Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live

Ali Kiba Akoshwa na 'Natamba' ya Aslay

$
0
0
Ali Kiba Akoshwa na 'Natamba' ya Aslay
Msanii Alikiba ambaye hivi sasa anaendelea kufanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' amefunguka ya moyoni na kumpa sifa msanii ambaye alikuwa anaunda kundi la Yamoto Band, Aslay na kusema kuwa anajua sana.

Alikiba amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram wakati na kusema mdanii huyo anaweza pale aliposikiliza kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Natamba' ambayo imetoka siku mbili zilizopita na kuendelea kufanya vyema na kupokea vizuri na mashabiki.
Ngoma hiyo ya Aslay 'Natamba' ni kati ya ngoma kumi na tisa ambazo ameachia nyota huyo toka ameanza kufanya kazi kama 'Solo Artist' nyimbo ambazo zimeweza kumpatia mashabiki wengi zaidi nchini na kufanya kazi zake kuendelea kupendwa zaidi kutokana na tungo zake.

Hakuna Malaya Hapa Duniani ni Unafiki tu Unatusumbuwa, Na Hakuna Demu wa Bure Duniani hili Lieleweke Vizuri

$
0
0
Habarini za jumamosi wapendwa wa jukwaa hili. Happy sabbatical.

Naenda direct kwenye point yangu nimekuwa nakerwa kwa muda mrefu kwa watu wasiowaelewa kuwasakama baadhi ya kina dada kuwaita malaya.

Leo mimi ndio Advocate wao ambaye nimejitolea bure kuwatetea na kuweka fact and evidence tubishane kwa hoja.

Mimi binafsi kwanza nina umri wa kuweza kugombea Urais ninajiamini nina exposure ya kutosha ndani ya nchi na nje.

Ni sisi wanaume 98% tukisafiri upenda kupata ukarimu wa ngono kwa wasichana wa eneo husika, na ukute unakaa siku mbili tu, ukikalimiwa imeshakuwa shida, malaya umesahau wewe mwenyewe malaya.

Ukimuuliza mtu ni mwanamke gani umewahi kutembea naye hujampa pesa huwezi kupata jibu ukweli ni kwamba wanawake wote wanapokea pesa after kumaliza kwa kisingizio cha nauli.

Lakini hapa wapo wadada ambao wao wameweka wazi ukitaka kuwamega mkatie pesa kiasi fulani basi mchezo umekwisha hawa ati wanaitwa wauza mbunye kosa lao liko wapi? Ni mwanamke gani anayetowa bure? Aje hapa hadharani akanushe hili.

Haya ngoja niwape mifano hai kuna dogo huyu Diamond eti naye kapachikwa jina la malaya!! Jamani tumuogope Mungu huyo Diamond ni maarufu tu hana umalaya wowote, wanawake wote aliodate nao wanahesabika wakati sisi tunaomnyooshe kidole binafsi kwangu hata ukiwajaza kwenye fuso halitoshi labda ulete treni ya Mwakyembe na ukinipa kitabu niwaandike siwezi kuwakumbuka ila huyu mtu maarufu wanawake aliotembea nao kwa 99% wanajurikana hii same applied kwa Wema Sepetu.

Issue iko hivi kuna wanawake hawatoi nyuchi zao kwa mfumo wa kupatana bei lakini wastani wake wa kuliwa na wanaume kwa mwezi anamzidi huyu tunayeamini na kumuita muuza mbunye hii siyo sawa hata kidogo.

Ninajuwa vyema wako wanawake wachache mno very independent lakini ukiwachunguza kwa undani walishaumizwa na wanaume ndio sababu kwakuwa wana cash mwanaume ukikaa na mwanamke kama huyo anakuonesha power of independence woman, anaclear bill na anaweza kukupa cash.

Mimi nawapa moyo sana madada wote wanaotowa ngono kwa mapatano ya cash kwanza siyo wanafki ni wawazi hawana usumbufu na 90% ni wadada ambao wapo kwenye viwango vya kuitwa warembo.

Nihitimishe tu hoja yangu kwa kumtaka mwanaume yeyote anayejiona yeye si malaya ajitokeze hapa na mwanamke yeyote anayesema yeye hauzi anatowa bure pia ajitokeze hapa.

Tanzania bila unafiki inawezekana.

By Mchambuzi Matola

Michepuko Kulitenganisha Kundi la Roma, Stamina

$
0
0
Michepuko Kulitenganisha Kundi la Roma na Stamina
WANAMUZIKI wanaounda kundi linalotikisa Bongo kwa sasa la Rostam, Roma Mkatoliki na Stamina, wamefunguka kuwa, endapo mmoja kati yao akibaini mwenzake amechepuka, basi ndiyo itakuwa mwisho wa uhai wa kundi hilo. Wawili hao kwa sasa wanatamba na wimbo wao wa Huku Ama Kule ambao unafanya vizuri kwenye vituo vya redio na runinga.

