Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

ZITTO AMJIBU MWANASHERIA MKUU ADAI KUWA NI MUONGO MKUBWA YEYE ALISHAMPA MAJINA SIKU NYINGI

0
0
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema atamjibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema juu ya kauli aliyoisema bungeni kwamba mbunge huyo hana majina ya Watanzania walioficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi. Zitto alisema kwa kuwa Jaji Werema alimshambulia kupitia bunge naye atatoa majibu bungeni ili ukweli uweze kujulikana.

Zitto alitoa kauli hiyo jana nje ya ukumbi wa Bunge alipokuwa akizungumza na Rai iliyotaka kujua msimamo wake baada ya Jaji Werema kuliambia Bunge Zitto aliiambia kamati iliyoundwa na Serikali kuchunguza sakata la Watanzania wanaodaiwa kuficha fedha nje ya nchi kwamba hana majina.

“Nilimsikia Mwanasheria MKuu wa Serikali akinishambulia jana (juzi), nitakachokifanya ni kwamba wiki ijayo nitamjibu hapa bungeni baada ya kumuomba Spika anipe nafasi ya kuwasilisha maelezo binafsi.

“Mwanasheria Mkuu ni muongo, nasema totally ni muongo kwa sababu kwenye kamati yao nimehudhuria mara nne na nikawakabidhi majina ya watuhumiwa.

“Tena kibaya zaidi, niliwakabidhi mpaka jina la mchunguzi wa kimataifa anayeweza kuwasaidia katika uchunguzi wao, halafu leo anasema nilikuwa naikwepa kamati ni muongo, nasema ni muongo, lakini, hoja iliyopo ni je, mabilioni yapo au hayapo,” alisema Zitto kwa kifupi.

Juzi, Jaji Werema aliliambia Bunge jinsi ambavyo Zitto alikuwa akikwepa kutoa taarifa za watu walioficha fedha nchini Uswisi.

Jaji Werema alisema licha ya mbunge huyo kukaririwa mara kadhaa akisema anayo majina ya walioficha fedha hizo nje ya nchi lakini mara kadhaa alikuwa akikwepa kuhojiwa na kamati iliyoundwa na Serikali kufuatilia fedha hizo.

Alisema kutokana na tabia hiyo Serikali imeazimia kuchukua hatua za kisheria dhidi yake na kusisitiza hawawezi kukubali mtu alidanganye Bunge.

Jaji Werema alisema hayo alipokuwa akihitimisha mjadala wa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala.

“Lakini leo hapa amesema Serikali haina nia ya kurudisha fedha zilizofichwa Uswisi, kwa maana hiyo Mheshimiwa Naibu Spika, Zitto Kabwe ni mzito na nakubaliana na Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) aliyesema hapa kwamba Zitto alete majina hayo,” alisema Jaji Werema.
-MTANZANIA

MCHEZAJI OKWI SASA NI YANGA DAMU SAMU-ATIA SIGN YANGA SIMBA MLIE TUUU

0
0
Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.

Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.

Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku wa Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa kihistoria  klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.

Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji  watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.

Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.

ASKARI WA JESHI LA POLISI AMWAGA MATUSI MAKUBWA HADHARANI AKIWA KAZINI

0
0
ASKARI wa Jeshi la Polisi nchini, Koplo Genja mwenye namba E-8455 ametukanwa na kudhalilishwa hadharani na dada mmoja mwenye asili ya Asia, baada ya afande huyo kutokubaliana na amri ya dada huyo ya kuacha kuchukua picha za gari lilohusishwa na makosa ya kiusalama barabarani.

Tukio hilo limetokea jirani na makutano ya barabara za Bibi Titi Mohammed na Zanaki, majira ya saa mbili na nusu asubuhi ya Ijumaa baada ya juhudi za askari wa jeshi hilo kumsihi kijana mmoja wa kiasia aliyekuwa akiendesha gari dogo aina ya Carina lenye namba za usajiri T642 CLQ kugoma kutekeleza maelekezo na amri kadhaa za askari waliokuwepo eneo la tukio.

Awali kijana huyo hakutekeleza amri iliyomwelekeza kuingia barabara ya Zanaki kutoka barabara ya Bibi Titi wakati msafara ulioongozwa na Jeshi la Polisi ulipokaribia kupita eneo hil. Amri iliyotolewa na PC John mwenye namba G-9487 aliyekuwepo eneo hilo, badala yake kijana huyo alikaidi na kuendelea mbele kidogo ndani ya barabara hiyo na kuegesha gari eneo finyu baada ya kulazimishwa asiendelee mbele zaidi.

