Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Florah Mbasha Awagawa Wachungaji…Baadhi yao Wadai Hawawezi Kuhudumiwa na Mwimbaji Mzinzi

$
0
0
Mpasuko  wa  ndoa  ya  wasanii  wa  nyimbo  za  Injili, Emmanuel  Mbasha  na  mkewe  Florah  umewagawa  wachungaji  wa  makanisa  mbalimbali  nchini  baada  ya  kibao  kumgeukia  Flora  kwamba  ndiye  anadaiwa  kusuka  mpango  wa  kumwangamiza  mumewe  ili  afungwe  kwa  kosa  la  ubakaji…..

Wakizungumza  na  wanahabari  wetu  kwa  nyakati  tofauti,  wachungaji  hao  walisema  endapo  itabainika  ni  kweli  Flora  ameshiriki  kumsaliti  mumewe  kwa  kutembea  na  mmoja  wa  wachungaji  maarufu    nchini  hapatakuwa  na  haja  ya  kumwalika  kwenye  huduma  zao  kwani  hawawezi  kuhudumiwa  na  mwimbaji  mzinzi.

Mchungaji  Ambonile  Mwakipesye  na  Amani  Joseph  wa  makanisa  ya  Tanzania  Assemblies  of  God ( TAG)   walisema  kuwa  kama  kulikuwa  na  matatizo  kwenye  ndoa  yao  walipaswa  kuwaona  watumishi  wa  Mungu  na  kusuluhisha  badala  ya  kutengenezeana  mitego  na  kuingizana  majaribuni  kama  inavyodaiwa  kutokea  kwa  Mbasha….

Wakati  wachungaji  hao  wakisema  hivyo, mchungaji  Thomas  Methew  yeye  alisema  kuwa  ukweli  wa  jambo  hilo  wanaujua  wanandoa  wenyewe  kwani  mpaka  sasa  hakuna  anayelijua  tatizo  kubwa  mpaka  wakafikia  hatua  ya  kutengana

Taarifa kwa umma juu ya kutelekezwa na chama changu (NCCR Mageuzi)

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUTEREKEZWA NA CHAMA CHANGU.

Ndugu Watanzania na wale wote wanaojali UTU wa mtu, kwa kweli leo imenibidi niseme tu kutokana na hali yangu inavyozidi kuwa mbaya kutokana na chama changu NCCR-Mageuzi kunitelekeza baada ya kupata ajali nikiwa nasimamia uchaguzi wa mdogo wa marudio wa udiwani huku mimi nikiwa mwandamiz wa chama kitengo cha vijana wa NCCR-Mageuzi mwaka jana 2013 kabla sijawa Mjumbe wa Halmashauri kuu mwaka 2014..

Uchaguzi mdogo wa mwaka jana 2013 wa udiwani kata ya Nyampulukano wilayani Sengerema tulipata ajali jumamosi ya kuamkia uchaguzi tukiwa na viongozi wa jimbo la Sengerema mimi nikiwa mbele tukitoka kukagua vituo vya kupigia kura baada ya kuambiwa vimehamishwa na nikiwa ndio msimamizi mkuu wa uchaguzi huo. 

Ajali hiyo ilisababisha nipate maumivu makali lakini viongozi wangu wakatibu gari tu na kuacha kutibu mwili wa binadamu. Swala hili hata siku ya uchaguzi mkuu wa chama januari mwaka huu2014 ndani ya ukumbi wa diamond Jubilee nililisema lakini mpaka leo sijasikilizwa wala kuhudumiwa na chama hata kufikiriwa nikiendelea kuteseka na huku familia yangu ikiumia hasa wanangu na mke wangu.

Ombi langu kwa Serikali na asasi za kirai naomba msaada wenu ili nikachunguze afya yangu kwani inazidi kuwa mbaya.

Nasikitika sana mfumo wa upinzani kama vijana tunaumia kazini lakini hatujaliwi unadidimiza imani ya Taifa kwa Vijana na kujenga kukosa imani na Upinzani.

Kipimo cha Mwanasiasa Bora ni kujali Utu.

