Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Zari Afunguka..'Mambo Aliyonifanyia Diamond Hayawezi Nipotezea Hadhi yangu'

$
0
0
Baada ya Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul  ‘Diamond Platnumz’ kukiri kuzaa mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobeto, hatimaye mama watoto wake Zari Hassan ‘Zari’ azidi kumuweka njia panda msanii huyo juu ya uhusiano wao.

Mwanamama huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kupokea ushauri uliotolewa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii.

“Watu wakiamua kuchepuka au  kudanganya ni sawa na kujipotezea muda, ingawa wanahisi wanakuchezea wewe, hivyo usikate tamaa na usijilaumu kwa ajili ya makosa ya wengine, maisha lazima yaendelee,”

“Mambo yaliyotokea hayawezi kunipunguzia hadhi yangu, usijilaumu kwa yaliyotokea, zingatia malengo yako na kufanya maisha yaendelee,” amesema.

Amesema kuwa yale yote yaliyosemwa katika sakata hili yanabaki yalivyo na muda huu anaamua kuyaweka kando na kuelekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya sherehe ya kumbukumbu ya  kuzaliwa kwake.

Sakata hili limeibuka siku moja baada ya Zari kujibu mapigo katika mtandao wa Snapchat akionya asihusishwe na kitendo alichokifanya Diamond cha kuzaa na Mobeto.

Awali katika maelezo yake mwanamuziki Diamond amesema ameshazungumza na mpenzi wake huyo kuhusiana na mtoto aliyezaa na Hamisa na kwamba ameelewa na hakuna tatizo tena.

Magufuli Amwagia Sifia Mbunge wa CHADEMA

$
0
0
Rais John Pombe Magufuli ambaye leo Septemba 20, 2017 yupo kwenye ziara ya kikazi mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro amefunguka na kumsifia Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya na kusema ni mbunge mchapakazi.

Rais Magufuli amesema Ole Millya ni mchapakazi kutokana na ukweli kwamba mbunge huyo amelelewa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukulia ndani ya chama hicho hivyo sasa yupo CHADEMA lakini moyo wake ni CCM.

"Miliya ni mchapakazi, kwa sababu amelelewa na CCM, unaweza kumuona ni CHADEMA lakini moyo wake huyu ni Chama Cha Mapinduzi (CCM)" alisema Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa Mungu huenda alikosea kuipa Tanzania madini ya Tanzanite kwani madini hayo yamekuwa yakiibiwa huku Watanzania wenyewe wakishindwa kunufaika na mapato ya madini hayo.

"Mungu alifanya makosa alileta Tanzanite kwa Watanzania, lakini kama hakufanya makosa basi tubadilike jinsi ya kutumia Tanzanite. Tanzanite ingekuwa inatumika vizuri kusikungekuwa na tatizo la barabara hapa Simanjiro, hapa Simanjiro msingekosa hata Ambulance moja lakini kwa kuwa hamna gari hata moja ya wagonjwa basi mimi nitaleta gari ya wagonjwa hapa nitajua nifanya nini, nitawakata kata huko tutapata gari" alisema Rais Magufuli.

WhatsApp Yaboreshwa...Sasa Utaweza Kufuta Ujumbe Uliotuma Kwa Mtu Bahati Mbaya Kabla Hajausoma

$
0
0

 WhatsApp Yaboreshwa...Sasa Utaweza Kufuta Ujumbe Uliotuma Kwa Mtu Bahati Mbaya Kabla Hajausoma
Kwa muda mrefu watumiaji wa mtandao maarufu wa WhatsApp moja ya jambo lililokuwa linawahuzunisha na kuwakera ni pale wanaposhindwa kufuta ujumbe waliotuma kwa mtu.

Kuna wakati unaweza kutuma ujumbe fulani kwa bahati mbaya na kugundua umefanya kosa katika kuutuma ujumbe huo lakini ukashindwa kuufuta kwa sababu tayari umeshautuma.

Lakini kwa sasa jambo hilo la kufuta ujumbe uliokwisha tumwa linawezekana. Ndio, unaweza kuufuta ujumbe uliokwisha utuma iwe kwa bahati mbaya au la.



 WhatsApp Yaboreshwa...Sasa Utaweza Kufuta Ujumbe Uliotuma Kwa Mtu Bahati Mbaya Kabla Hajausoma
WhatsApp kupitia watumiaji wa toleo la Beta (WhatsApp Tester) wameanza kuwezesha kutumia huduma hiyo ya kufuta ujumbe uliokwisha tumwa.

WhatsApp Beta ni toleo ambalo linamuwezesha mtumiaji wake kuwa wa kwanza kila WhatsApp wanapojaribu kitu kipya. Huwa wa kwanza kupata huduma hiyo kabla ya kuwafikia watumiaji wa kawaida wa WhatsApp.

Namna ya kufuta ujumbe uliotuma ni rahisi sana. Ni kubonyeza kwa kushikilia ule ujumbe ulioutuma na kwa juu upande wa kulia kutafungua menu itakayokuwezesha kufuta ujumbe huo.

Utaweza kufuta ujumbe ndani ya dakika tano baada ya wewe kutuma, nje ya hapo ukiufuta utakuwa umefutika kwako tuu. Na pia hii haikupi uhakika ya kwamba ujumbe utakaotuma hautasomwa na uliyemtumia, ila kama uliyemtumia atakuwa amechelewa kuingia WhatsApp ndani ya hizo dakika 5 basi upo salama.

Zoezi hilo la kufuta ujumbe unaweza kulifanya kwa mtu mmoja mmoja au kwa kundi (WhatsApp group).


Na pindi ukifanikiwa kuuufuta huo ujumbe uliouandika ni kwamba uliyemtumia atapata ujumbe unaoeleza kwamba kuna meseji imefutwa.

Kama wewe ni mtumiaji wa WhatsApp Beta na bado hujafikiwa na maboresho hayo basi muda si mrefu yatakufikia. Na kama ni mtumiaji wa kawaida wa Whatsapp basi endele kusubiri mpaka huduma hiyo itakapo kufikia.

Mwisho mwa mwaka jana WhatsApp walitoa taarifa ya kuwa na mpango wakuja na wazo la kuwezesha ufutwaji wa meseji zilizotumwa.

Maboresho haya ni kwa watumiaji wote wa iOS na Android. Je wewe unapokeaje boresho hili kwa app ya WhatsApp?

Ushauri: Nina Naumbile Madogo ya Uume (Kibamia), Naogopa Kutembea na Wasichana

$
0
0
Ushauri: Nina Naumbile Madogo ya Uume (Kibamia), Naogopa Kutembea na Wasichana
Amakweli mungu hakunyimi vyoote na haupi vyoote pia. Mimi ni kijana wa miaka 21, mwembamba kiasi nina body naturaly,maji ya kunde, mrefu wastani sio handsam sana but mtanashati najiheshimu, mstaarabu kutokana na sifa nilizo kuwa nazo imepelejea kupendwa sana na wanawake.
Wengine hupigana na kupelekana hadi polisi kwajili yangu pasipo mimi kuwa na mahusiano nao yani ni wivu tu na nimetongozwa na wanawake tangu nikiwa na miaka 15 na wengine ni wakubwa kwangu na wengine wanakuja hadi mbele ya mama na kueleza hisia zao kwangu ila mimi sina mpango nao kabisa yani.

