Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Spika Ndugai Awataka Wabunge Watoe Nusu ya Posho zao Kuchangia Matibabu ya Tundu Lissu

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewaomba wabunge watoe nusu ya posho zao kwa siku kuchangia gharama za matibabu ya Tundu Lissu.

Ndugai amesema leo  bungeni kuwa gari ya Tundu Lissu ilipigwa jumla ya risasi 28 hadi 32,lakini zilizompata Tundu Lissu ni tano ambapo zilimjeruhi tumboni na mguuni.

Lissu aliondolewa Hospitali ya General Dodoma  Usiku wa kuamkia leo na kupelekwa nchini Kenya  kwa Matibabu zaidi

Maskini Kundi la Vijana Wambaka Msichana wa Miaka 20 Hadi Kufa na Kumtupa Jalalani

$
0
0
Kundi la vijana wasiofahamika wamembaka msichana wa miaka 20 hadi kufa na kisha kumtupa jalalani maeneo ya jirani na nyumbani kwao Madale Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wakisimulia tukuio wazazi wa binti huyo, wamesema kuwa mpaka majira ya saa nne usiku kuamkia Jana Septemba 7 alikuwa nyumbani kabla ya kuwasili kwa vijana watatu waliokuja na pikipiki (bodaboda) na kuanza kuzungumza naye kama marafiki kwa takribani saa nzima na baadae binti yake kuaga akitaka kuwasindikiza na hakurudi tena hadi alipopewa taarifa za kifo hicho.

Aidha Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Madale, Gration Mbelwa ameliomba Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kuwaomba wanafamilia pamoja na rafiki za binti huyo kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwakamata watuhumiwa hao.

Magufuli 'Tulitumia Ukachero Kupata Taarifa za Acacia'

$
0
0
RAIS John Magufuli ameelezea jinsi ofi si yake ilivyotumia mbinu ya ukachero na uchunguzi na kupata taarifa zote za namna rasilimali mbalimbali za madini ikiwemo dhahabu, almasi na tanzanite zinavyoibwa nchini.

Pamoja na hayo, amebainisha kuwa serikali yake haiko tayari kutishiwa na mtu yeyote anayetumia rasilimali za Watanzania kwa manufaa yake binafsi, na kwamba iko tayarikusimamisha migodi yote isichimbwe kuliko kuruhusu madini hayo kuvunwa na kunufaisha wachache. Dk Magufuli aliyasema hayo Dar es Salaam Ikulu jana wakati akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ripoti mbili za Kamati za Bunge zilizoundwa na Spika Job Ndugai kwa ajili ya kuchunguza biashara za madini ya tanzanite na almasi.

Alisema kabla ya kuunda kamati mbili za kuchunguza makinikia ya dhahabu mapema mwaka huu, tayari ofisi yake ilishafanya utafiti kwa kutumia mbinu mbalimbali na kupata taarifa yakiwemo mawasiliano ya namna ya kuiba rasilimali hizo. “Wakati nikianza kuzungumzia masuala ya wizi, wapo wengine waliona ninazungumza tu kutoka hewani, nataka niwaeleze tumefanya research ya kutosha, tulitumia baadhi ya wafanyakazi, forensic investigation, mfano kwenye dhahabu tuna information zote,” alieleza Dk Magufuli.

Alisema kupitia mbinu mkakati hizo, walifanikiwa kufyonza data za kwenye migodi yote, na hata wahusika waliposhtuka na kubadilisha kompyuta zao walikuwa wameshachelewa kwani taarifa zao zote zilikuwa zimedukuliwa. “Tuna communication zao zote, nataka niwaeleze Watanzania mjue, walivyokuwa wanawasiliana, walivyopanga mikakati ya kuiba, wakishirikiana na watendaji wengine Watanzania, tuna information zote.

Tulitumia watu wetu,” alisisitiza. Alisema wako Watanzania wazalendo, waliotumia nafasi zao wakiwemo baadhi yao walionekana kama wachimbaji, maaskari na hata wenye vyeo vikubwa ambao kazi yao ilikuwa ni kukusanya taarifa kamili za namna wizi unavyofanyika. “Tumekuwa tukitumia maisha ya baadhi ya Watanzania katika kupata taarifa stahiki. Mfano hili suala la tanzanite, nimeambiwa kuna video kwenye flash, lakini mimi ninayo yangu, nimekaa nayo kwa muda mrefu kutoka kwa Watanzania wanaofanya kazi kizalendo kwa ajili yetu,” alisema.

