Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Sakata la Madini Lazidi Kupeleka Vigogo Lukuki TAKUKURU

$
0
0
Sakata la Madini Laendelea Lazidi Kupeleka Vigogo Lukuki  TAKUKURU
 Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) inawahoji vigogo wa Serikali wakiwamo waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini kwa nyakati tofauti huku polisi ikitua katika mgodi wa almasi uliopo Mwadui.

Taarifa ambazo gazeti hili limezipata zilisema miongoni mwa vigogo waliohojiwa na Takukuru kwa vipindi tofauti mpaka jana ni mawaziri wa zamani wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na William Ngeleja.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili jana, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola japo hakuwataja mawaziri hao wastaafu alikiri vigogo kadhaa kuhojiwa.

Mwandishi: Kuna taarifa kuwa Takukuru inawahoji waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na William Ngeleja. Ni kweli?

Mlowola: Wanaohojiwa hapa ni wengi.

Mwandishi: Sawa, lakini nilitaka kujua kama kweli hao wawili leo mnawahoji?

Mlowola: Unajua tumekabidhiwa jukumu la kuchunguza masuala ya madini, kwa hiyo hilo linafanyika hapa.

Mbali ya ripoti za kamati teule za Bunge zilizochunguza mwenendo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya almasi na Tanzanite zilizowasilishwa kwa Rais John Magufuli kuwataja Profesa Muhongo na Ngeleja, pia ziliwataja aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ujenzi, Edwin Ngonyani kuhusika kwa namna moja au nyingine katika masuala ya kiutendaji yaliyokwenda kinyume na mikataba.

Hata hivyo, Rais Magufuli alisema Profesa Abdulkadir Mruma aliyetajwa katika ripoti hiyo kuwa mmoja wa wahusika alikuwa alipandikizwa kwa maadui ili kuibua taarifa ya namna nchi inavyoibiwa.

Profesa Mruma ndiye aliyeongoza kamati ya kwanza ya Rais ya kuchunguza mchanga wa madini ambayo pamoja na mambo mengine ilimtaja Profesa Muhongo kuhusika na upotevu wa mapato ya madini na hivyo kutakiwa kujiuzulu Mei 24.

Ngeleja ambaye pia alikuwa Waziri wa Nishati na Madini katika awamu ya nne ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete alitajwa katika kashfa kadhaa za madini ikiwamo ya mchanga wenye madini maarufu kama makinikia.

Mbali na kashfa hiyo, vilevile alitajwa katika kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow ambayo hata hivyo hivi karibuni alitangaza kurejesha Sh40 milioni zilizotolewa na mfanyabiashara James Rugemalira.

Mawaziri wengine wastaafu wa Nishati na Madini katika awamu ya tatu na nne waliotajwa katika kashfa za madini na kamati za Rais ikiwamo ile ya pili ya makiniki iliyoongozwa na Profesa Nehemia Osoro ni pamoja na Daniel Yona, Abdallah Kigoda (marehemu) na Nazir Karamagi.

Wengine waliotajwa ni waliokuwa wanasheria wakuu wa Serikali; Andrew Chenge na Johnson Mwanyika.

Vilevile wamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba, Felix Mrema na waliokuwa makamishna wa Wizara ya Nishati na Madini, Mary Ndosi na Dk Dalali Kafumu, wanasheria akiwamo Jaji Julius Malaba na baadhi ya maofisa wa TRA.

Akizungumza baada ya kupokea ripoti za biashara ya almasi na Tanzanite wiki iliyopita, Rais Magufuli aliagiza viongozi wote waliotajwa katika ripoti hiyo kujiuzulu mara moja kupisha uchunguzi.

Pia, aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wote waliotajwa, huku akiwataka Watanzania kuwa na uzalendo.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro alisema jeshi hilo limeshaanza kufanyia kazi ripoti walizokabidhiwa na Rais Magufuli kuhusu masuala ya wizi, ufisadi, uzembe pamoja na rushwa zilizosababisha nchi kupata hasara kutokana na biashara ya madini.

“Wale wote waliotajwa kwenye ule uchunguzi wa biashara ya madini ni vizuri sana wakajisalimisha wao wenyewe kwa mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ili waweze kuhojiwa na uchunguzi ufanyike halafu tuweze kufahamu wanahusika kwa kiasi gani na wasisubiri kukamatwa,” alisema.

Maofisa Tanzanie One washikiliwa

Maofisa saba wa kampuni ya Tanzanite One inayochimba madini ya Tanzanite katika eneo la Mererani wilayani Simanjiro wakiwamo wakurugenzi wawili wanashikiliwa na polisi mkoani Manyara kwa mahojiano kutokana na taarifa za utoroshwaji wa madini ya Tanzanite.

Wakati maofisa hao wakishikiliwa Jeshi la Polisi mkoani humo hivi sasa limechukua jukumu la ulinzi wa migodi ya Tanzanite iliyopo sehemu hiyo ili kuzuia vitendo vyovyote vya utoroshaji wa madini na uvamizi ndani ya Tanzanite One.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe alisema maofisa hao wanahojiwa kutokana na tuhuma za utoroshwaji wa madini kama ambavyo iliainisha na kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza sekta ya Tanzanite.

