Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Rais Kenyatta: Uamuzi wa Kufuta Matokeo ya Uchaguzi ni 'Mapinduzi ya Mahakama'

0
0
Rais Kenyatta: Uamuzi wa Kufuta Matokeo ya Uchaguzi ni  'Mapinduzi ya Mahakama'
Rais wa kenya Uhuru Kenyatta ameutaja uamuzi wa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais kuwa ''mapinduzi ya mahakama''.

Viongozi hao wawili walikuwa wakijibu uamuzi kamili wa mahakama ambapo majaji wa mahakama ya juu walitoa sababu zao kwa nini walifutilia mbali matokeo hayo ya urais.

Idadi kubwa ya majaji hao walisema kuwa matokeo hayo hayakuwa na 'uwazi wala kuhakikiwa'.
Viongozi hao wawili hatahivyo waliangazia uamuzi wa majaji wawili waliopinga uamuzi hao ambao walisema kuwa kesi iliowasilishwa katika mahakama hiyo haikuwa na uzito wowote.
Rais Kenyatta alisema kuwa hakuna uchaguzi usikumbwa na makosa madogo madogo.

Mkutano wa Majaji wa Nchi za Jumuiya za Madola Kukutana Tanzania kwa Mara ya Kwanza

0
0
Mkutano wa Majaji wa Nchi za Jumuiya za Madola Kukutana Tanzania kwa Mara ya Kwanza
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano wa mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika nchini kwa mara ya kwanza kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu.

Hilo limethibitishwa leo na Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma kwenye ukumbi wa Mahakama ya rufaa jijini Dar es salaam.

Jaji Ibrahimu amesema Makamu wa Rais atafungua mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 354 kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Madola.
Jaji Mkuu amesema katika mkutano huo Tanzania itawakilishwa na wajumbe 50 ambao ni Majaji na mawakili kutoka Tanzania bara na visiwani.

Ujumbe mwingine mzito wa watu 13 ambao ni Marais na Majaji kutoka Austaria, Zambia, Afrika Mashariki na Pakistani utakuwepo kwenye mkutano huo.
Aidha Jaji amebainisha kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein atafunga mkutano huo mnamo Septemba 28 mwaka huu.

Watu 36 Washikiriwa na Polisi kwa Kufanya Vurugu Jangwani

0
0
Watu 36 Washikiriwa na Polisi kwa Kufanya Vurugu Jangwani
Watu 36 wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kuhusika kufanya vurugu eneo la bonde la Jangwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema leo Alhamisi kuwa bomoabomoa inaendelea eneo hilo na ulinzi umeimarishwa.

"Tumewakamata watu 36, bado tunaendelea kuwasaka waliofanya fujo akiwemo kiongozi wa mtaa wa Jangwani anayetuhumiwa kuhamasisha vurugu hizo," amesema.

Kamanda Hamduni amesema kiongozi huyo (jina tunalihifadhi kwa sasa) jana Jumatano aliwahamasisha wananchi kuwapiga mawe maofisa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala waliokuwa wakisimamia bomoabomoa kupisha mradi utakaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa).


Ebitoke Alizwa na Penzi la Ben Pol Aomba Msaada

0
0
Ebitoke Alizwa na Penzi la Ben Pol Aomba Msaada
Mchekeshaji maarufu bongo Ebitoke alizwa na kitendo cha anayedaiwa kuwa mpenzi wake Ben Pol kutopokea simu wala kujibu meseji zake, na kuomba msaada kwa watu kumuuliza msanii huyo kwa nini anafanya hivyo, licha ya kuwa na mipango mingi ya baadae.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ebitoke amesema kitendo hicho kinamuweka njia panda, hivyo anashindwa kujua kama anampenda kweli au alikuwa anachezea moyo wake.

Kampeni ya 'Fataki' la Kuongeza Uelewa wa Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Kuanzishwa Tena

0
0
Kampeni ya 'Fataki'  la Kuongeza Uelewa wa Maambukizi
Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids) iko mbioni kurudisha kampeni za ‘Tuko wangapi’ na ‘Fataki’ ili kusaidia kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU).

Kaimu mkurugenzi mkuu wa tume hiyo, Jumanne Issango amesema miaka ya nyuma kampeni hizo ziliendeshwa kwenye vituo vya redio na televisheni lakini hazikuendelea kutokana na upungufu wa rasilimali fedha.

“Fedha zilizokuwa zikitumika kuendesha kampeni si endelevu kutokana na wafadhili kuja na baada ya muda wao kuisha wa kufanya kazi nasi huondoka na kuacha pengo,” amesema.

Amesema watazirejesha kampeni hizo kutokana na kuwepo mazungumzo na wafadhili ambao wameona mchango wake katika kupiga vita maambukizi ya VVU.

Issango amesema kurudi kwa kampeni hizo kutaenda sambamba na utafiti wa mwenendo wa Ukimwi nchini wa mwaka 2016/17 mwishoni mwa Novemba.