Kufuatia tukio hilo PC John aliwaomba msaada kwa askari wenzake wanaotumia pikipiki waliopita eneo hilo kumhoji huku yeye akiendelea kuongoza magari ambayo kwa asubuhi hiyo yalikuwa mengi sana. Ni katika mahojiano hayo kijana huyo aliposhindwa kutoa ushirikiano kwa askari hao ambao nao waliomwita Koplo Genja kwa msaada zaidi.

Koplo genja alipofika eneo hilo alimuomba kijana huyo kushuka kwenye gari akagoma, alichokifanya ni kufungua kidogo kioo cha gari hilo kilichokuwa hakionyeshi ndani “tinted” na kuendelea kujibu maswali aliyoulizwa.
Mwishowe alifunga kioo na kuonekana akipiga simu kwa jamaa zake ambapo baada ya dakika chache alifika dada mmoja ambaye alimhoji afande Genja juu ya kinachoendelea. Ni katika mazungumzo hayo hawakuelewana ndipo afande aliamua kutoa kamera ndogo na kupiga picha kama vielelezo.

Tukio hilo lilionekana kumuudhi dada huyo kiasi cha kutamka  mara kadhaa maneno “…Do not take pictures” na hatimaye kusikika akitamka neno “Stupid”. Neno hilo ndilo lililowashtusha na kuwafadhaisha raia kadhaa waliokuwa wakishuhudia tukio hilo akiwemo mwandishi wa habari hii.

VIDEO:ANGALIA HOTUBA YA RAIS KIKWETE ILIYOSIFIWA NA DUNIA NZIMA KWENYE MSIBA WA MANDELA JANA

0
0
Earlier today President Jakaya Mrisho Kikwete of Tanzania delivered a moving eulogy when paying tribute to the late Nelson Madiba Mandela during the final burial ceremony for Madiba at Qunu, Eastern Cape-South Africa. During his speech, President Kikwete highlighted a couple of things especially the rare and deep relationship between Tanzania and South Africa from the earlier days of freedom struggle and the bond between former Tanzanian President, Late Julius Nyerere[Mwalimu] and Nelson Mandela. Here is the video of the speech.
VIDEO HII HAPA:

VIDEO: HUU NDIO USHAHIDI WA MAMA SWAI AKIMRUDISHIA MANDELA VIATU ALIVYOVIACHA TANZANIA

0
0

Late #Madiba Receiving his boots in 1995 which he left them in Tanzania 1962 from Mama Swai. On 11 January 1962, Nelson Mandela secretly left South Africa to travel around the continent and drum up support for the African National Congress. He visited 14 countries, including Tanzania - where he left behind a pair of his boots. Below Vicky Swai recounts the story of how she kept the boots for 33 years
 TAZAMA VIDEO HAPA MAMA SWAI AKIONGELEA HIYO HABARI

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MWANZA AUWAWA KWA KUPIGWA MAWE.

0
0
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini Mwanza.

Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wananchi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani? 

Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani. Kwa mujibu wa Katibu wa CCM ndg Joyce Masunga (maarufu kama Maziwa Fresh) ni kweli kuwa tukio hili limetokea na tunaendelea kufuatilia kupata habari zaidi.
Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kushambuliwa 

Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa Bungando.

BABY MADAHA"TAREHE 22 DEC PALE GOLDEN TULIP NITAMUONESHA DIAMOND MIMI NI NANI"

0
0

"Tarehe 22 Jumapili Disemba mwaka huu pale Golden Tulip nitamuonyesha Diamond,kuwa Queen of Swagg ni nani,ambapo yeye alizindua Single moja ya ngololo pale Serena mimi ninazindua single 4 moja ikiwa ni Soundtrack na Move yangu mpya ya the Galbladder, iliyonigarimu mamilioni kuitengeneza nje ya nchi,huku show nzima ikidhaminiwa na Heinekein ambao pia ndiyo wadhamini wa lebo ya Candy& candy ya jijini Nairobi, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa kiongozi mzito kutoka Ikulu ya Rais Kikwete pale Magogoni jijini Dar es Salaam"alisema Baby Madaha.

TEAM YA GOR MAHIA YAPATA PIGO WACHEZAJI VINARA AKIWEMO IVO MAPUNDA WAONDOKA

0
0
WAMEIBOMOA Gor Mahia. Ndivyo unavyoweza kusema kuhusiana na hatua ya Simba ya Tanzania kuwasajili kipa, Ivo Mapunda na beki Donaldi Musoti.

