Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Jeshi la JWTZ Laanza Kutekeleza Agizo la JPM Waanza Kujenga Ukuta

0
0
Jeshi la JWTZ Laanza Kutekeleza Agizo la JPM Waanza Kujenga Ukuta
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ limeanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kujenga ukuta na kuweka kamera katika eneo linalopatikana madini ya Tanzanite huko Mererani.

Meja Jenerali Michael Isamuyo ametua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa Helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimbaji na wananchi wa Manyara wamefurahia na kuahidi ushirikiano.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo jana alipokuwa akiwahutubiwa wananchi wa Simanjiro kabla ya kufungua barabara ya KIA – Mererani yenye kilomita 26.

Mobetto Amekosea Kulala Katika Kitanda Cha Mwanamke Mwenzake Alitakiwa Kuwa na Huruma -Davina

0
0
Mobetto Amekosea  Kulala Katika Kitanda  Cha Mwanamke Mwenzake Alitakiwa Kuwa na Huruma -Davina
STAA wa filamu Bongo Halima Yahya ‘Davina’ amemlipua mwanamitindo maarufu, Hamisa Mobetto kutokana na ishu ya kuzaa na Mbongo Fleva ambaye ni mwandani wa Zarina Hassan ‘Zari Boss Lady’.

Akizungumza na Star Mix kutokana na sekeseke hilo baada ya mwanamuziki huyo kuweka wazi kwamba ni kweli mtoto huyo ni wake alisema, kitu  ambacho anakiona wote wawili wana makosa, iweje Mbongo Fleva huyo alale na mtu mwingine kitanda anacholala na mwanamke wake, pia kwa nini Mobetto alikubali kulalia kitanda hicho bila huruma kwa mwanamke mwenziye.

“Hili swala kilichonifurahisha ni baada ya huyo mwanaume kukiri kumzalisha Hamisa, lakini nikiongea kwa kumshauri kama mwanamke mwenzangu, hata kama alikuwa naye hakupaswa kukubali kulalia kitanda kimoja,” alisema.

Neema Yazidi Kumdondokea Mobetto Baada ya Rav4 Sasa Diamond Kumnunulia Prado

0
0
Neema Yazidi Kumdondokea Mobetto Baada ya Rav4 Sasa Diamond Kumnunulia Prado
Mwanamitindo ‘hot’ ambaye kwa sasa amegeuka mswaki kutokana na kuongelewa kila kona, Hamisa Mobetto, amewaacha watu njia panda baada ya kupost picha ya gari aina ya Prado yenye thamani ya zaidi ya milioni 50, mashabiki wanadai baada ya ile Rav 4, hiyo ni zawadi nyingine anatarajia kupewa na mzazi mwenziye ambaye ni Mbongo Fleva aliyezaa pia na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Mobetto aliposti picha ya gari hiyo na kuandika jina la mtoto wake.
“Dee Platnumz”
Kufuatia kauli ya Mobetto ya kudai kwamba yeye ndiye mwanamke pekee anayependwa na mwanamuziki huyo, mashabiki wakasema kwamba inawezekana ameagiziwa ndinga hiyo kwa ajili ya kumpeleka mtoto kliniki.

Serikali Yaitaka Bodi TTCL Kujikita Kwenye Ubunifu wa Kiushindani

0
0
Serikali Yaitaka Bodi  TTCL  Kujikita Kwenye Ubunifu wa Kiushindani
Serikali imeaiambia bodi mpya ya wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kuacha kuremba, badala yake wajikite kwenye ubunifu huku wakijielekeza kwenye ushindani dhidi ya kampuni zingine za mawasiliano nchini.

“Nataka bodi mjue tunakwenda wapi katika kampuni hii, lakini pia tunahitaji kufanya kazi kwa juhudi kushindana na kampuni nyingine za simu,” alisema Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akizindua bodi hiyo jana ambapo aliongeza kuwa; “Mhakikishe mapato makubwa yanatoka kwenye data, halikadhalika mnapaswa mjue nguvu yenu iko wapi maana tusipojibu maswali haya hatuwezi kufanya ushindani na kampuni nyingine.”

