Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Ben Pol Afunguka Sifa za Mwanamke Anayempenda Kuwa Naye Kimapenzi

$
0
0
Ben Pol Afunguka Sifa za Mwanamke Anayempenda Kuwa Naye Kimapenzi
Msanii Ben Pol amesema kitu pekee anachokiangalia kwa mwanamke ambaye ataweza kumzimikia na kuwa naye kimapenzi ni lazima awe anajiamini pindi wakiwa wanaongea au hata wakiwa wana-chat.

Ben Pol amefunguka hayo baada ya kupita siku chache tokea aliyekuwa anadaiwa kutoka naye kimapenzi ambaye ni msanii wa vichekesho nchini Anastazia Kisaveli 'Ebitoke' kulalamika kwamba hapokelewi simu yake wala kujibiwa ujumbe mfupi pindi amtumiapo Ben.
"Endapo nikimpenda msichana sifa kubwa huwa naangalia 'confidence' yake pindi tukiwa tunaongea na ku-chat, U-smart, umakini na uharaka katika kujibu vitu ambavyo anaulizwa kwa wakati huo", amesema Ben Pol.
Ben Pol kwa sasa anatamba na kazi yake mpya iliyopewa jina la 'Kidume' ambaye amemshirikisha msanii kutoka Nigeria anayejulikana kwa jina la Chidinma.

Jeshi la Polisi Kufanya Uchunguzi wa Maiti Zinazookotwa Baharini

$
0
0
Jeshi la Polisi Kufanya Uchunguzi wa Maiti Zinazookotwa Baharini
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa majini wanaendelea na uchunguzi dhidi ya matukio ya mauaji yanayoendelea kutokea katika baadhi ya maeneno na kisha miili kutupwa kwen

Kamanda Mambosasa ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, na kusema kwamba matukio hayo yanaonekana kudhamiriwa na watu wanaofanya hivyo kwani miili yote inakutwa imefungwa kamba.

"Jeshi la polisi tunaendelea na ufuatiiaji tukishirikiana na askari wa majini kwa sababu matukio haya yanatokea huko, kama kanda tunaendelea tena kwa uchunguzi wa hali ya juu, na hawa wauaji wanakuwa wanadhamiria kabisa kufanya hivyo. Ni vifo vya mashaka kwa kweli na yote inakutwa imefungwa hii inamaanisha huyo mtu anadhamiria", amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa ameendelea kwa kuzungumzia miili mingine ambayo iliokotwa katika fukwe za pwani ya Msasani, na kusema kwamba miili ile haikujulikana ni kina nani na hakukuwa na mtu alikwenda kuripoti kupotelewa na ndugu yake, hivyo waliikabidhi Manispaa kuizika.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio mfululizo ya watu kuuawa na kutupwa baharini, na kisha miili yao kuokotwa ikiwa imefungwa kwenye viroba, ambapo jana miili mitatu imeokotwa huku mwili mmoja ukiwa umefungwa jiwe shingoni.

Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Lawataka Wananchi Kuchukua Tahadhari ya Ugonjwa Huo

$
0
0
Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Lawataka Wananchi Kuchukua Tahadhari ya Ugonjwa Huo
Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (Nacopha) limesema licha ya takwimu kuonyesha kwamba maambukizi ya VVU yanapungua nchini bado wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari.

Takwimu za Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids) zinaonyesha maambukizi yalipungua kutoka asilimia saba mwaka 2003 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2012.

Akizungumza leo, Mratibu wa Kanda ya Dar es Salaam wa Nacopha, Edna Edson amesema  wananchi wasibweteke na kupungua kwa maambukizi bali wachukue hatua kukabiliana na virusi.

Amewaeleza waratibu wanaopata mafunzo ya kusimamia ruzuku ya mradi wa Sauti yetu unaoendeshwa na baraza hilo kwamba elimu kwa wananchi ndiyo suluhisho katika kukabiliana na maambukizi mapya.

Amesema  mradi huo utatekelezwa kwenye halmashauri 46 nchini huku ukilenga kuelimisha jamii ili ione sababu za kutafuta ushauri na upimaji wa virusi vya Ukimwi.

“Mradi huu pia unalenga kuelimisha jamii ya watu wanaoishi na VVU ili kuongeza upatikanaji wa huduma na kuhakikisha wanaendelea kupata tiba,” amesema  na kulishukuru Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) kwa kufadhili mradi huo.

Baadhi ya halmashauri utakakotekelezwa mradi huo ni pamoja na Temeke, Kilombero, Lindi, Korogwe Morogoro na Masasi.

Kwa upande wake, Daisy Majamba aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kama hatua hazichukuliwi Ukimwi unaweza kuleta athari katika jamii na uchumi wa nchi kwa ujumla.

“Mradi huu na elimu itakayotolewa itamfanya kila mmoja wetu kupata uelewa na hivyo kujikinga na maambukizi,” amesema.

Ametaka uongozi wa baraza hilo kutekeleza mradi huo na kuhakikisha kwamba unawafikia walengwa ili jamii nzima ya watanzania iweze kunufaika.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nacopha, Deogratius Rutatwa aliwataka waratibu hao kuzingatia mafunzo ili ruzuku zitakazotolewa kwa ajili ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ziweze kutumika kama ilivyokusudiwa.

