Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104427 articles
Browse latest View live

Spika Mstaafu Pius Msekwa Apigilia Msumari Suala la Kupinga Matokeo ya Uchaguzi wa Rais Tanzania Mahakamani..Adai Wakati Umefika

0
0
Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Pius Msekwa amesema wakati wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais mahakamani umeshafika na kilichobaki ni kupitisha rasimu ya Katiba ambayo ina ibara inayotoa haki hiyo.

Msekwa, ambaye pia alikuwa makamu mwenyekitiwa CCM, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili kuhusu hatua ya Mahakama Kuu ya Kenya kubatilisha uchaguzi wa rais wa nchi hiyo uliofanyika Agosti 8 baada ya mgombea wa upinzani kufungua kesi, akidai kulikuwa na ukiukwaji wa sheria.

Kwa uamuzi huo, ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta, anayewania kuongoza taifa hilo kwa kipindi cha pili mfululizo, umebatilishwa na sasa atapambana tena na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga wa muungano wa NASA.

Wakati ibara ya 140 ya katiba ya Kenya inaruhusu mtu yeyote kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais mahakamani ndani ya siku saba tangu kutangazwa kwa mshindi, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakataza.

Ibara ya 74(12) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema hakuna mahakama yoyote nchini itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba.

Hilo ni jambo ambalo limekuwa likijadiliwa tangu kubatilishwa kwa uchaguzi wa rais wa Kenya, lakini alipoulizwa kuhusu suala hilo, Msekwa muda umefika.
“Jibu ni ndiyo,” alisema Msekwa.

“Tunaweza kufikia hatua hiyo na tumeshaifikia. Katiba Mpya iliyopitishwa na Bunge mwaka 2014 inasema matokeo ya urais yanaweza kupingwa mahakamani.

“Katiba ya sasa hairuhusu, lakini katiba inayopendekezwa imeruhusu. Tunachosubiri ni referendum (kura ya maoni) tu.”

Mchakato wa kubadili Katiba ulianzishwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka 2011 lakini ukakwama mwaka 2014 ukiwa katika hatua ya kura ya maoni baada ya NEC kueleza kuwa haikuwa na muda wa kutosha .

Hata hivyo, mchakato huo uliingiwa na dosari baada ya baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba, hasa kutoka vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD kuususia wakidai kuwa chombo hicho kiliacha Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuingiza ajenda za chama tawala.

Hata hivyo, wajumbe waliosalia waliendelea na mchakato na kupitisha Katiba Inayopendekezwa.
Hata hivyo, Rais John Magufuli ameshasema kuwa Katiba mpya si kipaumbele chake kwa kuwa kwa sasa anataka “kuinyoosha nchi”.

Kuhusu suala hilo, Msekwa alisema hawezi kuzungumzia utawala wa sasa kwa kuwa una utendaji wake.
“Mambo ya utawala wa sasa siwezi kuyasemea,” alisema Msekwa.
“Swali lako la msingi ni kama tunaweza kufikia hatua ya kupinga matokeo ya urais na nimesema ndiyo tunaweza.”

Kada mkongwe wa CCM aliyewahi kuwa waziri katika utawala wa Mwalimu Julius Nyerere na ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini, alisema hata kabla ya kupata Katiba mpya vyama vya upinzani vilishakubaliana na Kikwete mambo manne, likiwemo la kupinga matokeo ya urais.

“Wagombea urais kupingwa mahakamani ni jambo zuri, “ alisema.

“Kimsingi vyama vya upinzani na na Rais Kikwete walishakubaliana baada ya mchakato wa Katiba kukwama. Sijui kwa nini hayakutekelezwa.

“Mambo manne waliyokubaliana ni kupinga matokeo ya urais, mgombea urais atangazwe kushinda akifikisha asilimia 50 na zaidi ya kura, kuwa na tume huru ya uchaguzi na kuwa na mgombea binafsi. walikubaliana kabisa, sijui kwa nini hayakutekelezwa. Waulize wapinzani.”

Kwa upande wake Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Mohamed Bakari alisema ili Tanzania ifikie mabadiliko ya Kenya, ni lazima mapambano ya kudai Katiba mpya yaongezeke.

“Ukichukua uzoefu wa Kenya, mpaka katiba imepatikana kulikuwa na mapambano makali sana yakihusisha vyama vya siasa, asasi za kiraia na wananchi wanaopenda demokrasia. Msukumo kama huo ni mdogo Tanzania,” alisema Dk Bakari.

Kwa upande wake, Njelu Kasaka, waziri wa zamani enzi za utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi, alisema ili kufikia mabadiliko ya Katiba ni lazima wananchi wenyewe waidai.


“Nawapongeza Wakenya kwa sababu wameweza kujitawala kwa kuweka uongozi wanaoutaka na kuuondoa wenyewe. Sisi tunaweza kufikia hatua hiyo kwa kudai Katiba nzuri na kuweka taasisi zitakazoisimamia, kama Bunge na Mahakama,” alisema Kasaka.

Alisema licha ya Tanzania kuwa mstari wa mbele katika vita ya ukombozi wa Afrika miaka ya sitini, imebaki nyuma kidemokrasia tofauti na nchi zilizokuwa nyuma.

“Tuliwalaumu makaburu wa Afrika Kusini kwa kukandamiza demokrasia, tukasema demokrasia itawale hadi Zimbabwe, lakini leo tumeshindwa kuwawajibisha viongozi wetu,” alisema.

“Wananchi waanze kudai Katiba mpya, lakini hatuwezi kuifikia kama hatuna kambi ya upinzani imara. (Kama) Bado hatujawa na vyama vya upinzani imara, kwa sababu kwa sasa vinabanwa na bado wananchi wengi hawaonyeshi mwamko. Lazima tusawazishe nguvu ili kupata mabadiliko.”

