Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Mkuu wa Majeshi Atoa Tahadhari kwa Wananchi

$
0
0

Mkuu wa Majeshi Atoa Tahadhari kwa Wananchi
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ametoa tahadhari kwa wananchi kwamba kuna matapeli wanaojifanya wanaajiri vijana kujiunga na jeshi.

Amesema watu hao wanadai fedha ili kuwasajili vijana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), jambo ambalo ni kinyume na taratibu za jeshi kuajiri vijana kwa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Mabeyo ameonya kwamba mtu yeyote atakayetapeliwa na watu hao basi naye atahesabika kama mmoja wa watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na kuchukuliwa hatua mara moja.

"Maongezi ya mtu na mtu hatuyatambui, ukitapeliwa nyamaza kimya kwa sababu ukilalamika kwetu na wewe utachukuliwa kama sehemu ya watoa rushwa," amesema Jenerali Mabeyo.

 Mkuu huyo wa majeshi amebainisha njia mbalimbali ambazo wanazitumia kuajiri vijana jeshini kuwa ni kuwachukua wale waliopitia mafunzo ya JKT au pale wanapotaka watu wenye taaluma adimu kama vile madaktari, wahandisi au wanasheria.

Amebainisha kwamba jeshi linapokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na wanachukua hatua kila wanapopata taarifa ikiwa ni pamoja na kuwatafuta wahusika na kuwakamata.

 "Kuna mmoja alikusanya vijana 15 na kila kijana akatakiwa kulipa Sh1 milioni. Aliwapangia chumba sehemu kisha akatoweka," amesema Mabeyo na kusisitiza kuwa wengi wanaofanya vitendo hivyo ni raia, wanajeshi ni wachache na wanachukuliwa hatua za kinidhamu mara moja.

Kuhusu matukio ya watu kupigwa risasi, CDF amesema wakati wote yanapotokea matukio hayo, vyombo vya ulinzi na usalama vinakabiliana nayo mara moja na hali inakuwa shwari.

 "Kwa ujumla hali iko shwari, huwezi kusema Tanzania siyo salama kwa sababu ya matukio mawili ya kijambazi. Mambo tunayotaka kujiridhisha nayo kwa sasa ni wapi wanapata silaha na wanatoka wapi," amesema Mabeyo.

       
 

Polisi Sumbawanga Wamepiga Stop Maombi Ya Kuombea Tundu Lissu

$
0
0
Polisi  Sumbawanga Wamepiga Stop Maombi Ya Kuombea Tundu Lissu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) mkoani Rukwa, leo Jumatano kimeshindwa kufanya maombi maalumu kwaajili ya kumuombea Mbunge Singida Mashariki,  Tundu Lissu aliyejeruhiwa kwa risasi hivi karibuni baada ya polisi mkoani humo kuzuia kwa kueleza kuwa haliruhusu mkusanyiko.

Mwenyekiti wa Chadema mkoa huo,  Sadrick Malila amesema wameskitishwa sana na hatua ya jeshi hilo kwani suala la kumuombea mbunge  huyo kamwe lisingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Amesema kuwa Chadema mkoa ilikuwa imewaalika viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali na wachungaji walikuwa tayari wamejiandaa kwaajili ya maombi hayo,  lakini wamelazimika kusitisha baada ya Kamanda wa Polisi, George Kyando kuwaeleza kwamba  wasitishe.

Mwenyekiti huyo aliwatangazia wanachama wa Chadema na wananchi wengine waliokuwa na nia ya kumuombea Lissu kuwa kila mtu afanye maombi binafsi kwani anaamini Mungu ni mwema na atajibu maombi yao.

Malila alitumia fursa hiyo kuliomba jeshi la polisi kuhakikisha linawasaka watu wanaoitwa kuwa hawafahamiki waliomjeruhi Lissu kwa risasi pamoja na ofisa wa jeshi aliyejuruhiwa kwa kupigwa risasi juzi jijini Dar es Salaam wanasakwa mpaka wapatikane ili kukomesha vitendo hivyo.

"Naliomba sana polisi kama wameshindwa kulinda raia na mali zao, basi waache kulinda mali watalinda wananchi wenyewe wao wawalinde raia tu kwa kuwa inawezekana majukumu yamewazidia wabaki na kitu kimoja na wanachi wawasaidie kitu kingine," alisema.