Serikali Kufanya Ukarabati Hospitali Aliyolazwa Tundu Lissu

$
0
0
Serikali Kufanya Ukarabati Hospitali Aliyolazwa Tundu Lissu
Serikali imeahidi kupeleka Sh 500 milioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa lengo kulifanyia ukarabati jengo la upasuaji ambalo pia lilitumika kumhudumia Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi nyumbani kwake Area D mjini.

Lissu alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu na kupelekwa hospitalini hapo kwa ajili ya huduma ya utengemavu kabla ya kupelekwa Nairobi nchini Kenya ambapo hadi sasa anaendelea matibabu.

Akizungumza wakati alipoitembelea hospitali hiyo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jafo amesema kuwa ukarabati huo unalenga katika kukarabati miundombinu ili kuendana na mahitaji ya mji wa Dodoma kwa sasa.

“Hatuwezi kuvumilia hili tunataka tulete fedha tuikarabati ili iendane na hali halisi ya mahitaji ukizingatia sasa hivi Dodoma ni mji mkuu.

Tunataka viongozi na wananchi waweze kutibiwa katika hali nzuri na ya kisasa zaidi ya hapa,”amesema.

Hatua hiyo ilifuatia Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Caroline Damian jengo hilo limekuwa likitumika kufanya upasuaji kwa wastani wa watu 500 kwa wiki.

“Kwa siku tumekuwa tukifanya upasuaji kwa watu kati ya 15 na 20, ili kukidhi mahitaji imebidi kubalisha vyumba vingine ambavyo havikuwa vya upasuaji kuwa vya upasuaji,”amesema.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Kiologwe amesema kwamba awali wakati jengo hilo linajengwa kuna aina ya upasuaji ambazo zilikuwa hazifanyiki mkoani hapa lakini sasa zinafanyika.

“Zamani kuna aina ya upasuaji ulikuwa haufanyiki lakini sasa unafanyika. Tuna madaktari wazuri wanaojituma lakini changamoto ipo katika miundombinu,”amesema.

Kuhusu ujenzi wa jengo la wakinamama  na watoto, Jafo amesema ameridhika na kazi inayoendelea bali amemtaka mkandarasi kuhakikisha kazi hiyo inakamilika Oktoba 20 ili lianze kutumika.

“Nimewapa maelekezo wahakikishe kuwa jengo hilo linakuwa na mfumo wa gesi ya oksijeni ili kuepuka wahudumu ama wauguzi kukimbizana na mitungi mara kunapokuwa na mahitaji ya kuokoa maisha ya mama na mtoto,”amesema.

Meneja Msaidizi wa Mradi huo, Mhandisi Frank Mabubu amesema jengo hilo limekamilika kwa asilimia 85 na kwamba ujenzi utakamilika Oktoba 20.

Mtandao wa Whatsap Wafungiwa

$
0
0
Mtandao wa Whatsap Wafungiwa
Mtandao wa WhatsApp umeingia kifungoni nchini China ukiifuatia na Instagram, Twitter, Facebook, Gmail, Snapchat na Pinterest.

WhatsApp imeanza kufungiwa taratibu katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kwa mujibu wa taasisi inayoratibu masuala ya mitandao duniani, Open Observatory of Network Interference (OONI).

Mtandao wa Shirika la Utangazaji CNN unaripoti kuwa katika miezi ya hivi karibuni WhatsApp imekuwa ikipatikana kwa shida.

Mtandao huo ulianza kufungiwa taratibu wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa chama tawala cha Communist, utakaoanza Oktoba 19 mwaka huu.

Kwa kawaida nchi hiyo hudhibiti matumizi ya mtandao katika kipindi cha uchaguzi mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.

China inatumia mtindo wa Great Firewall katika kudhibiti matumizi ya intaneti ambayo hujumisha sera na teknolojia.

Watu Wawili Wauwawa katika Nyumba ya Kulala Wageni

$
0
0
Watu Wawili Wauwawa katika Nyumba ya Kulala Wageni
UTATA umeibuka baada ya miili ya watu wawili waliouawa na watu wasiojulikana kukutwa katika nyumba ya kulala wageni mjini Tanga ikiwa haina nguo na imefungwa kamba za miguu na mikononi.

Katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedicto Wakulyamba miili ya watu wawili, wote wanaume, iligunduliwa jana majira ya saa mbili asubuhi na mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Bomai Inn iliyopo Kata ya Majengo jijini hapa.

Kamanda Wakulyamba aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa jana kuwa mhudumu wa nyumba hiyo ambaye hakumtaja kwa jina, alibaini kuwapo kwa miili hiyo alipotaka kufanya usafi ndani ya chumba hicho.

"Majira ya saa mbili asubuhi wakati mhudumu alipoingia ndani ya chumba hicho namba 303 kwa ajili ya kufanya usafi, alikutana na miili ya watu hao wawili wote ni wanaume ikiwa imelala chini, imefungwa kamba miguuni na mikononi," alisema.

Kamanda huyo alisema miili hiyo ni ya watu wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35 na 40 ambao hawakutambulika mara moja.

Alisema kuwa kwa mujibu wa kumbukumbu za kitabu cha wageni cha nyumba hiyo ya kulala wageni, mtu anayeitwa Rashid Omari alijiandikisha kutumia chumba hicho siku hiyo.

Alisema kwa mujibu wa kumbukumbu hizo, Omari ni Msafa kwa kabila, mkazi wa Dar es Salaam na ni mfanyabiashara.

