Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Hii Hapa Habari Njema Kuhusu Tundu Lissu Akiwa Hospitalini Jioni ya Leo

$
0
0
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jioni hii na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya CHADEMA, Hemedi Ali kutoka Nairobi Kenya ambapo Tundu Lissu amelazwa zinasema kuwa kiongozi huyo ametolewa salama katika chumba cha upasuaji baada ya masaa 7 na kudai upasuaji umefanyika kwa mafanikio.

"Mh Tundu Lissu ametolewa salama katika chumba cha upasuaji baada ya Masaa 7 tangu saa nne asubuhi hadi sasa saa kumi na moja jioni na upasuaji umefanyika kwa mafanikio hivyo yupo 'Executive ICU' kwa uangalizi wa karibu zaidi. Na tunawahakikishia kuwa madaktari wametueleza hakuna tishio lolote kiafya yuko macho na fahamu zote na hii ndio ilikuwa hatua ngumu na Mungu ametupitisha hivyo tuendelee kumuombea apone haraka" aliandika Hemedi Ali

Huu ndio ujumbe wa Ebitoke kwa Ben Pol kwenye birthday yake

$
0
0
Ni vizuri kumuandikia ujumbe mtu wako wa karibu anapokuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ili kumuonyesha jinsi unavyomjali.

Ebitoke ametumia vizuri nafasi hiyo kwa kumwandikia ujumbe muhimu kupitia mtandao wa Instagram, Ben Pol ambaye pia anadaiwa kuwa na mahusiano naye japo yamekuwa na mashaka kwa watu wengine.

“Help me wish my handsome! #HappyBirthday #HappyNewAge 😘😘😘 @iambenpol #Kidume #Bentoke,” ameandika Ebitoke kwenye mtandao huo.

Usiteseke na Jino Linalouma, Tiba Hii Hapa

$
0
0
Meno ni muunganiko wa mfupa wa jino, Fizi na Mishipa. Maranyingi watu wengi huwa pale wanapoumwa na jino wanakimbilia kung’oa jino eti dawa ya jino kuling’oa jambo ambalo si kweli.

Tambua ndugu yangu kuwa unapokwenda kung’oa jino unang’oa Mfupa sio Fizi wala mishipa ambayo hakuna madhara kwa bakteria anaesababisha jino kuuma.

Tambua kuwa kwenye kinywa cha mwanadamu kuna bakteria wanaoishi mdomoni wanaitwa NORMAL FRALER. Bakteria hawa ndio wanaotengeneza ute wenye Acid unaolainisha chakula kwa haraka mdomoni. Na ndio kazi yao.

Lakini wanasababisha ugonjwa unaoitwa GINGIVAITES, ugonjwa huu husababisha fizi kutoa damu haswa unapopiga mswaki, lakini ukiachwa ukawa sugu unasababisha ugonjwa wake kuwa sugu na hujulikana kama MACHODIFECE ugonjwa huu husababisha na hufanya meno kuoza, ama kutoboka kutokana na bakteria AFINOTOBALASAD ndio wanaosababisha na huwa wanaingia ndani kwenye fizi kwa ajili ya kula damu. Hapo ndipo mtu hupatwa na tatizo la  kuumwa na jino au meno.

 Ili kuondoa tatizo hili, ni lazima uwaue hao bakteria na si kong’oa jino kwani wadudu hao walivyo unapong’oa jino moja wao huwa wanahamia jino jingine.

Tiba rahisi ya jino au meno yanayouma bila kung'oa wala kutumia dawa za hospitali tumia mojawapo kati ya hizi hapa:

Tengeneza na kunywa juisi ya bilinganya (Bringal).
Jino linalouma au fizi zilizovimba: Ponda ponda tangawizi mbichi kisha itie chumvi. Weka kwenye jino linalouma au fizi ilipovimba.

Saga majani makavu ya mint kutengeneza unga wake, kisha tia chumvi na weka kwenye jino linalouma.

Saga karafuu kuwa unga. Weka kiasi cha unga huo kwenye jino linalouma. Pia kama una mafuta ya karafuu, chukua nyuzi za pamba (cotton wool) chovya kwenye mafuta hayo na weka wool hiyo kwenye jino linalouma.

Tiba hizi tunazo majumbani kwetu tunamoishi lakini tumekuwa hatujui kuwa ni tiba, badala yake huwa tunakimbilia kung'oa meno yanayouma! CHANGAMKA!

Jinsi ya Kuondoa Weusi Kwenye Magoti na Mikononi

$
0
0
Ngozi nyeusi katika magoti na nyuma ya mikono hutokana na mkusanyiko wa cells zilizokufa, na hata unavyoweka pressure kwenye magoti na vipepsi vya mikono yako. Kama ukiwa unaweka mikono kwenye meza ukiwa kazini, ule msuguano unafanya ngozi iwe nyeusi.

Kama una magoti myeusi na nyuma ya mikono pia ni peiusi, tumia hizi njia asili kuweza kuondoa weusi huo:


Tumia Aloe Vera Juice.

Juice ya Aloe Vera inasaidia kuondoa weusi, all you have to do ni kupaka juice hiyo kwenye sehemu yenye weusi na uache kwa nusu saa kisha nawa na upake moisturizer. Rudia kufanya hivi mara mbili kila siku.


Tumia Binzari Manjano, Asali na Maziwa.

Changanya vyote hivi utapata mchanganiko mzito, paka kwenye magoti na kwenye mikono yako palipo na weusi. Kaa nayo kwa dakika 30, nawa na paka moisturizer. Rudia hii kila siku kwa wiki 3-4, utapata matokeo mazuri.



Tumia Ndimu.

Chukua pamba na uitumie kupaka juice ya ndimu katika sehemu zenye weusi. Au unaweza kuikata tu ndimu na kuipaka directly kwenye sehemu zenye weusi. Kaa nayo kwa lisaa 1 kisha nawa. Rudia hivi kila siku hadi weusi utakapopotea.


