Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Ndugai Atoa Ufafanuzi wa Adhabu Anazozitoa Bungeni

$
0
0
Ndugai Atoa Ufafanuzi wa Adhabu Anazozitoa Bungeni
Spika wa Bunge la Tanzania, Mh. Job Ndugai  amefafanua kauli yake ya kuhusu adhabu ambazo huwa anazitoa bungeni ikiwepo kauli ya kutaka kumzuia Zitto kuzungumza bungeni na kusema hizo huwa ni adhabu za Spika kutokana na dharau ambazo zinaonyeshwa.

Akizungumza hivi karibuni na East Africa Radio Mh. Ndugai amesema kwamba ingawa huwa kuna adhabu ambazo hutolewa na kamati ya Maadili lakini yeye kama Spika huwa ana adhabu ambazo analazimika kuzitoa kwa kuwa ana mamlaka ndani ya bunge na ndiyo mwenye nafasi ya kutoa au kuzuia ruhusa wakati wa uchangiaji bungeni.

"Zipo adhabu za Kamati ya Maadili ambazo hutolewa lakini pia Spika ndani ya bunge anauwezo na mamlaka ya kutoa nafasi ya kuongea ndiyo maana hata wakati wa kuongea sentensi ya kwanza huwa wanasema Mh. Spika sasa anapotokea mtu ambaye anakudharau na anakutukana hadharani bila sababu kwa nini umpatie nafasi ya kuzungumza mtu huyo? amekuwa shangazi yako? Ni suala la kuheshimiana tu. Kama humuheshimu mtu kwa nini wewe uheshimiwe? Ndugai

Spika Ndugai ameongeza kwamba  " Mara nyingi Wabunge ambao huwa wanaofanya vitendo hivyo ni wale ambao wameshaingia bungeni hata mara ya nne lakini utamkuta anamdhalilisha Spika bila sababu na hata akipelekwa kwenye kamati ya maadili akihojiwa na Wabunge wenzake utakuta hana sababu maalumu ya kutoa"
Msikilize Spika Ndugai hapa chini akifafanua wakati akifanya mahojiano na kipind cha East Africa Breakfast


Askofu Niwemugizi: Niko Tayari Kuitwa Mchochezi Tunahitaji Katiba Tena Katiba Nzuri

$
0
0
Lugha ya Kiswahili si Kikwazo Katika Muziki Wangu Najivunia Kutumia Lugha Yangu- Ali Kiba
Askofu wa Kanisa Katoliki Ngara, Severin Niwemugizi amesema yuko tayari kuitwa mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa kama wachochezi.

Askofu Niwemugiza amesema yeye kama kiongozi wa dini anaongozwa na maadili, haki na ukweli hivyo hajali namna wengine watakavyomchukulia.

Akifungua mkutano wa asasi za kiraia uliolenga kujadili kuhusu Katiba Mpya leo Jumatano, Askofu Niwemugizi amesema imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri.

Amesema hakuna mtetezi wa haki za binadamu anayetaka nchi iingie kwenye machafuko kwani wote lengo lao ni kuchochea maendeleo, amani na utulivu.

Askofu Niwemugizi amesema kuanza kutokea kwa matukio ya kuteka watoto, vifo katika mazingira ya kutatanisha na ongezeko la watu wasiojulikana ni ishara mbaya.



"Hizi sio dalili nzuri kwa Taifa lenye afya njema. Ni vielelezo vyenye dira mbaya. Imefika wakati tukae kama Taifa tukubaliane kuwa tunataka dira njema ambayo ni Katiba."

Amesema anatambua jitihada anazofanya Rais John Magufuli katika kupambana na ufisadi na kutaka rasilimali ziwanufaishe wanyonge lakini ni muhimu juhudi hizo zilindwe na Katiba nzuri.

"Rais anafanya mengi mazuri na alipoanza kila mmoja aliona dalili za matumaini lakini juhudi hizo zinaweza zisiwe endelevu kama hakuna ulinzi wa Katiba,”

"Tunahitaji Katiba tena Katiba nzuri ambayo haitaruhusu kuchezewa na yeyote kwa maslahi au matakwa yake binafsi."

Amesema, "Namshauri Rais achunguze kwa makini yatakayozungumzwa kwenye mkutano huu,  ayaone kuwa yana nia njema na ayafanyie kazi."

