Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

REPORT MPYA YA KUHUSU SHAMBULIO LA WESTGATE NAIROBI ILIYOTOLEWA NA MAREKANI

$
0
0
Magazeti ya Marekani yameripoti kuwa shambulizi lililofanyika nchini Kenya kwenye jumba la Westgate Naiorbi lilifanywa na watu wasiozidi wanne tu ambapo ripoti hiyo iliyofanyiwa uchunguzi na kitengo cha polisi cha jiji la New York, inapingana na ripoti zilizotolewa na idara za ulinzi nchini Kenya ambazo zilisema shambulizi hilo lilifanywa na watu zaidi ya 15 wakiwemo raia wa nje.
Zaidi ya watu 60 pamoja na wanajeshi sita walipoteza maisha kwenye shambulizi hilo Septemba 21 na magaidi wa kikundi cha al shabab kinachoshirikiana na al qaeda ambapo baada ya kulizunguka jengo la Westgate kwa siku mbili, mamlaka za usalama za Kenya zilithibititsha taarifa kuwa zimerejesha hali ya usalama huku magaidi wanne wakiwa wameuwawa.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumanne asubuhi, kamishna wa polisi wa New York Ray Kelly amesema wapelelezi hawakujua watu wangapi walihusika na shambulio hilo lakini waliamini kuwa walikuwa watu wanne.
Ripoti hiyo ya NYPD ilisema washambuliaji walibeba silaha nyepesi na hakukuwa na ushahidi unaoonyesha kuwa magaidi hao walijaribu kushika watu mateka baada ya saa 12 na dakika 15 septemba 22.
Ripoti hiyo pia inasema kuwa gaidi kutoka Uingereza ambaye anafahamika kwa jina la White Widow hakuhusika moja kwa moja na tukio hilo japo taarifa nyingi zilionyesha kwamba alihusika na alikuwemo ndani ya Westgate siku ya tukio.

Ripoti nyingine inasema kuwa wanajeshi wa Kenya waliiba vitu kwenye maduka ya westgate na mmoja wa viongozi wa idara ya polisi ya New York mpelelezi Kevin Yorke ambaye aliaandaa na kuwasilisha ripoti hiyo, alikanusha taarifa zilizothibitishwa na Wakenya kuwa magaidi wote walifariki dunia baada ya milipuko kutokea.
Ripoti hiyo inasema kuwa magaidi wanne waliogawanyika kwenye timu mbili za watu wawili waliendesha shambulizi hilo huku wakiwasiliana kwa simu za mkononi na uwezekano upo kabisa kwamba wote walitoroka wakiwa hai.




WABUNGE WAZIDI KUMWANDAMA WAZIRI MKUU PINDA

$
0
0
Mzimu wa kung’olewa unazidi kumwandama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR), akitaka Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani naye.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana, mbunge huyo alienda mbali zaidi na kuomba Naibu Spika, Job Ndugai kuwaongoza wabunge kupiga kura hiyo ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Pia alitaka kung’olewa kwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia akisema haiwezekani aendelee kuwepo wakati fedha za wafadhili zinaliwa bila yeye kuchukua hatua.

Mkosamali anakuwa mbunge wa tatu kupendekeza kung’olewa kwa waziri mkuu, akitanguliwa na Mbunge wa Mwibara, alphaxard Lugola (CCM) na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR).

Mkosamali alisema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinaonyesha hakuna ufuatiliaji wa fedha zinazoidhinishwa na Bunge na kupelekwa katika Halmashauri nchini.

Alisema taarifa zinaonyesha asilimia 20 ya bajeti ya Serikali huingia mifukoni mwa watu na kuongeza kuwa hata Bunge likapitisha bajeti ya Trilioni 40 bado asilimia 20 zitakwenda mifukoni mwa watu.

Mkosamali alisema katika semina mbalimbali wabunge walielezwa kuwa taarifa za CAG zinazofichua ufisadi wa kutisha pamoja na taarifa za Kamati za Bunge zimekuwa hazifanyiwi kazi na Serikali.

