Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Mapya yaibuka Familia ya Tundu Lissu na Bunge

0
0
Mapya yaibuka familia ya Lissu na BungeWakati Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi, familia yake imefanya kikao cha siri na uongozi ya Bunge kujadili matibabu ya mbunge huyo.

Kikao hicho kimefanyika leo Jumatatu jijini Dar es Salaam na imeelezwa kimehudhuriwa na Spika Job Ndugai, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, Mbunge wa Hanang’, Dk Mary Nagu na ndugu watatu wa Lissu, wanaume wawili na mwanamke mmoja.

Baada ya kupata taarifa za uwepo wa kikao hicho Mwananchi iliweka kambi nje ya Ofisi Ndogo za Bunge tangu saa 3:55 asubuhi na kushuhudia shughuli za kawaida zikiendelea huku kukiwa na watu wachache wanaoingia na kutoka ndani ya ofisi hizo.

Ilipofika saa 7:40 mchana, alitoka Mbatia akielekea kwenye gari lake baada ya kumaliza kikao hicho. Mwandishi alimfuata kujua kilichojiri ndani ya kikao hicho, Mbatia alikiri kuwepo kwa kikao hicho lakini hakutaka kuzungumza lolote na kuelekeza aulizwe Spika Ndugai.

“Ni kweli tulikuwa kwenye kikao na familia ya Lissu, lakini siwezi kusema tumezungumzia nini.  Kwa taarifa zaidi nendeni kwa Spika au Katibu wa Bunge, walikuwepo pia ndugu zake watatu, wafuateni wanaweza kuwaeleza,” alisema Mbatia.

Msemaji wa familia ya Lissu, Alute Mughwai alipotafutwa alisema kikao hicho kimefanyika kati ya familia na uongozi wa Bunge kuhusu mambo yanayomhusu Lissu, hata hivyo alisema hakijakamilika kwa sababu ya kukosekana kwa upande wa Chadema.

Mughwai alisema kikao hicho kimeahirishwa mpaka wakati mwingine pande zote zitakapotimia ili kulijadili suala hilo kwa ukamilifu wake. Alisema Chadema kupitia kwa mwenyekiti wake Freeman Mbowe walipewa mwaliko lakini hawakuweza kufika.

“Siwezi kukwambia tumezungumzia nini, moja ya masharti tuliyopeana ni kutokusema hadharani mambo tuliyoyajadili lakini yanamuhusu Lissu. Wote ‘interest’ yetu ni kuona Lissu anapona na kuendelea na majukumu yake kama kawaida,” alisema Mughwai.

Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Spika wa Bunge pamoja na Katibu wa Bunge zilishindikana baada ya simu zao kuita bila kupokelewa.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alipoulizwa kuhusu kikao hicho amesema taarifa kuhusu kikao hicho zilipelekwa Ofisi ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na siyo kwenye chama.

Biashara ya Kununua Madiwani Hata Iringa ilifanyika – Mhe. Peter Msigwa

0
0
Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa amesema jimboni kwake pia biashara ya wabunge wa Chadema kununualiwa na CCM ilifanyika hivyo Mkurugenzi wa TAKUKURU, Valentino Mlowola kufungua jalada.

Akizungumza nae leo nje ya Ofisi za TAKUKURU, Mhe. Msigwa alieongozana na Wabunge Nassari na Lema kuingia katika ofisi hizo amesema wahusika wakuu ni RC na DC na baadhi ya polisi wanahusika na biashara hiyo.

“Kwa kifupi iringa mjini nako biashara ya kununua madiwani ilifanyika na nina ujasiri mkubwa mhusika mkuu ilifanyika na nina uhakika biashara ya kuwa nunua madiwani Iringa mjini ni ofisi ya RC pamoja na DC na baadhi ya mapolisi kwahiyo hii ilikuwa ni episode mliona ya Arusha vilitumika vifaa vyua Uingereza lakini kwetu sisi tulitumia vifaa vya Australia na sisi tutafungua jalada kama Mkurugenzi wa TAKUKURU alivyotushauri,” amesema Msigwa.

“Kwahiyo tusubiri kwasababu tumekabidhi kwenye korido za serikali na tunataka sheria ichukue mkondo wake ili uongo uongo wa kusema kuna watu wanmaunga mkono utendaji tunataka ufike mwisho ili watu wakae kwenye nafasi zao kwa haki na jinsi watu walivyopamua kuwa na kuwa chagua kwa kifupi ndo hivyo.”

Siamini Kwenye Kujichubua – Vanessa Mdee

0
0
Msanii wa Bongo Flava, Vanessa Mdee amedai kuwa haamini katika kujichubua ili kubadili rangi ya ngozi yake.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Kisela’ ameiambia Dj Show ya Radio One wengi wanaofanya hivyo ni wale waliokosa kujiamini.

“Mimi kama Vanessa siamini kwenye kujikoboa, kujichubua au kujibadilisha kwenye rangi yako ya kawaida au mwili wako wa kawida am belief in temporary, so ukaweka make-up au nywele kuongeza hiyo ni kitu temporary ambayo ukiamua usiku unatoa lakini vile vitu vya kufanya moja kwa moja siviamini,” amesema Vanessa.

“Na pia ile ishu ya confidence, mtu ukiwa in secured inaweza ukafanya hivyo vitu ukiwa unataka kujiboresha au kujiridhisha mwenyewe ukidhania ukijibadilisha utakuwa bora zaidi but I don’t think I need to do that,” ameongeza.

Vanessa ameendelea kwa kusema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na imani yake na dini imekataza na anachofanya yeye ni kumshukuru kwa hatua aliyofikia sasa.

Elizabeth ‘Lulu’ Michael Amepata Dili Nono

0
0
Malengo ya Diamond Platnumz yanazidi kutimia kila kukicha. Moja wapo ni kuhakikisha kuwa jina lake linavuka kutoka kujulikana Afrika na kutambulika kwenye mabara mengine hasa Ulaya na Marekani.

Ikiwa Jumatatu hii ya Octoba 2, ni siku ambayo msanii huyo anasherekea siku yake ya kuzaliwa, taratibu ameanza kupata tobo, mtandao maarufu ambao unaonyesha siku ya kuzaliwa ya mastaa wakubwa duniani, Famous Birthday umempa shavu muimbaji huyo wa Hallelujah.

