Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104670 articles
Browse latest View live

Trump Aagiza Vifaa vya Kijeshi Kuwekwa Marekani

$
0
0
Trump Aagiza Vifaa vya Kijeshi Kuwekwa Marekani
Rais wa Marekani Donald Trump ameondoa marufuku iliowekwa na Obama kuhusu kuwapatia maafisa wa polisi vifaa vya kijeshi.

Agizo hilo la rais sasa litawaruhusu maafisa wa polisi kupokea vifaa vya kijeshi ikiwemo magari ya kijeshi na kofia zisozoweza kuingia risasi.

Mwanasheria mkuu Jeff Sessions amesema kuwa lengo lake kuu ilikuwa kuimarisha usalama miongoni mwa raia.
Bwana Obama alilizuia jeshi kutowapatia maafisa wa polisi vifaa vyake kufuatia mgogoro wa Missouri.

Marufuku hiyo ilifuatia shutuma kwamba maafisa wa polisi walikuwa wazito kupitia kiasi kukabiliana na waandamanaji kufuatia mauaji kijana mmoja mweusi yaliotekelezwa na polisi mzungu 2014.

Rais huyo wa zamani alikuwa na wasiwasi kuhusu maoni ya raia kuhusu maafisa wa polisi waliovalia magwanda mazito ya kijeshi akisema kuwa ilikuwa muhimu kwamba maafisa wa polisi walifaa kuonekana kuwa miongoni mwa jamii badala ya kuonekana kuwa maadui.
Lakini bwana Sessions alidai kwamba hatua hiyo ya Obama ilikuwa imepita mipaka.

Jengo Maarufu la 92 Hotel Lavunjwa Kwa Amri ya Mahakama

$
0
0
Jengo Maarufu la 92 Hotel Lavunjwa Kwa Amri ya Mahakama
Jengo maarufu la 92 Hotel lililopo eneo la Shekilango, Sinza limevunjwa kutokana na amri ya Mahakama kutokana na kesi ya madai.

Watu walioshuhudia jengo hilo likivunjwa wamesema kazi hiyo ilianza majira ya saa 11 alfajiri.

Akizungumza katika eneo la tukio, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Rimina, Abdallah Bakari, amesema wao wanatekeleza kazi hiyo kutokana na amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.

Bakari amesema kabla ya kuvunja jengo hilo lenye maduka na ambalo pia linatumika kwa shughuli za ibada, walitoa notisi ya siku 14, ili kuwapa muda watu waliomo ndani wahamishe mali zao.

Hata hivyo, baadhi ya wapangaji wamesema hawakupatiwa taarifa jambo lililosababisha baadhi ya mali zao kuharibika wakati wa kazi hiyo.

       

Mshtuko na hofu Bado Afrika Kusini Katika Kisa cha Ulaji Nyama ya Binadamu

$
0
0
Mshtuko na hofu Bado Afrika Kusini Katika Kisa cha Ulaji Nyama ya Binadamu
Hofu imekumba kijiji cha Shayamoya katika jimbo la KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini, baada ya kupatikana kwa maiti ya binadamu iliyonyofolewa myama yote.

Familia ya Zanele Hlatshwayo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye ametoweka tangu mwezi Julai mwaka huu, ikiaminika kuwa ni mhasiriwa wa genge la watu walaji nyama ya binadamu, ambapo tayari watu watano wamekamatwa.

Mwili wa mwanamke huyo ambo ulikuwa umeoza, ulipatikana baada ya mwanamume mmoja kudai kuwa mganga wa kienyeji, kuamua kujisalimisha kwa polisi juma lililopita, na kukiri kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Polisi nchini Afrika kusiri awali walipuuza taarifa hiyo.

