Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

Tanzania Yajipanga Kwenda India Kujisafisha Sakata la Madalali Tapeli wa Zao la Korosho

$
0
0
Tanzania Yajipanga Kwenda India Kujisafisha Sakata la Madalali Tapeli wa Zao la Korosho
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage  amekiri kupokea wito wa kwenda nchini India kwa ajili ya kusafisha jina la Tanzani baada ya watu wanaodaiwa ni madalali tapeli wa zao korosho kulichafua.

Mh. Mwijage ameyasema hayo jana ambapo amedai kuwa anaoushahidi  kuwa kampuni hizo za udalali zilivyochafua jina la nchi hivyo ni lazima awafikishe katika mikono yua sheria.
“Vitendo hivi vinavyofanywa na makampuni haya havivumiliki kwani mchezo huu ni mauti kwetu na nitahakikisha wanachukuliwa hatua kwani ninao ushahidi unaotosheleza,”alisema Mwijage.

Mh. Mwijage amefafanua kwa kusema kwamba watu wametapeliwa kwa kuambiwa pindi wanapoagiza mazao kuwa watoe pesa ya kianzio ambayo ni kuanzia dola za Marekani 123,000, sawa na Sh275 milioni na dola 200,000 sawa na Sh448milioni za kitanzania.
“Nimepokea wito kutoka India kwa ajili ya kwenda kusafisha jina la nchi kutokana na taswira ilisababishwa uwepo wa matapeli hao,”alisema Mwijage.



Masogange Ajutia Ustaa Wake

$
0
0
Masogange Ajutia Ustaa Wake
VIDEO queen mwenye umbo tata Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa, hakuna jambo analolijutia kama kuwa staa.

Masogange aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, alipokuwa hajulikani alikuwa akifanya vitu vyake kwa uhuru bila kutazamwa na mtu yeyote tofauti na sasa.

“Unajua mtu anaweza kusema ukiwa na jina unakuwa furaha sana, lakini si kweli kabisa, kuna wakati najuta huwa nakosa uhuru wa kufanya kitu chochote kama binadamu wa kawaida,” alisema Masogange mwenye umbo la kuvunja shingo za wanaume wakware.
Stori: Imelda Mtema, Dar


SOMA Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Vituo vya Mitihani ya Darasa la Saba Vitakavyofanya Udanganyiu Kukiona- NACTE

$
0
0
Vituo vya Mitihani ya Darasa la Saba Vitakavyofanya Udanganyiu  Kukiona- NACTE
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA), limetishia kuvifutia usajili vituo vyote vya kufanyia mitihani ya Darasa la Saba inayotarajiwa kufanyika kesho Jumatano Septemba 6 na Alhamisi, Septemba 7, 2017 nchini kote.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde wakati akizungumza na wanahabari Makao Makuu ya NECTA, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

“Baraza linawataka wamiliki wa shule zote kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya kufanyia mitihani, hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani hiyo.

“Baraza halitasita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo litabaini na kuthibitisha pasina shaka kuwa kituo hicho kinajihusisha na udanganyifu wa mitihani. Tunatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa kipindi hiki cha ufanyikaji wa mitihani ili wanafunzi wafanye kwa utulivu.

“Tunawaasa walimu, wamiliki wa shule, wasimamizi na jamii kwa ujumla kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote. Wataokiuka haya hatutasita kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi,” alisema Msonde.

Awali alieleza kuwa wanafunzi hao watafanya masomo matano ambayo ni: Kiswahili, Hisabati, Maarifa ya Jamii, Sayansi na English ambapo mitihani hiyo imeshasafirishwa kupelekwa vituoni.
   

Sasa Ntawaonyesha Udhaifu Wangu Mliokuwa Mnasema- Ndugai

$
0
0
Sasa Ntawaonyesha Udhaifu Wangu Mliokuwa Mnasema- Ndugai
Mara baada ya kikao cha kwanza kwenye mkutano wa 8, wa Bunge la 11, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amesema wale waliokuwa wanamtuhumu kuwa mdhaifu katika kufanya maamuzi, sasa wataona dhahiri udhaifu wake uko wapi.