Lugha ya Kiswahili si Kikwazo Katika Muziki Wangu Najivunia Kutumia Lugha Yangu- Ali Kiba

$
0
0
Lugha ya Kiswahili si Kikwazo Katika Muziki Wangu Najivunia Kutumia Lugha Yangu- Ali Kiba
Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' amefunguka na kusema kuwa lugha ya Kiswahili si kikwazo kwake na muziki wake kufika kimataifa na kusema yeye anajivunia kutumia lugha hiyo ambayo kwa sasa ni kati ya lugha kubwa duniani.

Alikiba alisema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz wiki kadhaa zilizopita na kusema anajisikia fahari kutumia lugha ya Kiswahili katika muziki wake na kusema kufanya hivyo inasaidia pia kukuza lugha yetu ya Kiswahili ulimwenguni.

"Hakuna kizuizi cha lugha kwenye muziki zamani tulikuwa tunapenda miziki ya Kiringala lakini tulikuwa hatujui nini wanaimba, tulikuwa tunapenda miziki kutoka Congo lakini hatuelewi wanaimba nini na bado mpaka sasa kuna watu wanapenda miziki ya kizungu lakini hawaelewi kizungu hivyo hakuna kizuizi cha lugha kwenye muziki. Kiswahili ni lugha kubwa Afrika na ni lugha ambayo inaheshimika sana barani Afrika na tunapoendelea kuimba Kiswahili tunaikuza lugha yetu kwanza mimi najivunia kuwa Mswahili nasaidia kukuza lugha yetu ya Kiswahili ifike kote inapotakiwa kufika kwa sababu tayari ni lugha kubwa duniani" alisema Alikiba

Aidha Alikiba aliendelea kusema kuwa kwa sasa sehemu ambazo anakwenda kufanya matamasha yake nje ya Tanzania mashabiki wamekuwa wakiimba nyimbo zake hizo japo si kwa kupatia lakini ni hatua kuwa wanapenda anachoimba licha ya kutoelewa maana yake na kudai hiyo ni njia moja wapo ya kuzidi kukuza lugha ya Kiswahili.

"Kuimba Kiswahili hakukwamishi kabisa muziki wetu kufika mbali kinachotakiwa kufanya muziki mzuri tu, mimi nishafanya matamasha mbalimbali nje ya Tanzania mfano Finland sikuwaimbia tu wabongo au Wakenya, nishafanya matamasha Oman na sehemu zingine watu wanaimba wewe hawajali yaani, Wanaigeria wanaimba ngoma zangu mimi, wanaimba japo hawapatii kabisaa lakini wanahisi nimeimba vizuri ndiyo maana wanapenda na kuimba na mimi" alisema Alikiba

Kubenea Atoa Siku Mbili Serikali Kulifungulia Gazeti la Mwanahalisi

$
0
0
Kubenea Aitaka Serikali Kulifungulia Gazeti la Mwanahalisi
WAHARIRI wa Gazeti la MwanaHalisi linalomilikiwa na Mbunge, Saed Kubenea lililofungiwa na serikali wamekanusha taarifa ya serikali kuwa gazeti hilo linaandika habari za uongo, wamedai kuwa wao hawajawahi kuandika uongo na badala yake huandika habari kwa weledi na ukweli.

Hayo wameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na wanahabari baada ya gazeti lao kufungiwa kwa muda wa miezi 24 (miaka miwili).

Aidha mmiliki wa Gazeti hilo, Saed Kubenea amesema kampuni yake Hali Halisi Publishers, imeiandikia barua Wizara ya Habari wakiitaka serikali kulifungulia Gazeti lao la MwanaHalisi ndani ya siku mbili (jana na leo), vinginevyo wataenda mahakamani kuidai serikali fidia ya Tsh. 141 Milioni kwa kila toleo.

