Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Nyarandu Azidi Kuokoa Uhai wa Watu Afanikisha Safari ya Mgonjwa

$
0
0
Nyarandu Azidi Kuokoa Uhai wa Watu Afanikisha Safari ya Mgonjwa
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM) mchana wa leo Septemba 26, 2017 amefanikisha safari ya mgonjwa Bw. Samson Mwanga mkazi wa kijiji cha Mipilo Singida Kaskazini anayeishi Manyara ambaye amepasuka mishipa kichwani na kuwaishwa KCMC.

Lazaro Nyalandu amesema kuwa ndege iliyotumika kumbeba mgonjwa huo imetoka nchini Kenya hivyo amewashukuru madaktari na wafanyakazi wa hospitali ya Rufaa ya Hydom kwa utumishi wao kumuhudumia mgonjwa huo wakati wakisubiri mgonjwa huyo kusafirishwa kwa matibabu zaidi ili kuokoa maisha yake. 
"Nimewasili uwanja wa ndege wa Hospitali ya Hyadom kwa ajili ya dharura ya kumsafirisha mgonjwa, Bw. Samson Mwanga, mkazi wa kijiji cha Mipilo, Singida Kaskazini, aishiye kijiji cha Gidika (Manyara) aliyepatwa na kupasuka mshipa kichwani na kusababisha kuhitaji kile madaktari walichokiita 'Immunogloblin Injections" ili kunusuru maisha yake. Tumempandisha ndege ya Shirika la "Flying Medical Doctors", iliyotokea Nairobi na kuwasili hapa Hydom mchana huu." alisema Nyalandu 
Mbunge huyo aliendelea kuwashukuru madaktari hao 
"Nawashukuru madaktari na wanafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Hydom kwa utumishi wao uliotukuka, na kwa kumhudumia mgonjwa Samson Mwanga hadi tukaweza kumpandisha ndege kwenda Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Kilimanjaro mchana huu" alisema Nyalandu 
Hii ni mara ya tatu kwa Mbunge huyu kufanikisha safari za wagonjwa kwenda kwenye matibabu mbalimbali alianza kwa kufanikisha safari ya watoto watatu walionusurika kwenye ajali ya gari ya shule ya Lucky Vicent jijini Arusha, akafanikisha kuwapeleka watoto wawili hospitali waliovunjika miguu kwenye ajali ya gari ya mizigo la mnadani na sasa amefanikisha safari ya mgonjwa huyu Samson. 

Video: Vodacom Wazindua Pindua Pindua kwa Wateja Wake

$
0
0
Mtandao wa Simu ya Mkononi vodacom wamezindua huduma ya kifurushi kipya cha pinduapindua kwa facebook, dakika, sms bure

Pinduapindua ni kifurushi huru na cha kipekee zaidi kuliko vifurushi vingine vinavyowapangia wateja wa kampuni zingine za mawasiliano nchini,Bando hili litawapatia vijana na wateja uhuru wao wa kuchagua kiasi cha kupangia kwenye data, kupiga simu (voice) au ujumbe mfupi (SMS) kulingana na mahitaji ya wakati huo. “Pinduapindua” pia itamwezesha mteja kutumia Facebook (ikiwa pamoja na picha), Whatsapp (maandishi na picha) na SMS hadi 200 bure.


Jinsi yakupata vifurushi vya bando hili ni rahisi mteja atahitaji kupiga namba *149*01# kisha kuchagua kifurushi cha siku, cha wiki au cha mwezi. Vifurushi hivi vinaweza kulipiwa kupitia muda wa maongezi au Mpesa na mara baada ya kununua, mteja atapatiwa kifurushi chake, Facebook BURE, Whatsapp BURE na SMS, vyote ambavyo vitatumika kwa muda wote wa kifurushi alichochagua

Petit man Atetea Ndoa Yake Azikana Picha Zake na Mobetto Zinazosambaa Mitandaoni

$
0
0

Petit man  Atetea Ndoa Yake Azikana Picha Zake na Mobetto Zinazosambaa Mitandaoni
SIKU chache baada ya baba mzazi wa mtoto wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto, kujitokeza hadharani na kukiri mtoto ni wake, ghafla, katika hali ya kushangaza zikasambaa picha mitandaoni zikimuonyesha mwanamitindo huyo akiwa katika pozi za mahaba na mdau wa muziki, Petitman Wakuache. Baada ya kuziona picha hizo Petit ameibuka na kutoa kauli nzito.

