Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Inasikitisha Mtoto Mchanga wa Siku moja Aokwotwa Katika Shimo la Choo

0
0
Inasikitisha Mtoto Mchanga wa Siku moja Aokwotwa Katika Shimo la Choo
Mtoto mchanga wa kike anayekadiliwa kuwa na umri wa siku moja ameokotwa kwenye shimo la choo kinachotumika katika mtaa wa Lumala Kata ya Kawekamo Wilayani Ilemela mkoani Mwanza akiwa hai baada ya kutupwa na mzazi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema baada ya muda mchache kupita toka kichanga hicho kutupwa kwenye shimo hilo la choo,  polisi walipata taarifa na kwenda kusaidia kumtoa mtoto huyo ambaye sasa amepelekwa hospitali ya Sekou Toure kwa matibabu zaidi.
"Inadaiwa kuwa baada ya muda mchache kupita toka mtoto alipotupwa, palikuwa na mtu aliyekwenda kujisaidia chooni ndipo akiwa chooni alisikia sauti ya mtoto mchanga akilia toka ndani ya shimo la choo. Inasemekana kuwa baada ya mtu huyo kusikia sauti hiyo ya mtoto akilia, alikwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa serikali za mtaa ambapo uongozi wa mtaa ulifika mahali hapo kisha ulitoa taarifa kituo cha polisi" alisema Msangi
Aidha Msangi aliendelea kuelezea
"Askari baada ya kupokea taarifa hiyo walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kushirikiana na wananchi waliokuwepo eneo hilo na kufanikiwa kutoa kichanga hicho cha mtoto toka ndani ya shimo la choo kikiwa hai. mtoto amepelewa hospitali ya mkoa ya sekou toure kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri. Polisi wapo katika upelelezi na msako katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza, ili kuweza kubaini mzazi/wazazi wa mtoto huyo ambao wamefanya ukatili huo dhidi ya mtoto, ili baadae waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao na iwe fundisho kwa wengine" alisema Msangi
Kamanda Msangi ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kutenda ukatili dhidi ya watoto ikiwepo vitendo vya kutupa watoto kwani ni kosa la jinai na endapo mtu atabainika kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.


Watu Hawa Wanapambana na Hali Zao, Waliniuliza Bomberdia Ndo Nini?- Nape

0
0
Watu Hawa Wanapambana na Hali  Zao, Waliniuliza Bomberdia Ndo Nini?- Nape
Mbunge wa Mtama(CCM), Nape Nnauye ameeleza kuwa wananchi wamemuuliza Bomberdier ndiyo nini.

Katika ukurasa wake wa Twitter ambao unaonyesha Nape akiwa katika picha na wananchi wa kijijini ameandika hivi “Watu hawa wanapambana na hali zao! Waliniuliza bomberdia ndio nini? Na sie wa vijijini tutafaidikaje au ni kwenu mjini tu!??


Waziri Mwakyembe Akanusha Kufungia Mashindano ya Miss Tanzania

0
0
Waziri Mwakyembe Akanusha Kufungia Mashindano ya Miss Tanzania
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametolea ufafanuzi kauli yake na kusema kuwa hajasitisha mashindano ya Miss Tanzania na tuzo za muziki nchini bali ametoa angalizo kwa waandaaji wa mashindano hayo kuwa na uhakika wa kuyaendesha.

Dk Mwakyembe amesema hayo leo Jumatatu kwenye ziara yake mjini Mtwara baada ya taarifa kuenea kuwa amefuta shindano hilo.

Mwakyembe yuko mkoani Mtwara katika ziara ya kuzungumza na watendaji walio chini ya wizara yake na kuzungukia viwanja vya michezo.

Amesema mashindano na tuzo hapa nchini huanzishwa bila kuwa na andiko la uendelezaji, hivyo ametoa agizo kwa Baraza la Sanaa (Basata) kwamba mtu yeyote akija na shindano au wazo la tuzo watamruhusu pale tu atakapotoa msingi wa mwendelezo na siyo kwa kuwa amepata mfadhili wa muda.

“Hata mashindano ya ulimbwende tumeshachoka watoto wa kike wanahangaika, watajipodoa  lakini zawadi zikitangazwa unaambiwa mshindi wa kwanza gari namba mbili pikipiki ila sijawahi kuona hata mmoja ambaye amewahi kuzipata au ikatokea utoaji wa zawadi usio na kelele,” amesema.