Mkurugenzi Mtendaji ATCL Amehukumiwa na Mahakama Kwenda Jela

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji ATCL Amehukumiwa na Mahakama Kwenda Jela
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na mwenzake kulipa faini ya Sh35 milioni kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka sita jela.

Mbali na Mattaka, mshtakiwa mwingine ni Elisafi Mathew aliyekuwa kaimu ofisa mkuu kitengo cha fedha cha ATCL.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.

Akitoa hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa alimuachia huru  William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa Hesabu za ndani ATCL, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka dhidi yake.

Mahakama pia imeamuru Mattaka na Mathew  kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni Dola 143,442.75 za Marekani ndani ya mwezi mmoja.

Washtakiwa walitiwa hatiani katika mashtaka sita yaliyokuwa yakiwakabili ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Serikali.



Manji Apokonywa Shamba la Heka 714 na Serikali

$
0
0
Manji Apokonywa Shamba la Heka 714 na Serikali
Serikali imelifuta shamba la mfanyabiashara Yusuf Manji, lenye ukubwa wa eka 714.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amesema shamba lingine la kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa.

Waziri amesema mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa  watashitakiwa.

"Muyaache maeneo hayo kama yalivyo mkijenga tutakuja kuvunja," amesema.


Jeshi Linawashikilia Watu wa Tano kwa Kuhusika Katika Shambulio

$
0
0
Jeshi Linawashikilia Watu wa Tano kwa Kuhusika Katika Shambulio
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu Watano ambao wanadaiwa kuhusika na tukio la kumshambulia kwa silaha hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Masasi, Khalfan Ulaya na kumsababishia kifo kilichotokea Septemba 8 mwaka huu

Akizungumaza na waandishi wa habari ofisini kwake, kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Naibu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya amesema hatua hiyo imekuja baada ya kufanyika msako mkali ulioanza baada ya tukio hilo, huku watuhumiwa wote wakikiri kuhusika baada ya kuhojiwa.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limesema kumeibuka tabia ya wizi wa mafuta katika viwanda vya saruji vya Dangote Industries Limited na Mtwara Cement, pamoja na wizi wa vifaa vya ujenzi katika kampuni zinazojenga barabara mkoani humo.

Msikilize hapa chini kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Naibu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya akiongelea tukio hilo.

Nimesikitishwa na Spika Muda Wowote Naweza Nikaitwa Nipo Nairobi Kumuuguza Lissu Ambaye Awezi Kula Wala Kuinua Mkono- Lema

$
0
0
Nimesikitishwa na Spika Muda Wowote Naweza Nikaitwa Nipo Nairobi Kumuuguza Lissu Ambaye Awezi Kula Wala Kuinua Mkono- Lema
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka na kudai amesikitishwa na kitendo cha Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwataka wabunge wawili kufika mbele ya Kamati ya Maadili na mwengine kamati ya ulinzi na usalama kuhojiwa juu ya kauli zao walizozitoa

Mhe. Godbless Lema amesema hayo leo akiwa mjini Nairobi nchini Kenya alipokwenda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye ameshambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
"Nimesikitishwa sana na kitendo cha Mhe. Spika kuwataka wabunge wawili, Mhe. Zitto Kabwe na Saed Kubenea kutokea  katika kamati ya maadili na mwingine kamati ya ulinzi na usalama na pengine baada ya maneno yangu haya na mimi naweza nikaitwa lakini siyo kitisho tena kwangu kuitwa mahali popote. Nipo Nairobi kumuangalia mbunge wetu na rafiki yangu, Mhe. Lissu ambaye hawezi kula wala kuinua mkono baada ya kupigwa na risasi na watu wasiojulikana", amesema Lema.
Pamoja na hayo, Lema ameendelea kwa kusema "Nilitarajia Mhe. Spika aliposikia taarifa za mbunge wake kupigwa risasi pengine shughuli za Bunge zote angesimamisha kama ambavyo alivyoamuru kukamatwa kwa wabunge wawili wapelekwe Polisi akiwemo Kubenea hapo awali", amesisitiza Lema.

Kwa upande mwingine, Mhe. Godbless Lema amedai alitarajia kuona mabadiliko ya katika Bunge kwa kupitisha sheria kwa pamoja ili kusudi wabunge waweze kupatiwa ulinzi wa kutosha kuanzia majumbani kwao mpaka wao wenyewe lakini imekuwa tofauti na yeye alivyokuwa akifikiri.



