Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Serikali Yapewa Saa 72 Kuwashtaki Maafisa wa Tume ya Uchaguzi Wa IEBC Kenya

$
0
0
Serikali Yapewa Saa 72 Kuwashtaki Maafisa wa Tume ya Uchaguzi Wa IEBC Kenya
Upinzani nchini Kenya Nasa umempatia mkurugenzi wa mashtaka nchini humo Keriako Tobiko saa 72 kuwafungulia mashtaka maafisa wa IEBC wanaotuhumiwa kuharibu uchaguzi wa Agosti 8.
Wakati huohuo upinzani huo umeapa kuwafungulia mashtaka ya kibinafsi maafisa hao wa IEBC.
Nasa imesema kuwa mahakama ya juu siku ya Jumatano haikuwaondolea lawama maafisa wa IEBC na kwamba ni sharti washtakiwe kwa kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo.

''Kufuatia uamuzi uliotolewa na mahakama ya juu, afisi yako imesema kwamba inaangazia uamuzi huo kwa kina na kufanya uamuzi wa iwapo itawafungulia mashtaka ya uhalifu maafisa wa IEBC au la.Uelewa wetu ni kwamba makamishna na wafanyikazi wakuu wa IEBC walitekeleza uhalifu'', alisema Mbunge Mathare MP Anthony Olouch.

Aliongezea: Kutokana na uchaguzi wa marudio uliotangzwa kufanyika tarehe 26, kctoba 2017, maafisa waliorodheshwa hapa chini hawataruhusiwa kusalia afisini ili kuendeleza uhalifu waliotekeleza.

Na hadi pale uchunguzi kuhusu uhalifu uliotekelezwa na maafisa hao utakapofanywa na mashtaka kufunguliwa dhidi yao baada ya saa 72, sisi tutawashtaki kulingana na kifungu cha 28 ya mshataka ya umma.

Maafisa wa IEBC ambao Nasa inataka wafunguliwe mashtaka ni pamoja na afisa mtendaji Ezra Chiloba, mwenyekiti Wafula Chebukati, Betty Nyabuto, Immaculate Kassait, James Muhati, Praxedes Tororey ambaye amejiuzulu, Moses Kipkogei, Abdi Guliye, Molu Boya na Marjan Marjan.


Diamond Aamua Kumfuata Mama Watoto Wake 'Zari' Afrika Kusini

$
0
0
Diamond Aamua Kumfuata  Mama Watoto Wake 'Zari' Afrika Kusini
Ikiwa zimepita siku nne tangu mwanamuziki Diamond Platnumz akiri kumsaliti mpenzi wake Zari, hatimaye ametua nyumbani kwa mwanamke huyo nchini Afrika Kusini.

 Leo saa 5.40 asubuhi mwanamuziki huyo aliposti video katika mtandao inayomuonyesha akicheza na mtoto wake wa kwanza, Latifah huku kwa mbali ikisikika sauti ya Zari.

Dada wa mwanamuziki huyo, Esmah Khan aliposti video hiyo katika mtandao wa Instagram: “Tuko na Tiffah na mamy tunaita raha ya mtoto apewe mapenzi kwa baba na mama jamani.”

Leo ilikuwa siku muhimu kwa Zari kwani anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Rais John Magufuli Atangaza Ajira 3000 za JWTZ

$
0
0
Rais John Magufuli Atangaza Ajira 3000 za JWTZ
Rais John Magufuli ametangaza kutoa nafasi 3,000 kwa vijana waliopitia mafunzo ya ukakamavu kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Akizungumza baada ya kuwatunuku nishani ya Luteni Usu maofisa 422 wa jeshi, Magufuli amesema lengo la kutoa nafasi hizo ni kuhakikisha jeshi linakuwa na askari wa kutosha.

“Jeshi haliwezi kuwa na maofisa tu, tutaongeza na askari wa kawaida, wengi watakaopata nafasi hizi nataka wawe wamepitia JKT, tunataka tujenge jeshi la kisasa.”