Amesema kuna dalili kuwa maambukizi mapya ya VVU yanapungua katika jamii kupitia utafiti huo.

Kaimu mkurugenzi huyo amesema semina na kampeni zinazoendeshwa kitaifa za kuzia maambukizi ya Ukimwi zimechangia  kupunguza maambukizi mapya.

Amesema mkakati huo unalenga kupunguza nusu ya kiwango cha maambukizi mapya ya VVU kutoka asilimia 0.32 mwaka 2012 hadi 0.16 mwaka 2018 pia kupunguza kiwango cha vifo vitokanavyo na Ukimwi.

Issango amesema wameongeza wigo katika utafutaji takwimu kwa kuwatumia watoto kuanzia umri 0 hadi miaka 49.

Hii Hapa Siri ya Timu ya Azam Kutoruhusu Mabao Msimu Huu wa Ligi Kuu

0
0
Hii Hapa Siri ya Timu ya Azam Kutoruhusu Mabao Msimu Huu wa Ligi Kuu
Beki wa Azam, Aggrey Morris amesema ubora, umoja na morali iliyopo katika safu yao ya ulinzi ndio siri ya kutoruhusu bao lolote mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu

Azam na Simba ndio timu pekee ambazo hazijaruhusu nyavu zao kutikiswa kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara msimu mpaka sasa.

Morris alisema wamejiwekea malengo msimu huu ya kuhakikisha wanaweka rekodi ya kuwa timu ambayo haijaruhusu bao msimu huu ingawa amekiri si kazi nyepesi lakini bidii na kujituma inawasaidia kutimiza malengo yao.

" Hakuna kingine kiinachoibeba safu yetu ya ulinzi kama umoja tulionao na kila mmoja kujua nini anatakiwa kufanya na kusaidiana.Hali hii imetufanya kutengeneza ukuta wa chuma ni ngumu kupitika kirahisi.

Yametimia Nyimbo ya Zilipendwa Yaipiku Seduce Me ya Ali Kiba Kwa Kutazamwa na Wetu Wengi

0
0
Yametimia ZILIPENDWA yaigaragaza SEDUCE ME ya Ali Kiba...
.
.
Hiii ni baada ya Mange Kuhamisha Amsha Amsha yake Kwenye Michango ya Tundu Lissu.....
.
.
TEAM DIAMOND SEMA *Oyoooo*

Ni Nani Aliyekutuma Kuoa Mwanamke Flat Screen?

0
0
Naongea na wanaume wenzangu wale walio owa wanawake wenye makalio madogo halafu wakiona wa wenzao wenye makalio makubwa wanaanza kupiga mikelele.

Utakuta uko na mkeo matembezini uku kafungashia kidogo basi mijanaume isiyokuwa na akili inaanza kupiga mayowe oh wakubwa wanafaidi ohh marshallah.

Kwanini na wewe usioe au kutafuta mwanamke mwenye makalio na ukaacha kutamani vya wenzao. Kwanza unamkosea adabu mwanaume mwenzio kupiga miyowe utadhani umeona utupu wa mzazi wako.

Acheni ujinga tuacheni tuenjoy na wake zetu maana hatukuwatuma kuoa flat screen.

By Nitonye

Wanawake wa Haya makabila Kitandani ni Wabovu Sana

0
0
Hiyoooooooooooooo ndo habari kwani kuna baadhi ya makabila ukiwa una mgegeda hata hatingishiki yeye ni kutulia kama gogo tu wala hawezi hata kukukuruka kwanza wachaga, wapare, waha, wasukuma, wangoni, wakikuyu, wakurya, waluguru, wagogo, wamasai na mengine kibao yani ni shida hadi wanafanya papuchi zao kua za baridi sana jaman badilikeni, haya toeni uzoefu wenu na ninyi

Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE.

Zitto Kabwe Ajitetea Kwa Hoja 10 Mbele ya Kamati

0
0
Maelezo ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (Mb), mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati,

Mnano tarehe 13 Septemba, 2017 nilipata wito wa kufika mbele ya Kamati yako kutoa ushahidi wa masuala mbalimbali. Nilipata wito husika saa nane na dakika 40 mchana, nikitakiwa kufika mbele ya kamati yako, hapa Dodoma saa saba mchana siku hiyo hiyo.

Nililetewa wito huo na RCO Mkoa wa Kigoma nikiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kigoma Ujiji. Sikuweza kufika, isingewezekana katika mazingira hayo niwe na uwezo wa kusafiri kutoka Kigoma na kufika mbele ya kamati yako hapa Dodoma. Kwanza muda ulishapita, lakini hata taratibu za kiusafiri pamoja na umbali kati ya Kigoma na Dodoma hazikuwezesha Jambo hilo.

Siku iliyofuata nilipata ajali, ambapo nyumba yangu iliwaka moto wakati nikiwa njiani kwenda Nairobi kumuona mbunge mwenzetu mgonjwa, ndugu Tundu Lissu. Jana tarehe Septemba 20, 2017 nikiwa natokea Kigoma ili kuja kwenye Kamati nilikamatwa na Polisi ili kufikishwa mbele ya Kamati yako.

