Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

Sumaye Atema Cheche Kuhusu Kuchuliwa Mashamba Yake na Serikali

$
0
0
Sumaye Atema Cheche Kuhusu Kuchuliwa Mashamba Yake na Serikali
 Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema kunyang'anywa mashamba yake si sababu ya yeye kufikiria kurudi CCM.

“Kunyang’anywa mashamba yangu najua ni uamuzi wa juu haunidhoofishi nifikirie  kurudi CCM’’

Sumaye amesema mashamba yaliyofutwa na Serikali yalikuwa yanalipiwa kodi na yalikuwa yanamilikiwa kisheria.

"Wanataka nirudi CCM, mimi sitaki kurudi CCM, kwanini wananilazimisha?  Nilisema sababu za kuondoka huko, waseme wazi sababu za kuyafuta ni za kisiasa tu," amesema Sumaye leo katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.



Kinga ya Kidiplomasia ya Bi Mugabe Yapingwa na Mawakili

$
0
0

Kinga ya Kidiplomasia ya Bi Mugabe Yapingwa na Mawakili
Wakili wa Gabriela Engels, mwanamitindo wa Afrika Kusini ambaye alidaiwa kupigwa na mke wa Mugabe bi Grace Mugabe ameambia BBC kwamba atawasilisha ombi katika mahakama kuu mjini Pretoria kukabiliana na kinga ya kidiplomasia iliopewa bi Mugabe.

Willie Spies aliambia BBC kwamba mawakili wa bi Engels wanakichukulia kisa hicho kama unyanyasaji kwa lengo la kutaka kumjeruhi mteja wao.
Aliongezea kuwa bi Mugabe hafai kupewa kinga hiyo ya kidiplomasia na kwamba serikali ya Afrika Kusini ilikiuka sheria.

''Sheria zetu kuhusu kinga za kidiplomasia ziko wazi. Moja inasema kuwa sheria hiyo haifai kutumiwa iwapo mtu amejeruhiwa na kwamba haifai kutumiwa iwapo uhalifu mbaya umefanyika.Kupiga mtu kwa lengo la kumjeruhi ni uhalifu''.

Anasema kuwa mawakili wa bi Engels wataliangazia ombi hilo mahakamani ili kumpa fursa jaji kuweza kubaini iwapo uamuzi huo ulifaa kuchukuliwa ama iwapo unaweza kutengwa

Ushahidi Waanza Kesi ya Manji .. Apinga Mkojo Wake Kukutwa na Madawa

$
0
0
Ushahidi Waanza Kesi ya Manji .. Apinga Mkojo Wake Kukutwa naMadawa
KESI inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji ya kutuhumiwa na matumizi ya dawa za kulevya leo Ijumaa, Agosti 22, 2017 imeanza kutolewa ushahidi wa vipimo vilivyochunguzwa kwa mkemia mkuu wa serikali na majibu yake huku wakili wake akipinga kielelzo hicho cha mkojo hakikuwa halali.

Ushahidi huo umeanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwa nyakati tofauti shahidi wa kwanza alikuwa Ofisa Mkuu wa Makosa ya Jinai na Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam, Ramadhan Kindai na Askari Polisi Kitengo cha Upelelezi cha Makosa ya Jinai, Christopher.

Wakifafanua mahakamani hapo wameeleza hatua zote walizozifuata tangu Manji aliporipoti Kituo Kikuu cha Polisi, Februari 9 mwaka huu na kupelekwa kwa mkemia kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya mkojo na hatimaye kugundulika anatumia madawa ya kulevya.

Kwa upande wa utetezi, Wakili wa Manji, Hoodson Ndusiepo aliukataa ushahidi wa barua iliyoandikwa ya Manji kupelekwa kwa Mkemia Mkuu ili kuchukuliwa vipimo vya mkojo kwa madai kuwa barua hiyo ilitakiwa kuwa na sahihi ya mteja wake kuridhia akachukuliwe vipimo hivyo.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkeha ameiahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano, Agosti 23

Roma: Mimi si Kada wa CHADEMA na Sijawahi Kuwa Kada wa Chama Chochote

$
0
0

Roma: Mimi si Kada wa CHADEMA na Sijawahi Kuwa Kada wa Chama Chochote
Msanii Roma Mkatoliki ambaye anaimba muziki wa Hip hop kwenye game ya bongo, amekikana chama cha CHADEMA na kusema kuwa hajawahi kuwa mwanachama wa chama hicho kama ambavyo wengi wanaamini, na hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote.


