Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

TCU Yatangaza Idadi ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Kikuu Mwaka wa Masomo 2017/18

$
0
0
TCU Yatangaza Idadi ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Kikuu Mwaka wa Masomo 2017/18
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetaja idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu awamu ya kwanza ya udahili katika mwaka wa masomo 2017/18.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Eleuther Mwageni ameeleza kuwa waliochaguliwa kujiunga na elimu ya juu kwa awamu hii ni 44,627 ambao ni 57.4% na waliosalia ni 33,129 ambao ni 42%. Ambao wamesalia hawakuchaguliwa kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoziomba

Soko la Gikomba, Nchini Kenya Lateketea kwa Moto

$
0
0
 Soko la Gikomba, Nchini Kenya Lateketea kwa Moto
Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa imeteketea baada ya moto kuzuka katika soko kuu la wazi nchini kenya, soko la Gikomba jijini Nairobi.
Moto huo ulizuka mwendo wa saa tisa usiku.


Ijumaa asubuhi, baada ya moto huo uliowaka kwa saa kadha kuzimwa, wachuuzi walikuwa wakichakura kutafuta bidhaa ambazo hazikuungua moto.
Soko la Gikomba ni miongoni mwa masoko makubwa zaidi Afrika Mashariki.
Wengi wa wachuuzi huuza nguo na bidhaa nyingine za mitumba.
Mmoja wa wachuuzi amemwambia mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi kwamba amepoteza marobota 250 ya nguo ya thamani ya karibu dola 23,000 za Marekani (Ksh2.3m).

Sheria Inasemaje Kuhusu Madai ya Kulea Mtoto ya Mobetto

$
0
0
Sheria Inasemaje Kuhusu Madai ya Kulea Mtoto ya  Mobetto
Baada ya taarifa kusambaa kuwa Mrembo Hamisa Mobeto ambae ni Mzazi mwenzake na Diamond Platnumz kwamba amempeleka Staa huyo Mahakamani kwa madai ya kutomuhudumia mtoto wake, Mwanasheria wa kujitegemea Jebra Kambole amefungua picha kamili ya sheria yenyewe.

Jebra amesema “Kwanza Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inapiga marufuku kwa mtu yeyote ambae ni Mwandishi wa Habar kutoa taarifa au picha za Mtoto ambae kuna kesi yake Mahakamani lakini kwa kesi ambazo zinahusiana na Wazazi au madai ya matunzo ya mtoto hiyo sio kesi ya mtoto bali ya Watu wazima”

“Kesi za Wazazi kwa Wazazi Baba na Mama wanapopelekana kuhusu matunzo ya mtoto ni kesi ambazo ni za kimadai na zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya madai, Wazazi wanapodaiana kuhusu matunzo Mahakama inazingatia kuangalia zaidi mtoto wakati wa kuendesha shauri hilo”

“Mahakama mara nyingi kwenye kesi kama hii inazingatia madai na kuyapima, wakati wa kutoa gharama za matunzo Mahakama inaangalia vitu kadhaa ukiwemo uwezo wa kipato cha Wazazi wote wawili lakini pia inaangalia majukumu ya kiuchumi ya Mzazi anaedaiwa”

Unapenda Habari za Siasa? Download App ya Mchambuzi Hapa

$
0
0
Kama we ni Mpenzi wa Habari za Siasa Usipitwe na Hii Application ya Mchambuzi.....

Bonyeza HAPA Kudownload kwenye Simu yako

Breaking News: Kiwanda cha Super Doll Chateketea kwa Moto

$
0
0
Kiwanda cha Super Doll Chateketea kwa Moto
Moto mkubwa umeteketeza kiwanda cha Super doll kilichopo barabara ya Nyerere Dar es Salaam mchana wa leo, na kuteketeza mali za kiwanda hicho.

Akiongea na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Kamanda wa polisi mkoa wa Temeke, Gilles Muroto, amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, na jeshi la zimamoto linafanya jitihada za kuzima moto huo.
"Ni kweli tuko hapa jeshi la zimamoto linaendelea kuzima moto likishirikiana na jeshi la polisi, na mpaka sasa bado hatujajua chanzo cha moto huu", amesema Kamanda Muroto.
Katika tukio hilo la kuzima moto huo kulijitokeza changamoto kubwa ya magari ya kuzima moto, ambapo kati ya magari 10 ya zimamoto moja ndilo lenye uwezo wa kuzima moto katika kiwanda hicho.

