Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Kimbunga Nate Chawaua Watu 20 Amerika ya Kati

0
0
Kimbunga Nate Chawaua Watu 20 Amerika ya Kati
Kimbunga Nate kimewaua watu zaidi ya 20 nchini Costa Rica, Nicaragua na Honduras huku kikielekea kaskazini upande wa Marekani.
Hali ya dharura imetangazwa katika mataifa kadha ya Amerika ya Kati ambapo watu zaidi ya 20 bado hawajulikani walipo.

Kimbunga hicho kimesababisha mvua kubwa, maporomoko ya ardhi na mafuriko.
Barabara nyingi hazipitiki, madaraja yameporomoka na pia kimesababisha uharibifu mkubwa kwenye nyumba za watu na majengo.
Nchini Costa Rica, watu karibu 400,000 hawana maji na maelfu wengine wameachwa bila makao na wanalala kwenye vyumba vya muda.

Nchini Costa Rica, safari zote za treni zimesitishwa na safari kadha za ndege pia zimefutwa.
Mbuga kadha za taifa ambazo ni maarufu kwa watalii pia zimefungwa kama tahadhari.
Kimbunga hicho pia kimesababisha uharibifu mkubwa kwenye miundo mbinu Nicaragua.
Masachapa Masachapa, about 60km from the city of Managua on October 5, 2017Haki miliki ya pichaAFP

Watabiri wanasema kimbunga Nate kitaimarika na kuwa kimbunga cha ngazi 1 kabla ya kufika tena ardhini pwani ya kusini mwa Marekani siku ya Jumapili.
Kampuni za mafuta zinazohudumu katika Ghuba ya Mexico zimesema zinawahamisha watu kutoka kwenye visima vyake ambavyo vipo maeneo ambayo inatarajiwa kimbunga hicho kitapitia.


Nipo Kwenye Hatari Kubwa Nafatiliwa na Watu Wanaovalia Ninja Nyumbani Kwangu- Ester Bulaya

0
0
Nipo Kwenye Hatari Kubwa Nafatiliwa na Watu Wanaovalia Ninja Nyumbani Kwangu- Ester Bulaya
Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Ester Amos Bulaya, amesema yupo katika hatari kubwa kutokana na kufuatiliwa na watu ambao anahisi sio wazuri huku wakiwa wamevalia mavazi ya ninja, nyumbani kwake wilayani Bunda.

Bulaya ameto taarifa hiyo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Television, na kusema kwamba watu hao walimfuata nyumbani kwake wakiwa na gari ya Noah huku wamevalia kinija, bahati nzuri hakuwepo nyumbani hivyo ndugu zake wakamwambia asirudi  nyumbani siku hiyo.
Ester Bulaya ameendelea kuelezea kwamba watu hao walizunguka kwa baadhi ya ndugu zake akiwemo bibi yake na kumkosa, lakini alienda kutoa taarifa polisi na mkuu wa kituo kuanza kufuatilia suala hilo, lakini haikuchukua muda akahamishwa kituo cha kazi.

Mkuu wa Polisi wa Catalonia Kufikishwa Mahakamani

0
0
Mkuu wa Polisi wa Catalonia Kufikishwa Mahakamani
Mkuu wa polisi latika jimbo la Uhispania la Catalonia, nchini Uhispania Josep Lluis Trapero, anatarajiwa kufika mahakama mjini Madrid kama mshukiwa katika uchunguzi kuhusiana na madai ya kuchochea uasi dhidi ya taifa.

Vikosi vyake vimekuwa vikishutumiwa kushindwa kulinda polisi wa taifa dhidi ya waandamanaji kabla ya kura ya maoni yenye utata juu ya uhuru kufanyika.
Afisa mwingine wa polisi wa Catalonia na wanaharakati wawili wa uhuru watahojiwa kama washukiwa.

Mzozo wa kisiasa juu ya azma ya Catalonia ya kutaka kuwa huru umewaacha maafisa wa polisi katika jimbo hilo katika hali ngumu.
Maafisa wamejipata njia panda katika kuamua juu ya utekelezaji wa wajibu wao wa kikazi wa kulinda sheria na huruma kwa wanaotaka kujitenga kwa jimbo Catalonia na Uhispania.
Wengi walichagua kutotekeleza maagizo ya kusitisha kura ya maoni ya uhuru siku ya Jumapili na kuliachia jukumu la kukabiliana na waandamanaji jeshi la polisi la serikali kuu ya Uhispania.

