Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Amber Lulu Ashtushwa na Picha za Utupu za Video Qeen Amber Rutty

0
0
Amber Lulu Ashtushwa na Picha za Utupu za Video Qeen Amber Rutty
Msanii wa Bongo Flava na video vixen, Amber Lulu amedai anachokifanya sasa video vixen mwenzie Amber Rutty katika mitandao ya kijamii kwa kuachia picha za utupu hata yeye kinamshtua.

Amber Lulu ambaye sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Only You’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa licha kile anachokifanya mwenzie kumshtusha, hawajawahi kuwa na beef kama watu wanavyodhani.

 “Namjua nilishakutana naye mara moja tukasalimiana fresh, mtu mpaka kafanya hayo yote ina maana ananikubali haina haja ya kumkasirikia mtu, huwezi kuwa wewe kila siku,” amesema.

“Siyo nimemu-inspire kupiga picha za utupu, sema yeye anafanya hadi anazidi mpaka mwenyewe nilikuwa nashtuka, siku moja nikamtumia ujumbe Instagram fanya lakini jitahidi kidogo kujistiri, mimi mwenyewe sijawahi kufanya hivyo,” ameongeza.

Wiki iliyopita katika mtandao ilivuja picha ya utupu ya Amber Lulu na Young Dee kitendo kilichopelekea kukamatwa na Young Dee na kupelekwa polisi kwa madai yeye ndiye alivujisha picha hiyo, hata hivyo amekuwa akikanusha madai hayo.



Roma, Stamina na Khaligraph Jones Kuachia Wimbo wa Pamoja

0
0
Roma, Stamina na Khaligraph Jones Kuachia Wimbo wa Pamoja
Wakali wa muziki wa hip hop Bongo, Roma na Stamina ‘Rostam’ wameingia studio kufanya kazi na rapper Khalighraph Jones kutoka nchini Kenya.

Rostam ambao walienda nchini humo kwa ajili ya ziara yao ya kimuziki wameweka picha pamoja na video katika mitandao wakielezea kuna ngoma inakuja kati yao na Khalighraph Jones.

Hiyo juzi katika mahojiano na kituo cha Radio Maisha Stamina alieleza rapper wa Kenya ambao anawakubali na kufuatilia kazi zao na miongoni mwao alikuwa ni Khalighraph Jones na kwa pamoja waliaidi kutoondoka nchini humo bila kufanya kolabo na msanii yeyote.

“Nawakubali wote, napenda sana kazi zao, napenda sana kazi za Octopizzo, napenda kazi za King Kaka, napenda kazi za Khalighraph lakini changuo ni kwa King Kaka,” alisema Stamina.

Kwa upande wake Roma alieleza mipango ya albamu ya Rostam kukamilika, “hadi sasa tuna nyimbo nane, tuna wimbo na Beka Flavour, Ben Pol na wasanii wengi, so before 2017 hajaisha tutatoa hii albamu,” alieleza.

Khalighraph Jones ameshafanya kazi na wasanii kadhaa kutoka Bongo akiwemo Rayvanny, Christian Bella na Rosa Ree.




Hawa Hapa Wezi Walioiba Gari na Wakarudisha Wakiwa Kama Walivyozaliwa

0
0
Hawa Hapa Wezi Walioiba Gari na Wakarudisha  Wakiwa Kama Walivyozaliwa
Ule msemo wa ‘mwizi siku zake ni arobaini’ asubuhi ya leo August 6, 2017 umedhihirika baada ya vijana wawili wanaoripotiwa kuwa wezi wa gari waliloliiba siku za nyuma kulirudisha gari hilo wakiwa uchi wa mnyama na wakionekana kuwa wamerukwa akili jambo lililokusanya umati wa watu kuwashangaa.

Tukio hili lilitokea kwenye mji wa Bamburu Mtambo huko Mombasa Kenya ambapo vijana hao walifika eneo hilo na gari hilo walilokuwa wameliiba Nissan KBV 717Y ya rangi ya silva na kutoka nje ya gari wakiwa uchi, wakiwa wanaongea lugha isiyoeleweka na baadae kuanza kuosha gari hilo kwa matope kabla ya wao kuanza kujipaka matope hayo.

