Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Tetesi: Mbunge wa Geita Mhe. Msukuma Achukuliwa Mkojo ili Ukapimwe kwa Mkemia Mkuu

$
0
0
Habari kutokea Geita zinasema Mbunge wa Jimbo hilo Msukuma amechukuliwa Mkojo ukapimwe, hii nikutaka kujua viashiria vya uchochezi ambavyo vinasababishwa na matumizi ya dawa za kulivya.

Hatua hii imekuja baada ya kufuatilia utetezi wa matumizi ya Bangi uliofanywa na mbunge huyo bungeni hivyo polisi wanafwatilia uhusika wake kwenye bangi

Askofu Niwemugizi asema yuko tayari kuitwa mchochezi .......Atoa Ushauri Mzito kwa Rais Magufuli

$
0
0
Askofu wa Kanisa Katoliki Ngara, Severin Niwemugizi amesema yuko tayari kuitwa mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa kama wachochezi.

Askofu Niwemugiza amesema yeye kama kiongozi wa dini anaongozwa na maadili, haki na ukweli hivyo hajali namna wengine watakavyomchukulia.

Akifungua mkutano wa asasi za kiraia uliolenga kujadili kuhusu Katiba Mpya leo Jumatano, Askofu Niwemugizi amesema imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri.

Amesema hakuna mtetezi wa haki za binadamu anayetaka nchi iingie kwenye machafuko kwani wote lengo lao ni kuchochea maendeleo, amani na utulivu.

Askofu Niwemugizi amesema kuanza kutokea kwa matukio ya kuteka watoto, vifo katika mazingira ya kutatanisha na ongezeko la watu wasiojulikana ni ishara mbaya.

"Hizi sio dalili nzuri kwa Taifa lenye afya njema. Ni vielelezo vyenye dira mbaya. Imefika wakati tukae kama Taifa tukubaliane kuwa tunataka dira njema ambayo ni Katiba."

Amesema anatambua jitihada anazofanya Rais John Magufuli katika kupambana na ufisadi na kutaka rasilimali ziwanufaishe wanyonge lakini ni muhimu juhudi hizo zilindwe na Katiba nzuri.

"Rais anafanya mengi mazuri na alipoanza kila mmoja aliona dalili za matumaini lakini juhudi hizo zinaweza zisiwe endelevu kama hakuna ulinzi wa Katiba,”

"Tunahitaji Katiba tena Katiba nzuri ambayo haitaruhusu kuchezewa na yeyote kwa maslahi au matakwa yake binafsi."

Amesema, "Namshauri Rais achunguze kwa makini yatakayozungumzwa kwenye mkutano huu,  ayaone kuwa yana nia njema na ayafanyie kazi."

Nassari, Lema Wakubali Kupeleka Ushahidi wao TAKUKURU

$
0
0
Wabunge wa Chadema, Godbless Lema na Joshua Nassari wamesema watapeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ushahidi kuhusu madiwani saba waliojiuzulu katika majimbo yao wanaowatuhumu kupokea rushwa ili kujiuzulu nafasi zao.

Lema ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini, amesema leo Jumatano kuwa, wanashukuru Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola kuwakaribisha kupeleka ushahidi.

"Tunashukuru sana mkurugenzi mkuu wa Takukuru kutukaribisha, tutapeleka ushahidi wetu ofisini kwake na tunaamini atafanyia kazi tuhuma hizi," amesema.

Amesema mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki, Nassari ambaye madiwani watano katika jimbo lake wamejiuzulu amekwenda Nairobi nchini Kenya kuonana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kupata baraka zake kabla ya kwenda Takukuru.

"Nassari amekwenda Nairobi kuonana na Mwenyekiti Mbowe ili kumweleza tukio hili na akirudi tutakwenda naye moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Mlowola," amesema.

Kubenea Afunguka, ni Baada ya Gazeti lake la Mwanahalisi Kufungiwa

$
0
0
Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL) inayomiliki magazeti ya Mwanahalisi, Mawio na Mseto imesema itafungua kesi mahakamani endapo Serikali haitaondoa zuio la kulifungia kwa miaka miwili Mwanahalisi.