Mwanasiasa asiyejali utu sio mwanasiasa ,sio mtu mwema bali ni adui wa wale anaowa-inspire,ni adui wa wale anaowaongoza,ni adui wa jamii na Taifa ambalo linajali misingi ya utu katika kujenga taifa lililostarabika linalojali haki

Tusisite kutangaza vitaya kutetea haki zetu dhidi ya wanasiasa wa aina hii na Mungu ambaye Wengi wanamsujudia atakua nasi.Najua wengi Mmeumizwa/Tumeumizwa.Naelewa Maumivu haya ambayo baadhi yetu tumepitia,tunaendelea kuyapitia na kitu bora zaidi -Tuyatarajie.

Maisha yetu halisi yawe mfano wa kile tunachopigania.Tuwe principled.Hii ni kwa wote bila kujali itikadi zetu.

Ndugu wanahabari naiomba Serikali inasidie kwani sina jinsi nami nimeshatelekezwa ninatembea nikiwa nimeshaumizwa bila matibabu sitahiki.


DEOGRATIUS KISANDU
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA-NCCR MAGEUZI.
0786 025 609
13/06/2014

Kuoa wanawake waliokulia maisha duni, ni kujichimbia kaburi.. hawana shukrani

$
0
0
Heshima kwenu wadau..

Nipo kijiweni bar ya jirani hapa tunacheki world cup Brazuca..

Kuna jamaa amezua hoja nzito kwamba kamwe hawezi kuoa mwanamke anaetoka familia ya kimaskini maana wengi wao hawana shukrani maishani.. anakwambia angalau watoto wa kishua japokuwa wavivu kazi za ndani ndogo ndogo but wanajua kupenda na hata cheating ni ngumu sana.

But mwanamke anaetoka familia yenye dhiki wengi wao vigeu geu mwepesi sana kubadilika badilika.. na ametoa mifano hai mingi tu ya ndoa za tunaowafahamu..

Wadau hii mnaonaje? je kuna ukweli wowote hapo

Kwanini ni Rahisi Clouds FM Kumpata Mh Rais Kuliko Taasisi Nyingine?

$
0
0

Nimeshangazwa, eti Kikwete ataudhuria Tamasha lililoandaliwa na Clouds Media Dodoma, tena ataambatana na mawaziri. 

Najiuliza, hivi ni kwa nini Clouds wanapo mtaka Mh Rais huwa anapatikana kilahisi namna hii, lakini taasisi nyingine zinapomualika katika mambo ya msingi ya kitaifa kwa mfano, Katika mijadala ya Katiba mpya, katika midaharo ya hali ya kisiasa hapa nchini, kikwete huwa haonekani?? lakini mambo ya clouds tena mengine yanafanyika usiku kabisa kama lile tamasha la kitapeli lililowahi kufanyika pale leaders, mh rais alihudhuria mpaka late night.

hii imekaaje WADAU: au ndo ule msemo wa Lipumba unajidhiirisha kuwa kikwete ni hodari wa matamasha??

Mchumba wa Ney wa Mitego Siwema Atoa Machozi ya Furaha Baada ya Kuona Nyumba Mpya ya Ney Yenye Thamani Kubwa

$
0
0
Katika Harakati za Ney wa Mitego kuonesha Mali zake ambapo juzi ametuonesha gari lake aina ya Murano lenye Thamani ya Milion 36, Jana ameonyesha nyumba yake mpya yenye Thamani ya Mil 170 ambayo ipo Maeneo ya Kimara , Katika tukio hilo la kuonesha nyumba pia alimsuprise mpenzi wake Siwema Ambae alikuwa hajui Kama anajenga ambapo kitendo hicho kilimfanya Siwema Atokwe na Machozi ya Furaha ....
Angalia Picha hizo za Nyumba yake Mpya hapa Chini:


Picha:Bongo5
udakuspecially.com

Baada ya Kimya Kirefu Mr Blue Ametoa Wimbo Mpya ..Unaweza Kusikiliza na Kudownload Hapa

$
0
0
Baada ya Kimya Kirefu Mr Blue Ametoa Wimbo Mpya ..Unaweza Kusikiliza na Kudownload Hapa Bonyeza Hapa Chini Kusikiliza au Kudownload:

Mama Amkubatia kwa Upendo Mahakamani Mtu Aliyemuua Mwanae

$
0
0
Uchungu wa mwana aujuae mzazi, na ukitaka kujua thamani ya mtoto kwa mama hatarisha maisha yake. Lakini hii imekuwa tofauti kwa mama huyu aliyezingatia sababu ya kifo cha mwanae.

