Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Walioshindwa Uchaguzi CCM Wapinga Matokeo

$
0
0
Walioshindwa Uchaguzi CCM Wapinga Matokeo
Matokeo ya uchaguzi wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), yamepingwa katika wilaya nne kati ya saba za Mkoa wa Mwanza kutokana na madai ya kugubikwa na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi.

Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Acheny Maulid alitaja wilaya ambazo matokeo yake yamewekewa pingamizi kuwa ni Magu, Nyamagana, Misungwi na Sengerema.

Aliwataja wenyeviti ambao ushindi wao unapingwa ni Zebedayo Athumani kutoka Nyamagana, Daudi Gambadu (Misungwi), Zabloni Makoye (Magu) na Agostine Makoye wa Sengerema.

“Vikao husika vitakutana kujadili na kuamua pingamizi hizo kwa mujibu wa katiba na kanuni za uchaguzi ndani ya chama,” alisema Maulid.

Uchaguzi wa wenyeviti wa wilaya wa CCM katika wilaya zote saba za Mkoa wa Mwanza ulifanyika Oktoba 5. Wenyeviti wengine waliochaguliwa ambao hawajawekewa pingamizi hadi juzi ni Peter Muyanga kutoka Kwimba, Ally Mambile (Ukerewe) na Nelson Mesha wa Ilemela.



Jakaya Kikwete Afunguka Kinachokwamisha Afrika

$
0
0
Jakaya Kikwete Afunguka Kinachokwamisha Afrika
Rais Mstaafu wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete amesema uchangishaji fedha kwa ajili ya miundombinu na kilimo ni lazima uende kwa pamoja kwa sababu masuala hayo ni masuala mtambuka kwa maendeleo ya taifa lolote duniani.

Dk. Kikwete amesema hayo leo wakati akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa jijini New York, nchini Marekani, baada ya kushiriki kikao cha ngazi ya juu cha Wiki ya Afrika ambapo masuala ya tabia nchi, miundombinu, kilimo na vijana yamejadiliwa.
Dk. Kikwete amesema uchangishaji usiotosheleza wa fedha katika sekta ya kilimo unakwamisha wakulima kushiriki kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu zisizo na ubora na kusababisha wakulima kukosa mavuno yenye tija.
"Ukiendeleza kilimo unasaidia watu wengi sana na umasikini wa Afrika una sura ya vijijini kwamba masikini wengi waliopo Afrika wapo vijijini na tatizo kubwa la kilino ni kwamba tunatumia dhana za zamani jembe la mkono linatumika zaidi kuliko mashine na mitambo, asilimia 4 tu ya kilimo chetu tunatumia umwagiliaji na mvua ya mwenyezi Mungu, tatu kilimo chetu hatutumii mbegu bora tunatumia mbegu za asili ambazo hazizalishi sana" alisema Jakaya Kikwete

Odinga: Hakutakuwa na Uchaguzi Kenya 26 Oktoba

$
0
0
Odinga: Hakutakuwa na Uhaguzi Kenya 26 Oktoba
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesisitiza kwamba muungano wake hautashiriki uchaguzi wa marudio wa urais ambao umepangiwa kufanyika Alhamisi.
Amesema kwamba haamini kwamba utakuwa huru na wa haki.
Bw Odinga aliongoza mkutano wa kisiasa Bondo, magharibi mwa Kenya Rais Kenyatta alipokuwa anaongoza maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa jijini Nairobi.
Ameahidi kutoa tangazo kwa wafuasi wake Jumatano.

Emmanuel Mbasha Amtupia Lawama Mzazi Mwenzie, Madam Flora kwa Kumzuia Kuonana na Mtoto Wake.

$
0
0
Emmanuel Mbasha Amtupia Lawama Mzazi Mwenzie, Madam Flora kwa Kumzuia Kuonana na Mtoto Wake.
Msanii wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha amemshutumu mzazi mwenzie, Madam Flora kwa kumzuia kuonana na mtoto wake.

Wawili hao ambao wote ni waimbaji ndoa yao ilishavunjika na Madam Flora kuolewa. Akizungumza na TBC Fm amedai kitu anachokifanya siyo kizuri na amekuwa akifanya jitihada za kuonana mwanaye ila imeshindikana.