Kamanda Wakulyamba alisema miili hiyo haikuwa na jeraha lolote zaidi ya michubuko ya kawaida na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini sababu za mauaji hayo na waliohusika kuyatekeleza ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Vifo vya watu hao vimezua utata kutokana na waliouawa kutofahamika kwa wakazi wa eneo hilo, mazingira ya vifo vyao kuashiria mauaji, wauaji kutojulikana pamoja na kitendo cha uongozi wa nyumba hiyo ya kulala wageni kuruhusu wanaume wawili walale chumba kimoja, kinyume cha taratibu za uendeshaji wa biashara hiyo.

"Watu wawili tena wanaume kuuawa ndani ya chumba kimoja na kusiwe na hata mtu aliyesikia kurupushani za mauaji hayo... inatia hofu kubwa na inawezekana kuna mpango maalum wa wauaji hao," alisema Asha Ramadhan, mmoja wa walioshuhudia tukio hilo la utoaji miili hiyo.

Hamza Issa, mkazi mwingine wa maeneo hayo, alisema huenda mauaji hayo yalipangwa na aliyelipia kutumia chumba hicho kabla ya kukutwa miili ya watu wawili.

Mkazi mwingine wa maeneo hayo, Anthon Aloys, alisema huenda maiti hizo ziliingizwa ndani ya chumba na mkodishaji chumba hicho baada ya watu hao kuuawa eneo jingine.

WATU WATATU
Matukio ya wanaume zaidi ya mmoja kuuawa wakiwa katika chumba kimoja cha nyumba za wageni yalififia kwa muda lakini si uhalifu ambao ni mgeni.

Machi 21, mwaka jana watu watatu walikutwa wakiwa wameuawa kwa kunyongwa katika nyumba ya kulala wageni ya Mexico, mjini Kyela mkoani Mbeya, ikiwa na majeraha ya kuunguzwa kwa moto.

Mganga mfawidhi wa Hosptali wa Wilaya ya Kyela, Dk. Francis Mhagama alikaririwa akisema maiti hizo za watu watatu zilikuwa zimenyongwa pamoja na majeraha ya moto.

Kwa mujibu wa kitabu cha wageni cha nyumba hiyo, majina ya watu hao yalikuwa Hassan Ally, Mariam Hassan na Adam.

Aidha, Agosti mosi, mwaka jana pia watu wawili walikutwa wamefariki katika nyumba ya wageni ya Kings Rest House iliyopo Mtaa wa Bumila, Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam huku miili yao ikiwa imeungua moto.

Watu hao waliofariki walikuwa wafanyabiashara wanaouza ng’ombe katika mnada wa Pugu na mara nyingi walipokuja jijini walifikia hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alisema mmoja wa waliofariki alijiandikisha kama Lameck Ludovick, mfanyabiashara na mkazi wa Dar es Salaam.

Hapatatokea Upelelezi Kutoka Nje Uhalifu Unaofanywa Nchini Utapelelezwa na Vyombo Vyetu- Mwigulu

$
0
0
Hapatatokea Upelelezi  Kutoka Nje Uhalifu Unaofanywa Nchini Utapelelezwa na Vyombo Vyetu- Mwigulu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wananchi nchini kuendelea kuwa na imani kubwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini katika kulinda Raia na mali zao

Waziri Mwigulu akizungumza kuhusu watu wanaotaka wapelelezi kutoka nje na hatua wanazochukua juu ya watu wasiojulikana.

Waziri Mwigulu amesema kuwa kama yeye ndiye aliyepewa dhamana ya usalama wa Raia na mali zao katika wizara ya mambo ya ndani basi hapatatokea hata kakitongoji kamoja au kauchochoro ambacho kitaonekana kimeshindikana ndani ya nchi yetu, Ameyasema hayo akizungumza na wananchi wa kata ya Kinampanda wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Aidha Waziri Mwigulu amesema kuwa hata watu wanaoshambulia watu watashughulika nao mmoja mmoja hasa waliobeba jina la watu wasiojulikana, kwahiyo wananchi waendelee kuliaamini jeshi la polisi nchini wakati huu ambapo wanaendelea na kazi ya upelelezi wa kuwakamata watu wote waliohusika na mashambulio kwa Mbunge Tundu Lissu, Afisa mstaafu wa jeshi la wananchi na hakimu huko Mtwara kwani uchunguzi huo auna ukomo mpaka upate wote katika idadi yao waliohusika na mashambulizi.

Waziri mwigulu ameongeza kuwa nchi hii ni nchi huru inajitegemea na kuna watu wanasema wanataka vyombo vya nje vifanye uchunguzi, hawa watu wanao fanya uhalifu nchini, upelelezi utafanywa na watu wetu, watakamatwa na vyombo vyetu na watafikishwa katika vyombo vya sheria vya hapahapa  tunatakiwa kuamini vyombo vyetu, kama serikali tutashugulikano kwelikweli na si kama hatujaanza nao tunashughulika nao.

Ukomo wa Umri wa Rais Pasua Kichwa Uganda

$
0
0
Ukomo wa Umri wa Rais Pasua Kichwa Uganda
Kikundi cha wafuasi kindakindaki wa chama tawala cha NRM wakiwemo baadhi ya wenyeviti wa majimbo wameelezea pendekezo la kufuta Ibara ya 102 (b) ya Katiba ili kuondoa ukomo wa umri wa rais ni jaribio la kupindua sheria mama.

