Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Mahakama Nchini Kenya Imewaruhusu Upinzani Kukagua Mitambo ya Tume ya Uchaguzi

$
0
0
Mahakama Nchini Kenya Imewaruhusu Upinzani Kukagua Mitambo ya Tume ya Uchaguzi
Mahakama ya Juu nchini Kenya imeukubalia muungano wa upinzani nchini humo National Super Alliance (Nasa) kupekua sava zilizotumiwa na tume ya uchaguzi nchini humo wakati wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti.

Mahakama hiyo imesema muungano huo utaweza kusoma data kwenye sava hizo chini ya uangalizi kuhakikisha usalama wa mitambo ya IEBC hauhujumiwi.

Mgombea wa Nasa Raila Odinga amewasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee.
Mawakili wa Bw Odinga wameruhusiwa na mahakama kunakili data kutoka kwenye sava hizo kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu uchaguzi huo.

Miongoni mwa mengine, upinzani utapata utambulisho wa sava zilizotumiwa wakati wa uchaguzi, ukuta wa kinga uliotumiwa kulinda sava hizo pamoja na mitambo ya dijitali ya uchaguzi wa Kenya (KIEMS) dhidi ya wadukuzi na mfumo endeshi wa mitambo hiyo pamoja na nywila zilizotumiwa kuingia katika mitambo hiyo.
Kadhalika, wataweza kupata taarifa kuhusu yaliyojiri katika mitambo hiyo ya uchaguzi kuanzia Agosti tano hadi leo.

Aidha, wataruhusiwa kusoma nakala za Fomu 34A na 34B (fomu za matokeo katika vituo vya kupigia kura na ngazi ya maeneo bunge) ambazo zilitumiwa kutangaza matokeo.
Taarifa kuhusu mchakato wa upinzani kupekua sava na mitambo hiyo ya IEBC itawasilishwa kwa mahakama hiyo kesho jioni.
Majaji saba wa mahakama hiyo ya juu wameanza kusikiliza kesi hiyo iliyowasilishwa na Bw Odinga leo.

Kwa mujibu wa matokeo ya IEBC, Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.

Ali Kiba na Diamond Watajwa Tuzo za AFRIMA 2017 Hawa Hapa Wasanii Wengine 8 Kutoka Tanzania Waliotajwa Kwenye Tuzo Hizo

$
0
0
Ali Kiba na Diamond Watajwa Tuzo za AFRIMA 2017  Hawa Hapa Wasanii Wengine 8 Kutoka Tanzania Waliotajwa Kwenye Tuzo Hizo
Ni taarifa nzuri kwa muziki wa Tanzania baada ya Waandaaji wa All African Music Awards ‘AFRIMA’ wametangaza list ya wasanii wanaowania tuzo katika vipengele mbalimbali kwa mwaka 2017 ambazo hujumuisha Mastaa kibao katika tasnia ya muziki wa Afrika November 10-12, 2017.

Kuna jumla ya wanamuziki 33 waliotajwa kuwania tuzo mbalimbali lakini wamegawanywa katika Kanda Tano ambazo ni Afrika ya Kati, Afrika Mashariki, Afrika Kusini, Afrika Kaskazini na Afrika Magharibi huku pia kukiwa na tuzo zinazojumuisha Afrika nzima.

Muziki wa Bongofleva haujaachwa kwenye list hiyo ambapo mastaa kutoka Tanzania Diamond Platnumz, Alikiba, Darassa, Lady Jay Dee, Vanessa Mdee, Nandy, Feza, Msafiri Zawose na Topher Jaxx.

Best Female Artiste Eastern Africa
ArtisteTrackCountry
Chess NthussiGive it to youKenya
FezaWaleteTanzania
Juliana KanyomoziI am Still HereUganda
Lady JaydeeSawa Na WaoTanzania
NandyOne DayTanzania
Vanessa MdeeCash MadameTanzania
Victoria KimaniGiving You ft SarkodieKenya
Wayna WondwossenYou are not aloneEthiopia


Best Male Artist, Eastern Africa
ArtisteTrackCountry
AlikibaAje ft M.ITanzania
Diamond PlatinumzEnekaTanzania
Eddy KenzoShauri YakoUganda
Henok & Mehari BrothersFikir YishalaEthopia
Kibrom BirhaneEskista ft Nassmbu BarasaEthiopia
Mura K.EExcuse my LanguageKenya
OctopizzoTBTKenya
Sinishaw LegesseSelam EthopiaEthiopia
QritiqualMalikaKenya