“Kiukweli mtoto sijaonana naye muda, yeye mwenyewe hajataka kunipa mimi mtoto, nimeshafanya jitihada na anajua na hata kama sasa hivi anasikia anajua mtoto ameninyima na kitu anachokifanya siyo kizuri kwa mtoto” amesema Mbasha.

“Ni muda mrefu, mara mwisho nimeona naye (mtoto) mahakamani, muda mrefu kipindi wanakaribia kufunga harusi. Inaniumiza sana ni mtoto wa kipekee, ni mtoto ambaye nampenda na nimeishi naye kipindi chote tangu mdogo”

Usain Bolt Ametangaza Nia Yake ya Kujiunga na Soka

$
0
0
Usain Bolt Ametangaza Nia Yake ya Kujiunga na Soka
Mkimbiaji Usain Bolt ametangaza nia yake ya kujiunga na soka mwaka ujao na tayari vilabu kadhaa vimejitokeza kutaka huduma yake.

Bolt amesema kuwa alitamani kuanza kucheza soka mwaka huu lakini alipata majeraha ya misuli ya paja mwezi Agosti hivyo akashindwa kufanya mazoezi lakini anaamini mwaka 2018 ataanza vizuri maisha mapya ya soka.
“Nataka kuanza kucheza soka mwakani, kwasababu ni mchezo unaonivutia na nimesema hilo mara nyingi lakini mwakani nitaanza rasmi kuwa mwanasoka na tayari klabu nyingi zimeshajitokeza kutaka nizichezee”, amesema Bolt wakati anafanya mahojiano na FIFA.com.

Shabiki huyo wa kutupwa wa Manchester United hajaweka wazi ni klabu gani ataichezea hali ambayo imeacha maswali mengi kwasababu aliwahi kusema anatamani kuwa mshambuliaji wa Manchester United.
Bolt mwenye umri wa miaka 31 amestaafu kukimbia mwaka huu akiwa bingwa mara nane wa Olimpic pamoja na Ubingwa wa dunia mara 11 akitwaa medali za dhahabu.

Baba Mzazi wa Lulu Akataa Posa ya Lulu

$
0
0
Baba Mzazi wa Lulu Akataa Posa ya Lulu
Baba Mzazi wa muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, Mzee Michael Kimemeta, amekataa kupokea posa ya binti yake huyo ambaye amekuwa akiwatoa udenda wanaume wengi kwa urembo wake.

Mzee Kimemeta amefunguka hayo alipokuwa akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba hatopokea posa ya mwanaume atakayekwenda kumuoa Lulu, kikubwa atakachoangalia ni furaha ya binti yake kwenye maisha yake.
“Suala la kuoana ni la watu wawili anayeoa na anaye olewa, yeyote atakayemleta sisi tunambariki, posa haiko kwenye msamiati wangu, siuzi mtoto, wala sitaki posa yoyote, posa yangu ni amani ndani ya nyumba yao, ndio posa watakayoniletea”, amsema Mzee Kimemeta.
Mzee Kimemeta ameonekana kuwa bega kwa bega na mwanaye kwenye kesi ya mauaji inayomkabili binti yake, iliyoanza kusikilizwa tena wiki hii.

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumamosi

JE Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo, Kufika Kileleni Haraka na Kushindwa Kurudia Tendo ?

$
0
0

JE, UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO, KUFIKA KILELENI HARAKA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO AU MAUMBILE MADOGO YA UUME?
       Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume husababishwa na mambo mengi kama KISUKARI, UNENE ULIOPITILIZA, KUJICHUA  (MASTER BLASHION), HOMONI kushindwa kufanya kazi ipasavyo n.k.
     Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.
      BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.
     Kwa kutumia mimea na matunda @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6 hadi 7  @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130,000/=

      BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA ZIMETHIBITISHWA KIAFYA.
    KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA
  ulipo duniani kwa (+255)
           0767447444 na
              0714335378
        UTAPATA HUDUMA
    NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

Mume Ampiga Stop Koletha Kucheza Filamu

$
0
0
Mume Ampiga  Stop Koletha Kucheza Filamu
MSANII wa filamu za Kibongo, Koletha Raymond anadaiwa kupigwa stop kucheza filamu na mumewe Temba ndiyo maana amejikita kwenye mambo mengine kwa sasa.

