Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Rais Kenyatta Aijia Juu Mahakama kwa Kubatilisha chaguzi

$
0
0
Rais Kenyatta Aijia Juu Mahakama kwa Kubatilisha chaguzi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amelitaja jopo la majaji wa mahakama ya juu liliobatilisha uchaguzi wake wa urais kuwa 'Wakora'

Awali alikua ametaka kuwepo na utulivu na kusema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama lakini baadaye akaonyesha msimamo tofauti katika mkutano wa hadhara.
Mahakama hiyo ilisema kuwa uchaguzi wa mwezi uliopita ulikumbwa na udanganyifu na kuagiza kufanyika kwa uchaguzi mwengine katika kipindi cha siku 60.
Uchaguzi huo uliokuwa umezua wasiwasi wa kutokea kwa ghasia za baada ya uchaguzi kama zile zilizotokea 2007.

Ijapokuwa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi uliopita hazikufikia kiwango cha 2007, ghasia za siku kadhaa zilisababisha vifo vya watu 28.
Tume ya uchaguzi nchini Kenya ilikuwa imemtanfaza rais Kenyatta kuwa mshindi kwa kiasia cha kura milioni 14 lakni matokeo hayo yakapigwa mahakamani na mpinzani wake mkuu Raila Odinga.

Katika hotuba aliyotoa katika runinga, rais Uhuru kenyatta alisema kuwa ni muhimu kuheshimu sheria hata iwapo unatofautiana na uamuzi wa mahakama ya juu.Alitaka kuwepo kwa utulivu akisema: Jirani yako ataendelea kuwa jirani yako licha ya lololote litakalotokea.
Ujumbe wangu muhimu leo ni Amani. Lakini alikuwa na msimamo mwengine wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika soko moja jijini Nairobi.
Raila Odinga akifurahia uamuzi wa mahakama uliofutilia mbali uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta  

Raila Odinga akifurahia uamuzi wa mahakama uliofutilia mbali uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta
Aliwatyaja jaji Maraga na majaji wenzake kua wakora, akisema aliamua kubatilisha uchaguzi wake.
Aliomuonya jaji Maraga kwamba baada ya uchagyzi huo kufutiliwa mbali bado yeye ndio rais na sio tena rais mteule kama ilivyokuwa.

Munanielewa? Maraga anafaa kujua kwamba hivi sasa anakabiliana na raius aliye mamlakani , alisema bwana Kenyatta mwenye umri wa miaka 55.
Tunawaangalia kwa karibu.Lakini wacha tumalize uchaguzi mwanzo,Hatuogopi.
Kufuatia uchaguzi huo waangalizi wa kimataifa kutoka muungano wa Ulaya , ule wa Afrika pamoja na wale wa Marekani walikuwa walisema kuwa hakuna udanganyifu uliofanyika na kumtaka Odinga kukubali kushindwa.


Mbunge wa Mteule wa CUF Kuzikwa Kesho

$
0
0
Mbunge wa Mteule wa CUF Kuzikwa Kesho
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya amesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko kifo cha Mbunge mteule wa Viti Maalum Hindu Mwenda

Hindu alifariki dunia ghafla jana nyumbani kwake Kibada Kigamboni na anatarajiwa kuzikwa kesho saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala,  Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, leo Jumamosi Septemba 2 Sakaya amesema  Hindu alikuwa ni mpambanaji  na mtu mwenye kukijenga chama hicho  kuanzia miaka ya 90  hivyo ni pigo kubwa kuondoka kwake.

‘’Hata ukifika  Tabora leo hii hakuna mwanachama wa CUF asiyemjua Hindu’ ’amesema Sakaya.

“Sijui niseme nini maana zilikuwa zimebaki siku chache tu aende Dodoma kuapishwa baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwezi uliopita,” amesema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua Tabora.

Ruto Ataka Tarehe Mpya ya Uchaguzi Kutangazwa Kenya

$
0
0
Ruto Ataka Tarehe Mpya ya Uchaguzi Kutangazwa Kenya
Naibu rais wa Kenya , William Ruto, ameiambia tume ya uchaguzi ya Kenya kutaja rasmi siku ya kurudiwa kwa uchaguzi wa urais nchini humo.

