Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Rekodi mpya iliyoandikwa na Nigeria usiku wa jana kwenye kombe la dunia

0
0
Timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ jana iliweka rekodi mpya katika michuano ya kombe la dunia, baada ya ushindi dhidi ya Bosnia.
Super Eagles jana walipata ushindi wa kwanza kwenye michuano hiyo tangu mashindano ya mwaka 1998 yaliyofanyika Ufaransa.
Goli pekee la mshambuliaji wa Stoke City Peter Odemwingie lilivunja mkosi wa kutokushinda mechi kwa Nigeria katika kipindi cha miaka 16 iliyopita.
Nigeria sasa wamefikisha pointi 4 wakishika nafasi ya pili nyuma ya Argentina ambao tayari wameshafuzu.
Mechi za mwisho ya kundi hilo zitakazowakutanisha Nigeria vs Argentina na Iran vs Bosnia ndio zitaamua timu gani itakayoungana na Argentina kwenda kwenye hatua ya pili ya michuano hiyo

Unataka kujua Marcio Maximo anatua lini Yanga – taarifa hii hapa

0
0
Maandalizi ya msimu wa ligi kuu ya Tanzania yameanza kupamba moto huku vilabu vikijaribu kujiimarisha tayari kwa mapambano, kwa upande wa klabu ya Yanga wameanza kwa kuimarisha benchi la ufundi kwa kumuajiri kocha Marcio Maximo.
Kocha huyo mbrazil anayeheshimika zaidi nchini, Marcio Maximo atatua Jangwani ndani ya siku nne kuanzia leo Jumamosi. Bosi huyo ambaye anasifika zaidi kwa msisitizo wake katika nidhamu za wachezaji atatua Jumanne ikiwa ni mapema kabla ya uchaguzi wa Simba utakaofanyika Juni 29 Jijini Dar es Salaam. Mwanaspoti linajua kwamba Maximo yuko jijini Brasilia akifanya kazi ya uchambuzi wa mechi za Kombe la Dunia kwenye televisheni ya Taifa ya Mexico na mkataba wake unamalizika Jumatatu.
Yanga imethibitisha kwamba Maximo ameshaanza maandalizi ya safari hiyo tangu juzi ambapo katika hilo pia amewajulisha baadhi ya maofisa wa Ubalozi wa nchi hiyo nchini kuwa atakuwa Tanzania mapema wiki hii kumalizia maongezi yake na mabosi wa Yanga.
Yanga wamemleta Maximo mapema kufanya maandalizi ya uhakika katika kikosi cha timu hiyo ikiwa ni kuwawahi wapinzani wao wa jadi Simba ambao bado wapo katika mchakato wa uchaguzi.
“Ilikuwa kuna baadhi ya viongozi waende Brazil kumalizia mazungumzo na kusainishana mkataba  lakini hilo limebadilishwa. Maximo ndiyo atakuja Dar es Salaam kuepuka gharama,”alisisitiza mmoja wa viongozi wa Yanga.
Source: Mwanaspoti

Baadhi ya Wadada ni Mizigo Katika Mahusiano ya Kimapenzi

0
0
Leo itanibidi niseme tu hata mkinitusi manake mmezidi jamani kuwapa mizigo hawa kaka zetu alafu na wengi wao hata hawashtuki mpaka pale mambo yanapomwendea mrama, utakuta dada mzuri kweli wa sura na umbo yupo kwenye mahusiano na mkaka yaani huyo dada yeye kazi yake ni kumchuna tu jamaa mara sina vocha na hata ukimpa yeye kazi yake kukubeep apigiwe mara leo sijui nimeona nguo mwenge na mengine mengi ila unakuta hakuna yeye kitu anafanya kwa huyo mwanaume ili ajione na yeye ni mtu kweli , basi hata mawazo ya jinsi ya kupata hela mpe basi , kazi yako wewe starehe tu ijumaa ikifika ndo wakwanza kupanga viwanja vya kwenda kujirusha hata hujui jamaa yako hela kapata wapi...Alafu ndo unakaa unajiuliza mbona siolewi? Bibie Kuelewa yahitaji kujitoa usione Vinaelea jua vimeubwa....

MSAMI Adai Kulala Mzungu wa Nne Kitanda Kimoja na Irene Uwoya..!

0
0
Msanii wa muziki wa bongo flava Msami amemkana kiaina mrembo na msanii wa bongo movie Irene Uwoya akitia ugumu kukubali moja kwa moja kama ni wapenzi.
Msami katika mahojiano na Mamu Africa Blog alikuwa mgumu kukubali moja kwa moja kama wana mahusiano ya mapenzi na Uwoya akisisitiza kuwa mrembo huyo ni zaidi ya rafiki.
Akaenda mbali zaidi akisema mara kadhaa amekuwa analala na Uwoya kitanda kimoja hata siku mbili mpaka tatu lakini wanalala mzungu wa nne.

Unajua Uwoya ni best friend wangu sana sana,wakati mwingine nakwenda kwake tunapiga stori mpaka usiku,tunaangusha pamoja hata siku mbili tatu kitanda kimoja lakini huwa tunalala mzungu wa nne tu” alisema Msami.
Msami aliendelea kuzunguka kuukubali akitumia neno kwa mfano kama ni wapenzi na Uwoya kukutana kwao ni baada ya kazi zao kwakuwa kila mmoja ana majukumu yake ya kikazi.

“Unajua kwa mfano tuna imagine kuwa Uwoya ni mpenzi wangu,mara nyingi tunakutana baada ya mihangaiko yetu ya kila siku.
Baada ya danadana za hapa na pale na kubanwa hatimaye Msami akakiri kuwa kweli anatoka kimapenzi na Uwoya.
Aidha Msami amesema anashangaa watu wanaosema kuwa Uwoya anatoka na Serengeti boy wakati hawaujui ukweli wa jambo hilo,kwakuwa yeye ana umri mkubwa zaidi ya mrembo huyo.
Amesema amemzidi Uwoya kwa kuzaliwa kwa miezi kadhaa kwahiyo yeye sio Serengeti boy kwakuwa ni mkubwa kwake.
“Nawashangaa watu wanasema eti Uwoya anatoka na Serengeti Boy yaani hata ukweli hawaujui mimi ni mkubwa nimemzidi miezi kadhaa wanasemaje eti ni Serengeti Boy waache hizo” Msami alisema.

