Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Mkuu wa Shule ya Sekondari Migukulama, wilayani Sengerema AJINYONGA

$
0
0
Mkuu wa Shule ya Sekondari Migukulama iliyopo Halmasahauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Benerdicto Lweikiza (45) amejinyonga hadi kufa akiwa chumbani kwake.


Taarifa za kujinyonga kwa mwalimu huyo zilianza kusambaa wilayani Sengerema na kuthibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Halmashauri ya Buchosa, Crispin Luanda.

“Ni kweli mwalimu huyo amejinyonga alikuwa mkuu wa Shule ya Sekondari Migukulama na amefikia uamuzi huo majira ya saa tisa mchana wa leo (jana) nyumbani kwake Mtaa wa Kilabela mjini Sengerema,” alisema Luanda.

Mmoja wa wanafamilia wa mwalimu huyo, Martin Kalemera alisema kuwa wao kama familia wanashangazwa na suala hilo na hawaamini kilichotokea ikiwa ni miaka mitano imepita tangu mke wake afariki dunia.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alithibitisha kupata taarifa ya kifo cha mwalimu huyo na kusema kuwa hajafahamu chanzo cha kufikia hatua ya kujinyonga na kamba chumbani kwake.

Alisema vyombo vya dola vinafuatilia kwa kina ili kubaini sababu.

Tukio hilo lilitokea saa chache baada ya gari aina ya Toyota Hiace kutumbukia ndani ya Ziwa Victoria na kuua zaidi ya watu 12 katika eneo la Kivuko cha Kigogo wilayani Misungwi.

Shuhudia Maajabu ya Chief Sultan Mzee...Mtaalamu wa Nyota za binadamu

$
0
0
ONA MAAJABU YA CHIEF SULTAN MZEE

  •  Mtaalamu wa Nyota za binadamu Africa Mashariki na dunia nzima,
  • Amewasaidia watu wengi kujua nyota zao na jinsi ya kuzing'arisha,
  • Anarudisha Mpenzi,Mume,Mke mliyeachana NDANI ya masaa manne(4) tu,
  • Anaweza kuongeza ROMANCE na MAHABA kwa Mwenzi wako
  • Anatoa pete ya BAHATI pamoja na kukupa uwezi wa Kupata faida kubwa katika biashara yako,
  • Kwa wale mnaosumbuliwa na Chuma ulete tatizo hilo analiondoa kabisa,
  • Anakuwezesha kushinda kesi iliyodumu siku nyingi nk.
  • KWA USTAA,UMARUFU UTAPATA UTAJIRI WA MAISHA NA BILA MASHARTI YOYOTE, UTAPEWA NGUVU ZA KUJILINDA NA UTAJIRI, MALI NA AFYA YAKO,Karibu kwa CHIEF SULTAN MZEE akupatie Pete za Bahati na utajiri.Wachungaji wengi duniani, Wanasiasa na Wasanii Maaarufu duniani Tayari wamejiunga pia wamefaidika na wamebadirisha  Maisha yao toka umasikini mpaka utajiri,kujua mengi zaidi na kutatuliwa Matatizo yako yoote kwa usiri na Uaminifu piga simu namba 0762-846979 au 0672-202509

Wakili Anayemtetea Lema Katika Kesi ya Kumtukana Rais Magufuli Ajitoa Ghafla

$
0
0
Wakili Anayemtetea Lema Katika Kesi ya Kumtukana Rais Magufuli Ajitoa Ghafla
WAKILI Sheck Mfinanga, anayemtetea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, katika kesi ya kumtukana Rais John Magufuli, amejitoa ghafla.

MBUNGE WA ARUSHA MJINI, GODBLESS LEMA.
Kujitoa kwa wakili huyo kulimfanya Lema aiombe mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi siku nyingine, ili apate muda wa kumtafuta wakili mwingine.

“Mheshimiwa Hakimu, mimi ni mbunge na ni mwanasiasa; si wakili, hivyo kujitoa kwa wakili wangu kumenishtua, naomba muda zaidi nitulize akili kisha nitafute wakili mwingine na nikimkosa nitajitetea mwenyewe,” aliomba Lema.

Baada ya ombi hilo, Hakimu Desderi Kamugisha aliwahoji mawakili wa serikali ambao ni Khalili Nuda na Alice Mtenga ambapo,
Nuda aliieleza mahakama kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa ushahidi wake jana na Wakili Mfinanga amejitoa, hivyo ni haki ya mshtakiwa kupewa muda Zaidi, ili atafute wakili mwingine.

Wakili Kamugisha alikubaliana na ombi la mawakili wa serikali na Lema na kuongeza muda hadi Novemba 14, mwaka huu.
Kesi hiyo ipo Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.

