Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Silinde Afunguka Sababu Iliyopelekea Wabunge wa Upinzani Kususia Kuapishwa Wabunge 7 wa CUF

$
0
0
Silinde Afunguka Sababu Iliyopelekea Wabunge wa Upinzani Kususia Kuapishwa Wabunge 7 wa CUF
Mbunge wa jimbo la Momba (CHADEMA) Mheshimiwa David Silinde amefunguka na kutoa sababu kuu iliyopelekea wabunge wa upinzani leo kususia zoezi la uapishwaji wa wabunge saba wa CUF na kusema wao wamefanya maamuzi hayo kupinga bunge kutumika na serikali

Silinde amedai kuwa Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekuwa likikandamizi upinzani lakini pia limekuwa halifuati sheria za nchi kitu ambacho wao wanaona siyo sawa ndiyo maana wameamua kususia zoezi la uapishwaji wa baadhI ya wabunge hao wa CUF.

"Kama ambavyo leo mmetuona hatujaingia wakati wa kuapishwa kwa baadhi ya wabunge na sababu kubwa ya kutoingia ni kwamba tunapinga bunge kutumika na serikali kukandamiza upinzani pili kutofuata sheria za nchi na jambo la tatu na kubwa kuliko yote ni kwamba tunawaunga mkono wabunge wote waliondolewa na hatufurahii, kuna vitu vikubwa sisi tunekuwa tukikasirika navyo kama serikali ku- entetain maamuzi katika chama ambacho kipo kwenye mgogoro kwamba unapendelea upande mmoja unaacha upande mwingine" alisema Silende

Aidha Silinde aliendelea kudai kuwa " Hiyo ndiyo tumekuwa tukipigania siku zote hatutaki bunge kuendelea kutumika tunataka kuwa na bunge imara waone mifano kama ilivyotokea kule Kenya kama mahakama inaweza kusimama peke yake tunataka na bunge letu liendelee kusimama peke yake" alisisitiza Silinde

Wabunge hao wa upinzani walirejea ndani ya ukumbi wa bunge baada ya zoezi la kuapishwa wabunge hao wa CUF kukamilika


Man city Yashitakiwa na La Liga Matumizi Makubwa ya Fedha

$
0
0
Man city Yashitakiwa na La Liga Matumizi Makubwa ya Fedha
Shirikisho la soka nchini Hispania (La Liga) limeliandikia barua shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) wakitoa malalamiko kuhusu ukiukwaji wa sheria za matumizi Financia Fair Play (FFP) unaofanywa na klabu ya Man City.

Raisi wa La Liga Javier Tebas alitoa malalamimo kuhusu wamiliki wa klabu ya Manchester City ambao pia ni wamiliki wa klabu ya PSG kutokana na matumizi makubwa ya kifedha wanayoyafanya.

Lakini baadaye shirikisho la soka la UEFA lilitoa majibu kuhusiana na barua iliyoandikwa na Rais wa La Liga kwa kusema kwamba shirikisho hilo halitaichunguza klabu hiyo na taarifa nyingine kinyume na hapo ni uongo.

Kiki Zinamchango Mkubwa Katika Muziki- Roma

$
0
0
Kiki Zinamchango Mkubwa Katika Muziki- Roma
Msanii wa muziki Bongo, Roma amedai kuwa kiki zinaweza kuwa na mchango fulani katika muziki wa msanii.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ‘Zimbabwe’ ameiambia Radio Maisha kuwa ingawa zina mchango ila zifanyike kwa kiasi.

“Sana sana inasaidia, sema inatengemea unaifanyaje ikifeli inakuwa mbaya zaidi, ukianza nayo inabiki uwe na ule mwendelezo, yaani baada ya hapo ifuate nyingine na nyingine usirudi tena ukawa wa kawaida,” amesema Roma.

“Unafanya ndio entertainment industry yetu ipo hivyo inataka vitu hivyo sema kuna vingine vinaboa, halafu kuna nyingine unajua hizi hapa ni za uongo kabisa,” ameongeza.

Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe Anashikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam

$
0
0
HABARI MPYA: Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe anashikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa siku nne sasa. Kamanda Lazaro Mambosasa amethibitisha.