Dk Mwakyembe amesema amekuwa akifuatwa na warembo kadhaa ofisini kwake wakilalamikia kutopewa zawadi zao mara baada ya mashindano ya Miss Tanzania, amesema alikaa na Basata miezi miwili iliyopita na kuwapa maagizo,  “Kuanzia sasa chombo chochote au kampuni inayoendesha mashindano ya ulimbwende ambayo iliwahi kuahidi vijana wetu wa Kitanzania zawadi na haijatoa tusigombane, watoe zawadi zote wawatafute warembo wawape.”

Mad Ice ampa makavu Harmorapa

0
0
Msanii Mad Ice ambaye kwa muda mrefu alikuwa kimya kwenye game ya bongo fleva, ameibuka na issue ya kumpondea Harmorapa, akisema msanii huyo hafai kuwa msanii.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mad Ice amesema kwa upande wake anamuona Harmorapa kama msanii wa vichekesho, hivyo mtu akisema anafanya muziki anamuona ana matatizo ya akili.

"Nimesikia hilo jina Harmorapa nikasikitika sana, kwa sababu kuna vitu tunaharibu sanaa yetu wenyewe, kuna wasanii wanahitaji kupewa fursa,  mimi nimemuona kama mchekeshaji, ukiniambia ni comedian nitaheshimu lakini unaponiambia unamlinganisha na mimi nitakuona una kitu kinakusumbua kichwani”.

Kauli hiyo ya Mad Ice sio mara ya kwanza kusikika kwani hata producer mkongwe bongo Master Jay, aliwahi kuzungumza kuwa Harmorapa hastahili kuitwa msanii wa muziki kwani hajakidhi sifa, isipokuwa ni sawa na mchekeshaji.

Kwa Staili Hii Mnayotumia Wanawake wa Mjini Single Mother Wataongezeka Maradufu

0
0
Inasikitisha kwa kweli!

Sijui Mungu aliwapa ubongo wa aina gani hawa wanawake

Muda kama miezi mitatu imepita nilikutana na binti mmoja ivi hapa mtaani, tukafanikiwa kuyaanza maisha ya mapenzi huku tukifurahia maisha hasa chachu ya penzi letu ikiwa ni kugegedana!

Ajabu huyu mwanamke nimekaa naye miezi mitatu yote hii wala hata hanishirikishi mipango yake, mafikirio yake kwangu kumbe ilikuwa ni kumuoa kabisa, lakini hii haikua shida

Shida imekuja baada ya yeye kujitegeshea mimba tena kimya kimya na hadi sasa inaumri wa mwezi ndio ananipa taarifa!

Enyi wanawake nipende kuwambieni tu kwamba, mimba sio kigezo cha kuolewa!
Mimba huhusisha mipango ya mume na mke, lini wazae na maisha ya mtoto yatakuaje

Sasa nyie mnakurupuka tu eti unatega mimba ahahahahah

Kwa mtindo huu single maza mtakuwa wengi sana huku mtaani na mtaishia kutulaani tu na laana wala hazitatufikia kwa namna hii, tutawatelekeza sana

Kwanini Mtoto wa Kiume ni Rahisi Kusahau Nyumbani Kuliko wa Kike?

0
0
Habari wapendwa, poleni na majukumu.

Naomba kuuliza ni kwanini baadhi ya watoto wa kiume wakishaondoka nyumbani kwa kuwa na familia yake au kuishi peke yake, huwa inakuwa vigumu kukumbuka nyumbani ukilinganisha na watoto wengi wa kike ambao mara nyingi hukumbuka nyumbani?

Toa Maoni yako

Video ya Fiesta Mwanza Yamtia Jirani Yangu Matatani..Anaswa Akija

0
0
Wakuu, leo kwa jirani yangu pamechimbika mke wake kaliamsha dude.

Wakuu mda so mrefu nimeingia kwangu nikitokea kuijenga Tanzania ya viwanda, ila baada ya kufika ndani nasikia kwa jirani yangu makonde mazito yanatembea huku matusi na kelele zikisindikiza mpambano huo wa aina yake ulionivutia niufatilie.

Baada ya kuona ugomvi huo kati ya jirani yangu na mkewe hauishi, nikaamua kuenda kusikiliza kipi kimewasibu ila kabla sijafika nikasikia mke anatukana huku anasema wewe uliaga umeenda lindo kumbe umeenda Fiesta maneno hayo yakanipa hamasa ya kufuatilia kulikoni, kufika pale nikagonga mlango kwa nguvu jamaa kafungua nikauliza vipi mbona mnauana jamaa akijiandaa kujibu mkewe akatoka ndani na kuanza kumshtakia mme wake kwangu.