Wakazi wa eneo hilo wameeleza kuwa wanaamini mmiliki wa gari hilo alikwenda kwa mganga wa kienyeji na kuwaroga watu hao kutokana na kuliiba gari lake.





BREAKING NEWS: JPM Awatumbua Ngereja, Muhongo na Simbachawene Sakata la Almasi na Tanzanite

0
0
JPM Awatumbua Ngereja, Muhongo na Simbachawene Sakata la Almasi na Tanzanite
Rais Magufuli amewataka viongozi mbalimbali wa serikali ambao wametajwa kwenye ripoti za bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite wamepishe nafasi zao ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri kuwachunguza.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akikabidhiwa ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kusema amesikia baadhi ya viongozi mbalimbali wengine ambao amewateuwa yeye kuwa wameusishwa kwenye wizi huo hivyo amewataka wapishe.
"Wako watu wametajwa tajwa, na wengine mimi ndio nilihusika kuwateua sasa ukishatajwa tajwa, naagiza vyombo vya ulinzi na usalama vifuatilie hili tena kwa haraka, Wale ambao wametajwa tajwa kwenye ripoti hii ambao ni wateule wangu, ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri, ni matumaini yangu watakaa pembeni" alisema Rais Magufuli

Katika ripoti hiyo ambayo iliwasilishwa jana mjini Dodoma na leo kukabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliweza kuwataja baadhi ya viongozi wa serikali ikiwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Taifa Hili Limepigwa Sana Kama Lingeweza Kusema Lingesema- Zungu

0
0
Taifa Hili Limepigwa Sana Kama Lingeweza Kusema Lingesema- Zungu
Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi ya biashara ya madini Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema kilichopelekea taifa kulizwa kila leo kuhusiana na biashara ya madini ni kutokana na kuwepo na mikataba mibovu ambayo imetolewa nje ya nchi na kuja kusainiwa.

Mhe. Zungu ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa fupi kwa Rais Magufuli katika yale yaliyofanywa na kamati ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na kamati maalum mbili zilizoundwa na spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.

"Taifa hili limepigwa sana, kama lingeweza kusema lingesema nimepigwa sana na kitu pekee kinachotupiga ni mikataba mibovu, mkataba huu tumegundua kwa kauli ya IG anaamini imetoka nje na kuja kusainiwa tu hapa kwetu. Kwa hiyo maneno ya muwekezaji ndiyo yametupiga lakini laiti wataalamu na wachimbaji wa serikali wangekataa sidhani kama mgodi huu ungeharibika maana mgodi siyo mapapai kwamba yasipochimbwa yataoza, wataalamu wapo lakini wameshindwa kutumia utaalamu wao katika kusaidia taifa hili", amesema Zungu.

Aidha, Mhe. Zungu amesema watu pekee waliyoweza kuingiza nchi katika hasara kubwa ni wale ambao waliodhaminiwa na wananchi pamoja na serikali katika kulinda rasilimali hizo za nchi.
"Watu walidhaminiwa ya kulinda mali na wamekula kiapo mbele yako lakini bado wamekuwa wakipoteza mali za nchi, kwa hiyo Mhe. Rais kazi uliyokuwa nayo sisi tupo nyuma yako kukuunga mkono kwenye hilo. Mhe. Rais bodi ambayo ndiyo yenye dhamana kubwa ya kusimamia rasilimali za nchi ili wasaidie nchi iweze kupata mapato yake lakini wao wamekuwa wakiuwangusha mgodi huu tokea uwanze kwa kutosimamia vyema mali za watanzania", amesema Zungu.