Best Artist or Group in African Contemporary.
ArtisteTrackCountry
Adekunle GoldMy LifeNigeria
AlikibaAje (Ft M.I.)Tanzania
Anselmo RalphPor Favor DJAngola
BusiswaIngqondoSouth Africa
Ferre GolaKipelekieseDRC
Oumou SangareYere Faga ft Tony AllenMali
P-SquareBank AlertNigeria
Soul BangsFare Bombo MbaiGuinea
Wande CoalIskaba ft Dj TunezNigeria
WerrasonDiembaDRC


Best African Collaboration.
ArtisteTrackCountry
AlikibaAje (Ft M.I.)Tanzania (Nigeria)
BeccaNa Wash (ft Patoranking)Ghana (Nigeria)
C4 PedroLove Again (Ft Sauti Sol)Angola (Kenya)
DavidoCoolest Kid in Africa (ft Nasty C)Nigeria (South Africa)
Fuse ODGDiary (Ft Tiwa Savage)Ghana (Nigeria)
Jah PrayzahWatora Mari (ft Diamond Platnumz)Zimbabwe (Tanzania)
LockoSupporter (ft Mr Leo)Cameroon (Cameroon)
Oumou SangareYere Faga (Ft Tony Allen)Mali (Nigeria)
R2BeesTonight (ft Wizkid)Ghana (Nigeria)
ZeynabNoctambule (ft Shado Chris)Benin (Cote d’Ivoire)


Best Artist or Group in African RnB & Soul.
ArtisteTrackCountry
Ali KibaAje (Ft M.I.)Tanzania
Anselmo RalphEnsina-me a AmarAngola
C4 PedroLove Again (Ft Sauti Sol)Angola
Degg J Force 3AkolonGuinea
Diamond PlatnumzMarry You (Ft Neyo)Tanzania
MimieDance Fi YouCameroon
NoziphoAng’kakaze Ngizizwe NjeSouth Africa
Topher JaxxI Want YouTanzania
Victoria KimaniGiving You (ft Sakordie)Kenya


Best Artist in African Pop.
ArtisteTrackCountry
DaphneCaleeCameroon
Diamond PlatnumzEnekaTanzania
LockoSupporter ft Mr LeoCameroon
MimieDance Fi YouCameroon
Tiwa SavageAll OverNigeria
ToofanTere TereTogo
WizkidCome Closer  (Ft Drake)Nigeria
Yemi AladeMarry MeNigeria


Best Artist or Group in African Traditional.
ArtisteTrackCountry
BombinoAkhar ZamanNiger
Gani NdaniBiiwa YannouBenin
Hamelmal AbateHararEthiopia
Kibrom BirhaneEskista (ft Nassmbu Barasa)Ethiopia
Msafiri ZawoseAsili YanguTanzania
NobuntuWoza NganeZimbabwe
RenissMamumuhCameroon
ZoroGbo Gan Gbom (ft Flavour)Nigeria


African Fans’ Favorite.
ArtisteTrackCountry
DarassaMuziki (ft Ben Pol)Tanzania
DonaldRaindrops (ft Tiwa Savage)South Africa
EbonyPoison (Ft Gatdoe)Ghana
Kandia KoraRetirerGuinea
Nonso AmadiTonightNigeria
NyashinkiAminiaKenya
OlamidePepper Dem GangNigeria
The DoggShuukifa KwiiNamibia
Young ParisBest of Me (Ft Ben Bronfman)DRC


KASSIM MGANGA : Natumbuiza Kwenye Harusi kwa Tsh. Milioni 5

$
0
0
KASSIM MGANGA : Natumbuiza Kwenye Harusi kwa Tsh. Milioni 5
Msanii wa Bongo Flava, Kassim Mganga arigia kiasi cha fedha anachokipata kutokana na kutumbuiza kwenye harusi ukilinganisha na show za kawaida.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kitendawili’ aliyoshirikishwa na Mrisho Mpoto, ameiambia FNL ya EATV kuwa harusi moja huweza kumuingizia Tsh. Milioni 5 na anafanya hivyo kutokana kwa sasa ana band.

“Arts kama arts unatakiwa ufanye kazi na kazi zina mazingira mengi sana, mimi ninafanya vitu vingi sana, nimeanza game tangu 2005 mpaka leo. Sasa hivi nina band natumbuiza kwenye harusi kwa milioni tano,” amesema.

“Sasa thamani ya arts ambaye anatumbuiza kwenye harusi kwa kiasi cha milioni tano na arts ambaye anakwenda Morogoro kila kukicha kwa milioni moja hapo vipi?,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Kassim amekanusha taarifa kuwa yeye kujikita zaidi katika harusi kunashusha muziki wake kwa kueleza msanii anatakiwa kufanya vitu vingi.