Waliamua kukubali taarifa hiyo baada ya mtu huyo kutoa mkono na mguu wa binadamu uliojaa damu kama ushahidi, hapo ndipo alipokamatwa mara moja na maafisa wa polisi.
Aliwaongoza hadi katika nyumba ya kukodishwa, ambapo polisi walipata masikio 8 ya binadamu, ndani ya chungu cha kupikia.

Inaaminika kuwa zingetumika kuwalisha wateja wakeambao wanaaambiwa yana nguvu za miujiza ya kumpa mtu pesa, nguvu na ulinzi wa kutosha.
Viungo vingine kadhaa vya mwili wa binadamu vilipatikana ndani ya mkoba.

MAN WATER: WCB Kutoa nyimbo Baada ya Ali Kiba Watapotea Tuu

$
0
0
MAN WATER: WCB Kutoa nyimbo Baada ya Ali Kiba Watapotea Tuu
Producer wa ‘Seduce Me’ Man  amezungumzia ishu ya wasanii kuachia wimbo baada ya saa chache msanii mwingine kuachia wimbo mda mchache na kusema lazima wasanii wanapoachia nyimbo zao lazima wapeane nafasi na kama wimbo uliotoka baada ya Alikiba basi hautadumu kwenye soko, utapotea.

>>>”Wasanii ufike wakati tusifanye kwa ushindani – kama upande mmoja umeshaachia wapeane nafasi kama tunataka kujenga na kutengeneza hits vinginevyo tusipoangalia tutauwa tunaziua na wasanii watapotea kwa haraka sana kwa sababu hazitokuwa kazi zaubunifu bali za kupanic.

“Kama kuna ngoma imetoka katika hali ya ushindani, nina uhakika kwamba asilimia kubwa itapotea. Siitabirii vibaya ila kuna mambo ya kujipanga ili kupeana nafasi.” – Man Water.

Mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba aliachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Seduce Me’ ambao umekuwa gumzo ambapo saa chache baadaye WCB wakiongozwa na Diamond Platnumz waliachia video yao mpya pia ‘Zilipendwa’ kitendo kilichopokelewa kwa hisia tofauti.

Young Dee Aomba Radhi Mashabiki Picha Zake za Utupu Yeye na Amber Lulu

$
0
0
Young Dee Aomba Radhi Mashabiki Picha Zake za Utupu Yeye na Amber Lulu
Rapper Young Dee amewaomba radhi mashabiki wake kutokana na picha ya utupu iliyosambaa leo mitandaoni , akiwa na Amber Lulu ambaye ndiye aliyekaa utupu.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Young Dee ameandika kwamba picha hiyo imevujishwa na watu wasiojulikana, ambayo ilikuwa na lengo la tangazo la nguo.

“Nasikitishwa kwa picha inayosambaa mitandaoni.. imevuja bila ridhaa yangu ni picha iliyokua imepigwa 'behind the scene' lengo haswa la 'photoshoot' ni aina hii mpya ya mavazi ya aina ya ki"Scortish" kama sketi. Naomba radhi sana kwa hili! na kwa mashabiki wote”, aliandika Young Dee.
Picha hiyo ambayo imesambaa kwa kasi sana kwenye mitandao ya kijamii imeonekana kushtua watu wengi kwenye mitandao, na haifai kuwekwa wazi.

MUBENGA: Ommy Dimpoz Amepoteza Dira Toka Niache Kumsimamie

$
0
0
MUBENGA: Ommy Dimpoz Amepoteza Dira Toka Niache Kumsimamie
MUBENGA aliyekuwa meneja wa msanii, Ommy Dimpoz, ameibuka na kusema kuwa tangu aache kumsimamia msanii huyo, amepoteza dira kimuziki, ndiyo maana hatoi nyimbo kwa wakati.