Aliongeza: “Mwingine unaweza ukamuona ni mchimbaji tu, mlinzi, wanatumia mbinu mbalimbali kama kwenye vita. Hii ni vita na ndiyo maana hata askari wanapokuwa kwenye vita, hutuma mashushu wao kwenye vikosi vya maadui,” Alisema katika vita, askari hutuma askari wao kwa upande wa adui na askari hao hulazimika kupigana kwa upande huo kwa lengo la kuaminiwa ili wapate taarifa kamili na sahihi ingawa kwa kufanya hivyo maisha yao huwa hatarini hasa pale wanapobainika.

“Asipoangalia anaweza akauawa na watu wake, mpaka pawe na mtu ayakayesema jamani huyu ni mtu wetu, na anaweza kutambulishwa hivyo akiwa tayari ameshakufa. Nawaambia ukweli katika mchakato huu wapo wenzetu tuliowatuma,” alibainisha. Alisema katika mbinu hizo za kupata taarifa siku tano zilizopita, serikali ilikamata almasi yenye kilo 15.5 ikiwa imegawanyika katika madaraja matatu na inayodaiwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 14.

Hata hivyo, kupitia Watanzania hao wazalendo waliowekwa huko na serikali, baada ya kuzipima na kuzithaminisha, almasi hizo katika daraja la kwanza pekee linalodaiwa kuwa na kilo nne, mpaka juzi zilipopimwa zilibainika kuwa zaidi ya kilo nane. “Sasa hapo bado class ya pili na ya tatu, nina imani kabisa hiyo thamani inayodaiwa ya Dola za Marekani milioni 14, ikawa zaidi ya Dola za Marekani milioni 20 hadi 25. Jambo la kusikitisha Wizara ya Nishati na Madini ambayo ni msimamizi hata vifaa vya kuthibitishia madini hayo kabla hayajasafirishwa haina,” alisema.

Alisema endapo hali hiyo itaendelea ya wizara kukosa vifaa stahiki vya kupimia madini kabla hayajasafirishwa ni sawa na kupigana vita na kumuomba adui unayepambana naye silaha. “Mtashangaa anayeifanya hiyo kazi, aliyevumbua hayo mabaya, anayetupa information zote za kule mpaka tukajua tulikuwa tunapigwa vibaya ni Profesa Mruma (Abdulkarim). Alikuwa ni askari tuliyempeleka kule,” alibainisha Dk Magufuli.

Wakati akiwasilisha matokeo ya ripoti ya Kamati ya Bunge ya kuchunguza biashara ya madini ya almasi, Mwenyekiti wake, Mussa Azzan Zungu alimtaja Profesa Mruma ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kuwa ni mmoja wa watendaji wa serikali ambao hawakuwa makini na kuisababishia hasara serikali.

Alisema Profesa Mruma ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa Madini nchini, aliisababishia hasara nchi kwa kuruhusu madini hayo ya almasi yapotee kwa uzembe. Hata hivyo, Dk Magufuli alimtaja msomi huyo kuwa ni mmoja wa wazalendo waliojitolea kama askari na kufanya kazi kama sehemu ya adui kwa faida ya nchi yake.

Akizungumzia maendeleo ya mazungumzo baina ya wawekezaji wa madini ya dhahabu nchini wa Kampuni ya Acacia na serikali, Dk Magufuli, alibainisha kuwa mazungumzo hayo yanaendelea vizuri tofauti na maneno yanayozungumzwa mitaani. “Nataka niwahakikishie kuwa wapo Watanzania wazalendo wanaofanya kazi kwa ajili ya nchi yao.

Ndiyo maana hawa wazungu wa dhahabu wapo hadi leo wanazungumza, walikuja 14, lakini mpaka leo wameongezeka na kufikia 25, wanaenda kule wanajaribu wanaongezeka, sisi idadi ya watu ni wale wale,” alieleza. “…Nimesikia wengine wanatishia kufukuza wafanyakazi, nilitamani waseme wanaondoka, wakiondoka tutachukua wananchi wa kawaida watajazana mle kuchimba madini. Wao watafukuza 200, tukiruhusu wananchi wetu tutangeneza ajira milioni moja, hii ni rasilimali yetu,” alisisitiza.

Aliwaonya wawekezaji hao wasijaribu kuitisha serikali bali wao ndiyo wajiandae kutishika. Alisema fedha zinazoibiwa kupitia madini ni nyingi kiasi kwamba huenda Tanzania ndiyo ikawa inafadhili nchi zilizoendelea badala ya yenyewe kufadhiliwa. “Sisi tunatengeneza bajeti ya Sh trilioni 20 hadi 30 wao wanachukua Sh trilioni 600, wanakuja hapa wanasema wao ndiyo wafadhili, sisi ndiyo wafadhili,” alieleza.