Utakumbuka kipindi Belle 9 na G Nako wanatoa wimbo wao ‘Ma-Ole’walitangaza kuanza kazi ya kutumbuiza kwenye harusi kupitia ngoma hiyo na iwapo mteja atahitaji zaidi wapo tayari kumtungia wimbo mwingine.

VIDEO: Zari Avalishwa Pete ya Uchumba na Diamond?

$
0
0
VIDEO: Zari Avalishwa Pete ya Uchumba  na Diamond?
Ni video iliyotengeneza Gumzo kuwa Zari The Boss Lady anavalishwa Pete ya uchumba wiki hii na msanii mkubwa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anaandamwa na skendo kubwa ya kuzaa na model maarufu Tanzania Hamisa Mobetto.


Rais Magufuli Afanya Ziara Ofisi za TAKUKURU Makao Makuu

$
0
0
Rais Magufuli Afanya Ziara Ofisi za TAKUKURU Makao Makuu
Ulinzi umeimarishwa katika ofisi za makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) zilizoko Upanga, jijini Dar es Salaam huku ikielezwa kuwa Rais John Pombe Magufuli anatembelea ofisi hiyo.

Saa 3:17 asubuhi yaleo Agosti 28, msafara wenye magari yapatayo 10 uliingia katika ofisi hiyo.

Katika kuimarisha ulinzi,barabara zinazoingia kwenye ofisi hiyo nazo zimefungwa.

Hospital ya Kairuki Matatani Kwa Kusahau Vitu Tumboni Kwa Mjamzito......

$
0
0
Mkazi  wa jijini Dar es Salaam, Khairat Omary, ameishtaki Hospitali ya Kairuki na kudai fidia ya Sh milioni 155 kwa kumsababishia matatizo katika mfuko wa uzazi yaliyofanya aondolewe kizazi.
Khairat kupitia Kampuni ya Uwakili ya Jonas amefungua kesi ya madai namba 184 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na imepangwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Katika madai hayo, mdai anadai alikuwa akihudhuria kliniki wakati wa ujauzito katika hospitali hiyo na Desemba 15 mwaka jana alijifungua kwa upasuaji, akaruhusiwa Desemba 17 mwaka huo na kutakiwa kurudi tena Desemba 21.

Mdai akiwa nyumbani alianza kusikia maumivu ikiwamo kutapika, ilipofika Desemba 21 alirudi hospitali akaeleza maumivu anayopata kwa daktari ambaye alielekeza afanyiwe kipimo cha Ultra Sound.
Majibu yalipotoka daktari akampatia dawa za kutuliza maumivu na kumtaka apumzike hali itaendelea kuimarika.

“Akiwa nyumbani hali iliendelea kuwa mbaya, alisikia maumivu makali ya kichwa na alianza kubadilika rangi ambapo alikimbizwa hospitali ya jirani, walipompima wakaelekeza apelekwe Regency Hospital kwa matibabu zaidi.
“Regency walimfanyia vipimo na kubaini kuna tatizo katika mfuko wa uzazi na kumuhamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia walimfanyia vipimo na kubaini wakati alipofanyiwa upasuaji kuna vitu vilibakia kama pamba ambavyo vimesababisha mfuko wa uzazi kuharibika,” ilisema sehemu ya hati hiyo ya madai.

Anadai ili kuokoa maisha yake alishauriwa kuondolewa kizazi, hata hivyo licha ya kuondolewa alibakia na tatizo la fístula lililosababishwa na pamba zilizoachwa wakati anajifungua.

Mdai anadai kutokana na uzembe huo wa kutokuwa makini wakati wa kumzalisha anaomba mahakama iamuru alipwe Sh milioni 20 gharama za matibabu, Sh milioni 25 fidia kwa kukosa kipato wakati anaumwa, Sh milioni 80 gharama za adhabu na Sh milioni 30 fidia.

Wadaiwa wanatakiwa kupeleka utete wao mahakamani na kesi hiyo itatajwa Agost 31, mwaka huu.

Mchekeshaji Idris Sultan Amkana Wema Sepetu Live Mchana Kweupe...

$
0
0
Mchekeshaji Idris Sultan Amkana Wema Sepetu Live Mchana Kweupe...
Msanii wa filamu na mchekeshaji, Idris Sultan ameweka bayana kuwa kwa sasa hayupo katika mahusiano na mtu yeyote.

 Idris ameeleza hayo wakati wa uzinduzi wa filamu ya ‘Heaven Sent’ siku ya Jumamosi baada ya kuingia ukumbini akiwa na Wema Sepetu, jambo lilowapatia tafsiri mashabiki na wadau kuwa wawili hao wamerudiana.