Wabunge Kupewa Donge Nono la Fedha Ili Kutoa Ushauri Ukomo wa Umri wa Urais

$
0
0
Wabunge Kupewa Donge Nono la Fedha Ili Kutoa Ushauri Ukomo wa Umri wa Urais
Kila mbunge anatarajiwa kupewa kiasi fulani cha fedha zitakazomsaidia kupata ushauri kwa wapigakura jimboni kwake kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria wa 2017 unaolenga kuondoa ukomo wa umri kwa wagombea urais.

Baada ya muswada huo kusomwa kwa mara ya kwanza na Raphael Magyezi, mbunge wa Igara Magharibi kutoka chama tawala cha NRM, kisha kupelekwa katika Kamati ya Kudumu ya Sheria na Huduma za Bunge, Jumanne Spika Rebecca Kadaga aliwataka wabunge kwenda kushauriana na wapigakura wao.

Baada ya uamuzi huo wa Spika, mnadhimu mkuu bungeni Ruth Nankabirwa amesema Tume ya Bunge inafikiria kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kuwarahisishia wabunge.

“Tume ya Bunge inajiandaa kutengeneza bajeti kwa sababu ni Bunge ambalo litaturahisishia sisi sote …Tutaelezwa ni kiasi gani na namna gani kila mbunge atapata na kwenda kushauriana kwa sababu tunahitaji usafiri,” Nankabirwa ameviambia vyombo vya habari.

Nankabirwa hakuweka wazi undani wa bajeti hiyo akisema tu kwamba Tume ya Bunge ndiyo itapanga na kubainisha kiasi kinachohitajika. Lakini mbunge wa Kakumiro kutoka NRM, Robinah Nabbanja ambaye ni mjumbe wa Tume ya Bunge alisema mgawo huo utakuwa kwa wabunge wote bila kujali vyama vyao.

“Tutakutana haraka na kukubaliana. Sitaweza kukutajia kiwango kwa sasa kwa sababu bado hatujakubaliana. Huwezi kuwatuma wabunge (kupata ushauri) bila kuwawezesha kiasi,” amesema Nabbanja.

Kuhusu suala la wapi fedha hizo zitatoka hasa ikizingatiwa hazijatengwa katika bajeti ya sasa, Nabbanja amesema watapunguza kutoka kasma ya safari za nje.

“Jambo lolote linapokuwa la dharura, kwa kawaida huwa tunagusa fedha za usafiri wan je, tunaweza kuhamisha vifungu ndani ya bajeti,” amesema.

Mnadhimu wa kambi ya upinzani Ibrahim Ssemujju amepuuza uwezeshaji huo akiuelezea kuwa ni jaribio la “kusafisha rushwa kwa wabunge”.

Kundi la Kupinga Silaha za Nyuklia Lashinda Tuzo ya Amani ya Nobel

$
0
0
Kundi la kupinga silaha za nyuklia lashinda Tuzo ya Amani ya Nobel
Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka huu imetunukiwa kundi la kimataifa linalopigania kupigwa marufuku kwa silaha za nyuklia duniani.

Kamani ya Nobel nchini Norway imesema kundi hilo limekuwa shirika kuu la kiraia linaloongoza juhudi za kupigwa marufuku kwa silaha hizo chini ya sheria za kimataifa.
Kamati hiyo, inayoamua mshindi wa tuzo hiyo, imezihimiza nchi zenye silaha za nyuklia kuanzisha mazungumzo kuhusu kumaliza silaha hizo polepole.

Mwaka uliopita, Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ndiye aliyeshinda tuzo hiyo kwa sababu ya juhudi zake za kusitisha vita nchini humo kwa kufanikisha mkataba wa kusitisha vita na waasi wa Farc nchini humo.

Wolper Afunguka Salamu ya Harmonise Siku ya Birthiday ya Daimondi Asema 'Salamu Aikataliwi Yeye ndo Kaja Kunisalimia Maskini'

$
0
0
Wolper Afunguka Salamu ya Harmonise Siku ya  Birthiday ya Daimondi Asema 'Salamu Aikataliwi Yeye ndo Kaja Kunisalimia Maskini'
Muigizaji wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameweka wazi juu ya salamu aliyosalimiana na  ex-boyfriend wake Harmonize katika private part ya Diamond siku ya tarehe 02/10/2017.