Massawe alisema wakurugenzi wa Tanzanite One ambao wanashikiliwa ni Hussein Gonga na Faisal Shabhai na pia kuna maofisa wengine watano ambao wanaendelea kuhojiwa.

“Tumewashikilia kupata taarifa kuhusiana na tuhuma mbalimbali ambazo zimetolewa na kamati ya Bunge,” alisema.

Akizungumzia ulinzi katika migodi ya Tanzanite, Massawe alisema jeshi hilo limeongeza askari wake ambao watalinda migodini ili kuzuia utoroshaji wa madini. “Kuanzia sasa tutakuwa tunalinda migodini ili kulinda watu wasitoroshe madini na kuhakikisha tunadhibiti matukio ya uvamizi migodini,” alisema

Kukamatwa kwa maofisa hao kumetokana na agizo la Rais Magufuli linalotaka ufanyike uchunguzi juu ya tuhuma mbalimbali huku pia viongozi wa Serikali waliotajwa wakitakiwa kujiuzulu kupisha uchunguzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Nishati na Madini, Kampuni ya Tanzanite One inamilikiwa kwa ubia baina ya Shirika la Madini ya Taifa (Stamico) na kampuni ya Sky Associates Group Limited kuanzia Januari 30 mwaka 2015 .

Kampuni hiyo inamilikiwa na Hussein Gonga mwenye hisa 35, Faisal Shabhai hisa 25 na Rizwan Ullah mwenye hisa 40.

Katika mgodi huohuo wenye leseni ya ML 490/2013 uliopo eneo la kitalu C, Stamico kwa sasa inamiliki asilimia 50 ya hisa na Sky Associates asilimia 50 ya hisa.

Akizungumzia kamatakamata ambayo inaendelea Mererani, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Manyara, Sadiki Mnenei aliwataka wanachama wao kuwa watulivu wakisubiri uchunguzi wa Serikali.

“Ni kweli kuna wachimbaji wanashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi, sisi kama chama tunawataka wachimbaji kuwa watulivu kipindi hiki,” alisema.

Kutoka Shinyanga, kikosi maalumu cha upelelezi kinachoundwa na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam tayari kimeanza kazi ya kuchunguza shughuli za uzalishaji na biashara ya madini ya almasi katika mgodi wa Mwadui unaomilikiwa na kampuni ya Williamson Diamonds Limited (WDL).

Kutokana na mahojiano yanayoendelea, shughuli za mgodi huo uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga zimesimama kuanzia juzi kutoa fursa kwa viongozi na watumishi wa vitengo nyeti vinavyosimamia uchimbaji, uthamini na usafirishaji kuhojiwa.

Akizungumza kwa njia ya simu jana asubuhi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack alithibitisha uwapo wa kikosi kazi hicho mkoani humo na kufafanua kuwa shughuli za mgodi huo zitarejea kama kawaida baada ya mahojiano kukamilika.

“Hawajafunga mgodi. Kinachofanyika ni mahojiano na uchunguzi unaofanywa na maofisa wa ngazi za juu kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Yakikamilika shughuli zitarejea kama kawaida,” alisema Tellack.

Licha ya kuthibitisha uwepo wa kikosi kazi hicho mkoani mwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alisema hawezi kuzungumzia utendaji wake kwa sababu kinahusisha na kusimamiwa na maofisa kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

Bila kutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo, Ofisa Uhusiano wa mgodi huo, Joseph Kaasa aliliambia Mwananchi kwa njia ya simu kuwa yuko kituo cha polisi na kuahidi kutoa taarifa atakapokamilisha kilichompeleka kituoni hapo.

WDL juzi ilisitisha kwa muda baadhi ya shughuli za uzalishaji mgodini, huku uongozi wa kampuni hiyo katika taarifa kwa wafanyakazi iliyotolewa Jumamosi kwa tangazo namba 3311 ukisema kwa mtazamo wa uchunguzi ulioanzishwa na Serikali na kwa sababu za kiusalama, umeamua kusitisha kwa muda baadhi ya shughuli za uzalishaji katika mgodi huo.

Taarifa hiyo ilisema shughuli ambazo zitaendelea ni za huduma maalumu za ulinzi, tiba, umeme, maji, zimamoto na usafiri unaohitajika katika huduma hizo.

“Huduma za kiutawala zitaendelea kufanya kazi. Tutawajulisha wakati uzalishaji utakaporejea,” ilisema taarifa ya kampuni hiyo.

WDL ilisema inasubiri kuachiwa kifurushi namba WI-FY18 cha almasi iliyokuwa ikisafirishwa nje kutoka mgodini.

Waziri wa Fedha, Philip Mpango akizungumza wakati alipopokea ripoti kuhusu shehena ya almasi iliyozuiliwa katika Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alisema, “Tanzania ‘imepigwa vyakutosha’ hivyo wale wote waliohusika katika upigaji huo washughulikiwe.”


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Kimemtaka Rais Magufuli Kufanyia Marekebisho Sheria ya Adhabu ya Kifo

$
0
0
LHRS Kimemtaka Rais Magufuli Kufanyia Marekebisho Sheria ya Adhabu ya Kifo
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemtaka Rais John Magufuli kuanzisha mchakato wa kuifanyia marekebisho sheria inayotoa adhabu ya kifo.