Roma ambaye hivi karibuni alikutwa na sakata la kutekwa na kuibua sintofahamu nyingi, amesema kwamba hajawahi kuwa mwanasiana na hajawahi kuwa na kadi ya chama chochote.

"Mtu akisema nipo kwenye siasa za upinzani siyo jambo sahihi na siyo jambo ambalo nalifurahia kwa sababu mimi sina kadi ya chama chochote, mimi siyo mwanachama wa chama chochote, na mtu akisema nusu ya watanzania wanajua uko CHADEMA sijui ana uthibitisho gani kwa sababu sina kadi ya chama, na mimi nasimama kati kati", alisema Roma Mkatoliki.

Roma hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya wa 'Zimbabwe' ambao umeibua hisia kwa wengii, kwa kuelezea tukio zima la utekwaji wake ulivyokuwa. Wimbo ambao mpaka sasa umeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja na kitu ndani ya wiki moja.

Maneno ya Afande Sele kwa ‘umarioo’ Asema Unapunguza Nguvu za Kiume

$
0
0
Maneno ya Afande Sele kwa  ‘umarioo’ Asema Unapunguza Nguvu za Kiume
Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Afande Sele amedai kuwa vijana wa kiume kujihusisha katika mapenzi na wakubwa zao ili kusaidiwa kiuchumi ni moja wa sabubu zinazopelekea upungufu wa nguvu za kiume.

Afande Sele ameeleza kuwa kitendo hicho kinamnyima uhuru binafsi muhusika kwa sababu unapokaa na mtu ambaye kila kitu unamtengemea unakosa uhuru wa maisha.

“Hata uwezo wako wa kufikiri unapungua kwa sababu unajikuta muda mwingi unafikiria kumfurahisha mtu. Muda mwingine hata mapenzi unakuta hujisikii kwa sababu mapenzi nayo ni ratiba lakini kwa sababu unaishi na mtu anakulea utafanya tu,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.

“Ndio maana leo hii suala la nguvu za kiume limekuwa ni agenda kubwa kwa sababu wanafanya vitu na watu siyo machaguo yao ila wakijiari kwenye vitu kama kilimo watakuwa na maisha ya uhuru sana,” amesisitiza.


Masikini Mwanaume Auwawa kwa Kupigwa Kisa Kuku

$
0
0
Masikini Mwanaume Auwawa kwa Kupigwa Kisa Kuku
Mwanaume mmoja mkazi wa kitongoji cha Busulwa kata ya Ngulla Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ameuawa na kikundi cha watu wasiyojulikana kwa kosa la kuiba kuku watano wa Ester Robert ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ngulla.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, DCP Ahmed Msangi amemtaja mwanaume huyo kuwa ni Leonard Mathias (23) ambapo kabla ya kuuawa alipigwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kuchomwa moto hadi kupoteza maisha na kikundi cha watu wanaojichukulia sheria mkononi mnamo tarehe 21.08.2017 majira ya saa 2:45 asubuhi.
Inasemekana kuwa marehemu aliiba kuku hao nyumbani kwa Bi. Ester kisha kukimbia nao kijiji cha jirani cha Mwabomba ambako huko mwananchi walipomuona walipata mashaka kisha kumkamata na baadaye kutoa taarifa Kijiji cha Ngula ndipo mwenye Kuku alipofika na kukabidhiwa kuku wake.

DCP Msangi amesema mara baada mwenye mali kupokea Kuku wake, wananchi walimchukua na kwenda naye kituo cha Polisi lakini wakiwa njiani walianza kumshambulia kwa kumpiga kwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake na baadae kumchoma moto. Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema ndipo walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo na tukio na kufanikiwa kuwakamata watu saba ambao wanadaiwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.