Mwanamke mmoja wa Florida, Marekani ameonesha moyo wa huruma na uelewa alipokuwa mahakamani baada ya kumkumbatia kwa upendo Jordyn Howe mwenye miaka 16 baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kufyatua risasi mwaka 2012.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo, Howe alikuwa na umri wa miaka 14 aliichukua bastola ya baba yake wa kambo na kwenda nayo shuleni ambapo alifika na kuanza kumfanyia utani rafiki yake aitwa Lourdes Guzman –DeJesus aliyekuwa na miaka 13.

Howe alijaribu kufyatua risasi chini kwenye ardhi na bahati nzuri hakuna kilichofanyika na risasi haikutoka, baada ya kuona hivyo alimnyooshea bunduki rafiki yake kiutani lakini wakati huu alipofyatua risasi ilitoka kweli na kumpiga Lourdes, tukio lililopelekea kifo chake.

Baada ya kusomewa mashitaka mtoto huyo alikiri mara moja kufanya kosa na kumuua rafiki yake na kisha kuomba msahama.

“Nasikitika kwa kumuondoa na naomba radhi kwa kufanya kile nilichokifanya.” Alisema.

Maelezo ya mama huyo yalimuingia moyoni na ikambini aseme huku akiishiwa maneno.

“Ni uzoefu unaoumiza sana.” Alizungumza huku akiwa anatetemeka mikono. “Wazazi wawili hawatakiwi….hapana…siwezi.”

Mtoto huyo alipewa kifungo cha miezi 22 gerezani. Mwanzoni mama wa mtoto aliyepigwa risasi aliitaka mahakama kumpa adhabu kali, lakini baada ya maelezo hayo alibadili msimamo na kumkumbatia mtoto huyo kisha kuzungumza na hakimu namna nyingine ya kuyamaliza.

Hakimu aliamuru mtoto huyo kutumia mwaka mmoja katika kituo/mahakama ya watoto na kisha yeye na mama huyo watapewa nafasi ya kuzunguka Florida wakihamasisha watu kuachana na matumizi ya silaha za moto.

“Nimemsamehe kwa sababu nimekuwa na amani, kwa sababu nahisi kama binti yangu sasa hivi yuko katika sehemu ya amani. Siwezi kumrudisha mwanangu, lakini angalau naweza kulitunza jina lake kuwa hai.” Alisema mama huyo.
udakuspecially.com

Muamuzi Kutoka Japan Ageuzwa Sababu kubwa ya Ushindi wa Brazil

$
0
0
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Croatia Niko Kovac, ametoa tahadhari kwa maafisa wa shirikisho la soka duniani FIFA, kuwa makini na waamuzi wanaochezesha michezo ya fainali za kombe la dunia ambazo zimeanza jana nchini Brazil.

Kovac, ametoa tahadhari hiyo kufuatia hisia kumtuma kikosi chake hakikutendewa vyema wakati wa mchezo wa ufunguzi ambao ulishuhudia wenyeji wakichomoza na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Kocha huyo ambae aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Croatia kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2008 amesema muamuzi kutoka nchini Japan Yuichi Nishimura, hakuwatendea haki kufuatia maamuzi ya kuwazawadia penati wenyeji ambayo amedai haikuwa sahihi.

Kovac mwenye umri wa miaka 42, amesema anaamini mashabiki wote duniani waliokuwa wanaufuatilia mchezo huo hawakuridhishwa na maamuzi hayo isipokuwa wachache wenye mapenzi na Brazil.

Amesema hata ukiangalia kwa mara ya pili picha za televisheni za tukio lililosababisha penati kwa wenyeji, utaona ni vipi mshambuliaji wa Brazil Frederico Chaves Guedes Fred, alivyomuahadaa muamuzi kwa kumuaminisha alisukumwa na beki wake Dejan Lovren.

Mchezo wa ufunguzi kati ya Brazil dhidi ya Croatia ulimalizika kwa wenyeji kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja ambayo yalifungwa na wachezaji chipukizi Neymar da Silva Santos Júnior aliyefunga mabao mawili pamoja na Oscar dos Santos Emboaba Júnior huku beki wa pembeni Marcelo Vieira da Silva Júnior akiwazawadia bao la kufuta machungu wageni baada ya kujifunga mwenyewe.

