Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Viongozi Wapya wa Bodi ya Ligi Kuu Kupatikana Leo

$
0
0
Viongozi Wapya wa Bodi ya Ligi Kuu Kupatikana Leo
Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), leo inatarajiwa kupata viongozi wapya kufuatia uchaguzi mkuu utakaofanyika leo Oktoba 15 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salam.

Jumla ya wajumbe 44 wanashiriki Mkutano huo wa uchaguzi wa Baraza Kuu la TPLB. Wajumbe hao ni klabu 16 za Ligi Kuu, klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na wawakilishi wanne wa klabu za Ligi Daraja la Pili.
Wanaowania nafasi ya Mwenyekiti wa TPLB ni Clement Andrew Sanga kutoka Yanga na Hamad Yahya Juma wa Mtibwa Sugar. Nafasi ya makamu mwenyekiti inawaniwa na Shani Christoms Mligo wa Azam FC.
Nafasi tatu za kuwakilisha klabu za Ligi Kuu kwenye Kamati ya Uongozi zinawaniwa na wagombea wawili ambao ni Hamisi Mshuda Madaki (Kagera Sugar) na Ramadhani Marco Mahano (Lipuli).
Almasi Jumapili Kasongo kutoka Ashanti United FC amejitokeza kuwania nafasi ya uwakilishi wa klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Wakati Edgar William Chibura kutoka Abajalo FC anawania nafasi ya uwakilishi ya klabu za Ligi Daraja la Pili kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB.

"Hatua za Kuwabana Mafisadi Wapo Watanzania Wasio na Hatia Wanaoathirika Kinachotakiwa Uvumilivu Yatapita" Tu- Rais Magufli

$
0
0
"Hatua za Kuwabana Mafisadi Wapo Watanzania Wasio na Hatia Wanaoathirika Kinachotakiwa Uvumilivu Yatapita" Tu- Rais Magufl
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka watanzania kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho nchi inajitahidi kujikwamua kiuchumi.

Rais magufuli ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, zilizofanyika katika uwanja wa Amani Zanzibar.
Kwenye hotuba hiyo Rais Magufuli amesema nchi yoyote inyopitia mabadiliko ya kiuchumi, ni kawaida kupitia kwenye wakati mgumu hivyo watanzania ni vyema wakawa na uvumilivu na subira, ili kuingoja neema itakayokuja.
"Licha ya ukweli kutokana na hatua tunazozichukua za kuwabana mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma, wapo wananchi wa kawaida ambao si wezi wala mafisadi wanaoathirika, hili ninalifahamu, lakini kama kweli tunataka kupambana na wizi na ubadhirifu pamoja na kuleta maendeleo kwa nchi yetu, athari hizi hatuwezi kuzikwepa, mabadiliko ya aina yoyote ile lazima yana athari kama hizi, lakini jambo la kututia moyo ni kwamba athari hizi mara nyingi ni za kipinzdi kifupi", amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameendelea kwa kusema kwamba ..."Mabadiliko ni magumu mwanzoni, yatakuwa machungu yanapofikia katikati, lakini mwishoni matokeo yake ni mazuri au ni matamu, hivyo nawaomba wananchi na watanzania tuvumile katika kipindi hichi cha mpito, baada ya muda mfupi mambo yatakuwa mazuri, lakini hata kama hayatakuwa mazuri hivi karibuni, watoto na wajukuu zetu watanufaika, na huo ndio uzalendo".
Pamoja na hayo Rais Magufuli amesitiza kwamba uchumi wa nchi unaendelea kukua, na kwamba wanaosema hivyo ni waongo na wazushi, na kuwataka watanzania wawapuuze.

Nkamia Kufunguka Juu ya Hoja Yake ya Kuongoza Muda wa Rais

$
0
0
Nkamia Kufunguka Juu ya Hoja Yake ya Kuongoza Muda wa Uras
Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia amesema ataweka wazi taarifa za hoja yake binafsi ya kutaka muda wa Rais kukaa madarakani uongezwe kwa miaka miwili zaidi.

Kwa sasa Rais anachaguliwa kuongoza nchi kwa miaka mitano, lakini Nkamia anataka uongozwe kuwa miaka saba.

Tayari mbunge huyo alishawasilisha kwa katibu wa Bunge barua ya kutaarifu kuhusu mpango huo ambao iwapo utapita, utaandaliwa muswada wa mabadiliko ya 15 ya Katiba ili uchaguzi uwe unafanyika kila baada ya miaka saba.

Nkamia alisema jana kuwa kesho ataweka hadharani taarifa yake kuhusiana na minong’ono inayoendelea nchini kuwa ameondoa hoja yake.

“Nitazungumza na waandishi wa habari Jumatatu nitaeleza ukweli,” alisema Nkamia alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na uvumi huo wa kuondoa hoja yake.

Miongoni mwa maelezo ya sababu za kutaka marekebisho hayo ni gharama za kuendesha uchaguzi kwa wakati mmoja, yaani Uchaguzi Mkuu na wa serikali za mitaa.

