Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Bakwata Yatangaza Sikukuu ya EID September Mosi

$
0
0
Bakwata Yatangaza Sikukuu ya EID September Mosi
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeir amesema Septemba Mosi itakuwa ni Sikukuu ya Eid El-Adhaa baada ya mwezi Dhil-Hijjah (mfungo tatu) kuandama Magharibi ya Agosti 22 mwaka huu.

Mufti ameeleza hayo katika mkutano na  wanahabari leo Alhamisi  Agosti 24 katika hotuba yake iliyosomwa na msemaji wake Sheikh Khamis Mataka.

Mkutano huo umefanyika katika makao makuu ya Baraza la  Kuu la Waislam  Tanzania (Bakwata), Kinondoni ambapo Mufti Zubeir amesema baada ya mwezi huo kuandama na Agosti 23 mwaka huu ilikuwa ni sawa na Mwezi Mosi Mfungo Tatu  (Dhul-Hijjah)1438 Hijiriyyah.

"Napenda kuutangazia umma kuwa nimethibitisha mwandamo wa mwezi  na kwamba siku ya Agosti 31 ni siku ya kufunga Sunna ya Araf.Wakati Septemba Mosi ni sikukuu,"amesema Mufti Zubeir kupitia msemaji wake huyo.

Amesema maadhimisho ya sikukuu hiyo kitaifa yatafanyika Dar es Salaam na swala itafanyika katika uwanja wa Garden, nyumba ya Msikiti wa Taqwa uliopo Ilala Bungoni huku Baraza la Eid likifanyikia katika eneo hilo pia.

Kupitia sikukuu hiyo, Mufti Zubeir amewahimiza Waislamu kuzidisha ibada na kufanya kheri katika siku 10 tukufu za mfungo tatu na kuichukua vyema falsafa  ya Hijja katika kudumisha umoja ja mshikamano miongoni mwao.

"Waislamu watumie kipindi hiki cha mwisho  wa mwaka wa Kiislamu kutafakari na kumchamungu na kuimarisha maadili mema ndani ya jamii itakayokuwa bora na ya kupendana,"amesema Mufti Zubeir.



LHRC Walaani Vitendo vya Ukiukwaji wa Haki za Binadamu Vinavyoendelea Nchini.

$
0
0

LHRC Walaani Vitendo vya Ukiukwaji wa Haki za Binadamu Vinavyoendelea Nchini
Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) kimelaani vikali vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoendelea nchini.

Pia wamelaani  kitendo cha Wakala wa barabara nchini (Tanroads) kuidharau mahakama na kuminywa kwa haki za wanasiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Hellen Kijo-Bisimba amesema wameshangazwa na uamuzi wa Tanroads wa kubomoa nyumba za wananchi wa Kimara hadi Kiluvya wakati wanapingamizi la Mahakama.

"Tunalaani kitendo hiki na tunaona ilichofanya Tanroads ni kuidharau Mahakama ambapo kwa lugha ya kisheria tunaita Contempt of Court(kuiingilia Mahakama) "amesema

Mkurugenzi huyo pia amesema wanalaani kitendo cha kukamatwa ovyo kwa wanasiasa na kusema kitendo hicho ni kuminywa kwa haki za kisiasa.

"Hali hii imejitokeza sana kwa kuwanyanyasa wabunge wa vyama vya upinzani bila kufuata misingi ya kisheria na haki za binadamu "amesema

Amesema  ukamatwaji wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya aliyekamatwa akiwa hotelini kwa tuhuma za kutaka kuhudhuria mkutano nje ya jimbo lake na kidai kuwa huo ni ukiukwaji wa haki na kunyimwa uhuru wa vyama vya upinzani kufanya kazi yake.




Maskini Husna Aumbuka na Mimba Bandia

$
0
0
Maskini Husna Aumbuka na Mimba Bandia
MIMBA ya Husna Maulid ilikuwa ya  kughushi.  Imemuumbua baada ya kugundulika kuwa hakuwa nayo, badala yake alikuwa akiweka matambara tumboni kuonesha ana mimba. Kwa  mujibu chanzo makini, Husna hakuwa na mimba, lakini alikuwa akiweka matambara hayo kwa ‘utashi’ wake ili aonekane tu ana ujauzito lakini hakuwahi kuwa nayo.

“Nilikuwa  na MIMBA ya kughushi aliyokuwa akiiweka Video Queen wa Bongo, Husna Maulid imemuumbua baada ya kugundulika kuwa hakuwa nayo, badala yake alikuwa akiweka matambara tumboni kuonesha ana mimba.
ninashangaa sana kwa nini Husna, alikuwa akiweka matambara ili aonekane ana mimba kitu ambacho wengi waliamini hivyo,” kilisema chanzo. Gazeti hili lilimtafuta Husna ili kuzungumzia ishu hiyo ambapo badala ya Husna kujibu hoja, aliangua kicheko na kusema yote ni ya walimwengu. “Daah sijui nizungumzeje hiyo ishu maana yote ni ya walimwengu bwana wee yaache si unajua tena mjini hapa,” alisema Husna.

Malinzi na Wenzake Mambo Bado Magumu Mahakamani

$
0
0
Malinzi na Wenzake Mambo Bado Magumu Mahakamani
KISUTU leo upande wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa maelekezo mahususi kwa upande Serikali kuharakisha upelelezi dhidi ya washitakiwa, kinyume na hapo Mahakama iwasikilize na iwaachiwe huru.