Hii inapelekea hadi mama yangu kupoteza imani na mimi kwa kuhisi huenda mwanae ni shoga ama sifanyi kazi kama dume.Ila mimi sio kama siwatamani au siwataki ila nina tatizo moja linalonifanya mpaka nishindwe kujielewa wakati mwingine najipiga ukutani kwa hasira, but nashindwa nifanye nini.
Ninawaza sijui nimwambie mama yangu au baba yangu ila nawaza nitaanza je kuwaambia tatizo langu ikiwa baba ni mkali sana na mda mwingine hataki hata salamu na katika familia walio nitangulia kuzaliwa ni wanawake wote daaaah.! inaumasana ninapo muona mamayangu akitoa chozi pindi akiwa na waschana Wanaokuja mbele yake kwaajili yangu.

Pia hii imenifanya nishindwe hata kutembea mtaani kwa kuhisiwa mimi ni shoga ila tatizo langu sio kabisa yani daah..! Nawaza nitafanya vipi mapenzi na msichana ikiwa mimi nina UUME MDOGO saana nilipo upima kwa rula ni wa nchi 4 so hivi msichana yeyote anaweza kuhisi uume huu kweli daaah..
Why mimi waungwana naombeni msaada ni nini nifanye nimwambie mama akamueleze baba labda atanisaidia kupata dawa au kama kuna dawa ni wapi napata na ni ipi coz naona ninakoelekea sio kabisa.

Naombeni msaada naombeni

Dawa za Asili 6 zinazootesha Nywele na Kuondoa Upara

$
0
0
Hakuna kitu kinavutia zaidi kama kuwa na nywele nzuri za kutosha na zenye afya yake ya asili. Hata hivyo tatizo la kupotea kwa nywele au upara ni tatizo kubwa linalowapata watu wengi kila pembe ya dunia.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea kupotea kwa nywele kama vile:

a)Sababu za kimazingira,

b)Kuzeeka,

c)Msongo wa mawazo (stress),

d)Kuvuta sigara kupita kiasi,

e)Lishe duni,

f)Homoni kutokuwa sawa,

g) Kurithi

h) Maambukizi kwenye ngozi ya kichwa

i)Matumizi yasiyo sahihi ya vipodozi vya nywele

j)Baadhi ya dawa za hospitali

k)Matatizo katika kinga ya mwili

l)Upungufu wa madini chuma

m)Na magonjwa mengine sugu

Ni jambo la kawaida kupotea nywele 50 mpaka 100 kwa siku lakini unapoanza kupoteza zaidi ya hapo kwa siku ni muda muafaka kwako kuchukua hatua kurudishia kiasi hicho cha nywele kinachopotea.

Leo nimekuletea hapa orodha ya dawa za asili 6 zinazoweza kuotesha na kuzipa afya upya nywele zako ambazo zimeanza kupotea na hivyo kuondoa huo upara bila gharama sana.

Uvumilivu unahitajika zaidi kwani ni tiba inayochukua muda mrefu kwa kawaida.

Dawa za asili 6 zinazootesha nywele na kuondoa upara

1. Uwatu

Uwatu unajulikana kwa miaka mingi kwa kutibu tatizo la kupotea kwa nywele kichwani. Mbegu za uwatu zina homoni mhimu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘antecedents’ ambayo huhamasisha kukuwa kwa nywele na kuamsha upya vinyweleo vya nywele.

Mbegu hizi pia zina  protini na asidi amino nyingine iitwayo kwa kitaalamu kama ‘nicotinic‘ ambayo huhamsisha kukuwa kwa nywele.

Loweka katika maji kikombe kimoja cha mbegu za uwatu kwa usiku mmoja.
Asubuhi yake zisage upate kama gundi (paste).
Pakaa hiyo gundi kwenye nywele zako na ujifunike na kofia ya kuogea kwa dakika 40.
Fanya zoezi hili kila siku asubuhi kwa mwezi mmoja hivi.

2. Juisi ya kitunguu maji


Juisi ya kitunguu maji husaidia kukuza nywele sababu inayo sulfur nyingi ya kutosha ambayo husaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenda kwenye vinyweleo vya nywele, huvifufua upya vinyweleo vya nywele na kupunguza uvimbe.

Kitunguu maji huua bakteria wabaya kitendo kinachosadia kuua vimelea na wadudu  wa magonjwa kwenye ngozi ya kichwa vitu ambavyo huweza kupelekea kupotea kwa nywele (upara).

Utafiti unaonyesha juisi ya kitunguu kuwa na uwezo mkubwa kutibu tatizo la kupotea kwa nywele kwa mjibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Dermatology mwaka 2002 huku wakitoa majibu ya zaidi ya asilimia 74 ya washiriki wa utafiti huo kupata kurejeshewa nywele zao zilizokuwa zimeanza kupotea.

Chukua juisi ya kitunguu maji kimoja na uipake moja kwa moja sehemu ambayo nywele zimeanza kupotea na uache kwa dakika 30 kisha jioshe baadaye na shampoo


Au changanya pamoja vijiko vikubwa vitatu vya chakula vya juisi ya kitunguu maji na vijiko vikubwa vingine viwili vya jeli ya aloe vera. Unaweza pia kuongeza kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni na upake mchanganyiko huo kichwani sehemu ambayo nywele zimeanza kupotea. Acha kwa dakika 30 ujisafishe na shampoo baadaye.
Rudia zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa wiki kwa wiki kadhaa.

3. Aloe Vera (mshubiri)


Mmea wa Aloe vera una vimeng’enya ambavyo huhamasisha ukuwaji wa nywele. Ina sifa pia ya kuweka sawa usawa wa asidi na alkalini (pH) ya nywele jambo linaloweza kupelekea kuhamasisha kuota kwa nywele.

Ukiacha hilo la kuotesha nywele aloe vera pia hutibu mba kichwani.

Chukua majimaji ya mshubiri fresh (jeli) na upakae kichwani sehemu ambayo nywele zinanyonyoka na uache kwa masaa kadhaa na ujisafishe na maji ya uvuguvugu.

Fanya zoezi hili mara 3 mpaka 4 kwa wiki.

Unaweza pia kunywa juisi fresh ya mshubiri kikombe kimoja kila siku asubuhi tumbo likiwa tupu kuongeza ufanisi wa ukuwaji wa nywele zako na afya yako kwa ujumla.