Tumia Olive Oil na Sukari.

Changanya vizuri, hii itakuwa kama exfoliation/scrub kwa ajili ya magoti na mikono. Paka katika hizo sehemu zenye weusi kisha kuwa kama una-massage polepole. nawa kwa maji ya uvuguvugu kisha paka moisturizer.

Kutana na Mtabibu wa Nyota Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH...AL_WATWAN MAFUSHO

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH...
 AL_WATWAN MAFUSHO

ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote

..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na AL_WATWAN MAFUSHO Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA).
Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?
Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
AL_WATWAN MAFUSHO Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.
Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA.
 Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.
Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,
HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp +255 759 084 996

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote..

Taarifa Kutoka Ikulu Kuhusu Mazungumzo ya Makinikia

$
0
0
Mazungumzo kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na timu ya kutoka Barrick Gold Corporation yameendelea leo Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yanafanyika kufuatia uchunguzi uliofanywa na tume mbili zilizoundwa na Mhe. Rais Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya dhahabu na kubaini uwepo wa upotevu mkubwa fedha katika biashara ya makinikia ya dhahabu ambayo husafirishwa kwenda nje ya nchi.

Wakati mazungumzo hayo yanaendelea wananchi wanataarifiwa kuwa na subira na watajulishwa mara baada ya mazungumzo hayo kukamilika ama kwa hatua yoyote itakayofikiwa.

Kamati Maalum ya Tanzania inayofanya majadiliano na timu kutoka Barrick Gold Corporation inaongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi.

Hii Hapa Idadi ya Risasi ZilizompatabTundu Lissu Mwilini

$
0
0

Kufuatia tukio lililowashtua wengi jana la Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi, Spika wa Bunge, Job Ndugai (Mb) ametoa taarifa kwa ufupi kuhusu tukio hilo kabla ya kuendelea kwa mkutano wa nane wa Bunge mjini Dodoma.

Akimnukuu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Spika Ndugai amesema kuwa, katika tukio la kushambuliwa kwa Mbunge Tundu Lissu, kati ya risasi 28 hadi 32 zilifyatuliwa katika gari lake.

Kuhusu risasi zilizompata Tundu Lissu, Spika amesema kuwa alilengwa na risasi 5. Kati ya risasi hizo, 1 ilimlenga mkononi, 2 zilimpata tumboni na 2 zikamlenga mguuni.

Baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, amesema kuwa wao kama Bunge tayari walikuwa wameandaa ndege ya kumsafirisha hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu zaidi ambayo ilikuwa uwanjani saa 10 jioni, lakini familia yake ikaomba kwamba apelekwe kutibiwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi.

Akitolea ufafanuzi huo ambao upo nje ya utaratibu wa Bunge, Spika Ndugai alisema kwamba, familia hiyo siyo kwamba hawana imani na hospitali au watalaamu wa Tanzania, lakini walisema wangejisikia faraja kama ndugu yao angetibiwa Nairobi, hivyo wakakubaliana nao.

Kufuatia mabadiliko hayo, ilitafutwa ndege nyingine, ambapo majira ya saa sita za usiku, Tundu Lissu akiwa na mkewe, Daktari Bingwa wa Mkoa wa Dodoma, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, waliondoka Dodoma kuelekea Nairobi kwa ndege ya Flying Doctors ambapo wamewasili salama.

Spika Ndugai amesema kuwa tukio hilo ni la kipekee kuwahi kutokea kwa mbunge kushambuliwa hivyo tena wakati ambapo vikao vya bunge vinaendelea.

Aidha, amewataka wabunge na watu wengine, kutoanza kutoa shutuma kwa upande wowote kwani ni mapema bado, na kuwasihi kuviachia kazi hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vilete ripoti iliyo kamili.

Tundu Lissu alishambuliwa jana mchana alipokuwa akitoka bungeni kwenda nyumbani kwake eneo la Area D Dodoma ambapo risasi zilifyatuliwa kuelekea kwenye gari lake na kumsababishia majeraha kadhaa.

Kingine Ambacho RC Makonda Amekifanya kwa Jeshi la Polisi DSM

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo September 8, 2017 amekabidhi Pikipiki za Traffic 10, Computer 100 na Baiskeli za kisasa 200 kwaajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Polis Dar es Salaam na kulifanya kuwa la kisasa.

Kupatikana kwa vitendeakazi hivyo ni matokeo ya jitiada binafsi za RC Makonda kutafuta Wahisani kwa lengo la kuleta mapinduzi makubwa kwa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ikiwemo magari, pikipiki za kawaida na za Traffic, Baiskeli za doria, silaha na Computer ili kuwarhisishia mazingira mazuri ya kufanyia kazi.




Dunia yapaza Sauti Alichofanyiwa Tundu Lissu

$
0
0
Matamko kutoka sehemu mbalimbali yametolewa kumuombea afya njema mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na kulaani shambulio la risasi dhidi yake na kutaka hatua kali zichukuliwe kwa waliohusika.

Lissu alipigwa risasi juzi akiwa katika gari lake mjini Dodoma na watu wasiojulikana, tukio ambalo limezua mshtuko mkubwa nchini

Spika wa Bunge, Job Ndugai jana alisema kuwa risasi zilizompata Lissu katika mwili wake ni tano; mbili mguuni, mbili tumboni na moja mkononi. Risasi 28 mpaka 32 zilishambulia gari lake.

Matamko hayo yalianza kumiminika juzi jioni wakati Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) kilipolaani kupigwa risasi kwa Lissu ambaye ni rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Rais wa LSK, Isaac Okero alisema tukio hilo limewashtua wanasheria wote wa Kenya.

Naye mwenyekiti wa zamani wa LSK, Eric Mutua ameiomba Serikali ya Kenya kumpa Lissu ulinzi wakati akiwa hospitalini hapo.

“Hatuna uhakika kama watu waliotaka kumuua (Lissu) nchini Tanzania, hawatafikiria kuja hapa kutimiza lengo lao. Ni muhimu kwa Serikali (ya Kenya) kuweka askari watakaomlinda kuhakikisha anakuwa salama,” alisema Mutua.

