Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Trump Aapa ''Kuikabili'' Korea Kaskazini Ziarani Bara Asia

$
0
0
Trump Aapa ''Kuikabili'' Korea Kaskazini Ziarani Bara Asia
Rais wa Marekani Donald Trump atasafiri kuelekea katika mataifa matano ya bara Asia mnamo mwezi Novemba ili kushiriki katika mikutano ya kieneo, Ikulu ya Whitehouse imetangaza.
Atazuru Japan, China, Korea Kusini, Vietnam, Ufilipino na Marekani ya Hawaii kwa ziara ya siku 11.

Ziara hiyo ya marais itaimarisha harakati za kimataifa kukabiliana na tishio la Korea Kaskazini, taarifa hiyo ya Whitehouse imesema.
Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni.

Je maswala muhimu ya rais Trump katika mikutano hiyo yatakuwa nini katika ziara yake ya kwanza bara Asia?
Taifa hilo ambalo limetengwa kiuchumi lilifanya jaribio lake la sita la kombora la kinyuklia mapema mwezi huu licha ya shutuma za kimataifa, imeahidi kufanya jaribio jingine katika bahari ya pacific.
Katika hotuba kwa Umoja wa Mataifa, bwana Trump ameahidi kuiangamiza Korea Kaskazini akisema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-Un ''anajihatarisha''.

Katika taarifa isiokuwa ya kawaida bwana Kim aliapa kumkabili rais huyo wa Marekani aliyedai kuwa na ''akili punguani kwa vita''.
Bwana Trump ataomba kuungwa mkono na majirani wa taifa hilo ikiwemo China kuendeleza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini.

Waziri Atoa Agizop Ataka Nyumba ya Mwekezaji Ibomolewe

$
0
0
Waziri Atoa Agizop Ataka Nyumba ya Mwekezaji Ibomolewe
Naibu Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, William Tate Olenasha ameagiza nyumba ya mwekezaji iliyojengwa kwenye mfereji wa kupeleka maji katika mashamba ya wakulima wa ushirika Ruvu ibomolewe haraka ili kuruhusu maji kumwagiliwa mashambani.

Naibu Waziri huyo alitoa, agizo hilo leo alipokuwa ametembelea shamba la mpunga la kilimo cha ushirika Ruvu (CHAURU) ambapo alielezwa kuwa kuna mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji wa kichina aitwaye Guo Ming Tang ambaye aliingia mkataba batili na uongozi wa awali wa ushirika huo mwaka 2012 kwa niaba ya  CHAURU.

Mwenyekiti wa CHAURU, Sadala Chacha amemweleza Naibu Waziri kuwa  mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu na kuwa kuziba mfereji huo kumesababisha ekari 24 kutokulimika  kwa miaka mitano na kusababisha upotevu wa  wastani wa kilo 236,000 za mpunga zenye thamani ya sh. 200,600,000.

Baada ya kuelezwa migogoro kadhaa kati ya wakulima na mwekezaji huyo, ikiwemo huo wa kuziba mfereji  na pia kuwauzia maji wakulima,ya kumwagilia kwa saa moja kwa bei ya sh. Laki moja naibu waziri alitoa maagizo kadhaaa  sambamba na kuvunjwa kwa nyumba hiyo ya mwekezaji.

Kauli ya Diamond baada ya ‘Hallelujah’ Kufikisha Views Milioni 1 Ndani ya Masaa 15

$
0
0
Kauli ya  Diamond baada ya ‘Hallelujah’ Kufikisha Views Milioni 1 Ndani ya Masaa 15
“Nyota njema huonekana asubuhi,” hilo limeanza kuonekana katika wimbo mpya wa Diamond, Hallelujah.

Msanii huyo wa WCB, kupitia mtandao wa Instagram ameonyesha kutoamini kwa kile kinachotokea kupitia wimbo wake huo baada ya kuweka rekodi ya kutazamwa zaidi ya mara milioni moja katika mtandao wa YouTube ndani ya masaa 15.