Rais Magufuli amewataka Watanzania kutoa ushirikiano kwa jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili viendelee kufanya kazi yao kwa ufanisi, amani na utulivu viendelee kutawala nchini.

Dogo Janja Aliamsha Dude Asema ' Young Dee Mteja Hawezi Kufanana na Sikubali Kufananishwa na Mtumia Ngada'

$
0
0
Dogo Janja Aliamsha Dude Asema ' Young Dee Mteja Hawezi Kufanana na Sikubali Kufananishwa na Mtumia Ngada'
Baada ya Rappa Young Dee kuomba asifananishwe na wasanii kama Dogo Janja kutoka Arusha na Young Killer wa Mwanza, Dogo Janja amesema hawezi kumjibu msanii huyo kwani hajui kama atakuwa anamjibu mtu mwenye akili timamu au tayari amekula unga.

Dogo Janja amesema kuwa Young Dee kuomba asifananishwe na msanii kama yeye ni sawa kwani hata yeye hataweza kukubali kufananishwa au kukaa na m tu anatumia dawa za kulevya kitu kinachomfanya we anazungumza vitu vya ajabu

"Young Dee ni Mteja, na hawezi kufanana na mimi. Mtu mwenye akili timamu hawezi kutukana kwenye media matusi makubwa kama alivyofanya Young Dee. Akiacha Unga ndo ninaweza kuzungumza kitu kuhusu yeye, kwa sasa hivi nikimzungumzia siwezi jua kama ntakua nabishana nayeye au mteja. Mtu mwenye akili timamu unamsamehe tu maana inawezekana kashavuta mambo yake na yupo kwenye dunia yake nyingine" Dogo Janja.

Dogo janja ameongeza, kuwa hakatai kufananishwa na mtu lakini inatakiwa aangaliwe ni mtu aina gani ambaye anafananishwa naye kwani si kila mtu ni sahihi kufananishwa nae.

"Mimi pia sipendi kufananishwa japo sijakataa kufananishwa, Young Killer mimi nilishawahi kuwa role model wake  kwa hiyo kufananishwa naye si kitu kibaya lakini kunifananisha na mla unga ni kukosea....... Young Dee akiacha kula unga tutakaa mezani kuzungumza lakini kufananishwa naye sasa hivi sitaki kwani ni mtu ambaye ukumuacha gheto unawaza kama utaikuta TV " amesisitiza.

Hivi karibuni Young Dee alifunguka na kutoa onyo kwa watu na watangazaji kuwa wasimfananishe na Ma Rapaa kama Dogo Janja na Young Killer kwani yeye anafanya mziki mkubwa huku akitoa maneno makali kuwalenga.
Tazama video hapa Chini



Jenerali Mabeyo Awatahadhalisha Wanajeshi Matumizi ya Mitandao ya Kijamii

$
0
0
Jenerali Mabeyo Awatahadhalisha Wanajeshi Matumizi ya Mitandao ya Kijamii
Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ameagiza wanajeshi kuacha kujihusisha na matumizi mabaya mitandao ya kijamii kwani kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za jeshi.

Jenerali Mabeyo amesema hayo leo Jumamosi katika hafla ya kutunuku nishani  ya  Luteni Usu kwa maofisa 422 wa jeshi iliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Amesema jukumu la wanajeshi ni ulinzi wa Taifa hivyo kujiingiza katika mambo yasiyofaa ni ukiukwaji wa taratibu za jeshi hilo.

Mabeyo amewataka wanajeshi kuepuka kuliingiza jeshi kwenye siasa na badala yake wanatakiwa kuwa na uzalendo kwa Taifa lao.

“Niwasihi msimame kwenye kiapo mlichoapa leo. Wapo baadhi ya askari husahau kwa haraka na kukiuka kiapo, msifike huko. Matamshi uliyoyatoa leo yanaelekeza wajibu wako, utii, kuilinda katiba, kumtii Rais na kumtumikia.”