Hizi Hapa Sababu Alizozitoa Nuhu Mziwanda Zilizosababisha Ndoa Yake Kuvunjika

$
0
0
Hizi Hapa Sababu Alizozitoa Nuhu Mziwanda Zilizosababisha Ndoa Yake Kuvunjika
MSANII wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Nuh Mziwanda ambaye jina lake la kuzaliwa ni Naftal Mlawa, ni mmoja kati ya vijana wanaofanya vizuri katika ulimwengu wa Bongo Fleva kwa sasa.
Miaka michache iliyopita, jina lake lilikuwa kubwa katika vyombo mbalimbali vya habari, lakini si kwa muziki, bali kwa uhusiano wake wa kimapenzi uliopata umaarufu akiwa na msanii mwen-zake, Zuwena Mohamed ambaye jina lake la kisanii ni Shilole a.k.a Shishi Baby.
Na walipata kujulikana sana kwa sababu ya uwepo wa madai kuwa Nuh alikuwa mdogo kiumri kuliko Shilole ambaye mara kadhaa alikuwa akimtetea mpenzi wake huyo kwa kudai alikuwa sawa naye.
Hata hivyo baadaye wawili hao waliachana na kila mmoja kuchukua ‘time’ yake na maisha yakaendelea. Juzikati, Nuh alikutana na Risasi Vibes na kupiga stori mbili tatu.
Swali: Tuanze na kazi yako ya muziki, unamiliki studio, Last Born Records, vipi utendaji wake kwa sasa na je, una wasanii?
Nuh: ‘Ofcoz’ wasanii wapo tena wako mbioni kutoa track zao na wakiwa tayari nitaweka wazi, lakini upande wa studio inaendelea vizuri kwa sababu kwa sasa imefanya ngoma kubwa tatu ambazo ni Anameremeta, Bao la Ushindi na wimbo wa Ali Kiba ambao unahusu kampeni za huko Kenya.
Swali: Baada ya ujio wako wa sasa wa Bao la Ushindi, kuna ‘project’ nyingine ambayo unaweza kuizungumzia?
Nuh: Hapana, acha Bao la Ushindi isumbue kwanza kwenye gemu, maana bado inafanya vizuri.
Swali: Katika ‘plan’ zako za baadaye kuna msanii yeyote wa nje ambaye unatamani kushirikiana naye kwenye kazi?
Nuh: Hapana. Ninapohitaji kufanya kolabo huwa siplan, lakini naangalia wimbo ninaotaka kufanya unamtaka nani, na yule ambaye atafiti bila kujali yupo ndani ya nchi ama nje nitamshirikisha.
Swali: Mbali na kazi, kuhusu maisha yako binafsi, tangu uachane na mkeo maisha yanaendaje?
Nuh: Safi tu, ninafurahia maisha kama kawaida.
Swali: Na vipi kuhusu malezi ya mtoto, anaishi na nani na mawasiliano kati yenu na mzazi mwenzako yapoje?
Nuh: Mtoto anaishi na mama yake. Lakini huwa ninawasiliana naye katika hali ya kufahamu anaendeleaje. Na kiukweli nipo  bega kwa bega na mwanangu.
Swali: Hata hivyo kuna wasomaji ambao mpaka sasa hawafahamu sababu ya wewe na mkeo kuachana, wengine wanadai kwamba Shilole ndiye alisababisha ndoa yako ikavunjika, kuna ukweli wowote kwenye haya?
Nuh: Hapana, Shilole hajahusika na lolote lile mimi kuachana na mama mtoto wangu. Sema kama ujuavyo Watanzania, wao wape picha tu, kepsheni wataandika wenyewe.
Walipokuwa wananiona na Shilole pengine kwenye shoo au sehemu yoyote ile wao wanaunga doti kwamba tunatoka, lakini si kweli.
Swali: Kipi hasa ni sababu kubwa ya wewe kuachana na mzazi mwenziyo?
Nuh: Wazazi wake. Kwa sababu ambazo mpaka leo sijazielewa lilitoka shinikizo ndani ya familia yake kwamba niachane naye. Kwa hiyo yeye pia aliwasikiliza wazazi wake akaamua kuolewa na mtu mwingine.
Swali: Siyo kwamba mlikuwa na tofauti zozote?
Nuh: Hapana.
Risasi Vibes: Pia hamkuzu-ngumza zaidi juu ya hili kabla hajaolewa kwingine?
Nuh: Tulizungumza sana, lakini wazazi walikuwa na nguvu kuliko mimi.
Swali: Ikitokea leo akarudi na kukuomba msamaha kwa yote na kukutaka mrudiane, utakubali?
Nuh: Siwezi kukubali. Sifikirii kurudiana naye, siwazi na wala sitamani. Hiyo ilikwishapita, itabaki historia.
Swali: Umekuwa kwenye uhusiano na staa, baadaye mtu wa kawaida, kwa sasa unahitaji mwanamke wa namna gani?
Nuh: Kwa sasa nipo ‘single’, sijafikiria wala kuhitaji mwanamke, bado akili yangu nahitaji itulie kwanza.
Swali: Asante sana kwa ushirikiano wako, labda mwisho una lolote kwa mashabiki wako?
Nuh: Niwatake wazidi kunipa sapoti zaidi. Video ya Bao la Ushindi ndiyo hiyo nimeachia Ijumaa, wategemee kazi nzuri zaidi kutoka kwangu.
Ukiachana na ngoma zake zilizowahi kutamba hapo nyuma kama Jike Shupa na Aname-remeta, kwa sasa wimbo wake wa Bao la Ushindi unaki-mbiza kwenye chati mbali-mbali.
.