Leo nimefika mbele yenu na nitajibu wito wenu kama ifuatavyo:

A: Kwamba maoni yangu kwenye mtandao wa Twitter kuwa "Bunge siku hizi ni Idara ya Tawi la Utawala" yanadhalilisha Mhimili Wa Bunge.

Maneno hayo ni ya kwangu na nimeyatoa kama raia wa Tanzania. Ninaamini kwa dhati kuwa Bunge la Kumi na Moja limekuwa likifanya kazi kwa kuingiliwa na Serikali chini ya ndugu Rais John Pombe Magufuli.

Maneno na vitendo vya Rais yanaashiria kuwa Bunge halina Uhuru wake, na mimi kama Mbunge nina wajibu wa kuonyesha kutopendezwa kwangu na hali hiyo. Nina mifano kumi (10) kuthibitisha maelezo yangu hayo kama ifuatavyo:

1. Kuzuiwa kwa "Bunge Live" kwa kisingizio cha kupunguza gharama za uendeshaji wa mhimili wa Bunge, wakati Mikutano yote ya mhimili wa Serikali, hasa ya Rais ikirushwa live (mubashara) ni dalili ya wazi ya kufifisha sauti ya Bunge na kupandisha sauti ya serikali. Hata vituo binafsi ambavyo vilipanga kurusha bunge Live bila malipo (na hivyo kutokuwa na gharama) vilizuiwa, lakini vinarusha Live mikutano ya Rais.

2. Kitendo cha Uongozi wa Bunge kurudisha serikalini shilingi Bilioni 6 bila ridhaa ya wabunge kwa kisingizio kwamba zimebaki kutokana na kubana matumizi. Hii ni dalili ya wazi ya Bunge "kujipendekeza" kwa serikali. Wakati Uongozi wa Bunge ukirejesha kiwango hicho cha Fedha, kuna taarifa kwamba kamati nyingi za Bunge zinashindwa kutekeleza wajibu wake kwa sababu ya ukata.

3. Maelekezo ya mhimili wa Serikali kwa mhimili wa Bunge, kupitia maagizo ya Rais Magufuli kwa Spika Ndugai kuwa "Awashughulikie wabunge" (kwa kuwafukuza bungeni) aliowaita "waropokaji" ili waje wazungumze nje ya Bunge na yeye Rais (Serikali) apate nafasi ya kuwashughulikia. Kauli hii ya Rais aliyoitoa wakati akipokea Ripoti ya Prof. Osoro kuhusu Mikataba ya Madini, Juni 12, 2017 inaonyesha picha iliyo dhahiri kuwa Bunge linapokea Maelekezo kutoka Serikalini ya kuwadhibiti wabunge hasa wanaoiwajibisha serikali. Na hatuwahi kuliona Bunge likiyakana maelekezo hayo ya Rais kwa Spika.

4. Kitendo cha Bunge kuhariri hotuba za kambi ya upinzani kwa kushinikiza kuondolewa kwa vipengele vinavyoikosoa Serikali. Mathalani, Wakati wa Bunge la Bajeti, hotuba ya Msemaji wa Kambi ya upinzani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ndugu Godbless Lema, iliamriwa kuondolewa maneno yanayohusu kashfa ya Mkataba wa Lugumi, kumhusisha Rais na kuuzwa kwa nyumba za Serikali, Mauaji ya wanasiasa, pamoja na Bunge kulinda wahalifu.

5. Kauli ya Rais Magufuli ya Novemba 4, 2016 akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuwa "mzizi wa mhimili wa serikali ni mrefu zaidi kuliko mihimili mingine" mara baada ya kuulizwa juu ya matumizi ya Serikali Nje ya Bajeti iliyoidhinishwa na bunge, unaonyesha dhahiri fikra ya Rais na Serikali yake juu ya ukuu wa mhimili wa Serikali dhidi ya Bunge.

6. Kitendo cha Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Tanzanite na Almasi kusomwa nje ya Bunge na kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu na Rais bila kuwasilishwa na kujadiliwa Bungeni ili kuwekewa azimio la Bunge. Kitendo hiki kinaifanya Kamati hiyo kuonekana kuwa ya Serikali badala ya Kamati ya Bunge.

7. Kauli ya Rais kuwa Spika alimpigia simu kumuuliza juu wajumbe wa kuwaweka kwenye Kamati za Bunge za Tanzanite na Almasi inaonyesha dhahiri kuwa Spika anafanya kazi kwa maelekezo ya Rais. Na Bunge na Spika hawajawahi kuikana kauli hii ya Rais.