Jamani Hii siyo Mechi ya Mpira Bali ni Usaili wa Kazi Uhamiaji

$
0
0
Jamani hii siyo mechi ya mpira bali ni hali halisi ya ajira nchini tz... hapa ni uwanja wa taifa wamejitokeza maelfu ya vijana kuja kwenye usaili uhamiaji. Nafasi watu wanaohitajika ni 70 tu..

Henry Kilewo Asema Kuna Mkono wa Mtu Kuchomwa Soko la Karume..Historia Inaonyesha

$
0
0

"Nikiwa kama kiongozi wa Chama ndani ya jiji la Dar es salaam, ninalaani tukio la uchomwaji moto la wafanyabiashara wadogo Karume jijini Dar es salaam. Kilichofanyika ni unyama wa hali ya juu na unapaswa kupingwa na wananchi wote.

Historia inaonyesha kuwa kila serikali itakapo Wafanyabishara kuondoka maeneo fulani ya biashara basi maeneo hayo hukubwa na moto. Mfano Mwanga kilimanjaro, Moshi, mbeya na sasa Dar es salaam.

Ili kukomesha vitendo hivi dhalimu wafanyabiashara wa Karume popote pale mlipo unganisheni nguvu zenu kupinga udhalimu huu na Kamwe msiondoke mpaka mtakapo pata haki zenu za msingi ikiwamo haki ya kulipwa gharama ya hasara mliyoingia..

Kumbukeni Haki haiombwi bali huchukliwe(Nobody can give u freedom but you take it )"
 Henry Kilewo

Alichokiandika Wema Sepetu Kuhusu Ugomvi Uliyokuwepo Kati Yake Na Kajala Masanja

$
0
0
Wemasepetu 
"Good morning instagramers.... Hope you all well... If y'all must know mimi ni mtu ambaye huwa nasomaga sana comments.... Na kama nimekosa kusoma comment yako ujue ni kwamba zinakuwa nyingi mno na nashindwa soma zote.... Ni kwa muda mrefu sana mnaniona nakaa tu kimya na sisemi chochote khs my friendship life... But mimi binafsi na muhusika ndo tunajua... saa nyingine
mnaongea hadi nakereka but nakaa kimya... Nilitaka tu kusema mimi sina kinyongo na mtu... na kama kuisha mbona yalishaisha...Au ndo mlikuwa mnataka kuona bega kwa bega...? In my life siwekagi vinyongo... nyi wenyewe mnajua... So jus so u want to know hayo yalishapita na maisha yanaendelea... ni hayo tu... Have a good day everebadi"

But chakushangaza Mlimbwende huyo wa Tanzania wa mwaka 2006 hakuweza kuweka picha ya shostito wake huyo kwenye hiyo post badala yake akaweka picha ya Shostito wake wa sasa Aunty Ezekiel ndio aliepamba post hiyo. Mmmmh je hapo unalionaje hilo? mdau.

Back to the Topic:: upande wa pili nao ulitoa shwangwe kwa kupost maneno haya:: 
kajalacelebrity2014 Hellow Africa!!!!I officially announce this#Finallyhakuna bifu wala chuki kati ya @new_kajala na @wemasepetu!!!Wameisha reconcile na kusolve differences zao, finally madam@wemasepetu ameweka wazi kwamba hana kinyongo tena shosti akeee Kay na hata Kajala amekubali kwamba hana bifu na madam, hizi ndo habari za ukweli kutoka kwa wahusika!!!!!Namalizia kwa kusema hivi," When destiny forgets to tie some people in blood relation...., it corrects that mistake by making them true friends!!!! @new_kajala @wemasepetu may God be with u!!!!

Punguzo la P.A.Y.E Kwa Asilimia 1 ni Dhihaka kwa Wafanyakazi!