Akiongea kupitia kU-Heard ya Clouds Fm, mrembo huyo ameeleza kuwa  jambo la yeye kumsalimiana na Harmonize halikuwa tatizo kwani salamu haikataliwa.

“Siwezi kumshangaa sasa kwa nini nimshangae, mimi siwezi kumshangaa bhana yeye si ndo kaja kunisalimia masikini, coz nilikuwa nimekaa na Aunty akaja akanisalimia sasa sijui kama salamu inakataliwa, hata ingekuwa wewe umesalimiwa ungekataa hata ingekuwa wewe ungekataa,” amesema mrembo huyo.

Pia Wolper akadai kuwa hakutokea na mpenzi wake huyo katika sherehe hiyo kwani w alikuwa anaumwa kwa takribani siku tano na kuhusu kufutwa kwa picha zake mtandao wa kijamii wa Instagram, mrembo huyo amedai hafahamu kuhusu ilo kwani hajaingia katika mtandao huo.

Kigaila Alitupia Lawama Jeshi la Polisi Kushindwa Kumkamata Kijana Anaeendelea Kuandika Vitisho Mtandaoni Juu ya Lissu

$
0
0
Kigaila Alitupia Lawama Jeshi la Polisi Kushindwa Kumkamata Kijana Anaeendelea Kuandika Vitisho Mtandaoni Juu ya Lissu
Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda, Benson Kigaila amefunguka na kulilamikia jeshi la polisi kushindwa kumkamata kijana ambaye anaendelea kuandika vitisho kwenye mtandao wa jamii juu ya Tundu Lissu.

Kigaila amesema kuwa kabla ya Mbunge wa Singida Mashariki kupigwa risasi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma huyo kijana kupitia mitandao ya kijamii aliomba apewe ruhusa ya kumuuwa Lissu kwa mikono yake mwenyewe. Kigaila amedai kuwa kijana huyo hivi sasa ameendelea kuandika ujumbe mbaya zaidi kupitia mitandao hiyo hiyo ya jamii bila ya polisi kumchukulia hatua zozote zile.
"Sasa huyo kijana anaandika vibaya zaidi anasema 'Anasikitika sana kwa mtu aliyefanya hilo tukio la kumpiga Lissu anasema alitegemea asikie Lissu amekufa siyo kwamba Lissu amejeruhiwa na anasema wanamsubiri Lissu atakaporudi Tanzania mara hii hawatafanya kosa, wanasema walifanya kosa Dodoma sasa huyu mtu awe ni yeye kweli au si yeye aliyefanya tukio hilo, awe ni mwendawazimu au si mwendawazimu tulitegemea polisi wawe wameshamkamata wapo naye wanamuuliza haya anayosema ni kwa sababu gani lakini polisi halimuoni huyo kijana" alisema Kigaila
Aidha Kigaila amesema kuwa kitendo cha polisi kutomchukulia hatua kijana huyo kinazidi kuwapa mashaka kuwa huenda wanamtambua huyo kijana lakini hawataki kumkamata kwa sababu zao binafsi.

Imamu Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 30 Jela kwa Kosa la Kulawiti

$
0
0
Imamu Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 30 Jela kwa Kosa la Kulawiti
Mkazi wa Gongo la Mboto, Dar es Salaam, Imamu Hassan (37) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka 13.

Hassan amehukumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Rita Tarimo, wakati wa shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya hukumu.

Hakimu Rita amesema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi watano ambao wamethibitisha shitaka pasi kuacha shaka.

Akipitia baadhi ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu Rita amesema mtoto huyo alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo mara kwa mara na baadae kumpa sh. 2,000 huku akimuamuru asidhubutu kumwambia mtu yoyote.

Mpinzani wa Kagame Diane Rwigara Afikishwa Mahakamani Rwanda

$
0
0

Mpinzani wa Kagame Diane Rwigara afikishwa mahakamani Rwanda
Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara, mamake na dadake wamdefikishwa mahakamani mjini Kigali kwa mara ya kwanza wiki mbili baada ya kuzuiliwa na polisi.
Watatu hao wameshitakiwa kuchochea uasi nchini, mashtaka wanayokanusha wakisema yana misingi ya kisiasa.

Diane Rwigara alizuiwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mwezi wa 8 mwaka huu ambapo Rais Paul Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana mjini Kigali anasema chumba cha mahakama kilikuwa kimejaa watu wengi miongoni mwao wanadiplomasia wa baadhi ya nchi za Magharibi na Marekani.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa, watuhumiwa hao watatu waliingizwa mmoja baada ya mwingine katika chumba cha mahakama huku wakifungwa pingu.

