzania Kuwa Wazalendo
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wote wahakikishe wanaboresha mshikamano wao pamoja na kuimarisha uzalendo kwa Taifa lao huku akisema uzalendo ni muhimu sana.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea udaktari nchini Cuba.

“Uzalendo ni muhimu sana kwa sababu tumekosa fursa nyingi za kimaendeleo kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa wazalendo kwa Taifa lao.”

Hata hivyo Waziri Mkuu alisema Serikali inatambua uwepo wao wa kimasomo nchini Cuba na kwamba inatarajia kupata mchango mkubwa kutoka kwao punde wamalizapo masomo yao.“Nawaomba msome kwa bidii na mfaulu mitihani yenu. Elimu yenu iwasaidie katika ajira na muweze kurejesha mikopo mliyopewa na Serikali ili iwanufaishe wengine.”

Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi hao kuzingatia sheria za nchi waliyoko pamoja na kukumbuka kurudi nyumbani mara wamalizapo masomo yao.


Watu Wanne Washtakiwa kwa Kula nyama ya Binadamu Afrika Kusini

0
0
Watu Wanne Washtakiwa kwa Kula nyama ya Binadamu Afrika Kusini
Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.

Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu.
Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana.
Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua.

Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban.
Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa.
Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza.

Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za binadamu, kwa kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu kadhaa.
Mwezi mmoja uiopita mjini Durban, mwanamume mmoja alikamatwa akiwana na kichwa cha binadamu ambacho inanamiwa alikuwa na mpango wa kikiuza kwa daktari ya kitamadunia.

Viongozi wa Serikali Mkoani Tabora Washikiliwa na Polisi kwa Mauaji

0
0
Viongozi wa Serikali Mkoani Tabora Washikiliwa na Polisi kwa Mauaji
Jeshi la Polisi Mkoani Tabora limewafikisha katika Mahakama ya hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Nzega Mkoani humo watuhumiwa 32 wakiwemo viongozi wa kijiji na kata kwa mauaji ya wanawake watano wa kijiji cha Udoma kata Uchama.

Mwendesha Mashtaka wa jeshi la Polisi Wilaya ya Nzega Merito Ukongoji,mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo Sarafina Nsana, ameiambia Mahakama hiyo mnano tarehe 25 mwezi uliopita katika kijiji cha Undomo watuhumiwa hao waliwashambulia kwa kuwapiga na kuwachoma moto hadi kufa wanawake hao watano kwa tuhuma za ushirikina.

Merito amewataja wanawake hao waliouwa kwa kuchomwa moto ni pamoja na Sukuma Masali, Ester Kiswahili, Christina Said, Mwashi Mwanamila pamoja na kabuka Kagito, lakini watuhumiwa hao hawakupaswa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na Mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Baadhi ya Viongozi waliokamatwa kwa tuhumu hizo ni pamoja na Malewa Malonji, mtendaji wa kata ya Uchama, Karoli Masanja Diwani wa kata ya Uchama, pamoja na Doto Saraganda ambaye ni mtemi wa Sungusungu na kesi hiyo itatajwa tena tarehe 4 mwezi ujao na watuhumiwa wamerudishwa tena rumande.

Hata mauaji hayo yalitekelezwa Mwishoni mwa mwezi Julai huko katika kata ya Uchama Wilayani Nzega Mkoani Tabo kwa madai kuwa wanatekeleza imani za ushirikina.

Trump Aapa Kushinda Vita Afghanistan

0
0
Trump Aapa Kushinda Vita Afghanistan
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Afghanistan kutaacha pengo ambalo huenda likajazwa na magaidi.

Alisema kuwa mapango yake ilikuwa ni ya kuondoa vikosi vya Marekani, lakini badala yake ameamua wanajeshi hao kubakia ili kuzuia kurudia makosa ambao yalitokea nchini Iraq.
Amesema pia kuwa anaongeza idadi ya wanajeshi watakao pelekwa nchini Afghanstan.

Akizungumza kupitia Televishen, Rais Trump amesisitiza kuwa kipaumbele cha Marekani ni kutekeleza masuala yenye maslahi katika usalama wa taifa hilo, kutokomeza mtandao wa ugaidi
Amesisitiza pia kuwa kitendo cha Marekani kujiondoa kwa haraka Afghanistan, kitatatoa mwanya kwa ugaidi kujiimarisha zaidi kama ilivyotokea Iraq.

