Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Imefichuka Sehemu Alipo Dereva wa Tundu Lissu...Hayupo Tanzania..Mbowe Ataja Alipo

$
0
0
Mwenyekiti wa (CHADEMA) Freeman Mbowe amefunguka na kuweka wazi sehemu alipo dereva wa Tundu Lissu ndugu Simon Mohamed Bakari na kusema kwa sasa yupo nchini Kenya akipatiwa huduma za kisaikolojia kufuatia kushuhudia tukio hilo la kinyama.

Mbowe amesema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo ameweza kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu sakata hilo na kusema kuwa waliona ni busara kumchukua dereva huyo na kuwa naye nchini Kenya kwa ajili ya kupatiwa msaada huo hadi watakapooona hali yake ya kiafya na uhakika na usalama wake ndiyo anaweza kurejea nchini Tanzania.

"Dereva wa Mhe. Lissu, Simon Mohamed Bakari naye tunaye hapa Nairobi akiendelea kupata huduma za kisaikolojia. Alishuhudia shambulio lile na aliokoka kimiujiza. Anasumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo. Naye hatukuona busara kuendelea kumwacha nchini hadi hapo hali yake ya kiafya na kiusalama itakapohakikishwa. Ni dhahiri kwa aina ya shambulio lilivyokuwa, wauaji walikusudia kuwauwa wote, Mhe. Lissu na hata Dereva wake" alisema Freeman Mbowe

Mbali na hilo Mbowe amewataka wabunge wa upinzani kuwa na tahadhari kubwa akidai kuwa kama wasipokuwa makini huenda kiongozi mwingine anaweza kupata matatizo kama hayo hata hivyo amesema kuwa tamko la chama chake litakuja karibuni.

"Tutamuenzi Baba wa Taifa aliyetuasa: “tukiwa waoga tutatawaliwa ma madikteta!” Wabunge na Viongozi wa Upinzani ndiyo “Target”. Nawasihi viongozi na wabunge wetu wachukue kila tahadhari. Wanachama nao wawe tayari kulinda na kupigania wajibu wetu, usalama wa viongozi na chama chetu kwa ujasiri. Tusipochukua hatua, kesho atadhurika mwingine!Tamko na agizo rasmi la Chama litafuata karibuni" alisema Freeman Mbowe.

Freman Mbowe amedai kuwa Tanzania si sehemu salama tangu umefanyika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 na kudai kuanzia hapo yalianza kujitokeza kwa mauaji ya viongozi kikiwepo kifo cha Mhe. Alphonce Mawazo Mkoani Geita, Kupotea kwa kina Ben Saanane. Kutekwa  wasanii na kufanyiwa mateso makubwa pamoja na Wabunge kufungwa na kushtakiwa kila siku.

Gwaji Boy Sio wa Mchezo Kabisa..Aaamua Kumfungia Safari Tundu Lissu Kenya

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameahidi kesho Septemba 11, 2017 kwenda jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kumuona Mbunge wa Singida Mashariki na kumfanyia maombi ili aweze kupona kwa haraka na kurudia katika hali yake ya zamani.

Gwajima amesema hayo leo alipokuwa kwenye kanisa lake la Ufufuo na uzima na kudai kwa wale ambao wanachukia au watakuwa hawajapenda kwa maamuzi hayo aliyofanya amewapa pole na kuwaambia atakwenda na kumuombea Mbunge huyo ili apone.

"Kesho mimi nitakwenda kumuona Tundu Lissu, nasema nitakwenda kumuona kama kuna kitu kinakuudhi shauri yako, nitakwenda na nitamuombea tena huko huko apone haraka na kurudi akiwa na nguvu zaidi, tumuombee mtu wa Mungu na mtu aliyerusha risasi kwa Lissu ajue kuwa zitarudi kwake pia" alisema Gwajima

Aidha Mchungaji Gwajima amesema kuwa huu si wakati wa kutoa lawama zozote kwa jeshi la polisi waachwe ili wafanya kazi yao na kudai kuwa wakiweza kuwapata au kutowapata hao waliofanya shambulio hilo basi watakuja kuongea baadaye.