Hii ni baada ya hatua ya Ijumaa ya mahakama ya juu zaidi kubatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta , wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita , ikisema kulikuwa na dosari kubwa zilizokiuka katiba ya Kenya.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliyeusifu uamuzi huo wa mahakama, papo hapo alishtumu vikali tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC na pia kuwalaumu waangalizi wa kumataifa kwa kile alichokitaja ' kuhalalisha udanganyifu uliotokea na kutaka uchunguzi zaidi ufanyike.
Mahakama yafutilia mbali ushindi wa Kenyatta

Amewataka waliohusishwa na udanganyifu huo kujiuzulu , kufutwa kazi na hata kuchukuliwa hatua za kisheria wakisema kamwe hawawezi kuaminiwa kusimamia uchaguzi ujao.
Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta amesema japo anauhesimu hakubaliani na uamuzi huo uliofutilia mbali ushindi wake na kwamba yuko tayari kwa marudio ya uchaguzi huo unaotakiwa kufanyika katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Yanga Kuhamishia Hasira Zao Kwa Lipuli

$
0
0
Yanga Kuhamishia Hasira Zao Kwa Lipuli
Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema kuwa watahakikisha wanamaliza hasira zao za kutoka sare na Lipuli kwenye mchezo wao dhidi ya Njombe Mji.


Yanga itaumana na Njombe Mji Septemba sita kwenye Uwanja wa sabasaba mjini Njombe ukiwa ni mchezo wa pili wa msimu huu.

Akizungumza na Nipashe jana, Nsajigwa, alisema kuwa matokeo dhidi ya Lipuli yamewanyong’onyesha mashabiki wao na sasa wanataka kuwarudishia furaha yao.

Alisema kuwa wanajiandaa kupambana na hali yoyote watakayokutana nayo Njombe kwenye mchezo huo wa ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tunaenda huku tukiwa na matokeo ambayo hayajatufurahisha, kwa namna yoyote tutakayopambana nayo tutahakikisha tunapata ushindi ili kurudisha furaha ya mashabiki wetu,” alisema Nsajigwa.

Aidha, nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasubiri kuona kile watakachokifanya kwenye mchezo huo wa ugenini.

“Kikubwa mashabiki waendelee kuwa na imani na sisi, matokeo ya sare na Lipuli wala yasiwaumize, tutarudi kwenye mstari wetu kuanzia mchezo ujao (dhidi ya Njombe Mji),” alisema Cannavaro.

Alisema kikosi chao kinazidi kuimarika baada ya mshambuliaji Obbrey Chirwa kuruhusiwa kucheza na TFF baada ya kuona hana hatia kufuatia vurugu mchezo wa mwisho wa ligi kuu msimu uliopita dhidi ya Mbao FC

Straika Nicholas Gyan Rasmi Simba

$
0
0
Straika Nicholas Gyan Rasmi Simba
Klabu ya Simba imefunguka na kuweka sawa kuwa straika wao mpya raia wa Ghana, Nicholas Gyan ametua nchini Tanzania na kujiunga rasmi na klabu hiyo ambayo kwa sasa ndiyo klabu inayoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara 2017/2018.

Nicholas Gyan ni kati ya wachezaji ambao walikipiga siku ya Simba Day Agosti 8, 2017 ambapo Simba SC ilicheza game ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda katika uwanja wa Taifa Dar es salaam ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

"Baada ya kusajiliwa na kucheza kwenye siku ya Simba Day kisha kurudi Ghana kumalizia utaratibu, Nicholas Gyan amewasili rasmi kuitumikia Simba Sc. Ikumbukwe kuwa Nicholas alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Ghana. Karibu sana Nicholas Simba Sc" alisema taarifa ya Simba


Joti Aja na Mpya Seduce Me Vs Zilipendwa.....Itazame Hapa

$
0
0

Pale ambapo vijana wanamletea babu umende ndio amsha amsha linaanza huku  Seduce Me kule Zilipendwa haya sasa tuone.
VIDEO:

Muhimbili Yatoa Taarifa Kuhusu Wagonjwa Wasiofahamika Wanakotoka

$
0
0
Muhimbili Yatoa Taarifa Kuhusu Wagonjwa Wasiofahamika Wanakotoka
September 2, 2017 by Global PublishersTunapenda kuwataarifu kuwa tulipokea wagonjwa wasiofahamika wanakotoka (unknown patients).
Wagonjwa hawa wapata matibabu na afya zao zinaendelea kuimarika lakini hawajaweza kutoa taharifa sahii kuhusu wanakotoka na pia taarifa za ndugu zao.
Hivyo ndugu, jamaa na marafiki wanaowafahamu wagonjwa hawa wenye picha zifuatazo wafike Hospitali ya Taifa Muhimbili, kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Ofisi namba C5 I

Shamsa Aford Amtolea Maneno Mazito Mume Wake Chid Mapenzi

$
0
0
Shamsa Aford Amtolea Maneno Mazito Mume Wake Chid Mapenzi
Mrembo kutoka kiwanda cha filamu Bongo,  Shamsa Ford  ametimiza mwaka mmoja wa ndoa yake na mumewe mfanyabiashara Rashidi Saidi maarufu kama Chidi Mapenzi.

Katika kusherekea mwaka  mmoja huo , Shamsa amempa  mzito mumuwe kuhusu  ndoa yao, yenye mwaka mmoja.

“Leo tumetimiza mwaka mmoja wa ndoa yetu.Tumepitia changamoto nyingi sana kwa muda mfupi wa ndoa yetu ila hatujawahi kuchokana kwasababu Mwenyezi Mungu ndo alituunganisha. Upendo wako kwangu unanifanya nijione mwanamke mwenye bahati duniani na inatosha..Mwenyezi Mungu azidi kutupigania kwenye hii safari ndefu tuliyoianza. Nakupenda, na nakuheshimu sana mume wangu RASHIDI..HAPPY ANNIVERSARY TO US,” ameandika Shamsa katika mtandao wa Instagram.

Shamsa aliolewa mwaka jana Septemba 2, ndoa hiyo iliudhuriwa na watu wa karibu wa mrembo huyo na wa mumewe. Kwa mwaka mmoja wa ndoa ya wawili hao bado hawajabahatika kupata mtoto.

Huyu ndo Jaji Jasiri Aliyebatilisha Uchaguzi wa Urais Kenya

$
0
0
Huyu ndo Jaji Jasiri Aliyebatilisha Uchaguzi wa Urais Kenya
Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi AgostiHaki miliki ya pichaEPA

Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti

Wakenya wamempongeza Jaji Maraga kwa kuwa jasiri kutengua uchaguzi wa mtu aliyemchagua rais Uhuru Kenyatta mbali na kurudisha imani katika idara ya huru wa mahakama.Magazeti kadhaa ya Kenya yamemtaja jaji Maraga kuwa mtu wa maadili kutokana na hatua yake ya kuwa muumini shupavu wa kanisa la Seventh Day.

Aliripotiwa akiliambia jopo lililokuwa likimhoji kwamba iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu nchini Kenya hatosimamia kesi siku ya Jumamosi , ambayo ni siku ya kupumzika kwa wanachama wa kanisa hilo.

Wengine wamedai kwamba huenda hii ndio sababu kikao cha kwanza cha kesi ya kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta kilianza mwendo wa saa moja usiku siku ya Jumamosi baada ya ya siku ya Sabato kuisha.


Imeripotiwa kuwa wakati alipokuwa akikaguliwa alikabiliwa na madai kwamba alikula hongo.
Aliwashangaza wengi kwa kutangaza katika runinga za taifa akiapa kwa kushikilia kitabu kitukufu cha Biblia kwamba hajawahi kuchukua hongo katika maisha yake.

Jaji Maraga mwenye umri wa miaka 66, alifuzu kama wakili miaka 40 iliopita kutoka chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuhudumu kama wakili wa kibinafsi.
Alichaguliwa jaji 2003 na kujiunga na mahakama ya rufaa 2012. Ameoa na ana watoto watatu.
Mwaka uliopita kufuatia kustaafu kwa jaji mkuu Willy Mutunga, aliwashinda majaji wengine 10, mawakili na wasomi kuteuliwa jaji mkuu.