4. Juisi ya Kiazisukari. (Beetroot)


 
Juisi ya kiazisukari ina wanga, protini, potasiamu, , phosphorus, calcium na vitamini B na C. Viinilishe hivi vyote ni mhimu sana kwa ajili ya kukua na kuota kwa nywele na afya ya nywele kwa ujumla.

Mara kwa mara kunywa juisi fresh ya kiazisukari pia juisi ya karoti fresh ili kuongeza afya ya nywele zako.
Au twanga majani kadhaa ya kiazisukari na uyachemshe kwenye moto kidogo ukichanganya na hina na upake mchanganyiko huo kichwani sehemu ambayo nywele hazioti. Acha kwa dakika 15 na ujisafishe na maji safi. Rudia tendo hili mara kadhaa katika wiki.

5. Tui la Nazi


Tui la nazi lina kiasi kingi cha protini na mafuta mengine mhimu ambavyo huhamasisha kukuwa na kuota kwa nywele na hivyo kuzuia upara. Likitumiwa kwa ajili ya kazi hii tui la nazi halikawii kuleta matokeo mazuri.

Tengeneza tui lako zito kidogo ukitumia nazi, ili kupata tui zito na jingi nakushauri kisha kukuna nazi yako iweke kwenye blenda na maji kidogo kwa mbali kisha iblendi kwa dakika kadhaa ndipo ukamuwe upate tui zito kabisa na jingi.


Mimina tui hilo kwenye sufuria na uweke kwenye moto kama dakika 3 au 4 hivi kisha ipua


Subiri tui hilo lipowe na mwisho pakaa kichwani kichwa chote au sehemu ambayo nywele zimepotea na uache hivyo kama dakika 20 kisha safisha kichwa na shampoo ya aloe vera (mshubiri).


Kufanya dawa iwe na nguvu zaidi unaweza kuongeza ndani ya tui la nazi nusu kijiko cha achai cha unga wa pilipili manga nyeusi na kiasi hicho hicho cha unga wa mbegu za uwatu.

6. Mafuta ya habbat soda

Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele. Bidhaa nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji kuliko faida zake. Kwahiyo kwa wale wenye tatizo la upala, nywele zisizokuwa na kwa wale ambao nywele zao hazina afya mnashauriwa kuchagua mafuta haya kwa matatizo haya yote.

Ingawa haieleweki ni kwa namna gani mafuta haya yanakuza nywele lakini wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo ya uwezo wake mkubwa wa kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake.

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa na huwa mazito kidogo.

Matumizi: Sugulia kipande cha limao fresh eneo ambalo nywele zimenyonyoka na kisha pakaa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya habbat soda ya nywele na uache kama dakika 15 hadi 20, unaweza kuacha hivyo hivyo au ujisafishe na maji safi, unaweza kufanya kutwa mara 1 au 2 kwa muda wa mwezi mmoja hadi miwili.

Ifanye Ngozi Yako kuwa Nyeupe Bila Mkorogo

$
0
0
Habari ya leo tena ndugu, ni matumaini yangu siku yako imekuwa njema sana leo!!!

Je unataka kuwa na ngozi nyeupe? ili iweje?. Wakati mwingine nakutana na wadada au wamama wamejichubua ngozi zao kutoka kwenye ueusi na kuwa nyeupe! nashangaa zaidi unakuta dada mwingine ni mweupe wa kuzaliwa kabisa lakini bado anapakaa madudu ya dukani eti ili awe mweupe zaidi!!



Hivi nini huwa ndiyo sababu kwa watu wenye tabia hizi? kwanini hamjiamini?

Haya ili kuwa na ngozi nyeupe kwa njia za asili na bila gharama yeyote na bila kukuachia madhara yoyote fuatilia dawa ifuatayo ya asili. Hii hasa haikufanyi uwe mweupe kabisa bali unaisafisha ngozi yako vizuri ili iwe na afya ile inastahili na kama imeaanza kufubaa basi itarudi kuwa na rangi yake ya asili na yenye kupendeza.

Ifanye Ngozi Yako kuwa nyeupe bila mkorogo

Hatua za kufuata:

Mahitaji:

Asali kijiko kimoja cha chai
Juisi (maji maji ya limau) kijiko kimoja cha chakula
Maji ya uvuguvugu kiasi
Jinsi ya kutengeneza mchanganyiko wako

1. Changanya juisi ya limau na asali katika chombo kimoja kisafi na uchanganye ukitumia uma au kijiko cha kawaida kwa dakika kadhaa.

Matumizi
1. Osha uso vizuri ukitumia sabuni (kama unapata sabuni ya habbat soda inakuwa vizuri zaidi) na maji ya uvuguvugu kisha jifute na kitambaa kisafi
2. Jipake ule mchanganyiko wako usoni na maeneo yote ya shingoni taratibu huku ukijimasaji hivi kwa dakika 10
3. Osha uso kwa maji safi, mwisho jifute kwa taulo safi

Mhimu: Fanya zoezi hili kwa wiki mara 1 mpaka mara 3 na matokeo yake utaniletea hapa hapa

Safari ya Tundu Lissu Kupelekwa Marekani Yaota Mbawa...Madaktari Wachomoa

$
0
0


Lazaro Nyalandu Ameandika haya kupitia Ukurasa wake wa Facebook:

"TUNAFAHAMU kwamba, tangu Alhamisi, Septemba 7, siku ambayo Mh #TunduLissu, Mb., (Singida Mashariki-CHADEMA) alishambuliwa kwa kupigwa risasi mjini DODOMA, Watanzania wengi wamesononeshwa na kulia sana, na kubwa zaidi, WOTE wameungana katika kuomba Sala na Dua kwa ajili ya Mh #TunduLissu, ili mkono wa Mkombozi, aliye MUNGU wetu, upate kumgusa tena na kumponya dhidi ya majeraha, maumivu na mateso anayoyapitia.

MAPEMA leo, baada ya kutembelea #NairobiHospital asubuhi, nimefanya mazungumzo mchana wa leo na Mh #FreemanMbowe, ambapo kwa pamoja tumeelezwa kuwa MADAKTARI #NairobiHospital wameendelea na kumtibu Mh #TunduLissu, ikiwa ni pamoja na kuanza upasuaji, na huduma zingine za Kitabibu walizomwanzishia tangu awasili Nairobi siku ya Alhamisi, Septemba 7. IMEELEZWA vilevile kuwa kwa sasa Mh #TunduLissu ataendelea na TIBA hospitalini hapo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hali yake bado ni "Critical but stable", na KWAMBA mwili wake unaendelea kuitikia vema matibabu lukuki anayofanyiwa kwa wakati mmoja.

KWA SASA, mipango ya kumsafirisha Mh #TunduLissu NJE itasimama, kutokana na ushauri wa MADAKTARI #NairobiHospital, ili kuruhusu kukamilishiwa huduma za TIBA ambazo tayari ameanzishiwa, hadi hapo itakavyoshauriwa vinginevyo, ama endapo kutatokea umuhimu wa kufanya hivyo katika SIKU zijazo. 