Kampuni hiyo imesema endapo leo na kesho Serikali haitalifungulia gazeti hilo watafungua kesi na kuiomba Mahakama ifute zuio hilo na kudai fidia ya Sh41 milioni kwa kila chapisho tangu zuio lilipoanza kutekelezwa.

Septemba 19, Serikali ilitangaza kulifungia gazeti hilo ikisema hatua hiyo imefikiwa kutokana na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za uchochezi na kuhatarisha usalama wa Taifa.

Mhariri Mtendaji wa Mwanahalisi, Saed Kubenea leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari amesema gazeti hilo kwa miaka 12 tangu lianzishwe haliandiki upotoshaji bali ukweli.

Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo amesema kufungiwa kwa magazeti ya kampuni hiyo ni uonevu licha ya kukiri baadhi ya maonyo waliyopewa na Serikali.

Kubenea amesema habari zilizotumika kulifungia gazeti hilo ni za ukweli.

JE Umeshawahi Sikia Kauli ya Kubemenda Mtoto...? Huu Hapa Ukweli Kuhusu Kubemenda

$
0
0
Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni mchanga na ananyonyeshwa.

Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya mapenzi.

Je, kuna ukweli wowote?
Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa!
kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi.

Ni baada ya muda gani mwanamke aliyejifungua anaweza kufanya mapenzi?
unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kujifungua, na wewe kujisikia vizuri na kuwa tayari kushiriki katika mapenzi. pia, mnaweza kusubiri mpaka wiki 6 zipite toka ulivyojifungua.

Je, kuna athari yoyote ya kufanya mapenzi baada ya kujifungua?
Kufanya mapenzi baada ya kujifungua hakuwezi kuleta madhara kwa mtoto endapo hamna maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu). ikiwa mwanaume ana vvu anaweza kumuambukiza mama na kisha mtoto kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.

Ikiwa mnafanya mapenzi kabla ya damu damu ya ukeni kukata, maambukizi ya bakteria yanaweza kutokea kwenye tumbo la uzazi (endometritis). pia kuna uwezekano wa mama kupata ujauzito miezi 6 ya kwanza ya kunyonyesha.

Nini kinasababisha afya ya mtoto kuzorota?
Kama tulivyoona, kufanya mapenzi hakusababishi mtoto kubemendwa. afya ya mtoto inaweza kuzorota kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo;

Kukosa maziwa ya mama ya kutosha
Mtoto kushindwa kunyonya vizuri
Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.
Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.
Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.
Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).

Kufanya mapenzi na mwenzi wako hakusababishi mtoto kubemendwa. baada ya kujifungua mtoto hutegemea kupata lishe bora kutoka kwenye maziwa ya mama, hivyo nyonyesha mtoto wako vizuri. ukiona ukuaji wake unazorota, onana na daktari.

Madhara ya Kutofanya Tendo la Ndoa Muda Mrefu

$
0
0
Habari zenu, nimeona niwaletee hili nina imani mtajifunza hasa kwa wale wasiofahamu,Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya tendo la Ndoa madhara yake ni kama haya:


  • Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,
  • kupendelea sana kuangalia picha za uchi,
  • Kusahausahau,
  • Kupendelea story za mapenzi,
  • Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),
  • Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),
  • Kuumwa na kichwa,
  • Kukakamaa mgongo (wanaume),
  • Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,
  • Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),
  • Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,
  • Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala

Hizi Ndio Aina Kumi za Dawa Ambazo Hazipatani na Pombe Kabisa.

$
0
0
Kumekua na kesi mbalimbali za vifo sababu ya watu kumeza dawa kisha kujisahau na kunywa pombe.hii ni changamoto kubwa sana kwenye sekta ya afya..kawaida dawa yeyote anayopewa binadamu kutibu kitu fulani ni sumu na ikichanganywa na baadhi ya kemikali kama pombe huweza kudhuru na kuua kabisa hivyo leo naenda kuzungumzia dawa kadhaa amabazo ukiona umezimeza usiguse pombe kabisa.