Mbunge huyo aliwasihi wabunge wenzake kuchukua hatua na kuhakikisha kuwa kabla ya kumalizika kwa mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma mawaziri kadhaa wawe wameng’oka.

Akinukuu Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Mkosamali alisema, Waziri Mkuu ndiye atakuwa na madaraka ya juu katika udhibiti na usimamizi wa Serikali.

Aliongeza kusema “Kwa nini tusipige kura ya kumwondoa?... Mheshimiwa Naibu Spika wewe kama kiongozi wetu ndio unapaswa kutuongoza kupiga kura ya kuwaondoa hawa watu.”

Mkosamali alisema wabunge wanatoa mapendekezo hayo kwa vile wameshindwa kufanya kazi ambayo walipatiwa na kusisitiza kuwa wameshawapima na kubaini kuwa hawawezi kazi tena.

“Hatuna chuki na mtu….Hata tukiwaambia tunajua hamtafanya tumeshawapima tunajua hamtaweza sasa tunawashauri nini tena?” alihoji Mkosamali wakati akijenga msingi wa hoja yake hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul (Chadema), alisema ni vizuri mkuu akaondoka mapema na mawaziri wake walioshindwa kazi na ambao wamepuuza ushauri na mapendekezo ya Bunge.

Hata hivyo Gekul alisema kuwang’oa Pinda, Ghasia na mawaziri mizigo hakutasaidia kwani mfumo mzima wa serikali umegubikwa na rushwa na kwamba suluhisho pekee ni kuing’oa CCM madarakani.

“Wataanzania waadhibu CCM kwa kuwaondoa kwenye masunduku ya kura kwa sababu hata wakiletwa wengine(mawaziri)bado mfumo wa rushwa ni ule ule na CCM kimeshindwa kuikemea Serikali” alisema.

Akizungumzia suala la mishahara hewa, alisema waziri Ghasia aliwahi kuliambia Bunge kwamba ameanzisha mfumo wa Epica na kwamba suala la kuwapo malipo hewa ya mishahara litakuwa ndoto.

“Lakini katika ripoti hii 1.5 bilioni zimelipwa kama mishahara hewa imeliwa katika ngazi ya Halmashauri, kwani Mheshimiwa Waziri (Ghasia) usiwajibike? alihoji Mbunge huyo.

Alisema mbali na malipo hayo, lakini yapo malipo mengine ya Sh693 milioni…. Hizi fedha zingeweza kuwalipa walimu 1,400 posho za mazingira magumu ya sh500,000 kila mmoja”alisema Gikul.

Katika mchango wake huo alionekana kuishambulia zaidi Serikali ya CCM kwamba imeshindwa kuongoza nchi, hali ambayo ilimuinua kwenye kiti chake Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.

“Tunafika mahali ambapo hatuelewani naomba tujielekeze kujadili taarifa za kamati tatu badala ya kujadili ripoti ya CAG japo siwafungi kujadili jambo lililo nje ya hili”alisema Ndugai.

Gekul alisema kinachojadiliwa ni pamoja na taarifa ya kamati ya Serikali za Mitaa (Laac) na imekuwa ikieleza yale yale aliyokuwa akisema na taarifa ya kamati hiyo nayo imeegemea ripoti ya CAG.

Hata hivyo baada ya kumaliza kuchangia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kudai mchango wa Gekul ulivunja kanuni ya 64(1) ya Bunge.

“Nimemvumilia sana Mbunge wa viti maalum sikutaka kumkatisha dada yangu katika hotuba yake… Sio kwamba sisi hatuwezi kusema lakini katika hotuba yake yote amevunja kanuni ya 64”alisema.