Mwananchileo

Kauli ya Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige baada ya ACACIA kutangaza kupunguza Shughuli zake katika mgodi wa Bulyanhulu

$
0
0
Kauli ya Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige baada ya ACACIA kutangaza kupunguza Shughuli zake katika mgodi wa Bulyanhulu
Nimepata taarifa ya Acacia kupunguza shughuli zake BULYANHULU na hivyo kuleta tiahio la madhara ya kiuchumi kwa wafanyakazi zaidi ya 1,200; wakandarasi zaidi ya 800 na wananchi kaka maelfiu Kakola na maeneo jirani. Hali hii haipaswi kuachwa hivi hivi.

My immediate reaction kwa hali hii ni KUIOMBA SERIKALI IRUHUSU WANANCHI AMBAO NI WACHIMBAJI WADOGO KWA MAISHA YAO YOTE, WAANZE KUCHIMBA REEF 2 na maeneo mengine yenye madini ndani ya leseni ya Acacia pembeni ya mgodi ili maisha yaendelee.

Ni vema pia seriklai ikasimamia kuhakikisha haki za wananchi, hasa wafanyakazi na wakandarasi wenye mikataba zinalindwa wakati huu. Serikali isiwaache wafanyakazi wakafanyiwa anachopenda mwekezaji. Ni muhimu SERIKALI ifanye hivyo ili wajue there are consequences for any action they take.

Nawasihi wananchi wangu (hasa wafanyakazi, wakandarasi na wengine ambao wamepata madhara ya moja kwa moja) tuendelee kuwa watulivu tukiamini Mazungumzo yanayoendelea kati ya SERIKALI na Barrick yatapelekea haki zetu zilizoporwa siku zote kurejeshwa na neema endelevu kupatikana.

Mawasiliano rasmi kati ya ofisi yenu (ya Mbunge) na SERIKALI kuhusu maombi mnayopenda SERIKALI iyafanyie kazi kwa jinsi mambo yanavyokwenda yanafanyika.

Agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani la Kibaguzi na Kinyume na Sheria- Kishoa

$
0
0
Agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani la Kibaguzi na Kinyume na Sheria- Kishoa
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Jesca Kishoa amesema agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba la kuwataka wabunge wanawake wafanye mikutano katika vyama vyao badala ya mikoa wanayotoka ni la kibaguzi na kinyume cha Katiba.

Kishoa amesema hayo baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni alipoomba mwongozo wa Spika kuhusu kauli aliyodai ilitolewa juzi Septemba 3 na Mwigulu.

"Kauli hii inatofautiana na aliyoitoa Machi kwamba, wabunge wa viti maalumu wanaruhusiwa kufanya mikutano katika mkoa na wabunge wa majimbo kwenye majimbo yao tu," amesema.

Hata hivyo, Spika Job Ndugai amemjibu mbunge huyo kwamba, alichomaanisha Mwigulu ni kuwa wabunge wa majimbo  wanaruhusiwa kuzungumza na wapiga kura.

“Sasa wapiga kura wenu wapo kwenye mikutano ya hadhara?" amehoji Ndugai.


Dayna Nyange Afunguka Siri ya Kuingia Kwenye Sanaa ya Muziki

$
0
0
Dayna Nyange Afunguka Siri ya Kuingia Kwenye Sanaa ya Muziki
Msanii wa Bongo Flava Dayna Nyange amedai kuwa kipindi cha nyuma muziki wa AY na Fid Q ulimpelekea kupenda muziki na atimaye kutumbikia katika tasnia hiyo.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Chovya’ kipindi cha awali alikuwa akifanya na muziki wa rap kabla ya kuanza kuimba.

“Sasa hivi nikitaka kufanya hicho kitu itanichukua muda sana, lakini mimi nilikuwa napenda kwa uandishi na kuna watu wanaflow, hapo nilikuwa nampenda AY alivyokuwa anaflow lakini kwenye maneno Fid Q ni mtu ambaye alikuwa na maneno,” amesema Dayna.

“Unajua muziki una utofauti unaweza ukawa na maneno makali lakini kwenye flow ukawa na utofauti, mwingine anaflow kiasi kwamba unaleta ladha fulani. Kwa hiyo nikawa napenda maneno ya Fid Q alikuwa na maneno fulani makali na magumu,” ameongeza.