Mtandao huo umeonyesha kuwa Diamond amezaliwa siku moja na mastaa wengine kama Mahatma Gandhi ambaye ni kiongozi wa kukumbukwa aliyepigania uhuru wa India, Roberto Firmino (mchezaji wa Liverpool), Sting (mwanamuziki wa Rock), Kelly Ripa (mtangazaji wa runinga), Lene Nystrom (mwanamuziki wa Pop) na wengine.

MAKALA: Fahamu utofauti uliyopo kati ya VEVO na YouTube

0
0
Kumekuwa na maswali katika mitandao ya kijamii hususani hapa Tanzania kuhusu msanii kutumia akaunti ya VEVO au ya YouTube huku wengi wakienda mbali kuwa YouTube kuna ujanja mwingi kuliko VEVO kuanzia mfumo wake wa kupata views.



Hapa chini nimeorodhesha vitu ambavyo bila shaka vitakusaidia kuelewa utofauti uliopo na jinsi mitandao hii inavyofanya kazi.

 

Website ya YouTube imeanzishwa mwaka 2005 na mmiliki wake ni kampuni ya Google wakati website VEVO imeanzishwa mwaka 2009 na inamilikiwa na Sony Music Entertainment, Universal Music Group na Abu Dhabi Media.

Je, ukiwa Tanzania unaweza kuingia VEVO kama unavyoingia YouTube?

Ukweli ni kwamba hauwezi kuingia moja kwa moja kwenye website ya VEVO (vevo.com) kama unavoingia kwenye website ya YouTube (youtube.com). Hii ni kwa sababu vevo haijaanza kufanya kazi Tanzania wakati YouTube inapatikana karibia nchi zote duniani labda zile ambazo serikali imezuia mtandao huo kwa sasa vevo inafanya kazi nch i 20 tu duniani nazo ni Australia, Brazil, Canada, China,Ufaransa, Germany, India, Ireland, Italia,Japani, Mexico, Uholanzi, New Zealand, Poland, Korea Kusini,Hispania, Thailand, Uingereza na Marekani.



Je, ni watu gani wanaotumia mitandao hii mikubwa duniani?

Mtandao wa YouTube kwa sasa unatumiwa na kila mtu (Wasanii, Makampuni, na Wafanyabiashara) na kujiunga ni rahisi ili mradi uwe na barua pepe ya G-mail lakini ni tofauti na VEVO ambapo ni Wasanii/Wanamuziki pekee ndio wanatumia mtandao huo kwa kuweka kazi zao hivyo usitarajie kuingia kwenye mtandao wa VEVO na kukuta video za vichekesho au video za maelekezo kama ilivyo YouTube.

Faida na hasara ya msanii kutumia akaunti ya VEVO au YouTube.

Kwanza kaa ukijua kuwa YouTube ndio mtandao mkubwa na wenye watu wengi duniani kuliko VEVO na ndiyo maana VEVO wakachukua uamuzi wa kufanya kazi pamoja na Youtube mwaka 2010 baada ya kugundua kuwa wangeendelea kufanya kazi kivyao basi wangekuwa na watazamaji wachache.

Kwa hiyo kabla ya kuangalia uzuri wa msanii kujiunga na VEVO inakupasa uelewe hilo kuwa kusingelikuwepo kwa makubaliano ya kibiashara kati ya YouTube na VEVO basi mtandao unaoitwa VEVO usingepata hata umaarufu tunaouzungumzia leo. Kwa hiyo mtandao wa VEVO ulijiunga na YouTube kwa makubaliano ya kibiashara, na hii ndiyo maana hata VEVO wenyewe wana akaunti yao ndani ya mtandao wa YouTube.



1-Faida ya msanii kuwa VEVO ni kwamba atasaidiwa nyimbo zake kupigwa promo na VEVO wenyewe kwa sababu hao wapo kibiashara zaidi wakati YouTube hawafanyi hivyo badala yake msanii anategemea ukubwa wa mashabiki wake yaani (Subscribers).

2-VEVO wanabana uhuru wa msanii wa kuposti videos ambazo sio rasmi kama matamasha yao au hata video za behind The Scene hao wanataka (Official Release Videos) wakati kwenye mtandao wa YouTube msanii anakuwa huru kuposti videos zozote alizorekodi ilimradi zisivunje sheria zilizowekwa na YouTube. Na hapa ndio maana kuna baadhi ya wasanii wanaotumia akaunti za VEVO wanalazimika kuwa na akaunti mbili yaani akaunti ya Youtube na VEVO ili wapate uhuru wa kuposti matukio mbalimbali . Mfano Lady Gaga, Diamond Platnumz nk.

3-Faida nyingine ya kutumia VEVO ni kwamba inasaidia msanii kutafutwa kwa urahisi na mashabiki wake hususani youtube pale unapotafuta kazi za Msanii husika au jina lake.

4-Malipo ya mtandao wa VEVO ni makubwa ukilinganisha na YouTube hii ni kwa sababu akaunti za wasanii wengi za VEVO zipo chini ya makampuni au lebo za muziki zinazowasimamia wakati YouTube hao wanalipa msanii kadri ya matangazo yanavyozidi kucheza kwenye channel yake hakuna makubaliano rasmi ya malipo.

5-Usimamiaji wa akaunti za VEVO na YouTube. YouTube channel zake zinaongozwa na mtumiaji mwenyewe lakini akaunti za VEVO zinafunguliwa na kuongozwa na watu maalumu kutoka VEVO, hivyo msanii hatakuwa huru kukagua akaunti bali atakuwa anapata notifications tu kutoka VEVO.

Je, wasanii wa Afrika wanatumia mtandao wa VEVO kupata views?

Hapana wasanii wa Afrika na nchi nyingine ambako VEVO haipatikani na wamefungua akaunti za VEVO hupata views kupitia YouTube na sio VEVO hii ni kwa sababu akaunti zao za VEVO zipo ndani ya YouTube.

Kiufupi VEVO inapata views wengi kutoka kwenye mtandao wa Youtube duniani hii ni kutokana na ushirikiano wake wa kibiashara kuliko hata views wanaopatikana moja kwa moja kutoka kwenye mtandao wa VEVO yaani (vevo.com)

Je, msanii anaweza kununua Views YouTube au VEVO?

Ukweli ni kwamba kuna uwezekano wa kununua views kwenye mtandao wa YouTube ila kwa zile akaunti ambazo hazioneshi matangazo na kitendo hicho endapo kitafanywa na akaunti zilizounganishwa na matangazo (Google Adsense) upo uwezekano akaunti husika kufutwa. Mchezo huu kwa akaunti za VEVO hakuna kabisa kwani zinaongozwa na wenyewe VEVO.