PETITMAN ANENA!
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Petit alipost picha akiwa na mke wake Esma ambaye ni wifi yake Mobeto, kwa sababu anazaliwa mama mmoja na baba mtoto wake. Na kuandika ujumbe ufuatao:


NENO LA MWANDISHI
Kila binadamu ana jana yake, leo na kesho ambayo ni fumbo, kwa sababu ameshasema kwamba picha hizo ni jana yake, ambayo haiuhusiani kabisa na leo yake. Basi ni vyema hao wanaohusika na usambazaji wa picha hizo, mkasitisha zoezi hilo, kwani Petit ni mume na baba wa familia kwa sasa.

Mobeto naye ana maisha yake mengine kabisa, kwa hiyo kuvujisha picha hizo kunaweza kusababisha migogoro katika familia hizi mbili ambazo zina uhusiano wa karibu.


BREAKING NEWS:Basi la abiria Lateketea kwa moto

$
0
0
BREAKING NEWS:Basi la abiria Lateketea kwa moto
Basi aina ya Yutong iliyokuwa ikitoka Tanga mjini kuelekea Dar es salaam, limeungua moto maeneo ya Pongwe karibu na mizani majira ya saa 8: 30 mchana wa leo.

Kwamujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Benedict Michael Wakuyamba amesema basi hilo lenye namba za usajili T T361 DCF limewaka moto katika eneo la Pongwe jiji Tanga, na hakuna madhara yoyote kwa binadamu zaidi ni hasara ya mizigo ilikuwa imewekwa kwenye buti.

Basi hilo liliokuwa likiendeshwa na dereva  Hemedi Ali (35) mkazi wa Tanga lilikuwa likitokea Tanga kuelekea jijini Dar es salaam likiwa limebeba abiria 29 lilipofika eneo hilo liliwaka moto

 Kamanda Benedict amesema kwamujibu maelezo ya awali ya Dereva huyo anadai alianza kuhisi paipu ya gari inawaka  na ndipo aliposimamisha gari hilo, Mpaka sasa Jeshi hilo bado linaendelea kumuhoji dereva huyo.


Wolper Atoa Somo Kuhusu Watu Wenye Lengo la Kumshusha Mtu Kimaendeleo

$
0
0
Wolper Atoa Somo Kuhusu Watu Wenye Lengo la Kumshusha Mtu Kimaendeleo
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameanza kuwa mshauri wa mambo kadhaa katika maisha ya kila siku.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, mrembo huyo ametoa ushauri juu ya baadhi ya binadamu wanaotaka kumshusha mtu kimaendeleo na kutaka kumkwamisha pindi wakimuona na furaha.

"Basi leo nataka niwaambie kitu hakuna binadamu anaependa hivyo ww ulivyo na ndio maana unakuta wanazua mambo mengi ili wajaribu kukufanya ujione mdhaifu,Binadam bwana wanaweza wakatafuta tatizo pasipo kuwa na tatizo!Wakiona mtu yupo happy anajitafutia,anafanya yanayo muhusu wanaona hilo ni kosa na mbaya zaidi wakigundua una furaha wanajaribu kukufanya uwe down,Ingawa sio wote lkn wapo hawa watu na wengine tupo nao majumbani mwetu tunaishi nao..Unakuta mtu unafanya kitu kizuuuri lkn haupongezwi kwa lolote mbaya zaidi wanakiponda ili ujikatie tamaa na hiyo yote kwasababu wao hawana basi wanataka ww uwe km wao…Sasa niwashauri ndugu zangu tusiwe watu wakuchulia kitu km kilivyo kuna wengine wanataka kukuona tu umeshindwa hiyo ndo furaha yao wao,fanya mwenyewe,amua mwenyewe na pia jipongeze mwenyewe ikiwezekana nyamaza kabisa wasijue yako ila wape nafasi ya kuona mafanikio yako..Usikubali kumpa mtu mwingine nafasi zaidi ya ww unavyotakiwa kujipa..Jipe nafasi,Jipongeze na jiamini bila kujali mwingine anasema au atasema nn…Pambana na uwezo wako cha msingi usishindane nao…Amini unaweza kupitia wewe mwenyewe!