Spika Ndugai ameeleza hayo wakati akiwakaribisha wabunge 7 wapya wa Chama cha Wananchi (CUF) waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

“Taratibu zote zilifuatwa kwa wabunge hawa kuingia hapa bungeni, wapo baadhi ya lile kundi wiki mbili kabla ya mambo haya kutokea walisema Spika dhaifu, nikasema sasa udhaifu wangu ndiyo utaonekana. Kama una akili yako maneno kama haya hayana umuhimu”, alisema Spika Ndugai.
Samabamba na hilo, Spika Ndugai aliwakaribisha wabunge walioapishwa huku akiwafunda wabunge wengine, kwamba kiapo walichokula wenzao leo kiwa kumbushe utii na uaminifu kwa kwa tiba ya nchi.

“Kiapo hiki cha uaminifu kina tukumbusha wengine ambao tuliapa utii wa Katiba na kiapo chetu kwa ujumla wake, kuhusiana na uaminifu na utii.  Ni vizuri kuisoma Katiba na kuipitia ili uweze kujua nafasi ya vyama vya siasa na uhusiano wa mbunge na chama cha siasa”, alisisitiza Spika Ndugai.
Wabunge hao walioapishwa leo wanatarajiwa kupangiwa kamati na kuanza kazi mara moja, kama ambavyo Spika amewataka kufanya hivyo.

Polisi Yamkabidhi Manji Mahakamani Baada ya Kumaliza Kumuhoji

$
0
0
Polisi Yamkabidhi Manji Mahakamani Baada ya Kumaliza  Kumuhoji
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemkabidhi mfanyabiashara Yusuf  Manji na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumaliza kumuhoji katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa washtakiwa hao wamerudishwa kama Mahakama ilivyoamuru warudishwe baada ya Polisi kumaliza kuwahoji.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itaendelea na utaratibu kama ilivyo awali, ambapo ameahirisha hadi September 8, 2017.

Awali Mahakama hiyo iliruhusu Yusuf Manji na wenzake watatu kwenda kuhojiwa na Polisi kwa lengo la kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi wanayokabiliwa nayo.

Mbali na Yusuf Manji, washitakiwa wengine waliokabidhiwa ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza Stoo, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.






TRA Yatoa Ufafanuzi Deni la Trilion 424 Inayoidaiwa Acacia

$
0
0

TRA Yatoa Ufafanuzi Deni la Trilion 424 Iayoidai Acacia
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa deni la Tsh 424 trilioni inayoidai Migodi ya Bulyanhulu  Gold Mine (BGML) na Pangea Minerals (PML) inayoendeshwa na Acacia limekokotolewa na wataalamu wa kodi waliobobea waliokuwa miongoni mwa wajumbe  wa kamati mbili za kuchunguza makinikia zilizoteuliwa na Rais Magufuli.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na gazeti la MTANZANIA jana, Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa TRA, Gerald Mwanilwa alisema,

“Deni la Acacia halikuja kibahati mbaya, lilikokotolewa na wataalamu wabobezi wa masuala ya kodi tangu (BGML na PML) walipoanza kukwepa kodi hadi tulipobaini jambo ambalo limesababisha deni kuonekana kubwa.”

Afisa huyo alisema kwamba, wote wanaodhani TRA imezikomoa kampuni hizo kwa kuzipa deni hilo, wanakosea kwa sababu deni hilo limetokana na malimbikizo ya ukwepaji kodi.

Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Acacia baada ya kupata madai hayo ya TRA ilionyesha kuwa deni hilo la USD 190 bilioni, BGML wanadaiwa USD 154 bilioni na PML wakidaiwa USD 36 bilioni.

Katika USD 190 bilioni, USD 40 bilioni ni malimbikizo ya kodi na USD 150 bilioni zikiwa ni riba na faini kutokana na kukiuka sheria.

