Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live

Vigogo Waliokamatwa na Almasi za Bilioni 32.3 Uwanja wa Ndege Wafikishwa Mahakamani Leo

0
0
Waliokamatwa na  Almasi Uwanja wa Ndege Wafikishwa Mahakamani Kisutu
Watuhumiwa waliokamatwa na mzigo wa almasi zenye thamani ya Sh 32.3 bilioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), wamefikishwa mahakamani Kisutu asubuhi leo Ijumaa.

Watuhumiwa hao walikamatwa na mzigo huo ambao ulizuliwa na Serikali ili ufanyiwe tathimini upya kujua thamani halisi baada ya thamani iliyotumika kutiliwa mashaka na Serikali.

Jeshi la polisi liliwashikilia watuhumiwa wanne kwa uchunguzi na hatua nyingine za kisheria baada ya kuzuia mzigo huo.

Mzigo huo wa almasi ulikuwa unatoka mgodi wa Mwadui ambao ni wa ubia kati ya Serikali na kampuni ya Petra Diamonds ya Afrika Kusini kwa hisa 25 za Serikali na Petra  Diamonds hisa 75.



Dereva wa John Heche Avamiwa na Kushambuliwa na Watu Wasiojulikana

0
0
Dereva wa John Heche  Avamiwa na Kushambuliwa na Watu Wasiojulikana
Dereva wa Mbunge John Heche amevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga Mjini Tarime majira ya saa 2 usiku na hali yake siyo nzuri.

Mbunge John Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kutokana na taarifa alizopata kupitia Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri Dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.

Chaurembo: Makosa ya Mwaka 2016 Ndo Chanzo Cha Yusuph Manji Kuvuliwa Udiwani

0
0
Chaurembo: Makosa ya Mwaka 2016 Ndo Chanzo Cha Yusuph Manji Kuvuliwa Udiwani
Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo amesema aliyekuwa Diwani wa Mbagala Kuu (CCM), Yusuf Manji alivuliwa cheo hicho kwa kosa la kutohudhuria vikao sita vya mwaka 2016 bila kutoa taarifa.

Manji aliyekumbwa na mikosi ya kesi tangu mwaka huu uanze jana aliachiliwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akiwa na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kukutwa wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) zenye thamani ya Sh 192.5 milioni.

Kesi hiyo imefutwa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kusema hana nia ya kuendelea nayo.

Mbali na kesi hiyo, Manji pia anakabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya heroin aliyosomewa Februari 17, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Septemba 6, Meya Chaurembo aliwaambiwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa walimwondoa kwenye nafasi ya udiwani kwa kukosa sifa ikiwa pamoja na kutohudhuria mikutano sita ya Baraza na Kamati za  Madiwani.

Hata hivyo, Manji alishaeleza kuhusiana na kutokubaliana na hatua ya kumvua udiwani na mara baada ya kuachiwa huru, aliulizia kuhusu malalamiko yake aliyowasilisha mahakamani hapo kuhusu udiwani wake yako vipiu lakini Hakimu Shaidi alimueleza kwa kuwa yuko huru ataenda kulishughulikia hilo.

Akizungumza jana kwa njia ya simu na gazeti hili, Chaurembo alisema makosa ya Manji yalitendeka mwaka 2016 kabla hata mikosi ya kukamatwa na kufunguliwa kesi haijaanza.

“Ungekuja ofisini kwa Mkurugenzi wa Manispaa uone ‘correspondence’ (barua) tulizokuwa tukiwasiliana na Manji ndiyo ujue kwamba tuliwasiliana naye kabla. Vikao ambavyo Manji hakuhudhuria ni vya mwaka 2016 kabla hata hajakamatwa kwa tuhuma za dawa za kulevya,” alisema Chaurembo.

Alisema mbali na kosa hilo, baadhi ya wananchi wa Kata ya Mbagala Kuu walishawasilisha malalamiko ya kukosa mwakilishi katika Baraza la Madiwani, huku chama chake cha CCM nacho kikiridhia avuliwe udiwani.