Wafuasi hao wanasema wazo la kuondoa ukomo wa umri wa mgombea urais linachochewa na uroho

Katika taarifa yao iliyosomwa jana na Dennis Sekabira, ambaye ni mwenyekiti wa Jimbo la Nakaseke Kusini, kikundi hicho kiliwaambia waandishi wa habari kwamba wanapinga msimamo wa wabunge wa chama hicho kwa sababu mradi wao huo hauna maslahi kwa amani ya nchi.

“Huu ni mwelekeo hatari na unahatarisha amani tuliyoifaidi nchini,” alisema Sekabira ambaye ameeleza kwamba kikundi hicho kina wajumbe 121 wa Halmashauri Kuu ya Taifa, chombo cha pili kwa ukubwa katika uongozi wa chama.

Mwenyekiti huyo alisema wajumbe hao hawaungi mkono juhudi za kuzuia maoni ya wengi dhidi ya kusudio la kuondoa ibara hiyo na kwamba inahitajika amani wakati wa kukabidhi madaraka.

“Tumeamua tusiinyime haki nchi yetu nafasi pekee ya kubadilisha mamlaka kwa amani,” alisema. “Badala ya kuhutubia suala la ukomo wa umri, wabunge wa NRM wanapaswa kujikita katika utekelezaji wa Ilani ya chama.”

Mwaka 2015 Waganda walibadili katiba kuondoa ukomo wa mihula kumwezesha Rais Yoweri Museveni kugombea muhula wa tatu na kuendelea na sasa ukiondolewa ukomo wa umri wa miaka 75, rais huyo mwenye umri wa miaka 73 sasa atakuwa huru kugombea tena mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 77.


Mfalme Mswati Ameoa Mke wa Miaka 19 Na Kuwa Mke wa 14

$
0
0
Mfalme Mswati Ameoa Mke wa Miaka 19 Na Kuwa Mke wa 14
MFALME Mswati wa Tatu wa Swaziland kwa mara nyingine ameongeza idadi ya wanawake kwa kuoa mwanamke mwingine. Katika kuadhimisha Ngoma ya Umhlanga ambayo hufanyika kila mwaka kwa kumpa mfalme fursa ya kuchagua mwanamke wa kuoa, mfalme huyo hivi karibuni alimchagua Siphele Mashwama mwenye umri wa miaka 19 kuwa mkewe wa 14.


Msichana huyo ambaye ni binti wa waziri Jabulile Mashwama katika serikali ya nchi hiyo, alipewa manyoya maalum mekundu ya ndege anayejulikana kama emagwalagwala ambaye huhusishwa na sherehe hiyo maalum ya kifalme. Mswati ambaye ana umri wa miaka 49 huchagua wanawake waliovuka umri wa miaka 19.

Pamoja na talaka kupigwa marufuku katika nchi hiyo ya kifalme, Mfalme Mswati amewahi kuwataliki wake zake watatu. Siphele ambaye ni mhitimu wa Waterford Kamhlaba World University College, alifuatana na Mfalme Mswati alipohudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni.
Habari hiyo ilifichuliwa na msimamizi wa sherehe za kifalme, Hlangabeza Mdluli, aliyethibitisha kwamba Mswati alikuwa amefuatana na mkewe huyo ambaye kwa umri ndiye mdogo zaidi.

Wake wengine wa Mswati.
Wake zake wengine ni pamoja na: Inkhosikati LaMatsebula, Inkhosikati LaMotsa, Inkhosikati LaMbikiza, Inkhosikati LaNgangaza, Inkosikati LaMagwaza (ameachika), Inkhosikati LaHoala (ameachika), Inkhosikati LaMasango, Inkhosikati LaGija (ameachika).

Wakiwa kwenye sherehe za mwaka.
Wengine ni: Inkhosikati Magongo, Inkhosikati LaMahlangu, Inkhosikati LaNtentesa, Inkhosikati LaNkambule, Inkhosikati Ladube na Inkhosikati LaFogiyane. Mfalme King Mswati, anayejulikana pia kama Ngwenyama, yaani simba, anasemekana kuwa na watoto zaidi ya 13 ambao ni pamoja na binti yake mkubwa zaidi aitwaye Sikhanyiso, Sibahle Dlamini, Makhosothando Dlamini, Majaha Dlamini, na Tiyandza Dlamini.

Mswati akikagua gwaride.
Wengine ni Sakhizwe Dlamini, Saziwangaye Dlamini, Bandzile Dlamini, Lindaninkosi Dlamini, Mcwasho Dlamini, Temtsimba Dlamini na Temaswati Dlamini, among others. Baba yake Mswati, Mfalme Sobhuza wa Pili, alioa wanawake 70. Mswati amekuwa akishutumiwa kwa kujilimbikizia utajiri wakati watu wake wengi ni maskini.
Hivi karibuni, nchi hiyo ndogo ilitumia kiasi cha Dola milioni 2.2 (sawa na Sh. bilioni 5) kwa kununua magari ya anasa aina ya BMW 740i na pikipiki 80. Magari hayo yalikuwa ni kwa ajili ya viongozi wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrikca (SADC) waliyoyatumia kwa ajili ya mkutano wa siku mbili.

