Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Diamond Platnumz...Sifikirii Kumuacha Zari..na Ikitokea Kaniacha Nitapiga Magoti Mpaka South Africa

0
0
Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa alishaongea na Zari na kumwambia kuhusu kuwa na mtoto na Hamissa Mobetto na amemsamehe, na ikitoa Zari Akamuacha basi atampigia magoti kuanzia Tanzania mpaka South Africa kumuomba msamaha...

Msukuma Apandishwa Kizimbani kwa Tuhuma za Kuratibu Vurugu Katika Mgodi wa GGM

0
0
Msukuma Apandishwa Kizimbani kwa Tuhuma za Kuratibu Vurugu Katika Mgodi wa GGM
Mbunge wa Geita Joseph Musukuma leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama Hakimu Mkazi Geita, kujibu tuhuma zake zinazomkabili, baada ya kushikiliwa na polsi tangu jumapili ya wiki iliyopita.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Tlevision, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo, amethibitisha kumpeleka Mahakamani mbunge huyo, ambaye anatuhumiwa kuhusika na kuratibu vurugu katika mgodi wa GGM mkoani humo.
"Wamepelekwa Mahakamani asubuhi hii", amesikika Kamanda Mwabulambo akisema
Mbunge Joseph Musukuma pamoja na baadhi ya wadiwani na wananchi, walikamatwa na polisi kwa kufunga njia inayoeleka kwenye mgodi wa GGM na kuleta vurugu, kushinikiza mgodi huo kulipa dola milioni 12.

Waziri Maghembe Awajia Juu Wliolima Ndani ya Hifadhi

0
0
Waziri Maghembe Awajia Juu Wliolima Ndani ya Hifadhi
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ameagiza wote waliolima ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha kinyume cha sheria waondoe mazao na kusitisha shughuli zozote za kibinadamu kwenye eneo la hifadhi.

Profesa Maghembe ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), kupitia hifadhi hiyo kuhakikisha hilo linatekelezwa.

"Ni marufuku mtu yeyote kuonekana akilima katika eneo hili, wekeni askari hapa, atakayeonekana piga pingu, hatuwezi kushuhudia watu wanalima ndani ya hifadhi tukae kimya, ni lazima tuchukue hatua. Watangaziwe na wapewe muda wa kuondoa mazao yao, ndani ya siku 30 au 40 wawe wameshaondoka," ameagiza waziri.

Agizo hilo amelitoa akiwa ziarani katika hifadhi hiyo iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha kukagua shughuli zinazofanywa na hifadhi, ikiwemo maeneo yenye mgogoro kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi.

Awali, akiwasilisha taarifa kwa waziri, Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Steria Ndaga amesema eneo hilo ambalo pia linajulikana kama shamba namba 40 na 41 limekuwa na mgogoro tangu mwaka 1990 baada wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado kulivamia wakitoa hoja kadhaa, ikiwemo madai kuwa ni maeneo yao ya asili waliyoyamiliki tangu zamani.

Amesema hoja nyingine wanazozitoa wananchi ni kuwa, walipewa mashamba hayo na Serikali wakati wa operesheni ya uanzishwaji wa vijiji mwaka 1975 na 1976.

Pia, wanadai hawakushirikishwa kwenye mchakato wakati wa ugawaji wa mashamba hayo na Tanapa haina hati miliki ya mashamba hayo.

Ngada amesema hoja hizo zinakinzana na ukweli kuwa, shamba hilo lilimilikishwa kwa Tanapa mwaka 1980 baada ya kutolewa tangazo kwa wadau wanaoweza kuliendeleza kutokana na mwekezaji wa awali kushindwa kuliendeleza, hivyo kufutiwa hati miliki na Rais mwaka 1979.

 Amesema wadau kadhaa waliomba umiliki wa shamba hilo ikiwemo Halmashauri ya Kijiji cha Olkung'wado, lakini Kamati ya Ushauri ya Ardhi ya Mkoa wa Arusha ikaishauri Serikali mashamba hayo yamilikiwe na Tanapa, hivyo waliandikiwa barua ya kukubaliwa kupewa shamba na Idara ya Ardhi Mkoa.