Hatahivyo mapema mwaka huu aliripotiwa kumkemea mtu aliyemchagua, rais Uhuru Kenyatta.
Wakati akifanya kampeni nyumbani kwa jaji Maraga rais Uhuru Kenyatta alinukuliwa akisema kuwa wakaazi wa eneo hilo wanafaa kumpigia kura kwa sababu alimpatia kazi ''mwana wao''.
Hatahivyo jaji mkuu kupitia idara ya mahakama JSC alisema kuwa yeye sio mradi wa serikali.
Jaji Maraga na wenzake katika mahakama ya juu nchini KenyaHaki miliki ya pichaEPA

Jaji Maraga na wenzake katika mahakama ya juu nchini Kenya
Rais Uhuru Kenyatta hapo awali alikuwa amesema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama , ijapokuwa alihoji ni kwa nini watu sita wanaweza kutoa uamuzi unaokwenda kinyume na matakwa ya Wakenya.
Hatahivyo baadaye alisema kuwa majaji hao walikuwa wamelipwa na ''watu wa kigeni pamoja na wajinga wengine''.

''Maraga na wahahalifu wake wameamua kubatilisha uchaguzi. Sasa mimi sio tena rais mteuliwa bali rais aliye mamlakani. Maraga anapaswa kujua kwamba sasa mimi ni rais anayehudumu''.
Licha ya vitisho hivyo , rais hana uwezo wa kumfuta kazi jaji mkuu ambaye muhula wake mmoja unakamilika wakati atakapofikisha miaka 70.

Kwa Sasa Sina Mpango Wa Kuoa - Chege

$
0
0
Kwa Sasa Sina Mpango Wa Kuoa - Chege
Msanii wa muziki Bongo, Chege amedai kwa sasa bado hajafikiria mipango ya kufunga ndoa.

“Ni suala jema na ambalo linatakiwa lipewe nguvu na Mwenyenzi Mungu pamoja na juhudi zangu. Nikisema Mwenye Mungu ni kumpata mtu ambaye ni right choice kama mke ambaye nitaishi naye”. Kauli hiyo aliitoa Chege katika mahojiano na Bongo5 na kuendelea;

“Unajua kuoa ni kujifunga kabisa huyo ni wa milele ingawa inatokea bahati mbaya mtu unaweza ukaacha mwanamke lakini inabidi uchagua chaguo ambalo unaweza ukaishi nalo. Isiwe unaoa kwa sababu ya trending za watu, mimi siwezi kuoa kwa style hiyo,” amesema Chege.

Pia amesema kuwa familia yake hasa mama yake mzazi, kaka na ndugu wamekuwa wakimuuliza kuhusu jambo hilo na jibu lake siku zote limekuwa ni hilo hilo.

Chege kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Run Town’,  pamoja na ‘Najiuliza’ aliyowashirikisha Ray C na Sanaipei Tande.


Idris Afunguka Sababu ya Wema Sepetu Kutofika Katika Uzinduzi Wake

$
0
0
Idris Afunguka Sababu ya  Wema Sepetu Kutofika Katika Uzinduzi Wake
Katika uzinduzi wa viatu vya ‘SultanXforemen’, mchekeshaji Idris Sultan ametaja sababu ya mrembo Wema Sepetu kutofika katika uzinduzi huo.

Akiongea na Bongo5, Idris amesema alimualika mrembo huyo ambaye alikuwa date wake katika uzinduzi wa filamu ya ‘Heaven Sent’ wikiendi iliyopita na ila mrembo huyo hajafika kutokana na  udhuru aliyopata hivyo akampa ridhaa.

“Nilimualika Wema sema unajua nyie wanawake mambo yenu hivyo ameshindwa kuja ikabidi ni mpe ridhaa, wakati naongea naye kwenye simu alivyosema sitaweza kufika basi nikamjibu uliza kiatu,” amesema Idris.

Idris na Wema wamekuwa wkionekana mara kadhaa katika event mbalimbali ,hivyo kukosekana kwa mrembo huyo kuliibua maswali kadhaa jambo ambalo Idis alinyoosha maelezo.