Kwa sasa mrembo huyo amejikita katika biashara ya mavazi na duka lake limekuwa likitengeneza nguo kwa kuzishona.

Kiongozi wa Upinzani Amekamatwa na Polisi

$
0
0
Kiongozi wa Upinzani Amekamatwa na Polisi
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dr. Kizza Besigye, amekamatwa na polisi nchini humo kufuatia sakata la baadhi ya wabunge na wananchi nchini humo kupinga suala la ukomo wa urais.

Dr. Besigye amekamatwa leo mchana katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala, ambako alikuwa amekwenda kuhamasisha wafuasi wake dhidi ya kuondolewa kwa Ibara ya 102 (b) ya katiba ya nchi hiyo, ambayo inaweka kikomo cha umri wa urais akiwa na umri wa miaka 75.
Wakati wa tukio hilo Dr. Besigye alikataa kushuka kwenye gari yake alipoamrishwa na polisi, na kuwalazimu polisi hao kuliburuza gari hilo hadi kituo cha polisi na kulipaki, huku Kizza Besigye akiwa ndani ya gari.
Mbali na Dr. Besigye  Mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Fred Mukasa naye amekamatwa na polisi kufuata tukio hilo.

Hukumu ya Kesi ya Dawa za Kulevya ya Mfanyabiashara Yusuph Manji Octoba 6

$
0
0
Hukumu ya Kesi ya Dawa za Kulevya ya Mfanyabiashara Yusuph Manji Octoba 6
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu kesi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji, October 6, 2017 baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wake wa mashahidi saba.

Hatua hiyo inatokana na Wakili wa Manji, Hajra Mungula kumueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwamba wamefunga ushahidi wao wa mashahidi saba ambapo baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha amesema kutokana na kufungwa ushahidi huo anatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo, October 6, 2017.

Awali, Manji kupitia Wakili wake Mungula, aliiambia Mahakama hiyo kwamba angekuwa na mashahidi 15 lakini hadi leo September 26, 2017 ni mashahidi saba tu waliotoa ushahidi wao.

Katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya February 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Lulu Diva Akanusha Kujichubua Afunguka Mboga Mboga Zinavyo Badirisha Ngozi Yake

$
0
0
Lulu Diva Akanusha Kujichubua Afunguka Mboga Mboga Zinavyo Badirisha Ngozi Yake
Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma ya 'Give it to me', Lulu Diva amekanusha zile tuhuma za yeye kujichubua ngozi yake na kudai kinachofanya aonekane kuwa mweupe ni kutokana na kula mboga za majani na matunda kwa sana.

Lulu Diva ameeleza hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo kutoka East Africa Radio baada ya watu wengi kuanza kumuoneshea vidole kuwa anajipiga kitaulo (anajichubua) kwa maana rangi yake ya awali haikuwa hivyo.
"Unajua kwamba msanii unatakiwa uanze kujitengeneza mwenyewe kuanzia mwili wako, ngozi pamoja na vitu unavyokula. Naweza sema nakula sana mboga mboga na matunda, kuna baadhi ya vyakula vinasaidia hata kung'arisha ngozi", amesema Lulu Diva.