Akizungumza leo Jumanne, Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba amesema wamefurahishwa na kauli ya Rais Magufuli kwamba hawezi kusaini hukumu ya kifo.

Rais Magufuli alionyesha kutofurahishwa na adhabu hiyo jana Jumatatu wakati wa hafla ya kumwapisha Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma.

Dk Kijo Bisimba amesema kwa kuwa Rais haipendi adhabu hiyo, hata Watanzania wengine hawaipendi pia.

Amesema Rais atumie nafasi yake kusimamia mchakato wa kurekebisha sheria na adhabu hiyo.

Mkurugenzi huyo amesema hata marais wa Serikali za awamu ya tatu na nne Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete hawakusaini ili kutoa adhabu ya kifo.

Amesema pamoja na kutosaini lakini hawakusema kuwa hawaipendi adhabu hiyo.

"Tunamshukuru Magufuli angalau ameonyesha kutoipenda adhabu ya kifo, sasa aifanyie marekebisho sheria," amesema.



Spika wa Bunge Anajua Ninavyomuheshimu Kama Imefika Haoni Heshima ya Bunge Inavyoporomoka Namsikitikia- Zitto

$
0
0
Spika wa Bunge Anajua Ninavyomuheshimu Kama  Imefika Haoni Heshima ya Bunge Inavyoporomoka Namsikitikia- Zitto
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumjia juu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kusema kuwa anamsikitika sana kama haoni jeshi heshima ya Bunge inavyoshuka.

Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuagiza na kuwataka wabunge Zitto Kabwe pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo wamezitoa hivi karibuni.

Kufuatia wito huo Zitto Kabwe amesema yeye atafika kwenye kamati hiyo ya maadili na Madaraka ya Bunge kama ambavyo Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza na kusema kuwa spika huyo kama angeweza kujua nguvu yake wala asingehaika na wabunge ambao wanakosoa kwa staha.

"Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu kama imefikia haoni heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya Maadili, Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu kushuhudia mbunge anapigwa risasi mkutano wa bunge ukiendelea wabunge wazoefu tulikuwa na matumaini makubwa na spika Ndugai tulimpigania dhidi ya njama za kumhujumu kutoka Ikulu anatuangusha angejua nguvu aliyonayo kukabili udikteta unaonyemelea nchi yetu asingehangaika na ukosoaji wenye staha tunaoufanya" alisema Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe amesema kuwa Ndugai alitamani kufikia japo robo marehemu Sitta katika kuongoza shughuli za bunge lakini ameshindwa kufikia hata asilimia ya Anna Makinda.
"Kwenye mazishi ya Spika wa watu Mzee Sitta, Ndugai aliomba afike japo robo ya Sitta. Hajafika hata 10% ya Anna Makinda miaka 2 sasa hatujawahi kuwa na Spika anayedhalilishwa na Rais kwamba aliuliza wajumbe gani awaweke Kamati za uchunguzi za Bunge" alisema Zitto Kabwe




Tukio la KushambuliwaLissu Limepangwa na Watu Wengi Ila Baada ya Muda Kila Kitu Kitajulikana- Mbowe

$
0
0
 Tukio la KushambuliwaLissu Limepangwa na Watu Wengi Ila Baada ya Muda Kila Kitu Kitajulikana- Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema watu waliopanga na kutekeleza shambulio la risasi dhidi ya mwanasiasa machachari wa upinzani, Tundu Lissu watajulikana muda si mrefu.

Ameliambia Mwananchi kwa njia ya simu akiwa Nairobi, Kenya, alipokwenda kusimamia matibabu ya Lissu kuwa shambulio hilo lilipangwa kwa muda mrefu na kwamba waliofanya hivyo hawawezi kujificha tena.

“Tukio hili lilipangwa na kuratibiwa kwa muda mrefu. Kuna magari mengi yamekuwa yakimfuatilia Lissu kwa muda mrefu na hili jambo halikupangwa na mtu mmoja, limepangwa na watu wengi na baada ya muda kila kitu kitajulikana,” alisema.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) alishambuliwia kwa risasi zaidi ya 30 nyumbani kwake Area D mjini Dodoma muda mfupi baada ya kutoka kwenye ukumbi wa Bunge.

Watu wasiofahamika walilifuatilia gari lake tangu alipotoka bungeni saa saba mchana na alipofika nyumbani kwake alisita kushuka baada ya kuona gari hilo likiendelea kumfuata na ndipo aliposhambuliwa.



Wabunge wa Upinzani Waendeleza Mgomo Bungeni

$
0
0
Wabunge wa Upinzani Waendeleza Mgomo Bungeni
Mapema leo Septemba 12, 2017  umetokea mgomo mwingine Bungeni kutoka kwa wabunge wa upinzani wakigomea kuapishwa kwa wabunge wateule wa Chama cha Wananchi CUF.

Huu unakuwa ni mwendelezo wa mgomo ule wa awali Septemba, 5 mwaka huu ambapo wabunge wa upinzani walitoka nje ya ukumbi wa bunge wakieleza kutounga mkono kitendo cha kuapishwa kwa wabunge Saba wa CUF.

