Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Serikali Yaanzisha Mpango wa Kuwapatia Ulinzi Wabunge

$
0
0
Serikali Yaanzisha Mpango wa Kuwapatia Ulinzi Wabunge Nchini
SERIKALI imetangaza kuanza mchakato wa kuwapatia ulinzi wabunge nchini ikiwa ni wiki tatu tangu mwakilishi wa wananchi wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kunusurika kifo baada ya kupigwa risasi tano mwilini na miguuni na watu wasiojulikana.


Wabunge hawatambuliwi kisheria kupewa ulinzi kama ilivyo kwa viongozi kadhaa wa serikali.

Akizungumza kwenye mahojiano na redio moja ya jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwingulu
Nchemba, alisema masuala ya ulinzi kwa viongozi yapo kwa mujibu wa Sheria, lakini kuna baadhi ya watu ambao hawajatambulika kupewa ulinzi.

"Kwa sasa suala hilo la ulinzi kwa waheshimiwa wabunge linashughulikiwa na tutaongeza ulinzi kwenye maeneo yote ya viongozi na kufanya doria za mara kwa mara," alisema Mwigulu.

"Hata Lissu alipodai kutishiwa tuliongeza ulinzi, lakini shida ni jinsi alivyokuwa anatoa taarifa hadharani."

Watu waliomshambulia Lissu ambaye amelazwa katika Hospitali ya Nairobi, Kenya, kwa risasi mfululizo kutoka katika bunduki inayodhaniwa kuwa SMG, wanadaiwa kuwa katika gari nyeupe aina ya Nissan.

Lissu alishambuliwa na watu hao saa 7:30 mchana akiwa ndani ya gari lake, akiwa amefika nyumbani maeneo ya Area D, Manispaa ya Dodoma, baada ya kutoka kwenye kikao cha Bunge. Imedaiwa risasi tano zilimpata tumboni na miguuni.

Mashuhuda wa shambulizi hilo la kwanza la aina yake dhidi ya Mbunge nchini, walisema Lissu wakati akiingia kwenye lango la nyumba yake alikuwa ameongozana na magari mawili.

Shuhuda mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini kwa sababu za kiusalama, alisema aliona mtu mmoja akishuka kutoka moja ya magari mawili hayo na kwenda kwenye Toyota Landcruiser ya Lissu ambapo alimshambulia kwa risasi na kisha kupanda gari na kuondoka.

Alisema hali hiyo ilizua taharuki ya watu kukimbizana huku milio zaidi ya risasi ikisikika hewani kabla ya majambazi hao kutokomea kusikojulikana.

"Baada ya kupigwa niliona gari zilizokuwa zimefuatana naye zikitoka kwa kasi huku namba zake zikiwa zimefichwa," alisema shuhuda huyo.

Alieleza kwenye gari alikuwapo Lissu na dereva wake aitwae Simon ambaye alitoka na kuanza kuomba msaada, ili akimbizwe hospitalini, alisema shuhuda huyo.
Alieleza kuwa baada ya hali ya taharuki kutulia walijitokeza wasamaria wema ambao ni wanawake, waliosaidiana na dereva huyo kumwingiza kwenye gari dogo kwa ajili ya kumkimbiza Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma.

ONGEZA ULINZI
Waziri Mwigulu alisema: "Baada ya (Lissu) kusema anatishiwa maisha tuliongeza ulinzi, lakini shida ni jinsi alivyokuwa anatoa taarifa hadharani. Hii ingeweza hata kuwapa mwanya wale waliokuwa wanapanga njama za kumdhuru kujipanga zaidi.

"Lissu alipotaja gari iliyokuwa inamfuatilia niliagiza lisakwe na hilo lilifanyika na watu walikamatwa na kuhojiwa.

"Lakini ilibainika gari lilikuwa tofauti na lile alilolitaja na gari hilo lilionekana halijafanya safari yoyote kwenye maeneo ambayo Lissu alikuwapo."

Aidha, waziri huyo alisisitiza kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea, lakini kutokana na mazingira ya sasa hawatasema chochote hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

"Tunahakikisha kuweka nguvu kubwa kutafuta ukweli wake na undani wake kwa sababu tukio hili halikubaliki na ni tukio linaloudhi," alisema Mwigulu.

"Kuna vitu vingi ambavyo bado tunasita kuvisema hadharani, tunaomba wananchi wawe na imani na kazi ambayo tunaendelea kuifanya na watapewa taarifa."

Aidha, Waziri Mwigulu alisema Serikali inaendelea kupata taarifa za maendeleo ya afya ya Lissu kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, ingawa yeye hajakwenda kumwona.



Mrembo Sanchoka Alipwa Dola 10,000 Kigali. Kafanya Show Gani?

$
0
0
Katika hali ya kustaajabisha mrembo wa Bongo anayekimbiza kwa shape matata ametupia katika ukurasa wake wa snapchat akiwashukuru Kigali kwa kumuingizia $10,000. Jamani kwa umbumbumbu wangu mwenye kunijuza anisaidie kujua huyu Sanchoka ni msanii wa fani gani? Na kigali alifanya Show gani na wapi kwa kipaji kipi hadi kulipwa pesa nyingi hivi? Mbona vipaji vimekuwa kimyakimya hivi?
Baada ya kuingia na kutoka bureau de change

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Je, Dada Unapenda Kuwa Mrembo? na Kaka Unapenda Kuwa Mtanashati na Kurudisha Heshima ya Ndoa?