"Shem rafiki yako aliondoka Jumamosi jioni akaniambia anaenda guard (lindo) alafu akarudi jpili asubuhi basi siku imepita sasa leo nikaamua niingie you tube ili kuona Fiesta mwanza ilikuwaje make sikuenda kwasababu sikuwa na kampani mke, mume wangu aliaga ameenda lindo, ila cha ajabu nikiwa naendelea kuangalia nkamuona mume wangu akiwa anashangilia huku kalibambia limalaya limoja lina mikalio kama Sarah Bahtman nimejisikia kuishiwa nguvu make mi aliniaga anaenda kazini kumbe anaenda fiesta Kirumba"

 Nb: Wakuu mkienda kwenye starehe ambazo unajua kuna mtu hutaki ajue uwepo wako pale epuka kuonekana kwenye mipicha na mavideo yanayochukuliwa na watu maana unaweza umbuliwa one day.

JF

Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE.

ZUNGU: ‘Hakuna Sheria itayotungwa na Bunge itakayozuia Mimba Mashuleni

0
0
Mwenyekiti wa bunge na mbunge wa Ilala, Mussa Zungu leo September 25 2017 amealikwa kwenye mahafali ya 15 ya kidato cha nne katika shule mfano ya sekondari ya wasichana ya Barbro Johansson na moja ya ishu aliyoizungumzia ni hii ya mimba mashuleni.

Akizungumza wakati wa hotuba yake……
’Hakuna sheria yoyote itakayotungwa na bunge itakayozuia mimba mashuleni, mimba shuleni zitazuiwa na wanafunzi pamoja na wazazi na jamii kwa ujumla, mtoto akiwa mhuni na mzazi wake naye mhuni’

Jaji Mkuu wa Tanzania Ampongeza Jaji Mkuu wa Kenya Kwa Ujasiri wake wa Kulinda Uhuru wa Mahakama

0
0
Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga ametua nchini katika mkutano wa majaji na mahakimu akionekana kivutio kwa wengine.

Jaji huyo ni mmoja wa majaji wakuu 13 kutoka nchi mbalimbali duniani wanaohudhuria mkutano majaji na mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku tatu..

Maraga amegeuka kivutio baada ya kushangiliwa na majaji waliohudhuria mkutano huo wakati alipotambulishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Profesa Juma amempongeza Maraga kwa kuwakilisha mfano bora wa kulinda uhuru wa Mahakama kwa nchi nyingine duniani.

Kiongozi huyo ameonekana akiwa ameambatana na walinzi wanne ambao wanamfuata popote anapotembea nje ya mkutano huo.

Hata hivyo, Maraga amekataa kuzungumza na vyombo vya habari kwa madai amekuja kuhudhuria mkutano huo na siyo kwa jambo jingine lolote.

Mkutano huo umefunguliwa leo Jumatatu na Makamu wa Rais, Samia Suluhu ukiwa na kauli mbiu "Kujenga Mahakama Shirikishi, Thabiti na Inayowajibika."

Jaji Maraga kwa siku za hivi karibuni amekuwa maarufu baada ya kutoa uamuzi wa kufuta Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliokuwa umempa ushindi Rais Uhuru Kenyatta.

Waziri wa Afya Aipiga Marufuku Muhimbili kutoa rufaa za nje hata kwa Rais Maguful

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa agizo kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhakikisha haitoi rufaa ya matibabu nje ya nchi ikiwa wana uwezo wa kutibu maradhi husika hapa nchini.

Ummy amesisitiza wataalamu kutowaogopa wanasiasa ikiwa wana uwezo wa kumtibu mgonjwa hapa nchini haina ulazima wa kumwandikia rufaa nje ya nchi hata akiwa ni Rais John Magufuli.

Ametoa agizo hilo leo Jumatatu wakati akipokea msaada wa vifaa vipya kwa ajili ya vyumba viwili vya upasuaji vya watoto wadogo na wodi ya watoto ya upasuaji vyenye thamani ya Dola za Marekani 675,000 sawa na Sh1.5 bilioni,  kutoka kwa wataalamu na wahisani kutoka nchini Uingereza kupitia taasisi ya Archie Wood Foundation.

"Rais aliponiteua aliniagiza kwamba lazima niachane na rufaa za nje, hatuwezi kuachana nazo ikiwa magonjwa yanayoweza kutibiwa ndani yatatibiwa nje," amesema Ummy.