Hata hivyo, amesema katika kikao cha wadau wa uhifadhi kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mei 11 iliazimiwa na kuridhiwa na Bodi ya Wadhamini ya Tanapa kuwapa wananchi eka 366 ya shamba hilo na kubakiwa na eka 600.

“Kikao pia kiliridhia Tanapa kuweka vigingi vya mpaka katika shamba hilo, Mei 14 zoezi hilo lilianza na jumla ya vigingi 26 viliwekwa,” amesema.

Hata hivyo, amesema kumekuwepo taarifa kuwa baadhi ya wanakijiji wa Kitongoji cha Momella walifungua kesi mahakamani wakidai Kijiji cha Olkung'wado kimenyang'anywa ardhi na Tanapa.

Amesema Serikali ya kijiji imekana kwa maandishi kuhisika na ufunguzi wa kesi hiyo ikisema imefunguliwa na mtu binafsi.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Dk Allan Kijazi amesema maagizo yote aliyoyatoa waziri ya kusitisha shughuli za kibinadamu ndani ya eneo hilo yatafanyiwa kazi na atapewa mrejesho wa utekelezaji wake.

Majaji Wametakiwa Kuwa Makini na Matumizi ya Mitandao ya Kijamii

0
0
Majaji Wametakiwa Kuwa Makini na Matumizi ya Mitandao ya Kijamii
Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, ametoa angalizo kwa Majaji wafawidhi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii katika mahusiano pamoja na kutoa michango kwenye mitandao hiyo juu ya jumbe zisizofaa.

Jaji Mkuu ametoa  angalizo hilo wakati akifunga mkutano wa Majaji wafawidhi wa kanda nchini, uliofanyika Jijini Arusha
"Katika suala la matumizi ya mitandao, kuweni makini. Msi- like picha ambazo hazina maadili au kuchangia kwa kutoa maoni katika mitandao ya kijamii," alisema.

Aidha, amewataka kuwa makini na ndugu au jamaa wanaowatembelea, akisema baadhi yao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali ya kijinai.
Aliwataka majaji hao kujenga tabia ya kupenda kujisomea na kuelewa mabadiliko yanayofanywa na Bunge kwa kurekebisha sheria ili kuweza kugundua makosa mbalimbali yanayofanywa na Mahakama za chini na wafundishane namna ya kuboresha hukumu zinazotolewa ili kupunguza mrundikano wa mashauri.

"Ni vizuri kuelewa mabadiliko yanayofanywa na Bunge wakati wa kurekebisha sheria, kazi na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa katika kufungua mashauri," alisema.
Kuhusu migongano kati yao na vyombo vingine vya serikali, aliwataka kutambua mipaka ya vyombo hivyo na wao watambue mipaka yao huku akisisitiza kwamba kila chombo kikitambua mipaka yake wataheshimiana na hakutakuwa na mgongano katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mkutano huo wa majaji wafawidhi ulikuwa mahususi kutathmini na kuweka mikakati ya kumaliza mrundikano wa mashauri 2,198 yaliyopo Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, kati yao mengine yamekaa zaidi ya miaka 10.


Viwanda Zaidi ya 900 Htarini Kufutiwa Hati ya Mliki

0
0

Viwanda Zaidi ya 900 Htarini Kufutiwa Hati ya Mliki
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama amesema wameanza utaratibu wa kufuta hati miliki ya ardhi katika viwanja zaidi ya 900 ambavyo wamiliki wake wameshindwa kuviendeleza kwa zaidi ya miezi 36.

Mshama amesema jana Jumatatu kuwa ameshawasilisha barua kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya kusudio la kuanza mchakato wa kufuta miliki katika viwanja 189 kwa ajili ya viwanda na taasisi mbalimbali.

Pia, miliki katika viwanja 754 vya watu binafsi baada ya wamiliki kushindwa kutekeleza maagizo waliyopewa ya kuviendeleza na wengine anuani zao hazijulikani.

