Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Diamond Platnumz Kutumbuiza Kilele Cha Mwenge Oktoba 14, Zanzibar

$
0
0
Kwamujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi RC Ayoub Mahmoud, ambako ndipo kutafanyika kilele cha maadhimisho ya mbio za mwenge kitaifa, Posti hiyo inaeleza kuwa tayari msanii Diamond Platnumz na kundi lake la WCB wamethibitisha kuwa watatumbuiza siku hiyo ya tarehe 14/10/2017.

Posti hiyo inasomeka hivi:-

#icantwait Nikiwa Kama Mkuu wa Mkoa Wa Mjini #zanzibar napenda kukukaribisha wewe mdogo wangu @diamondplatnumz pamoja na team Yako nzima katika siku ya tarehe 14/10/2017 Katika viwanja vya amani!. Ni matarajio yangu wana mkoa wa mjini magharibi wanakusubiri kwa hamu!. Confirmed diamond platinum live performance at Amani Stadium!. #kilelechamwengezanzibar #MiminaWewe #karibuninyote

Ndoa ya Zamaradi Yawaweka Kitimoto Antonio Nugaz na Adam Mchomvu

$
0
0
Ndoa ya Zamaradi Mtetema na mwanaume mmoja ambaye hakutambulika jina kale mara moja huku wengi wakidai ni ndugu wa kiongozi wa juu ya serikali ya awamu ya tano, imezua mtafaruku katika mitandao ya kijamii.

 Mrembo huyo ambaye ni mama wa watoto wawili aliozaa na Mkurugenzi wa Vipindi vya Clouds Media, Ruge Mutahaba alifunga ndoa ‘kimyakimya’ mwisho wa wiki iliyopita.

Zamaradi alivunja ukimya kwa kuweka kwenye Instagram picha ya ndoa yake na mumewe ambaye hakuonekana vizuri sura na kuandika, “ALHAMDULILLAH!!”

Hata hivyo baada ya picha hizo kusambaa mitandaoni watu wengi walikuwa hawaamini kama ni kweli mrembo huyo ameolewa na mwanaume mwingine tofauti na bosi huyo wa Clouds Fm kutoka na wawili hao kuwa wasiri zaidi katika mahusiano yao.

Umma ulianza kuamini kwamba ni kweli mrembo huyo ameolewa na sio movie kama baadhi ya watu walivyokuwa wanafikiria baada ya watu wake wa karibu kumpost katika mitandao ya kijamii wakimpongeza kwa hatua waliyoifikia.

Mtangazaji wa Kipindi runinga cha Kambi Popote, Antonia Nugaz siku chache baada ya mrembo huyo kufunga ndoa alimpongeza mrembo huyo kwa kumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa ikiwa ni siku chache toka afunge ndoa.


“Moyo wako siku zote ndio kiashiria cha mitendo vyako, kheri ya siku ya kuzaliwa kwako allah Bariki, Zamaradi Mtetema,” Hii ni kauli ya Nugaz ambayo ilimfanya Adam Mchomvu kukomenti ujumbe ambayo ilionekana akimtuhumu Zama kumrekodi bosi wake Ruge.

Ujumbe wa Adam Mchomvu ambao aliutoa kupitia post ya Nugaz, iliibua maswali mengi mtandaoni huku mashabiki wengi wakiporomosha maneno ya kejeli huku vijembe vingi zikielekezwa kwa bosi huyo wa Clouds.

Bongo5 ilimtafuta Nugaz lakini mtangazaji huyo alitakaa kulizungumza sakata hilo kwa madai watalimaliza kiofisi.

Bongo5

Alikiba na Diamond ‘Mkizembea’ Aslay na Rayvanny Watawanyamazisha

$
0
0
Kwa sasa ukizungumzia wasanii wa Bongo Fleva wanaofuatiliwa zaidi nchini Tanzania kwenye muziki na maisha yao nje ya muziki, haipingiki kuwa ni Diamond Platnumz na Alikiba.


 Kufuatiliwa kwao ni kutokana na wingi wa mashabiki wao na uzuri wa muziki wanaoufanya hiyo ndiyo sababu kubwa inayowafanya kuvuna mashabiki kila uchwao.

Hakuna ubishi kuwa vipaji vyao ni vikubwa na huenda pia muziki wao umewashawishi baadhi ya wasanii kuingia kwenye tasnia hiyo, ila umeshawahi kujiuliza uwepo wa Aslay na Rayvanny kwenye muziki wa Bongo Fleva?

Bila shaka kwa miaka 7 jina la Aslay limekuwa likisika kwenye masikio ya wengi kutokana na kazi zake ingawaje watu wengi mwanzoni walikuwa wanachukulia muziki wake kama unalenga zaidi watoto, inawezekana dhana hiyo ilitokana na umri wake.

Hata hivyo umri ukasogea kidogo Aslay akaingia kwenye kundi la Yamoto Band kundi ambalo lilikuwa linaundwa na wasanii wanne Beka Flavour, Maromboso, Enock Bella na Aslay.

Hakuna ubishi kuwa kundi hili lilikua kwa muda mfupi sana Afrika Mashariki na kutajwa kwenye tuzo nyingi kubwa barani Afrika.


Kutokana na kukua kwa kundi hilo la Yamoto Band jina la Aslay lilikuwa halisikiki kwa sana, hii ilisababisha watu wengi wasione uwezo wake lakini ukweli ni kwamba alikuwa na msaada mkubwa kwenye kundi hilo.

Ukweli kuwa Aslay ana kipaji cha kipekee na uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba umekuja kudhihirika mwaka huu mwezi Mei baada ya kundi la Yamoto Band kusambaratika na kila msanii kuanza kufanya kazi kivyake.