“Tukizungumza kwa namna ambavyo mimi nimefanya kazi na Ommy, vitu vingi vinavyomtokea sasahivi sielewi hata mimi nashangaa, kwa sababu ukiangalia hata kwenye gemu yetu hafanyi vizuri tena, sijui anakosea wapi, hata kazi zake hazina ubora na hazitoki kwa wakati.
“Nakumbuka wakati tunafanya kazi kuanzia Nai Nai, Baadaye, Ndagushima, Me and You, Tupogo, Wanjera ni nyimbo ambazo zilikuwa zinatoka kwa wakati, na mapokezi yake yalikuwa ni makubwa sana.

MUBENGA aliyekuwa meneja wa msanii, Ommy Dimpoz
Dimpoz Alivyosaini Katika Label Rockstar
“Sijui labda yeye mwenyewe anajiona wapi, lakini mimi simuoni pale ambapo nilikuwa nimemfikisha,” amesema Mubenga.

Baada ya kutemana na Mubenga, Ommy Dimpoz kwa sasa yupo chini ya menejimenti ya Rockstar, ambayo ndiyo inayomsimamia Ali Kiba.

Kamanda wa Polisi Dar Azungumza kwa Mara ya Kwanza Awataadharisha Waharifu

$
0
0
Kamanda wa Polisi Dar Azungumza kwa Mara ya Kwanza Awataadharisha Waharifu
Kamanda Mpya wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Kamishina Lazaro Benedict Mambosasa amewapa salamu watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu Jijini humo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza na Waandishi wa habari katika makao makuu ya kanda ya jeshi hilo, Kamanda Mambosasa ametamka kuwa yeye yupo kikazi zaidi na hivyo wahalifu watafute mikoa mingine ya kukimbilia na sio Dar es salaam.

Hata hivyo Mambosasa ameeleza kuwa katika kipindi chake atahakikisha Polisi wake wanafanya kazi kwa uweledi mkubwa ili kuepuka uonevu kwa Wananchi.

Aidha Mambosasa amemaliza kwa kusema kuwa yote hayo yatafanikiwa endapo wananchi watashirikiana na Jeshi la Polisi ili kupafanya Dar es salaam kuwa sehemu ya amani na utulivu.

Afande Sele Achambua Mashabiki wa Ali Kiba na Diamond

$
0
0
Afande Sele Achambua Mashabiki wa Ali Kiba na Diamond
Msanii mkongwe wa muziki, Afande Sele amefunguka kwa kudai kuwa katika utafiti wake mdogo alioufanya amegundua Alikiba ana mashabiki wengi mjini huku Diamond akidai anapendwa sana vijijini.

Wawili hao wamekuwa kwenye ushindani wiki hii baada ya kila mmoja kuachia wimbo mpya huku wimbo wa Alikiba, Seduce Me ukionekana kufanya vizuri mtandaoni.

Wasanii na viongozi wengi wa serikali wamekuwa wakitoa pongezi kwa kila msanii.

Kwa upande wa rapa Afande Sele ametoa uchambuzi mdogo kuhusu wasanii hao baada ya kuonekana kushindanishwa sana mitandaoni.

“Juzi Kati Nilipokua Kiteto Ndipo Nikasikia Habari Ya Kwamba Kiba Na Chibu Wote Wametoa Ngoma Mpya…Lkn Baada Ya Hapo Kuanzia Pale Kiteto Na Maeneo Yote Ya Vijiji Na Miji Niliyokua Napita Wkt Wa Kurudi Moro Nikawa Nausikia Wimbo Wa Chibu Tu Aliowashirikisha Wadogo Zake Ingawa Mimi Kama Mdau Wa Mziki Nilikua Ninashauku Ya Kuusikia Wimbo Wa
Kiba Pia….Nilishindwa Kuingia Mitandaoni Kuutafuta Kwakua Nilikua Naendesha Gari Muda Wote Wa Safari Hivyo Nilivumilia Hadi Nilipofika Nyumbani Ndipo Nikazama Mitandaoni Ambapo Huko