Jambazi Sugu Aliyeongoza Mauaji Auwawa na Polisi Dar

$
0
0
Jambazi Sugu Aliyeongoza Mauaji Auwawa na Polisi Dar
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, jana Septemba 12, maeneo ya Kivule Chanika lilifanikiwa kumuua jambazi sugu aitwae Anae Rashid Kapela aliyekuwa akitafutwa na jeshi hilo kwa muda mrefu akituhumiwa kushiriki matukio mbalimbali ya ujambazi likiwemo la mauaji ya polisi wanane wilayani Kibiti.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mambosasa alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar.

“Baada ya kupewa taarifa na wasamalia wema, Jeshi hilo lilifika na kuizingira nyumba alimokuwa lakini alifanikiwa kutoka na kutaka akitoroka. Polisi walipomsimamisha alikimbia ndipo wakampiga risasi ya goti na kuanguka.

“Alipohojiwa aliwataja wenzake pamoja na matukio makubwa ya uhalifu aliyoshiriki kuyafanya likiwemo hilo la kuwaua Askari Polisi wanane na kupora silaha zao kisha kukimbia,” alisema Mambosasa.

Je Dada Unapenda Kuwa Mrembo ? na Kaka Unapenda Kuwa Mtanashati na Kurudisha Heshima ya Ndoa?

$
0
0
JE, DADA UNAPENDA KUWA MREMBO? NA KAKA UNAPENDA KUWA MTANASHATI NA KURUDISHA HESHIMA YA NDOA? Tumia Bidhaa halisi za MARKSON kwa mafanikio ya uhakika na bila madhara.

 Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kuthibitishwa kiafya.

Pata hizi

1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @130,000/=
2. Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa (a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge  @180,000/=
3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:-  (1)Mafuta  @130,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a) Gely ya kupaka @150,000/=
(b) Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @150,000/= (c)Handsome up original >kifaa kinachoongeza maumbile kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea  @250,000/=
6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150,000/=
7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula  @130,000/=
8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
    (a) Dawa ya kunywa au kupaka @130,,000/=
(b) Mkanda wa kawaida @100,000/=
(c) micro-computer belt unaovaibret @250,000/=
9 .Kupunguza  maziwa na kuyasimamisha @130,000/=
10. Kushepu miguu na kuwa minene na kuondoa kigimbi @130,000/=
11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @100,000/=
12. kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @120,000/=

   NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
        Wasiliana nasi :-
(+255) 0767447444 na
  0714335378
     Follow us on instagram  @Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr

MBUNGE Sugu Aitaka FBI ifanye Uchunguzi wa Kupigwa Risasi Tundu Lissu

$
0
0
Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, amesema anaunga mkono hoja ya viongozi wengine wa CHADEMA kutaka serikali iruhusu vyombo binafsi vya usalama kuchunguza tukio la Tundu Lissu la kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Sugu ameandika ujumbe akisema kwamba serikali iruhusu uchunguzi kutoka vyombo binafsi vya kimataifa, ili kuwatambua na kuthibitisha waliompiga risasi Tundu Lissu.

"Nami naunga mkono kuitaka serikali iruhusu uchunguzi wa kimataifa kutoka vyombo kama FBI au 'Scotland Yard' ili kuwatambua na kuwathibitisha waliohusika na kitendo hiki ili wawajibishwe kwa hili jaribio la mauaji lisilo na maana, na hao wasiojulikana sasa wajulikane", ameandika Sugu.

Pia kwenye ujumbe huo Sugu ameweka wazi kuwa alitakiwa kusafiri kwenda nchini China kikazi lakini amelazimika kusitisha safari hiyo kwa sababu ya matatizo ya Tundu Lissu.

Takururu Imemtaja Mmiliki wa Vichwa vya Treni Vilivyokutwa Bandarini na rais Magufuli

$
0
0
Mkurunzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlowola ametaja mmiliki wa vichwa vya treni utata vilivyobainika kuwepo katika bandari ya Dar es Salaam.


Baada ya Wizara ya ujenzi na Mawasiliano kusesema haina taarifa ya Vichwa vya treni ambavyo vipo bandarini, rais akaagiza vyombo vya usalama kufuatilia baada ya ununuzi wake kuwa na utata.