AIDHA, SOTE tuzidi KUMWOMBEA MUNGU na kushiriki katika CHANGIZO za kusaidia gharama za matibabu yake.

NI DHAHIRI kwamba Wana Singida, na Watanzania WOTE tumeumia, tumekwazwa, na tumesononeshwa sana kwa uonevu na dhuluma aliyotendewa ndugu yetu Mh #TunduLissu. Kitendo hiki hakikubaliki mbele za MUNGU na mbele za wanadamu.

Tunaiomba Serikali yetu iendeleze juhudi zake na kuchukua hatua za haraka kuwasaka, kuwakamata, na kuwatia mbaroni watu wote waliohusika kupanga na kutekeleza shambulio hili la kigaidi dhidi ya Mh #TunduLissu. Aidha, shambulio hilo walilolifanya watu wasiojulikana limedhalilisha taifa, na kudhoofisha taswira ya kukomaa kwa demokrasia inayoruhusu kuvumiliana na kuheshimiana licha ya tofauti zetu za kiitikadi na mitazamo ya kisiasa.

HALIKADHALIKA, kwetu sote kama TAIFA, huu ni wakati wa Watanzania wote kuwa wamoja, bila kujali tofauti zetu za kiitikadi, kidini, wala kikabila, tuungane na kulaani kitendo hiki na vitendo vyote vya uonevu na kuumizana. TANGU zamani, IMEANDIKWA: Haki HUINUA Taifa.

Lazaro S Nyalandu, Mb.
Singida Kaskazini-CCM
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (TAIFA) #prayforlissu
 mazungumzo yetu leo mjini Nairobi, Kenya)

Nani Anagharamia Matumizi ya Lema, Msigwa na Mbowe Huko Nairobi?

$
0
0
Nani Anagharamia Matumizi ya Lema, Msigwa na Mbowe huko Nairobi?
Kwanza natanguliza pole na kumtakia mema Kamanda wetu Tundu Lissu. Lakini najaribu kufikiri kwanini Msigwa na Lema bado wako Nairobi?

Kwa gharama za nani? Kama za kwao kwanini wasirudi nyumbani kisha hizo fedha wachangie kwenye matibabu?

Tena lile jopo limeambatana na Wake na wenza wao, WHY?

Yawezekana na wao ni sehemu ya matumizi ya fedha zinazochangwa na Watanzania walalahoi........

Jamani rudini nyumbani tuhamasishe michango maisha ya Nairobi ni ghali sana......

By Kurzweil/JF


Kufuatia Sakata la Diamond Kumkubali Mtoto wake, Faiza Ally Amchana Mh.Sugu "Ex Husband Wake"

$
0
0
Kufuatia Sakata la Diamond Kumkubali Mtoto wake, Faiza Ally Amchana Mh.Sugu "Ex Husband Wake"
Kufuatia Sakata la Diamond Kumkubali Mtoto wake, Faiza Ally Amchana Mh.Sugu "Ex Husband Wake" Ameandika haya katika ukurasa wake wa Instagram:

Sugu Amjibu Faiza Ally na Kuweka Mpaka Risiti Alizolipia Ada ya Mtoto..Faiza Amshukia Tena

$
0
0
Sugu Amjibu Faiza Ally na Kuweka Mpaka Risiti Alizolipia Ada ya Mtoto..Faiza Amshukia Tena
SUGU:
Huwa sipendi kupost mambo haya lakini imenibidi, hizi ni bank slips za ada ya mwisho niliyolipa kwenye shule ya kindergarten aliyokuwa anasoma mwanangu za mwezi wa 5 mwaka huu 2017 ambako alishamaliza . Na mwezi huu wa 9 ilikuwa nimuanzishe shule Feza Nursery pale Mikocheni, lakini from no where mama yake ghafla akanizuia na kusema ahitaji tena nilipe ada na hata kunizuia nisimuone tena Sasha! Na kwamba ana uwezo wa kumpeleka shule anayotaka yeye na ndio akampeleka huko Hazina International, ambako pia hata hivyo nilishaanza kuwasiliana na uongozi ili niendelee tu kulipa ada hata kama nimepigwa marufuku kumuona mwanangu bila sababu... # Hivi kama ni nyie mngefanyaje ? Na nyie mnaotukana ovyo mitandaoni bila kuwa na ukweli mnaoujua tafadhali sana naomba hebu kwanza KABILIANENI NA HALI ZENU kwenye maisha... Asanteni