$
0
0
Punguzo la 1% (kutoka 15% hadi 14%) kwenye kodi ya mishahara (PAYE) ni dhihaka kwa wafanyakazi wa Tanzania kwani gharama za maisha ziko juu sana kufuatia mfumuko mkubwa wa bei. Ifike wakati sasa serikali iwaonee huruma wafanyakazi kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi badala ya kufawafanyia mzaha kama huu. Wafanyabiashara wakubwa na mafisadi kibao wanasamehewa kodi lakini mfanyakazi masikini anazidi kukandamizwa tu kila kukicha. Hii haikubaliki hata kidogo.

Kwa jinsi serikali ilipokuwa inatamba kwa mbwembwe kwamba itapunguza kodi ya mishahra, sikutegemea kwamba mwisho wa siku wangekuja kupunguza kiasi kidogo kama hiki cha kodi. Ni aibu kwa kweli. Wafanayakazi mnanapaswa kutambua kwamba seriklali ya CCM haina nia njema katika kuwapunguzia ukali wa maisha, hivyo basi fanyeni uamuzi sahihi hapo mwaka 2015 ili kurejesha nidhamu kwa serikali hii isiyokuwa na mwelekeo. 

Kana kwamba hili halitoshi, bado wafanyakazi hao hao watakamuliwa Tsh 2500 kama kodi ya kumiliki simu kwa kila mwezi! Wananchi mmnatakiwa kuacha uzezeta—amkeni tukawafundishe adabu hawa mafisadi mwaka 2015. Saa ya ukombozi ni sasa. Bila kufanya hivyo, tutaendelea kukandamizwa hadi mwisho wa dahari. 

Tafakari, chukua hatua!

Spain Yachezea Kichapo Cha Mbwa Koko Kutoka Kwa Holand

$
0
0
Michuano ya kombe la dunia imezidi kushika kasi kwa michezo miwili iliyopigwa leo.
Mchezo wa kwanza leo hii ulikuwa kati ya wawakilishi wa Afrika Cameroon dhidi ya Mexico, na wamexico wakaondoka na ushindi wa goli moja kwa bila.
Mechi ya pili iliyomalizika hivi punde ilishuhudia mabingwa watetezi Spain wakidhalilishwa kwa kipigo kizito kutoka kwa Uholanzi.
Spain walianza kuliona lango la Uholanzi kwa mkwaju wa penati wa Xabi Alonso, lakini Robin van Persie akaisawazishia Uholanzi kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Uholanzi walirudi kwa kasi na kufanikiwa kuongeza magoli mengine manne kupitia Van Persie, Robben aliyefunga mawili na beki Stephan de Virj akaongeza la tano. Mpira ukamalizika kwa Spain kufungwa 5-1.

Baada ya Soko la Karume Kuungua Kitu cha Ajabu Chenye Mfano wa Mtu Chaonekana

$
0
0

Hiki ni kitu ambacho kilipatikana mara baada ya moto kuzimwa eneo hilo la soko,Kila mtu ana maswali mengiiiiii bila majibu Je ni kitu gani hicho?au wewe ndugu msomaji unaweza tambua ni kitu gani Hiki?

Dawa za nywele zinazosababisha uvimbe wa kizazi kwa wanawake

$
0
0
Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

“Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

“Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

“Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,” anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.


Zanzibar Kimenuka Tena , Bomu Lalipuka Karibu na Msikiti na Kuua

$
0
0

Mtu 1 amefariki na wengine kujeruhiwa baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu, kurushwa karibu na msikiti, darajani Zanzibar. 

Kuna taarifa ya kutokea mlipuko na mlio mkubwa mithili ya bomu umetokea maeneo ya Darajani karibu na msikiti na kujeruhi Wahadhiri waliokuwepo katika msikiti wa Darajani mara baada ya kumalizika Sala ya Isha.

Mlipuko huo unasemekana umetokea baada gari ambalo lililopita mbio na kurusha kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kwenye gari ambalo wangelitumia wahadhiri waliokuwa katika Muhaadhara ndani ya Msikiti

Kuna taarifa kwamba mtu mmoja mpaka sasa amepoteza maisha.

Flora Mbasha Avamiwa na Watu Wasiojulikana, Polisi Wamuokoa

$
0
0
SIKU chache baada ya tuhuma za ubakaji na mzozo wa familia ya mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha na mumewe, Emanuel Mbasha, mambo mengine yameibuka.