Winga wa Azamu Joseph Kimwaga Nje ya Dimba kwa Miezi Minne

$
0
0
Winga wa Azamu Joseph Kimwaga  Nje ya Dimba kwa Miezi Minne
WINGA wa Azam FC, Joseph Kimwaga, anatarajia kukaa nje ya dimba kwa muda miezi minne baada ya kubainika ya kuwa amechanika mtulinga wa kati ‘meniscus’ kwenye goti lake la mguu wa kushoto.

Kimwaga hivi sasa yupo nchini Afrika Kusini tokea Ijumaa iliyopita akifanyiwa matibabu ya goti lake hilo, aliloumia wakati Azam FC ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Ndanda ulioisha kwa matajiri hao kushinda bao 1-0 wiki mbili zilizopita.

Kwa mujibu wa Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, aliyeambatana na Kimwaga nchini humo, ameuambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuwa mchezaji huyo alifanyiwa vipimo jana Jumatatu na Dr. Nickolas kwenye Hospitali ya Vincent Palloti iliyopo jijini Cape Town nchini humo.

“Jumatatu (4/9/2017)alifanyiwa vipimo na kuthibitika amechanika Meniscus upande wa kati (meniscus mfano wake tunautoa kwa mafundi anapofunga nati anaweka washa kwanza halafu ndio anakaza nati juu yake Mwenyezi Mungu amemuaamba kila binadamu na hiyo washa inayoitwa meniscus, ipo katikati ya goti kuimarisha goti, ipo upande wa kati na pembeni. Hebu gusa sikio lako pembeni, meniscus inafananishwa au kulinganishwa na kuta za sikio lako).
“Vile ameumia mtulinga wa kati ACL(Anterior Cruciate Ligament),” alisema kwenye ripoti aliyoipokea kutoka kwa Dr. Nickolas.

Mwankemwa alisema baada ya kufanyiwa kipimo hicho, Kimwaga anatarajiwa kulazwa kesho Jumatano saa 9.00 Alasiri, huku akitarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo (athroscopy) siku inayofuata Alhamisi kabla ya kutoka hospitalini Septemba 9 mwaka huu na kurejea nchini siku nne baadaye (Septemba 13) saa 12.00 jioni kwenye Uwanja wa Mwl Julius Nyerere (JNIA).

Upasuaji wa kwa njia ya Athroscopy ni ule wa kisasa kabisa ambao wataalamu hutumia vifaa maalum, ambavyo huingizwa kwenye goti ambavyo hufanya matibabu na kuondoa matatizo yote katika eneo hilo, faida yake humfanya mchezaji kurejea mapema uwanjani kuliko ule wa kupasuliwa goti zima.

Winga huyo mara baada ya kufanyiwa upasuaji Alhamisi anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi minne kutoka siku ya upasuaji.
Azam FC tunamtakia kila kheri Kimwaga katika matibabu yake hayo, yaweze kwenda salama kama yalivyopanga na hatimaye aweze kurejea dimbani mapema.


Mwili wa Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Handeni Muhingo Rweyemamu Waagwa

$
0
0
Mwili wa Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Handeni Muhingo Rweyemamu Waagwa
Waandishi wa habari wametakiwa kuyaishi aliyoyafanya mwandishi mkongwe na mkuu wa wilaya mstaafu, Muhingo Rweyemamu ikiwa ni ishara ya kumuenzi.

Akizungumza wakati wa kuaga mwili wa mwanahabari huyo mjini hapa, kwa niaba ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Jesse Kwayu amesema hakuna cha zaidi cha kufanya kama wanahabari zaidi ya kutafakari aliyofanya Muhingo.

"Sisi TEF tuna msiba mkubwa si tu kwa kuondokewa na Muhingo kama mwanahabari, bali kama miongoni mwa wahariri watano waanzilishi wa jukwaa hili," amesema Kwayu.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ambaye ni mwanahabari kitaaluma, amesema pamoja na mengi mazuri aliyofanya Muhingo atamkumbuka kwa kumfungulia njia ya utendaji katika wilaya hiyo. Muhingo aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Amesema atayaishi yale aliyoyaamini Muhingo ikiwemo utendaji wa kazi uliotukuka.