8. Kwa mara ya kwanza kwenye Historia ya Nchi yetu tumeshuhudia Mbunge akishambuliwa kwa risasi wakati Mkutano wa Bunge ukiwa unaendelea. Haijapata kutokea katika historia ya Bunge letu, Wabunge kukamatwa hovyo mbele ya mageti ya Bunge na kusafirishwa usiku usiku bila hata Spika kujulishwa kama taratibu za Mabunge ya Jumuiya ya Madola zinavyotaka. Kitendo cha 'Watu Wasiojulikana' kummiminia risasi zaidi ya thelathini Mbunge wa Singida Mashariki, ndugu Tundu Lissu, wakati akitokea Bungeni, tena kwenye makazi yake, ambayo kwa mujibu wa sheria ni sehemu ya Bunge, ni dharau ya hali ya juu kwa Mhimili huu. Ni tukio linalolenga kuliziba mdomo Bunge. Makala yangu ya Nani alitaka kumwua Tundu Lissu (kwa lugha ya Kiingereza) naiambatanisha katika maelezo yangu haya.

9. Kitendo cha Serikali kutowasilisha 'Taarifa za Utendaji wa Robo Mwaka' kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti ya mwaka 2014 ni dharau kubwa kwa Mhimili wa Bunge. Ni dharau zaidi kwamba Serikali ilileta Muswada wa sheria kuondoa kifungu kinacholazimisha Waziri wa Fedha kutoa Taarifa hizo, na Bunge kupitisha kuwa Sheria, hivyo kuondoa kabisa Uwajibikaji wa kibajeti wa Serikali ndani ya Bunge, hivyo kudunisha hadhi ya bunge.

10. Bajeti ya Bunge kutowekwa kwenye Mfuko wa Bunge kwa mujibu wa sheria, na Spika kutakiwa kuomba vibali vya safari za Wabunge kwa Mkuu wa Tawi la Utendaji (Serikali) ni maelezo tosha kuwa Bunge ni Tawi la Utendaji na sio Mhimili unaojitegemea.

Ninayo mifano mingine mingi tu ya kuonyesha kama ushahidi wa jambo hili, kwa sasa hiyo 10 naomba itoshe.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nchi yetu ina mihimili mikuu mitatu ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Katiba na Sheria mbalimbali za nchi zimewekwa kuhakikisha kila mhimili unafanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa na mhimili mwingine. Kikatiba, mbali na wajibu wake wa  kutunga sheria, Bunge lina wajibu wa kuisimamia serikali. Kwa lugha nyingine, katika utekelezaji wa majukumu yake, Bunge ni "Kiranja" wa kuibana na kuisimamia Serikali.

Tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano, kumekuwepo na kauli na matendo ya viongozi wa serikali na Bunge yanayoashiria uelekeo wa serikali kuminya na kuingilia uhuru wa Bunge. Baadhi ya vitendo hivi vimefanywa hata na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kutambua wajibu wangu katika kulinda heshima, uhuru, hadhi, haki, ufanisi na madaraka ya Bunge katika kutekeleza majukumu yake, mara kadhaa nimekumbusha na ilipobidi kuonya ndani na nje ya Bunge dhidi ya vitendo hivi.

Maoni yangu yaliyonifanya niitwe hapa, pamoja na Mifano kumi (10) niliyoitoa hapo juu vinaonyesha wazi nia yangu njema ya kuonya na kutaka kulindwa kwa hadhi, heshima, haki na madaraka ya Bunge letu tukufu. Naamini bunge lilipaswa kunipongeza ni kunishajiisha kwa kazi hiyo, na si kinyume chake ninapotuhumiwa na kuletwa mbele ya Kamati yako kuwa nimelidhalilisha bunge pamoja na spika wa bunge. Jambo hili litavunja morali ya wabunge kutetea hadhi ya bunge letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti (Mzee George Huruma Mkuchika),

Wewe ni miongoni mwa wazee ninaowaheshimu sana hapa nchini, nilivyo sasa kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya malezi yako kwangu hapa bungeni, umeshiriki kunifinyanga niwe mbunge imara kwa busara na hekima zako, pamoja na kunipa ujasiri wa kuisimamia kutokana na uzoefu wako. Nakutambua kama muumini wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, iliyotangazwa kupitia Azimio la Arusha. Napenda ninukuu sehemu ya Azimio la Arusha kuhusu Uhuru wa mawazo. Azimio linasema "kwamba TANU inaamini: kila Raia wa Tanzania ana haki ya Uhuru wa Mawazo..."

Napenda kusisitiza kuwa kama Mtanzania ninao Uhuru wa Mawazo na Maoni, hiyo ni kwa mujibu wa Katiba yetu, Ibara ya 18. Kitendo cha mimi kuitwa mbele ya Kamati yako kwa maoni yangu haya, naamini ni mwendelezo wa kufinywa kwa haki na uhuru wa mawazo na maoni ya raia.

Mimi kama mtanzania ninaruhusiwa kuwa na maoni yangu, na pia nina haki ya kutoa maoni yangu hayo. Kunituhumu kwa maoni yangu binafsi kuwa yanavunja heshima, hadhi, haki na mamlaka ya bunge, na kuwa maoni yangu hayo ni kulidhalilisha Bunge na Spika si sahihi kabisa, ni uonevu dhidi yangu, ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kinyume na Haki za Binadamu, hasa kwa kuwa mifano hiyo 10 niliyoitoa imeonyesha usahihi wa maoni yangu hayo.