Ni kweli VEVO inatumiwa na wasanii maarufu pekee?

Hapana, VEVO inatumiwa na kila msanii/Mwanamuziki kinachohitajika ni kufuata utaratibu wa kujisajili. Kuna wasanii wakubwa hawatumii VEVO wapo YouTube na kuna wasanii wengine wadogo wapo YouTube, Kwa sasa wasanii ambao wanatumia akaunti za VEVO hapa Tanzania ni Diamond Platnumz, Alikiba, Jux,  Gosby, Grace Matata, nk.

Kwa hiyo VEVO ni mtandao unaojitegemea ila upo ndani ya Youtube kama Partnership kibiashara na mamilioni ya views kwenye video za VEVO yanatoka YouTube.

Kwa hiyo kama VEVO ikijitoa kwenye biashara na YouTube basi mtandao huo utakuwa na watazamaji wachache mno duniani kwani hata nchi ambako mtandao wa VEVO unapatikana bado mtandao wa YouTube una watumiaji wengi na hata VEVO muda mwingine hutumia mtandao huo kupromoti kazi za wasanii wao.

Kwa wepesi ni kwamba website ya VEVO ipo syndicated kwenye website YouTube ili kufanya kazi kiurahisi kwa nchi ambazo VEVO haipatikani.

Msanii wa Bongo Fleva Ochu Akiri Kuwa Mume Bwege Mbele ya Witness

0
0
Msanii Ochu Shegy ambaye ni mpenzi wa msanii Witness anayefanya muziki aina ya Hip hop, amekiri ni kweli huwa anakula magengeni badala ya nyumbani kama ambavvyo inatakiwa kwa mwanaume ambaye anaishi na mke ndani.

Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV, Ochu Sheggy amesema ni kweli anakula chips za magengeni kama Witness hajapika, kwani muda mwingine anakuwa amechoka hivyo hawezi kumlazimisha kumpikia.

"Huwezi ukatoka na mwanamke ye anafanya muziki we unafanya muziki, muda mwengine mnakuwa na 'studio session' mnarudi nyumbani saa 7 usiku, unamuingizaje jikoni mtoto wa watu? Kachoka tunaenda kutafuta chakula tule wote, sio robot yule", amesema Ochu.

Ochu Shegy ameendelea kwa kumtetea mpenzi wake huyo ambaye inasemekana anampelekesha kutokana na ubabe wake, na kusema kwamba Witness sio mbabe na hawezi kumfanyia ubabe, kwani iwapo angekuwa anafanya hivyo, angeshaondoka na kwenda kwa wengine.

"Nahisi napendwa zaidi, mimi sio mtu ambaye naweza nikatulia sehemu jambo likiwa limeniumiza, naosha dakika sIfuri tu kwa sababu kuna bebes kibao, kwa nini ung'ang'anie sehemu unayoteseka? Siteseki, nafurahia", amesema Ochu Sheggy.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi za wawili hao kuachana, lakini Ochu alikanusha tetesi hizo kuwa hazina ukweli wowote, kwani bado wanapendana sana.

Mwanaume, Fanya Haya Ili Kumroga Mwanamke, Hata Kama Huna Kitu..!!!

0
0
Salam Enyi Watanzania wenzangu.

Mungu kanituma niwaeleze haya mambo mazuri kwa ajili ya kudumisha mahusiano yetu, hasa mke na mume au wachumba nk.

Kwanza kabisa, wanawake wana akili sana katika kututawala sisi wanaume na wana uelewa na creativity kubwa sana ya kukusoma vizuri mwanaume kila unachofanya na kila unakokwenda na issues zako zote. Hata kama hakwambii, elewa anajua kila kitu, anakustahi tu.

Kujiamini ni nguzo muhimu sana kwa sisi wanaume kumkalisha mwanamke chini, awe billionea, awe professor, awe na cheo nk kwako si kitu kama mwanaume unayejiamini.

Asijue kitu fulani hujui, asijue kitu fulani huna, asijue kama umeshindwa mahali. Wanawake hutumia "failures" za mwanaume kuwa "opportunities" kwao. Atafanya ya ajabu kwakuwa anajua huwezi kitu fulani, huna kitu fulani, huna uwezo fulani.

Hata kama ikitokea ndani hakuna kitu, mwambie tu 'kuna mtu nimemwelekeza ataleta hapa nyumbani'. Hata kama huna hela mwambie tu 'kuna jamaa anatuma sasaivi kwenye mpesa'.

Hata kama huyo mtu asipoleta, huyo mtu asipotuma kwenye simu, we kauka tu...endelea hivyohivyo kubadili visentensi ili aridhike, huku wewe unaplan/unastruggle kinyakimya kuhakikisha chochote kuhakikisha mambo yanakaa vyema.

Usirogwe ukamwambia mwanamke "siwezi, sijui, sina, nitaangalia, ngoja kwanza, ". Otherwise atafanya anachoweza kuhakikisha anapata kila kitu na hata kukulisha wewe.

Kujiamini, kujiamini, kujiamini ndo dawa ya 'Eva' huku duniani.

Mambo Usiyopaswa Kufanya Kwenye Kundu la Whats App

0
0

Katika nyakati tunazoishi sasa mawasiliano yamekuwa jambo jepesi na rahisi kuliko hapo awali. Tofauti na wakati wa kutumiana barua kupitia posta ambapo barua ilikuwa inaweza kuchukua mpaka mwezi mzima pasipo kumfikia muhusika.

Matumizi ya simu na tarakilishi (computer) pamoja na mtandao (internet) kumeyafanya mawasiliano kuwa rahisi sana. Hii imepelekea wataalamu kuunda programu mbalimbali za kurahisisha mawasiliano baina ya watu wawili au zaidi wanaotumia simujanja (smartphone) au tarakilishi (computer).

Programu hizo ni kama vile WhatssApp, Telegram, Twitter, instagram, facebook na nyingine nyingi.

Imefikia hatua mpaka programu hizo zinawawezesha watumiaji wake kuunda makundi ya majadiliano na mazungumzo.

Katika kundi kunakuwa na watu wengi na wenye imani, malezi, uwezo, elimu na tabia tofauti tofauti.