MAINDA:Hata Mkinisema na kunicheka siachi ULOKOLE Ng`oo…!

0
0
Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’  amefunguka kuwa kwa sasa hatakubali tena kusumbuliwa na wanaohoji juu ya maisha yake mapya ya wokovu.
Akizungumza na paparazi wetu, Mainda alisema mwanzoni alikuwa anapata shida sana kuishi na watu kwani yeye kama msanii kila anachofanya watu wanachukulia ndivyo sivyo na hata katika wokovu pia wanahoji kama atauweza kitu ambacho anaamini hatotetereka.

Nimejifunza vitu vingi sana kutokana na ustaa wangu, watu wengi wananiangalia kwa jicho linginewanataka kuona je Mainda ana mabadiliko gani baada ya kuokoka? Ninapoteleza kama mwanadamu utasikia watu wanasema mimi si mlokole, siwajali kwa sasa,’’ alisema Mainda

Siri nzito Mnada wa Kuuza bidhaa za machinga Zilizokamatwa

0
0
Kilichotokea mnadani

Katika eneo la mnada wa kuuza vitu vya machinga vilivyokamatwa lililopo katika Soko la Kibasila Gerezani, kulikuwa na makundi ya watu wa aina mbili; waliokwenda kununua vitu vingi kwa bei ndogo na wengine ni wale ambao bidhaa zao ndizo zilikuwa zinapigwa mnada na hawakuwa na uwezo wa kushinikiza wauziwe wao.

Wafanyabiashara waliokuwapo katika eneo hilo jana, walisikika wakisema wamekwenda kununua vitu vya dhuluma na kwamba walilazimika kununua kwa kuwa hakukuwa na njia nyingine ya kufanya.

Leonard Mwagike alisema baada ya bidhaa zake kukamatwa alijaribu kwenda kuzikomboa lakini alishindwa baada ya Mahakama ya Jiji kumwamuru alipe faini ya Sh400,000.

“Kinachoendelea hapa ni dhuluma tu, haiwezekani mzigo wangu wa Sh50,000 uniambie nilipe faini ya Sh400, 000, bora kuja hapa kuununua tena kama nitaweza,” alisema kwa huzuni.

Mfanyakazi wa kampuni moja ya udalali jijini, iliyopewa mamlaka ya kuuza bidhaa hizo, alikuwa akifungua mzigo mmoja baada ya mwingine na kuwataka wafanyabiashara hao wapange bei.

Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, alionekana kutaka kuchukua kila bidhaa aliyoiona ni nzuri, huku akiwaambia wanunuzi kuwa alikwishaichunguza mizigo hiyo kwa hiyo anajua upi ni mzuri.

Mzigo wa kwanza kufunguliwa ulikuwa una vyombo vya plastiki vya kuwekea chakula, ambavyo vyote viliuzwa kwa Sh10, 000. Zilifuata nguo za watoto na chupa za chai, kisha ukafika wakati ulioleta msuguano kiasi cha kutishia mnada kuvunjika.

“Sasa kwenye mzigo huu kuna mali nzuri wengine wameshaiona si ndiyo? Eeh! Ni madera (magauni), mfuko mzima shilingi ngapi?” Anauliza dalali, lakini kabla hajapata jibu anasema:

“Jamani yupo shemeji yenu (mke wake) lazima naye apate hizi nguo (huku minong’ono ikianza kusikika anachukua magauni matatu na kuyaweka pembeni).”

Kitendo hicho kiliwakasirisha baadhi ya machinga waliokuwapo katika eneo hilo, huku wakisema iwapo angeuona mapema mzigo huo angeuchukua wote.

“Mali mmetunyanganya sisi na hata tunazonunua hapa mtazichukua tena, halafu bado mnachukua hata mnazouza, hili halikubaliki,” alisema mfanyabiashara mmoja.

Baada ya kuuzwa kwa bidhaa mbalimbali zikiwamo feni, viatu na suruali, linapatikana tena furushi lenye madera na hali ikawa kama ilivyokuwa awali.

Dalali: “Ule mzigo huu hapa tena, lakini saa hizi tuuweke pembeni kwanza, mimi ninaweza kuuchukua wote.” Kauli hiyo inapingwa huku kila mtu akitaka magauni yote yahesabiwe.

Wakati uuzaji ukiendelea, Mmachinga mmojawapo anabaini kuwa mzigo wake uliokuwa umekamatwa umeuzwa kwa mtu mwingine hivyo anaamua kumfuata na kuongea naye.

“Haiwezekani mzigo wangu mkubwa vile wa mikoba anunue mtu kwa Sh8,000 tu,” anasema huku akiondoka.

Hamisi Kiwanuka anasema alikamatwa kwa kosa la kupanga na kuuza feni barabarani, lakini alipojaribu kuzitafuta baadaye hakuzipata, badala yake aliziona nyingine zimevunjika, ambazo hazikuwa zake.

“Hawa jamaa wanauza hapa vitu vilivyobaki baada ya kuchambuliwa sana, vizuri vyote wamechukua,” alisema.

Pia, mama mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Mama Kuluthumu, ambaye alifanikiwa kununua sufuria 17 kwa sh10, 000, alisema:

“Baadhi ya sufuria ziliondoka na wali na nyama sijui ziko wapi?”