FAIZA ALLY:
We baba mjing* lol angalieni risiti za mwaka gani na sasha alianza kusoma lini ?
Ka***mbe mbele na sita kuacha mpaka unyooke ! Mnafki mkubwa ! Toa hata risiti 1 tu ya mwaka 2016 .... zote za mwaka 2017 Tena muhula wa mwisho ! Una haya ada term 2 ku prove kwa watu... wewe na wa p*mbavu wenzie wana kujaz k*ambeni mbele ukweli unaujua kwenye nafsi yako !
Naona umeona aibu mtoto mdogo kama Diamond anavyoweza kuwa reaponsible na watoto pamoja na ujinga wote unaoendelea HAYA NA AIBU ikakushika kuona kuna watoto uliowazidi umri wanakuzidi akili ukajihisi hapa watu watashtuka hapa wataniona mimi bwege maana huyu Diamond kama kavua nguo mababa loosers wote, mbona siku zote ulikuwa hujitetei!? Nimeanza kulalamika leo mimi!? Eti leo huyo unaonesha risiti mbili tu ambazo hata mimi niliwahi kuzipost humuhumu maana nilishtuka, Aibu imekushika, asante Diamond kwa kutushtulia mapunga zeze kama haya.. sasa tufanye kitu kimoja we si unataka kumpeleka Feza, mbele ya watanzania leo NAKUKABIDHI HUYO HAPO njoo umpeleke tuone kama utaweza, na nakukabidhi mbele za watu sababu huongei na mimi na wala hutaki kuwasiliana na mimi juu ya maendeleo ya mtoto na mimi sina shida na hilo sababu siwezi lazimisha mtu aelewe umuhimu wa baba na mama kuwasiliana juu ya mtoto kwa maendeleo yake (mtoto) nenda kalipe Feza uone kama atagoma kusoma, ila leo NIMEKUDHARAU ZAIDI nilijua we ni mgumu ila sikuwahi kufahamu kuwa kumbe unajua kwamba UNACHOKIFANYA KIBAYA deep down na ndiomana leo umedhihirisha kwa kujitetea uongo, unajitetea nini kama unayoyafanya ni sawa!? We si unaona sahihi kutojua hata mtoto anaishije, hebu sema basi hata mara ya mwisho ni mwaka gani kuona hata tigo pesa yako tu ya hata elfu hamsini, naachaje kuwa na uchungu, nalisha, nasomesha, navalisha na hata comfort kwa mtoto ni mimi maana hata kuongea nae tu umegoma, kweli leo unathubutu kutoa risiti zako za muhula eti kujionesha unahudumia mtoto!??? Aisee umenishtua sana, umenitoka zaidi joseph, we ni m*uaji, ila sikushangai umeweweseka na Diamond mtoto mdogo kakuvua nguo we mtu mzima na mizigo yako kwenye suruali.
Nilishawahi kuomba kuweka suluhu hadi na mwanamke wako ili tuwe na amani na mtoto apate amani zaidi kimalezi nikadharauliwa, jiulize Ni mara ngapi nimehangaika kuomba tukae chini tuongee kama wazazi tusolve angalau uweze kuwa kwenye maisha ya Sasha na ukakataa!? Nimemfata rafiki yako Mungai kuongea nae tuweze kukutana kwa ajili ya mtoto uligoma, nimefunga safari hadi Zanzibar mimi kwenda kwa Baba yako wa hiyari unaemuheshimu kuomba tukae chini ajenda ikiwa mtoto tu na ukagoma, hata simu yangu unasema huwezi kupiga wala kutaka kuwasiliana na mimi matokeo unamnyima haki mwanao, hivi kweli juhudi zote hizo mimi leo unathubutu kusema nimekukatalia mtoto!!? Kilichotokea ulimtaka Sasha aje mbeya na ukamtuma mtu aje kukuwakilisha huku ukisisitiza hutaki kabisa kuongea na mimi, kama mzazi na MWANAMKE naruhusu vipi mwanangu aende sehemu ambayo ntashindwa hata kumpigia baba yake kumuuliza tu vipi anaendeleaje, hata akiumwa hutaweza kuniambia sababu eti hutaki kabisa kuongea na mimi, hilo ndio la kusema nilikataza mtoto asije, ni dharau kiasi gani kupigia mtu hata asieishi na mimi kumwambia unataka aniambie anaomba mtoto aje, unajionaje labda, watu wana jinsi wanavyonitafsiri kutokana na maisha yangu mengine lakini laiti kama wangejua naapa hakuna ambae angekutazama mara mbili, na hata kama kweli niliwahi kukosa ama nakukosea, sasa mtoto wako vinamuhusu nini!? Tufanye nisingekuwa na uwezo wa kuhudumia inamana ungemuacha awe chokoraa kama mwanao wa kwanza ambae ni fundi garage uliemtupaga wala hujui alipo uliemkimbizia kijijini kuogopa aibu ya kufatwafatwa kuulizwa na vyombo vya habari, usinijali mimi ila muogope hata MUNGU basi, ogopa kudanganya, unajua mimi sidanganyi na unajua ukweli, nna risiti sio chini ya saba, na bado maisha ya kila siku, kula, nguo kuvaa, michezo bata nnalompa mwanao sijajumlisha hata kimoja leo we risiti mbili unajiita mwanaume zinakusimamisha shingo kweli!?? Hujiskii hata vibaya ukimuona mwanao amependeza labda, mtoto mzuri ana maendeleo mazuri nafsi haikusuti ama hata kuona tu huyu kiumbe anakua na atayajua hayo mambo yako, hauniadhibu mimi unamuadhibu mwanao na zaidi haunikomoi mimi unajikomoa mwenyewe ..

Zitto Akamatwa na Kusafirishwa Chini ya Ulinzi wa Polisi

$
0
0
Zitto Akamatwa na Kusafirishwa Chini ya Ulinzi wa Polisi
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesafirishwa na polisi kwenda Dodoma.

Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya ACT-Wazalendo, Mohamed Babu imesema Zitto amesafirishwa kwa gari saa 10:00 usiku akitokea kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA).

Amesema kamati hiyo inafuatilia kwa umakini hatua kwa hatua kuhakikisha usalama wake ikiwataka wanachama na wananchi kuendelea kuwa watulivu.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema Zitto amesafirishwa kwa gari la Bunge akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Zitto anatakiwa kufikishwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge

Mzee Akilimali Aliamsha Dude Ataka Makamu Mwenyekiti wa Yanga Ajiuzulu

$
0
0
Mzee Akilimali Aliamsha Dude Ataka Makamu Mwenyekiti wa Yanga Ajiuzulu
Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali amemtaka Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Clement Sanga kujiuzulu kwa madai kuwa yeye ndiye chanzo cha matatizo yote yanayotokea ndani ya Klabu hiyo.

Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali.
Mzee Akilimali amesema wamegundua mgomo uliotokea hapo jana kwa wachezaji kutohudhuria mazoezi ni njama iliyopangwa na Sanga wakidai kuwa wachezaji hawajalipwa mishahara yao suala ambalo sio sawa.
"Mimi naona tu kwamba Sanga sasa imefikia hapa, ili tufanye vizuri nawasihi Watanzania wote hususani wana Yanga na wapenzi wa Yanga bwana Sanga sasa hivi atamke kujiuzulu, chonde chonde Bwana Sanga iache Yanga watu tuketi pamoja na wewe mwenyewe tuchague viongozi Yanga tusonge mbele" amesema Mzee Akilimali
Mzee Akilimali amesema siku moja kabla ya mazoezi alionekana Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sanga akiwa na Nahodha wa Timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' pamoja na Mshambuliaji wa Kimataifa Thaban Kamusoko ambapo baada ya kutoka hapo timu ikasema haijapata mshahara wa mwezi uliopita pamoja na mwezi huu hivyo wanaamua kugoma suala ambalo amesema ni njama.

Akilimalia anadai kuwa Sanga amewataka wachezaji kutokusikiliza maneno ya baadhi ya viongozi ambayo yanalenga kurudisha nyuma maendeleo ya Klabu kwani Klabu hiyo itakaposhindwa kufanya vizuri lawama zote zitaangukia kwa Klabu wakiwemo viongozi.
"Kama Yanga ikifanya vibaya hivi sasa na mpaka ikafikia hatua ya kushuka daraja hivi atalaumiwa nani na hasara ya nani? Mimi niwaonye wachezaji kwamba sio vizuri wala sio nidhamu kugomea mazoezi,mtu hagomei mazoezi bali anagomea mchezo, hata kama unadai mwezi wa kwanza, wapili, watatu wewe mazoezini nenda kwasababu unajiweka tayari wakikulipa waajiri wako lazima ukatekeleze kazi yao, sasa leo unagomea mazoezi pesa watatafuta wanakupa, unakwenda kukutana na Ndanda FC unafungwa, utawaambiaje waajiri wako, kama pesa wameshakulipa" alisema Mzee Akilimali

Msigwa Afunguka Mateso na Magumu Aliyopitia Lissu Wakati Anasafirishwa Kwenda Nairobi kwa Matibabu

$
0
0
Msigwa Afunguka Mateso na Magumu Aliyopitia Lissu Wakati Anasafirishwa Kwenda Nairobi kwa Matibabu
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ameelezea mateso na uchungu ambao mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alipitia wakati alipokuwa akisafirishwa kwenda Nairobi, Kenya kwa matibabu baada ya kupigwa risasi mjini Dodoma.