Dawa za kutibu bacteria[antibiotics];
hizi ni dawa ambazo hutumika mara kwa mara kwenye jamii kutibu magonjwa mbalimbali kama vidonda, kikohozi, kifua kikuu, madonda ya tumbo na kadhalika.matumizi ya dawa hizi na pombe huweza kuua. mfano fragile. isoniazid,grisiofulvin. lakini pia  na baadhi ya dawa za malaria kama quinine na dawa za ya mseto ya malaria ni hatari zikitumika na pombe.

Dawa za kuzuia damu kuganda[ant cougulant]; 
kuna dawa amabazo hupewa kwa wajawazito mara nyingi kulainisha damu ili isigande....sasa matumizi ya pombe hufanya dawa hizi kushindwa kufanya kazi na kusabisha damu kuganda hivyo kuziba mishipa ya damu ana kuleta kifo..mfano warfin

Dawa ya kupunguza mgandamizo wa mawazo[ant depressant];
pombe huingilia kazi ya dawa izi na kufanya dawa hizo ziongezeke kwenye damu kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyopangwa. hii humfanya mgonjwa alegee sana mfano amitriptyline.

Dawa za kutibu kisukari[ant diabetic]; 
dawa za kisukari hutengenezwa kwa ajili ya kushusha kiasi kikubwa cha sukari mwilini, sasa matumizi ya dawa hizi na pombe husababisha hali moja kitaalamu kama lactic acidosis... dalili ya hali hii ni maumivu ya misuli,tumbo kuuma na kusikia usingizi.hali hii isipodhibitiwa hospitali huua.mfano metformin vidonge.

Dawa za mafua na aleji;[ant histamine]
hizi dawa hutolewa kutibu mafua, miwasho ya ngozi na kikohozi lakini dawa hizi pia husababisha usingizi na uchovu kila zikitumika.pombe huongeza uzingizi huu na uchovu mara duvu na kufanya mtu ashindwe kazi. mfano promethazine maarufu kama fenigani  na chlropherinamine maleate maarufu kama piriton.

Dawa za magonjwa ya akili;
dawa za akili kama chlopromazine hutolewa kwa wagonjwa wa akili kupunguza dalili a magonjwa haya kwa kuwapa usingizi...sasa matumizi ya pombe huongeza usingizi huu maradufu na kuwafanya washindwe kupumua hivyo huweza kuleta kifo.

dawa za kutibu madonda ya tumbo;
mara nyingi madonda hutibiwi na mchahnganyiko wa dawa tatu kitaalamu kama triple therapy, sasa moja ya mchanganyiko huo kama cimetidine, metronidazole,scenidazole au tinidazole hazitakiwi kuchanganywa na pombe kabisa sababu ya madhara ambayo zimeonyesha.

Dawa za moyo;
hichi ni kikundi kikubwa cha dawa ambacho hutumika kutibu matatizo ya moyo. matumizi ya dawa hizi wakati mwingine huingilia mfumo wa kazi wa mwili na kusababisha kizunguzungu na kuanguka wakati wa kusimama mfano methyldopa, hydralazine na isosorbine mononitrate na dinitrate lakini pia matumizi ya pombe hupunguza uwezo wa dawa ya presha kitaalamu kama propanalol na kuzuia uwezo wake wa kufanya kazi.

Dawa za maumivu makali;
kuna dawa za maumivu kali sana ambazo hutolewa kwa wagonjwa wenye maumivu makali kama ya kansa, uzazi na maumivu ya ajali. pombe huongeza wingi wa dawa hizi kwenye mfumo wa damu na kusababisha overdose yaani dawa kua nyingi mwilini pale inapomezwa na pombe hata kama ulimeza dozo sahihi.mfano morphine,pethidine, codeine,meperidine...hali hii huleta kifo mara nyingi kwani wasanii wakubwa kama michael jackson na prince waliuawa na hali hizi.

Dawa za usingizi;
dawa za usingizi kama valium hutumika kwa wagonjwa wenye kushindwa kupata usingizi na wakati mwingine kwenye chumba cha upasuaji. dawa hizi huleta usingizi mkali...matumizi ya dawa hizi na pombe huongeza usingizi huu, hupunguza mapigo ya moyo, hupunguza uwezo wa kupumua, kupoteza fahamu na kifo lakini pia dawa za kifafa kama phenytoin  hupunguzwa uwezo wake na pombe na kushindwa kuzuia uwezo wake wa kuzuia degedege za kifafa.