Hata hivyo Trump amekwepa kuzungumzia moja kwa moja muda wa mwisho wa ushiriki wa Marekani nchini Afghastan na idadi kamili ya ongezeko la wanajeshi.

Rais Trump ameitupia lawama Pakistan kwa madai kuwa inawahifadhi magaidi ambapo amesema suala hilo linapaswa kuachwa mara moja.
Katika hatua nyingine amezungumzia mpango wa Marekani kuimarisha mpango wa ushirikiano na India.

Timu ya Yanga Yatoa Onyo kwa Wafanyabiashara Kuacha Kuuza Vifaa na Jezi Zenye Nembo za Yanga Kuanzia Leo

0
0
Timu ya Yanga Yatoa Onyo kwa Wafanyabiashara Kuacha Kuuza Vifaa na Jezi Zenye Nembo za Yanga Kuanzia Leo
Klabu ya Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kupitia Afisa habari wake Dismas Ten amewataka wafanyabiashara kuacha kuuza vifaa na jezi zenye nembo za Yanga kuanzia leo na endapo watakaidi agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.


Hayo yameibuka ikiwa imebakia siku moja kuelekea katika mechi ya watani wa jadi inayotarajiwa kupigwa siku ya Jumatano (kesho), ambapo kipindi chote baadhi ya wafanyabiashara huwa wanajipatia kipato chao kwa kuuza jezi za Yanga pamoja na vifaa vingine kwa wachezaji ambao wana lengo la kuingia ndani ya uwanja kutazama mechi.

"Klabu inatoa tahadhari (onyo) kwa watu wote ambao kwa namna moja ama nyingine watashiriki kuuza vifaa au jezi zenye nembo ya Yanga SC kuanzia leo, watakamatwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao", alisema Dismas katika taarifa yake aliyoitoa.

Pamoja na hayo, Dismas aliendelea kwa kusema "kikosi maalum kimeandaliwa kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa jambo hili, na wahujumu wote watakamatwa".

Kwa upande mwingine, klabu ya Yanga kesho itashuka dimbani kuminyana na Simba huku ikiwakosa wachezaji wake watatu akiwepo mshambuliaji mwenye uraia wa Zambia Obrey Chirwa , Benno Kakolanya na Mwasiuya kutokana na kuwa majeruhi.

Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE.

Mr Nice Azushiwa Janga Lingine Nchini Kenya

0
0
Mr Nice Azushiwa Janga Lingine Nchini Kenya
Msanii wa mkongwe wa muziki, Mr Nice ambaye kwa sasa anaishi nchini Kenya amekuwa alizushiwa mambo mabaya na vyombo vya habari kila kukicha ambapo Jumatatu hii katika sherehe za kuapishwa kwa Sonko amezushiwa kitu kingine.

Muimbaji huyo katika show hiyo alidaiwa kuibiwa baadhi ya vitu baada ya kuvamiwa na mashabiki kitu ambacho amekanusha.

“Waandishi vilaza mnapenda kurukia sana hata msilolijua mimi katika show ya kuapishwa Sonko leo sijaibiwa na mtu yoyote,” Mr Nice aliandika Facebook “Kifupi ni kwamba mashabiki waling’ang’ana kucheza na mimi na bahati mbaya wakajikuta wamekata cheni zangu na pia leseni yangu ikadondoka nilikuwa nayo kwa mfuko wa koti la suti,”

Aliongeza, “Mkome kabisaaaa kutengeneza ishu za kipumbavu ili muuze vijikaratasi vyenu huko mtaani. Kenya iko sawa na hakuna tatizo lolote kabisaaaaaa na bado 21/8/2017 tuwache rafiki yangu Sonko achape kazi na Nairobi ifaidike naye,”

Miezi miwili iliyopita muimbaji huyo alizushiwa kifo kupitia mitandao ya kijamii.



Peter Msigwa na Mbunge Msukuma Kimewaka...Msigwa Amponda Msukuma na Kudai Ana Uwezo Mdogo wa Mambo ya Kisheria

0
0

Mbunge wa Iringa mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa ameibuka na kumchana Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku na kusema uelewa wake juu ya hoja za Mwanasheria Tundu Lissu ni mdogo sana.