Hata alipoulizwa sababu za kumhukumu Manji kwa kosa alilofanya mwaka 2016, Chaurembo huku akimtaka mwandishi kwenda ofisi za Manispaa ya Temeke, alisema walikuwa wakiwasiliana na CCM kwanza.

“Wakati huo tulikuwa pia tunawasiliana na chama chake ambacho kilitupa ‘go ahead’ tuchukue sheria. Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 inataja vikao vya madiwani vinane, vinne vya Baraza na vinne vya Kamati ya Madiwani. Diwani asipohudhuria vikao vitatu bila kutoa maelezo anavuliwa udiwani,” alisema Chaurembo.

“Manji hakuhudhuria vikao na hakutoa taarifa mpaka sisi tulipomtafuta na ndipo akajibu. Tukawasiliana na chama chake wakasema tuendelee na taratibu. Kuhusu kuadhibiwa kwa kosa la mwaka 2016, mtafute Mkurugenzi wa Manispaa atakwambia, mimi kwa sasa niko kijijini kwetu,” alisisitiza Chaurembo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke, Nassib Mbaga alipotafutwa kwa njia ya simu alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu yuko safarini.

“Mimi niko safarini, nenda ofisini utapewa taarifa. Taratibu zote zilifuatwa lakini siwezi kukumbuka ni barua ya lini aliandikiwa au ya lini alijibu,” alisema Mbaga.

Manji aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga alikuwa pia akikabiliwa na kesi ya kuajiri wafanyakazi 25 wa kampuni yake ya Quality Group waliokuwa wakidaiwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

Aprili 19 mwaka huu, wafanyakazi 16 kati ya hao ambao pia ni raia wa India, walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kila mmoja au kulipa faini ya Sh 22 milioni baada ya kupatikana na hatia kwa mashtaka matano yanayowakabili, ikiwemo kufanya kazi nchini kinyume cha sheria na kuzuia maofisa Uhamiaji kutimiza majukumu yao.


Hamrmolapa Amnanga Sarah wa Harmonize Asema ni Kibibi Amshauri Hamonize Atafute Mpenzi Anayeendana Naye

0
0
Hamrmolapa Amnanga Sarah wa Harmonize Asema ni Bibi Amshauri Hamonize Atafute Mpenzi Anayeendana Naye
MSANII wa anayechipukia kwa kasi nchini kwenye miondoko ya Hip Hop, Harmorapa, amefunguka mengi juu ya mpenzi wa mwanamuziki mwenzake, Harmonize, anayefahamika kwa jina la Sarah na mpenzi wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Madam Wema Sepetu, akisema wote ni mabibi yaani watu wenye umri mkubwa.

Akizungumza kuhusu mpenzi huyo wa Harmonize, alifunguka kwamba: “Mimi namuona yule Mzungu wa Harmonize ni bibi tu, hajaopoa demu pale ila kaopoa mpenzi ambaye ni bibi. Yaani ni kama mimi niishi na bibi yangu, ndo Harmonize kama anaishi na bibi mzaa mama yake.”
Harmorapa alishawahi pia kufunguka mengi juu ya yeye kumpenda Wema aliposema yupo tayari kumlipia fedha yoyote ile kwa ajili ya kuishi naye. Lakini, baadaye aligeuka na kumponda mrembo huyo akidai ana umri mkubwa pia.
Mwanamuziki huyo machachari ‘alimshauri’ Harmonize atafute mpenzi anayeendana na umri wake.