Nkamia alisema hoja yake haimaanishi kuwa Rais aliye madarakani ndiye aanze kwenda miaka saba, bali ni kwa viongozi wote na kama wazo lake likitimia wakati Rais John Magufuli akiwa madarakani nayo si vibaya.

Awali Nkamia alieleza gazeti hili kuwa ataipeleka hoja hiyo katika mkutano wa Bunge wa mwezi Novemba na kwamba anategemewa kuanza maandalizi ya hatua hiyo katika vikao vya kamati za Bunge vilivyofanyika mjini Dodoma.

Lakini hoja hiyo imepingwa na spika wa zamani, Pius Msekwa ambaye alisema wazo hilo lilishajadiliwa na CCM na kuona madhara yake.

Mwanasiasa huyo mkongwe alisema tayari anaona kuna tafakari nyingi zilizofanywa kabla ya Taifa kuamua kipindi cha utawala kuwa miaka mitano na si vinginevyo.

Msekwa alisema hoja hiyo inabidi iangaliwe kwa umakini mkubwa kutokana na ukweli kuwa, iwapo kiongozi atakuwa mbaya, maisha yanaweza kuwa ya mateso kwa wananchi katika kipindi cha miaka saba na kuongeza kuwa hata Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere aliliona hilo.

“Ni kwamba miaka kumi tu inatosha, ili kama mtu ni mbaya tuvumilie kwa hiyo miaka kumi na siyo kwamba haikufikiriwa. Na sidhani kama CCM itakuwa na nafasi ya kujadili hilo kwa sasa,” alisema Msekwa.

Lazima Tuondoke na Ushindi Kutoka kwa Mtibwa Leo- Omog

$
0
0
Lazima Tuondoke na Ushindi Kutoka kwa Mtibwa Leo- Omog
Kocha wa Simba, Joseph Omog amesema anaifahamu vyema Mtibwa Sugar kuwa ni timu nzuri na ina wachezaji bora hivyo haitakuwa mechi rahisi kushinda, lakini lazima waondoke na ushindi leo.

Mechi hiyo inawakutanisha Simba na Mtibwa kwenye uwanja wa uhuru ikiwa ni siku moja baada ya mechi ya watani zao Yanga walioibuka na ushindi jana Jumamosi.

Matokeo ya Yanga ya mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar yanawapa presha Simba kucheza kufa na kupona ili kuibuka na pointi tatu zinazoweza kuwarejesha kileleni mwa msimano wa Ligi Kuu leo.

Calisah: Nipo Tayari Kufanya Chochote kwa Aajili ya Pesa Ila Haitobadilisha Uanaume Wangu

$
0
0
Calisah: Nipo Tayari Kufanya Chochote kwa Aajili ya Pesa Ila Haitobadilisha Uanaume Wangu
Mwanamitindo wa kiume Bongo anayejulikana kwa jina la Calisah, amesema pamoja na kwamba yuko tayari kufanya chochote kwa ajili ya pesa, lakini hatkuna kiwango cha pesa kitakachoweza nunua uanaume wake.

Calisah ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television, na kusema kwamba hatothubutu na hawezi kuruhusu pesa ibadilishe utu wake, na kupoteza sifa yake ya kuwa mwanaume.
"Ni suala baya kwa mwanaume kuvaa kitu cha kike, unajua Tanzania bado tuko nyuma kwenye vitu vingi sana, kwenye muziki, kwenye movie bado tuko nyuma, sasa inabidi watokee watu wawe wanapiga step kwenye kutambulisha kitu kipya ili tuendelee kukua, nitavaa bikini, nitavaa gauni, kitu ambacho sitafanya, hakuna kiaasi cha pesa ambacho kinaweza kikabadilisha uanaume wangu kuwa kitu kingine, chochote kitakachonitofautisha kuwa mwanaume, yaani nisiwe na sifa za mwanaume, sitafanya kamwe kwa pesa yoyote ile", amesema Calisah.
Hivi karibuni Calisah alikumwa na kashfa ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, baada ya kuonekana kwa picha zake akiwa amevaa viatu vya kike.

Sababu, Dalili na Tiba ya Tatizo la Nguvu za Kiume Pamoja na Maumbile Madogo ya Uume..Soma Hapa

$
0
0

SABABU, DALILI NA TIBA YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME  PAMOJA NA MAUMBILE MADOGO YA UUME? SOMA HAPA


       Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume husababishwa na mambo mengi kama KISUKARI, UNENE ULIOPITILIZA, KUJICHUA  (MASTER BLASHION), HOMONI kushindwa kufanya kazi ipasavyo n.k.
     Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.
      BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.
     Kwa kutumia mimea na matunda @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6 hadi 7  @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 7  hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130,000/=
      BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA ZIMETHIBITISHWA KIAFYA.


Wasiliana nasi (+255)
           0767447444 na
              0714335378

        UTAPATA HUDUMA
NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

Rais Magufuli Amehudhuria Misa Kanisa Katoriki Jimbo la Zanzibar Askofu Atoa Neno Juu ya Utendaji Wake

$
0
0
Rais Magufuli Amehudhuria Misa  Kanisa Katoriki Jimbo la Zanzibar Askofu Atoa Neno Juu ya Utendaji Wake
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Agustino Shao amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa hatua anazochukua za kurekebisha mambo muhimu kwa maendeleo ya Taifa, licha ya kuwepo changamoto katika kipindi cha mpito.