Alisisitiza kuwa muda wa Tanzania kuchezewa na kuibiwa umekwisha kwani Watanzania wengi wanaishi maisha ya kimaskini, miundombinu mibovu, huduma muhimu kama elimu na afya hazipatikani ipasavyo, huku fedha nyingi zikipotea. “Ukiangalia maeneo ya machimbo au karibu na mgodi wowote wa dhahabu au tanzanite unaweza kuona maisha ya wanaoishi karibu na hiyo migodi.

Angalia maisha yao, Shida walizonazo, najua leo Watanzania wanatuangalia hapa leo, kila mmoja ajiangalie yeye na jirani yake wana maisha gani,” alisema. Alisema kutokana na utajiri ambao Tanzania imebarikiwa ikiwemo kuwa nchi ya pili baada ya Brazil kwa kuwa na vivutio vingi, Watanzania hawastahili kuishi maisha ya kimasikini.

Awali, wakizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhiwa ripoti za uchunguzi wa biashara ya almasi na tanzanite, wenyeviti wa kamati hizo, Mussa Zungu na Dotto Biteko walibainisha namna kamati zao zilivyoibua madudu ikiwemo kuwepo kwa mikataba mibovu, usimamizi mbovu wa rasilimali hizo za madini namna madini hayo yanavyoibiwa.

Kwa upande wake, Zungu alisema kamati yake ilibaini udanganyifu mwingi ulioitia hasara serikali ikiwemo uwepo wa mitambo ya zamani huku taarifa zikionesha ni mitambo mipya pamoja na kuchenjuliwa kwa makinikia ya almasi yaliyochimbwa miaka 40 iliyopita huku taarifa zikionesha yamechimbwa hivi karibuni. “Tumegundua Stamico iliufanya mgodi wa almasi kama shamba la bibi, yapo madeni ambayo mgodi huu unadaiwa lakini nina uhakika yakihakikiwa yatakuwa si ya kweli, mfano kwa sasa mgodi unadaiwa Dola za Marekani milioni 238, lakini deni hili likihakikiwa haliwezi kufikia dola za Marekani milioni 15,” alifafanua.

Naye Biteko pamoja na kuzungumzia namna serikali ilivyoingia mikataba mibovu kwenye biashara ya tanzanite, pia alieleza jinsi kamati hiyo ilivyobaini kuwepo kwa watu waliokabidhiwa dhamana ya usimamizi wa madini walivyoshindwa kuyasimamia. Alisema katika kamati yake walikuwa na hadidu za rejea tano na walihoji mashahidi 159, walipitia na kuchambua nyaraka 150 za umma na binafsi na kubaini kuwa mkataba uliopo wa tanzanite na Stamico hauna tija kwa taifa. “Mfumo wa usimamizi uliopo ni dhaifu, kwani tanzanite yote iliyochimbwa nchini mapato yaliyopatikana kwa Tanzania ni asilimia 12 tu, wakati madini haya yanayopatikana nchini pekee, yanatoa ajira zaidi ya 500,000 India,” alisema

Rungwe Afunguka Baada ya Kuachiwa kwa Dhamana Baada ya Kukaa Selo Kwa Siku Nane

$
0
0
September 6 2017 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam liliamchia kwa dhamana, mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma ‘CHAUMMA’ Hashim Rungwe baada ya kumshikilia kwa siku 8 kwa kile kilichodaiwa kuhusika katika utapeli wa Dola za Kimarekani 30,800 ambazo ni sawa na Tsh Milioni 73 kwa nyakati tofauti akiwa kama Wakili anayeendesha biashara kati ya raia wa Uturuki Ally Riza Bilgen na Kampuni ya Les Tropiques Group Mining SPRL Limited.

Inaelezwa kuwa raia huyo wa Uturuki alikuja Tanzania kwa lengo la kununua korosho tani 15 na kuandikishana mkataba wa malipo ya Dola 72,000 kama gharama za bidhaa hiyo na usafirishaji lakini tangu wamesainishana mkataba huo November 2016, hakuna kilichofanyika na malipo hayo ya awali yalifanywa kwenye akaunti ya Rungwe katika Bank ya CRDB.

Angalia VIDEO Akielezea:

Hatimaye Hotel ya Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi 'Sugu' yafunguliwa

$
0
0
Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ alianza kuijenga hoteli yake toka mwaka 2016 jijini Mbeya na aliweka wazi kabisa kwamba alipata mkopo wa kuijenga kutoka CRDB BANK.