Viongozi wanena

Mwenyekiti wa Operesheni ya kuwaondoa Wamachinga barabarani jijini hapa, Msongoro Songoro, alisema wapo wafanyabiashara wa aina mbili ambao wanalengwa katika zoezi hilo la safisha jiji; wanaotoa bidhaa ndani ya maduka na kuzipanga nje na wale wanaoweka barabarani.

Wafanyabiashara wanaopatikana na kosa la kupanga bidhaa nje hutozwa faini ya papo kwa papo ya Sh50, 000 na kupewa onyo, ambapo fedha inayopatikana hupelekwa katika halmashauri husika na zile zinazopatikana kwenye mnada hupelekwa ofisi ya jiji.

“Lakini anayepanga bidhaa barabarani, akikamatwa anafikishwa mahakamani na mali yake inataifishwa kwa sababu hana leseni ya kufanya biashara hiyo,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema hadi kufikia Juni 12 mwaka huu jumla ya wafanyabiashara 711 walifikishwa mahakamani, huku baadhi yao wakihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au faini kati ya Sh100,000 na Sh400, 000.

Alipoulizwa kuhusu tuhuma za askari wa Jiji kula chakula cha wafanyabiashara, Songoro alisema kuwa taarifa hizo siyo za kweli kwa sababu kutokana na vurugu zinazokuwapo wakati wa ukamataji siyo rahisi chakula hicho kufaa kuliwa tena.

Watanzania Tunaweza, Mengi akava jarida la fobres africa la july 2014

0
0
'Barefoot to $550milion' Ndio maneno yaliyopo kwenye picha ya mwenyekiti mtendaji wa IPP iliyopo kwenye cover la jarida la Fobres litakalotoka JULY mwaka huu..
Kwenye jarida hilo Mengi amesimulia kutoa alivokuwa anatembea kwa peku hadi kuwa na utajiri wa dola milioni 550.

Agenda ya siri ya CUF katika mchakato wa Katiba Mpya

0
0
Wakati viongozi wa CCM wakizunguka jimbo kwa jimbo kutetea Mfumo wa Muungano wa Serikali mbili, Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema hakiungi mkono hata pendekezo lililotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba la kutaka Muungano wa Serikali tatu.

Migongano hiyo ya kimtazamo inazidi kuliweka taifa katika umbile la mshazari, huku matumaini ya kupatikana kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano yakionekana kupotea kutokana na kundi la wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kukataa kuendelea kushiriki Bunge la Katiba kwa madai kuwa CCM imekuja na rasimu yake.

Hata hivyo misimamo hiyo si kwamba inaonekana kuwachanganya wananchi tu bali pia inazidisha taharuki ya wananchi kutoelewa hatima ya upatikanaji wa Katiba na mfumo upi ambao ni sahihi katika kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofikisha umri wa miaka 50.

Kundi la Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd limeeleza neema, fanaka na matunda ya Muungano wa Serikali mbili kiuchumi, kisiasa, kiulinzi na kiusalama.

Wakati huohuo kundi la viongozi wa CUF chini ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, linasisitiza kuwa lazima Zanzibar ipate mamlaka kamili ya dola.

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Ismail Jussa Ladhu, akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Vuga, amesema CUF iliunga mkono pendekezo la Serikali tatu kama ngazi ambayo ingekisaidia chama hicho kufikia malengo ya kupatikana mamlaka kamili ya Zanzibar.

Jussa anasema bila Zanzibar kupata uraia wake, hati ya kusafiria, mambo ya nje, kiti Umoja wa Mataifa, Sarafu na benki kuu, Serikali tatu hazina tija wala faida yeyote kwa Wazanzibar.

Anasema madai ya msingi ya Wazanzibari ni kupatikana kwa mamlaka huru za Tanganyika na Zanzibar.

Anasema yatakapopatika masuala hayo na kubaki katika mikono ya Zanzibar kama dola kamili, Zanzibar itakapoweza kujikwamua na kupiga hatua nyingi za kiuchumi, kinyume na hali ilivyo sasa ya kuwa kama mgeni mualikwa katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Amesisitiza kuwa lengo kuu la kukutana kwa Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Novemba 5 mwaka 2009, licha ya kusaka maridhiano ya kisiasa na kuzika uhasama, ilikuwa ni mpango wa kuweka nguvu ya pamoja ili kuipatia Zanzibar mamlaka kamili.

Bila ya kupepesa maneno Jussa amesema kwamba kwa bahati mbaya warithi wa Dk Karume wamekuwa wakiyumba, huku wakishndwa kuungana na kudai masuala ya msingi

Bila ya Wazanzibari kuungana na kusimama pamoja, madai yao hayataweza kufikiwa.

Maalim Seif kwa upande wake anasema kwa kuwa CCM wanataka kubaki na serikali mbili, basi moja iwe ya Tanganyika na ya pili ya Zanzibar; zote zikiwa na mamlaka kamili .

Akijibu mapigo ya Maalim Seif na Jussa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Mtoni , Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Stephen Wasira anasema kimsingi wanachokitaka CUF na viongozi wake si Muungano bali wana nia na dhamaira ya kuligawa taifa na kuvunja Muungano.

Anasema kudai kiti Umoja wa Mataifa, sarafu, uraia au Benki Kuu ni mwelekeo wa kuvunja Muungano. Akamtuhumu Jussa na wenzake kuwa ni mawakala wa mabeberu na wakoloni wanaopigania Zanzibar irejee katika mikono ya watawala waliopinduliwa mwaka 1964.

Wassira anasema Jussa amekuwa akikerwa na kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi kwani hata wakiwa kwenye Kamati za Bunge maalumu la Katiba ametaka siku ya Januari 12,1964 iondolewe katika orodha ya siku kuu za kitaifa.