Chanzo kilieleza kwamba kutokana na tabia za baadhi ya wasanii wa kike kutojiheshimu hata kama wakiwa kwenye ndoa, mume wa Koletha ameamua kumpiga stop kucheza filamu ili kulinda ndoa yao isije kukumbwa na kimbunga kwani ndoa nyingi za mastaa zimekuwa hazidumu.

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania

$
0
0
Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tercisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi Mhashamu Castory Msemwa, kilichotokea, Oktoba 19 mwaka huu nchini Oman.


Kiwango cha Ufaulu Mtihani wa Darasa la Saba Kimeendelea Kupanda

$
0
0
Kiwango cha Ufaulu Mtihani wa Darasa la Saba Kimeendelea Kupanda
Kiwango cha ufaulu katika mtihani wa darasa la saba kimeendelea kupanda kwa miaka mitatu mfululizo.

Ufaulu umepanda kwa zaidi ya asilimia mbili, mwaka 2015 ukiwa asilimia 67.84, mwaka 2016 (asilimia 70.36) na mwaka 2017 (asilimia 72.76).

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), wanafunzi 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani wa darasa la saba, wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema watahiniwa waliofaulu wamepata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata.

Msonde alisema idadi hiyo ya waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76. Alisema kati yao wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 (asilimia 74.80).

Dk Msonde alisema mwaka 2016 waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.

Akizungumzia takwimu za matokeo, Dk Msonde alisema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 ikilinganishwa na mwaka 2016.

“Kwa masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii, ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97 ikilinganishwa na mwaka 2016,” alisema.

Dk Msonde alisema watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili, ambalo kiwango cha ufaulu ni asilimia 86.86, lakini kiwango cha Kiingereza ni asilimia 40.30.

Katika matokeo hayo, Msonde alizitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni St Peter, St Severine, Mwanga na Rweikiza zote za Mkoa wa Kagera, Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga), Palikas (Shinyanga), Hazina na St Anne Marie (Dar es Salaam) na Martin Luther (Dodoma).

Dk Msonde alizitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni Nyahaa, Mntamba na Ikolo zilizopo mkoani Singida, Bosha, Kishangazi na Mkulumuzi (Tanga), Ntalasha (Tabora), Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi) na Kitwai A (Manyara).

Aliitaja mikoa 10 iliyoongoza kitaifa kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, Katavi na Tabora.

Dk Msonde aliwataja watahiniwa 10 bora kuwa ni Hadija Azizi Ally, Naseem Kareem Said na Insiyah Kalimuddin wote kutoka shule ya Sir John.

Wengine ni Ibrahim Shaban kutoka shule ya Tusiime, Kadidi Mkama Kadidi (Paradise), Mahir Ally Mohamedy na Mbarak Faraj (Feza), Colletha Masungwa na Philimon Damas (St Achileus) na Acius Job Missingo (St Peter Claver).

Aliwataja wasichana 10 bora kitaifa kuwa ni Hadija Azizi Ally, Naseem Kareem Said, Insiyah Kalimuddin, Linah John Lameck, Saada Ahemd Omary na Khadija Salim Omary wote kutoka shule ya Sir John; Colletha Masungwa (St Achileus), Hannat Ramadhani (Dar-Ul-Muslimeen), Efrosina Geofrid (Omukaliro) na Nancy Elirehema Mejooli (Tusiime).

Wavulana 10 bora kitaifa ni Ibrahim Shaban wa Tusiime, Kadidi Mkama Kadidi (Paradise), Acius Job Missingo (St Peter Claver), Mahir Ally Mohamedy (Feza), Mbarak Faraj (Feza), Philimon Damas (St Achileus), Huruma Godfrey (Mwanga), Hamza Azael Almas (Hazina), Gobbons Roy (Fountain of Joy) na Erastus Joseph (St Peter Claver).

Dk Msonde alizitaja halmashauri 10 zilizoongoza kitaifa kuwa ni Kinondoni, Moshi, Arusha, Ilala, Mafinga Mji, Mlele, Kigamboni, Nzega Mji, Mpanda na Chato.

Katika hatua nyingine, Necta imezuia matokeo ya watahiniwa 65 waliougua au kupata matatizo na kushindwa kufanya mitihani yao yote au baadhi ya mitihani.

Wanafunzi hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwakani.