Mchungaji Msigwa amesimulia tiba anayoipata Lissu na ulinzi ulivyoimarishwa hospitalini alikolazwa huku pia akidokeza mipango ya kusaka Sh550 milioni za kukodi ndege maalumu ya kumsafirisha kwenda ng’ambo kwa matibabu zaidi.

Akizungumza jana baada ya kutembelea chumba cha habari cha Mwananchi, Tabata Relini jijini Dar es Salaam, Msigwa alisema mwanasheria huyo mkuu wa Chadema, alivuja damu nyingi na kama asingepata huduma ya haraka angefariki dunia.

“Nataka tu niwaambie Watanzania kwamba Tundu Lissu aliumizwa sana katika jaribio la kuchukua uhai wake. Watu wasichukulie kama ni jambo dogo, ni jambo kubwa lililoharibu hata akili za watu tuliokuwa karibu naye,” alisema Msigwa kwa hisia kali. “Mimi mwenyewe ambaye nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza tuliokuwa naye, nikafika mahali nikaona risasi siiogopi tena kwa maumivu aliyokuwa nayo. Nisingependa kama Taifa tufikie huko.”

Alisema kwa hali aliyokuwa nayo, hata walipofika Nairobi, madaktari walishangaa kuona Rais huyo wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) akiwa hai.

Safari ilivyokuwa

Akieleza hali ilivyokuwa ndani ya ndege baada ya kuondoka Dodoma, Msigwa alisema, “Tulipata shida, kuna wakati kitanda kwenye ndege kilifyatuka mimi nikawa nashikilia, mwenyekiti (wa Chadema, Freeman Mbowe), kuna hewa ya Oxygen alikuwa anashikilia mirija kutoka kwenye mtungi ilikuwa imetoboka. Kwa hiyo muda mrefu mimi nimeshikilia kitanda, madaktari wale nao wameshikilia drip za maji,” alisema na kuongeza kuwa kimo kifupi cha ndege hiyo nacho kilikuwa changamoto.

“Kwa hiyo kisaikolojia unaathirika kwa kuona mateso aliyopata. Lakini tumefika Nairobi vizuri wametupokea wakaanza kushughulika naye, mpaka mambo yakaenda vizuri, lakini niseme mwenzetu ameumizwa sana.”

Msigwa alisema Lissu amekuwa akihudumiwa na jopo la madaktari 10 wanaofanya kazi kwa kushirikiana na kila siku wanatoa ripoti.

“Kwa hiyo utaona lile jopo la madaktari 10, wengine ni wa mifupa, wengine wa saikolojia, wengine wa ndani ya tumbo na maeneo mengine, wote wanakaa kumhudumia,” alisema. Kuhusu kumpeleka nchi nyingine kwa matibabu zaidi, Msigwa alisema timu ya viongozi wa Chadema inaendelea kujadiliana na madaktari hao wanaokutana nao kila siku huku akirejea kusema kwamba sababu ya kumwondoa nchini zilikuwa za kiusalama.

“Tulipomwondoa hapa, hatukusema kuwa madaktari wetu hawawezi. Sababu kubwa ni security (usalama), lakini ni ukweli usiopingika kuwa hospitali ya Muhimbili haina tofauti na hospitali ya Jomo Kenyatta kule Kenya ambayo nayo ni ya Serikali. Lakini hospitali tuliyompeleka siyo ya umma, ina gharama kubwa lakini ina huduma kubwa,” alisema.

Kupelekwa ng’ambo

Kuhusu gharama za matibabu, Msigwa alisema ikiwa Lissu atalazimika kupelekwa Marekani au Ujerumani kwa matibabu zaidi watahitaji dola 250,000 za Marekani ambazo ni takriban Sh550milioni kwa ajili ya kukodi ndege maalumu ya matibabu (air ambulance) huku akiwaomba wananchi kuendelea kuchangia.

“Watanzania wenye nia njema waendelee kumchangia walichonacho kwa ajili ya matibabu. Wananchi wasione ni jambo dogo, imani yetu ni kuwa watatuunga mkono kwa sababu imeonekana kwa mara ya kwanza Watanzania wameweka tofauti zao pembeni na kuguswa na jambo la kupigwa risasi, ” alisema Msigwa.

Alisema mpaka sasa wameshatumia hadi Sh160 milioni kwa matibabu tu, mbali na gharama za viongozi wa chama hicho kuishi jijini Nairobi.

Kuhusu kufuata utaratibu wa Serikali uliobainishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai wa kupelekwa Muhimbili kisha Apollo, India, Msigwa alisema isingewezekana kwa kuwa hali ilikuwa mbaya.

“Tuna wataalamu wengi hapo Muhimbili, lakini hatuna vifaa vya kutosha na madaktari, kimekuwa kilio chao kikubwa. Sasa Lissu yuko katika hali ya dharura, unasema tufuate ‘procedures’ (utaratibu) kwamba aende Dar es Salaam, madaktari wakae!” Alikosoa huduma za afya wanazopewa wabunge nchini akisema wenzao wa Kenya wanawashangaa.

Alisema suala la Bunge kumtibu Lissu siyo ombi, bali ni wajibu wake kwa kuwa wabunge wanaisaidia Serikali.

“Tunasimama kwenye jukwaa, tunakamata microphone, tunawaambia Serikali imekosea 1,2,3… tunawaambia bombardier imekamatwa, wawekezaji wanaondoka, sisi tunaisaidia Serikali, sisi ni marafiki. Serikali inapaswa iwalinde hawa watu wanaoisaidia Serikali,” alisema.

Pia alizungumzia usalama wa wabunge akisema, “Ukiangalia wenzetu (Kenya), mbunge analindwa na Serikali, walinzi zaidi ya wanne ambao wako full armed (wana silaha), lakini na nyumbani wako wawili, kwa sababu huyu ni mbunge anayeisimamia Serikali...,” alisema Msigwa.

Alililaumu Jeshi la Polisi akishangaa kwa nini hadi sasa hajakamatwa mtu yeyote anayehisiwa kuhusika.

“Kibaya zaidi hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kutokana na tukio lile...Viongozi wa Chadema vitisho tulivyokuwa tunasema sasa vimeanza kutokea wazi katika maisha yetu,” alisema.

Kuhusu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, alisema siku waliyofika nchini humo hawakumkuta wala ofisa yoyote uwanja wa ndege.

“Balozi kweli alikuwa Tanzania, lakini hatukukuta mtu yeyote. Kule ubalozini kuna mwambata wa Jeshi, kuna mwambata wa usalama wa Taifa, kuna watu wa visa, uchumi, angalau tungekuta mtu. Hakukuwa na official arrangement,” alisema Msigwa.