Balozi Seif anasema ikiwa wajumbe wa Ukawa wataendelea kushikilia msimamo wao wa kukataa kurudi bungeni ili kujenga nguvu ya hoja na kupatikana katiba bora, watakaopoteza turufu na kupata hasara ni Wazanzibari

Anasema kwa kiasi kikubwa madai ya Zanzibar ili iweze kujikwamua kiuchumi na kushamirisha maendeleo yake, yamezingatiwa katika Rasimu ya Katiba Mpya, hivyo ni jukumu la Wazanzibari kutambua jambo hilo na kupigania kupatikana Katiba Mpya.
CHANZO:Mwananchi.

MBASHA: Maisha ya Jela hayafai kabisa.

0
0
Kufuatia  Mahakama  ya  Ilala  jijini  Dar  kumuachia  kwa  dhamaa  Emmanuel  Mbasha  ambaye  ni  mume  wa  muimbaji  wa  nyimbo  za  Injili  maarufu  nchini  Flora  Mbasha  anayekabiliwa  na  tuhuma  nzito  za  kumbaka  mdogo  wa    mkewe, inaelezwa  kuwa  siku  moja  tu  aliyokaa  mahabusu  ilimfanya  kubadilika  muonekano  kutokana  na  kudhoofika…..

Emmanuel  Mbasha  ambaye  alifikishwa  mahakamani  kwa  mara  ya  kwanza  juni  17  mwaka  huu  na  kukosa dhamana  kutokana  na  kushindwa  kutimiza  mashariti, alilazimika  kutupwa  mahabusu  katika  gereza  la  Keko, kabla  ya  juni  19  kupandishwa  tena  kizimbani  ambapo  aliachiwa  kwa  dhamana  baada  ya  kutimiza  masharti  hayo….

Baadhi  ya  watu  ambao  walimshuhudia  Mbasha  katika  viunga  vya  mahakama  hiyo  walioneklana  kulengwa  na  machozi  huku  wengine  wakitamka  kwamba  wanamuachia  Mungu

Mume  huyo  wa  Flora  aliwasikitisha  zaidi  watu  kutokana  na  kuwa  na  mawazo  mengi  huku  miguuni  akiwa  amevaa  malapa  ambayo  thamani  yake  haizidi  sh. 2000  wakati    katika  hali  ya  kawaida  huwa  anavaa  mavazi  ya  bei  mbaya  na  kujiweka  msafi  muda  wote…..

“Maskini  Imma  amevaa  ndala  na  amekonda.Hakika  yupo  katika  kipindi  kigumu  sana. Jela  mtu  hukonda  siku  moja  tu.Jela siyo  kuzuri  hata  hata  kidogo,”  alisema  raia  mmoja  nje  ya  mahakama  hiyo.

Hakimu  aliyesikiliza  kesi  hiyo  Wilberforce  Luhwago  aliahirisha  kesi  hiyo  hadi  July  17  mwaka  huu  itakapo tajwa  tena…..

Baada  ya  kuachiwa, Mbasha  alitoka  nje  ya  mahakama  hiyo  kwa  kasi  na  kuingia  kwenye  gari  kisha  kutoweka  eneo  hilo….

Akizungumza  na  mwanahabari  wetu, mmoja  kati  ya  ndugu  wa  Mbasha  ambaye  hakupenda  jina  lake  litajwe  alisema  kuwa  mume  wa  mwanamuziki  huyo  aliwaambia  hana  hamu  na  jela,

“Mbasha  alisema  kuwa  jela  hakufai  kabisa  na  alisisitiza  kuwa  asaidiwe  kutoka  kwa  dhamana. Alisema  siku  moja  aliyoishi  mahabusu  ni  kama  mwaka  mzima,” alisema  ndugu  huyo.



Aidha  ndugu  huyo  alisema  kwamba  kitendo cha  Flora  kutomtembelea  mume  wake  ni  cha  kinyama  na  hakuna  aliyekitarajia.

“Hakwenda  kumuona  mume  wake.Kwa  kweli  jambo  hili  limetushangaza  sana  na  kutuumiza  sana, sijui  mwisho  wake  utakuwa  vipi  lakini  tunaamini  yatakwisha, kwa  uzuri  au  ubaya,” alisema.

Baadhi  ya  mahabusu  ambao  walikuwa  selo  moja  na  Mbasha  katika  gereza  la  Keko  wamesema  kwamba  wamefurahi  kuwa  na  nyota  huyo  kwani  wamekuwa  wakimsoma  kwenye  magazeti  tu

Kituko cha Mwaka Kondomu Zanaswa Ukumbi wa Bunge

0
0
Inaweza kuonekana ni kituko cha aina yake, lakini ni kweli kimetokea kwenye Ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Nairobi na kuwaacha wabunge vinywa wazi.

Katika hali isiyo ya kawaida, boksi la kondomu lilikutwa ndani ya ukumbi huo na kuwashtua wabunge wote akiwamo spika wa bunge hilo.
Mwakilishi wa eneo la Karura, Kamau Thuo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuliona boksi hilo na kuwashtua wabunge wengine hali iliyoibua mjadala mzito.
Kutokana na sintofahamu hiyo Spika Alex Ole Magelo aliwataka wahudumu kufungua boksi hilo kujua kilichomo ndani yake ndipo walipokuta kondomu

Nafahamu wote humu ni watu wazima, lakini ninachoshangaa ni nani ambaye ameleta kondomu hizi ndani ya ukumbi huu,” alihoji Spika Magelo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Manoah Mboku aliwaondoa hofu wabunge na kueleza kuwa kondomu hizo zilipaswa kuwekwa kwenye vyoo vya wanaume hata hivyo kwa bahati mbaya zikapelekwa mahali kusikohusika.