Necta pia imefuta matokeo yote ya watahiniwa 10 waliofanya udanganyifu.


Jay Mo Atoboa Siri kwa Watanzania Kuhusu Marehemu Ngwea

$
0
0
Jay Mo Atoboa Siri kwa Watanzania Kuhusu Marehemu Ngwea
Msanii Jaymo amefunguka kitu ambacho watanzania wengi walikuwa hawakijui ambacho kilikuwa kifanyike kati yake na msanii mwenzake ambaye ni marehemu kwa sasa, Albert Mangwea.

Akipiga stori kwenye Back Stage ya Bongo Fleva Top 20, Jamo amesema walikusudia kufanya kazi kwa pamoja baada ya kuona kazi ya habari ndo hiyo ya Mwana Fa na AY, hivyo wakatamani nao watengeneze albam ya pamoja.
"Tulikuwa tunapanga kufanya albam ya pamoja mimi na marehemu, na 'insipiration' kubwa tuliipata kutoka kwa Mwana FA na AY, walipofanya 'Habari ndo hiyo', na tayari tulishakuwa tumefanya nyimbo nyingi pamoja na ambazo zilishatoka, na Majani tulishamwambia, lakini ndio hiyo bahati mbaya ikatokea na hiko kitu hakikutokea", amesema Jay Mo.
Wasanii hao tayari walishafanya kazi pamoja kama cheza kwa step, kimya kimya na kimafia ambazo zilifanya vizuri na bado zinadai.
Albert Mangwea alifariki May 2014, akiwa nchini Afrika Kusini ambako alienda kwa ajili ya kazi zake za sanaa.

Miss Tanzania Aliyeteuliwa Kushiriki Miss World 2017 Awasili China

$
0
0
Miss Tanzania Aliyeteuliwa Kushiriki Miss World 2017 Awasili China
Mrembo kutoka Tanzania Julitha Kabete aliyechaguliwa kwenda katika mashindano ya urembo wa dunia, Miss World 2017 kwaajili ya kuiwakilisha taifa kwa mwaka huu ameshafika nchini China.

Julitha aliondoka siku ya Oktoba 19, mwaka huu kuelekea nchini humo katika mji wa Sanya, kwaajili ya shindano hilo linalohusisha nchi zipatazo 120 duniani kote.

Kilele cha mashindano ya Miss World 2017 yanatarajiwa kufanyika ifikapo Novemba 18 mwaka huu, katika ukumbi wa Sanya City Arena na kituo cha E! na Phoenix TV, ndiyo watakaorusha matangazo hayo mubashara.

Alichosema Squeezer Kuhusu Harmorapa 'Nilishawahi Kumuona Anakimbia Bastola, Napenda Vituko Vyake Kuliko Muziki Wake

$
0
0
Alichosema Squeezer Kuhusu  Harmorapa 'Nilishawahi Kumuona Anakimbia Bastola, Napenda Vituko Vyake Kuliko Muziki Wake
Msanii Mkongwe wa Bongo Flava, Squeezer amejibu iwapo anamjua Harmorapa.Squeezer ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sitamani’ katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm aliulizwa iwapo anamjua Harmorapa na kujibu;

“Nilishawahi kumuona anakimbia bastola, napenda vituko vyake kuliko muziki wake, siwezi kuelezea chochote juu ya muziki wake, let’s talk about me” amesema Squeezer.

Katika hatua nyingine amesema kuwa hawezi kufanya kiki kama njia ya kujitangaza zaidi kwani anaamini katika uwezo wake wa kimuziki.

Ndege Iliyokuwa Imebeba Wanasiasa Nchini Kenya Imeanguka

$
0
0
Ndege Iliyokuwa Imebeba Wanasiasa Nchini Kenya Imeanguka
Ndege moja inayodaiwa kuwa ni ya mmiliki binafsi iliyokuwa imebeba wanasiasa nchini Kenya imeanguka katika Ziwa Nakuru nchini humo.