Lord have Mercy! I can’t even Explain how grateful i am…1 Million Youtube Views within 15 hours…..Thank you so much for this Love and Support…. Let’s take our African Music to the World….🙏
(Nawashkuru sana kwa Upendo, Sapoti na kuendelea kupokea kidogo changu niwapacho… Nawashkuru sana, Niwashkuru pia kwa kuifanya #Hallelujah kuwa imetizamwa mara Milioni 1 ndani ya Masaa 15….Tuendelee kushikana na kuupeleka Mziki wetu Duniani zaidi….🙏)


Lema Aomba Msaada kwa Rais Magufuli

$
0
0
Lema Aomba Msaada kwa Rais Magufuli
Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema amefunguka na kumuomba Rais Magufuli kuwasaidia askari polisi wa Arusha na Tanzania kiujumla kuwaboreshea makazi yao kwa kuwajengea nyumba bora kwani anadai polisi walio wengi wanaishi nyumba za hali ya chini sana

Lema alisema hayo jana na kusema kuwa ni aibu kubwa kuonekana polisi wanachangiwa pesa ili kuweza kufanya marekebisho katika nyumba ambazo ziliteketea kwa moto juzi jijini Arusha.

"Mimi ni wito wangu kwa askari polisi pamoja na mchango wake kwa polisi hao lakini namwambia tu askari polisi nchi nzima wanaishi kwenye nyumba zenye hadhi ya chini sana, serikali inaweza kufanya 'commitment'ikajenga nyumba za maana maghorofa na askari wote wanaoishi mtaani wakarudi kuishi hapo, ni aibu kwa jeshi la polisi kutembeza kibaba kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga nyumba za askari polisi hao watu wanakesha usiku na mchana kulinda usalama wa watu na mali zao hawa watu hawatakiwa kufanyiwa 'donation'" alisema Godbless Lema

Aidha Mbunge huyo anasema yeye anaamini serikali inaweza kuchukua jukumu la kujenga nyumba za polisi Arusha tena kwa haraka kama ambavyo Rais Magufuli aliamua kujenga hostel za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kipindi kifupi sana. 

Natamani Kupata Mimba Ila Simtamani Atakayenipa- Snura

$
0
0
Natamani Kupata Mimba Ila Simtamani Atakayenipa- Snura
Msanii wa bongo fleva, Snura Mushi maarufu kama Malkia wa uswazi ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa 'zungusha' amefunguka na kudai anatamani kupata ujauzito ila hamtamani atakayempa.

Snura ameeleza hisia zake hizo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram asubuhi ya leo na kufanya kuwashangaza watu kwa kile alichokiandika, huku wengine wakitaka kupatiwa wao nafasi hiyo ya kumpatia ujauzito.

"Nimetamani mimba ila sijamtamani mwenye kunipa mimba", ameandika Snura.
Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kutoa kauli kama hizo kwani hapo awali alishawahi kusema pia anatamani kumpatia mwanaume atakaye funga naye ndoa watoto wawili ili aweze kukamilisha idadi ya watoto wanne ambao ni ndoto yake aliyekuwa nayo.



Article 13

$
0
0
Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili
 08:14

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE.

Zamaradi Ambwaga Bosi wa Clouds, Aolewa na Mwanaume Mwingine

$
0
0
Mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema amefunga ndoa wiki hii na kijana anayedaiwa kuwa ni mtoto wa kigogo.

Mrembo huyo ambaye ni mama wa watoto wawili, amepost picha akiwa mtandaoni akiwa na mwanaume huyo aliyefunga naye na kuandika ujumbe wa kumshukuru mungu.

“ALHAMDULILLAH!!,” aliandika Zamaradi baada ya kupost picha hiyo hapo juu.
Rafiki wa karibu wa Zamaradi, Faiza Ally amempongeza rafiki yake huyo kwa kumtakia maisha marefu katika ndoa yake.