Yaliyoibuka safari hii ni taarifa kwamba, juzikati, Flora alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Tabata Kimanga jijiini Dar dakika chache baada ya yeye kuingia na gari akitokea mafichoni anakoishi kwa sasa.

Kwa mujibu wa chanzo, siku ya tukio ilikuwa  saa 9.15 alasiri ambapo Flora aliingia nyumbani kwake na kufunguliwa geti kubwa kisha kuingiza gari ndani na geti kufungwa tena.
“Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao hawatafungua,” kilisema chanzo.

Chanzo kikazidi kudai kwamba, ilibidi Flora apige simu polisi ili wafike kumuokoa yeye na familia yake.
“Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa na bunduki na kukuta wale watu wamekimbia maana walimsikia Flora akiongea na polisi kuomba msaada.

“Lakini polisi wenyewe ilibidi watumie nguvu kubwa kugonga geti na kujitambulisha ndipo akatokea Flora na kuchungulia nje kupitia dirisha dogo. Alipowaona polisi akafungua mlango,” kilisema chanzo hicho.
Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.

Alizungumza na gazeti hili baada ya tukio, Flora alisema: “Unajua kwa sasa nina hofu sana na nilihisi wale watu walikuwa wakinifuatilia kwa karibu kila sehemu, sasa naogopa kuendelea kuishi hapa, wanaweza kurudi na sijui lengo lao.”

Hata hivyo, baada ya askari hao kuondoka katika eneo hilo, Flora naye aliingia kwenye  gari lake akiwa na mdogo wake na kuondoka.
Mume wa Flora, Mbasha naye yupo mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka binti wa miaka 17 ndani ya nyumba yao huku utata ukitawala kuhusu ukweli wa tukio hilo ambalo limeigawa jamii.
GPL

Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Muda Mrefu Jack Wolper Anaswa Live Live Ndani ya Malavidavi

$
0
0
Stori: shakoor jongo
KABANG! Baada ya kutoonekana katika pozi za kimahaba kwa muda mrefu, kwa mara ya kwanza, staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’ amenaswa ‘live’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu, Risasi Jumamosi limesheheni.

Kwa muda mrefu Wolper amekuwa makini na picha zake za kimahaba tangu alipokuwa akitoka kimapenzi na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Abdallah Mtoro ‘Dallas’.

CHANZO CHAMWAGA MTONYO
Awali, chanzo makini kilipenyeza habari kuwa kuna mawasiliano yamenaswa ‘kimafia’ ambayo yalitoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki yake yakionesha anabanjuka na mwanaume huyo wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Gee.

YADAIWA NI MUME WA SHOSTI YAKE
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni mume wa mtu, mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na mawasiliano hayo yalivyosomeka.

“Mashabiki kila siku huwa wanamtetea Wolper na skendo zake, sasa nakutumia picha pamoja na ‘chating’ zake alizokuwa akichati na shoga yake kuhusiana na jamaa huyo,” kilisema chanzo hicho.

PICHA ZATUA RISASI JUMAMOSI
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wa Risasi Jumamosi alimtafuta sosi huyo na kufanikiwa kuzitia kibindoni picha hizo kisha kazi ya kuwasaka wahusika ikaanza.

Wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Gee ambaye kwa mujibu wa vyazo tofauti, ilidaiwa kuwa kwa sasa hayupo Bongo na hakuacha mawasiliano yoyote tangu alipoondoka.

WOLPER SASA!
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, paparazi wetu alimtwangia simu Wolper ambaye alieleza kila kitu:
Paparazi: Mambo vipi Wolper, nasikia makelele unaweza kusogea sehemu yenye utulivu kuna ishu nataka tuongee?

Wolper: Niko msibani na sasa hivi ndiyo zoezi la kuaga mwili, ngoja niingie kwenye gari nikupigie.
Baada ya dakika 45

Wolper: Haya niambie wangu niko sehemu nzuri.
Paparazi: Ni hivi, kuna habari imetufikia ikiambatanishwa na picha na baadhi ya chating inakuhusu wewe!
Wolper: Habari gani hiyo mbona unanitisha?

Paparazi: Kuna picha zinakuonesha wewe ukiwa katika pozi la kimalavidavi na jamaa anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu. Ukiachana na picha hizo, zimeambatanishwa chating zinazoonesha ulikuwa ukichati na rafiki yako kumueleza kuwa mwanaume uliye naye ni mume wa mtu!