Ili kuepuka kuonekana kikwazo au kero katika makundi ya majadiliano ya mitandaoni kama ‘whatApp groups’ inabidi uyazingatie yafuatayo;

Usitumie majina ya kejeli

Tumia majina ya utani na ya kusisimua lakini angalia kwa pande zote, isije ikawa jina unalolitumia linawakwaza wengine. Kumbuka ni kundi la ‘kuchati’ na hauko peke yako.

Usitume jumbe zenye maneno mengi

Ukweli ni kwamba jumbe zenye maneno mengi huwa hazisomwi na huwakera watu wengi. Hivyo ili kuepuka kuwakera wengine na kuonekana msumbufu basi tumia maneno machache kueleza ujumbe wako. Vile vile kama ujumbe unaoutuma una jambo la muhimu unalotaka watu wengine walifahamu, kuna uwezekano mkubwa wasilifahamu kama una maneno mengi. Jitahidi kufupisha. @swahilitimes.com

Usijiondoe (left) kwenye kundi pasipo taarifa

Kabla ya kujiondoa katika kundi hakikisha kuwa unatoa taarifa kwa wanakikundi na ikiwezekana uwaambie sababu ya kujiondoa ili watambue kuwa hautokuwepo nao tena. Siyo vizuri ‘kuleft’ pasipo taarifa.

‘Usi-screenshot’ chochote pasipo kuomba ruhusa

Watu wengi wamekuwa na tabia ya ‘ku-screenshot’ jumbe ama picha za wengine pasipo kuomba ruhusa kwa wahusika pasipo kujua kwamba ni kosa na ni kuhatarisha usalama wa wengine katika kundi. Acha tabia hiyo mara moja.

Usitume jumbe nyakati za usiku sana

Kuna watu wengi wamekuwa wakikesha ndani ya makundi ya whatsApp na kutumiana jumbe moaka saa 9 usiku. Unashangaa unaamka saa 12 asubuhi unakuta jumbe 1765 ambazo hukuziacha wakati ulipoenda kulala. Kwa wote wenye tabia ya ‘kuchat’ usiku wa manane wanapaswa kuiacha tabia hii kwani wengine nao wanahitaji muda mzuri wa kupumzika na kulala usingizi mwororo.

Usiwe mtazamaji

Kwenye makundi ya whatsApp kuna baadhi ya watu huwa ni watazamaji tu (observers). Watu wa aina hii huwa hawachangii chochote zaidi ya kuwa wanasoma jumbe za wengine na kucheka kimoyomoyo. Usiwe na tabia hii, hakikisha na wewe unashiriki mijadala mbali mbali inayoanzishwa na wengine katika kundi.

Usiligeuze kundi kuwa sehemu yako ya kupeleka malalamiko au ya kujisifia

Wako watu wanaoyageuza makundi ya whatsApp kama ‘therapy session’ ambapo wanaenda kujieleza mambo yote yanayowasumbua, namna maisha yanavyowaendea na magumu yote wanayoyapitia. Wengine hutumia makundi hayo kama sehemu ya kujisifia kuhusu wanalivyofanikiwa kimaisha, wanawake warembo waliokuwa nao, vyakula wanavyokula, maeneo ya starehe waliyohudhuria  na vingine vya kufanan na hivi. Kumbuka siyo kila mmoja anataka kusikia hayo malalamiko au sifa zako.

Usiiweke kazi yako hatarini kisa jumbe za makundi ya whatsApp

Utakuwa ni mtu wa ajabu sana kama utaamua kuendekeza na kuzipa kipaumbele ‘whatsApp charts’ kuliko kazi yako. Hakikisha kuwa ‘una-mute notifications’ za makundi yote pale unapokuwa na kazi muhimu za kufanya. Ukiendekeza sana whatsApp unajua kitakachokukumba pale utakapokamatwa na mkuu wako wa kazi. Utakapofukuzwa kazi, hakuna hata mmoja ndani ya kikundi atakayekuajiri. Fikiri kwa kina.

Usiwe mtoa taarifa kila mara

Baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya ‘ku-share’ jumbe, taarifa, sauti na video kila wanapoipata kutoka kundi lingine. Wengine wamekuwa na tabia ya kusema kila wanachokiona katika televisheni. Mfano watu wanaangalia mpira, mara goli linafungwa.. wewe haraka unakimbilia kwenye kundi kutoa taarifa. Usione watu wamekukalia kimya ukadhani wanafurahishwa. Pengine wanadharau unachokifanya na kukuona usiye na akili. Jaribu kutokuonekana kero kwa wengine.

JE Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo, Kufika Kileleni Haraka na Kushindwa Kurudia Tendo?

0
0
JE, UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO, KUFIKA KILELENI HARAKA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO AU MAUMBILE MADOGO YA UUME? Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume husababishwa na mambo mengi kama KISUKARI, UNENE ULIOPITILIZA, KUJICHUA (MASTER BLASHION), HOMONI kushindwa kufanya kazi ipasavyo n.k. Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa ☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni ☆Uume kusinyaa katikati ya tendo ☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa. Kwa kutumia mimea na matunda @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250000@250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6 hadi 7 @150000@150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200000@200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150000@150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130000@130,000/= BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA ZIMETHIBITISHWA KIAFYA. KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI

TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :@markson_beauty_pr

Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa (+255) 0767447444 na 0714335378

 UTAPATA HUDUMA NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. < WELCOME ALL>

Majadiliano kati ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold Corporation kuhusu Makinikia Bado Yanaendelea

0
0
Wakati majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold Corporation kuhusu wizi unaodaiwa kufanywa kwenye uchimbaji na usafirishaji wa mchanga wa madini (makinikia) yakiingia siku ya 64, Ikulu imesema majadiliano hayo yanaendelea.

Majadiliano hayo yanafanyika kipindi ambacho Watanzania wengi wana shauku ya kuona rasilimali za madini zinanufaisha Taifa.

Katika majadiliano hayo yaliyoanza Julai 31, timu ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa amesema majadiliano yanaendelea na wananchi wasubiri wataelezwa kitakachojiri.

“Majadiliano bado yanaendelea, wakiwa tayari watasema kwani hawawezi kuwa wanajadiliana mara wanakwenda kusema katika media," amesema Msigwa.

Mazungumzo hayo yalianza kufanyika kipindi ambacho Rais John Magufuli alikuwa amekwishapiga marufuku ya kusafirisha nje makinikia hadi mgogoro wa kimaslahi kati ya wawekezaji hao na Serikali utakapomalizika.