Nilishangaa Kukuta Hali Ni Tofauti Kabisa Na Ilivyo Mitaani Hasa Kule Vijijini….Wkt Huko Mitaani Habari Kuu Ni Wimbo Wa Chibu…Huku Mitandaoni Habari Kuu Ni Wimbo Wa Kiba….Hapo Nikajifunza Kitu Kwamba Inawezekana Kuwa Kiba Anakubalika Zaidi Na Watu’fulani’Wa Mjini Halafu Chibu Anakubalika Sana Na Watu Wa’kawaida’Ktk Maeneo Yote Hasa Vijijini….Kwa Kuzingatia Hilo Nikagundua Kuwa Kibiashara Na Kick Za Kijamii Chibu Yupo Vizuri Zaidi Tofaut Na Kiba Ambae Kiheshima Na Utanashati Yupo Juu Wkt Wote….Jambo Muhimu Nililoliona Kwa Wote Ni Kwamba Kila Mmoja Anakitu Cha Kujifunza Kwa
Mwenzake….Chibu Anaweza Kujifunza Utulivu…Usikivu Na Umakini Wa Hali Ya Juu Alionao Kiba Ktk Kupangilia Kazi Zake Kutoka Hatua Za Awali Mpaka Anapozitoa Hewani…Yeye Kiba Anayo Nafasi Ya Kujifunza Kuwa Timu Nzuri Ni Ile Inayofanya Usajili Mzuri Na Yenye Kufanya Mikakati Ya Ushindi…Nje Ya Mziki Ally Kiba Ni Mwanasoka Bila Shaka Anafahamu Falsafa Ya Mpira Pasi Mziki Pia Upo Hivyo…Zaidi Ya Vyote Nawapongeza Wote Kama Wadogo Zangu Na Wasanii Hodari Wa Nyakati Hizi Ingawa Nawapa Angalizo Kuwa Waendelee Kukomaa Kwani Wao Sio Wasanii Wazuri Kuliko Wote Ingawa Wanapewa Nafasi Kuliko Wote…Huo Ni Mtazamo Wangu Mimi Tu Wala Sio Sheria…Zaid Ya Hapo”Wacha Nilewe…Nilewe Tuu”….



Aunty Afunguka Sababu Ya Kuhudhulia Uzinduzi wa Filamu ya Wema Bila Iyobo

$
0
0
Aunty Afunguka Sababu Y a Kuhudhulia Uzinduzi wa Filamu ya Wema Bila Iyobo
Mrs Iyobo kwa sasa Aunty Ezekiel, ameamua kutoa ufafanuzi wa kutinga peke yake katika usiku wa kuitazama filamu mpya ya shoga yake Wema Sepetu iitwayo ‘Heaven Sent’.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyo ambaye amejulikana kupitia filamu ameeleza kuwa hakufika na waubani wake, Moses Iyobo kutokana na mtoto wake Cookeis kuugua.

“Moses hajaja kwa sababu mtoto alikuwa hayupo sawa, so nikaona sio vizuri wote tukija huku na nikisema mimi nibaki. Wema she is my friend so inakuwa sio vizuri, nikasme awacha mie nije ye abaki,” amesema mrembo huyo.

Filamu ya Heaven Sent ilizinduliwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi na mastaa kibao wahudhuria uzinduzi huo akiwema Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Steve Nyerere.



Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Lawafungia Cheka na Miyeyusho

$
0
0
Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Lawafungia Cheka na Miyeyusho
Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) limewafungia na kuwapiga faini ya Tsh. 200,000/ mabondia Cosmas Cheka na Francis Miyeyusho wakidaiwa kufanya vurugu baada ya kushindwa katika mapambano yao.


Shirikisho hilo limechukua hatua hizo kutokana na fujo zilizotokea usiku wa kuamkia jumapili katika michezo iliyofanyika ukumbi wa Vijana Social hall Kinondoni Dar es salaam.

Kutokana na kitendo hicho kamisheni imewaonya Bondia wote watakao jihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wa michezo mahali popote kuwa watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kulipa faini.