Klabu hiyo ya Tanzania ambayo maofisa wake walikuwapo jijini Nairobi wakati wa mashindano ya Cecafa Senior Challenge Cup yaliyomalizika juzi Alhamisi, walikamilisha usajili wa wawili hao jana Ijumaa.

Mapunda aling’ara katika michuano hiyo akiwa na timu ya Tanzania Bara, wakati Musoti alikuwa katika kikosi cha Kenya. Mapunda amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wakati Musoti amesaini miaka miwili.

Musoti alisema: “Nimefurahi sana kusaini Simba, nakwenda kufanya kazi na Loga (Zdravko Logarusic) ambaye nimekaa naye Gor Mahia kwa mafanikio.

“Nina uzoefu wa kutosha na soka la Afrika Mashariki na ninadhani nitafanya kazi nzuri na Simba kama Wakenya wenzangu waliopita, kikubwa ni ushirikiano tu.”

Katika kikosi cha Gor Mahia,Musoti hucheza sambamba na Ivan Anguyo au Edwin Lavatsa.

Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Gor Mahia, Faz Ochieng, amekiri kuwa kuondoka kwa wawili hao ni pigo kwao na watakaa kujadiliana nini cha kufanya.

“Sijapata taarifa rasmi za kuondoka kwao, lakini mikataba yao inamalizika mwezi huu na ilikuwa tukae nao kujadiliana juu ya mikataba mipya,” alisema.

Gor Mahia itakuwa imepata pigo kubwa baada ya wachezaji hao kusaini Simba kwani walikuwa tegemeo kwao na waliibeba kwenye Ligi Kuu Kenya msimu uliomalizika ambapo timu hiyo ilitwaa ubingwa.

Mapema wiki hii matajiri wa Gor Mahia walijinadi kuwa watahakikisha kwa gharama yoyote ile wanawabakiza wachezaji hao jambo ambalo limegonga mwamba kwani viongozi wa Simba waliowasili usiku wa Jumanne iliyopita wameshamaliza kazi.

Kuthibitisha jinsi klabu hiyo ilivyopata pigo, baadhi ya mashabiki wa Gor Mahia jana Ijumaa walivamia ofisi za timu hiyo zilizopo maeneo ya uwanja wa soka wa Nyayo wakiwa na mavuvuzela na kuwapigia kelele viongozi wao wakiwahoji imekuwaje wamewaachia wawili hao kujiunga na Simba.

Mashabiki hao waliokuwa zaidi ya 50 wamechukizwa na jambo hilo na kuwaoana viongozi wao ni wazembe kwani klabu hiyo ni kubwana ina fedha za kuwabakiza.

REGINALD MENGI AMJIBU PROF MUHONGO

0
0
1.  Nafurahi kwa nafasi ya kuwa nanyi leo kwa kuwa sekta binafsi itapata nafasi ya kipekee  kesho tarehe 16 Desemba 2013, ya kuwa na mkutano chini ya Mhe. Rais Kikwete kama mwenyekiti.
 

2.   Mimi binafsi nitapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta binafsi chini ya TPSF. Lakini limekuwepo tatizo la mambo yaliosemwa na Mhe. Profesa Muhongo kunihusu ambayo ningependa niyafafanue ili nisiende kwenye kikao cha kesho zikiwepo fikra kwamba mambo hayo ni ya kweli.
3.   Katika tarehe za mwanzo wa mwezi Septemba mwaka 2013 Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba: 


  
 Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu.” 





4.   Ukweli ni kwamba mimi siyo mbinafsi na pili sijawahi kuomba upendeleo wa kupewa kitalu cha gesi bali ninapigania Watanzania kwa ujumla.

5.   Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Mhe. Profesa Muhongo alitoa takwimu za kunihusu ambazo siyo sahihi.

6.   Ukweli ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita mojaya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.

7.   Naomba nisisitize kwamba mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza kibiashara. Ukweli ni kwamba ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, (National Economic Empowerment Act, 2004) ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania katika rasilimali zao.

8.   Ninamatumaini makubwa kwamba katika mkutano wa kesho ambao utatoa fursa kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uwenyekiti wa Mhe. Rais utatuwezesha kupata muafaka wa ni jinsi gani tutashirikiana katika juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi wetu.
 

Dkt. Reginald A. Mengi

Dar es Salaam

15 Desemba 2013

MANGI AAMUA KUCHOMA NYUMBA MOTO KISA KADHULUMIWA PENZI NA MKEWE

0
0
Nyumba ya familia moja huko mtaa wa ugombolwa Kata ya Segerea  ikiwa inateketea kwa moto usiku huu mara baada ya Baba wa familia hiyo kuhisi kuwa mke ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mmoja na kuamua kuichoma moto nyumba hiyo sababu ya wivu wa mapenzi. 
 Nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mkali
 Kwa moto huu hakuna kilichoweza kuokolewa mpaka sasa
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.