$
0
0
JE, DADA UNAPENDA KUWA MREMBO? NA KAKA UNAPENDA KUWA MTANASHATI NA KURUDISHA HESHIMA YA NDOA? Tumia Bidhaa halisi za MARKSON kwa mafanikio ya uhakika na bila madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kuthibitishwa kiafya.

Pata hizi 

1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @130000@130,000/=
2. Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa (a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200000@200,000/=
(b)Vidonge @180000@180,000/=
3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @130000@130,000/=
(11)Vidonge @150000@150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150000@150,000/=
5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a) Gely ya kupaka @150000@150,000/= (b) Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @150000@150,000/= (c)Handsome up original >kifaa kinachoongeza maumbile kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250000@250,000/=
6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150000@150,000/=
7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula @130000@130,000/=
8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:- (a) Dawa ya kunywa au kupaka @130000@130,,000/= (b) Mkanda wa kawaida @100000@100,000/= (c) micro-computer belt unaovaibret @250000@250,000/=
9 .Kupunguza maziwa na kuyasimamisha @130000@130,000/=
10. Kushepu miguu na kuwa minene na kuondoa kigimbi @130000@130,000/=
11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @100000@100,000/=
12. kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @120000@120,000/= NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

  Wasiliana nasi :-
(+255) 0767447444 na 0714335378 

Madiwani wa Chadema Wanashikiliwa na Polisi

$
0
0
Madiwani wa Chadema Wanashikiliwa na Polisi
Madiwani wawili wa Chadema Emmanuel Mwalupasa na Jailo Mwandute katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba wanashikiliwa na polisi  wakituhumiwa kwa makosa tofauti ya jinai.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange amesema Mwalupasa ambaye ni diwani wa Mpande anatuhumiwa kufunga ofisi ya mtendaji kata kwa siku tatu mfululizo.

Kuhusu diwani Mwandute wa Kata ya Katete, amesema anatuhumiwa kwa wizi wa zaidi ya Sh10 milioni ambazo ni kwa ajili ya maendeleo ya kata hiyo.

Kamanda Nyange amesema madiwani hao  walikamatwa jana Alhamisi jioni na kufikishwa kituo kikuu cha polisi mjini Tunduma ambako wanaendelea kushikiliwa.

Amesema wanaendelea na uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili madiwani hao.

Meya wa Ubungo Matatani Ahojiwa kwa Saa Tatu

$
0
0
Meya wa Ubungo Matatani Ahojiwa kwa Saa Tatu
MEYA wa Ubungo, Boniface Jacob (Chadema), amehojiwa kwa saa tatu na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kwa madai ya kutumia ofisi za umma kufanya vikao vya chama.

Akizungumza baada ya kumaliza kuhojiwa jana jijini Dar es Salaam, Jacob alisema, alitoa utetezi wake kuwa hakufanya kikao isipokuwa alitembelewa na wageni wa chama, lakini kama wanaona anastahili kuwajibishwa wafanye hivyo.

Kadhalika Jacob alisema alitoa ushaidi wa matumizi mabaya ya ofisi za umma, yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Nimewaeleza Sekretarieti kuwa,  pia CCM, kimekuwa kikifanya vikao vyake Ofisi za Ikulu na wamenieleza hakuna aliyewahi kulalamika. Hivyo nimelazimika kuandika barua ya malalamiko juu ya kitendo hicho,” alisema.

Kuitwa na kuhojiwa kwa Jacob na Sekretarieti hiyo kumetokana na kitendo chake cha kumkaribisha ofisini kwake Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani.

Mke wa Mzee Small Atengwa Asimulia Magumu Anayopitia Toka Mumewe Afariki

$
0
0
Mke wa Mzee Swall Atengwa Asimulia Magumu Anayopitia Toka Mumewe Afariki
Mke wa mwigizaji nguli, Said Ngamba ‘Mzee Small’, Fatuma Said amesema yupo kwenye kipindi kigumu cha maisha kutokana na upweke alionao na kwa sababu marafiki wa marehemu mumewe wamemtenga si kwa salamu wala barua.

Akizungumza kwa uchungu na mwanahabari wetu nyumbani kwake Tabata-Kimanga jijini Dar, mama Small alisema tangu mumewe afariki ni miaka mitatu sasa, lakini mara kwa mara amekuwa akimkumbuka na kuishia kulia.

Alisema kwa sasa anapambana mwenyewe kimaisha bila ubavu wake hivyo kujikuta akipata ugumu wa maisha.

“Kwa kweli nina maisha magumu japo namshukuru Mungu niko mzima wa afya, sina kazi ninayoitegemea zaidi ya biashara yangu ya kuuza chapati kwani hata ule mradi wa maji tuliokuwa nao kabla mume wangu hajafariki, sasa ni kama haupo.