Wakili Mfinanga alidai hataweza kuendelea kumtetea mteja wake kutokana na kushindwa kupata mwenendo wa shauri hilo licha ya kuomba mara tatu, ili aweze kukata rufani Mahakama Kuu.

Kujitoa kwa Wakili Mfinanga kulifanyika mahakamani hapo kabla ya kuanza usikilizwaji wa kesi inayomkabili mteja wake ya kutoa matamshi mbalimbali ya kumtukana Rais.

Alisema: “Ninaomba nijitoe kuendelea na kesi hii sababu nimeomba nakala ya mwenendo wa kesi zaidi ya mara tatu.

“Leo hii (jana) pia nimeomba, ili nimsaidie mteja wangu kukata rufani, hakimu umeninyima sasa kwa misingi hii naomba kujitoa na sipo tayari kuendelea kumtetea.”

Spika wa Bunge la Ethiopia Ajiuzulu

$
0
0
Spika wa Bunge la Ethiopia Ajiuzulu
Spika wa Bunge la Ethiopia, Abadula Gemeda, amejiuzulu wadhifa wake huo bila kutoa sababu za maamuzi hayo.

Bw. Abadula ametangaza kujiuzulu kupitia televisheni ya taifa ya nchi hiyo, ameahidi kutoa sababu za maamuzi hayo katika tarehe ya baadaye.
Hata hivyo watu wengi wanadhani uamuzi wa Spika kujiuzulu ni hatua ya kupinga jinsi serikali kuu inavyoshughulikia hali ya usalama katika majimbo ya Oromia na Somali, ambapo watu wengi wameuwawa na maelfu kuondolewa kwenye makazi yao.

Spika wa Bunge ni miongoni mwa wanasiasa muhimu nchini Ethiopia na uamuzi wake wa kujiuzulu umewashangaza wengi. Kabla ya kuchaguliwa Spika, Bw. Abadula alikuwa ni Mkuu wa Jeshi, Waziri wa Ulinzi na pia Mkuu wa Jimbo la Oromia

Moto Mkubwa Wasababisha Maafa California, Marekani

$
0
0
Moto Mkubwa Wasababisha Maafa California, Marekani
Maeneo ya jimbo la California ambayo hukuza mizabibu yameathiriwa na moto mkubwa ambao unaenea kwa kasi sana na kusababisha vifo vya watu 10.
Mamia ya watu wamehamishwa makwao na inakadiriwa kwamba zaidi ya nyumba 1,500 zimeharibiwa na moto huo.
Watu saba waliuawa katika wilaya ya Sonoma, maafisa wamesema.
Watu zaidi ya 20,000 wamekimbia wilaya za Napa, Sonoma na Yuba baada ya moto mbaya zaidi wa nyika kuzuka maeneo hayo.

Moto unawaka katika maeneo 14 katika wilaya nane za kaskazini mwa California
"Moto huu umeharibu sana nyumba na miundo mbinu mingine na unaendelea kutishia maelfu ya nyumba, jambo ambalo limesababisha haja ya kuwahamisha maelfu ya watu," taarifa ya gavana imesema.
Kando na watu waliofariki Sonoma, wengine wawili wamefariki Napa na mwingine mmoja Mendocino.
Inaarifiwa kwamba kuna majeruhi wengine zaidi na wapo pia watu ambao bado hawajulikani waliko.


Marian Williams mkazi wa Kenwood, Sonoma amesema yeye na majirani zake waliutoroka moto huo kwa msafara wa magari.
"Ni moto mkubwa ajabu, hatujawahi kuona moto kama huo," ameambia shirika la utangazaji la NBC.
Mkuu wa idara ya misitu na kinga dhidi ya moto California Kim Pimlott, amesema nyumba 1,500 kufikia sasa zimeharibiwa.
Chanzo cha moto huo uliozuka Jumapili usiku bado hakijabainika.
Mkuu wa kukabiliana na moto wilaya ya Napa amesema hali ya kiangazi katika eneo hilo inaathiri juhudi za kuukabili moto huo na kwamba wameomba usaidizi kutoka wilaya nyingine jirani.
.
Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa imetoa tahadhari eneo lote la San Francisco na kusema "moto ukizuka basi kuna uwezekano utaenea kwa kasi sana".
Kwa Picha: Moto mkubwa California
Mmiliki mmoja wa mizabibu aliambia gazeti la LA Times kwamba anaamini shamba lake limeharibiwa baada yake na familia yake kukimbilia usalama Jumapili.
"Upepo ulikuwa unazuka na kufifia. Ndimi za moto zilituzingira," amesema Ken Moholt-Siebert.
Maafisa wa kuzima moto California wanakadiria kwamba eka 70,000 zimeteketezwa na moto huo.