Hivi Ndivyo Balozi Nyumba 10 Alivyosimulia Alivyoona Kichwa na Kiwiliwili Vikiungua kwa Mganga

$
0
0
Balozi Nyumba 10 Asimulia Alivyoona Kichwa na Kiwiliwili Vikiungua kwa Mganga
Balozi wa Nyumba 10 katika Kitongoji cha Chang’ombe Kijiji cha Chamwino Ikulu, Simango Asheri amesema alishuhudia mwili wa Mariam Said (17) anayedaiwa kuuawa nyumbani kwa mganga wa kienyeji, Ashura Mkasanga (33) ukiwa utupu, umetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku ukiungua moto kichwani.

Mauaji hayo yalitokea Agosti 8 mwaka huu saa 10 usiku, umbali wa kilometa mbili kutoka mahali ilipo Ikulu ya Chamwino mkoani hapa.

Akizungumza nyumbani kwake hivi karibuni Asheri alisema wakati akiwa anafanya shughuli zake za ujenzi nyumbani kwake saa 3 asubuhi alipita mwenyekiti wa tawi la CCM akamweleza kuhusu tukio hilo.

“Akaniambia kuna mtu kafa kwa Malita Mkasanga (Ashura), tukakimbia (kwenda) mwenzangu alikuwa na baiskeli mimi nilikuwa peku, tukafika tukakutana na wazee wamekaa tukakaribishwa nendeni mkaangalie tukio,” anasema.

“Tulipofika ndani tukakuta mtu amelala chali sebuleni kuangalia tukaona moto unaendelea kufuka kichwani, alikuwa hana nguo, tulitoka lakini baada ya muda tuliingia tena kutazama tukakuta shingo imesogezwa kwa kukatwa,” anasema.

Balozi huyo anasema walipomuuliza Ashura ilikuaje hadi mtu huyo akafia nyumbani kwake, aliwaambia kuwa akiwa amelala ndani mtoto wake wa kiume alisikia kelele nje.

“Alituambia kuwa marehemu alipiga mlango na kuingia ndani na kudondoka sebuleni huku moto ukaendelea kuwaka, tuliendelea kumuhoji kama mlango uliokuwa umefungwa aliupiga na kuingia ndani mbona ni mzima haukuvunjika, alijibu hata yeye anashangaa,” anasema.

Alipobanwa na wazee wa kijiji kuhusu ni wapi majivu yaliyokuwa ndani ya nyumba hiyo yalipotokea, aliwajibu kuwa hata yeye anashangaa kwa sababu hajui yalipotoka.

“Alipoulizwa kuhusiana na mchanga uliokuwepo ndani ya nyumba hiyo, pia alijibu anashangaa ulipotokea. Kutokana na majibu hayo tulimwacha tukiwasubiri polisi waje,” anasema.

Asheri anasema kuwa pembeni mwa mwili wa marehemu kulikuwa na lundo la mchanga ambalo baada ya kufukuliwa ilibainika kuwa chini kulikuwa na damu iliyofukiwa.

 Uhalali wa kazi ya mganga

Hata hivyo, balozi huyo anapoulizwa iwapo alikuwa anafahamu kuwa Ashura alikuwa mganga wa kienyeji, anasema hafahamu na kwamba watu wanaofanya shughuli hizo kijijini hapo wote wanajulikana.

“Wanasema kuwa ni mganga, lakini mimi tangu amehamia hapa miaka mitano hivi namfahamu kama mkulima na mumewe anafanya kazi katika gari moja la kusombea mchanga huko,” anasema.

Badala yake anasema kuwa Ashura alikuwa akishiriki vizuri shughuli za jamii yake kwa kuchanga michango mbalimbali na  kushiriki kwenye mikutano ya kitongoji na kijiji.



Ndugu wachukua watoto

Mjomba wa mumewe wa mganga huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, anasema baada ya tukio hilo polisi waliwachukua watu wote waliokuwepo ndani ya nyumba hiyo wakiwemo watoto.

“Lakini baadaye tuliambiwa kuwa watoto wameachiwa wamerudi nyumbani, tukaamua twende tukawachukue ili ndugu wa marehemu wasije wakawadhuru,” anasema.

Anasema watoto hao walipelekwa kwa bibi yao na wataishi huko hadi wazazi wao watakapomaliza matatizo yaliyojitokeza.