Amesema hayo alipozungumzia utekelezaji wa agizo alilotoa mwezi uliopita kwa wawekezaji na watu binafsi kutumia siku 30 kuendeleza maeneo yao na kama kuna tatizo wafike kujieleza ili kupata muafaka.

Mkuu wa wilaya amesema waliotekeleza agizo hilo ni wamiliki wachache.

Wilaya ya Kibaha ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Pwani inakabiliwa na changamoto ya wawekezaji, taasisi  na watu binafsi kuhodhi maeneo na kutoyaendeleza hivyo kusababisha kuwepo mapori.


Waliooana kwa Miaka 75 Wafariki Siku Moja

0
0
Waliooana kwa Miaka 75 Wafariki Siku Moja
Wanandoa walio oana kwa miaka 75 wamefriki siku moja wakiachana kwa saa tano tu, ikiwa ni mwezi mmoja tangu washerekee ndoo yao wa miaka 75.
George mwanajeshi wa zamani na Jean Spear walikutana mwaka 1941 karibu na London wakati George akitoa huduma zake nchini Uingereza wakati wa vita vya pili vya dunia.
Wawili hao walifariki kwenye hospitali ya Ottawa siku ya Ijumaa baafa ya Bi Spear 94 kulazwa hospitalini.

Alipewa tuzo la juu zaidi la Uingeza mnamo mwaka 2006.
Bi Spear na mumewa wa miaka 95 walikutana na Duke na Duches wa Cambridge wakati waliitembelea familia ya kifalme mwaka 2011.

Bw. Spear alilazwa katika hospitali ya Queensway Carleton siku ya Jumatano, siku moja baada ya mke wake kulwzwa, na kulala usingizi mkubwa.
Wahudumu wa hospitali walijaribu kumhamisha Bw Spear kwenda chumba alichokuwa mkewe, lakini Bi Spear akafariki alipokuwa akilala siku ya Ijumaa mwendo wa 04:30 kabla ya hilo kufanyika.

Bwana Spear naye alifarki muda mfupi baadaye mwindo wa saa 09:45.
Wameacha watoto wawili wakubwa Heather na Ian.

Gigy Money Atoa Somo kwa Wanawake Utaowasaidia Kutoka Kimaisha

0
0
Gigy Money Atoa Somo kwa Wanawake  Utaowasaidia Kutoka Kimaisha
Msanii Gigy Money amewausia wasichana ambao wameingia kwenye 'game' ya bongo fleva na kuwataka waache kuimba vitu vigumu na badala yake watafute vyepesi ili waweze kuwafikia mashabiki zao kwa wepesi kama alivyofanya yeye.

Gigy Money amesema hayo baada ya kuwepo wimbi kubwa la wasanii wapya wakijikuta kutumia vitu vingi katika kuimba na mwishowe kutofikisha malengo yao waliyoyaweka kwa wakati huo.

"Nitoe ushauri kwa wasichana ambao wanaimba, unajua wasichana wengi wana vipaji vya kuimba lakini wanafeli.  Ukishajijua huwezi kuimba acha kuimba vitu vingi, huna uwezo wa kuimba alafu mambo unayoimba mlolongo kibao, vingereza, sijui nini utajikuta unafeli. Sasa neno kama 'papa' lipo uswahilini, rahisi kwa watu kuelewa", amesema Gigy Money.

Hivi karibuni Gigy Money ameachia wimbo wake wa 'papa' ambao unazidi kufanya vizuri mtaani, na kusema kwamba lengo lake lilikuwa kuwafikia watu wa rika lote, na anahisi amefanikiwa katika hilo.

Sikufikiria Kama Ntaweza Kuumizwa na Kupata Uchungu Nipo Kama Mwendawazimu- Zitto Kabwe

0
0
Sikufikiria Kama Ntaweza Kuumizwa na Kupata Uchungu Nipo Kama Mwendawazimu-  Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Mh. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwamba uchungu anaoupata baada ya nyumba yake ya kwanza kuungua moto umemfanya kuwafikiria wananchi wanaobomolewa nyumba zao bila fidia.