Waziri Kalemani Aivyoepuka Mishale Nishati na Madini

$
0
0
Waziri Kalemani Aivyoepuka Mishale Nishati na Madini
Kwa wanamichezo kuna msemo maarufu kwamba makocha wanaajiriwa ili kufukuzwa na kuna wakati wadadisi wa masuala ya kisiasa nchini walizitazama wizara mbili; Maliasili na Utalii na ile ya Nishati na Madini katika sura hiyo.

Katika kipindi cha miaka 12, Maliasili na Utalii imeongozwa na mawaziri saba huku Nishati na Madini wakiwa sita kuanzia mwaka 2005 kabla ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri lililofanywa mwishoni mwa wiki na Rais John Magufuli.

Mabadiliko hayo ya mara kwa mara ikilinganishwa na wizara nyingine na sababu za kufanyika kwake ndiyo ambayo yamekuwa yakiibua maswali ya iwapo walioteuliwa watavuka salama pasi na kutumbukia kwenye tanuri la kashfa ambalo limewakumba wengi wa watangulizi wao katika wizara hizo.

Hata mabadiliko yaliyotangazwa na Rais Magufuli Jumamosi iliyopita yalitokana na kutenguliwa kwa uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Tamisemi) na Edwin Ngonyani (Naibu Waziri wa Ujenzi).

Sababu za kutenguliwa kwa nyadhifa zao ni pamoja na ripoti za uchunguzi wa usafirishaji mchanga wa madini nje ya nchi, uendeshaji, usimamizi na udhibiti wa almasi na Tanzanite kubainisha ubovu wa mikataba, udhaifu wa sheria katika uendeshaji wa biashara ya madini.

Katika mabadiliko hayo makubwa ya kwanza kufanya na Rais Magufuli tangu aingie madarakani Novemba 5, 2015, ameigawa wizara hiyo na sasa Nishati inasimama yenyewe kama ilivyo kwa Madini.

Dk Medard Kalemani, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini ambayo pia imekuwa ikikumbwa na kashfa za mara kwa mara kutokana na mikataba mibovu na tata ya umeme kama ya uingiaji mkataba mbovu wa uzalishaji umeme wa IPTL, Richmond, ndiye aliyepewa jukumu la kusimamia Nishati huku Angela Kairuki akikabidhiwa Wizara ya Madini.

Uteuzi wa Dk Kalemani katika wizara hiyo kumeibua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii ambako kwa ujumla, hoja kubwa imekuwa ni jinsi alivyoepuka mishale na kupanda hadi kileleni katika wizara hiyo.

Mjadala huo unatokana na ukweli kwamba mbunge huyo wa Chato, aliyeingia bungeni akichukua nafasi ya Dk Magufuli, amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali katika Wizara ya Nishati na Madini ikiwamo ya mkurugenzi wa sheria.

Katika mijadala hiyo, wapo waliogusia pia kuwa huenda Rais amejiridhisha kuwa hahusiki na makandokando ya mikataba mibovu iliyoisababishia hasara Taifa ambayo imewakumba mawaziri na vigogo wengi katika wizara hiyo.

Lakini wapo wanaoiangalia hoja hiyo kwa mtazamo tofauti, wakisema kuwapo kwake wizarani hapo kwa muda mrefu akiwa mwanasheria na baadaye mkurugenzi, hakuwezi kumuacha salama dhidi ya ubovu wa mikataba inayoibuliwa hivi sasa.

Madai hayo yameshikiwa bango na mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa akisema Dk Kalemani alikuwapo katika kipindi chote ambacho wizara hiyo ilikuwa ikikumbwa na kashfa mbalimbali zikiwamo za mikataba mibovu, “Unawezaje kumtofautisha mkurugenzi wa sheria na mikataba mibovu ambayo sasa imeiingiza nchi katika sitofahamu?

Mwaka 1999, Kalemani alifanya kazi katika Wizara ya Nishati na Madini akiwa ofisa mwandamizi wa sheria mpaka mwaka 2006. Baadaye mwaka 2013 hadi 2015, alikuwa mkurugenzi wa sheria.

Hata hivyo, waziri mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Njelu Kasaka alitofautiana na Msigwa akisema bila shaka Rais amejiridhisha kuhusu usafi wa waziri huyo.

“Unajua Rais ana macho mengi, pia ana njia nyingi za kujua mtumishi yupi ni msafi au amechafuka. Ukiwa nje huwezi kujua nani kachafuka lakini yeye ana uwezo wa kupata taarifa endapo mtumishi huyo alijiingiza moja kwa moja katika uchafu au wakati wanafanya uchafu huo yeye alijitenga pembeni.