“Huyu ndugu yetu awali alikuwa akiishi na dada yangu, lakini walikuwa hawaelewani kwasababu mama yake alikuwa akimwambia aachane naye kwasababu ni mshirikina lakini alikataa,” anasema.

Anaongeza kuwa baada ya muda walinunua shamba na hivyo kuondoka kwa mama yake na kwenda kuanzisha mji wao.

Hata hivyo, mmoja wa watoto wa mganga huyo, (jina tunalihifadhi), anasema kuwa siku ya tukio hakulala nyumbani.

“Niliporudi nyumbani asubuhi ndiyo nilikutana na tukio hilo wala sikufahamu ilikuaje,” anasema mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika moja ya shule wilayani humo.

 Nyumbani kwa mganga

Mazingira ya nyumba hiyo ambayo ipo umbali wa takriban mita 300 kutoka kwa majirani zake, yamegubikwa na utulivu mkubwa huku milango ikiwa imefungwa.

Nje ya nyumba hiyo iliyojengwa kwa matofali ya udongo kuna kisima kilichochimbwa kienyeji kikiwa na maji machache, mabua ya mtama uliovunwa na pembeni kukiwa na nyumba iliyoanza kujengwa kwa matofali ya saruji.

Inaelezwa kuwa katika nyumba ya jirani kuna mzee anaishi lakini hata hivyo wakati mwandishi wa habari hizi

anafika hakukuwa na mtu.

Hata hivyo, tofauti na matukio mengine hakuna kiongozi wa kijiji hicho cha Chamwino Ikulu aliyekuwa tayari kuelezea tukio hilo kwa sababu mbalimbali.

 Waganga wazungumza

Akizungumza hivi karibuni mmoja wa waganga wa tiba asilia mjini hapa, Dk Harun Kifimbo anasema Serikali ihakikishe mipango inayopangwa kudhibiti watu wanaojifanya waganga wa tiba asilia inasimamiwa.

“Tatizo pia liko kwa baadhi ya waratibu wanaotoa vyeti kwa waganga wasiostahili na ndiyo wanaofanya mambo haya ambayo yanaenda kinyume na tiba ya asili,” anasema Kifimbo.

Anasema chama cha waganga wa tiba asili mkoani Dodoma kimepanga kuendesha msako na kuwakamata watu wanaojishughulisha na tiba hizo bila kuwa na leseni, cheti cha kuthibitishwa mahali wanapofanyia kazi zao na dawa zao kutokuwa na usajili kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, anawalamu baadhi ya waganga kuwa wamekuwa wakijiharibia mambo yao wenyewe kwa kufanya mambo ambayo yanakatazwa kisheria wakati Serikali imewawekea mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa ambaye sasa amehamishiwa Dar es Salaam, alisema waliwakamata watuhumiwa 11 na kuwahoji, kati yao watano wanaendelea kuwa chini ya ulinzi.

“Kule Chamwino wanamamlaka ya kuwafikisha mahakamani wakimaliza uchunguzi wao,” anasema.

Mambosasa alisema jumla ya watu 11 walikamatwa katika tukio hilo ambalo Mariam aliuawa kwa kukatwa shingo yake na kutenganishwa na kiwiliwili na kuchomwa moto kichwa chake na kubakia vufu lisiloweza kutambuliwa sura yake.

“Baadhi ya sehemu za mwili wake ziliunguzwa kwa moto ambazo ni mkono wa kushoto, shingo, kifuani na sehemu za siri,” alisema.

Alisema mazingira ya tukio hilo yanaonyesha kuwa mganga huyo asiyekuwa na kibali cha kuendesha shughuli za tiba asili analaza wagonjwa nyumbani kwake, anafanya matambiko, anapiga ramli chonganishi na anafanya tohara.

“Katika nyumba yake alikutwa kalaza watu wanane kati yao wanawake sita na wanaume wawili,” anasema.