Pamoja na hayo, Mhe. Zungu ameendelea kwa kusema "kamati hizi mbili za Almasi na Tanzanite zilizoundwa na Mhe. Spika ni wabunge ambapo ndani yake kuna watalamu na wenye ujuzi mbalimbali lakini hawana utaalamu mkubwa kama baadhi ya watu ambao wapo kwenye bodi waliyosomea mambo ya madini. Mhe. Rais huwezi kuamini 'chairman of audit committee' anavyoulizwa juu ya gharama za kuendesha mgodi anazipitia vipi na kuzihakiki vipi anakujibu alikuwa hana muda wa kulifanyia hilo kwa kuwa anaamini kile alichokuwa analetewa na watendaji wa chini", amesisitiza

Kwa upande mwingine, Mhe. Zungu amewataka watu watumbue kwamba vita ya biashara ya madini siyo ya Rais peke yake bali ni ya watu wote kwa kuwa mali ni za watanzania na zinapaswa zibakie Tanzania.


Kutana na Mtabibu wa Nyota Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH...AL_WATWAN MAFUSHO

0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH...
 AL_WATWAN MAFUSHO

ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote

..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na AL_WATWAN MAFUSHO Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA).
Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?
Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
AL_WATWAN MAFUSHO Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.
Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA.
 Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.
Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,
HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp +255 759 084 996

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote..

Taifa Hili Limepigwa Sana Kupita Maelezo Kutokana na Mikataba na Usimamizi Mbovu

0
0
Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi ya biashara ya madini Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema kilichopelekea taifa kulizwa kila leo kuhusiana na biashara ya madini ni kutokana na kuwepo na mikataba mibovu ambayo imetolewa nje ya nchi na kuja kusainiwa.

Mwenyekiti wa kamati ya Spika iliyochunguza uchimbaji wa Almasina Tanzanite, Mhe. Azzan Mussa Zungu.

Mhe. Zungu ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa fupi kwa Rais Magufuli katika yale yaliyofanywa na kamati ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na kamati maalum mbili zilizoundwa na spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.

"Taifa hili limepigwa sana, kama lingeweza kusema lingesema nimepigwa sana na kitu pekee kinachotupiga ni mikataba mibovu, mkataba huu tumegundua kwa kauli ya IG anaamini imetoka nje na kuja kusainiwa tu hapa kwetu. Kwa hiyo maneno ya muwekezaji ndiyo yametupiga lakini laiti wataalamu na wachimbaji wa serikali wangekataa sidhani kama mgodi huu ungeharibika maana mgodi siyo mapapai kwamba yasipochimbwa yataoza, wataalamu wapo lakini wameshindwa kutumia utaalamu wao katika kusaidia taifa hili", amesema Zungu.

Aidha, Mhe. Zungu amesema watu pekee waliyoweza kuingiza nchi katika hasara kubwa ni wale ambao waliodhaminiwa na wananchi pamoja na serikali katika kulinda rasilimali hizo za nchi.
"Watu walidhaminiwa ya kulinda mali na wamekula kiapo mbele yako lakini bado wamekuwa wakipoteza mali za nchi, kwa hiyo Mhe. Rais kazi uliyokuwa nayo sisi tupo nyuma yako kukuunga mkono kwenye hilo. Mhe. Rais bodi ambayo ndiyo yenye dhamana kubwa ya kusimamia rasilimali za nchi ili wasaidie nchi iweze kupata mapato yake lakini wao wamekuwa wakiuwangusha mgodi huu tokea uwanze kwa kutosimamia vyema mali za watanzania", amesema Zungu.

Pamoja na hayo, Mhe. Zungu ameendelea kwa kusema "kamati hizi mbili za Almasi na Tanzanite zilizoundwa na Mhe. Spika ni wabunge ambapo ndani yake kuna watalamu na wenye ujuzi mbalimbali lakini hawana utaalamu mkubwa kama baadhi ya watu ambao wapo kwenye bodi waliyosomea mambo ya madini. Mhe. Rais huwezi kuamini 'chairman of audit committee' anavyoulizwa juu ya gharama za kuendesha mgodi anazipitia vipi na kuzihakiki vipi anakujibu alikuwa hana muda wa kulifanyia hilo kwa kuwa anaamini kile alichokuwa analetewa na watendaji wa chini", amesisitiza

Kwa upande mwingine, Mhe. Zungu amewataka watu watumbue kwamba vita ya biashara ya madini siyo ya Rais peke yake bali ni ya watu wote kwa kuwa mali ni za watanzania na zinapaswa zibakie Tanzania.