"Mimi nilikuwa nje ya nchi kwa siku zaidi ya 80 hivyo mtandao wangu haujakaa sawa ila nasema hivi nitawajua, Kwenye hatua hii hatuwalaumu polisi, ila wakiwapata au kutompata hao watu hapo ndipo tutakuja kuogea baadaye" alisema Gwajima

Mbali na hilo Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA Said Kubenea naye amesema kesho atakwenda nchini Kenya kwenda kumuoona Tundu Lissu na kusema licha ya kuwa ni mbunge mwenzake lakini pia ni rafiki yake wa karibu.

Zitto Kabwe Acharuka Baada ya Kuulizwa Kuhusu Kauli yake ya Ben Saanane Kutaka Kumuwekea Sumu

$
0
0
Mtumiaji mmoja wa Twitter anajiita @moringesokoine1 alimuuliza hivi "@zittokabwe Unakumbuka Tarehe 27/03/2013 Ulidai Mjumbe Wa Bavicha Ben Saanane Alitumwa Kukuwekea Sumu Kwenye Kinywaji Lunch Time Hotel?"

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa twitter ameweka wazi msimamo wake huo wa kutoyumbishwa na watu hao ambao wameanza kusambaza taarifa mbalimbali kuhusu Zitto Kabwe na kusema hizo ni ajenda wanazofanya kutaka kumtoa kwenye mstari wa sakata kuhusu wahusika halisi ambao wamefanya shambulio la risasi kwa mbunge Lissu

"Hizi ni propaganda za dola ili kuhamisha mjadala kuhusu wahusika halisi wa shambulio la risasi dhidi ya Mbunge Tundu Lissu. Sitawapa muda" alisisitiza Zitto Kabwe

Taarifa ya Mwana FA na AY Kuzuiwa Kuingia Katika Matamasha ya TIGO Fiesta, Ruge na Tigo Wafunguka

$
0
0
Waandaaji wa Fiesta, Kampuni ya Clouds Media Group wamesema hakuna mtu aliyezuiwa kuingia katika tamasha hilo.

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds, Ruge Mutahaba amesema wao wanafanya biashara hivyo hawawezi kuzuia mtu kuingia kwenye tamasha hilo.

Fiesta kwa msimu huu ilizinduliwa jana Jumamosi jijini Arusha. Tamasha hilo linafanyika kwa mwaka wa 18 na limekuwa likiwashirikisha wasanii wa ndani na kimataifa.

Ruge ametoa kauli hiyo alipotakiwa na Mwananchi kuzungumzia tweet ya mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA. Akim-tag rafiki yake, kupitia ukurasa wake wa Twitter, MwanaFA aliandika: “Unapogundua sio tu huruhusiwi kuperfom bali hata kwenda kuangalia burudani kwenye tamasha lolote linalohusisha ile kampuni @AyaTanzania.”

Baadaye aliandika tena: “Kwa hiyo haturuhusiwi mpaka tusamehe bilioni 2.2 taslimu fedha za kiTanzania? bro, tumekwisha.”

Tamasha la Fiesta msimu huu linadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, ambayo nayo imesema hakuna aliyezuiwa.

“Hakuna anayezuiwa kuingia kwenye tamasha. Hatukumzuia yeyote mwenye tiketi kuingia tamashani,” amesema Woinde Shisael, meneja mawasiliano wa Kampuni ya Tigo.

Taarifa zilizopo zinasema msanii huyo hakuzuiwa kama habari zinavyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Inaelezwa akiwa ameambatana na watu waliokuwa na mwaliko wa kukaa eneo lililotengwa kwa ajili ya watu mashuhuri (VIP) yeye alizuiwa kwa kuwa hakuwa amealikwa.

MwanaFA na msanii mwenzake Ambwene Yesaya maarufu AY wamefungua kesi mahakamani ikihusisha kampuni ya Tigo wakitaka kulipwa fidia ya Sh2.1 bilioni kwa kukiukwa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, kwa kutumia kazi zao (nyimbo) kama miito ya simu bila ridhaa wala makubaliano nao.