Marekani yasema ni upuuzi

Taarifa ya ubalozi wa Marekani nchini ilielezea kusikitishwa na tukio la kushambuliwa risasi mbunge huyo ikisema, “Tunalaani kitendo hiki cha kipuuzi na cha kutumia nguvu.”

Ubalozi huo ulisema unaungana na Watanzania kumtakia nafuu ya haraka Lissu ili arejee katika majukumu yake.

Ulaya, THBUB walaani

Ukiacha Wamarekani, Umoja wa Ulaya (EU) ulitoa tamko kulaaani shambulizi hilo na kutaka wahusika wake wasakwe, wakamatwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, EU ilisema inaungana na Serikali ya Tanzania, Bunge na vyama vya kiraia kulaani tukio hilo

“Ujumbe wa Umoja wa Ulaya unaungana na Serikali ya Tanzania, Bunge na taasisi za kiraia kulaani vikali jaribio dhidi ya maisha ya Tundu Antiphas Mughway Lissu,mbunge wa Singida Mashariki wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” inasema taarifa ya EU.

Taarifa hiyo fupi inataka mamlaka ziwafikishe haraka wahusika mbele ya sheria “wale waliohusika katika shambulio hilo lisilokubalika dhidi ya demokrasia”.

Mbali na taasisi hizo, magazeti na vyombo vingine vya habari vya kielektroniki na mitandao duniani, viliripoti habari za shambulio hilo, baadhi vikihusisha na siasa na vingine vikihusisha na kesi zake alizofunguliwa hivi karibuni.

Kwa upande wake, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesema tukio hilo ambalo limetokea siku chache baada ya ofisi za wanasheria wa kampuni ya Immma jijini Dar es Salaam kushambuliwa, limejenga hofu siyo kwa familia ya Lissu pekee, bali kwa wananchi wengi.

“Isitoshe, matukio haya hayaleti picha nzuri kwa nchi inayoheshimu demokrasia, haki za binadamu na utawala bora. Hivyo, tume inalitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linakamilisha haraka upelelezi wa tukio hilo na kuwapeleka wahusika katika vyombo vya sheria,” inasema sehemu ya taarifa ya tume hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wake, Bahame Nyanduga.

Amnesty International

Mbali ya kulaani tukio hilo, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeungana na wengine kuzitaka mamlaka zinazohusika kuithibitishia dunia kuwa shambulio hilo halikuwa na sura ya kisiasa.

Naibu mkurugenzi wa Amnesty wa kanda ya Afrika Mashariki na Maziwa Makuu, Sarah Jackson alisema kushambuliwa kwa Lissu si tu kunatuma ujumbe wa kutaka kuwatisha watetezi wa haki za binadamu, bali pia kunaacha maswali mengi.

“Hili shambulio la kikatili dhidi ya mwanasiasa ambaye aliyeweka nyuma woga, linatia wasiwasi wa hatima ya watu wanaojitoa kwa ajili ya kutetea haki za binadamu. Mamlaka zinazohusika zinapaswa kuwajibika kwa kuueleza ulimwengu kuwa mashambulizi haya hayakufanywa kwa misingi ya kisiasa,” alisema.

Ndugai aeleza Lissu alivyojeruhiwa

Kuhusu shambulio hilo, Spika Ndugai alisema Lissu alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 na 32, huku tano zikimpata mwilini.

Akitoa taarifa ya tukio hilo bungeni mjini Dodoma jana, Ndugai alisema risasi mbili zilimpata kwenye miguu, mbili tumboni na moja mkononi.

Alisema watu wasiofahamika wakiwa kwenye gari aina ya Nissan, walimpiga risasi kisha kutoweka.

“Baada ya tukio hilo watu hao walikimbia,” alisema.

Ndugai alisema Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa kutumia gari la familia ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa kuwa wanaishi jirani.

Alisema ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uliandaa ndege saa 10:30 jioni kwa ajili ya kumpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi. Hata hivyo, baada ya kushauriana na familia na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe waliona ni vyema mgonjwa huo apelekwe  Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi.

“Hivyo kwa kushirikiana na ofisi ya Bunge ilipatikana ndege nyingine ya flying doctors (madaktari wanaofanya kazi popote) na kuondoka na mgonjwa saa 6:00 usiku kuelekea Nairobi,” alisema.

Spika alisema kuwa tukio hilo liliripotiwa polisi ambao waliahidi kufanya msako kuwatafuta watu hao na kwamba Serikali itatoa taarifa kamili kwa kuzingatia utaratibu wa kibunge.

Aliongeza kuwa tukio hilo ni la kwanza la aina yake tangu Bunge lilipohamia Dodoma na kwamba haijawahi kutokea mbunge akashambuliwa kwa risasi.

Alisema ingekuwa mbunge huyo anatakiwa kusafirishwa nje ya nchi, Serikali ina mkataba na Hospitali ya Apollo ya India na kuwa, Lissu alipelekwa Nairobi kwa sababu familia iliomba.

“Kwa nini mwenzetu alipelekwa Nairobi, ni kwa sababu familia iliomba. Nimnukuu mheshimiwa Mbowe kwa niaba yake si kwamba wana shaka na umahiri na uwezo wa madaktari wetu,” alisema  Ndugai.

Pia, aliwataka Watanzania kuendelea kumuombea kiongozi huyo katika kipindi hiki kigumu na kuwawashauri wabunge walioanza kutuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kutumia maneno ya hekima badala ya kuendelea kuzichonganisha pande mbili.

Wabunge wajawa hofu

Wakizungumzia tukio hilo, wabunge wamevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua kuhakikisha kuwa matukio ya aina hiyo yanadhibitiwa.

Mbunge wa viti maalumu (CCM), Ritta Kabati alisema malalamiko yamekuwa mengi na ndio maana Bunge limeona kuna umuhimu wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kukaa na vyombo vya usalama kujua sababu za matukio yasiyoeleweka.