Roma amesema: “Yaani sisi kila mtu hapa alipo anamlinda mwenzake kuhakikisha hapigi, hachepuki licha ya kwamba kuna vishawishi vingi ambavyo tunakutana navyo wakati tukisaka ugali wetu wa kila siku.
“Kama ikitokea siku m i m i nimemfuma Stamina au yeye akanifumania nipo na mwanamke mwingine tofauti na mke wangu tukifanya mambo ya kimapenzi, basi hapo ndiyo utakuwa mwisho wa kundi hili.”

Akaunti ya You Tube ya Aslay Iliyohakiwa na Watu Wasiojulikana Imerudishwa

$
0
0
Akaunti ya You Tube ya Aslay Iliyohakiwa na Watu Wasiojulikana Imerudishwa
Account ya YouTube ya Aslay ambayo ilihakiwa na watu na kuiwekea vikwazo kwa watu wanaotaka kutazama kazi zake, imerudishwa baada ya kuhangaika nayo kwa muda mrefu.

Taarifa ya kurudishwa kwa account hiyo imetolewa na mmoja wa mameneja wake Mx Carter ambaye ni mtaalamu wa masuala ya mitandao na mpiga picha maarufu hapa bongo, kupitia ukurasa wake wa twitter.
Kwenye taarifa hiyo Mx Carter ameandika  'Usiyempenda karudi", na kuweka picha ya Aslay.
Leo asubuhi Mx Carter alitoa taarifa kuwa account hiyo imehakiwa, na kuwataka watu kuwa wapole wakati wanahangaikia kuirudisha.
Hivi karibuni Aslay amekuwa msanii ambaye anafanya vizuri zaidi mtaani kwa kutoa kazi kali mara kwa mara, na hivi juzi kaachia video yake mpya ya 'Natamba'.

Kamati ya Zabuni ya Simba Kumtangaza Mwekezaji Mpya Leo?

$
0
0
Kamati ya Zabuni ya Simba Kumtangaza Mwekezaji Mpya Leo?
Klabu ya Simba huenda leo ikaingia kwenye ukurasa mpya wa uendeshaji wa timu ambapo kamati maalum ya kusimamia mchakato wa zabuni ya kumpata mwekezaji kwenye muundo mpya wa klabu ya hiyo leo Saa 5:00 asubuhi inatarajiwa kukutana na Waandishi.

Taarifa ya Simba SC kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu, Hajji Sunday Manara imesema kwamba mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Kivukoni 3 uliopo ndani ya hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam.
Kamati hiyo iliyoundwa mapema mwezi uliopita, ipo chini ya Mwenyekitil, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo na Wajumbe wengine wanne, ambao ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu’, Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Abdul-Razaq Badru, Wakili Dk. Damas Ndumbaro na Yusuph Maggid Nassor.
Agosti 20, mwaka huu wanachama 1,216 wa klabu ya Simba waliridhia mfumo wa klabu yao kuuza Hisa baada ya Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (MNICC), Dar es Salaam.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri wa Afya Jinsia na Watoto, Dk Hamisi Kigwangala, Kaimu Mwenyekiti wa klabu, Salim Abdallah 'Try Again' alisema kwamba asilimia 50 ya hisa zitauzwa kwa mwekezaji au wawekezaji watakaoungana wasiozidi watatu, kwa sharti moja tu la kuwa wanachama wa klabu hiyo.  Mwekezaji anatakiwa kuweka dau lisilopungua Sh. Bilioni 20 ili kupatiwa asilimia 50 ya hisa za klabu, wakati kwa kuanzia wanachama wote wa Simba wamepewa asilimia 10 ya hisa.

Vyama vya Siasa Kuchuana Katika Uchaguzi wa Udiwani kwa Kata 43

$
0
0
Vyama vya Siasa Kuchuana Katika Uchaguzi wa Udiwani kwa Kata 43
Katika soka huwa kuna dirisha dogo la usajili ambalo linapofunguliwa, timu huchuana kusaka wachezaji.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa vyama vya siasa ambavyo vinajiweka sawa kuchuana kuwania kata 43 zilizotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa utafanyika Novemba 26.

Uchaguzi huo unafanyika kutokana na nafasi hizo kuwa wazi baada ya madiwani waliokuwapo kufariki dunia, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa mahakamani.

Katika maandalizi hayo, naibu katibu mkuu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya alisema chama hicho kiliamua kujifungia kwa siku mbili mfululizo kujadili namna kitakavyoshiriki uchaguzi huo na kuibuka kidedea.

“Jana (juzi) baada ya NEC kutangaza uchaguzi viongozi tulikutana na kufanya kikao hadi saa sita usiku. Miongoni mwa mambo tuliyoyajadili ni pamoja na kupitia kata moja baada ya nyingine ili kujua nguvu ipo wapi ili tuweze kushiriki kwa asilimia 100.

“Tuliwasiliana pia na viongozi wa wilaya ili kujua uhai wa chama wakati wa kuelekea katika uchaguzi huu wa marudio,” alisema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua, Tabora.

Sakaya ambaye yupo katika kundi la uongozi wa chama hicho linalomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, alisema kuna baadhi ya maeneo ambayo CUF itashiriki kwa asilimia 100 na mengine asilimia 50 kulingana na nguvu na kukubalika kwake.