Zitto amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya kutazama nyumba yake ya kwanza iliyoteketea kwa ajali ya moto mwishoni mwa wiki iliyopita.

"Sikudhani kabisa kuwa naweza kuumizwa na kupata uchungu kwa tukio kama hili na ninajiuliza huu uchungu ni wa nini? Kumbe ni uchungu wa nyumba ya kwanza. Nawafikiria wananchi wenzangu wanaobomolewa nyumba zao bila fidia, na wengi ni nyumba zao za kwanza na pekee. Uchungu wao nausikia. Hasira zao nazihisi" Zitto ameandika.

Ameongeza kuwa "Nafikiria wanaobomolewa maeneo ambayo yamekuwa sehemu ya maisha yao na kuwapa kipato na familia zao. Nausikia uchungu wao.Sio uchungu wa nyumba ya kwanza. Uchungu wa kupoteza kabisa walichonacho na pengine kupoteza matumaini ya maisha"

Pamoja na hayo Zitto amesema kuwa ameridhika kwamba kilichotokea kwenye nyumba yake kuungua moto ni ajali ya kawaida na wala watu wasichukulie kwa muktadha wa matukio yanayoendelea nchini kwetu hivi sasa.

"Ni ajali na funzo ni kuchukua tahadhari zaidi. Hasara ni kubwa sana lakini muhimu ni kuwa maisha yanaendelea na Mungu ataleta uwezo wa kuendeleza mengine. Nilipata salaam kutoka kwa watu wengi na napenda kuthibitisha kuwa ni ajali tu" Zitto.

Mbali na hayo Mh. Zitto Kabwe amesema kuwa nyumba yake imeungua siku moja baada ya yeye kuondoka Kigoma na akiwa njiani kuelekea nchini Kenya ndipo alipatiwa taarifa kuhusu ajali hiyo.
"Ajali imetokea siku moja tu baada ya mimi kutoka Kigoma, Septemba 15 ,  2017. Hata hivyo muda wote wa siku 2 nikiwa nje ya Kigoma, sikupata hisia kabisa. Labda ni kwa sababu ya safari yangu ya Kenya ambayo nayo haikuwa ni kwa jambo la kawaida" Zitto.

Aidha Mh Zitto ameongeza "Leo asubuhi nimeamka na kurudi kutazama nyumba hii. Imekwisha yote nimezunguka zaidi ya mara 3 kutazama gofu lile lile nililotazama jana baada ya kufika. Nimechungulia chumba nilichokuwa nalala zaidi ya mara moja. Nipo kama mwendawazimu" alisisitiza Zitto Kabwe.

Nyumba ya Zitto Kabwe iliyoungua huko Mwandiga mkoani Kigoma inadaiwa ndiyo nyumba yake ya kwanza baada ya kupata  ridhaa ya kuwa mbunge


Diamond Aliamsha Dude Afunguka Kuzaa na Hamisa Mobetto Asema Nilitaka Mwanangu Aitwe Dylan

0
0
Diamond Aliamsha Dude Afunguka Kuzaa na Hamisa Mobetto Asema Nilitaka Mwanangu Aitwe Dylan
Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema jina alilotoa apewe mtoto wake kwa Hamisa Mobetto ni Dylan lakini kwa sababu za kutafuta umaarufu mwanamke huyo alimwita Abdul Nassib.

Amesema Hamisa alimwita mtoto huyo Abdul ambalo ni jina la baba yake mzazi ili iwe rahisi watu kufahamu kuwa mtoto huyo ni wa kwake baada ya kukubaliana kufanya uhusiano wao kuwa wa siri.

“Mimi jina ninalolitambua ni Dylan hata niliposikia wamemwita Abdul nilisema poa tu lakini akija kwangu nitamwita ninalolitaka mimi kwa sababu nataka aitwe DD (D Square).”