“Haupo kwa sababu serikali imejitahidi kuweka mabomba ya maji baridi, hivyo watu hawawezi kununua maji ya chumvi labda itokee maji yamekatika, hayatoki.
“Pia nategemea hela za wapangaji lakini hivyo sio nyingi zinasaidia kumsomesha mtoto shule tu.
“Kama unavyojua sasa hivi hali ya uchumi ni ngumu. Kila kitu ni ghali, nadunduliza hivi katika chapati lakini fedha zote unajikuta umezitumia kwenye mahitaji mengine.

“Mwanaume ni mwanaume tu. Alipokuwepo mume wangu nilikuwa sipati maumivu haya kwani angalau yeye alikuwa na wadau wake wa sanaa ambao walikuwa wakimpa fedha za kutufanya tuishi vizuri.

“Kwa sasa kama unavyoona hapa naishi mwenyewe na wanangu watatu alioniachia na mmoja wake niliyemlea, shughuli zao za kubangaiza tu, kama huyo mwingine alitamani awe msanii lakini hakupata wa
 kumshika mkono,” alisema mama Small.

Akiendelea kuzungumzia maisha yake ya sasa, mama huyo alisema pamoja na yote, anajivunia kuona anapo mahali pa kuishi kwani marehemu aliacha nyumba mbili na familia ya mumewe yuko nayo vizuri bila tatizo.

“Sina tatizo na yeyote yule na wala sina mwanaume wa kuziba pengo lake tangu aondoke mume wangu, ila akitokea wa kunioa nitakubali, kinachoniumiza sana ni wasanii wenzake kunitupa mfano Tupatupa alikuwa kama pacha wake lakini hata watoto hawajulii hali,” alisema mama Small.

Kambi ya Jeshi Yashambuliwa Somalia

$
0
0
Kambi ya Jeshi Yashambuliwa Somalia
Taarifa kutoka Somalia zinasema wanamgambo wa Alshabaab wameishambulia kambi ya jeshi katika mji wa Barire magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Shambulio hilo limetokea Ijumaa alfajiri na wakaazi wanasema waliamshwa kwa sauti za milipuko miwili mikubwa.

Kundi la Alshabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo na limeeleza kwamba liliidhibiti kambi ya jeshi la Somalia na kufanikiwa kuwaua wanajeshi kadhaa.
Hatahivyo maafisa wa serikali katika eneo hilo wamekana tuhuma hizo za Alshabaab, lakini wamekiri kwamba kumekuwa na shambulio.

Kambi hiyo ya jeshi mjini Barire katika eneo la Lower Shabelle ni mojawapo ya kambi zilizo bora na zenye vifaa vya hali ya juu vya kijeshi nchini Somalia.

Katika siku za hivi karibuni kundi la Alshabaab limebadili mtindo wake wa mashambulio kwa kutokabiliana na vikosi vya usalama moja kwa moja, badala yake vimekuwa sasa vikishambulia kambi za jeshi katika maeneo tofuati Somalia.

Wiki kadhaa zilizopita raia 10 waliuawa katika operesheni ya pamoja ya jesh la Somalia na Marekani katika eneo hilo.

Serikali ya Somalia ilidai kwamba si raia waliouawa bali ni wapiganaji wa Alshabaab, lakini baadaye ilibadili kauli na kuthibitisha kwamba ni wakulima na iliahidi kulipa fidia.

Shilole Hausiki Kuvunja Ndoa Yangu Bali ni Wazazi wa Nawal- Nuhu Mziwanda

$
0
0
Shilole Hausiki Kuvunja Ndoa Yangu Bali ni Wazazi wa Nawal- Nuhu Mziwanda
Mwanamuziki Nuh Mziwanda amekanusha suala linaloongelewa na watu kuwa kuvunjika kwa mapenzi kati yake na mzazi mwenzie chanzo chake siyo Shilole bali ni wazazi wa binti huyo.

“Unajua watanzania ukiwapa picha tu, basi wao wataandika maneno wataandika wenyewe Shilole hausiki hata kidogo kuvunjika kwa mahusiano yangu.”

“Wahusika ni wazazi wake ambae yeye aliamua kuwasikiliza wazazi wake kwa kuolewa na mtu mwingine na hatukuwa na ugomvi wowote ila ndio hivyo wazazi walikuwa na nguvu sana kunizidi mimi,” aliongeza.

Aidha Nuh Mziwanda aliongeza kuwa mahusiano yake ameyaweka kando na yupo kupambana na hali yake, lakini anashukuru Mungu mtoto wake bado anaendelea vizuri na anapata taarifa zote muhimu kumuhusu mtoto wake lakini mengine imebaki stori.

Mbunge Msukuma Kuanika Siri za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita

$
0
0
Mbunge Msukuma Kuanika Siri za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita
MBUNGE wa Geita Vijijini (CCM), Josephat Kasheku Musukuma, anajiandaa kuanika siri za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Lotson Mponjoli baada ya kushindwa kutimiza sharti lake la kumwomba radhi kutokana na madai ya kumdhalilisha.