Hudda Ampa Makavu Diamond Sakata la Kuzaa Nje ya Ndoa

$
0
0
Hudda Ampa Makavu Diamond Sakata la Kuzaa Nje ya Ndoa
Diamond Platnumz ni kama centre ya ubuyu Bongo. Mrembo wa Kenya Huddah Monroe ameonekana kuwa upande wa adui yake Zari The Bosslady katika sakata zito la Diamod kuzaa na Hamisa Mobetto.

Baada ya bosi huyo wa WCB kuonekana kuishinda kwa asilimia kubwa vita ya usaliti kwa kuzaa nje, kupitia mtandao wa Snapchat, Huddah ameamua kumshushia maneno mazito msanii huyo. Haya ndio maneno aliyoandika Huddah kwenye mtandao huo.









Wama Atoa Neno Sakata la Kushambuliwa Tundu Lissu Asema Lissu Atarudi na Nguvu Mpya

$
0
0
Wama Atoa No Sakata la Kushambuliwa Tundu Lissu Asema Lissu Atarudi na Nguvu Mpya
Baada ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kupigwa risasi Septemba 7 mwaka huu eneo la ‘area D’ Dodoma na watu wasiojulikana, Malikia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu amesema anakumbuka harakati za mbunge huyo.

Wema kupitia mtandano wake Instagram ameeleza kuwa Watanzania wote wanaimani kubwa kwamba atarudi na nguvu mpya zaidi ya aliyokuwa nayo.

We still Cant wait for You to get up on your feet… Our Hero… Our True Leader… And By his Grace You will Be Up once Again… We sure do miss you… Tunakumiss sana… Tunamiss Harakati zako, na hata pale ulipokuwa unaonewa na tukisononeka pamoja na wewe… Basi watanzania wote tuna imani kubwa kwamba u will come back Powerful than you have ever been because What doesn’t kill u, Only makes you Stronger… You are in our Prayers… We love you… May God Keep His Close watch upon You… Amen…!!🙏🏼🙏🏼🙏🏼

Lissu alipelekwa Nairobi katika hospitali ya Aghakhan ambapo hadi sasa anapopatiwa matibabu.


Polisi Lawashikilia Watu Wawili kwa Kukutwa na Dawa za Kulevya

$
0
0
Polisi Lawashikilia Watu Wawili kwa Kukutwa na Dawa za Kulevya
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu wawili kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 44  walizokuwa wakisafirisha kutoka Sirali kwenda mwanza kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Watu hao wawili waliofahamika kwa majina ya James lawrence (51), mkazi wa Tarime – Mara, amekamatwa akiwa na mirungi kiasi cha kilo 35, aliyokuwa akisafirisha toka Sirali kwenda Mwanza kwenye bus lenye namba T.498 DAK, aina ya Youtong, na Magabe Mirumbe (45), mkazi wa Tarime –Mara, amekutwa na mirungi kiasi cha kilo 09, aliyokuwa akisafirisha kutoka Sirali kwenda Mwanza kwenye bus lenye namba T. 201 DAN aina ya Youtong, jana Septemba 22 majira ya saa mbili usiku.

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mwanza inasema kuwa askari walikuwa kwenye kizuizi tajwa hapo juu wakisimamisha na kupekua magari yote yaliyokuwa yakipita kwenye barabara ya mwanza kwenda musoma, ili kuweza kubaini madereva na abiria wanaosafirisha madawa ya kulevya. aidha wakati wakiendelea kusimamisha na kupekua magari hayo waliweza kukamata magari tajwa hapo juu yakiwa na abiria hao waliokuwa wakisafirisha mirungi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi Ahme Msangi amethibitisha kutkamatawa kwa watu hao na kusema kwamba anatoa wito kwa wakazi wote wa jiji na mkoa wa Mwanza na wamaeneo ya mikoa ya jirani kuacha kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwani ni kosa la jinai, bali wananchi wafanye kazi halali ya kujipatia kipato na wala sio vinginevyo.
Aidha pia anatoa raia kwa madereva na wamiliki wa mabasi kuacha kusafirisha madawa ya kulevya kwani kosa kisheria.