Segerea, Dar Es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa Ugombolwa Kata ya segerea Jijini Dar  imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine. 

Hali hiyo imetokea usiku huu majira ya Saa tano Kasoro usiku katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia moto nyumba hiyo.

Mmoja wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana Ebu Ona Sasa mwanaume Mzima Anateketeza Nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya Shilingi kisa Mkewe anatembea nje ya ndoa Sasa ona watoto wake wataishi wapi?..watu wengine ni wajinga sana Kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea Shuhuda huyo

Mpaka Mtandao huu unaondoka eneo la tukio nyumba hiyo ilikuwa bado ikiteketea kwa moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwaajili ya kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au laah huku ikikadiriwa kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto kwani mpaka tunaondoka hakuna kikosi cha zimamoto kilichofik eneo la tukio wala majirani hawakuonyesha dalili zozote zile za kuuzima mot huo.


Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi wala watu kupoteza maisha katika ajali hiyo ya moto.

WANAWAKE WAREMBO NDIO WATEJA WAKUBWA WA WAGANGA UKILINGANISHA NA WALE WA KAWAIDA

0
0
Nasikia masista duh na warembo wengi ndio wqashiriki wakubwa wa mambo ya kiganga na dawa za mapenzi ukilinganisha na wasichana wenye sura za kawaida.
Pia utafiti usio rasmi unaonyesha kuwa wanawake warembo ndio wanaoongoza kwa kugombea mabwana kulinganisha na wale wasio na sura zenye wingi wa vikwerombwezo

SABABU ZA KWANINI HOTUBA YA JAKAYA KIKWETE KUMUAGA MANDELA ILIKUWA BORA ZAIDI

0
0
Ndugu zangu, 

NOTHING can come from NOTHING. Wamesema hili Wanafalsafa wa Uyunani ya Kale .

Nimemwona na kumsikiliza Rais wetu Jakaya Kikwete akizungumza kwenye siku muhimu ya kumuaga kwa mara ya mwisho Mzee wetu Nelson Mandela. 

Muda wote wa hotuba yake, JK alibaki kwenye mstari kwa namna ile ile ya kuweka bayana kwa ulimwengu, kuwa ' msione vinaelea'. 

Hakika alichofanya JK leo ndicho haswa alipaswa kukifanya, na amekifanya kwa kutumia weledi wake kwenye diplomasia na kuchanganya uzoefu wake kwenye uongozi wa kisiasa na dola kwa ujumla.

Ni kuitumia fursa ile ambapo macho na masikio ya dunia yalielekezwa Quni, kwa yeye rais kuiambia dunia, na si kuisubiri CNN au vyombo vya habari vya Kimagharibi kuifanya kazi hiyo, juu ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo mchango wa Tanzania kumfanya Mandela na viongozi wengine wa Kiafrika kuonekana kama walivyoonekana kwenye macho ya dunia. 

Hakika, JK anastahili pongezi kwa kazi njema aliyoifanya leo ya kuiweka tena Tanzania katika ramani ya dunia, si tu kama nchi ile ya mbuga za wanyama na Mlima Kilimanjaro, bali ' Taifa Kubwa' lililochangia kushiriki mikakati ya ukombozi ikiwemo kutoa misaada ya silaha, mafunzo na hata makazi kwa wapigania ukombozi wa Afrika.

JK aliipitia historia ya mchango wa Tanzania ambayo wengi waliokuwa wakimsikiliza, ama waliisahau au hawakuijua kabisa.

Lakini, tujiulize pia kama Watanzania, katika aliyoyasema JK kule Quni, ni Watanzania wangapi wanayajua? Inahusu umuhimu wa kuipitia historia yetu ili, kama Watanzana, tuweze kumiliki ' K3'- Kujitambua, Kujiamini na kuthubutu. Imefika mahali tunaionea aibu hata historia yetu.

Na nyongeza katika yale aliyoyasema JK leo ni kumbukumbu ya kihistoria ambayo haitajwi pia, kuwa Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, ndiye aliyempa hifadhi Tanzania, Rais wa Pili wa Afrika Kusini huru, Thabo Mbeki baada ya kutoroka Afrika Kusini. Baadae Thabo Mbeki akaenda kusoma Uingereza.