Jaji alifungua kikao kwa kusikiliza hoja ya watuhumiwa, Diane Rwigara na Mamake Adeline Rwigara wamesema wana tatizo la kuwasiliana na mawakili wao.
Wamesema wameweza kuwasiliana mara moja tu kabla ya mawakili kukataliwa kuwaona tena huku Dadake Anne Rwigara yeye akisema kuwa hajapa wakili.
Wote wameomba kesi kuahirishwa ili kupata muda zaidi wa kutayarisha kesi dhidi yao.

Hoja hiyo imekubaliwa kwa kesi kuahirishwa hadi Jumatatu wiki ijayo.
Mashitaka yanayowakabili yalikuwa tayari yamewekwa hadharani na mwendeshamashtaka kabla ya wao kufikishwa mahakamani leo.Wote watatu wameshitakiwa kuchochea uasi miongoni mwa wananchi.

Zaidi ya hayo, Diane Rwigara ameshtakiwa kughushi nyaraka huku Mamake Adeilne Rwigara akishtakiwa pia kosa la kugawa wananchi kwa misingi ya kikabila.
Awali walipokuwa katika ngazi ya upelelezi wa mwanzo walishitakiwa makosa ya kutaka kuiangusha serikali na ulaghai wa

Wote wanapinga mashitaka dhidi yao wakisema yana misingi ya kisiasa.Diane Rwigara mwenye umri wa miaka 35 alizuiliwa kugombea kiti cha urais uliofanyika mwezi wa 8 mwaka huu.
Tume ya uchaguzi ya Rwanda ilisema kwamba alifanya ulaghai katika kutafuta saini za wafuasi wake ili kutimiza matakwa ya tume hiyo.

Tangu ulipoanza mchakato huo wa kutaka kuingia ikulu,Diane Rwigara amejitokeza kama mpinzani na mkosoaji mkuu wa chama tawala RPF.
Na baada ya kukataliwa kugomea urais alianzisha vugugugu alilotaja kuwa na lengo la kupinga uonevu na kupigania haki miongoni mwa wananchi.
kukwepa kulipa kodi, lakini makosa hayo yalifutwa.

Hatimaye Siri yafichuka Kuhusu Alikiba na Jokate

$
0
0
Mahusiano kati ya msanii Alikiba na aliyeaminika kuwa mpenzi wake Jokate Mwegelo, ambaye ni mwanamitindo na mjasiriamali anayetazamwa na dunia nzima, bado yanaendelea kwa upande wa kazi za sanaa, ambapo wawili hao ni mtu na bosi wake.

Siri hiyo imetolewa na msanii Abby Skills ambaye pia ni mtu wa karibu na Alikiba na moja ya msanii ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Alikiba, alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, na kusema kwamba Jokate yupo chini lebo ya Alikiba, ambayo pia yeye yupo.

 “Mimi pia nipo chini ya lebo yake, Alikiba  ni bosi wangu, kuna Abdu Kiba, kuna Salim, kuna Heri, kuna Jojo Jokate”, amesikika Abby Skills akitoa siri hiyo ambayo hakutakiwa kuiweka wazi kwa mujibu wake mwenyewe.

Alikiba na Jokate waliwahi kuwa na tetesi kuwa na mahusiano ya kimapenzi, na hivi karibuni Alikiba alisikika akisema hadharani kwamba hana mahusiano na mwanamitindo huyo.

TID na Prezzo Watoleana Povu Kisa Amber Lulu...Prezzo Ashauriwa Kutumia Condom

$
0
0
Hali si shwari kati ya wasanii wawili TID wa bongo na Prezzo wa Kenya, baada ya wawili hao kurushiana maneno ambayo yalionekana kumkera mmoja wapo kisa kikiwa ni Amber Lulu.

Balaa limeanza pale ambapo TID alimshauri Prezzo kutumia kinga tena ya gharama zaidi, iwapo anajihusisha kimapenzi na Amber Lulu, kitendo ambacho kimemchukiza Prezzo.

“Prezzo kula bata mwanangu fanya mambo na Amber Lulu, Prezzo pole sana jiongeze mtu wangu, tumia mpira (condom) ya gharama zaidi ambayo hujawahi kutumia kabla, kwa sababu sehemu unayokwenda ni moto”, amesema TID.