Wolper: Kiukweli kabisa bila ya hata kupepesa macho hizo picha ni zangu na zimepigwa kwa kutumia simu yangu tangu mwaka juzi lakini kuhusiana na hizo chating siyo zangu hata wewe unaweza kuwa shahidi kwani mara nyingi huwa tunachati na unajua vizuri ‘floo’ yangu katika kuandika SMS.
Paparazi: Ok, sawa, lakini turudi katika suala la picha, huyu ndiyo bwana’ko wa sasa?
Wolper: Hapana, huyo ni mshikaji wangu tu na tulipiga picha hizo tukiwa baa tena kipindi kile nahamia tu Mwananyamala (Dar) na sasa hivi hata sijui huyo mshikaji yuko wapi.

Paparazi: Ina maana huna mawasiliano naye kwa muda mrefu, mtu ambaye mlipiga naye picha kimahaba namna hii?

Wolper: Kweli kabisa, sina mawasiliano naye kitambo nikimaliza tu kuongea na wewe nitamtafuta na kumuuliza kulikoni picha hizo kuvuja.

Paparazi: Si ulisema umepiga katika simu yako wewe si ndiyo wa kujiuliza kwa nini picha zimevuja?
Wolper: Nilimzawadia simu kama rafiki yangu na picha zikiwa humohumo sikuzifuta.
Paparazi: Haya Wolper ngoja nikuache mi niendelee na majukumu.
Wolper: Poa wangu baadaye nitakucheki.

WOLPER HUYUHUYU
Hii ni mara ya pili kwa Wolper kutuhumiwa kukwapua bwana wa rafiki yake. Hivi karibuni mshiriki wa Miss Tanzania 2012, Husna Maulid alilalamika kuwa Wolper kamchukulia bwana’ke aliyemtaja kwa jina moja la Rajab, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Si Wolper pekee, ‘trendi’ inaonesha kuwa mastaa wengi wa kike hasa wa filamu wamefanya ishu ya kuporana wanaume kuwa sehemu ya utamaduni katika tasnia hiyo bila kujua wanajiondolea heshima mbele ya jamii.

Kauli ya Wema Sepetu Kuhusu Penzi lake na Diamond 'Tunapenda Mpaka Tumepitiliza'

$
0
0
Wema Sepetu amesema uhusiano wake na Diamond Platnumz kwa sasa ni imara kwakuwa wamepitia mambo mengi pamoja yaliyowafunza mengi.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni akiwa jijini Durban, Afrika Kusini alikoenda kuhudhuria tuzo za MTV MAMA, Wema alisema hakuna ambacho hawajawahi kukupitia katika uhusiano wao ulioanza tangia mwaka 2014.
“Tumeexperiance good time together, bad time together, sad time, happy times. Sasa hivi tumefika point tumetulia. Tumeshaumizana, yeye kashaniumiza, mimi nilishamuumiza kwahiyo imefika point tumetulia. What we are looking for is just to make our future better na ndio maana you can see tunasapotiana kwenye vitu vingi kwasababu tayari nimeshajua kwamba he is my man, am his woman,” alisema Wema.

“Kitu ambacho kinaspice up the relationship ni kwamba tuna true love for each other, tunapendana mpaka tumepitiliza,” aliongeza.

Bibi kizee Mchawi adondoka kutoka Angani huko Jijini Mwanza

$
0
0
Kila mtu alikuwa na lake kuhusu bibi huyu anayedaiwa kukutwa akiwa uchi huku wengine wakisema ni mgonjwa wa akili na wengine wakidai ni mchawi kaanguka na ungo.

Alipokuwa akihojiwa amedai ametoka Bariadi lakini wenzie aliokuwa nao walimshusha baada ya kutokea ugomvi.

Amedai walikuwa wanne kwenye safari yao hata hivyo wapo wengine waliosema kuwa ni mgonjwa akili na tangu jana amekuwa akionekana maeneo ya hospitali ya sekoutoure akiranda randa.

Mpaka naondoka eneo hilo Polisi walikuwa wamefika ili kutoa msaada kutokana na kundi la watu waliokuwa wamemzunguka na baadhi yao wakitaka apigwe kwa madai ni mchawi.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images