Vigogo Waliotajwa Ripoti ya Almasi na Tanzanite Mtegoni...Waambiwa Wajiengue Wenyewe

0
0
Rais Magufuli amewataka viongozi mbalimbali wa serikali ambao wametajwa kwenye ripoti za bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite wamepishe nafasi zao ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri kuwachunguza.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akikabidhiwa ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kusema amesikia baadhi ya viongozi mbalimbali wengine ambao amewateuwa yeye kuwa wameusishwa kwenye wizi huo hivyo amewataka wapishe.

"Wako watu wametajwa tajwa, na wengine mimi ndio nilihusika kuwateua sasa ukishatajwa tajwa, naagiza vyombo vya ulinzi na usalama vifuatilie hili tena kwa haraka, Wale ambao wametajwa tajwa kwenye ripoti hii ambao ni wateule wangu, ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri, ni matumaini yangu watakaa pembeni" alisema Rais Magufuli

"Nitashangaa sana endapo watu waliotajwa hawataaanza kukamatwa hata iwe leo wakamatwe tu" alisisitiza Rais Magufuli

Katika ripoti hiyo ambayo iliwasilishwa jana mjini Dodoma na leo kukabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliweza kuwataja baadhi ya viongozi wa serikali ikiwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na viongozi wengine mbalimbali ambao Rais ameagiza washughulikiwe haraka.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema Prof. Abdulkadir Mruma ambaye pia ametajwa katika ripoti hizo alipandikizwa kwa maadui ili kuibua taarifa ya namna nchi inavyoibiwa madini.

BREAKING NEWS: Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene Aliyetajwa Kwenye Ripoti Amejiuzulu

0
0
Taarifa :Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, George Simbachawene amejiuzulu.

 Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ametangaza kujiuzulu nafasi yake kutokana na kutajwa kwenye ripoti za uchunguzi wa tanzanite na almasi

BREAKING NEWS: Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu Adaiwa Kupigwa Risasi

0
0
BREAKING NEWS: Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu Adaiwa Apigwa Risasi
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu  baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa amweetoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.

Kwa Taarifa zilizotufikia hali yake ni mbaya sana baada ya mashambulio hayo ya risasi

Hivi Hapa Viingilio Mechi ya Simba na Azam

0
0
Hivi Hapa Viingilio Mechi ya Simba na Azam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’ limetaja viingilio vya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baina ya timu ya Simba SC dhidi ya Azam FC mchezo utakao chezwa katika dimba la Azam Complex Septemba 9 mwaka huu.

Katika duru la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania ‘VPL’ Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, ilianza na ushindi mwembamba baada ya kuichapa NdandaFC  bao 1-0, katika mtanange uliyochezwa katika dimba la Nangwanda Sijaona.

Wakati Simba SC wao wakianza msimu vyema baada ya kuichapa mabao 7-0 Ruvu Shooting huku mchezaji wao raia wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi akifunga manne kati ya hayo.






Wastara Mahaba Niue na Kibenteni Kipya Baada ya Kumwagana na Bond

0
0
Wastara Mahaba Niue na Kibenteni Kipya Baada ya Kumwagana na Bond
Makubwa! Ikiwa ni siku chache tangu amwagane na aliyekuwa mchumba’ke wa ‘kuvaliana tisheti’, Bond Suleiman Bin Sinaan, mwigizaji mkali Bongo, Wastara Juma anatengeneza tena kichwa cha habari baada ya picha zake akijiachia kimahaba na kijana mdogo (kibenteni) kunaswa na gazeti hili, twende aya kwa aya. Jumatatu ya wiki hii, mwandishi wetu akijiandaa kuondoka ofisini, mishale ya saa moja usiku, alipokea simu kutoka kwa ‘snichi’ makini kuwa, Wastara yupo maeneo ya Mwenge akiwa na bwa’mdogo huyo wakioneshana vitendo vya kimahaba huku wakipigwa picha.