“Bismalah mashallah @zamaradimketema ndoa yako iwe ya kheri Inshallah,” aliandika Faiza Ally.
Wadau wa mambo wanadai mume wake huyo ni mtoto wa Kigogo mzito na inadaiwa wamekuwa pamoja kwenye mahusiano kwa miaka kadhaa sio wa kukurupukia ndoa kama wengine wanavyodhani.

JE Wajua Mayai yasipoiva ni Hatari

$
0
0
Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips.

Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri.
Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai.

Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza.

Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaiva nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu.

Hata ukienda kwa wakaanga chipsi, utakuta wanawauliza wateja wao kama wanapokaanga na mayai wakaushe au wasikaushe. Hii inaashiria kuna watu wanataka wale chipsi zikiwa na mayai ambayo halijaiva sawasawa.

Kuna watu wengine wanaamini kwamba kula mayai mabichi kunafanya sauti inakuwa nyororo, hivyo wale waimbaji huwalazimu kufanya hivyo ili kufanya nyimbo zao zivutie.

Si hivyo tu, kuna baadhi ya watu huamini pia dawa ya kikohozi ni kunywa yai bichi lililochanganywa na asali. Hizi ni imani ambazo zimejengeka kwenye jamii na watu hufanya hivyo ili kufikia malengo waliyokusudia.

Katika siku za karibuni, imevuma kuwa mayai ya kwale yanatibu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na kifua.

Katika mpango huo, wanapendekeza wahusika kula mayai mabichi ya kwale tena kwa kutafuna hadi kaka lake, yaani ganda la nje.

Hali hii imesababisha biashara ya mayai ya kwale kuwa kubwa na hata wafugaji wameongezeka mara dufu.

Serikali Yapata Msaada wa Bilioni 29.4 Kutoka China

$
0
0
Serikali Yapata Msaada wa Bilioni 29.4 Kutoka China
Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi 29.4bilioni kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu, utalii wa kijiolojia na kuukarabati Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong.

Katibu huyo amesema 22.4bilioni  zitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera.
“Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” amesema   James
Ameeleza kwamba  kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho.

“Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu wake watakaochangia kukuza sekta ya uzalishaji na hatimaye kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini” amesema  James
Katibu Mkuu huyo amesema China, itatoa 6.7bilioni kwa ajili ya kuukarabati Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.

“Katika makubaliano yetu ya msaada wa kuendeleza Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000, China itatoa msaada wa kiufundi na vifaa vya kisasa vya michezo na utaalamu katika usimamizi na ukarabati wa uwanja” Amefafanua James
Amesema  kiasi kingine cha shilingi 300milioni zitatumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuanzishwa kwa aina mpya ya utalii ujulikanao kama utalii wa kijiolojia “Geopark Project” katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, mkoani Arusha.

Alisema lengo la utafiti huo ni kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika na maajabu mbalimbali ya kitalii yaliyopo nchini ambayo hayajatumika kikamilifu kuvutia watalii watakaoongeza pato la Taifa
“Tanzania ina kila sababu ya kujifunza kutoka katika Hifadhi ya Kimataifa ya Jiolojia ya Jiaozuo ya Yuntaishan ya China, iliyoanzishwa mwaka 2000 ambayo inaongeza asilimia 37.2 ya watalii kila mwaka na huchangia asilimia 12 ya pato la Taifa la nchi hiyo”
Tangu miaka ya 1960 mpaka sasa nchi hiyo imeendelea kuisaidia  Serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo upanuzi wa Chuo cha Polisi Moshi, Ujenzi wa Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong, amesema ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Veta huko Ngara mkoani Kagera utaanza haraka kama ilivyopangwa.
Kuhusu masuala  ya utalii wa kijiolojia katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, amesema Tanzania ina bahati ya kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini haijavutia idadi kubwa ya watalii kutoka China kuja kuvitembelea.