Mwisho;
kutaja dawa hizi haimaanishi kwamba dawa zote ambazo sijataja hapa zinafaa kunywa na pombe, hapana..kuna dawa bado zinafanyiwa utafiti kama zina madhara zikitumika na pombe lakini pia ni vizuri kujenga tabia ya kutokunywa pombe kabisa kama uko kwenye dozi ya ugonjwa wowote na hata kama una ugonjwa ambao unataka kumeza vidonge maisha yote kama kisukari, presha, ukimwi, kifafa na kadhalika basi ni vizuri ukaacha pombe kabisa.

Diamond Platnumz inabidi Apewe Uwaziri au Ukuu wa Mkoa Kwa Maana Amelifanyia Mambo Makubwa Sana Taifa Hili

$
0
0
Diamond Platnumz inabidi Apewe Uwaziri au Ukuu wa Mkoa Kwa Maana Amelifanyia Mambo Makubwa Sana Taifa Hili
Huyu bwana mdogo Diamond Platunumz amefanya mambo mengi makubwa makubwa sana hapa nchini kuliko hata viongozi wemye dhamana hiyo tena amemzidi hata rais magufuli kwa kujitolea misaada mbalimbali kwa wananchi wenye uhitaji.

Kwa haraka haraka ukipiga mahesabu misaada aliyoitoa kwa miaka kadhaa inafikia Bilioni 20+.

Asilimia kubwa ya mapato yake hutumia kusaidia vijana na wazee wasiojiweza.


Wasanii chipukizi wengi wamepewa sapoti ya kimawazo na kifedha na diamond platnumz ingawaje wakishatoka wanasahau fadhila .

 Hawa watoto wamepata bahati ya kusomeshwa shule ya kimataifa inayofanya mtaala wa Cambridge na ada isiyopungua milioni 20 kwa mwaka mpaka watakapo fika ngazi ya chuo kwa kitendo chao tu cha kuibuka washindi kwa kucheza ngololo.


Mbali na haya diamond pia amechimba visima vya maji visivyopungua 15 kwa shule mbalimbali hapa nchini hususani kwa mkoa wa dar es salaam.

Katika kusaidia vijana diamond pia hayupo nyuma ,kuna wakati alikuwa anamlipa Haruna Moshi Boban nusu ya mshahara anaolipwa kipindi anachezea timu ya Friends Rangers.

Vilevile amesaidia kwa kiasi kikubwa sana kukuza na kuibua vipaji vya wasanii mbalimbali hapa nchini kwa mfano Rayvan kipindi yupo Tip Top alikuwa hajulikani sana na ila Mondi akamchukua na kumsaidia kumtangaza mpaka akafanikiwa kuchukua tuzo ya BET mwaka huu ,wasanii wengine kama vile Harmonize ,Lavalava queen darlin nk.


Pia diamond hayupo nyuma kusaidia wasanii wenzake , mara kwa mara amekuwa akiwasaidia kuwapa pesa za kufanyia video wasanii wenzake na vilevile huwapa ofa ya kuchagua mavazi kwenye maduka yake ya nguo mara kwa mara.

Diamond pia alimsaidia Diva kumnunulia simu yenye thamani isiyopungua milioni moja.


Pia hata zile milioni 13 alizotoa Wema kumdhamini kajala zilitoka mikononi mwa diamond ila hakutaka ijulikane kwa watu wengi.


Diamond mara kwa mara amekuwa akisifika kuwanunulia magari wasanii wenzake hasa katika sherehe za siku zao za kuzaliwa.

Diamond vilevile hayupo nyuma kwenye kusaidia mambo ya dini kuna kipindi alitaka kujenga msikiti utakao kuwa mkubwa kushinda yote hapa Africa Mashariki ingawaje suala hilo lilipingwa vikali sana na viongozi wa dini kwa kudai kuwa pesa zake ni haramu hazifai kujengea msikiti na hata kama akijenga yeye diamond hatopata thawabu zozote kwa hiyo itakuwa sawa na bure tu .