Hemedy 'Nimechafua Sana More than Sana sasa Nataka Kutulia na Kuoa, Huyu Ndo Mchumbwa Wangu'

0
0
Muna akiwa kwenye pozi tata
Msanii wa filamu nchini Hemedy aka PHD mwenye mikogo kuzidi mabilioni ya Dr dre amesema baada ya kuchafua sana sasa anataka kutulia na kuoa kabisa.Hemedy alisema hayo alipokuwa akiongea na paparazi, Phd alisema kuwa "Nimechafua sana more than sana nikaona hii bora iishe maana mama yangu anataka vitu ving kutoka kwangu so nimepata msichana ninaye mpenda na yeye ananipenda so natarajia kufunga ndoa mwezi november

William Malecela " Issue ya Flora Mbasha na Mumewe ni Another Time Bom in The Waiting Kama Nguza na Wanawe'

0
0
ANOTHER TIME BOM IN THE WAITING HII CINEMA ILIANZA KAMA MCHEZO MCHEZO LAKINI KAMA UNAISOMA KWA MAKINI SASA IT IS SLOWLY TURNING UGLY TENA POLE POLE NA HUKU WANANCHI TUKIANGALIA KWA MACHO YETU, NA TUKISIKIA KWA MASIKIO YETU HATUJUI UKWELI WA NDANI WA TATIZO LA FLORA NA MUMEWE LAKINI KUNA NENO MOJA KATIKA ISHU YAO YA FLORA MBASHA KUWA KIMADA WA MCHUNGAJI GWAJIMA HUKU AKIWA BADO MKE HALALI WA MBASHA HALINA UBISHI JUU YA UKWELI WAKE, USHAHIDI MWINGI WA MTAANI TAYARI UMESHATOLEWA NA GWAJIMA MWENYEWE AMESHINDWA MPAKA LEO KUKANUSHA, KAMA KINACHOSEMWA NI KWELI NA UKWELI NI KWAMBA MBASHA ANAKARIBIA KWENDA KUOZA JELA KAMA NGUZA NA WANAWE KWA SABABU AMBAZO NI TATA!!

- SASA HAYA YOTE YANATOKEA MBELE YA MACHO YETU NA MASIKIO YETU HII JAMII,  SIJASIKIA MWANAUME YOYOTE MWENYE NGUVU KATIKA JAMII YETU AKIJITOKEZA KUSEMA LOLOTE ON THIS ISHU NA SISI WANAUME WENGINE WOTE TUMENYAMZA KIMYAA ILA AKIFUNGWA MAISHA JELA SASA UTAONA MAKELELE WAKATI KUMBE KAMA NI MAKELELE YA DHULUMA YANATAKIWA KUPIGWA SASA, USHAHIDI MWINGI WA MTAANI UNAONYESHA KAMBA FLORA MBASHA NDIYE MCHAWI HAPA KWA SABABU PIA ALIWAHI KUMSINGIZIA MCHUMBA WAKE WA KWANZA KUWA ANA UKIMWI, NA THE FACT KWAMBA MDOGO WAKE ANAYEDAIWA KUBAKWA HAPA TAYARI AMEWAHI KUTENGENEZA VIDEO YA NGONO NA MRISHO NGASSA WA YANGA NA IPO MITANDAONI NI DALILI TOSHA KWAMBA HII KESI INA UTATANISHI SANA, SIO SIRI FLORA ANA NGUVU YA PESA KULIKO MUMEWE NA HASA UKIZINGATIA KWAMBA ANA GWAJIMA WITH HER NA NGUVU YA PESA NIMEIONA JUZI MBASHA ALIPOPELEKWA RUMANDE, NOW PEOPLE THIS IS ANOTHER TIME BOMB IN THE WAITING KAMA KWELI SISI NI WAPENDA HAKI BASI WAKATI NI HUU KUMSAIDIA MBASHA, INGAWA BINAFSI NAOMBA KUSEMA UKWELI WANGU I DON'T LIKE BOTH OF THEM THE MAZAFANTAZAZZ I MEAN FLORA NA MUMEWE KWA SABABU NAWAONA NI WASANII WA AJABU SANA WALIOISHI KISANII KWA MUDA MREFU SANA KWA KUWADANGANYA MASIKINI NA KUCHUKUA HELA ZAO ZA SADAKA MPAKA MUNGU ALIPOAMUA KUWAFICHUA USANII WAO HIVI KARIBUNI NA THIS KESI HATA MBASHA SIAMINI KWAMBA HE IS A REAL MAN KWA SABABU ANGEKUWA HE SHOULD HAVE FIND A SOLUTION LOONG TIME AGO KWA SABABU INAELEKEA WALIKUWA NA MATATIZO KWA MUDA MREFU SANA LAKINI MBASHA HANA PESA SO ALIKUWA AKITEGEMEA PESA ZA FLORA NDIO MAANA WAMEDUMU MUDA MREFU AND YES I SAY THIS KWA SABABU HAKUNA A REAL MAN DUNIANI ANAYEWEZA KUMUONA MKE WAKE WA NDOA ANAISHI NA GWAJIMA LAKINI BADO AKAMVUMILIA THE MAZAFANTAZZ I SAY NO WAY!! NDIO MAANA NAWAITA WOTE WAWILI WASANII WA AJABU INFACT INGEKUWA UWEZO WANGU NINGEWAWEKA JELA KWA HATA MWEZI MMOJA TU KWA KUDANGANYA UMMA KWAMBA NI WATU WA MUNGU SANA THE MAZAFANTAZZ THEY ARE NOT HAWA WOTE WAWILI THEY BELONG IN JAIL!!, LAKINI FOR THE SAKE OF THIS SUBJECT NASEMA HIVI HII KESI HAIKO SAWA AS OF USHAHIDI WOTE WA MTAANI ULIOTOLEWA SO FAR!! NI UAMUZI WETU WANANCHI KUMSAIDIA MBASHA AU KUNYAMAZA MPAKA AFUNGWE MAISHA NDIO TUANZE KULIA LIA DHULUMA!!, JAMANI ASUBUHI NJEMA SANA!! - LE MUTUZ SYSTEM

Intagram Kimenuka:Team Wema Washikana Uchawi, Account Maarufu kwa Mipasho zafungiwa..Wema Mwenyewe Hana Habari

0
0
Kwa kile kinachoonekana ushabiki wa kupitiliza kwa wema Team mbali mbali zilizoanzishwa instagram kwa ajili ya kumshabikia Wema na Nyingine kuwananga wanao mchukia wema kwa sasa zimeingia katika mgogoro mkubwa wa sinto fahamu baada ya picha ya Mama Wema Kuediwa na kutundikwa mtandaoni cha kushangaza ni jinsi wanavyoshikana uchawi Wenyewe kwa wenyewe kwa kile kinachodaiwa ni Ushabiki Feki Kwa Wema..