Korea Kaskazini Yafyatua Kombora Kupitia Anga ya Japan

0
0
Korea Kaskazini Yafyatua Kombora Kupitia Anga ya Japan
Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido nchini Japan.
Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa kombora hilo limefyatuliwa kutoka maeneo ya karibu na mji mkuu wa Pyongyang.
Mwandishi wa BBC mjini Tokyo anasema kuwa kombora hilo lilipita anga za juu zaidi na kwenda mbali zaidi ikilinganishwa na kombora la awali.
Jaribio hilo linakuja siku chache tu baada ya baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuidhinisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani Rex Tillerson ametoa wito kwa China na Urusi kuchukuwa hatua za moja kwa moja dhidi ya Pyongyang, huku waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akitaja jaribio hilo la hivi punde kuwa ni kitendo cha kuudhi.
"China huiuzia Korea kaskazini mafuta yake huku Urusi likiwa ndio taifa lililowaajiri raia wengi wa Korea kaskazini.
China na Urusi lazima zionyeshe kwamba zimechoshwa na hatua ya Korea Kaskazini kuendelea kufanyia majaribio makombora yake kwa kuichukulia hatua ya moja kwa moja.
Dakika chache baada ya ufyatuzi huo Korea Kusini ilifyatua makombora mawili ya masafa marefu baharini katika hatua ya kuionya Korea Kaskazini kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.
Rais Moon Jae-in alifanya kikao cha dharura na kuonya kwamba kombora hilo litasababisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea kaskazini.
Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa jaribio hilo la hivi karibuni ,likiwa la kwanza tangu vikwazo dhidi ya Korea kaskazini kuimarishwa wiki iliopita lilifanyika katika eneo la Sunan Kaskazini mwa Pyongyang.
Na kama kombora la hapo awali, hili la sasa pia lilipitia katika anga ya kisiwa cha Japan kilichopo kaskazini mwa taifa hilo cha Hokkaido na kuanguka katika bahari ya pacific.
Ving'ora vililia katika eneo hilo vikitoa tahadhari kwa raia kujificha.
Kulingana na makadirio ya awali, kombora hilo lilirushwa juu zaidi ya lile lililorushwa mnamo Agosti tarehe 29 ambalo Pyongyang ilionya ni operesheni yake ya kwanza ya kijeshi katika eneo la Pacific.
Waangalizi wanasema kuwa kombora hilo ni la masafa ya wastani , ijapokuwa maafisa wa Japan wanasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba ni kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ICBM.
Eneo la Guam linalomilikiwa na Marekani katika bahari ya Pacific ambalo Korea Kaskazini imeonya kulishambulia liko kilomita 3,400 kutoka Pyongyang hivyobasi linaweza kufikiwa na kombora hilo.

Natamani Kuongea Hali ya Usalama Nchini na Mashambulio ila Nahofia Usalama Wangu- Ney wa Mitego

0
0
Natamani Kuongea Hali ya Usalama Nchini na Mashambulio ila Nahofia Usalama Wangu- Ney wa Mitego
Msanii Ney Wamitego kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu hali ya usalama ilivyo hapa nchini kufuatia matukio ya mauaji ya watu mbali mbali, na shambulio la risasi la Tundu Lissu ambalo limetikisa nchi nzima.

 Ney amesema ingawa wasanii ndiyo watu ambao wakipaza sauti zao zinaeleweka kwa wengi hata wasiofuatilia siasa, lakini ameona bora ayaache masuala hayo kwa wenyewe wanasiasa kutokana na uoga alionao.
Ney ameendelea kwa kusema kwamba anatamani kuongea lakini kutokana na hali ilivyo kwa sasa anahofia usalama wake, maana mpaka familia yake inamkalisha chini kumuonya na kuamua kukaa kimya, na kuwaachia wanasiasa waendelee kupambana wenyewe

Ripoti ya Shambulio la Tundu Lissu Yaota Mbawa Kamati ya Bunge Yashindwa Kuwasilisha

0
0
Ripoti ya Shambulio la Tundu Lissu Yaota Mbawa Kamati ya Bunge  Yashindwa Kutoa Ripoti
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge imeshindwa kuwasilisha ripoti juu ya shambulio la risasi la Mbunge wa Sindida Mashariki Tundu Lissu, ambayo ilitakiwa kuwasilishwa leo kabla ya Bunge halijaghailishwa.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Adadi Mohamed Rajabu ambaye ni Mbunge wa Muheza kwa kudai muda waliopewa kukamilisha ripoti hiyo ni mdogo hivyo hawakuwahi kukamilisha.

Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama ya Bunge inatarajiwa kukutana kuanzia kesho ili kujadili na kuiwasilisha ripoti hiyo katika bunge  lijalo litakaloanza mwezi Novemba 2017.
Ikumbukwe kwamba baada ya kutokea tukio la kushambuliwa kwa risasi Tundu Lissu, Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe aliwasilisha hoja ya kulitaka bunge liunde kamati maalum ya kuchunguza tukio hilo ili iweze kubainika aliyefanya tukio hilo, na Spika Mhe. Job Ndugai alikubali na kupitisha hoja hiyo.

Hali ya Lissu Inaimarika Yale Yaliokuwa Yanatishia Uhai Wake Yamepungua kwa Kiasi Kikubwa- Mbowe

0
0
Hali ya Lissu Inaimarika Yale Yaliokuwa Yanatishia Uhai Wake Yamepungua kwa Kiasi Kikubwa- Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa ile hofu iliyokuwepo Mbunge Tundu Lissu aliyeshambuliwa na risasi kuwa huenda angepoteza maisha imezidi kupungua na kudai madaktari wanatoa matumaini makubwa hali yake inaimarika.

Freeman Mbowe amesema hayo leo kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa Mbunge huyo sasa anaweza kuzungumza japo anaendelea kupatiwa matibabu na kudai pia ataendelea kufanyiwa upasuaji mwingine, aidha Mbowe amewataka wananchi kutosikiliza taarifa za watu wengine kuhusu hali ya mgonjwa na kusema taarifa rasmi juu ya hali ya mgonjwa itatolewa na wao ambao wapo na mgonjwa Nairobi Kenya.

"Kuhusu hali ya Mhe. Lissu, kwa sasa ile hofu ya kupoteza maisha imezidi kupungua, madaktari sasa wanatoa matumaini makubwa kuwa hali yake sasa inaimarika. Yale yote yaliyokuwa yanatishia pengine uhai wake, usalama wake, yamepungua kwa kiasi kikubwa na madaktari wanatoa matumaini makubwa. sasa hivi, Mhe Lissu anaweza kuzungumza, nimezungumza nae, japo bado anapatiwa matibabu na ataendelea kwenda 'theatre' kwa ajili ya upasuaji na kutibu majeraha mbalimbali aliyoyapata. Anazungumza na anatoa salamu kwa Wanaafrika Mashariki, anatoa salamu kwa Watanzania, niseme tu kwamba sisi ambao tuko nae muda wote ndo tunajua hali halisi ya mgonjwa" alisema Freeman Mbowe

Mbali na hilo Freeman Mbowe amedai kuwa Mbunge huyo hana athari zozote zile kwenye kifua chake kama ambavyo baadhi ya taarifa zinasema kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kudai Mwanasheria Mkuu huyo wa CHADEMA yupo imara.

"Mhe. Lissu hana 'infection' ya kifua, kwa sasa yuko vizuri yuko imara, bado ni 'critical' lakini bado yuko stable. Tuendelee kumuombea kila siku, wakati wote, aweze kupona kwa haraka na kuruhusiwa kutoka hospitali" alisema Mbowe

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa kwenda jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyopata, ambapo mpaka sasa yuko huko kwa matibabu.



Mlipuko Umeripotiwa Kutokea Kwenye Treni Nchini Uingereza

0
0
Mlipuko Umeripotiwa Kutokea Kwenye Treni Nchini Uingereza
Ripoti kutoka nchini Uingereza zinasema kuwa mlipuko umetokea kwenye treni zinazokwenda chini kwa chini katika eneo la Kusini magharibi mwa mji mkuu wa London.

Abiria katika kituo cha wazi cha Parsons Green wamesema katika mitandao ya kijamii kwamba baadhi ya watu wamepata majeraha ya uso na kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa wakati watu walipokuwa wakijaribu kutoka katika treni hiyo.


Mashahidi wameelezea kuona abiria mmoja akiwa na majeraha ya uso.
Wengine wamesema kuwa kulikuwa na wasiwasi huku abiria wakitoka ndani ya treni hiyo katika kituo cha treni cha Parsons Green.

Huduma ya ambalensi inasema kuwa imetuma kikosi cha kukabiliana na majanga katika eneo hilo.
Mtangazaji wa BBC Riz Lateef aliyekuwa katika kituo hicho cha treni akielekea kazini alisema: kulikuwa na wasiwasi mwingi huku watu wakitoka ndani ya treni hiyo wakihofia maisha yao huku wakisema kulikuwa na mlipuko.