“Zaidi ya watalii milioni moja kutoka China wanatembelea nchi mbalimbali dunia lakini kati ya hao, Tanzania inapokea watalii 20,000 tu kila mwaka kutoka China, lakini kwa kuanzisha mradi huu, watalii wengi kutoka China watavutiwa kuja nchini kufurahia utalii wa miamba, mandhari nzuri, urithi wa dunia, na kutembelea hifadhi za Taifa” ameongeza Haodong
Akizungumzia masuala ya uchumi, Balozi huyo amesema  hivi sasa China imekuwa mwekezaji mkubwa zaidi nchini Tanzania kwa kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani 1.77bilioni  na kukuza ajira nchini.

Ameitaja baadhi ya miradi mikubwa iliyowekezwa kuwa ni pamoja na mradi wa miundombinu ya mtandao (Tanzania ICT broadband backbone), Bomba la gesi la kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, mradi wa kuboresha miundombinu ya bandari ,barabara na madaraja.

Waziri wa Afya Ajiuzuru

$
0
0
Waziri wa Afya Ajiuzuru
Waziri wa afya nchini Marekani, Tom Price amejiuzulu baada ya kukodi ndege binasfi ikiwa ni kwa ajili ya shughuli za kiserikali.

Waziri Price aliomba radhi kwa kufanya safari akitumia ndege za kukodi mara 26 tangu mwezi May kwa gharama za dola za kimarekani 400,000 zikiwa ni fedha za walipa kodi nchini humo.
Nchini Marekani maafisa wa serikali isipokuwa wale wanaoshughulikia masuala ya usalama wanatakiwa kutumia ndege za abiria katika safari za kikazi. Habari zinasema mawaziri wengine watatu katika utawala wa Trump wanachunguzwa kwa kutumia ndege binafsi za kukodi kwa shughuli za serikali.

Taarifa ya Ikulu imesema Rais Trump ameridhia kujiuzulu kwa Price na tarifa hiyo kuainisha kwamba Don J Wright atakaimu nafasi hiyo kwa sasa Wright ni Naibu Waziri wa Afya katika serikali hiyo.

Rais wa Zanzibar Dkt. Shein Amefanya Uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu

$
0
0
Rais wa Zanzibar Dkt. Shein Amefanya Uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu
Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 94(2) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais Shein amewateua Khamis Ramadhan Abdalla na Aziza Iddi Suweid kuwa majaji wa Mahakama hiyo.

Pia, amemteua Kubingwa Mashaka Simba kuwa Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mujibu wa uwezo wake chini ya Sheria ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 4 ya 2015, kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 4 ya 2017, Kifungu cha 10(a)(1).

Katika uteuzi mwingine, Rais Shein amemteua George Joseph Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala  Bora anayeshughulikia masuala ya Katiba na Sheria.

Dk Shein chini ya kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya 1997, amemteua Kapteni Juma Haji Juma kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari.

Serikali Yapiga Marufuku Watu Kusafiri

$
0
0
Serikali Yapiga Marufuku Watu Kusafiri
Serikali ya Cameroon imepiga marufuku mikusanyiko ya wazi pamoja na kusafiri katika jimbo ambalo wakazi wake wengi hutumia lugha ya kingereza kuongea, kuelekea maandamano ambayo yamepangwa kufanyika kesho ya kutaka kujitenga kwa eneo hilo.

Jimbo hilo la kusini magharibi lililopo mpakani mwa Nigeria limezuiwa pia kwa watu kuingia ambao wanaonekana kuwa ni tishio kwa umoja wa taifa hilo la Cameroon.
Maandamano ya kuunga mkono ya kujitoa kwa jimbo hilo yamepangwa kufanyika kesho ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 56 ya umoja wa Cameroon, kwa kile kinachodaiwa kwamba watu wanaoongea kiingereza wengi wao wamekuwa wakibaguliwa kutopata nafasi kubwa za ajira serikalini na kwamba lugha ya kifaransa na mfumo wa kisheria imewekwa dhidi yao kuwa kandamiza.