TTCL ambayo ilibaki nyuma kiushindani kwa muda mrefu, hivi sasa imeibuka kwa nguvu baada ya Serikali kuamua kuirejesha mikononi mwake kutoka kwenye ubia baina yake na Airtel.

Hata hivyo, Profesa Mbarawa alisema asingependa kuiona ikijivutavuta katika hali ya sasa ya soko la mawasiliano ambalo linahitaji ubunifu na mikakati mathubuti ili kuweza kumiliki soko.

Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TTCL, Omary Nundu alisema tangu ateuliwe wamefanya mambo mengi hadi sasa ikiwamo kuifufua kampuni hiyo, kushirikiana na wadau wengine wa mawasiliano pamoja na kuanzisha huduma ya utumaji na upokeaji wa fedha maarufu kama TTCL Pesa.

Nundu alisema mwaka 2016, TTCL ilipata Sh0.21 bilioni katika soko na mwaka huu wanatarajia kupata Sh0.3bilioni na kwamba wanatarajia faida ya zaidi ya Sh40 bilioni ifikapo 2022 baada ya makato ya kodi.

Huyu Hapa Bwana Mpya wa Wema Mahaba Moto Moto Wafumwa Wakifanya Yao Kwenye Kochi

0
0
Huyu Hapa Bwana Mpya wa Wema Mahaba Moto Moto Wafumwa Wakifanya Yao Kwenye Kochi
MALKIA wa Filamu za Bongo, Wema Sepetu amenaswa LIVE akiwa na mwanamme anayedaiwa kuwa ni bwana wake mpya. Wawili hao wamenaswa wakijiachia tena mchana kweupe peee huku Wema akijibebisha kwenye kifua cha jamaa huyo!

Wakiwa wanapiga stori za hapa na pale na mara anasikika Wema akitema madongo kumponda mpenzi wake wa zamani ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, kwamba alishamshauri aiboreshe perfume hiyo kama anataka iwe na viwango lakini mwenyewe akamwambia kwamba anataka aiuze kwa watu wa daraja la chini na kati.

Utaratibu ni Upi Katika Matibabu ya Lissu Kutokana na Kauli Hizi za Viongozi

0
0
Utaratibu ni Upi Katika Matibabu ya Lissu Kutokana na Kauli Hizi za Viongozi
Hizi ndizo kauli zilizotolewa na viongozi kuhusu matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu baada ya kupelekwa jijini Nairobi.

Katika kauli hizo Spika wa Bunge, Job Ndugai anaeleza kuwa utaratibu wao wa kumpeleka Lissu nje ni lazima apitie Muhimbili kwa kuwa Bima ya Afya ndivyo inavyotaka.

Hata hivyo, Mbunge wa Iringa Mjini(Chadema), Mchungaji Peter Msigwa anasema kuwa bima walizo nazo wabunge hazifanyi kazi nje ya nchi ndiyo maana hata Kenya wamewashangaa.

Lakini Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu hivi sasa anasema Serikali iko tayari kumtibia Lissu mahali popote duniani. Sasa swali la kujiuliza utaratibu ni upi?

Amber Lulu Afunguka Alivyokimbiwa Hotelini Mpenzi Wake Rammy Galis

0
0
Amber Lulu Afunguka Alivyokimbiwa Hotelini Mpenzi Wake Rammy Galis
MSANII na mnenguaji  wa kwenye video za wasanii (video vixen) Amber Lulu, ambaye  anatamba na wimbo wake wa Only You amefunguka kuhusu kukimbiwa hotelini na aliyekuwa mpenzi wake wa kwanza tangu anafika Dar es salaam, mwigizaji Rammy Galis, bila sababu.

Alipoulizwa juu ya  stori hiyo, Amber Lulu alifunguka na kusema:
“Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa Rammy Galis kipindi nafika Dar, tulikubaliana vizuri na Rammy tukaenda hotelini tukaagiza vyakula tukala na mambo mengine yakaendelea. Baadaye akaniambia nakuja, nikamwambia poa lakini mwisho wa siku sikumuona.  Nikawa napiga simu yake mara asipokee na akipokea basi akawa ananiambia nisubiri kidogo.  Sikujua kwa nini alikuwa anafanya hivyo.”