Wengi walipata majeraha ya kukatwa wakijaribu kutoroka eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Sophie Raworth anasema kuwa alimuona mwanamke mmoja akiwa na majareha ya moto usoni na miguuni.

BREAKING NEWS: Askofu Gwajima Amefutiwa Kesi ya Kushindwa Kutunza Siraha

0
0
BREAKING NEWS: Askofu Gwajima Amefutiwa Kesi ya Kushindwa Kutunza Siraha
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefutiwa kesi ya kushindwa kutunza silaha baada ya mahakama kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo, na kuamuru arudishiwe mkoba wenye silaha yake.

Chadema Kufanya Maombi ya Kitaifa ya Kumuombea Tundu Lissu Jumapili

0
0
Chadema Kufanya Maombi ya Kitaifa ya Kumuombea Tundu Lissu Jumapili
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA taifa (BAVICHA), Patrick ole Sosopi amefunguka na kusema wao kama chama wameamua kuwakutanisha wanachama wao mbalimbali wa imani tofauti kwa ajili ya kufanya maombezi ya kitaifa kumuombea Mbunge Lissu.

Akiongea na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya CHADEMA, Sosopi amesema kuwa jambo hilo halihusiani na mambo ya kisiasa bali wameamua kukutana kwa lengo la kuombea taifa katika mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kuliombea jeshi la polisi ili wafanye kazi zao kwa kufuata misingi ya haki na usalama zaidi.

"Madaktari wamefanya kazi kubwa sana kuendelea kuokoa maisha ya Tundu Lissu na sisi tumekaa na kufikiri kwamba ni bora tukutane ili kwa pamoja tuweze kufanya maombezi, tunajua chama chetu kina kila aina ya watu wenye imani mbalimbali ya dini, hivyo Baraza tumeandaa maombo maalum kwa ajili ya Mhe. Tundu Lissu na kuita 'Tanzania National youth Prayer for Lissu' tutafanya maombi hayo ya kitaifa na kutoa wito kwa watu wote, jambo hili si la kisiasa na wala halina sura ya kisiasa " alisisitiza Sosopi

Aidha Sosopi amesema kuwa wanategemea kufanya maombezi hayo siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam maeneo ya Sinza Darajani viwanja vya TP na kudai kwamba mpaka sasa wamefanya maandalizi yote ikiwa pamoja na kuandika barua kwa taasisi zote za dini kuweza kufika kwa ajili ya maombezi hayo.

Mbali na hilo Sosopi amedai kuwa kwa kuwa wanaamini jambo hilo halina sura ya kisiasa hivyo wanatemea kuona jeshi la polisi nchini likifika kwa lengo la kutoa ulinzi kwa raia ambao watafika kwa ajili ya maombezi hayo na si vinginevyo.

"Naomba jambo hili lisitafsiriwe vibaya sisi kama viongozi wa kisiasa tutakwenda pia kusikiliza maombi na si kwenda kuongea chochote, tutakwenda uwanjani kwa sababu sisi kama CHADEMA hatuna kanisa wala msikiti kufanya maombezi hayo ndiyo maana tunakwenda uwanjani hapo, tunaamini hapo ni sehemu sahihi kuweza kuwakutanisha watu wetu wote bila kujali itikadi zao" alisema Sosopi

Watathimini wa Almasi Washtakiwa kwa Kuitia Serikali Hasara ya Bilioni 2.4

0
0
Watathimini wa Almasi Washtakiwa kwa Kuitia Serikali Hasara ya Bilioni 2.4
Watathmini wa Serikali wa Madini ya Almas wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Bilioni 2.4.

Vigogo hao ni Mkurugenzi wa Tathmini wa Madini ya Almas, Archard Kalugendo mwenye umri wa miaka 49 na Mtathmini wa Madini, Edward Rweyemamu mwenye umri wa miaka 50.

Kwa pamoja wamesomewa makosa yao na Wakili wa Serikali, Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.