Akizungumza na Nipashe jana, Musukuma alisema baada ya muda aliokuwa ametoa kwa kamanda huyo kuomba radhi kupita, ataweka hadharani madudu yote yanayofanywa na RPC huyo wiki ijayo atakapokuwa amerejea mkoani humo akitokea Zanzibar aliko kwa sasa.

"Niko Zanzibar naumwa na kwa leo (jana) sitaweza kulizungumza kwa kina hilo suala," alisema Musukuma ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na ambaye alikaa mahabusu kwa siku tatu kabla ya kufikishwa mahakamani Septemba 19.

Msukuma na wenzake nane wanakabiliwa na mashtaka manne ya jinai, likiwamo la kula njama.

"Nikirudi (Geita) tu nitaitisha mkutano na waandishi wa habari na kuweka hadharani yale niliyokuwa nimeyaahidi nilipozungumza wiki iliyopita."

Wiki iliyopita, Musukuma alimpa siku nne Mponjoli kumwomba radhi la sivyo ataweka hadharani alizodai kashfa zake, ikiwamo madai ya kujilimbikizia mali.

Musukuma alilalamikia hatua ya RPC huyo kumkamata katika mazingira aliyoita ya kumdhalilisha kwa kumshika suruali nyuma kama mhalifu, wakati yeye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Geita na mwakilishi wa wananchi.

Alisema RPC huyo asipoomba radhi ataanika hadharani alichoita maovu yake, ili vyombo vya uchunguzi kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), vianze kuchunguza.

Musukuma alimlaumu Kamanda huyo kwa kumkamata na kumweka mahabusu wakati angeweza kumwita na kuzungumza naye kwa staha kwa kuwa yeye ni kiongozi wa chama na mwakilishi wa wananchi.

"Tangu CCM iundwe mwaka 1977 mimi nimeweka rekodi ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza kuwekwa ndani na RPC wangu," alisema zaidi Musukuma na kulalamika zaidi:

"Nakwambia RPC kwa kuwa umenichokoza, na kwa kuwa umeamua kuingia kwenye hii ligi, basi jiandae. Umeliamsha dude na mimi nitaliamsha kwelikweli." Alisema kama Mponjoli anataka amani atafute wazee wanaomheshimu kama Mwenyekiti wa CCM na kwenda kuzungumza.

Aliwataka wakazi wa Geita kukaa mkao wa kusikiliza sababu za yeye kukamatwa na RPC huyo na kwamba vitu vyote ambavyo RPC huyo amewekeza mkoa wa Geita na mengine angetaja baada ya siku hizo. Amekuwa kimya hata hivyo.

Alipotafutwa kwa njia ya simu kupata maoni yake juu ya kauli hiyo ya Musukuma jana, Kamanda Mponjoli alisema yeye anazungumzia masuala ya jinai tu.

"Mkiniuliza mambo ya uhalifu nitawaambia, lakini hayo mambo anayosema Mbunge siwezi kuyazungumzia," alisema RPC Mponjoli.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita ilidaiwa washtakiwa, kwa pamoja, Septemba 13, mwaka huu, majira ya saa nne asubuhi katika ukumbi wa Gedeco unaomilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Geita, walipanga njama ya kuweka mkusanyiko usiokuwa na kibali, kuharibu mali na kuweka vizuizi katika barabara ya kuingia Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM).

Mbali na Musukuma ambaye pia ni Mbunge wa Geita, washtakiwa wengine ni Steven Werema (mkulima), Costantine Molandi, Winifrida Malunde, Ngundugu Joseph, Martine Kwilasa, Khadija Said, Maiko Kapaya na Maimuna Mengisi (wote madiwani).

Shtaka la pili Mwasinga alisema linawahusisha watuhumiwa nane kati ya tisa, ambapo alidai kwamba Septemba 14, majira ya saa 12 asubuhi katika kijiji cha Mtakuja, walifanya mkusanyiko usio halali.

Mwasinga alisema kuwa katika shtaka la tatu, Septemba 14, majira ya saa 12 asubuhi, washtakiwa hao nane walitenda kosa la kufunga barabara ya kuingia na kutoka GGM na kusababisha wafanyakazi wa mgodi na watu wengine kushindwa kutumia barabara hiyo.

Katika shtaka la nne, Mwasinga alidai mahakamani hapo kuwa Septemba 14, majira ya saa 12 asubuhi, washtakiwa hao nane kwa pamoja walitenda kosa la kuharibu bomba la maji katika kijiji cha Nungwe linalosafirisha maji kwenda GGM, hali iliyosababisha hasara ya Sh. milioni 12.25 na kupungua kwa huduma ya maji katika mgodi huo na kwa wananchi wa mji wa Geita.

Washtakiwa wote tisa kwa pamoja walikana mashtaka hayo huku mwendesha mashtaka wa serikali akiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa madai upelelezi haujakamilika.

Akiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 10, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ushindi Swalo alisema dhamana kwa washtakiwa hao iko wazi na kila mmoja alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh. milioni tano.

Washtakiwa walitimiza masharti ya dhamana na wote wako nje. Washtakiwa wanatetewa na mawakili Neema Christian na Deo Magengeli.