Mwandamanaji anayeunga mkono uhuru wa Catalonia akiwa karibu na mji wa Barcelona
Kesi hizi zina uhusiano na tukio jingine la awali ambapo maafisa wa polisi walikwama miongoni mwa waandamanaji waliokuwa na hasira wakati wa uvamizi wa majengo ya serikali ya Catalonia.
Catalonia kujitangazia uhuru karibuni
Kamanda wa polisi wa Catalonia, Josep Lluis Trapero, alisifiwa kwa namna alivyoshughulikia shambulio la kigaidi la Barcelona.
Lakini sasa anakabiliwa na maswali kama mshukiwa.

Irene Uwoya Awataka Mashabiki Zake Kukaa Karibu na Rimoti Wanapotazama Filamu Zake

0
0
Irene Uwoya Awataka Mashabiki Zake  Kukaa Karibu na  Rimoti Wanapotazama Filamu Zake
STAA wa filamu Bongo, Irene Uwoya ametoa sharti kwa mashabiki wake kwamba kila wanapokuwa wanataka kutazama filamu zake hasa zile za mapenzi ni vema wakawa na rimoti karibu maana huwa anakuwa ‘deep’ katika kutekeleza ‘script’ inavyotaka, hivyo ni bora kuwa na rimoti kama kutakuwa na watoto
pembeni au watu wanaoheshimiana.

Akichonga na Staa Mix, Uwoya alisema kuwa, amekuwa akijituma ipasavyo katika screen za mapenzi kwa sababu ni miongoni mwa scene anazopenda kucheza kwenye filamu, kwa hiyo rimoti ni muhimu kwa watazamaji.

“Katika sanaa nasimamia mwongozo wa script, inapojitokeza suala la scene za mapenzi huwa nakamua vibaya sana, baadhi ya watu wanakwazika kwa namna ninavyocheza, lakini ushauri kwa wale wazazi ambao ni mashabiki wangu ni vema kila wanapotazama filamu zangu wawe karibu na rimoti ili kuondoa sehemu ambazo zinawakera,” alisema Uwoya.

Kesi ya Yusufu Manji Hukumu Yake Kusomwa Leo

0
0

Kesi ya Yusufu Manji Hukumu Yake Kusomwa Leo
Mfanyabiashara Yusuph Manji (41) amewasili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili yakusomewa Hukumu hii leo Ijumaa.

Manji anakabiliwa na shtaka lakutumia dawa za kulevya na tayari upande wa mshtaka umeshatoa ushahidi na upande wa utetezi umeshatoa utetezi .


Hukumu inatarajia kutolewa leo Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kufunga ushahidi.

CCM Monduli, Shinyanga Wapata Viongozi Wapya

0
0
CCM Monduli, Shinyanga Wapata Viongozi Wapya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli kimemchagua Wilson Lengima Kurambee kuwa mwenyekiti wa chama hicho wilaya baada ya kupata kura 429 akiwaacha mbali washindani wake Amani Silanga Mollel(78) na Hamisi Ramadhani Puzza(9).

Katibu wa CCM wilaya ya Monduli, Gurisha Mfanga ameliambia Mwananchi kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa amani kwa kuzingatia kanuni za chama hicho za kuwapata viongozi wake hatua inayokifanya kuwa chama cha kupigiwa mfano barani Afrika.

Mfanga alisema nafasi ya Katibu Mwenezi wa Wilaya ilinyakuliwa na Lorinyu Mkoosi baada ya kupata kura 68,Jeremia Laizer kura 11 na Sakaya Kabuti hakupata kitu huku waliochaguliwa kuwa wajumbe wa mkutano mkuu taifa ni Paulo Oljumbe Kiteleki aliyepata kura 364, Hussein Ally Warisama (292) na Magdalena Richard Mhina (235).