UVCCM Wawajibu Vijana wa CHADEMA Kuhusu Tundu Lissu...Wawataka Waache Viherehere

$
0
0
Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM kupitia Kaimu Katibu Mkuu, Shaka Hamdu amewataka BAVICHA kuacha tabia ya kiherehere ya kuingilia taratibu za kitawala na kipelelezi pindi yanapotokea masuala mazito yanayohusisha moja kwa moja maisha ya watu

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu akiwa pamoja na Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana UVCCM taifa.

Shaka amebainisha hayo leo ikiwa imepita siku moja tokea Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Patrobas Katambi, alipotoa kauli yake ya kuwataka viongozi wote wa vijana wa chama hicho kushughulika na watu wanaoitwa 'wasiojulikana' ili waweze kutokomeza matukio ya kihalifu ambapo amedai pengine watu hao wananguvu kuliko vyombo vya dola na kuahidi endapo litashindikana jambo hilo basi atajiudhulu wadhfa aliokuwa nao katika chama chake.

"Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM tunawakanya BAVICHA na kuwataka waache tabia ya viherehere ya kuingilia taratibu za kitawala na upelelezi pindi yanapotokea masuala mazito yanayohusisha maisha ya watu, kushambuliwa au kutekwa na wao wakataka kuyageuza kuwa ya kisiasa. BAVICHA wamejaribu kuyaunganisha matukio kadhaa walioyaita yamefanywa na watu wasiojulikana bila ya kufanya upelelezi wa aina yeyote na kutaja baadhi ya majina ya watu waliyokumbwa kwenye matukio hayo na kukwepa kutaja mfululizo wa mauaji ya viongozi wa CCM na serikali huko Kibiti mkoani Pwani", amesema Shaka.

Pamoja na hayo, Shaka amesema kwa mara ya kwanza UVCCM umemuunga mkono Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe kwa kutoa matamshi ya kuwataka wananchi kutoonyesheana vidole juu ya tukio lililotokea huku akivitaka vyombo vya dola kuwajibika ipasavyo ili kubaini aliyetenda tukio hilo la kiuhalifu.

"Mbowe ametamka matamshi yaliyopevuka kifikra na kisiasa tofauti na povu lilivyo watoka vijana wake na kuonyesha uchanga katika siasa huku wakilitumia tukio la Lissu lenye huzuni kama jukwaa lao la kisisasa", amesisitiza Shaka.

Kwa upande mwingine, Shaka amewataka vijana wote Watanzania na wana CCM kumuombea dua Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa yaliyomkuta ili aweze kupona na kurudi kuendelea na kushirikiana na Watanzania wenzake katika kulijenga taifa la Tanzania.

Ushahidi Huu Hapa Mungu Amekataza Mapenzi Kinyume na Maumbile

$
0
0
Kitabu cha Biblia kinaeleza waziwazi huu uchafu unaofanywa na binadamu kama matendo ya ushoga,kutembea na binamu yako pamoja na wake za watu,kupitia vifungu vifuatavyo :

USHOGA NA ULAJI TIGO MAMBO YA WALAWI 20:13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume,kama alalavyo na mtu mke,wote wamefanya machukizo hakika watauwawa

KUTEMBEA NA MKE/MUME WA MTU MAMBO YA WALAWI 20:10 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine,na mwanamke aziniye na mtu mume hakika watauwawa

NA WALE MNAOKULA KUKU NA MAYAI YAKE [MAMA NA MWANA] MAMBO YA WALAWI 20:12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauwawa,Tena mtu mume akimuoa mke pamoja na mama yake ni uovu mkuu

WALE WANAOTEMBEA NA WANYAMA MAMBO YA WALAWI 20:15 Tena mtu mume akilala na mnyama, na mwanamke akimkaribia mnyama yeyote na kulala pamoja naye,mtamwua huyo mwanamke

KUTEMBEA NA BINAMU YAKO MAMBO YA WALAWI 20:19 Usifunue utupu wa umbu la mama yako wala umbu la baba yako

Tunakumbushana tuu Jamani

By Eddy Love

Ukiona Mwanaume Ana Miaka 27 Bado Hajajitegemea Huyu ni Hasara

$
0
0
Sifa ya mwanaume kujituma, kutafuta pesa na kujipanga. Hivi unakuta kijana umri unaenda bado anategemea kwa wazazi msosi ni hotpot family huyu ni hasara.