Leo Azam TV walimhoji Mkurugenzi wa taasisi ya kupambana na Rushwa Nchini Valentino Mlowola, amesema Walibaini mchakato wa kununua hivyo Vichwa ulishaanza mwaka 2014/15, lakini hawakufika mwisho na hapakuwa na mkataba wuliosainiwa wa hivyo vichwa kufika nchini au kununuliwa nchini. Shirika linalohusika na Usafirishaji wa reli, ulishaanza mchakato wa ununuzi wa hivyo vichwa hivyo lakini hapakuwa na mkataba wa vichwa hivyo. Ameongeza mmliki wa hivyo vichwa ni Electro-Motive Diesel ya nchini Marekani ndo alivileta hapa nchi lakini hakuna Mkataba wa Mauziano kati ya hiyo kampuni la TRL

Amesema huu uchunguzi kuna vitu viwili vinatoka, unaweza kukuta utaratibu wa kiutawala zilikiukwa au makosa ya jinao yalitendwa. Bado tunaliangalia sababu watuhumiwa wote wameshahojiwa na vielelezo vyote tunavyo. Na kama kuna hatua za kujinai tutapeleka jalada letu kwa mwendesha mashitaka wa Serikali. VIDEO:

Nimemkuta Mpenzi Wangu na vitu Nisivyovielewa, Naomba Msaaada Wenu Kuvielewa

$
0
0
Nipo na mpenzi Wangu ambaye ninaamini ndie nampenda kuliko wanawake wote na ninamatarajio ya kufunga naye ndoa. Mara kwa mara huwa anakuja kulala kwangu hata Siku 2 na kurudi kwao.

Juzi aliponitembelea na kuingia bafuni nikashawishika kuchungulia ndani ya kipochi chake. Nikashituka baada ya kukuta vitu viwili.

1. Kikaratasi chenye unga wenye chembechembe ambazo zinaonekana ni mizizi iliyotwangwa kikiwa kimeandikwa "kuchoma".

2. Hiki kingine ambacho sijakitambua ni vijiti viwili. Kirefu na kifupi vikiwa vimeunganishwa na kamba. Kwa anayejua kuhusu hivi vijiti anisaidie uelewa.

JE Wajua Kuwa ni Watu Wawili tu Duniani Ndio Kamwe Hutaweza Kuwa’Bloku’ Facebook...?

$
0
0
Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan ndio watu pekee ambao huwezi kuwablock katika mtandao maarufu wa kijamii wa Facebook.

Mwanzoni kabla ya Mark Zuckerberg kumuoa Priscilla ni yeye pekee ndiye ambaye hakukuwa na uwezekano wa Kumbloku. Mark huandika taarifa nyingi kuhusu maboresho ya Facebook na taarifa mbalimbali kuhusu maisha yake binafsi au mambo mengine ya kijamii.

Kublock mtu ni njia mojawapo ya kutotaka aone posti zako wala zake. Njia hii unaweza kufanya asiwe rafiki yako (Unfriend) au kukufuata (Unfollow).



Ni kwamba unaweza kumblock mtu yeyote facebook kasoro yeye na mkewe tu! Ukiingia kwenye ukurasa wake option ya kumbloku ipo lakini haifanyi kazi. Ukibonyeza “block” inakuambia Block error.


Mark Zuckerberg na Priscilla Chan  walikutana mwaka 2003 wote wawili wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Havard, na mwaka 2012 walioana baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu.

Kwa mujibu wa ripoti ndani ya The Independent, machapisho yote (ndani ya facebook) huonekana katika mifumo ya malekezo ya kitarakimu ya Facebook inayofahamika kama ‘algorithm’ na mwishowe kuzipeleka kwa wachangiaji mbalimbali.



Hivyo kumzuia mwasisi wa Facebook na mkewe kulikuwa ndiyo njia mwafaka ya kuepuka machapisho yanayorushwa kwenye kurasa za mtandao huo kuonekana kabla ya kupigwa kabisa marufuku. Zuio (Block) hilo limekuwapo tangu mwaka 2010

Kama utapenda kujaribu kumbloku Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan ingia katika kurasa zao unajaribu uone kama utaweza. Je huu si udikteta flani hivi?