Maoni yangu yalilenga kulinda hadhi, haki, heshima na madaraka ya bunge letu tukufu. Ni maoni yaliyolenga kulinda heshima ya spika, ili azitumie nguvu alizonazo kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Bunge kulinda heshima na hadhi ya Bunge isiporomoke, ni maoni yaliyolenga kuonyesha imani niliyokuwa nayo juu yake (Spika), ni maoni yaliyolenga kulizindua Bunge juu ya hali ya kukosa mshawasha/msisimko ambao Watanzania wameuzoea.

Tafsiri kuwa maneno yangu kuwa Spika hajafikia viwango vya Maspika waliotangulia kabla yake kuwa ni kumdharau si sahihi. Maoni yangu hayakulenga kuonyesha dharau, bali yalilenga kutaka Bunge liyalinde yale mambo mazuri yaliyosimikwa na Maspika hao wa nyuma katika kuisimamia Serikali.

Jambo hili (la kutaka kuendelezwa na kulindwa kwa mambo mazuri ya maspika wa nyuma yaliyoimarisha hadhi ya Bunge) ni ahadi ya Spika wetu, ndugu Ndugai, wakati wa kikao maalum cha Bunge cha msiba wa Spika wa Bunge la 9, ndugu Samuel John Sitta. Hivyo ni dhahiri, mimi kukumbushia ahadi hiyo ya Spika mwenyewe haiwezi kwa namna yoyote ile kuwa ni kudhalilisha Bunge na kumdhalilisha Spika, bali kitendo cha kuitwa hapa mbele ya kamati yako kwa maoni yangu binafsi nje ya bunge, maoni yaliyolenga tu kukumbushia ahadi husika, hakika kinalidhalilisha Bunge na Spika wa Bunge

Kuona mawazo huru haya yangu kuwa ni kudhalilisha Bunge si sawa. Ni kinyume kabisa na misingi ya TANU iliyoasisi Utaifa wetu, ni kinyume na Utanzania wetu. Wananchi wangapi wataletwa mbele ya Kamati yako kuhojiwa kwa kutoa maoni yao juu ya hadhi ya mhimili wa Bunge?

Imani yangu ni kuwa, Hadhi, Heshima, Haki na Madaraka ya Bunge haitotokana na kuhoji wanaotoa maoni juu ya mwenendo wa bunge, kutumia maguvu ya Jeshi la Polisi, wala vitisho vya Kiongozi wa Mhimili wetu huu dhidi ya wabunge, bali ni mwenendo wake wa kuisimamia Serikali mbele ya umma ndio utakaojenga hadhi, heshima, haki na madaraka ya Bunge kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti

Iwapo Bunge litaendelea kuwa 'paraded ' Ikulu kila wakati na kupewa maelekezo na wakati mwengine kusimangwa na Serikali, kupitia Rais, umma utaona sio Bunge lao bali ni Tawi tu la Serikali, na kamati yako itakuwa na kazi ya kuita maelefu ya Watanzania.

Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.

Naomba Kuwasilisha.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto,
Mbunge, Kigoma Mjini - ACT Wazalendo ,
Dodoma .
Septemba 21, 2017.

Hamisa Mobetto Kufunguka Jumatatu na Kueleza Jinsi Diamond Alivyo Ahidi Kumuoa

0
0
Jumatatu kuanzia saa saba mchana Ndug Hamisa Mabeto atafunguka kupitia Clouds Fm kwenye kipindi cha XXL!Hii.imekuja baada ya mzazi mwenzie Diamond Platinumz kufunguka wazi na kueleza mengi kuhusu wao na kumkana hadharani japo alimkubali mtoto...
Moja ya mambo yaliyo mkera Hamisa ni kitendo cha Diamond kusema hawakuwa na ahadi yeyote ile wakati ukweli ni kwamba Diamond Platinumz alimuahidi kumuoa kabisa na ndio maana alikubali kutembea nae na anasema Diamond alisema anampenda yeye kuliko Zari!

Pamoja na hilo Hamisa anakuja kukanusha kuhusu mambo mengi aliyo yasema Diamond hasa ya kusema alikuwa anampa kila siku elfu 70+ na kumkubali mtoto toka mwanzo...jambo ambalo Hamisa anasema ni urongo...

Sasa anasema jumatatu atasema mengi na atasema kila kitu na kuhusu aliyekuwa ana record video zao na aliyekuwa ana husika kuzivujisha....

Wana jamvi naomba niishie hapa na tusubiri jumatatu saa 7 clouds Fm.

NB: Huu unaweza kuwa mwaka mbaya kwa Diamond maana Hamisa anakuja kumwaga mboga na kutoboa masufuria kabisa...
Wale ambao hampendi habari za Diamond na Zari nawashauri.msitumie Smart phone mpaka mwakani maana hii iliyobaki ni ya habari zao tuuu...

Wasalaam...

