Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104744 articles
Browse latest View live

Mbowe Amwaga Upupu Matibabu ya Tundu Lissu....Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Septemba 23

$
0
0
Mbowe Amwaga Upupu Matibabu ya Tundu Lissu....Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Septemba 23
Advertisement

Mbowe Aishangaa Serikali kwa Kutaka Kumtibu Tundu Lissu

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemshangaa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuwa Serikali iko tayari kumtibu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu popote duniani.

Mbowe ametoa mshangao huo leo Ijumaa alipokuwa akitoa taarifa kuhusu matibabu ya Lissu yanayoendelea jijini Nairobi.

Amesema wakati walipoamua kumpeleka Lissu jijini Nairobi, Waziri Ummy alikuwepo lakini walitaka Lissu apelekwe Muhimbili.

Mbowe amesema wanachama, watu mbalimbali wamechangia matibabu ya Lissu ikiwa ni hata wanachama wa vyama vingine walioguswa na tukio hilo.

“Sasa wiki mbili baadaye ndio anatoka Waziri wa Afya anasema Serikali iko tayari kumtibu popote duniani, eh kweli? Mama Ummy Mwalimu anasahau kauli yao wakinieleza mimi pale Dodoma, wamuogope Mungu, walikataa ‘categorically’  pengine walifikiri wao ni miujiza mheshimiwa Lissu kupona na sisi tulisema lazima tumpeleke Nairobi ndiyo mahali tunaona kweli kunawezekana kukaokoa yale maisha,”amesema Mbowe.

“Ilikuwa ni hatari na ni maamuzi yalikuwa magumu sana, watu ambao wana mamlaka, Waziri wa Afya yuko pale, Spika yuko pale nawaambia fanyeni maamuzi tumuokoe huyu mtu wanasema hatuwezi kumpeleka Nairobi, mimi nikasisitiza sisi tunampeleka Nairobi wakasema basi utalipa mwenyewe, nikasema sawa tutalipa wenyewe.”

Mbowe amesema hiyo ni hali halisi ambayo ameona awaambie Watanzania.

Mbowe Amshangaa Spika na Waziri Ummy Mwalimu Matibabu ya Tundu Lissu

$
0
0
Mbowe Amshangaa Spika na Waziri Ummy Mwalimu Matibabu ya Tundu Lissu
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemshangaa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuwa Serikali iko tayari kumtibu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu popote duniani.

Mbowe ametoa mshangao huo leo Ijumaa alipokuwa akitoa taarifa kuhusu matibabu ya Lissu yanayoendelea jijini Nairobi. Amesema wakati walipoamua kumpeleka Lissu jijini Nairobi, Waziri Ummy alikuwepo lakini walitaka Lissu apelekwe Muhimbili kwanza na baadaye kama angepata rufaa angepelekwa nchini India.

“Sasa wiki mbili baadaye ndio anatoka Waziri wa Afya anasema Serikali iko tayari kumtibu popote duniani, eh kweli? Mama Ummy Mwalimu anasahau kauli yao wakinieleza mimi pale Dodoma, wamuogope Mungu, walikataa ‘categorically’ pengine walifikiri wao ni miujiza mheshimiwa Lissu kupona na sisi tulisema lazima tumpeleke Nairobi ndiyo mahali tunaona kweli kunawezekana kukaokoa yale maisha,”amesema Mbowe.

“Ilikuwa ni hatari na ni maamuzi yalikuwa magumu sana, watu ambao wana mamlaka, Waziri wa Afya yuko pale, Spika yuko pale nawaambia fanyeni maamuzi tumuokoe huyu mtu wanasema hatuwezi kumpeleka Nairobi, mimi nikasisitiza sisi tunampeleka Nairobi wakasema basi utalipa mwenyewe, nikasema sawa tutalipa wenyewe.”

Pamoja na hayo Mh. Mbowe amesema kwamba Spika wa bunge kupitia wasaidizi wake alimtafuta siku chache zilizopita na kumtaarifu kwamba Serikali inaweza kusaidia matibabu ya Lissu lakini kwa masharti matatu, ikiwa ni wakubali apelekwe India, aandikie barua ya maombi na tatu apeleke taarifa yote kuhusu matibabu ya hospital ya mgonjwa na kwa upade wake alikataa.

Ameongeza "Jana Ummy anasema familia iandike maombi siyo chama maana mimi nilikataa. Wabunge kutibiwa na serikali ni stahiki. Wabunge wengi wametibiwa kwa nyakati tofauti  labda kama ingekuwa anaumwa mtoto wa Lissu na anatibiwa kwa kofia ya baba yake ndio baba yake angeomba. Lakini kuhusu mimi kuandika sitaweza kuandika labda Spika ajiandikie yeye, au familia ya Lissu iandike lakini mimi nimesema kama kiongozi wake wa chama sitaweza.

Hata hivyo Mbowe amesema hiyo ni hali halisi ambayo ameona awaambie Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwashukuru watu mbalimbali waliochangia  matibabu ya Lissu na kuwaomba kuendelea kuchangia matibabu ya Tundu Lissu.