Teknokona

Maandamano Mabaya Yashuhudiwa Ethiopia

$
0
0
Maandamano Mabaya Yashuhudiwa Ethiopia
Takriban watu 2 wameuawa kwenye maandamano nchini Ethiopia.
Zaidi ya watu 600 wamehama wakati wa makabiliano ya siku ya Jumanne katika miji iliyo mashariki mwa nchi

Waandamanaji wanawalaumu polisi kwa kutekeleza mauaji na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu dhidi ya watu wa Oromo.
Serikali imesema kuwa ghasia hizo zimesabaishwa na mzozo wa mpaka kati ya watu wa Oromo na majirani zao walio eneo la Somalia nchini Ethiopia

Serikali imesema kuwa sasa imetuma jeshi kwenda kufanya kile kile ilichokitaja kuwa kutwaa silaha
Mzozo umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa lakini umechaha wiki hii na kugeuka kuwa makabiliano makali.

Mwezi Agosti serikali iliondoa amri ya tahadhari iliyowekwa kufuatia maandamano ya zaidi ya miaka miwili yanayoipinga serikali.

Uamuzi wa Kesi ya Wema Sepetu Octoba 4

$
0
0
Uamuzi wa Kesi ya Wema Sepetu Octoba 4
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji nyumbani kwa Wema Sepetu ifikapo October 4 2017.

Hatua hiyo inatokana na kuwasilishwa kwa pingamizi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kutoka kwa wakili wa utetezi , Peter Kibatala, kwamba kielelezo hicho kina mapungufu kisheria, hivyo kisipokelewe.

Katika hoja zake wakili wa serikali, Constantine Kakula amedai kuwa hati hiyo ipo sahihi, hivyo ipokelewe na Mahakama. Kutokana na maelezo hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi October 4, 2017 kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Mbali ya Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa  na Matrida Abbas ambapo wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Neema Yazidi Kuwashukia Singida United Waongeza Mdhamini

$
0
0
Neema Yazidi Kuwashukia Singida United  Waongeza Mdhamini
Klabu ya soka ya Singida United imeendelea kujiimarisha kiuchumi baada ya kuongeza mdhamini atakayesimamia huduma ya maji katika timu hiyo.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema wanaendelea kukusanya wadau ambao watashirikiana nao kuhakikisha wanaimarisha timu yao ili kuleta ushindani kwenye ligi na hatimaye kuondoa ufalme wa Simba na Yanga.

Singida United itapata huduma ya maji kwa misimu miwili kutoka kampuni ya Bhakresa Food Product. Kwa upande mwingine nyota wa timu hiyo Dany Usengimana amerejea kikosini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda.

Timu hiyo iliyopanda ligi kuu msimu huu inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu bara msimu 2017/18 ikiwa na alama tatu baada ya kushinda mchezo mmoja na kupoteza mmoja.


Ofisa wa Chama cha UDP Ametekwa na Watu Wasiojulikana Mbele ya Mkewe

$
0
0
Ofisa wa Chama cha UDP Ametekwa na Watu Wasiojulikana Mbele ya Mkewe
Ofisa mmoja wa chama cha upinzani cha Union for Peace and Development (UPD), Leopold Habarugira ametekwa na watu wasiojulikana juzi jioni mjini hapa alipokuwa akitembea barabarani na mkewe.

Kwa mujibu wa mkewe, Liberty Nzitonda kiongozi huyo mwenye miaka 54 ambaye ni mweka hazina wa UPD alitekwa na watu wanne, mmoja kati yao akiwa na sare za polisi aliyekuwa na bunduki, wakamweka kwenye gari na kuondoka naye.

“Nina hofu kwa sababu najua kwamba watu wamekuwa wakitekwa hapa nchini kisha miili yao kuonekana baadaye au kupotea kabisa,” Liberty aliliambia shirika la habari la AFP.

Rais wa UPD, Chauvineau Mugwengezo ambaye yuko uhamishoni alisema kutekwa kwa Habarugira “kunafanana na mbinu wanazotumia SNR (Idara ya Usalama wa Taifa)”

Polisi hawakupatikana kuzungumzia tukio hilo.

Habarugira ni mfanyabiashara na mmoja wa wapinzani wachache ambao walikuwa nchini Burundi licha ya mashambulizi dhidi ya wakosoaji wa Serikali. Liberty amesema mumewe aliponea chupuchupu jaribio la kuuawa mwaka 2016.