Simba Kujiweka Shinyanga kwa Maandalizi ya Mechi yao Dhidi ya Stand United

$
0
0
Simba Kujiweka Shinyanga kwa Maandalizi ya Mechi yao Dhidi ya Stand United
Klabu ya Simba leo inatarajiwa kutua mkoani Shinyanga kwaajili ya maandalizi ya mchezo wake wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Stand United wiki ijayo.

Simba imeanza safari mapema leo kutokea Mwanza ambako ilicheza mchezo wake wa raundi ya nne dhidi ya Mbao FC ambao ulimalizika kwa sare ya 2-2.
Kwa upande mwingine msemaji wa Simba Haji Manara amethibitisha kuwa winga wa timu hiyo Shiza Kichuya anaendelea vizuri na atapumzika kwa simu 2 kuanzia leo kisha atakuwa fiti kwaajili ya mchezo dhidi ya Stand United.
Kichuya aliumia kipindi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC ikiwa ni baada tu ya kufunga bao lake la kwanza msimu huu.

Esha Kufanya Sherehe Kubwa ya Kumtoa MwanaeMwanae

$
0
0
Esha Kufanya Sherehe Kubwa ya  Kumtoa MwanaeMwanae
MSANII wa filamu za Kibongo, Esha Buheti leo anatarajia kumwanika mwanaye kwa ndugu na marafiki ambapo atamfanyia sherehe ya nguvu.

Esha ameamua kufanya sherehe hiyo pamoja na kumshukuru Mungu kwa kumjalia kujifungua salama na kumlinda mwanaye huyo ambapo itafanyika nyumbani kwake Kijitonyama, Dar na itahudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wasanii wenzake.

“Jumamosi (leo) ninatarajia kumtoa mwanangu rasmi hivyo sherehe itafanyika hapa nyumbani kwangu, unajua nafanya hivi kwa ajili ya kumshukuru Mungu na kufurahia zawadi hii aliyotupatia katika familia yetu na siyo kwa ajili ya kujionesha,” alisema Esha.

Iran Yafanyia Majaribio yA Kombora Lake

$
0
0
Iran Yafanyia Majaribio  yA Kombora Lake
Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.
Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa.
Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000.
Marekani yaiwekea Iran vikwazo
Ahmadinejad azuiwa kuwania urais Iran
Marekani yasikitishwa raia wake kuhukumiwa Iran
Iran yaitahadharisha Marekani kuhusu vikwazo
Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo.
Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo.
Jaribio hilo lilifanywa siku chache baada ya Rais Trump wa Marekani kushambulia Iran katika hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ametetea hatua ya taifa lake kuimarisha zana zake kwa lengo la kujitetea.

Mchungaji Afungwa Miaka 30 Jela kwa Kubaka Muumini Wake

$
0
0
Mchungaji Afungwa Miaka 30 Jela kwa Kubaka Muumini Wake
MCHUNGAJI wa kanisa la kilokole la Victoria lililopo Sokoni One jijini Arusha, Chrisantus Mboya (35), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka muumini wake wa chini ya miaka 16.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Arusha, Nestori Ballo, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Juni 3, mwaka huu na mahakama imeridhika na mashahidi sita waliotoa ushahidi.

Hakimu Ballo alisema katika hukumu yake kuwa, muathirika (jina tunalihifadhi), aliieleza mahakama jinsi alivyobakwa na mchungaji huyo nyumbani kwake na mahakama kujiridhisha mchungaji huyo kutenda kosa hilo.

Alisema daktari wa hospitali ya Mkoa ya Mount Meru ambaye alikuwa shahidi wa nne katika kesi hiyo, aliieleza mahakama kuwa muathirika hakukutwa na majeruhi sehemu ya siri, lakini aliingiliwa bila ya ridhaa yake.

Hakimu Ballo alisema, shahidi wa pili ambaye ni dada wa muathirika, alidai mahakamani hapo kuwa mchungaji aliwaambia kuwa muathirika alikuwa na pepo hivyo alipaswa kuombewa na maombi hayo yanapaswa kuwa maalumu nyakati za usiku kwa ajili ya afya yake.