Alisema kanuni hiyo inasema Mbunge hatazungumzia jambo ambalo haliko kwenye mjadala kwa sababu yote anayozungumza hapa hayapo kwenye hotuba…amezungumza matusi makubwa”alisema.
-Mwananchi


NIMEGUNDUA MKE WANGU ANAVUTA SIGARA KUBWA (BANGI)

$
0
0
The beautful wife of mine smook weed. 
Jamani juzi kati nimembamba mke wangu akiwa analipuliza. Tena alipo niona wala hakushtuka
kwa mapoozi akaendelea kulikoka.. ahh! mi nikazani sigara kwani huwa anapiga siku moja moja 
anadai inaondoa stress na kwa sababu nilikua tungi nikazama ndani.
Leo nimepewa notes na baba mwenye nyumba kwa mke wangu kuvuta bangi hadharani (Ila hii sio ishu nitamalizana nae).

Mke wangu nikimuuliza anasema mbona wewe unakunywa?.. Kwani tatizo nini?... 

BAADA YA KUSINGIZIWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA BRAZIL ASHA BUI AONEKANA SALOON SINZA

$
0
0
Mwigizaji wa filamu za kibongo aliyesemekana kuwa amekatwa nchini brazil akiwa na madawa ya kulevya Aisha Bui ameonekana nchini hivi karibuni akiwa kwenye salooni ya mwanadada mwingine muigizaji Nisha iliyopo maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.

Mwadada huyo ambaye tayari ameigiza filamu kadhaa na mastaa wenzake alionekana kwenye saloon ya Salma Jabu(Nisha) akiwekwa sawa nywele zake kama anavyoonekana pichani.

BASI LA BURUDANI LAPATA AJALI MBAYA LIKITOKEA KOROGWE KUELEKEA JIJINI DAR

$
0
0
Hospitali ya wilaya ya Korogwe.
Majeruhi wakipatiwa matibabu.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo ( kushoto) akiangalia mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu.
Manesi wakiendelea na matibabu kwa majeruhi.
Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa kwenye benchi.
Wananchi wakiwa eneo la Hospitali.
Basi la Burudani leo limepata ajali kijiji cha Taula Wilaya ya Handeni, watu 12 hadi sasa wamefariki na majeruhi zaidi ya 55. Watu 4 wamepelekwa MOI na KCMC. Tuwaombee majeruhi.
PICHA ZOTE NA MKUU WA WILAYA YA KOLOGWE, MRISHO GAMBO

‘SAUZI’ YAMTAFUTA MKALIMANI FEKI WA VIZIWI KWENYE IBADA YA KUMKUMBUKA MANDELA

$
0
0
AFRIKA Kusini inamtafuta mkalimani feki wa kutumia ishara za viziwi ambaye alishindwa kufasiri walichokisema viongozi mbalimbali kutoka duniani wakati wa ibada ya kumkumbuka  aliyekuwa rais wa nchi hiyo Nelson Mandela iliyofanyika Jumanne wiki hii.

Mtu huyo asiyefahamika na aliyekuwa na pasi zilizotolewa kwa ajili ya usalama eneo hilo, alikuwa amesimama karibu na viongozi hao wakati wanahutubia katika uwanja wa Soccer City wenye uwezo wa kuingiza watu 95,000 ambapo jamaa huyo alionekana akifasiri lugha mbalimbali kimakosa.

“Ulikuwa ni upuuzi mtupu, hakupatia chochote na alishindwa hata kutoa alama ya kusema ‘asante’,” alisema  Delphin Hlungwane, mkalimani wa ishara wa chama cha viziwi cha Afrika Kusini ( DeafSA) ambacho kimelaani tukio hilo.

Pamoja na kwamba serikali ya nchi hiyo ilikuwa msimamizi wa sherehe hiyo, lakini jamaa huyo asiyefahamika mwaka jana alifanya hivyohivyo kwenye mkutano wa chama cha African National Congress cha nchini humo ambapo Rais Jacob Zuma alikuwa anahutubia.