                               Sakata lenyewe lilianza hivi:
Baada ya Picha Feki ya Mama Wema Kuwekwa mtandaoni na instagram account ijulikanayo kama Homa_ya_jiji_Team_Dengue na Account Nyingine Maarufu ya Kumtetea Wema Ijulikanayo kama Dogiemasta13 ilifanya kazi ya ziada kumshawishi Homa_ya_jiji_Team_Dengue kuidelete hiyo picha na baada ya muda ilideletiwa , kwa Masharti kuwa Dougiemasta13 aifunge account yake, na account ikafungwa kweli

Sasa Jana katika kutafuta nani mwenye account ya Homa_ya_jiji_Team_Dengue akaibuka Mshabiki maarufu wa Wema Anayejiita Tilda_Mati kwenye Insta na kusema kuwa Aliyehusika kuweka picha ya Mama Wema Insta ni Mwenye Account ya Usipojipanganitakupanga nitakupanga ambae nae pia ni mshabiki wa Wema kwa maana kuwa ana account mbili kwa tofauti moja ya kumponda wema na ingine ya kumshabikia soma hapa alichosema:

Baada ya Shutuma Hizo kwa Usipojipanganitakupanga kutoka kwa Tilda_mati naye Usipojipanga akaandika hivi kupangua shutuma:


Leo Asubuhi huyu Tilda Mati account yake imefungwa nadhani baada ya watu wengi kuireport Instgram, Pia account ya Homa_ya_jiji_Team_Dengue nayo imefungwa, Dougiemasta baada ya kufunga account yake ya dougie masta 13 amefungua account nyingine leo kwa jina la dougiemasta 14 na kusema haya:
Vita vya wenyewe kwa Wenyewe Vyaendelea .....Hizi Team zina Mambo angalieni tu msitoane Macho, Wema Mwenyewe Wala Hana Habari na Team Zenu na Alishasema Hajamtuma Mtu Kufanya huo Ujinga na kutukanana .
UdakuSpecially

Ni Ulimbukeni (UBOYA) Kuwa na Simu ya Gharama Wakati Hata Kitanda Huna

0
0
Ninasikitishwa na ulimbukeni wa vijana hasa wa kibongo kutumia fedha nyingi kununua simu za gharama ili mradi eti kufanana na fulani au nae aonekane...unakuta kijana mwingine kapanga chumba hana hata hata stuli lakini utamkuta ana galaxy note! mbaya zaidi hata kutumia hawezi kila siku wanakuja kusumbua humu mara nimeilock oh mara siwez kufungua net...pumbavu kabisa iyo hela kwanini usinunue itel.. elfu 35 halafu iliyobaki ukachonga kitanda na meza pale geto kwako?

Bob Junior Amkumbuka Mkewe Aliyemwacha Asema Kuondoka Kwake Imekuwa Msiba Kwake..Ataka Warudiane

0
0
Mapenzi ni kitu Kingine Jamani Acheni tu, Unaweza kumuona leo hafai ile kesho ukamlilia yule yule uliesema hafai..Kama mnakumbuka wakati Bob Junior anaachana na mke wake aliongea mengi tu ikiwemo ameamua kila mtu achukua zake kwa vile Mwanamke anawivu sana na kumfutilia kila mahali....ila sasa Bob Junior anajutia Kitendo hicho na kusema amemmisi sana na yupo mpweke na amekiri kuwa yule mwanamke ndio aliyemfundisha mapenzi, leo hii anakula vibandani....Mzee mzima mpaka ameamua kumtungia wimbo akimlilia basi ujue kiukweli anataka warudiane.....
Tujifunze kwa hili Raha za muda Mfupi zisikufanye uisahau familia na kuona haina thamani....Wakati ndoa ya Bob inavunjika alijitokeza dada Mmoja (Toto Ashley) na Kudai Anatoka nae Haya Leo yupo Wapi....(Tusamini Familia Zetu)

Breaking News:Majambazi yaua mtawa (Sister) mmoja kwa risasi Riverside, Ubungo

0
0
SISTA wa Parokia ya Makoka iliyopo Kibangu, Dar ameuawa na majambazi yaliyokuwa kwenye bodoboda wakati akiingia kwenye gari akitokea dukani eneo la River Side, Ubungo jijini Dar es Salaam hivi punde.
Kabla ya kuuawa sista huyo, dereva wake alipigwa risasi mkononi na majambazi hayo.
 Mwili wa mtawa ukiwa umefunikwa.

Risasi nyingine ikapigwa hewani watu wakaanza kukimbia ndo wale majambazi wakaingia ndani ya ile taxi na kuchukua pochi ya sister
Dereva akionesha kidole gumba kilichopigwa risasi.

Ila walibugi stepu maana pesa hazikua kwe pochi zilikua kwe gari. Mungu ailaze pema roho ya sister na Dereva apone haraka ili arudi kazini salama.

Jiji la Dar Lina Uhaba wa Wanawake Warefu

0
0
Siku zinavyozidi kusonga mbele hapa jijini naona asilimia zaidi ya 75 ni wafupi, sijaelewa ni nini kimetokea ila ukweli ni kwamba wanawake warefu wamekuwa wachache sana Dar es Salaam.

Hata ukija na jazba, ukweli ndio huo kuwa wanawake warefu jijini Dar wameadimika sana.