“Uchaguzi umefanyika kwa amani na utulivu, kipekee ninawashukuru wapigakura na mkuu wetu wa wilaya, Idd Kimanta kwa ushirikiano mkubwa aliouonyesha katika zoezi zima hii inamaanisha Monduli imezaliwa upya na hakuna tena kupangiwa viongozi kama zamani,”alisema Mfanga

Alisema uchaguzi huo unatoa ishara njema ya chama chake kufanya vizuri kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Moita Novemba 26 mwaka huu ambayo diwani wake kupitia Chadema, Edward Sapunyo alijiuzulu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Wakati Monduli wakipata viongozi hao Kanali Tajiri Maulidi aliyekuwa anatetea kiti chake cha uenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ameangukia pua kwa kupata kura 162 dhidi ya mpinzani wake Abubakar Gulam aliyepata kura 246.

Hata hivyo, licha ya Maulid kusema kwamba hana kinyongo na mshindi huyo lakini alisema “zipo kasoro katika chaguzi nawaomba wasimamizi lazima waondoe kasoro hizo, kama vile kura zikizidi lazima mtu alalamike,” alisema bila kufafanua huku akiahidi kutoa ushirikiano

Katika uchaguzi huo wapiga kura walikuwa 408.

Kwa upande wake aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi Jumnne Kitundu ambaye ni katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga aliwataka viongozi hao wasitumie maneno makali ya kuwakashifu wenzake pia aliwataka viongozi wawe na mshikamano ili chama kiweze kusonga mbele.

Awali Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Haula Kachwampa aliwataka viongozi wote waliochaguliwa katika uongozi wawe na upendo kwa kufuata misingi ya chama.

Hayo ameyasema jana kwenye uchaguzi wa mwenyekiti na wajumbe CCM wilaya ya Shinyanga mjini uliofanyika katika ukumbi wa CCM Kambarage.

“Kwa kweli mimi binafsi sijapendezwa na hali ya kuchafuana kwani asili ya chama chetu ni kupendana na kudumisha upendo hivyo tunaomba mtuamini majina tuliyowaletea chama kimejiridhisha,” alisema Kachwampa.

Mauno ya Tshishimbi Yawa Gumzo Mitandaoni Mashabiki Wamtolea Povu

0
0
Mauno ya Tshishimbi Yawa Gumzo Mitandaoni Mashabiki Wamtolea Povu
KIUNGO mkabaji wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DR Congo, jana Alhamisi alikuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya kuzagaa kwa video yake fupi aliyojirekodi akiwa chumbani huku akiimba pamoja na kucheza.

Tshishimbi aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na umahiri wake wa kukaba, alikuwa gumzo kutokana na mazingira ya video hiyo ambayo inamuonyesha aking’ata midomo pamoja na kukata viuno kitendo ambacho kilipokelewa vibaya na baadhi ya mashabiki.

Mashabiki hao walimshambulia kiungo huyo kutokana na kitendo hicho kwa kusema kuwa hakistahili kufanywa na mtu kama yeye ambaye ni miongoni mwa wachezaji wenye majina makubwa kwa sasa hapa nchini.

Nyota huyo aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Mbabane Swallows ya Botswana, wikiendi iliyopita hakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichocheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulimalizika kwa suluhu. Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Uhuru, Dar.

Championi Ijumaa, lilifanya jitihada za kumtafuta kiungo huyo ili aiongelee video hiyo, lakini juhudi zake ziligonga mwamba.

Uingeleza Yaanza kwa Mbwebwe

0
0
Uingeleza Yaanza kwa Mbwebwe
Baada ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi timu ya taifa ya England imethibitisha kuwa na mechi za kujipima uwezo mwezi Novemba dhidi ya Ujerumani na Brazil.

England imefuzu jana usiku kutoka Kundi F bara la Ulaya baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Slovenia. Timu hiyo imefikisha alama 23 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka kundi hilo hata akipoteza mchezo wa mwisho na timu zingine zikashinda.
Baada ya kufuzu chama cha soka nchini humo FA asubuhi hii kimethibitisha kuwa timu yao itacheza michezo ya kujipima uwezo dhidi ya timu za Ujerumani na Brazil ambazo nazo zimefuzu kucheza fainali hizo.

Mchezo kati ya England na Ujerumani utachezwa Novemba 10 kwenye uwanja wa Wembley. Baada ya hapo timu hiyo itacheza na Brazil siku nne baadae kwenye uwanja huo huo.