Amesema alisikitishwa pia na kitendo cha mwanamke huyo kumualika baba yake katika sherehe ya kutimiza siku arobaini ya mtoto huyo akimdanganya kuwa angekuwepo.

“Walimwalika mzee Abdul na nguo wakampelekea ili ahudhurie, yote hiyo ili mradi tu wapate cha kuzungumziwa mitandaoni,” amesema.


“Mimba ni yangu na sitokaa nikaachana na Zari,” amesema Platnumz.

Ambapo amesema amemgharamia Hamisa pamoja na mtoto tangu kipindi cha ujauzito wake mpaka mtoto anazaliwa ili kuhakikisha mama na mtoto huyo wanakuwa salama.

Amesema pamoja na yaliyotokea alimwambia mama yake mzazi kuhusu kilichotokea amemuomba msamaha Zari na hawana shida yoyote.

“Mimi ni mwanadamu na kilichotokea kimetokea na niko tayari kumhudumia mtoto,” amesema Diamond.

Diamond amesema kuwa alimuonya Hamisa kutokumtukana Zari kwani hausiki na chochote kilichotokea na badala yake ajishughulishe na mambo mengine.





Zari Amjia Juu Diamond Amtaka Asimuhusishe Kwenye Mambo Yake na Apambane na Mtatatizo Yake

0
0
Zari Amjia Juu Diamond Amtaka Asimuhusishe na Apambane na Mtatatizo Yake
Drama za sakata la Diamond na mwanamitindo Hamisa Mobetto limechukua sura mpya baada ya Zari kujibu mapigo katika mtandao wa Snapchat akionya asihusishwe.

Awali katika maelezo yake mwanamuziki Diamond amesema ameshazungumza na mpenzi wake huyo kuhusiana na mtoto aliyezaa na Hamisa na kwamba ameelewa na hakuna tatizo tena.

Wakati Diamond akiendelea na mahojiano katika kituo cha Clouds FM, Zari aliandika katika mtandao huo akisema: “Hahahaha unajidanganya, unasema uongo kuhusu mimi kujua kuhusu michepuko yako, malizana na balaa ulilolianzisha. Mimi kunyamaza haimaanishi ni mpumbavu. Kuwa makini na maneno yako.”

 Aliendelea kuandika: “Inawezekana mimi ni mama wa watoto wako ndio maana nimeamua kunyamaza kimya. Labda ugoogle kuhusu ‘defamation of character law suit’, usinijaribu.”

Diamond alipoulizwa kuhusu kauli hizo amesema anamwelewa kwa kuwa kuna baadhi ya mambo hakumweleza na kwa mara ya kwanza huenda ameyasikia wakati huo.






Baada ya Interview ya Diamond Platnumz, Zari Aamua Kujibu Makelele ya Diamond

0
0
Mwanadada Zari the boss lady amejibu kelele za Diamond alizokua anzipiga Clouds Fm kwa maneno machache sana lakini yaliojaa misumeno na mikato ya kila aina.

JE Zari atachukua hatua kweli?

Soma Hapa Chini Alichosema:


Kwa hili la leo Hamisa Mobetto Aingizwe Kwenye Orodha ya Mashujaa wa vit

0
0
Hakika baada ya Diamond kuhepa hepa kuhusu Mtoto Nasib Abdul leo amekiri kuwa ni suna yake.......

Hamisa ni shujaa kwasababu hakurudi nyuma aliendelea kuchokonoa hadi Mzee Baba yakamfika shingoni inabidi ajitokeze kusafisha hewa.......

Kama Diamond angepuuza makombora ya Hamisa hakika yule Binti wa Kiganda angeibuka Shujaa lakini kwakua makombora yameifikia Ngome ya Madale na kwa Madiba basi mshindi Sukari ya Kitanzania Hamisa.....

Pia Watanzania tumemuunga mkono Diamond mpaka amekuwa lulu lakini uzazi kahamishia kwa Mjukuu wa IDD Amin Dada..... Kwa hili Hamisa ni shujaa wetu kurudisha uzazi nyumbani Tanzania....... Na Sasa tumepata mrithi wa Mali za Diamnond ambaye ni Mtanzania halisi kabisa......