Ametoa ushauri huo leo Jumapili akihubiri wakati wa misa iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Minaramiwili ambayo imehudhuriwa na Rais Magufuli.

Askofu Shao amesema hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli za kupambana na rushwa, kupigania rasilimali za Watanzania, kuimarisha nidhamu na uwajibikaji, kukabiliana na wizi na ubadhilifu wa mali za umma na kubana matumizi zinapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote.

“Hatutaweza kusema tunaimaliza rushwa wakati tunaendelea kuishi kwa kupata fedha ambazo hujazifanyia kazi, ni lazima tuishi machungu ya kuimaliza rushwa, ni lazima tuishi machungu ya kuweka uadilifu katika utendaji wetu, tusipoishi machungu hayo tutaishi dunia mbili, dunia ya rushwa na dunia ya kujenga uchumi na uadilifu wa Watanzania,” amesema.

Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari imesema baada ya misa kumalizika Rais Magufuli amemshukuru Askofu Shao kwa mahubiri.

Amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali inachukua hatua za kupambana na rushwa na kulinda rasilimali za nchi ili ziweze kuwanufaisha wananchi.

Rais Magufuli amesema Baba wa Taifa, Julius Nyerere ambaye jana Jumamosi iliadhimishwa miaka 18 tangu kifo chake alipiga vita rushwa na alipigania rasilimali za nchi, hivyo ametaka Watanzania wote kuungana katika juhudi hizo.

Dk Magufuli amechangia Sh1 milioni kwa ajili ya kwaya ya kanisa hilo na Sh5 milioni  kwa ajili ya maendeleo ya kanisa.

Mrisho Gambo Amshusha 'Presha' Lema

$
0
0
Mrisho Gambo Amshusha 'Presha' Lema
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amemtoa wasi wasi mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema, juu ya hofu ambayo amehisi anayo, kwamba anatengeneza mazingira ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkoani Arusha, Mrisho Gambo amesema hofu anayopata Lema juu yake hapaswi kuwa nayo, kwani hana mpango wa kugombea nafasi hiyo, isipokuwa yeye anatekeleza majukumu yake kama mkuu wa mkoa kwa wananchi wake, huku akimtaka Godbless Lema kutekeleza majukumu yake kwa wananchi, na sio kuleta porojo ambazo wananchi hawazihitaji kwa sasa.
“Godbles Lema, akipita kwenye ziara zake nyingi badala ya kuzungumza maendeleo ya watu wetu, anazungumza kwamba mkuu wa mkoa msione anafanya hivi, kwa sababu anataka ubunge, mi nikisikia hivyo najua ana hofu, amejipima pima akaona pengine kivuli changu kinamtisha, mwambieni aache uoga, mi ni mkuu wa mkoa ambaye halmashauri zote, wabunge wote wapo chini yangu, sijawahi kuwa na wazo tofauti na kazi hii ninayofanya sasa, mwambie tu ahangaike na shida za watu asinihofie mimi”, amesema Mrisho Gambo.
Mrisho Gambo ameendelea kwa kushauri watu wa namna hoyo waache ujanja ujanja, kwani wananchi sasa hivi hawataki usanii.

Mwiguru Nchemba: Wizara Yangu Itahakikisha Itbadirisha Sheria ya Kuwabana Wahamiaji Haramu

$
0
0
Mwiguru Nchemba: Wizara Yangu Itahakikisha Itbadirisha  Sheria ya Kuwabana Wahamiaji Haramu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema wizara yake itahakikisha inawabana ipasavyo wahamiaji haramu pamoja na kubadilisha sheria ili ziwabane zaidi.

Waziri Mwigulu ameyasema hayo alipotembelea Gereza la Kigongoni wilayani Bagamoyo na kugundua robo tatu ya wafungwa ni wahamiaji kutoka nchi jirani ikiwemo Ethiopia.
Taarifa ya Mkuu wa magereza Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, SACP Boyd Mwambingu imebainisha kuwa wafungwa ambao ni raia wa Ethiopia waliofungwa katika Magereza ya Mkoa huo ni 334, Mahabusu 12 na wanaosubiri kusafirishwa ni 91 ambao jumla ya raia kutoka Etheopia ni 437 wa Malawi ni 1 Msomali ni 1 wa DRC ni 1 wa Burundi 2 na Kenya ni 2.
Kufuatia taarifa hiyo Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesema haiwezekani wahamiaji haramu wagharamikiwe na taifa ikiwemo kusafirishwa kwa gharama za serikali pamoja na kupatiwa Chakula na Matibabu.

“Tutafanyia kazi ili sheria iseme kama watakamatwa watafungwa au mambo mawili, nchi yao iwachukue au warudi kwa gharama zao wenyewe lakini sheria lazima iwe kali itakayotoa fundisho kwa wengine”, amesema Mwigulu.