Lakini Sakaya akisema hakutakuwa na ushirikiano miongoni mwa vyama vinavyounda Ukawa na kwamba kila chama kitasimama kivyake.

Kwa upande mwingine, Salim Bimani, mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano kwa umma wa CUF unaompinga Profesa Lipumba, alikuwa na mtazamo tofauti akisema ushirikiano huo wa vyama vinne uliopewa jina la umoja wa katiba ya wananchi ndiyo utakaosaidia kuiangusha CCM.

“Kesho tutatoa taarifa rasmi kuhusu uchaguzi huu. Hata hivyo, nimesikia upande wa Profesa Ibrahim Lipumba hautaki ushirikiano, nawaambia hivi hawawezi kushinda hata kata moja endapo watasimama peke yao,” alisema Bimani.

Kuunga mkono hilo, naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema chama hicho kinatarajia kukutana wiki ijayo kupanga namna ya kushiriki uchaguzi huo kwa kushirikiana na wana Ukawa ambao ni CUF, NCCR-Mageuzi, NLD. “Huu uchaguzi siyo wa kawaida kutokana na hali halisi ilivyo... Nitawashangaa sana wale watakaotoka nyumbani kwao na kwenda kupigia kura CCM,” alisema Mwalimu.

Pia, katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Juju Danda alisema maandalizi yalishaanza na yanaendelea kufanyika kwa kushirikiana na Ukawa ili kujua namna watakavyoweza kuachiana kata katika uchaguzi huo.

Wakati Sakaya na Ukawa wakisema hayo, katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema chama hicho, kimeshajipanga na hakina maneno yoyote ya kuzungumza.

“CCM imefanya kazi kubwa na ukweli unaonekana kupitia Serikali ya Awamu Tano na ukweli utadhihirika baada ya matokeo,” alisema Polepole.

Alisema wagombea wote watakaopitishwa ni wale wanaokubalika ndani ya CCM hadi kwa wananchi na wakishinda watakuwa viongozi na watumishi kwa watakaowaongoza.

Bi Mugabe Aonya Kufanyika kwa Mapinduzi Zimbabwe

$
0
0
Bi Mugabe Aonya Kufanyika kwa Mapinduzi Zimbabwe
Mke wa rais Robert Mugabe , Grace Mugabe ameonya kwamba kuna uwezekano wa kufanyika kwa mapinduzi huku kukiwa kuna wasiwasi mkubwa nchini humo kuhusu harakati za kumrithi rais Mugabe.

Anasema kuwa washirika wa makamu wa rais Emmerson Mnangangwa wanatishia maisha ya wale ambao hawamuungi mkono kumrithi rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93.
Bi Mugabe yeye binafsi na bwana Mnangagwa wako kifua mbele na uadui wao umekigawanya chama tawala cha Zanu PF .

Mgogoro huo unajiri baada ya bwana Mgangagwa kudai kwamba aliwekewa sumu katika chakula chake mwezi Agosti.
Wafuasi wake wamesema kuwa wapinzani wake ndani ya Zanu PF ndio wa kulaumiwa, ijapokuwa bwana Mnangagwa amejitenga na madai kama hayo.

Alikiambia chombo cha habari cha taifa hilo anasalia kuwa mtiifu kwa rais Mugabe.
Bi Grace Mugabe aliyekasirika alimshutumu bwana Mnangagwa katika hafla moja mjini harare .
''Tunatishiwa usiku na mchana kwamba iwapo mtu fulani hatokuwa rais , tutauawa'', alisema.

Mwanamitindo Atoboa Siri Asema Kuoga Mara Moja kwa Wiki Kunasaidia Kutozeeka Mapema

$
0
0
Mwanamitindo Atoboa Siri Asema  Kuoga Mara Moja kwa Wiki Kunasaidia Kutozeeka Mapema
Mwanamitindo Vivienne Westwood mwenye umri wa miaka 76 kutokea  nchini Marekani, amesema kuwa kuoga mara moja kwa wiki ni siri kubwa ya kumfanya mtu asizeeke na daima kuonekana kijana.

Mume wake mwanamitindo huyo ambae ni Andreas Kronthaler alifanya mahojiano na Paris Fashion week baada ya kuulizwa kuhusu siri kubwa ya wao kuonekana vijana na kafunguka kuhusu siri hiyo.

Andreas Kronthaler ambaye ni mume wa Vivienne Westwood ameweka wazi kuwa yeye huoga mara moja kwa mwezi wakati mke wake Vivienne Westwood huwa anaoga mara moja kwa wik

Breaking Newz: Rais Magufuli Afanya Mabadiriko Katika Baraza la Mawaziri

$
0
0
Breaking Newz: Rais Magufuli Afanya Mabadiriko Katika  Baraza la Mawaziri
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya mabadiriko katika baraza lake l mawaziri ambapo baadhi ya mawaziri wamepoteza nafasizao huku baadhi ya wengine wakipanda  huku wengine wapya wakiteuliwa miongoni mwao naibu wa nishaati amepanda cheo na kuwa waziri

Mabadiliko ya hayo yaliyofanyika yamefanya kuongezwa kwa wizara mbili, hivyo kufikia wizara 21 kutoka 19 ambazo zilikuwepo.