Mjini Kuna Mambo Mambo Zari amdhihaki hamisa, Hamisa Ajibu Hivi

0
0
As usual wazazi mwenza wa mondi bin laden aka chibu dee aka simba baba Abdul,au baba latifa Leo wameendeleza drama na kutuacha wambea wa snap chat name IG hooii baada ya Mama watano kutuma ujumbe huu km dongo kwa mama
Hamisa sio mchache akajibu hivi  



Ngoma draw ila hapo mobeto ataonekana mkorofi maana bibie bossylady kafuta fastaa baada ya kuona kachenjiwa na mashabiki

Ngoja tuendelee kufaidi uhondo na hivi hali zenyewe za kupambana nazo wallahi mjini patamu

My advice Zari na hamisa ninyi wazazi acheni utoto kama kiki mshapata inatosha msiwajengee chuki watoto wenu na kati yenu nyote mahawara hakuna mwenye ndoa

Jitambueni bwanaa mbea mimi mnanikwaza japo umbea mtamu

Jaji Mkuu Aibuka 'Waliompiga Lissu Risasi Watashughulikiwa, Asisitiza Wapelelezi wa nje Hawana Uwezo wa Kukusanya Ushahidi"

0
0
Jaji Mkuu Prof I. Juma amesema suala la kupigwa risasi Lissu, upelelezi ukikamilika na ushahidi ukawepo, watalishughulikia kama Mahakama

Amesisitiza hakuna wapelelezi wanaweza kutoka nje na kuweza kukusanya ushahidi

"Tukio hilo ni la kihalifu , uhalifu Mkubwa, ni jaribio la kuua na kitu cha kwanza ni kukusanya ushahidi na huo ushahidi utakusanywa hapa hapa Tanzania, asikudanganye mtu kwamba mtu atakayetoka nje atakuwa na uwezo wa kukusanya ushahidi" amesema jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma. VIDEO:

Majaliwa Azindua Mradi wa Maji Longido

0
0
Majaliwa Azindua Mradi wa Maji Longido
Baadhi ya wabunge wa CCM wameonekana kumpigia kampeni za chinichini aliyekuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Longido (CCM), Dk Steven Kiruswa kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 mbele ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliyekwenda kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Longido.

Juni 29, 2016, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitengua ushindi wa mbunge wa Longido, Onesmo Ole Nangole (Chadema) na sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) inasubiriwa kutangaza kama liko wazi na tarehe ya uchaguzi.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha (CCM), Catherine Magige alitumia nafasi ya kusalimia wananchi aliyopewa na mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo kumtambulisha Dk Kiruswa na kusema amekuwa akimtuma bungeni kuzungumzia matatizo ya Longido.

“Yale ambayo nimekuwa nikiyazungumza bungeni kuiomba Serikali, huyu hapa (akimwonyesha) Dk Kiruswa ndiyo alikuwa ananiambia, kila siku ananisumbua kwenye simu. Yeye hakushinda ubunge lakini anatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia mimi,” alisema Magige.

Dk Kiruswa alisimama jukwaani na kuwasalimia wananchi na kuwaahidi kwamba hata umeme ambao wamekuwa wakiulilia wataupata.

Alisema, “…umeme pia nasikia mtaupata, nimekuwa nikiwasumbua kwa ajili ya vile vijiji ambavyo hakuna (umeme).”

Gambo aliwatambulisha wabunge wengine wa CCM akisema wamekuwa wakilizungumzia Jimbo la Longido katika kipindi chote cha mwaka mmoja ambacho wamekuwa hawana mbunge.

“Huu ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na nilipokuwa naongea mambo ya maji nilikuwa nafikiria Longido, nilikuwa nafikiria Mererani, nilikuwa nafikiria Orkesmet,” alisema Mary Nagu, mbunge wa Hanang’ alipokuwa akisalimia wananchi.

Naye mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Amina Mollel alisema kwa miaka miwili hawakuwa na mbunge, anaamini kwamba hawatafanya kosa tena kuchagua mtu mwingine.

“Dk Kiruswa oyeee! Huyu ndiye wa kwenu, hajaondoka popote, halafu ni dokta kwa kusoma vidato vyote hivyo. Hamjisikii kuwa na furaha, hamuoni kwamba akija kule anasaidia kutupika ili tuwe wanasiasa wazuri,” alisema Mollel wakati akisalimia wananchi.

Gambo naye alisisitiza kwamba Dk Kiruswa amekuwa akimsumbua kuhusu shida za wananchi wa Longido. “…kwa sababu mimi sina kinga kama za wabunge, mimi nawatakia kila la heri wananchi wa jimbo hili.”

Baada ya tambo na kampeni hizo za chinichini, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alianza hotuba yake akisisitiza kwamba Serikali itahakikisha inakabiliana na changamoto zote katika Wilaya ya Longido ikiwamo uhaba wa maji.

Majaliwa alizindua ujenzi wa mradi wa maji wa Longido ambao unaanzia kwenye chanzo cha maji cha Mto Simba kilichopo Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, umbali wa kilomita 65 mpaka Longido. Mradi huo utagharimu Sh15.8 bilioni na utahudumia watu 26,145 utakapokamilika Julai, 2018.

