Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

TFF Yatangaza Viingilio Mechi ya Simba ,Yanga

$
0
0
TFF Yatangaza Viingilio Mechi ya Simba ,Yanga
Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza viingilio vya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania VPL, raundi ya nane kati ya wenyeji Yanga SC dhidi ya Simba siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Taarifa kutoka shirikisho imebainisha kuwa watazamaji watakaotaka kuketi kwenye jukwaa kuu watapaswa kulipia shilingi elfu ishirini 20000/= ili kuona mchezo huo wa watani wa Jadi.
Watazamaji watakaoketi eneo la mzunguko watalipia shilingi elfu kumi, 10000/= ili kushuhudia mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee kutokana na aina ya wachezaji walisajiliwa msimu huu wa 2017/18.

Yanga na Simba zitaingia uwanjani zote zikiwa na alama 15, Simba ikiwa juu kwa tofauti ya mabao hivyo mshindi wa mchezo huo ana nafasi kubwa ya kuongoza ligi huku akisubiri matokeo ya Mtibwa Sugar dhidi ya Singida United.

Serikali Kununua Meli Itakayofanya Kazi Bukoba na Mwanza

$
0
0
Serikali Kununua Meli  Itakayofanya Kazi Bukoba na Mwanza
Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania imetangaza tenda ya kununua Meli itakayokuwa inafanya safari zake kwenye ziwa Victoria kati ya Miji ya Bukoba na Mwanza.

Hilo limebainishwa leo na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam, wakati akitoa hotuba baada ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa kamati ya Madini iliyofanikisha uchunguzi wa Mchanga wa madini (Makinikia) pamoja na mikataba ya madini kati ya serikali na kampuni ya Barrick.
“Fedha zipo nyingi ndio maana tunaweza kuanzisha miradi mbalimbali na sasa tumetangaza tenda ya kununua na kujenga Meli mpya itakayokuwa inafanya kazi ziwa Victoria kwasababu hakuna Meli tangu ndugu zetu wapoteze uhai kwenye ajali ya MV Bukoba”, amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais ameongeza kuwa tayari nchi ya Korea ya Kusini imeshaonesha nia ya kuchukua Tenda hiyo ya kununua na kujenga Meli itakayokuwa inatoa huduma ndani ya ziwa Victoria.

Madili ya Zari Yamkosesha Usingizi Ester Kiama

$
0
0
Madili ya Zari Yamkosesha Usingizi Ester Kiama
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Ester Kiama amesema kuwa, kila akimt azama Mwan amama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ a napolamba madili ya matangazo huwa anakosa usingizi kwa kujiuliza yeye anapataje na siyo Mbongo?
Ester aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, madili makubwa anayoyapata Zari yanatakiwa kuwafanya mastaa wa Bongo wajifunze na wajiulize maswali mengi ya kwa nini yeye tu na siyo wao!
“Kiukweli fursa anazopata Zari, kuna wakati mwingine zinanichanganya sana kwa sababu ninajiuliza mbona sisi hatuwezi?” alisema Ester.

Gavana Mteule Atoa Neno Baada ya Uteuzi Wake

$
0
0
Gavana Mteule Atoa Neno Baada ya Uteuzi Wake
Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amesema amepokea kwa heshima kubwa dhamana aliyopewa na Rais John Magufuli na anatambua changamoto za nafasi hiyo.

Profesa Luoga ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) - Taaluma, amesema leo Jumatatu Oktoba 23,2017 kuwa atatumia wataalamu wa BoT kufanya kazi.

Amesema anahitaji ushirikiano wa kila mtu katika kufanikisha kazi aliyopewa.

“Nimepokea kwa heshima dhamana niliyopewa nikitambua kwamba zipo changamoto. Nitakwenda kujifunza zaidi kwa sababu sijawahi kuwa Gavana, nitatumia wataalamu waliopo katika kutekeleza majukumu yangu,” amesema Profesa Luoga.

Soma: Profesa Luoga Gavana mpya BOT

Rais Magufuli Julai 11,2017 alimteua Profesa Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akichukua nafasi ya Bernard Mchomvu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Novemba mwaka jana na bodi hiyo kuvunjwa.

Profesa Luoga ni mtaalamu katika masuala ya sheria za kodi na amefundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1986 kabla ya kupandishwa cheo na kuwa profesa mshiriki (Associate Professor) mwaka 2005.