“Mtu kavamiwa unasikia kuwa wanafanya upelelezi halafu baadaye hatupati mwisho wake ni nini? Tukio la Lissu linasikitisha sana. Tukio hili limetuchanganya akili, kumbe hatuko salama sana,” alisema.

“Limetokea katika jengo la mawaziri, naibu spika na wabunge. Huwa tunaamini kuna maaskari (maeneo hayo), lakini nao wamepitwa.”

Mbunge wa Mtwara Mjini (CUF), Maftaha Nachuma alisema tukio hilo limemsikitisha hasa ikizingatia kuwa Dodoma ni makao makuu ya nchi na kwa hiyo Serikali yote iko hapo na Bunge linaendelea na vikao vyake, lakini mbunge akapigwa risasi na watu hawajulikani.

“Kimsingi ni jambo ambalo linatia simanzi sana hasa upande wetu  kama wabunge kwa sababu leo ni kwa Tundu Lissu, kesho mimi keshokutwa kwa mwingine hatuwezi kujua,” alisema.

Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete alisema mshtuko mkubwa alioupata ni kwa sababu katika jamii alitegemea mbunge angekuwa mtu salama zaidi, lakini anashambuliwa na kuhoji kuwa usalama wa wananchi mitaani ukoje.

“Lakini pili niuombe sana umma katika kipindi hiki kizito wawe watulivu kwa sababu haya mambo yanapotokea yanaweza kuwa na sura nyingi na tafsiri nyingi,” alisema.

“Lakini tuviamini vyombo vyetu vitatuletea majibu sahihi ambayo yatatoa  mwanga jinsi gani limetokea, ukweli na kuona tunatokaje kuanza hapa.”

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye alisema Lissu ni miongoni mwa wabunge waliolalamika kufuatiliwa na magari na hadi akataja namba, rangi na idadi ya watu waliokuwa wakimfuatilia, lakini kinachomsikitisha hakuona kama jambo hilo lilipuuzwa.

“Sasa Bunge limepeleka katika kamati, ninaamini baada ya pale hatua zitachukuliwa,” alisema.

“Tusipokomesha, jambo hili linajenga chuki kati ya Watanzania na Serikali yao, kati ya Watanzania na chama kilichounda Serikali, lakini linapeleka sura mbaya duniani.”

Mbowe awatoa hofu wananchi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema Lissu ni mzima, lakini hayuko katika hali nzuri.

Mbowe alisema hafikirii kama wahuni ndiyo waliofanya shambulio hilo kwa kuwa Lissu hana maadui nje ya siasa.

“Tunashuku kuna msukumo wa kisiasa katika shambulio hili, ikizingatiwa silaha nzito iliyotumika na idadi ya risasi zilizofyatuliwa. Ni wazi wahusika walikuwa na nia ya kumuua na sio kumuibia au kuchukua chochote kutoka kwake,” alisema.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema katu wanachama wa chama chake hawataogopa kupaza sauti na wataendelea kupambana kuhakikisha demokrasia inasimama.

Vyombo vya habari kimataifa

Baadhi ya magazeti yaliyoripoti tukio hilo la Lissu ni Independent Times la Uganda, Daily Nation la Kenya, Newyork Times la Marekani na mashirika mbalimbali ya habari.

Imeandikwa na George Njogopa, Elizabeth Edward, Tumaini Msowoya, Sharon Sauwa na Aggrey Omboki

Matukio ya Uvamizi ya Watu Wasiojulikana Ambayo Hayajawahi Kutolewa Majibu

$
0
0
Tukio la kushambuliwa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu limeibua maswali mengi na kukumbusha mengine kama hilo, ambayo uchunguzi wake haujaweza kuwashughulikia wahusika.

Lissu alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 na 32 zilizolenga mlango wa abiria wa gari lake aina ya Toyota Land Cruiser alikokuwa amekaa, huku risasi tano zikipiga mwilini.

Inawezekana kukawa na matukio kadhaa yanayoelekea kufanana na hilo, lakini Mwananchi inaangalia matukio mengine sita yanayohusu kutekwa au kushambuliwa kwa watu maarufu, huku wanaofanya vitendo hivyo wakiendelea kuwa “watu wasiojulikana”.

Watu hao maarufu ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari, Dk Steven Ulimboka; msaidizi wa Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, Ben Saanane; mbunge wa Mtama, Nape Nnauye; mwanamuziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki; mwandishi wa habari Absalom Kibanda na ofisi za kampuni ya mawakili ya Immma ambayo ililipuliwa usiku.

Kutekwa kwa Dk Ulimboka

Juni, 2012 watu wasiojulikana walimteka Dk Ulimboka na kumpeleka katika msitu wa Mabwepande ambako alipigwa hadi kupoteza fahamu.

Aliyekuwa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Namala Mkopi alisema Dk Ulimboka alipigiwa simu na watu ambao walimteka na kumpeleka porini nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambako alipigwa na kupoteza fahamu mpaka wasamaria wema walipomkuta asubuhi siku iliyofuata akiwa katika hali mbaya na kumpeleka kituo cha polisi.

Dk Ulimboka alitekwa saa sita usiku na watu watatu waliodaiwa kuwa na silaha aina ya short gun na bastola. Tukio hilo lilitokea eneo la barabara ya Tunisia, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wa wakati huo, Suleiman Kova katika mkutano wake na waandishi wa habari alisema polisi wameanza uchunguzi wa kina juu ya kutafuta watu waliohusika katika tukio hilo na kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika.

Kamanda Kova alikanusha dhana kwamba tukio hilo limefanywa na wanausalama, huku akitaka raia wema kusaidia katika uchunguzi huo.

Kusisitiza katika hilo, Serikali iliahidi bungeni kuwa ingetoa  kauli juu ya hatua ambazo itazichukua dhidi ya madaktari, baada ya juhudi zote za kumaliza mgomo dhidi ya madaktari kushindikana.