Majaliwa alisema Rais John Magufuli aliahidi kwenye kampeni zake za uchaguzi kwamba atapeleka maji kwenye wilaya hiyo na sasa ametimiza.

“Nataka niwahakikishie, mkakati wa kupeleka maji uko kwenye kampeni iliyoanzishwa na Rais wetu ya kumtua mama ndoo kichwani. Kampeni hii imewezesha ongezeko la fedha za bajeti kwenye wizara yenyewe,” alisema Waziri Mkuu.

Kiongozi huyo alisema lengo la Serikali ni kuongeza pia maji kwa ajili ya kunywesha maji ili mifugo ya wananchi nayo iweze kupata maji sambamba na matumizi mengine ya majumbani.

Alisema bado kuna haja ya kutumia vyanzo vya maji ya mvua ili kuvuna maji hayo kwa ajili ya kujaza mabwawa ya kunyweshea mifugo. Alisema mradi huo ni mkubwa na maji yatakuwa ya uhakika na mengi yatapatikana.

“Namuagiza Waziri wa Maji, endelea kufuatilia vyanzo vingine vya maji, leta wataalamu waje wafuatilie vyanzo vya maji. Ukitoka hapa uende na Loliondo, wataalamu wako watafute vyanzo vya maji ili kumaliza kabisa tatizo la maji,” alisema.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge alisema mradi wa maji wa Longido umekuwepo tangu mwaka 2010, lakini Serikali ya Awamu ya Tano imetenga fedha na kuanza kuutekeleza.

Alisema upatikanaji wa maji Longido ni asilimia 15 pekee, kiwango ambacho bado kipo chini ukilinganisha na kiwango cha kitaifa cha upatikanaji wa maji cha kitaifa ambacho ni asilimia 72 huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 85.

“Wananchi nanyi mjenge utamaduni wa kuvuna maji ya mvua wakati ujenzi wa mradi huu unaendelea,” alisema Lwenge na kuwataka wakandarasi watakaojenda mradi huo kufanya kazi kwa viwango vilivyowekwa na kuhakikisha unakamilika kwa wakati.



Trump Atangaza Kuongeza Vikwazo Zaidi kwa Korea Kaskazini

0
0
Trump Atangaza Kuongeza Vikwazo Zaidi kwa Korea Kaskazini
Rais Donald Trump amesaini sheria mpya ya kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini juu ya mpango wake wa nuklia.
Waziri wa fedha wa Marekani ameidhinisha vikwazo hivyo dhidi ya makampuni ya fedha yanayofanya biashara zake ndani ya Korea Kaskazini.
Rais Trump pia amesema kuwa Benki Kuu ya Uchina iliagiza benki nyingine za Uchina kuacha kufanya biashara na Korea Kaskazini.

Hatua hii inakuja katika kipindi cha chini ya wiki mbili baada ya Umoja wa Mataifa kuidhinisha vikwazo ipya dhidi ya taifa hilo kwasdababu ya jaribilo lake la hivi karibuni la nuklia.
Hali ya wasi wasi imetanda katika kipindi cha wiki za hivi karibuni kutokana na hatua ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu, licha ya shinikizo kutoka kwa mataifa tajiri zaidi duniani.

Kajala Awatolea Povu Wanaomsema Anatoka na Mume wa Mtu

0
0
Kajala Awatolea Povu Wanaomsema Anatoka na Mume wa Mtu
STAA kiwango kunako filamu Bongo, Kajala Masanja kwa mara ya kwanza ametokwa povu kuwa hakuna kitu ambacho anakichukia katika maisha yake kama mtu kumbambikia kiki ambazo zinahusiana na kutembea na mume wa mtu au bwana wa mtu kwa sababu haimjengei chochote kwenye jamii zaidi ya kumuharibia.

Akizungumza na Ijumaa, Kajala, alisema kuna watu wengi wako radhi kutengeneza kiki kama hizo za kuchukuliana mabwana lakini kwake hazitaki na zinamkera sana kwa sababu mambo hayo yameshapita na wakati na kwanza pia hayamjengei chochote kwenye jamii zaidi ya kumuharibia.

“Kiki kama hizo sizitaki kabisa kuzisikia kwanza zinaniharibia wala hazinijengi chochote kwenye jamii yangu zaidi ya kuniletea picha tofauti kwenye jamii yangu,” Kajala alitoa povu.

Tume ya Uchaguzi Kenya Imebadirisha Tarehe ya Uchaguzi wa Marudio

0
0
Tume ya Uchaguzi Kenya Imebadirisha Tarehe ya Uchaguzi wa Marudio
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), imebadilisha tarehe ya kufanyika uchaguzi wa marudio wa Urais ambao sasa utafanyika Oktoba 26.

Awali, uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Oktoba 17, siku 60 baada ya uamuzi wa Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya uchaguzi wa awali uliompa ushindi Uhuru Kenyatta wa Chama cha Jubilee.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Tume hiyo, Wafula Chebukati imeeleza uamuzi huo umefikiwa ili kuipa IEBC muda wa kujiandaa zaidi na hasa katika masuala ya teknolojia.