Aliongeza kwamba: “Alinipokea mizigo vizuri tukaingia hotelini baada ya hapo ndo akafanya alivyoamua kufanya, basi mimi nikampigia dad’angu simu nikamuelezea akaniambia hayo ni mambo ya kawaida basi dada  akanitumia pesa nikalipia kila kitu. Baada ya hapo nikarudi zangu nyumbani na sikuwahi kuwasiliana naye tena  tangu siku hiyo. “

Amber ni mwanamke asiyeishiwa kiki na skendo mjini lakini hajalikitu, anaangalia maisha yake tu.  Ni msichana ambaye haogopi kufunguka mambo yanayohusiana na mahusiano yake.  Haogopi kiki bali anazipenda kiki.

Rais Mugabe Amshambulia Trump

0
0
Rais Mugabe Amshambulia Trump
Rais Robert Mugabe amemshambulia Rais Donald Trump wa Marekani katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa akimkejeli kuwa sawa na sanamu kubwa la Goliath lililonakshiwa kwa dhahabu.

Akihutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) ambako shutuma za viongozi wengine hazikulenga mtu binafsi, kiongozi huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 93 alimsuta Trump kwa sera zake na mwonekano wake.

"Baadhi yetu,” alisema Mugabe na kusita kidogo kuweka msisitizo “tulikerwa sana kama si kuogofywa na kile kilichoonekana ni kurejea kwa “Goliath Mkubwa wa Dhahabu” aliyetajwa kwenye biblia.

Katika Biblia Takatifu, Goliath anatajwa kuwa alikuwa askari mkubwa, mwenye nguvu na kiongozi madhubuti wa jeshi, lakini aliuawa kwa jiwe lililorushwa kwa silaha dhaifu aina ya kombeo tena na kijana mdogo Daudi.

"Je, tunaye Goliath wa kwenye biblia miongoni mwetu, ambaye anatishia kuzifuta nchi nyingine kwenye uso wa dunia?" alihoji Mugabe kauli iliyoamsha watu kumshangilia kwa nguvu kwenye ukumbi huo huku wanadiplomasia wawili wa Marekani wakisikitahayari.

"Na labda nitoe wito kwa Rais wa Marekani kwamba Bwana Trump tafadhali piga tarumbeta kunakshi muziki wa kuelekea kuimarisha tunu za umoja, amani, ushirikiano, mshikamano, majadiliano ambazo mara zote tumekuwa tukisimamia na ambazo zimeandikwa vizuri katika waraka wetu unaoheshimika sana, Katiba ya Umoja wa Mataifa.”

Trump aliwashangaza watu wengi katika UN Jumanne iliyopita aliposimama kwenye jukwaa kutishia “kuiangamiza” Korea Kaskazini huku akimwita kiongozi wake Kim Jong-Un kuwa "Rocket Man" yaani Mzee wa Maroketi.

Kwa muda mrefu Mugabe ana uhusiano mgumu na nchi za Magharibi ambazo zimemwekea vikwazo vya kiuchumi kushinikiza demokrasia katika nchi yake aliyoiongoza kwa miaka 37 sasa.

Katika hotuba hiyo, vilevile Mugabe alipaza sauti hasa kuhusu mipango ya Trump kuiondoa Marekani kwenye mkataba wa Paris unaohusu mabadiliko ya tabia nchi.

Mugabe alihimiza ushirikiano "kwa lengo la kuzuia mwenendo usiofaa utakaosababisha uharibifu wa mazingira ambayo sote tunategemea kwayo”

 

Lema Amjibu Waziri wa Afya Baada Serika Kukubali Kumtibia Lissu Asema Familia ya Lissu Haijashindwa Kumgharamikia Matibabu

0
0
Lema Amjibu Waziri wa Afya Baada Serika Kukubali Kumtibia Lissu Asema Familia ya Lissu Haijashindwa Kumgharamikia Matibabu
Mbunge wa Arusha Mjini Gobless Lema amemjibu Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu kauli aliyotoa jana kuwa serikali ipo tayari kumtibu Lissu endapo familia yake itaomba kwa serikali, Lema amesema kuwa familia ya Lissu hajashindwa kumgharamia matibabu.