PRODYUZA ALIYEFUKUZWA NA WEMA AFUNGUKA "WEMA ALITAKA NIWE KUWADI WAKE

$
0
0
BAADA  ya kudaiwa kufanya ngono katika magari ya Kampuni ya Endless Fame inayoongozwa na Wema Issac Sepetu, Prodyuza, Rashid Mohammed ‘Chid Classic’ amefunguka na kusema chanzo cha yote ni mshahara  na ukuwadi ndani ya kampuni hiyo wala siyo uzinzi, Amani linakujuza. Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, Chid amesema hajafukuzwa katika kampuni hiyo kama alivyodai mratibu wa kampuni hiyo, Petit Man bali ameondoka baada ya kuchoka  kufanya kazi bila ya kulipwa mshahara.

“Ni uongo kusema kwamba nimenaswa nikifanya uzinzi Coco Beach nikiwa ndani ya magari ya Wema, sijawahi hata siku moja kufanya hivyo kwani nina kwangu ambako nina uwezo wa kumwingiza mwanamke wakati wowote,” alisema.

“Tangu kampuni ianzishwe haijawahi kulipa mishahara unadhani nitakuwa na moyo wa kufanya kazi, sikwenda pale kufanya ukuwadi kama wengine, tena nawaomba wasiendelee kusema uongo kwani nina mengi nayajua ya Endless Fame,” aliongeza Chid.
Baada ya kusikia maelezo hayo, Amani lilimtafuta Wema bila ya mafanikio ndipo likaongea na meneja wake, Martin Kadinda.

“Nina wasiwasi na kauli za Chid kwanza tatizo siyo mshahara na hayo masuala ya ukuwadi ni uongo na uzushi, kama ni kweli kwa nini asiongee siku zote hadi lilipoibuka hili la kunaswa akifanya uzinzi kwenye gari?” alihoji Kadinda.

PINDA"KAMA IKITOKEA LEO HII NIKAVULIWA UWAZIRI MKUU NA RAISI NITAFURAHI SANA"

$
0
0
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliambia Bunge muda mfupi uliopita  kwamba kama ikitokea Rais akamng'oa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu, yeye  atafurahi sana  kwa kuwa kazi anayoifanya ni mzigo mkubwa.

"Kama ningeambiwa LEO ningeondolewa katika nafasi hii, basi dada Rukia mimi ningefurahi kwa kuwa ningekuwa nimetua mzigo
"Dada Rukia, hii kazi huombi, Rais anaangalia na anakuchagua kuwa Waziri Mkuu. Anaweza kuangalia akakuchagua hata  wewe dada Rukia, kwa hiyo LEO Rais  akisema basi, nianchie ngazi, mimi niko tayari, nitafurahi," amesema Pinda katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Waziri Pinda ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Rukia aliyetaka  kujua  msimamo wake kutokana na kauli ya Kamati ambayo yeye na mawaziri wengine waliambiwa wapime kama wanastahili kuendelea kuwa mawaziri  kutokana na ufisadi wa kutisha  TAMISEMI.

ZITTO AKATA RUFAA KUPINGA MAAMUZI YA CHADEMA KUMVUA UONGOZI

$
0
0

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe (MB) amewasilisha barua ya kupinga uamuzi wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kumvua nafasi zake za uongozi ndani ya chama hicho.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando akizungumza na waandishi wa habari, amesema tayari mteja wake ametoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Chadema kumjulisha nia yake ya kukata rufaa Baraza Kuu la Chama hicho kupinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu dhidi yake kumvua nyadhifa zake ndani ya Chama.

Msando amesema mteja wake amewasilisha sababu mbili za msingi za kukata rufaa; moja ikiwa ni Utaratibu wa kuchukua hatua za nidhamu ulikiukwa na ya pili ikiwa ni sababu za kuchukuliwa hatua hazi kuwa na mashiko.

“…Utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji ni kama ifuatavyo; Kanuni ya Uendeshaji 6.5.6 inasema; Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka yake kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.

“…Pia tunapenda ijulikane kwamba Kanuni ya Uendeshaji 6.5.2 (a), (b), (c) na (d) kama ilivyorekebiswa Januari 2013 inasema; Kwa mujibu wa ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza; a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa
majibu katika muda usiopungua wiki mbili.”

“…b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika. c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa. d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika,” alisema Msando akizungumza na waandishi wa habari.