Alisema anaamini kuwa Rais amejiridhisha na Dk Kalemani kwamba alikuwa msafi na kusisitiza kwamba aachwe afanye kazi aliyoagizwa.

Kasaka pia alimpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kuigawa wizara hiyo na kusema endapo waziri aliyepewa jukumu la kuiongoza akiitendea haki, italeta mafanikio.

“Hii wizara ilikuwa kubwa sana nishati pekee ina mambo mengi ilihitaji kugawanywa muda mrefu hata hivyo, hatujachelewa jambo la msingi ni kufanya kazi kwa lengo la kuleta maendeleo,” alisema.

Ivana Trump: Melania Ajibizana na Mke wa Zamani wa Trump

$
0
0
Ivana Trump: Melania Ajibizana na Mke wa Zamani wa Trump
Msemaji wa Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump ameeleza tamko la mke wa zamani wa Donald Trump Ivana kuwa "ya kujitafutia makuu na kelele za kutaka kujifurahisha".
Ivana Trump alikuwa amesema kwenye kipindi cha Good Morning America cha runinga ya ABC kwamba yeye ni "kimsingi mke wa kwanza wa Trump, mimi ni mama wa taifa".
Alisema huwa ana namba ya simu ya moja kwa moja White House lakini kwamba huwa hataki kupiga simu mara kwa mara huko kwa sababu hangependa kusababisha "wivu wa aina yoyote".
Mke huyo wa kwanza wa Trump anavumisha kitabu chake kwa jina Raising Trump (Kumlea/Kumuinua Trump), ambacho kitaanza kuuzwa Jumanne.
Aliolewa na Donald Trump mwaka 1977 lakini walitalakiana miaka ya 1990 baada ya Trump kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye angekuwa mke wake wa pili, Marla Maples.
Ivana na Donald walijaliwa watoto watatu - Donald Jr, Ivanka na Eric Trump.
Ivana Trump aliambia GMA kwamba huwa anawasiliana na mume wake wa zamani angalau mara moja kila wiki mbili.

"Nina namba ya simu ya moja kwa moja White House, lakini huwa sitaki kumpigia (Trump) akiwa huko kwa sababu Melania yuko huko,2 amesema.
"Sitaku kusababisha aina yoyote ya wivu au jambo kama hilo kwa sababu kimsingi mimi ni mke wa kwanza wa Trump. Mimi ni mama wa taifa, Sawa?"
Melania Trump alijibu kwa ukali kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stephanie Grisham.
"Bi Trumpameifanya ikulu ya White House kuwa nyumbani kwa [mwanawe wa kiume] Barron na Rais," taarifa hilo imesema.

"Hupenda sana kuishi Washington, DC na anachukulia kuwa heshima kubwa kwake kuwa Mama wa Taifa wa Marekani. Anapanga kutumia cheo na majukumu yake kuwasaidia watoto, na si kuuza vitabu.
"Ni wazi kwamba hakuna chochote cha maana kutoka kwa mke wake huyo wa zamani. Inasikitisha kwamba anajitafutia tu makuu na kutaka kelele za kutaka kujifurahisha kwa kelele zake mwenyewe."
Majibizano hayo ni ya kwanza kutokea hadharani kati ya mke wa zamani wa rais na Mke wa Rais.
Kabla ya Trump, Ronald Reagan alikuwa rais pekee ambaye aliwahi kumpa talaka mke wake.

IGP Sirro Aomba Msaada Kutoka kwa Viongozi wa Dini

$
0
0
IGP Sirro Aomba Msaada Kutoka kwa Viongozi wa Dini
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP simon siro amewaomba viongozi wa dini na wanasiasa mkoani iringa kushirikiana katika kutokomeza vitendo vya ulawiti na ubakaji ambavyo vinazidi kushamiri mkoani humo.

IGP  Siro Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani iringa.
IGP Siro amesema kuwa ili vitendo hivyo vitokomezwe ni lazima elimu izidi kutolewa kwa jamii hususani masuala ya imani za kishirikina ambayo yametajwa kuwa chanzo kikubwa cha kuchangia matukio hayo .
"Hili ni tatizo kwa watanzania inabidi elimu iendelee kutolewa sana. Tuna kazi kubwa ya kutoa elimu kwa hao ndugu zetu. Hayo mambo yalishapitwa na wakati, huwezi kupata utajiri kwa kumbaka mtoto wa umri wa  miezi miwili hadi mitatau. Tunaomba sana viongozi wa dini na siasa watusaidie katika hili. Sisi kama chombo cha dola tuna wajibika sana katika hili kwani elimu ni kitu cha kwanza kabla ya kutumia sheria, ili hata akifanya baadae akiwa na elimu unajua kabisa huyu anafanya makusudi," amesema Kamanda Sirro.
Aidha IGP Sirro  amezungumzia suala la watu ambao wamemshambulia mbunge wa Singida Mashariki  hivi karibuni Tundu Lissu na kusema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo.
Sambamba na hayo, amewasihi askari kufanya kazi kwakuzingatia misingi ya sheria bila kumuonea mtu yoyote kwakuwa hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria.