Jambo hilo linathibitishwa katika kitabu alichoandika msomi mahiri wa Afrika Kusini, William Gumede. Anasema;

" In 1962, Thabo slipped out of the country to which he would not return for twenty -eight years, travelling through Botswana to Rhodesia, where he was arrested and held in a Bulawayo prison for several weeks. The white Rhodesian authorities intended to deport him back to South Africa and waiting for security police, but British Labour MP, Barbara Castle intervened after being lobbied by the ANC, and Mbeki was granted asylum in Tanzania by President Julius Nyerere." ( William Gumede, Thabo Mbeki and The Search For Soul of The ANC, pg 36)

Naam, ni wakati sasa wa viongozi wengine, bila kujali itikadi zao, wanapokuwa kwenye majukwaa ya kimataifa, kuzitafuta fursa za kuonyesha yale ambayo huko nyuma tumekuwa na uwezo nayo, na bado, kama nchi, tunaweza kuaminika katika kutoa mchango wa uzoefu wetu kwenye masuala mbali mbali ya Kimataifa. 

Usiku Mwema.

Maggid Mjengwa.
Iringa.

HARUSI NYINGI ZA SIKU HIZI WANAWAKE HUWA HAWAPENDEZI UKILINGANISHA NA MWANAUME

0
0
Nimekuwa nikishuhudia harusi nyingi ambapo wanaume tu ndio wanaopendeza, . kinachopelekea hali hii ni mkorogo ulipita kiasi na kupelekea hata sura ya huyo mwanamke isiwe natural look, na ikawa mchina hivi, especialy kama mwanamke ni mweusi na bwana ni mweupe kwa rangi. hapa kwenye sekta ya reception ambapo upakaji wanja, lipstic na mafuta usoni na mchanganyiko mwingineo unakuwa too much mpaka anakuwa kama mcheza ngoma za kienyeji hivi. na mwonekano wake mpya unapelekea kama ulikuwa unamjua bibi harusi, umwone ni mgeni machoni na yule uliyekuwa unamfahamu kabla. pengine wana jamvi ningeomba maoni yenu kwenye hili jambo.

HATIMAYE LULU AFUNGUKA SAKATA LA KUFUMANIWA WAKIDUU NA YOUND D KWENYE GARI

0
0
MWISHONI mwa wiki iliyopita, taarifa zilienea katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari Bongo kwamba msanii wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young Dee’ na nyota wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wamebambwa na polisi wa doria wakivunja amri ya sita ndani ya gari aina ya Hyundai, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tukio lililojaa utata mkubwa.
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao walinaswa wakifanya uchafu huo na askari waliokuwa doria lakini wakawavuta chobingo na baada ya muda, wakawaachia na kutokomea kusikojulikana.
Ili kupata ukweli wa tukio hilo la aibu, paparazi wetu alianza kwa kumvutia waya Young Dee na kumsomea mashtaka yake ambapo alifunguka kuwa ni kweli amezisikia habari hizo lakini akakana kwamba ishu hiyo siyo ya kweli bali imezushwa na kundi la watu wenye lengo la kumharibia jina lake mbele ya jamii.
 “Siyo kweli kabisa, isitoshe nina kama mwezi mzima sijaonana na huyo Lulu, huku ni kutaka kuchafuliana majina tu,” alisema Young D.
Habari zinadai kuwa licha ya Young Dee kukanusha kuwa hajaonana na Lulu kwa muda mrefu, siku ya tukio walikuwa pamoja ingawa hawakutaka kuonekana na mtu yeyote.
Kwa upande wa Lulu alipotafutwa, alifunguka: “Kweli nimesikia ishu kama hiyo ila kinachonishangaza na kunisikitisha ni kwamba siku hiyo ya tukio inayotajwa mimi nilikuwa nyumbani na siku nzima sikutoka kwenda popote, hata hiyo Mbezi iliyotajwa mimi siielewi kabisa, hata lile gari mimi sina gari la aina hiyo wala sijawahi hata kulipanda gari hilo na huyo Young Dee nina muda mrefu sana sijaonana naye,”
“Usiku wa kuamkia leo nilimpigia mtangazaji mmoja ambaye aliirusha habari hiyo redioni, nikataka kujua ameipata wapi habari hiyo? Akanijibu kwamba amepata tetesi tu. Sasa kama ni tetesi kwa nini asichunguze kabla hajanichafulia jina?”
“Pia alisema kuna askari wa doria walitukamata, nikamtaka anipeleke hicho kituo cha polisi tulikopelekwa ili tuthibitishe kama ni kweli maana ishu hii inanichafua mimi na familia yangu, akashindwa kufanya hivyo.
“Yaani naomba ieleweke kuwa sijafumaniwa na siwezi kufumaniwa na mtu kama Young Dee maana  kwanza hata sijawahi kukutana naye hivi karibuni, sipendi kuchafuliwa na haya yote namuachia Mungu atawajibu wote wanaonizushia,” alisema Lulu

PRESIDENT JAKAYA KIKWETE'S SPEECH AT MANDELA FUNERAL SHAMED KENYATTA REGIME

0
0

Tanzania’s President Jakaya Murisho Kikwete was accorded a stunning ovation in his tribute to the late Nelson Mandela.