Afisa Wa Serikali Ajinyonga Hadi Kufa

$
0
0
Afisa Wa Serikali Ajinyonga Hadi Kufa
Afisa mmoja wa serikali katika jimbo la Nandi nchini Kenya, Kevin Kamboi amejinyonga hadi kufa kwa kile kilichoelezwa kuhusishwa na tuhuma za uhujumu uchumi na rushwa nchini humo.

Kamboi ambaye alikuwa anafanya kazi katika Idara ya Afya kama Afisa Ugavi, aliacha ujumbe akieleza kuwa amepata msongo wa mawazo baada ya kutolewa amri na Gavana wa jimbo hilo, kuchunguzwa iwapo amehusika na vitendo vya uhujumu uchumi, huku akiwataja maafisa wenzake ndiyo waliostahili kubeba msalaba huo.
Kamanda wa Polisi wa jimbo la Nandi nchini Kenya, Peter Wambani amesema marehemu alimuomba mke wake akamuandalie kikombe cha chai huku akiendelea kutazama mpira sebuleni, lakini aliporudi hakumkuta mumewe na baada ya kumtafuta alikuta mwili wake ukining'inia kwenye mti karibu na banda la ng'ombe.
Tukio hilo limetokea huku baadhi ya maafisa wengine wa idara hiyo wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi, kutokana na kupotea kwa fedha za serikali.

Mywether Aonyeshaya Jeuri ya Pesa Anunua Mjengo wa Bilioni 56

$
0
0
Mywether Aonyeshaya Jeuri ya Pesa Anunua Mjengo wa Bilioni 56
KWA watu wengi, kumiliki majumba Las Vegas na Miami ingetosha kuwafanya waone wameshamaliza kazi, lakini Floyd Mayweather yupo tofauti na wengi.

Bondia huyo Mmarekani ambaye hajawahi kupigwa katika pambano lolote kati ya mapambano yake 50 aliyocheza, anaendelea ku­furahia maisha ya kustaafu baada ya kumchapa Muiri­shi, Conor McGregor jijini Las Vegas.

Baada ya kumchapa McGregor katika raundi ya 10, inadaiwa Mayweather aliweka kibindoni zaidi ya pauni milioni 250 (Sh bil­ioni 752).

Bondia huyo ambaye amekuwa hajivungi ka­tika matumizi ya fedha na kufurahia jasho lake, amemwaga kitita cha pau­ni milioni 18.9 (zaidi ya Sh bilioni 56) kununua jumba kubwa la kifahari, katika eneo la watu wazito la Beverly Hills.

Kumbuka kuwa, Mayweather, 40, ana jumba jingine jijini Las Vegas, pia analo jingine Miami ambalo lina thamani ya pauni milioni 5.69 (zaidi ya Sh bilioni 17).

Jumba hili jipya alilonunua, lina vyumba sita vya kulala na mabafu kumi. Pia lina chumba maalu­mu cha sinema ambacho wanaweza kukaa watu 50 kwa raha kabisa, likiwa na mbwembwe nyingi zikiwemo mvinyo, bisi, chocolate na pipi.

Mayweather amecheza ngumi kwa miaka 21 na alistaafu Agosti 26 akiwa ameingiza fedha nyingi zaidi ya bondia yeyote yule kihistoria

Mmarekani huyo anadai kuwa yeye ndiye bondia wa kwanza kuingiza zaidi ya dola bilioni moja (zaidi ya Sh trilioni 2) katika mchezo huo mgumu zaidi.

Ukiachana na mkwanja aliotumia katika ku­nunua jumba hilo, inasemekana pia kuwa May­weather ametumia kiasi cha pauni 369,000 (zaidi ya Sh bilioni moja) kwa ajili ya kununua vitu vya ndani.






Msigwa: Chama cha Mapinduzi Kimechoka Polisi Acheni Kukisaidia

$
0
0
Msigwa: Chama cha Mapinduzi Kimechoka Polisi Acheni Kukisaidia
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kulitaka jeshi la polisi nchini kutokisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema wamuache yeye na CHADEMA wapambane kukiondoa chama hicho madarakani kwani kimeshachoka

Msigwa amesema kitendo cha polisi juzi kumkamata wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kibunge kimemuudhi sana na kusema ni jukumu la Mbunge yoyote yule kuelimisha jamii, kuwapa habari wananchi pamoja na kuikosoa serikali.
"Mimi nilikuwa sifanyi uchochezi kazi ya Mbunge kuelimisha, kuhabarisha, kuikosoa, kuisimamia serikali na kuchochea maendeleo katika jimbo kwa hiyo kama Mbunge ninayo haki ya kuzungumzia Demokrasia na haki ya kuzungumzia mambo ya utawala bora, nina haki ya kuzungumzia haki za binadamu , kitendo cha polisi kunikamata juzi kimeniudhi sana hao polisi waniache mimi na chama changu tupambane na CCM, wasiisadie CCM kwani saizi imechoka ipo dhohofu yaani ipo taabani wanajaribu kuitetea CCM, wajitokeze CCM wenyewe wajibu hoja" alisema Msigwa
Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye ni Mbunge ana haki ya kuikosoa serikali iliyopo madarakani hata kuichonganisha na wananchi ili wasiichangue tena mwaka 2020 anadai huo ndiyo wajibu wake kisiasa na ndiyo maana anakuwa mpinzani.