MCHUNGUZI HURU

Wajumbe baraza kuu CHADEMA wawalipua Mbowe na Slaa

0
0
TAARIFA YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU WA CHADEMA KWA UMMA.
A. UTANGULIZI
Ndugu wanahabari.
Mbele yenu ni viongozi halali wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kutoka mikoa yote ya Tanzania kwa uchache tumekutana jumla ya wajumbe 78 kuwakilisha wenzetu walioshindwa kufika kwa sababu mbali
Sisi ni wajumbe wa Baraza Kuu na mkutano mkuu wa Chama ambapo pamoja nasi tumejumuika na wenyeviti wa mabaraza ya WANAWAKE WA MIKOA YA TABORA NA SINGIDA, MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TABORA pamoja na MUASISI WA CHADEMA kutokea mkoa wa SINGIDA na mwenyekiti wa M4C wilaya ya SINGIDA hivyo tunafanya jumla ya tuliokutana kwa jambo hili kuwa ni wanachadema 82.
Tumewaita kuwaeleza namna ambavyo tumekuwa tukisononeshwa na mwenendo wa chama chetu kwa kipindi kirefu sasa, hivyo tunaomba mtusaidie kuufikishia umma mawazo ya wanachadema tunaowawakilisha huko mikoani tutokapo.
B. KUSHINDWA KWA UONGOZI WA KITAIFA.
Tunasikitika kuona kwamba kadri siku zinavyoenda Uongozi wa juu wa chama unazidi kushindwa kufanya kazi ya kukiimarisha chama.
Baada ya jitihada tulizozifanya kwenye uchaguzi wa 2010 sehemu mbali mbali, ni dhahiri ushindani kwa sasa ungekuwa mkubwa sana kiasi cha chama kushika dola uchaguzi ujao iwapo chama kingejikita kwenye jitihada za ujenzi wa chama.
Badala yake uongozi wetu umewasaliti Watanzania waliokuwa na tumaini kubwa sana na chadema na kuwekeza nguvu nyingi sana kwenye Kuimarisha migogoro baina ya viongozi wakuu wenyewe kwa wenyewe, wanaimarisha ubinafsi miongoni mwa wanachama, wanaimarisha Udini na Ukabila pamoja na ubadhilifu wa mali za chama.
Matendo haya ya viongozi wetu ni UNAFIKI wa kisiasa, kiasi cha kutumia mabilioni ya shilingi kwenda kumshambulia ama kummaliza kisiasa kiongozi mwenzao (Zitto Kabwe) na kuacha ujenzi wa chama ukiendelea kuporomoka.
Kwenye ujinga huu, hakuna wa kumlaumu zaidi ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe na na Katibu Mkuu Dkt.Wilbrod Slaa. Hawa wanafaa sasa kuhukumiwa na watanzania wanaopenda mabadiliko ya kweli kwa kurudisha nyuma jitihada za kuwakomboa na kukiimarisha chama na badala yake wamekuwa wakitumia nguvu kubwa na rasilimali nyingi za chama kujiimarisha wao wenyewe.

C. UBADHILIFU WA FEDHA NA MALI ZA CHAMA.
Ndugu WanaHabari.
Mtakumbuka kwamba baada ya uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2010 ruzuku ya chama iliongezeka kutoka million 56 mpaka milioni 239 kwa mwezi.
Tunasikitika kuona kwamba mpaka sasa chama kimeshindwa kufanya uwekezaji wenye tija ili kukisaidia chama kiweze kujiendesha bila kutegemea Ruzuku ama kukopa kutoka kwa Mbowe kama mwenyewe anavyopenda tuwe tunafanya.
Mpaka sasa chama kimepokea jumla ya shilingi BILIONI 10.038 kama ruzuku kutoka serikalini ili chama kijiendeshe. Ni narudia, mpaka sasa chama kimepokea kutoka serikalini jumla ya SHILINGI BILLION KUMI, NA MILIONI THELASINI NA NANE.
Cha kusikitisha kwa kipindi chote hicho na kiasi chote hicho cha pesa zitokanazo na kodi za waTatanzania pesa ambazo zinasababishwa na kazi kubwa tuliyoifanya ya kukipigania chama kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, leo chama hakina hata jengo moja la OFISI MIKOANI KOTE na OFISI zote za mikoa tunapanga kwenye FREMU za maduka na hata Pango la fremu hizo tunajilipia wenyewe kwa kuchangishana, Mbowe na Slaa wanatumia MABILIONI HAYA KURUKA NA CHOPA sisi huku chini tunaendelea kumenyeka kwa kigezo cha UKAMANDA ,huu ni utumiaji mbaya wa mali za chama.
Tunasikitishwa sana na kitendo cham mwenyekiti MBOWE kusema anajilipa madeni aliyokikopesha chama kila siku, kiasi cha zaidi ya MILLIONI 700 Mbowe anajilipa kama madeni aliyokikopesha chama. Sasa tunashindwa kuelewa deni hili ni deni gani lisiloisha?, na je deni hili alikikopesha chama kwa mkataba gani?, na aliusaini mbele ya nani huo mkataba wa mkopo?, Taratibu za chama kukopa zipo wazi je zilifuatwa?. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Tunasikitishwa na kitendo cha mwenyekiti mbowe kukiuzia chama MAGARI CHAKAVU kwa zaidi ya million 600, Huku akijua ni chakavu na kwamba kabla ya kukiuzia chama alikuwa anakikodisha magari hayo
Masikitiko yetu ni kitendo cha MBOWE kununua LANDCRUISER V8 VX 2 kwa pesa za chama na kasha kuja kukiuzia chama, lakini kama haitoshi mpaka leo hii Gari hizo zimesajiriwa kwa majina ya MBOWE HOTELS. Haya ni matumizi mabovu mno ya mali za umma na kwamba yampasa sasa ajitathmini kama anapaswa kuendelea kuwa kiongozi mtetezi wa wanyonge ama mnyonyaji wa wanyonge.
Tunahudhunishwa na kitendo cha Dkt. SLAA kutufanyia huduma ya kutuuzia ukombozi, haiwezekani kwa akili ya kawaida, ukawa katibu mkuu unayelipwa zaidi ya million 130 kwa mwaka na chama halafu makatibu na viongozi wako wa mikoani wanalipwa 0 kwa mwaka. Huu ni udalali na unafiki wa kisiasa.