Miongoni mwa kinachojadiliwa ni kodi ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeitaka Kampuni ya Acacia kuilipa Serikali ya Tanzania Dola za Marekani Bilioni 190 ambazo ni zaidi ya Sh 434 trilioni zinazodaiwa kutokana na malimbikizo ya kodi na adhabu.

Msingi wa mazungumzo hayo ni baada ya Rais Magufuli kuunda tume mbili kuchunguza madai ya wizi na ufisadi unaodaiwa kufanywa na wawekezaji hao kwa zaidi ya miaka 19 iliyopita tangu walipoanza uzalishaji wa dhahabu.

Serikali Yataja Sababu za Bomoabomoa inayoendelea Nchini

0
0
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema bomoabomoa inayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini inatokana na ujenzi holela na kutofuata ramani za mipango miji.

Mabula amesema sababu hizo ndizo zinawasababishia hasara wananchi ya kuvunjiwa makazi.

“Watu wengi wamejenga katika maeneo yasiyo rasmi hasa mjini,” alisema na kuongeza:

“Jambo hili linachangia vilio kwa kiasi kikubwa hasa unapofika wakati wa kuweka miundombinu ya maeneo husika.”

Naibu waziri huyo alisema hivyo akimaanisha vilio vinavyotokana na watu kubomolewa makazi yao.

“Wakati huo wahusika kama Dawasco (Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam) au Tanroads (Wakala wa Barabara)hujikuta wanalazimika kuvunja baadhi ya nyumba zilizopo katika maeneo yao ili waweze kufanya kazi iliyokusudiwa,” aliongeza Mabula.

Sababu hizo za bomoabomoa alizitoa jana wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Tayari baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam waliojenga pembezoni mwa Barabara ya Morogoro wamepoteza makazi yao baada ya Tanroads kubomoa nyumba ili kupisha mradi wa barabara ya kisasa ya njia sita.

Katika hotuba yake, naibu waziri huyo aliwaonya watu wanaoendelea kujenga kiholela katika maeneo yaliyopangwa akisema urasimishaji unaoendelea nchini hauwatagusa wale ambao tayari maeneo yao yana mipango kabambe.

Alisema kuwa urasimishaji huo usiwe chachu ya watu kuendelea kujenga holela kwa kufikiri wizara itarasimisha makazi yao.

Pia, alisisitiza kwamba hawatarasimisha maeneo ambayo tayari yana mpango kabambe wa uendelezaji mji (master plan), hivyo watakaojenga bila kufuata utaratibu na bomoabomoa ikiwakuta hawatahangaika nao.

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Ujenzi wa Nyumba Mwenge, Hilary Mdaki alisema mbali na kuzingatia ujenzi wa nyumba katika maeneo yaliyo ndani ya mipango miji, changamoto mbalimbali zimekuwa zikiwakwamisha katika kufikia malengo yao ikiwamo ugumu wa upatikanaji wa ardhi.

Lowassa, Ndesamburo Watajwa Kufutwa Kwa Uchaguzi wa CCM Moshi, Hai, Siha

0
0
 Kivuli cha aliyekuwa mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa na mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (marehemu) vinadaiwa kuitesa CCM.

Habari kutoka ndani ya chama hicho katika wilaya za Moshi, Siha na Hai zinadai kuwa vivuli vya wanasiasa hao ndiyo kiini cha kufutwa kwa uchaguzi wa mwenyekiti katika wilaya hizo.

Wiki iliyopita, chama hicho kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole alisema mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), umefuta uchaguzi katika wilaya nne. Mbali ya wilaya hizo tatu za Mkoa wa Kilimanjaro, nyingine ni Makete ya Iringa.

Alisema sababu ya kufuta matokeo hayo ni kubainika kwamba wagombea waliojitokeza hawakuwa na sifa pamoja na kubainika kuwepo na viashiria hatarishi kwa chama hicho kikongwe nchini.

Kutokana na uamuzi huo, Polepole alisema wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa uchaguzi katika ngazi hiyo. Taarifa zilizopatikana jana kutoka Moshi Mjini zimeeleza kuwa tayari makada kumi na moja walikuwa wameshachukua fomu.

Taarifa zilizovuja kutoka ndani ya chama hicho katika wilaya za Hai, Moshi na Siha, zinadai kuwa mojawapo ya ‘viashiria hatari’ ni uwepo wafuasi wa Lowassa na Ndesamburo waliojitokeza kuwania nafasi hizo.

Wagombea katika wilaya ya Moshi ni Christopher Lyimo, Alhaji Omar Shamba, Consolata Lyimo na Elizabeth Minde ambaye ni mwenyekiti aliyemaliza muda wake na anayetetea nafasi hiyo.

Habari hizo zimedai kuwa kikundi kimoja cha makada wa CCM, kilichotwaa majukumu ya maofisa usalama wa chama, kinadaiwa kumwaga sumu kuwa mmoja wa wagombea alikuwa kwenye payroll ya Ndesamburo.

Hayati Ndesamburo alikuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa vipindi vitatu (2000-2015) alipoamua kustaafu mwenyewe. Alifariki dunia ghafla mapema mwaka huu.

“Hicho kikundi kinaoongozwa na kada mmoja (jina linahifadhiwa) kinajifanya usalama na kusema, (anamtaja mgombea) alikuwa kwenye payroll ya Ndesamburo ambaye ni marehemu,”

“Hivi wewe unavyoona ana shida gani mpaka awe analipwa na Ndesamburo wakati akiwa hai? Ni siasa za kuchafuana na hicho kimetengenezwa na huyo kada na kundi lake,” alidai kada mwingine wa CCM.

Mbali na mgombea huyo, lakini mgombea mwingine kati ya hao wanne anatajwa kuwa “haaminiki”, lakini haikuelezwa sababu za kuwajumuisha wagombea wote hadi uchaguzi wao kufutwa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Moshi Mjini, Priscus Tarimo alipoulizwa kuhusu uamuzi huo wa Nec alisema umekuwa ni changamoto kwao kwa sababu walishajiandaa kwa uchaguzi.

“Ni uamuzi wa vikao vya juu kutokana ni taarifa za kiusalama kwa hiyo sisi hatuna budi kuupokea na leo (jana) wanachama wetu wameanza kuchukua fomu upya. Tunaenda vizuri,” alisema Tarimo.