Kusambaratika kwa kundi kukaruhusu Aslay kuanza kurudisha makali yake kwa kuanza kufanya kazi kama ‘Solo Artist’ na ukweli ni kwamba tangu aanze kufanya kazi mpaka sasa ni miezi mitano na tayari ameachia ngoma kali saba.

Wimbo wake wa kwanza ulikwa ni Angekuona, Usiitie ndoa doa akiwa na Khadija Kopa, Muhudumu, Baby, Likizo, Pusha na wimbo wake mpya aliouachia jana (Jumatano) Natamba.


Ukweli ni kwamba nyimbo zote hizo tayari zimeshatazamwa na zaidi ya watazamaji milioni 1 kwenye mtandao wa Youtube, na kati ya nyimbo hizo hakuna wimbo ambao haujaingia kwenye Top 10 za Radio na TV hapa nchini.

Hakuna ubishi Aslay nyimbo zake zote akipanda jukwaani anaimba na mashabiki mwanzo mwisho hii ni ishara kuwa muziki wa Aslay unasikilizwa sana nchini na kikubwa ni kwamba ameuacha muziki wake ufanye kazi na sio kwa kiki au kwa maneno maneno ili asikike kwenye media.


Nakumbuka kuna kipindi Beka ambaye walikuwa wote kwenye la Yamoto Band baada ya kumuona Aslay anang’ara kwa kuachia ngoma mfululizo alianza kutoa kauli za kumpinga lakini Aslay hakumjibu hii yote ili kuufanya muziki wake umtambulishe yeye na sio jina lake lijulikane kwa stori tofauti na muziki.

Anachokionesha Aslay kipo sawa pia na anachokifanya Rayvanny kutoka WCB kwani naye ni moja ya vijana ambao nadiriki kusema tunajivunia kuwa nao kwenye muziki wetu wa Bongo Fleva.

Kipaji chake nae pia kilianza kuonekana toka kitambo kwenye mashindano ya Serengeti Fiesta Super Nyota huko mkoani Mbeya.

Licha ya kipaji chake na uwezo wa kutumia vifaa mbalimbali vya muziki, kuimba na kurap kwa pamoja na uwezo mkubwa wa utunzi lakini mafanikio yake yalianza kuonekana mapema alipojiunga na lebo ya WCB ingawaje amekaa muda mrefu chini ya kundi la Tip Top.


Kwa miezi mitano Rayvanny ameachia ngoma nne kali ambazo ni Mbeleko, Chuma ulete, Unaibiwa na Zezeta na nyimbo zote tayari zimetazamwa na watazamaji zaidi ya milioni 1 kwenye mtandao wa Youtube na kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali za radio na runinga hapa nchini na kuoneshwa na vituo vikubwa vya runinga barani Afrika.

Rayvanny pia ndani ya mwaka mmoja aliojiunga na WCB amefanikiwa kupata tuzo ya BET na kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuchukua tuzo hiyo kubwa duniani.

Rayvanny ameanza kufahamika kwa watu wengi mwaka jana baada ya kuachia ngoma yake ya ‘Kwetu’ na tayari amepata mafanikio makubwa ikiwemo tuzo ya BET ambayo yote hayo yamekuja kutokana na uwezo wake na kuacha muziki wake mzuri umtambulishe zaidi kwa mashabiki kuliko kuzungumziwa kwa kiki/drama kwenye muziki wake.

Kama utakuwa ni mfuatiliaji wa show za Rayvaany utaungana nami kuwa hakuna shabiki asiyeimba naye awapo jukwaani.

Bila shaka wasanii wote hawa wawili ukiwatazama kwa sura ya muziki unaona kabisa safari yao ya muziki inaelekea kuzuri na Watanzania wameshaanza kuwaamini kwa kile wanachokifanya na hakuna ubishi wanaweza watafika mbali.

Kwanini nasema Diamond Platnumz na Alikiba wasibwete hapa walipo?

Kama nilivyosema awali uwezo wa wasanii hawa ni mkubwa na wamepata mafanikio makubwa kwenye muziki ila muziki wao umejaa skendo na hao wameshajijengea mazingira hayo na hawataki muziki wao uende bila kutupiana vijembe mitandaoni au kwenye media.

Ifikie mahala mtambue kuwa hata wasanii wadogo kwa sasa kutokana na nyinyi kuishi maisha hayo, na wao wanapigania kufanya muziki uliojaa na drama ili mradi wajulikane na wapate show. Imefikia muda hata wasanii wanatafuta interview kwenye media sio kuongelea kazi zao ila kutafuta kiki kwa kuwakashifu wasanii wengine.

Ninaposema ‘MKIZEMBEA’ nimemaanisha kuwa endapo mtaendelea kufanya kazi kwa mazoea kwa sababu ya ukubwa wa majina yenu huku mkitupiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, bila shaka wasanii kama Aslay na Rayvanny ambao wapo bize wakikesha kuumiza vichwa kwa kiu ya kuwafikia kimafanikio. Hakuna ubishi safari yao ya kuwafikia itakuwa fupi na watawaacha midomo wazi kama hadidhi ya Mr. Nice na Dudubaya.

Kumbukeni waswahili wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha, sasa ili kugeuza huu msemo msiridhike kwa kelele za mashabiki endeleeni kukaza buti na maneno ya mashabiki yabaki kuwa changamoto kwenu.

TRA Wajibu Kuhusu Picha za Magari Yaliyofanana Plate Number

$
0
0
TRA imesema kuwa, namba za magari zilizofanana ambazo zinasambazwa mitandaoni ni za siku nyingi, na zilishafanyiwa kazi


Mambo Usiyopaswa Kusema Wakati wa Interview

$
0
0
Tumekuwa tukiambiwa kuwa usidanganye hata kidogo katika usahili wa kazi uliyoiomba. Ni kweli hupaswi kudanganya, kwa sababu utakapogundulika kuwa umedanganya utajiweka katika hatari ya kuikosa kazi unayoiomba.

