Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Wakazi Awapa Makavu Watu WanaomdhihakiChid Benz Baada ya Kusema Amefanya Collabo na Tupac

$
0
0
Wakazi Awapa Makavu Watu WanaomdhihakiChid Benz Baada ya Kusema Amefanya Collabo na Tupac
Msanii wa muziki wa hip hop bongo Wakazi, ameonyesha kuchukizwa na kitendo cha watu kumdhihaki msanii Chid Benz aliposema kuwa amefanya collabo na marehemu Tupac, na kusema kuwa huenda msanii huyo yuko sahihi kwenye kile alichokifanya.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Wakazi ameandika ujumbe akionyesha kusikitikishwa na watu waliomuelewa vibaya msanii huyo na kumtuhumu kuwa amerukwa na akili kwa matumizi ya madawa ya kulevya, na kusema kuwa huenda Chid Benz yuko sahihi kwani hata wasanii wa Marekani wanaamini Tupac hajafa.

Lakini pia Wakazi aliendelea kusema kuwa huenda msanii huyo ameamua kufanya hivyo ili kuzima kiki za mitandaoni zilizopo, na aweze kupata nafasi ya kuachia kazi zake.

“Inawezekana alichoongea ni ishara ya ukosefu wa akili, ila hakina tofauti na Dayna Nyange kusema Drake ni shemeji yake, au Young Dee kusema atachukua RB kwa mtu aliyevujisha picha zake za utupu alizopiga mwenyewe kwa hiari. Je, kama Chid  ameamua kutafuta kiki kwa kufanya kitu kwa hasira na kuondokana na 'seduce me/zilipendwa'?! Hilo ndio jina la mchezo, kiki halafu unafuata muziki au sio?! Hata hivyo jamii ya hip hop ya Marekani yote inasemaga Tupac yupo Cuba siyo Eminem siyo Kendrick Lamar”, alisema Wakazi.

Wakazi aliendelea kwa kusema kwamba muathirika wa madawa ya kulevya ni mgonjwa ambaye akili yake haiwi sawa, lakini kama kitendo hicho alichokifanya sio kiki na dalili ya kuhitaji msaada, basi kila mmoja anatakiwa kutoa msaada wake.


Kumbe Chid Benzi Alikua Anatania Collabo na 2Pac? Hivi Ndivyo Alivyofunguka Kwa Mashabiki Zake

$
0
0
Kumbe Chid Benzi Alikua Anatania Collabo na 2Pac? Hivi Ndivyo Alivyofunguka Kwa Mashabiki Zake
Rapa Chid Benz ambaye sasa anafanya poa na wimbo wake 'Muda' akiwa ameshirikiana na mkongwe Q Chillah amefunguka na kuwataka mashabiki wake kutosikiliza maneno ya watu na kudai wapinzani wake wamekuwa wakimuongelea vibaya kwa lengo la kumchafua


Chid Benz anasema muda mwingine kwenye maisha yake ya kila siku amekuwa ni mtu wa utani sana kiasi kwamba utani mwingine huwa hapendi hata ufike kwenye 'Camera' za watu kwa kudai unaweza kutafsiriwa ndivyo sivyo.

Rapa huyo ameibuka na kusema hayo ikiwa ni siku moja imepita toka alipotoa kauli kwamba anataka kumleta marehemu 2Pac nchini na kusema msanii huyo wa Marekani ni mzima na wala hajafa na kudai tayari wameshafanya naye wimbo.


Waislamu Milioni Mbili Waanza Ibada ya Hajj Mecca

$
0
0
Waislamu Milioni Mbili Waanza Ibada ya Hajj Mecca
Mahujaji karibu milioni mbili kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza kuwasili Saudi Arabia kwa ibada ya Hajj ambayo hufanyika kila mwaka.
Walianza machweo Jumatano kwa kuzunguka Kaaba katika Msikiti Mkuu wa Mecca, eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiislamu.

Raia wa Iran kwa mara nyingine wanashiriki baada ya kukosa Hajj ya mwaka mmoja kutokana na mkanyagano uliotokea mwaka 2015.

Kulikuwa na taarifa za kukinzana kuhusu idadi kamili ya mahujaji wanaohudhuria kutoka taifa jirani la Qatar, ambalo limekuwa kwenye mzozo mkali na Saudi Arabia.

Kamati ya Taifa ya Haki za Binadamu, ambayo inafadhiliwa na serikali ya Qatar, imesema ni raia wachache sana wa Qatar ambao wamevuka mpaka, ambao ulifunguliwa wiki mbili zilizopita na serikali ya Saudia kuwawezesha Waislamu kuhiji.


Lakini gavana wa Mecca amesema raia 1,564 wa Qatar wanashiriki ibada hiyo ya Hajj, idadi ambayo imeongezeka ukilinganisha na 1,210 mwaka jana.

Kwa Waislamu, Hajj ndiyo nguzo ya tano na ya mwisho ya dini ya Kiislamu.
Ni ibada ambayo Mwislamu yeyote aliyekomaa anashauriwa kutimiza angalau mara moja maishani mwake iwapo anaweza kulipia gharama na ana nguvu za kimwili kuweza kutimiza abada hiyo.

Serikali ya Saudia imesema imechukua tahadhari kuzuia kutokea tena kwa mkanyagano sawa na uliotokea miaka miwili iliyopita.
Maafisa wa Saudia wanasema mahujaji karibu 800 walifariki wakati wa mkanyagano huo, lakini takwimu zisizo rasmi zinasema watu zaidi ya 2,400 walifariki.
Iran pekee ilikuwa na raia 464 waliofariki na baada ya hapo iliwatuhumu maafisa wa Saudia ikisema wanafaa kulaumiwa kwa vifo vilivyotokea.
Maafisa wa Saudia walikanusha tuhuma hizo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Saudia Meja Jenerali Mansour al-Turki amesema maafisa wa usalama zaidi ya 100,000 wametumwa katika maeneo mbalimbali ya Mecca na Medina kulinda na kuwaelekeza mahujaji.
Aidha, kuna kamera nyingi sana za usalama.