Akiieleza mahakama hiyo wakili wa utetezi, Domician Rwegoshora amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kwamba wanautaka upande wa mashtaka uharakishe upelelezi kwa sababu kesi hiyo haina dhamana, hivyo washtakiwa wakiendelea kukaa ndani wanateseka.

”Naiomba Mahakama itoe maelezo mahususi kwa upande wa mashtaka kwa muda mfupi, au washtakiwa wasikilizwe ikiwezekana Mahakama iwaachie.” alisema Domician.
Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali, Vitalis Piter akaeleza kuwa upelelezi upo katika hatua ya mwisho na muda si mrefu itaanza kusikilizwa.

Naye Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9, mwaka huku akiutaka upande wa Serikali kuharakisha na ikiwezekana katika tarehe hiyo watoe taarifa kuhusu upelelezi ulipofikia.

Kesi Inayomkabili Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent Bado Nzito

$
0
0
Kesi Inayomkabili Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent Bado Nzito
Mahakama ya ya Wilaya ya Arumeru imehairisha kesi inayomkabili mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent, Innocent Moshi hadi Septemba 11 mwaka huu huku Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Desdery Kamugisha akitoa onyo kwa Jamhuri iweze kukamilisha hoja za awali

Akitoa onyo hilo amesema kesi hiyo ilifika Mahakamani hapo tokea Mei 12 mwaka huu na rekodi zinaonyesha upelelezi umekamilika, hivyo endapo hoja za awali hazitasomwa tarehe iliyotajwa ya kusikiliza kesi hiyo, Mahakama itachukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria na haitaahirisha tena.

Akizungumza Mahakamani hapo Wakili wa serikali, Khalili Nuda aliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo ili wakamilishe kuandaa hoja za awali ambazo kwa sasa bado hawajaziandaa. Ambapo kwa upande wake Wakili wa Utetezi Method Kimomogolo ameiomba Mahakama hiyo kuahirishwa kwa mara ya mwisho kwa kesi hiyo.

Awali wakisomewa mashitaka yao Mei 12, mwaka huu na Mwanasheria wa serikali, Rose Sulle alisema Mahakamani hapo kuwa  washtakiwa  hao walitenda makosa hayo Mei 6 mwaka huu, katika eneo la Kwa Morombo jijini Arusha.

Sulle amedai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa wa kwanza anadaiwa  mnamo Mei 6 eneo la kwa Morombo  akiwa mmiliki wa gari aina ya Toyota Rosa lenye namba za usajili T.871 BYS, alimruhusu dereva wake kuendesha gari la abiria  kwenye barabara ya umma bila ya kuwa na leseni ya usafirishaji jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Mwanasheria wa serikali, Sulle amesema katika shitaka la pili Moshi anadaiwa kuruhusu gari hilo kuendeshwa bila kuwa na bima na shitaka la tatu ni kushindwa kuwa na mkataba na dereva wake ambaye kwa sasa ni marehemu Dismas  Gasper.

Mmiliki huyo wa Lucky Vicent alisomewa shitaka la  nne  analodaiwa kuruhusu gari lake kubeba abiria waliozidi uwezo wa gari ambapo abiria 13 walizidi.
Wakili huyo wa serikali akisoma shitaka mwalimu Mkama, alidai kuwa akiwa na nafasi ya Mwalimu Mkuu Msaidizi  na mwandaaaji wa safari hiyo aliruhusu kupakia abiria zaidi ya 13 kwenye gari liliosababisha vifo vya watu 35.

Washitakiwa hao walikana mashitaka yao ambapo washitakiwa hao wapo nje baada ya kukidhi masharti ya dhamana yaliyowataka wawe na wadhamini wawili wenye vitambulisho na kusaini hati ya shilingi  Milioni 15 kwa kila mmoja na kutosafiri nje ya mkoa wa Arusha mpaka kesi hiyo itakapomalizika mahakamani hivyo wakatakiwa kukabidhi hati za kusafiria mahakamani hapo.

Mnamo Mei 6, mwaka huu wanafunzi 32 ,walimu wawili na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent waliofariki kwa ajali eneo la Rhotya ,wakielekea mjini Karatu katika shule ya msingi Tumaini kufanya mtihani wa ujirani mwema.

BAVICHA Waliamsha Dude Waitaka Polisi Imuachie Tundu Lissu Imkamate Ngereja

$
0
0
BAVICHA Waliamsha Dude Waitaka Polisi Imuachie Tundu Lissu Imkamate Ngereja
Baraza la Vijana Chadema wamelitaka jeshi la polisi nchini kumkamata, William Ngeleja kwa kukutwa na mali ya wizi kutoka (Escrow) na kumuachia Tundu Lissu kwa kusaidia kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu ndege ya Tanzania kukamatwa huko nchini Canada.

Akisoma barua aliyoiandika kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Simon Sirro, na Mkurugenzi wa makosa ya upelelezi mbele ya wanahabari  mapema leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi amesema aliyekuwa Waziri wa Nishati na Mdini, Mh. William Ngeleja kupitia pesa alizozirudisha hivi karibuni ni wazi kuwa ni mtuhumiwa ambaye anaweza kutaja wenzake wote kisha wakarudish bilioni 307 ambazo zilichotwa kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.

Katambi amesisitiza kwamba hakuna haja ya kumshikilia Lissu pasipokuwa na sababu za msingi kutokana na mamlaka waliyonayo bali wanapaswa kuhakikisha wanawaweka ndani watuhumiwa waliosababishia serikali hasara ya mabilioni ikiwepo kampuni ya Lugumi pamoja na watu waliogawana pesa za Escrow.