"Muhingo alikuwa mwalimu, kaka na kiongozi. Wananchi wa Handeni wameupokea kwa masikitiko msiba huu," amesema Gondwe.

Jane Mihanji, makamu mwenyekiti wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania amesema Muhingo amemaliza kazi aliyotumwa duniani, hivyo jukumu kwa waliobaki ni kuyaishi aliyoyatenda.

Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari, Absalom Kibanda amesema kuondokewa na Muhingo ni pigo kwa tasnia ya habari.

Amesema mbali ya kumfahamu katika habari, pia ni zaidi ya ndugu yake na kwamba, mazishi hayo ni furaha kwa sababu Muhingo alijiandaa kulala milele.

"Mara nyingi nikiwa nyumbani kwake, pembeni mwa kitanda chake pale Hospitali ya Aga Khan alikuwa akimsubiri mkewe aondoke na kuniambia nimechoka nataka kupumzika," amesema Kibanda.                      

Waziri wa Habari, Dk Harrison Mwakyembe amesema msiba huo ni pigo kwa wanahabari wote.

Amesema alimfahamu Muhingo tangu kijijini kwao Kyela ambako alikuwa akienda kumsalimia kaka yake aliyekuwa daktari wa zahanati ya kwanza.

"Nimemfahamu siku nyingi, naelewa utendaji wake ni pigo kwa tasnia na Taifa kwa jumla," amesema.


Huu Hapa Ushauri wa Ali Kiba Kwa Bongo Movie

$
0
0
Huu Hapa Ushauri wa Ali Kiba Kwa Bongo Movie
Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Seduce me' ameamisha mashambulizi yake upande wa bongo movie na kuwaambia hali mbaya waliyokuwa nayo katika kipindi hiki ni kutokana na kutokuwa na umoja baina yao.

Alikiba ameeleza hayo baada ya kuwepo tetesi ya baadhi ya wasanii wa bongo movie kuwa wanashindwa kusaidiana katika kazi zao na kuogopana jambo ambalo linaleta makundi kati yao na kuwafanya kushindwa kuwa kitu kimoja.

"Mimi siku zote nitawapigania bongo movie kwa sababu wakishafanya kazi zao na kuzipeleka sokoni kwa ajili ya kufanya mauzo ndiyo basi tena lakini sisi wanamuziki tunauwezo wa kufanya 'show' ambazo zitatulinda sisi hata kama wananchi wamesikiliza ngoma zetu na kuzi-download bila malipo hatuwezi kupata hasara kwa kuwa tunategemea show ambazo ndiyo zinalipa, kwa hiyo umoja ni kitu cha msingi sana na ndiyo maana wenzetu wa Nigeria wanasaidiana katika mambo yao na siyo kwamba wanaogopana", amesema Alikiba.

Pamoja na hayo, Alikiba aliendelea kwa kusema "Mimi binafsi ningefurahi sana kama wasanii tungekuwa na umoja, sisi ni wamoja siyo lazima mpaka tukutanishwe kwenye janga fulani!", amesisitiza Alikiba.

Kwa upande mwingine, Alikiba aliendelea kuwashauri wasanii wenzake kuendelea kusaidiana kwa kuwa ni jambo zuri ambalo anaamini litaweza kuwatoa sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kwa wasanii wote kwa ujumla bila ya kujali aina ya kazi anazozifanya.


SIKILIZA na Download Wimbo Huu Mzuri wa Kuabudu Unaitwa Haja ya Moyo Wangu Ulioimbwa na Regina Roberts na Maho Charles

$
0
0
SIKILIZA na Download Wimbo Huu Mzuri wa Kuabudu Unaitwa Haja ya Moyo Wangu Ulioimbwa na Regina Roberts na Maho Charles


 

Wanawake Wenye Misambwanda hawanivutii kabisa..Piteni Mbali Nami

$
0
0
Sijui kwanini me sipendi warembo wanene,yani akipita kimbaumbau utaona mijicho inavyonitoka.

Sijui ile wanaita misambwanda na mimi vitu viwili tofauti,siwezi kupoteza mda wangu kugeuka nyuma kuusindika Kwa macho msambwanda.