Wanachama wa CCM Wampinga Polepole Sakata la Ubunge, Madiwani

$
0
0
Wanachama wa CCM Wampinga Polepole Sakata la  Ubunge, Madiwani
Wakati katibu wa oganaizesheni wa CCM, Pereira Silima akikanusha kupitishwa kwa sharti la ukazi kwa wagombea udiwani na ubunge, chama hicho kimewataka watumishi wa umma walioshinda uchaguzi katika ngazi ya wilaya kuamua moja; ajira au siasa.
Juzi, katibu wa uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema katika kipindi cha redio cha Times FM kuwa wanaogombea udiwani na ubunge mwaka 2020 watatakiwa kuwa wakazi wa maeneo wanayogombea, lakini mara moja akapata maswali kutoka kwa wanachama.
Lakini jana, Silima alisema CCM haiwezi kuweka sharti hilo kwa kuwa linakiuka Ibara ya 67 (1 a-c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inaeleza sifa za mtu ambaye hatakuwa na sifa za kugombea, hali kadhalika Sheria za Uchaguzi.
“Nikiwa katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa mwenye dhamana ya uchaguzi, napenda kuwajulisha kwamba Chama cha Mapinduzi kimefanya mabadiliko katika katiba yake,” anasema Silima.
“Mabadiliko ambayo yamepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliofanyika 12/03/2017, pamoja na kanuni za uchaguzi wa chama na hakuna mahali popote palipoandikwa kuwa wagombea wa udiwani na ubunge watajadiliwa kwa sifa ya kuishi jimboni.”
Silima amewataka wanachama kuzipuuza habari hizo.
Katika hatua nyingine, makamu mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula amewataka watumishi waliogombea na kushinda nafasi za uenyekiti na ujumbe wa wilaya, kuchagua moja; ajira au uongozi.
Katika toleo la juzi la Uhuru, gazeti la chama hicho tawala, Mangula amekaririwa akisema CCM itawashughulikia watendaji wake pamoja na watu ambao walikiuka maelekezo ya waraka unaozuia watendaji wa Serikali kuwania uongozi ndani ya chama.
Mangula alisema baadhi ya wilaya na mikoa ilikiuka kwa makusudi waraka huo kwa kutoa tafsiri potofu kama vile kueleza nafasi zilizozuiwa ni za utendaji, jambo ambalo alidai si kweli.
Mangula amekaririwa akisema waraka huo umeeleza bayana kwamba watumishi wa Serikali hawaruhusiwi kuwania uongozi ndani ya chama. Alisema katika hali ya kushangaza, baadhi ya watendaji kwa kushirikiana na wajumbe wengine wa vikao vya uteuzi, wamewapitisha na wengine wameshinda nafasi mbalimbali.
Alisema CCM inaliona hilo kama tukio la uvunjaji wa kanuni za maadili ya uongozi na hivyo inawataka wahusika kuanza kuwajibika kabla ya kusubiri uamuzi wa vikao vya juu.
Mangula alisema chama kinaweza kuchukua uamuzi wa kufuta matokeo ya uchaguzi katika baadhi ya wilaya kitakapojiridhisha kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni kwa kuwa suala la rushwa ni kinyume na maadili ya viongozi wa CCM.
Watumishi wa umma walioshinda
Wanachama waliotangazwa kushinda ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM ni wakuu wa mikoa ya Mtwara, Halima Dendego na Morogoro, Dk Kebwe Stephen.
Wakuu wa wilaya waliogombea uongozi ndani ya CCM na kushinda ni Simon Odunga (Chemba), Christina Mndeme (Dodoma) na Elizabeth Kitundu (Bai) mkoani Dodoma.
Mkoani Morogoro, wakuu wa wilaya waliogombea na kushinda ni Alhaji Mohamed Utaly (Mvomero) na Seriel Nchembe (Gairo).
Wakuu wa wilaya wengine walioshinda ni Raymond Mushi (Babati, Manyara), Herman Kapufi (Geita), Kaul Kiteleki (katibu tarafa wa Makuyuni, Arusha), Alexander Mnyeti (mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Arusha), Salum Palango (katibu tawala wa Nanyumbu, ambaye alishinda ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM.
Wengine ni Salvatory Richard (mtumishi Idara ya Elimu, Mvomero) na dereva wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Wengine walioshinda nafasi ya ujumbe ni Elishilia Kaaya ambaye ni mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) na Dk Daniel Mrisho.
Katika hatua nyingine, CCM mkoani Morogoro imesema inasubiri maelekezo ya uongozi wa Taifa kuwafyeka watumishi wa umma walioshiriki uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.
Katibu wa mkoa, Kulwa Milonge amesema chama hicho hakitasita kuwachukulia hatua wanachama wake ambao ni watumishi wa umma waliochaguliwa katika nafasi za uongozi ndani ya chama iwapo wataelekezwa kufanya hivyo na uongozi wa Taifa wa CCM