Tanzania Imejitoa Katika Mpango wa Uendeshaji wa Shuguli za Serikali kwa Uwazi

$
0
0
Tanzania Imejitoa Katika Mpango wa Uendeshaji wa Shuguli za  Serikali kwa Uwazi
Serikali imejitoa katika Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership-OGP) hatua ambayo inazua wasiwasi kuhusu utekelezaji wa sera ya uwazi iliyoasisiwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Hatua hiyo ya kujitoa kwa Tanzania ilitarajiwa kutangazwa wakati wowote na Kamati ya Uongozi ya mpango huo inayokutana katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea New York, Marekani.

Tanzania ilijiunga na mpango huo mwaka 2011 na hivyo kuwa nchi ya pili barani Afrika ikitanguliwa na Afrika Kusini ambayo ilikuwa ya kwanza kusaini makubaliano hayo yanayotaka nchi kuondokana na kasumba ya kuendesha mambo kwa usiri kati yake na wananchi.

Zaidi ya nchi 70 duniani zimesaini mpango huo unaohimiza dhana ya uwazi na ukweli. Rais mstaafu Kikwete alikuwa mstari wa mbele kuunga mkono mpango huo na alifanikisha mkutano wake uliofanyika kwa mara ya kwanza nchini 2015 ikiwa miezi michache kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu.

Wakuu wa mpango huo wanakutana New York wakijadiliana mambo mbalimbali ikiwamo ajenda inayoangazia kuongezeka kwa hali ya kutoaminiana kati ya Serikali na wafanyabiashara. Pia, wanaangalia njia zinazopaswa kuchukuliwa ili pande hizo ziweze kurejea katika hali yake ya kawaida.

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania bado haijaweka hadharani juu ya hatua yake iliyochukua ya kujitoa kwenye mpango huo. Pia, haikuweza kufahamika mara moja kama maofisa wake walioko mjini New York watapeleka ujumbe uliochukuliwa nyumbani na Serikali.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Augustine Mahiga yuko New York akimwakilisha Rais John Magufuli mkutano wa Umoja wa Mataifa.

Alipoulizwa kuhusiana na hatua hiyo iliyochukuliwa na Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alikataa kueleza lolote lakini akasema kuwa Serikali itatoa ufafanuzi wake muda utakapowadia.

“Nisikilize, sisi (Serikali) tutalieleza hilo tutakapoona inafaa,” alisema Waziri Kairuki ambaye hakukanusha wala kukiri lolote.

Lakini, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Aziz Mlima alikiri kuhusu Tanzania kujiondoa katika mpango huo.

“ Ndiyo ni kweli lakini ni kwa muda tu kwa sababu Serikali inataka kuutathmini mpango huo kama unaendana na masilahi ya Taifa,” alisema.

“ Kuna mambo tunahitaji kwanza kuyatekeleza kabla ya kutekeleza mpango huu,” alisema. Hata hivyo, vyanzo vya kuaminika vimelidokeza gazeti hili kuwa utawala wa Rais Magufuli unapenda kujikita zaidi katika utekelezaji wa Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora barani Afrika (APRM).

Kabla ya kujitoa katika mpango huo wa OGP, Tanzania ilikuwa tayari imepitia hatua mbili za utekelezaji na sasa ilikuwa ikijiandaa kutekeleza mpango mkakati wa tatu uliokuwa uanze 2016/17-2017/18.

Katika mipango hiyo, Tanzania ilikuwa imeainisha maeneo saba ya kuweka mkazo ikiwamo Sheria ya Kupata Habari, Bajeti ya Uwazi, Uwazi katika ardhi na madini.

Akizungumzia mpango huo mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Faraja Kristomus alisema wengi waliitazama OGP kama mpango wa nje zaidi na kukosa uungwaji mkono katika taasisi za kiserikali.

Katika makala zake zilizochapishwa na gazeti la Citizen, Kristomus ameandika kuwa wizara iliutazama mpango huo kama chombo chenye urasimu na haukusaidia kukaribisha mageuzi.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema hatua ya Tanzania kujiondoa katika mpango huo ni ishara nyingine ya kuanguka kwa demokrasia na uwazi serikalini. “Kitendo cha kujiondoa ni kuiambia dunia kuwa hatuko tayari kwa uwazi,” alisema.

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alisema uwazi kwa serikali ilikuwa silaha tosha ya kukabiliana na rushwa.

“Tanzania ilikuwa haitekelezi kikamilifu mahitaji yote ya OGP. Lakini naamini kuwa angalau ilikuwa njia sahihi ya mwelekeo wetu. Hatua ya kujiondoa ilikuwa siyo wazo nzuri. Tunarudi nyuma katika eneo la utawala bora,” alisema.



Kimbunga Maria Chasababisha Kisiwa Chote cha Puerto Rico Hakina Umeme

$
0
0
Kimbunga Maria Chasababisha Kisiwa Chote cha Puerto Rico Hakina Umeme
Kimbunga Maria kimekata umeme katika kisiwa chote cha Puerto Rico, chenye watu milioni 3.5.
Abner Gómez, ambaye ni mkuu wa utoaji huduma za dharura alisema kuwqa hakuna mtu anayetumia umeme aliye na huduma hiyo kwa sasa.

Kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema kuwa mafuriko makubwa yanaikumba nchi hyo.
Maria kwa sasa kinaondoka nchini Puerto Rico na kumepunguza nguvu zake hadi kiwango cha pili.

Baada ya kimbunga Maria kuipiga Puerto Rico, gavana ameamrisha watu kusalia manyumbani mwao kuanzia saa kumi na mbili jioni na hadi saa kumi na mbili asubuhi.
Hi ni hatua ya kuwazuia watu kupata ajali kutokana na nyaya za umeme zilizoanguka na vifuzi vilivyo barabara za mji.

Mapema Bw Rossello alimuomba Rais Donald Trumo kukitangaza kisiwa hicho kuwa eneo la janga baada ya kimbunga kusababisha mafuriko makubwa na upepo unaotishia maisha.

Alisema kuwa kuna uwezekano wa uharibu mkuwa licha ya vitisho 500 kubuniwa kuwalinda watu.
Kimbunga hicho tayari kimesababisha vifo vya watu 7 katika kisiwa cha Dominica ambacho kiliathiriwa vibaya siku ya Jumatatu

Huddah, Wema Wanunua Ugomvi wa Mobetto na Zari Waamua Kuingilia Kati

$
0
0
Huddah, Wema Wajnunua Ugomvi wa Mobetto na Zari Waamua  Kuingilia Kati
Wakati kitendawili cha nani ni baba wa mtoto wa pili wa mwanamitindo Hamisa Mobeto kikiteguliwa baada ya mwenyewe kukiri hadharani jana, wasichana wawili ambao waliwahi kutoka kimapenzi na baba wa mtoto huyo, Wema Sepetu na Huddah Monroe wamejitokeza na kuingilia ugomvi kati ya Zarinah Hassan ‘Zari’ na Hamisa Mobeto.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa mtoto huyo wa Hamisa aliyepewa jina la Abdulatif Nasibu Abdul ni wa msanii mmoja mkubwa wa muziki wa kizazi kipya, ingawa kwa muda alikuwa akikanusha. Lakini jana, akihojiwa na kituo kimoja cha redio jijini, msanii huyo ambaye pia amezaa watoto wawili na Zari, alikiri kushiriki mapenzi na mwanamitindo huyo na kwamba amekuwa pia akimhudumia kwa kumpa kiasi cha shilingi laki tano kwa wiki, sambamba na kumnunulia gari.