Tarimo alipoulizwa iwapo waliogombea awali na kuonekana baadhi yao hawana sifa na wana viashiria hatarishi wataruhusiwa kugombea tena, alisema wanaruhusiwa kwa sababu hawakuzuiwa.

Minde aliyemaliza muda wake, ambaye ni wakili kwa taaluma alipoulizwa jana kuhusu hatima yake alisema yuko nje ya Moshi lakini atarejea leo na atachukua tena fomu kuwania nafasi hiyo.

Mbali na wilaya ya Moshi, taarifa kutoka wilaya za Hai na Siha zinadai kiini cha kufutwa kwa uchaguzi wao, ni baadhi ya wanaowania kutajwa kumuunga mkono Lowassa 2015.

Habari hizo zimedai kuwa baadhi ya wagombea ambao ndiyo wenye nguvu na wanaoonekana watashinda uchaguzi huo, wanatajwa kuwa katika mtandao wa Lowassa wakati akiwania urais ndani ya CCM.

Mara baada tu ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, alifanya mkutano wake wa kwanza ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam na kulalamikia uwepo wa makada wasaliti.

Aidha, tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015, chama hicho kimekuwa kikitekeleza mkakati wake wa kujiimarisha na kuwaondoa makada waliokisaliti katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na ushindani mkali.

Ushindani huo ulikuwa baina ya Dk Magufuli na Lowassa ambaye licha ya kuondoka CCM na kugombea kwa tiketi ya Ukawa, bado alikuwa na kundi kubwa linalomuunga mkono ndani ya CCM.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne y a Octobre 3

0
0
 

Vu 


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne y a Octobre 3

Jinsi Ya Kumwacha Mpenzi Wako Kwa Amani.....

0
0

Ziko njia mbili tu ambazo uhusiano baina ya wapenzi wawili utaandika historia. Ama uhusiano utadumu hadi kifo kiwatenganishe ama utavunjika. Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa kwa walio wengi hawajaweza kuwa kwenye uhusiano wa kudumu, wanakuwa wamepitia katika mahusiano mengine na hivyo kupitia awamu Fulani Fulani za kuvunja mahusiano.Na kuna namna mbili ambazo uhusiano utavunjika. Ama kwa amani ama kwa ugomvi.


Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba. Kumbuka "The Golden Rule": Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni:


1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya: Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka "Maamuzi magumu". Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya kuwa na wewe ama anaweza akaamua na yeye kukukomoa na kukuacha kabisa wakati kumbe bado una hisia za mapenzi na yeye . Hata hivyo kama una uhakika kwamba ni kweli hauutaki uhusiano uliopo basi kuwa tayari kukata kabisa mahusiano yenu la sivyo kuwa tayari kukiona cha moto . . . maana utakuwa unachezea hisia zako.

2. Fikiria Sababu za Kuvunja Uhusiano: Uhusiano unapovunjika mara nyingi ndugu, jamaa na marafiki wanapenda kujua sababu. Unapojua sababu zinazopelekea wewe kuvunja mahusiano itakusaidia kutoa majibu ya uaminifu pale unapoulizwa. Pia itakusaidia kumaliza mahusiano katika namna njema. Hata kama mwenzi wako hataamini au ataamini juu ya kuvunjika kwa uhusiano wenu, kuwa honest au mkweli ni muhimu. Mweleze unahitaji kusonga mbele na maisha yako bila yeye na mjibu maswali yote kwa uaminifu. (Fikiria huko nyuma kama uliwahi kuachwa bila sababu ulivyojisikia)

3. Maliza Mahusiano Wewe Binafsi: Kama umekuwa na mpenzi wako kwa muda mrefu au kuipindi chochote ambacho uliwekeza muda na nguvu zako za kujenga mapenzi, basi ni busara mahusiano hayo yakamalizwa na mwenyewe binafsi. Usitumie njia yoyote ile zaidi ya wewe mwenyewe, usitumie SMS, usitumie IM "Chat", usitumie simu au email au barua au mtu yeyote kufikisha ujumbe. Ukitaka kumaliza mahusiano kwa amani, tafuta muda wa kukaa na mwenzi wako in person au face to face ili kuumaliza uhusiano huo katika hali njema.


4. Chagua Mahali Panapofaa. Mahali pazuri panapofaa ni pale ambapo wewe unayetaka kumwacha mwenzako ungekuwa wewe unaachwa ungependa iwe mahali gani ili uelezwe? Be on his/her shoes. Public Places si mahali pazuri sana kwani mwenzi wako anaweza kujisikia kadhalilishwa. Kama ukiweza chagua mahali patakapomfanya mwenzi wako awe confortable na kurelax kama yuko nyumbani kwake.

Angalizo: Kama una uhakika kuwa mwenzi wako anaweza kuleta ukorofi, basi chagua Public Place kama kwenye restaurant ambapo wapo watu wengine. Hii itasaidia kuondoa uwezekano wa kuleta vurugu. Public Place patakufanya ujiamini. Pale mambo yatakapochachamaa unaweza kuondoka tu bila tishio la ugomvi kwa kuwa kuna watu. Ukiona hali si shwari ni vema uanze kuondoka wewe kuliko yeye kuondoka kwanza.


5. Msikilize Mwenzi Wako: Hata kama umeshaamua huwezi kubadili mawazo juu ya kuvunja mahusiano yenu haina maana kuwa usimsikilize mwenzi wako. Kumsikiliza mwenzi wako kutamfanya mwenzi wako atoe yote aliyokuwa nayo moyoni kitu ambacho kwa uhakika kitasaidia kumaliza mahusiano kwa amani. Pia unaweza kujifunza baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia katika mahusiano yako yanayofuata.


6. Kuwa Mpole Na Dhibiti Hisia Zako: Moja ya sababu kubwa ya mahusiano kuvunjika ni pamoja na wahusika wote kutokuwa na furaha na amani na mwenzi wako. Wakati wa kuvunja mahusiano hayo pia yanaweza kujitokeza hasa pale mtakapoanza kulaumiana na kuonyeshana vidole ni nani mwenye makosa. Hakikikisha unadhibiti hasira hisia zako na hasira hata kama anachoongelea mwenzio kitakutia hasira. Ukifanya hivyo utafanikisha kuwa na mazungumzo ya amani.