Chanzo: Mwananchi

Taarifa Hii Kutoka Kwa Paul Makonda Ukifikie Kama wewe ni Mkazi wa Dar es Salaam

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua zoezi la Ulipaji wa fidia kwa Wakazi wanaopitiwa na Mradi wa uboreshaji wa Barabara kwa maeneo yasiyopangwa DMDP ambao wataanza kulipwa Fedha zao kuanzia kesho sambamba na kufanya ziara ya ukaguzi wa Miundombinu ya Barabara akiwa ameambatana na Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta.

Mradi huo utahusisha  uboreshaji wa Barabara, Mabonde ya Mito, Ujenzi wa Mitaro ya Maji, Taa za Barabarani, Njia za watembea kwa Miguu, Vizimba vya taka, alama za Barabarani na Soko la Mwananyamala ambapo unagharimu kiasi cha Shilingi Billion 230.

Miongoni mwa Barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni Barabara inayoanzia Morocco hotel hadi Sinza Kijiweni Km 5, Barabara ya Tandale Kisiwani kuelekea Mwananyamala na Barabara za Makumbusho, , TANESCO Msasani, Simu200, Kilungule na MMK.

Makonda amesema mradi huo utafanya jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa la kisasa na kufikia azma yake ya Dar Mpya.

Amewataka wananchi watakaolipwa fidia kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri kwa kufungua miradi itakayowaingizia kipato.

Aidha Makonda amesema kuwa Kata za Tandale, Mburahati na Mwananyamala zitaingizwa kwenye idadi ya Kata 14 zinazopandishwa viwango kwa kuwa Barabara za kisasa maana ya kuwa na Lami,Taa na Mitaro ya Maji.

Hata hivyo amesema Mto Ng’ombe pia utatengenezwa kwa kiwango cha kisasa urefu wa Km 7.5 ili kuwezesha Maji kwenda moja kwa moja hadi Baharini kupitia eneo la Jangwani kutakapojengwa mfumo wa kusafirisha maji taka.

Makonda amempongeza Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta na Manispaa hiyo na kuwataka kuhakikisha kila anaestahili kulipwa fidia analipwa kile anachostahili bila usumbufu.

Mpenzi Wangu Anataka Nimpe Mapumziko ya Miezi Mitatu, Nifanyeje?

0
0

Mpenzi wangu wa miaka 3 anataka tupeana muda wa kupumzika wa miezi mitatu, anasema kwamba tunagombana sana na hakuna furaha tena kwenye mahusiano yetu na anahisi njia pekee ya kufanya au kurudisha mahusiano yawe mazuri ni pale tukipeana mapumziko ya muda wa miezi 3 ili kila mtu apate muda wa kujifikiria kama anamtaka mwenzie.

Katika hiyo miezi 3 hamna mtu anayeruhusiwa kufanya mapenzi na mtu mwingine. Mie tangia nianze mahusiano sijawahi kusikia watu kupeana mapumziko hata siku moja na mimi kama mwanaume rijali nitavumilia kweli muda wote huo bila kufanya ngono? sidhani!

Je, unadhani inaweza ikawa kwamba anataka kucheza cheza na wanaume wengine na ndo maana anataka muda wa kupumzika? simwelewi na wala sielewi haya mambo ya kupeana mapumziko. Niachane naye tu au nimvumilie?

Mume Wangu Anataka Tufanye Mapenzi na Wapenzi Wengine Kwa Pamoja

0
0
Mimi na mume wangu tuna uhusiano murua kati yetu, hatuna tatizo kitandani vilevile. Hata hivyo ana wazo hili la kiwazimu la kuwaingiza wanawake wengine katika shughuli yetu ya kupigana miereka ili kuboresha mambo.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 52 na ninahisi majaribio kama hayo –ya wapenzi watatu au wane kusakata dimba kwa wakati mmoja – huenda yakaharibu uhusiano wetu.

Hatahivyo, mpenzi wangu anasema anaweza kutenganisha mapenzi na kitendo cha ngono. Lakini kwangu siwezi kustahimili kumwona na mwanamke mwingine na Mume wangu wakisakata dimba.

 Sitaki kuzuia shauku za mume wangu na nimejaribu kujihakikishia kwamba naweza kustahimili hili. Lakini sehemu ya moyo yangu inahisi kwamba hii ni kunivunjia heshima.

Isitoshe, anasema iwapo siko tayari, angependa kufanya hivyo pekee yake.

Nahisi kukwazwa moyoni, sijui nifanye nini....Naombeni Ushauri

Raila Odinga Aichachamalia Tume ya Uchaguzi Kenya

0
0
Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umedai kutaka mabadiliko yafanyike ndani ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mpya wa urais.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, amesema Tume ya Uchaguzi haiaminiki na haiwezi kusimamia Uchaguzi utakaokuwa huru na haki kama Mahakama Kuu ilivyoagiza.

Kauli ya Odinga imekuja baada ya kuanza kwa kampeni zao za kwanza jijini Nairobi leo kutokana na uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Juu Ijumaa iliyopita ambapo ilibatilisha matokeo ya ushindi wa Uhuru Kenyatta .

Pamoja na hayo Odinga amekosoa kauli ya Rais Kenyatta ya kuwashtumu Majaji kwa kudai kuwa upinzani hawataki uchaguzi lakini wanataka serikali ya muungano, madai ambayo Odinga amepuuzilia mbali na kusema hawawezi kushirikiana na wezi wa kura.

Kenya inaelekea kwenye Uchaguzi mpya ndani ya siku 60 baada ya Mahakama ya Juu kufuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kwa kubaini kuwa, haukuwa huru na haki.

Kenya imekuwa nchi ya kwanza, barani Afrika kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais na kuingia katika vitabu vya historia.