Amesema Watanzania wana imani na  Muhimbili  na hivi sasa wengi wanatoka hospitali za kulipia na kufuata matibabu ila changamoto iliyopo ni majengo lakini wapo mbioni kujenga jengo la ghorofa kwa ajili ya wagonjwa wa kulipia.

"Msitoe rufaa ya mgonjwa kama hamjajiridhisha kwamba mnaweza kumtibu hapa hata kama awe Rais, waziri au nani msitoe rufaa kwani maana yake mtakuwa mmeshindwa ni lazima ninyi mseme kwamba hamuwezi na sisi tutashughulikia," amesema.

Amewatahadharisha wataalamu hao na wanasiasa kwamba lazima wahakikishe kweli hawawezi kutibu na kwamba wizara ipo tayari na itawaunga mkono.

Ndugai: Tundu Lissu ana Bima ya Bunge, Hapaswi Kutibiwa kwa Michango

0
0
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hayawezi kufanyika kwa kuchangishana michango kwa kuwa ana bima yake na haki zake ndani ya Bunge.

Spika Ndugai amebainisha hayo leo asubuhi wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kutoka East Africa Radio baada ya kuulizwa swali kwamba kuna utaratibu gani endapo mbunge akiumia ama akiumwa akiwa kazini.

"Utaratibu ni kwamba wabunge wote wana bima pamoja na mimi mwenyewe, Mawaziri wote wana bima ndani ya bunge kwa sababu ni wabunge kwanza kabla ya kuwa Mawaziri. Kwa hiyo bima zao ndiyo zinazowahudumia na tunahudumiwa kupitia hospitali zote za serikali, tunalazwa kama watanzania wengine wowote wale. Ikitokea yanahitajika matibabu ya nje ya nchi, yatatoka mapendekezo katika hospitali ya Muhimbili kwamba matibabu ya huyo mtu  yanapaswa yakafanyikie nje ya nchi kutokana na upungufu wa jambo fulani hapa nchini", amesema Spika Ndugai.

Pamoja na hayo, Spika Ndugai aliendelea kwa kusema "Tukirudi kwa Mhe. Lissu ni kwamba tulikuwa wote hapa Dodoma, baada ya kuombwa na familia pamoja na Mhe. Mbowe kwamba ni vyema apelekwe kutibiwa katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya tulikubaliana kwa pamoja kuwa ni vizuri aende huko. Lakini alienda huko kama vile ni hospitali binafsi ambayo ipo nje kidogo ya mkondo wetu wa kawaida. Kwa hiyo bado bima yake ipo hapa bungeni na utaratibu wa kumtibu upo".

Aidha, Spika Ndugai amesema bunge kwa ujumla haliwezi kumtupa Mhe. Lissu hata kidogo kuhusiana na masuala ya matibabu yake.

"Sisi kama bunge hatujamtupa mwenzetu na bahati nzuri serikali imetoa tamko lake kuwa halijamtupa, ni suala la kuwekana sawa tu badala ya matamko kwenye vyombo vya habari, magazeti ambayo yamekuwa yakipotosha tu na kuleta malumbano ambayo hayana sababu. Kwa hiyo wito wangu kwa wahusika wote ikiwa ni pamoja na familia ya Lissu, CHADEMA, uongozi wa bunge na serikali endapo tukikaa pamoja hakuna ambacho kitashindwa kuzungumzika, hatuwezi kumtibu mwenzetu kwa michango ya kuchangishana wakati ana bima yake na haki zake", amesisitiza Spika Ndugai.

Deni Linalotokana na Gharama za Matibabu Nje ya Nchi Lafikia Bilioni 35

0
0
Deni Linalotokana na Gharama za Matibabu Nje ya Nchi Lafikia Bilioni 35
Serikali imesema deni linalotokana na gharama za matibabu nje ya nchi limefikia Sh35 bilioni na kuitaka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhakikisha inatoa rufaa kwa kuzingatia taratibu.

Akizungumza na Mwananchi jana, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kutibu magonjwa ambayo yanaweza kutibiwa ndani ya nchi kwa kuwa imeshasomesha wataalamu wa kutosha na kwamba vifaa pia vipo.

Ummy alisema nchi imekuwa ikitumia Sh5 bilioni kila mwaka kwa ajili ya matibabu nje na kwamba magonjwa ya saratani na upandikizaji wa vifaa vya usikivu yanaigharimu zaidi Serikali.

“Hivi sasa deni la matibabu nje ya nchi linafika Sh35 bilioni na hilo ni deni la miaka minne iliyopita,” alisema Ummy.