Hivi Ndivyo Jopo la Madaktari 10 Walivyojaribu Kuokoa Uhai wa Lissu Ndani ya Saa 10

$
0
0
Hivi Ndivyo Jopo la  Madaktari 10 Walivyojaribu Kuokoa Uhai wa Lissu Ndani ya Saa 10
Jumla ya madaktari bingwa 10 walitumia saa 10 kwa ajili ya kunusuru maisha ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma hadi Uwanja wa Ndege kabla ya kusafirishwa Nairobi.


Muda huo ulijumuisha tangu Lissu alipopigwa risasi saa 7:30 mchana Septemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake mtaa wa Area D mjini hadi aliposafirishwa kwenda Nairobi nchini Kenya saa 6:17 usiku.


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Kiologwe akizungumza na Mwananchi amesema lilikuwa tukio lenye changamoto zake.
“Nina timu nzuri kwa maana nina uongozi mzuri wa hospitali ya mkoa lakini nina madaktari na watoa huduma ambao wana ‘commitment’ ya hali ya ajabu,” amesema.
Amesema wakati tukio hilo linatokea yeye alikuwa mbali kidogo na hospitali lakini baada ya kupata taarifa na kufika alikuta tayari Lissu ameshaanza kuhudumiwa.

“Tulikuwa na timu ya zaidi ya watu 20 ambao walishiriki kwa njia mbalimbali. Unajua kuna ushiriki wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja. Kwenye macho ya watu huwa anaonekana daktari pekee lakini ukweli ni kwamba hawezi kufanya kazi pekee yake lazima wawepo watu
wengine,”amesema.
Amesema kati ya timu hiyo 10 walikuwa ni madaktari bingwa katika fani mbalimbali walikuwa kazini wakati huo ambao Lissu anafikishwa hospitalini baada ya kuumia.
Pia katika timu hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya ambaye ni mtaalam bingwa wa usingizi alishiriki hadi saa 6.17 usiku Uwanja wa Ndege wa
Dodoma kabla ya Lissu kwenda jijini Nairobi nchini Kenya.
Hata hivyo, amesema walikuwa na vitendea kazi vya kutosha na ndio maana walisema kuwa wanaweza kumhudumia mgonjwa huyo.
“Jambo hilo halikuwa na nia ya kuwatuliza watu hapana, bali lilikuwa linamaanisha kuwa uwezo tunao kweli,”amesema

“Ni kweli tukio kama lile lilikuwa na changamoto zake. Changamoto ya kwanza ni tukio ambalo limewagusa watu wengi sana kisaikolojia. Watu wengine wangependa kumuona mgonjwa kwa hiyo mwananchi anaweza kukimbia kuja kumuona,” amesema.
Hata hivyo, amesema hawakuweza kuwaruhusu kwa sababu za kiutaratibu ambapo kwa muda huo madaktari wanahitaji zaidi kuokoa maisha ya mgonjwa.
“Suala la kumuona na kujua ameumiaje wakati huo hauwezi kumsaidia kwa wakati huo halikuwa muhimu. Niwashukuru sana wananchi wa Dodoma pamoja
na viongozi walikuwa ni wasikivu unapowapa maelekezo walikuwa wanatekeleza,”amesema.
Amesema walipata ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa watu mbalimbali wakati wa tukio hilo jambo ambalo liliwasaidia katika utekelezaji wa kazi hiyo.

Polisi Wazingira Ofisi za Upinzani, Bunge na Maeneo Muhimu ya Jiji la Kmpala

$
0
0
Polisi Wazingira Ofisi za Upinzani, Bunge na Maeneo Muhimu ya Jiji la Kmpala
Maofisa polisi wamesambazwa katika maeneo mengi muhimu katika jiji la Kampala ulinzi unaohusiana na mjadala juu ya pendekezo la kufutwa Ibara ya 102 (b) ya Katiba likilenga kuondoa ukomo wa umri wa rais.

Makao makuu ya ofisi za chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) kinachoongozwa na Dk Kiiza Besigye kuanzia jana yamezingirwa na polisi wa kawaida, wa kuzuia ghasi na wa kupambana na ugaidi. Ofisi hizo zilizopo Najjanankumbi katika barabara ya Kampala-Entebbe zimezungukwa na polisi wenye silaha.

Msemaji wa Polisi Asan Kasingye alisema jana kwamba maofisa hao wamesambazwa kwa ajili ya kukabiliana na kitisho cha aina yoyote. Kadhalika maeneo mengi nyeti, eneo lililojaa shughuli za kibiashara na Bunge yote yanalindwa.

Polisi wa kijeshi pia wamesambazwa maeneo ya Constitution Square ambako wameweka mahema sawa na bungeni, eneo muhimu kwa ajili ya mjadala unaotarajiwa kuwasilishwa leo kuhusu kuondolewa ukomo wa umri.

Kusambazwa kwa wingi kwa askari hao kumefanyika katikati ya kampeni zinazofanywa na za vikundi vya kisiasa na sasi za kiraia kupinga marekebisho ya katiba yanayolenga kufuta ukomo wa umri wa rais wa miaka 75. Hoja ya marekebisho hayo ilitarajiwa kuwasilishwa leo baada ya
kushindikana

Mwakyembe Ataka Tiketi Zenye Kuonyesha Namba ya Siti Uwanja wa Taifa

$
0
0
Mwakyembe Ataka Tiketi Zenye Kuonyesha Namba ya Siti Uwanja wa Taifa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema anamtaka mkandarasi atakayeshughulikia uwanja wa taifa aweze kutoa tiketi zenye kuonesha namba siti ambayo mtu ataenda kukaa moja kwa moja na siyo masuala ya ubabaishaji.