Rais wa zamani wa chama hicho na msemaji wa UPD aliuawa mwaka 2015. Burundi inakabiliwa na mgogoro kati ya Serikali na wapinzani ambao hutoweka na kuteswa, huku wengi wakilazimika kwenda kuishi uhamishoni.

Ofisa mwingine UPD aliyeuawa katika mazingira ya kutatanisha ni Patrice Gahungu na inadaiwa sababu kubwa ni upinzani wake dhidi ya kusudio la Rais Pierre Nkurunziza kuwania Urais kwa muhula wa tatu kinyume cha Katiba.

Mapacha Walioungana Maria na Consolata Waanza Masomo ya Chuo Kikuu

$
0
0
Mapacha Walioungana Maria na Consolata Waanza Masomo ya  Chuo Kikuu
Pacha walioungana Maria na Consolata wamewasili katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Ruaha (Rucu) kujiandaa kwa masomo ya shahada ya elimu.

Wamesema leo Jumatano kuwa wamefurahi na wanaushukuru uongozi wa chuo na wanafunzi kwa kuwapokea kwa furaha na kuwaandalia mazingira mazuri ya kusomea na kuishi.

Pacha hao wamesema wamewasili mapema chuoni kwa sababu wanataka kujifunza kompyuta ili waendane na spidi ya wanafunzi wengine.

Kwa mujibu wa pacha hao, ndoto yao ya kufika chuo kikuu imetimia, hivyo wanalishukuru shirika la wamisionari la masista wa Consolata kwa kuwalea na kuwapa moyo. Pia wamewashukuru wafadhili waliojitolea kuwalea mpaka walipofikia.

Mtawa Consolata kutoka shirika hilo, amesema wamewawahisha chuoni ili wajifunze kompyuta iwasaidie katika masomo yao.

“Sisi tuliwatunza tukiwa Kilolo, hapa watatunzwa na masista wa Teresia ambao wamewaandalia mazingira mazuri ya kuishi kama walivyoomba. Tumeridhika na tunawatakia kila la heri. Tutakuwa tunakuja kuwaona mara kwa mara,” amesema sista Consolata.

 Pacha hao wameandaliwa vyumba vitatu, jiko, sebule na maliwato inayojitegemea ndani ya chumba chao.

Makamu Mkuu wa Chuo (Fedha na Utawala), Padri Kelvin Haule amesema wanajisikia vizuri kuwapokea pacha hao.

Amesema masomo yao ya elimu ya juu yanaanza mwishoni mwa Oktoba lakini masomo ya kompyuta yataanza kesho.

Mwalimu wa kompyuta katika Chuo cha Rucu, Robert Manase amesema atahakikisha anawasaidia.

“Maria na Consolata wanafahamu kidogo kompyuta lakini kutokana na mazingira yao nitahakikisha wanajua zaidi kwa sababu wameamua kuja mapema kusoma,” amesema.

 

Mobetto Aamua Kumrusha Roho Zari na Mavazi ya Bibi Harusi

$
0
0
Mobetto Aamua Kumrusha Roho Zari na Mavazi ya  Bibi Harusi
Wakati Watanzania wakiendelea kujiuliza kuhusiana na nani ni baba wa mtoto wa Mwanamitindo machachari Bongo, Hamisa Mobetto, amezua tena utata kufuatia picha zinazosambaa mitandaoni zikimuonyesha akiwa katika mavazi mithili ya bibi harusi.

Baada ya picha hizo kutapakaa kila kona, utata ukawa ni, je Hamisa kafunga ndoa? Na kama ni ndoa kaolewa na nani? ni yule yule msanii wa Bongo Fleva au?

Baadhi ya mashabiki wakasema kwamba kama ni ndoa na ameolewa na yule mwanamuziki anayehisiwa kuzaa naye, basi anapendwa sana maana anavyoonekana na alivyopendeza kama siyo mchepuko vile.

Kauli ya ‘kama siyo mchepuko vile’, ni kwa sababu mwanamuziki huyo ni mzazi mwenza na Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’, hivyo kitendo cha Mobetto kuzaa na kufunga naye ndoa, huku akivimba na picha zake kwenye mitandao ya kijamii, basi atakuwa anajiamini kama mmiliki halali wa Mbongo Fleva huyo.