Mimi siko na mtu yeyote kimahusiano, am single ,” amesema Idris pia akaongeza kuwa “Niliona amepost kuwa anataka date mie nikasema nampitia kwa hiyo sikuwa na haja ya kuomba date wala nini nikasema maana mzuri nampitia, kwa bahati nzuri nikakuta hamna mtu aliyempitaia huwenda waliokuwa anatolewa baru.”

Vile vile mchekeshaji huyo afunguka kuwa Mke haachi, hii ni baada ya kuulizwa kuwa huwa anatokaga ma mrembo huyo.

Kilombero Yapigwa Marufuku Uuzwaji Mpunga

$
0
0
Kilombero Yapigwa Marufuku Uuzwaji Mpunga
Serikali wilayani Kilombero imepiga marufuku usafirishaji mpunga kwenda maeneo mengine,badala yake waukoboe na kusafirisha mchele ili kuongeza thamani ya zao hilo.

Marufuku hiyo imeelezwa inalenga kuwawezesha wakulima kunufaika na kilimo cha mpunga, kujikwamua na umasikini na kukuza uchumi.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunjo amesema hayo baada ya kuzungumza na wadau wa kilimo cha mpunga wakiwemo wakulima kutoka wilaya za Mvomero,Kilombero,Ulanga na Malinyi pamoja na mashirika na taasisi zinazojihusishana kusaidia wakulima wa zao hilo.

Ihunjo amesema wilayani mwake wameweka vizuizi viwili kudhibiti wafanyabiashara wanaokaidi agizo hilo.

“Mpunga unaouzwa lazima uchakatwe ili kuongeza thamani jambo linalomfanya mkulima aweze kufaidika,”amesema

Tundu Lisu Apingwa Mgomo wa Mawakili Nchi Nzima

$
0
0
Tundu Lisu Apingwa Mgomo wa Mawakili Nchi Nzima
Wakili wa kujitegemea na mmiliki mwenza wa Smile Stars Attorneys, Leonard Tungaraza Manyama amepinga wito uliotolewa na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kutaka wanachama wote wa TLS kususia kwenda mahakamani kwa siku mbili.

Akiongea na waandishi wa habari Leonard Tungaraza Manyama amepinga wito huo na kuwataka Wanachama wote wa TLS kuendelea na shughuli zao kama kawaida na amewataka watendaji wa TLS kutoigeuza taasisi hiyo kama chama cha siasa au taasisi inayoendesha shughuli zake kwa mtindo wa kiharakati na badala yake kibaki kwenye majukumu yake ya kutoa huduma kama taasisi ya kitaaluma.

Aidha Manyama amesema yeye kama mwanasheria na mwanachama wa TLS, amesikitishwa na tukio la shambulizi kwenye ofisi za IMMMA Advocates na kuitaka TLS kutoa muda kwa vyombo vya dola kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Mbali na hilo Manyama amedai mawakili na wanasheria ni watumishi wa idara ya mahakama na kwamba tukio lolote la kutofanya kazi katika siku mbili hizo kutaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wa kipato cha chini ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta haki zao kwa muda mrefu, huku mpango wa kuhakikisha kesi za muda mrefu zinapunguzwa mahakamani nao ukikwama.

Leonard Tungaraza Manyama ameibuka siku moja baada ya Rais wa TLS  Tundu Lissu kuwataka mawakili kutohudhuria kwa siku mbili shughuli za mahakama Jumatatu na Jumanne kama ishara ya kulaani tukio la shambulizi lililofanywa kwenye ofisi za kampuni ya mawakili ya IMMMA    

Mkojo wa Masogange Naye Wakutwa na Chembechembe za Dawa za Kulevya

$
0
0
Mkojo wa Masogange Naye Wakutwa na  Chembechembe za Dawa za Kulevya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 28, 2017 imepokea taarifa ya Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyoonesha kuwa sampuli ya mkojo wa Agnes Gerald maarufu kama Masogange una chembechembe za dawa za kulevya.

Taarifa hiyo imepokelewa baada Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kutoa uamuzi wake ambapo amesema Mahakama imepokea taarifa hiyo na pingamizi la utetezi limetupiliwa mbali.

Pingamizi la upande wa utetezi ni kwamba fomu zilizopelekwa kwa Mkemia Mkuu hazikufuata sheria.

Hakimu Mashauri amesema Mkemia huyo Elia Mulima ambaye ni Shahidi wa kwanza ana haki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti Mahakamani.