Ahadi hiyo ya Serikali ilitolewa na Waziri Mkuu wa wakati huo, Mizengo Pinda mbele ya Bunge, kufuatia Naibu Spika wa Bunge wakati huo, Job Ndugai kuombwa muongozo na aliyekuwa Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi kuhusiana na mgomo huo wa madaktari.

Hata hivyo, mtu aliyetajwa kuwa ni raia wa Kenya, Joshua Mulundi alikamatwa baada ya kujitokeza na kutangaza kuhusika na tukio hilo na kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu.

Agosti 6, 2012, aliyekuwa Mkurugenzi  wa Mashitaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi  alimfutia kesi ya kujaribu kumuua na kumteka Dk Ulimboka baada ya kuona hana haja kuendelea kumshtaki kwa makosa hayo ambayo yalikuwa hayana dhamana na kisha siku hiyo akamfungulia kesi mpya ya kutoa taarifa za uongo polisi.

Hata hivyo, mahakama ilimkuta na hatia ya kutoa taarifa za uongo na ilimuhukumu kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh1,000.

Mwandishi wa habari wa Redio Times, Chipangula  Nandule  aliyekuwapo mahakamani hapo alijitolea kumlipia faini hiyo ya Sh1,000 na sekunde chache baadaye askari polisi walimkamata Mulundi na askari hao kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini kwa maelezo kuwa wao siyo wasemaji wa jeshi, walisema Mulundi ni raia wa Kenya, hivyo wanamshikilia ili waweze kuandaa taratibu za kumrejesha nchini kwao.

Kupotea kwa Saanane

Novemba mwaka jana kulitokea taarifa za kutoweka kwa  Ben Saanane baada ya chama chacke cha Chadema kutoa tamko rasmi kwamba hawajui alipo msaidizi huyo wa Mbowe.

Tangu kupotea kwa Saanane taarifa kutoka vyombo vya dola zimekuwa zikifanana kuwa ‘wanashughulikia’ kumtafuta.

Saanane alipotea katika mazingira ya kutatanisha na tangu kipindi hicho hadi sasa hajulikani alipo, huku familia yake na baadhi ya viongozi wa Chadema wakihofia kwamba huenda ameuawa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahi kunukuliwa akisema  hana uhakika kama mwanasiasa huyo chipukizi yupo hai ama ametangulia mbele ya haki. Hofu ya Waziri Mkuu na wengine inatokana na ukweli kwamba hakuna taarifa zozote za kiintelejinsia na polisi zinazoonyesha kama yupo hai, kwani hapatikani kwenye simu yake na hata kwenye makundi ya mitandao ya kijamii aliyojiunga.

Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi wa mambo ya nje wa Chadema, John Mrema amewahi kunukuliwa akisema, “…ni wakati wa polisi kutueleza wameshindwa nini kumpata Ben Saanane, mbona mtu akicomment kwenye magroup wanamtafuta na kumpata, kwani wameshindwa kumpata Ben au wanajua alipo?”.

Wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Aprili mwaka huu, Freeman Mbowe alimuuliza Majaliwa kama vyombo vya ndani vya dola vimeshindwa kujua Saanane alipo kwa nini wasiombe ushirikiano kutoka nchi nyingine ikiwamo Uingereza kwa kitengo cha ‘Scotland Yard’ kama Kenya walivyofanya kumsaka kiongozi wa nchi hiyo Robert Ouko aliyefariki dunia, lakini baada ya kuchunguza wakapata taarifa.

Katika majibu yake, Majaliwa alisema uchunguzi wa suala la kutoweka kwa Saanane hauna kikomo na mara utakapokamilika Serikali itatoa taarifa yake.

Nape atishiwa bastola

Machi 23, 2017 aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alitishiwa bastola na mtu aliyeelezwa anatoka katika vyombo vya dola akiwa hajavaa sare yoyote, alipokuwa akijaribu kumzuia asizungumze na waandishi wa habari nje ya hoteli ya Protea, Dar es Salaam.

Nape alilazimika kuzungumza na waandishi akiwa amesimama juu ya gari nje ya ukumbi wa hoteli hiyo baada ya polisi kutaka kuuzuia mkutano huo usifanyike.

Hata hivyo, waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alisema kitendo cha askari  kuchomoa bastola hakikubaliki na alimwagiza mkuu wa jeshi la polisi kutumia picha zilizopigwa wakati wa tukio hilo kumsaka mhusika.

“Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni Mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana rekodi ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea bastola sio cha kiaskari, sio cha Kitanzania na sio cha kiMungu, kama mtu ameweza kutoa bastola mbele ya kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoroni angefanya nini,” aliandika Mwigulu kwenye ukurasa wake wa twitter.

“Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.”

Hata hivyo, hadi sasa hakuna majibu ya kujitosheleza kuhusu mtu aliyemchomolea bastola Nape.

Roma Mkatoliki atekwa

Aprili 2017, wasanii wa hip hop, Ibrahim Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki, Monii Central Zone, Bin Laden na Imma ambaye ni mfanyakazi wa mama mzazi wa mmiliki wa studio za Tongwe Records iliyopo Masaki, Dar es Salaam, J Murder walitekwa na watu wasiojulikana  baada ya kuvamiwa.

Uvamizi huo ambao ulizua taharuki, ulidaiwa kufanyika saa 1:30 usiku. Kukamatwa kwa wasanii hao kulitafsiriwa kuwa ni mwendelezo wa tukio lililomkuta msanii Emanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego, ambaye alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro na kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam kabla hajaachiwa kwa amri ya Rais John Magufuli.

Ingawa haikujulikana sababu za kutekwa Roma na wenzake, pia watekaji hawajafahamika mpaka sasa.

Tukio hilo lilimsukuma Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Chadema) kuomba mwongozo wa Spika katika mkutano wa Bunge uliopita.

Kutokana na ombi hilo, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliiagiza Serikali kuchukua hatua haraka ili kufahamu ukweli wa suala hilo na kulipatia ufumbuzi.