Alisema shahidi huyo alikubaliana na ushauri wa mchungaji na muathirika aliambiwa na kupelekwa mapema kanisani kwa ajili ya maombi hayo, lakini hilo halikufanyika na badala yake alimpeleka nyumbani kwake na kumvutia chumbani na kuanza kumbaka.

Baada ya mahakama kumtia hatiani mchungaji Mboya, Hakimu Ballo alimpa nafasi Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Rose Sulle, kutoa maoni yake ambaye alitaka adhabu kali itolewe kwa mchungaji huyo ili iwe fundisho kwa wengine wenye kukiuka maadili ya kiimani.

Sulle alisema jamii ina imani na wachungaji kuwa ni watu wenye maadili.

Alisema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa wachungaji wengine wanaotumia mwanya kwa waumini kuwa na
matatizo ya kiafya kufanya vitendo viovu vya kubaka.

Aidha, mchungaji huyo alipopewa nafasi ya kujitetea, aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana familia.
Hata hivyo, utetezi huo haukumsaidia na kupewa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela.

Aidha, aliambiwa kama hajaridhika na hukumu hiyo anaweza kukata rufaa mahakama kuu kupinga
hukumu hiyo.

Hospitali Aliyolazwa Lissu Yapokea Fedha Kutoka Tanzania Bila Kupewa Maelezo

$
0
0
Hospitali Aliyolazwa Lissu Yapokea Fedha Kutoka Tanzania Bila Kupewa Maelezo
Ofisa Kitengo cha Habari na Itikadi wa Chadema, Hemed Ali amesema Hospitali na Nairobi nchini Kenya imethibitisha kupokea fedha kutoka Tanzania lakini zikiwa hazina maelezo.

Jana ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kuelezea mchakato wa utumaji wa fedha hizo kiasi cha Sh 43 milioni ikisema kuwa zilitumwa tangu Agosti 20. Ofisi hiyo ilikuwa ikifafanua taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyewaambia waandishi wa habari kuwa alikuwa hajapa mchango huo wa wabunge.

Ali aliyepo Nairobi amesema amethibitishiwa na Hospitali ya Nairobi kupokea fedha hizo kutoka Tanzania ingawa kulikuwa hakuna maelezo zaidi.

“Wamenieleza kuna fedha zimeingizwa kutoka Tanzania ila hazina maelezo ndiyo wanafuatilia benki,” amesema ofisa huyo.

Nimeona Shida ya Ikulu ni Mateso Kuwa Rais- Magufuli

$
0
0
Nimeona Shida ya Ikulu ni Mateso Kuwa Rais- Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt John Pombe Magufuli amesema ameona shida ya Ikulu na kwamba ni mateso kuwa Rais wa chi na yeye amekiri kuwa  ameshuhudia mateso hayo japo aliomba nafasi hiyo ya uongozi  kwa kujaribu.

Akiwa mkoani Arusha baada ya akiwatunukia Kamisheni Maafisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Rais magufuli amesema kwamba aliomba nafasi hiyo kuongoza kwa kujaribu  lakini mwishowe akasukumiziwa na sasa anaona mateso yake hivyo hana budi kutatua shida za watanzania.

"Naifahamu hii kazi nayoifanya ni ngumu, ni msalaba inahitaji kumtanguliza Mungu kweli kweli . Kwa sababu ni kujitoa sadaka lakini nimekubali kuwa sadaka kwa ajili ya watanzaniakwa ajili ya kuwanyoosha mafisadi waliozoea kuwaibia watanzania" amesema

"Ninaamini inawezekana hapatatokea mwingine ambaye atajitoa hivi. Najua siku moja mtakumbuka  Hamju mateso ninayoyapata. Ni shida kuwa Rais.  ndi maana Baba wa Taifa aliwahi kyusema pale Ikulu ni mateso. Mimi nimeyaona mateso niliomba kwa kujaribu wakanisukumizia huko. Magufuli