Kuna mwanaume mpaka anaoa bado yupo kwa wazazi na mke anampeleka hapo hapo kwenye nyumba ya familia, ndiyo hapo ndoa inakua ngumu kwa mawifi na mashemeji na wazazi zinaanza chokochoko kibao. Wanaume wa hivi ni walaini sana, hadi kitandani ni walaini.

Wapo sana wanaume wa hivi ila kiukweli mwanamke anavutiwa na mwanaume mgumu yaani anayejua kuhangaika na kujitegemea. Hawa wanategemea hadi siku ya ndoa wapewe zawadi ya kiwanja, au nyumba na wazazi. Wanataka sofa, kitanda, vyombo vya ndani siku ya harusi.

Shosti ukiona mwanaume wa hivi shituka mapema ni mwanaume Hotpot Family....

Kutana na Mtabibu wa Nyota Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH...AL_WATWAN MAFUSHO

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH...
 AL_WATWAN MAFUSHO

ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote

..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na AL_WATWAN MAFUSHO Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA).
Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?
Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
AL_WATWAN MAFUSHO Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.
Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA.
 Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.
Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,
HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp +255 759 084 996

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote..

VIDEO: Kwanini Dereva wa Tundu Lissu Akimbizwe Nairobi Kabla ya Kuhojiwa?

$
0
0
Mheshimiwa Mbowe anasema eti dereva ameenda Nairobi kwa ajili ya kuwekwa sawa kisaikolojia. Kwa nini asingeojiwa kwanza ndio akaenda huko Nairobi. Kulikuwa kuna uharaka gani wakati yeye alikuwa mzima kabisa? Je hao wanasaikolojia hapa hawapo mpaka Nairobi? Au kwa usalama wake nae kama Lissu? Najaribu kuwaza tu wadau

VIDEO:

Kaka Aliniambia Kuhusu Gari Linalomfuatilia - Mdogo Wake Tundu Lissu Afunguka

$
0
0

Vincent, mdogo wake Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kabla ya kaka yake kushambuliwa kwa kupigwa risasi aliwaeleza kwamba kuna mtu anafuatilia gari lake.

Akizungumza wakati wa ibada ya kumwombea Lissu iliyofanyika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima leo Jumapili, amesema alimwona kaka yake akiwa amelala kitandani hospitalini mwili ukiwa na damu.

Amesema alipoamka leo asubuhi alielezwa na mtu kuwa kuna ibada maalumu ya kumwombea Lissu, hivyo akaamua kuhudhuria katika kanisa hilo la Mchungaji Josephat Gwajima.

Vincent amesema baada ya kaka yake kushambuliwa Alhamisi wiki hii, alienda Dodoma na kwamba anawashukuru madaktari waliofanya kila waliloweza kuokoa maisha ya ndugu yake.

Amesema kaka yake ni mpenda haki tangu akiwa mdogo na ameomba wananchi wazidi kumuombea.

Lissu hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi nchini Kenya.

Katika shambulio lililofanywa na watu wasiofahamika nyumbani kwa Lissu Area D mjini Dodoma, mbunge huyo alipigwa risasi tano.

– Mwananchi

Nawafahamu...Tundu Lissu Afunguka..Magazeti ya Leo Jumatatu

$
0
0

Nawafahamu...Tundu Lissu Afunguka..Magazeti ya Leo Jumatatu

Julius Mtatiro Afunguka 'Mbinu hii ya Kuvamia na Kuua ina Madhara Makubwa Sana'

$
0
0
Julius Mtatiro Afunguka 'Mbinu hii ya Kuvamia na Kuua ina Madhara Makubwa Sana'
Mbinu hii ya kuvamia na kuua ina madhara makubwa sana, kama lengo lake lilikuwa ni kuwatisha wanasiasa na wanaharakati, walioibuni hawaku-calculate madhara yake.

Madhara yake makuu huwa ni visasi, visasi, visasi - na visasi hugusa pande zote, zilizoathiriwa na zilizoathiri. Mwisho wa siku visasi huzaa machafuko! Tusimame imara, tuseme hapana! Tuseme NO!