Muziki wa Vigodoro Wapigwa Marufuku Tanga

$
0
0
Muziki  wa Vigodoro Wapigwa Marufuku Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga R.P.C Benedict Michael Wakulyamba, amepiga marufuku Vigodoro ndani ya jiji hilo kutokana na vitendo hivyo kuhamasisha uhalifu.

Akiongea ofisini kwake R.P.C Benedict amesema miongoni mwa viashiria vya uvunjivu wa amani ni Vigodoro, ambavyo vinatumika kukusanya vijana wenye umri mdogo wakijiandaa kufanya uhalifu.
“Miziki ya kigodoro ni miziki ambayo ukiangalia namna inavyochezwa na hata washiriki wake ni vijana ambao wanatumia kama sehemu ya maficho kwaajili ya kufanya uhalifu”, amesema R.P.C Benedict.
Hata hivyo Kamanda Benedict ameongeza kuwa hakutakuwa na ruhusa yoyote ya kufanya Vigodoro katika eneo lolote na wananchi wanatakiwa kulinda utamaduni kwa njia nzuri na sio miziki inayovunja maadili.

Naibu Waziri Makani Afunguka Wanyama Waliochukuliwa Tanzania

$
0
0
Naibu Waziri Makani Afunguka Wanyama Waliochukuliwa Tanzania
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani ametolea ufafanuzi suala la masalia ya mijusi mikubwa (Dinosaria) waliogunduliwa Tanzania na kuchukuliwa na wageni, na kusema kwamba serikali imefuatilia jambo hilo lakini haitaweza kuirudisha.

Akizungumza kwenye kipindi cha East Afrika Breakfast baada ya kuulizwa juu ya suala hilo, Injinia Makani amesema mifupa ya mijusi hiyo ni mikubwa sana kuisafirisha na pia imekaa 'delicate' sana, hivyo watafiti hao walishauri ni vyema waje wachimbe mingine ili ibaki hapa nyumbani, na sio kuirejesha mifupa hiyo.

Pia Injinia Makani amesema kuhusu masalia ya 'Dinosaria' waliogunduliwa mkoani Songwe hivi karibuni na kupewa jina la 'Songwenians shingopana', bado haijapata taarifa rasmi hivyo idara husika itafuatilia suala hilo.
Msikilize hapa chini


Inasikitisha Binti wa Darasa la Tatu Apewa Mimba

$
0
0
Inasikitisha Binti wa Darasa la Tatu Apewa Mimba
Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13 wa darasa la tatu katika shule ya msingi Makutano, kitongoji cha Igole kijiji cha Makutano wilayani Kilombero amelazimika kukatizwa masomo yake kwa kufukuzwa shule baada ya kupewa ujauzito.

Mtuhumiwa anayesadikiwa kutenda kosa hilo Samuel Daudi  ametoroka  na kwenda kusikojulikana.
Hali ya mimba za utotoni kwa wanafunzi wakiwemo wa shule za msingi wilayani Kilombero inadaiwa kuchangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo vishawishi na kurubuniwa kwa wasichana wadogo kutokana na umbali wa shule hizo na makazi ya watu, ambapo wazazi wa binti huyo ambaye hutembea umbali mrefu sana kwenda shule, wamesema hawakugundua mapema kama kwa umri wake binti yao angeweza kubebeshwa ujauzito.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makutano, Fabian Undole amesema wamekuwa na taratibu za kuwapima afya wanafunzi wa kike shuleni hapo kila baada ya miezi mitatu na kwamba jamii ya wafugaji imekuwa ikiongoza kwa matatizo hayo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Denis Londo amekiri changamoto kama hizo kujitokeza katika baadhi ya maeneo ingawa wameendelea kuchukua hatua kali na sasa wanaongeza nguvu kudhibiti kabisa hali hiyo.