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumanne

$
0
0

Mauzo ya Soko la Hisa Yazidi Kushuka

$
0
0
Mauzo ya Soko la Hisa Yazidi Kushuka
Mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), yameendelea kupungua hadi Sh1.5 bilioni Oktoba 6, kwa wiki ya pili sasa.

Takwimu za DSE zinaonyesha wiki iliyoishia Septemba 22, mauzo ya soko hilo yalikuwa Sh53 bilioni ambayo yalipungua kwa Sh50 bilioni Septemba 29. Kutoka Sh3 bilioni za Septemba 29, wiki iliyoishia Oktoba 6 mauzo yameshuka kwa nusu na kufikia Sh1.5 bilioni.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Orbit Securities, Simon Juventus alisema kupungua kwa mauzo hayo ni kwa sababu wawekezaji wanalitazama soko kwanza kuona namna wanavyoweza kufaidika kama lilivyo lengo la wafanyabiashara wote.

Licha ya mauzo, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kutoka 800,000 Septemba 29 hadi 600,000 Oktoba 6.

Hata hivyo, ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa sokoni hapo umeongezeka kwa Sh431 bilioni kutoka Sh20.3 trilioni wiki iliyoishia Septemba 29 hadi Sh20.8 trilioni. Ongezeko hilo linatajwa kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za Kampuni ya Acacia kutoka Sh4,980 hadi Sh5,710, Vodacom kutoka Sh770 hadi Sh850, Nation Media Group (NMG) kutoka Sh2,360 hadi Sh2,390.

Juventus alisema hisa za Vodacom zinapanda kwa sababu watu wana imani na kampuni hiyo kwa matarajio kuwa itafikia malengo yake na wao watapata gawio wanalotarajia.

UN Yapiga Marufuku Meli Nne Juu ya Korea Kaskazini

$
0
0
UN Yapiga Marufuku Meli Nne Juu ya Korea Kaskazini
Umoja wa Mataifa umepiga marufuku meli nne dhidi ya kufika kwenye bandari za kimataifa baada ya kubainika kwamba zilikiuka vikwazo vilivyowekewa Korea Kaskazini na umoja huo.
Hugh Griffiths, mkuu wa jopo la UN kuhusu vikwazo vya Korea Kaskazini, amesema meli hizo zimekuwa zikisafirisha "bidhaa zilizoharamishwa".
Amesema hatua ya kupiga marufuku meli hizo si ya kawaida.
Umoja wa Mataifa uliongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini mwezi jana baada ya Pyongyang kufanya jaribio la silaha za nyuklia.
Bw Griffiths amesema ni "mara ya kwanza katika historia ya UN" kwa marufuku kama hiyo kutekelezwa.

"Kuna meli nne ambazo zimewekewa marufuku na kamati (ya UN). Hatua hii haina maana ya kuzuiwa kwa mali au marufuku ya usafiri. Ni marufuku ya kutotembelea bandari," alisema Jumatatu baada ya mkutano kuhusu utekelezwaji wa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini.
Meli ambazo zimepigwa marufuku ni Petrel 8, Hao Fan 6, Tong San 2 na Jie Shun.
Kwa mujibu wa tovuti inayofuatilia safari za meli ya MarineTraffic Petrel 8 imesajiliwa Comoros, Hao Fan 6 visiwa vya Saint Kitts na Nevis, na Tong San 2 imesajiliwa Korea Kaskazini.
Haijabainika Jie Shun imesajiliwa katika taifa gani.

UN iliidhinisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini mwezi Septemba
Korea Kaskazini imeshutumu hatua ya UN na Marekani kuiwekea vikwazo.
"Hatua hii ya kuwekea vikwazo na shinikizo kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea itawazindua tu watu wa Korea kuchukua hatua na kuimarisha nia yao ya kutaka kulipiza kisasi udhalimu wa Marekani na kufikisha mikomo uhasama wa miongo mingi," taarifa katika vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini ilisema Jumatatu.

Shamsa Ford Apambana na Ndoa Yake Asema Hawezi Kumuacha Mumewe Kwa Sababu ya Amemsaliti

$
0
0
Shamsa Ford Apambana na Ndoa Yake Asema Hawezi Kumuacha Mumewe Kwa Sababu  ya Amemsaliti
Mwigizaji wa Filamu Shamsa Ford amesema hawezi kumuacha mumewe kwa sababu amemsaliti na mwanamke mwingine.