“Njooni huyu dogodogo naona ndiyo mtu wake sasa hivi maana kila anapozunguka anakuwa naye, tena bahati nzuri huyu waliyemuomba awapige picha za kimahaba ni mshikaji wangu, amepiga kwa simu yake kisha amewarushia katika simu zao na yeye amebaki nazo.

“Sasa kwa kuwa yeye hajui haya mambo ya ubuyu, mimi nimemrubuni hapa fasta kwa kumzuga natumia simu yake kisha nikazituma katika simu yangu kwa hiyo msiwe na wasiwasi kama mkiwakosa, nitawapa nilizoziiba,” kilisema chanzo hicho. Mwanahabari wetu alifika fasta katika eneo walipokuwepo na kuwakuta Wastara na ‘mtu wake’ huyo wakiwa ndani ya gari wakijiandaa kuondoka eneo hilo. Hata hivyo, Wastara alipomuona mwanahabari wetu, alishusha kioo na kuanza kumsema kwamba kama amefuata tukio ameumbuka maana wanaondoka zao.

Hata hivyo, Wastara ambaye alikuwa ameketi katika siti ya abiria ya gari hilo wakati bwa’mdogo huyo akiwa katika siti ya dereva, aligeuka mbogo baada ya kuambiwa kwamba kuna mtu amemwaga ubuyu kuwa walikuwa wakijiachia kimahaba hivyo habari hiyo itaandikwa. “Acheni mambo yenu, ina maana mimi siruhusiwi kuwa karibu na mtu yeyote au kuna mtu anayenipangia niende wapi, niwe na nani na kwa sababu zipi? “Mbona mnakosa
mambo ya maana ya kuulizana na kama mnataka tuvunjiane heshima endeleeni, yaani hadi nashangaa jamani.

“Huyu kijana ni mtu ninayefanya naye kazi, tena ni prodyuza wa muziki na muongozaji mkubwa tu wa filamu, makazi yake yako nchini China, lakini kwa sasa yuko hapa Bongo kubadilisha mfumo wa filamu zetu kwa kuongeza ubora katika video na picha, lakini pia amesomea mambo haya ya sanaa. “Kwa kuwa mimi ni mhangaikaji, nahangaika kwa ajili ya wanangu na hali hii niliyonayo, nikaona ni vyema niwe naye karibu kwa kuunganisha nguvu ili angalau tuboreshe kazi zetu.

Wakifanya yao.
“Tulipokuwa tukivurunda kwenye ubora wa kazi zetu mlisema, sasa wanapokuja wenye maarifa na uelewa mkubwa tukiwa nao karibu mnaanza kuingiza mambo yenu ya ajabuajabu, tulikuwa Mwenge kuna mahitaji aliomba nimsindikize akanunune, tukiwa kwenye gari kuna picha alikuwa ametumiwa akawa ananionesha,” alisema Wastara kwa hasira.

Mwanahabari wetu alipombana zaidi na kumwambia kuna mtu amewaona wakivuka mipaka hadi ya kubusiana na picha zipo, Wastara alifunguka: “Kuhusu busu nina mipaka ya kumbusu mtu, wewe huwezi kumbusu hata dada yako kwa mfano?,”


Alihoji Wastara na kumalizia: “Sikia, huyu kijana anaitwa Jukya, ana familia na mkewe, kama kuna mtu amewatuma kutuharibia kazi zetu na kututoa kwenye mstari, mmeshindwa na hamuwezi. Najiheshimu na kwa sasa naangalia kazi.

“Hivi juzi nimetoka kutoa wimbo wangu wa Mwanamke nikiwatia nguvu wanawake waliovunjika mioyo, leo tena unaniuliza habari hizo, ole wako uandike, nitaingia na tingatinga hapo ofisini kwenu, mimi ni kichaa,” alisema Wastara kisha kumuamuru bwa’mdogo huyo waondoke eneo hilo. Licha ya kukosa zile picha walizopiga kimahaba, mwanahabari wetu alifanikiwa kupata picha alizokuwa amepewa na snichi wake ambazo zimepamba ukurasa wa nyuma wa gazeti hili.