Uchaguzi Liberia: George Weah Akiri Kuwasiliana na Charles Taylor

0
0
Uchaguzi Liberia: George Weah akiri kuwasiliana na Charles Taylor
Mmoja wa wagombea katika uchaguzi wa urais nchini Liberia na nyota wa soka George Weah amekiri kuwa na mawasiliano na kiongozi wa zamani wa taifa hilo Charles Taylor.
Bw Taylor anatumikia kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makossa uhalifu wa kivita baada ya kuhukumiwa na mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa.

Bw Weah amesema kuwa alipokea simu kutoka kwa mbabe huyo wa kivita, lakini akakanusha kwamba Charles Taylor ana ushawishi wa mambo nchini humo.
Wiki iliyopita, Bunge la Congress nchini Marekani liliidhinisha azimio la kushutumu juhudi zozote za mbabe huyo wa zamani wa kivita za kujaribu kuwa na ushawishi kwenye uchaguzi nchini Liberia kutoka gerezani.

George Weah ni mmoja wa wagombea 11 ambao wamejitokeza kutaka kumrithi Rais Ellen Johnson-Sirleaf ambaye anastaafu.
Makamu wa rais wa Johnson Sirleaf, Joseph Boakai, pia anawania katika uchaguzi huo utakaofanyika Jumanne tarehe 10 Oktoba.
Charles Taylor anatumikia kifungo cha miaka 50 jela UingerezaHaki miliki ya pichaAFP

Kuna mwanamke mmoja pekee aliyejitokeza kuwania, MacDella Cooper, ambaye alikuwa mwanamitindo lakini kwa sasa ni mfanyakazi wa hisani.
Jewel Howard-Taylor, 54, mke wa zamani wa Charles Taylor ni mgombea mwenza wa Bw Weah.

Wadukuzi wa Mitandao Wafanya Yao Waipeperusha 'Natamba' ya Aslay You Tube

0
0
Wadukuzi wa Mitandao Wafanya Yao Waipeperusha 'Natamba' ya Aslay  You Tube
Kwa sasa ukimtaja Aslay basi hautaacha kutaja uwezo wake aliyonao katika muziki wa Bongo Flava, kwani amesha toa hits kadhaa kwa kipindi kifupi ikiwemo ‘Natamba’ ambayo imezua kizaazaa katika mtandao wa YouTube.

Ngoma ya ‘Natamba’ ilikuwa namba mbili trending siku ya jana  YouTube, ila kutokana na hali ya sinto fahamu ngoma hiyo imepotea katika mtandao huo na kushuka kabisa katika nafasi iliyokuwepo.

Kwa mujibu wa meneja wake MX Carter ameripoti kusikitishwa na tukio hilo na amedai kuwa kuwepo kwa  watu  wasiopenda maendeleo ya msanii huyo na kuamua kuiripoti ‘Natamba’ ishuke Youtube.

“Naona wabaya wasiopenda maendeleo ya AslayIsiaka wamereport video ishuke YouTube… bahati nzuri team ya ufundi inajitaidi kuweka sawa,” ameandika Mx katika Twitter.

Akaongeza kuandika katika mtandao wa Instagram “Poleni kwa mnaopata usumbufu kuiona Video mpya ya AslayIsihaka kama ujumbe unavyoongea hapo juu tuko kwenye jitiada za kuirudisha popote ilipokuwa ikionekana haswa kwenye trending mungu akipenda. Video imekuwa reported na iko Undereview na Youtube na tunajitaidi kuiweka sawa! Ukitaka kuangalia video ya aslay for Now ingia kwenye Bio yake au Search on YouTube.”

Peter Okoye wa P-Square Asaini Mkataba Mnono na Kampuni ya Marekani

0
0
Peter wa P-Square Asaini Mkataba Mnono na Kampuni ya Marekani
Peter Okoye maarufu kama Mr P, kutoka kundi la P-Square amesaini mkataba na kampuni ya usambazaji wa muziki ya Empire kutoka Marekani.

Neema hiyo imemdondokea msanii huyo baada ya hivi karibuni kuibuka kwa tetesi za kuvunjika kwa mara ya pili kwa kundi lao la muziki ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu walipoliunda tena baada ya kuvunjika mwaka jana.

Msanii huyo ameonyesha kufurahia hatua hiyo kwa kuandika kwenye mtandao wake wa Instagram, “Thank you Lord🙏🏽😇 RepostBy @empire: “Just had a digital distribution deal with @peterpsquare! Welcome to the #EMPIRE family!” (via #WhizRepost @AppsKottage).”