"Kumkamata Mhe. Lissu hakuwezi kufanya ndege yetu iliyokamatwa kurejeshwa nchini kwani yeye amewasaidia watanzania kufahamu nini kinachoendelea. Sisi ni upinzani tunaopinga na kutoa njia elekezi, katika barua yetu tumemtaka IGP amkamate Ngelleja na wenzake watoe bilioni 307 zetu na Lugumi bilioni 38 kisha wakalipie ndege iliyokamkatwa kwa pesa ya bilioni 87 ili iendelee na kazi lakini siyo kusingizia upinzani kwamba wanapotosha au wanafanya uchochezi"

"Tufanye kama jinsi ilivyokuwa kwenye Biblia kwamba yule mfungwa Baraba aliachiwa huru kisha Yesu akasulubiwa, basi na Lissu tumuachilie kwani hana kosa zaidi ya kuzungumza ukweli na Ngelleja aliyekiri hadharani kwa kurudisha pesa za wizi awekwe ndani na asaidiane na jeshi la polisi".

Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo ambaye ni Mwanasheria kitaaluma ameongeza kuwa iwapo jeshi la polisi litashindwa kuwatia nguvuni Mh. Ngeleja na wenzake wao wenyewe watafanya kazi hiyo kwa kutumia sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya 2002 ijulikanayo kama "Arrest by private person'.

Aidha Katambi amesema kuwa kupitia barua hiyo wasipopata majibu  yao watafanya maandamano ya amani nchi nzima ili kuweza kushinikiza haki za kisheria, kiuchumi na kisiasa nazo zifuatwe huku wakiwafundisha vijana namna ya kudai haki zao za msingi.

Maneno ya Haji Manara Baada ya Kuwafunga Watani Wao wa Jadi Yanga

$
0
0
Maneno ya Haji Manara Baada ya Kuwafunga Watani Wao wa Jadi Yanga
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa ushindi wao walioupata dhidi ya Yanga SC katika mtanange wa Ngao ya Jamii unatokana na ubora wa kikosi walicho nacho msimu.

Manara amesema, “Timu bora siku zote inashinda haijalishi ni katika mazingira gani lazima ipate ushindi na mipango yetu ilikuwa ni kupata magoli matano kwa mazingira yoyote yale iwe ni penati ama ndani ya dakika 90 ilikuwa lazima yapatikane hivyo tunashukuru ni mwanzo mzuri wa ligi.”

Ameongeza, “Mara ya mwisho niliwaambia Yanga kama waamuzi wakichezesha kwa haki hawatatufunga kokote mechi zote walizoshinda walikuwa wakibebwa kwa hiyo nawaomba shirikisho lampira wa miguu Tanzania (TFF) waendelee kupanga waamuzi bora hata huyu waleo alikuwa na mapungufu lakini ya kwake ni ya kibinadamu kila mtu ameyaona kwa pande zote mbili.”

“Kesho kikosi chetu kitapumzika ila tutaingia kambini jioni kwaajili ya mechi yetu ya Jumamozi dhidi ya Ruvu Shooting tunawashukuru sana wachezaji wetu wamefanya kazi kubwa sana lakini pia wengi bado wapya hivyo mwalimu ataendelea kuiboresha zaidi,” amesema Haji Manara.

Ongeza Hips, Makalio na Mapaja, Kuwa Mweupe na Softi Kwa Kutumia Product za Markson Beauty

$
0
0
MAMBO HAYOOOO!! ONGEZA HIPS, MAKALIO NA MAPAJA, KUWA MWEUPE NA SOFTI, ONGEZA MAUMBILE YA KIUME, NGUVU NA HAMU YA TENDO N.K
      Markson BeautyTunakuletea bidhaa bora zenye matokeo ya uhakika na haraka zisizo na kemikali wala madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa kiafya.
             NB. Matokeo ni uhakika na garantii na risiti

          BIDHAA ZETU:-
 
1.Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @130,000/=
2.Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge  @180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @170,000/=
3.Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:-
(1)Mafuta  @130,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a)SHARK POWER gely ya kupaka (Inaongeza inch 6-7) @150,000/=
(b)Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
(C)HANDSOME UP ORIGINAL- kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo @250,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150,000/=
7.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula  @130,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @130,000/=
(b)Mkanda wa kawaida @120,000/=
(c)Micro-computer belt wa umeme @200,000/=
9.Kupunguza  maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @130,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @130,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @120,000/=
12.Kurudisha usichana  (bikra) @120,000/=
        Wasiliana nasi :- (+255)
             0767447444 au.      
                0714335378
m
  TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
 Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ...............
     Follow us on instagram  @Markson_beauty_pr

Steve Nyerere Awakanya Vikali Ali Kiba na Diamond...Adai Wamegusa Pabaya....

$
0
0
Msanii wa filamu Bongo, Steve Nyerere ametoa ushauri kwa kile kinachoendelea kati ya Diamond Platnumz, Alikiba na Ommy Dimpoz kwenye mitandao ya kijamii.

Wasanii hawa wa Bongo Flava wamekuwa wakitupiana maneno yenye mafumbo katika mitandao ya kijamii tangu Diamond aliposhirikishwa katika remix ya ngoma ya Fid Q ‘Fresh’ ambayo ilitoka hiyo juzi na kudaiwa kuna maishairi ya Diamond yalimlenga Alikiba.

Kupitia mtandao wa Instagram Steve Nyerere amewataka wasanii hao kumaliza tofauti zao kwa kuzingatia hatua ambayo wamefikia kwa sasa hasa pale Ommy Dimpoz alipoweka picha Instagram akiwa na mama mzazi wa Diamond na kuandika ujumbe wenye utata.