7. Kuwa Mtulivu na Makini: Unahitaji kuumaliza uhusiano na kuondoka mahali mlipo. Hata hivyo ni busara kuwa mtaratibu na mpole. Kama kuvunjika kwa uhusiano wenu kutakuja kama Suprize kwa mwenzio, basi bila ya shaka atahitaji muda wa kuyameza unayomwambia, kuyatafakari ili aende sambamba na wewe katika mazungumzo yenu. Inaweza ikawa si habari njema kwa mwenzi wako kwa hiyo utulivu wako na upole katika maongezi yenu kutamfanya apunguze maumivu.


8. Mkimaliza Maongezi Ondoka Haraka: Iko hivi: Kwa kiasi kikubwa anayeachwa anaweza kuwa alikuwa hajui kuwa ataachwa kwa hiyo hatakuwa na furaha kwa yeye kuachwa. Anaweza akakulaani sana na kukuita majina yote mabaya anayoyajua na hivyo kukufanya na wewe uwe na hasira. Tulia. Jizuie. Kwa kuwa umeshaongea na pia umemsikiliza kistaarabu, huna haja ya kuendekeza ugomvi au malumbano. Ondoka. Hakuna faida utakayoipata kwa kuendelea kutoa maelezo yoyote ya ziada. Kama ni mwelewa na mmemaliza maongezi kwa amani basi mwage na nenda zako.


Je, ni nini uzoefu wako kuhusu kuacha au kuachwa katika mahusiano mbalimbali uliyopitia? Na je, kuna lolote la kujifunza?

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa leo Jumanne


Je,una Upungufu Wa Nguvu Zakiume,kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa,kufika Kileleni Mapema Na Kushindwa Kurudia ????

0
0
Tatizo la kukosa au kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya kiume husababishwa na mambo mengi kama,KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURUMA,MAUMIVU YA KIUNO,UNENE KUPITA KIASI,KUJICHUA nk.

Upungufu wa nguvu za kiume husababisha tendo la ndoa kutofanyika kwa kujiami nakwa usahihi nahivyo husababisha ndoa, mahusiano mengi kuvunjika.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI,
1 KUKOSA HAMU YA TENDOL LA NDOA
2 UUME KISIMAMA KWA KULEGEA
3 KUWAHI KUFIKA KILELENI
4 KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA WAKATI
5 KUCHOKA SANA BAADA YA ROUND YAKWANZA NAKUKINAI TENDO LA NDOA KABISA.

TUMIA 3 POWER KWA TATIZO LA UKOSEFU(UPUNGUFU)WA NGUVU ZA KIUME NAHAMU YA TENDO LA NDOA.FINA HUBORESHA MAUMBILE YA KIUME KWA KUNENEPESHA KWA SAIZI UIPENDAYO HAIJARISHI UMRI.

PIA KUNA DAWA ZA KURUDISHA MPENZI KWA MUDA MFUPI SANA NAZAKUPATA KAZI,KESI,KUDHULUMIWA,NK

WASILIANA NA SHEIKH OMARY AKUTATULIE MATATIZO YAKO HATA KAMA UMEHANGAIKA SANA PASIPO MAFANIKIO

Pia sheikh omary anatibu busha bila opresheni,kisukari,ngiri,presha vidonda vya tumbo,korodani kuvimba,na anatoa dagu za utajiri kwa wanaohitaji bila masharti yoyote magumu.ANAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM, NAUTALETEWA POPOTE ULIPO TIBA HII

SIMU; NO 0767145357/0629034550.
WHATS APP 0759030343

Serikali ya Tanzania Yakopeshwa Mabilioni Kukuza Utalii na Benki ya Dunia

0
0
Serikali ya Tanzania Yakopeshwa Mabilioni Kukuza Utalii na Benki ya Dunia
Benki ya Dunia (WB) imeipatia Tanzania mkopo wa Dola za Marekani 150 milioni sawa na Sh336 bilioni kwa ajili ya kusaidia uhifadhi wa mazingira na kukuza utalii wa asili katika maeneo ya mikoa ya kusini mwa nchi.

Fedha hiyo ilitolewa na Shirika la maendeleo la kimataifa la benki hiyo (IDA) kupitia mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya utalii (REGROW) baada ya kuidhinishwa wiki iliyopita.

Fungu hilo litakalotumika kwa miaka sita, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, litazinufaisha kiuchumi kaya takriban 40,000 zilizopo katika hifadhi kwa kuwa kutajengwa miundombinu na fursa mpya za kiuchumi kwa lengo la kuongeza usimamizi wa hifadhi za asili.

Mpango huo una lenga kukuza uhifadhi wa mapori ya Taifa, mbuga, maporomoko ya mto Ruaha na kupunguza mwingiliano wa kimakazi kati ya binadamu na wanyama pori.

Maeneo yatakayohusika na mpango huo ni Mbuga za Katavi, Kitulo, Mahale, milima ya Udzungwa, Mikumi na Ruaha, Pori la Selous, Mito inayopitiwa na bonde la ufa (Nyansa na Tanganyika) .

Kuhusu Mpango huo, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bella Bird alisema utalii ni eneo muhimu kwa maendeleo ambalo linaweza kuongeza ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa asilimia 10 ya pato la Taifa (GDP) kwa hesabu za mwaka 2015.

“Nchi hii imejaliwa wanyama wengi na vivutio vya asili lakini vinavyotambuliwa na kujulikana zaidi ni vile vya maeneo ya Kaskazini mwa nchi. Kuanza kuyajali maeneo haya ya kusini kutaongeza idadi ya watalii, hivyo kuongeza faida za kiuchumi,” alisema Bird.

Alisema Tanzania imefanikiwa kuongeza idadi kubwa ya watalii ndani ya muda mfupi kutoka watalii 500,000 kwa mwaka 2000 hadi watalii zaidi ya milioni moja kutokana na kuvitangaza vivutio vyake.

“Ukaichilia mbali sifa ya kutunza vivutio, Serikali inapata mapato na sekta hii hutoa ajira nyingi, mpaka sasa Tanzania ni zaidi ya watu 400,000 walioajiriwa katika sekta hiyo,” alisema Bird.

Kwa upande wake mtaalamu wa mazingira wa Regrow, Daniel Mira alisema endapo eneo hilo la kusini litafanywa kuwa maalumu kwa vivutio Tanzania itakuwa imejiimarisha katika utalii.

“Hata mapato yatakayokuwa yakipatikana yatakuwa na uwezo wa kuendeleza vivutio vya kipekee jambo ambalo litalifanya eneo hilo kuwa kitovu cha ukuaji wa kikanda na la mfano,” alisema Mira.