Sasà kakipita kadogo Dogo hivi basi kamoyo kanaanza kwenda mbio mbio bhana

Ila kama unajijua upo kama hawa hata usinishobokee maana wee sio wa type yangu...Napenda Vimodel tuuuu

By Deadbody/JF

Uchawi Unaotumika Kummaliza Kisanii Diamond Platnumz Wagundulika.....

$
0
0
Msanii wa kimataifa ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya WCB Diamond Platnumz hatimaye uchawi unaotumika kumshusha na kummaliza kabisa kisanii wagundulika.

Katika utafiti nilioufanya kwa miezi kadhaa hatimaye nimegundua kuwa kitendo cha diamond kulinganisha kazi zake za kimuziki na wasanii aliowazidi kimafanikio na kiuimbaji hasa huyu Ali kiba kinamrudisha nyuma sana diamond wakati huo huo mpinzani wake anafaidika sana kupitia mchuano huo ndio maana hataki bifu lao liishe.


Miaka kama miwili mitatu iliyopita diamond alipiga hatua kubwa sana za kimuziki mpaka akawashtua wasanii wakubwa duniani kama vile Chris Brown, Nelly, Neyo,Jiddena,Trey Songz,na wengineo wengi sana.

Na kikubwa kilichomfanya diamond kupiga hatua hiyo ni kitendo cha yeye kutoshughulika na wasanii wa kitanzania badala yake alipenda kulinganisha uwezo wake na wasanii kutoka nchi zingine hasa Nigeria.

Na mpinzani wake mkubwa kutoka Nigeria alikuwa David Adeleke Adedeji (DAVIDO) na kiasi kikubwa ilimsaidia diamond kujulikana sana Nigeria mpaka mashabiki wa muziki wengi walimtambua diamond kama msanii kutoka Nigeria.

Kipindi hichohicho pia Kenya walikuwa walishaanza kumtangaza Diamond kuwa ni msanii kutoka nchini kwao na kudai kuwa uthibitisho wanao.

Lakini kitendo cha Diamond kurudi nyuma na kulinganisha kazi zake na Ali Kiba kama hapo awali kimemrudisha nyuma sana Diamond na thamani yake halisi imeanza kufifia.


Rai ; Nikiwa kama shabiki nguli wa diamond napenda sana kumhusia aachane na Ali kiba , Kiba anatembelea nyota ya diamond kwa sasa na anaitumia kama daraja ili kuweza kuzivusha kazi zake za kimuziki mbali zaidi huku yeye diamond akizidi kufifia kimuziki.

Msaani Ali Kiba Anatumbuiza Leo Usiku Katika Sherehe Maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (NASA) Kenya

$
0
0
EXCLUSIVE: Msaani Ali Kiba anatumbuiza leo usiku katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (NASA) kwa ajili ya kuwashukuru wapiga kura wao.

Habari hii imethibitishwa na meneja wake Seven Mosha kwa njia ya simu. "Ali yupo kweli Kenya na alialikwa kupitia Ali Hassan Joho - Gavana wa Mombasa ambaye ni rafiki yake wa karibu".

Ali Kiba ambaye ndani ya wiki mbili amevunja rekodi na wimbo wake wa "Seduce Me" ni miongoni mwa wasanii wa muziki wanaoongoza Afrika Mashariki kwa umaarufu.

Maskini...Watoto Wawili Waliotekwa Arusha Wapatikana Wamekufa Kwenye Shimo la Chooo

$
0
0
Arusha. Miili ya watoto wawili ambayo haijatambuliwa imeopolewa shimoni eneo la Mji Mpya katika Mtaa wa Olkerian jijini Arusha.

Mwenyekiti wa mtaa huo, uliopo Kata ya Olasiti, Daudi Safari amethibitisha tukio hilo lililovuta wananchi wengi waliojitokeza kushuhudia kuopolewa kwa miili hiyo.

Kazi ya uopoaji ikitekelezwa na  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Shimo hilo lipo kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika.

Mwananchi:

Kenya Wapiga Kura Kati ya Seduce na Zilipendwa Ipi Kali....Hili Ndio Jibu Lao

$
0
0
Uchaguzi mdogo uko Kenya ulifanyika kati ya nyimbo mbili zinazobamba hapa bongo za vigogo wa muziki.
Asilimia tatu(3) kama uonavyo matokeo jinsi ulivyokawa,wanasema hawafungamani na pande zozote.