Itafahamika kwa jina Hotel Desderia

Tayari hoteli imefunguliwa na kuna nafasi za kulaza wageni kwenye room zilizojengwa kisasa lakini pia hata kwa chakula ni bora ambapo mchakato wa kumpata Mpishi ulipatikana kwa njia ya usaili, ukitazama kwenye hizi picha hapa chini utaona chakula alichokitoa Mpishi alieshinda kwenye huo usaili.

Hongera umehustle sana na maisha
Politics ni ajira nzuri naona umuhimu wa wizara ya elimu kuongeza somo la siasa kwenye mtaala ili watu waijue miiko yake kwa sababu watu wengine ni wabwabwajaji kama baadhi ya viongozi wa siasa kutoka ccm na upinzani, siasa inakumfanya mtu kuwa brand kubwa na uwezekano wa kuitumia kibiashara upo.

Sugu ni akili kubwa hutosikia akiburuzwa mahakamani na serikali kila leo hana muda huo he is always thinking of business.

Thumb Up kwa Mh Sugu au Jongwe kama yeye anavyopenda kujiita

VIDEO: CHADEMA Watoa Taarifa Rasmi Kuhusu Tundu Lissu Kupigwa Risasi na Watu Wasiojulikana

$
0
0
Siku moja baada ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuvamiwa na kupigwa risasi nyingi mwilini mwake, Leo Septemba 8, CHADEMA kimetoa taarifa rasmi kupitia kwa Katibu mkuu wa chama hicho Ndugu Vincent Mashinji Juu ya kilichotokea na kinachoendelea mpaka sasa kumuhusu Mbunge na mwanasheria wa Chama hicho Tundu Lissu ambaye alilazimika kupelekwa Jijini Nairobi Nchini Kenya kwa matibabu, ambapo taarifa hiyo iliambatana na maagizo kadhaa. FULL VIDEO:

Manji Afunguka Mahakamani "Sitambui Kuvuliwa Udiwani Kama Ilivyotangazwa"

$
0
0
MFANYABIASHARA Yusuf Manji ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hatambui kuvuliwa udiwani kama ilivyoandikwa kwenye vyombo vya habari.

Manji amesema anatambua kuwa yeye ni Diwani wa Mbagala Kuu na kwamba mahakama imuagize Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) awaambie Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kwamba walimkamata na sababu za kutohudhuria vikao kwa miezi miwili ni kwa kuwa hana dhamana.

Ameyasema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Amesema yeye amechaguliwa na wananchi na kwamba kama wanataka aende kwenye vikao, DPP aombe hati ya kumtoa gerezani ili akaudhurie vikao au wamuandikie barua yenye ajenda na kumbukumbu za vikao ili ajibu akiwa gerezani.

"Nimetumia zaidi ya milioni 70 kwa fedha zangu na sio za halmashauri kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wangu na nilikuwa nahudhuria vikao kabla sijakamatwa kwa kesi hii nzito.

Kwa kuwa naheshimu mahakama na kesi hii na kwa kuwa naheshimu mahakama hii na ukubwa wa kesi sikuomba dhamana," amesema Manji. Hakimu Shaidi amewataka upande wa mashitaka kufuatilia suala hilo na kwamba maombi yake yamechukuliwa.

Risasi Alizopigwa Tundu Lissu Zamnyima Zitto Kabwe Usingizi...Afunguka Makubwa

$
0
0
Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa, anaeleza Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

“Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu,” amesema Zitto katika taarifa aliyoitoa leo Ijumaa.

Lissu alijeruhiwa kwa risasi jana Alhamisi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi, Kenya.

Mbunge wa Singida Mashariki, Lissu alisafirishwa jana usiku baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Zitto amesema, “Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama nchi, kama Taifa.”

Amesema kilichotokea kwa Lissu jana Alhamisi ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana na utamaduni wa ustahimilivu na udugu ambao nchi imekuwa ikisimamia.

“Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia,” amesema.

Amesema Watanzania wanaolitakia mema Taifa wana kila sababu ya kulaani na kukataa utamaduni wa kimafia kuzoeleka nchini.

“Tusimame kulaani kwani #HuuSiUtanzania,” amehitimisha Zitto katika taarifa yake.

Tukio la Tundu Lissu Lawafanya Wabunge Waondoe Tofauti zao...Wamchangia Milion 43 za Matibabu

$
0
0
Wabunge wamekubali kuchangia nusu ya posho yao kwa siku moja kuchangia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi, Kenya.

Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwaomba kuchangia fedha hizo na wabunge wakapiga makofi kuashiria kukubali.

Hakuna kiwango kamili kilichotangazwa kama malipo ya wabunge kwa siku ambayo yameainishwa kwa uwazi lakini baadhi ya wabunge wanataja kuwa posho ya kikao ni Sh220,000 hivyo nusu yake ni Sh110,000 hivyo kuwezesha kukusanywa zaidi ya Sh43 milioni.

Lissu alishambuliwa jana Alhamisi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Spika Ndugai akizungumzia safari ya Lissu Nairobi amesema lilikuwa ni ombi maalumu kutoka kwa wanafamilia na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Spika Ndugai amewaomba wabunge na Watanzania kutulia na kuendelea kumuombea Lissu badala ya kuendelea kulaumiana kupitia mitandao ya kijamii.

Amsema tukio hilo ni la kwanza na la aina yake kutokea tangu Bunge lilipohamia Dodoma na hasa katika kipindi ambacho Bunge linaendelea na vikao.

Donald Trump Alaani Shambulio la Risasi la Tundu Lissu

$
0
0
SERIKALI ya Marekani inayoongozwa na Rais Trump kupitia ubalozi wake ulioko hapa nchini, imeeleza kusikitishwa na tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
“Marekani imesikitishwa sana kuhusu kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, Mbunge na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika. Tunalaani kitendo hiki cha kipuuzi na cha kutumia nguvu. Tunaungana na Watanzania kutoa matumaini yetu ya dhati ili apone haraka.
———————————
The United States is deeply saddened by the shooting of Tundu Lissu, Member of Parliament and President of the Tanganyika Law Society. We condemn this senseless act of violence and join Tanzanians in expressing our sincere hopes for his full and speedy recovery.” Imesema taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Ubalozi huo umesema unaungana na Watanzania katika kumtakia kheri Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ili apone haraka.

Lissu jana Alhamisi saa sita usiku alisafirishwa kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya.
Awali, alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma baada ya kushambuliwa. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema leo Ijumaa asubuhi kuwa, Lissu alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 hadi 32, huku tano zikimpata mwilini.
 Akitoa taarifa ya tukio hilo kwenye kikao cha Bunge, Ndugai amesema risasi mbili zilimpata Lissu kwenye miguu, mbili tumboni na moja kwenye mkono.
Aidha, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji amesema kuwa amepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti  wa Chama hicho, Freeman Mbowe kuwa Tundu Lissu amezinduka leo asubuhi akiwa katika Hospitali ya Aga-Khan jijini Nairobi nchini Kenya,  kwa sasa ameshazinduka anajitambua na anaendelea vizuri.

Pata Habari Zetu Kupitia Application ya Udaku Special Kwenye Simu yako Bila Kufungua Website

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Remove Se.x From a Relationship, 90% of Women Have Nothing to Offer. Is it true?'

$
0
0
Remove se.x from a relationship you will discover that over 90% of women have nothing to offer in that relationship.

Remove money from a relationship you will discover that over 90% of women see no reason to be in that relationship!

Wadau hii ni kweli?

Nimegundua Ana Mimba ya mtu Mwingine Baada ya Kumchumbia na Kunikubalia Kumuoa

$
0
0
Salaam zetu, habari hizi zinanisikitisha kidogo ,kijana mmoja ambaye ni mtu wangu wa karibu , amekuja kuniomba ushauri Na maelezo yake yako hivi

"Miezi kadhaa iliopita nilikutana Na msichana Mrembo anasoma chuo, lakin Alikuwa akimaliza masomo yake ya diploma, tukawa tumekuwa marafiki ,nikawa nami nasafiri kwenda mkoani kwa siku 14, lakin nikiwa uko uko mkoani nikaamua kumu approach kupitia mawasiliano akasema ni vema nikirudi ndo tukae tuzungumze, nikarudi toka mkoani tukakutana hotelin tukazungumza kwa Kina ,nilimuelezea mipango yangu ya kwanini nataka niwe naye kwa mahusihano, naye akakubali, tukawa wapenzi kabisa.