Kauli hiyo ya TID imeonekana kumkera Prezzo na kusema kwamba hakukuwa na haja ya kuyapeleka kwenye TV.

“Namshangaa mshkaji wangu, kuna watu huwa wananiingia kwa kona mbaya, ukiingia kwa kona mbaya mimi ni msela nitakuzingua, kitu ambacho sijafurahia ni kwenda kutangaza kwenye TV,  yeye ni mshkaji wangu angenipigia simu akaniambia, na sio kuniharibia 'mood' yangu”, amesema Prezzo.

Prezzo amekuwa hapa nchini takriban wiki, na amekuwa akionekana na msani Amber Lulu akiwa naye kwenye chumba cha hoteli, kitendo ambacho kimeibua gumzo kwa mashabiki wengi.

Wema Sepetu Ajibu Tuhuma za Kurudiana na Diamond...Adai Hawezi Rudia Matapishi

$
0
0
MUIGIZAJI mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Sepetu ‘Keki ya Taifa’, amekanusha ishu ya inayovuma mitandaoni kuwa anatamani kurudiana na X-wake ambaye ni Mbongo Fleva, kwa kusema hawezi kamwe kurudiana naye kwani mpenzi wake wa sasa anampa furaha ya kutosha.

Wema alifikia hatua ya kuandika ujumbe wa kukanusha skendo hiyo, baada ya hivi karibuni kuenea kwa ubuyu kuwa yeye na Mbongo Fleva huyo wamerudiana tena, anadiriki hadi kwenda kwake kupika, jambo ambalo lilimchanganya na kuamua kulitolea ufafanuzi.

Wema na X-wake huyo, waliwahi kuwa ‘Couple’ ambayo ilitikisa jiji, baadaye wakamwagana na kisha X-wake huyo kujiingiza kwenye ulimwengu wa huba na mfanyabiashara maarufu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss lady’ ambapo amezaa naye watoto wawili, lakini pia ni baba wa mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobeto anayeitwa Prince Abdul.

Lawrence Masha Ampa Ushauri Rai Magufuli Sakata la Lissu

$
0
0
Masha amesema hayo akiwa kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na wanahabari, leo mchana na kusema kwamba  kwa sasa Watanzania wana hofu pamoja na hisia tofauti juu ya usalama wao hivyo ni vyema kukubali vyombo vya nje kufanya uchunguzi ili kupunguza hisia hizo.

"Kuomba msaada siyo fedheha. Msaada siyo jambo geni, kwa uzoefu wangu nilipokuwa Waziri  askari wengi walikuwa wanafanya 'training' nje naamini hata mpaka sasa. Tunapoomba msaada siyo kwamba haina uwezo bali inasaidia kuondoa hofu kwa wananchi. Ninachokuomba Rais waagize makamanda wako kuomba msaada ili Watanzania wasiishi kwa hofu" Masha.

Ameongeza kwa kusema kwamba "Tusikatae misaada, kwani hakuna aliyesema askari wa Watanzania siyo waadilifu japo wachache siyo. Siyo maisha yetu kukuta watu wamekufa ufukweni hofu kwa Watanzania hatujaizoea.

Pamoja na hayo Mh. Masha amekiri wazi kumshangaa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba pamoja na Inspekta Jenerali wa Tanzania Simon Sirro kwa kukataa msada wa kutoka nje wa kiuchunguzi ili kusaidia kupunguza hisia na hofu kwa Watanzania kwani ndiyo kazi ya jeshi la polisi.

Hata hivyo ameongeza na kutoa rai kwa serikali kwamba matukio hayo hayaathiri Watanzania tu kwani hata mataifa ya nje wanajiuliza kuhusu usalama wa Tanzania.

Familia ya Lissu: Hatutaki Suala Hili Kufanywa Kisiasa! Hatuoni Umakini Upelelezi wa Ndani, Twataka Wapelelezi Toka nje

$
0
0
Tunashukuru sisi kama wanafamila kwa kuitikia wito wetu

Alute Simon Mughwai, kaka wa Tundu Lissu ni wakili na ofisi yangu ipo Arusha.
Sababu za kuita hii press conferess ni kama zifuatazo;