Kampuni ya Empire ambayo makao yake makuu ni San Franciscomjini California, inafanya kazi na wasanii wakubwa kama Kendrick Lamar pamoja na makampuni mengine makubwa duniani.

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Wema Sepetu Afunguka Kurudiana na Daimond Asema 'Sijawahi Kufikiria Kurudisha Moyo Wangu'

0
0
Wema Sepetu Afunguka Kurudiana na Daimond Asema 'Sijawahi Kufikiria Kurudisha Moyo Wangu'
MUIGIZAJI mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Sepetu ‘Keki ya Taifa’, amekanusha ishu ya inayovuma mitandaoni kuwa anatamani kurudiana na X-wake ambaye ni Mbongo Fleva, kwa kusema hawezi kamwe kurudiana naye kwani mpenzi wake wa sasa anampa furaha ya kutosha.
Wema alifikia hatua ya kuandika ujumbe wa kukanusha skendo hiyo, baada ya hivi karibuni kuenea kwa ubuyu kuwa yeye na Mbongo Fleva huyo wamerudiana tena, anadiriki hadi kwenda kwake kupika, jambo ambalo lilimchanganya na kuamua kulitolea ufafanuzi.

Wema na X-wake huyo, waliwahi kuwa ‘Couple’ ambayo ilitikisa jiji, baadaye wakamwagana na kisha X-wake huyo kujiingiza kwenye ulimwengu wa huba na mfanyabiashara maarufu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss lady’ ambapo amezaa naye watoto wawili, lakini pia ni baba wa mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobeto anayeitwa Prince Abdul.

Watu Watano Wauawa Kwa Katika Mjibizano ya Risasi na Polisi

0
0
Watu Watano Wauawa Kwa Katika Mjibizano ya Risasi na Polisi
Watu watano wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wameuawa katika eneo la Toangoma jijini Dar es Salaam, katika  majibizano ya risasi na Polisi yaliyotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Lukula amesema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna njama za uhalifu zimepangwa kufanyika maeneo hayo usiku wa jana, hivyo wakajipanga kwa ajili ya kudhibiti.

Amesema ilipofika muda  walioambiwa kweli wahalifu hao ambao idadi yao haikuweza kupatikana, lakini walikuwa wengi, wakafika eneo la tukio na kupambana na polisi.

“Majibizano ya silaha yalikuwa makubwa kwa sababu walikuwa na silaha nzito, lakini Jeshi la Polisi lilijipanga imara kuwadhibiti na kufanikiwa kuua watano na wengine wakatokomea kusikojulikana,” amesema.

Amesema wananchi wasiwe na hofu na waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kunusuru usalama wao na mali zao.

“Tumejipanga na tunapopata taarifa za uhalifu, pamoja na askari wetu kuwa doria maeneo hayo, lakini hujipanga upya kwa ajili ya kupambana na tukio husika.” 

IGP Sirro Atoa Onyo kwa Wapinzani Awataka Kuacha Kuingilia Kazi ya Polisi Katika Upelelezi wa Shambulio la Tundu Lissu

0
0
IGP Sirro Atoa Onyo kwa Wapinzani Awataka Kuacha Kuingilia Kazi ya Polisi Katika Upelelezi wa Shambulio la Tundu Lissu
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro amefunguka na kuwataka wanasiasa nchini kuacha kuingilia kazi ya jeshi la polisi ikiwepo upelelezi wa tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

IGP Sirro amesema hayo siku moja baada ya viongozi mbalimbali wa upinzani kutoa kauli kuhusu jeshi hilo la polisi na kusema kuwa hawana imani na uchunguzi ambao unafanywa na jeshi hilo dhidi ya tukio la kupigwa risasi kwa Mbunge Tundu Lissu Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.

Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Godbless Lema wa Arusha pamoja na Mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini ni kati ya wabunge ambao walionyesha kusikitishwa na kauli ambayo aliitoa IGP Sirro akiwa mkoani Mtwara kuhusu uchunguzi wa sakata la Tundu Lissu na kusema kuwa dereva wa Lissu anachelewesha upelelezi wa sakata hilo.