NIMEKAA NIMEJIFIKIRIA NIMEONA NISEME KIDOGO, DUNIA MAMA ANA HESHIMA YAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE, MAMA NI KIOO CHA FAMILY MAMA NI NGUZO YA FAMILY MAMA NI KIMBILIO LA FAMILY , TUNAWEZA KUKOSEA KOTE LAKINI SI KWA MAMA NDOMANA AMNA LAANA YA BABA ILA LANA YA MAMA IPO NA INAFANYA KAZI HARAKA KULIKO KITU CHOCHOTE, SIZANI KAMA TUNA ELIMISHA JAMII KUPITIA MATUSI YA KUZALILISHA WAZAZI, NYINYI NI KIOO CHA JAMII, LAZIMA MUWE NA KIFUA CHA KUBAKISHA MANENO , MIMI NILIZANI HIZI NGUVU MNAZOTUMIA MNGEWEKEZA KWENYE MZIKI WENU TUNGEFIKA MBALI SANA , MMEJIJENGEA HESHIMA NA MMELITAFUTA JINA KWA SHIDA , ILA MNASAHAU JINA HILO LINAWEZA POTEA KWA SEKUNDE, NAWASHAULI NA NAKUSHAULI WEWE UNAYEZARAU WAZAZI FUTA KAULI NA OMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI ZAKO USUSANI KINA MAMA WOTE AMBAO NAAMINI NI MASHABIKI WAKO NA NDIO WALIOKUFANYA UKAFIKA HAPO, HATUKATAI NYINYI NI BINADAMU INAWEZEKANA MMEPISHANA KAULI ILA KWENYE KUPISHANA WEKENI AKIBA YA MANENO, KUNA KESHO HUJUI ATAKAYE KUSTILI, HAKIKA BUSARA ITUMIKE , YANI NINGEKUWA MIMI NDIO UMEMGUSA RITA WANGU IVO DOOOO, MJINGA HAJIBIWI, KICHAA HAKIMBIZWI , MWIZI SI RAFIKI, NANI KAMA MAMA, ESHIMA ITAWALE ASANTE BY #####UZALENDO KWANZA,

Zitto: Sasa Mlitaka Lissu Akahoji Matumizi Mabaya ya Rais Chooni, Shimoni au Chumbani au Kazi ya Mbunge ni Nini?

$
0
0
Zitto: Sasa Mlitaka Lissu Akahoji Matumizi Mabaya ya Rais Chooni, Shimoni au Chumbani au Kazi ya Mbunge ni Nini?
Ziito Kabwe Kupitia Facebook Ameandika:

Bei ya Ndege moja aina ya Bombadier Q400 ambazo Tanzania ina/menunua ni USD 31m. Deni tunalodaiwa pamoja na riba ambalo Serikali imekiri na kuahidi kulipa ni USD 37m.

Hivyo Serikali yetu ingeweza kununua Ndege nyengine mpya iwapo ingeshughulikia vema kesi ya kampuni iliyoshikilia Ndege yetu. Hasara za namna hii ndio hurudisha nyuma Serikali za Afrika kwenye juhudi za Maendeleo.

Jambo la kushangaza ni pale Mbunge mwenye mamlaka ya Kikatiba kuihoji Serikali anapotimiza wajibu wake anakamatwa na kushtakiwa Kwa ' kutaja makosa ya Rais hadharani '. Sasa Mbunge ataje makosa ya Rais chooni? Chumbani? Shimoni? Mbunge wa Upinzani ni lazima ataje HADHARANI makosa ya Kiongozi wa Serikali ya Chama kinachoongoza dola.

Kazi ya Upinzani ni kuhoji. Ni kazi ya kimantiki na ya kikatiba.

Haya Ndiyo Maswali 22 ya DC Hai kwa Walimu Yaliyopelekea Mwalimu Kuwekwa Selo

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa

Kwa ufupi
Tukio hilo la Byakanwa kudaiwa kuamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu mwalimu huo wa Shule ya Sekondari Lerai, Erasto Mhagama, ndilo limekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Moshi. Wakati sakata la Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa kumsweka mahabusu mwalimu wa sekondari kwa kushindwa kutaja jina lake likiendelea kuzua mjadala, imedaiwa kuwa siku hiyo aliwauliza walimu aliokuwa na kikao nao maswali 22.

Tukio hilo la Byakanwa kudaiwa kuamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu mwalimu huo wa Shule ya Sekondari Lerai, Erasto Mhagama, ndilo limekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Mbali na kubamba mitandao ya kijamii, walimu katika mijumuiko mbalimbali na kupitia Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na makundi ya WhatsApp ya walimu, tukio hilo ndilo linalojadiliwa zaidi katika mitandao hiyo.

Inadaiwa baada ya mwalimu huyo kushindwa kuandika jina la mkuu wa wilaya, kiongozi huyo alimtaka achague mojawapo ya adhabu kati ya kupiga pushup au kwenda mahabusu ya polisi.

Mwalimu huyo alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa asingeweza kupiga pushup kwa kuwa ana matatizo ya kiafya, ndipo mkuu wa wilaya alipoita polisi na kumpeleka mahabusu.

Hata hivyo, Byakanwa alikaririwa na gazeti hili akisema hakuamuru kuwekwa mahabusu kwa mwalimu huyo kwa sababu ya kushindwa kutaja jina lake, bali kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Lakini mkanda wa sauti ambao ulirekodiwa kwa kutumia simu ya mkononi siku hiyo ambao gazeti hili umeusikia unamkariri kiongozi huyo akiwauliza walimu hao maswali 22.