DAYNA NYANGE: Natamani Kungekua na Sheria Inayowabana Wanaume Wanaokataa Mimba

$
0
0
DAYNA NYANGE: Natamani Kungekua na Sheria Inayowabana Wanaume Wanaokataa Mimba
Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange amesema anatamani kungekuwa na sheria inayowabana wanaume ambao wana tabia ya kukataa ujauzito, kwani kitendo hicho hakifai kwenye jamii.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Dayna amesema yeye kama miongoni mwa wanawake ambao wanalea mtoto bila msaada wa mzazi mwenza, anaumizwa na tabia hiyo, hivyo anatamani nchi ingeweka sheria kuwabana watu hao.

Akielezea suala hilo kwa hisia hadi machozi yakianza kumtoka, Dayna alisema "hicho kitu kinaniumiza sana, yani natamani kungekuwa na sheria fulani ikitokea tu umekataa tu mimba, bado hadi mtoto anazaliwa unakataa, upewe adhabu ambayo itakuumiza sana maishani mwako".

Dayna ambaye ana mtoto ambaye yuko darasa la 5 sasa na anapambana mwenyewe kuhakikisha anapata mahitaji yote, amesema yeye alipitia wakati mgumu mpaka alikuwa na chuki juu ya mzazi mwenzake, hali ambayo ilimfanya afunge na kumuomba Mungu ili aweze kuondoa roho ya chuki dhidi ya mzazi mwenzake, mpaka sasa wako sawa kimaelewano.


Mkuu wa Mkoa wa Zanzibar Awapost Ali Kiba na Diamond Awapa Ushauri Huu

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Zanzibar Awapost Ali Kiba na Diamond Awapa Ushauri Huu
Wakati kukiwa bado fukuto kwa mashabiki mitaani kuhusu ni Ngoma ya Nani kali kati ya Aliyoachia Alikiba 'Seduce Me' na Zilipendwa ya WCB, basi hata serikalini wasanii hao wameendelea kugawagawa viongozi, ambapo Imeonekana Posti hii ya Diamond na Alikiba kwenye ukurasa wa Instagram wa mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mahmoud iliyoambatana na ujumbe huu

"Nimeuelewa sana wimbo wa vijana wetu #wcb wakiongozwa na ndugu @diamondplatnumz hakika nimewaelewa sana kwenye wimbo wao wa #ZILIPENDWA, hii na pia nathamini kazi kubwa iliofanywa na kijana wetu ndugu yangu @officialalikiba, hakika wimbo wako ni wimbo nilio tokea kukubali.

kama kiongozi niko proud sana na kazi nzuri zinazofanywa na vijana wetu kwa kutuwakilisha vyema nje ya mipaka yetu

Ushauri wangu kwenu ni kua,tofauti zenu ziwe za kibiashara na sio vyenginevyo, #seduceme #fire#song

#teammzikimzuri" Aliandika RC Ayoub

Hospitali ya Muhimbili Yazindua Uduma ya Malipo Kwa Njia ya Kielectroniki

$
0
0
Hospitali ya Muhimbili Yazindua Uduma ya Malipo Kwa Njia ya Kielectroniki
Uongozi wa hosptali ya Muhimbili kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wa hosptali hiyo Profesa Lawrence Maseru, amezindua mfumo mpya wa malipo ya matibabu kwa njia ya kielektroniki mapema leo mchana katika hosptali hiyo.
hosptali ya Muhimbili

Akizungumza na waandishi wa habari, profesa Maseru amesema, lengo la kusimikwa kwa mfumo huo katika hosptali ya Muhimibili ni kuondoa adha kwa wagonjwa au ndugu mbalimbali wa wagonjwa kwa kukaa muda mrefu kwenye foleni za kulipia huduma mbalimbali zinazo tolewa na hosptali hiyo.
hosptali ya Muhimbili

“Dhumuni la kuja na mfumo huu kwanza kuondoa kadhia na lapsha zilizokuwepo wakati ndugu wa wagonjwa walipokuwa wakifanya malipo ya huduma mabalimbali zitolewazo na hosptali yetu. Vilevile ni kudhibiti mapato ya serilikali ambayo inawezekana kwa njia moja ama nyingine yalikuwa yakipotea,” alisema Masaju.
hosptali ya Muhimbili

Akitoa ufafanuzi namna wateja watakavyoweza kutumia mfumo huo, mkurugenzi wa fedha na mipango wa hosptali ya muhimbili Gerladi Jeremih amesema, kutakuwa na matumizi ya kadi maalumu(Muhimbili card) na kupitia mitandao mbalimbali ya simu kama Mpesa, Tigo Pesa Aitel Money nk.
“Wateja wetu watatumia kadi maalumu ambayo ataipata kutoka kwa mawakala wa Maxcom ambapo atatakiwa kujaza fedha, kisha ataelekea kwenye eneo la kulipia gharama zake za matibabu, huko atapewa mashine maalumu ambayo akipachika kadi hiyo , kiasi anachodaiwa kitakatwa na atapata risiti yake.

“Hivyo hivyo kwa watakao hitaji kulipia kwa njia mitandao ya simu, anachotakiwa kufanya ni kuchukua bili yako ya malipo na kupiga ‘menu’ ya kulipia pesa kisha unachagua kipengele cha lipa bili halafu unafuata maelekezo,” alisema Jeremiah

Mke wa Roma: Kama Roma Akitaka Kumuoa Mange Sina Shida Amuoe Tu

$
0
0
Mke wa Roma: Kama Roma Akitaka Kumuoa Mange Sina Shida Amuoe Tu
Kwenye mitandao ya kijamii August 30, 2017 gumzo lilikuwa post ya mke wa Roma Mkatoli, Mama Ivan kwenye Instagram yake baada ya kuelezea kipande cha wimbo mpya wa Roma ‘Zimbabwe’ akisema kila anapokisikia hupata wivu.