Fifa Yataka Mechi kati ya Afrika Kusini na Senegal Kurudiwa

0
0
Fifa Yataka Mechi kati ya Afrika Kusini na Senegal Kurudiwa
Mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya Afrika Kusini na Senegal itarudiwa tena baada ya refa aliyesimamiwa mechi hiyo kupigwa marufuku na Fifa.
Refa huyo raia wa Ghana Joseph Lamptey, alipiwa marufuku kwa kusimia mechi kwa njia isiyofaa.
Aliwapa penalti Afrika Kusini ambao walishinda kwa mabao 2-1 mwezi Novemba mwaka uliopita kwa kunawa mpira lakini kanda ya video baaadaye ilionyeha kuwa mpira huo ulimgonga kwenye goti mlinzi wa Senegal Kalidou Koulibaly.

Mechi hiyo itachezwa tena Novemba mwaka huu.
Lamptey alipigwa marufuku ya maisha mwezi Machi lakini jana Jumatano marufuku hiyo ilibatiliswa na mahakama ya michezo.

Lamptey, ambaye pia alisimamia mechi katika mashindano ya Olimpki huko Rio mwaka uliopita alikataa na kungea na BBC baada ya kupigwa marufuku ambayo ilikuja baada ya Senegal kulalamika.
Senegal na Afrika Kusini kwa saa wako nafasi ya tatu na nne mtawalia katika kundi la la D nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde.
Ni timu moja pekee ya kwanza katika kundi ambayo itafuzua kwa meche za kombe la dunia nchini Urusi mwaka ujao.

Bila Rais Magufuli Nchi Isingefikia Hatua ya Kupambana na Ufisadi wa Madini- Ndugai

0
0
Bila Rais Magufuli Nchi Isingefikia Hatua ya Kupambana na Ufisadi wa Madini- Ndugai
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai bila ya Rais Magufuli nchi isingeweza kufika katika hatua ya kupambana na ufisadi wa madini hivyo watanzania wanapaswa wamshukuru kwa kuweza kujitoa kusimamia rasimali za nchi bila ya woga.

Spika Ndugai amebainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya ripoti ya kamati ya uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na kamati maalum mbili.
"Kumpata Rais aliyejitoa kusimamia rasimali za nchi si jambo rahisi wala jepesi. Mwalimu alijaribu kufanya hivyo awamu ya kwanza pakawa na tabu mtindo mmoja lakini watanzania walishikana naye kwa magumu yote yaliyokuwepo hadi mwisho kwa hiyo sasa lazima tushikamane na Rais wetu hata kama tunapo kwenda tutakuwa na magumu yeyote yale kwa maana kwamba lazima rasimali za nchi ziwafaidishe watanzania kwa namna moja ama nyingine, hatusemi asilimia 100 iwe yetu hatuwezi kwa sababu tunahitaji teknolojia, fedha na mambo mengine kutoka wa wabia wenye nia njema ili nasi tupate", amesema Ndugai.

Pamoja na hayo, Mhe. Ndugai ameendelea kwa kusema "ndugu zangu watanzania tunapaswa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kumpata Rais Magufuli, sisemi haya kwa sababu yupo mbele yangu, nyinyi wenzangu mnafahamu nchi zetu za Afrika hizi historia zetu za Afrika na jinsi tulivyokuwa tumeneemeshwa na Mwenyezi Mungu lakini wajanja wachache wanachukua mali za

Afrika na kuiacha haina lolote tangu wakati wa mkoloni na baada ya mkoloni", amesisitiza Ndugai.
Kwa upande mwingine, Mhe. Ndugai amewasisitizia wabunge kuwa na umoja katika mambo ambayo yanawaunganisha ambapo moja wapo ni kuhusu rasimali za taifa huku akipiga dongo kwa kusema wanaopaswa kukosa uzalendo ni Simba na Yanga kwa sababu wao wanaimba kabisa uzalendo umewashinda pindi wawapo uwanjani.