Nikawa namuita tunakutana tunaongea habari mbali mbali. Bila kishiriki tendo la ndoa,

Sasa baadae wiki Jana amenipigia simu kuwa ninaomba nikwambie Jambo please, nkasema sawa akasema naomba usishtuke nataka kukwambia lakin naogopa, nkasema kuwa huru akasema mpenzi Nina mimba ya mvulana tuliyeachana ambaye nimekueleza Na ina miez 2, kwakweli nimepigwa Na butwaa ni msichana Mrembo nampenda, nimeshawajulisha hadi wazazi wanamjua, Sijawahi shiriki naye tendo la ndoa kwa kusema ngoja nisubiri tuoane,
Baada ya kunambia nilivuta pumzi nikakaa kimya kidogo nkasema tuwasiliane baadae, nikawazaaa, sasa ananambia mimba aitoe kwa kutumia madawa ya kichina, ambayo yanaharibu mimba inatoka kama damu,
Sasa najiuliza ndugu yangu
1. Je hayo hayataaribu kizazi kamwe hakose mtoto tukiwa wote mbeleni?
2. Zambi za mtoto huyu hazitatutafna? Maana ukiua lazima IPO siku utajutia uamzi UO,
Nimeenda kwa marafiki zangu wakasema haina shida mpe elfu 60 atoe, lakin mmoja akasema kwanza nenda naye hospital uhakikishe maana wasichana siku hizi wajanja mno, Anaweza kukupiga hela TU, tumeenda kwa Dokta ni kweli Ana mimba , mbaya zaid dokta kanipongeza Mimi kwamba hongera mkeo Ana mimba,
Nifanye nini? "

Mwisho wa kunukuu anaomba ushauri, this is true story

By Venchwa

Mh. Fredrick Sumaye Afunguka Aitupia Lawama Serikali Sakata la Tundu Lissu

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Fredrick Sumaye amedai endapo serikali ingekuwa inawajibika ipasavyo, matukio ya kiuhalifu yasingekuwa yanaendelea kujitokeza mara kwa mara nchini.

Mhe. Sumaye ameeleza kupitia mkutano wa chama hicho na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo ikiwa imepita siku moja tokea kwa tukio lililompata Mhe. Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma 'Area D' na watu wasiofahamika.

"Katika serikali yeyote ambayo inawajibika ipasavyo kazi ya kwanza ya serikiali ni kulinda uhai wa wananchi wake, hiyo ndiyo kazi ya msingi ya serikali. Kwa hiyo kama ni serikali inayowajibika ipasavyo, basi haya matukio yanayoendelea kutokea yasingekuwepo kabisa au basi tukio linapotokea wahusika wangekuwa wanakamatwa kwa haraka na kupelekwa sehemu husika lakini unapokuwa huoni hatua zinazoridhisha zikichukuliwa basi kuna ulakini katika nchi", amesema Sumaye.

Pamoja na hayo, Sumaye ameendelea kwa kusema "kwa sababu serikali ni yetu sote bila ya kujali itikadi ya chama husika. Kwa hiyo mimi nasema kama kweli serikali inawajibika inavyotakiwa basi haya mambo yote ambayo yanatokea yalitakiwa yapatikane majibu ya uhakika na kwani yanapoachwa baadhi ya maeneo yapo gizani basi wengi tunaanza kufikili kwamba utawala unaowajibika unakosekana ama kwa makusudi au kwa uwezo".

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti  wa chama hicho Prof. Abdallah Safari amesema kabla ya Mhe. Tundu Lissu kupigwa risasi alikuwa mtu mwenye wasiwasi mkubwa juu ya maisha yake kutokana na baadhi ya watu waliokuwa wanamfuatilia kwa ukaribu kila kukicha.

"Kabla ya tukio hili kutokea Mhe. Lissu alishawahi kusema katika mkutano wake na waandishi wa habari alikuwa na hofu na maisha yake kutokana na kufuatiliwa na watu wenye gari aina ya Nissan Premier yenye namba za usajili T460 CQV hapa hapa Dar es Salaam. Kwa hiyo maisha ya Lissu yamekuwa yapo hatari kwa kipindi kirefu", amesema Prof. Safari.

Kwa upande mwingine, Prof. Safari amevitaka vyombo vya usalama vitekeleze kazi zake kwa uweledi kama ambavyo wanaweza kufanya katika matukio mengine ya kiuhalifu.

Nape Nnauye: Gari Lililotumika Kumshambulia Lissu Limewahi Kuripotiwa Kuwa Linawafuatilia Baadhi ya Wabunge

$
0
0
Dodoma. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ametoa yake ya moyoni na kusema;.

"Mimi hili nalisema hadharani. Hii gari imekuwa ikifuatilia baadhi ya Wabunge hapa, mimi nikiwa mmoja wapo. Tulienda tukaripoti kwamba jamani kuna gari inatufuatiliana hatuelewi ni gari ya nani.