Licha ya kudai kuwandika maneno hayo kama utani huku wengi wakiyachukulia serious hadi kupelekea Mange Kimambi kuyanasa na kisha kuya post kwenye Istagram na kumuomba Mke wa Roma amruhusu awe mke mwenza ili amsaidie kumlinda Roma asiibiwe na wanawake wangine.

Mke aliandika Instagram...“Kiukweli kila nikisikiaga huu msatari napata sanaaa wivu, utani utani hivi hivi mwisho wa siku inakuwa kweli, mimi mwenyewe alinianza kiutani utani hivi hivi, yani nyie!! wanaume hawa!! Kuolewa na msanii kunahitaji moyo” – Mke wa Roma

Mke wa Roma alihojiwa na kufunguka akisema hakuwa serious bali kama Roma ataamua kumuowa Mange hatakuwa na usemi kwa kuwa mwanaume ndio mwenye maamuzi ingawa amedai hategemei kuona akioa mke mwingine kwa sababu dini hairihusu.





Wanawake Muwe na Huruma Ndugu zanguni..Tunateseka Wenzenu

$
0
0

Wanaume wakiwa kazini kubomoa nyumba hii yenye ghorofa kwa kutumia nyundo. Ni kazi ngumu na ya hatari kwa kutumia vifaa vya karne ya 10 kama sikosei.

La kusikitisha kuna huyu baba na kaka hapa akitoka jioni anaenda kukaa Bar au Kilabuni anatumia na akina Mwantumu, Siwatu, Zuena, Chausiku na Jackline.

Hawa wadada watataka simu mpya, wigi na maelfu ya shilingi za kulipia saluni. Pasipo kujali mateso anayopata huyu mwanaume hapa.

Na bado haitoshi atamwita mwanaume huyu buzi na kumnyanyasa sometime. Akina baba na akina kaka pesa mnazopata pelekeni kwa wake na watoto wenu.

Chonde chonde dada zanguni. Nawasihi msitufanyie hivyo wenzenu. Pesa tunapata kwa shida na kuhatarisha maisha yetu. Muwe na ubinadamu.

Aliyekuwa Mpinzani wa Kagame Diane Rwigara Atoweka...Ni Yule Alikuwa na Skendo ya Picha za Uchi

$
0
0
Diane Rwigara, aliyekuwa mpinzani wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwenye mchakato wa uchaguzi uliopita amepotea. Ndugu zake wamelitupia lawama jeshi la polisi wakilihusisha na tukio hilo.

Mjomba wa mwanasiasa huyo ameiambia BBC kuwa watu waliokuwepo wakati anachukuliwa wanadai alifungwa pingu na kuondoka na wanafamilia watano ambao wote walifikishwa kwenye kituo cha polisi.

Hata hivyo, msemaji wa jeshi la polisi la nchi hiyo, Theos Badege amekanusha taarifa hizo akieleza kuwa jeshi hilo halikumkamata bali linachokifanya hivi sasa ni kumtafuta.


“Hao wanasema wanapotaka wao wawepo, na kwasababu kazi yetu ilikuwa kuwatafuta ambayo ni sehemu ya uchunguzi kama nilivyosema awali, hatufahamu walipo,” alisema Badege.

Msemaji huyo wa jeshi hilo ameongeza kuwa walichokifanya ni kushikilia kompyuta na baadhi ya vifaa vya kielektroniki vya Rwigara kwa lengo la kuvitumia kusaidia uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Chanzo: BBC Swahili

Wema Sepetu Afunguka Baada ya Mahakama Kukataa Vielelezo vya Misokoto ya Bangi Aliyokutwa Nayo

$
0
0
August 31 2017 kesi ya Mwigizaji Wema Sepetu kuhusu bangi iliendelea tena kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo mpaka mwisho Mahakama hiyo ilikataa kupokea vielelezo vya ushahidi wa msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema Mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro  “Nakubaliana na hoja kwamba msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua Mahakamani“

Hiyo imekua habari njema kwa Wema Sepetu na wengine walie upande wake ambapo baada ya maamuzi hayo ya Mahakama Wema Sepetu alionekana mwenye furaha na kukumbatiana na wafuasi wake akiwemo Mama yake mzazi.

Alichokisema baada ya kutoka Mahakamani ni hiki  “nimefurahi kwasababu naona kabisa kwamba haki inatendeka, nawashukuru Mawakili wangu, tunasubiria hiyo siku September 12″

Dakika 30 za PLO Lumumba za imaliza NASA ya Odinga Mahakamani Kenya, Wanasheria wa Tanzania Jifunzeni

$
0
0
Huyu professor PLO LUMUMBA, ametumia dakika 30 tu kulegeza msimamo wa NASA na imani ya kwamba wameibiwa kura,

Amefanya hivyo mahakamani ambako kulikuwa na pingamizi la ushindi wa Uhuru Kenyatta,

Swali langu hivi kweli umahiri au uimara wa wanasheria wetu unafikia wa wakenya?

Niwe mkweli kwa ninachokiamini, Tanzania kila jambo limechanganywa na siasa, ndo maana hata weledi Hakuna.

Kwa wanaojua lugha ya kiingereza pitia video hii. Pia uwe na kamusi pembeni maana English ya PLO Lumumba haijawahi acha vichwa salama.

Maelezo kwa kifupi ya Prof Lumumba ni haya baadhi

1. Wamefungua kesi bila kuwa na hoja ya msingi iliyosababisha kesi kufunguliwa.

2. Affidavit badala ya kuwa nafsi ya kwanza umoja kwa mujibu wa sheria, yao inaonesha ni nafsi ya kwanza wingi. Haina mdai inshort.