Jeshi la Polisi linaendelea na mahojiano ya watuhumiwa hao na pindi uchunguzi utakapokamilika kishha ikithibitika kuwa walihusika katika mauaji hayo watafikishwa Mahakamani

Korea Kaskazini Yatishia Kujibu Zoezi la Kijeshi la Marekani

$
0
0
Korea Kaskazini Yatishia Kujibu Zoezi la Kijeshi la Marekani
Korea Kaskazini imetishia kujibu vikali zoezi la pamoja la kijeshi lililofanywa na majeshi ya Korea Kusini pamoja na yale ya Marekani.
Msemaji wa jeshi kutoka Kaskazini alisema kuwa anatazama kwa makini kile ilichokitaja mchezo wa kivita wa Marekani .

Pyongyanga imetishia kurusha makombora katika bahari ya kisiwa cha Guam ambacho kina kambi kubwa ya wanahewa wa Marekani .

Wasiwasi huongezeka wakati wa zoezi hilo la pamoja la kila mwaka, na kwamba hali imezidi kuwa mbaya zaidi baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la masafa marefu linaloweza kushambulia Marekani.
Mwaka uliopita Pyongyang ilijibu zoezi hilo la kijeshi kwa kufanyia majaribio kombora lake.

Masau Bwire Aonekana Kukerwa na Kelele za Mashabiki wa Simba na Yanga Asema Aoni cha Kujifunza Katika Mechi Hiyo

$
0
0
Masau Bwire Aonekana Kukerwa na Kelele za Mashabiki wa Simba na Yanga Asema Aoni cha Kujifunza Katika Mechi Hiyo
Msemaji mkuu wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire ameonekana kukerwa na kelele za mashabiki wa Simba na Yanga huku akidai kuwa timu hizo hazina mpira wa kuvutia zinapokutana.

Masau Bwire amesema inapokaribia pambano la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga watu wanakosa raha mitaani kwa makelele ya mashabiki wao lakini inapofika siku ya pambano uwanjani hakuna chochote wanachokionesha zaidi ya vurugu na utoto.

“Nikuambieni hawa jamaa hawana lolote hasa kama unazungumzia uwanjani, Mimi naona ni mambo ya kitoto tu, gumzo kubwa kila sehemu mtaani hadi hatuna raha inafika siku yenyewe labda tutapata cha kujifunza lakini unakuta ni vurugu na utoto unatawala uwanjani sioni cha kujifunza kwa kweli”,amesema Masau Bwire kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari.
Kauli hiyo ya Masau Bwire imekuja katika kipindi hiki ambacho mashabiki wa Simba na Yanga wanasubiri pambano la mechi ya ngao ya hisani hapo kesho jumatano Tar 23 2017

Balozi Mark Green Awa Kiongozi Mkuu Mpya wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

$
0
0

 Balozi Mark Green Awa Kiongozi Mkuu Mpya wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).
Bunge la Seneti la Marekani limemuidhinisha  Balozi Mark Green kuwa Kiongozi Mkuu mpya wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

Akiwa Kiongozi Mkuu wa USAID, Balozi Green atasimamia taasisi kubwa za  Serikali ya Marekani inayojihusisha na misaada ya maendeleo,  inayoendesha shughuli zake katika zaidi ya nchi 100 kwa lengo la kukabiliana na umasikini uliokithiri na kuzisaidia jamii imara na za kidemokrasia kupata maendeleo kwa kadri ya upeo wa uwezo wao.

Balozi Green anaingia katika wadhifa huu akiwa na hazina kubwa ya uzoefu kutokana na kuwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania.

Pia aliwahi kuwa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Chama cha Republican (International Republican Institute) ambayo imekuwa ikitekeleza programu kadhaa za USAID nchini Tanzania na katika nchi mbalimbali duniani.