Lema amesema kuwa anaamini familia ya Tundu Lissu ni Watanzania wote ambao wanapenda haki na Demokrasia ndani ya nchi, na wote ambao wanaumizwa na jambo hilo bila kujali itikadi zao hivyo watachanga shilingi moja moja kwa ajili ya matibabu ya Tundu Lissu na hata ikibidi mali zao watauza ili kuweza kumuwezesha Tundu Lissu kupata matibabu.
"Familia ya Lissu ni Watanzania wote wanaopenda utawala wa sheria, Utawala wa Demokrasia, familia ya Lissu ni Watanzania wote bila kujali itikadi zao ambao wanajisikia vibaya kwa matendo ya kihalifu kwa wabunge kupigwa risasi hadharani na bunge lisichukue hatua stahiki hii ndiyo familia ya Lissu, mtu yoyote ambaye anaguswa na ubinadamu na familia hii haijashindwa kumlipia matibabu tutachanga shilingi moja moja ikiwa ni lazima sana tutauza hata mali zetu kuhakikisha kwamba Mhe. Tundu Lissu akosi fedha za matibabu" alisema Godbless Lema


Waziri wa Ujenzi Atoa Agizo kwa Balaza la Ujenzi

0
0
Waziri wa Ujenzi Atoa Agizo kwa Balaza la Ujenzi
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameliagiza baraza la ujenzi nchini kuhakikisha linaandaa taarifa kamili kuhusuiana na ujenzi ili kuondoa changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara kwa mara pindi miradi inapotaka kuanza.

Prof. Mbarawa amesema hayo leo katika kikao chake na baraza la ujenzi, ambapo kimewakutanisha wataalamu wa ujenzi kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuangalia changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo na kuzitafutia ufumbuzi.

"Kwa sasa hakuna taarifa sahihi kuhusu masuala ya ujenzi nchini, sekta ambayo inachangia kwa asilimia 14 ya pato la taifa na haikui kiushindani na nchi zilizoendelea kwa kiwango cha kisasa", amesema Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi nchini, Prof. Mayunga Mkunya amesema hakuna ushirikiano mzuri katika sekta ya ujenzi hali ambayo inachangia kukosa kuwa na mipango endelevu.




Hamisa Mobetto Kuamia Madale Atupa Dongo Awataadhalisha Wapangaji Awaambia Mwenye Nyumba Kaja

0
0
Taarifa zinazosamba kwa sasa kuhusu Hamisa Mobetto na Diamond Platnumz zimekuwa nyingi huku Udaku mwingi ukipatikana kwenye SnapChat zao

Kuna tetesi tatu kubwa kwa sasa zinazohusu Hamisa kununuliwa gari aina ya #Prado Land Cruise , Hamisa Mobetto Kuhamia State House, Nyumbani kwa Diamond Platnumz Madale, Na Hamisa kutafuta Mpacha na Diamond.
Maneno haya kwenye SnapChat yamezua tetesi kuwa Hamisa anataka Mpacha na Diamond 
Na Snap hii kuhusu wapangaji imezua tetesi kuwa Hamisa Mobetto anampango wa Kuhamia State House na Diamond Platnumz

Mwanamke Kutoka Burundi ‘HONEY JESCA’ Afunguka Kuzaa Mapacha na Diamond

0
0
Mwanamke Kutoka Burundi ‘HONEY JESCA’ Afunguka Kuzaa  Mapacha na Diamond
Drama mpya kwenye mtandao wa Instagram Tanzania imeibuka 9/21/2017 baada ya mwanamke anayejiita Miss Burundi 2012 #HoneyJesca kusema watoto wake mapacha ni watoto wa msanii wa Bongo Fleva DIAMOND PLATNUMZ,

Kwa mujibu wa Hizi Post zake na maneno yake anasema alijifungua watoto hawa mwaka 2013.