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Serikalini na Makampuni Binafsi Leo

$
0
0

Bunge Lamemjibu Mbowe Kuhusu Milion 43 za Kumtibu Lissu

$
0
0
Bunge Imemjibu Mbowe Kuhusu Milion 43 za Kumtibu Lissu
OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeijibu kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye mapema leo akizungumza na wanahabari alisema Spika Job Ndugai amezuia Sh. Milioni 43 zilizochangwa na wabunge kusaidia matibabu na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayetibiwa Nairobi Kenya baada ya kupigwa risasi.

Ofisi hiyo imeeleza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa, michango ya wabunge kusaidia matibabu ya Tundu Lissu tayari zimeshatumwa Nairobi Hospital anakotibiwa mbunge huyo.
Taarifa ya ofisi ya Spika inasema kuwa fedha hizo zimetumwa siku ya tarehe 20 Septemba, 2017 kupitia benki ya Barclays Tawi la Huriringham akaunti namba 045 11553318.

Shetta Aonyesha Urijali Wake Apata Mtoto Mwingine

$
0
0
Shetta Aonyesha Urijali Wake Apata Mtoto Mwingine
Msanii wa muziki wa bongo fleva Nurdin Bilal maarufu kwa jina la Shetta, ameonyesha urijali wake kwa kubahatika kupata mtoto wa pili aliyezaliwa leo.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Shetta amepost picha akiwa amebeba kichanga huku akiandika maneno ya kumkaribisha mtoto huyo duniani.
"Karibu duniani mwanangu....!! Asante Mungu kwa huyu mwingine, sasa Kayla uache kuringa", ameandika Shetta.
Kufuatia kuzaliwa kwa mtoto huyo Shetta atakuwa na watoto wawili, ambapo wa kwanza anaitwa Kayla.


Kodi ya Nyumba Yamrudisha Mainda Nyumbani Kwao

$
0
0
Mange Kimambi Atajwa Mhamasishaji Bora wa Kuchangisha Fedha ya Matibabu ya Lissu
STAA wa Filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ juzikati alizua timbwili nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni jijini Dar alipotembelewa na waandishi wetu waliotaka kujua ukweli wa madai kwamba, eti kaamua kurudi kwao baada ya kukosa kodi ya kulipa huko alikokuwa akiishi.
Hatua hiyo ilikuja kufuatia ubuyu uliovujishwa na sosi wetu aliyedai kuwa, mwanadada huyo kwa sasa mambo yake siyo ‘mswano’ kama ilivyokuwa huko nyuma na ameamua kwenda kuanza moja nyumbani kwao.
MSIKIE SOSI
“Hivi mnajua kuwa Mainda karudisha mpira kwa kipa? (Kaenda kuanza moja kwao) Kama hamjui basi habari ndiyo hiyo, fuatilieni licha ya kwamba mwenyewe hataki watu wajue wala wamtembelee,” kilidai chanzo hicho.
RISASI LATINGA KWAO
Baada ya kuinasa habari hiyo, mapaparazi wetu juzi Jumanne walitinga nyumbani kwao ili kupata ukweli ambapo walimkuta Mainda na kuongea naye.
ALIAMSHA DUDE, MSIKIE…
“Mmekuja kufanya nini hapa nyumbani? Mbona mimi sihitaji waandishi hapa, mimi sio staa tafadhalini na wala sihitaji kuongea na waandishi, kwanza mmekuja bila taarifa,” alisema Mainda kwa sauti ya kufoka.
Alipobanwa sababu za kuwepo nyumbani kwao alisema yupo pale kwa ajili ya kumuuguza mama yake mdogo ambaye aliyejifungua kwa upasuaji.
AZUA TIMBWILI
Aliporushiwa madai kwamba yupo pale kwa sababu ya kukosa kodi huko alikokuwa akiishi, staa huyo alianza kuongea kwa jazba kabla ya kuliamsha timbwili akiwataka waandishi kuacha kufuatilia maisha yake.
“Jamani nilishawaeleza kuwa mimi sitaki, naomba muondoke haraka sana, mimi kuja kwetu kuna ajabu gani sasa? Kwani nakatazwa? Hata kama nimekosa kodi nyinyi linawahusu nini?
Niacheni jamani,” alisema Mainda ambaye alikuwa akiongea kwa sauti hadi kuwafanya watu wajazane eneo hilo. Kufuatilia hali hiyo, waandishi wetu waliamua kuwa wapole na kuondoka nyumbani kwa staa huyo ili kuepusha shari.
NENO LA MHARIRI
Gazeti hili linamuomba Mainda kuwa mpole huku akiweka akilini mwake kuwa kukosa leo siyo kukosa kesho na tunamuombea apate kile anachokihitaji. Endapo watu wanazusha yale yanayosemwa ni vyema akatoa ufafanuzi kama staa kuliko kuibua shari.