  • Kuwashukuru ninyi wanahabari kwa namna ambavyo mmendelea kutuhabarisha na kutoa habari kwa wananchi kwa umma juu ya maendeleo ya matibabu ya Mhe. Tundu
  • Kwa niaba ya familia, naomba niweze kuwapa mrejesho juu ya hali ya Mhe. Tundu. Anaendelea vizuri ana imarika, amefanyiwa upasuaji mara kadhaa na sasa hivi yupo vizuri. Ameanza kula kwa njia ya kawaida na ameanza kuzungumza vizuri. Ndugu yetu ambaye ameenda kule mara ya mwisho juzi ameleta salamu kwamba yupo sawasawa na jana tumezungumza na mke wake
  • Nilivyokwenda Nairobi tarehe 9, tulifanya kikao sisi wanafamilia, uongozi wa Chadema pamoja na uongozi wa chama cha wanasheria Tanganyika kwamba atakayekuwa natoa taarifa juu ya matibabu ya Tundu ni Mhe. Mbowe pekee. Yeye ndio atatoa taaarifa rasmi na wali si mwingine yeyote


Kama ambavyo wengi wenu ambavyo mtakuwa mmepata habari, sisi familia tuliandika barua serikalini kuomba kwamba kwenye jambo la uchunguzi la huo uovu ulikwisha fanywa, lifanyiwe upelelezi wa kina, wa haraka na wa kitaalam ili hao waovu wakamatwe na wapelekwe kwenye mikono ya sheria.

Kwenye kuifuatilia barua hiyo, tumeonana na Waziri wa sheria na mambo ya katiba jana na leo mchana huu tumetoka kuonana na mwanasheria mkuu wa serikali kufuatilia habari ya hiyo barua. Wametupokea vizuri na wanaishughulikia

Katika kufutilia swala hili na kufanikiwa, Sisi kama familia tunadhani hatuwezi ku-ignore serikali lazima tuende nao mpaka hapo tutakapoona kwa mfano hiyo njia imefungwa. Sisi kama familia tunataka jambo hili liende kwa utaratibu wa kawaida sheria ifuatwe bila kuingiza siasa. Siasa kama itakuja ije wakati bwana Tundu yupo barabarani anatembea

Katika barua ile tulikuwa tumependekeza serikali kupitia jeshi la polisi waweze kushirikisha wataalamu wengine wa uchunguzi kutoka nje

Katika gazeti moja nilisoma wakimnukuu Waziri wa mambo ya ndani Mwiguli, sijui kama walimnukuu sawasawa ila kama walimnukuu sawa alisema "Tanzania ni nchi huru, inajitegemea, na ina vyombo vyote vya upelelezi na kadhalika ambavyo hinahitajika kufanya kazi na haitaji input ya vyombo kutoka nje"

Kwa mujibu wa sheria na sheria tuliyoitaja kwenye barua hiyo ni sheria ya ushirikiano katika mambo ya jinai. Sisi kweli ni huru, lakini sisi(Tanzania) ni sehemu ya jumuiya ya kimataifa. Hivyo tunashirikiana na nchi nyingine

Nimeona kwenye gazeti la leo likimnukuu IGP akizungumzia habari za yule dereva wa Mhe. Tundu aliopo Nairobi kwamba arudi nchini ili aje ahojiwe. Nadhani ameripiwa sawasa, sasa sisi ushauri wetu ni kwamba kwa nini Polisi wasimfuate kule Nairobi amekaa kwa takribani wiki tatu.

Aliyefanya uhalifu hajakamatwa maana yake maisha ya huyo dereva si yatakuwa yapo hatarini kuna utaratibu wowote wa kuhakikisha juu ya usalama wake. Isije ikawa anavuka Namanga kuja nchini anakatishwa pale njiani.

Hatupo tayari jambo hili likafanywa siasa, halafu na Tundu wanamfanya mpira wa kona, sisi tutakuwa wapi sasa tutakuwa washika vibendera au namna gani. ' we are not interested'

Vicent Mughwai (Mhadhiri wa Chuo Kikuu) anaongea na kusema;

Nakumbuka Lissu alifanya press conferenss tarehe 18/8 akasema kuwa kuna watu wanamfuatilia kila aendapo akataja hata aina ya gari na plate namba za hilo gari na nakumbuk anilona clip ya video akimtaka IGP na mkuu wa mashataka ili wawaambie wale vijana wafanye kazi nyingine na waache kumfuatilia. Na hawa ndio ilikuwa wa kuanza nao

Sasa tunavyoambia mpaka leo hakuna aliyeshikwa pamoja na kwamba gari lilijulikana na plate namba ilitajwa. Nasikia waziri alisema hilo gari lipo Arusha na halijawahi kufika Dar, mimi nilipata kigugumizi kidogo kwa sababu hivi unajuaje halijawahi kufika Dar au mmelishika Arusha kumbe linajulikana ni la nani!