Japan Kuja na Teknolojia Mpya Kuleta Gari za mbao

$
0
0
Japan Kuja na Teknolojia Mpya Kuleta Gari za mbao

Ikiwa nchi mbalimbali duniani zimeanza kufanya utafiti wa kutengeneza magari yasiyotumia mafuta, Japan pia imeanza kufanya utafiti wa kutengeneza magari ya mbao ngumu.

Hili linategemewa kuanza kufanyiwa utekelezaji kuanzia miaka 10 ijayo ikiwa ni pamoja na tafiti kuhusu kutengeneza magari ya material ya plastic ambayo yatakuwa rafiki kwa joto na kuchukua nafasi ya magari ya metali.

Wataalamu wanaeleza kuwa lengo kubwa ni kupunguza uzito wa magari pamoja na athari za hewa chafu na kelele ambapo watafiti katika Chuo Kikuu cha Kyoto wameeleza kuwa mbao kwa karne nyingi imetumika kutengeneza meli, nyumba na mengineyo na hivyo gari hizo za mbao zitakua na ubora uleule kama magari ya metali lakini yatapungua uzito kwa asilimia 80.

Jukwaa la Kitaifa La Wadau wa Rasiliamali za Mji Kuzinduliwa

$
0
0
Jukwaa la Kitaifa La Wadau wa Rasiliamali za Mji Kuzinduliwa
Wizara ya Maji na Umwagiliaji inatarajia kuzindua jukwaa la kitaifa la wadau wa sekta mtambuka katika usimamizi wa rasilimali za maji.

Jukwaa hilo litazinduliwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge Jumatano Oktoba 4 jijini hapa.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo katika taarifa amesema uzinduzi huo umeandaliwa na wizara kwa kushirikiana na Taasisi ya 2030 Water Resources Group.

Amesema baada ya uzinduzi kitafanyika kikao cha kwanza cha jukwaa Oktoba 5 ambacho kitajadili changamoto za usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji nchini.

Dk Mkumbo amesema kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ni fursa ya kubadilishana uzoefu na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia na hasa kuhusu utekelezaji wa mipango ya pamoja ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji.

Amesema jukwaa linatarajiwa kutoa ushauri kwa wizara kuhusu namna bora ya kuboresha ushirikiano baina ya sekta mbalimbali katika usimamizi wa rasilimali za maji, hivyo kurahisisha uamuzi wa Bodi ya Maji ya Taifa na Bodi za Maji za Mabonde.

Jukwaa hilo pia litatoa mchango wa mambo ya kupewa kipaumbele na Kituo Mahiri cha Rasilimali za Maji kinachotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.

“Jukwaa litahusisha wadau na washirika mbalimbali wa maji kujadili, kuchangia mawazo na kubuni njia zitakazowezesha upatikanaji na usalama wa maji,” amesema.

Amesema jukwaa litawezesha wadau kujifunza, kutoa maoni, ujuzi na kushauri kuhusu masuala ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji nchini.

Chimbuko la kuanzishwa jukwaa hilo ni kutokana na changamoto zinazotokana na uratibu hafifu wa sekta, taasisi na wadau katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji.

Changamoto hizo zimesababisha kupungua na kukauka kwa vyanzo vya maji na kuongezeka kwa migogoro kutokana na ongezeko la mahitaji ya maji kwa shughuli za kiuchumi.

Fid Q Namba Nyingine Kabisa Hakuna Wimbo Wake Nisio Ujua- Wolper

$
0
0
Fid Q Namba Nyingine Kabisa Hakuna Wimbo Wake Nisio Ujua- Wolper
Muigiza wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameeleza mahaba yake ya kimuziki kwa rapper Fid Q.