Mchekeshaji Erick Omondi Atoa Mpya Akipigana Ulingoni na Jitu la Miraba Minne.....

0
0
Mchekeshaji Erick Omondi Atoa Mpya Akipigana Ulingoni na Jitu la Miraba Minne.....Tazama Video hapa Uongeze siku kwa kucheka....

VIDEO:

Kutana na Mtatibu Wanyota za Binadamu Duniani Kote Maalim Fadhili Rashid Kutoka Comoro

0
0
KUTANA NA MTABIBU WANYOYA ZA BINADAMU DUNIANI KOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO

KWA SASA YUPO TANZANIA MAALIM FADHILI RASHIDI ANA IWEZO WAKUJUWA JAMBOLAKO NAKULI TATUWA KWAMUDA MFUPI

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE

MAALIM FADHILI RASHIDI NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA MIGUU KUWAKA MOTO

KISUKARI VIDONDA VYATUMBO PUMU TEZI NA UVIMBE TUMBONI PUMU ANA UWEZO WAKURUDISHA MTU ALIE POTEA KIMAZINGIRA

(MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA

KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABU MAALUM ANATOWA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA YA MASHARITI YEYOTE

NAKUMILIKI MALIZA MAJINI KWAYULE ANAE HITAJI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZA KIUME ANAYO

DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEPU KUWA NA UMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASA (24)

ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YAMVUTO WABISHARA KUUZA MALIYAKO KWA HARAKA KUZUIYA CHUMA ULETE

KUSAFISHA NYOTA NAKUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHAKUTESEKA NJOO UWONE MIUJIZA YA MAALIM FADHILI RASHIDI

CALLING+255719362806/ +255763276239

KWA WHATSAPP IMO +255785786436

Hukumu ya Kenya Yaendelea Kutikisa Nchini....Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Septemba 4

0
0

Hukumu ya Kenya Yaendelea Kutikisa Nchini....Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Septemba 4

Kijana wa Miaka 18 Asimulia Jinsi Alivyowateka Watoto Wanne Arusha

0
0
Kijana wa Miaka 18 Asimulia Jinsi Alivyowateka Watoto Wanne Arusha
Matukio ya utekaji watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi baada ya kijana wa miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alipokamatwa katika mji wa Katoro wilayani Geita alikofanya tukio jingine la utekaji.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Samson Petro alisema watoto wawili aliwarudisha kwa wazazi wao baada ya kupewa Sh300,000.

Alisema wengine wawili aliwatelekeza mtaani baada ya wazazi wao kutotoa kiasi cha fedha walichotakiwa kumpa.

Samson alisema alianza ‘shughuli’ hiyo ya utekaji watoto kutokana na mahitaji ya fedha na kwamba, aliacha shule akiwa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lutozo iliyopo Katoro.

“Naishi na wazazi wangu, lakini nao ni masikini, nilifanya hivi ili nipate fedha na nilikuwa nikimchukua mtoto naandika ujumbe kwenye karatasi, naandika na namba ya simu napeleka karibu na familia ili wanitafute,” alisema Samson.

Awali, kamanda wa polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema walimkamata kijana huyo katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mjini Katoro juzi saa mbili usiku.

Mwabulambo alisema polisi mkoani Geita kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha walifanya uchunguzi na kubaini mtuhumiwa alikuwa Katoro.

Alisema walipata taarifa za kutekwa Justin Ombeni (2) Septemba Mosi nyumbani kwao katika eneo la Shilabela ambako mtuhumiwa alikwenda na kuwakuta watoto wanne wakicheza nyuma ya nyumba.

Alisema aliwagawia pipi na kuondoka na Justin. Kamanda huyo alisema polisi ilipata taarifa kuwa kijana huyo yupo chumba namba 103 katika nyumba hiyo ya wageni ambako waliweka ulinzi kuizunguka.

Alisema walipoingia katika chumba hicho walimkuta akiwa na
mtoto huyo. Mwabulambo alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Ombeni Mshana ambaye ni baba wa Justin alisema mtekaji huyo alimpatia ujumbe mtoto wa jirani uliomtaka kutuma Sh4 milioni na walipokuwa wakiwasiliana na mtuhumiwa alishusha kiwango hadi Sh1 milioni.

Alisema polisi walimtahadharisha kwamba asitume fedha hizo.Kamanda Mwabulambo alisema tukio la kutekwa Justin ni la pili katika kipindi cha miezi minne baada ya mwingine kutekwa.

Kesi kuhusu tukio hilo la kwanza inaendelea mahakamani baada ya mtoto kupatikana.

Katika hatua nyingine, kikosi kilichoundwa na wananchi mkoani Arusha kikiongozwa na mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Kata ya Olasiti, Daudi Safari na familia za watoto wawili waliotekwa kimewakamata watuhumiwa wawili na kuwafikisha polisi.

Watoto hao ambao bado hawajapatikana ni Moureen David (6) anayesoma darasa la kwanza shule ya msingi Lucky Vincent na Ikram Salim (3).

Wakizungumza jana nje ya kituo kikuu cha polisi Arusha baada ya kuwafikisha kituoni watuhumiwa hao, Safari na wazazi wa watoto hao, David Njau na Salim Kassim walisema kwa nyakati tofauti wameanzisha msako baada ya
kuona siku zinakwenda bila watoto kupatikana.

Moureen alitekwa Agosti 21 saa 11 jioni akiwa anacheza nyumbani kwao eneo la Olasiti, wakati Ikram alitekwa Agosti 26 saa 12 jioni akiwa anacheza na watoto wenzake nyumbani kwao, Burka - Olasiti.

Safari alisema wamemkamata mtu mmoja (jina linahifadhiwa)
ambaye simu yake ilitumiwa na watekaji kuomba fedha kwa mzazi wa Ikram Salim.