Sasa gari hiyo hiyo, namba hizo hizo, idadi ya watu hao hao, halafu watu wanaripoti hatua hazichukuliwi mpaka mwenzetu anafikia hatua ya kupigwa risasi, mimi nadhani ni jambo kubwa.

Ndo maana nikasema, yeye lisu ambaye Maswahiba yamemfika, sisi wengine tuliambiwa wanatufuatilia na tukathibitisha kwamba kweli wanatufuatilia, lakini yeye yamempata kabisa!..kwa kushambuliwa. Nadhani yeye anaweza kutueleza mengi kabisa. Nina hakika Lissu, dereva wake, wana mengi ya kusimulia juu ya hili.

Kwa kuwa alililalamikia kwa muda mrefu basi nadhani ni vizuri yeye aje atueleze. Ukiacha vyombo vya usalama kuchukua hatua lakini na yeye aje atuambie experience, naamini yale aliyoyasema wakati wa nanii yake na wandishi wa habari hakuyasema yote, aje aseme na mengine ambayo hakuyasema". Ameongeza Nape.


Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe niwatuhumiwa, hama CCM mjomba.

”Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu walipokutana jana kabla ya mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Nape Nnauye jana kabla ya Tundu Lissu kupigwa risasi majira ya saa 7 mchana anadai alikutana naye na kuongea naye katika viwanja vya bunge na baadaye kuja kupata taarifa kuwa amepigwa risasi na watu wasiojulikana.

"Masaa machache kabla ya kushambuliwa kwa risasi jana! Naamini mjomba utarudi utueleze ukweli wa wauaji hawa! Hasa 'the T460CQV' uliyoilalamikia"aliandika Nape Nnauye kweye mitandao yake ya jamii.

Mpaka sasa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yupo nchini Kenya akipatiwa matibabu kufuatia majeraha ambayo ameyapata katika mwili wake

Dogo Janja Atimiza Ndoto yake Kwa Kukutana na Alikiba

$
0
0
Msanii wa Bongo Flava kutoka kundi la Tip Top Connection, Dogo Janja hatimaye amefanikiwa kutimiza moja ya ndoto yake.


Dogo Janja anayehit na ngoma ya ‘Ngarenaro’ amefunguka hayo baada ya kukutana na mkali wa ‘Seduce Me’, Alikiba na kupiga naye picha.

“Alhamdulilah leo nimetimiza ndoto yangu ingine yakupiga picha na alikiba @officialalikiba #Ngarenaro Link In My Bio,” ameandika Jajaro baada ya kukutana na Alikiba jijini Arusha.

Alikiba na Dogo Janja ni moja ya wasanii watakoshambulia jukwaa la muziki la Fiesta linalotarajiwa kuanza rasmi katika Mkoa wa Arusha hapo kesho Jumamosi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kuhusu Tundu Lissu Kupigwa Risasi

$
0
0
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesitushwa na kusikitishwa na kitendo cha Mhe. Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika kupigwa risasi, tukio lililotokea Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.

Tume inalaani vikali kitendo hicho kwani ni kitendo cha uvunjifu mkubwa wa sheria na haki za binadamu.

Tukio hili ambalo limekuja siku chache tu baada ya tukio la ofisi za wanasheria wa IMMMA zilizoko jijini Dar es Salaam kulipuliwa kwa bomu siyo la kawaida, na limeleta hofu siyo kwa familia ya Mhe. Tundu Lissu pekee, bali kwa wananchi wengi nchini.

Isitoshe, matukio haya hayaleti picha nzuri kwa nchi inayoheshimu demokrasia, haki za binadamu na utawala bora.

Hivyo, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora:
1.Inalitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linakamilisha haraka upelelezi wa tukio hilo na kuwapeleka wahusika katika vyombo vya sheria.

Tume inaamini kuwa iwapo wahusika wa tukio hili watachukuliwa hatua kali itasaidia kukomesha vitendo vya aina hii vinavyofanywa na makundi ya watu wanaojichukulia sheria mkononi ambayo yanaonekana kujitokeza hivi karibuni.

2.Aidha, inapenda kukumbusha kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora na kuepuka ukiukwaji wa Katiba na sheria za nchi.

3. Mwisho, inamtakia Mhe. Tundu Lissu kila la kheri katika matibabu yake ili apone haraka.

Imetolewa na:
Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Septemba 8, 2017

Hussein Bashe: Kwanini Tundu Lissu Ameshambuliwa kwa Risasi Mbele ya Nyumba za Mawaziri?