Shahidi: Namfahamu Manji kwa Miaka 19 Sasa Nashangaa Kusikia Anatumia Dawa za Kulevya

$
0
0
Shahidi: Namfahamu Manji kwa Miaka 19 Sasa Nashangaa Kusikia Anatumia Dawa za Kulevya
Jumanne, September 26, 2017 Kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Mfanyabiashara Yusuf Manji imeendelea kwa siku ya pili kati ya tatu za kusikiliza ushahidi mfululizo ambapo leo umetolewa ushahidi wa mashahidi watatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika kesi hiyo, shahidi wa tano, Maria Rugalabumu (63) amemueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa yeye ni Sektretari wa Manji (Katibu Muktasi) na Ofisi ya Quality Group Ltd.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi Hajra Mungula, amedai kuwa anafanya kazi katika kampuni hiyo tangu mwaka 1994 hadi sasa, wakati huo Manji akiwa anasoma.

Alipoulizwa na Wakili Mungula kwamba anamfahamu vipi Manji, amesema anamfahamu tangu anasoma na kwenye masuala ya kazi anamfahamu tangu 1997 baada ya kurithi mikoba ya baba yake.

Pia alipoulizwa kama kuna vitu vya Manji huwa anavitunza, akajibu ndio ambapo miongoni mwa vitu anavyomtunzia ni Sigara.

Aidha, amedai kuwa anashangazwa kusikia kuwa Manji anatumia dawa za kulevya hali ya kuwa amemfahamu takribani miaka 19 akisema kuwa majukumu yake ni uangalizi wa ofisi yake na ya Manji, pia kuchapa barua, kupokea wageni na kutuma barua zinazotoka ofisi yao na kusema kuwa Manji ni mchapakazi na anaweza kufanya kazi kwa muda mrefu na huwa anapenda kazi zake.

Shahidi huyo, amedai kuwa amemfahamu tangu Manji anasoma Chuo, pia alivyoanza kufanya kazi kwa Baba yake na kuieleza Mahakama kwamba yeye ndiye aliyetoa kopi ya nakala ya dawa za Manji kutoka kwa Dokta wake Marekani.

Nakala hiyo aliipata kwa njia ya e-mail, ambapo baada ya kuitoa nakala alimpatia askari ili ampe Manji ambaye alilazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, hivyo anaomba Mahakama ipokee kama sehemu ya kielelezo.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis alipinga kupokelewa kwa barua hiyo kwa sababu haina uthibitisho wa kiuhalisia na daktari aliyeituma.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Mkeha alitoa uamuzi ambapo alikubaliana na Wakili Vitalis, ambapo alisema Mahakama haiwezi kupokea kielelezo hicho.

Kadinda: Napata Wakati Mgumu Kumsimamia Wema Kutokanana na Tabia Zake

$
0
0
Kadinda: Napata Wakati Mgumu Kumsimamia Wema Kutokanana na Tabia Zake
Mbunifu wa mavazi maarufu hapa bongo Martin Kadinda ambaye pia ni meneja wa msanii Wema Sepetu, amesema anapata wakati mgumu kumsimamia msanii huyo mkubwa na mrembo, kutokana na tabia zake zisizobadilika, ikiwemo kutokuwa kimawazo.

Martin Kadinda ameyasema hayo alipokuwa akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba licha ya Wema Sepetu kuwa mtu muhimu kwenye maisha na kazi zake, amekuwa mtu ambaye habadiliki, hivyo inamuwia vigumu kumtengenezea mazingira mazuri ya kazi zake na kesho yake.

'Changamoto kubwa kwake unajua Wema ni mtoto hakui, yani miaka inakwenda bado yuko vile vile, kikubwa ni kuweza kumtengenezea mazingira ili kesho na kesho kutwa aweze kuheshimika”, amesema Martin Kadinda.

Martin ameendelea kwa kusema kwamba ...”Wema ana maisha yake binafsi, ana vitu vyake anavyovipenda kwa hiyo ninachokifanya zaidi ni kuweza dhibiti mambo yake binafsi yasimfanye kesho na kesho kutwa kushindwa kupata ugali wake wa kila siku”.
Kwa sasa Martin Kadinda amesimama kumsimamia msanii huyo kutokana na kubanwa na masomo, huku akisema kwake atabaki kuwa msimamizi wa msanii huyo pale panapohitajika mchango wake.