“Kwa sasa tumepunguza kwa kuwa wale ambao tulikuwa tunawapeleka nje kwa ajili ya kwenda kuwekewa vifaa vya usikivu ambao tulikuwa tunatumia zaidi ya Sh2 bilioni kwa mwaka, sasa tunafanyia ndani ya nchi hatutumiia fedha nyingi,” alisema Ummy.

Kuhusu matibabu nje ya nchi, Ummy alisema Serikali haijazuia wagonjwa kupelekwa nje ikiwa wana uwezo wa kujigharimia.

Ummy alisema utaratibu wa wagonjwa kusafirishwa ulibadilishwa.

“Zamani wizara ndiyo ilikuwa inatoa rufaa, siku hizi hatutoi mpaka tupate taarifa ya daktari ya Muhimbili, MOI, JKCI au Ocean Road. Waseme hatuwezi na tukishapata hiyo taarifa sasa ndiyo tunasema sawa tutampeleka,” alisema Ummy.

“Wenye fedha zao binafsi hatuwezi kuwazuia, tunasema wale ambao wanataka kugharamiwa na Serikali.”

Waziri Ummy aliwatahadharisha wataalamu hao na wanasiasa kwamba lazima wahakikishe kweli hawawezi kutibu na kwamba Wizara ipo tayari na itawaunga mkono.

Kwa upande wake, mkurugenzi mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema wapo tayari kutibu magonjwa yote yanayowezekana hapa nchini na hilo litafanikiwa ikiwa watakuwa na rasilimali watu na vifaa vya kutosha.

Alisema Muhimbili imeanza kuchukua hatua baada ya kuanza kutoa huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu Juni mwaka huu.

Alisema mafanikio hayo yanatokana na kujenga uwezo wa ndani kwa kusomesha watu na kuwekeza kwenye vifaa.

“Tunatarajia hivi karibuni kuanza upandikizaji wa figo kwa kuwa ni ugonjwa ambao Serikali imekuwa ikipeleka nje wagonjwa wengi kwa matibabu na kwamba utaratibu wa maandalizi umefikia tamati,” alisema.

“Hivyo tutakuwa tunawekeza kwenye vifaa na rasilimali watu ili kuendana na azma ya Serikali ili wagonjwa watibiwe hapa nchini kadri inavyowezekana . Hatusemi kwamba tutatibu wote, kwa wengine vitahitajika vifaa na ujuzi zaidi ambao hatuna.”

Wakati huohuo, Ummy amepokea msaada wa vifaa vipya kwa ajili ya vyumba viwili vya upasuaji watoto wadogo na wodi ya watoto ya upasuaji vyenye thamani ya dola 675,000 za Kimarekani (awa na Sh1.5 bilioni), vilivyotolewa na taasisi ya Archie Wood Foundation ambayo ni ya wataalamu na wahisani kutoka Uingereza.

Kwa upande wake Profesa Museru alisema msaada huo utasaidia vyumba vya upasuaji watoto.

“Kuna vifaa mbalimbali kama taa za kufanyia upasuaji, vitanda, mashine za usingizi na monitor zake, mashine za kuzuia damu kupotea wakati wa upasuaji, mashine ya kusafisha vifaa vya upasuaji na vifaa vyake,” alisema Profesa Museru.

Alisema msaada huo utawezesha kitengo cha upasuaji wa watoto kuwa na vyumba viwili vya upasuaji ambavyo vimekamilika na vyenye vifaa vya kisasa hivyo upasuaji utafanyika mara 10 kwa wiki badala ya ya mara tatu kwa wiki.

Akikabidhi msaada huo, mshauri mwelekezi wa taasisi hiyo, Profesa George Youngson alisema wataendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kupitia MNH katika kutoa huduma za hali ya juu ili kupunguza rufaa zisizokuwa za lazima.

Alisema wataendelea kutoa msaada wa vifaatiba na ikiwezekana kuleta wataalamu nchini kufanya upasuaji ili kujenga uwezo wa wataalamu wa Tanzania.

Benki Iliyohusika na Mauaji ya Kimbari Nchini Rwanda Yachunguzwa

0
0
Benki ya Iliyohusika na Mauaji ya Kimbari Nchini Rwanda Yachunguzwa
Nchi ya Ufaransa inadaiwa kuanzisha uchunguzi dhidi ya benki ya BNP Paribas, kufuatia madai kuwa ilihusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuawa.