Nipashe

TFF Yaanika Viingilio Mechi ya Tanzanite Dhidi ya NIigeria

$
0
0
TFF Yaanika Viingilio Mechi ya Tanzanite Dhidi ya NIigeria
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka wazi viingilio vya mchezo wa marejeano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria itakayopigwa, Jumapili Oktoba mosi, mwaka huu.

Mashabiki wataingia kwenye uwanja wa Azam Complex kwa viingilio vya kawaida kushuhudia mechi hiyo timu ya taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ itakayocheza dhidi ya Falconets ya Nigeria.

Viingilio vitakuwa ni Sh. 500 tu kwa mashabiki watakaoketi eneo la mzunguko huku kwa wale watakaokaa jukwaa kuu (VIP) watalipia Sh. 1,000 tu katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam, Chamazi ulioko nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kocha wa Tanzanite, Sebastian Nkoma, amesema kwa namna alivyokiandaa kikosi chake ana imani kitaweza kupindua matokeo ya awali ambayo Tanzanite ililala mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Samuel Ogbemudian, ulioko Jimbo la Benin nchini Nigeria, wiki mbili zilizopita.

Serikali ya Denmark Kuendelea Kuwekeza Tanzania

$
0
0
Serikali ya Denmark Kuendelea Kuwekeza Tanzania
Balozi wa Denmark nchini Einar Jensen amesema Serikali ya Denmark itaendelea kufanya uwekezaji katika sekta ya afya, elimu na vita dhidi ya umasikini.

Balozi Jensen amezungumza hayo  mbele ya viongozi wa hospitali ya Marie Stopes iliyopo Mwenge wakati wa hafla ya ufunguzi wa hospitali hiyo ambayo imefanyiwa marekebisho.

Amesema Serikali ya Denmark kupitia Shirika la msaada la Denmark (Danida) itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto mbalimbali za jamii na uchumi.

"Tutaendelea kuwekeza kwenye sekta muhimu zaidi afya, elimu na vita dhidi ya umaskini. Lengo ni kuunga juhudi za serikali katika kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati," amesema Jensen.

Pia ameipongeza hospitali ya Marie Stopes kwa kuendelea kutoa huduma bora na za bei nafuu kwa wananchi ikiwemo huduma ya uzazi inayotolewa hospitalini hapo.

Balozi Jensen pia amezindua kitengo cha huduma kwa wateja kilichoanzishwa hospitalini hapo ambacho kinatoa fursa kwa wateja kupiga simu bure na kupata ufafanuzi kuhusu huduma zinazopatikana kwenye hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Marie Stopes nchini, Anil Tambay amesema marekebisho yaliyofanyika katika hospitali hiyo itaboresha utoaji wa huduma bora zaidi.

Hospitali ya Marie Stopes pia imeanzisha huduma ya upimaji bure wa magonjwa ya kansa, ukimwi ya siku tatu kuanzia leo mpaka Ijumaa mpaka Jumapili.

Apewa Siku 14 Seth Kupelekwa Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kutibiwa

$
0
0
Mahakama Yaamuru Seth Kutibiwa Katika Hospitali ya Taifa Muhimbil
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kwa mara nyingine mshtakiwa Harbinder Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ndani ya siku 14.
Korti imesema iwapo hilo halitatekelezwa, mkuu wa gereza afike mahakamani kujieleza. Sethi yupo mahabusu katika Gereza la Segerea.

Amri hiyo ya mahakama imetolewa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kudai kesi ilipangwa leo Ijumaa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, hivyo aliomba shauri lipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo, wakili Joseph Makandege anayemwakilisha Sethi alieleza kuwa kumekuwepo mfululizo wa amri za Mahakama zikiagiza mteja wake akapatiwe matibabu na kufanyiwa uchunguzi Muhimbili.
“Hadi leo asubuhi tuliwasiliana na mteja wetu na kubaini hajapelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kama amri za Mahakama zilivyoagiza, hivyo ni rai yetu kwamba kitendo hicho cha kutotekelezwa amri za Mahakama ni ukaidi wa amri halali za Mahakama yako tukufu,” amesema Makandege.

Amesema kwa kuwa upande wa mashtaka umekaidi amri za Mahakama, anaomba itoe adhabu inayostahili.
Makandege amesema kitendo cha upande wa mashtaka cha kutotekeleza amri za Mahakama kinasigana na kukiuka mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka .
“Mkurugenzi wa Mashtaka katika kutekeleza majukumu yake anapaswa kuongozwa na kutenda haki, lengo ni kutogeuza mashtaka ya jinai na mahakama kuwa ni vyombo vya utesaji,” amesema.
Ameomba Mahakama itoe adhabu stahiki kwa kuwa hilo linaonyesha dhahiri kuwa mashtaka yaliyopo ni ya hila yenye lengo la kuwaadhibu washtakiwa na hasa mshtakiwa wa kwanza Sethi kabla hawajahukumiwa.