Polisi Watumia Mabomu Kuwatawanya Waandamanaji Nchini Kenya

$
0
0
Polisi Watumia Mabomu Kuwatawanya Waandamanaji Nchini Kenya
Polisi wamelazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi wa vyama vya Jubilee na muungano wa upinzani wa Nasa baada ya kuzua vurugu katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) zilizoko jengo la Anniversary Towers.

Wafuasi wa Nasa waliokuwa wakiimba nyimbo “Chiloba lazima ang’oke” walikabiliwa na wafuasi wa Jubilee waliokuwa wakiimba “Tunataka amani”. Makundi yote mawili yalitimua mbio baada ya polisi wa kuzuia ghasia kuwarushia mabomu ya kutoa machozi.

Huku wakikohoa na wakitafuta mahali salama, wote walikimbia kukwepa kukamatwa.

Maandamano hayo yamefanyika kuitikia wito uliotolewa jana na kiongozi mkuu wa Nasa Raila Odinga kwamba wafuasi wake wajitokeze kwa wingi kuandamana hadi kwenye makao makuu ya IEBC lengo likiwa kumtoa kwa nguvu Ofisa Mtendaji Mkuu wa IEBC Ezra Chiloba kwa madai ya kuhusika kuvuruga uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 8.

Maandamano hayo yanafanyika siku chache baada ya Mahakama ya Juu kufuta ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Katika mji wa Kisumu, ambao unatajwa kuwa moja ya ngome za Nasa baadhi ya wakazi waliandamana hadi ofisi za IEBC na baada ya kufika walitoa wito maofisa wa ngazi za juu akiwemo Ezra Chiloba wajiuzulu.

Walimshutumu Chiloba na kikundi chake kwa kufanya njama za kuingilia mchakato wa uchaguzi mkuu ambao matokeo yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta yalifutwa na Mahakama ya Juu.

Waandamanao waliokuwa wamebeba matawi ya miti, mabango huku wakipiga yowe na honi za pikipiki walianzia barabara ya Obote wakaenda mtaa wa Oginga Odinga kabla ya kuchukua Barabara Kuu ya Kenyatta na baadaye Mtaa wa Ang’awa katikati ya jiji.

Kigwangala Ameiagiza TAKUKURU Waliochakachua Fedha za Zahanati

$
0
0
Kigwangala Ameiagiza TAKUKURU Waliochakachua Fedha za Zahanati
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwakamata watu wote waliohusika kuchakachua fedha za ujenzi wa jengo la Zahanati ya Neruma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara yake ya kuimalisha sekta ya afya wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo aliweza kukagua jengo  jengo la Zahanati ya Neruma,iliyopo Kata ya Neruma Wilayani Bunda, Mkoani Mara na kubaini milioni 29 fedha za ujenzi zikiwa zimechakachuliwa.

Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Isaack Mahela alimweleza Naibu Waziri kuwa, ujenzi wa jengo hilo umegharimu jumla ya milioni 29 kwa ajili ya kupanua na kuweka fremu za milango pamoja na madirisha, kitu ambacho kimeonekana hakiendani na uhalisia wa fedha hizo.
"Nakuagiza Mkurugenzi, uhakikishe unawasilisha nyaraka zote za fedha za jengo hili kwa TAKUKURU na wale wote waliohusika kupitisha fedha hizo na uwakabidhi TAKUKURU ili wafanye uchunguzi na kuchukua hatua zichukuliwe", amesema Dkt. Kigwangalla.
Dk. Kigwangalla amesema kuwa taifa linataka kusonga mbele hivyo watu wanaokwamisha mchakato wa Rais wa kuwaletea maendeleo wananchi wake lazima wachukuliwe hatua ili watu wengine waogope kutafuna fedha za umma.
Jengo hilo ambalo pia limeonekana kuwa chini ya kiwango katika maeneo kuta zake, mchakato wa ujenzi wa jengo ulianza tokea  mwaka 2015 kwa nguvu za wananchi na baadae Halmashauri ilitenga fedha za kumalizia mchakato kiasi cha milioni 29, ambazo zimebainika kutafunwa na watendaji waliokuwa wanashughulikia zoezi hilo.