$
0
0
Mbungu wa nzenga mjini ambaye ni miongoni mwa wabunge wanaotikisa sana katika bunge la jamhuri wa muungano wa tanzania katika kutoa hoja madhubuti ndugu Hussein Bashe leo ameomba mwongozo bungeni kuhoji suala la Tundu lissu kuvamiwa


Msikilize hapa

LEMUTUZ Afunguka "Tuaachie Serikali Itoe Majibu ya Nani Anahusika na Shambulio la Lissu Msituchanganye Wananchi"

$
0
0
EXTRA STRAIGHT TALK:- Unaporusha rusha maneno ya kichochezi kuhusu kushambuliwa kwa Mh. Tundu Lissu bakisha maneno na tafuta Facts kwanza ....

naomba nikukumbushe kwa FACTS .....Mauaji ya Waisilamu Mwembe Chai Mwezi May, Mwaka 1998 je Rais hakuwa Magufuli!....Wakati wafuasi wa CUF Pemba wanapigwa mabomu Mwaka 2001 January na kuuliwa wafuasi wao 20 Rais hakuwa Magufuli ....Mwaka 2002 September 2, Muandishi wa Habari Daudi Mwangosi alipouliwa na Bomu Iringa Je Rais hakuwa Magufuli! ....January 5, 2011 Wananchi 3 waliuawa kwa Risasi za Polisi Arusha kuthibiti maandamano yasiyokuwa na kibali vipi Rais hakuwa Magufuli! ....June 28, 2012 Dr. Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana akiwa Leaders Club anapata supu asubuhi je Rais hakuwa Magufuli! ....Mwezi May, 2013 Muandishi wa Habari maarufu Absalom Kibanda alipotekwa na kupigwa vibaya je Rais hakuwa Magufuli....na June/2008 Makamu wa Mwenyekiti Chadema aliyekuwa anataka kugombea Uenyekiti wa chama hicho na kuishia kufariki kwenye ajali ya ajabu Dodoma Rais hakuwa Magufuli ....October, 2013 Mwigamba alipopigwa mpaka kuzimia kwa kudai mahesabu ya Chadema Rais hakuwa Magufuli!


....please msijaribu kupandikiza chuki baina yetu wananchi tutaendelea kuwakumbusha kuwa hakuna ushahidi so far wa nani anahusika na kupigwa kwa Mh. Tundu Lissu ...wote tunamuombea apone haraka ila tutaendelea kupinga hukumu za bila Facts against Serikali ....kuhusu matibabu kwa utaratibu wa Serikali ili Mbunge akatibiwe nje ya nchi na kulipiwa na Serikali ni lazima ithibitishwe na Matabibu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwamba WAMESHINDWA na jana ni FAMILIA YA LISSU ndiyo iliyodai kutaka Lissu akatibiwe nje na sio Madaktari wa Muhimbili kama utaratibu unavyotaka na sababu walisema wanahofia usalama wake ...now Serikali ya Rais Magufuli haina cha kufanya isipokuwa kuwaruhusu familia yake wafanye wanachotaka ....Thanks tutaendelea kuwekana sawa kwa FACTS kuhusu kinachoendelea na some of us tutaendelea kusimamia Ukweli tu ...kushambuliwa kwa Lissu hakumfanyi anyone kuwa na haki ya kuhukumu wengine bila FACTS Taifa ni letu wote so relax guys ...kama hamna FACTS nyamazeni iachieni Serikali ifanye kazi yake STOP THE MADNESS! - le Mutuz

Watu Wasiojulikana...Watajulikana Lini? Haya Ndio Matukio Waliyoyafanya

$
0
0
WATU WASOJULIKANA..
.
#Walimteka na kumng'oa meno kiongozi wa madaktari Ulimboka hawakujulikani,

#Walimteka na kumng'oa jicho kiongozi wa wanahabari Absalom Kibanda hawakujulikana,

#Wamempoteza Bensaanane

#Wakamtolea bastola hadharani na kumtishia Waziri Nape Nnauye hawakujulikana.

#Wakamteka Roma Mkatoliki na wenzake na upelelezi unaendelea,

#Wakalipua Ofisi za kiwakili za Imma Advocates katikatika ya mitaa inayolindwa sana na upelelezi unaendelea,

#Wamempiga risasi 32 mbunge na Kiongozi wa Wanasheria wa Tanganyika pia hawatajulikana na upelelezi utaendelea!

#Jamhuri hii iliyoleta uhuru mwaka 1961,miaka 50 baadaye iko chini ya "watu wasiojulikana"

By Julius S. Mtatiro
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images