Msigwa amesema haya siku moja baada ya Mbunge Msukuma kudai kuwa yeye anaunga mkono kauli ya serikali kuhusiana na wanasiasa kuchochea sakata la ndege huku akiwatuhumu kuwa wapinzani wanatafuta kiki na kusema ni waongo watupu.

"Msukuma anasukumwa na uelewa Mdogo wa mambo ya kisheria na kimataifa kwa uelewa wake juu ya hoja za Tundu Lissu ni sawa na kobe kushindana na twiga kwa uwezo wa kuona Mbali" alisema Peter Msigwa

Aidhaa Mchungaji Msigwa ameitaka serikali kutoa majibu yanayoridhisha kuhusiana na ndege inayoshikiliwa nchini Canada

"Hoja zilizotolewa na Serikali juu ya kukamatwa kwa ndege yetu huko nchini Canada Bombadier Q 400 zinafedhehesha Taifa na kuondosha weledi na umahiri wa Serikali katika kukabiliana na maswala makubwa ya nchi yetu. Kinachoshangaza Serikali badala ya kujibu hoja kuntu za Mh, Lissu imeendeleza kufanya mazengaombwe yasioleweka kwa watanzania ikisaidiwa na Msukuma mbunge wa Geita. Mpaka sasa Serikali haijatoa majibu ya kuridhisha kuhusiana na sakata hili" alisisitiza Msigwa

Mchungaji Msigwa ameeleza kuwa serikali inapaswa kuja na majibu katika hoja kadhaa ambazo Tundu Lissu aliziibua

"Lissu anawataja wanasheria wa serikali kutowajibika katika kuishauri serikali kinyume na taaluma zao . Watu hawa wamekuwa hawana Masada kwa Serikali wamekuwa wakiingiza mkenge Serikali kila mara na siwashangai kina Prof. Kabudi , Dr. Mwakyembe mithili ya Dr. Benson Banna ambae kila siku amekuwa akiidhalilisha taaluma ya wasomi.

"Serikali mpaka sasa , haijawapa watanzania uhakika ni kwa namna gani mali za watanzania ikiwemo majengo ya balozi zetu zilizopo nje ya nchi zitakuwa salama . Watanzania wanataka majibu yenye uhakika juu ya mali zao kuendelea kunaswa huko nje" alimalizia Peter Msigwa

Ukweli Mchungu...Kinachoendelea Nchini ni Ubaya Kwa Ubaya...Hatuna Budi Kujirekebisha Kabla Mambo Hayajaaribika

0
0

Bila shaka wote tunafahamu ni nani ametufikisha hapa! Jamii zinafanyiana ubaya ubaya. Ubaya unalipwa kwa ubaya!

Nimekuwa nikifuatilia sana mijadala inayiendekea juu ya matukio ya kisiasa na kijamii yanayiendelea nchi hii. Kwa ufupi naweza kusema nchi imepoteza kabisa mshikamano.

Tumekuwa kama familia maadui na mahasimu kiasi kwamba kila familia inaiombea nyingine majanga au ishindwe katika jambo fulani.

Tumefikaje katika hatua hiyo?
Wapinzani na wafuasi wao wamejengewa chuki na serikali iliyopo madarakani. Serikali iliyopo madarakani imewafanyia wawakilishi wao ubaya.......imewabeza, imewafunga, imewadharirisha, imewatukana na kuwanyima haki zao za kikatiba! Wapinzani wamekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yao,kila wanachosema kinabezwa!

Lakini kubwa zaidi na linalouma ni kudhalilishwa na kufanyiwa ukandamizaji wa hali ya juu. Hili limeleta chuki kubwa sana.

Hata sharia ya makosa ya mitandao utekelezaji wake umekuwa wa kibaguzi. Wanaokamatwa ni wale Wanaoukashifu upande fulani. Lakini Lowasa, Mbowe, Lissu, Maalimu Seif wanakashifiwa na kutukanwa sana. Hapo ndipo wafuasi wa niliowataja hapo juu wanaona kumbe sheria zinatungwa kibaguzi kama wakati wa makaburu South Afrika.

Mfuasi wa Tundu Lissu hawezi kuwa tayari kuiunga mkono serikali wakati unamtesa na kumdhalilisha mwakilishi wake. Mfuasi wa Bulaya na Heche anaona uonevu anaofanyiwa mbunge wake,hivyo amejengewa chuki ya hali ya juu sana. Serikali ikishindwa kwake ni furaha.