Serikali Yaifungia Gazeti la Mwanahalisi kwa Miaka Miwili

0
0

Serikali imelifungia Gazeti la Mwanahalisi kwa miaka miwili.

Imesema hatua hiyo imefikiwa kutokana na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za uchochezi na kuhatarisha usalama wa Taifa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abassi ametangaza uamuzi huo leo Jumanne mbele ya waandishi wa habari.

Dk Abassi amesema uamuzi huo umechukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2017.

Amesema kwa muda mrefu idara hiyo imekuwa ikiwakumbusha wahariri wa gazeti hilo juu ya kufuata misingi ya taaluma bila mafanikio.

Amezitaja baadhi ya habari zilizochapishwa na gazeti hilo ni ile iliyotolewa Januari 5 iliyobebwa na kichwa cha habari "Ufisadi ndani ya Ofisi ya JPM".

Dk Abassi amesema, "Habari hii ilisheheni nia ovu dhidi ya Rais wakati suala husika lilihusu Shirika la Elimu Kibaha, wahariri walikiri udhaifu wakaomba radhi na kupewa onyo kali."

Amesema Gazeti la Mwanahalisi toleo la  jana lilichapisha makala yenye matusi, dhihaka na maneno yasiyofaa dhidi ya Rais John Magufuli.

"Tulipowaita wakajitetea kwa kutumia neno mubashara yaani walichukua maneno yanayotolewa mitandaoni. Serikali imeona utetezi huo ni dhaifu kwa kuwa habari lazima izingatie maadili," amesema.

Mahakama: Mpemba wa Magufuli Atakiwa Kuacha Kuwalalamikia Mawakili wa Serikali

0
0
Mahakama: Mpemba wa Magufuli Atakiwa Kuacha Kuwalalamikia  Mawakili wa Serikali
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo September 19, 2017 imemtaka mshtakiwa Yusuf Ally maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ na wenzake watano katika kesi ya Meno ya Tembo yenye thamani ya Tsh. Milioni 785.6 kuacha kuwalalamikia Mawakili wa Serikali, badala yake iwalalamikie Mawakili wao ili kesi hiyo iharakishwe.

Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Elia Athanas kudai kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa ambapo washtakiwa walilalamika kwamba kesi hiyo inachelewa.

Hakimu Simba aliwataka washtakiwa hao kuacha kuwalalamikia Mawakili wa Serikali, bali wawasumbue Mawakili wao huhu alimtaka pia Wakili wa Serikali, Athanas afuatilie kesi ili wakati ujao wajue imefikia wapi.

Baada ya kueleza hayo kesi imeahirishwa hadi October 2, 2017.

Mbali ya Yusuf Alli, washtakiwa wengine ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa ambao wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Tsh. Milioni 785.6.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya January, 2014 na October 2015, wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Tsh Milioni 392.8 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Polisi Kuzuia Maombi Ya Lissu Haitoathiri Afya Yake Ila Waliotangulia Mbele za Haki Wanamuombea Moja kwa Moja- Sugu

0
0
Polisi Kuzuia Maombi Ya Lissu Haitoathiri Afya Yake Ila Waliotangulia Mbele za Haki Wanamuombea Moja kwa Moja- Sugu
Mbunge  Joseph Mbilinyi, ‘Sugu’ amedai marufuku ya jeshi la Polisi kuzuia  maombi maalum kwa ajili ya Tundu Lissu haitaathiri afya yake kwani yeye anaamini viongozi na wanachama wa chama waliotangulia mbele za haki wanamuombea moja kwa moja kwa Mungu

Sugu aliyasema hayo  wakati wa Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa viti Maalum kupitia (CHADEMA) jiji la Mbeya Esther Mpwiniza aliyefariki dunia ghafla Septemba 16, mwaka huu kutokana na Shinikizo la damu.