D. UVUNJIFU WA KATIBA NA KANUNI ZA CHAMA.
Mpaka sasa viongozi wakuu hawa, wamevunja katiba ya chama kwa mambo makuu matatu yafuatayo.
1. Kitendo cha kutoka na kususia kwenye Bunge la katiba bila kuruhusiwa na vikao halali vya chama.

Bunge la katiba lilikuwa ni mazao ya Juhudi zetu sisi wanaCHADEMA tuliopambana nchi nzima kuidai katiba.
Chama chetu kilikuwa na fursa kubwa ya kutuwakilisha kwenye kuandika katiba hiyo na kufanya marekebisho makubwa kwa kadri tulivyoazimia.

Lakini kususa Bunge la katiba lililotokana na Sheria mliyoishiriki kuitunga, ni kutufanya sisi sote tunaowakilishwa na viongozi hawa tuonekane ni majuha.

Kwa kuwa CHADEMA ni miongoni mwa waasisi wa mchakato huu wa Katiba. Ni kuwasaliti Watanzania na kuikosesha nchi fursa ya kuandika katiba kususa.

2. Kitendo cha Kuunda Baraza Kivuli la mseto na vyama tulivyowaaminisha watanzania kuwa vina ushirika na CCM.

Kwenye hili, chama kinapaswa kuelezwa kama mazingira yaliyowafanya wenzetu hawa kuungana na CCM yamebadilika ama bado yapo?, Chama kinapaswa kuelezwa na mbowe na Slaa kuwa Uteuzi wa Mbatia kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais wa CCM umebatilishwa ama la?.

Lakini chama pia kitueleze kama Nafasi ya juu ya viongozi wa CUF kwenye serikali ya mseto na CCM kule Zanzibar haipo tena. Vinginevyo viongozi wetu wote walioshiriki hili wanatakiwa wawajibike haraka iwezekanavyo.

3. Kutokuitishwa kwa mkutano wa Baraza Kuu. Katiba yetu inatuagiza Kuwa Baraza kuu la chama litaitishwa kila baada ya miezi kumi na mbili. Kwa kuwa baraza kuu la mwisho liliitishwa February 2013, kulipaswa kuitishwa tena baraza kuu lingine kabla ya mwezi February 2014 kuisha.


E. AGIZO

· Tunawaagiza viongozi wetu waitishe haraka MKUTANO WA BARAZA KUU ili pamoja na mambo mengine viongozi wetu wajieleze mbele ya Wajumbe ni kwanini Tusiwachukulie hatua za kinidhamu kwa makosa ya UBADHILIFU, KUSALITI NDOTO ZA WATANZANIA, na KUHAMASISHA MGAWANYIKO NA UBAGUZI NDANI YA CHAMA.

· MBOWE na Dkt. SLAA wanatakiwa wajipime wenyewe kama ni sahihi chama kukodi HELKOPTA (CHOPA) 3 na kutumia zaidi ya BILIONI 1.4 za ruzuku ambazo ni kodi za Watanzania halafu eti tunashinda KATA TATU kati ya zaidi ya KATA 27, Yaani kila HELKOPTA MOJA imeleta KATA MOJA ama kila SHILINGI MILLIONI 466.6 kwa KATA MOJA, halafu chama hakionyeshi kushtuka wala Kujali

· MBOWE na Dkt. SLAA wajipime zaidi kama wanafaa kuendelea kuwa viongozi wa chama huku chama kikizidi kudidimia kila uchao kiasi cha KUDHARIRISHWA KWA kupata KURA 2000 CHALINZE na KURA 5000 KALENGA huku chama kikitumia zaidi ya MILLIONI 600 kushiriki CHAGUZI HIZO.


…………………………..
0756767672
KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TABORA
MJUMBE BARAZA LA MASHAURIANO KANDA YA MAGHARIBI
MJUMBE WA MKUTANO MKUU CHADEMA TAIFA.

Uwezi Amani Wale Wasanii Mapacha wa Anti-Virus Wameomba Poo Clouds FM sasa Beef Kwishney..Watoa Wimbo Mpya Feat Lulu Michael

0
0
Katika Exclusive interview waliyofanya kupitia kipindi cha XXL ya Clouds Fm,Mapacha wamesema kwa sasa wameamua kuweka tofauti pembeni zilizokuwepo mwanzo kwani bifu waliyokuwa wameitengeneza wamegundua haikua na faida yoyote.

Wimbo unaitwa ‘time for the money’ umetengenezwa kwenye studio za Soround Sound zilizopo THT na producer wa wimbo huu ni Tudd Thomas ambapo ndani kashirikishwa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’
Bonyeza play kusikiliza.

Watano wauwawa kwenye shambulizi lingine la tatu Kenya

0
0

Watu watano wanadaiwa kuuawa katika shambulizi lilifanywa na kundi la watu wenye bunduki katika eneo la Pwani ya Kenya, karibu na eneo la Mpeketoni ambalo wiki yalifanyika mashambulizi mawili yaliyosababisha vifo vya watu 60.

Kwa mujibu wa BBC, maafisa wameeleza kuwa watu wenye silaha walivamia kijiji cha Witu, kilichoko kilometa 15 kutoka mji wa Mpeketoni, Jumanne alfajiri (Leo).

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hili la tatu.

Kundi la Al-Shabab lilidai kuhusika na mashambulizi mawili ya wiki iliyopita katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu.

Hata hivyo, rais Uhuru Kenyatta alipinga na kudai kuwa mashambulizi hayo yanatokana na uchochezi wa wanasiasa wapinzani
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images