Wabunge wa Upinzani hususani wale wanaotoka vyama vinavyounda Ukawa wametoka nje ya Ukumbi wa Bunge leo wakipinga kuapishwa kwa mbunge mmoja wa CUF upande wa Lipumba aliyekuwa amebaki kati ya wale Saba walioapishwa Septemba 5 mwaka huu.

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo amesema wameamua kutoka nje baada ya kuona 'Order Paper' ikionyesha kuna Mbunge wa CUF anaapishwa.Lyimo amesema wataendelea kususia tukio lolote linalohusisha wabunge hao wapya wa CUF.

Kumekuwepo na mgogoro ndani ya CUF hali iliyopelekea kuwepo kwa makundi mawili moja likiwa ni kundi linalilomuunga mkono Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya siasa Profesa Lipumba, huku kundi lingine likiwa ni upande wa Katibu Mkuu wa CUF taifa Maalim Seif.



Bado Najisikia Uzito Kueleza Jamii Hali ya Lissu Mwili Wake Umevunjwa Vunjwa- Mashinji

$
0
0
 Bado Najisikia Uzito Kueleza Jamii Hali ya Lissu Mwili Wake Umevunjwa Vunjwa- Mashinji
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vincent Mashinji amefunguka na kudai anajisikia uzito kuelezea hali ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu inavyoendelea huku akimtaka aliyefanya kitendo hicho ajitafakari.

Katibu Mkuu wa chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vincent Mashinji.
Mashinji ametoa kauli hiyo leo asubuhi wakati CHADEMA ikitoa msimamo wake na kuelezea hali ya Mbunge huyo wa Singida Mashariki ambaye bado anapatiwa matibabu nchini Kenya kufuatia kushambuliwa kwa risasi kwa mbunge huyo.

"Bado najisikia uzito wa kuelezea jamii ya Watanzania hali ya kiongozi wetu Tundu Lissu, najua nina jukumu kubwa kama mtendaji wa chama kutaarifu umma juu ya hali ya Lissu inavyoendelea. Ni majonzi makubwa sana na kama kuna mtu katika taifa hili alifanya hicho kitendo anatakiwa ajitafakari sana. Mpaka jana asubuhi ameenza kupatwa na matatizo ya kifua kutokana na kulala kitandani muda mrefu, na kwa sababu mguu wake wa kulia umevunjwa vunjwa kwa risasi, nyonga yake pia mkono wake umevunjwa kwa risasi lakini 'inshallah' kama nilivyosema awali kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayeamua kuchukua roho ya nani na aache ya nani", amesema Mashinji.

Aidha, Mashinji amesema wamemuumiza sana Lissu ila hawataacha kumpigania ili aweze kupona na kutoka katika hali aliyokuwa nayo kwa sasa ili aweze kurudi kuendelea kuwapigania Watanzania.
"Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, kwa kweli wamemuumiza kwa hiyo ndugu zangu hiyo hali ya Lissu jana ilikuwa mbaya mpaka wakamuwekea mipira ya kupumulia lakini ilipofika wakati wa mchana hali yake ilikuwa inaendelea vizuri. Tunasafari ndefu ya kuhakikisha Lissu anapona, sasa hivi wamemtibu zile sehemu za ndani ambazo zingeweza kuhatarisha maisha yake kwa zile risasi zilizopita tumboni na sehemu nyingine", amesema Mashinji.

Pamoja na hayo, Mashinji ameendelea kwa kusema "Mhe. Lissu ni kweli tuliambiwa alipigwa risasi tano katika mwili wake lakini kulingana na hali ya mwili ulivyobomolewa yawezekana zilizidi. Leo ni siku ya tano akiwa anatibiwa hospitali na mpaka sasa hivi ameshafanyiwa oparesheni tatu nadhani itabidi kuzisitisha kidogo ili kumpa ahueni aweze kupumzika na yeye. Tulitegemea ingekuwa suala la kawaida tu yeye kwenda kutibiwa na kurudi lakini imekuwa tofauti. Msilie wala kusononeka kwa sababu Lissu bado yupo hai anaendelea kupigana na sisi, kuhakikisha kwamba anapona na kurudi kuendeleza ukombozi Watanzania ili kufikia uhuru wa kweli na mabadiliko ya kweli", amesisitiza Mashinji.

Kwa upande mwingine, Mashinji amesema wanajiandaa kisaikolojia kumpokea Lissu na hali ambayo atarudi nayo kwa kuwa hiyo ndiyo zawadi waliyopewa na Mwenyezi Mungu.


Rais Magufuli Amtembelea Hospitali Meja Jenerali Mstaafu Mribata Aliyejeruhiwa Kwa Kupigwa Risasi

$
0
0
Rais Magufuli Amtembelea Hospitali Meja Jenerali Mstaafu Mribata  Aliyejeruhiwa Kwa Kupigwa Risasi
Rais John  Magufuli leo Jumanne ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana  mchana na kisha kupelekwa katika hospitali ya jeshi Lugalo kwa matibabu.

Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Rais Magufuli kuwa Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.

Katika taarifa hiyo ya Msigwa ameeleza kuwa  Mritaba amemshukuru Rais Magufuli kwa kumjulia hali na kumuombea dua ili apone haraka.

Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo pia ametembea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu

Halima Mdee Atakiwa Kuripoti Polisi

$
0
0
Halima Mdee  Atakiwa  Kuripoti Polisi
Jeshi la Polisi nchini limewataka watu mbalimbali akiwemo Mbunge Halima Mdee, walioripoti kwenye mitandao ya kijamii na kusambaza picha ya askari wake akihusishwa na tukio la Tundu Lissu kuripoti kwa DCI kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Taarifa hiyo imetolewa leo na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini ACP Barnabas David kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, na kuwataka watu hao akiwemo mbunge huyo wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA kujisalimisha wenyewe kwa kutoa taarifa za uongo.
ACP David ameendelea kwa kusema kwamba jeshi la polisi kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandaoni kinaendelea na uchunguzi, kuwabaini wote waliohusika na kusambaza kwa taarifa hizo za uongo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.


Mahakamani: Ulikutwa Msokoto wa Bangi Kwenye Kabati la Vyombo Vya Wema

$
0
0
Mahakamani: Ulikutwa Msokoto wa Bangi Kwenye Kabati la Vyombo Vya Wema
Ofisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Wille ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alikuta msokoto wa bangi kwenye Kabati la vyombo la Wema Sepetu.

Inspekta Wille ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula kutoa ushahidi katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wenzake.

Akitoa ushahidi wake Mahakamani hapo, alidai kuwa anakumbuka February 4, 2017 aliitwa na Mkuu wake wa kazi na kupewa jukumu la kufanya upekuzi nyumbani kwa Wema ambapo aliongozana na Maofisa wenzake pamoja na Wema hadi nyumbani kwa Wema Ununio.

Alidai baada ya kufika nyumbani kwa Wema walimkuta dada wa kazi ambaye walimuomba waonane na Mjumbe wa Shina la maeneo hayo.

”Mjumbe alifika na tulimwambia tunataka kufanya uchunguzi katika nyumba hiyo ili kutafuta dawa za kulevya.”

Shahidi huyo alidai kuwa kabla hawajaingia ndani, Wema aliomba wakati upekuzi unafanyika dada yake awepo na alipofika akawapeleka ndani.

”Tulianza kupekua jikoni, ambapo juu ya Kabati la vyombo tulikuta msokoto mmoja wa Bangi na Lizra. Pia tukaingia kwenye chumba cha Wema anapohifadhia nguo ambapo tukakuta msokoto mmoja unaodhaniwa ni Bangi juu ya dirisha.”

Aidha, amedai kuwa baada ya hapo walifanya uchunguzi ndani ya chumba cha wadada wa kazi ambapo walikuta msokoto wa Bangi uliotumika ndani ya Kibiriti na baadaye walijaza hati ya ukamataji, kisha kuondoka na Wema hadi Kituo cha Polisi.

”Hivyo, February 8, 2017 tulimpeleka Wema Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanya vipimo vya mkojo, tulivyomaliza vipimo tulikabidhi sampuli hiyo.”

Baada ya kuelez hayo, shahidi huyo aliiomba Mahakama ipokee kielelezo hicho cha ukamataji mbele ya Mahakama ambapo hata hivyo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala alipinga kupokelewa kwa hati hiyo, akidai ina mapungufu kisheria.

Kutokana na mvutano huo, Hakimi Simba ameahirisha kesi hiyo hadi September 13, 2017 kwa ajili ya kutoà uamuzi wa kupokea kielelezo hicho ama la.


Rais Uhuru Kenyatta Kuhutubia Bunge Nchini Kenya

$
0
0
Rais Uhuru Kuhutubia Bunge Nchini Kenya
Bunge linasubiriwa kufunguliwa nchini Kenya leo ambapo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutoa hotuba.

Hata hivyo wabunge wa upinzani wamesema kuwa watasusia sherehe hiyo ya kufunguliwa kwa bunge, wakati kuna malumbano kuhusu marudio ya uchaguzi wa urais.
Hata hivyo hiyo jana Rais Kenyatta alisema kuwa shughuli za bunge zitaendelea kama kawaisa bila ya kewepo wabunge wa upinzani.

Bunge linafunguliwa huku wakenya wakijiandaa tena kupiga kura tarehe 17 mwezi Oktoba.
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya iliamrisha uchaguzi wa urais kurudiwa kutoka na hitilafu zilizotokea kwenye uchaguzi mkun uliofanyika tarehe 8 mwezi Agosti.

Hatuna Nia Mbaya Lakini Hatuna Imani na Uchunguzi Utakaofanya na Polisi Kuhusu Shambulio Alilofanyiwa Lissu- Prof. Safari

$
0
0
 Hatuna Nia Mbaya Lakini Hatuna Imani na Uchunguzi Utakaofanya na Polisi Kuhusu Shambulio Alilofanyiwa Lissu- Safari
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara na Wakili wa kujitegemea Tanzania. Prof Abadallah Safari amesema wao kama CHADEMA hawana imani na uchunguzi utakaofanywa na jeshi la polisi au serikali kuhusu shambulio la kujaribu kumuua Mbunge Tundu Lissu.