Watu 40 Wauawa Kwenye Moto wa Nyika California

$
0
0
Watu 40 Wauawa Kwenye Moto wa Nyika California
Watu 40 wameuwa na mamia ya wengine hawajulikani waliko baada ya siku sita za moto wa nyika ambao umeharibu maeneo makubwa ya ardhi katika jimbo la California nchini Marekani.
Gavana wa California anasema kuwa ni moja ya majanga makubwa zaidi jimbo hilo halijawahi kushuhudia.
Prisoners at Oak Glen Conservation Camp leave for work deployment under the authority of Cal Fire on September 28, 2017Haki miliki ya pichaAFP
Upepo unaovuma kwa kasi ya hadi kilomita 70 ulisababisha moto huo kusambaa zaidi na kulazimu watu zaidi kuhama.
Moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni mji wa Santa Rosa ambapo hadi watu 3000 walihamishwa siku ya Jumamosi.
Moto mkubwa wasababisha maafa Marekani
"Uharibifu ni mkubwa," Gavana Jerry Brown alisema alipofaya ziara katika mji huo.

Huo ndio moto mbaya zaidi katika historia ya jimbo hilo. Zaidi ya watu 100,000 wamehamishwa na vijiji vingi vimegeuka majivu
Moto huo mkubwa umesababisha moshi na majivu hadi anga ya San Francisco, karibu umbali wa maili 50, na hata kwenda miji ya mbali kusini.
Kikosi cha Watu 10,000 chapambana na moto California
Katika bonde na Naqa takriban viwanda 13 vya mvinyo vimeharibiwa. .Mmiliki mmoja wa kiwanda cha mvinyo huko Santa Rosa anasema moto huo umeharibu mviyo wa mamilioni ya dola.

Flynt Atangaza Zawadi ya Dola Milioni 10 Kumuondoa Trump Madarakani

$
0
0
Flynt Atangaza Zawadi ya Dola Milioni 10 Kumuondoa Trump Madarakani
Mchapishaji wa jarida la picha chafu za utundu, Larry Flynt, amechapisha tangazo katika gazeti la Washington Post, akiahidi kulipa zawadi ya dola milioni 10, kwa mtu mwenye habari, zitazopelekea Rais Trump kushtakiwa na kuondoshwa madarakani.
Bwana Flynt, anayemiliki jarida la "Hustler", amesema ni wajibu wa kila Mmarekani, kumuondoa Bwana Trump, kabla ya kuchelewa.
Mwanzilishi wa Playboy aaga dunia
Roboti inayoweza kushiriki ngono kutengezwa
Utafiti: Kerengende wa kike ''hujiuwa'' ili kukwepa tendo la ngono
Tangazo hilo, linatoa nambari ya simu ya kupiga na anuani ya barua pepe.
Larry Flynt, ambaye alikuwa mfuasi mkubwa wa Hillary Clinton katika kuania urais, ametoa matangazo kama hayo kabla, lakini hakuwahi kutoa zawadi kubwa kama hiyo.

Federer na Sharapova Watisha Kwenye Tennis

$
0
0
Federer na Sharapova Watisha Kwenye Tennis
Bingwa wa Wimbledon Roger Federer ametwaa ubingwa wa Shanghai Masters baada ya kumfunga mchezaji namba moja duniani kwa ubora Rafael Nadal seti 6-4 6-3 katika fainali iliyomalizika mchana huu.

Federer raia wa Uswis ametwaa taji lake la sita ndani ya mwaka 2017, akiwa ndiye mchezaji pekee aliyemshinda Nadal mara nne ndani ya mwaka huu.
Mswis huyo mwenye umri wa miaka 36, alikuwa kwenye kiwango kizuri leo baada ya kumlaza Nadal kwa muda wa dakika 72 pekee.
Federer sasa ndio mchezaji pekee ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Nadal kama mchezaji namba moja duniani mwishoni mwa mwaka huu, lakini michuano ya ATP kwenye uwanja wa London 02 mwezi ujao ndio itaamua.

Kwa upande wa wanawake Maria Sharapova ameshinda taji la kwanza tangu Mei 2015, baada ya kumpiga Aryna Sabalenka 7-5 7-6 10-8 katika fainali ya Wazi ya Tianjin mchana wa leo

Kutana na The Great Maalim Hussein Aweze Kutatua Matatizo yako Kwa Tiba za Asili, Dua na Nyota..

$
0
0
THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.
Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..

Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107

Ule Umati Mlimani City Dada Anatunyoosha Nyumbani Kwetu- Lulu

$
0
0
Ule Umati Mlimani City Dada AAnatunyoosha Nyumbani Kwetu- Lulu
Ule msemo wa nabii hakubaliki kwao! Umeweza kujidhihirisha kwa mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, na mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ambaye juzi alitua Bongo akitokea South Afrika na kupokelewa kwa nderemo na vifijo na umati mkubwa wa watu, ambapo umati huo ukajitokeza tena  jana katika ukumbi wa Mlimani City, alipotinga kwa ajili ya kuzindua kampuni ya DANUBE,  hali hiyo ya kupokelewa mithili ya Mfalme, imemshtua Diva kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ Ambaye amempigia saluti Zari na kusema  mastaa wa Bongo hawana budi kumpenda tu, kwani licha ya kuwa siyo Mbongo ila ana mashabiki wengi Bongo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Lulu alipost picha ya Zari na kuambatanisha na maneno yanayoashiria kushangazwa na jinsi mwanamama huyo alivyopokelewa na Watanzania kama vile ni Mtanzania halisi.