Kadushi amedai washtakiwa wanakabiliwa na kosa moja la kuisababishia Serikali hasara, ambapo kosa hilo wamelitenda kati ya August 25 na 31, 2017 katika maeneo ya Dar es Salaam na Shinyanga wakidaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Kimarekani, Milioni 1,118,291.43 ambazo ni sawa na Tsh. Bilioni 2.4.

Baada ya kuelezwa Kadushi amedai upelelezi upo mbioni kukamilika, ambapo Hakimu Mwijage amesema Mahakama hiyo haina mamlaka na maombi ya dhamana wapeleke Mahakama Kuu, hivyo washtakiwa hawaruhusiwi kujibu.

Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko amedai amekaa na wateja wake kwa muda mrefu tangu walipokamatwa na anaamini upelelezi umefanyika mkubwa na sehemu iliyobaki ni ndogo sana, haiwezi kuchukua muda mrefu na wanaomba upelelezi ukamilike haraka.

Baada ya hapo kadushi amedai watahakikisha upelelezi unakamilika kwa wakati.

Hakimu Mwijage amesema upelelezi ukamilike ili mwenye hatia afungwe na asiyekuwa na hatia aachiwe, ambapo ameahirisha kesi hadi September 29, 2017.

Ndugai Awafunda Wabunge Wanaokaa Bar Hadi Saa Nane za Usiku Na Kuwataka Kuwa Makini na Usalama Wao

0
0
Ndugai Awafunda Wabunge Wanaokaa Bar Hadi Saa Nane za Usiku Na Kuwataka Kuwa Makini na Usalama Wao
 Spika wa Bunge, Job Ndugai amewatadharisha wabunge kuwa makini na usalama wao mahali popote wanapokwenda kufuatia matukio mengi ya uhalifu nchini.

Akizungumza muda mfupi leo Ijumaa kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, Ndugai aliwataka wabunge kutokaa sana katika mabaa.

“Yaani tuchukue hatua tu katika maisha yetu kama mnavyosikia matukio ni mengi katika nchi yetu. Ni vizuri usalama unaanza na wewe mwenyewe kwanza,”amesema.

Amesema vyombo vya usalama vinavyowalinda vinakuwa vinaongezea kidogo na kuwataka kutazama nyendo zao za namna ambavyo wanaishi.

“Kwa wale tuliozoea sana saa 7 ndio tunarudi nyumbani  basi tuanze kurudi mapema kidogo. Lakini pia tuangalie usalama wa familia zetu na tuwaambie wapigakura naona siku hizi watoto wanapotea, watoto wanauawa,”amesema.

Amewataka wabunge kuwapelekea huo ujumbe kuwa wawe makini na watoto wao wakati wa kwenda shule na maeneo mengine kwa kuhakikisha wanajua mtu anayewapeleka shule na kuwachukua.

“Hayo mambo yanayofanana na hayo. Ushauri ni wa ujumla tu,”amesema.

Aliwataka wabunge kuendelea kumuombea Tundu Lissu na wale watakaopata nafasi ya kwenda kumuona jijini Nairobi wampelekee ujumbe.

Amesema pia wabunge wawaombee wenzao ambao wamekwenda kumuuguza mbunge huyo lakini wanatukana kwa sababu hawajui watendalo.

Ushauri huo umekuja siku chache baada ya Lissu kujeruhiwa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.



Safari Za Treni Dar- Mwanza na Kigoma Zasitishwa

0
0
 Safari Za Treni Dar- Mwanza na Kigoma Zasitishwa
Kampuni ya reli Tanzania TRL imetangaza kusitisha safari zake za treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda mikoa ya Mwanza na Kigoma kwa tarehe 19 na 21 kutokana  na matengenezo makubwa ya daraja katika njia ya treni mkoani Morogoro.

Kaimu Naibu Mkurugenzi wa TRL Bwana Focus Makoye amesema safari zitaanza mara baada ya matengenezo hayo tarehe 21 Septemba 2017 na kwamba kati ya abiria 2000 wataathirika kutokana nakusitishwa kwa safari hizo.