Hata hivyo TPBC imewaomba radhi kwa fujo zilizotokea na kuwaahidi kutotokea tena mahali popote.
Adhabu za mabondio hao zinatarajia kuanza kutekelezwa Septemba 5 mwaka huu.



Msuva Anatarajiwa Kuwasili Usiku wa Leo

$
0
0
Msuva Anatarajiwa Kuwasili Usiku wa Leo
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Difaa EL Jadida,  Simon Msuva anatarajiwa kuwasili nchini usiku wa leo (Jumanne) kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Botswana.

Msuva ni miongoni mwa wachezaji saba wanaocheza nje walioitwa na Kocha Salum Mayanga kwa ajili ya mchezo huo wa Septemba 2 utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru.

Leo mchana kwa saa za Morocco, Msuva ataiongoza Al Jadida kuivaa FUS Rabat katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchini 'Botola Pro League.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema mchezaji huyo ataungana na wenzake ambao wameshaanza maandalizi ya mchezo huo.

"Wachezaji wa ndani wapo na Mbwana Samatta pia amewasili, leo usiku tunamtarajia Msuva kutoka Morocco," alisema Lucas.

Wachezaji wengine wanaocheza soka nje waliotwaa ni pamoja na Orgenes Mollel anayecheza FC Famalicao, Ureno na kiungo wa Sony Sugar ya Kenya, Hamis Abdallah.

Msafara wa Mkuu wa Wilaya Karagwe Washambuliwa

$
0
0
Msafara wa Mkuu wa Wilaya Karagwe Washambuliwa
Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya  Karagwe, Godfrey Mheluka uliokuwa katika operesheni ya kuwaondoa watu wanaodaiwa kuvamia maeneo ya wafugaji katika Kijiji cha Kashanda, Kata ya Nyakahanga, umeshambuliwa na watu wasiojulikana.

Katika shambulizi hilo lililotokea leo Agosti 29 saa tano asubuhi, diwani wa Nyakahanga, Charles Bechumila amejeruhiwa na amepelekwa katika Hospitali Teule ya Nyakahanga.

Mkuu wa wilaya hiyo, Mheluka amesema bado hajawa sawa, hivyo atazungumzia tukio hilo  baadaye.

Ofisa Tarafa ya Bugene Nyaishozi, Rozaria Christian amesema walikuwa kwenye operesheni halali na wakulima hawana na taarifa.

Amesema baada ya kuwakamata wawili ndipo kundi la watu lilijitokeza likionyesha kuwa lilijiandaa kuwashambulia.

Christian amesema watu kadhaa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika kumjeruhi diwani huyo.

Shuhuda wa tukio hilo aliyekuwa kwenye msafara huo amesema baada ya kufika kijijini humo aliwakuta baadhi ya watu wakilima na walikamatwa.

Baada ya kukamatwa amesema kundi hilo la watu liliwashambulia kwa mishale na mikuki hivyo walikimbia ndipo diwani alipojikwaa na kuanguka na watu hao wasiofahamika walimshambulia kwa  kumchoma mishale na kumkata kwa panga.


   

Hii Hapa Picha Iliyomsababisha Young Dee Kuomba Radhi Mashabiki

$
0
0
Hii Hapa Picha Iliyomsababisha Young Dee Kuomba Radhi Mashabiki
Inasemekana Rapa Young Dee na Amber Lulu wanajipanga kutoa ngoma yao pamoja baada ya picha ya kimahaba yenye utata mwingi kuachiwa leo mitandaoni.

Picha hii inamuonyesha Young Dee akiwa anashanga makalio ya Amber Lulu, Ni miongoni mwa picha zitakazotoka katika photoShoot ya kazi yao mpya.