Post ya Kwanza Jesca anasema >>“Abo ni batoto ma pacha nilizalaka na @diamondplatnumz toka 2013 mupaka leo tulikutanaga nae wakati alikuyaka kwetu burundi kwa ajili ya kuimba ndipo alipo nionaga na kumtuma kijana aitwae #mafya ila tokea hapo hajawai kunipatiya huduma yoyote mupaka leo nakama haamini nipo tayari tuende kupima DNA japokuwa kuko batu benye banazania miye natafuta kiki no no no but nipo serious kwa hili na ukweli haujifichi pls @diamondplatnumz nimelea toka mwanzo now nataka ukuye ubakamate na aba ba mapasa ubaleye nimechoka“

Post ya Pili Jesca anasema >>@zarithebosslady Umejitaidi mpaka umefanikiwa kuhack account yangu ambayo ilikuwa na followers 450K
Saaa ulikuwa unaogopa nisikuumbuwe nataka niweke wazi ukweli woote wewe ni mganda na mimi ni mrundi halisi kujuwana mimi na wewe isiwe tabu

1. Mimi toka nilipo zaa na @diamondplatnumz toka mwaka 2013 mpaka leo hajawai hata kutowa shilingi100 ya kumnunuliya hata mtoto sukari ila nina mlea mtoto wangu bila kumtegemea mtu yoyote
2. Mimi nina miaka 24 ila wewe una miaka 46 na ukikataa nitapost photocopy ya passport yako ninayo
3. Wewe uliniporaga #diamond wakati ulikuwa unajuwa ni shemeji yako na mimi nikiwa kama your best friend ila tamaa zikakufanya unigieuke

Saaa leo nataka niweke ukweli woote kwa maana mimi ninakujuwa kuliko baba yako mzazi

Naomba watu woote mjuwe kuwa @zarithebosslady hana kitu chochote kila ni mwanamke aliyejaa tamaa saana akiendaga uganda anaenda sehem moja inaitwa kabaragara anakodisha magari ya kifahari alafu wana tengeneza bati lipo kama pleti number linaandikwa jina lake alafu anapiga nayo foto shoot

Hivi hamujiulizi swali?

1. Huyo zari anavyopendaga sifa za pic kibao
Kuna siku ameshagaonyesha hata check ya 100$? 2. Angekuwa ana pesa kwa nini ashindwe kujenga kaburi ya mama yake mzazi?

@zarithebosslady ulipo onaga #diamondkanitelekeza na mtoto huku burundi ulinichekaga saaana sasa why leo unaumia kumuona #diamond amezaa na @hamisamobetto?  Mimi ni mtoto wa kirundi nataka nikupe adabu

Zari Atoa Tamko Kali..."Sitaki Mtoto wa Hamisa Mobeto Awe Karibu na Watoto Wangu"

0
0
Siku zote Tembo wakipigana zinazoumia ni nyasi! Hiyo imejidhihirisha kufuatia ‘vita ya penzi’ inayoendelea kuunguruma mitandaoni kati ya mwanamitindo Hamisa Mobeto na mfanyabiashara, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ambao wote wawili wamezaa na mwanaume mmoja ambapo vita hiyo sasa wameihamishia kwa watoto, Zari ameibuka na kusema hataki kabisa ukaribu kati ya watoto wake na mtoto wa Mobeto.

 Zari alifikia hatua ya kumtaka mtoto huyo akae mbali mita zisizohesabika na watoto wake, baada ya kuona ‘amewa-follow’ kupitia akaunti yake ya Instagram anayotumia jina la Prince Dylan, alilopewa na baba yake, ambaye ni mbongo Fleva.

Baada ya kitendo hicho, mashabiki hawakumuacha salama Zari. Wakamshushia kichambo cha mwaka huku wakimwambia kuwa ugomvi wao usiwahusishe watoto kwani hao watabaki kuwa ndugu milele na hakuna cha kubadilisha ukweli huo.

Habari Njema Kinga ya Ukimwi Yapatikana...Inauwezo wa Kukukinga Kwa Asilimia 99%

0
0
`Wanasayansi wamekuwa wakitengeneza chembe chembe za kinga ya mwili zinazoweza kushambulia asilimia 99% ya virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi na hivyo kuzuwia maambukizi kuendelea.