Akizungumzia matukio ya vurugu na vitisho ambavyo baadhi ya viongozi wa Chadema wamekuwa wakipata kutoka kwa baadhi ya wanachama mikoani, hasa wanaofanya ziara za chama hicho, Msando amesema mteja wake hausiki na matukio hayo aliyoyaita ya kusikitisha ambayo mengine yamefikia mahali kuwa fujo na vurugu ikiwa ni pamoja na kurushiwa mawe Katibu Mkuu wa Chama.

“…Vurugu hizo baadhi zimehusishwa na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na baadhi ya watu. Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na hayo yanayoendelea na anayakemea na kuwashauri wanachama wote kuwa watulivu na kuendelea kuwaheshimu viongozi wa kitaifa,” alisema mwanasheria Msando.

LEMA "ZITTO NIPE MAJINA YA WATU WAALIOFICHA HELA USWIZI NIKUSAIDIE KUYATAJA"

$
0
0


Dodoma, Tanzania. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati akichangia  taarifa ya Kamati ya Sheria na Katiba muda mfupi uliopita  amemtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazni Zitto Kabwe kumkabidhi AG majina ya watu wote walioficha fedha Uswis ambayo alisema anayo.

Lema ameliambia Bunge kama Zitto na serikali wameshindwa kuwataja watu hao, wampe Lema majina hayo ili awataje.

Amefafanua kwamba hatahitaji kinga yeyote kuwataja wezi hao walioficha fedha Uswis ndani ya Bunge au nje ya Bunge.

"WAJINGA USEMA KWAMBA CCM NDIO ILILETA UHURU TANGANYIKA" PROF MBELE

$
0
0
Kiwango cha ujinga Tanzania kinatisha. Utawasikia wengi wakisema kuwa CCM ilileta Uhuru Tanganyika mwaka 1961.

Wajinga wengine, kuanzia wanasiasa hadi watu wa mitaani, husema kuwa CCM imekuwa madarakani kwa miaka 52.Utamsikia mwanasiasa anaiponda CCM kwa kuuliza, "Miaka yote 52 ya utawala wa CCM, wananchi mmenufaika vipi?" 

Na utammsikia kada wa CCM akitamba, "CCM ni chama chenye uzoefu wa miaka 52.

Hapakuwa na CCM mwaka 1961. Chama kilicholeta Uhuru Tanganyika ni TANU. Wala CCM haijawa madarakani miaka 52. Kuna mengi katika historia ya Tanganyika na Tanzania ambayo yanasahaulika au kupotoshwa kwa sababu ya uzembe wa wa-Tanzania.

Wajinga wengine wanasema kuwa tunasherehekea kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania au Tanzania Bara. Mwaka 1961 hapakuwa na nchi iliyoitwa Tanzania wala Tanzania Bara. Nchi iliyopata Uhuru mwaka ule ni Tanganyika. Inasikitisha.

JE WAJUA KUWA INSTAGRAM INAKUWA HARAKA KULIKO TWITTER..MASTAA WA BONGO INSTAGRAM NDIO HABARI YA MJINI

$
0
0
Facebook, Twitter na Instagram ndio mitandao ya kijamii inayotawala maisha ya mtandaoni kwa watu wengi duniani. Hadi sasa Facebook ina watumiaji bilioni 1 duniani kote, Twitter ikiwa na watumiaji milioni 250 na Instagram ikiwa na watumiaji milioni 150.

Hata hivyo, takwimu zinazonesha kuwa Instagram inakua haraka zaidi kuliko Twitter na utumiaji wake kwa sasa ni mkubwa kuliko Twitter. Ikumbukwe kuwa vita kati ya Twitter na Instagram ilianza December mwaka jana baada ya Instagram inayomilikiwa na Facebook, kuacha kushirikiana na Twitter.

Kabla ya hapo, watu walikuwa na uwezo wa kuona picha za Instagram kirahisi kupitia Twitter hivyo Twitter ilikuwa inapata watumiaji wengi Instagram. Baada ya urahisi huo kuondelewa, watumiaji wengi wa Twitter wamejikuta wakiitumia zaidi Instagram.