Alisema pia wamemkamata wakala wa fedha wa kampuni moja ya simu (jina tunaihifadhi) aliyetoa Sh300,000 kwa watekaji baada ya fedha kutumwa na mzazi wa Ikram.

Imeelezwa kuwa wakala huyo amekamatwa kwa kuwa fedha hizo zilitolewa pasipo kuorodheshwa popote na mpokeaji hakuonyesha kitambulisho chochote.

Akizungumzia operesheni hiyo, Njau alisema hawatapumzika mpaka watoto wao wapatikane.

Alisema ufuatiliaji walioufanya kupitia minara ya kampuni za simu unaonyesha wahusika walikuwa eneo la Kwa Mrombo jijini Arusha walipopiga kuomba Sh4.5 milioni ili wamwachie Doreen na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya Ikram.

Watekaji hao kupitia ujumbe waliotuma nyumbani kwa Njau walidai kama wasipopewa fedha wangempoteza mtoto huyo japokuwa hawana nia hiyo.

Kassim Salim ambaye ni babu wa Ikram alisema, “tunaendelea kuomba msaada zaidi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na vyombo vya dola watusaidie tuwapate watoto wetu.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema juzi kuwa watu watatu wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo akiwapo dereva wa bodaboda mkazi wa Olasiti aliyetumwa kuwarejesha watoto wawili waliokuwa wametekwa.

Matukio ya utekaji yalianza kuibuka Agosti 21 baada ya kutekwa watoto wanne. Watoto wawili Ayoub Fred na Bakati Selemani wakazi wa eneo la FFU, kata ya Murieti jirani na kata ya Olasiti walirejeshwa

Mambo 7 Yanayoonyesha Wewe na Mpenzi Wako Mna Uhusiano Imara

0
0
Mambo 7 Yanayoonyesha Wewe na Mpenzi Wako Mna Uhusiano Imara
Haijalishi ni kwa namna gani uhusiano umeanza au umeisha, kila mara tunapokuwa katika uhusiano lazima kuna somo tunajifunza.

Hakuna uhusiano ambao ni mkamilifu, lazima mtazozana kwa maneno au vitendo na wakati mwingine kugombana kabisa. Lakini kuzonazna huko hakumaanishi kwa uhusiano wenu umefikia mwisho, japokuwa mkiwa watu wa kugombana kila siku, inabidi mkae chini mzungumze kuweza kufahamu tatizo ni nini.

Kuwa na furaha ni jambo moja, lakini kujua kuwa upo katika uhusiano ambao utadumu licha ya kuwa mnapitia magumu kiasi gani, ni jambo jingine ambalo kila mmoja analitamani.

Hapa chini ni ishara saba ambazo zinazungumza kuhusu uimara wa uhusiano wenu.

Mawasiliano
Kikubwa ni kujiuliza mnazungumza kuhusu nini na mna mazungumzo ya aina gani. Manaweza mkawa mnazungumza kuhusu jinsi ya kufanya maamuzi, tabia nzuri amba mbaya zinazowakera au kuhusu maisha yenu ya mbeleni.

Chagua muda sahihi na mahala sahihi pakuzungumzia jambo lako, dunia haitaisha kama ukiamua kusubiri saa moja ili uweze kupata sehemu sahihi ya kuzungumza na mwenza wako. Fahamu unataka kusema nini, utakavyokisema na mazingira utakayosemea ili kuwa na mawasiliano madhubuti.

Makubaliano
Hii sio kwenye uhusiano wa kimapenzi pekee, hata kwa rafiki wa kawaida ni muhimu kuzingatia hili kwani huwezi ukawa kila mara wewe unapokea tu, lazima pawepo wakati wa wewe kutoa pia.

Mnapoingia katika uhusiano, kila mmoja huwa na tabia zake na uelewa wake juu ya mambo, lakini wapenzi ambao ni imara, watakaa na kujadili kuona namna bora ya kuweza kuchanganya tabia zao na kutoka na moja ambayo wote wataikubvali.

Ukiwa wewe hutaki kubadilika ila unataka mwenzako ndio kila mara abadilike kufuata mawazo yako, hakika kila mara mtaishia kugombana.

Uaminifu na kusamehe
Vitu hivi viwili ni muhimu sana katika uhusiano wako, kila mmoja anatakiwa kuweka nguvu sawa kuhakikisha vinaendelea kuwa nguzo muhimu kati yenu wawili. Usiwe na nafasi ya kuwa na mawazo hasi na mwenzako, na unapokuwa na wasiwasi, mwambie na yeye akueleza ukweli pasi na kupepesa macho.

Jifunze kusamehe na kusahau, haiwezekani kwenye uhusiano kila mara nyie mkawa ni watu wa kugombana tu, mtapata wapi muda wa kufurahia uwepo wa mwenzio? Samehe na sahau vitu ambavyo hamuwezi mkaendelea kuvijadili. Haiwezekani mkawa mnaendelea kujadili tatizo lililotokea mwezi uliopita.

Jitambue
Hili huwakumba zaidi wanawake. Wanapoanza kuwa kwenye uhusiano, wapenzi wao huwa ndio dunia yao.  Huwapoteza marafiki zao na kuacha kufanya vile vitu alivyokuwa akivipenda, na badala yake sasa anafanya vitu ambavyo mpenzi wake anavipenda.

Hii huwa haitokei sana kwa wanaume, ni mara chache sana utakuta mwanaume ameacha kuangali mpira kwa sababu tu mpenzi wake hapendi aangalie.

Hakikisha unaendelea kuwa na marafiki, na kufanya vitu ulivyokuwa ukivipenda hata baada ya kuwa kwenye uhusiano. Hivyo vitakusaidia wewe endapo chochote kitatokea katika uhusiano wenu. Hata ikitokea mkaachana na huyo mpenzi wako, bado una marafiki wa kukusaidia.