Zilipendwa Imepata Asilimia 77 hivyo ndio nyimbo inayopendwa zaidi kenya kuliko Seduce

Toa maoni yako ni kweli inaweza ikawa hivyo.

Hivi Yuko Wapi Mwanadada Ruby?

$
0
0
Mambo zenu wadau,

Ningependa kujua yule mwanadada machachari kabisa aliyetamba na kibao chake cha "Na yule" amepotelea wapi maana naona hasikiki kabisa siku hizi toka alivyotangaza kutoka mikononi mwa Clouds Media, ni kwamba amebuma kabisa kutokana na ukosefu wa promo au bado anajipanga kuja kumshinda Nandy?


Dogo Janja Amkana Irine Uwoya

$
0
0
Msanii Dogo Janja ambaye hivi karibuni amekumbwa na tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji wa filamu bongo aliyemzidi umri Irene uwoya, na kuweka wazi sababu za kuweza kufanya hivyo.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema kuwa na mahusiano na wanawake waliomzidi umri kwanza ni sunna kwa imani ya dini yake ya Kiislam, lakini pia wanawake wakubwa wanatulia kwenye mahusiano, tofauti na wasichana wadogo ambao wanakuwa wasumbufu.

"Cha kwanza ni sunna, cha pili watoto pasua kichwa, ukiwa na mtu ambaye amekuzidi umri anaweza kukuongoza, siyo unakuwa na mwanamke anajua kuendesha gari halafu hajui kupika wali, unakuwa na mtu ameshakuwa na uzoefu wa maisha, kwa hiyo anataka kutulia", alisema Dogo Janja
Pamoja na kauli hiyo Dogo Janja amekanusha tetesi za kuwa na mahuisano na Uwoya, huku akiwataka mashabiki wake kufuatilia zaidi kazi zake ambapo sasa ana kazi mpya ya Ngarenaro, na sio kufuatilia skendo zake.

Ndoa ya Shilole Yaota Mbawa....Uchebe yamkuta ya Nuh Mziwanda kwa Shilole

$
0
0
WASWAHILI wanasema mwenzako akinyolewa, wewe tia maji nywele zako, sina hakika kama Uchebe, ambaye ni mpenzi mpya wa Diva kutoka kiwanda cha Bongo fleva na muvi, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ alijipanga kukutana na mbilingembilinge zilizowahi kuwakuta wapenzi wa mwanadada huyo, akiwemo mwanamuziki Nuh Mziwanda.

Mara zote Uchebe alikuwa akiposti picha na kuandika ujumbe mzito wa kumsifia mpenzi wake huyo na kuwataka vizabizabina wakae kando, kwani wapo kwenye dimbwi zito la mahaba. Mashabiki wanadai kwamba kwa sasa hali si shwari baina ya wapenzi hao, na hii ni kutokana na posti yake ya hivi karibuni, kuwa haina uwiano na zile za mwanzo.

Kupitia ngoma yake ya ‘Jike Shupa’, Nuh Mziwanda alielezea tabia za Shishi, kwamba ni mwanamke mbabe, anayependa kusikilizwa, sifa ambazo zina fanana kidogo na posti ya Uchebe.

Imetimia ACACIA Waanza Taratibu za Kuukabidhi Mgodi wa Buzwagi....

$
0
0
Kufuatia kuvunjwa kwa makubaliano ya kimkataba kati ya serikali ya Tanzania na ACACIA, hatimaye kampuni hiyo ya uchimbaji madini imeanza rasmi taratibu za kuukabidhi mgodi wa dhahabu wa Buzwagi baada ya kuwa na nia ya kutokuendelea na uwekezaji katiaka mgodi huo.

Taarifa zaidi zinasema hatua hiyo imekuja baada ya ACACIA kuamua kwenda mahakama ya kimataifa kudai fidia baada ya serikali kukiuka mkataba kati yao.

MWANANCHI NEWS PAPER

Mawakili wa serikali kaeni mkao wa safari za nje na makabrasha!
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images