Taarifa kutoka kwa Mwandishi wetu amesema kwamba Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na serikali ya nchi hiyoimesema kwamba wealiokuwepo ndani ya ndege hiyo ni wanasiasa wa Jubilee ambao walikuwa wakienda kufanya kampeni
Haijabainika ni wanasiasa wa Kiwango kipi ambao walikuwepo ndani ya ndege hiyo iliyoanguka.
Taarifa iliyotolewa kwa wanahabari naMkuu wa kukabiliana na majanga haijasema chanzo kilichosababisha ndege hiyo kuanguka.
Hata hivyo inadaiwa kwamba nchi hiyo tangu usiku wa kuamkia leo kulikuwa na mvua kubwa.
Msemaji wa serikali anatarajiwa kuzungumza kutoa taarifa kamili pamoja na idadi ya hao wanasiasa.

Simba Kibaruani Leo Kuikaribisha Njombe Mji

$
0
0
Simba Kibaruani Leo  Kuikaribisha Njombe Mji
Ligi kuu ya soka Tanzania bara VPL inaendelea leo kwa jumla ya mechi Sita kupigwa kwenye viwanja tofauti ambapo vinara wa ligi Simba SC watakuwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuikaribisha Njombe Mji.

Simba ambayo ina alama 12 baada ya raundi Sita leo itaingia uwanjani saa 10:00 jioni kusaka alama zingine tatu kwenye raundi ya Saba ya VPL kisha baada ya hapo itajiandaa na raundi ya Nane ambayo itakuwa dhidi ya Yanga Oktoba 28.
Simba inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na mabadiliko kwenye benchi lake la ufundi ambapo kocha mpya msaidizi Masoud Juma atasimama kwenye mstari baada ya kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyejiuzulu mapema wiki hii.
Taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa baada ya mchezo wa leo timu itasafiri kwenda Visiwani Zanzibar kwaajili ya Kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya watani wao wa Jadi Yanga ambao kesho watakuwa mkoani Shinyanga kucheza na Stand Unite

Mrembo Caroline Joseph Amefunguka Kuhusu Ujauzito wa Kiba

$
0
0
Mrembo Caroline Joseph Amefunguka Kuhusu Ujauzito wa Kiba
BAADA ya picha na habari kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba ana ujauzito wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’, mrembo Caroline Joseph amefunguka na kueleza anavyotishiwa maisha.
Akielezea sakata hilo ‘lililokiki’ mitandaoni wiki hii, Caroline alisema alishtushwa na taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba ana ujauzito wa Kiba jambo ambalo si la kweli kwani hajawahi kuwa na uhusiano naye na anamuheshimu kama kaka na ndugu yake.
“Sina mimba jamani na sina uhusiano na Kiba, kuna mtu amefungua akaunti feki kwa kutumia jina langu kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram ambaye anasema ana ujauzito wa Kiba na ameweka picha zangu eti na picha ya ultrasound ya mtoto tumboni na kusema Princes wa Kiba anakuja.
“Kiukweli nimeumia sana maana imenipa usumbufu hivyo nilienda kuripoti polisi katika kitengo cha makosa ya mtandao (Cyber Crimes) na wako kwenye uchunguzi wa kumpata huyo mtu anayetumia jina langu na kuweka picha zangu kunichafua ili achukuliwe hatua,” alisema Caroline.
Aidha, Caroline alieleza kuwa kutokana na sakata hilo amekuwa akipokea meseji za vitisho kwenye simu yake kwa namba ngeni kwamba watamfanyia kitu mbaya kwa kuwa anamchafua Kiba kwa kusema ana ujauzito wake.
“Nimepata vitisho kwenye simu yangu kwamba watanipoteza kwa kuwa ninamchafua Kiba lakini nimekuwa nikiwaambia waangalie kwenye Instagram mimi natumia jina la Dorothea-caroline9 lakini huyo aliyeweka picha na kusema ana mimba anatumia ambayo haina 9 mwisho na mimi sina wafuasi wengi ni mia saba tu.
“Nimeamua kwenda polisi ili huyo mtu akamatwe maana naweza kupata jambo baya wakati sina hatia yoyote, huyo mtu inawezekana anatafuta wafuasi kwa ajili ya kufanya biashara zake,” alisema Caroline.
Ili kuleta usawa wa habari, Risasi Jumamosi lilimtafuta Kiba kupitia kwa meneja wake, Aidan Seif hakupokea simu na hata alipotumiwa picha na maswali kuhusu habari hii kwa njia ya mtandao wa WhatsApp meseji zilionekana kumfikia na kuzisoma lakini hakujibu hata moja.
Kiba na Caroline waliwahi kuingia kwenye vichwa vya habari baada ya picha zao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii wakiwa hotelini ambapo mwanadada huyo alifafanua kwamba alipiga picha kama shabiki wake tu.