Akizungumza na wanahabari wakati wakitoa taarifa ya kamati kuu kupitia kikao walichokaa mwishoni mwa wiki iliyopita, Prof. Safari amesema kuwa wao hawana nia mbaya ya kutaka uchunguzi kufanywa na wachunguzi wa mambo ya nje lakini hii ni kutokana jinsi tukio lilivyotokea.

"Hatuna nia mbaya lakini sisi kama CHADEMA hatuna imani na serikali pamoja na jeshi lake la polisi katika uchunguzi wa jaribio la mauaji ya Mbunge wetu. Serikali pia  isipokubali kuleta wachunguzi kutoka nje tafsiri ni kwamba wanaogopa kuunguzwa na lipo jambo wanaloficha kuhusiana na shambulio la jaribio la kutaka kumuua ndugu yetu Tundu Lissu ambaye kwa sasa bado anapigana na kutaka kuokoa maisha yake kwani hali yake bado si nzuri" alisema Prof Safari.

Pamoja na hayo Prof. Safari amedai anamshangaa sana Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini , IGP Simon Sirro, kwa kauli yake ya kwamba Tundu Lissu hakufika kuripoti tukio la kufuatiliwa na watu asiowajua na kusema kuwa huko ni kutojua sheria ya mmwenendo wa makosa ya jinai.
Amesema kuwa Sheria hiyo inaeleeza namna jeshi lapolisi linavyotakiwa kufanya kazi zake na kwamba kutokana na aslimia 90 ya wananchi basi jeshi la polisi kazi yake ni kufuatilia  na kufanya upelelezi juu ya taarifa kwani wao ni walinzi wa amani na kuongeza kwamba Lissu tayari alieleza kila kitu lakini polisi hawakujali.

"Hatuamini kama walikuwa hawajui kama kuna taarifa Lissu alizitoa kuhusu yeye kufuatiliwa au waliamua tuu kutotilia maanani" alisisitiza Prof. Safari.
Mbali na hayo Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Vicent Mashinji ameeleza kwamba kwa sasa wanachohakikisha ni kwamba hospitali aliyopo Lissu inazidi kuimarishwa ulinzi lakini pia hatoweza kuzungumzia hali yake kwa undani kutokana pia na kuwepo watu wasiokuwa na nia njema.


Jeshi la Polisi Limekanusha Taarifa za Askari Wao Kuhusishwa Kwenye Tukio la Kuvamiwa Lissu

$
0
0
Jeshi la Polisi Limekanusha Taarifa za Askari Wao Kuhusishwa Kwenye Tukio la Kuvamiwa Lissu
MSEMAJI wa Jeshi la Polisi nchini, Barnabas Mwakalukwa, amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikionyesha picha za polisi kuhusika na shambulio lililomjeruhi kwa risasi Mbunge Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mwakalukwa amesema kuwa taarifa hizo zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii Septemba 11 mwaka huu, hivyo jeshi la polisi limekanusha taarifa hizo kuwa ni za uongo na zenye lengo la kumchafua askari huyo na jeshi la polisi kwa ujumla.

“Askari huyo hayupo Nairobi kama ilivyoenezwa na picha iliyotumika mitandaoni, picha hiyo ilipigwa hapa nchini Januari 7 mwaka huu ambapo askari wetu alikuwa kwenye sherehe ya mahafali ya mtoto wa kaka yake.

“Kuhusiana na safari ya Nairobi, askari huyo alikuwa nchini Kenya kwa kozi ya kimafunzo kuanzia Septemba 4 hadi 8 mwaka huu aliporejea Tanzania baada ya mafunzo na kuongeza kwamba Tundu Lissu alipelekwa nchini Kenya usiku wa Septemba 8 mwaka huu baada ya kupatwa na mkasa huo wa kujeruhiwa kwa risasi,” alisema Mwakalukwa.

Mwakalukwa alisema kwamba jeshi la polisi limekemea vikali kitendo hicho chenye lengo la kumharibia maisha yake askari wao na ametoa onyo kwa wote wanaofikiri kuwa wanaweza kukaa na ‘kupika habari’ ili waweze kuivuta jamii iwe upande wao na kuchafua upande wa serikali.

Huyu Hapa Mbunge Aliyetaka Wabunge Wanawake Kutoa Ushahidi wa Wanaume Waliotahiriwa Wanavyonogesha Tendo la Ndoa

$
0
0
Huyu Hapa Mbunge Aliyetaka  Wabunge Wanawake Kutoa Ushahidi wa Wanaume Waliotahiriwa  Wanavyonogesha Tendo la Ndoa
Mbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF) amezua vicheko bungeni baada ya kuuliza swali ambalo linalohoji tafiti zinaonyesha kwamba wanaume waliotahiriwa wanakuwa active zaidi na wananogesha zaidi yale mambo (mapenzi).

Mbunge Khatibu ameuliza swali hilo leo bungeni mjini Dodoma, ambapo spika Ndugai alipinga kuwa hilo sio swali “hilo nalifuta sio swali sio swali” amesema Spika Ndugai.

“Tafiti zinaonyesha kwamba wanaume waliotahiriwa wanakuwa active zaidi na wananogesha zaidi yale mambo, Je Mhe. Spika katika hali hiyo wabunge wanawake kupitia bunge hili mtoe kidogo ushahidi wa haya wanaume waliokuwa hawajatahiriwa waige mfano huo?

alihoji Mbunge Khatibu.