Hata hivyo, Byakanwa alipoulizwa jana kuhusu kuwauliza walimu maswali hayo, hakukanusha wala kuthibitisha akitaka wanahabari wajiridhishe kama sauti ni ya kwake.

“Nyinyi kama vyombo vya habari mjiridhishe kama sauti ni ya DC maana mimi sijampa mwandishi yoyote sauti iliyorekodiwa ya hiyo siku,” alisema.

Byakanwa aliwataka waandishi wa habari wavute subira kwani atazungumzia tukio hilo na mengine yaliyojitokeza katika ziara yake atakapomaliza kutembelea shule zote za wilaya yake.

Ilielezwa kuwa katika kikao hicho na walimu wa shule mbili za sekondari Boma na Lerai, mkuu huyo wa wilaya alianza kwa kugawa karatasi na kuwauliza walimu kama kuna anayemfahamu.

Alipowauliza swali hilo walimu wa Shule ya Lerai, ni mmoja tu aliyesema anamfahamu ndipo alipowataka wengine wote kuandika jina lake kwenye karatasi.

Baadaye alimsimamisha mwalimu mmoja baada ya mwingine akitaka waende ubaoni kuandika maneno au kuweka majibu ya maswali atakayowauliza na maswali hayo yalikuwa kama ifuatayo:

Maswali 22

1.Nani ambaye ananifahamu?

2. Kila mmoja aaandike jina langu kwenye hiyo karatasi

3. Waziri mkuu wa awamu ya tatu ni nani?

4. Nitajie kirefu cha CDF (Chief of Defence Forces)

5. Nitajie Waziri wa Nishati na Madini

6. Andika kirefu cha DC (District Commissioner)

7. Andika neno IGP na kirefu chake

8. Andika neno CDF na kirefu chake

9. Andika CUF na kirefu chake

10. Andika CAF na kirefu chake

11. Andika neno Tanu na kirefu chake.

12. Andika TLP na kirefu chake

13. Agronomy means what?

14. Nani ni viongozi wakuu wa CUF. Baada ya kujibiwa ni Profesa Ibrahim Lipumba na Maalim Seif Sharifu Hamad akauliza mkutano wao mkuu wa mwisho ulikuwa lini?

15. Nani ni kiongozi wa CAF (Confederation of African Football)

16. Nitajie IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) ni nani na CDF (mkuu wa majeshi) ni nani kwa majina

17. Mwenye cheo cha CDF ni nani

18. Mwamunyange mnamfahamu? Ni Nani

19. Baada ya kustaafu Mwamunyange akaja nani?

20. Mkuu wa Majeshi kwa Kiingereza anaitwaje?

21. Rais wa CAF ni nani?

22. Andika pale ubaoni Chief of Defence Forces

Dar Yabainika Kuwa Kinara wa Matusi, Mwanza Wizi

$
0
0
Dar Yabainika Kuwa Kinara wa Matusi, Mwanza Wizi
 Imebainika kwamba pamoja na uwepo wa sheria ya makosa ya mtandao lugha ya matusi imeendelea kutumika huku mkoa wa Dar es Salaam ukiwa kinara.

Pia Mkoa wa Mwanza nao umebainika kuwa kinara kwa upande wa  makosa ya wizi fedha mtandaoni ukilinganisha na mikoa mingine.

Takwimu zilizotolewa na jeshi la polisi zimeonyesha kuwa jumla ya matukio 327 ya matusi mtandaoni  yameripotiwa kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu.

Msemaji wa Jeshi hilo ACP Barnaba Mwakalukwa amesema matukio mengi ya makosa ya  matusi yanatokea wilaya ya Temeke.

Hata hivyo Mwakalukwa amesema takwimu hizo inaonyesha kupungua ikilinganishwa na mwaka jana ambapo matukio kama hayo 911 yaliripotiwa na wilaya ya  Kinondoni iliongoza.

"Jumla ya matukio 1663 ya wizi wa fedha kwa njia ya mtandao zimeripotiwa huku mkoa wa Mwanza ukionekana kuwa kinara ikifuatiwa na Ilala na Kinondoni.

"Unaweza kuuliza kwa nini Mwanza, ule mji umekua kuna wafanyabiashara wakubwa, wahalifu nao wanabuni mbinu mpya," amesema

Amesema jumla ya watuhumiwa 315 walikamatwa kuhusiana na makosa ya uhalifu mtandaoni na kesi 153 zimefikishwa mahakamani.

Kati ya kesi hizo wahusika katika kesi 19 walikutwa na hatia na nyingine zipo chini ya upelelezi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi  Zanzibar  Hamza Hassan amesema ipo haja ya kuendelewa kutolewa elimu kuhusu sheria ya mtandao ili kupunguza vitendo vya ukiukwaji maadili.

"Unaweza kufanya jambo leo mtandaoni halafu athari zake zikaanza kuonekana baada ya miaka kadhaa, tuitumie vyema mitandao na elimu zaidi itolewe,"

Hassan akiwa na kamati yake wametembelea Mamlaka ya Mawasiliano TCRA na kupewa semina kuhusu sheria ya makosa ya mtandao.

       


Tanzania Kujengwa Maabara ya kisasa ya Afrika

$
0
0
Tanzania Kujengwa Maabara ya kisasa ya Afrika
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara ya Teknolojia ya Nyuklia kwenye Tume ya Nguvu za Atomiki nchini (TAEC) Arusha, maaabara ambayo inatarajiwa kuwa ya kisasa kwa vifaa Afrika.