Serikali ielewe kwamba hivi ndivyo namna magaidi wanavyozaliwa, Boko Haram na Alshabaab ndivyo ilivyoanza, jamii moja kuona inaonewa na nyingine.

Maana yake ni kwamba Serikali imekuwa ikilazimisha mshikamano wakati matendo yake ni kinyume.

Wakati upinzani ukiomba intelijensia za nje kama CIA isaidie kumtafuta Ben Saanane serikali inasema hapana,hapo unategemea wafuasi wa Ben, wafuasi wa upinzani na ndugu wa Ben wanaitafasiri vipi serikali?

Dola ionekane ikitenda haki badala ya kusema tu wananchi waiunge mkono serikali! Binafsi naona kuna mambo serikali inafanya poa, lakini ninapooana wapinzani wananyanyaswa namna hii, najikuta sioni cha kuipongeza serikali, yoote yanakuwa yamemezwa kwenye uonevu

Imeandikwa na  Boban Sunzu

Kubet kumekuwa Kimbilio la Watanzania Vijana Mpaka Wazeee...Mungu Tunusuru na Janga Hili

0
0
Hii michezo ya bahati na sibu sasa imeshika hatamu. Mtanzania haambiliki, hashauriki, wala hasikiliziki linapokuja swala la kubet hasa ligi ya Ulaya inapoanza.

Je hii ni dalili ya kukata tamaa? Hizi nguvu zikiwekwa kwenyw Kilimo na Ujasiliamali hakika tunaweza kutusua. Kama vipi Nchi ianzishe Bahati nasibu ya Taifa kama ile ya Sebodo ili watu washinde baiskeli na zana za kilimo bila kusahau nyumba na viwanja.

Huku tunakoelekea nahisi tumepotea.





Mida ya Kubet

Mcheza Mpira Okwi Ajitapa Kufunga Goli Moja Katika Mchezo wa Kesho

0
0
Okwi Ajitapa Kufunga Gori Moja  Katika  Mchezo wa Kesho
Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi amefunguka kwa kujitapa kuwa kuelekea mechi dhidi ya watani wa jadi Yanga 'Ngao ya Hisani' kesho (Jumatano) atahakikisha anaifunga Yanga japo amepatwa na kitete kusema ni magoli mangap

Okwi ameeleza hayo kupitia mahojiano maalum aliyofanya na klabu yake na kusema hawezi kusema ni magoli mangapi atawapachika 'gongo wazi' Yanga kwa kuwa ni klabu ambayo anaiheshimu.
"Game ya Yanga siku zote haiwagi rahisi kwa upande wowote kwa kuwa ni timu yenye wachezaji wazoefu wengi japo na sisi tunawachezaji wazoefu wengi kama wao, tunategemea mchezo wa kesho utakuwa mzuri pia tunamatumaini tutashinda", alisema Okwi.

Pamoja na hayo, Okwi aliendelea kwa kusema "nitahakikisha timu yangu inashirikiana vizuri na wachezaji wenzangu ili tuweze kutoka na matokeo mazuri katika mchezo huo. Siwezi kusema tutawafunga magoli mangapi kwa kuwa ni timu ambayo ninaiheshimu lakini sisi tutajipanga kuhakikisha tunatoka na matokeo mazuri", alisisitiza Okwi.

Okwi ameanza tambwe hizo ikiwa imebakia siku moja kuchezwa kwa mechi ya watani wa jadi siku ya kesho (Jumatano) ambapo mchezo huo umekuwa ukisubiliwa na watu mbalimbali waweze kujua ni nani siku hiyo ataweza kumfunika mwenzake.





Kweli Maisha Magumu..Huyu Hapa Daktari ‘FEKI’ Aliyewahi Kukamatwa Muhimbili, Adakwa Tena Amana

0
0
Huyu Hapa Daktari ‘feki’ Aliyewahi Kukamatwa Muhimbili, Adakwa  Tena Amana
Mkaazi  wa  jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana.

 Juma alinaswa jana ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.

Kukamatwa kwa Juma  kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari.

Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu  huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.

Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo. Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi  vya Ukimwi (WAVIU),    Shani Mwaruka alikiri kukamatwa kwa  kwa mtuhumiwa huyo.

Alisema, Juma alinaswa baada ya uongozi kupata malalamiko kutoka kwa  watu waliokuwa wakihitaji huduma  katika hospitalini hiyo.

 Alisema tayari hospitali hiyo iliweka mtego imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.

Baadhi ya watu waliodaiwa kuombwa fedha na  daktari huyo feki, wamesema aliahidi kuwatafutia kazi mbalimbali katika hospitali hiyo.

Nae mwananchi aliyekwenda kupata huduma hospitali ya Amana Cecilia alisema  Agosti 9 mwaka huu, kijana  huyo aliwaeleza kuwa kuna kazi  katika hospitali ya Amana na yeye kama daktari bingwa anayefanya kazi hapo anaweza kuwasaidia.

“Alituambia kuwa  fomu zinatolewa katika  hospitali ya muhimbili sh. 150,000 lakini kwakuwa wao ni madakatari atatufanyia kwa sh. 100,000 tu. Tulichanga fedha hiyo na ilifikia 800,000 tukampatia,”alieza Cecilia.

Aliongeza,Juni  19 mwaka huu aliwaita katika hospitali ya Amana ili kufanyiwa usahili lakini hakutokea na simu akawa hapokei.

“Tuliamua kuuliza kwa madakatari kama wanamfahamu lakini hakuna aliyemfahamu ndipo tulipobaini kwamba tumetapeliwa na kuamua kufanya mtego kwa kushirikiana na uongozi uliofanikisha kumnasa  leo ,”alieleza.


Mahakama Nchini India Yapiga Marufuku Talaka ya Kiislamu

0
0
Mahakama Nchini India Yapiga Marufuku Talaka ya Kiislamu
Mahakama ya juu nchini India imeamua kuwa talaka ya mara moja katika dini ya kiislamu ni kinyume na katiba, uamuzi ambao umekuwa ni ushindi mkubwa kwa haki wanawake.
India ni moja ya nchi chache ambapo mwanamume muislamu anaweza kumtaliki mkewe kwa kutamka neno talaq mata tatu.

Uamuzi huo wa mahakama unafutia kesi zilizokuwa zikipinga talaka hiyo.
Kesi hizo ziliwasilishwa mahakamani na wanawake watano waislamu waliokuwa wamepewa talaka kwa njia hiyo pamoja na na makundi mawili ya kutea haki.

Miaka ya hivi karibuni visa vingi vimeibuka ambapo wanaume waislamu huwataliki wake zao kwa kutamka neno talaq mara tatu, kwa njia ya simu au kwa kutuma ujumbe ya sms, kupitia WhatsApp na Skype.

Licha ya njia hiyi ya kutaliki kutumiwa kwa miongo kadha hiajatajwa popote pale kwenye Sharia au Koran

Serikali Yatoa Miezi Mitatu kwa Halmashauri Zote Nchini Kujenga Vyumba vya Upasuaji Kwenye Zahanati na Vituo vya Afya

0
0
Serikali Yatoa Miezi Mitatu kwa Halmashauri Zote Nchini Kujenga Vyumba vya Upasuaji Kwenye Zahanati na Vituo vya Afya
Serikali imetoa miezi mitatu kwa halmashauri zote nchini kujenga vyumba vya upasuaji kwenye zahanati na vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla amesema Rais John Magufuli alishatoa maelekezo kwa nchi nzima kuhakikisha zahanati na vituo vya afya,vinakuwa na huduma za upasuaji.

Dk Kigwangalla pia ametoa mwezi mmoja kwa halmashauri ya Meru wilayani Arumeru, kuhakikisha  imefunga mifumo ya kielektroniki kwenye zahanati na vituo vya afya ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Amesema Serikali haipo tayari kuona mapato yanaendelea kukusanywa kwa kutumia mfumo wa zamani wa kutumia vitabu.

Amesema lazima vituo vya afya na zahanati ziwe na mashine za vipimo vya magonjwa, na upasuaji mdogo lazima ufanyike ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za wilaya na mikoa.

"Serikali ipo katika hatua za kuboresha huduma za afya  hivyo lazima kituo cha afya na zahanati zifanye uchunguzi wa magonjwa na upasuaji," alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Christopher Kazeri, amesema halmashauri yake, imejipanga kutekeleza maelekezo hayo kabla ya Desemba mwaka huu.