Tukio hilo limetokea leo ambapo Rais Magufuli pia amezigawa Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na kuwa wizara ya Kilimo pekee na Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake, pamoja na Wizara ya Nishati na Madini kuwa wizara mbili tofauti.

Sambaba na hilo pia Rais Magufuli amemteua Mh. George Haruna Mkuchika kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora, ambaye kabla alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mawaziri hao wanatarajiwa kuapishwa siku ya jumatatu Oktoba 9, 2017, Ikulu jijini Dar es salaam.

CUF wanaomuunga Mkono Maalim Seif Waionya CCM

$
0
0
CUF wanaomuunga Mkono Maalim Seif Waionya CCM
Chama cha wananchi CUF, kimetoa msimamo wake kuhusu uchaguzi mdogo wa madiwani kwamba hakitakurupuka kutoa wagombea bali watashirikina vema na UKAWA ili kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa kwenye vyama vya upinzani na siyo kuipa ushindi CCM.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa upande wa Maalim Seif, Naibu Mkurugenzi Maharagande Mbarala inasema kwamba anawataka viongozi na wanachama wote makini walipuuze genge la Lipumba na kwamba CUF haitasita kuongeza nguvu zake kwa kushirikiana na upinzani wengine katika kata watakazo zimamisha wagombea wao ili kufanikisha ushindi kwa vyama vya upinzani katika maeneo yatakayoainishwa.

Taarifa inasema kwamba CUF haitafanya maamuzi ya kukurupuka, itazingatia vigezo vya matokeo ya Chaguzi zilizopita 2015/2017,  kwamba Kata ilikuwa inaongozwa na Chama gani kabla ya uchaguzi kama Kata ilikuwa inaongozwa na NCCR au CHADEMA hakuna sababu ya CUF kusimamisha Mgombea eneo hilo na kinyume chake kwenye ngome za CUF hakuna sababu vyama vingine kusimamisha wagombea wao.

Ameongeza kwamba Kurugenzi ya Mipango na Uchaguzi CUF Taifa inaendelea kufanya mawasiliano na viongozi wa chama wa maeneo husika na kupitia ‘Database’ yake kwa kufanya uchambuzi yakinifu ili itoe taarifa sahihi kwa maslahi mapana ya CUF, upinzani na watanzania Wwapenda mabadiliko kwa ujumla.
Mbali na hayo Mbarala ameonya na kusema kwamba taarifa zilizotolewa na vibaraka wa CCM kwamba CUF itawasimamisha wagombea katika kata zote 43 zinazorudia uchaguzi ni za uongo na kupuuzwa kwani CUF haikuundwa kuwa Chama cha kuisadia CCM iendelee kutawala Tanzania.

Kigwangala Asema Serikali Haiko Tayari Kuwavumilia Watendaji Wazembe

$
0
0
Kigwangala Asema Serikali Haiko Tayari Kuwavumilia Watendaji Wazembe
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala, amesema serikali haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe kwa kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Waziri Kigwangala ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa instagrama, ambapo ameeleza kwamba watendaji hao wanachelewesha maendeleo ya nchi, hivyo watafikisha taarifa kwa mwenye mamlaka zaidi ili wachukuliwe hatua.
“Halmashauri chache zenye viongozi na watendaji wazembe zitabaki nyuma. zitatuangusha. Hatuko tayari kuvumilia, tutapendekeza kwa mwenye mamlaka hatua kali zichukuliwe”, ameandika Dkt. Kigwangala.
Dkt. Kigwangala ameendelea kwa kuandika kwamba kutokana na watu hao wanaingiwa na mashaka kuwaacha wasimamie miradi mikubwa ambayo inapaswa kutekelezwa, ikiwemo uboreshaji wa vituo vya afya, kitendo ambacho kinawatesa wananchi.
“Wizara ya Afya tumepata wafadhili ambao watatuwezesha kuboresha vituo vya Afya150 kwa kupeleka milioni za kitanzania 500 kwenye kila Kituo. Pesa hizi bado hazijaenda kwenye halmashauri mpaka sasa. Nachelea kusema tukiwapelekea viongozi na watendaji wa namna hii wanaweza kushindwa kuzisimamia ipasavyo, kuacha kupeleka ni kuwaadhibu wananchi wasio na hatia”, ameandika Dkt. Hamisi Kigwangala.
Hivi karibuni waziri Kigwangala amekuwa akifanya ziara kwenye vito vya afya mbali mbali nchini, kutathmini changamoto ambazo zinavikabili na kuvitafutia njia za ufumbuzi.

Niyonzima Ajitoa Kiaina Simba

$
0
0
Niyonzima Ajitoa Kiaina Simba
HARUNA Niyonzima amejitoa kiaina Simba huku akiweka masharti ya kupewa wiki mbili ili aweze kujiweka fiti zaidi kwa kuboresha kiwango chake ili kuzima kelele za mashabiki wanaomlaumu kucheza chini ya kiwango.