Akizungumza na viongozi mbali mbali wa mkoa huo na watumishi wa taasisi hiyo, Waziri Ndalichako amesema maabara hiyo ni ya watanzania na hivyo watumishi wanaofanya kazi katika tume hiyo  wasifanye kazi kwa ubinafsi na badala yake watangulize maslahi ya Taifa mbele.

Majengo ya maabara hiyo ya kisasa yanatarajiwa kukamilika Februari Mwaka 2018 ambapo yatagharimu kiasi cha shilingi   Bilioni 2.3, na ikikamilika Umoja wa Ulaya itafunga vifaa vyenye thamani ya Sh. Bilioni 11 ambapo  tayari baadhi ya vifaa vya Sh. Bilioni 2.6 vimekwishawasili nchini.

Pia Waziri na viongozi wengine wa Wizara wametembela Chuo cha Veta sehemu ya kuzalishia umeme kikuletwa pamoja na Chuo cha Ualimu Elimu Maalumu Patandi, kwa lengo la kukagua miundombinu ya chuo hicho pamoja kujionea vifaa vya kufundishia wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Viongozi wengine ambao waliambatana na waziri kwenye ziara hiyo ni pamoja na Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Mhandisi Stella Manyanya na Naibu Katibu Mkuu, Profesa Saimon Msanjila

MSIGWA: Pole Pole Hana Uwezo wa Kumuondoa Kwenye Jimbo la Iringa

$
0
0
MSIGWA: Pole Pole Hana Uwezo wa Kumuondoa Kwenye Jimbo la Iringa
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa ameibuka na kumjibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na kumwambia kuwa hana uwezo wa kumuondoa kwenye jimbo la Iringa Mjini 2020 kama alivyoahidi.

Mchungaji Msingwa amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumtaka Humphrey PolePole kuwauliza wenzake ambao walimtangulia katika nafasi yake hiyo ya Uenezi kuwa watampa majibu.

"PolePole huna uwezo huo waulize wenzio waliokutangulia , mimi sijateuliwa kama wewe" alisema Mchungaji Msingwa

Siku mbili zilizopita Mchungaji Msigwa alisema kitendo cha Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma kusema anamkumbuka Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye ni ishara kuwa Humphery PolePole ameshindwa kuvaa vizuri kiatu alichoachiwa kama Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ndipo hapo PolePole alipokuja na kumwambia Msigwa kuwa huu ni wakati wake wa mwisho kama Mbunge wa Iringa Mjini.

"Kitu kimoja nakuahidi, hii ni 'term' yako ya mwisho, tunakurudisha kufanya kazi ya Uchungaji maana naona Mchungaji anajichanganya na mbuzi" alisema Humphery PolePole
Hata hivyo siku moja baada ya ahadi ya Humphery PolePole madiwani watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Iringa Mjini walitangaza kujiuzulu nafasi zao kwa kile walichodai kuwa viongozi wa juu wa chama hicho Iringa wamekuwa wakiwatenga na kuwatuhumu kuwa ni wasaliti, hivyo wameamua kujiuzulu nafasi zao kama madiwani.

Kesi Inayomkabili Scopion Shashindwa Kuendelea Leo

$
0
0
Kesi Inayomkabili Scopion Shashindwa Kuendelea Leo
Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete (31) maarufu kama Scorpion, imeshindwa kuendelea baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo Flora Haule kuwa na udhuru.

Kesi hiyo inayoendeshwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ilipaswa kuendelea leo Agosti 24 kwa upande wa utetezi kutoa ushahidi wao katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya msingi.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga ameiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja leo kwa ajili ya upande wa utetezi kutoa ushahidi wao katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya msingi, lakini Hakimu anayesikiliza shauri hilo amepata udhuru hivyo, hivyo aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mkazi Adelf Sachore ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuendelea.


Dereva wa Daladala Aiyesababisha Ajari Mkoani Morogoro Akamatwa

$
0
0
Dereva wa Daladala Aiyesababisha Ajari Mkoani Morogoro Akamatwa
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia dereva wa basi lenye namba za usajili T 438 ADR Charles Diamond, kwa kusababisha ajali iliyopoteza uhai wa watu mkoani Morogoro na kusababisha majeraha kwa baadhi ya watu.


Akitoa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Kamanda wa Polisi mkoani humo Urlich Matei, amesema mpaka sasa idadi kamili ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo ni watu watatu, ambapo wawili ni wanawake na mmoja ni mwanaume, huku mmoja wao akiwa ni mwanafunzi.

Majeruhi wa ajali hiyo ni 27 ambao wamepelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, lakini suala la utambuzi wa miili ya marehemu bado halijafanyika mpaka pale uchunguzi utakapofanyika.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi iliyohusisha gari aina ya daladala ikielekea Mvumi kugonga treni iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, kulikopelekea kuburuzwa kwa gari hiyo na kusababisha vifo.


Niwe Mkweli: Katika ile Orodha ya Wana CCM 40 Waliotaka Urais 2015 Simwoni wa Kumzidi Magufuli

$
0
0
Baada ya kuushuhudia uongozi wa Dr Magufuli kama mkuu wa nchi kwa takribani miaka miwili sasa nimeridhishwa kabisa na utendaji wake.

Kwa hakika nikiwaangalia wale wengine waliochukua form, na hasa wale walioingia 5 bora simwoni yeyote ambaye angeweza kuleta mageuzi ya kimaendeleo tunayoyaona sasa. Na kwa wale wagombea vijana ndio hawajulikani kabisa walipo ingawa naambiwa vijana wale wote walipewa uwaziri.