President Kikwete’s speech made shame of Jomo Kenyatta regime that failed to help ANC set base in Kenya. Kikwete highlighted the support given by Mwalimu Julius Nyerere to the struggle against apartheid in South Africa.

Kikwete named TANU, ANC, ZANU PF, FRELIMO and SWAPO as comrades, KANU was left OUT!

“Tanzania under Julius Nyerere helped Black people struggle for emancipation in SA. Kenya under Jomo Kenyatta helped Boers/Whites to oppress and subjugate Black people in SA. Today, Jakaya Kiwete was global platform to pay tribute to global icon” George Nyongesa posted in his Facebook Page.

Here is president Kikwete’s full speech.

PICHA ZA JAMAA ALIYEFANANA NA MAREHEMU ALBERT MANGWEA

0
0

Kijana Aliye Fanana na Marehemu mwanamuzi Ngwea Akiwa katika ofisi za Clouds Fm...
Ametisha ...Dahh utafikiria ni Mapacha...au Sio Jamani?

VIDEO MPYA YA ROSE MUHANDO "WOLOLO" CHINI YA SONY MUSIC AFRICA COMPANY

0
0
Muimbaji wa muziki wa injili nchini Rose Muhando hatimaye amevunja ukimya kwa kuachia video chini ya label ya kimataifa inayomsimamia kwa sasa Sony Music Africa.




Hivi karibuni Bongo5 ilizungumza na Mkuu Wa Vipaji na Biashara Mpya wa Rockstar 4000 / Sony Music Africa, Seven Mosha, ambaye aliahidi kuwa kazi mpya za Rose zitaanza kutoka mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni tarkribani miaka miwili toka muimbaji huyo asaini ‘record deal’ na label hiyo ya kimataifa.

Video ya Rose Muhando ‘Wololo’ pia imekuwa certified na mtandao wa video za muziki wa Marekani VEVO. Video hii imepandishwa youtube December 13 kupitia channel ya RoseMuhandoVEVO.



KIGOMA ALL STARS WAPIGA SHOW KALI MOMBASA-RECHO ATIA AIBU, MAUNDA ZORO AZOMEWA

0
0
Wiki iliyopita, wanamuziki wa Kigoma Allstars akiwemo Diamond Platnumz na wengine walikuwa mjini Mombasa, Kenya kwenye show ya sehemu ya ziara yao katika nchini za Afrika Mashariki. Pamoja na kupiga show kali,  kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, Recho aliwatia aibu kubwa wasanii wenzie wakati wakiongea na waandishi wa habari baada ya show.

"Mwanamuziki wa Tanzania aliwashangaza waandishi wa habari pale alipoongea mbele ya camera kuwa alihitaji kuridhishwa kimapenzi,"mtandao wa Standard Digital News, SDE umeandika.

"Recho, aliyekuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya show mjini Mombasa, alisema alihitaji mwanaume wa kulala naye usiku huo. Akifedheheshwa kwamba hitaji lake halikufaniwa, muimbaji huyo maarufu kwa wimbo wake Upepo, aliwaponda waandishi na watu wengine waliokuwepo pale kuwa hawakuweza kum’handle’ mwanamke,"uliandika.

Mtandao huo uliongeza: Recho hakuwa msanii pekee aliyefedheheshwa usiku huo kwani mwenzake Maunda alionekana backstage akilia baada ya kuzomewa atoke jukwaani na umati.

Habari hiyo kwenye mtandao huo imeandikwa:

Recho begs for sexual satisfaction
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/entertainment/thenairobian/article/3325/tanzanian-superstar-begs-for-sexual-satisfactionRecho begs for sexual satisfaction
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/entertainment/thenairobian/article/3325/tanzanian-superstar-begs-for-sexual-satisfaction
Recho begs for sexual satisfaction

Tanzanian musician shocked journalists when she screamed to the cameras that she needed to be ‘sexually satisfied’. Recho, who was talking to reporters after the Kigoma All-stars concert in Mombasa, said that she wanted a man to ‘end the night with.’