Chembe chembe hiyo ya kinga imetengenezwa kwa ajili ya kushambulia sehemu tatu muhimu za virusi na hivyo kuvifanya virusi hivyo kushindwa kuhimili mashambulizi yake.

Kazi ya utengenezaji chembe chembe hizo za kinga ya mwili imetokana na ushirikiani baina ya Taasisi ya Marekani ya Afya na kampuni maduka ya dawa ya Sanofi.

Shirika la kimataifa la kukabiliana na ukimwi -International Aids Society linasema kuwa huu ni "ugunduzi wa kihistoria ".

Majaribio ya kinga kinga hiyo ya mwili kwa binadamu yataanza kufanyika mwaka 2018 kuangalia kama dawa hiyo inaweza kuzuwia ama kutibu maambukiziya HIV

Miili yetu huhangaika kupigana na virusi vya HIV kwasababu virusi hivyo vina uwezo mkubwa wa kujibadilisha katika hali nyingine pamoja na muonekano wake.

Aina kadhaa za virusi vya HIV - katika mgonjwa mmoja zinaweza kufananishwa na zile za mafua wakati wa msimu wa baridi.

Kwa hiyo mfumo wa kinga ya mwili najipata katika vita dhidi ya magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababishwa na HIV.

Lakini baada ya miaka kadhaa ya maambukizi, wagonjwa wachache hujenga silaha kali ya mwili ambapo " Mwili hupunguza uharibifu wa kinga ya mwili " kwa kushambulia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya HIV.

Watafiti wamekuwa wakijaribu kutumia uwezo wa mwili wenyewe wa kupunguza uharibifu wa kinga ya mwili kama njia ya kutibu HIV, ama kuzuwia maambukizi hayo mapema.

Kajala Ashutumiwa Kuongoza Kukwapua Mabwana wa Wenzake

0
0
KUFUATIA uwepo wa tuhuma kwamba anaongoza kwa kukwapua mabwana wa watu, muigizaji kiwango, Kajala Masanja ameibuka na kukanusha vikali madai hayo na kusema anayachukia.

Akizungumza na Amani, Kajala alisema watu wamekuwa wakimwita nyakunyaku na yeye halipendi hilo jina hata kidogo ni bora skendo zote azipitie lakini sio hiyo ya kuiba wanaume za watu.
“Hakuna kitu ninachokichukia kama mtu kuniona mimi ni wa kuchukua mabwana za watu na kunifananisha na nyakunyaku, nakereka mno,” alisema Kajala.

Katika historia yake ya maisha, Kajala amekuwa akihusishwa kukwapua bwana wa Wema Sepetu, maarufu kama CK pamoja na msanii wa Bongo Fleva.

 Stori: Imelda Mtema

Mbowe Apinga Kauli ya Serikali Asema Lissu Hatosafirishwa Nje ya Kenya Kwa Matibabu

0
0
Mbowe Apinga Kauli ya Serikali Asema Lissu Hatosafirishwa  Nje ya Kenya Kwa Matibabu

Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe, amesema Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hatosafirishwa kwenda popote mpaka pale madaktari watakaporuhusu.