Katika majibu yake, Ndugai alisema: “Katika hili niseme tu Serikali ilifuatilie haraka na kulipatia ufumbuzi maana siwezi kutoa ufafanuzi zaidi, maana ndio ninalisikia hapa kwako kwa mara ya kwanza.”

Hadi sasa bado hakuna majibu ya kina kuhusu tukio hilo.

Kibanda aumizwa vibaya

Machi, 2013 mwandishi wa habari ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda alinusurika kifo baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake kisha kupigwa na kujeruhiwa vibaya.

Kibanda alipigwa na kitu kizito chenye ncha kali kichwani, kutobolewa jicho la kushoto na kung’olewa ukucha wa kidole cha mkono na meno.

Katika tukio la Kibanda, inaelezwa kuwa watuhumiwa hao ambao hawajakamatwa walimtendea unyama huo akiwa anakaribia kuingia nyumbani kwake eneo la Mbezi Beach usiku wa saa sita akiwa ndani ya gari akingojea kufunguliwa geti.

Kibanda alisema kuwa akiwa amesimama langoni ghafla alishtukia gari lake likivunjwa kioo na katika harakati za kutaka kutambua nini kinaendelea, alivamiwa na watu hao.

Baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam liliwataka waandishi wa habari kushirikiana katika kutoa taarifa ya uchunguzi ya wahalifu waliomteka na kumjeruhi Kibanda.

Aliyekuwa kamanda wa kanda hiyo, Kova alisema kuwa ni mapema kuwabaini waliohusika katika tukio hilo. Kova alisema Kibanda ndiye anafaa kuwa shahidi wa kwanza katika tukio hilo wa kusema kilichotokea lakini kutokana na hali yake hawezi kuhojiwa hadi apate ahueni.

Kova alisema tukio hilo ni kubwa na Jeshi la Polisi Makao Makuu lilitoa askari wanne ambao wangeungana na wale wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ambao wamebobea katika uchunguzi. Hata hivyo, hadi sasa watuhumiwa wa tukio hilo la Kibanda bado hawajafahamika wala kukamatwa.

Ofisi za Immma zalipuliwa

Agosti mwaka huu ofisi za uwakili za Kampuni ya Immma Advocates zilizo chini ya wanasheria Fatuma Karume na wenzake zimechomwa moto na watu wasiojulikana na hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Profesa Safari azungumza

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari ameitaka Serikali kuchukulia mambo hayo kwa uzito wake yanapotokea, hususan yanayohusu usalama wa raia.

Nipo Tayari Kumuoa Brown Wangu- Wolper

$
0
0
Nipo Tayari Kumuoa Brown Wangu- Wolper
TOFAUTI na mila na desturi za Kiafrika kwa mwanaume kumuoa mwanamke, mrembo Jacqueline Wolper amevunja ukimya kwa kusema, yuko tayari kumuoa ‘benten’ wake anayejulikana kwa jina la Brown.

Wolper alisema Wabongo wengi wamezoea kuona mwanaume ndiyo anatoa mahari na kuoa jambo ambalo kwake anaona ni utaratibu na uamuzi tu, si dhambi mwanamke kumlipia mahari mwanaume.

“Unajua watu wengi wanachukulia mahari ni lazima atoe mwanaume kitu ambacho siyo sahihi kabisa maana hata India siku zote mwanamke ndiyo anatoa mahari na mimi nataka kuanzisha hivyo Bongo.

Wolper.
“Najua katika hili, watu wengi wataanza manenomaneno kuwa mimi ndiyo nimeoa lakini sitajali,” alisema Wolper.

Staa huyo aliendelea kutiririka kuwa, kwenye maisha yake anapenda kuwa na furaha na kwa kuwa Brown anampa furaha ya kweli, atamlipia mahari ili kukamilisha furaha yake.

“Ninapokuwa na Brown, nakuwa na furaha sana, moyo wangu pia unajaa amani hivyo basi nahitaji kuona furaha hiyo inaendelea ndani ya moyo wangu ndiyo maana nahitaji kuwa naye muda mrefu, nimtolee mahari, tuishi na hata tuzae watoto ndiyo kitu kikubwa ninachokihitaji,” alisema Wolper.


Kimbunga Irma Chawasili Cuba

$
0
0
Kimbunga Irma Chawasili Cuba
Kimbunga hicho ambacho kimeendelea kuimarika saa chace zilizopita kinatarajiwa kuathiri miji ya pwani. Kifikia sasa watu ishirini wamerikpotiwa kufariki katika visiwa vya Carebean.

Msemaji wa kituo cha kushughulikia majanga, nchini Marekani,amesema kimbunga hicho huenda kika-muangamiza mtu yeyeyote ambaye hatajiepusha nacho.
Kumeshuhudiwa msongamano mkubwa wa magari na upungufu wa petroli, wakaazi wa Florida wakielekea maeneo ya kaskazini.

Wakati huo huo kimbunga Ema kinachoendelea kusonga kwa kasi,sasa kimeingia nchini Cuba.
Kimbunga hicho, kinaandamana na upepo mkali na mvua kubwa kuelekea visiwa vya kaskazi mwa Caribbean.

Bahamas hata hivyo imenusurika na kimbunga hicho baada ya upepo kubadilisha mkondo. Visiwa vya mashariki vilivyokuwa vimekumbwa na
mafuriko makubwa sasa ya yanakabiliwa na tishio la kugongwa na kimbunga kingine.
Shughuli ya kuwaondoa watu katika kisiwa cha Barbuda ilikamilika.