3. Wamewasilisha hoja zenye takwimu na zenye mantiki, lkn wanaitaka mahakama ijikite kutoa uamuzi kwa kuzingatia maneno matupu(mantiki) na siyo takwimu ambazo zinaonesha odinga kapigwa.

4. Nasa walitangazia umma kuwa hata wakishindwa hawataenda mahakamani maana hawaiamini, leo wameenda kwenye mahakama ambayo wameshautangazia umma kuwa haitendi haki. Prejudice!

5. Wamefungua kesi wakidai aliyefungua kesi ni wananchi wa Kenya, wakati wananchi wa kenya walishapiga kura na kumpa ushindi mnono Uhuru. Sasa waliompa ushindi Uhuru, wanaanzaje tena kuupinga? Inaonesha siyo wakenye, bali ni kikundi cha baadhi ya wakenya wasioheshimu mchakato wa democrasia.

 TAZAMA VIDEO:

Jinsi Ya Kutoka Katika Kifungo Cha Umaskini

$
0
0
Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra.

Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani  maana ya kifungo hicho.

''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo.

Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya.

Mara kadhaa maisha yetu yamekuwa ni yale yale kwa asilimia kubwa hii ni kutokana na uongo ambao kila mmoja aweka ndani ya nafsi yake, na uongo huo huo bila kujali kama una madhara makubwa katika maisha yetu ndio tumekuwa tukiusujudu kwa namna moja ama nyingine.

Unajua binadamu huongozwa kwa asilimia kubwa na mtazamo, mtazamo huo huo umegawanyika katika makundi mawili hapa nina maanisha mtazamo chanya na mtazamo hasi.

Na pia kama unaamini katika kujifunza kama mimi utagundua ya kwamba watu wengi ambao wamefanikiwa, watu hao kwa kiwango kikubwa huwa na mtazamo chanya sana. Lakini ni kwanini watu wengi ambao hatupo katika mtazamo chanya maisha yetu daima yapo vilevile ?
Hii ni kutokana tumezoea kufanya vitu kawaida  kwa njia ile moja huku tukiamini mafanikio yanakuja kwakufanya hivyo. Kufanya hivyo ni kuendelea kujidanganya.

Wito wangu kwako kama nilivyoanza hapo juu tuache kujidanganya wenyewe kama kweli tunataka mafanikio . Huenda tangu hapo juu hadi nilipofikia hujanielewa mtu huwa anajidanganyaje? Shusha pumzi kidogo huku na mimi nikizidi kutumia halmashauri yangu ya kichwa na mamlaka ya mkono kukujuza zaidi kama ifuatavyo.

Binadamu ni kiumbe wa kujifajiri sana hata sehemu isiyo farijika unashangaa wala usishange afisa mipango nakandamiza kwa kupaka wino mweusi kwa kusema huo ndio ukweli.

Tujikite japo kwa sekunde chache japo ni nyingi kimaana katika kuuleza yafuatayo, tuangalie wafanyabiashara wangapi ambao hutumia vinywa vyao katika kuzidanganya nafsi zao ambazo huwa zinaathiri mafanikio yao kwa ujumla?
Ukijaribu kumuuliza mtu ambaye anafanya biashara kwamba biashara yake inaendeleaje? Hata kama biashara hiyo haiendi vizuri kiasi gani atakwambia biashara ni nzuri, mmh huku ndiko kujifariji kwenyewe, kwanini tusiwe wakweli wa nafsi zetu.

Hebu taangalie wale ambao ni wasomi ambao bado wanatumia kalamu zao katika kupata ujuzi zaidi, na hao hao ukiwauliza unaendeleaje na masomo hata kama anafeli kwa kiasi gani katika masomo yake utamsikia msomi huyo huyo atakwambia naendelea vizuri, aah tunakwenda wapi kwa kujifajiri kwa vitu ambavyo vimekuwa havitusaidii hata chembe zaidi kuendelea kufeli?
Siku zote tuache kujifariji kwa kuwadandanya wengine ya kwamba tunaendelea vizuri wakati uhalisia wake hauko hivo. Kuendelea kujidanganya wenyewe. binafsi ni sawa na kutumia muwa kama fimbo ya kutembea kwani utafika mahali utautafuna tu.

Inawezekana pia licha kuendelea kuidanganya nafsi yako kwa namna moja ama nyingine, umekuwa ukiitumia fimbo hiyo hiyo kuwafariji wengine na huku kufanya hivyo unahisi kutamsaidia mtu huyo kumbe ukweli na uhalisia wake haupo hivyo hata chembe.

Kuna usemi fulani ulikuja kwa ndege unaseme ''the only truth shall set you free" kwa kibantu ukiwa na maana "ukweli pekee ndio utaokuweka huru" haina haja ya  kuinua macho angani kutafakari katika kujua msemo huo maana unajieleza kabisa na upo wazi kwa maana unaeleweka kabisa.

Kuanzia sasa badili mtazamo wako kwa kuwa na fikra chanya ambayo itakufanya ujisemee ukweli, wewe binafsi na watu wengine kwani kufanya hivi kutakupa uhuru mkubwa kwa jambo ambalo unalifanya na huku matokeo ya kimafanikio yakija kwa upande wako kwa asilimia kubwa zaidi. Pia tuwakumbuke wahenga ambao wazidi kutupa hamasa kwa kusema hatma ya maisha yako unayo wewe mwenyewe.

Ni matumaini yangu makubwa unakwenda kubadilikia kuanzia sasa na mafanikio makubwa yatakwenda kuwa ukweli endapo utakwenda kuchukua hatua madhubuti zenye matokeo chanya.