Lakini siyo nyakati zote unapaswa kusema ukweli katika usahili wa kazi. Mambo mengine huwa ni ya kweli lakini yatakuharibia sifa yako na pengine utaikosa kazi unayoitafuta.

Hakuna mtu aliye tayari kuikosa kazi anayoiomba. Kila mmoja atafanya jitihada kuhakikisha kuwa anakuwa bora zaidi katika usahili na kuwazidi wengine.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo hata kama ni ya kweli hutakiwi kuyasema katika usahili wa kazi.

Usiandike kila kitu katika wasifu wako (CV)

Unapoenda katika usahili wa kazi, uasiandike kula jambo ulilowahi kulifanya katika wasifu wako (CV). Baadhi ya mambo yanaweza kumpa wasiwasi mwajiri wako. Hebu fikiri uliwahi kufanya kazi katika kampuni fulani, baada ya miezi miwili ukafukuzwa kazi kutokana na uzembe, ukiiweka hiyo kazi katika wasifu wako kisha muajiri akakuuliza kwa nini uliifanya kwa muda mfupi, utamjibu nini?

Usimsemee vibaya muajiri wako wa zamani

Jambo kubwa linalowafanya watu wengi kuacha kazi walizokuwa wakizifanya ni pamoja na mahusiano mabaya na waajiri wao. Unapoenda katika usahili wa kazi mpya, usimsemee vibaya muajiri wako wa awali hata kama hamkuwa na mahusiano mazuri. Eleza kuwa umejifunza mambo mengi kutoka kwake. Hii itakusaidia wewe na itamfanya muajiri wako mpya akufikirie mara mbili katika usahili huo.

Usieleze sababu iliyokufanya uache kazi uliyokuwa unaifanya awali

Ukweli ni kwamba watu wengi huacha kazi moja na kutafuta nyingine kwa sababu ya mambo kama vile, mahusiano mabaya na waajiri au wafanyakazi wenzao, ugumu wa kazi yenyewe, kiwango cha mshahara na mengine yanayofanana na hayo. Lakini wakati unafanyiwa usaili hakikisha hutaji mambo hayo kama ndiyo sababu iliyokufanya wewe kutafuta kazi nyingine. Badala yake eleza ni kwa kuwa hii ndiyo kazi unayoipenda na utaifanya vizuri zaidi kuliko ya awali.

Hakikisha mambo unayoyapendelea yanaendana na aina ya kazi uliyoiomba

Usitaje unapendelea kunywa bia, kwenda kustarehe na marafiki, kuangalia filamu, kuchati na mengine yanayofanana na hayo, vinginevyo unaomba kazi kaztika kampuni ya bia ama inayohusiana navyo. Badala yake taja mambo kama vile kusoma vitabu, kuhudhuria warsha mbalimbali, kujifunza n.k

Mbunge CHADEMA Ataka Vyama Vingi Vifutwe

$
0
0
Mbunge CHADEMA Ataka Vyama Vingi Vifutwe
Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia CHADEMA John Heche, ameitaka serikali kufuta mfumo wa vyama vingi na kubakia na chama kimoja, kama wanaona uwepo wa vyama vya upinzani ni uhaini.

Akizungumza na moja ya Televisioni hapa nchini, John Heche amesema wamekuwa wakipokea vitisho vikali juu ya kufanya siasa na kukososa utendaji wa serikali, kitu ambacho ni wajibu wao kama vyama vya upinzani bungeni, hivyo kama wanaona wanafanya kosa basi ni heri wafute vyama hivyo.

John Heche ameendelea kusema kwamba kukosoa serikali sio uhaini bali ni kufanya kazi kadri ya sheria za nchi zinavyotaka, lakini kwa hali ya sasa hivi ilivyo imekuwa inaonekana kinyume, na kuhatarisha usalama wao na familia yao.

Aliyekuwa Msaidizi wa IGP Sirro Apangiwa Kituo Kingine cha Kazi na Rais Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Oktoba 2017, amemuapisha Meja Jen. Issa Suleiman Nassor kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki (aliyekuwa msaidizi wa IGP Sirro) kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia.

Akizungumza mara baada ya kula kiapo, Balozi Issa Suleiman Nassor amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha imani kwake na kumteua kushika nafasi hiyo na amemuahidi kuendeleza na kukuza uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Misri.

Balozi Nassor amemuahidi Mhe. Rais Magufuli kuwa atasimamia ipasavyo diplomasia ya uchumi ambayo kwa sasa ndio njia inayotumika duniani kukuza uhusiano wa kiuchumi baina ya mataifa mbalimbali.

Kwa upande wake Balozi Abdulrahman Kaniki amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumteua kushika nafasi hiyo na ameahidi kuendeleza uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Zambia ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Dkt. Keneth Kaunda.

Balozi Kaniki amemuahidi Mhe. Rais Magufuli kuwa atafanyia kazi dhamira ya kuliendeleza Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) ambalo limekuwa kiungo muhimu katika nyanja ya kiuchumi kati ya nchi hizi mbili.