Ameshika nafasi mbalimbali chuoni hapo ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa kamati ya misaada ya kisheria katika kitivo cha sheria mwaka 1993 - 1995, mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali (2005 - 2009), katibu wa baraza la chuo kikuu (2009 - 2013) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma (2013 hadi sasa).

Profesa Luoga aliyezaliwa mwaka 1958 ni wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Alihitimu shahada ya kwanza ya sheria UDSM mwaka 1985. Baadaye alikwenda kusoma Shahada ya Uzamili (LLM) katika chuo cha Queen’s University cha Canada (1988).

Mwaka 1988 alihitimu Shahada ya Uzamili ya Sheria za Kimataifa (MIL) katika Chuo cha Lund University cha Sweden (1991) na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Warwick cha Uingereza mwaka 2003.

Nipo Radhi Kufanya Dhambi ya Kuvunja Nyumba za Watu- Lukuvi

$
0
0
Nipo Radhi Kufanya Dhambi ya Kuvunja Nyumba za Watu- Lukuvi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Willium Lukuvi ameweka wazi mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli kwamba yupo radhi kufanya dhambi ya kuvunja nyumba za watu waliovamia kwenye eneo la mtanzania mnyonge ili eneo lirudi kwa

muhusika halali.
Waziri Lukuvi amebainisha hayo leo Ikulu Jijini Dar es salaam, baada ya Rais Magufuli kumaliza kuwapatia vyeti wanakamati waliofanya mazungumzo na kampuni ya Barrick Gold na wale waliofanya uchuzi wa thamani katika makinikia.
Amesema kwamba serikali haitawafumbia macho wavamiaji ambao wanawaonea wamiliki halali wa ardhi kwakuwa wao hawana pesa za kupambana nao kwa sababu wakati anakabidhiwa nafasi ya kuongoza wizara hiyo Mh. Rais alimuambia aende akawasaidie wanyonge.
Nitafanya dhambi ya kuvunja nyumba ya yule aliyevamia eneo la mwingine ili haki kamili irudi kwa mmiliki halali. Nilipokuwa Sumbawanga juzi Mbunge aliniambia viongozi wote wa Mkoa wameshindwa. Watu wababe wanatokea na kujenga kwenye viwanja vya watu maskini wale walio na hati ya umiliki. Serikali haitawafumbia macho wavamiaji kuwaonea wenye umiliki.
"Uliniambia niende wizara ile nikaondoe uonevu, kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria. Nipo kuhakikisha uonevu unakoma. Lazima nyumba zao tuziwekee alama ya X na tutazivunja. Lazima masikini wapatiwe haki zao. Japo najua changamoto ni nyingi na kwenye hii wizara kama unavyojua utajiri upo nje nje kwa sababu ya dhuluma niwaambie hatutawavumilia. Serkali tutasimama kuondoa ulaghai na wale wenye kujenga kwa kutumia mabavu tutawaondoa". Lukuvi
Ameongeza "Sitawafumbia macho watakaopora viwanja halali vya maskini kwa kuwa wao wanapesa, tutazivunja nyumba zao na miliki itarudishwa kwa mwenye nayo".

Watoto Walionusurika Ajalini Lucky Vincent Kupelekwa Tena Marekani

$
0
0
Watoto Walionusurika Ajalini Lucky Vincent Kupelekwa Tena Marekani
Waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Lucky Vincent ya mjini Arusha, walionusurika katika ajali ya basi na kupelekwa nchini Marekani kwa matibabu, huenda wakarejea nchini humo kuendelea na masomo ya elimu ya juu.

Doreen Mshana, Saidia Ismael na Wilson Tarimo walirejea nchini Agosti 18,2017 wakiwa na afya njema baada ya kunusurika katika ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva iliyotokea Mei 16,2017 wilayani Karatu. Hivi sasa wamemaliza elimu ya msingi shuleni Lucky Vincent.

Shirika la Siouxland Tanzania Educational Medical Ministries (Stemm) ambalo ndilo lilifanikisha matibabu ya wanafunzi hao limeanza majadiliano na taasisi kadhaa kuwezesha watoto hao kurejea Marekani kuendelea na masomo ya elimu ya juu.