USHAURI; Jinsi Ya Kuondokana Na Tabia Ya Matumizi Mabovu Ya Fedha Na Kuweza Kujiwekea Akiba

$
0
0

Mambo yote kuhusu fedha yanaanzia kwenye misingi miwili muhimu kuhusu fedha. Misingi hii ni mapato na matumizi. Kila kitu kuhusu fedha, iwe ni kuishiwa, kuwa masikini, kuwa tajiri na hata kuwa na akiba na kuwekeza kutaanza na misingi hiyo miwili, mapato na matumizi. Matatizo yote ya kifedha na hata mafanikio yote ya kifedha yanaanza na misingi hiyo miwili, wale wanaoweza kuisimamia vizuri wanapata mafanikio na wanaoshindwa wanaishia kuwa na changamoto za kifedha.

Karibu rafiki kwenye kipengele chetu cha USHAURI WA CHANGAMOTO mbalimbali ambazo zinatuzuia kufikia mafanikio tunayotaka kwenye maisha yetu. Kupitia kipengele hiki, wewe msomaji unaniandikia changamoto yako na mimi naijadili na kukushauri njia bora za kuondokana na changamoto hiyo. Kujua jinsi ya kutoa changamoto yako ili ushauriwe soma makala hii mpaka mwisho.

Leo katika kipengele hiki tutakwenda kujadiliana na kushauria kuhusu matumizi mabovu ya fedha ambayo yanawafanya watu kushindwa kuweka akiba na hivyo kubaki kuwa masikini. Karibu twende pamoja kwenye makala hii ya leo na mpaka kufika mwishoni utakuwa umepata mwanga wa hatua gani za kuchukua ili uweze kudhibiti matumizi yako na hatimaye kuweza kuweka akiba na hii kukufikisha kwenye uhuru wa kifedha.

Kabla hatujaingia kwenye kujadili mada ya leo, tupate maoni ya msomaji mwenzetu ambaye alituandikia kuomba ushauri juu ya changamoto hii ya kifedha;

Nikiwa na pesa mfukoni nikiona kizuri chochote na kununua bila kujali sina pesa nyingine ya akiba Na hatakama ninayo nyumbani nawaza kwenda kuichukua niwe nayo mfukoni. Naomba ushauri niondokaneje na hali hii.

Kama ambavyo tumesoma kwenye maoni ya msomaji mwenzetu hapo juu, tatizo lake ni kushindwa kudhibiti matumizi yake, badala ya yeye aiendeshe fedha, fedha imekuwa inamwendesha yeye.
Hili ni tatizo ambalo linawasumbua watu wengi, na limekuwa linawazuia wengi kufikia ndoto zao za kuwa na uhuru wa kifedha. Mtu anakuwa na mipango mizuri sana kabla hajapata fedha, ila akishazishika ile mipango yote inafutika na kujikuta anazitumia hovyo. Zikishaisha ndiyo anaanza kukumbuka kwamba alikuwa na mipango ya kifedha ambayo hajaitimiza.

Ni rahisi kuona hili kwa wengine kuliko kwetu binafsi, nenda popote na utakuta watu wakimzungumzia mtu ambaye amepata fedha nyingi kwa wakati mmoja, labda fedha za urithi au fedha za mafao, utasikia watu wakisema anatumia fedha vibaya. Lakini watu hao hao wape fedha na wataonekana wanatumia vibaya.

Fedha zimekuwa na changamoto nyingi sana kiasi ambapo zimewachanganya wengi, mpaka wengine wakaishia kuzipa majina mabaya. Na wengine wamekuwa wakiamini labda kuna nguvu zisizo za kawaida ambazo zinawaibia fedha zao. Hapa ndipo utakutana na watu wanakuambia kuna chuma ulete anawaibia fedha zao. Ukweli ni kwamba hakuna chuma ulete anayechukua fedha za mtu, bali mtu mwenyewe ndiye anakuwa chuma ulete wa fedha zake mwenyewe. Kama kungekuwa na mtu mwenye uwezo wa chuma ulete, asingehangaika na fedha ndogo ndogo za watu, badala yake angeenda kuchukua fedha nyingi benki kwa nguvu zake zisizo za kawaida.

Kama nilivyosema mwanzoni kwenye utangulizi wa makala yetu hii ya leo, changamoto zote za kifedha zinaanzia kwenye misingi miwili mikuu, mapato na matumizi.

Mapato ni ile fedha ambayo inakuja kwenye mfuko wako. Kitu chochote ambacho unafanya na watu wakakulipa ni njia yako ya kujipatia kipato. Na matumizi ni kile ambacho kinaondoka kwenye mfuko wako. Kitu chochote unachofanya kwa kutumia fedha yako ni matumizi.

Masikini wote kanuni yao iko hivi, matumizi yanakuwa makubwa kuliko mapato. Kwa njia hii wanaishi kwa madeni na hawawezi kuweka akiba yoyote. Wengi wanaishi kwa mkono kwenda kinywani, yaani chochote wanachopata wanakitumia.

Matajiri wote kanuni yao ni hii; mapato ni makubwa kuliko matumizi au matumizi ni madogo kuliko mapato. Kwa njia hii wanaweza kuweka akiba na kuwekeza, kitu ambacho kinawawezesha kupata zaidi na kufikia kwenye utajiri.

Kuna njia tatu za kutumia kanuni ya mapato na matumizi. Njia ya kwanza ni kuongeza mapato, njia ya pili ni kupunguza matumizi na njia ya tatu ni kufanya vyote kwa pamoja, kuongeza mapato na kuongeza matumizi.

Leo katika kumshauri msomaji mwenzetu tujikite kwenye kupunguza na kudhibiti matumizi. Hizo njia nyingine tutazijadili wakati mwingine.