Disappointed that her wish did not come true, the musician, famous for her song Upepo, told reporters and anyone who cared to listen that they ‘couldn’t handle a woman’.

Recho was not the only disappointed musician that night as her Tanzanian counterpart Maunda was spotted backstage crying after being booed offstage by the crowd.

BILIONEA DAR AJIUA KWA RISASI NDANI YA GARI LAKE

0
0
Stori: Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’
NI jambo lililotoa mshtuko kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani ambapo Desemba 10, mwaka huu, walikuta mwili wa binadamu ukiwa ndani ya gari lililopinduka, pembeni mwa Barabara ya Kisarawe - Mwaneromango.
Mbali na mwili, ndani ya gari hilo aina ya Toyota RAV 4 (milango mitatu new model) lenye namba za usajili T 273 AKP kulikutwa bastola moja, risasi 85 na magazini mbili.
Utata ukaanzia hapo, polisi wa wilaya hiyo wakiongozwa na mkuu wao (aliomba jina lisitiriwe kwa sababu si msemaji) wakajiuliza ni nani mtu huyo ambaye alikuwa amefariki dunia? Kumbe alikuwa Suleiman Muhema (42), bilionea kijana mkazi wa jijini Dar es Salaam.
polisi waliuchukua mwili wake na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Wilaya mpaka ndugu walipokwenda kuuchukua kwa mazishi.
SULEIMAN MUHEMA NI NANI?
Suleiman Muhema ni mkazi wa jijini Dar, amejenga jumba la kifahari Kijitonyama ambako aliishi na mke wake, Zihji Mvungi (42).
Mpaka kifo chake alikuwa mfanyabiashara wa magari kutoka Japan akiyauza Dar, pia alikuwa na kampuni ya usafirishaji, sifa zote kwa pamoja zinamfanya aitwe bilionea.
MAISHA SIKU CHACHE KABLA YA KIFO
Habari zinadai kuwa, marehemu alikuwa ndani ya mgogoro wa kifedha na mtu ambaye hakutajwa jina lakini ni wa karibu naye.
Inadaiwa kuwa, mgogoro huo ni wa muda mrefu na ulikuwa ukisuluhishwa na Dawati la Jinsia, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar.
SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio inadaiwa marehemu alikuwa Magomeni na watu (idadi yao haikujulikana). Baada ya hapo aliondoka  kwenda kusikojulikana lakini baadaye alimpigia  simu ndugu wa karibu na kumwambia kuwa yuko mahali (hakupataja) ametekwa na sauti anayoitoa inaweza kuwa ya mwisho kisha akakata simu.
MAELEZO YA POLISI SASA
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Kisarawe, Desemba 10, mwaka huu,  usiku wa saa nane,  marehemu alionekana akiwa ndani ya gari jeusi umbali wa kilomita saba kutoka Kisarawe Mjini lakini aliondoka baada ya kuliona gari la ‘patroo’ ya polisi.
Chanzo hicho kikasema kuwa dakika chache mbele polisi waliokuwa katika shughuli za ulinzi usiku huo waliliona gari hilo likienda pembezoni mwa barabara na kupinduka.
“Tulilifuatilia, tukalikuta limepinduka, ndani ya gari tulimkuta mtu amekufa kwa kujipiga risasi kwani sehemu ya kidevuni na kwenye utosi kulikuwa na tundu la risasi,” kilisema chanzo hicho.
MAREHEMU ALIDHANIWA MHALIFU
Habari zinasema katika upekuzi wa awali ambapo polisi walimkuta marehemu akiwa na bastola, risasi 85 na  magazini mbili walidhani alikuwa mhalifu aliyetaka kutekeleza uhalifu mahali ndani ya walaya hiyo.
NDUGU WA MAREHEMU WANA NENO
Kwa upande wao ndugu wa marehemu ambao waliomba majina yao yawekwe pembeni, walisema kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu kifo cha ndugu yao huyo kwa sababu hata kifo chake hawakielewielewi.
Akizungumza kwa hisia ya uchungu, ndugu mmoja alisema katika maisha ya jijini Dar, yeye ndiye baba wa marehemu lakini hakuna alichojua toka kifo hadi kuzikwa.
Alisema hata mazishi ya marehemu alishtukizwa  kwamba anazikwa siku hiyo jambo lililompa wakati mgumu kufikiria.
 “Sisi kama ndugu wa marehemu, tulipenda akazikwe nyumbani, Makete   (Njombe), lakini ghafla tukaambiwa anazikwa hapahapa Dar tena siku hiyohiyo tuliyopewa taarifa,” alisema ndugu huyo.
MKE WA MAREHEMU NAYE
Kwa upande wake mke wa marehemu Zihji alipoulizwa na mapaparazi wetu juzi kuhusu sakata la kifo cha mumewe alijibu kuwa kila mtu anaweza kuongea jambo lolote.
Aliongeza kusema anachojua yeye ni kwamba kifo cha mumewe kilitokea kama ambavyo mtu mwingine angeweza kufa.
KAMANDA WA POLISI ANASEMAJE?
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, ACP Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu alikutwa akiwa na jeraha la risasi moja hali ambayo ilionesha alijipiga risasi mwenyewe pengine kutokana na mambo yaliyokuwa yakimsonga kichwani.
BILIONEA AZIKWA DAR
Marehemu Muhema alizikwa Desemba 11, mwaka huu kwenye Makaburi ya Sinza jijini Dar. Ameacha mke na watoto watatu wa kike. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.
MASWALI TATA
Kifo cha Muhema kina maswali tata mengi. Kwanza, kama kweli alipanga kujiua kwanini alikwenda mbali na Jiji la Dar es Salaam?
Pili, kwa nini damu ndani ya gari ilikuwa kidogo wakati uzoefu unaonesha kuwa, mtu anayepigwa risasi ndani ya gari huacha damu nyingi?
Tatu, ndugu mmoja wa marehemu alikiri kuwa, Muhema alinunua bastola mwaka huu ili kujilinda, sawa kabisa. Je, kwa nini akutwe na risasi nyingi kiasi hicho kama alikuwa anakwenda kufanya uhalifu?
Nne, ilidaiwa alimpigia simu ndugu mmoja akidai ametekwa na huenda asisikike tena. Polisi walikuta simu kwenye gari lake, kwa nini waseme alijipiga risasi mwenyewe?
GLOBAL PUBLISHERS