JE Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo, Kufika Kileleni Haraka na Kushindwa Kurudia Tendo?

$
0
0
JE, UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO, KUFIKA KILELENI HARAKA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO AU MAUMBILE MADOGO YA UUME? Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume husababishwa na mambo mengi kama KISUKARI, UNENE ULIOPITILIZA, KUJICHUA (MASTER BLASHION), HOMONI kushindwa kufanya kazi ipasavyo n.k. Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa ☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni ☆Uume kusinyaa katikati ya tendo ☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa. Kwa kutumia mimea na matunda @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250000@250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6 hadi 7 @150000@150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200000@200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150000@150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130000@130,000/= BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA ZIMETHIBITISHWA KIAFYA. KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI

TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :@markson_beauty_pr

Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa (+255) 0767447444 na 0714335378

 UTAPATA HUDUMA NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. < WELCOME ALL>

Rais Mugabe Amchimba Mkwara Trump ‘Hakuna Taifa Dogo Kijeshi’

$
0
0
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemuonya Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa asijidanye kwa ulimwengu huu wa teknolojia kwamba Marekani itakuwa ndio nchi yenye nguvu pekee duniani ya kutengeneza silaha nzito za kivita.

Mugabe ameongea hayo Jumatano ya wiki iliyopita baada ya kurejea nchini Zimbabwe akitokea Marekani kwenye mkutano wa umoja wa Mataifa ambako Rais Trump alitamka kuwa endapo atapata ruhusa ya kuishambulia Korea Kaskazini basi ataiangamiza kwa muda mfupi.

Mugabe amesema kwa sasa kila nchi inauwezo wa kumiliki silaha za nyuklia na sio kwa nchi kubwa hiyo dhana imekufa huku akihimiza kila taifa lijitegemee kiutawala pasi kuingiliana.
Hakuna nchi inayoruhusiwa kuipelekesha nchi nyingine kwenye masuala ya kijeshi nadhani kila nchi ijitegemee, kila nchi ina nguvu yake hakuna taifa dogo kijeshi, kwa hiyo ningependa kumuonya (Trump) awe makini,“amesema Rais Mugabe kwenye mahojiano yake na gazeti la kiserikali la  Herald newspaper wakati akihutubia wanachama wa Chama tawala cha Zanu-PF waliojitokeza kumpokea.

VIDEO:

Joshua Nassari Amjibu Polepole..'Nikitoka Nairobi Nitaweka Hadharani Ushahidi'

$
0
0
Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nassari amefunguka kwa kumjibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole kwamba amemsikia alichokizungumza na kuahidi akirudi Tanzania ataweka ukweli wote hadharani.

Nassari amebainisha kupitia ukurasa wake maalum wa facebook jioni ya leo baada ya kusikia kauli kutoka kwa Humphrey Polepole ikidai kama kweli viongozi wa upinzani wanaushahidi wa rushwa ama kununuliwa madiwani waliohamia CCM wakitokea CHADEMA basi wanapaswa kuweka hadharani kwa kutaja hata majina ya wahusika na sio kulingishia.

"Nimemsikia ndugu Polepole. Nipo Nairobi, nikirejea tu nyumbani Tanzania nitaweka hadharani ushahidi huu, usiokuwa hata na chembe moja ya shaka. Ili tuone kama kweli CCM itachukua hatua kwa wateule wa rais", ameandika Nassari.

Hayo yote yamekuja baada ya kupita takribani siku mbili tokea mbunge Joshua Nassari kudai ana ushahidi usiotia shaka juu ya madiwani ambao wamepokelewa na Rais Magufuli wakati alipokuwa katika ziara yake mkoani Arusha kuwa wamenunuliwa na kupewa rushwa na siyo kwamba wamehama kwa lengo la kukubali kazi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano.