Kama ilivyo kawaida ya mashabiki baada ya kuiona Post hiyo hawakumuacha salama Lulu, wakamporomoshea koment za kumchamba kuwa anajipendekeza kwa mtu ambaye hana shobo na mastaa wa Bongo.


Wanachama 113 Wajitosa Kuwania Nafasi ya Uenyekiti Taifa

$
0
0
Wanachama  113 Wajitosa Kuwania Nafasi ya Uenyekiti Taifa
Wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.

Kwa sasa nafasi hiyo inashikiliwa na Mbunge wa Donge Visiwani Zanzibar, Sadifa Juma Khamis ambaye alichaguliwa katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2012.

Akizungumza leo Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamidu amesemma  wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM linafanya usahili wagombea waliomba nafasi mbalimbali za uongozi.

Amesema  usahili huo unafanyika kwa waliomba kugombea wa nafasi za mwenyekiti, makamu, wajumbe watano wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC), wajumbe watano wa baraza kuu la umoja huo Taifa na wajumbe wa kuwakilisha jumuiya hiyo katika jumuiya nyingine za chama.

Amesema zoezi hilo ambalo limeanza tangu Aprili limefanikisha kupatikana kwa viongozi mbalimbali wa ngazi za shina hadi wilaya na kwamba kinachofanyika hivi sasa ni mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi za kitaifa.

“Vijana 113 wamejitokeza kuomba nafasi ya uenyekiti. Huu utakuwa ni uchaguzi wa kihistoria kati ya chaguzi zote zilizowahi kufanyika tangu mwaka 1978 ilipoanzishwa jumuiya hii mwaka huu. Kwa maneno mengine tumevunja rikodi,”amesema.

Amesema kwa upande wa nafasi ya umakamu mwenyekiti waliomba kugombea ni 23 wakati ujumbe wa Nec 118  wanachuana kugombea nafasi tano zilizopo kikatiba.

Shaka amesema jumla ya wagombea ambao wanawafanyiwa  usahili katika kikao cha Kamati ya Utekelezaji wa baraza la Kuu la UVCCM ni 375 huku nafasi ya uenyekiti Taifa ikiongoza kwa waombaji wengi katika zoezi hilo.

Kwa mujibu wa Shaka, Kamati ya utekelezaji ni kikao cha awali ambacho kitatoa mapendekezo kwa Baraza Kuu la Taifa la umoja huu ambalo litakutana kesho kutwa  kutwa (Oktoba 17) kwa ajili ya kupokea mapendekezo ya kamati hiyo.

“Baraza Kuu litakutana hapa hapa Dodoma kwa ajili ya kupokea na kupendekeza nafasi zilizoombwa katika mikoa na Taifa. Sisi (Baraza Kuu la umoja huo) tunapendekeza kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa,”amesema .

Kwa mujibu wa utaratibu CCM kikao kitakachowachuja wagombea wa nafasi zote ambazo zinauwakilishi wa chama taifa ni Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM inayoongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa Dk John Magufuli.

Akizungumzia kuhusu chaguzi zilizopita za mashina hadi wilaya, Shaka alisema kuwa mambo yamekwenda vizuri katika chaguzi zote.

Alijitapa kuwa chama chao siku zote kimekuwa kikisimamia haki na usawa ili vijana waweze kupata fursa kwa nafasi wanazoziomba katika chaguzi mbalimbali nchini.

“Katika ngazi wilaya kuna changamoto mbalimbali kwenye uchaguzi ambazo zimejitokeza lakini jumuiya hii inaongozwa na kanuni na katiba ya chama chetu kwa hiyo tumeagiza viongozi wetu kuhakikisha kuwa wanashughulikia malalamiko yaliyojitokeza,”amesema

Amesema  malalamiko yaliyojitokeza katika chaguzi hizo ni pamoja na hofu kuwa kuna wagombea wamezidisha umri na dhana ya kutumia rushwa.

Hata hivyo, alisema chama hicho kimekuwa kikikemea vitendo vya rushwa na hivyo itakapodhibitiki uvunjaji wa kanuni watachukua hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

“Hatutadharau malalamiko yoyote yake, yote yatashughulikiwa na atakeyabainika kuvunja kanuni hatua zitachukuliwa,”amesema

Mbunge wa Mbinga Mjini (CCM) ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda alisema kujitokeza kwa wingi wa watu kuwania nafasi hiyo inaonyesha kuwa uelewa wa watu katika siasa umeongezeka na pia ni kukuwa kwa demokrasia.