Je unawezaje kudhibiti matumizi yako na kuweza kujiwekea akiba?
Hili ndilo swali ambalo tunahitaji kujiuliza ili kuweza kuondokana na matumizi mabaya, matumizi yanayotokana na msukumo wa hisia au mihemko. Hapa tutaangalia mambo muhimu ya kuzingatia ili kuweza kudhibiti na kupunguza matumizi ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha.

Kwanza jua matumizi yako kwa sasa ni yapi. Unaweza kujua matumizi yako kwa kuorodhesha kila kitu unachofanya kwa kutumia fedha yako. andika kila shilingi ambayo umetumia kwenye siku saba zilizopita. Na kama huwezi kukumbuka vizuri fanya zoezi hili kwenye siku saba zijazo. Kila siku andika matumizi yako yote ambayo umeyafanya, hata kama umetumia shilingi mia tano au mia moja iandike. Usiache chochote. Wakati unafanya zoezi hili usijihukumu kwa lolote, wewe andika kila shilingi ambayo umeitumia.

Baada ya kujua matumizi yako ya kifedha, pitia orodha yako na kata yale matumizi ambayo siyo muhimu kwako. Na umuhimu upime kwa kigezo hiki, kama hutakufa kwa kukosa matumizi hayo basi siyo muhimu, yakate. Kwa njia hii kata kila matumizi ambayo kwa kuyakosa hutaharibu afya yako wala mahusiano yako na wengine. Kwa mfano sijawahi kusikia mtu kafa kwa kutokunywa soda, au kwa kutokununua nguo mpya, au kwa kutokununua gazeti. Vitu vingi vya anasa vitaondoka kwenye orodha yako hiyo.

Ukishaondoa yale matumizi ambayo siyo muhimu, sasa unabaki na orodha yako ya matumizi muhimu, haya ndiyo utakayoyafanya pekee.

Sasa hili zoezi haliishi kirahisi hivi, kuna changamoto nyingi hasa pale manunuzi yanapotokana na msukumo wa kihisia, na ili kuondokana na msukumo huu fanya yafuatayo;

1. Usitembee na kiasi kikubwa cha fedha kwa wakati wowote.
Hivyo pia usiwe na kiasi kikubwa cha fedha ambacho unaweza kukifikia kwa haraka kama vile benki au kwenye mpesa/tigo pesa. Badala yake fanya zoezi la kupata fedha kuwa gumu sana kwako, kwa mfano fungua akaunti maalumu ya benki ambayo hutaomba kuwa na kadi ya atm wala huduma za kifedha. Maana yake ukitaka fedha ni lazima uende mpaka benki, upange mstari ndiyo uchukue fedhga. Na fedha hizi zikishakua kidogo ziondoe na wekeza sehemu ambayo huwezi kuziondoa haraka.


2. Chelewesha manunuzi yako kwa muda.
Mara nyingi watu wamekuwa wakikutana na kitui na kushawishika kununua, huenda kwa mwonekano au maneno ya muuzaji. Lakini wanapofika nyumbani wanagundua kitu kile hakikuwa muhimu kwako. Hii huwatokea sana wakina dada na wakina mama hasa kwenye mavazi. Kuondokana na hali hii chelewesha manunuzi yako. Pale unapohitaji kununua kitu, jikubalie kwamba utanunua, lakini usinunue muda huo, badala yake jipe angalau siku saba za kufikiria kama kweli unataka kitu hiko. Ikiwezekana jipe hata siku 30. Ukifikiria kwa siku hizo utashangaa vitu vingi utasahau hata kama ulikuwa unataka kununua. Na hapa unahitaji kuwa na tahadhari kwa sababu wauzaji wengi ni wajanja na wanajua njia ya kukusukuma ununue muda huo, wanakuambia ni ya mwisho na hutapata tena, au bei itapanda, siyo kweli usiwasikilize, utakapohitaji utapata tu.

3. Jiwekee ukomo wa vitu unavyohitaji.
Hasa kwenye mavazi au starehe. Matumizi ya aina hii usipokuwa na ukomo utajikuta matumizi yanaongezeka kila siku. Kudhibitio hili kuwa na ukomo ambao huwezi kuuvuka. Kwa mfano kwenye mavazi jiwekee ukomo kwamba hutanunua nguo mpya mpaka uwe umeshavaa zile zote ambazo unazo kwa sasa.

4. Yatumie matumizi yako kama hamasa ya kuongeza kipato.
Njia nyingine ya kudhibiti matumizi yako ni kuyatumia kama hamasa ya kuongeza kipato chako. Na hapa unachofanya ni pale unapoona kitu ambacho unataka kununua, jiambie utanunua kitu hiko kama utaweza kutengeneza fedha za ziada, tofauti na ulizonazo sasa. Na hapa iweke akili yako kazini ili kukuonesha njia mbadala za wewe kupata fedha za kununua kile unachotaka. Kwa njia hii utaacha matumizi hayo kama hutapata kipato cha ziada, na kama utakipata basi utakuwa umejiongezea njia za kipato.

5. Kula nyumbani badala ya kula kwenye migahawa, nunua vitu vya jumla badala ya kununua kwa reja reja.
Haya pia ni mambo ambayo yanakuwezesha kupunguza gharama zako za maisha hasa pale unapokuwa na familia. Badala ya kula vyakula vya kununua, ni vyema mkapika na kula nyumbani. Na badala ya kununua vitu kwa reja reja, nunua kwa jumla, hii siyo tu inapunguza gharama, bali inakuondolea usumbufu wa matumizi madogo madogo ya kila siku.
Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kuhusu kudhibiti na kupunguza matumizi ili uweze kufikia uhuru wa kifedha.

Bombadier ije ianze Kufanya Daladala ili Tulipe Deni la Watu Pole Pole- Rungwe

$
0
0
Bombadier ije ianze Kufanya Daladala ili Tulipe Deni la Watu Pole Pole- Rungwe
Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma), Hashim Rungwe ameibuka na kumtetea Tundu Lissu kwa kile alichofanya kutoa taarifa juu ya ndege ya Tanzania kuwekwa kizuizini Canada na kusema ametumia haki yake ya kikatiba ya kutoa habari kuhusu sakata hilo.