Hawa Hapa Wasanii 6 Anaowakubali Mbunge wa Nzega Bashe

$
0
0
Hawa Hapa Wasanii 6 Anaowakubali Mbunge wa Nzega Bashe
Mbunge wa Jimbo la Nzega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hussein Mohammed Bashe amefunguka na kutaja wasanii wake sita ambao anawakubali zaidi na kudai siku zote yeye ni mpenzi wa muziki wa hip hop.

Bashe amesema katika orodha ya wasanii ambao anawakubali na kupenda kazi zao ni pamoja na Roma Mkatoliki, Chid Benz, Prof Jay, Nay wa Mitego pamoja na Sugu alimaarufu kama Jongwe.
"Japo mimi ni mgonjwa wa muziki wa Hip hop ndiyo maana kwenye orodha yangu ya wasanii naowapenda yupo Roma, Chid Benz, Jay, Ney, Sugu ila Alikiba ni kielelezo cha msanii anayejua nini kinatakiwa mtu kuwa msanii, anaweza kuwa hana mafanikio kama wengine lakini huyu jamaa akiendelea hivi ana 'bright future' soko halitamchoka haongezi mashabiki kwa skendo, anakuza 'fan base' kwa muziki" alisema Bashe

Mbali na hilo Hussein Bashe aliendelea kumpa sifa Roma Mkatoliki na kusema tungo zake na muziki ambao unafanya unatosha kukupa picha uwezo wake na ni mtu wa aina gani kupitia tungo zake tu na kudai watu hawa wanastahili kulindwa.
"Nyimbo za Roma Mkatoliki zinataswira ya aina ya mtu na ubongo wake, sikiliza wimbo kama Mathematics, 2030 hawa ni watu wakulindwa na kuenziwa" alisema Hussein Bashe

Amber Lulu Nae Akana Katu Katu Kuvujisha Picha Akiwa Uchi na Young Dee...Ataka Uchuguzi

$
0
0
Baada ya kusambaa kwa picha yake chafu akiwa na Video Queen matata wa Bongo, Amber Lulu kwenye mitandao ya kijamii, hitmaker wa Ngoma ya Bongo Bahati Mbaya, David Genzi ‘Young D’, ameomba radhi kwa Watanzania kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Nasikitishwa kwa picha inayosambaa mitandaoni, imevuja bila ridhaa yangu, ni picha iliyokuwa imepigwa behind the scene, lengo hasa la photo shoot ni aina hii mpya ya mavazi ya aina ya ki”Scottish” kama sketi. Naomba radhi sana kwa hili! Na kwa mashabiki wote, inauma sana,” ameandika Young D.

Saa chache baada ya posti hiyo, Amber Lulu naye akajibu mashambulizi.
“Mimi kiukweli hakuna ninachofahamu hizo picha ni za siku nyingi kipindi cha Bongo Bahati Mbaya na hiyo picha hakuwepo kwenye hizo picha ambazo ndiyo zilistahili kutoka sasa Youngdaresalama, unasema mimi nimevujisha ili iweje, mimi sina picha hata moja wewe. Hiyo uliitoa wapi? Uliyoposti mara ya mwisho zinafanana zote za sketi au kwakuwa ndiyo Amber ameshazoeleka na vichupi kwa hiyo hata hiyo unaona ni mimi tu siyo hivyo jamani mimi sijui chochote uchunguzi ufanyike tujue usikute watu wana hasira za kufutwa (tattoo).
Naomba radhi kwa hili lililotokea sijui chochote,” ameandika Amber Lulu.
Young D na Amber Lulu waliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, lakini baadaye wakamwagana na kubaki kuwa marafiki.