Rais wa shirika hilo, Dk Steve Meyer amesema kwa ufadhili wao, watoto hao watajiunga na masomo ya sekondari jijini Arusha katika shule inayomilikiwa na Kanisa Katoliki nchini.

Amesema amesema yeye, mkewe na baadhi ya washirika wa Stemm watafika Tanzania Januari mwakani wakati watoto hao watakapokwenda kuanza masono.

Amesema, “Tupo katika majadiliano na taasisi kama Morningside na Briar Cliff  kuangalia namna ya kuwaleta Sioux City watoto hawa kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu,” amesema.

Wakati wakiwa Marekani watoto hao inaelezwa walivutiwa na mandhari ya mji wa Sioux kiasi cha kuonyesha hisia za kutaka kubaki huko.

Amesema watoto hao walitembezwa katika maeneo mengi na kujifunza vitu mbalimbali jambo lililowafanya wajihisi kuzoea kwa haraka mji huo.

Meyer amesema Wilson amepona kwa asilimia 95 na Sadia kwa asilimia 85, huku Doreen akihitaji mazoezi kidogo ili kukamilisha uponyaji wake. Doreen alipooza kutokana na ajali hiyo.

Watoto hao wamekuwa wakipata uangalizi wa karibu kutoka kwa wafanyakazi wa Stemm waliko nchini wakiendelea na kazi ya kujitolea.

Katika hatua nyingine, Meyer amesema yuko mbioni kuchapisha kitabu ambacho kitaelezea maajabu ya uponyaji wa watoto hao.

Amesema kitabu hicho tayari kimeanza kuandikwa na kinatarajiwa kukamilika wakati wowote kikiwa na jina la Answer the Call ikiwa na maana ya itikia wito kwa maana ya kutoa msaada kwa wahitaji.

Kenyatta Akutana na Mwenyekiti wa IEBC, Asema Yuko Tayari kwa Uchaguzi

$
0
0
Kenyatta Akutana na Mwenyekiti wa IEBC, Asema Yuko Tayari kwa Uchaguzi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) huku uchaguzi wa marudio ambao umekumbwa na utata ukiendelea kukaribia.
Rais amekutana na Bw Wafula Chebukati katika afisi ya Bw Kenyatta katika jumba la Harambee, Nairobi.
Mwenyekiti huyo wa tume alikuwa amekutana na mgombea wa upinzani Bw Raila Odinga Ijumaa.
Bw Odinga alijiondoa kutoka kwenye uchaguzi huo wa Alhamisi akisema hana imani uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.

Uchaguzi huo wa 26 Oktoba unaandaliwa baada ya Mahakama ya Juu kufuta uchaguzi wa kwanza uliofanyika tarehe 8 Agosti ikisema kulikuwa na kasoro nyingi.
Bw Chebukati wiki iliyopita alikuwa ameitisha mkutano wa wagombea wote wa urais lakini baadaye akauahirisha na baadaye akakutana na Bw Odinga kivyake.

Alidokeza kwamba anapanga kuwakutanisha Bw Odinga na Bw Kenyatta baadaye baada kukutana na rais huyo.

Taarifa kutoka ikulu imesema Rais Kenyatta amemwambia mwenyekiti huyo kwamba yuko tayari kwa uchaguzi huo wa marudio na hana masharti yoyote kwa tume hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Naibu Rais William Ruto pia amehudhuria mkutano huo.
"Tumeweka wazi kwamba hatuna masharti wala matakwa yoyote kwa kuhusu suala hili. Tumetoa fedha za kutumiwa na IEBC kufanya kazi yake. Sasa wanafaa kfuanya kazi hiyo," amesema Rais Kenyatta.
"Tunasisitiza tu kwamba uchaguzi ufanyike tarehe 26 Oktoba, huo ndio wakati uliowekwa na IEBC kwa mujibu wa matakwa yaliyoambatana na kufutwa kwa uchaguzi wa tarehe 8 Agosti."

Mahakama ya Juu, kwenye uamuzi wake ilikuwa imeagiza uchaguzi mpya ufanyike kwa kufuata katiba na sheria kikamilifu katika muda wa siku 60.
IEBC awali ilikuwa imetangaza uchaguzi mpya ufanyike tarehe 17 Oktoba lakini baadaye ikaahirisha tarehe hiyo hadi 26 Oktoba baada ya moja ya kampuni zilizokuwa zikitoa huduma muhimu kwa ajili ya uchaguzi huo kusema hazingekuwa tayari wakati huo.
Bw Odinga amekuwa akiitaka IEBC kuahirisha uchaguzi huo na ametangaza kwamba tarehe hiyo "hakutakuwa na uchaguzi".