Amesema kwa kuwa watanzania wamempa nadfasi ya kuongoza basi atawatumikia kwa uaminifu kwani hakutoa Rushwa      wala kuchangiwa hela na mafisadi kuingia ikulu ndiyo maana haogopi kutumbua na kuwahakikishia wananchi kwamba atazidi kutumbua kweli kweli
Pamoja na hayo amewatakaa wananchi waachane na mambo ya vyama kwani hayana faida kama watakuwa na njaa  


Young Dee: Nitamshikisha Adabu Dogo Janja Bila Mimi Yeye Asingekuwepo Nnina Mchango Kwenye Muziki Wake

$
0
0
 Young Dee:Nitamshikisha Adabu  Dogo Janja Bila Mimi Yeye Asingekuwepo Nnina Mchango Kwenye Muziki Wake
Msanii Young Dee amesema kitendo cha msanii mwenzake Dogo Janja kumtolea maneno machafu na kumtuhumu kuendelea kutumia madawa ya kulevya, ni kumvunjia heshima kwani yeye ana mchango mkubwa kwenye maisha yake, na pia inaonyesha hana akili.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Young Dee amesema kama asingekuwepo yeye hata Dogo Janja asingekuwepo, na inadhihirisha ni jinsi gani bado hajakua kiakili.
"Yeye kama anaongea kuhusu suala la madawa inabidi awe na ushahidi, kwa sababu mimi nimeongea niko na ushahidi kwamba kimuziki asingekuwepo Young Dee wala wao wasingekuwepo, mimi nina mchango kwenye muziki wao, aliposikia mimi naongea vile ilibidi ajiulize kwa nini nimekasirika, sasa kuanza kurusha maneno inaonyesha ni upumbavu na hana akili, inaonyesha ni jinsi gani bado mtoto", amesema Young Dee.
Pamoja na hayo Young Dee ameendelea kwa kusema kwamba ikibidi atamshikisha adabu msanii huyo, kwani sio mara ya kwanza amekuwa akimuimba na kumrushia maneno yenye chokochoko.
"Unajua unakuwa mstaarabu sana lakini kuna muda unashindwa, mimi sijawahi kumuimba mtu, lakini hawa machalii wamekuwa wakiniimba kila siku sasa inabidi ifike mwisho", amesema Young Dee.
Hivi kaibuni kumeibuka mgogoro mkubwa kati ya wasanii watatu akiwemo Young Killer, baada ya Young Dee kutaka kutofananishwa nao, na Dogo Janja kujibu kwamba Young dee anatumia madawa ya kulevya hivyo ni mtu ambaye hatakiwi kutiliwa maanani.




Polisi: Serikali Inaheshimu Misingi ya Utawala Bora Tatizo Watu Hawataki Kufuata Sheria

$
0
0
Polisi: Serikali Inaheshimu Misingi ya Utawala Bora Tatizo Watu Hawataki Kufuata Sheria
Kamishna wa Polisi Jamii, Musa Ali Musa amesema Serikali inaheshimu misingi ya utawala bora lakini tatizo lililopo ni kwamba watu hawataki kufuata sheria.

Akizungumza leo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani duniani ambayo Kitaifa imefanyika Wilayani Temeke na kushirikisha asasi mbalimbali, mashirika ya kimataifa pamoja na Jeshi la Polisi viongozi wa dini.

Kamishna huyo amesema amani iliyopo hapa nchini haitakiwi kuchezewa na kwamba Jeshi hilo halitavumilia vitendo vya uvunjaji wa Sheria utokanao na itikadi za kisiasa, dini au makabila.

Amesema, nchi yoyote yenye amani, watu wake wanafuata misingi ya Sheria na taratibu za nchi hivyo ili kudumisha amani ni lazima kila mwananchi akubali kuheshimu sheria.

"Tanzania ni nchi inayoheshimu haki na misingi ya utawala bora lakini Kuna fikra imejengeka kuwa kuwa huru ni kufanya jambo lolote bila kufuata taratibu za nchi, "amesema

"Jeshi la Polisi litafanya lolote liwezekanalo ili amani iliyopo idumishwe."