Kusema unasubiri mtu moja (dereva wa Lissu) zoezi limesimama, labda zoezi linaendelea lakini sisi kama familia tunaona hakuna seriousness wakati mtu alikuwa auwewe. Mtu ambaye amekuwa ma mchango mkubwa kwenye hii nchi.

Kwa msisitizo tu sasa zoezi hili haliendi itakiwavyo, labda kuna haja ya kushikisha wapelelezi toka nje. Kwasababu nia ni njema ya kutaka kujua aliyefanya hili tukio

Cha mwisho nitoe shukurani wa watanzania wote ambao kwa njia moja ama nyingine walikuwa wakimuombea Tundu kwa sala na kutoa michango mbalimbali.

Kauli Zawaponza Mwigulu, IGP Sirro..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamoi ya October 7

$
0
0


Kauli Zawaponza Mwigulu, IGP Sirro..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamoi ya October 7

Nilimwomba Mke Wangu Anilishe Limbwata.......

$
0
0
Nimelazimika kuandika hili kutokana na hali ambayo wakati mwingine nakutana nayo kutoka kwa jamaa zangu. ni miaka kadhaa sasa toka nimeoa na nimekutana na changamoto kadhaa mpaka kufikia hatua ya kusema liwalo na liwe.

Nlikuwa na marafik kabla ya ndoa na baada ya ndoa. popote pale wanapokusanyika binadamu kunakuwa na changamoto zake. ukiwa ofisini ukawa unafanya kazi kwa bidii na unafuata sheria na taratibu zote kuna watu watakuchukia na kukuona unajipendekeza au una shida sana hivyo unaogopa kuvukuzwa kazi. hali kadhalika ......

Kwa sisi ambao tumeamua kuwapenda wake zetu wanasema tumerogezewa au tumerogwa. ugomvi wangu ni jamaa zangu ni kuwa pamoja na wao kuwa wameoa ila ikifika saa 3 usiku mi naaga kuwa lazima nirudi home.wakati wao ndo kwanza kumekucha na wanawapigia simu wengine walio majumbani waje kuanza/kumalizia weekend. wanashangaa wakinambia twende sehemu ghafla, nawaambia sijamwaga wife. wao wanaona huo ni ufala. au nikiwa nao sehemu wife akipiga simu kuulizia nikimweleza wao wanashangaa sana. jamaa wamefikia hatua wamenitenga na hawataki tukae pamoja. siwalaumu labda nawabore kwa kuwa wao huwa wakiwa maeneo hayo hawapigiwi simu na wake zao na ikitokea wamepigiwa wanaweza wasipokee au mtu akawa mkali sana akifoka.

Kiuhalisia mimi kama nimepewa limbwata basi la namna hii nimelipenda na nashauri hata wewe mwingine kama una family yako mwambie mkeo akuwekee limbwata. haiwezekani sisi wanaume tunaenda kunywa na kurudi home saa nane au kumi alfajiri kwa kuamini tu mwanamke hana haki ya kuuliza as long as anakula na anavaa.

Imani ya kuwa kuomba ruhusa kwa mkeo ni udhaifu au ni kuonesha umetekwa ni moja ya imani mbovu sana. ukishakuwa na ndoa wewe tena hujimiliki. mwili wako na maamuzi yako si ya peke yako. si ajabu akakwambia hataki kuona umevaa nguo flan na ukalazimika kuvua. haya mambo wanaume tusidhani uana ume ni kuwa mbabe kwa mkeo. hayo ni maisha ya kizamani sana. miaka hii hatutangazi ubabe kwa wake zetu. wake ni marafiki,wapenzi,ndugu n.k

Wacha mimi niendelee kula limbwata la mke wangu na as long as nlimwomba kabla sijamwoa kuwa niwekee limbwata ( figuratively ) sijuti kabisa. na ninyi ambao ni wanaume hasa endeleeni kuonesha uana ume wenu.

By Sodoku

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Kutana na The Great Maalim Hussein Aweze Kutatua Matatizo yako Kwa Tiba za Asili, Dua na Nyota..

$
0
0
THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)
MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)
Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.
Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.
ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..
Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..

Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images