Diamond Ajipiga Moyo Konde na Kumtumia Zari Ujumbe Huu...Afunguka ni Kwanini Anampenda

$
0
0

Ujume Kutoka kwa Diamond kwenda kwa Zari Asubuhi ya Leo:

"Uzuri na Urembo pengine ningetembea nikakuta baadhi wanao pia... Lakini Akili, Hekma, pamoja na Roho yako ya kwenye Shida na Raha kwangu ndio kitu pekee kinachonifanya nikupende na kukuthamini zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda...... wanaposema kwenye kila Mafanikio ya Mwanaume kuna Mwanamke imara nyuma, hawamaanishi eti anaepika na kuosha vyombo sana ama kufua nguo kila siku... Hapana! ni mwanamke Mwenyekuwa bega kwa bega na Mpenzie kwenye Shida na Raha... Happy birthday General"

Mange Kimambi Atajwa Mhamasishaji Bora wa Kuchangisha Fedha ya Matibabu ya Lissu

$
0
0
Mange Kimambi Atajwa Mhamasishaji Bora wa Kuchangisha Fedha ya Matibabu ya Lissu
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewashukuru Watanzania wanaoendelea kumchangia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwataja wanaoongoza katika kuhamasisha uchangiaji mitandaoni akiwamo Mange Kimambi na Wema Sepetu.

Mbowe amesema mpaka leo Ijumaa jumla ya Sh204 milioni zimepatikana katika michango hiyo pamoja na msaada wa hali ambao wamekuwa wakipewa na Watanzania.

“Tunawashukuru wanaoendelea kuchangisha, tunamshukuru Mange Kimambi kwa kuwahamasisha diaspora kuchangia na katika mitandao akishirikiana na Wema Sepetu na wengine,” alisema Mbowe.

Mange alianzisha kampeni ya kumchangia Lissu katika mtandao wa Gofundme akilenga kupata dola za Marekani  50,000 na mpaka kufikia leo saa 10.41 katika mtandao huo kiasi cha dola za Marekani 23,380 ilikuwa imepatikana ambayo ni wastani wa Sh51.3 milioni.

Dada wa Diamond Esma Afunguka Kuhusu Zari 'Watu Hawajui Thamani yako Kwa Diamond'

$
0
0
Hawajui thamani yako kwa Naseeb walimtenda wengi mpk kufikia kudharauliwa majina kibao wakampa Mungu akakushusha, akakuvuta mbali ulipo ili umfute machozi ambayo siku zote alikuwa anatamani aje mtu amfute... ulimpa furaha na akili ya kuogopa nisitumie sana nikiweke akiba ili wanangu wawe ktk maisha mazuri na familia yangu... ulimpa nguvu ya kupambana usiku na mchana yote kwa ajili yenu... Mwanamke unayejua thamani ya Mwanaume uko mbali lakini pindi urudipo unahakikisha anakula nini anavaa nini na analala sehemu safi na salama tena kwa mikono yako huo ndo uanamke mwanamke... WE LOVE YOU MAMA TEE TUNAJUA THAMANI YAKO KWETU PLZ

Happy birthday to you love ❤
Najua wengi wanataka nafasi yako ila hawawezi kuipata Mama tee utaendelea kuw mama tee hakuna kama ww GENERAL

Waziri Ummy Aitetea Serikali Kuhusu Matibabu ya Lissu

$
0
0
Waziri Ummy Aitetea Serikali Matibabu ya Lissu
Waziri Ummy Mwalimu amejibu tuhumu zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya serikali baada ya kutaka kuombwa kugharamia matibabu ya Lissu, na kusema kwamba serikali imelazimika kufanya hivyo kwa sababu mgonjwa alijitoa kwenye utaratibu wa serikali.

Ummy Mwalimu ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ametoa maelezo hayo leo kwenye ukurasa wake wa twitter, na kusema kwamba serikali isingeweza kuingilia kati bila kuombwa na familia ya Tundu Lissu, kwani mgonjwa alishatolewa kwenye utaratibu wa serikali kwa kupelekwa Nairobi, na hiyo sio mara ya kwanza kwa serikali kufanya hivyo.

"Mgonjwa alitolewa kwenye utaratibu wa serikali alipopelekwa Nairobi, sasa gharama/tiba zaid yahitajika, serikali inaingiaje bila ridhaa ya familia? Na hii sio mara ya 1 kutokea. Mzee wetu S.Sitta (RIP), alikwenda matibabu London kwa utaratibu binafsi kisha alileta maombi serikali ishiriki", ameandika Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu ameendelea kwa kuandika akisema kwamba mgonjwa ni Mbunge anayehitaji matibabu zaidi, lakini kwa kuwa sasa hivi yupo nje ya utaratibu wa serikali, ili serikali iweze kushiriki ni lazima yawepo maombi ya kufanya hivyo.

hapo juzi serikali ilitoa tamko ikisema kwamba watakubali kusimamia matibabu ya Tundu Lissu popote duniani iwapo familia yake itaomba kufanya hivyo, na sio vinginevyo, kitendo ambacho kimeibua sintofahamu nyingi kwa baadhi ya wananchi wakiilaumu serikali kwa kutojali matatizo ya Tundu Lissu.