Katika kipindi chake akiwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania kuanzia mwaka 2007 hadi 2009, Balozi Green aliwezesha kuwepo kwa ushirikiano rasmi baina ya nchi hizi mbili katika baadhi ya programu kubwa zaidi za maendeleo zilizowahi kufadhiliwa na Marekani.


RCO Awaonya Wachimbaji wa Madini Wanaotumia Mabomu ya Kienyeji

$
0
0

RCO Awaonya Wachimbaji wa Madini  Wanaotumia Mabomu ya Kienyeji
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai wa Mkoa wa Manyara (RCO) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Joshua Mwafulambo amewataka wachimbaji wa madini  wenye mabomu ya kienyeji kuacha tabia hizo.

Amesema hayo akiwa anawatuhumu wachimbaji wa madini ya  Tanzanite wanaojihusisha na utengenezaji wa mabomu hayo akidai kwamba ni hatari kiusalama.

Amesema  endapo kuna mchimbaji anajifahamu kumiliki   mabomu hayo ajisalimishe  mwenyewe kwenye kituo cha polisi Mirerani, kabla hatua kali za kisheria hawajachukuliwa.

Mwafulambo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wamiliki na mameneja wa migodi ya madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


aMwanamke Achoka Kuwa Single Aamua Kupita Barabarani na Bango Akitafuta Mume wa Kumuo

$
0
0
Mwanamke Achoka Kuwa Single Aamua Kupita Barabarani na Bango Akitafuta Mume wa Kumuoa
Mwanamke mmoja nchini Kenya ameingia katika barabara za mji mkuu Nairobi, akiwa na bango lenye maandishi yanayosema kuwa anatafuta mwanamume wa kumuoa.

Akiwa amevaa nguo nyeupe sawa nguo inayovaliwa Bi harusi, Pris Nyambura mwenye umri wa miaka 28, ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, alikuwa na bango lililosema.

"Ninahitaji bwana, nina mtoto msichana wa umri wa miaka saba"

Kauli ya Ayoub Mohamedi kwa Watumishi wa Serikali Wasioendana na Kasi ya Rais Shein Watakiwa Kuacha Kazi

$
0
0
Kauli ya Ayoub Mohamedi kwa Watumishi wa Serikali Wasioendana na Kasi ya Rais Shein Watakiwa Kuacha Kazi
Kauli hiyo ameitoa mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi kisiwani Zanzibar Ayoub Mohamed Mahamoud mbele ya Waandishi wa habari kuwa kwasasa Serikali yake ya mkoa haitaweza kumvumilia mtumishi yeyote ambaye hatatekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa wakati na hivyo kuwataka wajitathmini wenyewe.

"Nataka nieleze, kwa watendaji ambao wanaona hawaendani na kasi yangu na ya Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein waanze kuachia ngazi wenyewe... Hatutaweza kumvumilia mtu yoyote anayekwamisha" Alisema RC Ayoub

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Rais Shein kutoa maagizo 13 kwa mkuu huyo wa mkoa na kuhakikisha yanatekelezwa kwa wakati.

RC Ayoub amesisitiza kuwa kila kinachofanyika kwasasa ni lazima kiende kwa kasi na kwa kiwango cha juu.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa Mkoa ofisi yake sasa inaanza mchakato kutathmini ili kubaini watendaji hao mara moja.

Imefichuka..Mange Kimambi Amlipua Diamond Vibaya...Adai Diamond Karanga si zake na Amezulumu Mwanamke Mjane Gari

$
0
0
Imefichuka..Mange Kimambi Amlipua Diamond Vibaya...Adai Diamond Karanga si zake na Amezulumu Mwanamke Mjane Gari
Malkia wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania mange kimambi amemjia juu diamond platnumz juu ya kumdhulumu mjane malipo ya gari alonunua
Kumbe diamond karanga sio za dai wala perfume sio zake heheee yeye kapiga tangazo tu
Amshutumu pia kwa kukataa watoto
Alichokiandika mange hiki hapa;

"Huyo mkataaa watoto hizo karanga hazimuhusuuuuu kabisaaaaaaa!!!! Yani ni Sawa na anavyofanyaga matangazo ya Vodacom alafu mmeseme vodacom ya kwake.... Hizo karanga za long time kishenziii tena zilikuwa zinauzwa tshs 200, kapewa matangazo basi... Hata perfume pia haimuhusuuuuu, keshapewa chake ila perfume ni ya Kusaga ndo anaepiga hela.....Nawashangaaga sana mnavyomuharakisha Kiba atoe bidhaa zake, ni bora atulie atoe kitu ambacho ni chake sio kunufaisha watu wengine abaki anajigamba kwa bidhaa ambazo hana hata shea kidunchu..