Hafla ya kuapishwa kwa mabalozi hao imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

05 Oktoba, 2017



Dar es Salaam

Diamond Afunguka " Nikimaliza na Alie South na Nikawa na Mwingine Nitaweka Wazi"

$
0
0
Diamond Amekasirika na kuamua kufunguka haya baada ya kila siku kusingiziwa anatoka na huyu na yule:


" Mara Diamond Kamla Huyu, mara sjui naskia anatembea na Huyu, Mara Ooh sjui inasemakana juzi alikuwa na Huyu...Yani kila Ukiamka limezuka jipya, Utazani yangu Ina Sukari au Nakojoa dhahabu.....Hebu Niacheni kidogo, niko Busy nahangaika kuipeleka Bongo fleva yetu Duniani.... Sijamkaza yoyote, na Sina Mahusiano na Yoyote anaetajwa, na Siku pia Nikimaliza Mahusiano yangu na Alie South na nikawa na Mwengine na ikifikia kuliweka wazi ntaliweka wazi Mwenyewe, Maana hakuna kitachonizuia coz Sijaoa na Hata nikioa Naruhusiwa niwe na wake Wanne PERIOD!!!.... " Diamond

Je,una Upungufu Wa Nguvu Zakiume,kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa,kufika Kileleni Mapema Na Kushindwa Kurudia ????

$
0
0

Tatizo la kukosa au kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya kiume husababishwa na mambo mengi kama,KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURUMA,MAUMIVU YA KIUNO,UNENE KUPITA KIASI,KUJICHUA nk.

Upungufu wa nguvu za kiume husababisha tendo la ndoa kutofanyika kwa kujiami nakwa usahihi nahivyo husababisha ndoa, mahusiano mengi kuvunjika.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI,
1 KUKOSA HAMU YA TENDOL LA NDOA
2 UUME KISIMAMA KWA KULEGEA
3 KUWAHI KUFIKA KILELENI
4 KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA WAKATI
5 KUCHOKA SANA BAADA YA ROUND YAKWANZA NAKUKINAI TENDO LA NDOA KABISA.

TUMIA 3 POWER KWA TATIZO LA UKOSEFU(UPUNGUFU)WA NGUVU ZA KIUME NAHAMU YA TENDO LA NDOA.FINA HUBORESHA MAUMBILE YA KIUME KWA KUNENEPESHA KWA SAIZI UIPENDAYO HAIJARISHI UMRI.

PIA KUNA DAWA ZA KURUDISHA MPENZI KWA MUDA MFUPI SANA NAZAKUPATA KAZI,KESI,KUDHULUMIWA,NK

WASILIANA NA SHEIKH OMARY AKUTATULIE MATATIZO YAKO HATA KAMA UMEHANGAIKA SANA PASIPO MAFANIKIO

Pia sheikh omary anatibu busha bila opresheni,kisukari,ngiri,presha vidonda vya tumbo,korodani kuvimba,na anatoa dagu za utajiri kwa wanaohitaji bila masharti yoyote magumu.ANAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM, NAUTALETEWA POPOTE ULIPO TIBA HII

SIMU; NO 0767145357/0629034550.
WHATS APP 0759030343

Hamisa Mobetto Amfungulia Kesi ya Madai Diamond Platnumz

$
0
0
Mwanamitindo Hamisa Hassan Mobetto amemfungulia kesi ya madai mzazi mwenzie, Msanii Naseeb Abdul @diamondplatnumz kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi pamoja na kutotoa fedha za matunzo ya mtoto wao, Abdul Naseeb Juma.
.
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa @hamisamobetto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.
.
Katika wito huo Diamond anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.
.
Wakili Zulu akizungumza na Gazeti la Mwananchi, amesema mteja wao Hamisa Mobetto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.
.
“Baada ya kuona kimya tulipeleka kes i katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.
.
Shauri hilo linatarajiwa kutajwa ifikapo Oktoba 30, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam

Zimbabwe: Aliyechapisha habari ya ''nguo za ndani za Bi Grace Mugabe'' aachiliwa Huru

$
0
0
Mwandishi wa Zimbabwe ambaye alikamatwa baada ya kuandika habari iliodai kwamba mbunge mmoja aligawanya nguo za ndani za mitumba kwa wafuasi wa chama tawala cha Zanu-PF kwa niaba ya mke wa rais bi Grace Mugabe amewachliwa kwa dhamana ya dola 200.

Kenneth Nyangani pia aliagizwa kuripoti kwa polisi katika mji wa mashariki wa Mutare mara moja kwa wiki.

Amekana mashtaka ya kuchafulia watu majina kufuatia chapisho la habari hiyo katika mtandao mpya wa kibinafsi wa NewsDay.

Maafisa wa polisi katika eneo la Mutare walimkamata bwana Nyangani Jumatatu kwa madai ya kuandika na kuchapisha habari kuhusu ufadhili wa chupi za mtumba zilizodaiwa kutolewa na mkewe rais Robert Mugabe kulingana na mawakili wa haki za kibinaadamu wa Zimbabwe katika taarifa yao.

Mbunge wa chama tawala cha Zanu-PF Esau Mupfumi alisambaza chupi hizo kwa wafuasi wa Zanu-PF mjini Mutare na kusema kuwa bi Mugabe alifadhili nguo kulingana na ripoti hiyo ya NewsDay.

Jack Wolper Akana Kuachana na Mpenzi Wake Brown

$
0
0
Msanii Jackline Wolper ambaye hivi karibuni amekumbwa na tetesi za kuachana na mpenzi wake, amekanusha taarifa hizo na kusema kwamba wakiachana mashabiki wake watajulishwa.

Akiongea na mwandishi wa East Africa Television, Jackline Wolper amesema ingawa kuna vitendo vinavyoashiria kuachana kwa wawili hao ikiwemo kufutwa kwa baadhi ya picha na kutompost mara kwa mara kama siku za nyuma, ni kutokana na baadhi ya mikataba ya kazi aliyoingia.