Yanga, Ndanda FC Kuonyeshana Ubabe Leo Uwanja wa Uhuru

$
0
0
Yanga, Ndanda FC Kuonyeshana Ubabe Leo Uwanja wa Uhuru
Timu ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inatarajiwa kushuka dimba la uhuru leo Jijini Dar es Salaam kuwavaa Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu mzunguko wa nne huku wakiendelea kumkosa mshambuliaji wake Amisi Tambwe.

Hayo yamewekwa wazi na Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa na kusema Tambwe ndiyo mchezaji pekee atakaendelea kuukosa mchezo huo wa leo.

"Kwa ujumla kikosi chetu kipo vizuri kabisa kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda FC", amesema Nsajigwa.

Amisi Tambwe amekuwa yupo nje (benchi) tokea ulipoanza msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na maumivu ya goti ambayo yalimuanza msimu uliopita.

Msemaji wa Serikali Ashangazwa na CHADEMA Kutaka Uchunguzi wa Kimataifa Amehoji 'Waje Wazungu? Wamekufa Watu Wangapi Kibiti Hatukuita Wazungu?'

$
0
0
Msemaji wa Serikali Ashangazwa na CHADEMA Kutaka Uchunguzi wa Kimataifa Amehoji 'Waje Wazungu?  Wamekufa Watu Wangapi Kibiti Hatukuita Wazungu?'
Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?

Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio.
Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu".

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na waru wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D' Dodoma alipokuwa akitokea bungeni mchana.






Je Wafahamu Kuwa Kupenda Ngono Kupita Kiasi ni Ugonjwa wa Akili (Sexual Disorder)?

$
0
0
Je Wafahamu Kuwa Kupenda Ngono Kupita Kiasi ni Ugonjwa wa Akili (Sexual Disorder)?
Wataalamu wa magonjwa ya mfumo wa uzazi wameeleza kuwa tabia ya kupenda ngono kupitia kiasi ni ugonjwa wa akili ujulikanao kwa jina la ‘mania’ (sexual disorder).

Akizungumza na Mwananchi, daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Colman Living amesema kufanya ngono mara kwa mara huimarisha ubongo lakini kupita kiasi husababisha madhara mbalimbali kwa mwili.

“Kiafya kuna madhara ikiwemo maambukizi ya magonjwa kama yapo sambamba na kukinai tendo, lakini hapohapo kuna mwingine anakuwa na  hulka ya kupenda tendo hilo kwa sababu ni mgonjwa tunaita ‘sexual disorder’ au kitaalamu unaitwa ‘mania’ huu ni ugonjwa wa akili kwamba yeye anakuwa hatosheki hivyo anafanya mara kwa mara na wakati mwingine na watu tofauti,” alisema Dk Colman.

Akielezea madhara kwa wanawake, Dk Colman alisema kwa anayependa tendo hilo licha ya kuchanika sehemu za siri, inategemea anafanya na watu wangapi, kama ni tofauti anaweza kupata magonjwa mbalimbali.

Alisema kufanya tendo la ngono sana humfanya mwanamke kuwa katika hatari kubwa ya kupata mimba zisizotarajiwa ambazo wakati mwingine zinaweza kuambatana na kifafa cha mimba, kuathirika kiuchumi sababu mama atakuwa na watoto wengi ambao hawezi kuwapa mahitaji ya muhimu ikiwemo elimu, chakula na matibabu.

“Kwa wanawake saratani za njia ya uke huwaathiri zaidi hasa ile ya shingo ya kizazi ambayo kwa ujumla wake karibu asilimia 90 ya aina hizi za saratani husababishwa na virusi vya HPV ambavyo huambukizwa au kuenezwa kwa njia ya ngono kama ambavyo anapata maradhi mengine kama Hepatitis B, HIV na mengine yasababishwayo na ngono zembe,” alisema Dk Colman.

Hata hivyo alifafanua kuwa ngono kupita kiasi husababisha maambukizi mengi katika njia mbalimbali za mwili zilizowazi kama mdomoni, kwenye uke na sehemu ya haja kubwa.

Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa Manundu Dispensary iliyopo Korogwe, Dk Ally Nzige amesema ikiwa mwanaume atafanya ngono mara kwa mara inamweka katika nafasi kubwa ya kuepukana na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza, lakini asipitilize kiwango na kubadilisha wapenzi.

Alisema kwa kawaida mtu anatakiwa kufanya tendo la ngono angalau mara tatu kwa wiki ni kiwango kizuri kwa afya.

“Umri sahihi kwa mwanaume kuanza kuwa tayari kwa tendo ni miaka 18 mpaka 35, hapa tunategemea kwamba awe ameshafanikiwa hata kupata watoto vinginevyo na hapo huyo atakuwa na matatizo ikiwa hatataka kujihusisha na tendo hilo hasa baada ya miaka 22,” amesema.

Dk Nzige amesema mwanaume anapokwenda zaidi ni kitu ambacho hakina shida ila inategemea na huyo patna amekubali au anamkomoa.