Mhe. Mbowe ameeleza hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari ikiwa imepita siku moja tokea serikali ya Tanzania itoe kauli yake kuwa ipo tayari kumtibia Lissu popote pale duniani kupitia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu.
"Tundu Lissu bado ni mgonjwa sana, hawezi kusafirishwa nje ama kutikiswa kwa njia yeyote katika kipindi hiki kwa hiyo mpango wowote wa kumuondoa hospitalini Nairobi kumpeleka nchi yeyote hautokuwepo kwa sasa mpaka hapo madaktari watakaporuhusu kulingana na hali yake", amesema Mbowe.
Pamoja na hayo, Mbowe ameendelea kwa kusema "Madaktari wametuhakikishia wana vifaa, dawa, utaalamu wa kukamilisha awamu ya pili ya matibabu ya Mhe. Lissu na yatafanyika hapo hapo katika hospitali ya Nairobi, Kama kutakuwa na ulazima katika hatua za baadae basi hizo zitafanyika kulingana na ushauri wa madaktari".
Aidha, Mbowe amesema wamelazimika kumuwekea ulinzi mkubwa Lissu katika hospitali aliyolazwa kutokana na kuhofia hali ya usalama iliyokuwa imetanda juu ya Mbunge huyo kutokana na shambulio alilofanyiwa na watu waliokosa utu.
"Nipende kusema tunawashukuru sana uongozi wa hospitali ya Nairobi, wenzetu walielewa hofu yetu na wametoa ulinzi wa ziada kwa ajili ya Mhe. Lissu masaa 24 ndani na nje. Kwa hiyo Lissu yupo chini ya uangalizi mkali sana na hili lilifanyika kutokana hofu iliyotanda na inayotanda kwa halali kabisa kwa sababu kuna watu walitaka kuondoa maisha ya Lissu lakini hawakuweza kufanikisha kazi yao, na hao watu hawana utu kabisa kwani tukiwapa nafasi hawatasita kukamilisha kazi yao", amesisitiza Mbowe.
Kwa upande mwingine, Mbowe amewataka wanachama wa chama hicho pamoja na watanzania kwa ujumla kutokuwa na hofu kuhusu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwani madaktari wameshawahakikishia kuwa Lissu atapona na kurudi kuendelea katika harakati zake alizokuwa anazifanya kama awali

Rais wa Malawi Amsifu Mugabe Asema Mugabe Ndo Shujaa Pekee Aliyebaki

0
0
Rais wa Malawi Amsifu Mugabe Asema Mugabe Ndo Shujaa Pekee Aliyebaki
Rais wa Malaw Profesa Peter Mutharika amempongeza Rais Robert Mugabe akisema utajiri mkubwa wa historia umemfanya kuwa shujaa pekee aliyebaki wa kupigania utaifa barani Afrika.

Profesa Mutharika alisema mara zote amekuwa akifurahia kukutana kwenye vikao na Rais Mugabe ambaye amemwelezea kama “shujaa pekee aliyesimama” na akaongeza kuwa anajifunza mengi kutoka kwa mwana huyo wa Afrika.

Rais Mugabe na mwenzake huyo wa Malawi wako New York kuhudhuria mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) lililoanza vikao vyake Jumanne.

Akizungumza baada ya kumtembelea Rais Mugabe hotelini kwake, kiongozi huyo wa Malawi alisema Malawi na Zimbabwe zina historia ndefu ambayo haiwezi kusahaulika.

“Tulizungumzia juu ya Malawi na Zimbabwe. Historia ndefe. Unafahamu Rais Mugabe ni kaka yangu. Rais wa zamani wa Malawi na mimi mwenyewe tumefanya kazi kwa upendo mkubwa.

“Zimbabwe na Malawi ni kama nchi moja. Hakuna mgogoro, hakuna mvutano wowote. Urafiki wetu ni asilimia 100,” alisema Profesa Mutharika.

“Nitapenda kwenda Zimbabwe nay eye pia anapenda kuja Malawi. Tumezungumzia juu ya kuendelea kubadilishana ziara katika siku chache zijazo,” alisema.

Kuhusu mikutano yake na Rais Mugabe alisema: “Mara zote huwa najifunza kutoka kwake. Unajua ana utajiri mkubwa wa historia. Huyu ndiye shujaa pekee aliyebaki wa kupigania utaifa wa Afrika na mapambano ya kudai uhuru. Ni kiongozi pekee aliyebaki amesimama. Ana utajiri mkubwa wa historia ya Afrika.

“Kila tunapokutana najifunza mengi kutoka kwake. Yeye huwa anatupatia mtazamo wa wapi tumetoka. Huwa nafurahishwa kukutana naye.”

Kiongozi huyo wa Malawi amezipuuzilia mbali nchi za Magharibi zilizokuwa na matarajio ya kumtumia kuvuruga uhusiano kati ya Malawi na Zimbabwe. Badala yake amezungumza kwa uwazi kuhusu uhusiano mzuri na kiongozi mwenzake wa Zimbabwe.