Je Wajua Kwanini Blog Nyingi za Kitanzania Hufa?

$
0
0
Je Wajua Kwanini Blog Nyingi za Kitanzania Hufa?
Blog ni jukwaa maarufu sana la kutolea na kupata taarifa na maarifa mbalimbali kwenye mtandao. Hivi leo mambo mengi tunayoyasoma kwenye mtandao yapo kwenye blog mbalimbali.


Hivyo basi blog ni jukwaa linaloweza kutumiwa kueneza habari, maarifa pamoja na kujiingizia kipato.

Kwa kulifahamu hili watanzania wengi wamekuwa wakianzisha blog lakini zinakufa au hazifanikiwi jinsi walivyotarajia. Ni vyema ukafahamu kuwa yapo mambo yanayosababisha blog nyingi za kitanzania kufa; hivyo soma mambo haya 8 hapa chini.

1. Kuanzisha blog kwa lengo kuu la kupata pesa

 blog nyingi za kitanzania hufa
Kwa nini blog nyingi za kitanzania hufa?
Ni lazima utambue kuwa pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu au kumpa mtu kitu au maarifa yenye manufaa kwake. Wamiliki wengi wa blog wa kitanzania hawana lengo tofauti la kuanzisha blog zaidi ya kulenga kupata pesa. Hii ndiyo sababu mtu anafungua blog leo kesho anaweka matangazo kuwa “tangaza nasi hapa”. Nani atatangaza na wewe wakati una watembeleaji 2 kwa siku? Ni lazima ujue kuwa kupata pesa kwenye blog ni lazima ukubali na uwe tayari kulipa gharama ya kufanya kitu chenye manufaa kwa watu.

2. Ubinafsi

Ubinafsi ni tatizo linaloua mambo mengi mazuri ya watu, yakiwemo blog. Watanzania wengi hawapendi kuwashirikisha watu wengine mawazo yao ili washirikiane kwa pamoja kuyatimiza. Ikiwa wewe una wazo fulani kuhusu blog, kwanini usimshirikishe mtu anayeweza kukusaidia mkatimiza wazo hilo? Vivyo hivyo kwa wanaoshirikishwa wengi hawapendi kufanyia kazi wazo lililoletwa na mtu mwingine. Wengi huliiba au kulinakili au hata pengine kulikwamisha tu.


3. Kulenga tu kupata watembeleaji (traffic) wengi

Wasomaji au watembeleaji hawaji tu kwenye blog yako kwa sababu unataka waje. Ni lazima kuwa na kitu au sababu inayowafanya watembelee blog yako. Ni lazima kabla hujawaza kuongeza watembeleaji kwenye blog yako ukaandaa vitu vyenye manufaa makubwa kwao. Kamwe, injini pekuzi kama Google na Bing havitoweza kuonyesha blog yako kwa watu kama haina kitu cha maana. Kutokana na jambo hili wengi hujikuta wakishindwa kupata watembeleaji kama wanavyotaka na kujikuta wakiacha kuendeleza blog zao.

4. Kunakili machapisho kutoka blog nyingine

Huu ni ugonjwa mkubwa unaozikabili blog nyingi za kitanzania hasa zile za habari. Habari ikishaandikwa kwenye blog moja, utaikuta kila mahali iko hivyo hivyo. Ni wazi kuwa injini pekuzi kama Google inafahamu makala iliandikwa wapi kwanza; hivyo huzichukulia blog nyingine zilizonakili kama blog zinazokusanya matakataka (blong scraping). Kwa njia hii blog yako kamwe haitapata daraja zuri kwenye matokeo ya utafutaji wa Google (Ranking in Search Engine Result Pages – SERPs).

Kama unataka kuona matokeo mazuri ni lazima ukubali  kutoa jasho uandike makala zako mwenyewe ambazo zitakupa manufaa makubwa.

5. Kutokuwekeza gharama stahiki

Kama nilivyotangulia kusema, blog ni kazi inayohitaji kuwekeza gharama fulani ili uweze kuona matokeo mazuri. Ni lazima uwekeze fedha na muda ili uweze kufanikiwa katika kazi hii. Gharama ya muda na kujitoa ndiyo inayohitajika zaidi kwenye blog. Utahitaji muda wa kutosha kuandaa makala (post) zenye tija kwa wasomaji wako. Muda huu utahusisha kutafiti, kupanga, kuandika na kuhariri machapisho yako ili yawe bora kwa wasomaji.