Kuhusu hoja ya kuwasilishwa maombi ya kupimwa mkojo Masogange, Hakimu amesema ni wazi Polisi walipeleka maombi kwa Mkemia na mshtakiwa alienda akiwa chini ya askari wawili, ambapo walipatiwa kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo wa Masogange

Watu Wawili Wa Familia Moja Wamefariki Dunia Kwenye Ajari

$
0
0
Watu Wawili Wa Familia Moja Wamefariki Dunia Kwenye Ajari
Watu saba wamefariki katika ajali mbili tofauti ambapo ajali ya kwanza watu wawili wa familia moja wamepoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya gari dogo aina ya Kluger iliyotokea eneo la Masaki mkoani Pwani leo.

Majeruhi sita wa ajali ya gari ndogo iliyotokea mkoani Pwani wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani na taratibu zinafanyika ili kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi kutokana na hali zao kuwa mbaya.

Aidha watu wengine watano wamefariki dunia na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori la mzigo lililokuwa limebeba abiria mkoani Singida.
Ajali zote mbili zimesababisha vifo vya watu saba huku wengine 26 wakiwa ni majeruhi Tundu Lissu apingwa

Watu Zaidi ya 50 Wanusurika Kifo kwa Ajari ya Basi la Kampuni ya Saibaba

$
0
0
Watu Zaidi ya 50 Wanusurika Kifo kwa Ajari ya Basi la Kampuni ya Saibaba
Abiria zaidi ya hamsini wamenusurika kifo baada ya basi la abiria la kampuni ya Saibaba aina ya scania lenye namba za usajili T 131 AZZ likitokea Dar es Salam kwenda Sumbawanga, kuacha njia na kupinduka eneo la Chimala wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Mohammed Mpinga, amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 1:20 usiku Agosti 27 mwaka huu na kusababisha majeruhi watano waliolazwa kwenye hosptali ya Chimala mkoani Mbeya.

Kamanda Mpinga amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo Hussein Mkwizu(52) mkazi wa jijini Dar es Salaam, alipojaribu kulipita lori na ndipo basi likapoteza mwelekeo na kupinduka.

Pia Kamanda Mpinga ametoa wito kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani, na kwamba Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria

Bomoa Bomoa Nyingine Kutikisa Dar Yaja

$
0
0
Bomoa Bomoa Nyingine Kutikisa Dar Yaja
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), limesema wakati wowote litaendesha operesheni ya kubomoa nyumba zote zilizojengwa kando ya Bonde la Mto Msimbazi kinyume cha sheria.

Operesheni hiyo itawahusu pia wale wote waliojenga vibanda katika Bonde la Mkwajuni eneo la Magomeni wilayani Kinondoni.

Akizungumza na wanahabari leo Agosti 28 katika eneo la Mto Msimbazi, Mwanasheria Mwandamizi wa Nemc, Manchare Heche amesema watu wanaoishi katika maeneo hayo wanatakiwa kujiandaa kuondoka katika bonde hilo.

Amesema wanaoishi eneo hilo wanavunja utaratibu kwa kuwa ni sehemu hatarishi kwa maisha yao na kwamba, walishapigwa marufuku lakini baadhi wamerudi kinyemela.

"Mfano hawa wenye vibanda ambavyo vinachomoza kila kukicha katika Bonde la Mkwajuni, tulishawapiga marufuku na hapa palikuwa peupe lakini wamerudi.Sasa nawaambia wajiandae kuondoka hapa, operesheni hii itawahusu,"amesema.

Alipoulizwa bomoabomoa inaanza lini, Heche hakutaka kusema zaidi ya kusisitiza wananchi wajiandae kuondoka ili kupisha operesheni hiyo.


Masau Bwire: Goli la Yanga la Kusawazisha Dhidi ya Lipuli ni Halali

$
0
0
Masau Bwire: Goli la Yanga la Kusawazisha Dhidi ya Lipuli ni Halali
Msemaji wa timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amenukuliwa akizima mjadala wa kuhusu goli la kusawazisha la  mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara 'Yanga' dhidi ya Lipuli FC kwa kudai kuwa timu hiyo haikubebwa na goli lililofungwa ni hala