“Lakini hii inamtaka mtu mwenye afya iliyokuwa nzuri, pamoja na hayo inasaidia mtu kutulia kwa wale ambao wapo kwenye ndoa pia hawa wanachelewa kupata matatizo mengi, lakini watu ambao hawajaoa wala kuolewa wanapata magonjwa mbalimbali ya msongo wa mawazo, lakini ni suala la msingi kuwa na utulivu katika ndoa kwani kama huna ratiba nzuri ya maisha vitu vingine vitakushinda,” amesema Dk Nzige.

Hata hivyo amesema hakuna madhara kwa mwanaume kufanya tendo la ndoa kupita kiasi, lakini iwapo atafanya na watu tofauti anaweza kupata maradhi mbalimbali yanayoambukizwa kwa njia ya ngono.

CHADEMA Wafunguka Sababu ya Kutofungua Kesi ya Shambulio la Lissu

$
0
0
CHADEMA Wafunguka Sababu ya Kutofungua Kesi ya Shambulio la Lissu
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe amefunguka na kujibu hoja za kwa nini mpaka sasa CHADEMA hawajafungua kesi kutokana na shambulio Tundu Lissu ni kutokana na kuwa kipaumbele chao cha kwanza ni kuokoa maisha ya Lissu.

Hayo Mh. Mbowe ameyasema wakati akizungumza jana na wanahabari ambapo amesema kuwa baada ya tukio la Lissu kutokea akili na mawazo ya Chadema yalikuwa kwenye kuokoa maisha ya Lissu na wanasubiri mambo yakiwa sawa wataangalia kufanya lolote linalowezekana kwan wakati huo.

"Kwa nini Chadema hatujafungua kesi? Kesi unafungua kwa nani? Anayechunguza ni nani? Chadema tumeshafungua kesi nyingi ya akiwepo Ben Saanane msaidizi wangu aliye[potea kusikojulikana, Kesi ya nyani unapeleka kwa Tumbili. Priority yetu sisi ni kumuokoa Lissu na siyo Kesi. Kupigania maisha yake ndicho kitu tuliona kinachofaa kufanywa na ndicho tunachofanya mpaka sasa", amesema.

"Ninaamini tu mambo yakikaa sawa vichwa vyote hivi vya Chadema vitajua kama tunaweza kufungua kesi au kitu gani kingine ambacho kinafaa kufanywa endapo tu afya ya Mh. Lissu ikishaimarika" ameongeza

Akizungumzia kwanini mpaka leo dereva wa Lissu hajarudi nchini ili kwenda kuripoti polisi kama jinsi jeshi la polisi lilivyoagiza, Mbowe amesema kwamba kijana huyo atarudishwa nchini pindi tuu wataalamu wa afya wanaomhudumia wakitoa ripoti afya yake kama iko salama na wao hawapo kwa ajili ya kumficha.

"Wiki iliopita nilisema dereva wa Mh. Lissu yupo Nairiobi kwa ajili ya matibabu ya kisaikolojia. Hatukuona kama ni busara kumtelekeza wakati alikuwepo kwenye matatizo na boss wake. Madaktari wakituthibitishia kuwa yuko timamu atarudi nchini kwani hatuko kwa ajili ya kumficha mtu. Yule kijana ni kama mtoto wa Lissu, dereva na mlinzi wake, wana miaka mingi pamoja tangu Lissu anagombea ubunge kwa mara ya kwanza" amesisitiza.
Ameongeza pia dereva atakuja kuzungumza nini kilitokea na yeye alijiokoaje naamini aliyekuwa anashambulia alikuwa hajalenga kumuacha hai mtu hata mmoja hivyo mimi siyo msemaji sana wa dereva wake Lissu lakini akipona ataelezea mwenyewe kila kitu.



Ua la Idriss Lamtokea Puani Wema Afunguka Lilivyosababisha Ugomvi kwa Mpenzi Wake

$
0
0
Ua la Idriss Lamtokea Puani Wema Afunguka Lilivyosababisha Ugomvi kwa Mpenzi Wake
STAA wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa Ua alilodaiwa kumpelekea Idris ambalo si lake limemsababishia kugombana na mpenzi wake kitendo kilichomkera sana kwani hajawahi kufanya hivyo na kwa sababu hiyo alikesha akilia.

Wema, alisema kuwa pamoja ya kuwa alimuomba msamaha Idriss kwa kutokwenda kwenye shughuli yake ya uzinduzi wa viatu lakini hakuwahi kumpelekea ua kama walivyomsingizia na ni maneno yaliyomkera kwani yamemsababishia kugombana na mpenzi wake ambaye alihisi ni ukweli na sakata hilo lilimliza sana.

“Jamani niliumia sana kuona vile kitu ambacho sijafanya mimi kabisa na sijaelewa kwa nini walinifanyia hivyo, nilikuwa kwenye wakati mgumu sana na mpenzi wangu ambaye nilikuwa naye maana hakuweza kunielewa kabisa.