Kiukweli sitegemei kuwaona tena vijana hawa 2020 sanasana tunategemea kuwaona kina Makonda, Polepole, Mavunde na the like hapo 2025. Kwa ule upande wa pili nadhani Zitto na Kitila wanaweza kuwakilisha muungano wa upinzani maana walau hawa sasa wana kauzoefu ka kuwemo serikalini. Ahsante!

By Martin George/Jamii Forums

Bombardier iliyokamatwa Canada Yamuibua Dr Slaa Mafichoni, Ampinga Tundu Lissu

$
0
0
Bombardier iliyokamatwa Canada Yamuibua Dr Slaa Mafichoni, Ampinga Tundu Lissu
ALIYEKUWA Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, ameibuka na kudai kwamba kampuni ya ujenzi inayotajwa kuishikilia ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-Dash 8, ilikwishatuhumiwa kwa uzembe bungeni.

Kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd, ndiyo, kwa mujibu wa maelezo ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, imeishikilia ndege hiyo iliyonunuliwa na Tanzania nchini Canada. Uamuzi huo wa kuishikilia unatajwa kuwa ni utekelezaji wa matakwa ya Mahakam a ya Kimataifa ya Usuluhishi, kuiwezesha kampuni hiyo kulipwa deni lake la dhidi ya serikali ya Tanzania la dola za Marekani milioni 38.7 ambazo ni takriban shilingi bilioni 87.

Msingi wa deni hilo ni kuvunjwa kwa mkataba wa kati ya serikali na kampuni hiyo wa ujenzi wa barabara kutoka eneo la Wazo Hill jijini Dar es Salaam hadi Bagamoyo, mkoani Pwani.

Akizungumzia kadhia hiyo Dk. Slaa alisema pamoja na hali hiyo, kampuni ya ujenzi ya Stirling si “nadhifu” katika kazi zake na hata wabunge walikwishailalamikia bungeni mwaka 2005, akisisitiza kuwa, yeye ni kati ya wabunge waliopata kuilalamikia kampuni hiyo.

Katika mawasiliano yake na gazeti hili, Dk. Slaa aliyepata kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 alisema; “Siamini kama serikali huwa inavunja mikataba ovyo. Kauli hiyo ni vema ikathibitishwa kwa ushahidi na hasa kuonyesha ni vipengele vipi vya mkataba vimevunjwa au sheria ipi imekiukwa. Si vema kutoa kauli za jumla jumla bila uthibitisho.

Kauli hiyo ya Slaa inapingana na madai ya Lissu ya hivi karibuni kwamba mkataba kati ya serikali na kampuni hiyo ulivunjwa ovyo, kinyume cha utaratibu na ndio maana, kampuni hiyo imekwenda kushitaki katika Mahakama ya Kimataifa na kushinda kesi.

Slaa anaeleza zaidi; “Kama ni suala la kushikiliwa Bombardier ninachokumbuka ni kuwa kampuni husika ilishindwa kumaliza ujenzi wa barabara hiyo (Wazo Hill hadi Bagamoyo) katika muda uliotajwa ndani ya mkataba.”

Alieleza kwamba hata sehemu ambayo kampuni hiyo ilikamilisha kipande cha ujenzi wa barabara, basi, ujenzi huo ulikuwa chini ya kiwango na pale kampuni hiyo ilipopewa muda kurekebisha udhaifu huo ilishindwa kufanya hivyo.

“Bungeni tulipiga sana kelele kuhusu ucheleweshaji huo na kazi isiyoridhisha. Nilikuwa Mbunge wa Karatu wakati huo na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kumbukumbu ziko kwenye hansard, tatizo watu hawapendi kufanya utafiti,” alisema Slaa.

Akizungumzia suala la Tanzania kushindwa kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa, Dk. Slaa alisema; “..hiyo haina maana ya kuwa kampuni hiyo ilikuwa “absolutely” na haki. Mahakama zinategemea zimeelekea wapi hasa hizi za biashara ya kimataifa ambazo kimsingi zinalinda maslahi ya nchi zao. Hili nililizungumzia sana bungeni hasa kutokana na uzoefu wangu katika Bunge la ACP/EU – Joint Assembly ambalo nilikuwa nikiwalisha Bunge la Tanzania mwaka 1996 hadi 2000 .Tuliitaka serikali yetu ichukue hatua bahati mbaya haikuchukua hatua.”

Madai ya Lissu

Agosti 18, mwaka huu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alifichua suala hilo la ndege ya Tanzania kuzuiwa na kampuni hiyo ya ujenzi ya Stirling.

Katika mkutano wake huo Lissu alisema ndege hiyo imeshindwa kuletwa nchini Julai mwaka huu kama ilivyopangwa kutokana na kuzuiwa nchini Canada kwa kuwa serikali inadaiwa fidia na kampuni hiyo.

Akifafanua alisema kutowasili kwa ndege hiyo kama ilivyopangwa licha ya kukamilika kutengenezwa nchini Canada kunatokana na uamuzi wa aliyekuwa waziri wa ujenzi, kwa wakati huo, kuvunja mkataba kati ya serikali na kampuni hiyo bila kufuata utaratibu na kisha kampuni hiyo kufungua kesi Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi.

Kampuni hiyo ilifungua kesi hiyo mwaka 2009 ikidai kukiukwa kwa mkataba na ilipofika Juni 2010 mahakama hiyo ya kimataifa ilitoa tuzo ya ushindi kwa kampouni hiyo ikiitaka serikali ya Tanzania ilipe fidia ya dola za Marekani milioni 25, na deni hilo likiwekewa riba ya asilimia nane.