Sugu alisema kwa kuwa jeshi la polisi limezuia ibada kwa ajili ya kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu aliyejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana yeye anaamini wanachama waliotangulia mbele za haki watafanya kazi hiyo kwa niaba ya wanachama.

Sugu aliendelea kusisitiza kuwa mbali na kupiga marufuku kufanya maombi pia serikali imekuwa ikiwazuia watu kwenda kwenye misiba ambapo alidai viongozi na wanachama walizuiwa kuhudhuria msiba wa aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini Marehemu, Philemon Ndesamburo.

“Naamini Kamanda wetu Esther saizi upo moja kwa moja na Malaika naomba ukamuombee Tundu Lissu apone haraka anyanyuke kutoka kitandani aendelee na kazi za ukombozi wa taifa letu, huku wametuzuia kufanya maombi lakini huko najua hawezi kufika kuwazuia,”alisema Sugu

Akizumzungumzia marehemu Mpwiniza Sugu alisema alikuwa ni mwalimu wa siasa na mpiganaji wa kweli kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa jiji la Mbeya pamoja na chama na kwamba mchango wake umefanikisha ushindi wake kwa kiwango kikubwa. Amedai marehemu alikuwa ni ngao na mtu mwenye tabia ya kuwaunganisha wanachama na kuondoa tofauti ambazo zililkua zinatoa mwanya wa kuwepo kwa makundi ndani ya chama hicho.



Rais Magufuli Kuanza Ziara ya Siku Tatu Mkoani Arusha Kesho

0
0
Rais Magufuli Kuanza Ziara ya Siku Tatu Mkoani Arusha Kesho
Rais John Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha kesho kwa ziara ya siku tatu.

Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema baada ya kuwasili, anatarajiwa kuzindua barabara ya KIA Mererani inayoanzia Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro hadi mji wa Mererani mkoani Manyara.

Kwa mujibu wa Gambo Septemba 23, Rais Magufuli anatarajiwa kutunuku kamisheni kwa maafisa wa jeshi, tukio litakalofanyika katika uwanja wa Shekh Amry Abedi jijini Arusha.

Pia amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuhudhuria sherehe hizo.

Sherehe hizo ambazo kwa kawaida hufanyika katika chuo cha maafisa wa jeshi cha TMA, zinafanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja huo jambo ambalo linatoa fursa kwa wananchi wa Arusha kushuhudia

Rio Ferdinand Kujiunga na Ndondi Baada ya Kustaafu

0
0
Rio Ferdinand Kujiunga na Ndondi Baada ya Kustaafu
Rio Ferdinand anazindua taaluma yake mpya kama mwanandondi miaka miwili baada ya kustaafu kutoka soka.
Hatua ya Rio mwenye umri miaka 38 kujiunga na ndondi imeiungwa mkono na kampuni ya kamari ya Betfair ambayo ilitangaza taraifa hizo leo Jumanne.

Mlinzi huyo wa zamani wa England na Manchester United pia ana kampuni yake ya nguo.
"Ninafanya hivi kwa sababu ni changamoto," alisema Rio." Nimeshinda mataji na sasa ninalenga kushinda mkanda."

Amechapisha video kadha katika mitandao ya kijamii miezi ya hivi karibuni zinazomuanyesha akirusha ngumi na kupata mafunzo.
Aliyekuwa nahodha ya kikosi cha kriketi cha England Andrew Flintoff, pia naye alizindua taalumaa ya ndondi baada ya kustaafu, alipata ushindi mwaka 2012 dhidi ya Mmarekani Richard Dawson kwa pointi.

Ni kampuni ya Betfair iliyomuomba Ferdinand kuanzisha taaluma hiyo na itamsaidia kufuzu na kupata leseni ya bodi ya ndondi ya Uingereza kabla ya kuanza kujifunza na kushindana.

Bombadier Yakwama Mwanza Abiria Washindwa Kusafili

0
0
Bombadier Yakwama Mwanza Abiria Washindwa Kusafili
Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyoondoka saa 12:00 asubuhi Dar es Salaam kwenda Bukoba kupitia Mwanza, imekwama jijini Mwanza baada ya kupata hitilafu.