Diamond mara kwa mara amekuwa akisaidia wakina mama wasiojiweza kwa kuwapa misingi ya biashara ili kuweza kuendesha maisha yao.

Diamond pia amekuwa akiwapa motisha walimu kutoka shule mbalimbali anazozitembelea kwa kuwapa pesa na nyenzo za elimu za elimu kama vile vitabu nk.

By Hance Mtanashati



Mke wa Mchekeshaji Kevin Hart Ametisha sana! Kama FBI vile Ataka Password Zote za Mumewe

$
0
0
Kevin Hart, ni American actor, alikutwa na skendo ya kumpa mimba binti mwingine wakati mke wake akiwa ni mjamzito.

Mke wake amejua, na jamaa akaomba msamaha kwa familia yake pamoja na fans wake. Mke kamsamehe jamaa kwamba kweli shetani alimpitia, ila AMETAKA PASSWORD ZAKE ZOTE NA AWE FREE NA SIMU ZA JAMAA WAKATI WOWOTE ANAPOTAKA, ili kuepusha shetani kupita tena.

Yan kitu chochote chenye namba ya siri au password ya aina yoyote, wife ametaka azijue, kuanzia akaunti, social networks, email etc, n simu awe nayo free kuikagua muda wowote anaotaka..!!

Hii ni zaidi ya FBI aisee.

Mh. Temba adai Yamoto Band ilisambaratishwa na Wenye Fedha

$
0
0
Msanii wa Bongo Mh. Temba amedai kuwa chanzo cha kundi la Yamoto Banda kusambaratika ni baada ya watu wenye fedha kuingia kati.

Temba ambaye alikuwa msamamizi na mmoja ya waanzilishi wa kundi hilo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa imekuwa kawaida watu kuona vipaji viking’aa ndipo wanajitokeza kwa mgongo wa kusaidia lakini hawataki kuibua vyao na ndicho kilitokea kwa Yamoto Band.

“Mimi nakupa mfano hawa Yamoto, utaona labda kuna mtu anasimamia msanii fulani, mbona hakumchukua mwanzo wakati hajulikani kabla hatujamkuza na kuwa superstar,” amesema Temba.

“Huyo mtu kama ana uwezo kwanini asingekuwa na vipaji vyake, wewe unaona tayari nuru inang’aa unaenda kuchomoa pale,” ameongeza.

Kundi la Yamoto Band ambalo liliundwa na Aslay, Beka Flavour, Marombosso na Enock Bella kwa sasa kila mmoja anafanya kazi na menejiment yake.

Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Askofu Ajitoa Mhanga Katiba Mpya..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Septemba 28

$
0
0

Askofu Ajitoa Mhanga Katiba Mpya..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Septemba 28

Mbunge Akiri Kukojoa Hadharani Mbele za Watu

$
0
0
Mbunge kutoka nchini Uganda, Ibrahim Abiriga amekiri kuwa alikojoa hadharani katika uzio wa Wizara ya Fedha baada ya kubanwa na mkojo.

Jana nilikuwa nimebanwa sana, nikaenda kukojoa, alisema Abiriga wakati akifanya mahojiano na na kituo cha runinga cha nbs.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari kwanini alifanya hivyo wakati ofisi za bunge zilikuwa jirani, alijibu kwa mshangao, akiuliza kwanini asifanye hivyo, kwanini abane mkojo?

Mbunge hiyo ni miongoni mwa wabunge wanaounga mkono kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa umri wa Rais ili kumruhusu Rais Museveni kugombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2021.

Katiba ya Kenya hairuhusu mtu anayegombea Urais kuwa na umri zaidi ya miaka 75, ambapo kama katiba haitobadilishwa, Museveni hatoweza kugombea tena kwani atakuwa amezidi miaka hiyo.

Comments

Madiwani Waliohama Chadema Kwenda CCM Arusha Wafunguka Kuhusu Ushahidi wa Rushwa wa Lema na Nassari

$
0
0
Baadhi ya Madiwani wa CHADEMA Arusha waliotimkia CCM wasema hawakununuliwa na ushahidi wa Lema na Nassari wanaodai wanao ni wa kutengeneza.