Ben Pol Afunguka Sababu ya Kutoa Albam Kimya Kimya Bila Promo

$
0
0
Ben Pol Afunguka Sababu ya Kutoa Albam Kimya Kimya Bila Promo
Msanii Ben Pol ametoa sababu ya kutoa albam yake kimya kimya bila promo yoyote na kusema kwamba amefanya hivyo ili kuipa nafasi kazi yake mpya aliyofanya na msanii Chidinma kutoka Nigeria inayoitwa 'Kidume'.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Ben Pol amesema ameamua kuacha kufanya hivyo ili watu wasifikirie kuhusu albam tu na waipe nafasi kubwa zaidi 'kidume', ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki, lakini hata hivyo atatoa taarifa namna gani mashabiki wake wanaweza kuipata albam yake mpya.

"Kwa sababu nilitaka focus zaidi iwe kwenye wimbo mpya Kidume, halafu kuanzia wiki ijayo nitaanza kuongelea album na sehemu inakopatikana", alisema Ben Pol.
Albam hiyo imebeba nyimbo  15 ambazo zilishatoka miaka ya nyuma na kufanya vizuri, imetoka kipindi ambacho watu walikuwa na kiu na Albam mpya ya Ben Pol ambayo alishawahi kuwaambia mashabiki kwamba atatoa albam mpya atakayoipa jina la mtoto wake, lakini imekuwa tofauti na kutoa albam yenye mjumuiko wa kazi zake za awali na mpya.

Mnada wa Magorofa ya Lugumi Kufanyika Leo

$
0
0
Mnada wa Magorofa ya Lugumi Kufanyika Leo
KAMPUNI ya Udalali ya Yono leo Septemba 9, 2017 itapiga mnada maghorofa yanayomilikiwa na kampuni ya Lugumi. Maghorofa hayo mawili yapo maeneo tofauti moja likiwa Mtaa wa Mazengo Upanga na lingine likiwa Mbweni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Yono, Scolastica Kevela amesema leo Ijumaa kuwa wametumia njia mbalimbali ili kufanikisha mnada huo kufanyika hasa kwa kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Amesema hawezi kutaja gharama halisi ya mali hizo na deni ambalo kampuni hiyo inadaiwa na Mamlaka ya Mapato(TRA) hivyo hao ndio wanaoweza kutoa majibu hayo.

“Kazi yetu sisi ni kupiga mnada tu, gharama ya deni na thamani ya mali hizo TRA ndio wanatakiwa kutolea majibu,” alisema Kevela.
Alisema fedha watakazozipata zitakwenda kusaidia nchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.



Simba na Azam Uso kwa Uso Leo Chamanzi

$
0
0
Simba na Azam Uso kwa Uso Leo Chamanzi
Michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi leo Jumamosi kwa kucheza mechi mbili na Jumapili mechi sita katika mzunguko wa pili baada ya kusimama kwa muda wa wiki moja.

Kwa mujibu wa ratiba mpya iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) chini ya Rais Wallace Karia, timu ya Tanzania Prison FC yenye makao yake makuu Mkoani Mbeya itakuwa katika kiwanja chake cha nyumbani Sokoine ikawakaribisha wapinzani wake Majimaji FC ya kutokea Songea majira ya saa 10:00 jioni huku Azam FC ikimkaribisha wekundu wa Msimbazi (Simba SC) katika kiwanja chake cha Azam Complex kilichopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar e Salaam saa 10:00 jioni.

Siku ya Jumapili timu ya Njombe Mji FC itawakaribisha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga katika kiwanja chao cha nyumbani Sabasaba, Mtibwa Sugar FC yenyewe watakichapa na Mwadui FC katika uwanja wa Manungu uliopo Morogoro, Lipuli FC itacheza dhidi ya Stand United FC katika kiwanja cha Samora mjini Iringa. Mechi zote hizi zitachezwa majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

Vile vile Singida United FC watashuka katika dimba la Jamhuri mkoni Dodoma kuzichapa na wakata Mbao wa Mwanza (Mbao FC), Kagera Sugar FC ikicheza katika uwanja wao wa Kaitaba uliopo mjini Kagera dhidi ya Ruvu Shooting FC huku ratiba kwa siku hiyo ikifungwa na timu ya Mbeya FC ikicheza na Ndanda FC katika dimba la Sokoine mkoani Mbeya ambapo kwa mujibu wa ratiba ya Ligi kuu timu zote hizi zitacheza saa 10:00 jioni.

Kwa upande wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka hivi sasa timu ya Simba ina pointi tatu ikifuatiwa na Tanzania Prisons, Mwadui, Azam FC, Mtibwa Sugar, Mbeya City pamoja Mbao FC zote zikiwa zinapointi sawa tatu huku Mabingwa watetezi Yanga wakiwa na alama moja na Lipuli FC.



Kiualisia Ndoto Yangu Kuwa na Watoto 12 Kwasababu Watoto Wanaufurahisha Moyo Wangu- Mongella

$
0
0
Kiualisia Ndoto Yangu Kuwa na Watoto 12 Kwasababu Watoto Wanaufurahisha Moyo Wangu- Mongella
Rais wa kwanza wa Bunge la Afrika na mwanaharakati wa haki za wanawake nchini,  Balozi Getrude Mongella amesema moja ya ndoto zake ilikuwa ni kupata watoto 12.

Akitoa simulizi ya namna alivyofanikiwa kutimiza ndoto zake katika tamasha la Jinsia la 4, lililofanyika kwenye viwanja Mtandao wa Jinsia Tanzania, Mongella amesema  ‘’kiuhalisia napenda watoto kwa sababu  wanaufurahisha moyo wangu’’.

Amesema  uzazi wa oparesheni ndiyo uliomfanya ashindwe kutimiza ndoto hiyo hata hivyo alipata watoto watatu.

Amewaambia wanachama wa TGNP waliokuwa wanamsikiliza kwa hamu kuwa mafanikio yake

kisiasa yanatokana na malezi mazuri ya wazazi wake.

“Baba yangu alipenda kuona natimiza ndoto zangu, alinisapoti  kila hatua na nilipokuwa nafanya mikutano alikuwa  ananisikiliza na kunipongeza ninapofanya vizuri,”anasema

Siri ya mafanikio ni kujiamini, kujituma na kuthubutu.“Hata kama roho inauma, nilijipa ujasiri nikathubutu,”anasema.