Bwire amesema anaamini bao lililofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe Donald Ngoma lilikua halali, kwani mpira ulivuka mstari wa goli na ndio maana mwamuzi aliamuru mpira upelekwe kati na sivyo kama watu wengine wanavyofikiria.
“Mimi nimeona mpira ulivuka mstari kabisa, hakuna utata wowote katika bao lile, nashangaa kuona watu wakisema Young Africans walibebwa! “Ukifuatilia vizuri ule mpira uliopigwa kwa kichwa na Ngoma, utaona dhahiri mpira ulivuka mstari, wakati mwingine wabongo wanapenda sana malumbao, na hii inatokana na ushabiki uliokithiri miongoni mwetu bila kuangalia jambo kwa umakini”, alinukuliwa
Ameongeza kuwa “Siwatetei Young Africans, ninasema kile nilichokiona katika mchezo wa jana ambao hata hivyo ulikua mzuri na wa kuvutia, kutokana na kikosi cha Lipuli kuonyesha soka safi ambalo liliwafanya wapinzani wao wasifurukute kabisa”

Idris Sultani Ampigia Saluti Joti Awataka Mashabiki Wake Wasimlinganishe Naye

$
0
0
Idris Sultani Ampigia Saluti Joti Awataka Mashabiki Wake Wasimlinganishe Naye
Mchekeshaji na Muigizaji maarufu nchini Tanzania, Idris Sultan ameweka wazi kwa kuwambia mashabiki wake waache kumfananisha na mchekeshaji mkongwe, Joti kwani kufanya hivyo ni kumvunjia heshima yake.

Idris Sultan amesema amekuwa akisikia minong’ono kutoka kwa wadau wa burudani wakimfananisha na Joti kitu ambacho yeye binafsi hakipendi kwani hadi kufikia hapa alipo ni kutokana na kujifunza kutoka kwa wakongwe wa tasnia ya uchekeshaji akiwemo Joti.

“Kuna kauli flani inasema Joti mkali kuliko Idris mara wengine wakisema Idris new generation comedy yuko vyema sana na blah blah nyingi ila tunasahau mkondo wa heshima na kuelewa kuwa Joti ni babu yangu kabisa yani kama tutasherehekea industry ya comedy naomba Joti asifananishwe na vitu vya kijinga kama mimi. Legends wapo level yao wenyewe”,ameandika Idris Sultan kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akikiri wazi kuwa kipaji cha Joti atabaki kuwa Joti na ataendelea kummheshimu siku zote.

“Narudi chini kidogo na kuinamisha kichwa naiacha heshima itutangulie na naomba nikushukuru sana Joti kwa kutuwekea mazingira uliyotuwekea wote tunaojaribu na wote wanaonifata”,ameandika Idris Sultan.

Idris Sultan ameendelea kuvuna idadai ya mashabiki nchini Tanzania kupitia kipaji chake cha uigizaji ingawaje kumekuwa na changamoto ya soko la aina ya uchekeshaji anaoufanya ‘Uchekeshaji Wima’ (Stand up Comedian).



Jeshi la Polisi Latoa Taarifa ya Awali Katika Tukio la Mlipuko Ofisi za Mawakili wa Imma

$
0
0
Jeshi la Polisi Latoa Taarifa ya Awali Katika Tukio la Mlipuko Ofisi za Mawakili wa Imma
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 26/8/2017 limetoa taarifa ya awali ya tukio la mlipuko uliotokea katika ofisi za mawakili wa IMMA zilizopo katika eneo la Upanga jijini Dar Es Salaam.

"Jeshi la Polisi linapenda kuufahamisha umma kuwa  uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kwamba usiku wa kuamkia tarehe 26/8/2017 majira kati ya saa 7:00-8:00 watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi kamili, walifika katika ofisi za mawakili wa kampuni ya IMMA (IMMA ADVOCATES) wakiwa na magari mawili wakijifanya ni askari na kuwarubuni kisha kuwachukua walinzi wa jengo hilo na kuondoka nao kwenye moja ya gari walilokwenda nalo,ambapo baadaye walinzi hao walikutwa maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui." alisema

Aidha, kundi lililobaki liliingia ndani ya Ofisi hizo na kuweka milipuko iliyotengenezwa kienyeji ambayo baada ya watu hao kuondoka ililipuka na kusababisha uhalibifu wa mali na jengo la ofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm linapenda kuwahakikishia wananchi kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu hao waliofanya tukio hilo pamoja na kujua dhamira yao ili wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.

Aidha tunapenda ifahamike kuwa wajibu wa Jeshi la Polisi ni kulinda maisha ya watu na mali zao  hivyo kamwe haliwezi kutumika kuhujumu maisha ya watu na mali za wananchi.

Tunaomba waathirika wa tukio hili na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na upelelezi wa tukio. Vilevile, tunatoa rai kwa wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia katika upelelezi waziwasilishe kwa Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi.