Shamsa amejilinganisha na Hillary Clinton aliyekuwa mke wa Rais wa 42 wa Marekani, Bill Clinton aliyewahi kuingia katika kashfa ya kuchepuka na Monica Lewnsinky.

Shamsa amesema anampenda mume wake kwa sababu anampenda na anajishusha kumuomba msamaha pale anampokosea.

“Nakupenda mume wangu halali wa ndoa aliyenipa mwenyezi Mungu. Sitoachana na wewe kwa ajili ya makelele ya wanadamu nitaachana na wewe kwa mapenzi ya mwenyezi Mungu,”

“Jamani sitokuja kumuacha mume wangu kwa ajili ya mwanamke hata siku moja labda afanye makubwa yasiyoeleweka kwenye jamii. ‘Amecheat’ Bili Clinton sembuse Rashid wangu? Alihoji mwigizaji huyo maarufu aliyecheza filamu ya Chausiku.

Katika siku za hivi karibuni mwigizaji huyo amekuwa akirusha vijembe kwa mwanamke anayedai kumtumia ujumbe mume wake na kutoa taarifa kwa wanahabari ili wamwandike vibaya.

Takukuru Yawataka CCM Wenye Malalamiko ya Uchaguzi Kutoa Ushirikiano

$
0
0
Takukuru Yawataka CCM Wenye Malalamiko ya Uchaguzi Kutoa Ushirikiano
Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Morogoro, Beutoz Mbwiga amewataka wanaolalamika kuhusu rushwa katika uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoa ushirikiano ili wahusika wakamatwe.

Tangu kuanza uchaguzi takriban miezi mitatu iliyopita Takukuru mkoani Morogoro imewahoji wanachama zaidi ya 10 wa CCM kutokana na malalamiko ya kutoa au kupokea rushwa lakini haijamfikisha yeyote mahakamani kutokana na tuhuma hizo kushindwa kuthibitishwa.

Kamanda Mbwiga akizungumza na Mwananchi amesema taasisi hiyo imekuwa ikipokea malalamiko kwa njia ya simu na maandishi kuhusu uwepo wa rushwa katika uchaguzi lakini wanapofuatilia wanashindwa kuthibitisha.

“Niwaombe wana CCM wanaolalamika watupe ushirikiano ili tuwatie hatiani wahusika, wanatupigia simu na tunatuma watu wetu kwa siri kwenye uchaguzi lakini hakuna ushahidi kama kuna rushwa inatolewa,” amesema Mbwiga.

Amesema kupambana na rushwa kunahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi wanaolalamika.

Kamanda Mbwiga amezitaja wilaya zinazoongoza kwa malalamiko ya rushwa kuwa ni Kilombero, Morogoro Mjini, Morogoro Vijijini, Gairo na Mvomero.

Amesema Takukuru pia imekuwa ikikabiliwa na changamoto inapomwita mwanachama au mgombea kumhoji wamekuwa wakilalamika kuwa inatumika kuwadhoofisha katika uchaguzi.

Akizungumzia rushwa katika uchaguzi, aliyekuwa mgombea wa nafasi ya katibu wa uenezi wilaya ya Mvomero, Abdallah Bozo amesema vitendo hivyo vilijitokeza na hakuna hatua zilizochukuliwa.

Mwanachama wa CCM, Rashid Abdallah mkazi wa Mvomero ameilaumu Takukuru kwa kutochukua hatua.

Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Kulwa Milonge amesema chama hicho kimesimama katika nafasi yake kuhakikisha hakuna kiongozi anayepatikana kwa kutoa rushwa.

Amesema kanuni za maadili za CCM ziko wazi kuwa ikibainika mgombea alitumia rushwa kupata ushindi ataondolewa na uchaguzi utarudiwa.

Nyota ya Zari Yazidi Kung'aa Apata Shavu Nono Mercedez- Benz

$
0
0
Nyota ya Zari Yang'aa  Apata Shavu Nono Mercedez- Benz
Mwanadada Zarina Hassan maarufu kwa jina la Zarithebosslady amepata dili la kuonyesha magari aina ya Mercedez-Benz ya kampuni ya AMG Performance Centre iliyoko nchini Afrika ya Kusini.

Hayo yameonekana baada ya mwanadada huyo kuweka picha katika ukurasa wake wa Instagram gari nyeupe aina ya Mercedez-Benz huku akiwa amevalia suti yenye rangi ya zambarau.

Katika kurasa huo aliweka picha tofauti tofauti na kuandika maneno yafuatayo ‘amgperformancecentremenlyn is your centre for class & #stateTheArt cars. Thank you for the car’ na nyingine akiweka #closeDealsInHeels.