Kutana na Mtatibu Wanyota za Binadamu Duniani Kote Maalim Fadhili Rashid Kutoka Comoro

$
0
0
KUTANA NA MTABIBU WANYOYA ZA BINADAMU DUNIANI KOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO

KWA SASA YUPO TANZANIA MAALIM FADHILI RASHIDI ANA IWEZO WAKUJUWA JAMBOLAKO NAKULI TATUWA KWAMUDA MFUPI

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE

MAALIM FADHILI RASHIDI NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA MIGUU KUWAKA MOTO

KISUKARI VIDONDA VYATUMBO PUMU TEZI NA UVIMBE TUMBONI PUMU ANA UWEZO WAKURUDISHA MTU ALIE POTEA KIMAZINGIRA

(MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA

KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABU MAALUM ANATOWA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA YA MASHARITI YEYOTE

NAKUMILIKI MALIZA MAJINI KWAYULE ANAE HITAJI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZA KIUME ANAYO

DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEPU KUWA NA UMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASA (24)

ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YAMVUTO WABISHARA KUUZA MALIYAKO KWA HARAKA KUZUIYA CHUMA ULETE

KUSAFISHA NYOTA NAKUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHAKUTESEKA NJOO UWONE MIUJIZA YA MAALIM FADHILI RASHIDI

CALLING+255719362806/ +255763276239

KWA WHATSAPP IMO +255785786436

Maalim Seif Atoa Mpya 'CCM Inataka Kuniua Kwa Kutumia Waganga wa Kienyeji"

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa kuna mkakati unaosukwa kuihusisha waganga wa kienyeji kutoka Naijeria, Sumbawanga, Pemba na Unguja kwa lengo la kutaka kumuua.

Maalim Seif alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho Wilaya ya Magharibi A, Unguja.



Juzi nasikia wamejaza meli ya Mapinduzi II. Kulikuwa na mkutano wa wananchi waliokuwa nje ya nchi, nadhani ni Dayaspora. Kulikuwa na mkutano uliofunguliwa na January Makamba kwa niaba ya Makamu wa Rais.

Jioni yake wakatiwa kwenye meli eti wanatembezwa kwenye visiwa mpaka mkondo wa Nungwi, meli ikasimama kwa saa mbili, ndani kuna kamati ya ufundi iliyoundwa na watu kutoka Naijeria, Sumbawanga, Pemba na Unguja, kumbe wanafanya kazi zao huku wanasema Dayaspora,” alisema Seif.

“Waganga hao wamepewa kazi nyingine, kuhakikisha wanamwondoa Maalim Seif duniani na nimeambiwa na wahusika wenyewe. Kwahiyo wenzetu kwa sasa wako hamkani hasa wakizingatia nilitoa miezi mitatu, sijui imebaki siku ngapi sasa.”

Aliwaambia wajumbe hao kuwa katika kipindi hiki watashuhudia mambo mengi ya kuzuia haki yao isipatikane lakini nguzo yao ni Mwenyezi Mungu kwakuwa hawana njia nyingine.

“Ukisimama kwenye nguzo ya Mwenyezi Mungu huwezi kuanguka. Wengine mna wasiwasi Mahakama iko upande wa Lipumba. Ninawaambia Mahakama haipo upande wowote, inatenda haki.

“Chama chetu sasa hivi kinapita katika kipindi kigumu. Kuna hujuma za Lipumba na genge lake ambao wote tunajua nyuma yake ni dola na ninyi ni mashahidi jinsi gani dola inavyomuunga mkono,” alisema Seif.

Comments

ALI Kiba 'Baraka The Prince Nimemfukuza Kwenye Lebo Yangu Rockstar Dunia Imfunze'

$
0
0
Baada ya muda mrefu wa maswali juu ya sababu iliyomfanya msanii Baraka The Prince kutoka kwenye lebo kubwa ya muziki ambayo ilimsaini ya Rockstar4000, hatimaye mmoja wa mabosi wa lebo hiyo msanii Alikiba aweka wazi kila kitu.

Akizungumza kwenye Planet bongo ya East Africa Radio alipokwenda kutambulisha wimbo wake mpya wa 'seduce me', Alikiba amesema utovu wa nidhamu ndiyo uliomfanya Baraka ashindwe kuendelea kuwepo chini la lebo hiyo.