“Watanzania wamezoea sana Instagram, usipompost bwana wako basi mmeachana, hawajui hata kama watu mumepata deal, mmeingia mikataba, hautakiwi kuweka mapicha ya mapenzi, mpaka wanataka utoe siri sasa, kuna issue siwezi kuiongelea, hivyo hakuna kitu kama hicho kikiwepo nitaongea”, amesema Wolper

Wolper amekutwa na tetesi za kuachana na Brown  baada ya kuonekana akishikana mkono kusalimiana na x wake, kwenye sherehe ambayo wawili hao walihudhuria.

VIDEO: Familia ya Lissu yafunguka kwa Mara ya Kwanza

$
0
0
Baada ya ukimya wa muda mrefu tangu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu Lissu kushambuliwa kwa risasi nyingi na watu wasiojulikana mchana wa Septemba 8, 2017 mkoani Dodoma, Leo Oktoba 5 Familia ya Mbunge huyo imezungumza na Vyombo vya habari kuhusu Hali ya mbunge huyo kwasasa ambaye anatibiwa Nchini Kenya, imeongea pia kuhusu mwenendo wa Uchunguzi, na kuhusu Dereva wa Lissu.

Nawakaribisha Huku Ukawa Wote Waliokatwa CCM- Lowasa

$
0
0
Nawakaribisha Huku Ukawa Wote Waliokatwa CCM- Lowasa
WAZIRI mkuu mstaafu, Edward Lowassa amesema kuwa anawakaribisha Chadema wale wote waliokatwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Alhamisi, Lowassa amesema, “Nimesoma na kusikia baadhi ya waliokuwa viongozi katika Chama Cha Mapinduzi wamekatwa ama kutetea nafasi zao au kugombea, kwa sababu mbalimbali. Na jina langu limekuwa likiendelea kutajwa tajwa humo,”
“Mimi nawaambia hawa Watanzania wenzetu waliokatwa huko CCM nawakaribisha huku Ukawa wafurahie demokrasia. Huku niliko kuna maisha mazuri ya kisiasa, uhuru wa fikra na demokrasia halisi.”

Lowassa amesema Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere alisema ni wakati muafaka kwa Tanzania kuwa na mfumo wa vyama vingi, pamoja na kwamba maoni ya Watanzania wengi wakati ule kupitia tume ya Nyalali (Jaji Francis) kutaka kuendelea na mfumo wa chama kimoja.
“Nataka kuwakumbusha Watanzania wenzangu hawa, uamuzi ule wa Baba wa Taifa, ulilenga kuwapa Watanzania demokrasia ya kuwa na uwanja mpana wa kufanya siasa,”

“Mimi nimetumia fikra hizo za mwalimu na hakika hivi sasa ninafurahia demokrasia halisi huku niliko. Kwa wote waliokatwa na wanahisi wameonewa waondokane na unyonge wa fikra kudhani kuwa bila CCM hakuna maisha… waje huku tufanye siasa kwa manufaa ya wananchi wetu.”

Lowassa amewaomba Wana-Chadema wenzake kuwapokea kwa mikono miwili na wale wanaoendelea kubaki huko CCM waendelee kushikamana hadi uchaguzi mkuu ujao 2020 ambapo upinzani utakapoonyesha makucha yao.
“Vitisho na nguvu ya dola inayotumika kujaribu kutunyamazisha sisi wa upinzani isiwatishe wala kuwaongofya hata mara moja.”

Mauaji Las Vegas: Chama cha Umiliki wa Bunduki Marekani Chaunga Mkono Mageuzi

$
0
0
Mauaji Las Vegas: Chama cha Umiliki wa Bunduki Marekani Chaunga Mkono Mageuzi
Chama cha taifa cha wamiliki wa bunduki Marekani (NRA) kimeonekana kubadilisha msimamo wake na kuunga mkono udhibiti wa vifaa ambavyo hutumiwa kuimarisha uwezo wa bunduki.
Kifaa kama hicho kilitumiwa na mwanamume aliyewaua watu 50 kwenye tamasha mjini Las Vegas.
Kundi hilo limesema: "Vifaa hivyo ambavyo huwezesha bunduki ambazo zina uwezo fulani wa kufyatua risasi mfululizo kuwa bunduki kamili za kufyatua risasi mfululizo kwa kujiendesha yenyewe."

Chama cha Republican kimesema kwamba kitajadili uwezekano wa kupiga marufuku kifaa hicho kwa jina 'bump-stock' ambacho huondoa haja ya mtu anayetumia bunduki isiyo na uwezo kamili wa kufyatua risasi mfululizo kutumia bega lake kuidhibiti bunduki wakati wa kufyatua risasi.

Wabunge wanapanga kuandaa vikao na kujadili mswada wa kupiga marufuku kifaa hicho.
Alhamisi, NRA walitoa wito kwa wadhibiti wa bunduki "kuchunguza mara moja iwapo vifaa hivyo vinafuata sheria za serikali ya taifa."

Rais Donald Trump baadaye aliwaambia wanahabari kwamba utawala wale utafikiria uwezekano wa kuzipiga marufuku "muda mfupi ujao."

"Baada ya shambulio hilo la kinyama Las Vegas, Wamarekani wanatafuta majibu kuhusu jinsi ya kuzuia maafa kama haya siku za usoni," wakuu wa NRA Wayne LaPierre na Chris Cox waliandika kwenye taarifa.
Hata hivyo, wamewakosoa wanasiasa ambao wanatetea udhibiti zaidi wa bunduki, wakisema kwamba "kupiga marufuku raia wanaotii sheria kumiliki bunduki kwa sababu ya kitendo cha kihalifu cha mwendawazimu hakutazuia mashambulio kama haya siku za usoni."
Kwa nini raia hawawezi kupokonywa bunduki Marekani
Taarifa hiyo ndiyo ya kwanza kutoka wka chama hicho tangu shambulio hilo la Jumapili Las Vegas ambapo watu 58 waliuawa na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa.
NRA hata hivyo wamesema vifaa hivyo viliidhinishwa na Shirika la Kudhibiti Silaha, Pombe na

Msemaji wa White House Sarah Sanders, akizungumza na wanahabari baada ya taarifa ya NRA kutolewa, amesema: "Wanachama wa vyama vyote viwili na mashirika mengi wote wanapanga kuangalia upya vifaa hivyo. Tunakaribisha hilo na tungependa kuwa sehemu ya mazungumzo yanayoendelea."