Wabunge hao walikwenda mbali zaidi na kusema wao wanaona jeshi la polisi halihitaji kufanya uchunguzi wa kina juu ya sakata hilo kwa kuwa jeshi hilo linafahamu nini kipo nyuma ya tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu akiwa mjini Dodoma. Kufuatia kauli hizo IGP ndipo amefunguka na kuwataka wanasiasa kuacha kuingilia kazi ya jeshi la polisi ikiwa pamoja na uchunguzi wa sakati hilo.

Tunda Aliamsha Dude Amuumbua Young Dee Hadharani

0
0
Tunda Aliamsha Dude Amuumbua Young Dee Hadharani
‘Couple’ ambayo haieleweki kama imeachana au Lah! Ni ya Hit Maker wa ngoma ya Kiutani Utani, David Genz ‘Young D’ na muuza nyago kunako video za wasanii, Tunda Sebastian, ambao hivi karibuni wamezua gumzo mitandaoni kufuatia kauli ya Tunda, aliyoahidi kuwa atamdhalilisha Mbongo Fleva huyo, kisa mzigo wake anaomdai.
Tunda alishangaza umma kwa ku-komenti kwenye picha ya Young D, na kumtolea kauli hiyo, na kuwaacha mashabiki njia panda huku wakijiuliza wawili hao wanadaiana nini? Na je hicho wanachodaiana walipeana lini na wapi? Wakati inasemekana kuwa walishapigana kibuti muda mrefu.

Wengine wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa Tunda na Young D, hawawezi kuachana kwani wanapendana sana, huku wengine wakimtupia lawama Mbongo Fleva huyo kuwa kwa sasa amekuwa mpenda kiki sana, kwani juzi tu alikuwa na ugomvi na Amber Lulu, kisa picha zao za utupu leo tena Tunda! Kwa hiyo inawezekana kuwa ni kiki tu ya ku-promote ngoma yake mpya ya Kiutani Utani.

Aunt Ezekiel Amshushia Mvua ya Matusi Aliyemtongoza Mose Iyobo

0
0
Aunt Ezekiel Amshushia Mvua ya Matusi Aliyemtongoza Mose Iyobo
USIONE chaelea kimeundwa! Huo ndiyo msemo uliopo akilini mwa muigizaji nyota nchini, Aunt Ezekiel, ambaye yu mapenzini na dansa, Mose Iyobo, ambapo ameshusha mvua ya matusi kwa mtu asiyejulikana kwa kile anachodai kuwa mtu huyo, anamtongoza mwandani wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Aunt alijikuta akijivua sifa ya mwanamke mwenye roho ya Kizungu, baada ya kushuhudia ‘vimeseji’ Inbox kwenye akaunti ya Mose ya Instagram, akitongozwa na mtu ambaye anamfahamu na huenda ni shoga’ake, ila hajataka kuweka wazi ni nani.
Kitu kikubwa alichokuwa akilalamikia Aunt, ni kwa nini hawakumtongoza Mose kipindi ambacho hakuwa naye? Tangu kamkamata na kumpa matunzo ndiyo wanamnyapianyapia!

Chadema Yawatupia Maswali kwa IGP Sirro,Mwigulu Sakata la Lissu, Saanane na Nape

0
0
Chadema Yawatupia Maswali kwa IGP Sirro,Mwigulu Sakata la Lissu, Saanane na Nape
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimehoji maswali kibao kwa  Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP), Simon Sirro kuhusu mambo yanayoendelea kwenye upelelezi wa Ben Saanane, Tundu Lissu na aliyemtishia Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

Saanane ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye hajulikani aliko na Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu.

Katika mkutano na waandishi wa habari leo Ijumaa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema ameanza kwa kusema,  “Ni siku 695 tangu Mawazo(Alphonce) auawe, siku 326 tangu Ben Saanane apotezwe na watu wasiojulikana na leo ni siku 26 tangu Lissu afanyiwe jaribio la kumuua na mpaka sasa polisi hawajasema lolote, zaidi ya Nissan 8 na zimehifadhiwa kusikojulikana,”

“Leo tunapozungumza, viongozi mbalimbali wanaendelea kutishwa, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya anatishwa na watu wamemfuata nyumbani kwake, Josua Nassari ametishwa, Lema(Godbless) ametishwa,”

“Ben Saanane alitishwa na alitoa taarifa Kituo cha Polisi Tabata na kapotea, Lissu alitoa taarifa kwamba anatafutwa na yaliyotokea mnajua,”