Upelelezi wa Kesi ya Vigogo wa TRA Waliokwepa Kodi na Kusababisha Hasara ya Bilioni 29 Bado Haujakamilika

$
0
0
Upelelezi wa Kesi ya Vigogo wa TRA Waliokwepa Kodi na Kusababisha Hasara ya Bilioni 29 Bado Haujakamilika
Upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia hasara ya Tsh Bilioni 29 Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ inayowakabili watu watatu akiwemo Mhasibu wa Mamlaka hiyo, Reuben Mwakasa, bado haujakamilika.

Mbali na Mwakasa, mkazi wa Msagara, Moshi, Kilimanjaro, washitakiwa wengine ni Meneja wa Tema Enterprises, Ephraim Magete, mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na mfanyabiashara Elizabeth Massawe, mkazi wa Makongo Juu.

Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika ambapo, baada ya kueleza hayo Hakimu Mwijage ameahirisha kesi hiyo hadi October 11, 2017.

Washtakiwa hao wanadaiwa walitenda kosa hilo, kati ya November 22, 2013 na August 21, 2017, katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Temeke na Ilala.

Inadaiwa washitakiwa hao kwa pamoja vitendo vyao waliisababishia TRA hasara ya kiasi hicho kwa kukwepa kulipa kodi.

Teksi ya Ndege Isiokuwa na Rubani Yazinduliwa Dubai

$
0
0
Teksi ya Ndege Isiokuwa na Rubani Yazinduliwa Dubai
Dubai imefanya jaribio la teksi ya kwanza ya ndege isio na rubani ambayo wanatumaini itatumika kama chombo cha uchukuzi mijini.
Ndege hiyo isio na rubani yenye nafasi ya watu wawili iliruka kwa dakika tano katika pwani ya ghuba.

Ndege hiyo ilitazamwa ikipaa angani na mwanamfalme Hamdan bin Mohammed.
Dubai ina malengo makubwa ya kuwa mji wa kiteknolojia huku ndege zisizo na rubani na roboti
Ndege yaangukia nyumba,watu wote wanusurika Marekani

Ndege hiyo ya teksi ilibuniwa na kampuni ya Ujerumani ya Volocopter na kampuni hiyo imesema inatumai kwamba ndege hiyo itaanza kufanya kazi katika kipindi cha miaka mitano.
''Utumizi wake utahusisha simu aina ya smartophone, programu na kuagiza ndege hiyo kuruka hadi katika eneo unalopania kuelekea'', alisema Afisa mtendaji wa kampuni hiyo Florian Reuter.

Teksi ndege isiokuwa na rubani awali ilifanyiwa majaribio nchini Ujerumani mnamo mwezi Aprili.
Teksi ndege isiokuwa na rubani awali ilifanyiwa majaribio nchini Ujerumani mnamo mwezi Aprili.
Kampuni pinzani ya China eHand ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuzindua msafara wa teksi ndege mjini humo lakini mipango yake ikaonekana kuchelewa.

Dubai imejiweka kuwa mji wa kiteknolojia duniani ikiwa na mipango ya magari ya kujiendesha kusimamia robo ya safari zote kufikia 2030.

Noel Sharkey ambaye ni mwanasayansi wa komyuta na ambaye pia ni mtaalam wa roboti katika chuo kikuu cha Sheffield alisema kuwa: Changamoo kuu itakuwa vikwazo visivyoepukika kama vile kukwepa teksi nyengine, majumba marefu, vindege na ndege zisizokuwa na rubani ambazo zinatumika kusafirisha mizigo.

Amber Lulu Afunguka Kuhusu Beef Lake na Gigy Money

$
0
0
Amber Lulu Afunguka Kuhusu Beef Lake na Gigy Money
Msanii wa muziki na video vixen Bongo, Amber Lulu amedai kuwa hana beef na Gigy Money kama ambaavyo imekuwa ikiripotiwa mtandaoni.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Only You’ amesema ni kweli wamewahi kungombana na ni kitu cha kawaida kutokea ila kwa sasa ni marafiki na wanashirikiana katika kazi.