“Ni dhahiri kuwa, kufutwa kwa uchaguzi kumeleta athari na hasa kwenye teknolojia itakayotumika,” amesema.

Chebukati amesema, “Ili kuhakikisha tume inajiandaa kuleta uchaguzi wenye viwango vinavyohitajika na Mahakama ya Juu, tunapenda kuujulisha umma na wadau wote kuwa uchaguzi mpya utafanyika Alhamisi Oktoba 26.”

Tume pia imesema itayapitia maagizo ya Mahakama ya Juu kuhusu uchaguzi wa marudio.

Kenya Septemba Mosi iliweka historia baada ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya Urais yaliyompa ushindi Rais Kenyatta kuwa madarakani kwa muhula wa pili.

Mgombea wa Muungano wa Nasa, Raila Odinga alifungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Agosti 8, akisema ulitawaliwa na udanganyifu ikiwemo kuchezewa mitambo ya kujumlishia matokeo.

Katika uchaguzi wa Agosti 8, Kenyatta alitangazwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27, huku mpinzani wake Odinga akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74.

Kichuya Aibuka Kidedea Mchezo wa Jana Dhidi Mbao

0
0
Kichuya Aibuka Kidedea Mchezo wa Jana Dhidi Mbao
Kiungo mahiri wa wekundu Msimbazi, Shiza Ramadhani Kichuya amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi iliyopigwa jana dhidi ya Mbao FC mchezo uliyopigwa katika viunga vya CCM Kirumba uliopo Jijini Mwanza.

Hayo yamewekwa wazi na taarifa iliyotolewa na ukurasa maalum wa Simba SC usiku wa kuamkia leo baada ya kiungo huyo kuisaidia timu yake kwa kuipatia bao la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC, katika mechi ya ufunguzi wa mzunguko wa nne katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea kutimua vumbi.

"Kiungo mahiri Shiza Kichuya amechaguliwa na wapenzi wa Simba kuwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Mbao FC. Shiza kichuya amekuwa akifanya vizuri katika nafasi ya kiungo mchezeshaji pia kweye safu ya ushambuliaji na hivyo kumfanya kuwa kiungo muhimu kwenye kikosi cha Simba", imesema taarifa hiyo.

Shiza Kichuya anakuwa mcheza wa pili kuchaguliwa na timu yake kuwa mchezaji bora tokea ilipoanza michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mwanamke Tajiri Zaidi Duniani Mmiliki wa L'Oreal Amefariki

0
0
Mwanamke Tajiri Zaidi Duniani Mmiliki wa L'Oreal Amefariki
Liliane Bettencourt, ambaye ni mrithi wa kampuni ya vipodozi ya L'Oreal, amefariki akiwa na umri wa miaka 94, familia yake imethibitisha.
Kauli ya familia inasema kuwa amefariki ''kwa amani'' nyumbani kwake wakati wa usiku.
Huku thamani ya makadirio ya mali zake mwaka 2017 ikiwa ni dola bilioni 33 ama dola bilioni $40 Bi Bettencourtalikuw andiye mwanamke tajiri zaidi duniani.
Aliondoka kwenye bodi ya kampuni hiyo 2012 na baada ya hapo alionekana mara chake katika umma , lakini alisalia katika habari kwasababu ya kesi yake iliyopata umaarufu iliyofuatia kupatikana kwake na ugonjwa wa ubongo.

Katika kauli yake, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya L'Oreal Jean-Paul Agon amesema: "sote tulimuhusudu sana Liliane Bettencourt ambaye wakati wote alisimamia kampuni ya L'Oreal, na wafanyakazi wake, ambaye pia alijivunia maendelea na mafanikio ya kampuni yake.
" Binafsi alichangia sana katika mafanikio yake kwa miaka mingi sana. Mwanamke bora wa urembo ametuacha na hatutamsahau."

Mrithi huyo wa Kampuni ya L'Oreal aliingia katika mzozo wa umma na binti yake , Francoise Bettencourt-Meyers, mwaka 2007.
Bi Bettencourt-Meyers aliwasilisha kesi yake mahakamani ambapo binti huyo alisema ana wasiwasi kwamba mama yake anatumiwa vibaya wasaidizi wake kikazi kutokana na afya yake ikiendelea kuzorota.
Ilifichuliwa mwaka 2008 kwamba mpigapicha ambaye alikuwa rafiki yake, François-Marie Banier, alizawadiwa zawadi zenye thamani ya mamilioni ya dola -ukiwamo mchoro wa Picasso pamoja na kisiwa cha heka 670 katika visiwa vya Ushelisheli.
Bi Bettencourt-Meyers alisema alichukua hatua za kisheria dhidi ya Bwana Banier baada ya kuambiwa na mfanyakazi wa nyumbani wa mama yake kwamba alikuwa anapanga kumuasili.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images