/

Download App ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu Yako Kupata Habari zetu Kwa Urahisi..Bonyeza Hapa

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Baada ya Mateso Mtoto wa Miaka Nane Apona Ugonjwa wa Kuvuta Sigara

$
0
0
Baada ya kuvuta sigara kwa miaka sita, Aldi Suganda maarufu kam Aldi Rizal  mwenye miaka nane sasa atibiwa ugonjwa huo uliokuwa ukimsumbua katika ukuaji wake.

Aldi Rizal ambaye anaishi na mama yake katika kijiji cha Teluk Kemang Sungai Lilin kusini mwa Sumatra nchini Indonesia, kwa sasa amepona na amekuwa mtoto wa kawaiada hata uzito wake uliokuwa mkubwa umepungua.

“It was hard for me to stop, If I am not smoking, my mouth taste is sour and my head feel dizzy, ameeelza mtotro huyo pia akaongeza kuwa “I am happy now. I feel more enthusiastic, and my body is feeling fresh.”

Naye mama wa kijana huyo Bi. Diana ameeleza kuwa anashukuru kuwa kijana wake amepata  matibabu ya ugonjwa huo ambao unawasumbua watoto wengi nchini humo na inakuwa ngumu kwa watoto wengi kupata matibabu.

Aldi Rizal aliigia katika orodha ya mlolongo wa watu wenye hisia za uvutaji sigara duniani. Hii ni kutokana na video yake kusambaa sehemu mbalimbali ulimwenguni. VIDEO:

Taifa Stars Yaichapa Botswana Bila Huruma, Msuva Noma Sana

$
0
0
MABAO mawili ya winga mpya wa klabu ya Difaa Hassan El- Jadida yameipa Tanzania ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Msuva aliyejiunga na timu ya Ligi Kuu ya Morocco mwezi uliopita leo alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya The Zebras na amefunga bao moja kila kipindi mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Elly Sasii aliyesaidiwa na Soud Lila na Frank wote wa Tanzania, hadi mapumziko Taifa Stars walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Simon Msuva alipokea pasi ndefu ya kiungo Hamisi Abdallah wa Sony Sugar ya Kenya, akaikontroo vizuri  na kumpasia kiungo wa Simba, Muzamil Yassin kabla ya kuiombea mbele na kuingia nayo kwenye boksi kwa kasi na kufumua shuti kali lililompita kama upepo kipa wa The Zebras, Mwambule Masule dakika ya sita.

Katika kipindi hicho, ilishuhudiwa Taifa Stars wakicheza vizuri zaidi na kutengeneza nafasi chache za kufunga, ambazo hata hivyo walimudu kuitumia vizuri moja tu kupata bao.

Mashambulizi ya Taifa Stars leo ambayo katika benchi la Ufundi imeongezewa nguvu na mchezaji wa zamani, Amy Ninje aliyecheza hadi Uingereza Ligi za Madaraja ya chini na kocha wa zamani wa Azam, Dennis Kitambi ambaye kwa sasa anafundisha AFC Leopards ya Kenya.

The Zebras nao hawakuwa wanyonge kabisa uwanjani, kwani walipeleka mashambulizi langoni mwa Taifa Stars na kukaribia kufunga mara mbili kama su uhodari wa kipa wa Simba, Aishi Salum Manula.

Kipindi cha pili, Zebras walirudi kwa nguvu na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Taifa Stars, lakini safu ya ulinzi ikiongozwa na mkongwe Kevin Yondan ilikuwa imara kudhibiti hatari zote.

Hatimaye Msuva akawainua tena vitini mashabiki wa nyumbani kwa kufunga bao la pili dakika ya 63 baada ya kugongeana vizuri na winga wa Simba SC, Shiza Ramadhani Kichuya.

Nahodha, Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji alicheza vizuri pamoja na kudhibitiwa vikali na akakaribia kufunga mara mbili – unaweza kusema bahati haikuwa ya kwake leo.

Kiungo wa Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa Dhofar ya Oman wote waliingia kipindi cha pili na wakacheza vizuri sawa na chipukizi, Emmanuel Martin wa Yanga aliyempokea Msuva.

MBUNGE Msukuma Afunguka Kuhusu Maiti iliyookotwa Mgodini GGM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Geita, Joseph Msukuma ambaye pia ni Mbunge wa Geita Vijijini amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na Serikali ya Mkoa kufuatilia kwa karibu ripoti ya Uchunguzi wa mtu aliyekutwa amefariki ndani ya mgodi wa Dhahabu wa Geita.