“Hapana hatuna upinzani, ni mshikaji, sisi ni marafiki wa siku nyingi ambapo kugombana ni vitu vya kawaida hata glass huwa zinagongana, halafu unajua watoto wa kike tuna mambo mengi,” Amber Lulu ameiambia Bongo5.

“LakinI sasa hivi Gigy ni mtu ambaye ni rafiki yangu, tunashirikiana katika kazi, tunashauriana, nadhani hata muziki umetufanya tuwe serious zaidi, kwa hiyo urafiki wetu mara nyingi ni kufanya kazi si kama ilivyokuwa before,” ameongeza.

Amber Lulu na Gigy Money walikuwa video vixen ila kwa sasa wote wameamua kuingaia katika muziki wa Bongo Flava.

Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani

$
0
0
Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani
Milango ya ustaa inazidi kufunguliwa kwa Diamond Platnumz.
Msanii huyo kutoka WCB ameonekana kuanza kuwateka mastaa wakubwa Marekani. Baada ya Dj Khaled kumfollow na rapper Rick Ross kumpost hitmaker huyo wa Eneka kwenye mtandao wa Instagram, Swizz Beatz na yeye ameamua kufuata nyayo kama hizo.

Swizz ameonekana katika kipande ha video akimtaja Diamond. Hata hivyo haikuishia hapo producer huyo ambaye pia ni mume wa msanii Alicia Keys ame-comment katika video hiyo ambayo Diamond ameipost katika mtandao huo.

“@diamondplatnumz Bless up King😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂,” ameandika Beatz katika video hiyo.

Rais Magufuli Aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Kilichoanza Leo

$
0
0
Rais Magufuli Aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Kilichoanza Leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu,wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alli Mohamed Shein,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd.

Makamu Mwenyekiti wa CCM) PhiliP Mangula (kulia) akikaribishwa ukumbini.

Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili ukumbini.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Mohammed Shein.

Rais Shein akisalimiana na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
RAIS na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo ameongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Ikulu jijini Dar es Salaam ambacho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
   

Chadema Yamsimamisha Katibu Wake

$
0
0
Chadema Yamsimamisha Katibu Wake
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kilimanjaro, kimezifuta barua walizoandikiwa madiwani sita wa Halmashauri ya Moshi, wakitakiwa kujieleza kwa usaliti.

Mbali na kufuta barua hizo zilizokuwa zimeandikwa na Katibu wa Chadema Wilaya ya Moshi, Emmanuel Mlaki chama hicho kimemsimamisha uongozi katibu huyo.

Madiwani hao akiwamo Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila walitakiwa kujieleza kwa madai ya usaliti kwa kumchagua makamu mwenyekiti wa halmashauri kutoka NCCR-Mageuzi.

Chadema na NCCR-Mageuzi ni vyama washirika katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unajumuisha pia CUF na NLD.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema imesema barua zilizoandikwa na Mlaki ni batili na ameagiza ziondolewe katika rekodi za chama hicho.

“Tunautangazia pia umma kuwa Emmanuel Mlaki amesimamishwa uongozi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake na tunautaka umma kusitisha mawasiliano rasmi ya chama kupitia kwake.”


Lema , Nassari Washukuru Kuitwa na Mkurugenzi wa Takukuru

$
0
0
Lema , Nassari Washukuru Kuitwa na Mkurugenzi wa Takukuru
Wabunge wa Chadema, Godbless Lema na Joshua Nassari wamesema watapeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ushahidi kuhusu madiwani saba waliojiuzulu katika majimbo yao wanaowatuhumu kupokea rushwa ili kujiuzulu nafasi zao.

Lema ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini, amesema leo Jumatano kuwa, wanashukuru Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola kuwakaribisha kupeleka ushahidi.

 "Tunashukuru sana mkurugenzi mkuu wa Takukuru kutukaribisha, tutapeleka ushahidi wetu ofisini kwake na tunaamini atafanyia kazi tuhuma hizi," amesema.

Amesema mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki, Nassari ambaye madiwani watano katika jimbo lake wamejiuzulu amekwenda Nairobi nchini Kenya kuonana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kupata baraka zake kabla ya kwenda Takukuru.