Uamuzi huo wa Niyonzima raia wa Rwanda umekuja baada ya kuwepo kwa minong’ono mingi juu ya kiwango chake kushuka, na sasa amepania kukirejesha katika hali yake ya siku zote.

Niyonzima ametoa msimamo huo akiwa tayari ameichezea Simba michezo minne ya Ligi Kuu Bara huku akikosa mchezo mmoja pekee dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kutokana na kuugua Malaria.
Kiungo huyo ndiyo ameanza kuutumikia mkataba wake wa miaka miwili Simba aliyojiunga nayo msimu huu baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyonzima alisema amezisikia lawama nyingi na za wazi kutoka kwa viongozi na mashabiki wa Simba wakimtuhumu kuwa kiwango chake kimeshuka kitu ambacho si sahihi.

Akisisitiza, Niyonzima alisema; “Ukweli ni kwamba, nilikosa maandalizi mazuri ya ‘Pre Season’ pamoja na wenzangu kutokana na kubanwa na baadhi ya majukumu nikiwa nyumbani Rwanda huku wao wakiwa kambini Afrika Kusini.
“Kiwango changu hakijashuka kama inavyoelezwa, ila tatizo lipo kwenye fitinesi ambayo nilichelewa kuitengeneza kwenye pre season na wenzangu.

“Leo (jana) nitakutana na kocha ili nimweleze hali halisi na nitamwomba aniandalie au nipewe programu maalumu ya mazoezi ya kuniongeza fitinesi ili niwe vizuri zaidi.
“Nataka iwe asubuhi nafanya kwenye gym na jioni kwenda kukimbia ufukweni, naamini nikiifanya vizuri programu hii, nitazima minong’ono yote ya mashabiki na viongozi wanaonituhumu.

“Baadhi ya viongozi wa Simba wamekuwa wakisema kuhusiana na mimi kiwango changu kimeshuka, kiukweli maneno hayo yananiumiza na kunikosesha amani, sasa nataka kuwaziba midomo,” alisema Niyonzima.
“Unajua sikwenda kambini Afrika Kusini, halafu nikarejea nchini siku moja kabla ya mechi na Rayon (SC ya Rwanda) kwenye sherehe ya Simba, hivyo nilicheza nikiwa sijafanya mazoezi.

“Niwaombe radhi mashabiki wa Simba, ninajua wanataka kuniona Niyonzima yule aliyekuwa anaichezea Yanga, ninaomba muda wa kujiweka sawa, ninawahakikishia watafurahi tu,” alimalizia Niyonzima.

Mtukufu Aga Khan Kuwasili Nchini Octoba 11 kwa Mwaliko wa Rais Magufuli

$
0
0
Mtukufu Aga Khan Kuwasili Nchini Octoba 11 kwa Mwaliko wa Rais Magufuli
Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani, Mtukufu Aga Khan anatarajia kutembelea Tanzania Oktoba 11 na 12 kwa mwaliko wa Rais John Magufuli.

Mtukufu Aga Khan atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa nne asubuhi akitokea Uganda atakakokwenda kuhudhuria sherehe za uhuru wa nchi hiyo kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni.

Akizungumzia ziara hiyo leo Ijumaa, Ofisa Mawasiliano wa Baraza la Aga Khan, Shelmina Shivji amesema ziara hiyo itafungua fursa katika sekta mbalimbali na kukuza uchumi wa Taifa.

Amesema mwaliko huo wa Rais Magufuli unaonyesha uhusiano mzuri kati ya Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) na Serikali ya Tanzania.

"Mtukufu Aga Khan amekubali mwaliko wa Rais Magufuli na katika ziara yake ya siku mbili nchini atakuwa na mazungumzo na Rais na kukutana na watendaji wa AKDN," amesema.

Shivji amesema Mtukufu Aga Khan ni mwekezaji mkubwa nchini katika sekta za afya, elimu, kilimo na maendeleo ya jamii.

Mratibu wa mawasiliano ya jamii ya Ismailia, Khan Ramji amesema maandalizi ya mapokezi ya kiongozi huyo yanaendelea vizuri kwa upande wa Serikali na Jumuiya ya Ismailia.

"Wananchi wajitokeze kwa wingi uwanja wa ndege wa JNIA kumpokea Mtukufu Aga Khan ambaye anatarajiwa kufika saa nne  asubuhi," amesema Ramji.

Julai 11, Jumuiya ya Waismailia nchini iliungana na wenzao duniani kuadhimisha miaka 60 ya uongozi wa Aga Khan ambaye ni Imamu wa 49 wa jumuiya hiyo.