Jeshi la Polisi Limewataka Waliotuma au Kutoa Maoni Picha ya Kachelo Akimfatilia Lissu Kenya Kujisalimisha

$
0
0
Jeshi la Polisi Limewataka Waliotuma au Kutoa Maoni Picha ya Kachelo Akimfatilia Lissu Kenya Kujisalimisha
Polisi imewataka wote waliotuma au kutoa maoni kwenye mtandao wa kijamii kwamba, askari wa kitengo cha Interpol yupo Nairobi, Kenya akimfuatilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ajisalimishe katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

"Kama unajijua uli-comment chochote kuhusu taarifa hiyo njoo mwenyewe kabla hujatafutwa, tuna njia zetu tunaweza kuwafikia," amesema Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa alipozungumza na waandishi wa habari leo Jumanne.

Jeshi la Polisi limekanusha taarifa hizo zilizosambaa tangu jana Jumatatu kwenye mitandao ya kijamii zikihusisha picha ya askari huyo.

Mwakalukwa amesema taarifa hizo hazina ukweli kwa kuwa kachero huyo alikuwa Nairobi kwa mafunzo maalumu na tayari amesharejea nchini.

"Askari huyo alikuwa nchini Kenya kwa kozi ya mafunzo kuanzia Septemba 4 hadi Septemba 8, wakati Lissu alijeruhiwa Septemba 7," amesema.

Mwakalukwa amesema, "Tunatoa onyo kwa wote wanaofikiri wanaweza kukaa na kupika habari ili waweze kuivuta jamii iwe upande wao na kuchafua upande wa Serikali."

Amesema polisi kupitia kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandao inaendelea na uchunguzi kuwabaini wanaohusika kusambaza taarifa za uongo.

Mbunge Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) alijeruhiwa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma, Alhamisi Septemba 7.

Baada ya shambulizi hilo lililotekelezwa na watu wasiojulikana alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi, Kenya.


Waliovamia Ofisi za Mawakiliwa Prime Attorneys Wakwapua 3.7 Milioni

$
0
0
Waliovamia Ofisi za Mawakiliwa Prime Attorneys Wakwapua 3.7 Milioni
Watu wasiojulikana waliovunja ofisi za mawakili za Prime Attorneys wameiba Sh3.7 milioni na nyaraka kadhaa, zikiwemo hati za viwanja.

Msemaji wa ofisi hiyo, wakili Asia Charli amesema licha ya jengo hilo kuwa na ofisi mbalimbali, maduka, saluni na gym ni ya kwao iliyopo ghorofa ya tatu ndiko kumeibwa nyaraka na fedha.

"Kuna nyaraka mbalimbali za wateja na zetu zimechukuliwa na ni za muhimu sana," amesema.

Charli amesema nyaraka kuhusu kesi za mfanyabiashara Yusuf Manji anayewakilishwa na kampuni hiyo zimesalimika.

Mmiliki wa saluni ya Posh Unisex, Fatma Ebrahim amesema wavamizi wasiojulikana wamevunja mlango wa saluni wenye thamani ya Sh2.5 milioni na hakuna mali yoyote iliyoibwa.

Ofisi ya mawakili ya Prime Attorneys imevamiwa usiku wa manane kuamkia leo Jumanne.

Wakili katika ofisi hiyo, Hudson Ndusyepo ambaye ni miongoni mwa mawakili wanaomtetea mfanyabiashara maarufu Manji katika kesi ya uhujumu uchumi, amesema kabla ya wizi huo, waliohusika walimfunga mlinzi kwa kamba.

Ofisi za kampuni hiyo zipo jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam jirani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amethibitisha tukio hilo akisema limetokea kati ya saa nane na saa tisa usiku wa kuamkia leo na uchunguzi unaendelea.

Barnaba Atarajiwa Kuachia Albamu Yake

$
0
0
Barnaba Atarajiwa Kuachia Albamu Yake
Baada ya msanii kutoka TMK, Chege kuweka wazi mipango ya kuachia albamu yake ya ‘Run Town’ wiki hii, naye Barnaba Classic ametangaza kuachia albamu yake.

Akipiga stori katika The Playlist ya Times Fm, mkali huyo  amesema kuwa baada ya  kushindikana kuachia albamu  hiyo hapo mwanzoni kutokana na matatizo aliyopata ila sasa ana mpango wa kuachia albamu hiyo yenye ngoma kumi hivi karibuni.

“Mimi ni muimbaji nimetamani kuiona albamu yangu ikienda sokoni, i wish watu wasikie albamu yangu ambayo inakuja hivi karibuni,” amesma msanii huyo baada ya kusikiliza nyimbo zake mbili ‘Tunafanana’ na ‘Loverboy’ na kuongeza kuwa “baada ya kuzikiliza nyimbo hizi mbili naona yani kama zimebeba nyimbo 100 ukiachia zile nane zilizo bakia.”