"Nassari amekwenda Nairobi kuonana na Mwenyekiti Mbowe ili kumweleza tukio hili na akirudi tutakwenda naye moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Mlowola," amesema.

Utendaji wa Rais Magufuli AsaidiaWafanya Tanzania Kuwa Kivutio Umoja wa Mataifa

$
0
0
Utendaji wa Rais Magufuli AsaidiaWafanya Tanzania Kuwa Kivutio Umoja wa Mataifa
Waziri wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika mashariki Augustine Mahiga amesema Tanzania imekuwa kivutio kikubwa katika viunga vya mkutano wa Umoja wa Mataifa kutokana na utendaji wa Rais Magufuli unaolenga kuwaletea huduma bora wananchi.

Akitoa Taarifa hiyo kutokea New York Dkt. Mahiga amesema kwamba katika mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutokana na kuenea kwa sifa za utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

"Nimekutana na wajumbe kutoka nchi za Afrika, Asia, Ulaya na Marekani na wengi wanasema nchi zao zipo tayari kumualika Rais Magufuli au viongozi wao wako tayari kuja Tanzania kupata uzoefu jinsi ambaavyo Rais anafanya mageuzi makubwa katika kipindi kifupi. Wanamuona ni mtu jasiri na mwenye upeo mkubwa katika kuwatumikia watu wake" Dkt. Mahiga

Ameongeza kwamba, Licha ya mpaka sasa kuhutubia kwenye baraza kuu la UN, nimeshafanya mikutano ya nchi na nchi au taasisi zipatazio 25 na wiki hii natarajia kufikisha mikutano 35.

Aidha Mahiga amesema pia mbali na sifa za Rais Magufuli uchache wa wajumbe walioongozana nae kwenda kwenye mkutano huo umekuwa kivutio kwani wengi wa watu wa mataifa mengine wameridhishwa na jinsi Tanzania inavyobana matumizi kwa kutumia vizuri pesa za walipa kodi ambao ni wananchi.

Balozi Mahiga ameungana na watu watatu kutoka katika Wizara yake pamoja na kuungana na Balozi kwenye umoja wa Mataifa Balozi Wilson Masilingi.

Wananifanyia Vitu vya Ajabu ili Kujinufaisha- Wema Sepetu

$
0
0
Wananifanyia Vitu vya Ajabu  ili Kujinufaisha- Wema Sepetu
Mlimbwende Wema Sepetu ambaye wengi humuita msanii mwenye nyota yake, amesema watu wanamfanyia vitu vya ajabu ili kujinufaisha likija suala la kuimba muziki, kwani kwake jambo hilo limeshindikana kabisa.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Wema amesema yeye hana mpango wa kuingia kwenye muziki, na hata wimbo wa Haitham alioshirikishwa hakuimba, lakini wamemgeuka na kuandika kwamba ameshirikishwa kuimba kwenye wimbo huo.

"Mi kuimba siwezi mwenzangu, kila nikijaribisha inabuma, ile nyimbo na Haitham umeshanisikia naipush, mi nafanyaga nilivyofanya halafau watu wananifanyia vitu vya ajabu, wananisaliti", amesema Wema Sepetu.

Hivi karibuni msanii Haitham ameachia wimbo unaoitwa Play boy huku ukiandikwa ameshirikishwa Wema Sepetu, lakini hakuna mahali ambapo msanii huyo amesikika kuimba wala kurap na kuibua maswali mengi kwa wadau kwanini imekuwa hivyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Apiga Marufuku Ubomoaji Nyumba

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Apiga Marufuku Ubomoaji Nyumba
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amepiga marufuku ubomoaji wa nyumba bila idhini yake.

Pia, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata madalali wa Mahakama wanaotumiwa kubomoa nyumba za wananchi bila kupata kibali kutoka kwake.

Amesema hayo leo Jumatano, alipozungumza na wananchi wa Kata ya Kunduchi alipotembelea eneo hilo akiwa ziarani kikazi kusikiliza kero za wananchi na kukagua miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Soko la Samaki.

Marufuku hiyo imetolewa baada ya Diwani wa Kunduchi, Michael Urio kutoa kero kwamba kuna watu wamevunjiwa nyumba pasipo viongozi wa maeneo husika kushirikishwa.