Kwenye taarifa yao, NRA walihimiza Bunge la Congress kupitisha pendekezo lao la kuhakikisha haki za kumiliki silaha zinatekelezwa kote nchini humo.
Chama hicho kinataka wamiliki wa silaha wenye leseni za kubeba silaha wakiwa wamezificha kwenye jimbo moja waruhusiwe kuingia kwenye majimbo mengine bila kujali iwapo sheria za umiliki wa silaha huko ni tofauti.

Kifaa hicho huwezesha risasi kufyatuliwa kwa kasi ya risasi 100 kwa sekunde saba
Mswada wa kupiga marufuku vifaa hivyo vya kuimarisha uwezo wa bunduki uliwasilishwa kwenye bunge la Seneti Marekani siku ya Jumatano na seneta wa chama cha Democratic kutoka California Dianne Feinstein.

Mswada mwingine wa aina hiyo unaowasilishwa na chama cha Republican huenda ukawasilishwa bungeni muda wowote kuanza siasa, seneta wa chama cha Republican kutoka Florida Carlos Curbelo amewaambia wanahabari.

Stephen Paddock, mshambuliaji aliyewaua watu wengi Las Vegas, alikuwa ameweka vifaa hivyo kwenye bunduki 12 alizozitumia kwenye shambulio hilo.

Vifaa hivyo hugharimu chini ya $200 (£150) na huwezesha bunduki kufyatua risasi hadi 100 katika sekunde saba pekee, kwa mujibu wa tangazo la moja ya kampuni zinazouza vifaa hivyo.
Slide Fire, moja ya kampuni zinazouza vifaa hivyo, imesema bidhaa walizounda zimenunuliwa zote baada ya wateja kufika kwa wingi kufuatia shambulio hilo la Las Vegas.

Miili ya Watu Waliokufa kwa Kunywa Gongo Yakabidhiwa kwa Mkemia Mkuu

$
0
0
Miili ya Watu Waliokufa kwa Kunywa Gongo Yakabidhiwa kwa Mkemia Mkuu
WAKATI idadi rasmi ya watu waliofariki kwa kudaiwa kunywa pombe haramu ya gongo jijini Dar es Salaam ikiongezeka na kufikia 10, Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa miili ya wafu hao imekabidhiwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi.

Hatua hiyo imefikiwa ili kubaini aina ya kemikali (sumu) iliyowasababishia umauti wanywaji wa pombe hiyo ambayo taarifa zisizo rasmi zilidai kuwa ilichanganywa kwa vikorombwezo kadhaa kwa nia ya kuiongezea makali, vikiwamo dawa ya kuondoa madoa maarufu kama Jik na dawa ya kutibu majeraha mabichi aina ya spirit. Uchunguzi huo wa kimaabara wa Mkemia Mkuu unatarajiwa kuanika ukweli wa kila kilichokuwamo kwenye pombe hiyo.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, aliiambia Nipashe juzi kuwa waliofariki kwa kunywa pombe hiyo kwenye eneo la Kimara Stop Over ni watu watano na kueleza kuwa upo uwezekano idadi hiyo kuongezeka kutokana na taarifa walizokuwa nazo kuwa waliokunywa pombe hiyo walikuwa wengi.

Aidha, Mwenyekiti wa Mtaa wa Stop Over, Godfrey Missana, aliiambia Nipashe kuwa wakazi wanane wa mtaa wake walibainika kufariki dunia baada ya pombe hiyo kuwapofua macho, kuwafanya baadhi yao kuendesha na kutapika na mwishowe kufariki dunia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamanda Mambosasa alisema kuwa hadi kufikia jana mchana, idadi rasmi ya wale waliothibitika kufariki ilifikia kumi na kwamba, miili ya wafu ilikabidhiwa kwa Mkemia Mkuu kwa uchunguzi zaidi wa kitaalamu, pamoja na vielelezo vingine kadhaa kutoka katika eneo la tukio.

Akieleza zaidi mbele ya waandishi wa habari, Kamanda Mambosasa aliongeza kuwa wakati Ofisi ya Mkemia ikiendelea kutafuta chanzo cha vifo hivyo, jeshi hilo linaendelea kumsaka mtuhumiwa aliyewauzia watu pombe hiyo haramu.

“Tunaendelea kumsaka mtu aliyewauzia pombe hiyo watu hawa waliopoteza maisha. Katika eneo la tukio ziliokotwa chupa tatu za ujazo wa lita moja zikiwa zimejazwa pombe inayodhaniwa kuwa ni haramu ya gongo,” alisema Mambosasa.

Aidha, akieleza namna ilivyokuwa, Kamanda Mambosasa alisema kuwa juzi alfajiri, walipokea taarifa kutoka kwa Matigo Ramadhani (38), ambaye ni  mkazi wa Kimara Stop Over, akiwaeleza kuwa ndugu yake, Maleo Ramadhani (45), alirudi nyumbani akilalamika kuumwa tumbo, kuishiwa nguvu huku akiwa na kizunguzungu na kumweleza kuwa alikunywa pombe ya kienyeji kwa mama Anoza.