Malinzi na Mwasigwe Mambo Bado Magumu Mahakamani

0
0
Malinzi na Mwasigwe Mambo Bado Magumu Mahakamani
Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Jamal Malinzi na wenzake wawili imeahirishwa hadi Septemba 21 baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo kuwa na dharura.

Hayo yameelezwa na Wakili wa serikali, Faraj Ngokah mbele ya Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam na kusema upelelezi wa kesi hiyo hujakamalika pamoja na Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Wilbard Mashauri amepatwa na dharura.

Kutokana na hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 21 mwaka huu itakapotajwa kwa mara nyingine tena

Kwa upande mwingine, viongozi hao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali  yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao pamoja na kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.


Naibu Waziri Ngonyani Aandaa Barua ya Kujiudhuru Kupisha Uchunguzi

0
0
 Naibu Waziri Ngonyani Aandaa Barua ya Kujiudhuru Kupisha Uchunguzi
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema anaandika barua ya kujiuzulu baada ya Rais John Magufuli kuwataka watu wote waliotajwa kwenye ripoti ya biashara ya madini ya almasi na Tanzanite kujiondoa wenyewe.

Kauli hiyo ameitoa leo baada ya hafla ya makabidhianao ya ripoti hizo, Ngonyani amesema amepokea kauli ya Rais kwa mikono miwili na sasa anaandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.

“Hata sasa unanichelewesha nipo naandika barua ya kujiuzulu, hii ni nafasi niliyopewa na ni lazima nimuunge mkono Rais katika hatua zake za kutaka kubadili mfumo wa nchi na kuufanya wenye manufaa kwa wananchi,” amesema Ngonyani.

Amesema hawezi kuongeza chochote juu ya kauli ya Rais na anaviachia kazi vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake kama ambavyo mkuu wa nchi amevitaka.



Hali ya Lisu Haielezeki na Lolote Linaweza Kutokea- Mbowe

0
0
Hali ya Lisu Haielezeki na Lolote Linaweza Kutokea- Mbowe
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi  na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Dereva wa Tundu Lissu aliyeshika nguo zenye damu
Akizungumza na kituo cha ITV Mwenyekiti wa CHADEMA Freeaman Mbowe amesema  "Hali ya Tundu Lisu ni mbaya Sana, na msishangae mkasikia lolote kuanzia sasa"

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji
Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.



Pendeza na Kessy Products: Badili Muonekano Wako na Kuweka Mwili Wako Sawa Bila Madhara yoyote

0
0
PENDEZA NA KESSY PRODUCT: BADILI MUONEKANO WAKO NA KUWEKA MWILI WAKO SAW KWA PRODUCT ZA ASILI ZISIZO NA MADHARA YEYOTE WALA KEMIKALI, MATOKEO NI KWAARAKA


1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _80,000/
2) KUREFUSH NYWELE  KUZIJAZA NA KUZUIAKUKATIKA 90,000/
3) TENGENEZA SHEPU YAKO KUWA NA UMBO ZURI (HIPS & BATKS)KUNADAWA AINA TATU (@)KUPAK (B) KUNYWA (C)VIDONGE_130,000/
  4)ONDOA NYAMA UZEMBE MIKONONI, KIUNONI KUPAK _90,000/
5)TOA  KITAMBI KABISA(@) KUPAK 10O,000/ (B)VIDONGE/SLIMING MAJAN 130,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KILO UNAZOITAJI WEWE
@) DAW YA MAJIN NA VIDONGE_130,000/
7)PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME KAMA MWANZO _80,000/
8) PIA UNA KUONGEZA MAZIWA SAIZI UNAYOHITAJI WEWE_80,000/
9)ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA_100,000/
10) ONDOA MICHIRIZI ILIYO SHINDIKANA_90,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KWENY MAPAJA KIKWAPAN_90,000/
13) KUWA MWEUPE WAKUPENDEZA(@) VIDOGO(WHITE SOLUTION)_130,000/(B)MAFUTA YAKUPAK 100,000/
14)TOA NDEVU VINYWELEO MILINI _90,000/
15/ ONGEZA NGUVU ZA KIUME (@)JELI_80,000/(B)VIDONGE MAX MAN_ 100,000/
16) ENGEZA MAUMBIL YA KIUME
@) (HANDSOME UP) MASHINE _200,000/
@) JELI NA VIDONG VYA SHARK_120,000/
17) RUDISHA HAMU YA TENDO NA KUCHELEWA KUFIKA KILELE_90,000/
18) RUDISH(BIKRA) 100,000/
19)ONDOA MAFUTA USONI _90,000/
20) ONDOA MIKUNJO USON_70,000/
(21) ENGEZA  MGUU_80,000/  