Sio kama namchukia ila ukweli ndo huo.....

Na nimetafutwa na ndugu zake mjane wa Seki yule alikuwa bwanake Lulu akafariki ghafla baada ya kuuwawa na majini ya Lulu, Jamani nataniaaaaaa , wanadai kwamba mkataa watoto kamdhulumu mke wa Seck hiyo X6. Marehemu Seck alimuuzia mkataa watoto hiyo x6 kwenye birthday yake ya 2014 akawa kalipa pesa kidogo mnoooo sasa bahati mbaya Seki akafa ndo mkataa watoto nae kajikausha na deni la marehemu na X6 anaitimba tu, mke wa Seki kamdai hadi kachoka kabaki analia. Embu mwambieni amuoneee huruma mjane wa watu jamani, ajifikirie yeye afe leo alafu Zari na Hamisa wadhulumiwe huku wana watoto wadogo angejisikiaje huko kaburini??? Kweli angeresti in pisi?? "

Haya Hapa Ndio Makosa Mawili Yaliyomwingiza Tundu Lissu Matatani Mpaka Kukamatwa na Polisi Leo.....

$
0
0

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu amehojiwa kwa tuhuma za kufanya makosa mawili;

1. Kumkashifu rais.

2. Uchochezi kuhusu kuzuiliwa na kushikiliwa kwa ndege ya serikali ya bombardier.

Makosa hayo yanadaiwa kufanywa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ijumaa iliyopita, Agosti 18, mwaka huu.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amekataa kutoa maelezo yoyote polisi, akitumia haki yake ya kisheria kuwa mtuhumiwa ana haki, kisheria, kutaja jina na anuani yake tu anapokuwa anashikiliwa na polisi hadi atakapopelekwa mahakamani ambako ndiko atataoa maelezo kujibu mashtaka anayotuhumiwa nayo.

Lissu ambaye ameendelea kuwa imara akiwa tayari kujibu mashtaka yake mahakamani, akiwa polisi amepata msaada wa kisheria kutoka kwa Wakili Faraji Mangula, ambaye pia anashughulikia uwezekano wa mteja wake kupata dhamana kwa mujibu wa sheria.

Chama kimeshatoa maelekezo kwa wanasheria wa chama kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi za kisheria iwapo Jeshi la Polisi halitampeleka mbele ya mahakama Lissu ndani ya muda unaoagizwa na sheria za nchi yetu.

Aidha, chama kinaendelea kusisitiza kuwa serikali bado inao wajibu wa kujibu hoja za msingi zilizotolewa na Chama kupitia tamko lililosomwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama Lissu kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania huko nchini Canada kwa sababu ya deni tunalodaiwa kama nchi la shilingi bil. 87.

Tunaikumbusha serikali kuwa mojawapo ya hoja zilizotolewa na chama katika tamko hilo ni pamoja na;

1. Kwanini Serikali, kupitia kwa Waziri wa Ujenzi wa wakati huo, John Magufuli ilivunja mkataba wa Kampuni ya Stirling Civil Engeering Ltd? Kitendo ambacho kimesababisha nchi yetu kuingizwa hasara kwa kudaiwa mabilioni ya shilingi.

2. Kwanini deni la Stirling Civil Engeering Ltd halikulipwa mara baada ya mahakama ya usuluhishi kutoa tuzo ya dola za Marekani mil. 25, kitendo ambacho kimesababisha deni hilo sasa kufikia dola mil. 38.711?