6. Kupuuza maarifa ya usanifu mtandao (web design)

Usanifu mtandao hauwezi kutengwa na blog. Kama unataka kuwa blogger mzuri ni lazima uwe pia unafahamu jinsi ya kutumia programu mbalimbali zitakazokuwezesha kutengeneza blog nzuri ambayo ni rafiki pia kwa wasomaji na vifaa vyao.

Manufaa ya kutengeneza blog nzuri:

Blog yako itaonekana ni rasmi na ya kitaalamu.
Injini pekuzi zitaifurahia na kuiweka juu zaidi kwa wasomaji wengi.
Itakuwa rafiki kwenye vifaa kama simu, tablet na kompyuta
Kama huna maarifa ya kusanifu blog, unaweza ukajifunza kwani ni rahisi. Pia unaweza ukatumia watu na kampuni mbalimbali zinazofanya huduma hiyo kwa bei nafuu.Mwonekano

7. Kukata tamaa na kukosa uvumilivu

Mambo mazuri yana milima na mabonde yake. Hili liko wazi pia kwenye blog; ikiwa unataka kufanikiwa kwenye blog basi ni vyema ukajifunza kutokata tamaa na kuwa mvumilivu. Watanzania wengi wenye blog wanakata tamaa pale wanapoona mambo hayaendi kama walivyopanga, huona kuwa blog hailipi wala haina manufaa na kuachia njiani. Lakini ni muhimu ukatafakari kuhusu tovuti kama Teknokona; je ilianza usiku mmoja? Naamini Ndugu Stephen wa TeknoKona anafahamu milima na mabonde waliyopitia kwa miaka kadhaa hadi kufika hapa ilipo leo. Jambo lolote zuri linahitaji kuvumilia na kufanya kwa moyo.

Blog ya TeknoKona imetimiza miaka 6, ilianzishwa tarehe 26 Septemba mwaka 2011. Soma makala yake ya kwanza hapa -> ‘Karibu Teknokona’

8. Makala duni

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kuwa watanzania wengi ni wavivu na hawapendi kusoma. Labda hili ndiyo sababu hata bloggers wengi wa kitanzania hawako tayari kujifunza jinsi ya kuandika makala nzuri kwa ajili ya wasomaji na injini pekuzi. Ni vyema ukafahamu mambo muhimu ya kuzingatia kwenye kila makala unayoiandika kama vile:

Uchaguzi mzuri wa kichwa cha makala
Mtindo rafiki wa uandishi kwa wasomaji
Matumizi ya picha
Uboreshaji wa injini pekuzi – Search Engine Optimization(SEO) n.k.
SOMA PIA:  Afrika yapata utambulisho wake(".africa") baada ya miongo mitatu
Ni wazi kuwa ukizingatia mambo haya utaweza kuandaa makala au machapisho (post) nzuri ambazo zitakubalika pia kwa wasomaji wako.

Hitimisho

Naamini sasa umefahamu kwanini watanzania wengi hawafanikiwi kwenye blog. Ni wazi kuwa blog ni kazi kama kazi zingine, hivyo inahitaji marifa stahiki na kuifanya kwa dhati. Naamini kama una blog au una mpango wa kuanzisha ya kwako hutokwamishwa tena na mambo tajwa hapo juu.

Je wewe una blog? Ina mafanikio kiasi gani? Au unafahamu sababu nyingine inayoua blog za watanzania? Tafadhali tuandikie maoni na maswali yako hapo chini kisha usisahau kuwashirikisha wengine.

Teknokona

Mchezaji Msuva si wa Mchezo..Awaonyesha Waarabu Mpira Mpaka Wamemchagua Mchezaji Bora

$
0
0
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Difaa Al Jadid, Simon Happygod Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti ndani ya klabu ya Difaa Al Jadid ya nchini Morocco.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania,Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi uliyopita ndani ya timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo inayojulikana kama Botola.

Msuva aliyejiunga na timu hiyo akitokea Dar es salaam Young Africans amekuwa akifanya vyema katika ligi hiyo huku akionekana tegemezi katika upachikaji mabao.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images