LEMA AMLIPUA BUNGENI NAIBU WAZIRI OLE MADEYE

0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemlipua bungeni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye kwa kumweleza kuwa sio mzigo tu, bali ni bomu hasa. Katika mchango wake kuhusu taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji wa shughuli zake kwa kuanzia Machi hadi Desemba 2013, Lema alimtuhumu Medeye kwa kuchochea ukabila mkoani Arusha.

“Taifa letu lipo katika mkanganyiko sana, chokochoko za udini na ukabila zinaletwa na wanasiasa wanapotafuta utawala…nashangaa kuona Ole Medeye aliwahi kushiriki mkutano wa ukabila uliokuwa na lengo la kuwatenga wakazi wa Arusha ambao sio wa kabila lake, ninayo DVD ya Medeye akitaka wenyeji wasiwauzie mashamba na mambo mengine wageni toka mikoa mingine.

Julai mwaka jana, viongozi  wa kimila wa kabila la Wamasai walitoa tamko wakiwataka wageni, wakazi na washirika wote kwa ujumla wao katika jiji la Arusha waonyeshe ushirikiano na kuwasaidia Malaigwanani kulinda na kuendeleza umoja, upendo, mshikamano, amani na siyo kuwa chanzo cha matatizo kwani hawatakubali kabisa.

Kabla ya tamko lao, baadhi ya viongozi hao walikuwa wakizungumzia mustakabali wa maisha ya Arusha mjini huku wakiwataka wageni (watu ambao sio Wamasai) kuacha kuleta vurugu katika eneo la Wamasai.

Akizungumzia kuhusu mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasiti jijini Arusha, Lema alisema wapo watu katika serikali wanafanyakazi karibu na shetani.

Alishangaa kuona tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika mkutano wa Chadema wa kuhitimisha kampeni ya uchaguzi wa madiwani jijini humo halijaelezwa katika taarifa ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama.

“Tuna ushahidi wa video nani aliyerusha bomu Soweto na tukataka iundwe kamati huru na sisi tutoe ushahidi wetu lakini hakuna lolote lililotokea hadi sasa,” alisema na kuongeza, “tunashangaa wanaotueleza tulijilipua wenyewe bomu.”

Pia Lema alipinga mapendekezo ya Kamati hiyo kuitaka Serikali kupitia upya sheria zake ili hatimaye iandae muswada wa sheria itakayoweka utaratibu mahususi wa watu kuandamana utakaozingatia siku, muda na mahali ili kumwezesha mwananchi atumie haki yake ya kuandamana bila ya kuingilia uhuru wa mtu mwingine.
CHANZO: NIPASHE
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images