Lowassa Amemtembelea Tundu Lissu Kumjulia Hali

$
0
0
Lowassa Amemtembelea Tundu Lissu Kumjulia Hali
Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa amemtembelea kumjulia hali Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Mhe. Tundu Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibu Nairobi nchini Kenya.

Mhe. Lowassa ameongozana mke wake Mama Regina Lowassa ambapo leo hii walifika hospitalini hapo kumjulia hali Mhe. Lissu

Tangu picha za Lissu kuanza kuonakana pindi watu wanapoenda kumjulia hali, viongozi wa juu na wabunge wamekuwa wakifanya hivyo. Miongoni mwao ni mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, Mhe. John Heche na mbuge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi ambao hivi karibuni wameonekana wakiwa katika picha ya pamoja.

Kutana na Mtatibu wa Nyota za Binadamu Maalim Fadhili Rashid Kutoka Comoro Kwa Sasa Yupo Tanzania

$
0
0
KUTANA NA MTABIBU WANYOTA ZABINADAMU    DUNIANI KOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO KWA SASA YUPO TANZANIA

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAUWEZO WAKUBAINI JAMBOLAKO NAKULITATUA MAALIM FADHILI RASHIDI ANATIBU MARADHI YA FUATAYO KAMA VILE


KAMA MIGUU KUUMA NA KUWAKA MOTO PRESHA KISUKARI VIDONDA VYA TUMBO PUMU TEZI NA UVIMBE TUMBONI ANAUWEZO WA KURUDISHA MTU ALIEPOTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE) KUMFANYA MKEMUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA

KUMUONA MBAYAWAKO LIVE KWASABABU MAALUM ANA TOWA PETE YA BAHATI ITAKAYO KULETEA PESA BILA YA MASHARITI NAKUMILIKI MALI UNAZOTAKA

DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVUZAKIUME PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPS SHEPU KUWA NA UMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASAA (24) ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YA MVUTO WABIASHARA KUUZA MALIYAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMAULETE KWENYE BIASHARA KUSAFISHA NYOTA NAKUTOWA MIKOSI TIBAHII NI KWADINI ZOTE MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKASANA LAKINI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE UTAPATA HUDUMA POPOTE ULIPO NCHI YEYOTE DUNIANI UTAPATA HUDUMAYANGU ACHAKUTESEKA NA MATATIZO ULIONAYO MAALIM FADHILI RASHIDI YUPO TANZANIA KWA AJILIYAKO


CALLING +255719362806/+255763276239/

Harmonize Ajibu iwapo Ana Beef na Idris Sultan

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Harmonize amesema si kweli kwamba ana beef na Idris Sultan.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Shulula’ ameiambia The Playlist ya Times Fm stori za kuwepo beef kati yao huwa zinatengenezwa na baadhi ya watu tu.

“Sina beaf na Idris na sijawahi kuonana naye am tell you, ni stori tu naona watu wanatengeneza kila siku halafu kingine mimi ni mtu wa kusamehe sana haya mtu akiwa amenikosea kabisa naamini kuwa ni binadamu hajakosea, inawezakana hata mimi nakoseaga watu” amesema Harmonize.

Kwa mujibu wa stori zilizokuwa sikizagaa zilidai kuwa wawili hao walikutana usiku wa party ya birthday ya Diamond, ila Idriss alipomsalimu Harmonize hakuitika kitu ambacho amekikanusha vikali.

Faiza Ally sasa Ahamishia Shambulio Kwa Mke wa Mh.Sugu...Adai ni Mke wa Mtu

$
0
0
Miezi kadhaa Baada ya mashambulio makali kwa mzazi mwenzake juu ya malezi ya mtoto,mrembo asiekwisha matukio Bongo Faizza Ally, amemshambulia vikali mtandaoni Mke wa mbunge sugu(happiness msonga), sababu zikiwa ni kuhisi kutukanwa na accounts fake za Mke huyo wa mheshimiwa sugu.