Dkt. Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati alipoenda kutembelea uwanja wa mpira wa miguu wa Nangwanda uliopo Mkoani Mtwara na kusema anahitaji mabadiliko katika viwanja vyote vya michezo ili viweze kuwa bora zaidi na kufanana na viwanja vingine vilivyopo duniani.

"Namtegemea mkandarasi anayekuja katika uwanja wa Taifa, na hili nitaeleza mpaka mwisho atuletee mabadiliko ambayo tunayataka na nitasisitizia hilo. Atakayetoa tiketi kwa namba za viti, siyo holela watu wanakaa sehemu za kutembelea kwa miguu. Maana sasa huelewi wameingia watu wangapi ?, ni lini Watanzania tutaweza kutendea haki hata viwanja vyetu vya kisasa. Kiwanja kipya kitakachokuja baada ya ukarabati, kitakachotokea pale ", amesema Dkt. Mwakyembe.
Mtazame hapa chini Dkt. Mwakyembe akiongelea zaidi kuhusu viwanja vya kimichezo vilivyopo chini Tanzania.



Mrithi wa Kocha wa Mbeya City Apatikana

$
0
0
Mrithi wa Kocha wa Mbeya City Apatikana
Baada ya kuachana na kocha wake raia wa Malawi Kinah Phiri hatimaye klabu ya Mbeya City leo imepata mrithi wa kiti hicho cha benchi la ufundi.

Mbeya City imefikia makubaliano na kocha Nsanzurwimo Ramadhani kuwa kocha Mkuu kwa mkataba wa msimu mmoja wa ligi ambao una kipengele cha kuongezwa endapo atafanya vizuri.
Msemaji wa Mbeya City Shah Mjanja amethibitisha hilo na tayari kocha huyo ambaye ni raia wa Burundi yupo nchini na mchana huu anatarajiwa kusafiri kuelekea Mwanza tayari kwa kujiunga na timu ambayo ipo mjini Shinyanga kwaajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui.

“Ni kweli timu yetu imepata kocha mpya ambaye amesaini mkataba wa awali wa mwaka mmoja na ataongezewa endapo atafikia malengo ambayo yapo kwenye mkataba, tayari yupo nchini na anasafiri na ndege ya mchana kwenda kanda ya ziwa kujiunga na timu”, amesema Mjanja.
Kocha Ramadhani amewahi kuwa kocha kwa nyakati tofauti katika vilabu mbalimbali kwenye nchi za Burundi, Rwanda, Botswana, Malawi, Uganda, na Afrika ya Kusini

Maalim Seif Amtembelea Tundu Lissu Hospitali

$
0
0
Maalim Seif Amtembelea Tundu  Lissu Hospitali
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad leo Septemba 26, 2017 ameingia jijini Nairobi Kenya kwenda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi.

Mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro amethibitisha hilo na kusema kuwa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa CUF wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya kwenda kumuona Tundu Lissu.
"Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad ameingia jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mhe. Tundu Antipas Lisu (leo) ambaye amelazwa Hospitali ya Nairobi" alisema Julius Mtatiro
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na kisha baadaye kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu zaidi.

Wilaya ya Temeke, Ilala Kinara wa Unyanyasaji wa Kijinsia

$
0
0
Wilaya ya Temeke, Ilala Kinara wa Unyanyasaji wa Kijinsia
Wilaya za Temeke na Ilala zimetajwa kuwa na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, ndoa za utotoni na kukithiri kwa vitendo vya ukeketaji, huku Kata ya Kitunda wilayani Ilala ikiongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha matukio yaliyoripotiwa.

Akizungumza leo Jumanne kwenye mkutano wa mrejesho wa mradi wa kuhamasisha jamii kutokomeza ndoa za utotoni, ukeketaji na mimba za utotoni, Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF), Koshuma Mtengeti amesema mradi huo ulilenga kuelimisha jamii juu ya madhara ya vitendo hivyo.

"Vitendo hivi vingi vimekuwa vikiripotiwa zaidi wilaya za Temeke na Ilala kwa mkoa wetu wa Dar es Salaam, hivyo CDF tukaamua kupeleka mradi wetu Kitunda ambako namba ya waathirika ulikuwa kubwa zaidi," amesema Mtengeti.Mkurugenzi Mtendaji wa CDF, Koshuma Mtengeti

Mkurugenzi Mtendaji wa CDF, Koshuma Mtengeti akizungumza katika mkutano wa mrejesho wa mradi wa kuhamasisha jamii kutokomeza ndoa za utotoni, ukeketaji na mimba za utotoni. Picha na Herieth Makwetta.

Amesema lengo ulikuwa kuondoa mila potofu kama ukeketaji pamoja na kutafuta ufumbuzi kwa pamoja wa jinsi gani jamii itashiriki katika kuwalinda watoto wa kike na kuhakikisha jamii inakuwa mstari wa mbele katika kutokomeza vitendo hivyo.

"Vitendo hivi vinawaathiri watoto wa kike hivyo tulilenga kuhakikisha kwamba  wanatambua haki zao na kuzitetea."