Pia msanii huyo akasisitiza kuwa jina la albamu yake  itaiwa ‘Eight eight’ (8/8) sawa na siku yake aliyozaliwa na akaeleza kuwa  alipanga itoke albamu hii siku nyingi ila kutokana na matatizo aliyopata ya kuibiwa ikacheleweshwa hivyo kwa sasa  wana kaa na menejimenti kupanga mipango mizuri zaidi ya kuito

TANZIA: Golikipa Aliyedaka Katika Mechi ya Simba Day Afariki Dunia Leo

$
0
0
TANZIA: Golikipa Aliyedaka Katika Mechi ya Simba Day  Afariki Dunia Leo
Golikipa wa Rayon Sports, Evariste Mutuyimana aliyedaka kwenye mechi dhidi ya Simba siku ya Simba Day jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Taifa , amefariki dunia leo Jumanne kwenye Hospitali ya Kigali nchini Rwanda.

 Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) limethibitisha kutokea kwa kifo cha mchezaji huyo, huku likitoa salamu za pole kwa klabu ya Rayon Sports.
Mchezaji huyo alijiunga na klabu hiyo msimu wa mwaka 2016/17 akitokea Sofapaka FC ya Kenya.

Wabunge Nchini Uganda Wamekubaliana Kuwasilisha Mswada Kuondolewa Miaka Urais

$
0
0
Wabunge Nchini Uganda Wamekubaliana Kuwasilisha Mswada Kuondolewa Miaka Urais
Wabunge kutoka chama kinachotawala nchini Uganda NRM wamekubaliana kuwasilisha mswada ambao unapendekeza kuondewa miaka ya kuwania urais nchini Uganda.

Ikiwa watafaulu mswada huo utamwezesha Rais Yoweri Museveni ambaye anaaminika kuwa mwenye umri wa miaka 73, kuwania tena uchaguzi wa mwaka 2021.
Amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 na kwa sasa anahudumu muhula wake wa tano madarakani.

Mswada ambao huo amabo unaungwa mkono na wabunge 200 wa NRM unataka kukifanyia mabadiliko kipengee cha 102 (b) cha katiba ya Uganda, ambacho kinaweka umri ambao mtu anaweza kuwania urais wa kati ya miaka 35 na 75

Wengi wanasema kuwa NRM ambacho kina wabunge wengi, kitasababisha mabadiliko ya katiba lakini wengibe ndni ya NRM waekana.
Wabunge wanasema kuwa watawasilisha mswada huo bungeni katika kipindi cha wiki moja.

WOLPER sio Mtu wa Mchezo, Amchamba Tena Harmonize Mpaka Kwenye Kope...Atishia Kuvujisha Voice Note

$
0
0
WOLPER sio Mtu wa Mchezo, Amchamba Tena Harmonize Mpaka Kwenye Kope...Atishia Kuvujisha Voice Note
Soma hapa Chini:

From @wolperstylish -  Kwahiyo baada ya kuona mm nimeendelea na maisha yangu ukaona unitungie wimbo sumu hahahaha!Uongee ya kurudi asubuhi kisa kwenda kuchukua ela kwa Sarah afu Mm siimbi lkn kuna kitu kinaitwa call recorder nikisema nifanye kitu uenda Sarah atafika Italy kwa mabawa!Unasahau kuwa nina voice zako za juzi kati hapa ulizonipigia unalia lia km king'ora cha wagonjwa wenye hali maututi??Usitake niseme vyote usinichokonoe nimwage mivoice Afu mm sina hasara maana simfich m2 wangu k2. Ila  ww na penzi lako la biashara ndo utakaepambana na yule mama kija wako!Niache kidogo bwana imba hata nyimbo ya kuhusiana na Tundu Lissu afu jina unaweka wasiojulikana asee utauza sn kuliko kumuongelea mtu ambae mmeachana afu kaamua ku moooooove on.....!Hivyo yani km umenimiss nipitie hata kwenye kale kanyimbo ulikoniopaka mafuta kwa mgongo wa chupa (#Niambie.) lkn sio kuniendea studio kuniimbia taarabu 🤣🤣Ujue tatizo lako unahisi mwanaume upo ww tu bongo 😝😝Polyeeee sn wimbo nimeusikia lkn nimependa beat tu....!Afu kuongea sipangiwi,kukwepesha ndo kitu niliachaga toka enzi nacheza makidamakida hehehe Kunyamaza kwa vitu vya kijinga pia siwezi hilo ndo tatizo langu....Haya wenye kutoa mapovu toeeeni weeeh nakuja na beseni,pipa km yatalipa ntapeleka dry cleaners niwauzie tupate wateja...!Afu mtakao pata ujumbe pia mscreenshot tu!afu pia sijaongea yotee cz nimejua sikuhizi watu wanauza mziki kwa kuchamba watu,so endelea kufanya kazi yako....!lkn kumbuka na mm msanii nikitoa series ntauza sn cz ni ukweli mtuuuupu 👌🏻

VIDEO: "Tundu Lissu Amevunjwa Miguu yake, Nyonga na Mkono"- CHADEMA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema mwanasheria mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu ameumizwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba alipigwa risasi nyingi tofauti na risasi tano zilizoelezwa.

Dk Mashinji amesema Lissu amevunjwa miguu yake, nyonga na mkono wa kushoto, jambo ambalo linawapa madaktari kazi kubwa na kuimarisha afya yake.

Tazama Video:

Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images