“Hofu ni kubwa, maiti zaidi ya 17 zimeokotwa Coco Beach hakuna ‘seriousness’ kwa matukio,” amesema Mrema

“Waziri anatishwa mbele ya kamera na hakuna jitihada, IGP anasema hajui alipo, hii inaonyesha hakuna ‘seriousness’ katika kupambana,” amesema Mrema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Kigaila Benson amesema, “Haya mambo si ya kawaida, yanafanywa na watu wasio wa kawaida, niseme tu hakuna aliye salama, hujui kesho yako,”

“Kuna kijana anaandika mambo ya ajabu, kwa nini polisi hawaoni, IGP anachagua mambo ya kusikia, kwa nini ukimkosoa Rais jioni yake unakamatwa,”

“Kama polisi wanaona, hawachukui hatua? Walipouawa polisi pale Mbagala, watu waliotuma picha walikuwa Mahenge, walikamatwa sasa huyu kijana anafanya nini?

“Wanasema wamekamata Nissan, hivi hizi Nissan zilikuwa wapi, zilikuwa zinaendeshwa na nani? Hii si ni kanya boya?

“Waziri Mwigulu anasema gari alilolitaja Lissu liko Arusha, waziri ametumia kigezo au kifaa gani kubaini gari halikuwahi kufika Dar? Kwa nini chombo hicho kisitumike kuwabaini waliomshambulia Lissu?

“Mwigulu kwa nini amechukua uwakili wa mtuhumiwa? Amehojiana vipi na huyo? Kwa nini mtu huyo anayetuhumiwa asikamatwe na sasa anafanya kazi ya kumtetea?

“Polisi wanatakiwa kutuambia, upo wapi usalama wa Rais,” “Tumesimama upepelezi wa tukio la Lissu kwa sababu ya dereva, ina maana kama dereva angekufa upepelezi usingekuwapo?

“Sisi hatuwezi kumficha dereva, anapata matibabu, ila kama wamesema wanafahamu gari lile lipo Arusha wanashindwaje kwenda kuzungumza na dereva,” amehoji Kigaila

“Sirro analitumia jeshi kisiasa, Sirro kwa nini asimuulize RPC Kaganda(Suzan) aliyekuwa Kinondoni ambaye alikuwapo siku Nape anatolewa bastola kwa nini hawakumkamata,”

“Jeshi la polisi ni letu sote, tusilitumie kisiasa, tunataka tueleweke kwamba IGP wanamjua huyu mtu,”

“Kwa nini wanamtafuta mtu ambaye walikuwa naye, hivi kwa nini maswali magumu wanakuwa na majibu ila maswali mepesi wanakosa majibu,”

Manji Aachiwa Huru Baada ya Serikali Kushindwa Kuthibitisha Madai Yake

0
0
Manji Aachiwa Huru Baada ya Serikali Kushindwa Kuthibitisha Madai Yake
Mfanya biashara Yusuf Manji leo Oktoba 6 2017 amefutiwa kesi iliyokuwa ikimkabili ya kutumia dawa za kulevya.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kufunga ushahidi.
Sababu ambayo imepelekea kufutwa kwa kesi hiyo imetajwa kuwa ni upande wa mashtaka ambao ni serikali kushindwa kuthibitisha kosa la mtuhumiwa, Yusuf Manji.
Katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya Februari 6 na 9, eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine

Mahakama imemuachia huru Manji ikiwa ni siku chache tangu shauri lake jingine la Uhujumu uchumi liondolewe Mahakani hapo na Mkurugenzi wa mashitaka (DPP) ambaye alieleza kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Manji amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga ambapo alijiuzulu wadhifa huo mapema mwaka huu. Pia Manji alikuwa Diwani wa Kata ya Mbagala kabla ya kuvuliwa nafasi hiyo baada ya kupoteza sifa.

Trump Huenda Akajiondoa Mkataba wa Nyuklia wa Iran

0
0
Trump Huenda Akajiondoa Mkataba wa Nyuklia wa Iran
Rais wa Marekani Donald Trump anapanga kuiondoa Marekani kutoka kwenye mkataba wa nyuklia kati ya nchi za Magharibi na Iran, taarifa kwenye vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti.
Iwapo atakataa kuidhinisha mkataba huo, bunge la Congress litalazimika kuamua iwapo litaiwekea tena Iran vikwazo.