"Baraka hayupo Rockstar, alitoka sababu za kukiuka vitu ambavyo hakutakiwa kufanya, Baraka nimemjua baada ya kuwa naye Rockstar400, lakini kiukweli sikufurahishwa na vitu ambavyo alikuwa akifanya, nadhani nilikuwa nikiona kama ni utoto lakini si utoto tena, ni kutokuwa na heshima nikaona haina haja, na mimi nikiwa kama mtu mzima sitakiwi kugombana na mtu mdogo inatakiwa umuache dunia imfunze kidogo, au kama kuna kitu ambacho amefanya au kalishwa sumu basi akapewe dawa itoke", alisema Alikiba

Alikiba aliendelea kusema kuwa msanii huyo alichukuliwa na Rockstar4000 kwa sababu waliona ana kipaji kikubwa, hivyo wakaona ni vyema kuwa ndani ya lebo hiyo.

Young Dee Afunguka Kumsweka Rumande Amber Lulu Kisa Picha za Utupu (Video)

$
0
0
Young Dee Afunguka Kumsweka Rumande Amber Lulu Kisa Picha za Utupu (Video)
Msanii wa muziki kutoka King Cash, Young Dee amedai tayari ameshamchukulia hatua za mwanzo muimbaji na video vixen, Amber Lulu baada ya kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesambaza picha chafu mtandaoni zinazomuonyesha msichana huyo akiwa mtupu huku rapa huyo akimshika makalio. Bongo5 ilimtafuta rapa huyo na kuzungumza naye sababu na kupiga picha hizo na madhara yaliyojitokeza baada ya kusambaa.

VIDEO:

Paul Makonda Awataka Watumishi Kupenda Kazi Kuliko Mshahara.....

$
0
0
Paul Makonda Awataka Watumishi Kupenda Kazi Kuliko Mshahara.....
Wauguzi na madaktari wametakiwa kuwa wavumilivu wanapotoa huduma kwa wagonjwa licha ya changamoto ambazo wanazo zipata wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.


Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alipokwenda kutembelea hospitali mpya ya mama na mtoto iliyopo Chanika wilayani ilala jijini humo.

“Wapo wakina mama ambao watakao kuja wakiwa na hasira na kukujibu majibu yasiyo mazuri , wengine utakuta wanakusonya tu bila sababu yeyote ,mwengine anweza hata kukutemea mate, basi chukulia ni moja ya sehemu yako ya kazi wala usijibizane nae”Alisema Paul Makonda.

Makonda amewataka madaktari na wauguzi hao kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kuwahudumia wote bila ya kujali rangi,sura,wala kabila na hata uwezo wa kipato chake.


Hakikisheni mnatoa huduma nzuri ili wakawe mabalozi wazuri huko kwenye makazi yao, na wakaitangaze hospitali ya chanika kuwa ni yenye kutoa huduma nzuriӀlisema Makonda.
Makonda amebaini upungufu wa madaktari ambapo amewaomba kufanya kazi kwa jitihada ili kuhakikisha mambo yote yanakwenda vizuri.

“Tunajua kama tunaupungufu wa Madaktari na wauguzi katika vituo vyetu vingi vya mkoa wetu wa Dar es salaam kwa mantiki hiyo tutalazimika kufanya kazi ngumu kidogo, kwa sababu nafasi ya mtu mmoja inapaswa kuchukua nafasi ya watu wawili au watatu, kwa wewe uliopo hapa unatakiwa kufanya kazi kama watu watatu”Alisema Paul Makonda.

Hospitali hiyo imengwa na wadau wa maendeleo kutoka Korea kusini, ambapo hospitali hiyo imekamilika kwa asilimia 100 na hivi karibuni itaanza kutoa huduma kwa mama na mtoto.
Viewing all 104670 articles
Browse latest View live




Latest Images