Baada ya ujumbe huo mashabiki wake wamempongeza kwa hatua hiyo hasa baada ya yote aliyoyapitia katika maisha yake ya mahusiano na msanii Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz.

Rais wa TFF Atembelea Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF

$
0
0
Rais wa TFF Watembelea Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF
Rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania Wallace Karia pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Kidao Wilfred wametembelea makao makuu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF na kukutana na Rais Bw. Ahmad Ahmad.

Ziara hiyo ya Rais Karia imefanyika jana ambapo walitua kwenye ofisi za CAF zilizopo Cairo nchini Misri na kupokelewa na Rais Ahmad Ahmad kisha kufanya kikao kilichojadili maendeleo ya soka nchini.

Aidha kikao hicho kilihudhuriwa pia na Rais wa Heshima wa TFF ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Bw. Leodegar Tenga.
Rais wa CAF ameahidi kuisaidia TFF katika mipango ya maendeleo ya soka nchini ili kuongeza umoja kwasababu soka siku zote hujenga umoja na mshikamano.

Rais Karia na wenzake waliingia madarakani August 12 mwaka huu ambapo tangu waanze majukumu yao wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha soka linapiga hatua kwa kutafuta wadhamini ambao watawezesha maendeleo hayo ya soka.

Wadukuzi wa Korea Kaskazini Waliiba siri za Kijeshi za Korea Kusini

$
0
0
Wadukuzi wa Korea Kaskazini Waliiba siri za kijeshi za Korea Kusini
Wadukuzi kutoka Korea Kaskazini walidukua mitambo ya kijeshi ya Korea Kusini na kuiba nyaraka nyingi zenye taarifa muhimu za kijeshi.
Miongoni mwa yaliyokuwemo kwenye nyaraka hizo ni mpango wa kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Mbunge wa Korea Kusini Rhee Cheol-hee amesema taarifa hizo zilitoka kwa wizara ya ulinzi ya Marekani.
Nyaraka hizo zilikuwa na mipango ya karibuni zaidi ya kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani.
Kwa Picha: Maisha taifa lenye usiri zaidi dunaini

Mwanafunzi anayetaka ukasomee Korea KaskaziniKorea Kusini mwezi mei ilifichua kwamba sehemu kubwa ya data iliibiwa na wadukuzi Septemba mwaka jana, madai ambayo Korea Kaskazini ilikanusha.
Jeshi la Korea Kusini limesema kufikia sasa asilimia 80 ya taarifa ambazo ziliibiwa kufuatia udukuzi huo bado hazijatambuliwa.
Mambo muhimu kuhusu hali ya kijeshi rasi ya Korea

Calisah Awajibu Waliomsema Baada ya Kuvaa Viatu vya Kike Asema Hata Gauni Atavaa

$
0
0
 Awajibu Waliomsema Baada ya Kuvaa Viatu vya Kike Asema Hata Gauni Atavaa
MWANAMITINDO maarufu Bongo, Calisah, ambaye hivi karibuni ameshangaza ulimwengu kwa kupiga picha akiwa amevaa viatu vya kike, amefunguka kuwa yeye ni mfanyabiashara kwa hiyo yuko tayari hata kupiga picha na gauni endapo atalipwa dau la shilingi milioni kumi.
Calisah ambaye kwa sasa ameganda kama ruba midomoni mwa watu kutokana na picha hizo, alisema:

“Siwezi kukataa Mkwanja kwa kuhofia watu wataongea, kitendo cha kuvaa viatu na kupiga navyo picha wala siyo vibaya, ingekuwa nazurura navyo mitaani hapo sawa. Waendelee tu kuongea mimi naingiza mtonyo na siyo viatu tu, mtu yeyote atakayeweza dau langu la milioni 10, hata gauni nitavaa.”

Pia mwanamitindo huyo alisema kuwa baada ya picha hizo kusambaa mitandaoni, familia yake ilichukia sana kiasi cha kumweka ‘kitimoto’ kwenye ‘Whatsapp Group’ la familia, kitu ambacho kilimuumiza sana, ila ilifika muda wakamuelewa.

Mtukufu Aga Khan Avikwa Nishani ya Juu ya Heshima na Rais Mseveni

$
0
0
Mtukufu Aga Khan Avikwa Nishani ya Juu ya Heshima na Rais Mseveni
Rais Yoweri Museveni amemvisha Mtukufu Prince Karim Aga Khan IV nishani ya juu ya heshima barani Afrika (Most Excellent Order of Pearl of Africa, The Grandmaster) ili kutambua miongo kadhaa ya mchango wake katika maendeleo ya Uganda.