Msukuma ametaka kufanyike uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vifo vya mara kwa mara vinavyotokea ndani ya Mgodi huo akisema kwamba hiyo sio mara ya kwanza kuokotwa maiti ndani ya GGM.

”Kumekuwa na matatizo yanayotokea kwenye mgodi mkubwa wa GGM. Niliwahi kuzungumza Bungeni kwamba kuna watu wanauawa katika mazingira ya kutatanisha lakini Jeshi la Polisi na Serikali ya Mkoa wa Geita haichukui hatua.

“Hali iliyotokea sasa, tarehe 18 imeokotwa maiti ndani ya Mgodi wakapewa watu kwenda kuzika lakini tarehe 23 mtu mwingine amefariki pale na amefariki katika mazingira ambayo wao walidai alitumbukia kwenye shimo – aliteleza kutoka juu.

“Tulipopata ile taarifa ilionesha ana majeraha kichwani ambayo hayalingani na maelezo kwamba ameporomoka kutoka juu.” – Mbunge Msukuma.
VIDEO:

Taarifa ya Serikali Kuhusu Upanuzi wa Barabara ya Morocco Mwenge

$
0
0

Dar es Salaam, Septemba 1, 2017: Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia Tanzania ruzuku ya Yen milioni 69 sawa na Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa awamu ya pili ya mradi wa upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.

Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Septemba 1, 2017, Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kwa niaba ya Serikali, Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Satoru Matsuyama.

Tukio hilo limekwenda sambamba na kuingia makubaliano kuhusu muda wa kukamilisha mradi huo pamoja na kupeana taarifa ya namna mradi huo utakavyotekelezwa.

Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).

Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Dkt. Mpango amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya msongamano wa magari kutoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Ameishukuru Japan kwa msaada huo wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo katika awamu ya kwanza, Japan ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 99.5. kujenga barabara ya njia nne katika kipande cha kilometa 12.9 kutoka makutano ya barabara ya Tegeta na makutano ya barabara ya Mwenge.

“Si mara ya kwanza kwa Japan kuisaidia Tanzania, wanajenga barabara za juu katika makutano ya Tazara, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma hadi Babati mkoani Manyara (km 188.15), Tunduru-Mangaka – Mtambaswala (km 202) na barabara ya Iringa hadi Dodoma (259.9)” alisisitiza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa upanuzi wa barabara ya Bagamoyo si tu kwamba itapunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam lakini pia utaunganisha Jiji na Bandari ya Bagamoyo ambayo ni muhimu kwa ajili ya usafirishaji wa watu, bidhaa na huduma kutoka Jijini, mikoa ya Pwani na maeneo mengine ya nchi.

Balozi wa Japan, Mhe. Masaharu Yoshida ameeleza kuwa kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa awamu ya pili ya barabara ya Morocco hadi Mwenge kumekuja baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza iliyohusisha ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Tegeta hadi Mwenge ili matokeo ya mradi huo yaweze kuonekana dhahiri.

Ameahidi kuwa baada ya kukamilika kwa usanifu wa kina wa barabara hiyo, Serikali ya Japan kupitia JICA, itasaini mkataba wa kuanza ujenzi huo Mwezi Juni mwakani.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama, amesema Japan imeamua kufadhili mradi huo baada ya utafiti kuonesha kuwa Barabara ya Bagamoyo ndiyo yenye msongamano mkubwa wa magari ambapo inakadiriwa kuwa magari 52,000 yanapita kila siku katika barabara hiyo.

Alielezea matumaini yake kwamba mradi huo utakapo kamilika utasaidi kukuza shughuli za kiuchumi katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuwa ndicho kitovu cha biashara  kwa maeneo mengine ya ndani ya nchi na kimataifa na kuwaomba wataalamu pamoja na TANROADS kuharakisha usanifu huo wa kina.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini-TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo hautahusisha ubomoaji wowote wa makazi ya watu wala majengo ya biashara.