3. Wananchi wanataka kujua katika kashfa hiyo ambayo ni dhahiri inalitia doa na aibu kubwa taifa letu kuwa halizingatii sheria na taratibu katika uendeshaji wa masuala yake, NANI atawajibika kijinai kwa kulisababishia taifa letu hasara ya bilioni 87?

4. Je serikali hii ya CCM ambayo imekuwa ikijigamba kuwa inao uwezo wa kutumbua majipu, je itaweza kutumbua hilo?

Leo ikiwa ni siku ya tano tangu CHADEMA kilipotoa hadharani tamko hilo kuhusu kashfa hiyo ya kuzuiliwa kwa ndege hiyo ya Bombardier huko Canada, Serikali haijajibu hoja zilizotajwa hapo juu kwa ukamilifu wake. Ni vyema serikali ikatoa hadharani na majibu yenye hoja badala ya kutaka kupindisha kwa kumkamata na kumshtaki Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lissu ambaye alisoma tamko hilo mbele ya viongozi wakuu wa chama kwa niaba ya wanaCHADEMA nchi nzima.

Makene

Mwanaume Mashine, Embu Pitia Hapa Uone Mashine za Kisasa Kwenye Kituo Kipya Cha TV Cha Lemutuz

$
0
0
Mwanaume Mashine, Embu Pitia Hapa Uone Mashine za Kisasa Kwenye Kituo Kipya Cha TV Cha Lemutuz
Wakati yakiwa yamebakia masaa machache kabla ya macho na maskio ya mamilioni ya watanzania kuhamishiwa downtown Bongo kwa tukio kubwa namba mbili mwaka huu ,huku namba moja likiwa lile la usomaji wa ripoti ya mchanga. Mmiliki wa kituo hicho kikubwa cha televisheni amewaonesha mashabiki wake mashine kadhaa alizonunua Marekani na Ulaya zikiwa katika majaribio ya mwisho mwisho.

Baadhi ya mashine za kisasa zilizobahatika kutambulishwa na Lemutuz ni mashine maalum za kuongelea(mics),vifaa vya kukalia (maarufu kama viti),kamera za kisasa kabisa zenye uwezo mkubwa,extension cables zenye urefu usioelezeka,acs pamoja na mashine nyingine ndogondogo kama vifaa vya kunywea chai na super coffee.

Lemutuz amedai ubunifu na kila kitu kwenye studio yake kunaenda kubadilisha jinsi watu wamezoea kupokea habari na uenda ikawa ni revolution itakayodumu kwa miaka 100 ijayo.

Pia Lemutuz ametumia muda huo kuwaomba vijana waliomaliza vyuo vikuu kuanza kutuma maombi ya ajira katika kampuni hiyo kuwa ya utangazaji

By Msaga Sumu

Sikiliza na Download Wimbo wa FID Q na Diamond Ambao Umeibua BEEF la Ali Kiba na Diamond Upya....

$
0
0
Sikiliza na Download Wimbo wa FID Q na Diamond Ambao Umeibua BEEF la Ali Kiba na Diamond Upya....
Sikiliza na Download Wimbo wa FID Q na Diamond Ambao Umeibua BEEF la Ali Kiba na Diamond Upya....

Wanawake Msikubali Kupigwa Picha Wakati wa Kufanya Mapenzi

$
0
0
Wanawake na wadada nawashauri msikubali kupigwa picha na wapenzi au waume zenu wakati wa tendo la ndoa...Hii kitu imekuwa ikitumika kuwarudi na kuwachafulia majina pale mnapoachana...

Anataka picha au video ya nini na wakati mpo nae ikatokea bahati mbaya uhusiano ukavunjika unadhani hizo data anapeleka wapi.

Wanaume wengi wamekua sio wastaarabu kabisa, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii picha nyingi za uchi zinazotumwa ni za wanawake na zimewekwa mtandaoni na waliokuwa watu wenu ambao mlikuwa mnawaamini mwanzo mwisho.....

Kuweni Makini....