Hizi hapa Sababu Chaz Baba Kupotea Katika Steji ya Mashujaa Bendi

$
0
0
Hizi hapa Sababu  Chaz Baba Kupotea Katika Game ya Muziki
BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu na kutoonekana katika steji ya Bendi ya Mashujaa aliyokuwa akiifanyia kazi, mwanamuziki Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ ameeleza sababu za kupotea kwake.
Chaz Baba alisema alikaa kimya kwenye steji kwa kuwa alikuwa bize kufanya nyimbo zake binafsi na anatarajia kurejea kwa kishindo hivyo mashabiki wakae mkao wa kula.
“Nimekaa kimya kwenye steji kwa muda mrefu lakini hivi karibuni nitaachia wimbo wangu mpya unaitwa Nuru na nina nyimbo nyingine mpya 13 ambazo nitazitoa kwa utaratibu moja baada ya nyingine mpaka ziishe,”

Serikali Yapiga Marufuku Madalali wa Bima

$
0
0
Serikali Yapiga Marufuku Madalali wa Bima
SERIKALI imepiga marufuku madalali kupokea fedha za wateja wa mashirika ya bima mbalimbali nchini, ili kuepusha malalamiko ya kutapeliwa.

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Stella Lutaguza, alisema hayo wakati wa mkutano wa kujadili mikakati ya kukabiliana na uhamiaji wa makao makuu mkoani.

Amepiga marufuku kwa wakala wa bima kutumia madalali kumletea wateja, badala yake wafuate sheria.
Alifafanua kuwa TIRA haipendi malalamiko ya wananchi kutapeliwa na madalali wa bima.

“Naomba watu wa bima wafuate sheria hiyo ya kutotumia madalali bila ya kufanya hivyo faini nyingi zitawahusu,” alisema Stella.

Alisema wanatarajia kuanza kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo mbalimbali kuhusu umuhimu wa bima, ili watu waweze kukata bima zao za magari, afya na nyingine ambazo zinaweza kuwasaidia kipindi wanapata majanga.

Alisema pamoja na changamoto wanazopata, lakini wanatakiwa kutoka kwenda vijijini kutoa huduma hiyo kwa jamii.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Yasinta Mboneno, akifungua mkutano huo alisema mawakala wa bima wanatakiwa kwenda na kasi ya awamu ya tano ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Aliwataka kuwa mstari wa mbele kuboresha huduma zao na kuacha tabia ya kuwazungusha wananchi haki zao.

Mhasibu wa TIRA Kanda ya Kati, Rogers Msagati, aliwataka mawakala kufanya kazi kwa weledi ili kuepuka usumbufu unaojitokeza kwa wateja.

Tanroan Yatangaza Neema Yaahidi Kupunguza Foleni ya Dar

$
0
0
Tanroan Yatangaza Neema Yaahidi Kupunguza Foleni ya Dar
IJI la Dar es Salaam ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi barani Afrika na ukuaji wake kuathiri sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi hasa usafiri na usafirishaji.

Tangu miaka ya 1990 kumekuwa na mipango mbalimbali ya kuboresha usafiri Dar es Salaam ikiwamo kuanzisha barabara za aina mbalimbali, kama za mabasi yaendayo kasi, maegesho ya magari ya kulipia na kuhamasisha kujengwa kwa majengo yenye maegesho ya magari.

Pamoja na jitihada za serikali ya jiji na serikali kuu kuboresha usafiri bado kuna kero kubwa ya usafiri wa abiria, hasa wakati asubuhi na jioni hali inayowalazimu wananchi  kuchukua takribani saa tatu barabarani badala ya dakika 15 hadi 30 , kwa mfano, kutoka Mbezi ya Barabara Morogoro hadi katikati ya jiji na Kariakoo.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, tangu mwaka 2008 Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam imetekeleza miradi maalum ya ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano katika barabara kuu za jiji.

Mhindisi Miradi wa Ofisi ya Tanroads Mkoa wa Dar Es Salaam, Julius Ngusa, anasema mradi wa ujenzi wa barabara za pembezoni wa awamu ya tatu ni moja ya mikakati ya serikali ya kushughulikia tatizo sugu la msongamano wa magari ambapo utekelezaji wake ulianza tangu 2008/2009.

Anasema kupitia mradi huo, serikali ilichagua barabara tisa kwa ajili ya kujengwa katika viwango vya lami nazo ni barabara ya Ubungo (bus terminal)-Kigogo-Kawawa yenye kilometa 6.4, barabara ya Jet Corner-Vituka-Davis Corner urefu wa kilometa 12, nyingine ni Kinyerezi-Kifuru-Msigani-Mbezi Mwisho yenye kilometa 10.

Barabara ya Mbezi- Goba- Tangibovu yenye kilometa tisa, kadhalika ya Kimara Baruti-Msewe-Changanyikeni yenye urefu wa kilometa 2.6.

Ngusa, anazitaja barabara nyingine kuwa ni pamoja na Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba-Mbezi ndani ya Morogoro yenye kilometa 20, Kigogo Roundabout-Jangwani-Twiga katika bonde la Msimbazi ikiwa na kilometa 2.72.

Anazungumzia pia Tabata Dampo-Kigogo na Ubungo Maziwa- Mabibo External inayoingia Mandela inayojengwa kilometa 2.25 za lami.

“Miradi hiyo inajengwa katika awamu tatu za utekelezaji, ambapo hadi sasa awamu ya kwanza ya miradi hiyo iliyohusisha ujenzi wa barabara zenye jumla ya kilometa 19.42 tayari imekwishatekelezwa na kukamilika tangu 2008.”