Imetolewa na:

Benny Mwaipaja

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Fedha na Mipango

Rais John Magufuli Aungana na Wasabato na Kuchangisha Mil 25.3 za Ujenzi wa Kanisa

$
0
0

Rais John Magufuli  ameungana na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato katika ibada ya sabato iliyofanyika Usharika wa Magomeni Mwembechai na kuchangisha zaidi ya Sh25.3 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.

Rais Magufuli akiwa na Mkewe Janeth Magufuli  katika ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo,  alisema  Serikali itaendelea  kushirikiana na viongozi wa dini katika kuwahudumia wananchi.

Rais Magufuli amewahakikishia waumini na viongozi wake kuwa Serikali inatambua mchango huo na itaendelea kushirikiana na madhehebu yote ya dini katika kuwahudumia wananchi.

“Baba Askofu na kushukuru  kwa mahubiri mazuri ya leo ambayo yamenigusa , madhehebu ya dini likiwemo hili la Waadventista Wasabato mnatoa mchango mkubwa sana kwa Taifa letu, nakuhakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nanyi” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alitoa mchango wa Sh5 milioni ya ununuzi wa mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa jipya la Waadventista Wasabato kwenye eneo hilo na Sh1 milioni kwa ajili ya kwaya za Kanisa hilo.

Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na maaskofu wengine akiwamo Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati, Joseph Mgwabi na Askofu wa Jimbo la Kusini Mashariki, Albert Nziku, Rais Magufuli aliendesha  harambee ya papo kwa papo ya kuchangia ujenzi wa Kanisa, na kufanikisha kupata  25.3 milioni.

Katika salamu zake,  Askofu Malekana alimshukuru Rais Magufuli kwa kuungana na waumini wa Kanisa hilo katika Ibada ya Sabato na kuchangia ujenzi wa kanisa, na ameongoza maombi ya kuliombea Taifa na Rais.

By Mwananchi

Idara ya Mahakama Kenya ina 'Tatizo' - Uhuru Kenyatta

$
0
0
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo lina 'matatizo' na idara ya mahakama ambayo inahitaji 'marekebisho'.

Alikuwa akizungumza katika hotuba uliopeperushwa moja kwa moja na runinga siku moja tu baada ya mahakama ya juu kubatilisha uchaguzi wake na kuagiza uchaguzi mpya katika kipindi cha siku sitini.

Rais Kenyatta alisema kuwa ataiangazia idara ya mahakama ,mbali na kurejelea ujumbe wake kwamba atauheshimu uamuzi wa mahakama hiyo.

Wameonya kuikabili idara hiyo baada ya uchaguzi

''Hata iwapo wewe ni mjinga jiulize hivi, matokeo ya uchaguzi wa MCA yalikubaliwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali mengi, matokeo ya maseneta na ya wabunge nayo yalitangazwa na tayari wameapishwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali. Matokeo ya magavana yalitangazwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali ,sasa inakuwaje watu wanne wanaamka na kusema kuwa matokeo ya urais yaliotangazwa yalikuwa na dosari.

Kivipi, kivipi? aliuliza rais Kenyatta katika ikulu ya rais alipokutana na viongozi wa chama cha Jubilee waliochaguliwa.

Rais huyo aliyeonekana kuwa na hasira alionya kukabiliana na majaji hao wa mahakama ya juu atakapochaguliwa.

''Tuna matatizo hapa. Mwanzo ni nani aliyewachagua? tuna tatizo na lazima turekebishe'', alisema.
Amesisitiza kuwa ijapokuwa anaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo ya juu na kwamba alikuwa tayari kushiriki katika uchaguzi mwengine alisema kuwa uamuzi wa mahakama hiyo ulikuwa na makosa.

''Mahakama ya juu iliketi chini ikaamua kwamba hiyo ndio yenye nguvu zaidi ya Wakenya milioni 15 walioamka alfajiri na kupanga foleni na kumpigia mgombea wa urais waliomtaka''.

''Mahakama ya juu haiwezi kufutilia mbali maono ya Wakenya.Na tutaliangazia swala hili.Niangalieni machoni na museme iwapo upendo wangu wa Wakenya kuishi kwa amani ndio unaonekana kuwa uoga, hatuogopi''

Mcheza Tenesi Serena Williams Ajifungua Mtoto wa Kike

$
0
0
Bingwa wa tennis kwa upande bi Serena Williams amejifungua mtoto wa kike katika hospitali moja ya mjini Florida Marekani.