“Vitu vingine vinauma jamani nilijisikia vibaya sana ilibidi nijifungie na kulia kwa uchungu mno kwa sababu nilijua wazi mtu wangu asingependa hata kidogo na hata jamii yangu maana ningeonekana ni mtu nisiyekuwa na msimamo hata kidogo” alisema Wema.

Waziri Mwakyembe Afunguka Sababu ya Kutowasuluhisha Diamond na Ali Kiba

$
0
0
Waziri Mwakyembe Afunguka Sababu ya Kutowasuluhisha Diamond na Ali Kiba
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema mvutano wa Diamond na Alikiba hauna haja ya kuhusuluhisha ikiwa ni wa kiuweledi na kitaaluma.

Dkt. Mwakyembe amesema haamini kama tatizo ni kubwa kiivyo bali ni kitu chenye afya tu kwa sababu kinaleta ushindani mzuri ambao unapeleka muziki katika ngazi nyingine.

“Kama kuna ushindani kati ya Alikiba na Diamond ambao ni kiuweledi, kitaaluma basi mimi nafikirii tungeuendeleza zaidi, hamna sababu ya kuwasuluhisha, waendelee kushindani vizuri tupate miziki mizito,” Dkt. Mwakyembe ameiambia Times Fm.

“Kwa hiyo mimi naomba Watanzania wachukulie mvutano huo ni mzuri katika tasnia, mradi mimi sijasikia watu wameshikiana mapanga,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwakyembe ameendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwaita pamoja Diamond na Alikiba ili kufanya ngoma pamoja kama alivyowahi kuhaidi hapo awali.

“Ukifika muda nitawaita wote watanisikiliza tu watatunga wimbo mmoja wa kukata na shoka pengine bara nzima la Afrika litatikisika, ni vijana wenye vipaji lazima tuendelee kuwatia moyo,” amesema.


Rais Magufuli Amewatunuku Kamisheni ya Luteni Maafisa 422 wa JWTZ

$
0
0
Rais Magufuli Amewatunuku Kamisheni ya Luteni Maafisa 422 wa JWTZ
Rais John Magufuli leo Jumamosi amewatunukia kamisheni ya luteni usu kwa maofisa 422 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania(JWTZ), katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kabla ya kutunuku kamisheni hizo Rais Magufuli alikagua gwaride la heshima lililondaliwa na maofisa hao.

Katika hafla hiyo Rais Magufuli alikabidhi zawadi kwa maofisa waliofanya vizuri wakati wa mafunzo hayo wakiongozwa na Hamis Mwanitega aliyetajwa kufanya vizuri zaidi kuliko wote.

Maofisa wengine waliopata zawadi ni Haji Kimaro aliyefanya vizuri darasani, John Mkua aliongoza kwenye mafunzo kwa vitendo huku Donatia Kimario akiibuka kidedea miongoni mwa wanawake walioshiriki kwenye mafunzo hayo.

Upande wa kikosi cha ubaharia Ally Kitawala aliibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi kwenye kikosi hicho.

Katika kundi la marubani wa ndege vita waliofanya vizuri ni Hamza Msuya na Albert Fanuel.

Kuchepuka si Diamond kwa Zari Pekee Hii hapa List ya Watu Maarufu Waliowahi Kuchepuka

$
0
0
Unakumbuka mkasa wa Bill Clinton na Monica Lewinsky au François Hollande na Julie Gayet.

Kati ya skendo kubwa za usaliti zilizowahi kuwakumba viongozi miaka ya hivi karibuni ni Bill Clinton akiwa rais wa Marekani na François Hollande akiwa Rais wa Ufaransa. Yalizungumzwa yakaisha lakini yanabaki kwenye historia.

Mwanzo wa wiki hii mitandao ya kijamii Tanzania ilipamba moto. Wapenzi wa burudani walioko huko walikuwa wakizungumza mada moja tu …Mtoto wa Hamisa Mobeto na Diamond Platnumz. Hili lilikuwa ikiwa ni baada ya takriban wiki tatu za kuwapo kwa tetesi kwamba, ujauzito alikuwa nao mrembo huyo ni wa Diamond.

Awali, Diamond alikataa katakata tuhuma hizo kiasi kwamba hata aliandika mstari kwenye remix ya wimbo wa Fresh wa Fid Q akithibitisha kwamba kinachozungumzwa na baadhi ya watu ni kusingiziwa tu licha ya kuwepo shahidi mbalimbali za kimazingira zilizokuwa zikimbana ikiwemo mama mzazi wa Diamond kwenda hospitali alipojifungulia Mobeto.

Lakini baada ya mtoto kuzaliwa na kupewa jina la baba mzazi wa Diamond, picha zinazomwonesha Mobeto na Diamond wakiwa kwenye malavidavi zikaanza kusambazwa— huku ikidaiwa kuwa zilisambazwa makusudi kumkomesha kwa kuwa alimkataa mtoto.

Lakini baada ya mambo kuwa magumu Diamond aliamua kwenda kwenye kituo cha redio na kukiri kwamba ni kweli anafahamu kuwa yeye ndiye mtoto wa Mobeto.