PICHA: Wabunge Uganda Wazichapa Ngumi Kavu Kavu Bungeni...Kisa Kizima Hichi Hapa

$
0
0
Wabunge Uganda wakigombana ndani ya ukumbi wa bunge baada ya kupishana kuhusu muswada wa marekebisho ya katiba, kipengele cha umri wa Rais.




Mchambuzi Blog

PICHA:Nyumba 13 za Polisi Arusha Mjini Zilivyoteketea Kwa Moto Usiku wa Jana

$
0
0
Jumla ya Nyumba 13 za Polisi zilizopo kata ya Sekei Jijini Arusha zimeteketea kwa moto. Chanzo kimedaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.


Wanamuziki wa P Square Katika Mgogoro Mzito Tena..Tazama Video Wakizichapa Ngumi Live

$
0
0
NIGERIA: P Square na Jude Okey manusura wapigane wakiwa ofisini kwa mwanasheria wao. Mwanasheria akanusha wake zao kuwa chanzo cha mgogoro.

Tazama VIDEO :


Siri NzitoYatawala Kikao cha Kamati Kuu ya CCM

$
0
0
Siri NzitoYatawala Kikao cha Kamati Kuu ya CCM
Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilianza jana chini ya Mwenyekiti wake, John Magufuli, lakini haikuweza kufahamika mara moja uamuzi uliofikiwa katika kuchuja majina ya wagombea wa nafasi za uongozi katika ngazi ya wilaya.

CCM imeanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wake kuanzia ngazi ya shina na sasa umefikia wilayani ambako majina ya wagombea yanachujwa na vikao vya juu ambavyo vinafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia jana hadi mwishoni mwa wiki.

Baada ya Kamati Kuu kumaliza vikao vyake vya siku mbili leo, CCM itakuwa na kikao cha Halmashauri Kuu ambayo itabariki mapendekezo ya chombo hicho cha utendaji cha chama hicho tawala.

Hakuna taarifa zilizotolewa jana kuhusu maazimio ya kikao hicho na juhudi za gazeti hili kupata wahusika ziligonga mwamba.

Matokeo yake, usiri huo uliibua ubashiri ulioenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa wabunge wachache ambao wamekuwa wakionekana kuikosoa Serikali, wamevuliwa uanachama.

Hata hivyo, gazeti hili halikuweza kuthibitisha habari hizo.

Picha zilizotumwa na Ikulu jana zinaonyesha wajumbe wa kamati hiyo wakiwa wamesimama kabla ya kuanza kikao, bila ya kuwapo katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Picha moja inamuonyesha Rais Magufuli akiingia kikaoni, akiwa ameongozana na naibu katibu mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo ambaye anaonekana kuwa ndiye aliyeshika nafasi ya Kinana.

Mpogolo pia anaonekana pembeni ya Magufuli ndani ya kikao kuthibitisha kuwa alishika nafasi ya Kinana sehemu fulani ya kikao hicho.

Hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu kutokuwepo kwa mtendaji huyo mkuu wa CCM na kama aliingia kikaoni baadaye.

Picha nyingine inamuonyesha Waziri Mkuu wa zamani, Salim Ahmed Salim, ambaye huenda alikaribishwa kuhudhuria kikao hicho.

Salim na marais wa awamu tatu zilizotangulia kabla ya Serikali ya Jakaya Kikwete, ndiyo waliofanya kazi kubwa ya kutuliza wajumbe wa Halmashauri Kuu mwaka 2015 wakati zogo lilipoibuka kutokana na jina la Edward Lowassa kuenguliwa na Kamati Kuu kuwania kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

Habari ambazo Mwananchi ilizipata jana zinaeleza kuwa Kamati Kuu ilianza kwa kupokea taarifa ya Kamati ya Maadili kuhusu mwenendo wa wagombea wakati wa mchakato wa kuchukua fomu hadi sasa.

Taarifa hiyo ndiyo inayotumiwa na Kamati Kuu kupitisha au kuondoa wagombea, ambao hawakuruhusiwa kujitangaza, kujipitisha kwa wapigakura wala kutumia mbinu nyingine yoyote kutafuta kura hadi watakapotambulishwa mbele ya wapigakura.