Pia, ameonya juu ya usambazaji wa taarifa za kichochezi kupitia mitandao ya kijamii hasa vijana na kuwataka kujishughulisha na shughuli za maendeleo.

Ametolea mfano, Mlipuko wa mabomu ya  Mbagala ya mwaka 2014 na kusema kuwa licha ya kuwa ilikuwa bahati mbaya jamii ijifunze kuheshimu amani ili hali kama hiyo isije kujitokeza.

Mratibu wa Mtandao wa kutetea haki za watoto, GNRC, Yusuph  Masanja amesema ni muhimu kwa jamii kuheshimu haki za watoto ili kuwa na kizazi bora siku zijazo.

China Yaiwekea Kikwazo Korea Kaskazini

$
0
0
China Yaiwekea Kikwazo Korea Kaskazini
Uchina imeimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ambapo imetangaza usitishaji wa ununuzi wa nguo kutoka Korea kaskazini mbali na uuzaji wa mafuta kwa taifa hilo kuanzia leo na baada ya muda fulani.
Hatua hiyo inaambatana na maagizo ya vikwazo yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku 11 zilizopita.
Wachanganuzi wanasema kuwa vikwazo hivyo vitaathiri sana raia wa Korea Kaskazini iwapo vitatekelezwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo ambao hauna doria ya kutosha.
Utengenezaji wa nguo ni huduma muhimu ya pili inayoletea Korea Kaskazini fedha za kigeni na sehemu nne kwa tano ya nguo hizo hupelekwa Uchina.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 100,000 wanafanya kazi katika sekta hiyo nchini Korea Kaskazini.

Haya Hapa Mjina ya Wachezaji Watakaounda Kikosi Kipya cha Taifa Stars

$
0
0
Haya Hapa Mjina ya Wachezaji Watakaounda Kikosi Kipya cha Taifa Stars
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza majina ya kikosi cha wachezaji watakaounda kikosi hicho kipya.
Kwa asilimia kubwa hakuna mabadiliko isipokuwa kipa Peter Manyika wa Singida United ameitwa kikosini hapo kuchukua nafasi ya Said Mohamed Nduda wa Simba ambaye kwa sasa ni majeruhi.
Manyika ni kipa wa zamani wa Simba ambaye aliondoka kikosini hapo baada ya kukosa nafasi na kudaiwa kuwa kiwango chake kilishuka.

Timu hiyo imeitwa kujiandaa na mechi ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya Fifa ambapo watacheza dhidi ya Malawi mnamo Oktoba 11, mwaka huu. Kikosi kamili kilichoitwa na kocha huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar ni hiki hapa:
Makipa
Aishi Manula
Peter Manyika
Ramadhani Kabwili
Mabeki
Bonifas Maganga
Abdi Banda
Gadiel Michael
Salim Mbonde
Erasto Nyoni
Adeyuni Salehe Arned
Viungo
Himid Mao
Hamis Abdallah
Mazamiru Yassin
Raphael Daud
Simon Msuva
Shiza Kichuya
Ibrahim Ajibu
Morel Ergenes
Abdul Hilal Hasan
Washambuliaji
Mbwana Samatta
Mbaraka Yusuph

Mbowe Atoa Sababu Kwa Nini Hawajafungua Kesi Yoyote Dhidi ya Shambulio la Tundu Lissu

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe amefunguka na kujibu hoja za kwa nini mpaka sasa CHADEMA hawajafungua kesi kutokana na shambulio Tundu Lissu  ambapo amesema ni kutokana na kuwa kipaumbele chao cha kwanza ni kuokoa maisha ya Lissu.

Mh. Mbowe ameyasema hayo wakati akizungumza jana na wanahabari ambapo amesema kuwa baada ya tukio la Lissu kutokea akili na mawazo ya Chadema yalikuwa kwenye kuokoa maisha ya Lissu na wanasubiri mambo yakiwa sawa wataangalia kufanya lolote linalowezekana kwan wakati huo.