Sasa suala hapa halikuwa tu kuhusu Diamond kumkataa mtoto, bali pia kukiri kwa Diamond kuhusu mtoto wa Mobeto ni sawa kabisa na kukiri kwamba alimsaliti mpenzi wake aliyezaa naye watoto wawili na kumvisha pete ya uchumba Zari —jambo ambalo matokeo yake yanasubiriwa kwa hamu hadi hivi sasa.

Hata hivyo, si Diamond pekee aliyewahi kukumbwa na maswahibu haya — wapo mastaa wengine nje ya Tanzania, waliowahi kuchepuka, siri ikavuja, wakakiri kwa namna moja ama nyingine.

Arnold Schwarzenegger

Mwaka 1991, mwigizaji na Gavana Mstaafu wa Jimbo la California, Marekani, Arnold Schwarzenegger pamoja na aliyekuwa mke wake kwa kipindi hicho, Maria Shriver walimwajiri Mildred Baena kama msaidizi wa nyumbani.

Hata hivyo, kumbe nyuma ya mgongo wa mke wake, Schwarzenegger alikuwa akitoka kimapenzi na Baena ambaye naye pia alikuwa ni mke wa mtu kwa kipindi hicho na uhusiano huu wa siri, ulifika mbali zaidi ambapo Baena alibeba ujauzito ambao ilithibitika kuwa ni baada ya miezi tisa, mtoto alipozaliwa, ilithibitika kuwa ni wa damu ya Schwarzenegger.

Kwa sababu hiyo, Baena aliachana na mume wake ambaye alikuwa akidhani kuwa yeye ndiye muhusika wa mimba aliyoibeba mkewe, wakati Arnold naye alikubali kwamba yeye ndiye baba wa mtoto aliyezaliwa na Baena na akapewa jina la Joseph.

Mwaka 2011 baada ya Arnold kumaliza muda wake wa ugavana, alikaririwa na vyombo vya habari akieleza kwamba alimuweka wazi mke wake kuhusu mtoto aliyezaa na Baena, hiyo ikiwa ni miaka zaidi ya miaka, na pia iliripotiwa kwamba kwa kipindi chote hicho Arnold alikuwa akimuhudumia mtoto wake kwa siri jambo ambalo linadaiwa kuwa lilisababisha mke wake kuomba talaka na wakatengana mwaka huo.

Tiger woods

Anatajwa kama ni miongoni mwa wacheza gofu waliopata mafanikio makubwa kimichezo na kiuchumi pia.

Mwaka 2010 Woods alitalakiana na mke wake Elin Nordegren ambaye alizaa naye watoto wawili huku sababu ya kuachana kwao ikithibika waziwazi kwamba ni mchezo mchafu wa kuchepuka alioufanya Woods.

Kilichotokea ni kwamba, mwaka 2009 Elin aligundua kuwa Woods anachepuka na mwanamke aitwaye Rachel Uchitel na kwa mujibu wa simulizi za Elin mwenyewe, anasema arobain za mwizi zilitimia usiku ambao Woods alikuwa nyumbani amelala.

Elin akachukua simu ya mume na kuanza kupekua ambapo alikuta meseji ya mume wake kwenda kwa Rachel ikisema: “Wewe ni mtu wa pekee niliyewahi kumpenda.”

“Nimekumiss.” Elin akatuma meseji nyingine ya namna hiyo akijifanya ni Woods ambapo baada ya muda, Rachel alijibu kwa kuuliza lini wataonana tena.

Tangu hapo hakukuwa na msalie mtume, Elin akamuamsha mume na nyumba ikawaka moto.

Hata hivyo, mwaka 2010, Tigerwoods alikiri kosa mbele ya vyombo vya habari na ndani ya mwaka huo huo walitalakina na Elin.

Kevin Hart

Kevin Hart ni muigizaji wa Marekani ambaye naye ni mmoja wa mastaa waliojaribu kuchepuka lakini kwa bahati mbaya wakanasa na siri zikavuja.

Kwa sasa Kevin ni mume na baba wa watoto wawili wawili aliozaa na mke wake Eniko Parrish ambaye pia ni mjamzito.

Wiki iliyopita, mitandaoni ilisambaa video inayomuonyesha Kevin Hart akiwa mtupu chumbani na mwanamke ambaye si mke wake. Kwa lugha nyepesi, alikuwa akichepuka.

Hata hivyo Hart alijaribu kupinga kile kilichosambaa lakini kwa muda mfupi sana alishindwa kuendelea kusimamia uongo wake na aliamua kukiri na hata kuomba radhi kwa mke wake, watoto, mashabiki na watu wake wa karibu kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Brad Pitt

Brad Pitt ni muigizaji wa Marekani ambaye aliwahi kuwa mume wa Angelina Jolie. Lakini kabla ya kuwa na Angelina, Brad Pitt alikuwa ni mume wa muigizaji Jennifer Anniston ambaye walitalakiana mwaka 2005 baada ya Brad kutokuwa muaminifu kati ndoa yake. Brad Pitt alikuwa akichepuka na Angelina na kunogewa mpaka alipofumwa.