Nimevumilia Nimeshindwa, Mpenzi Wangu Amerudi Amelewa na Hana Nguo ya Ndani 'Boxer'

$
0
0

Jamani nasumbuliwa na shemeji yenu ndoa hii ina tabu sana nimevumilia mpaka basi , Jana Mume Wangu karudi nyumbani saa nne usiku amelewa chakari , akajilaza tu kitandani na suti yake , nikaamua nimvue ili alale vizuri , cha kushangaza wadau nikakuta hana Nguo ya Ndani Bukta ama Boxer ambayo alivaa asubuhi baada ya kumpigia pasi....

Sasa nimebaki najiuliza maswali mengi ilikuwaje akaivua na alienda tu kazini na jioni aliniambia anapata moja mbili na marafiki zake?


Bado sijamuuliza nini kilitokea ila naombeni ushauri nifanyaje?

Mapenzi Kikohozi...Je Huyu Ndio Mpenzi Mpya wa Vanessa Mdee?

$
0
0
Mapenzi Kikohozo...Je Huyu Ndio Mpenzi Mpya wa Vanessa Mdee?
Msanii wa kike bongo kwenye game ya bongo fleva anayekimbiza kimataifa Vanessa Mdee, ameonekana kupata mbadala wa aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu Juma Jux, kwa kuanza kumposti mwanaume mwingine huku kukiwa na 'caption' zenye ujumbe wa mahaba.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram siku chache zilizopita Vanessa Mdee alimposti msanii wa Nigeria Run Town na kuandika ujumbe wenye utata kwa hali ya kawaida, huku mwenye we Run Town akijibu kwa kuandika 'Nakupenda babe'.

Lakini pia msanii huyo wa Nigeria alimposti Vanessa Mdee kumtakia heri kwenye siku yake ya kuzaliwa ambayo ilikuwa mwezi wa 6 na Vanessa kujibu kwa ujumbe wa mahaba, na pia Vanessa alimuweka Run Town na kuandika ujumbe mtamu na kisha Runtown kurudisha majibu kwa ujumbe mtamu zaidi wa mahaba.

Hivi karibuni Vanessa Mdee ameweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano yoyote kwa sasa huku akiweka wazi bado ana hisia juu ya mpenzi wake zamani Juma Jux, lakini kwa sasa inaonekana mambo yameenda sawa na kumpata mbadala wake.

Je Ali Kiba Tuendelee Kumuita King of Bongo Flava Au Tumpotezee...? Mwenye Afunguka Haya

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amesema atabaki kuwa mfalme wa muziki hapa Bongo ingawaje anaandamwa na watu aliokataa kuwataja moja moja.


Akitumia lugha ya mafumbo, Alikiba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameoneshwa kukerwa na jambo hilo na kuamua kutema cheche huku akihoji kama walimpa kitanda basi waje wamtandikie alale kabisa.

“The KING ll always Be a KING. je Umeshakitandika nilale MALKIA wangu wa nguvu ??”,ameandika Alikiba pasi kujua ujumbe huo umemulenga nani.

Jana Tarehe 21 Agosti, Rapa Fid Q aliachia remix ya wimbo wake ‘Fresh’ ambao amewashirikisha Diamond Patnumz na Rayvanny, wimbo ambao mashairi ya Diamond yameonekana kuleta utata huku watu wengi wakihusisha kumlenga Alikiba.

  Moja ya mashairi hayo Diamond anasema “Ukinichukia sikosi hela hivyo kwangu sio kesi, Kunicompare na Cinderella haiwezi kuwa fresh” hapa swali linakuja Cindeella ni nani? bila shaka wote mnafahamu wimbo WA Cinderella uliomtoa Alikiba kwenye game.

 Na mashairi mengine ambayo yanahusishwa moja kwa moja na posti ya Alikiba ni pale Diamond Platnumz alivyosema “Si walitaka kiti, nimewapa hadi kitanda wakalale” kwani Alikiba nae ameonekana kukerwa na mistari hiyo na kujibu “je Umeshakitandika nilale MALKIA wangu wa nguvu?”.
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live




Latest Images