Akizungumza na Planet Bongo ya EA Radio Wolper amesema amekuwa akifuatilia muziki wa Fid Q toka mwanzo msanii na huyo hajawahi kutoa wimbo kwake ukawa mbaya.

“Fid Q namba nyingine kabisa, namba chafu yaani ni mtu ambaye namkubali sana, nina ngoma zake toka anaaza muziki hadi ya jana Fresh,” amesema Wolper.

“Hakuna wimbo wa Fid ambao siujui na ambao siupendi napenda ngoma zake zote, sijawahi kuchukia ngoma yake hata moja na ninafikiri actually anajua,” ameongeza.



Zitto Afunguka Juu ya Mauaji Aitaka Polisi Kufanya Uchunguzi wa Kina

$
0
0
Zitto Afunguka Juu ya Mauaji Aitaka Polisi Kufanya Uchunguzi wa Kina
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amelitaka Jeshi la Polisi kufanyia uchunguzi wa kina matukio ya kiuhalifu yanayopelekea kuuawa kwa viongozi kwa madai kitendo hicho kinakaribisha siasa ya damu kuzoeleka katika taifa

Zitto amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalum wa facebook baada ya kupita siku moja tokea aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa (CUF) Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa (CUF) Wilaya ya Magharibi A. Zanzibar, Ali Juma Suleiman kufariki dunia katika hospitali ya Mnazi Mmoja kutokana na kile kinachoelezwa kuwa alivamiwa nyumbani kwake na kupigwa kisha baadaye kutupwa.
"Kuuawa kwa ndugu Ali Suleiman, Katibu wa Habari na Uenezi CUF, Wilaya ya Magharibi ni tukio lingine la kulaaniwa vikali. Kukalia kimya matukio ya namna Hii ni kukaribisha siasa ya damu kuzoeleka katika nchi yetu", amesema Zitto.
Pamoja na hayo Zitto ameendelea kwa kusema "Uchunguzi wa kina ufanyike kukomesha matukio ya namna hii, hakuna damu ya mtanzania inapaswa kumwagika kwa sababu ya siasa. Nawapa pole ndugu zetu wa CUF na wanazanzibar kwa msiba huu", amesisitiza Zitto.


Ushauri: Kila Nikirudi Nyumbani Nakuta Msichana wa Kazi Anaangalia 'Porn'

$
0
0
Mimi nimeoa na ninaishi na mke wangu lakini hatujabarikiwa kupata mtoto na wote tunafanya kazi mke wangu serikalin na mimi kwenye kampuni moja hapa mjini Dar kutokana na ubize wa kazi tuliamua kutafuta mfanyakazi na hivyo kuletewa huyu mdada wa kazi kutoka kijijini kwao na mke wangu, na mimi na mke wangu hua tunatoka asubui na kurudi jioni hua nampitia kazini tunarudi nyumbani baada ya kazi.

Huyu mdada wa kazi mke wangu alishanieleza kua anatoka kwenye mazingira magumu sana hivyo pamoja na kutufanyia kazi tuwe tunawakumbuka wazazi wake kwa chochote pale tunapojaliwa uwezo na mm nimekua nikifanya hivyo kama msaada kwa wazazi wa huyu binti.

Kilichofanya niombe ushauri kwenu ni kwamba, miezi miwili iliyopita nilisahau document za kazini nyumbani hivyo nilirudi kuzichukua kitu ambacho si kawaida mimi kurudi nyumbani mchana, kitu cha kushangaza nilimkuta huyu binti wa kazi ameweka mkanda wa porn(X) anaangalia na yupo exited aliponiona akashtuka sana na kuniomba msamaha basi mimi nikachukua nilichokua nimesahau na kurudi kazini kwangu huku nikiacha nimemkanya na kuchukua ile CD na kuiharibu.