Rungwe amezidi kuwashangaa watu ambao wanasema Tundu Lissu siyo mzalendo kwa kuwa alitoa taarifa hiyo na kusema uzalendo siyo kuficha  au kufanya siri ya mambo yanayohusu maisha ya Watanzania na kudai ni bora watu wajue ili mwisho wa siku hata maisha yanapokuwa magumu wajue kuwa zile fedha za Umma zimechukuliwa kwenda kulipa deni hivyo watu wafunge mkanda.

Aidha Rungwe ameitaka serikali kufanya mazungumzo na watu hao japo waweze kuwapunguzia au hata kama kulipa kwa awamu ili mwisho wa siku ndege hiyo iweze kuja Tanzania na kuanza kufanya safari zake.

"Kesi ile imefikia katika hatua ya mwisho kabisa ya utekelezaji, wanasheria wana mbinu nyingi wanaweza kufanya jambo wale watu ambao ni wadai wakaelewa angalau kutupunguzia tukapata kanafuu fulani au tukalipa hata kwa awamu ni nafuu ndege yetu ikaja ikaanza kufanya daladala yake hapa na kupeleka watu hapa na pale kuokoteza hata hizo senti inaweza kujilipa yenyewe ila ukitumia utemi utemi si kila kitu unaweza kutumia utemi" alisema Rungwe.

 VIDEO:

Kutana na Mtatibu Wanyota za Binadamu Duniani Kote Maalim Fadhili Rashid Kutoka Comoro

$
0
0
KUTANA NA MTABIBU WANYOYA ZA BINADAMU DUNIANI KOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO

KWA SASA YUPO TANZANIA MAALIM FADHILI RASHIDI ANA IWEZO WAKUJUWA JAMBOLAKO NAKULI TATUWA KWAMUDA MFUPI

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE

MAALIM FADHILI RASHIDI NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA MIGUU KUWAKA MOTO

KISUKARI VIDONDA VYATUMBO PUMU TEZI NA UVIMBE TUMBONI PUMU ANA UWEZO WAKURUDISHA MTU ALIE POTEA KIMAZINGIRA

(MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA

KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABU MAALUM ANATOWA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA YA MASHARITI YEYOTE

NAKUMILIKI MALIZA MAJINI KWAYULE ANAE HITAJI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZA KIUME ANAYO

DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEPU KUWA NA UMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASA (24)

ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YAMVUTO WABISHARA KUUZA MALIYAKO KWA HARAKA KUZUIYA CHUMA ULETE

KUSAFISHA NYOTA NAKUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHAKUTESEKA NJOO UWONE MIUJIZA YA MAALIM FADHILI RASHIDI

CALLING+255719362806/ +255763276239

KWA WHATSAPP IMO +255785786436

Humphrey Polepole "CCM Hatupo Tayari Kutoka Kwenye Reli"

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amewataka viongozi wa vyama siasa kuacha tabia ya kufikilia vibaya Mahakama kuwa haiwatendei haki pindi wanapokuwa na kesi zao Mahakamani.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole.
Polepole ameeleza hayo baada ya kushinda kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu ya mwaka 2015 kwa upande wa Ubunge katika jimbo la Longido  Mkoani Arusha ambalo lilikuwa likigombewa baina ya  Dkt. Steven Kiruswa kutoka CCM na Onesmo Nangole kutoka CHADEMA.

"Sisi kama chama cha Mapinduzi tumepokea uamuzi huo kwa faraja kubwa kwa sababu hivi karibuni kulikuwa na maneno kutoka kwa waakilishi wa vyama vya siasa vingine siyo vyote. Ambavyo vyenyewe huwa vinaamini kuwa Mahakama ikitoa haki kwao inakuwa imewatendea haki ila Mahakama ikitoa haki kwa wengine inakuwa haitendi haki. Sisi kama Chama cha Mapinduzi tunaamini Mahakama ipo pale ilipo kwa ajili ya kutenda na kutoa haki za watu wetu", alisema Polepole.

Aidha, Polepole amesema kwa upande wao wanaheshimu uamuzi uliyotolewa na Mahakama huku wakiomba Mahakama iendelee kufanya hivyo kila siku bila ya kujali itikadi ya chama husika.

"Kwa hiyo sisi huwa tunaheshimu uamuzi wa Mahakama na kwa uamuzi ambao umefanyika leo wa kutengua matokeo ya uchaguzi wa Ubunge katika jimbo la Longido, siyo tu kuwa umetupa faraja lakini sisi tunapenda kutoa rai kwa Mahakama iendelee kufanya kazi zake vizuri kwa uhuru, haki na isisikilize kelele za watu ambao huwa wanapenda Mahakama iseme nini ili ionekane inatenda haki. Kwa hiyo tutoe pongezi zetu kwa wananchi wa Longido na wana CCM kwamba madai yao ya haki kwamba Mahakama imeyathibitisha. Tuendelee kufanya siasa safi na tutoe uongozi bora lakini hatutakuwa tayari kuondolewa kwenye mstari, reli ya kutoa maendeleo kwa Watanzania", alisisitiza Polepole.

Kwa upande wake, Dkt. Steven Kiruswa amesema kwa mara ya nne Mahakama ya Tanzania imeweza kudhihirisha kwamba inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na inajali kuhakikisha haki haipotei kwa muhusika.