Japo mwenyewe na jamaa zake hawajatoa tangazo rasmi tayari kuna ujumbe wa kumpa hongera katika ukurasa rasmi wa Twitter akaunti ya US Open Tennis kutoka kwa kocha wake miongoni mwa wengine .

Itakumbukwa mwanamama huyo aliweka rekodi ya kushinda kinyanganyiro cha Australian Grand Slam kwa mara ya 23 mwaka huu January, japo alishindana akiwa mja mzito.

Serena alikiri kwamba alifichua kuhusu mimba yake kwa ulimwengu kimkosa mnamo mwezi Aprili baada ya kupakia picha katika Intagram kimakosa katika mtandao wa Snapchat.

Alishinda taji la Australian Open mnamo mwezi Januari akiwa mjamzito na katika taarifa yake katika jarida la Vogue mwezi uliopita alisema kuwa anataka kutetea taji hilo.

Wamiliki wa Malori ya Mchanga Kubeba Mchanga Bure Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu Dar

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu pamoja na wanachama wa Chama cha wamiliki wa malori Dar es salaam.
Chama cha wamiliki wa malori ya mchanga jijini Dar es salaam kimesema kitatoa huduma ya kubeba mchanga bure katika ujenzi wa ofisi za walimu 402 ndani ya Mkoa wa Dar es salaam ili kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika uwaletea wananchi maendeleo.

Mwenyekiti wa cha hicho, Emmanuel Godson Moshi katikati akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kuwaomba wadau na wananchi kuchangia fedha na vifaa ikiwemo mabati, nondo, saruji, kokoto, mchanga, mbao na vguvu kazi ya watu katika ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam ili kuwafanya walimu wafanye kazi katika mazingira mazuri.

Akiongea na waandishi wa habari katika kikao chao walichomualika mkuu wa mkoa huyo, Mwenyekiti wa cha hicho, Emmanuel Godson Moshi akiwa pamoja na wanachama wake zaidi ya ishirini, alisema wao kama wamiliki wa malori wameamua kutoa huduma ya kubeba mchanga bure katika mradi huo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika maendeleo ya jamii.

“Mh Mkuu wa Mkoa sisi tumekuita hapa kwanza kukupongeza kwa kazi nzuri ambazo unazifanya katika juhudi za kuwaletea maendeleo wananchi wa Dar es salaam. Sisi kama chama cha wamiliki wa malori Dar es salaam tumesikia kwamba unahitaji msadaa wa vitu mbalimbali katika ujenzi wa nyumba za walimu wetu 402 Dar es salaam, kama chama chetu tumependezwa na hicho unachokifanya na tumeamua kutoa huduma ya kubeba mchaka bure katika mradi huo mpaka unakamilika, suala la mchanga tuachie sisi, sisi tutatoa malori yetu kwaajili ya kufanikisha hili suala la mchanga kabisa,” alisema Emmanuel Moshi.



Kwa upande wa RC Makonda baada ya kupokea msaada huo aliwashukuru wamiliki wa malori na kuwataka wadau wengine waige mfano kwa kuwa jambo linalofanyika ni kwaajili ya kuiboresha sekta ya elimu huku akisema hatua hiyo itakwenda kuchochea maendeleo ya elimu ndani ya mkoa wa Dar es salaam.

“Nawashukuru sana kwa sababu mmenifanya niendelee kutembea kifua mbele na kupata usingizi, hiki kitu ambacho mmekifanya nikikubwa sana kwa mkoa wa Dar es salaam, kina manufaa kwa elimu yetu kwa ujumla, kwahiyo mimi niwashukuru kwa hatua hiyo pia wadau wengine watuunge mkono kwa sababu kama tumemaliza suala la mchanga bado kuna maeneo mengine kwenye mradi huu ambayo yanahitaji pesa,”

Amesema kuwa wananchi wanaweza kuchangia fedha kupitia Account ya
CRDB namba 0150296180200 au kuwasilisha michango yao Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ujenzi rasmi wa ofisi 402 za walimu utaanza rasmi Septemba 4 mwaka huu.

Source:Bongo5
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images