Kuharibika kwa ndege hiyo kumesababisha abiria waliokuwa wakielekea Bukoba kukwama hadi sasa bila kuelezwa hatima yao.

Akizungumza kwa simu, mmoja wa abiria ambaye alikuwa anaelekea kwenye msiba wa shemeji yake kutokea Mwanza, Muhiddin Khalid alisema alitakiwa kuripoti saa 12:15 asubuhi na walipanda ndege saa 2:15 asubuhi walitakiwa kufika Bukoba saa 3:15.

“Baada ya kupanda tulikaa muda mrefu ndani bila ndege kuondoka, baadaye tumeambiwa tushuke ndege mbovu, hivyo mpaka sasa saa 6:05 tupo hapa hatujui kinachoendelea tumeambulia kikombe cha chai,” alisema Khalid.

Meneja wa ATCL Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Theonestina Alchard amesema ni masuala ya kiufundi hivyo hawezi kuzungumzia zaidi kwa sababu yeye siyo msemaji wa kampuni.    

Jeshi la Polisi Lawakamata Watu Watano Wanaodaiwa Kuvamia Ofisi za Mawakili wa Manji

0
0
Jeshi la Polisi Lawakamata Watu Watano Wanaodaiwa Kuvamia Ofisi za Mawakili wa Manji
JESHI la Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatia mbaroni watu watano wanaodaiwa kuvamia, kuvunja na kuiba pesa kwenye ofisi za Prime Attorneys anazofanyia kazi wakili anayemtetea  Yusuf Manji, Hudson Ndusyepo.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema watuhumiwa wamekamatwa kufuatia oparesheni kali.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar mnamo Septemba 12, 2017 lilipokea taarifa za kuvamiwa kwa ofisi za Prime Attorneys ambapo watuhumiwa walivunja na kuiba pesa taslim Tsh. Milioni 3.7, kompyuta, laptop mbili, nyaraka za ofisi na za wateja wao.

Baada ya msako huo watuhumiwa walikamatwa na walipohojiwa, wote wamekiri kuhusika na tukio hilo huku wakitaja matukio mengine waliyohusika kupora. Pia wameonyesha pesa walizopora kwenye tukio hilo.

Watuhumiwa hao ni; Said Idrisa Saleh (47), mkazi wa Mbezi Luis, Musatapha Ibrahim Said (35), mkazi wa Magomeni Mwembechai, Somfi Nguza Somfi (52), mkazi wa Magomeni Mapipa, Imani Mbago Mhina (36), mkazi wa Kimara Mwisho na Hussein Hajji Suleiman (45), mkazi wa Kigogo Mbuyuni.

Aidha, Kamanda Mambosasa amesema jeshi lake linaendelea na upelelezi kubaini watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo.
Ofisi za kampuni hiyo zipo jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam jirani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala.

Flaviana Matata Afunguka Alipokutana na Jay Z, Beyonce

0
0
Flaviana Matata Afunguka Alipokutana na Jay Z, Beyonce
Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Bongo, Flaviana Matata ameeleza mambo machache kuhusu tukio la kukutana na Jay Z na Beyonce.

Weekend iliyopita Flaviana kupitia ukurasa wake wa twitter aliweka video akiwa na mastaa hao wa dunia. Akizungumza na XXL ya Clouds Fm Flaviana amesema walikutana katika maonyesho ya magari ya zamani ambayo yalikuwa ya kifahari lakini hawakuzungumza sana.

“Perfect nilikuwa kwenye event ya mambo ya magari, Hamptons nikakutana nao, Jay nimekutana naye mara nyingi sana, Beyonce this is first time I think but people get excited kwa sababu it had never meet to the internet,” amesema Flaviana.

“Sijawahi kuwa na video picha lakini those people we meet husalimii, kila mtu anaendelea na hamsini zake, pale tulikuwa tunasalimiana, hongea kwa watoto and then nikamsalimia Jay nikaenda zangu,” ameongeza
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images