Hata hivyo, anasema hakuna maelezo ya kutosha jinsi gani marehemu alifika kijijini hapo kutoka Kigoma na kwamba polisi inafanya uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

“Tukio hili halikubaliki hapa Dodoma na mahali popote ni fedheha kubwa sana kwa wanachamwino kuendelea kukumbatia ushirikina katika karne hii na Serikali imesogeza huduma za afya karibu na jamii, lakini bado hawataki kwenda kutibiwa hospitali na kukubali kuuawa kwa fedheha na waganga wachonganishi wa jadi,” anasema.


Quick Rocka Atoboa Siri ya Wasanii Kukopa Kwenye Musiki

$
0
0
Quick Rock Atoboa Siri ya Wasanii Kukopa Musiki
C.EO wa Switch Music Group(SMG) Quick Rock ametoa ufafanuzi juu aina ya muziki unaofanywa na kundi la OMG kutoka  ya lebo yake.

Msanii huyo amesema kuwa hakuna msanii anayefanya muziki  bila  kopi muziki  kutoka sehemu nyingine.

“Hakuna msanii mwenye style yake kila msanii kuna mtu amemu-inspire mimi sikuanza tu kuchana, nilianza kuimba kwaya kanisani Sunday Schoo lakini mimi kuchana Tang twist wakati nipo sekondari nilikuwa nasikiliza sana nyimbo za Buster Rhymes nilikuwa napenda kumsikiliza sana A.Y nilikuwa napenda kumsikiliza sana marehemu Mangwear na wengineo nilivutiwa sana na aina yao ya muziki,” amesema Quick Rock

Akaongeza “Nawaona mbali sana OMG  kwa sababu there very talented wana displine na wanapenda sana muziki na kitu wanachofanya, nawaona mbali sana kikubwa nacho waambukiza kuwa there is busness in music, unaweza ukawa unapenda sana muziki ukawa attach sana na muziki then ukasahau kuwa muziki ni biashara, so love the music , enjoy the music make music but don’t for get is busness.”




Natumia Mitandao ya Kijamii Kutoa Habari Zangu Mara kwa Mara Ila Sitengenezi Kiki- Diamond

$
0
0
Natumia Mitandao ya Kijamii Kutoa Habari Zangu Mara kwa Mara Ila Sitengenezi Kiki- Diamond
Msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnumz amekana suala la kutengeneza kiki katika mitandao ya kijamii.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Love You Dia’ aliyoshirikishwa na Patoranking, ameiambia Radio Maisha, Kenya kuwa mitandao yake anaitumia kuwajuza mashabiki taarifa mbali mbali na sii vinginevyo.

“Hamna, mimi kama kwa mfano kwenye Instagram na kwenye mitandao yangu ya kijamii nawapa habari zangu zinazotokea mara kwa mara. Kazi yangu mimi ni ya muziki, kwa hiyo watu wanakuwa wanaburudika,” amesema Diamond.

“Huwa naweka mwenyewe, wapo digital management pale ofisini kwetu lakini ile niwe active sometimes huwa nafanya mwenyewe,” ameongeza.

Diamond katika mtandao wa instgrama ana followers 3.9 milioni, twitter 429k facebook like 2. milioni.



Maafisa Polisi 92 Wamelazwa Hospitali Wakihofiwa Kuwa na Kipindupindu

$
0
0
Maafisa Polisi 92 Wamelazwa Hospitali Wakihofiwa Kuwa na Kipindupindu
Maafisa 92 wa polisi nchini Kenya wamelazwa hospitalini Nairobi na viunga vyake wakihofiwa kuugua ugonjwa wa kipindupindu, wizara ya afya nchini humo imesema.

Maafisa hao wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Kenyatta, hospitali ya Sinai na katika hospitali ya wanawake ya Nairobi Women’s.

“Polisi hao inashukiwa waliambukizwa kipindupindu katika mgahawa wa polisi katika eneo la Nairobi Area,” taarifa ya wizara hiyo imesema.

Mgahawa huo umefungwa kwa muda usiojulikana huku uchunguzi ukiendelea.

Waziri Cleophas Mailu amesema maafisa hao wanaendelea kupata nafuu hospitalini.