Pia ripoti hiyo itawaweka bayana wanachama ambao wamesukumwa na watu wenye fedha ili wawatumie kwa malengo binafsi baadaye.

Pia, taarifa zinasema mchujo huo utawagusa wale waliotahadharishwa kugombea kutokana na vitendo vyao vya ukuikwaji wa maadili ndani ya chama.

Taarifa zinaeleza kuwa licha ya kuweka miiko ya kugombea uongozi ndani ya chama, kama kuwakataza watumishi wa Serikali kugombea nafasi ambazo baadaye zitawalazimu kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kunadi sera za chama, bado baadhi walijitokeza kugombea na kupitishwa na vikao vya ngazi za chini.

Kikao hicho pia kinaangalia maadili ya walioomba kugombea ili kuepuka kupitisha wagombea ambao ni watuhumiwa wa ubadhirifu wa mali za chama, wasio wakazi wa maeneo husika na waliopitishwa baada ya wengine kuonewa katika uteuzi na kuwapo mgombea mmoja pekee aliyepitishwa badala kuwa na ushindani.

Ommy Dimpoz Amkataa Mtoto wake

$
0
0
Ommy Dimpoz Amkataa Mtoto wake
Msanii Ommy Dimpoz ambaye hivi karibuni ameachia 'video' yake mpya ya 'Cheche' amekanusha taarifa za kuwa na mtoto nchini Marekani, na kusema kwamba bado hajajaliwa kupata mtoto kabisa.

Ommy amezungumza kwenye eNewz ya East Africa Television, baada ya kuulizwa  kuhusu mtoto ambaye amekuwa akimpost kwenye instagram, kusema mtoto huyo siyo wake licha ya kuwa wanafanana.

"Mimi sina mtoto  kwa kweli yule ni mtoto wa rafiki yangu, kwa hiyo mimi kwake ni kama baba. Sema nilivyopost na unajua sura zetu kidogo kama zinafanana, watu wakasema mtoto wa Dimpoz, mimi siwezi kujisingizia lakini kama Mungu akijaalia kama wangu atakuwepo wala sitaleta kona kona nitasema jamani mtoto wangu huyu", amesema Ommy Dimpoz

Hivi karibuni Ommy Dimpoz alipost picha akiwa na mtoto mdogo wa kike na baadhi ya watu wakidai ni wake lakini cha kushangaza msanii huyo aliifuta picha ya huyo mtoto ambaye ilikuwa katika ukurasa wake na kuacha video moja inayomuonyesha yuko naye na kuzima kitufe cha maoni 'comment'.

Rado: Wema Siyo Aina ya Mwanamke Ninayeweza Kumuoa

$
0
0
Rado: Wema Siyo Aina ya Mwanamke Ninayeweza Kumuoa
Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Rado amefunguka kwa kudai Wema Sepetu siyo aina ya mwanawake ambaye anaweza kuoa au kuwa naye katika mahusiano kutokana na jinsi anavyodeka kila wakati.

Rado amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na filamu waliyocheza pamoja na Wema iliyopewa jina la 'Madame' ambayo ilizua utata katika mitandao ya kijamii ikidai wawili hao wanatoka kimapenzi nje ya kazi hiyo.

"Sijawahi kumpenda msanii yeyote wa bongo movie wala bongo fleva wa kike, sijawahi kuvutiwa na madame Sepetu kwa sababu naona kama yupo nje ya wanawake ambao mimi nawapenda. Unajua mimi nina mchanganyiko wa Usukuma na Unyakyusa kwa hiyo wanawake wa kudeka muda wote siwapendi, napenda wanawake fulani hivi ambao wamekaza", amesema Rado.

Pamoja na hayo Rado ameendelea kwa kusema "Kwa jinsi alivyokuwa mlegevu Madame sina uhakika  kama anaweza hata kufua nguo, kutokana na kudeka kwake".


Kwa upande mwingine, Rado amesema kwa sasa soko la filamu linaendelea kufanya vizuri sokoni kwa madai kileo chao kimeweza kusikika na hatimaye baadhi ya makampuni wamejitokeza katika kusimamia mauzo ya kazi zao ambao zinaingia mtaani.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images