Kwa mara ya kwanza kesi ya kupinga matokeo ya jimbo la Longido  mkoani Arusha Novemba 11 mwaka 2015, majuma mawili kuisha tokea kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliyofanyika Oktoba 25, 2015 ambapo Mahakama Kuu ya Arusha kwa mara ya kwanza ilibaini kuwa uchaguzi wa jimbo hilo haukuwa wa haki na kufikia June 6 mwaka 2016  Mahakama iliweza kutoa hukumu na kutengua Ubunge wa Onesmo Nangole na kupelekea jimbo hilo kuwa bila ya Mbunge yoyote kwa kipindi chote hicho kwa kuwa chama pinzani walikataa kurudia uchaguzi.


Rugemalira wa Escrow Agonga Mwamba Mahakama ya Mafisadi

$
0
0
Mshtakiwa wa kesi ya uchotaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, James Rugemalira amegonga ukuta katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi) baada ya kunyimwa dhamana.

Rugemalira ambaye anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, yenye mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana, alikimbilia mahakamani hapo kuomba afutiwe mashtaka ya utakatishaji fedha kisha aachiwe huru kwa dhamana kwa madai hati ya mashtaka yanayowakabili ina kasoro za kisheria.

Jana, Jaji Mfawidhi Firmin Matogolo alitupilia mbali maombi hayo akisema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpa nafuu alizokuwa akiziomba.

Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, jopo la mawakili wa Rugemalira waliieleza Mahakama kuwa hati ya mashtaka haina maelezo yanayoonyesha kosa la utakatishaji fedha.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Dk Zainabu Mango alipinga hoja hizo, akidai mashtaka yanayomkabili mshtakiwa hayana dhamana.

Akijibu hoja ya kasoro za hati ya mashtaka, Wakili Mango alidai maombi hayo yamepelekwa kwenye jukwaa ambalo si sahihi.

Alisema kesi hiyo haijafikia hatua ya kusikilizwa katika mahakamani hiyo na kwamba inaweza kuangalia uhalali wa mashtaka hayo, shauri hilo litakapohamishiwa mahakamani hapo kwa usikilizwaji.

Hata hivyo, Jaji alikubaliana na hoja za Wakili Mango kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kuchunguza uhalali wa hati ya mashtaka kwa kuwa suala hilo limefikishwa wakati ambao si muafaka.

Pia, Jaji Matogolo alisema kwamba Mahakama hiyo huwa na mamlaka ya kuchunguza uhalali wa mashtaka endapo maombi yangewasilishwa kwa njia ya mapitio na si dhamana.

Rugemalira na mshirika wake wa Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Singh Sethi wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Lusekelo Anthony 'Mzee wa Upako' Atoboa Siri...Adai Mwanaume Ukifanya Hili Kwa Mwanamke Hata Kaa Akuache

$
0
0

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar es Saalam, Lusekelo Anthony 'Mzee wa Upako' amefunguka na kuwashauri wanaume kuwa katika vitu ambavyo vinajenga ndoa na kuimarisha ndoa ni pamoja na mwanaume kuwa na makazi ya kudumu.

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar es Saalam, Lusekelo Anthony 'Mzee wa Upako

Mzee wa Upako alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha UJENZI kinachoruka kila Jumapili na kusema wanawake wanaojitambua na kujiheshimu tofauti na wale wasiojitambua na kujielewa basi wanaweza kumuheshimu sana mwanaume pindi mwanaume huyo anapojenga nyumba na kuwa na mji wake wa kudumu.

Mtatiro: Msajili Anataka Kubadili Sheria ili Awe na Mamlaka Ndani ya Vyama Lengo Kuua Upinzani na Kuweka Mamluki

$
0
0
Nimeiona Barua kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuvitaka Vyama vya siasa vitoe maoni kuhusu utungwaji wa Sheria Mpya ya Vyama vya Siasa. Nilijua kwamba jambo hili lingefuata. Serikali inachukua hatua hii wakati huu ili kubariki "UJINGA" wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa siku za usoni.

Lengo kubwa kuliko yote ni kuweka kipengele kitakachoeleza kuwa "Msajili wa Vyama vya Siasa anaweza kuingilia mambo ya ndani ya vyama vya siasa na kwamba uamuzi wake utakuwa wa mwisho."

Yaani, kumlinda mtu mmoja, LIPUMBA, ili aimalize CUF, kunafanya hadi sheria zibadilishwe haraka ili AIBU zinazofanywa na Msajili zilindwe.

Tumewahi kuwaeleza huko nyuma mara kadhaa, kwamba Mahakama Kuu imewahi kutamka bayana katika maamuzi mbalimbali, kuwa "Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya vikao vya vyama vya siasa kwa njia yoyote ile."

CUF ilipoanza kupigwa vita na LIPUMBA akiwa mtumiwaji mkuu, wapo watu walitucheka. Tuliwaambia shambulio dhidi ya CUF ni shambulio dhidi ya demokrasia.

Tusubiri wapitishe hiyo sheria yao, uone vyama vitakavyoporwa uhuru wa ndani. Na huko ndiko CCM inapenda twende, maana yanyewe haiwezi kuguswa na Msajili ambaye obvious anateuliwa na Mwenyekiti wa CCM.

#NOTE; Hata ikitungwa sheria hii hivi sasa, mashauri ya CUF yaliyoko mahakamani yatatumia viwango vya mamlaka ya msajili yaliyotajwa kwenye Sheria Namba 5 ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 (sheria ya sasa).

#Kama mngekuwa na akili mngetunga sheria ya kuhimiza ujenzi wa kiwanda kimoja kikubwa kila kata. Lakini mko likizo!

Mtatiro J

Diamond Platnumz Atajwa Mtanzania Pekee Kwenye List ya 100 Most Influential Young Africans

$
0
0
Diamond ndo mtanzania pekee alietajwa kwenye 100 most influential young Africans 2016 katika list iliotoka Leo katika kipengele cha sports and entertainment.
Kutoka East Africa, Uganda amechomoza Anna kansiime, huku Kenya wakichomoza lupita nyong'o na mtangazaji wa focus of Africa kutoka BBC anaitwa Sophie ikenye


Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images