FIFA Imefanya Mabadiriko ya Mashindano ya Kombe la Dunia

0
0
FIFA Imefanya Mabadiriko ya  Mashindano ya Kombe la Dunia
Shirikisho la soka la kimataifa FIFA limebadili utaratibu wa namna ya kupanga makundi katika fainali za Kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

FIFA imesema wakati wa kupanga makundi itazingatia viwango vya soka ambavyo huwa inavitoa kila mwezi kwa timu za taifa ambapo sahani (pot) zote 4 zitapangwa kulingana na viwango kwenye orodha ya FIFA. Awali sahani ya kwanza pekee ndio ilikuwa inazaingatia viwango hivyo lakini sasa itakuwa ni kwa pot zote.
Pia FIFA imethibitisha kuwa itatumia viwango itakavyotoa mwezi Oktoba. Hii inamaanisha sahani ya kwanza huenda ikawa na timu za Ujerumani, Brazil, Ubeligji, Argentina, Ureno pamoja na wenyeji Urusi, lakini hadi sasa Brazil na Ubeligji pekee kwenye nchi za juu ndio zimefuzu.

Kuna dalili kubwa ya mataifa ya Uingereza, Hispania na Ufaransa yakawa katika sahani ya pili endapo yatafuzu. Afrika Mashariki katika kuwania kufuzu inawakilishwa na Uganda pekee ambayo ipo nafasi ya pili kwenye kundi E ikiwa na alama 7 nyuma ya Misri yenye alama 9. Uganda inashika nafasi ya 71 kwenye viwango vilivyotolewa jana na FIFA wakati Tanzania ikiwa nafasi ya 125.

Mahakama Yamuachia Huru Gwajima na Kuamuru Arudishiwa Mkoba Wake Wenye Siraha

0
0
Mahakama Yamuachia Huru Gwajima na Kuamuru Arudishiwa Mkoba Wake Wenye Siraha
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefutiwa kesi ya kushindwa kutunza silaha baada ya mahakama kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo, na kuamuru arudishiwe mkoba wenye silaha yake.

Gwajima na wenzake watatu wamefutiwa mashtaka hayo mbele ya hakimu mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkehe.

Katika kesi hiyo ambayo Gwajima alikuwa akisimamiwa na Wakili Peter Kibatala, washtakiwa hao walikuwa wakidaiwa kuwa Machi 29, 2015 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A walikutwa wakimiliki Bastola aina ya Berretta yenye namba ya siri CAT 5802 bila ya kuwa na kibali toka kwa mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 32 (1) na cha 34 (1) (2) na(3) cha sheria ya Silaha na Milipuko sura ya 223 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.
Pia, walidaiwa kuwa siku ya tukio washtakiwa hao pia walikutwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya Shotgun.

Polisi Kula Sahani Moja na Wanaofanya Vitendo vya Uhalifu wa Makosa ya Mitandaoni

0
0
Polisi Kula Sahani Moja na Wanaofanya Vitendo vya Uhalifu wa Makosa ya  Mitandaoni
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa amewataka wananchi kwa ujumla wanaofanyiwa vitendo vya uhalifu mitandaoni wasiende TCRA bali wanapaswa kutoa taarifa katika jeshi la polisi.

ACP Mwakalukwa amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza katika mkutano wa pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu suala zima la uhalifu wa makosa ya mitandao ambapo kwa sasa limeshika kasi kubwa

"Chochote kinachofanyika ambacho ni kosa jinai nawaomba msiende Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa watoa huduma wa mitandao ya simu mbalimbali wala katika vyombo vya kutolea habari bali unapaswa uje katika kituo cha polisi utoe taarifa zako kama ni kosa la jinai kwa sababu mkienda huko uchunguzi utakuwa shida kwa maana wewe mwenyewe utaweza kusababisha hata yule aliyekutendea uhalifu atoroke", amesema ACP Mwakalukwa

Pamoja na hayo, ACP Mwakalukwa ameendelea kwa kusema "Kutokana na kukua kwa teknolojia vitu vingi vimekuwa vikifanyika 'online' kwa hiyo hii mitandao ya kijamii imeonekana ni muhimu sana kwenye maendeleo, lakini pia imebadilisha mbinu ya kufanya uhalifu katika mitandao ya kijamii kwa kutumiwa na baadhi ya watu kutapeli, hata kutishia kuua, hivyo jeshi la polisi limejipanga kwa ajili ya kushughulikia makosa ambayo yanatokana na mtandao", amesema Mwakalukwa.

Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa TCRA, Thadayo Ringo amesema analishukuru jeshi la polisi kwa kuweza kuwasaidia katika kuwatatulia changamoto mbalimbali hasa za kiusalama huku akiwataka wananchi watakaopata matatizo katika mtandao kwenda kutoa taarifa polisi ili waweze kuwasaidia kabla ya kufika kwao.

Wazee wa Kigoma Wamjia Juu Ndugai Wamtaka Kuacha Kiburi na Kusimamia Misingi ya Kuwaunganisha

0
0
Wazee wa Kigoma Wamjia Juu Ndugai Wamtaka Kuacha Kiburi  na Kusimamia Misingi ya Kuwaunganisha
Wazee wa Kigoma wakiwakilishwa na Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee ya Chama cha ACT Wazalendo, Alhaj Jaffar Kasisiko wamesikitishwa na kauli aliyotoa Spika Ndugai kuwa anaweza kumzuia Zitto Kabwe asiongee chochote mpaka ubunge wake utakapokwisha.

Wazee hao wanasema kitendo cha Spika kumzuia Zitto Kabwe kuongea bungeni ni sawa na kuwazuia wao wasiongee na shida zao zisiweze kutatuliwa na kudai inaonekana hiyo kauli imeshafanyiwa kazi na kitendo cha kumwita Zitto kwenye Kamati ni sawa na kupoteza muda tu na kudai jambo hilo halimtendei haki kijana wao Zitto Kabwe na wao wenyewe.
Aidha wazee hao wamemtaka Spika Job Ndugai na viongozi wengine wasiwe na kibri na watazame mambo ambayo yanawaonganisha kwa pamoja.



Waziri Mkuu Aahirisha Bunge Hadi Novemba 7 Mwaka Huu

0
0
Waziri Mkuu Aahirisha Bunge Hadi Novemba Mwaka Huu
WAZIRI Mkuu, Kasimu Majaliwa akitoa Hoja ya Kuahirisha Bunge mjini Dodoma leo amefafanua kuhusu hali ya wakulima na changamoto wanazokumbana huku akielezea mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano inavyopambana na changamoto kwa lengo la kukuza kipato cha mkulima.

Majaliwa amelieleza Bunge kuwa serikali imechukua jitihada za dhati za kuwataftia masoko wakulima pamoja na kupunguza tozo la kodi mbalimbali kwenye mazao.

Akizungumzia masuala ya elimu, Waziri Mkuu amewasihi wazazi na wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kukuza sekta hiyo. Ambapo Sekta Afya na Hatua ya Kimaendeleo iliyopiga katika sekta hiyo na jinsi wanavyo kabiliana na changamoto zote wanazo kumbana nazo.

Majaliwa pia ameeleza kuwa serikali inafanya jitihada kubwa kuwezesha sekta ya vijana na hususani kuwasadia katika kupata ajira.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Majaliwa aliwashukuru wabunge wote wa bunge hilo tukufu na kutoa hoja ya kuahilisha Mkutano wa Nane wa Bunge hadi Novemba 7, 2017.

Tanzania Yashangazwa na Uchunguzi wa UN Kuhusu Korea Kaskazini

0
0
Tanzania Yashangazwa na Uchunguzi wa UN Kuhusu Korea Kaskazini
Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, waziri wa mambo ya nje Dkt. Augustine Mahiga, amesema licha ya uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mnamo mwaka 2014, Tanzania imepunguza kabisa uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo.
Waziri Mahiga ameongeza kusema kuwa, uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla ya vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa.

Waziri huyo amesema anaelekea katika mkutano wa kawaida wa Umoja wa Mataifa, ambapo atatumia fursa hiyo kujibu tuhuma hizo kwa Baraza la Usalama
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live




Latest Images