"Kwa nini Chadema hatujafungua kesi? Kesi unafungua kwa nani? Anayechunguza ni nani? Chadema tumeshafungua kesi nyingi ya akiwepo Ben Saanane msaidizi wangu aliye[potea kusikojulikana, Kesi ya nyani unapeleka kwa Tumbili. Priority yetu sisi ni kumuokoa Lissu na siyo Kesi. Kupigania maisha yake ndicho kitu tuliona kinachofaa kufanywa na ndicho tunachofanya mpaka sasa", amesema.

"Ninaamini tu mambo yakikaa sawa vichwa vyote hivi vya Chadema vitajua kama tunaweza kufungua kesi au kitu gani kingine ambacho kinafaa kufanywa endapo tu afya ya Mh. Lissu ikishaimarika" ameongeza

Akizungumzia kwanini mpaka leo dereva wa Lissu hajarudi nchini ili kwenda kuripoti polisi kama jinsi jeshi la polisi lilivyoagiza, Mbowe amesema kwamba kijana huyo atarudishwa nchini pindi tuu wataalamu wa afya wanaomhudumia wakitoa ripoti afya yake kama iko salama na wao hawapo kwa ajili ya kumficha.

"Wiki iliopita nilisema dereva wa Mh. Lissu yupo Nairiobi kwa ajili ya matibabu ya kisaikolojia. Hatukuona kama ni busara kumtelekeza wakati alikuwepo kwenye matatizo na boss wake. Madaktari wakituthibitishia kuwa yuko timamu atarudi nchini kwani hatuko kwa ajili ya kumficha mtu. Yule kijana ni kama mtoto wa Lissu, dereva na mlinzi wake, wana miaka mingi pamoja tangu Lissu anagombea ubunge kwa mara ya kwanza" amesisitiza.

Ameongeza pia dereva atakuja kuzungumza nini kilitokea na yeye alijiokoaje naamini aliyekuwa anashambulia alikuwa hajalenga kumuacha hai mtu hata mmoja hivyo mimi siyo msemaji sana wa dereva wake Lissu lakini akipona ataelezea mwenyewe kila kitu.

Watu Hawakomi...Wawili Wakamatwa Wakisafirisha Dawa za Kulevya

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu wawili kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 44  walizokuwa wakisafirisha kutoka Sirali kwenda mwanza kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Watu hao wawili waliofahamika kwa majina ya James lawrence (51), mkazi wa Tarime – Mara, amekamatwa akiwa na mirungi kiasi cha kilo 35, aliyokuwa akisafirisha toka Sirali kwenda Mwanza kwenye bus lenye namba T.498 DAK, aina ya Youtong, na Magabe Mirumbe (45), mkazi wa Tarime –Mara, amekutwa na mirungi kiasi cha kilo 09, aliyokuwa akisafirisha kutoka Sirali kwenda Mwanza kwenye bus lenye namba T. 201 DAN aina ya Youtong, jana Septemba 22 majira ya saa mbili usiku.

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mwanza inasema kuwa askari walikuwa kwenye kizuizi tajwa hapo juu wakisimamisha na kupekua magari yote yaliyokuwa yakipita kwenye barabara ya mwanza kwenda musoma, ili kuweza kubaini madereva na abiria wanaosafirisha madawa ya kulevya. aidha wakati wakiendelea kusimamisha na kupekua magari hayo waliweza kukamata magari tajwa hapo juu yakiwa na abiria hao waliokuwa wakisafirisha mirungi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutkamatawa kwa watu hao na kusema kwamba anatoa wito kwa wakazi wote wa jiji na mkoa wa Mwanza na wamaeneo ya mikoa ya jirani kuacha kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwani ni kosa la jinai, bali wananchi wafanye kazi halali ya kujipatia kipato na wala sio vinginevyo.
Aidha pia anatoa raia kwa madereva na wamiliki wa mabasi kuacha kusafirisha madawa ya kulevya kwani kosa kisheria.
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images