Kala Pina Arudi Kwa Kishindo na Nyimbo ya 'Watu Wasiojulikana'

$
0
0
Msanii mkongwe wa Hip Hop Karama Maosud a.k.a Kala Pina amerudi na wimbo uitwao 'Watu wasiojulikana' ni nyimbo moja kali ila katoa teaser kiaia tu, official hajaitoa bado
Sasa sijui kamaitapigwa marufuku kuwa ni ya kichochezi au vipi

VIDEO:

Jeshi la Polisi: Askari wa Interpol Aliyekuwa Nairobi Alikuwa Kikazi, si Kama Inavyosambazwa Mitandaoni

$
0
0
Msemaji wa jeshi la Polisi Tanzania,Kamishna msaidizi Barnabas Mwakalukwa ameongea na kutoa taarifa kuwa,askari wa Interpol ambaye picha yake imesambaa mitandaoni kuwa ameonekana katika viunga vya Nairobi alisharudi nyumbani Tanzania.

Askari huyo alitiliwa mashaka sababu ya uwepo wa Tundu Lissu hospital Nairobi,na picha zake zilisambaa kwa kasi mitandaoni.

Msemaji wa Polisi anasema,askari huyo ni kweli alikuwepo Nairobi toka tarehe 04/09/2017 hadi 08/09/2017 kwa ajili ya mafunzo maalumu,na alirudi siku kadhaa zilizopita baada ya kuwa amemaliza mafunzo hayo.

Hivyo ni kweli alikuwa Nairobi,lakini si kwa kuhusishwa na tukio la Tundu Lissu,bali alikuwa kwa shughuli za kikazi ambazo amekwisha maliza na kurudi Tanzania.

Taarifa za uwepo wa "kachero" huyo katika viunga vya Nairobi,zilianza kusambaa kupitia account ya mtandao wa Tweeter wa Mbunge Halima Mdee,akisema kuwa wamepata taarifa za uwepo wa askari huyo na wanafuatilia nyendo zake katika jiji la Nairobi,maana inadhaniwa ametumwa kwa "kazi maalumu"

Jeshi la Polisi limeomba Wananchi kutokusambaza tena ujumbe huo baada ya ufafanuzi huo,na yoyote atakayeusambaza,atakuwa anatenda kosa la jinai na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Msikilize hapa chini msemaji wa Jeshi la Polisi

Kutoka Bungeni: Hawa Ghasia aitaka Serikali iifanye tohara kwa Wanaume kuwa ya lazima

$
0
0
BUNGENI, DODOMA: Mhe. Hawa Ghasia(Mb) ameitaka Serikali iifanye tohara kwa wanaume iwe lazima ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI.

Akijibu swali hilo, Naibu waziri wa afya Dkt. Hamis Kigwangalla amesema serikali haiwezi kulifanya suala la tohara kwa wanaume kuwa ni la lazima.

> Aidha mwanzo wa kikao hicho cha Bunge, Mbunge Mteule wa Viti Maalum kupitia chama cha Wananchi CUF, Rehema Migila aliapishwa na kukamilisha nafasi ya nane ya wabunge walioteuliwa baada ya mmoja kufariki dunia.


Hawa Ghasia Alilia Tohara kwa Wanaume Kilazima

$
0
0
Hawa Ghasia Alilia Tohara  kwa Wanaume Kilazima
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasia ameiomba serikali ya Tanzania kuangalia uwezekano wa kutoa huduma ya tohara kwa wanaume kilazima ili iweze kusaidia kupunguza maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Mhe. Ghasia ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anauliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kusema ni serikali inapata kigugumizi gani katika suala la tohara kwa wanaume lisiwe la lazima kama yaliyovyo magonjwa mengine yanayotolewa chanzo katika vituo vya afya.

Kutokana na hayo, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla amemjibu kwa kusema serikali haipati kigugumizi chochote juu ya jambo hilo kwa kuwa ni la hiyari na wala siyo lazima.

"Kwanza kiujumla ni lazima ieleweke dhana ya ridhaa kwenye huduma za afya na tiba kwa sababu ni jambo la hiyari kama vile ilivyo kwa matibabu mengine yote ni lazima mtu atoe ridhaa yake ndipo aweze kupatiwa huduma ya kufanyiwa tohara na haiwezi hata siku moja kuwa ni jambo la lazima. Na kwa msingi huo serikali haina kigugumizi chochote juu ya hilo", amesema Dkt. Kigwangalla.