Gazeti la kibinafsi la the Star linaweza baadhi ya maafisa walikuwa kazini wakati wa kutangazwa kwa uamuzi wa mahakama kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.

Gavana wa Nairobi Mike Sonke alikuwa Jumapili ametoa taarifa na kusema hali imethibitiwa.
Alisema hatua zimechukuliwa “kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.”


Odinga Aliamsha Dude Aibuka na Kupinga Tarehe ya Marudio ya Uchaguzi Kenya

$
0
0
Odinga Aliamsha Dude Aibuka na Kupinga Tarehe ya Marudio ya  Uchaguzi Kenya
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kuwa hayuko tayari kushiriki marudio ya uchaguzi mkuu wa urais nchini humo.
Bwana Odinga amesema kuwa anataka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika, kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo.

Bwana Odinga pia anataka mabadiliko kufanyiwa Tume ya uchaguzi nchini humo, ambayo imelaumiwa na mahakama ya juu kwa wa kuendesha uchaguzi kwa njia ambayo haiukuwa nzuri ambayo ilisababisha kufutiliwa mbali matokeo.

Jana Jumatatu Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya ilitangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alisema uchaguzi huo utashirikisha wagombea wawili pekee wa urais, Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

"Hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wa urais katika uchaguzi huo upya. Waliopinga matokeo ya uchaguzi kortini, Bw Raila Odinga na mgombea mwenza wake Stephen Kalonzo Musyoka na mshtakiwa wa tatu Rais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Samoei Ruto, watakuwa ndio wagombea pekee," taarifa ya bw Chebukati ilisema.

Katika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Mahakama ya Juu iliiwekea lawama Tume ya Uchaguzi.

Download App ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu Yako Kupata Habari zetu Kwa Urahisi..Bonyeza Hapa

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Z Anto Acharuka...Ataka Mashabiki Wasimgombanisha na Ali Kiba

$
0
0
Msanii Z Anto ambaye sasa ameanza kujipanga kurudi upya kwenye muziki amefunguka na kuwataka watu hususani kwenye mitandao ya kijamii kuacha kumtengenezea chuki kwa wasanii kama Alikiba na hasimu wake na kusema hapendi kuwagawa mashabiki zake.

Z Anto amefunguka ya moyoni baada ya chombo kimoja cha habari kutoa taarifa kuwa amesema anataka kuwakalisha Alikiba pamoja na hasimu wake kwenye muziki jambo ambalo amelipinga na kusema si kweli.

Mkali huyo ambaye awali amewahi kufanya vyema na ngoma kama binti kiziwi, mpenzi jini, kisiwa cha malavidavi ametangaza rasmi kurudi kwenye muziki wa bongo fleva siku ya Ijumaa kwa kuachia ngoma yake mpya pamoja na video.

Mlisema Spika Dhaifu Sasa Mtaona – Ndugai

$
0
0
Mara baada ya kikao cha kwanza kwenye mkutano wa 8, wa Bunge la 11, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amesema wale waliokuwa wanamtuhumu kuwa mdhaifu katika kufanya maamuzi, sasa wataona dhahiri udhaifu wake uko wapi.


Spika Ndugai ameeleza hayo wakati akiwakaribisha wabunge 7 wapya wa Chama cha Wananchi (CUF) waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

“Taratibu zote zilifuatwa kwa wabunge hawa kuingia hapa bungeni, wapo baadhi ya lile kundi wiki mbili kabla ya mambo haya kutokea walisema Spika dhaifu, nikasema sasa udhaifu wangu ndiyo utaonekana. Kama una akili yako maneno kama haya hayana umuhimu”, alisema Spika Ndugai.
Samabamba na hilo, Spika Ndugai aliwakaribisha wabunge walioapishwa huku akiwafunda wabunge wengine, kwamba kiapo walichokula wenzao leo kiwa kumbushe utii na uaminifu kwa kwa tiba ya nchi.