Sikumwambia mke wangu kwani yeye hua na hasira sana na kwa hali ile angemrudisha huyu mtumishi wetu wa ndani kwao, sikumwambia kwa sababu huyu binti hana msaada wowote na wazazi wake wana hali mbaya huko kijijini nilijua mke wangu akimfukuza ataenda kuteseka sana kwahiyo nikawa na siri moyoni as a man.

Cha kushangaza ni kwamba leo pia nimerudi nyumbani gafla nimemkuta anafanya mchezo ule ule kaweka CD ya X amejiachia kwa sofa amerelax anaangalia hana wasiwasi huyu binti wa miaka 16 aliponiona akapanic na kulia nimsamehe tena nikampa vibao viwili nikachukua kilichonipeleka then nikarudi kazini.

Hapa najiuliza ndugu zangu nimwambie mke wangu kwa maana atamtimua tu, au nimuonee huruma niendelee kumfichia siri kwa mke wangu kwani nikikumbuka wazazi wake na huyu binti wanavyonililia na kuniona tegemeo lao moyo unarudi nyuma.

Sasa hivi niko na mke wangu tunarudi nyumbani huku kichwani najiuliza kama nimwambie kinachoendelea au laa.

Msaada wa ushauri bila matusi nitauzingatia zaidi.

NASHUKURU

Petit Man afunguka ishu ya Kutoka Kimapenzi na Mobetto (Video)

$
0
0
Memeja wa County Boy, Billnass pamoja na wasanii wengine wa label ya LFLG, Petit Man amefunguka kwa kudai picha zilizosambaa mitandaoni zikimuonyesha akiwa na Hamisa Mobetto ni picha zake za zamani sana huku akidai picha hizo zilisambazwa kwa lengo baya. Petit ambaye amemuoa mdogo wake Diamond, Esma na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, wamerudiana hivi karibuni na baada ya wawili hao kutengana kwa muda.

VIDEO:

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa leo

$
0
0

Ndoa ya Zamaradi Yazua Gumzo Mitandaoni

$
0
0
Ndoa ya Zamaradi Yazua Gumzo Mitandaoni
Ndoa ya mtangazaji wa kipindi cha Take One kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds, Zamaradi Mketema imezua mijadala mtandaoni, huku wengi wakihoji iwapo ni kazi mpya ya sanaa ya mwandaaji huyo wa filamu ya Kigodoro.

Hata hivyo, taarifa zilizosambaa mtandaoni tangu usiku wa kuamkia leo Jumamosi zinaeleza mtangazaji huyo ameolewa na ndugu wa karibu wa kiongozi katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Zamaradi kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha ya harusi yake, huku sura ya bwana harusi ikiwa haionekani vizuri na kuandika 'Alhamdulilah'.

Katika mitandao baadhi ya watu wamepongeza mtangazaji huyo huku wengine wakionyesha kushangazwa na tukio hilo kwa madai kuwa limekuwa ni la muda mfupi.

Rafiki wa karibu wa mwanadada huyo, Faiza Ally amempongeza kupitia ukurasa wake wa Istagram kwa kuandikia, “Ndoa yako iwe ya kheri Inshaallah.”

Mwingine aliyetuma ujumbe ni Jumalokole2 aliyeandika kupitia ukurasa wake wa Istagram akisema, “Wanawake wote mnapaswa kumuiga @zamaradimketema nimependa sana sema nyie mwalimu wenu......mwenzenu katumia fursa ..kaacha mbili kaifuata 6.”

Baadhi ya wasanii nchini wamempongeza kupitia mitandao ya kijamii. Msanii wa filamu Johari Chagula ameandika kwenye mtandao wa Instagram akisema, “Hongera sana Zama Mungu akuongeze vyema katika maisha mapya hakuna kitu kizuri kama amani ya nafsi furaha ya moyo, hakika hakuna kinachoshindikana chini ya jua, Nina hakika nitafuata nyuma.”
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images