Anaitaja miradi iliyokamilika kuwa ni pamoja na barabara ya Ubungo-Kigogo-Kawawa iliyokamilika mwaka 2010 kwa gharama ya Sh bilioni 11.44, Kigogo-Msimbazi-Jangwani iligharimu bilioni 7.64 ambayo ilikamilika mwaka 2017 pamoja na barabara ya Jet Corner-Vituka-Devis Corner iliyomalizika mwaka 2011.

“Kuhusu awamu  ya pili yenye urefu wa kilometa 27.5 na ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40, kazi ilianza mwaka 2014 ambako hadi sasa zilizojengwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara ya Tangi Bovu (Samaki)-Goba iliyomalizika mwaka jana na kugharimu bilioni 8.6 ” anasema Ngusa.

Katika awamu hiyo mwaka 2016 serikali pia ilikamilisha ujenzi wa Barabara ya Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba-Mbezi Mwisho yenye kilometa 20, kwa gharama ya Sh bilioni 6.7.

Akifafanua zaidi Ngusa anasema miradi mingine iliyokamilika ni pamoja na Barabara ya Kilungule (Maji Chumvi)- External/Mandela yenye kilometa 3.3, ambapo mradi huo ulikamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Sh. bilioni 4.4.

Aidha mradi wa barabara ya Kimara Baruti-Msewe wenye kilometa 2.6 uliopaswa kukamilika mwaka jana umeshindishwa kuisha kwa wakati kutokana na kutokuwepo kwa nafasi ya kujenga barabara, ambapo hata hivyo hadi kufikia 30 Septemba, 2017 mradi huo ulijengwa kwa asilimia 80.

Mhandisi Ngusa anasema awamu ya tatu ya utekelezaji wa miradi hiyo ulioanza mwaka 2016 na 2017 unahusika ujenzi wa barabara za Kifuru-Msigani, Goba-Makongo na Goba-Madale zenye urefu wa kilometa 14.1 na unatarajia kukamilika mwanzoni na nyingine mwishoni mwa mwaka 2018.

“Miradi ya barabara ya Goba-Madale na Goba-Makongo hadi kufikia Septemba 30, mwaka huu imekamilika kwa asilimia 52 wakati ule wa Kifuru-Msigani umefikia asilimia 87, malengo ni kuhakikisha kuwa miradi hii inamalizika kwa wakati kwa kuzingatia ubora na viwango tulivyojiwekea” anasema Ngusa.

Baadhi ya changamoto inayokabili miradi hiyo ni pamoja na wamiliki wa nyumba nyingi kuhitaji fidia, ambapo Tanroads kwa kushikiana na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) zimeanza uthamini na malipo yatalipwa na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Anasema serikali pia inaendelea na ujenzi wa barabara za Msongola-Mbande zenye kilometa moja nyingine ni Ununio-Mbweni urefu wa kilometa moja pia , Kitunde-Kivule yenye urefu wa kilometa 3.2, pia kilometa nyingine moja zinajengwa za barabara ya Dege-Gomvu.

Kukamilika kwa miradi hii kutaongeza tija na ufanisi katika kuchochea kasi ya maendeleo ya Dar es Salaam na taifa .

Haya HapaMajina ya Mawazili Wanne Waliotemwa Uwazili

$
0
0
Haya HapaMajina ya  Mawazili Wanne Waliotemwa Uwazili
Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri kwa kuwatema mawaziri wanne waliokuwepo kwenye baraza la awali.

Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi,  Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.

Panga hilo limempitia pia aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri tangu aingie madarakani.

Jerry Muno Aliamsha Dude Awaponda Viongozi wa Chadema Amtaka Lema Kuacha Kujitekenya na Kucheka Mwenyewe

$
0
0
Jerry Muno Aliamsha Dude Awaponda Viongozi wa Chadema Amtaka Lema Kuacha Kujitekenya na Kucheka Mwenyewe
KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia aliwahi kuwa Msemaji wa klabu ya yanga, Jerry Muro ameibuka na kuwaponda viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku akiwataka waache porojo na badala yake wajikite katika kuwaletea maendeleo wananchi wao.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Muro amewataka viongozi wa Chadema wanaodai kuwa wanafuatiliwe na watu ili wauawe, waseme wanafuatiliwa na akina nani?
“Nimemsikia baadhi ya wabunge wa Chadema wakisema kuna watu wanawafuatilia, dada yangu kule Bunda (Ester Bulaya) akisema anafuatiliwa na watu waliovaa kininja, nani awafuatilie nyie? Kwani mmeiba makinikia?

“Lema naye anasema wamefungua nati za gari lake, pia anadai akiwa kwenye mwendokasi aliona watu wanamfuatilia akaruka kwenye gari akamwachia usukani mkewe, hivi kweli gari lipo kwenye mwendokasi unarukaje kichakani? Acheni maigizo jamani…” Nani akutafute wewe Lema? Mbona husemi wakati ukiwa na nywele za rasta ulikuwa unafanya nini kabla ya kuwa mbunge? alihoji Muro.
Ajibu kuhusu suala la madiwani wa Chadema Arusha waliohamia CCM, Muro amewataka Lema na Joshua Nassari waache kutembea na flshi (walizowasilisha TAKUKURU  kwa ajili ya uchunguzi) akidai kuwa hizo ni propaganda.