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Watoto na Ustawi wa Jamii Ilala, Joyce Maketa amesema jukumu la kumlinda mtoto ni la mzazi, mwalimu na mlezi na si mtu mwingine.

Ametoa rai kwa jamii kabla kumhukumu mtoto kuangalia mzizi wa tatizo.

Mahakama Yaamuru Adhabu ya Kifo Kwa Watu Sita wa Familia Moja

$
0
0
Mahakama Yaamuru Adhabu ya Kifo Kwa Watu Sita wa Familia Moja
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa imewahukumu adhabu ya kifo watu sita ambao ni ndugu wakazi wa Kalambo baada ya kupatikana hatia ya kumuua ndugu yao.

Ndugu hao wamedaiwa kwamba walifikia uamuzi wa kumuua ndugu yao huyo kwa madai ya kwamba anajihusisha vitendo vya kishirikiana.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne na Jaji Mahakama hiyo, Dk Adam Mambi baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliopeleka mashahidi sita ili kuthibitisha mashitaka hayo.

Waliokutwa na hatia katika shauri hilo ni Ferdinand Kamande, Peter Mpandisharo, Edes Kamande, Stephen Sikanda, Henrick Nguvumali na Anatory Kamande huku Alistid Kamande na Will broad Kamande wakiachiwa huru kwa kutokutwa na hatia.

Katika shauri hilo upande wa mashitaka uliongozwa na mawakili wa serikali ambao ni Scolastica Lugongo na Adolf Lema huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Mathias Budodi, ambapo ilidaiwa kwamba washitakiwa walitenda kosa hilo Septemba 27, mwaka 2014.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa siku ya tukio nyakati za usiku washitakiwa wakiwa na silaha za jadi kama vile mapanga, nondo, mawe, majembe walivamia nyumba ya Kamande na kugonga dirisha kisha kuvunja mlango ambapo Kamande alikimbia kuelekea kusikojulikana.

Ilielezwa kwamba baada ya hapo waliichoma moto nyumba hiyo na kuteketeza kila kitu kilichokuwemo ndani kisha kuondoka zao.

Wakati nyumba hiyo ikiteketea kwa moto Kamande aliyekuwa amekimbia ili kunusuru maisha yake, alikamatwa na watu hao na kuanza kupigwa huku wakimtuhumu kuwa ni mchawi na baada ya kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake walimchoma moto na kufariki papo hapo.

Ilidaiwa kwamba  washitakiwa hao walikamatwa na polisi Oktoba 10, 2014 na baada ya kuhojiwa na polisi walikana shitaka hilo.

Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mawakili wa Serikali waliiomba mahakama kutoa adhabu kali iwe fundisho kwani watu wamekuwa wakichukulia sheria mkononi na kuua watu kinyume cha sheria wakiwatuhumu kuwa ni washirikina.

Akitoa adhabu hiyo Jaji wa Mahakama hiyo, Dk Mambi amesema ameridhishwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka hivyo kwa kutumia Kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai Namba 196 Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2002 anawahukumu watu hao sita kifo kwa kunyongwa.

Mo Dewji Ajutia Kuchelewa Kuwekeza Katika Mambo Haya Mawili

$
0
0
Mo Dewji Ajutia Kuchelewa Kuwekeza Katika Mambo Haya Mawili
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji ametaja mambo mawili ambayo anayajutia kwa kutoyafanya na anahisi kuwa amechelewa kuyafanyia maamuzi.

Dewji ambaye kwa mujibu wa jarida la Forbes anashika nafasi ya 21 kwa watu matajiri Afrika amesema kuwa kushindwa kuwekeza katika benki na mawasiliano ya simu ni mambo ambayo yanamuumiza kichwa akiendelea kuyajutia.

Mfanyabiashara huyo ametuma sehemu ya mahojiano kwenye mtandao wake wa Twitter akielezea mambo hayo.

Akijibu swali lililotaka atoe ushauri wake nini ambacho hajakifanya Dewji alianza kwa kusema, “Nimekosa mambo mengi katika maeneo ambayo nilipaswa kuwekeza...nilipaswa nimewekeza katika benki. Ingawa sasa najaribu kununua benki lakini nadhani nimechelewa. Na jambo la pili ambako nimekosea ni kwa kushindwa kuwekeza katika biashara ya mawasiliano ya simu.”

Amesema hakuwa na mwamko wa kujiingiza katika uwekezaji wa mtandao wa mawasiliano ya simu kwa vile alihisi wananchi wengi walikuwa hawana uwezo kumudu kununua simu na kuwasiliana.

“Unajua nilikuwa nikifikiri kuwa hivi watu hawa watapata wapi fedha kununua simu lakini sasa ukiangalia kama Tanzania kila mtu anamiliki simu ya mkononi...Haya ndiyo mambo mawili ambayo nayajutia,” amesema mfanyabiashara huyo.

Miongoni mwa wafanyabiashara waliopata mafanikio makubwa kutokana na kuwekeza katika mtandao wa mawasiliano ya simu ni Mo Ibrahim raia wa Uingereza ambaye jarida la Forbes limemtaja kuwa ni mtu 692 kwa watu matajiri duniani.

Mfanyabiashara huyo mwenye asili ya Sudan sasa anasimamia taasisi yake ijulikanayo Mo Ibrahim Foundation ambayo inahimiza dhana ya utawala bora barani Afrika.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images