 TUNAPATIKAN DAR W SALAAM: NAKWA MIKOAN KOTE UTAPATA PIGA CM                      (+255) 0719955528
0756259180
0785371237
@dr_kessy_product
Delivery  POPOTE ULIPO

NEC Yamtangaza Rehema Migira Kuziba Nafasi ya Bi. Hindu Mwenda

0
0
NEC Yamtangaza Rehema Migira Kuziba Nafasi ya Bi. Hindu Mwenda
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima  Kombwey ametangaza kumteua Mbunge ndugu Rehema Juma Migira kuwa Mbunge wa viti maalum kupitia Chama Cha (CUF) kufuatia kifo cha mbunge mteule Bi Hindu Mwenda aliyefariki dunia Septemba 1, 2017.

Kailima amesema Tume ya Uchaguzi imefanya uteuzi huo baada ya kupata taarifa kutoka wa spika wa bunge, Job Ndugai kuwepo kwa nafasi moja ya ubunge kufutia kifo cha mbunge huyo mteule ambaye alifariki siku tatu kabla ya kuapishwa.

"Tume ya taifa ya uchaguzi imemteua ndugu Rehema Juma Migira kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata taarifa kutoka wa spika ambaye alitutaarifu kuwepo kwa nafasi moja ya wazi ya viti maalumu kupitia chama cha CUF baada ya aliyeteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum CUF kufariki dunia" alisema Kailima

Aidha Kailima aliendelea kusema kuwa tume hiyo imefanya uteuzi pia wa madiwani wa viti maalum watatu kujaza nafasi wazi katika halimashauri za Tanzania bara madiwani hao ni pamoja na ndugu Jane Chungwa kutoka CCM ambaye anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Itigi Singida, Ndugu Osana Mwinyi kutoka chama cha CCM anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Bahi Dodoma na ndugu Pili Mfaume kutoka chama cha CUF anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Temeke, uteuzi huo wa madiwani umefanyika baada ya tume kupata taarifa ya kuwepo kwa nafasi hizo wazi kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa.

MASKINI Zitto Kabwe Afunguka Haya Kwa Uchungu Baada ya Tundu Lissu Kupigwa Risasi

0
0
Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Taarrifa ya Lissu Kupigwa Risasi
Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mhe. Zitto Zuberi Kabwe amewataka wananchi kusimama imara na wasikubali kabisa kuruhusu siasa za mauji kupata nafasi nchini Tanzania.


Zitto ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa facebook mara baada ya kutokea taarifa ya kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu na watu wasiyofahamika.

"Mbunge mwenzetu wa Singida Mashariki amepigwa risasi nyingi na watu wasiojulikana. Kakimbizwa hospitali Dodoma.
Nchi yetu imefungua ukurasa mpya. Wananchi tusimame imara tusikubali Kabisa kuingia kwenye siasa za namna Hii. Mola amponye ndugu yetu", ameandika Zitto.

 Mhe. Tundu Antipas Lissu amepigwa risasi kadhaa mwilini mwake akiwa nyumbani kwake Dodoma eneo la 'area D' na watu wasiojulikana.


Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images