Brad alichepuka na Angelina Jolie, ambaye walikutana wakati wanatengeza filamu ya Mr and Mrs Smith ambayo waliigiza kama mume na mke.

Hata hivyo, licha ya kwamba mchepuko wa Brad Pitty ulifanikiwa kuwa mke, kwa sasa hawapo pamoja tena kutokana na kutengana mwishoni mwa mwaka 2016.

David Beckham

Mume wa mke mmoja na baba watoto wanne. Ni mwanasoka mstaafu aliyetamba mwanzoni mwa miaka ya 1990 hadi 2000 alipokuwa akiitumikia timu ya Manchester united.

Kuchepuka si Diamond kwa Zari Pekee Hii hapa List ya Watu Maarufu Waliowahi Kuchepuka
Mwaka 2003 alisajiliwa na timu ya Real Madrid ya Hispania na alipoanza kazi huko alikutana na mrembo Rebecca Roos ambaye baadae akawa mfanyakazi wake akimtumikia kama msaidizi binafsi.

Baadaye iligundulika kuwa Beckham na Rebeca sio tu walikuwa ni mtu na bosi wake, bali pia walikuwa wanatoka kimapenzi. Baada ya Rebeca kuacha kazi kwa Bechkam mwaka 2004, alifichua siri hiyo katika gazeti la News to The Word… hata hivyo, Beckahm hakuibuka kupinga juu suala hilo wala kukiri jambo ambalo linawafanya watu waunganishe nukta na kupata jibu. Beckham alikuwa na nafasi ya kutumia mahakama ili labda kulipwa fidia ya kuchafuliwa na gazeti lililochapisha habari hiyo.

Kristen Stewart

Supastaa wa filamu za Twilight, Kristen Stewart alikumbwa na skendo ya usaliti baada ya kufumwa na mwongozaji wake wa filamu za Hunts Man, Rupert Sanders.

Kristen aliyekuwa katika uhusiano na mwigizaji mwenzake, Robert Pattinson alijikuta katikati ya dunia ya usaliti baada ya paparazzi kupiga picha akijicinjari ndani ya gari na mwongozaji huyo.

Ni moja kati ya skendo za kukumbukwa kwani Kristern na Pattinson walikuwa wakitajwa kama ‘Power Couple’ wa Hollywood wakilinganishaw na Angelina Jolie na Brad Pitt kwa wakati huo.

Kris Jenner

Mama wa familia ya kina Kardashian, Kris Jenner amewahi kukiri kuchepuka wakati akiwa ameolewa na Robert Kardashian kwamba alifanya mchezo huo akiwa na mwongozaji wa filamu aliyocheza. Jenner alisema: “Ukiwa mdogo unafanya mambo mengi ya kukufadhaisha, ninachojutia ni kuwa nilimsaliti mume wangu.”

Chris Rock

Mchekeshaji maarufu duniani Chris Rock aliachana na mkewe baada ya kukiri kuchepuka na mwanamke mwingine. Ndoa yake na

Megalyn Echikunwoke ilivunjika na sasa ameanzisha uhusino mwingine akijiapiza kuwa mwaminifu

Bill Nass Afunguka Mapenzi Yake Kwa Nandy Asema Anavigezo Vyote Vya Kuwa Mke Wake

$
0
0
Bill Nass Afunguka Mapenzi Yake Kwa Nandy Asema Anavigezo Vyote Vya Kuwa Mke Wake
MSANII wa Hip Hop nchini Bill Nass anayetamba na wimbo wake mpya wa Sina Jambo amefunguka juu ya upendo wake kwa msanii mwenziye ambaye anafahamika kwa jina la Nandy,  akisema ana vigezo vyote vya kuitwa mke wake.

Bill Nass amesema kwa sasa hana mpango wa kuoa, pia amefunguka na kusema kuwa hata muda ukifika bado atakuwa na vigezo vyake anavyovizingatia.

Msanii mwenziye ambaye anafahamika kwa jina la Nandy.
”Sijakaa nikafikiria suala la kuoa kwa sababu mimi nina vigezo vyangu ambavyo nataka, najua namtaka mwanamke wa aina gani. Kwanza suala la kuoa kwangu limenipitia mbali sana, sifikirii kuoa kwa sasa.”
Alipoulizwa kuhusu mtu ambaye anaona anelekea kidogo kuwa mke wake,  alimtaja Nandy.

“Kiukweli kabisa katika hili suala la kumtaja ni zito lakini ni hivi, Nandy nimemuona ana asilimia sitini za kuolewa na mimi, kwa sababu ana vigezo vyote ambavyo navitaka,” alisema Bill Nass.
Tetesi zinazoendelea ni kwamba Bill Nass na Nandy wapo kwenye mahusiano lakini hawataki watu wayafahamu mahusiano yao.
Viewing all 104744 articles
Browse latest View live




Latest Images