Bw Trump ana hadi tarehe 15 Oktoba kufanya uamuzi wake.
Kiongozi huyo alikuwa ameukosoa sana mkataba huo kwenye kampeni za uchaguzi wa urais mwaka jana.
Alipokuwa anapigwa picha akiwa na viongozi wa kijeshi Alhamisi, Trump alisema kuna "utulivu kabla ya tufani" lakini akakosa kutoa maelezo zaidi.

Kulikuwa na fununu kwamba huenda alikuwa anazungumzia kuongezeka kwa uhasama kati ya nchi hiyo na Korea Kaskazini.

Lakini gazeti la New York Times limesema "watu ambao wamepashwa habari kuhusu suala hilo" wanaamini alikuwa anaizungumzia Iran.
Trump alionekana akiwa White House na mke wake, pamoja na viongozi wa jeshi, baada ya mikutano Alhamisi lakini kabla ya chakula cha jioni.
Huku akiashiria kwa vidole watu ambao walimzunguka, aliwauliza wanahabari iwapo wanafahamu "hili linawakilisha nini".
"Pengine ni utulivu kabla ya tufani," alisema.
Wanawahabari walipomsisitizia afafanue ni tufani gani alilokuwa akizungumzia, aliwaambia tu: "Mtagundua."

Trump na Rais wa Iran Hassan Rouhani walishutumiana mkutano wa UN mwezi jana
Alikuwa awali amewaambia maafisa wake wakuu wa ulinzi kwamba anatarajia wampe "njia nyingi mbadala za kijeshi ... kwa haraka zaidi" siku zijazo.
Urusi imesema mkataba huo wa silaha na Iran unafaa kudumishwa jinsi ulivyo.
Waziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov alisema taifa lake linatumai kwamba Marekani itafanya uamuzi wa busara bila kuumia upande wowote.
Maafisa wa Umoja wa Ulaya pia wamesema wanaunga mkono mkataba huo.
Nini kitafanyika sasa?

Vyombo vya habari Marekani vinasema rais huyo Alhamisi ijayo atatangaza kwamba hataidhinisha mkataba huo kwa sababu haujali maslahi ya Marekani kiusalama.
Lakini baadhi ya washauri wake wakuu wa usalama, akiwemo Waziri wa Ulinzi James Mattis wanaonekana kuunga mkono mkataba huo.
Rais wa Marekani hutakiwa kuidhinisha mkataba huo kila baada ya siku 90; na Trump ameuidhinisha mara mbili.

Iwapo atakataa kuuidhinisha wakati huo, bunge la Marekani litakwua na siku 60 kuamua iwapo litaiwekea tena vikwazo Iran.
Vyombo vya habari Marekani vinadokeza kwamba huenda Bunge likaamua kudumisha hali ya sasa bila kuweka vikwazo vipya.

Akiongea kwenye mkutano na wakuu wa jeshi White House, Trump alisema: "Utawala wa Iran huunga mkono ugaidi na umekuwa 'ukiuza nje' ghasia na vurugu kote Mashariki ya Kati."
"Ndio maana ni lazima tufikishe kikomo uchokozi huu wa Iran na ndoto zake za nyuklia. Mtasikia kutoka kwangu karibuni kuhusu Iran."

Mkataba huo wa mwaka 2015 ulitiwa saini kuzuia Iran kustawisha silaha za nyuklia.
Rais wa Marekani hutakiwa na kutoa idhini kwa Bunge la Congress kuendelea kuudumisha kila baada ya siku 90.
Ufaransa, Ujerumani, Uchina, urusi na Uingereza ni wahusika katika mkataba huo ambao uliondoa baadhi ya vikwazo ambavyo viliizuia Iran kufanya biashara masoko ya kimataifa na kuuza mafuta.

Kuondolewa kwa vikwazo hiyo kulitegemea Iran kusitisha mpango wake wa nyuklia.
Inafaa kupunguza shehena yake ya madini ya uranium, na isijenge vinu vingine vya nyuklia kwa miaka 15 na pia iruhusu wakaguzi nchini humo.
Trump amekwua akisema mara nyingi kwa Iran imekiuka "moyo" wa mkataba huo.
Katika hotuba kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Trump aliutaja mkataba huo uliofanikishwa na mtangulzii wake Barack Obama kuwa "aibu kwa Marekani".
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images