Tazama picha.

Zitto Aliamsha Dude Kuhusu Ndege za Bombardier

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo amefunguka na kusema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya awamu ya tano imekopa dollar milioni 500 kutoka benki ya Uswiss na pesa hizo ndiyo zimetumika kulipa ndege za Tanzania.

Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya jamii na kusema kuwa riba za mkpo huo ni mkubwa sana na kudai watu wa chini wakiwepo wavuvi wa Migebuka kutoka Kigoma watahusika kulipa deni hilo kupitia kodi zao.
"Serikali ya CCM ya awamu ya Tano imekopa $500m kutoka Benki ya Credit Suisse ya Uswiss Kwa riba kubwa Sana. Sehemu ya fedha hizo zimetumika kulipia ndege ambazo Serikali inanunua. Wavuvi wa Migebuka Kigoma watahusika kulipa deni hilo kupitia kodi zao" alisema Zitto Kabwe

Rais Magufuli leo amesema kuwa uchumi wa nchi unazidi kukuwa na kudai serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina pesa za kutosha ndiyo maana imeweza kununua ndege mpya zaidi ya sita kwa mara moja na kudai watu ambao wanasema uchumi umeshuka wanaichonganisha serikali na wananchi.

Mwigamba Afunguka Baada ya Kuhamia CCM

$
0
0
Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa ACT -Wazalendo, Samson Mwigamba ametaja sababu mbili zilizomfanya kukataa wito wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya chama hicho kwa ajili ya mahojiano.

Jumamosi Oktoba 21,2017 Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliwaeleza waandishi wa habari kwamba Kamati ya Uongozi ya chama hicho, ilimwita Mwigamba ili atoe maelezo baada ya kukituhumu chama hicho kukiuka misingi yake lakini hakufika.

Zitto alisema kamati hiyo baada ya kukutana na kujadiliana ilibaini hakuna misingi iliyokiukwa.

Mwigamba aliyekihama chama hicho na kujiunga na CCM, leo Jumatatu Oktoba 23,2017 amesema hakuona jambo jipya litakalojadiliwa dhidi yake katika kikao cha Kamati ya Uongozi kwa kuwa mengi aliyoyalalamikia alishayatolea ufafanuzi kwenye barua yake ya kujiuzulu.

Amesema jambo lingine lililomfanya kutohudhuria kikao hicho ni Kamati ya Uongozi kuwa na wajumbe 12 badala ya watano waliopo kwa mujibu wa Katiba ya ACT-Wazalendo.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho, Ado Shaibu amesema hawana muda wa kulumbana na Mwigamba na wanaheshimu uamuzi wake wa kujiuzulu, hivyo wanamtakia kila la kheri kwenye safari yake ya kisiasa.

Install Application ya MCHAMBUZI Kwenye Simu yako Kusoma Matamko ya Wanasiasa Kila Siku

$
0
0
Maswala ya Siasa na Matamko ya kila siku ya Wanasiasa Hakikisha Umedownload App ya Mchambuzi Kwenye simu yako

BonyezaHAPA

Kama we ni Mpenzi wa Habari za Siasa Usipitwe na Hii Application ya Mchambuzi..... Bonyeza HAPA Kudownload kwenye Simu yako


JE Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo, Kufika Kileleni Haraka na Kushindwa Kurudia Tendo ?

$
0
0
JE, UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO, KUFIKA KILELENI HARAKA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO AU MAUMBILE MADOGO YA UUME?
       Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume husababishwa na mambo mengi kama KISUKARI, UNENE ULIOPITILIZA, KUJICHUA  (MASTER BLASHION), HOMONI kushindwa kufanya kazi ipasavyo n.k.
     Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.
      BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.
     Kwa kutumia mimea na matunda @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6 hadi 7  @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130,000/=

      BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA ZIMETHIBITISHWA KIAFYA.
    KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA
  ulipo duniani kwa (+255)
           0767447444 na
              0714335378
        UTAPATA HUDUMA
    NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