“Kwanza kumbuka unaongelea chama kikubwa chenye wanachama milioni nane hadi milioni 10, chenye mashina yasiyohesabika, katika hali ya kawaida kwenye structure (muundo) ya leadership  (uongozi) ya watu wengi namna hiyo lazima utapata watu wengi ambao watakuwa uwezo wa kuongoza na kutaka kuongoza,”amesema.

“Lakini kubwa zaidi ni fursa ambazo chama kimetengeneza, uwezo wa kila mmoja kuwa popote.”

Mchambuzi wa  Masuala ya Kisiasa, Profesa Benson Bana alisema hiyo ni dalili nzuri inayomaanisha CCM ina hazina ya viongozi, ina mvuto na watu wengi wanaofikiri kuwa wanauwezo wa kuongoza chama hicho.

“Hii ni dalili njema kwa chama. Ukitangaza nafasi watu wakapungua wakawa watatu inamaana lazima ujitathimini kama ni kiongozi wa chama kwamba inawezekana kimekosa mvuto lakini kama kweli watu wote wameomba uongozi wa nafasi moja ni jambo jema kwa chama na wanachama wake,”amesema.

Siri na Mipango ya Mauaji ya Bilioni Msuya Kujulikana Kesho

$
0
0
Siri na Mipango ya Mauaji ya Bilioni Msuya Kujulikana Kesho
Siri na mipango ya mauaji ya mfanyabiashara tajiri wa Mirerani, Erasto Msuya na namna yalivyotekelezwa, zitaendelea kuanikwa kesho Jumatatu wakati kesi ya mauaji hayo itakapoendelea kusikilizwa.

Kesi hiyo inayovuta hisia za wananchi wengi wa miji ya Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Jiji la Arusha na miji ya Moshi na Bomang’ombe, inasikilizwa katika mahakama kuu kanda ya Moshi.

Mfanyabiashara huyo aliyekuwa akimiliki vitega uchumi kadhaa,  aliuawa kwa kufyatuliwa risasi 22 za bunduki aina ya SMG ambapo 12 ndizo zilizompata risasi na kusababisha kifo chake.

Tukio hilo la aina yake, lilitekelezwa Agosti 7,2013 katika eneo la Mijohoroni wilayani Hai na watu wasiojulikana lakini polisi inawatuhumu watuhumiwa saba kuhusika na mauaji hayo.

Kesi hiyo ilisimama kusikilizwa Machi 21 mwaka huu, baada ya upande wa mashitaka kuwasilisha notisi ya kukata rufaa kupinga uamuzi mdogo wa Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo.

 Awali kabla ya kusitishwa kwa usikilizaji wa kesi hiyo, kuliibuka mabishano ya kisheria kati yamawakili wa utetezi na mawakili waandamizi wa Serikali wanaoendesha kesi hiyo.

 Mabishano hayo yalitokana na hatua ya shahidi wa tisa, Inspekta Samwel Maimu kutoa ushahidi wa mdomo wa kukiri kosa wa mshitakiwa wa tatu, Ally Mussa Majeshi bila kuwasilisha maelezo yake.

Mawakili wa utetezi, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emanuel Safari na John Lundu, walipinga utaratibu huo, wakisema ni kinyume cha sheria kwa vile maelezo hayo hayajapokelewa mahakamani.

 Jaji alikubaliana na hoja ya mawakili wa utetezi na kuzuia ushahidi huo, hali ambayo iliwasukuma mawakili wa Serikali wakiongozwa na Abdalah Chavula kuwasilisha notisi ya kukata rufaa.

Kesi hiyo sasa imepangwa kuendelea kusikilizwa kuanzia Oktoba 16 hadi Novemba 16 baada ya jopo la majaji wa mahakama ya rufaa iliyoketi Jijini Arusha kuitupa rufaa ya upande wa Jamhuri.

Ratiba iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, Benard Mpepo, inaonyesha mashahidi 37 wa upande wa Jamhuri wataendelea kutoa ushahidi wao kutimiza idadi ya mashahidi 46.

 Washitakiwa katika kesi hiyo ni Sharifu Mohamed, Shaibu Jumanne au Mredii, Musa Mangu, Jalila Zuberi, Karim Kihundwa, Sadick Mohamed au Msudani au Mnubi na Ally Mussa au Mjeshi.

Wakati kesi ya Bilionea huyo ikiendelea kesho , mkewe Miriam Elisaria Msuya naye anasota mahabusu Jijini Dar Es Salaam kwa tuhuma za kumuua dada wa bilionea huyo aitwaye, Aneth Msuya.

Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana Mei 25,2016 katika eneo la Kibada Kigamboni Jijini Dar Es Salaam, mauaji ambayo yaliibua hisia na simanzi kubwa kwa familia ya bilionea huyo.

Mke wa Deo Filikunjombe Atoa Yamoyoni

$
0
0
Mke wa Deo Filikunjombe Atoa Yamoyoni
Ikiwa ni miaka miwili imepita tangu aliyekuwa Mbunge wa Ludewa Deo Haule Filikunjombe afariki dunia, mke wa wake Sarah Habiba amesema Tanzania ina pengo kubwa kwa kumpoteza Deo.