Wakili Makandege ameiomba Mahakama iitupilie mbali hati ya mashtaka na kuwaachia huru washtakiwa ili Sethi apate wataalamu wa matibabu yake katika hospitali ikiwemo Muhimbili.
Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amedai tatizo limeshajitokeza katika utekelezaji wa amri za Mahakama.
Swai amedai Magereza wamekuwa wakiwatibu wafungwa na mahabusu hata pasipokuwa na amri ya Mahakama.
Amesema kilichojitokeza ni utaratibu wa kumpeleka Sethi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Tumejitahidi kuwasiliana na Magereza wapo katika hatua za mwisho, tunaomba muda wa ziada ili tuiwezeshe Magereza kukamilisha utaratibu wa kumpeleka Sethi Muhimbili, hatujakataa tunaomba muda,” amesema Swai.
Hakimu Huruma Shaidi amesema ni lazima amri za Mahakama zifuatwe. Ameahirisha kesi hadi Oktoba 13.
Amesema hadi siku hiyo, Sethi awe ameshapata matibabu na iwapo atakuwa hajapatiwa, mkuu wa gereza alipo afike mahakamani kujieleza.

Katika kesi hiyo, Sethi na James Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi wakidaiwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kighushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola 22,198,544.60 za Marekani na Sh309,461,300,158.27.
Wanadaiwa kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
CREDIT: MWANANCHI

MCT Kuwashtaki Watakaovunja Uhuru wa Habari

$
0
0
MCT Kuwashtaki Watakaovunja Uhuru wa Habari
Baraza la Habari Tanzania  (MCT) limesema litaanza kuwashtaki watakaovunja uhuru wa Habari ikiwamo kuwazuia waandishi wa Habari kupata taarifa, vipigo na matukio yote ya udhalilishaji dhidi yao.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa MCT, Ofisa Miradi wa Baraza hilo Pili Mtambalike amesema matukio hayo yanaongeza hofu na kuwafanya waandishi  washindwe kutimiza wajibu wao kikamilifu.

Mtambalike amesema pamoja na hatua nyingine wataanza kuwachukulia hatua ikiwamo kuwashtaki wale watakaofanya hivyo huku akiwaasa wanahabari kutoa taarifa vinapotokea vitendo vinavyokiuka uhuru wa habari.

"Tukio likitokea tutalichunguza na tukijiridhisha na tukio linaweza kupelekwa mahakamani tutashtaki," amesema.

Hata hivyo amesema kwa mwaka huu zaidi ya matukio 11 yameripotiwa ikiwamo lile la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuvamia kituo cha  TV cha Clouds.

Rais wa MCT, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema baraza hilo lilianzisha Rejista ya  Matukio ya Uvunjaji Haki wa Habari  (PFVR) ili kuhakikisha kila tukio linaripotiwa na kuchukuliwa hatua.

Amesema lengo ni kuhakikisha kunakuwa  na takwimu sahihi za matukio hayo ili wanapowasiliana na Serikali kuwe na mfano halisi.

Mkuu wa Wilaya Aagiza Pombe za Kienyeji Zitungwe Sheria

$
0
0
Mkuu wa Wilaya Aagiza Pombe za Kienyeji  Zitungwe Sheria
Unywaji wa pombe za kienyeji ambao wakati mwingine huambatana na baadhi ya wanywaji kufanya vurugu, ukatili wa kijinsia, uporaji na hata kujeruhi umemsukuma mkuu wa wilaya kuagiza itungwe sheria.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga ameziagiza halmashauri mbili zilizopo wilayani humo zitunge sheria ndogo za udhibiti wa kutengeneza, kuuzaji na kunywa pombe hizo ili kukomesha matukio ya aina hiyo yanayotokea kila mara.

Mofuga alitoa agizo hilo juzi kwenye mkutano na wananchi uliolenga kukomesha matukio ya kikatili yanayosababishwa na unywaji wa pombe za kienyeji.

Alisema yapo matukio mengi ya kikatili yanayotokea sehemu tofauti katika eneo hilo yanayosababishwa na pombe za kienyeji, hivyo suluhisho ni utungwaji wa sheria ndogo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema endapo halmashauri ya mji na ile ya wilaya zikitunga sheria ndogo, maeneo yaliyokithiri kwa pombe za kienyeji katika kata za Dongobesh na Sanu yatamalizika.

Alisema japo kuna sheria mama inayoongozwa na Katiba, kutungwa kwa sheria hizo kutapunguza matukio hayo.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri ya wilaya hiyo, Melkiore Miniko alisema pia utungwaji wa sheria hizo utapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya kifamilia.

Miniko alisema matukio ya kikatili yanasababisha na pombe haramu ya gongo na zingine za kienyeji zinazochangia kurudisha nyuma maendeleo.

Alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi ya ukatili kwa watoto na kutelekezwa familia kunakotokana na wazazi wengi kujiingiza kwenye unywaji wa pombe haramu, hivyo suluhisho ni kuwapo na sheria ndogo. Ofisa huyo alisema kuwa licha ya kuwapo kwa sheria ya leseni ya vileo, inapaswa kuongezwa sheria ndogo ili kupunguza madhara hayo kwa jamii.