Kahaba wa Kizungu Afikishwa Katika Mahakama ya Kisutu Leo

0
0
Kahaba wa Kizungu Afikishwa Katika Mahakama ya Kisutu Leo
MWANAMKE Mzungu anayejulikana kwa jina la Monique Honsbeek anayedaiwa kufanya ukahaba katika Jiji la Dar es Salam leo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Victoria Nongwa na kusomewa shitaka moja la kuishi nchini bila kibali.

Mtuhumiwa amekana shitaka hilo  na akasaini  bondi ya dhamana ya Sh. milioni moja na wadhamini wawili wa Tanzania.  Kesi yake imeahirishwa hadi Septemba 27 mwaka huu.

Nipo Huru Nimetimiza Wajibu Wangu Sasa Mpira Upo Kwenu Kamati Kutenda Haki- Zitto Kabwe

0
0
Nipo Huru Nimetimiza Wajibu Wangu Sasa Mpira Upo Kwenu Kamati- Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwa sasa ametimiza wajibu wake kukutana na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kuweza kutoa sababu zake kwanini anaamini Bunge linatumiwa na serikali na kuwa ni bunge lisilo na meno.

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe .
Zitto Kabwe ambaye jana aliweza kukutana na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kufanya mahojiano nao amesema kuwa kwa upande wake yeye ametimiza wajibu wake hivyo sasa kazi imebaki kwenye Kamati husika kupima maelezo yake na kile anachotuhumiwa na kufanya maamuzi, lakini pia amesema anaamini Kamati hiyo itafanya maamuzi kwa haki na bila ya kuwa na woga wala hofu.

"Nipo huru baada ya masaa 24 tangu nikamatwe na polisi Uwanja wa Ndege Dar es Salaam na kuletwa Dodoma kwa gari. Nimekutana na Kamati ya Bunge ya Kinga na Haki na kuhojiwa. Nimetoa maelezo yangu yenye lengo la kulinda Uhuru wa maoni na kulinda hadhi ya Bunge kama mhimili wa dola dhidi ya kuingiliwa na Serikali. Nimetimiza wajibu wangu. Mpira sasa upo kwenye Kamati natumai wataamua kwa haki na bila woga na hofu" alisema Zitto Kabwe

Zitto Kabwe alikamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya Katibu wa Bunge Dr. Thomas D. Kashililah na kuweza kusafirishwa kutoka Dar es Salaam mbaka Dodoma chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwa lengo la kuhojiwa na kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kutokana na kauli zake alizowahi kutoa kupitia mitandao ya kijamii dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na Bunge.

Jeshi la Polisi Lawatia Mbaroni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu na Baba Yake Kwa Kukutwa na Bastora

0
0
Jeshi la Polisi Lawatia Mbaroni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu na Baba Yake Kwa Kukutwa na  Bastora
JESHI la Polisi Kanda Maalumya Dar es Salaam linamshikilia Robson Isack Maji (22) ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM na baba yake mzazi kwa kukamatwa na bastola aina ya Beretta na risasi sita.

Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa, Kamanda wa Polisi kandi hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa kijana huyo alikamatwa Septemba 20 majira ya saa 2:30 usiku  maeneo ya mwenge akiwa katika harakati za kutaka kuikodisha bastola hiyo.

“Siku ya tukio, askari walipata taarifa na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa Tabata Segerea. Alikamatwa akiwa na bastola aina ya Berretya yenye namba DAA316502 ikiwa na risasi sita ndani ya magazine.

“Mwanafunzi huyo alikuwa akitaka kukodisha silaha hiyo kwa majambazi kwa gharama ya Tsh. 400,000 lakini pia alikuwa tayari kuiuza kwa Tsh. Milioni 2,500,00.
“Kwa mahojiano ya awali na mtuhumiwa huyo ilibainika kuwa silaha hiyo aliiba kwa baba yake aitwaye Isack Maji ambaye naye siye mmiliki halali wa silaha hiyo. Kwa hiyo, baba na mtoto wote tunawashikilia ili watuambie waliitoa wapi silaha hiyo,” alisema Mambosasa.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images