Saidi Aliyetobolewa Macho na 'Scorpion' Mambo Yawa Magumu Kufikishwa Mahakamani

0
0
Saidi Aliyetobolewa Macho na 'Scorpion' Mambo Magumu Kufikishwa Mahakamani
SAKATA la Said Mrisho aliyedaiwa kutobolewa macho na Salum Njwete ‘Scorpion’ na mkewe Stara Sudy, linatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kushindwa kuelewana ngazi ya Ustawi wa Jamii.

Said na mkewe waliingia kwenye bifu zito siku chache zilizopita baada ya kumwagana na kufikishana Ustawi wa Jamii ambao waliafikiana wagawane mali, lakini Said amekuwa akisuasua jambo lilipelekea ishu hiyo ipelekwe mahakamani.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha karibu kilieleza kuwa, licha ya kuwekeana makubaliano hayo mbele ya maofisa wa Ustawi wa Jamii kwamba Said ampe Stara pikipiki mbili na Bajaj moja lakini Said amekuwa akitoa visingizio vya hapa na pale na kushindwa kutimiza ahadi hiyo, jambo lililopelekea maofisa wa Ustawi waidhinishe kesi hiyo kusikilizwa mahakamani.
Gazeti la Uwazi lilimtafuta Stara ambaye alikiri ni kweli wanapaswa waende mahakamani, kwa sababu Said ameshindwa kutekeleza kile alichoahidi.

“Tangu tulivyokubaliana anipe sehemu ya mali hadi leo hajatimiza ahadi yake zaidi ya visingizio tu na kutupiga kalenda na kibaya zaidi kuna pesa ambayo alitakiwa anipe kwa siku kwa ajiri ya kutunza watoto lakini nayo hatoi yote anatoa pungufu, ndiyo maana Ustawi wameona bora hili jambo liende mahakamani maana limewachosha,”alisema.

Baada kuzungumza na Stara mwandishi wetu alimtafuta pia Said ambaye alikiri ni kweli bado hajampa Stara vitu hivyo kwa kuwa, anashindwa kutekeleza matakwa yake ili na yeye nafsi yake iwe huru.

“Hivyo vitu nitampa lakini anashindwa kutekeleza masharti niliyompa, anatakiwa anipe hati ya kiwanja ambacho nilinunua kwa kaka yake, lakini hataki anasema watanirudishia pesa na wakati hiyo hati anayo, pia makaratasi yangu ya hospitali yeye ndiyo anayo hataki kunipa, sielewi sasa,”alisema.

TUJIKUMBUSHE
Kipindi kifupi cha nyuma Said na mkewe huyo aliyezaa naye watoto wanne aliingia kwenye mgogoro baada ya kijana huyo kumkimbia Stara akiwa na watoto wachanga mapacha na kwenda kuoa mke mwingine, ndipo sekeseke hilo likafika Ustawi wa Jamii na kuafikiana kugawana mali.

Polisi Watafuta Sababu ya Mauaji Las Vegas

0
0
Polisi Watafuta Sababu ya Mauaji Las Vegas
Polisi wanajaribu kugundua sababu ya ufyatuaji mkubw wa risasi uliosababisha vifo vya watu 59 na kuwajehi wengine 527 kwenye warsha moja huko Las Vegas.
Mauaji Las Vegas: Tunayoyafahamu kufikia sasa
Mtu mwenye silaha Stephen Paddock, 64, alifyatua risasi kutoka ghorofa ya 32 ya hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwa warsha moja ya mziki Jumapili usiku.

Polisi walipata bunduki 23 kwenye chumba chake cha hoteli na zingine 19 na vilipuzi nyumbani kwake huko Nevada.
Lakini hadi sasa hakuna sababu ya hatua hiyo yake iliyoibuka.
Kwa Picha: Mauaji Las Vegas, Marekani
Wachunguzi hawajapata uhusiano wowote na ugaidi licha ya kundi la Islamic State kudai kuhusika.

Baadhi ya wachunguzi wamedai mtu huyo kuwa na matatizo kisaikolojia lakini hio bado halijathibitishwa.
Mtu huyo hakuwa anafahamika kwa polisi.
Stephen Paddock aliishi katika jamii ya watu wazima kwenye mji mdogo wa Mesquite kaskazini mashariki mwa Las Vegas

Aliripotiwa kuishi na mwanamke kwa jina Marilou Danley ambaye kwa sasa yuko nchini Japan na polis wanasema kuwa yaonekana hakuhusika

Neema Yawashukia Wakulima wa Mbaazi Masoko Matatu ya Nje Yapatikana

0
0
Neema Yawashukia Wakulima wa Mbaazi Masoko Matatu ya Nje Yapatikana
Baada ya kukosa soko la uhakika kwa miezi mitatu huku wakulima vijijini wakilazimika kuuza mbaazi zao kati ya Sh150 na 200 kwa kilo, hatimaye masoko matatu yamepatikana nje ya nchi.

Masoko hayo yametajwa kuwa katika nchi za Dubai, Afrika Kusini na Uingereza. Katika baadhi ya maeneo ya vijijini ikiwamo mkoani Lindi, wakulima wa mbaazi wanauza hadi Sh150 kwa kilo.

Kudorora kwa soko la mbaazi nchini kulitokana na baadhi ya nchi ikiwamo India kuzuia uingizwaji wa zao hilo kutoka Tanzania.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Pulse Exporters, George Fererra alisema jana kuwa, kuanzia sasa wameanza kufungasha mbaazi baada ya kupata masoko hayo.

Kampuni hiyo ambayo ipo katika Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA), ililazimika kusitisha ununuzi na ufungashaji wa zao hilo, huku mzigo wenye thamani ya Dola 500,000 za Marekani (sawa na zaidi ya Sh1 bilioni) ukikosa soko.

Ferrera alisema uamuzi wa India kusitisha ununuzi wa mbaazi kutoka Tanzania umewaathiri wakulima na wafanyabiashara kutokana na kuporomoka bei kwa kuwa zilikuwa zikiuzwa kwa wingi nchini humo.

“Kampuni nyingi za Tanzania zilitegemea soko la India pekee na hatukuangalia sehemu nyingine. Hili ndilo kosa kubwa tulilolifanya,” alisema.

Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo wa EPZA, Lamau Mpolo alisema ili kukabiliana na ushindani wa soko ni muhimu kwa viwanda kuongeza tija kwenye uzalishaji.
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images