Tanzia: CUF Yapata Pigo Kiongozi Wao Afariki

$
0
0
Tanzia: CUF Yapata Pigo Kiongozi Wao Afariki
Kiongozi wa CUF Mheshimiwa Ali Juma Suleiman ambaye alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa (CUF) Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa (CUF) Wilaya ya Magharibi A. Zanzibar amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja.

Baadhi ya viongozi wa (CUF) na wanachama pamoja na wananchi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja kufuatilia mwili wa Marehemu Ali Juma Suleyman.

Naibu Katibu Mkuu (CUF) Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa Mheshimiwa Ali Juma alikuwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja kufuatia kuvamiwa nyumbani kwake na kupigwa kisha baadaye kutupwa katika maeneo ya Masingini na makundi ya watu yanayoendesha vurugu Zanzibar.

"Nasikitika kutangaza kifo cha Mheshimiwa Ali Juma Suleiman, Kaimu Mwenyekiti wa CUF Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Wilaya ya Magharibi A. Amefariki dunia majira ya saa 4 usiku hapa jana hapa Mnazi Mmoja Hospital baada ya kupigwa vibaya na Mazombi juzi usiku" alisema Naibu Katibu Mkuu CUF Nassor Mazrui

Viongozi wa CUF wamesema kuwa mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi tayari na sasa wamekabidhiwa kwa ajili ya kufanya mazishi ambayo yatafanyika leo katika makaburi ya Mwanakwereke, nje kidogo ya mji wa Unguja. 

Lijualikali Aachiwa Ahojiwa na Polisa Kwa Saa Nne

$
0
0
Lijualikali Aachiwa Ahojiwa na Polisa Kwa Saa Nne
Mbunge wa Kilombero mkoani Morogoro, Peter Lijualikali ameshikiliwa na kuhojiwa na polisi wilayani Malinyi kwa saa nne.

Pamoja naye, viongozi wengine watatu wa Chadema walishikiliwa jana Alhamisi wakidaiwa kufanya mkusanyiko bila kuwa na kibali cha polisi.

Akizungumza leo Ijumaa baada ya kuachiwa mbunge huyo amesema aliamriwa na polisi  kusimama alipokuwa akitoka kwenye kikao cha ndani cha viongozi na baadhi ya wanachama wa Chadema katika Kijiji cha Makerere wilayani Malinyi.

“Nilipoamriwa kushuka kwenye gari nilitii na kuongozana na polisi hadi kituo cha i Malinyi ambako nilihojiwa kwa nini nifanye kikao bila kibali. Nikawaambia kilikuwa ni kikao cha ndani wakasisitiza kuwa ni lazima tuwe na kibali,” amesema Lijualikali.

Amesema hakuna sheria inayowataka kuwa na kibali wanapofanya vikao vya ndani kwa kuwa hawahitaji ulinzi wa polisi katika vikao hivyo na hapakuwa na uwezekano wa kutokea vurugu.

Mbunge huyo amesema alipoona anahojiwa muda mrefu aliamua kumpigia simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei aliyemweleza yupo likizo.

Amesema aliamua kumpigia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na kumweleza kilichotokea ambaye aliahidi kushughulikia suala hilo.

“Nashukuru baada ya kuongea na Mwigulu niliachiwa. Niliondoka kituoni hapo saa nne usiku tangu wanishikilie saa 12:00 jioni. Walinitaka kuripoti kesho yake (leo) saa mbili asubuhi na niliripoti wakaniambia niripoti tena Oktoba 5,” amesema.

Wengine waliokamatwa pamoja na mbunge huyo ni Mwenyekiti wa Chadema Malinyi, Emmanuel Lukindo; Katibu wake, Sadi Lyampawe na Katibu Mwenezi wa wilaya, Lucas Lyambalimu ambao wote wameachiwa kwa dhamana.

Lema Amuwakia Mwigulu Asema Hana Sifa ya Kuwa Waziri

$
0
0
Lema Amuwakia Mwigulu Asema Hana Sifa ya Kuwa Waziri
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemjia juu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  na kusema Waziri huyo hana sifa za kuendelea kuwepo katika wizara hiyo kutokana na kuwa na majibu mepesi kuhusu matukio ambayo yanagharimu maisha ya watu.

Lema amesema hayo leo alipokuwa jijini Arusha akiongea na waandishi wa habari na kusema amesikitishwa sana na majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu sakata la miili ya watu kuokotwa baharini na sakata la shambulio la Tundu Lissu pamoja na kupotea kwa Ben Saanane ambaye alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe

"Mwigulu Nchemba amenisikitisha sana kwa kauli zake alizokuwa anatoa na sidhani kama anastahili kukalia ile ofisi hata kwa masaa 12 na ni wito wangu kwa Mhe. Rais Magufuli na naamini itakuwa hivyo hawezi kumuacha Waziri kama huyu kwenye ofisi ya serikali inayoshughulika na mambo ya ulinzi na usalama wa watu, matumaini yangu yupo hapo kwa muda tu, toka utamaduni wa maiti za watu kuanza kuokotwa zimeokotwa maiti za watu wengi sana lakini unaona kauli ya Waziri ni kama watoto wameokota maembe, amesema hawana mpango wa kuleta wachunguzi kutoka nje kuja kusaidia polisi kuchunguza tukio la Tundu Lissu hiyo ni hofu sababu wanajua nini kipo nyuma ya jambo hilo" alisema Lema