Alisema Matigo aliitaarifu polisi kuwa, walimpeleka ndugu yao Hospitali ya Mwananyamala na kupatiwa matibabu kisha walirudi naye nyumbani lakini alifariki dunia usiku wa siku hiyo.

“Baada ya muda alijitokeza mtoa taarifa mwingine aitwaye Paula Kisangila (53), mkazi wa Stop Over pia…naye alieleza kuwa aliporudi nyumbani kwake usiku akitokea kwenye shughuli zake, hakumkuta mlinzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Yona anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 20 hadi 30,” alisema.

Alisema kisangila alidai kuwa baada ya kumtafuta mlinzi huyo, walimkuta akiwa amefariki nje ya uzio wa nyumba.

Kamanda Mambosasa alisema walipata taarifa ya kuwapo kwa miili mingine saba katika Hospitali ya Mwananyamala na ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani ambayo ni ya Mohamed Issa (67), mkazi wa Kimara Saranga; Kabugh Rashidi (64), Stanslaus Joseph (58), Stephen Isaya (61) na Monica Rugaillukamu (42), wote wakiwa ni wakazi wa Kimara Saranga.

Kamanda Mambosasa aliwataja marehemu wengine katika tukio hilo kuwa ni Alex Madega, (41) mkazi wa Kimara Korogwe; Hamisi Mbala (35), mkazi wa Kimara Golani na Ekson Nyoni (28), mkazi wa Kimara Stop Over.

MWENYEKITI, MTOTO WA MAREHEMU
Juzi, mwenyekiti wa Mtaa wa Stop Over, Missana, aliiambia Nipashe kuwa kabla ya watu hao kufariki dunia, kulikuwa na taarifa kuwa baadhi yao walianza kulalamika macho yao kuwa mekundu sana, kuwauma na mwishowe kupoteza uwezo wa kuona ghafla kabla ya kukimbiziwa hospitali na majirani.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema kuwa pombe hiyo huuzwa katika kibanda kimoja kwenye eneo hilo na kwamba, miongoni mwa waliokufa ni pamoja na muonjaji ajulikanaye kwa jina la Mama Ramahuku mmiliki anayefahamika kwa jina la Dada Anoza akikimbilia kusikojulikana akihofia kukamatwa na Polisi.

Paulina Joseph, ambaye ni mtoto wa marehemu Joseph, aliiambia Nipashe juzi kuwa kabla ya kufariki dunia, baba yake alimkuta amezidiwa na kila mara alikuwa akimsindikiza chooni kutokana na kuendesha huku pia akilalamika macho yake kutoona tena.

Tanesco; Hitilafu ya Mitambo ya Songasi Chanzo cha Umeme Kukatika Ghafla Dar

$
0
0
Tanesco; Hitilafu ya Mitambo ya Songasi Chanzo cha Umeme Kukatika Ghafla Dar
Shirika la Umeme Tanzania limesema chanzo umeme kukatika ghafla umeme baadhi ya maeneo Dar es Salaam kumesababishwa  na hitilafu iliyotokea katika mitambo ya Songas.

Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji ameliambia gazeti hili kwa simu tukio lilitokea maeneo mbalimbali yakiwamo Ubungo na Mbezi.

"Tunaomba radhi wateja wetu kwa usumbufu uliojitokeza kwa kukosa huduma hii. Nawahakikishia mafundi wameshaanza kulifanyia kazi haitafika saa 5 usiku umeme utarudi katika hali yake.

Muhaji amesema tayari maeneo mengine ikiwamo Ubungo huduma imerudi katika hali yake ya kawaida baada ya mafundi kuanza kazi ya kurekebisha itailafu hiyo.

Alichokisema Kigwangalla Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

$
0
0
Alichokisema Kigwangala Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema…>>>”Asante Mungu kwa neema yako. Madaktari bingwa wa Macho kutoka Hospital ya Muhimbili, Hindumandal na Ebrahim Haji. Wameendelea kutimiza ahadi yao kutokana na zoezi letu la upimaji pamoja na matibabu ya Macho.”

“Gharama za upasuaji wa Macho ni kati ya Shillingi 900,000 hadi 1,000,000 pamoja na Miwani hivyo kwa Watu 1,000 ni sawa na Kiasi cha Shilling Billion Moja lakini kupitia wadau Wagonjwa hao watapatiwa matibabu na Miwani Bure ili waone Matunda ya Serikali ya awamu ya Tano kupitia RC Makonda. Mungu wangu atukizwe daima.”
Baada ya ujumbe huo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, ustawi wa jamii, jinsia, wazee na watoto Dr Hamisi Kigwangalla akamuandikia ujumbe uliosomeka…>>>”Mdogo wangu Paul Makonda, hii ni kazi ya utumishi kwa wanadamu hapa duniani leo hesabu imeandikwa kesho akhera! Mungu akubariki kwa kuwezesha kurudisha matumaini kwa wenzetu…Amina!”

Wachambuzi wa Masuala ya Kisiasa Watoa Sababu za Rais Magufuli Kurudia Rudia Mambo Katika Hotuba Zake

$
0
0
Wachambuzi wa Masuala ya Kisiasa Watoa Sababu za Rais Magufuli Kurudia Rudia Mambo Katika Hotuba Zake
Wakati Rais John Magufuli akitarajia kufikisha miaka miwili tangu alipoingia Ikulu Novemba 5 mwaka juzi, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameeleza sababu za kiongozi huyo kurudia rudia mambo katika kila hotuba anazozitoa.

Katika hotuba zake, Rais Magufuli mbali ya kuzungumzia mambo mengine, masuala ya watumishi hewa, vyeti feki, vita ya kiuchumi na mafisadi pamoja na mapambano dhidi ya dawa za kulevya amekuwa haachi kuyasemea.