“Wakati Lema anazungumza na flashi Dar Es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo anahangaikia miradi ya maji na barabara kwa wananchi wake. Mimi namjua Lema tangu zamani, nimetoka naye Machame, aache kupambana na mimi Muro badala yake afanye maendeleo kwa wananchi wake.” alisema Muro.

Hawa Hapa Waliotangazwa Katika Baraza Jipya la Mawazili Lililotangazwa Leo

$
0
0
Hawa Hapa Waliotangazwa Katika  Baraza Jipya la Mawazili Lililotangazwa Leo
Rais John Magufuli ametangaza baraza jipya la mawaziri lililoongezeka kutoka wizara 19 hadi 21.

Wizara hizo zimeongezeka kutokana na wizara mbili kugawanywa huku nafasi za manaibu wapya zikiwa tano.

 Akitangaza leo Jumamosi baraza hili jipya, Rais Magufuli amesema Wizara ya Nishati na Madini imegawanywa mara mbili, sasa kutakuwa na Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.

 Amesema hatua hiyo inatokana na umuhimu wa rasilimali hiyo kwa taifa na kwamba wizara hizo zote kila moja itakuwa na waziri na naibu wake.

 Rais Magufuli ametaja mabadiliko mengine katika Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo kwa sasa kutakuwa na Wizara ya Kilimo inayojitegemea na nyingine itakuwa ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Amesema sababu za kufanya mabadiliko hayo ni kutokana na umuhimu wa sekta hiyo inayoajiri asilimia 75 ya Watanzania nchini hivyo ni vyema ijitegemee. Kila wizara itakuwa na waziri na naibu wake.

Mabadiliko mengine ni katika wizara ya Tamisemi baada ya kuweka nafasi mbili za manaibu waziri kwa sababu ni wizara inayogusa sehemu kubwa ya wananchi.

 Pia yamefanyika katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Baraza la Mawaziri

Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika

 Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi

Mawaziri - Suleiman Jafo, manaibu waziri - Josephat Kandege na Joseph George Kakunda.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Waziri - January Makamba, Naibu Waziri, Kangi Lugola.

 Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu Waziri - Jenista Mhagama, manaibu Stella Ikupa na Anthony Mavunde.

Wizara ya Kilimo ni Dk Charles Tzeba na naibu wake Dk Mary Mwanjelwa.

Wizara wa Mifugo na Uvuvi ni Luhaga Mpina na naibu wake ni Abdallah Ulega

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na manaibu wake Atashasta Nditiye na Elias Kwandikwa.

 Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na naibu waziri ni Ashantu Kijaji.

 Wizara ya Nishati ni Dk Medard Kalemani na naibu wake ni Subira Mgalu.

 Wizara wa Madini ni Angellah Kairuki na naibu wake Haruni Nyongo.

 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi

Wizara wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustino Mahiga na naibu Dk Susan Kolimba.

 Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi

 Wizara ya Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na naibu wake Hamad Masauni.

 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na naibu ni Angelina Mabula.

 Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala na naibu wake ni Ngailonga Hasonga.

 Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na naibu wake ni Stella Manyanya.

 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na naibu wake ni  Wiliam Ole Nasha.

 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu na  naibu wake ni Dk Faustine Ndugulile.

 Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na naibu wake ni Juliana Shonza.

 Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwele na naibu wake ni Juma Aweso.



Jukwaa la Katiba Kufanya Maandamano Nchi Nzima Octoba 30

$
0
0
Jukwaa la Katiba Yamuomba Magufuli Kupokea Maandamano ya Kufufua Mchakato wa Katiba
Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) limetangaza kufanya maandamano ya amani nchi nzima October 30, 2017 ili kurudisha hamasa kwa wananchi kushiriki kwenye michakato ya Demokrasia nchini.

Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda amesema kazi ya Jukwaa hilo ni kukuza hamasa ya wananchi kuweza kushiriki kwenye mchakato wa kuandika Katiba mpya.

Mwakagenda amesema kuwa kutokana na mkutano Mkuu wa dharula wa Jukata uliofanyika September 26, 2017 mjini Dodoma wameazimia kufanya maandamano nchi nzima.

”Maandamano yatafanyika October 30, 2017 ambapo kitaifa yatakuwa Dar es Salaam yakianzia Ofisi ya Jukata saa 4 asubuhi na yatahitimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.”

Aidha, amesema kuwa tayari wameshapeleka barua kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa ajilii ya kusudio la kufanya maandamano akiongeza pia kuwa wamemuandikia barua Rais Magufuli kumuomba apokee maandamano hayo ya amani.

Mwakagenda amesema, lengo la kumuandikia barua Rais ni kwa sababu Jukata inatambua jitihada zake katika kusimamia mambo yenye manufaa kwa Watanzania na vizazi vijavyo.

”Sababu nyingine ni kufikisha ujumbe wa haja ya kurejewa kwa mchakato wa Katiba mpya ya Tanzania ili tuukamilishe na kupata katiba mpya ya wananchi.”
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live




Latest Images