Kwa mujibu wa ripoti, Twitter inapata shida zaidi kwa kupigwa chini na Instagram ambayo imeendelea kuneemeka tu. Kuna ubadilishanaji picha wa asilimia 59 tu kwenye Twitter ukilinganisha na asilimia 98% kwenye Facebook.

Tangu Instagram iache kusupport picha kwneye Twitter, mtandao huo umepata pigo kubwa kwa kupungua kwa matumizi ya picha huku Instagram kwa upande mwingine ikiendelea kukua ambapo ongezeko la followers limefika 41%.

Kwa utafiti wa kawaida tu na hata hapa Tanzania, utagundua kuwa kumekuwepo na watumiaji wengi mno wa Instagram.
Mastaa wa Tanzania wameonekana kuvutiwa zaidi na kuwa ‘active’ kwenye mtandao huo kuliko Twitter wala Facebook.

Kuna mastaa wengi ambao huwezi kuwaona Facebook wala Twitter lakini wako active zaidi Instagram. Kwa mfano kuna waigizaji wachache sana wa filamu Tanzania wanaotumia mtandao wa Twitter lakini wakiwa na followers wengi Instagram.

Sababu kubwa zinazochangia Instagram kupendwa zaidi ya Twitter na Facebook kwa mazingira ya Tanzania ni ule urahisi wa kuweka picha nyingi bila ulazima wa kuweka maelezo mengi na ile imani kuwa picha huongea maneno mengi kuliko maandishi kama ilivyo kwenye Twitter na pia Facebook ikiwa imetawaliwa na watu aina mbalimbali wakiwemo wakorofi na wanaopenda kutukana watu.

“Mi naweza kusema kwamba Instagram ni sehemu unayoweza kuona how crazy stars can be,” anasema Wema Sepetu kujibu swali la kwanini anapenda kutumia zaidi Instagram kuliko Twitter. “Watu wengi ambao nawafollow on Instagram ni macelebrities wa nje. So I follow people like Ellen Degeneres, I follow Soulja Boy, I follow 50 Cent, I follow Kim Kardashian, I follow the Kardashians, Nicole Ritchie, Rihanna. This is the only place ambayo ninaweza kuwaona how crazy they can get, it’s kila mtu amekuwa an ‘Instagram freak’ right now. Through profile ya mtu ya Instagram, unamjua mtu alivyo. It’s very hard to tell from Twitter cause it’s just mtu anaandika tu, ‘sasa hivi niko wherever’ anaweza akadanganya. Lakini kwenye Instagram, you can actually tell ‘Yeah nimeenda sehemu fulani nimepiga picha I’m here, nimepiga picha chakula changu, I am eating’ it’s just interesting.”

Kwa upande wake muigizaji wa filamu, Irene Uwoya anaamini kuwa mtandao wa Facebook ni kama daladala ambako kuna fujo za kila aina na ndio maana anaipenda zaidi Instagram kwakuwa watuamiji wake wengi ni waelewa.

“Facebook imechafuka sana,”anasema. Matusi, watu waandika vitu vya ajabu yaani changanyikeni, kila mtu yupo Facebook. Naweza nikatolea mfano kama usafiri, basi Facebook ni daladala. Instagram ni latest, kama ni gari basi ni Range new model, kama langu. Watu wanaoingia Instagram ni watu wa ukweli, watu wanaoingia huko ni wenye akili zao timamu, japokuwa kuna wachache waliotoka huko huko kwenye Facebook wanakuja kuchafua Instagram.

Irene anasema maudhi ya Facebook yalimfanya ajiondoe muda mrefu uliopita na wala hana akaunti tena.

“Kuna watu wanajifanya mimi sasa kwenye Facebook, wakati mimi sipo Facebook toka siku nyingi. Kuna akaunti kama saba za kwangu kila mtu ananiambia ‘nimekutumia meseji Facebook’ nawaambia ‘bwana mimi Facebook nilishatoka.”