Lissu aliwaambia waandishi wa habari aliokuatana nao kwamba serikali ilikataa kulipa fidia hiyo hadi Juni 30 mwaka huu wakati mahakama ya kimataifa ilipotoa kibali kwa kampuni hiyo kukamata mali zote za Tanzania zitakazokuwa katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada.

Athari kwa uchumi

Kama uamuzi huo utatekelezwa kwa kulipa fedha hizo kwa mdai huyo, ni dhahiri kwamba bajeti iliyoipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaathirika, kwa kuwa fedha hizo hazikuwa zimetengwa kwa ajili ya malipo hayo bali shughuli nyingine za kijamii na hata ulipaji madeni mengine, yakiwamo ya ndani.

Baadhi ya watumishi waandamizi serikalini waliozungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini wamedai kuwa shughuli za baadhi ya wizara au idara za serikali zitaathirika moja kwa moja wakihofia hata baadhi ya miradi ya maendeleo kuweza kuathirika pia.

“Ndege ya Bombadier ni sehemu ya alama za Rais Magufuli tangu aingie madarakani, yeye ndiye amenunua ndege hizo na hii kampuni ‘imemshika pabaya’. Kwa vyovyote vile ni lazima fedha hizo zitalipwa iwe kwa awamu ama vyovyote kama uamuzi wa mahakama hautatenguliwa. Magufuli hawezi kukubali kuona alama ya uongozi wake (ununuzi wa bombardier) inavurugwa,” alisema mmoja wa viongozi waandamizi serikalini.

Mmoja wa wakurugenzi wa halmashauri nchini katika mazungumzo yake na gazeti hili alieleza kwamba kati ya mafungu ya kibajeti yanayoweza kuathiriwa na deni hilo kama litapaswa kulipwa ni pamoja na mafungu ya “matumizi mengine” maarufu kama OC na hata baadhi ya miradi isiyotoa matokeo ya haraka “kisiasa”.

Msimamo wa serikali

Tayari serikali kupitia kwa naibu msemaji wake mkuu, Zamaradi Kawawa, imekwishazungumzia suala hili na licha ya kukiri kuzuiwa kwa ndege hiyo, ilisisitiza kwamba ufumbuzi wa kadhia hiyo unasakwa.

Akizungumza na waandishi wa habari siku moja mara baada ya Lissu kuzungumzia suala hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari, Zamaradi alisema serikali inatafuta suluhu ya suala hilo lakini kwa upande mwingine, aliwalaumu baadhi ya wanasiasa kwa kushirikiana na kampuni ya Stirling ili kampuni hiyo ifanikiwe kukamata mali za Tanzania.

Hata hivyo, licha ya kuwalaumu wanasiasa, Zamaradi hakutaja majina ya wanasiasa hao.

Tayari Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, ambaye ndiye aliyekuwa mwanasiasa wa kwanza kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuhusu ahadi ya serikali ya kuileta ndege ya bombardier mwezi uliopita kushindwa kutekelezeka, amezungumzia hali hiyo ya serikali kutuhumu wanasiasa wa upinzani kuhujumu taifa, akisema kazi ya wanasiasa hao wa upinzani ni “kuinyoosha” serikali pale inapokosea kiasi cha kuhatarisha masilahi ya umma.

Jackline Wolper Afunguka 'Nipo Tayari Kwenda Jela Aisee Ukinitukania Wazazi Wangu'

$
0
0
Jackline Wolper Afunguka 'Nipo Tayari Kwenda Jela Aisee Ukinitukania Wazazi Wangu'
Msanii wa filamu za bongo ambaye kwa sasa ni mjasiriamali mkubwa, Jackline Wolper, amekula kiapo cha kwenda jela iwapo mtu yeyote atamtolea maneno machafu mzazi wake.

Akizungumza na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Wolper amesema yeye kwa kawaida ni mpole lakini iwapo mtu atafanya kitu kibaya juu ya familia yake, hatofikiria mara mbili kumfanya kitu ambacho kitamsababishia kupelekwa jela.

Kwa mimi binafsi Jackline Wolper ni mpole, lakini ukija kwenye issue za wazazi mi nitaenda Segerea, ndiyo maana hujawahi kusikia Jackline Wolper kamuweka mama yake au baba yake kwenye instagram, kwenye Tv, yani sitaki wazazi wangu wahusike, nitukane mimi usitukane damu yangu, au usitukane mtu aliyenileta duniani, yani dakika sifuri nitapelekwa tu jela”, alisema Jackline Wolper.

Kumekuwa na tabia ya watu kwenye mitandao ya kijamii kutoleana maneno machafu mpaka kuwajumlisha na wazazi wa watu hao, kitu ambacho si kizuri kwenye jamii, kwani ni udhalilishaji wa watu wasio na hatia hususan wazazi.

Tundu Lissu Apata Dhamana Baada ya Kushikiliwa na Jeshi la Polisi Kwa Masaa 48

$
0
0
Tundu Lissu Apata Dhamana Baada ya Kushikiliwa na Jeshi la Polisi Kwa Masaa 48
Ndani ya mahabusu kwa saa 48 hatimaye Mwanasheria Mkuu wa Chama na rais wa TLS Mh Tundu Lissu amepewa dhamana ya Polisi majira ya saa 11 jioni.

Amepewa masharti ya kuripoti kituo cha polisi Jumatatu tarehe 28/8/2017 wakati wowote akiwa na muda.

Amedhaminiwa na mawakili wake Fred Kihwelo na Msemo.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images