Maalim Seif Amtembelea Tundu Lissu Nairobi Kenya

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad leo Septemba 26, 2017 ameingia jijini Nairobi Kenya kwenda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi.

Mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro amethibitisha hilo na kusema kuwa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa CUF wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya kwenda kumuona Tundu Lissu.

"Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad ameingia jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mhe. Tundu Antipas Lisu (leo) ambaye amelazwa Hospitali ya Nairobi" alisema Julius Mtatiro

Mhe. Shariff Hamad ameongozana na Mhe. Juma Duni Haji Nairobi kumjulia hali, Mhe Tundu Lissu.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na kisha baadaye kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu zaidi.

Nape Nnauye Amuwakia Aliyemuuliza Juu ya Posti yake ya Bombadier

$
0
0
Mbunge wa Mtama ameseikia akimuwakia mtu aliyekuwa akimuuliza juu ya tweet yake aliyoituma juu ya wananchi jimboni kwake kutojua nini maana ya Bombadier

Jamaa huyo alionekana kama anamshtumu Nape kuwa ameigeuka serikali aliyokuwa akiunga mkono na Nape aakasikika akimtukana mpu****

Msikilize:



Wema Sepetu Anaswa Akijibebisha Kwa Kidume Kipya

$
0
0
MALKIA wa Filamu za Bongo, Wema Sepetu amenaswa LIVE akiwa na mwanamme anayedaiwa kuwa ni bwana wake mpya. Wawili hao wamenaswa wakijiachia tena mchana kweupe peee huku Wema akijibebisha kwenye kifua cha jamaa huyo!

Anasikika Wema akitema madongo kumponda mpenzi wake wa zamani ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, kwamba alishamshauri aiboreshe perfume hiyo kama anataka iwe na viwango lakini mwenyewe akamwambia kwamba anataka aiuze kwa watu wa daraja la chini na kati.

Yanga, Singida United Kuzindua Uwanja

$
0
0
Yanga, Singida United Kuzindua Uwanja
Mechi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC dhidi ya Singida United itakayochezwa Novemba 4 mwaka huu katika mzunguko wa tisa wa michuano ya ligi kuu ndiyo itakayozindua rasmi uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Uwanja huo ambao umefungwa kwa muda ili kupisha matengenezo yaendelee, na utakapofunguliwa utatumika kama dimba la nyumbani kwa timu ya Singida United ambayo kwa sasa inatumia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma katika michuano inayoendelea ya ligi licha ya makazi yake kuwa mkoani Singida.

Akizungumza Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mdau mkubwa katika matengenezo hayo, amewahakikishia wapenzi wa kandanda mkoani humo kuwa uwanja huo utakuwa tayari kabla ya Novemba 4, 2017 na kuwataka wakazi wa Singida kujiandaa kuishangilia timu yao.

Kwa mujibu wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Singida United imeweza kushika nafasi ya tatu kwa alama tisa ikiwa mbele kwa alama moja dhidi ya Yanga SC ambayo imeshika nafasi ya sita kwa pointi nane.

Lema, Nassari Kusubiriwa na Takukuru Juu ya Tuhuma za Rushwa

$
0
0
 Lema, Nassari Mikononi mwa Takukuru Juu ya Tuhuma za Rushwa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakaribisha wabunge wawili wa Chadema, Joshua Nassari na Godbless Lema katika ofisi hizo ili wakabidhi taarifa na ushahidi wa tuhuma za rushwa dhidi ya madiwani waliojiuzulu katika majimbo yao.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola ametoa wito huo alipoulizwa na gazeti hili kuhusu tuhuma za rushwa zilizotolewa na wabunge hao.

Jumamosi iliyopita, Diwani wa Kimandolu (Chadema), Mchungaji Rayson Ngowi alitangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa tukio la Rais Magufuli kutunuku kamisheni kwa maofisa 422 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), jijini Arusha.