Maisha ya Pacha Waliozaliwa Wameshikana Hatarini

$
0
0
Maisha ya Pacha Waliozaliwa Wameshikana Hatarini
Maisha ya watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameshikana yako hatarini iwapo hawataondolewa ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa madaktari.
Alam Abu Hamna kutoka hspitali ya Shifa, ilisema kuwa hali inayowakumba watoto hao wasichana ni ngumu na kwamba haiwezi kutatuliwa na madaktari wa hospitali zilizo ukanda wa Gaza.
Ilisema kuwa matumaini ni kuwa watoto hao watasafirishwa ng'ambo ili watenganishwe
Watoto hao walizaliwa Jumamosi na mmoja wao anatajwa kuwa dhaifu kuliko mwingine.
Safari ngumu ya mapacha walioshikana kwenda kutenganishwa DRC
Mapacha barani Afrika hufa kuliko watoto wengine
Hata hivyo kila mmoja ana moyo wake na mapavu. Mapacha ambao hutumia kiungo kimoja mara nyingi hukumbwa wna hatari ya kuishi.
"Maisha yao yako hatarini, ni hali iliyo ngumu," Dr Abu Hamna alinukuliwa akisema na gazeti la Times la Israel.
Watoto hao walizaliwa Jumamosi na mmoja wao anatajwa kuwa dhaifu kuliko mwingine.
Alisema hali ya mmoja wa mapacha hao iko shwari la mwenzake yuko hali mbaya na anahitaji matibabu.
"Ikiwa watasafirishwa nje kwa haraka kupata matibabu nje, maisha yao yataokolewa," alisema.
Kitengo cha jeshi la Israel kinachohusika na kuratibu kuingia na kuondoka ukanda wa Gaza kinasema kuwa hakijapokea ombi lolote la mapacha kuondolewa eneo hilo.
Mapacha waliozaliwa wameungana kuanza shule
Pacha waliotungwa siku tofauti Australia
Mapacha waliozaliwa wakiwa wameshikana katika Ukanda wa Gaza mwezi Novemba mwaka 2016 baadaye walikufa.
Israeli na Misri wameka vizuizi vya ardhini na baharinin kwa Ukanda wa Gaza kwa miaka kumi katika jitihada za kuzuia mashambulizi kutoka kwa wanamgambo.

Kigaila Benson Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Tuhuma za Uchochezi

$
0
0
Kigaila Benson Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Tuhuma za Uchochezi
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, linamshikilia Mkurugenzi wa Operesheni na mafunzo wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema bwana Kigaila Benson kwa tuhuma za kutoa lugha zinazodaiwa kuwa za kichochezi.

Bw. Kigaila anashiikiliwa kwa tuhuma za kutoa lugha za kichochezi Oktoba 12 katika mkutano wake na waandishi wa habari, na amehojiwa na kunyimwa dhamana ambapo itaamuliwa hapo kesho kupewa dhamana ama kufikishwa mahakamani.
Mwanasheria wa Kigaila Frederick Kihwelo akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho leo Jumatatu amesema hatima ya dhamana ya Mkurugenzi huyo itaamuliwa kesho Jumanne.
Wakili Kihwelo amesema, “Kigaila amehojiwa kwa masaa 3 kuanzia saa 7 mchana hadi saa 10 jioni na amehojiwa kwa makosa aliyoyafanya katika mkutano wake Oktoba 12 na wamekataa kutoa dhamana labda hadi kesho” amesema
Mwanasheria huyo amesema katika mkutano huo alizungumza mambo mengi ikiwemo kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kutekwa kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

Umoja wa Mataifa Wataka Wapinzani Waliokamatwa Kuachiwa Huru

$
0
0
Umoja wa Mataifa Wataka Wapinzani Waliokamatwa Kuachiwa Huru
Umoja wa mataifa umetoa wito ya kuachiwa mara moja kwa watu 30, wa chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutoka korokoroni.
Wanachama wa vyama vikuu viwili vya Union for Democracy na wenzao wa Social Progress, walikamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, ulioko Kusini mashariki mwa nchi hiyo, baada ya polisi kuvunja mkutano waliokuwa nao.