“Kiapo hiki cha uaminifu kina tukumbusha wengine ambao tuliapa utii wa Katiba na kiapo chetu kwa ujumla wake, kuhusiana na uaminifu na utii.  Ni vizuri kuisoma Katiba na kuipitia ili uweze kujua nafasi ya vyama vya siasa na uhusiano wa mbunge na chama cha siasa”, alisisitiza Spika Ndugai.
Wabunge hao walioapishwa leo wanatarajiwa kupangiwa kamati na kuanza kazi mara moja, kama ambavyo Spika amewataka kufanya hivyo.

Pendeza na Kessy Products: Badili Muonekano Wako na Kuweka Mwili Wako Sawa Bila Madhara yoyote

$
0
0
PENDEZA NA KESSY PRODUCT: BADILI MUONEKANO WAKO NA KUWEKA MWILI WAKO SAW KWA PRODUCT ZA ASILI ZISIZO NA MADHARA YEYOTE WALA KEMIKALI, MATOKEO NI KWAARAKA


1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _80,000/
2) KUREFUSH NYWELE  KUZIJAZA NA KUZUIAKUKATIKA 90,000/
3) TENGENEZA SHEPU YAKO KUWA NA UMBO ZURI (HIPS & BATKS)KUNADAWA AINA TATU (@)KUPAK (B) KUNYWA (C)VIDONGE_130,000/
  4)ONDOA NYAMA UZEMBE MIKONONI, KIUNONI KUPAK _90,000/
5)TOA  KITAMBI KABISA(@) KUPAK 10O,000/ (B)VIDONGE/SLIMING MAJAN 130,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KILO UNAZOITAJI WEWE
@) DAW YA MAJIN NA VIDONGE_130,000/
7)PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME KAMA MWANZO _80,000/
8) PIA UNA KUONGEZA MAZIWA SAIZI UNAYOHITAJI WEWE_80,000/
9)ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA_100,000/
10) ONDOA MICHIRIZI ILIYO SHINDIKANA_90,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KWENY MAPAJA KIKWAPAN_90,000/
13) KUWA MWEUPE WAKUPENDEZA(@) VIDOGO(WHITE SOLUTION)_130,000/(B)MAFUTA YAKUPAK 100,000/
14)TOA NDEVU VINYWELEO MILINI _90,000/
15/ ONGEZA NGUVU ZA KIUME (@)JELI_80,000/(B)VIDONGE MAX MAN_ 100,000/
16) ENGEZA MAUMBIL YA KIUME
@) (HANDSOME UP) MASHINE _200,000/
@) JELI NA VIDONG VYA SHARK_120,000/
17) RUDISHA HAMU YA TENDO NA KUCHELEWA KUFIKA KILELE_90,000/
18) RUDISH(BIKRA) 100,000/
19)ONDOA MAFUTA USONI _90,000/
20) ONDOA MIKUNJO USON_70,000/
(21) ENGEZA  MGUU_80,000/    

 TUNAPATIKAN DAR W SALAAM: NAKWA MIKOAN KOTE UTAPATA PIGA CM                      (+255) 0719955528
0756259180
0785371237
@dr_kessy_product
Delivery  POPOTE ULIPO

Kesi ya Mpemba wa Magufuli Yaiva Kupelekwa Mahakama ya Mafisadi

$
0
0
Kesi ya Mpemba wa Magufuli Kupelekwa Mahakama ya Mafisadi
Hati ya mashtaka ya kesi ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo inayowakabili mfanyabiashara Yusuf Alli maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ inatarajiwa kupelekwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ‘Mahakama ya Mafisadi’.

Wakili wa Serikali, Elia Athanas amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba kuwa jalada la kesi hiyo limekamilika, hivyo wanaomba muda ili wapeleke hati ya mashtaka katika Mahakama ya Mafisadi.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi September 19, 2017.

Mbali ya Yusuf Alli, washtakiwa wengine ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa ambao wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Tsh. Milioni 785.6.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya January, 2014 na October 2015, wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Tsh Milioni 392.8 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Mashabiki Waitupia Lawama TFF Mechi ya Simba na Azam FC Kupelekwa Azam Complex

$
0
0
Mashabiki Kuitupia Lawama TFF Mechi ya Simba na Azam FC Kupelekwa Azam Complex
Mashabiki wa soka wamelalamika kitendo cha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Azam FC kupelekwa Azam Complex, Chamazi.