Ndikumana Atoa Onyo Kali Kwa Atayemuoa Iren Uoya Asema Atakayemuoa Anajitafutia Kifo

$
0
0
Ndikumana Atoa Onyo Kali Kwa Atayemuoa Iren Uoya Asema Atakayemuoa Anajitafutia Kifo
Madai ya Irene pancras Uwoya na kudai akitaka talaka yake kwa muda mrefu kutoka kwa aliyekuwa mumewe, hamad ndikumana ‘ndiku’ bila mafanikio, mwanaume huyo anaelezwa kutimiza matakwa hayo.
Inaelezwa kuwa, Ndiku aliridhia ishu hiyo huku akimpa tahadhari mwanaume atakayemuoa mwanamama huyo kuwa asipokuwa makini, basi atakuwa anajitakia kifo.

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo makini kililieleza kuwa, tayari Ndiku ameshamwandikia Uwoya talaka ya kimahakama kwa kuwa wawili hao walifunga ndoa kanisani.
“Si unajua ndoa ya kanisani huwa hakuna talaka? Ndiku ameona bora afanye utaratibu huo wa kupitia mahakamani maana huko huwa hakuna kizuizi.
“Hapa tunapoongea tayari Ndiku ameshampa talaka Uwoya kwa sababu amevumilia na kupitia kwenye misukosuko mingi wakati akiwa kwenye ndoa na mwanamama huyo.
NDIKU FULU KUJUTA

“Ndiku amekuwa akijutia namna alivyoingia mkenge, akaweka maisha yake rehani hivyo hata kama Uwoya asingedai talaka, mwanaume huyo asingeweza kumrudia tena,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Ndiku anasema sasa Uwoya yupo huru kuolewa na mwanaume mwingine lakini anamuonea huruma atakayemuoa kwani atakuwa anajitakia kifo.
HAWEZI KUSAHAU KOSA?

“Katika maisha yake, Ndiku anasema hawezi kusahau kosa alilolifanya la kumuoa Uwoya maana alijikuta katika wakati mgumu, alikonda na kuna wakati hata alitaka kujitoa uhai.
“Ni mambo mengi aliyopitia na mara nyingi huwa hataki kukumbuka maana ilibaki nukta tu afe kwa presha. Kama mtu ajui maumivu ya mapenzi, basi amuulize Ndiku.
“Ndiku anamshauri mwanaume atakayemuoa Uwoya awe na roho ngumu mno la sivyo naye atajikuta kwenye maumivu kama aliyoyapitia

“Lakini kinachomuumiza zaidi Ndiku anasema ni mtoto tu aliyezaa na Uwoya maana atakapokuwa mkubwa atadhani yeye kama baba alimtelekeza lakini ukweli ni kwamba alitengana na mkewe kwa kushindwa kuvumilia maumivu aliyokuwa anakumbana nayo,” kilitiririka chanzo hicho ambacho ni ndugu wa familia ya Ndiku aishie jijini Dar.
IJUMAA WIKIENDA NA NDIKU

Baada ya chanzo kutiririka hayo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Ndiku kwa njia ya mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo baada ya kuulizwa kuhusiana na ukweli juu ya masuala hayo yanayozungumzwa, alisema kuwa kwa miaka mingi alikuwa tayari kumpa talaka mzazi mwenzake huyo maana kilichokuwa kikimzuia kilishakwisha.
Alipoulizwa ni kitu gani kilichokuwa kikimzuia, Ndiku alisema kuwa, hawezi kueleza kwa kuwa wazazi wake wamemkataza asiseme hadharani na kwamba anawaheshimu kuliko kitu chochote ila watu wote wajue kwamba katika maisha aliyoishi na Uwoya, aliponea chupuchupu kupoteza uhai kutokana na mambo aliyokuwa akikutana nayo kwa mwanamama huyo.
KUMBE ALIKUWA TAYARI MIAKA MINGI

“Nipo tayari miaka mingi sana kutoa talaka maana kilichokuwa kinanizuia kilishaisha, kuna mtu wa mahakama nilimtuma ili akamilishe kila kitu kuhusu talaka ya Irene (Uwoya).
“Nilimwambia huyo mtu aniambie nini cha kufanya bila mimi kuja huko Tanzania (yupo nyumbani kwao nchini Rwanda) ili nimsainie hiyo talaka yake.
“Nimeponea chupuchupu na natamani niseme lakini ndiyo hivyo wazazi wangu wamenikataza na sijawahi kukataa kumpa Irene talaka,” alisema Ndiku na kuongeza:
TAHADHARI KWA MUOAJI

“Ninamtakia kila la heri atakayemuoa kwani kama hatakuwa makini atakuwa anajitakia kifo kama mimi nilivyoponea chupuchupu.”
WAMEFIKAJE HAPA?