Kwa upande wa Jokate Mwegelo, Twitter, Facebook na Instagram yote ni mitandao muhimu kwake.

“Mimi kotekote. Twitter napenda zaidi kuongeza mambo ya current affairs etc. Instagram picha zaidi na Facebook natoa mawaidha,” anasema.

Hata hivyo wataalam wanasema ingawa namba zinaonesha kuwa ni vizuri kuitegemea Instagram kwa sasa, watumiaji wa mtandao hawapaswi kusahau kuwa vitu vingine muhimu vinavyofanywa na Twitter. Mtandao huo hutoa vifaa zaidi ya kusambaza picha. Kwa biashara na watumiaji wa kawaida kuweza kuwafikia vizuri walengwa wao, wanatakiwa kupitia tena mikakati yao kwa kuchunguza mitandao mbalimbali ya kijamii kwa matumizi yanayofaa.

Pamoja na watu wengine kuanza kuikimbia Facebook kwa kuwepo na watu wengi wanaoitumia vibaya, bado imeendelea kuwa jukwaa muhimu linalotumiwa na makampuni, mashirika, viongozi na watu mashuhuri kuwasiliana na wateja ama mashabiki wao kwa haraka na kwa njia inayowafikia watu wengi.
-Bongo.com

MASIKINI:KILIMANJARO STARS YAIKOSA NAFASI YA 3 YA CECAFA

$
0
0
Timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imeshika nafasi ya nne michuano ya Kombe la CECAFA 2013 inayofanyika nchini Kenya baada ya kufungwa na timu ya Zambia kwa penalti 6-5.

Mchezo huo uliokuwa wa kutafuta mshindi wa tatu wa kombe hilo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo bao la Zambia lilifungwa na Ronald Kampamba katika dakika ya 51 na Kilimanjaro Stars ilisawazisha kupitia kwa Mbwana Samatta katika dakika ya 65 kipindi cha pili ambapo dakika 90 ziliisha kwa sare ya bao 1-1.

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars waliopata penalti ni Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhan Singano ‘Messi na waliokosa ni Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani.

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO MPYA WA YOUNG DEE FEAT..MWANA FA & BEN POL-FUNUNU

$
0
0
Sikiliza hapa ngoma mpya kutoka kwa Young Dee AKA Young Dar-es-Salaam akiwashirkisha Mwana FA na mkali wa R&B Ben Pol. Ngoma inaitwa ‘Fununu’.

DIAMOND PLATNUMZ ATINGA SURUWALI YAKE YENYE UTATA NA KUOMBA DUA ILI ASICHAMBWE HAHAHAHA

$
0
0
Hahaha Diamond kanichekesha sana leo. Baada ya kuandamwa na mafashion police kutoka kila pande pamoja na mashabiki wake kuhusu suruali yake aliyo vaa kwenye harusi ya P-Square (pichani), leo hii ameitinga tena na kurusha picha Instagram akiambatanisha na kadua ili watu wasimchambe.




MASHINDANO YA MISS UTALII YAFUNGIWA RASMI NA BASATA

$
0
0

Barua kutoka Basata kuhusu kufungiwa kwa Mashindano ya Miss Tourism Tanzania

MASTER JAY AFUNGUKA "WASANII WA BONGO FLAVA NI WEZI"

$
0
0
Producer mkongwe na C.E.O wa MJ Records Master J amesema kuwa wasanii wa Tanzania wanawaibia watayarishaji wa muziki.

“Huwezi kuchukua wazo langu uende kulitumia kutengeneza hela halafu uniambie kwamba ‘bwana mimi sikupi kitu’, wasanii ni wezi tu Bongo.” Amesema Master J.

Unaweza kudhani labda aliteleza kidogo kusema hilo, lakini kwa kuwa ana uhakika na anachokisema, producer huyo mwenye mchango mkubwa kwa muziki wa kizazi kipya hapa nchini aliweka mkazo kwenye maneno yake.