Wanahitaji kuwa kwenye Maisha yako
Hakuna mtu anayekuwaga ‘busy’ akashindwa kufanya kile anachokipenda. Kama kweli mpenzi wako anakupenda, atatafuta muda kwa ajili yako bila kujali ametingwa kiasi gani kwa sababu tu anakupenda.

Na anapotenga muda kwa ajili yako, mkiwa pamoja awepo pale kiakili na kimwili, sio mwingine akifika anaanza kuchezea simu yake na hakuna kuongeleshana.

Anakufanya ujisikie vizuri na mwenye furaha
Sio lazima uwe umejiremba ndio mpenzi wako aonyeshe kuvutiwa na wewe, hata kama ndio umeamka kutoka usingizi au umetoka kuoga na hujajiremba avutiwe na jinsi ulivyo na hicho kitakufanya ujiamnini na kujiona upo kwenye mikono salama.

Kuwa na mtu ambaye anakuthamini, anayeijua thamani yako, anayeyaweka mawazo yako mbele na  akikosea hasiti kuomba msamaha, mtu ambaye ukiwa naye unajisikia Amani kuliko ukiwa na mwingine yeyote.

 Kuwa wachangamfu (having fun)
Uhusiano wako ni salama, mpenzi wako ni msaidizi wako, uhusiano wako ni mbingu ndogo hapa duniani hauna haja ya kujificha na kutojionyesha wewe ni nani (the real you) ili tu mwenza kwako akukubali.

Ni ninyi wawili tu duniani, Hakuna mwingine, hivyo mnapokuwa na nafasi, furahini, kila mmoja awe huru kwa mwenzake.

Madhara ya Kubana Mkojo Kwa Muda Mrefu

0
0

Madhara ya Kubana Mkojo Kwa Muda Mrefu
Watu wengi huvumilia mkojo kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi wanaweza wakawa katika eneo ambalo hawezi kwenda haja ndogo lakini wengine ni uzembe ambapo wengi utakuta anaangalia tamthilia hivyo hataki apitwe, au anaona akienda haja ndogo hadi arudi umbea unaopigwa utampita na hivyo anaamua kubana mkojo, hayo yote yana madhara kwa mwili wako.

Je! Wewe hukojoa mara ngapi kwa siku? Mbili?, Tatu? Tano? Kwa mujibu wa watalaamu mbalimbali, wamesema kuwa kila mtu anatakiwa kukojoa kila baada ya saa 4 hadi 6, lakini kama utashikilia mkojo wako kwa muda zaidi, utakuwa uanajiweka kwenye hatari ya kukumbwa na matatizo mbalimbali.

Haya ni baadhi ya madhara yatakayokupata endapo utabana mkojo kwa muda mrefu zaidi;

1. Kujikojolea

Kwa mujibu wa Daktari Lauren Streicher akifafanunua hili alisema kwamba, mtu anapaswa kufikiria kibofu chake kama puto ambalo limejazwa maji kupitiliza. Puto hilo likatanuka hadi mwisho wake na kuwa zito, kadiri utakavyokuwa unazidi kuubana, ndivyo itakavyokuwa vigumu kwako wewe kutembea hadi chooni kabla hujajikojolea.

Itakuwa ni aibu kwa mwanamke mtu mzima kujikojolea eti kwa sababu hakwenda chooni kwa kunogewa na muvi au umbea ambapo pengine hauna faida.

2. Kulegea kwa misuli ya Pelvic

 Misuli ya Pelvic hutumika katika kuzuia mkojo usitokea au kuuruhusu utoke katika kibofu cha mkono. Ukiwa na tabia ya kubana mkono kwa muda mrefu sana, misuli hii itachoka na hivyo kuacha kufanyakazi kwa usahihi. Hilo linapotokea unashindwa kuzuia tena mkojo wako sababu misuli imelegea na hivyo mkojo ukija unapita moja kwa moja.

Hivyo, epuka kuharibu misuli hiyo kwa kubana mkojo kwa vitu ambavyo sio vya msingi. Kila unapohisi mkojo nenda kakojoe kisha rudi, endelea na ulichokuwa unafanya.

3. Maumivu

Kwa kawaida unaposhikilia mkojo kwenye kibofu kwa muda mrefu, unapatwa na maumivu makali, lakini maumivu hayo hutokomea mara tu unapokwenda haja ndogo. Maumivu hayo yanaweza yakawa ni mfumo wako wa maisha kama hutachukua tahadhari mapema.

Waswahili husema kuwa, tabia hujenga mazoea, na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa misuli ya mwili wako, ukizoea kubana mkojo kila mara, itakua ikiima kila mara.

4. Kutanuka kibofu

Basi tusema kwamba ukibana mkojo kwa muda mrefu, kibofu chako kinaweza kisipasuke kutokana na wingi wa mkojo lakini kikatanuka kuliko ukubwa wake unaotakiwa.

Tatizo la kutanuka kwa kibofu kutokana na kubana mkojo mara kwa mara ni kwamba mwili wako utakuwa haukupi taarifa kuwa unatakiwa kwenda kujisaidia. Hii ni kwa sababu umbo la kibofu limeongezeka. Taarifa hizo ambazo hutolewa na ubongo wakati kibofu kimejaa ni muhimu sana, lakini kibofu kikitanuka hutozipata.

Ni kweli wakati mwingine unaweza ukabanwa na mkojo na kuwa sehemu ambayo huweza kupata msaada ya kujisaidia, lakini epuka tabia hii kuwa mazoea.

Mahujaji 35 Wafariki Makkah Siku ya Kwanza ya Hijja......