Pamoja na hayo, Dkt. Kigwangalla ameendelea kwa kusema "Nichukue nafasi hii Mhe. Spika kutoa rai kwa wakina mama wote nchini kutumia fursa  ya kuwashawishi wenza wao kwa kuzungumza nao kwa upole, heshima na upendo wa hali ya juu ili wale ambao hawajafanya tohara waende kwa hiari yao katika vituo vya afya waweze kutahiriwa", amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Kwa upande mwingine, Dkt. Kigwangalla amesema tohara inapunguza maambukizo ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)kwa asilimia 60 hivyo amewataka wanaume wote ambao bado hawajafanyiwa tohara kutumia nafasi hiyo kwenda kwenye vituo vya kutoa huduma hiyo ili waweze kupewa huduma hiyo.

Jay Dee Kuachia Video ya Ngoma Mpya Ijumaa

$
0
0
Ni muda mrefu mashabiki wametamani kumsikia tena Lady Jaydee baada ya ukimya wake wa takribani miezi mitano.

Jay Dee Kuachia Ngoma Mpya Ijumaa
Hatimaye malkia huyo wa Bongo Flava, Jumanne hii ameachia wimbo wake mpya ‘I Miss You’ ambayo imetayarishwa na Man Walter. Lakini bado kiu ya mashabiki wanatamani kuiona video ya wimbo huo.

Akiongea na Bongo5, mmoja ya watu wa karibu wa msanii huyo amesema, video ya wimbo huo itatoka rasmi siku ya Ijumaa hii na imeongozwa na Justin Campos nchini Afrika Kusini.

Video ya mwisho ya Jide ilikuwa ni ‘Rosella’ aliyofanya na kundi la H_art The Band kutoka nchini Kenya ambapo pia wimbo huo unapatikana katika albamu yake mpya, Woman. Hizi ni baadhi ya picha zinazoweza kuonekana katika wimbo huo.










Mpigapicha Ashinda Kesi Kuhusu 'selfie ya Tumbili

$
0
0
Mpigapicha Ashinda Kesi Kuhusu 'selfie ya Tumbili
Mpigapicha mmoja ameshinda kesi iliyodumu kwa miaka miwili dhidi ya kundi la kutetea haki za wanyama kuhusu haki za kumiliki picha ambayo ilipigwa na tumbili.

Tumbili kwa jina Naruto alidaiwa kujipiga picha hiyo katika msimu mmoja Indonesia mwaka 2011 alipoichukua kamera iliyokuwa inamilikiwa na David Slater kutoka Monmouthshire.

Majaji nchini Marekani wamesema tumbili huyo hangekabidhiwa haki miliki ya picha hiyo.
Watetezi wa haki za wanyama kutoka kwa kundi la People for the Ethical Treatment of Animals (Peta), ambao walikuwa wamewasilisha kesi hiyo kwa niaba ya tumbili huyo, walisema mnyama huyo anafaa kufaidi kwa njia fulani.

Kesi hiyo ya Peta "kwa niaba ya tumbili" imetupiliwa mbali lakini Bw Slater amekubali kutoa asilimia 25 ya mapato yatakayotokana na picha hiyo siku zijazo.

Kwenye taarifa ya pamoja, Peta na Bw Slater, wamesema mpiga picha huyo atatoa robo ya pesa atakazopata kupitia uuzaji wa selfie za tumbili huyo kwa mashirika ya hisani yaliyosajiliwa "ambayo yamejitolea kulinda maslahi au makazi ya Naruto".

"Kesi hiyo ya Peta ilikuwa imezua mjadala mkubwa kimataifa kuhusu haki za kimsingi za wanyama kwa jumla, na si zaidi kwa jinsi wanavyotumiwa na binadamu kujifaidi," wakili wa Peta, Jeff Kerr amesema.

Bw Slater, kutoka Chepstow, alikuwa amejitetea kwamba anafaa kuimiliki picha hiyo akisema alifanya juhudi sana kabla ya kuipata picha hiyo.
Alisema juhudi zake hazingeweza kulipwa hata kwa kudai hakimiliki pekee.