Wachambuzi waliozungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya masuala hayo ambayo wameyaelezea kama ajenda yake kuelekea uchaguzi mkuu na wengine wakitaka asirudi nyuma, aendelee nayo.

Rais Magufuli, amekuwa akiyazungumzia masuala hayo huku akisisitiza Watanzania wazidi kumwombea kwa kuwa vita ya kiuchumi ni ngumu.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRD), Onesmo Ole Ngurumwa alisema kiongozi yeyote anapenda kuzungumzia maeneo aliyoyafanya tofauti na wengine ili kuonyesha mafanikio yake.

“Suala la vyeti feki halikuweza kufanyika huko nyuma... rasilimali amejaribu kwa namna moja au nyingine lakini waliopita nao walifanya,” alisema Ole Ngurumwa

“Lakini Rais anapaswa kuangalia pia yale yanayopaswa kuendelezwa na anapotekeleza hayo anayoyafanya anapaswa kuyaingiza katika Katiba ili huko mbele tusije kupata vyeti feki, watumishi hewa au wezi wa rasilimali,” alisema.

Wakati Olengurumwa akisema hayo, mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila alikuwa na mtazamo tofauti: “Nadhani ni mkakati wake kutumia maeneo hayo kama karata zake kwa uchaguzi wa 2020.”

Kafulila ambaye kwa sasa ni mwanachama wa Chadema alisema kwenye uchaguzi ujao yapo maeneo ambayo Rais Magufuli atayatumia kama karata yake na yapo maeneo upinzani utayatumia kutafuta dola.

Alisema maeneo hayo yatategemea mwenendo wa jumla wa hali ya siasa, uchumi na masuala mengine ya kijamii kufikia wakati huo.

“Inawezekana masuala ya vyeti feki, vita ya ufisadi, watumishi hewa yakawa ajenda za JPM 2020 wakati masuala ya demokrasia na mwenendo wa uchumi na biashara yakawa hoja za upinzani. Kila upande utatumia karata inayoweza kusaidia kuvuna ushindi kutegemea wakati huo hali itakuwaje,” alisema Kafulila.

Aliyekuwa makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut), Dk Charles Kitima hakuwa mbali na Kafulila, alisema Rais Magufuli amekuwa akirudiarudia mambo hayo ambayo anayaona yalikuwa ni tatizo sugu hivyo anataka kuwathibitishia wapigakura wake jinsi anavyoyashughulikia.

Alisema ili kukabiliana nayo, “Lazima yatolewe elimu ya kutosha kwanza. Mfano tunataka Tanzania ya viwanda, hatujaelezwa viwanda vya aina gani, wananchi watachangia nini, wakulima watachangia nini,” alisema Dk Kitima.

Alisema hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alitumia muda mwingine kuwaelimisha wananchi kupinga ubepari kwa kuhakikisha wanatambua jukumu lao, nchi inataka nini na wafanye nini na kwamba elimu ilisaidia kwa sehemu kubwa, “Nyerere alihakikisha wananchi wanakuwa na uelewa wa jambo na alipokuwa akianza utekelezaji kila mtu anajua wajibu wake na hiki ndicho tunakikosa kwa sasa na jukumu hilo si la Rais peke yake, hata wasaidizi wake kwenye wizara wanapaswa kumsaidia.”

Mbunge wa Mkuranga (CCM), Abdallah Ulega alisema masuala hayo ni miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakirudisha nchi nyuma kwa baadhi ya wachache kujinufaisha rasilimali za Taifa na kugeuzwa shamba la bibi.

Alisema Rais Magufuli anapaswa kutilia makazo masuala hayo ili nchi isije kurudi ilikotoka huku akisema hata yeye jimboni kwake amekuwa akizungumzia masuala hayo.

Mwanasiasa mkongwe nchini, Njelu Kasaka alisema: “Unajua kwa sasa tunashindwa kutoa maoni yetu kwa mambo yanayoendelea, tunataka kujua kwanza hivi wanaposema mchochezi au huyu si mzalendo wanamaanisha nini.”

Kasaka aliyekuwa miongoni mwa wabunge 55 walioasisi Kundi la G55 lililotaka kuundwa Serikali ya Tanganyika mwaka 1993, alisema kuna mambo anayoyaona lakini anashindwa kuyazungumzia ahikofia kuitwa mchochezi, “Nchi lazima tuijenge pamoja, hakuna mtu ambaye ni ‘perfect’ lazima asikilize wengine wanasemaje…kwa sasa tuko ‘carefully’ tunaona nchi inavyokwenda tu. Tunataka kuona hii tafsiri ya uchochezi inachukua sura gani.”

Mahakama Yazuia Kikao cha Bunge

$
0
0
Mahakama Yazuia Kikao cha Bunge
Mahakama ya Katiba Nchini Hispania, imezua kikao cha Bunge la Jimbo la Catalonia kilichopangwa kufanyika Jumatatu kuamua suala la uhuru wa jimbo hilo.

Mahakama hiyo imesema, hatua hiyo ni sawa na uvunjaji wa Katiba ambapo uamuzi huo umetokana na pingamizi lililowasilishwa na chama cha Kisoshalisti cha Catalonia ambacho kinapinga jimbo hilo kujitenga.

Mapema Waziri Mkuu wa Hispania, Mariano Rajoy, aliionya serikali ya Catalonia dhidi ya kujitangazia uhuru baada ya kura iliyopigwa Jumapili iliyopita kuamua hatma ya jimbo hilo.
Kiongozi wa Catalonia, Carles Puigdemont alidokeza kwamba, tangazo la uhuru wa jimbo hilo lingetolewa wiki ijayo katika kikao maalum cha Bunge.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images