Mashirika matatu ya umma yamepeleka kesi mahakamani dhidi ya benki hiyo, wakiilaumu benki hiyo kupitisha dola milioni 1.3 kwa muuza silaha ambapo pesa hizo zilitumiwa kununua silaha na kukiuka azimio la marufuku ya silaha la Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC linasema, Kanali wa kabila la Hutu ambaye alipokea silaha hizo, Theoneste Bagosora, anatumikia kifungo cha miaka 35 jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalitokea baada ya ndege iliyokuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana kutoka kabila la Hutu kudunguliwa Aprili 6, 1994.


Mashabiki wa Ali Kiba Sio Real Ila Ni Maadui wa Diamond- Mama Ashura

0
0
Mashabiki wa Ali Kiba Sio Real Ila Ni Maadui wa Diamond- Mama Ashura
Mchekeshaji kutoka Timamu, Mama Ashura amesema hakuumizwa na maneno makali katika mitandao ya kijamii kutoka kwa mashabiki wa Alikiba baada ya kumkosoa msanii huyo kwa kukaa muda mrefu bila kutoa wimbo.

Mwaka huu alikosoa vikali utaraibu wa Alikiba kukaa kipindi kirefu bila kutoa wimbo kitu ambacho kilipelekea kushambuliwa kwa maneno makali na team Kiba.

“Hao mashabiki Alikiba mwenyewe hawajui, halafu hawapi hata sapoti, mashiki wa Alikiba siyo wale real kabisa ni maadui wa Diamond,” amesema.

“Wanakuja kwa upande wa Alikiba wao wana-take advantage ya kumsapoti huyo ambaye yupo tofauti na huyu lakini wangekuwa real wasingekuwa wanatumia matusi,” Mama Ashura ameiambia Times Fm.

Katika hatua nyingine alimtaja Alikiba kama msanii asiyeonyesha ushirikiano kwa mashabiki wake na wale wanaomsapoti katika mitandao ya kijamii.

“Eric Omondi alitoa cover ya Zilipendwa na Seduce Me, Diamond alicomment ‘asante’ lakini Alikiba!!!! (hakufanya hivyo)” amesema.



Hii Hapa Picha ya Mobetto na Petiti Man Wakiwa Kwenye Mahaba Mazito Yazua Gumzo Mitandaoni

0
0
Hii Hapa Picha ya Mobetto na Petiti Man Wakiwa Kwenye Mahaba Mazito Yazua Gumzo Mitandaoni
Petitman mume wa Esma Platnumz ambaye ni dada yake Diamond amelazimika kuvunja ukimya baada ya picha zinazomuonyesha akiwa na Mobetto katika hali ya mahaba.

Petit ambaye ni meneja wa Billnass na Country Boy, amedai picha hizo zimesambazwa kwa lengo la kumchafua yeye pamoja na familia yake.

“Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni za zamani sana. Hazina uhusiano wowote na maisha yangu ya sasa au na yale yanayoendelea kuhusu Hamisa ambaye anaonekana pia katika picha hizo kwa sasa,” aliandika Petit Instagram.

Aliongeza,”Yeyote ambaye ameamua kuzisambaza ana nia moja tu. Kuniunganisha katika suala ambalo sihusiki na kunichafua. Mimi kwa muda mrefu niko na mke wangu mpendwa ambaye kila mtu anamjua na tuko busy kujenga familia yetu. Inawezekana jambo hili haliwafurahishi baadhi ya watu hivyo kuamua kusambaza picha za zamani kwa nia zao ovu. Niseme tu kwa kifupi hizo picha sio za kutilia maanani. Ni picha za zamani sana. Kwa sasa sio muda wa kuchafuana. Huu ni muda wa kila mmoja wetu kupambana kujijenga na kulea familia yake. Mimi kama baba wa familia jukumu langu ndio hilo”

Mobetto hivi karibuni amejifungua mtoto wa kiume, Abdul ambaye amezaa na muimbaji Diamond Platnumz.


Upinzani Nchini Kenya Kuandamana Leo Nje ya Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi IEBC