Museveni alimvisha nishani hiyo Jumatatu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bushenyi-Ishaka katika wilaya ya Bushenyi.

Mtukufu Aga Khan, ambaye ni Imam wa madhehebu ya Ismailia, kupitia taasisi ya Aga Khan ana miradi mingi ya maendeleo katika nyanja za elimu, nishati, afya, hoteli na utalii, vyombo vya habari.

Aga Khan aliwasili nchini Uganda Jumapili kuwahi maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru na alikuwa na kikao na Rais Museveni pamoja na maofisa waandamizi wa serikali katika Ikulu ya Entebbe.

Mapema wakati wa utoaji taarifa kwa waandishi wa habari katika Kituo cha Habari Uganda, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Esther Mbayo alidokeza sababu za kumtunukia nishani hiyo ya heshima Aga Khan.

“Atatunukiwa nishani ya heshima ya juu kwa sababu ya mchango wake mkubwa wa kiuchumi alioutoa kwa nchi yetu duniani kwa ujumla,” alisema Mbayo.

TRA Yatangaza Makusanyo ya Kodi kwa Robo ya Kwanza ya Mwaka

$
0
0
TRA Yatangaza Makusanyo ya Kodi kwa Robo ya Kwanza ya Mwaka
Makusanyo ya kodi kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 (Julia, Agosti na Septemba) yamefikia Sh3.65 trilioni ambayo ni ongezeko la asilimia 1.2 ukilinganisha na makusanyo ya kipindi hicho kwa mwaka uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema makusanyo hayo ni hatua nzuri kuelekea lengo la mwaka ambalo ni Sh17 trilioni.

Ametoa mchanganuo wa makusanyo hayo kwa kila mwezi ambao umeonyesha kuwa wamekusanya zaidi ya Sh1 trilioni.

“Julai tulikusanya Sh1.1 trilioni, Agosti Sh1.2 trilioni na Septemba Sh1.3 trilioni. Watu wamekuwa wakitaka makusanyo hayo yawe yanasomwa kila mwezi lakini tukitoa kila robo ya mwaka tunaonyesha kiasi kwa kila mwezi,” amesema Kayombo.

Ukizidisha makusanyo hayo mara nne ambayo ni tafsiri ya mwaka mzima jumla inakuwa Sh14.6 trilioni lakini Kayombo anasema makusanyo ya robo moja hayawezi kutoa picha ya jumla kwasababu misimu ya biashara inatofautina hivyo ana matumaini lengo litafikiwa.

Amevitaja vyanzo vikuu vya mapatio kuwa ni viwanda, ajira na uingizaji wa bidhaa lakini amesema vyanzo hivyo hutoa kodi zaidi kulingana na wakati.

Kadhalika Kayombo amewakumbusha wamiliki wa majengo nchi kulipa kodi zao mapema badala ya kusubiri mwishoni mwa mwaka na kusababisha misongamano na usumbufu usio wa lazima.

Pia wamewataka wenye michezo ya bahati nasibu wametakiwa kulipa kodi zao kama sheria inavyoelekeza. “Anayepaswa kulipa kodi kwa wiki alipe na anayepaswa kulipa kwa mwezi au mwaka naye afanye hivyo.”

Kayombo amewataka wananchi kutumia na kuziamini takwimu zinazotolewa na mamlaka hiyo kwani takwimu zote nyingine kuhusiana na mapato ambazo hazijatolewa na TRA sio za kuaminika. 

Askari Wawili wa Kulinda Amani Umoja wa Mataifa Kutoka Tanzania Wauwawa

$
0
0
Askari Wawili wa Kulinda Amani Umoja wa Mataifa Kutoka Tanzania Wauwawa
Askari wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, wameuawa kwenye mashambulizi makali yanayoendelea nchini Kongo.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Beni ambako Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani wanapigana na kikundi cha waasi cha Uganda (ADF), kilichoanza vurugu na ukiukaji wa haki za binadamu kwa kuua raia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amethibitisha kuuawa kwa wanajeshi hao kutoka Tanzania, huku akitoa tarifa kuwa askari wengine 18 kutoka nchi tofauti wamejeruhiwa.
Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amehimiza mamlaka za Kongo kuchunguza haraka tukio hilo na kuwachukulia hatua wahusika.

Hivi karibuni nchini Kongo kumekuwa na machafuko baada ya vikundi vya uasi kuanza tena vurugu na mauaji baada ya miaka kadhaa kupita kukiwa shwari, huku serikali ya nchi hiyo na Umoja wa Mataifa wakiishtaki ADF kwa ukiukaji wa hai za binadamu na mauaji ya watu zaidi ya 700 katika eneo la Beni, tangu Oktoba 2014.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images