Aidha Mbunge huyo amesema kuwa kitendo cha Waziri Mwigulu Nchemba kusema gari ambayo alikuwa anailalamikia Mbunge Tundu Lissu na yeye kusema gari hiyo imeonekana Arusha na haijawahi kutoka Arusha bila kuchukuliwa hatua yoyote ni jambo ambalo linaibua maswali mengine na kufanya wazidi kukosa imani na jeshi la polisi kuhusu kuchunguza sakata la Tundu Lissu.

"Gari ikiwa inatuhumiwa Waziri hasemi kuwa gari hiyo imeonekana Arusha na haijawahi kutoka Arusha ila gari ikiwa inatuhumiwa cha kwanza watu wanatakiwa kuwajibika lakini ukweli ni kwamba watu wanatumia namba feki kwa ajili ya matukio, jana Waziri anaongea vitu vyepesi mimi nasema siku za Waziri huyu kukaa pale kama Waziri wa Mambo ya Ndani siku zake zinahesabika na nyinyi mtaniambia, anasema hajui kama Ben Sanane amekufa au hajafa kama mpaka leo Waziri wa
Mambo ya Ndani hajui juu ya Ben Sanane kama amekufa au yuko hai polisi hawa tunasema hawawezi kuchunguza sakata la shambulio la Tundu Lissu ndiyo maana tunataka uchunguzi kutoka nje ya nchi waje kusaidia jambo hili" alisema Godbless Lema

Watu 22 Wafariki Katika Mkanyagano Kwenye Reli Mumbai

$
0
0
Watu 22 Wafariki Katika Mkanyagano Kwenye Reli Mumbai
Watu kumi na wawili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, kufuatia kisa cha mkanyagano baada ya daraja moja kuporomoka karibu na kituo cha treni, mjini Mumbai India.
Waliyoshuhudia wanasema, daraja hilo huenda liliporomoka kutokana mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati huo, hali ambayo iliwafanya watu kukimbilia mahala hapo kujikinga.
Mwandishi wa BBC mjini Mumbai, anasema mamlaka imekuwa ikilaumiwa kwa kutelekeza miundo mbinu katika mji huo licha ya kuwa mji huo unapokea watu wengi kila siku.

Watu waliojeruhiwa wamefikishwa katika hospitali iliyo karibu na maafisa wakuu wa reli wapo katika eneo la mkasa.
Msemaji wa shirika la reli Anil Saxena ameambia waandishi habari kuwa daraja hilo lililofunikwa lilikuwana shughuli nyingi kwasababu idadi kubwa ya wasafiri waliokuwa wanajikinga na mvua kubwa walijaribu kuondoka kwa wakatimmoja na abiria wengine.
Ameongeza kuwa mkasa huo utachunguzwa.

Ally Hapi Ashtushwa na Upungufu wa Wauguzi Mwananyamala

$
0
0
Ally Hapi Ashtushwa na Upungufu wa Wauguzi Mwananyamala
Changamoto ya Upungufu wa watumishi Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala imeelezwa kuwaelemea watoa huduma hali inayoathiri  huduma hospitalini hapo.

Hali hiyo imetokana na watumishi wakiwamo wauguzi  50 kuondolewa hospitalini hapo baada ya kubainika  kuwa na vyeti feki.

Hayo yamebainika leo, wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  Ally Hapi aliyetembelea hospitali hiyo kwaajili ya kukagua miundombinu pamoja kuzungumza na watumishi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Daniel Nkungu amesema, Hospitali hiyo ina watumishi 300 huku ikiwa na upungufu wa watumishi 200 hasa manesi na wauguzi.

"Wakati Hospitali hii inajengwa mwaka 1973 ilikuwa inatoa huduma kwa watu wachache lakini kumekuwa na ongezeko kubwa la watu hasa wajawazito na watoto," amesema

Amesema, idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na wagonjwa 2500 wanaofika kila siku Hospitalini hapo kwaajili ya kupata huduma.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ameahidi kufikisha suala hilo kwa Wizara ya Utumishi pamoja na Waziri wa Fedha kwaajili ya kuomba kuongeza watumishi hospitalini hapo.

"Inawezekana Vituo vyote vinakuwa treated bila kuzingatia idadi ya watu na mahitaji, mimi nimeona kuna shida," amesema Hapi

"Hospitali ya Mwananyamala inaweza ikawa inahudumia watu wengi kuzidi Hospitali ya Rufaa ya Bugando, tutaendelea kuwashauri viongozi wetu ili kwa sisi ambao tuna idadi kubwa ya watu tuongezewe watumishi," amesema Hapi

Aidha, amewataka kusimamia matumizi ya dawa na zinazotolewa na Bohari ya dawa(MSD) na kuonya watumishi wenye tabia ya kuziuza kwa wagonjwa
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images