0
0
Mahujaji 35 Wafariki Makkah Siku ya Kwanza ya Hijja......
Wizara ya Afya ya nchini Misri imeeleza kuwa Mahujjaj 35 wa nchi hiyo wamefariki dunia wakati wa siku ya kwanza ya Hijja iliyomalizika nchini Saudi Arabia kutokana na uchovu na umri mkubwa.

 Afisa mmoja wa Wizara hiyo, Ahmed el Ansary, amesema umri wa Mahujjaji waliofariki ni kati ya miaka 60 hadi 85.

Katika Ibada ya Hijja ya mwaka huu zaidi ya Mahujaji milioni mbili walihudhuria wakiwemo milioni 1.8 kutoka nje ya nchi.

Nyota ya Wema Sepetu Yazidi Kung'aa Apata Dili Nono la Milioni 400

0
0
Nyota ya Wema Sepetu Yazidi Kung'aa  Apata  Dili Nono la Milioni 400
Staa mkali wa sinema za Kibongo asiyechuja Bongo, Wema Isaac Sepetu, anadaiwa kulamba dili nono la shilingi milioni 400 kutoka kwenye kampuni moja kubwa ya ving’amuzi Afrika yenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini.

Habari kutoka kwenye chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa staa huyo zilieleza kuwa, dili hilo alilopata Wema ni kwa ajili ya kutengeneza tamthilia na sinema kupitia kampuni yake ya Endless Fame ambazo zitaruka kwenye kituo hicho na kuambulia donge hilo nono.

“Wema sasa hivi atakuwa mtu mwingine kabisa kwa sababu dili hilo akikabidhiwa kabisa atarejea kwenye ile status yake ya kuitwa pedeshee mwanamke na hata marafiki waliokuwa wameyeyuka watarudi,” kilinyetisha chanzo hicho.
Mpashaji huyo aliendelea kufunguka kuwa, Wema anatarajia kuwakusanya kampani yake yote ya Endless Fame kwa ajili ya tenda hiyo ambayo itakuwa ni ya aina yake.

Baada ya kudaka habari hizo njema kuhusu Wema ambaye wengine humuita ‘Keki ya Taifa’ au ‘Tanzania Sweetheart’, Ijumaa Wikienda lilimsaka lakini halikufanikiwa badala yake lilimpata mmoja wa waratibu wa kazi zake ambaye alikiri kuwepo kwa dili hilo, lakini bado halijakamilika mpaka leo (Jumatatu).

“Duh! Ninyi noma, mmeinyaka? Ni kweli hilo dili lipo, lakini nafikiri litakamilika Jumatatu ijayo (leo),” alinyetisha mdau huyo.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, simu ya Wema ilikuwa ikiita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS hakuwa amejibu

Marekani Kuipiga Korea Kaskazini Ikimgusa Mshirika Wake

0
0
Marekani Kuipiga Korea Kaskazini Ikimgusa Mshirika Wake
Waziri wa masuala ya ulinzi wa marekani James Mattis amesema kuwa tishio lolote kutoka korea kaskazini kwa Marekani ama washirika wake litajibiwa vikali na jeshi.
Mattis amezungumza hayo baada ya mkutano wake na Rais Trump juu ya masuala ya usalama wa nchi kufuatia jaribio la nyuklia huko Pyongyang.
Trump ameonya kuwa Marekani inaweza kusimamisha kufanya biashara na nchi yoyote inayoshiriki biashara na Korea Kaskazini.

China ndio mshirika mkuu wa baishara na Pyongyang, ameongeza kuwa korea kaskazini imekua tishio na imeleta fedheha kwa Beijing.
Alivyoulizwa na waandishi wa habari kama Marekani itashambuliwa na korea kaskazini, rais trump alisema kuwa tutaona''
Nayo korea kusini imesema kuwa imefanya majaribio matano kama majibu ya jaribio la nyuklia la korea kaskazini.

Rais wa Urusi na Raisi wa china wote wamesisitiza juu ya umuhimu wa kuondokana mzozo wa Korea.
Nao Japan wamesema kuwa jaribio hilo si la kusamehewa.

Jaribio hilo ni la sita kufanywa na kore kaskazini katika kipindi cha miaka 10.
Limesababisha tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 lilifika katika mkoa wa china uliokaribu na Korea Kaskazini.

Gabo Ndio Chanzo cha Kulega kwa Soko la Filamu Hapa Nchini- Duma

0
0
Gabo Ndio Chanzo cha Kulega kwa Soko la Filamu Hapa Nchini- Duma
Msanii wa filamu bongo, Duma amedai kwamba muigizaji mwenzake, Gabo Zigamba ndiye chanzo cha sanaa ya filamu kulega kwani ameaminiwa na watanzania wengi lakini ameshindwa kuwatendea haki kwa kutoa kazi tangu alipopata tuzo mwezi wa 12 mwaka jana.

Povu la Duma limekuja hivi karibuni alipofanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari kumpelekea kusema kuwa Gabo ni kirusi  kwenye filamu za bongo kwani anashindwa kujituma kama jinsi yeye anavyofanya

"Soko la filamu nchini ukweli halipo vizuri hususani kulega kwa filamu. Lakini yote haya yanasababishwa na Gabo kwa kushindwa kufanya kazi zake kama msanii. Unajua Watanzania wanamapenzi makubwa na Gabo lakini yeye ni msanii asiyejali. Alipopata tuzo mwaka jana tulijua kuwa angefanya mambo makubwa lakini cha ajabu ndiyo mzimekwenda kumpoteza. Naona anafurahi kuziona zikiwa zimejaa vumbi huku wananchi wakilia kupata muvi" Duma.

Duma ameongeza kuwa "Kuwapa watu filamu za 'online' hakukati kiu ya watu kutaka kuona kitu unachokifanya. Mfano mimi hapa nina muvi zangu nyingi zilizopo sokoni na zinafanya vizuri sana. Je yeye kwa nini asiitwe virus kwa kushindwa kufanya kazi? Sanaa inamuhitaji lakini yeye haijali ndiyo maana haoni umuhimu wa kufanya hata kazi za kimataifa.