Kwenye ukurasa wake wa instagram, Sarah Habiba ameandika ujumbe huo, wakiadhimisha miaka miwili ya kifo chake kwa kufanya ibada takatifu.
"Mume wangu leo umefikisha miaka miwili tangu upatwe na mauti, kiukweli umeacha pengo kubwa kwa watanzania, jamii na familia kiujumla, watoto wako wanakumiss sana, mimi mkeo, Mungu akulaze mahala pema peponi mpenzi wangu, ntakukumbuka daima mpenzi", ameandika Sarah Habiba.
Deo Filikunjombe alifariki )ctoba 15, 2015 kwa ajali ya helkopta akitokea Dar es salaam kwenda Ludewa, na kuanguka kwenye msitu wa mbuga ya Selous, akiwa na rubani wake William Silaa ambaye ni baba mzazi wa Jerry Silaa, na msaidizi wa Deo Filikunjombe, Bwana Mkwera.
Deo Filikunjombe atakumbukwa kwa uchapa kazi wake na juhudi alizozionyesha kwenye kamati ya Bunge kuibua sakata la Escrow akiwa na wabunge wengine, akiwemo rafiki yake wa karibu mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

Bomomoa Bomoa Kuhamia Kwenye Makanisa, Misikiti Kimara Kesho

$
0
0
Bomomoa Bomoa Kuhamia Kwenye Makanisa, Misikiti Kimara Kesho
Nyumba za ibada 24 zinatarajiwa kubomolewa kesho  na Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads)  ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro inayoanzia Kimara hadi Kiluvya.

Ubomoaji wa nyumba hizo za ibada ni mwendelezo wa uboamoaji wa nyumba takribani 1300 za wakazi wa maeneo hayo zinazodaiwa kujengwa ndani ya mita 121.5 ya barabara hiyo.

Nyumba zaidi ya 1000 zimebomolewa mpaka sasa hali inayosababisha baadhi ya wananchi kulala nje kutokana na kukosa makazi .

Akizungumza na gazeti la Mwananchi leo kwa njia ya simu Mhandisi wa Tanroads Kimara ambaye  anasimamia

ubomoaji huo ,Jonson Rutechula amesema kesho watakuwa na kazi maalum ya kubomoa nyumba za ibada tu.

“Tumewaambia viongozi wa misikiti na makanisa, waondoe vitu kesho  tunakuja kubomoa.Tutabomoa makanisa 14 na misikiti 10 kuanzia eneo la Kimara hadi Kiluvya”amesema

Amesema  shughuli ya ubomoaji wa nyumba imekamilika kwa asilimia kubwa ,zimesalia  nyumba za ibada tu.”Kama unavyoona karibu ubomoaji wa nyumba za makazi  umekamilika tulibakiza  nyumba za ibada”amesema

Ameongeza kwamba  “Kesho  tutabomoa makanisa 14 na misikiti 10 kuanzia eneo la Kimara hadi Kiluvya na tutaanza kazi hiyo asubuhi”amesema Rutechula.

Hata hivyo mwandishi wetu alitembelea Kanisa la Mtakatifu Maria Parokia ya Kimara  na kukuta baadhi ya waumini wakitoa  vyombo nje na walipoulizwa baadhi ya viongozi waliokuwepo kanisani hapo walikataa kuzungumza .

“Sisi siyo wasemaji, kama unataka habari njoo kesho na kamera zako uchukue  matukio lakini pia mtafute Paroko yeye atakwambia nini kinaendelea maana sisi si wasemaji”amesema  mmoja wa waumini hao

Askofu Amfananisha Magufuli na Mugabe kwa Uwajibikaji Wake

$
0
0
Askofu Amfananisha Magufuli na Mugabe kwa Uwajibikaji Wake
Askofu wa Jimbo Katoliki Zanzibar Agustino Shao, amefananisha Rais Magufuli na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kwa uwajibikaji na kukemea vitendo vya rushwa.

Kwenye taarifa iliyotolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa Askofu Shao ameyasema hayo kwenye ibada ambayo ilihudhuriwa na Rais Magufuli visiwani Zanzibar kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph, na kusema kwamba Rais Mugabe alichukua hatua za kupigania maslahi ya Wazimbabwe na sasa hivi wananeemeka na matunda hayo, kitendo ambacho amedai Rais Magufuli anakifanya kwa sasa, na kuwataka watanzania kumuunga mkono.
"Hatutaweza kusema tunaimaliza rushwa wakati tunaendelea kuishi kwa kupata fedha ambazo hatujazifanyia kazi. Ni lazima tuishi machungu ya kuimaliza rushwa. Ni lazima tuishi machungu ya kuweka uadilifu katika utendaji wetu, tusipoishi maisha hayo tutaishi dunia mbili, dunia ya rushwa na dunia ya kujenga uchumi na uadilifu wa watanzania, " amesema Askofu Shao.
katika salamu zake akimshukuru Askofu SHao kwa mahubiri mazuri, amewahakikishia Watanzania kuwa serikali itachukua hatua kupambana na rushwa kulinda rasilimali za nchi, na kuwataka Watanzania wote kuungana katika hilo.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images