Msanii huyo alisema baada ya kuelezwa na kuukubali ujauzito huo, alimtaka mpenziwe huyo kukaa kimya kwani yeye tayari alikuwa kwenye uhusiano na Zari na hakuwa tayari kuachana na mwanamke huyo aliyemzalia watoto wawili.

Kivumbi kiliibuka upya mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya Hamisa kuvujisha picha alizozipiga kwa siri, akiwa na msanii huyo wa Bongo Fleva, wakiwa kitandani kimahaba, picha ambazo ziliamsha upya gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimtuhumu msanii huyo kwa kumkana mwanaye wakati ushahidi wote upo wazi.

Ni kelele hizo ndizo zilizomlazimu msanii huyo wa Bongo Fleva kupitia kituo kimoja cha runinga na redio, jana kuibuka na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu picha zilizovujishwa na Hamisa, ambapo alitumia fursa hiyo kukiri hadharani kwamba yeye ndiye baba wa mtoto huyo.

“Tulikubaliana na Hamisa Mobeto kuwa ujauzito huo usitangazwe kuwa ni wa kwangu, na alikubali,” alinukuliwa msanii huyo. Inadaiwa mwanamitindo huyo hakukubaliana na suala la kufanya mambo yote kuwa siri, hivyo akawa anavujisha taarifa kwa mashosti zake ambao nao walikuwa wakiposti kwenye mitandao ya kijamii, jambo linalotajwa kumtibua msanii huyo na kusababisha apunguze fedha za matumizi mpaka shilingi laki mbili (200,000) kwa mwezi. Hatua ya kupunguziwa matumizi, inatajwa kuwa ilimkasirisha zaidi Hamisa ambaye aliamua kuposti picha zilizowaonesha wakiwa kitandani, ambazo zilichafua hali ya hewa.

Wakati mahojiano hayo yakiendelea redioni, wadau mbalimbali walijitokeza kuzungumzia hali hiyo, lakini wakigawanyika, wengine wakimuunga mkono Hamisa na wengine Zari. Wema Sepetu ambaye uhusiano wake na msanii huyo ulikuwa ndiyo habari ya mjini wakati huo, kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram, akionekana kumuunga mkono Zari, alisema anatambua wakati mgumu anaoupitia mwanamke huyo aliyempora bwana, katika kipindi hiki kigumu.

“Najua anaweza kusema maneno ya ovyo juu yangu, lakini najua hali anayopitia kama mwanamke, nadhani sasa ni wakati muafaka kwake kuweza kumvisha pete, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,” aliandika Wema. Huddah Monroe, mwanamitindo kutoka Kenya ambaye naye pia aliwahi kuhusishwa kushiriki mapenzi na msanii huyo, katika namna ya kumpiga kijembe Zari, alisema ‘mwanaume ni wako anapokuwa ndani kwako, akitoka siyo wako’.

Shamsa Ford Ampa Makavu Mobetto Kuchepuka na Mume wa Zari

$
0
0
Shamsa Ford Ampa Makavu Mobetto Kuchepuka na Mume wa Zari
Wakati sakata la Hamisa Mobeto kuzaa na mzazi mwenziye Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, likiwa bado bichi na watu wakiendelea kumuweka kikaangoni kwenye mitandao ya kijamii, Queen wa Bongo Muvi, Shamsa Ford, ameandika ujumbe ambao mashabiki wanadai ni kijembe kwa Mobeto.

Baada ya post hiyo, mashabiki wa Hamisa walimjia juu Shamsa na kumshushia kichambo wakimtaka aachane na ishu za mwanamitindo huyo, badala yake apambane na hali yake.

Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE.

Nemo Ataka Kutembelea Upepo wa Ommy Dimpozi

$
0
0
Nemo Ataka Kutembelea Upepo wa Ommy Dimpozi
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye yuko chini ya Combinatin Sound, Nemo, amesema sababu ya kumshirikisha Ommy Dimpoz kwenye wimbo wake wa 'Number One' ni kutembea na upepo wa Dimpoz ambaye alikuwa juu kwa kipindi hiko ili kutafuta njia ya kutoka

Nemo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, na kusema kwamba kwa hali ambayo alikuwa nayo kipindi kile ilimlazimu amtumie msanii kama Dimpoz, ili kutoboa kwenye game.

"Ilinibidi nimtumie Dimpoz kwa ajili ya trend ambayo ikikuwepo kipindi kile, na tayari alishajitengenezea njia kwa sababu Dimpoz ni msanii mkubwa ndani na nje ya nchi, kwa hiyo nikatembea na hilo", amesema Nemo.

Hivi sasa Nemo ameamua kurudi kwenye game baada ya kimya kirefu, ambapo ameachia kazi mpya inayoitwa 'kipotable', inayoendelea kufanya poa kwa mashabiki.

Lori la Dangote Ladakwa Likisafirisha Wahamiaji Haramu

$
0
0
Lori la Dangote Ladakwa Likisafirisha Wahamiaji Haramu
Wahamiaji haramu wanane kutoka Ethiopia wamekamatwa wakisafirishwa kwa lori la kampuni ya Dangote kwenda Mtwara.

Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Edward Chegero amesema leo Alhamisi kuwa, wahamiaji hao walikamatwa Kongowe wilayani Temeke.

Amesema wamekamatwa jana Jumatano baada ya idara kupata taarifa na baadaye kuweka mtego uliowanasa.

Chegero amesema mbali na wahamiaji hao, idara imewakamata Watanzania wanne waliokuwa wakiwasindikiza wahamiaji hao.

Amesema Watanzania hao walikuwa wakitumia gari aina ya Toyota Passo.

Kaimu kamishna amesema uchunguzi unaendelea ili kuwakamata wahusika wote wa mtandao huo.

Chegero amesema baadhi ya wahamiaji hao walikuwa na tiketi zinazoonyesha wanatoka Msata kwenda Dar es Salaam.

Amewataka madereva wa malori na usafiri mwingine kutosafirisha wahamiaji haramu kwa kuwa kufanya hivyo ni kuvunja cha sheria.

Kaimu kamishna pia amewaonya wamiliki wa nyumba za wageni zinazotumika kuwaficha wahamiaji hao akisema kiama kwao kinakuja.

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images