Pamoja na hayo Duma amesema Gabo hana  hadhi ya kuitwa staa kwani hana muonekano wa kisanii ndiyo maana anakosa hata mialiko mikubwa mikubwa.
"Gabo hana ustaa wowote, hana muonekano wa kisanii. Msanii gani anavaa suti moja kwenye 'event' tatu tofauti. Kama wewe ni msanii unatakiwa uwe na Swagg, muonekano uwe mzuri uweze kupata mialiko hata ya  special appearance kwa sababu hajui atatokaje. Duma aliongeza.



"Mimi nafanya kazi, Gabo ni kirusi kwenye tasnia ya filamu. Kwahiyo kama anataka kubadilika abadilike kwasababu huwezi kuwa staa halafu unaishi maisha sawa na watu wa kawaida. Mimi siyo shabiki wake na wala yeye siyo role model wangu lakini namwambia atoe kazi" alimaliza
Hata hivyo Baada ya Gabo kupigiwa simu kuhusu kujibu tuhuma za Duma alisema hawezi kumjibu Duma anaye mtuhumu hajui kuigiza, kwani mwaka 2017 watu sio wajinga tena.


Ali Kiba Kuwapa Mashabiki Wake Raha Katika Tamasha la Fiesta Jumamosi

0
0
Ali Kiba Kuwapa Mashabiki Wake Raha Katika Tamasha la Fiesta Jumamosi
MKALI wa Ngoma ya Seduce Me, Ali Kiba, anatarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasanii wa muziki watakaoangusha burudani Jumamosi hii (Septemba 9) katika Tamasha la Tigo Fiesta ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo ambao ndiyo wadhamini wa tamasha hilo, William Mpinga amesema tayari wanamuziki zaidi ya 17 akiwemo Kiba wameshasajiliwa kwa ajili ya kutoa burudani katika Tigo Fiesta ambayo itafanyika mikoa mbalimbali.
“Hadi sasa wasanii zaidi ya 17 akiwemo Kiba, Christian Bella, Shilole, John Makini, Mr. Blue, Saida

Karoli na wengine wameshasajiliwa, huu ni muda wenu wapenzi wa burudani kukata tiketi mapema kwa njia ya Tigo Pesa kupitia namba 0678888888 ambapo litatokea jina la Tigo Fiesta na atakayefanya muamala huo atapatiwa tiketi yake kwenye maduka ya tigo mkoa linapofanyika tamasha,” alisema Mpinga na kuongeza kuwa kwa mteja atakayenunua tiketi kwa njia hiyo atapata punguzo la asilimia 10.

Huyu Ndio Njiwa Aliyetumiwa Kusafirisha Mihadarati Hadi Gerezani

0
0
Huyu Ndio Njiwa Aliyetumiwa Kusafirisha Mihadarati Hadi Gerezani
Polisi nchini Argentina walimpiga risasi njiwa ambaye alitumiwa kusafirisha mihadarati kwenda gereza moja, kwa mujibu wa mamlaka za gereza.
Njiwa huyo alionekana akiruka hadi uwanja wa gereza lililo mji wa Santa Rosa.

Maafisa waligundua kuwa ndege huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake uliokuwa na vidonge vya madawa ya kulevya.
Njia hiyo ya kusafirisha madawa ilikuwa imegunduliwa na ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi.

Gazeti la Clarin lilichapisha picha ya njiwa huyo akiwa na mfuko mweupe uliokuwa na tembe 44 za madawa ya kulevya.
Magereza nchini Argentina yalionya mwaka 2013 kuwa walanguzi wa madawa ya kulevya walikuwa wakitumia njiwa waliokuwa wakifanya safari mara 10 hadi 15 kwa siku.

Watu watatu walikamatwa na njiwa 15 kupatwa baada ya uchunguzi wa mwaka 2013.
Mapema mwaka huu njiwa ambaye alikuwa na mfuko uliokuwa na tembe 178 za dawa ya kulevya alishikwa nchini Kuwait karibu na mpaka na Iraq.

Chid Benz: Madee ni Mbea na Mnafki

0
0
Chid Benz: Madee ni Mbea na Mnafki
Rapa Chid Benz ambaye kwa sasa amekuwa gumzo katika kila kona ya mitandao ya kijamii baada ya yeye kusema ana kolabo na 2pac, amefunguka kwa kumtolea povu Madee na kumwambia yeye ni mbea ndiyo maana haishi kumnanga kila kukicha.

Chid Benz ameeleza hayo kupitia kipindi cha 'Friday Night Live' (FNL), kinachorushwa na EATV pamoja na EA Radio baada ya siku kadhaa kupita tokea alipofanyiwa 'interview' na eNewz na kudai ana kolabo na 2pac, jambo ambalo watu wengi waliamini msanii huyo ameanza kuharibikiwa akili kutokana na dawa za kulevya na kupelekea Madee kutoa maoni yake binafsi kwa kudai ni bora yeye ambaye havuti hata sigara.