Mr. Chuz Atoa Siku 14 kwa Chama cha Waigizaji Kumuomba Radhi

$
0
0
Mr. Chuz Atoa Siku 14 kwa Chama cha Waigizaji Kumuomba Radhi
MKONGWE wa filamu Bongo anayewika na Tamthilia ya Closed Chapter, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’ ametoa siku 14 kuombwa radhi na Chama Cha Waigizaji Tanzania kutokana na kuchafuliwa kuwatumia kingono wasanii wa kike, wenye tamaa ya kuchomoka kisanaa.
Akizungumza na Ijumaa, Chuz aliyewika na Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu alisema kuwa, anasikitishwa na chama hicho kikubwa kutoa tamko kwenye vyombo vya habari kwa jambo la wazi lililo pangwa na genge la watu wachache.

“Nawapeleka mahakamani wale wasichana na mvulana alierekodi sauti ya kunichafua kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, tayari mwanasheria wangu ameshakamilisha taratibu zote na muda wowote kuanzia sasa nitawafikisha mahakamani.
“Najua ni njama zilipangwa kunichafua na siku chache baadae baadhi yao walinieleza mipango yao ililenga nini na aliepanga mpango huo wamemtaja tena kwa ushahidi wa sauti, lakini pia nakipa Siku kumi na nne chama cha waigizaji taifa kiniombe radhi kwa ushiriki wao wa kunichafua,” alisema Chuz.

Mr. Chuz.
Ijumaa lilimtafuta kiongozi wa tume iliyounda kutoka chama hicho ambaye pia ni msanii wa filamu, Michael Sangu ‘Mike’ na alipopatikana alisema;
“Nilikuwa mwenyekiti tu wa kamati iliyoundwa kumhoji Chuz, watuhumiwa kipindi hicho walikuwa wawili, Jumanne Mshindo (aliyerekodi video chafu) na Chuz. Tulishindwa kumfikia kwa kuwa alikuwa Lushoto huko Tanga, kama ameamua kwenda mahakamani ataushtaki umoja wa filamu siyo mimi.”
Hivi karibuni, Chuz alikwaa skendo ya kutoka kimapenzi na wasanii wake ambapo sauti ilisambaa ikieleza jinsi anavyowadhalilisha wasanii wa kike ambao wanakataa kutoka naye.

Mrembo Huyo Amweka Matatani Ben Kinyaiya Baada ya Kuvujisha Video Wakifanya Yao Kitandani

$
0
0
MTANGAZAJI maarufu Bongo, Benny Kinyaiya ameingia kwenye kashfa nzito baada ya video yake akiwa anapapasana kimahaba na mrembo wa Bongo Muvi, Suzan Michael ‘Prettykind’ kuvuja na kuzua mshangao.

Chanzo makini kilieleza kuwa video hiyo ya Benny na mrembo huyo walijirekodi kwa ajili ya mahaba yao lakini mrembo huyo aliamua kumfanyia kitu mbaya kwa kuivujisha mitandaoni na kusababisha ugomvi mkubwa kwenye familia ya mtangazaji huyo.

“Yaani unaambiwa Benny na mwanamke wake hapakaliki ndani maana mke aliiona ile video kwenye mitandao ya kijamii na kucharuka hatari,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya kupata ubuyu huo, Ijumaa lilimtafuta Benny ambaye alionyesha kusikitishwa na kitendo hicho na kusema inawezekana mrembo huyo ndiye aliyevujisha ila bado yupo kwenye kulifanyia uchunguzi suala hilo.

“Kiukweli hata sielewi imekuwaje, niko nafanya uchunguzi wa kina nijue ni nani aliyevujisha hiyo video, kwa sasa siwezi kusema ilikuwa ni wapi ngoja maana jambo hili limenichanganya,” alisema Benny.

Kwa upande wa mrembo huyo alipotafutwa na gazeti hili alisema hajui aliyeisambaza video hiyo ila hana uhusiano na mtangazaji huyo.

Alipobanwa imekuwaje kujiachia akiwa na kanga moja na mtangazaji huyo kitandani, mrembo huyo alijiumauma kabla ya kukata simu

SOMA Nafasi Mbali Mbali za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumamosi

$
0
0

Taarifa Rasmi ya Uchunguzi wa Mzigo wa Almasi Uliokamatwa Julius Nyerere International Airport

$
0
0
Jeshi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa linashikilia watu wanne kwa kushukiwa kutaka kusafirisha madini aina ya almasi yenye thamani ya shilingi bilioni 32.8 bila kufanyiwa ukokotoaji sahihi.

Zoezi hilo limefanikiwa kwa ushirikiano wa wizara ya nishati na madini, mamlaka ya mapato na vyombo vingine vya ulinzi na sasa mzigo yatafanyika mahesabu tena Kujua thamani halisi ya Madini hayo)

Baada ya taarifa hizi Serikali iliamua kuunda timu ya Uchunguzi na hii ndio taarifa ya uchunguzi huo ikiwasilishwa na Prof. Mruma tena kwa Waziri wa Fedha


Nimeikuta inaendelea katika television ya tbc 1:
Professor Mruma anatoa taarifa hiyo kwa Waziri wa Mipango na Fedha Dk. Mpango
Fuatilia matangazo hayo ya moja kwa moja.


UPDATES:

Dk Mpango;-Zilibaki dk 5 ndege inyanyuke.
Wezi waliriport karate 71,840=kg 14.03
= $ M.14,798,936.61 kumbe zilikuwa kg29
$ 29,509821.84 pungufu $14,710,885.23
= sh. Bil. 32.7. Stahili yetu ilikuwa mrabaha $882653.11 Ada $147108.85 =$1,029,796 = sh. Bilioni 2.3 ambazo tungepoteza katika mzigo huu tu.
Inakadiriwa kila mwaka husafirishwa karate 230,000 karate1=$200

TAZAMA HAPA:

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images