TFF imeamua kutangaza michezo ya Simba na Yanga dhidi ya Azam FC, sasa nayo itakuwa inachezwa Azam Complex tofauti na awali kutokana na ukubwa wake ilitakiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa au ule wa Uhuru.

Safari hii, Azam FC itaikaribisha Simba Chamazi katika mechi itakayopigwa Jumamosi ikiwa ni ya pili ya Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kila timu.

Mashabiki hao walioandika maoni katika mitandao ya Kijamii ya Salehjembe pamoja na blog yenye ya Salehjembe wamelia kutotendewa haki.

Kwa ujumla mashabiki hao wamelalamika kuhusiana na udogo wa uwanja wa Azam Complex wenye uwezo wa kuchukua watu 7,000.

“Nafikiri hii si sawa, wote tunajua uwanja huo ni mdogo na hii ni mechi kubwa. Wanatunyima haki ya kuona mechi hiyo.

“Angalau kungekuwa hakuna viwanja, lakini kuna Uhuru upo pale.”

Wengine walilalamikia umbali wa Chamazi na muda ambao mechi imepangwa Saa 1 usiku.

Lakini Azam FC imekuwa na kilio cha kutaka kucheza mechi zake nyumbani jambo ambalo hatimaye limetimia.


Msajiri wa Hazina: Taasisi na Mashirika 71 Hali Tete

$
0
0

Msajiri wa Hazina: Taasisi na Mashirika 71 Hali Tete
Msajili wa Hazina, Dk Oswald Mashindano amesema taasisi na mashirika 71 yaliyosaini mkataba wa utendaji kazi mwaka 2014/15 hayakufikia malengo.

Akizungumza leo Septemba 5 wakati wa utiaji saini mkataba wa taasisi na mashirika ya umma 30, Mashindano amesema baadhi zilishindwa kufikia malengo kutokana na mipango yao kutoendana na bajeti.

Amesema baadhi ya mashirika ya umma yameshindwa kukusanya mapato kulingana na mikataba waliyoingia.

Mashindano amesema baadhi ya mashirika ya umma yameshindwa kufikia malengo katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kuhusu mashirika yanayosaini mikataba leo, ametoa wito kwao kusimamia changamoto ambazo zimewafanya wenzao kushindwa kufikia malengo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda ametoa wito kwa viongozi wenzake wa mashirika ya umma na taasisi binafsi kuhakikisha wanamsaidia Rais John Magufuli kusimamia taasisi wanazoongoza ili ziweze kutoa mchango unaostahili kwa Taifa.



Putin: Vikwazo Dhidi ya Korea Kaskazini ni Bure

$
0
0
Putin: Vikwazo Dhidi ya Korea Kaskazini ni Bure
Rais wa urusi Vladimir Putin amesema kuwa vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini ni bure, akiongeza ni radhi wale nyasi kuliko kuachana na mpango wao wa nyuklia.
Marekani ilisema Jumatatu kuwa itapeleka azimio mpya kwa Umoja wa Mataifa la vikwazo zaidi, kufuatia hatua ya nchi hiyo kulifanyia majaribio bomu la nyuklia siku ya Jumapili.
Bwana Putin pia alisema kuwa hatua za kijeshi inaweza kuleta janga la dunia nzima.

Amesema kuwa mazungumzo ndiyo njia pekee.
China, mshirika mkuu wa Korea Kaskazini pia nayo imetaka kurejelewa kwa mazungumzo.

Putin alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa nchi za Brics ambazo ni (Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini) huko Xiamen nchini China.
Licha ya Putin kuishutumu Korea Kaskazini, alisema kuwa vikwazo havitasaidia.

Siku ya Jumatatu mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley, alisema kuwa vikwazo vikali vitasababisha tatizo hilo kutatuliwa kwa njia ya kidiplomasia.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel aliunga mkono pendekezo hilo akisema kuwa vikwazo vya haraka vinahitajika kukabiliana na tabia ya Korea Kaskazini kukiuka maazimio ya kimataifa.
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images