"Unaweza ukawa huvuti hata sigara lakini ukawa mbea, kwa sababu Madee watu tumnajua kama ni mbea na mnafki maana anapenda kuninanga, anahisi labda mimi ipo siku nitafanya kitu", alisema Chid Benz.
Pamoja na hayo Chid Benz aliendelea kwa kusema "mtu kama anaku-post kitu katika mitandao ya kijamii halafu chini yake anakuandikia 'ndiyo maana mimi sivuti hata sigara''that means' anaonyeshea watu kwamba kuna kitu Chid Benz anatumia au anavuta ndiyo maana yeye hatumii sigara kwa hiyo mimi amenitengenezea ubaya mpaka kupelekea watu ku-comment kwamba madawa yamenisababisha nichanganikiwe", alisisitiza Chid Benz



Kinara wa Utekaji Watoto Arusha na Geita Answa Kwenye Nyumba ya Kulala Wageni

0
0
Kinara wa Utekaji Watoto Arusha na Geita Answa Kwenye Nyumba ya Kulala Wageni
Matukio ya utekaji watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi baada ya kijana wa miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alipokamatwa katika Mji wa Katoro wilayani Geita alikofanya tukio jingine la utekaji.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Samson Petro alisema watoto wawili aliwarudisha kwa wazazi wao baada ya kupewa Sh300,000.
Alisema wengine wawili aliwatelekeza mtaani baada ya wazazi wao kutotoa kiasi cha fedha walichotakiwa kumpa.

Samson alisema alianza ‘shughuli’ hiyo ya utekaji watoto kutokana na mahitaji ya fedha na kwamba, aliacha shule akiwa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lutozo iliyopo Katoro.
“Naishi na wazazi wangu, lakini nao ni masikini, nilifanya hivi ili nipate fedha na nilikuwa nikimchukua mtoto naandika ujumbe kwenye karatasi, naandika na namba ya simu napeleka karibu na familia ili wanitafute,” alisema Samson.

Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema walimkamata kijana huyo katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mjini Katoro juzi saa mbili usiku.

Mwabulambo alisema polisi mkoani Geita kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha walifanya uchunguzi na kubaini mtuhumiwa alikuwa Katoro.
Alisema walipata taarifa za kutekwa Justin Ombeni (2) Septemba Mosi nyumbani kwao katika eneo la Shilabela ambako mtuhumiwa alikwenda na kuwakuta watoto wanne wakicheza nyuma ya nyumba.
Alisema aliwagawia pipi na kuondoka na Justin. Kamanda huyo alisema polisi ilipata taarifa kuwa kijana huyo yupo chumba namba 103 katika nyumba hiyo ya wageni ambako waliweka ulinzi kuizunguka.
Alisema walipoingia katika chumba hicho walimkuta akiwa na
mtoto huyo. Mwabulambo alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. 
Ombeni Mshana ambaye ni baba wa Justin alisema mtekaji huyo alimpatia ujumbe mtoto wa jirani uliomtaka kutuma Sh4 milioni na walipokuwa wakiwasiliana na mtuhumiwa alishusha kiwango hadi Sh1 milioni. 
Alisema polisi walimtahadharisha kwamba asitume fedha hizo.Kamanda Mwabulambo alisema tukio la kutekwa Justin ni la pili katika kipindi cha miezi minne baada ya mwingine kutekwa. 

Kesi kuhusu tukio hilo la kwanza inaendelea mahakamani baada ya mtoto kupatikana.

Katika hatua nyingine, kikosi kilichoundwa na wananchi mkoani Arusha kikiongozwa na mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Kata ya Olasiti, Daudi Safari na familia za watoto wawili waliotekwa kimewakamata watuhumiwa wawili na kuwafikisha polisi.
Watoto hao ambao bado hawajapatikana ni Moureen David (6) anayesoma darasa la kwanza shule ya msingi Lucky Vincent na Ikram Salim (3).
Wakizungumza jana nje ya kituo kikuu cha polisi Arusha baada ya kuwafikisha kituoni watuhumiwa hao, Safari na wazazi wa watoto hao, David Njau na Salim Kassim walisema kwa nyakati tofauti wameanzisha msako baada ya
kuona siku zinakwenda bila watoto kupatikana.
Moureen alitekwa Agosti 21 saa 11 jioni akiwa anacheza nyumbani kwao eneo la Olasiti, wakati Ikram alitekwa Agosti 26 saa 12 jioni akiwa anacheza na watoto wenzake nyumbani kwao, Burka – Olasiti.
Safari alisema wamemkamata mtu mmoja (jina linahifadhiwa)
ambaye simu yake ilitumiwa na watekaji kuomba fedha kwa mzazi wa Ikram Salim.
Alisema pia wamemkamata wakala wa fedha wa kampuni moja ya simu (jina tunaihifadhi) aliyetoa Sh300,000 kwa watekaji baada ya fedha kutumwa na mzazi wa Ikram.
Imeelezwa kuwa wakala huyo amekamatwa kwa kuwa fedha hizo zilitolewa pasipo kuorodheshwa popote na mpokeaji hakuonyesha kitambulisho chochote.
Akizungumzia operesheni hiyo, Njau alisema hawatapumzika mpaka watoto wao wapatikane.

Alisema ufuatiliaji walioufanya kupitia minara ya kampuni za simu unaonyesha wahusika walikuwa eneo la Kwa Mrombo jijini Arusha walipopiga kuomba Sh4.5 milioni ili wamwachie Doreen na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya Ikram.
Watekaji hao kupitia ujumbe waliotuma nyumbani kwa Njau walidai kama wasipopewa fedha wangempoteza mtoto huyo japokuwa hawana nia hiyo.

Kassim Salim ambaye ni babu wa Ikram alisema, “tunaendelea kuomba msaada zaidi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na vyombo vya dola watusaidie tuwapate watoto wetu.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema juzi kuwa watu watatu wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo akiwapo dereva wa bodaboda mkazi wa Olasiti aliyetumwa kuwarejesha watoto wawili waliokuwa wametekwa.
Matukio ya utekaji yalianza kuibuka Agosti 21 baada ya kutekwa watoto wanne. Watoto wawili Ayoub Fred na Bakati Selemani wakazi wa eneo la FFU, kata ya Murieti jirani na kata ya Olasiti walirejeshwa

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumatatu

0
0
Viewing all 104427 articles
Browse latest View live




Latest Images