IGP Simon Sirro Afunguka Juu ya Miili ya Watu Iliyookotwa Kwenye Viroba Pembezoni mwa Bahari

0
0
IGP Simon Sirro Afunguka Juu ya Miili ya Watu Iliyookotwa Kwenye Viroba Pembezoni mwa Bahari
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amezungumzia suala la kuokotwa miili ya watu kwenye viroba katika fukwe za bahari ya Hindi, na kusema suala hilo tayari lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio Sirro amesema kweli taarifa hizo zimelifikia Jeshi la Polisi, na kwamba tayari miili ipo wenye utambuzi kwa kuchukua vinasaba ili kujua ni raia wa nchi gani, na kisha litatangaza kwa watu walipotelewa na ndugu zao kwenda kuangalia kama ni wao.

Kamanda Siro aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na kwamba watu wanafikiria mauaji hayo yamefanywa na Jeshi la Polisi, wafahamu kwamba wao kama Jeshi la Polisi huwa hawana kificho, kama wamekutana kwenye mapambano wamewaua watu wataweka wazi kuwa wameua, na siyo kwenda kuwatumbukiza baharini.

Roma Mkatoliki Amtetea Mkewe...'Mke Wangu Kupost Instagram Atanipa Staili zote Hajakosea'

0
0
Msanii Roma mkatoliki akihojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo EA Radio amesema aliulizwa ni staili ngapi mkewe amempa, akasema kwa kuwa neno style lina herufi nne basi ni staili nne
Alipoulizwa mkewe hajashtuka alipoona post yake imeenea sana, alisema hakuwa na cha kushtuka kwa kuwa hajakosea

 TAZAMA VIDEO:

BREAKING NEWS: Tundu Lisu Adaiwa Kukamatwa Nje ya Mahakama na Polisi

0
0
BREAKING NEWS: Tundu Lisu Adaiwa Kukamatwa Nje ya Mahakama na Polisi
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu  amedaiwa kukamatwa leo Jumatatu mchana akitokea  Mahakama ya Kisutu.

Mwanasheria  huyo alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi  lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere mahakamani hapo.

Akielezea ilivyokuwa Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likazuiwa  na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police.

Wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Police.

Hatimaye Ester Bulaya Ahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili

0
0
Hatimaye Ester Bulaya Ahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH ) baada ya kufikishwa kwenye hospitali hiyo akitokea Hospitali ya Bugando, Mwanza.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Stephen ilieleza kuwa, Bulaya alifikishwa hospitalini hapo jana usiku. "Tulimpokea jana usiku,"alieleza kwa kifupi.

 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amethibitisha pia kulazwa mbunge huyo MNH,  "amelazwa private, Sewahaji, wodi namba 18," alisema Halima Mdee.


Tayari Kimenuka Ali Kiba Aamua Kujibu Mashambulizi Kwa Kutupa Dongo Hili

0
0
Tayari Kimenuka Ali Kiba Aamua Kujibu Mashambulizi Kwa Kutupa Dongo Hili
Kupitia ukurasa wa Twitter wa mwimbaji wa Bongofleva Alikiba uliandika maneno 12 ikiwa ni ujumbe kwa mtu ambaye anaonesha kumchukia kwa asilimia huku akionesha kutojali.

Alikiba aliandika>>>”I know that you hate me 100% but I give ZERO F**ks  #KingKiba”


Alikiba amefanya hivi siku moja baada ya hasimu wake katika muziki wa bongo kusikika katika moja ya wimbo ambao mashabiki wanahusisha baadhi ya mistari ya msanii huyo kwenda kwa Alikiba, ndipo hapo inasemekana Alikiba ameamua kujibu kwa kusema mfalme abakaki kuwa mfalme siku zote huku ikidaiwa akimfananisha hasimu wake huyo na malkia wake.

>>>”Ukinichukia sikosi hela hivyo kwangu siyo kesi, kunikompea na Sinderela haiwezi kuwa fresh. Simba toka Mbuga ya Tandale naona Swala wana force tuwe salesale, viuno vidogo wanataka pensi ya pepekale si walitaka kiti nimewapa hadi kitanda wakalale.”

Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images