0
0
Upinzani Nchini Kenya Kuandamana Nje ya Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi IEBC
Chama cha upinzani nchini Kenya NASA kimeitisha maandamano Jumanne nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi.
Hatua hii ni ya kushinikiza kujiuzulu kwa baadhi ya maafisa wa juu wa tume hiyo walioshiriki kuandaa uchaguzi mkuu wa August 8 mwaka huu uliobatilishwa na mahakama ya juu nchini.
NASA umeeleza kwamba hautovamia makao ya tume ya IEBC kama ilivyotajwa awali kuwatimua kwa lazima maafisa hao, badala yake unasema maandamano yatakuwa ya amani katika barabara za mji mkuu Nairobi kushinikiza kujiuzulu kwao.
Hilo ni mojawapo ya masharti iliyotoa NASA kushiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu.
Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kwa wapinzani ambao amesema watakumbana na mkono wa sheria iwapo maandamano yao yataingilia shughuli za kiuchumi za raia wa nchi hiyo.
Amesema, 'Endeleeni na maandamano yenu, mukigusa mboga za mama wanaouza barabarani, tuko na nyinyi. Mukigusa maduka ya watu tuko na nyinyi. Lakini kama hamuna lingine lolote la kufanya isipokuwa kutembea - tembeeni. Mimi nawaambia hata mukinitukana mpaka asubuhi, haitabadilisha dunia'.
Upinzani unasisitiza kuwa una haki ya kuandamana kwani hata upande wa serikali - Muungano wa Jubilee - umeshafanya maandamano kama hayo hivi juzi walipoelekea katika mahakama ya juu zaidi wakitaka majaji wa mahakama hiyo waondolewe.
Mmoja ya vinara waandamizi wa kambi ya upinzani, Musalia Mudavadi ameiambia BBC, kuwa mahakama ya juu zaidi ilisema IEBC ilishindwa kuandaa uchaguzi mkuu kulingana na sheria.
Ameeleza, 'Tume ya IEBC sio vyombo tu, bali ina watu ndani ambao ni maafisa wanaohudumu katika kitengo cha usajili wa watu, masuala ya teknolojia ya mawasiliano na kadhalika, walishindwa kutekeleza wajibu wao na ndio wanaoweza kuondolewa.
Muungano wa NASA unataka jumla ya maafisa 12 wa tume hiyo washtakiwe kwa kutowajibika katika uchaguzi uliobatilishwa wa Agosti 8.
Unataka pia mfumo wa teknolojia uliotumiwa wakati wa uchaguzi huo ubadilishwe.

Serikali Imetangaza Rais , Mawaziri na Viongozi Wote wa Nchi Kutibiwa Muhimbili

0
0
Serikali Imetangaza Rais , Mawaziri na Viongozi Wote wa Nchi  Kutibiwa Muhimbili
SERIKALI imekazia msimamo wake wa kutowapeleka viongozi wa nchi na wabunge katika hospitali za nje ya nchi kwa ajili ya matibabu isipokuwa kwa idhini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), na sasa hata kwa Rais.

Msimamo huo ulitangazwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, katika hafla ya uzinduzi wa wodi za upasuaji wa watoto MNH jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza katika halfa hiyo, Waziri Ummy alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Lawrence Museru kutotishika dhidi ya kauli za wanasiasa wanaolazimisha kutibiwa nje.

"Mkurugenzi wa Muhimbili naomba usitishike, awe Rais, niwe mimi, awe mbunge, akiomba kwenda kutibiwa nje kama nyie mna uwezo wa kumtibia huo ugonjwa wake msitoe ruhusa, msituogope, simamieni taaluma yenu," alisema waziri huyo.

Kauli hiyo imetolewa wakati kukiwa na mvutano baina ya serikali na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Nairobi, Kenya kutokana na kushambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma Septemba 7.

Katika mvutano huo, serikali inasisitiza itagharamia matibabu ya mbunge huyo ikiwa familia yake itafuata utaratibu iliouweka mwaka jana kwa maofisa wa serikali na viongozi kupata kibali MNH kutibiwa ughaibuni.

Januari 11, mwaka jana, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ikishirikiana na Wizara ya Afya ilitangaza masharti mapya kwa wafanyakazi na maofisa wa serikali kwenda kutibiwa nje ya nchi, ikifuta utaratibu uliokuwapo ambao ulikuwa rahisi kupata kibali cha kwenda kutibiwa ughaibuni.

Msemaji wa Wizara wa Afya, Nsanchris Mwamwaja, alisema mtu atakayetaka kwenda kutibiwa nje ya nchi, atalazimika kuidhinishiwa safari yake na jopo la madaktari bingwa wa MNH.

Mwamwaja alisema uamuzi huo umelenga kuondoa mwanya wa baadhi ya watumishi wa umma kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa maradhi ambayo yanaweza kutibiwa kirahisi katika hospitali zilizopo nchini.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo ilikabidhiwa kwa Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 27 na baadaye kuwasilishwa bungeni mjini Dodoma Aprili 13, hadi Juni 30, mwaka jana, deni la serikali katika hospitali za rufaa za India lilifikia Sh. bilioni 19.193.