Katika tukio hilo, Rais Magufuli aliuliza kama kuna mwanachama yeyote anayetaka kujiunga na chama hicho au kukihama, ajitokeze mbele na ndipo diwani huyo alijitokeza na kutangaza rasmi kujiunga na CCM kwa maelezo ya kuvutiwa na utendaji wa Serikali.

Hata hivyo, baada ya tukio hilo, Nassari ambaye ni Mbunge wa Chadema wa Arumeru Mashariki, alizungumza na waandishi akiwaeleza kwamba ana ushahidi wa kielektroniki unaoonyesha madiwani hao walivyopewa rushwa ili wajiuzulu nafasi zao.

Alipoulizwa kuhusu hilo, Mlowola alisema, “Bado hawajatuletea ushahidi wowote lakini tunasubiri watuletee, hakuna shida maadam wamesema hivyo, tunawakaribisha.”

Wakizungumzia uamuzi wa Mlowola kuwasubiri wabunge hao badala ya kuwafuata baadhi ya wachambuzi wamesema ni uamuzi sawa lakini hawaamini kama Takukuru wangependa Rais Magufuli achafuliwe.

Profesa George Shumbusho kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema haoni tatizo lolote kwa wabunge hao kuwasilisha ushahidi walionao kwa Takukuru.

“Sioni shida wakipeleka kama wanao kweli, halafu wao Takukuru ndiyo wataupima ushahidi huo, wakikabidhi Takukuru ndiyo wanaweza kusema hadharani sasa,”

“Nadhani hawajawafuata pengine wanaamini ni tuhuma za kisiasa tu,” alisema.

Profesa Shumbusho alisema tuhuma hizo ni kubwa na anaamini Takukuru isingependa kuona Rais Magufuli akichafuliwa.

Kwa upande wake, mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Gemma Akilimali alisema hakuna haja ya Takukuru kuhangaika kuanza kazi ya uchunguzi wakati ushahidi umeshapatikana kwa wabunge hao.

Alisema ni vyema wakapeleka ili kurahisisha kazi kwa chombo hicho.

“Kama wangesema tuna wasiwasi wa kuwapo mazingira ya rushwa na wangeiomba Takukuru ichunguze lakini sasa wameshasema ushahidi wanao tayari, kwa hiyo wapeleke ili ionekane kama ni uongo au ni ushahidi wa ukweli,” alisema Gemma.

Siku ya tukio wakati Mchungaji Ngowi anapokelewa na Rais Magufuli alisema madai ya rushwa hayana ukweli wowote na kama Nassari ana ushahidi ni vyema angeutoa hadharani.

Ngowi aliwashauri Chadema mkoani Arusha watatue matatizo yaliyopo ndani ya chama hicho na wasitafute visingizio kwa kuwa yeye ameamua kujiuzulu kwa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na hajapewa rushwa yoyote.

Madiwani wengine waliojiuzulu chama hicho ni Credo Kifukwe wa Kata ya Murieti jijini Arusha, Anderson Sikawa (Leguruki), Emmanuel Mollel (Makiba), Greyson Isangya (Maroroni) na Josephine Mshiu (Viti Maalumu) Solomon Laizer (Ngabobo).

Mmoja kati ya hao waliojiengua, Credo Kifukwe alisema hakuna chochote alichopewa kama rushwa kwa lengo la kujiuzulu, akimshauri Nassari autoe hadharani ushahidi anaousema na si kushusha tuhuma zisizo na mashiko.

Katika ufafanuzi wake, Nassari aliyekuwa ameongozana na Lema alisema ushahidi huo ameuhifadhi ndani ya ‘flash disc’ na yuko tayari kumkabidhi Rais Magufuli na vyombo vya uchunguzi.

Mbunge huyo alisema endapo ikithibitika kuwa ushahidi wake ni wa uongo yuko tayari kujiuzulu nafasi yake ya ubunge.

“Ninao ushahidi na kama Mheshimiwa Rais yuko tayari niko tayari kumpatia ninayo flash, ushahidi ninao kwa muda mrefu na tulijua watapokelewa juzi madiwani wawili lakini mmoja amekataa akaenda mmoja,” alisema Nassari.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images