“Watu wanaogopa kuongea, mimi ngoja niongee tu ukweli, wasanii wa Bongo ni wezi. Kitu wanachokifanya ni wizi. Unajua mwizi anakaaga kimya, lakini wanakwenda kwenye media wanaropoka ‘nimeingiza million 300 (kwa kutumikia haki ya Lamar bure na simpi kitu)’. Yaani unaiba halafu unaenda unatangaza kwenye media!” alifunguka Master J.

“Hata hawaogopi! Walivyokuwa hawajui kwamba sheria hairuhusu kufanya hivyo, na kiukweli akiamua kupania anapata cha kwake, sema tu maproducer hawafuatilii. Lakini wanavunja sheria kabisa na ni wezi. Huwezi kufanya hivyo halafu unaenda unatangaza, kaa kimya…kula na kipofu. Sio sawa wanavyofanya.” Aliongeza kwa msisitizo.

FILAMU ZA KIBONGO HAZIUZI BILA KUTUMIA WASICHANA WAREMBO

$
0
0
Bila wasichana warembo kwenye filamu ya kibongo, hakuna atakayeinunua na huenda waandaaji wakaishia kuiangalia tu nyumbani na familia zao

Kwa mujibu wa Tino, wasichana warembo ni ‘chambo’ kinachowavuta wanunuzi wa filamu za Tanzania. Ujuzi wa uigizaji na kipaji, si sababu kwao.

Akiongea na gazeti la Mwanaspoti, Tino alisema warembo hao pamoja na kuzifanya filamu zivutie pia huwa na juhudi katika kazi hiyo tofauti na wanaume na wanaipenda kazi yao.

“Kwa kweli bila kuweka wasichana warembo katika filamu yako hutauza kwa sababu wengi wana juhudi za kufanya mambo mapya kila kukicha, lakini pia wanakuongezea mvuto kwa kuwa warembo ni kama maua,”alisema Tino.

Pengine ndio maana waigizaji wa kike wanaotamba ni walewale akina Wema Sepetu, Lulu, Irene Uwoya, Jacky Wolper, Batulli na wengine waliojaaliwa sura za kuvutia
-Bongo5

HUYU AGNESS MASOGANGE MMHH..!! TAZAMA HOT PICHA ALIZOACHIA KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM

$
0
0
 
Pichani juu ni taswira za mpya za Video Queen wa Bongo, Agness Gerald 'Masogange' alizotupia kupitia ukurasa wake wa Instagram.

HATARI ! ETI LULU NA YOUNG D WAKUTWA WAKIBANJUANA NDANI YA GARI..MHH

$
0
0
Pata habari za bongo movies na nyingine nyingi punde zitokeapo. Tuma neno PERUZI kwenda 15368 sasa. Kwa wateja wa Vodacom Pekee


Jana kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha clouds FM chini ya bwana Sudi Brown ama Gossip Cop kulikuwa na FUNUNU kali iliyokuwa inamuhusu mwanadada wa bongomovies Elizabeth Bin Michael a.k.a LULU na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Young D al-maarufu kama Young Dar es salaam kama mwenyewe anavyojiita ya wawili hao kukutwa kwenye gari wakifanya lile tendo linaloruhusiwa kufanywa mara baada ya mdada na mkaka kufunga ndoa.

Kwa mujibu wa Sudi Brown = Gossip cop, wawili hao walikutwa maeneo ya Mbezi beach ndani ya gari aina ya Hyundai ya mwanadada lulu na polisi wa doria wakivunja amri hiyo iliyokatazwa na vitabu vyote vitakatifu kwa maana ya biblia, Quran na vitabu vingine vya dini ulimwenguni.

Habri zainasema Baada ya wawili hao kukutwa eneo hilo na polisi walipelekwa pembeni gizani na kuongeana polisi kabla ya wao kutokomea wasipojulikana na gari hilo.

Alipopigiwa simu mwanadada LULU alipokea na kukata muda mfupi na baadaye Young D alipopigiwa simu alitoa majina ya utata kama alivyoongea mwenyewe kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha clouds fm
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images