Zitto Kabwe Awapa Makavu Wanachama wa ACT- Wazalendo

$
0
0
Zitto Kabwe Awapa Makavu Wanachama wa ACT- Wazalendo
Mbunge wa Kigoma Ujiji ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amewataka wanachama ambao wanaamini chama hicho ni jukwaa la kuitetea serikali, kutoka ACT Wazalendo kwani sio mahali sahihi kwa wao kuwepo.

Zitto Kabwe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishiwa habari katika ofisi za chama zilizopo Kijitonyama jijini Dar es salaam, na kusema kwamba kama watu hao wapo ndani ya chama, ni vyema wakaondoka kama walivyofanya wanachama wengine walioondoka ACT-Wazalendo.
“Tunawaasa wote wanaodhani kuwa chama hichi kitakuwa jukwaa la kuisifia chama tawala na serikali, hili sio jukwaa sahihi kwao, wajitathimini ama kuendelea na uanchama au wajivue kama walivyofanya wenzao”, amesema Zitto Kabwe.
Kauli hiyo ya Zitto Kabwe imekuja siku chache tangu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Samson Mwigamba, kujiunga na chama cha CCM

Viongozi Watakiwa Kuwa Eneo la Kazi Muda Wote

$
0
0
Waziri Awataka Viongozi wa Kuwa Eneo la Kazi Muda Wote
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka viongozi wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO), kuwa katika eneo la mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) muda wote.

Waziri amesema hiyo itasaidia kuhakikisha mkandarasi anapata ushirikiano wa kutosha na hivyo kuwezesha mradi kukamilika kama ilivyopangwa ambapo takribani shilingi trilioni 2.8 zinatarajiwa kutumika.
Profesa Mbarawa amesema hayo alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), inayojengwa usiku na mchana kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro  yenye urefu wa KM 205 na kuzungumzia kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.

Pia Mh. Waziri  amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Edward Malima, kuhakikisha wanafunzi wa uhandisi wanapata nafasi ya kutosha ya kushiriki kwa vitendo katika ujenzi huo ili kuiwezesha nchi kuwa na wataalamu wa kutosha wenye uzoefu kwenye ujenzi na usimamizi wa miradi ya reli.
Naye  Mhandisi Edward Malima, amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kufanya ziara ya kustukiza usiku ambayo imechochea hamasa kwa wafanyakazi na mkandarasi na kuahidi  kumsimamia mkandarasi kikamilifu ili mradi huo ukamilike kwa wakati na uwiane na thamani ya fedha.

Mwalimu Ajiua kwa Kujichoma Kisu Kwenye Koromeo

$
0
0
Mwalimu Ajiua kwa Kujichoma Kisu Kwenye Koromeo
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi, Leonard Mwipugi (29) amejiua kwa kujichinja koromeo akiwa nyumbani kwake.
Taarifa zilizotolewa na Mratibu wa Elimu Kata ya Mtenga, Hebron Mwafungo zimeeleza kuwa mwalimu huyo amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja nyumbani kwake muda wa  saa sita mchana leo Jumamosi.
Amesema kuwa mwalimu huyo alikwenda kazini kwake na saa  5 asubuhi alirejea nyumbani na hakumkuta mkewe  na baada ya muda walipata taarifa kuwa mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo chumbani kwake.
Amesema kuwa mwalimu huyo alikua akiishi na mdogo wake nyumbani hapo na alipofika alimtuma mdogo wake  mbali kidogo ya nyumba hiyo na baada ya kurudi aliona damu na baada ya kuchungulia chumbani alikuta kaka yake amefariki dunia kwa kujichinja koromeo na kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji hicho

Amesema baada ya kumdodosa mdogo wa marehemu huyo alidai kuwa kaka yake  siku za nyuma alikua na mgogoro na mkewe lakini ulikwisha ila anahisi kitendo cha mkewe kuondoka nyumbani na kwenda mjini Namanyere huenda jambo hilo lilimkasirisha na kuchukua hatua hiyo ya kujichinja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana lakini polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kilichomsibu mwalimu huyo kiasi cha kuchukua maamuzi ya kujiua kikatili namna hiyo.


Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images