Kwenye ripoti hiyo, CAG Assad anazitaja hospitali za rufaa za India zinazoidai Tanzania kuwa ni Ahmedabad Sh. bilioni 2.056, Bangalore Sh. milioni 548.323, Chennai Sh. bilioni 6.164, Madras Sh. milioni 5.274, Hyderabad Sh. bilioni 2.594 na New Delhi Sh. bilioni 7.824 zinazotengeneza jumla ya Sh. bilioni 19.193.

Ripoti ya CAG kwa mwaka 2014/15 iliyowasilishwa bungeni Aprili 24, mwaka jana, ilionyesha kuwa mbali na kudaiwa Sh. bilioni 16.94 na hospitali za rufaa za India, Tanzania pia ilikuwa inadaiwa Sh. milioni 448.144 kwa ajili ya malipo ya matibabu ya nje ya nchi ya maofisa wa balozi mbalimbali.

Ma- DC, RC Wapewa Onyo Kali Uwekaji Kiholela Watumishi Mahabusu

0
0
Ma- DC, RC Wapewa Onyo Kali Uwekaji Kiholela Watumishi  Mahabusu
Alianza aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kutekeleza majukumu yao huku wakijiweka kando na uwekaji mahabusu watu mara kwa mara.

Kisha, Septemba 16 alifuata Naibu waziri wa wizara hiyo, Selemani Jafo aliyewataka wakuu wa mikoa na wilaya kuitumia vizuri sheria inayowapa mamlaka ya kuwaweka ndani watu katika maeneo yao.

Jana, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aliwataka wakuu hao kuacha tabia ya kuwaweka mahabusu watumishi wa umma kwa makosa ya kitaaluma.

Ummy alitoa wito huo mjini hapa wakati akizindua majengo la wodi ya wazazi na matibabu ya dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo yaliyojengwa kwa udhamini wa Taasisi ya Dhi Nureyn.

Alisema makosa kama hayo yanapaswa kushughulikiwa na mamlaka wanazofanya kazi chini yake, lakini kitendo cha kuwaweka ndani kinawaondolea morali na ali ya kufanya kazi. “Nakushukuru mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo sijawahi kusikia umefanya kitendo cha namna hiyo. Ukiona makosa ya kitaaluma walete juu tutawashughulikia,” alisema Ummy.

Marekani Yailalamikia Korea Kaskazini

0
0
Marekani Yailalamikia Korea Kaskazini
Marekani imeilalamikia Korea Kaskazini, kwa kauli yake kuwa ina haki ya kuzitungua ndege za kivita za Marekani hata kama zipo nje ya anga la taifa hilo.
Msemaji wa ikulu ya Marekani ya white house Sarah Huckabee Sanders, amewaambia waandishi wa habari kuwa kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea Kaskazini kwamba Marekani imetangaza vita,ni ya kipuuzi.
Kauli hiyo ya waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini ni kufuatia ujumbe wa Rais Trump kupitia ukurasa wake wa twitter,uliokuwa ukisema utawala wa Pyongyoung hauwezi kudumu kwa muda mrefu.
Akizungumza katika kituo cha mafunzo cha kimataifa mjini Washington,Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha, amesema dunia inapaswa kupatiwa nafuu na maudhi ya Korea Kaskazini.
"Hakika, hii inaonyesha kuwa Korea kaskazini itaendeleza maudhi yake, na katika mazingira kama haya,sisi Korea Kusini na umoja wa mataifa tunapaswa kulishughulikia suala hili kwa umakini mkubwa,ili kutoendeleza hofu ya madhara ya kijeshi katika ukanda wetu.
Hatuwezi kuwa na vita nyingine katika ukanda wetu,hatuwezi kuwa na vita katika rasi ya Korea. Madhara yake hayawezi kuwa kwa bara la Asia tu,bali hata kwa kaskazini mashariki mwa Asia na jamii ya kimataifa kwa ujumla.Hatuwezi kuhatarisha usalama wa raia wetu,waliofanya kazi ya kujenga demokrasia kwa miongo saba sasa na ujenzi wa uchumi kutokana na vita vilivyowahi kutokea..")
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon Kanal Robert Manning amesema iwapo Korea kaskazini haitaacha vitendo vyake vya kuudhi,watatoa idhini kwa Rais kuchukua hatua dhidi ya Korea Kaskazini. Naye Balozi China wa umoja wa mataifa Liu Jieyi amesema suala hili linaingia katika hatua ya hatari.
Korea Kakskazini mbali ya kuwekewa vikwazo,imeendelea na majaribio yake ya Nyuklia na makombora,kinyume na msimamo wa umoja wa mataifa
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images