Mwanasoka huyo wa zamani wa Rayon Sports ya nyumbani kwao, Rwanda na Uwoya walifunga ndoa mwaka 2009 na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume kabla ya kutengana mwaka 2011 ambapo wiki iliyopita mwanamama huyo alilalama kuwa anahitaji talaka ili aendelee na maisha yake mengine.
Katika kipindi chote hicho alichokuwa kwenye mgogoro na Ndiku, Uwoya aliwahi kutajwa kutoka kimapenzi na mastaa wenzake wa Bongo Movies akiwemo Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wengineo. Mbali na hao, Uwoya aliwahi kuhusishwa na ‘vitoto’ vya Bongo Fleva, Msami Baby na Dogo Janja kabla ya kutajwa kutoka na mwanamuziki wa nchini Kenya, Jaquar.



Goli Kipa wa Simba Said Mohamed Apelekwa India kwa Matibabu

$
0
0
Goli Kipa wa Simba Said Mohamed Apelekwa India kwa Matibabu
Klabu ya Simba inapenda kuwajulisha wanachama na mashabiki wake kuwa,Golikipa wake wa kimataifa,Said Mohamed Nduda amepata matatizo ya goti ambayo yamempelekea kueleka India kwa ajili ya matibabu.

Nduda aliumia mazoezini wakati timu ikijiandaa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga wiki ilipita,Matibabu hayo yatamuweka mchezaji huyo nnje kati ya wiki nne hadi sita kabla ya kujiunga tena na wenzake kwa ajili ya mazoezi na anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa wiki hii.

Klabu pia inayofuraha ,kuwaambia kuwa wachezaji wake John Bocco na Haruna Niyonzima ,ambaye alipata majeraha madogo juzi wameshaanza mazoezi na wenzao hii leo.

Huku pia Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu naye anatarajiwa kuanza mazoezi siku chache zijazo baada ya madaktari kuthibitisha uzima wa afya yake.

Mwisho,Klabu inaufahamisha umma wa watanzania kupitia vyombo vya habari kuwa taarifa zote rasmi za klabu ya Simba zitakuwa zikitolewa katika mfumo na barua hii(Heading paper)

Pia Klabu inawaomba washabiki wake kote nchini kuendelea kuiunga mkono timu yao ili iendelee kufanya vizuri kwenye ligi kuu iliyoaanza wikiendi iliyopita.


AT Anunuliwa Gari na Ali Kiba?

$
0
0
AT Anunuliwa Gari na Ali Kiba?
Msanii AT mfalme wa mduara ambaye sasa yupo nchini Marekani amefunguka na kuelezea mambo mengi juu ya Alikiba na kusema kwa muziki ambao ameachia sasa Alikiba 'Seduce me' kuwa unathamani kubwa zaidi ya gari kwake.

AT amedai kuwa kitendo cha wimbo huo kupokewa vizuri ni ishara tosha kuwa umependwa na watu wamekuwa wakielewa muziki mzuri, aidha AT amefunguka kuwa kwa sasa nchini Marekani amepata mtu ambaye anamsaidia katika muziki wake.

TFF Imeanza Kupangua Ratiba ya Ligi Kuu

$
0
0
TFF Imeanza Kupangua Ratiba ya Ligi Kuu
Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya mabadiliko kidogo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kama ifuatavyo.

Michezo ambayo imefanyiwa mabadiliko ni kati ya Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea; Azam FC na Simba, Njombe Mji na  Young Africans; Mtibwa Sugar na Mwadui FC ambayo sasa itachezwa Septemba 6, 2017.

Pia tarehe hiyo ya Septemba 6, mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Lipuli na Stand United; Singida United na Mbao; Kagera Sugar na Ruvu Shooting wakati Mbeya City na Ndanda FC .

Michezo mingine ambayo imesogezwa hadi Septemba 11, 2017 ni kati ya Azam na Kagera Sugar wakati Mbao na Tanzania Prisons utachezwa Septemba 21, mwaka huu.

Kadhalika mechi nyingine zitachezwa Oktoba 11, mwaka huu ni kati ya Mbao na Azam FC; Kagera Sugar na Mwadui; Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na Singida United.

Tarehe hiyo pia Oktoba 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Njombe Mji na Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons; Lipuli na Majimaji wakati Stand United na Young Africans watacheza Oktoba 12, mwaka huu.

Novemba 15, 2017 Mbao itacheza na Young Africans; Kagera na Mbeya City; Stand United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting; Singida na Njombe Mji; Lipuli na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda itacheza na Simba.

Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images