Hapi amesema kumekuwa na kesi nyingi ofisini kwake kuhusu kubomolewa nyumba na watu aliowaita matapeli na kwamba, kuanzia sasa hakuna atakayebomoa bila ya yeye kujua.

Amesema lengo ni kuhakikisha nyumba zinazobomolewa zimeainishwa na Mahakama kwa kuwa madalali wengine wanaghushi hukumu.

"Ni marufuku mtu kuvunja nyumba bila mimi na vyombo vyangu kuwa na taarifa. Hatuwezi kuvumilia huu mchezo, kama kuna dalali amekwenda kuvunja nyumba ambayo haijaainishwa kwenye hukumu ya Mahakama akamatwe mara moja," amesema.

Hapi amesema, "Zipo kesi zimetokea kwenye wilaya yetu, wale madalali wamekuwa wakivunja nyumba ambazo hazijaainishwa, Mahakama inasema nyumba namba 13 wao wanavunja nyumba namba 23," amesema.

Uchaguzi wa Marudio CCM Hapatoshi Vurugu Zatanda

$
0
0
Uchaguzi wa Marudio CCM Hapatoshi Vurugu Zatanda
Vurugu zimeibuka katika uchaguzi wa marudio wa kumpata mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM) Wilaya ya Nyamgana baada ya wajumbe kutoka Kata ya Mahina kuzuiwa kuingia ukumbini kupiga kura wakidaiwa si wajumbe halali.

Vurugu zimesababisha walinzi wa chama hicho (Green Guard) kuzuiwa kufanya kazi yao na badala yake mgambo wa Jiji la Mwanza kusimamia uchaguzi huo. Akizungumza nje ya ukumbi leo Jumatano, Katibu wa wajumbe hao, Samora Msiba amesema baada ya kuhoji sababu ya wao kuzuiwa kuingia ukumbini walielezwa kiongozi wao wa kata hana mawasiliano au mahusiano mazuri na Serikali.

“Tunaomba viongozi wa ngazi za juu waliangalie suala hili kwa kuwa hata sisi tuna haki ya kupiga kura na si kusukumwa na kususiwa ovyo kwa kuhusishwa na kesi zisizotuhusu,” amesema Msiba

Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mahina, ambaye pia ni Katibu wa Green Guard wilayani Nyamagana, Kagambo Paul amesema amekerwa na kitendo cha kuporwa jukumu lake la kusimamia uchaguzi na kupewa jeshi la akiba la mgambo ambalo halihusiani na chochote kwenye uchaguzi huo.



Uchaguzi kwa mara ya kwanza ulifanyika Septemba 23 ambao mshindi hakupatikana kutokana na kura kutofikia nusu ya zilizopigwa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala amesema uchaguzi umerudiwa kwa sababu hakuna mgombea aliyepata nusu ya kura zilizopigwa.

Wagombea hao waliopitishwa na Halmashauri Kuu ya Mkoa ni Hassan Mambosasa aliyepata kura 37 kati ya 336 zilizopigwa, mwingine ni Philipo Magori aliyepata kura 137 na Yusuph Rudumo aliyepata kura 148.

Wanaorudia uchaguzi ni Philipo Magori na Yusuph Rudumo. Matokeo bado hayajatangazwa

Mwigulu Nchemba Kujenga Kituo Kikubwa Cha Afya

$
0
0
Mwigulu Nchemba Kujenga Kituo Kikubwa Cha Afya
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Kinampanda ameanza ujenzi wa kituo kikubwa cha Afya katika kata hiyo.

Waziri Mwigulu amesema ujenzi utaanza Oktoba 2 mwaka huu ambapo kwa kuanza yeye ametoa mifuko 300 ya Simenti na Nondo 100 huku akiwataka vijana wajitolee kufyatua matofali.

Tayari mkandarasi wa ujenzi huo ameshapatikana na anaanza kazi Jumatatu ya Oktoba 2 ambapo matarajio mpaka ifikapo mwakani kituo hicho kianze kufanya kazi.

Aidha kwa upande wa Vijana wa Iramba wakiwakilishwa na Katibu wa vijana CCM Abel Makala wamesema wapo tayari kuweka kambi sehemu kunapofanyika ujenzi huo mpaka ukamilike kuunga mkono juhudi za kupatikana kituo.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images