David Slater amesema ilimchukua siku tatu za 'kazi ngumu' kupata picha hiyo
Bw Slater akijitetea alisema ilimchukua siku tatu za 'kazi ngumu' kupata picha hiyo. Alisema pesa zinazotokana na kutumiwa kwa picha hiyo, aliyoipiga katika kisiwa cha Sulawesi nchini Indonesia mwaka 2011, ni zake.

"Ilinichukua siku tatu za kutoa jasho kupata selfie hii kuhakikisha ninakubalika na kundi la kima kabla yao kunikubali kiwakaribie vya kutosha na kuwaonyesha kamera yangu," Bw Slater aliambia BBC mwaka 2015.
"Tatizo ni kwamba, watu wengine wanajaribu kuiba haki zangu za umiliki na nitapinga hilo."

Slater alikuwa amesema angekuwa taabani kifedha akishindwa kwenye kesi hiyo au aamrishwe kulipa gharama ya kesi
Selfi hiyo ilisambazwa sana kote duniani na mtandaoni.
Waliompinga Slater wanasema hawezi kuwa na hakimiliki ya picha hiyo kwa sababu ilipigwa na mnyama.

Bw Slater amesema yeye ni mhifadhi wa wanyama na mazingira na kwamba kuvuma kwa picha hiyo kumewasaidia sana wanyama Indonesia.
Kesi hiyo ilikuwa imeorodheshwa kama "Naruto v David Slater" lakini kulikuwa pia na mzozo kuhusu utambulisho wa tumbili aliyehusika.
Peta walidai alikuwa tumbili jike kwa jina Naruto lakini naye Bw Slater akadai alikuwa tumbili tofauti wa kiume.

Lakini majaji wa mahakama ya rufaa mjini San Francisco wamekubali hoja za Bw Slater baada ya vuta nikuvute ya miaka miwili mahakamani.
Taarifa ya pamoja ya Peta na Bw Slater imesema kesi hiyo "iliibua masuala muhimu kuhusu kupanuliwa kwa haki za kisheria kwa wanyama, ambao si binadamu".

Spika Ndugai Aagiza Kubenea Kusakwa, Zitto Kufikishwa Kwenye Kamati ya Maadili

$
0
0
Spika Ndugai Aagiza Kubenea Kusakwa, Zitto Kufikishwa
Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuagiza kutafutwa kwa namna yoyote Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea apelekwe kesho kwenye Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ili ahojiwe kuhusu kauli aliyoitoa ya kumtuhumu Spika kuwa amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),  Tundu Lissu.

Pia  Spika Ndugai ameagiza Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka kwa tuhuma mbili tofauti                       

Zitto anatuhumiwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili fulani, wakati Kubenea ni kwa kumtuhumu Spika kusema uongo wa idadi ya risasi alizopigwa Lissu.

Spika Ndugai ametoa maagizo hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne.

 

Serikali Tunalaani Uvamizi Alofanyiwa Tundu Lissu Sasa Jambo Hili Lipo Polisi Tuwaachie Wafanye Kazi - Masaju

$
0
0
Serikali Tunalaani Uvamizi Alofanyiwa Tundu Lissu Sasa Jambo Hili Lipo Polisi Tuwaachie Wafanye Kazi - Masaju
Mwanasheria Mkuu wa Serikali nchini Tanzania, George Masaju amefunguka kuhusu sakata la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kupigwa risasi na watu wasiojulikana na kusema kuwa kwa sasa jambo hilo waachiwe polisi na vyombo vya usalama.

Akiongea leo bungeni George Masaju alianza kwanza kwa kutoa pole kwa Mbunge Tundu Lissu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana na kusema serikali inalaani vikali kitendo hicho alichofanyiwa Tundu Lissu.

"Naomba kutoa pole kwa Tundu Lissu kwa majeraha aliyopata kutokana na kupigwa risasi na watu wasiojulikana sisi kama serikali tunalaani vikali jambo hili, kwa kuwa sasa jambo hili lipo kwa jeshi la polisi, tuviachie vyombo vya usalama naamini watafanya upelelezi kwa haraka" alisema George Masaju
Mbunge Tundu Lissu kwa sasa yupo nchini Kenya akipatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.



Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images