Utawala wa Rais, Joseph Kabila, umepiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa kisiasa, pamoja na maandamano ya upinzani, tangu muda wake wa kuhudumu kama Rais kisheri, ulipomalizika mwaka mmoja uliopita.
Rais Joseph Kabila amesalia mamlakani hata baada ya muhula wake kuhudumu kumalizika mwaka mmoja uliopit

Rais Joseph Kabila amesalia mamlakani hata baada ya muhula wake kuhudumu kumalizika mwaka mmoja uliopita
Tume ya uchaguzi nchini humo, imesema kuwa, haitakuwa rahisi kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais, kabla ya mwezi Aprili mwaka ujao wa 2019.
Chama kingine cha upinzani- Union for the Congolese Nation, kimesema kwamba, kitajiondoa katika serikali ya ugawanaji mamlaka, kuhusiana na kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu.
Maandamano ya mara kwa mara ya upinzani nchini humo umekabiliwa vikali na utawala wa Rais Joseph Kabila.

Cristiano Ronaldo Ashinda Tuzo Ya Mchezaji Bora wa Dunia wa Fifa

$
0
0
Cristiano Ronaldo Ashinda Tuzo Ya Mchezaji Bora wa Dunia wa  Fifa
Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa Fifa 2017 baada ya kuwapiku wachezaji Lionel Messi na Neymar katika kipengele hicho.

Tuzo hizo zimetolewa Oktoba 23 ambapo mchezaji huyo aliyeambatana na mpenzi wake na mwanae amewashukuru waliompigia kura kwa kuweza kushinda pamoja na mashabiki na wachezaji wenzake.

“Nashukuru wote mlionipigia kura kwa kunifanya nishinde tuzo hii,” amesema Ronaldo.

Mbali na tuzo hiyo Ronaldo ametajwa katika kikosi bora cha mwaka 2017 ambacho kimewajumuisha Messi na Neymar na nyota wengine akiwemo Sergio Ramos, Toni Kroos, Andres Iniesta, na Dani Alves.

Tuzo ya mchezaji bora wa kike wa Fifa 2017 ilienda kwa Lieke Martens ambaye hakuudhuria katika utoaji wa tuzo kutokana na kujiandaa na kujiandaa na mechi ya kufuzu kombe la dunia la wanawake.

Ukumbi ulilipuka kwa shangwe wakati linatangazwa goli bora la mwaka ‘Puskas’ ambapo katika magoli 10 bora mashabiki walisikika wakimtaja nyota wa Arsenal, Olivier Giroud ambaye alitangazwa kama mshindi.

Wengine walioshinda tuzo za Fifa 2017 ni Zinedine Zidane (Kocha bora kwa waume), Sarina Wiegman (kocha bora kwa wanawake) Gianluigi Buffon (Kipa bora), Mashabiki wa Celtic (Kikundi bora), Francis Kone (Mchezo wa kiungwana).

Serikali Kuwashughurikia Watumishi Wanaoshiriki Vitendo vya Rushwa

$
0
0
Serikali Kuwashughurikia Watumishi Wanaoshiriki Vitendo vya Rushwa
Serikali imesema mtumishi anayefanya kazi katika Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) akibainika kushiriki vitendo vya rushwa atachukuliwa hatua mara moja.

Mkurabita ilianzishwa kwa lengo la kumsaidia anayemiliki ardhi kimila atambulike kisheria na apewe hati itakayomwezesha kupata mkopo ili aendeleze biashara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika alitoa onyo hilo alipotembelea taasisi hiyo. Alisema asingependa kusikia kuna mwananchi anatafuta hati au wanataka eneo lake lipimwe lakini mtumishi wa Mkurabita anamweleza kuwa ili kazi yako iende haraka lazima ‘waonane’ jambo ambalo si sawa.

“Naomba muelewe, anayepambana na rushwa ni Rais mwenyewe kwa sababu Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa) ipo chini yake. Pia, Mkurabita ipo chini ya Ofisi ya Rais Ikulu. “Maana yake Waziri wa Mkurabita ni Rais John Magufuli, mimi namsaidia kwa hiyo mnapofanya kazi hapa mjue mkuu wa nchi ndiyo mwenye wizara,” alisema Kapteni Mkuchika ambaye pia ni Mbunge wa Newala Mjini (CCM).

Mratibu wa Mkurabita, Seraphia Mgembe alisema licha ya mafanikio walionayo kuna changamoto ya kutopata fedha za kutosha ili kujiendesha. Alisema mwaka 2009 Mkurabita iliomba Sh43 bilioni kwa ajili kufanya shughuli zake kulingana na mpango kazi wao, lakini fedha walizopata hadi sasa ni asilimia 55 sawa na Sh23 bilioni.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images