Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Wapinzani Wazungumzia Mikutano ya Hadhara Wakiwa Ikulu

$
0
0
Wapinzani Wazungumzia Mikutano ya Hadhara Wakiwa Ikulu
Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo na wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana waliibua suala la mikutano ya hadhara wakati walipopewa nafasi ya kuzungumza katika hafla ya Rais iliyofanyika Ikulu.

Wote wawili walitaja “mikutano ya hadhara” wakati walipokuwa wakikamilisha ushauri wao mfupi wakati wa hafla ya kutunuku wajumbe wa kamati mbili zilizoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza mchanga wa madini unaosafirishwa nje, biashara, sheria na mikataba ya madini.

Wakati Profesa Lipumba alisema ametumia nafasi hiyo kutoa yake kwa kuwa mikutano ya hadhara imezuiwa, Cheyo alisema hawezi kuzungumza mengi kuepuka kuonekana amegeuza fursa hiyo kuwa mkutano wa hadhara.

Cheyo alijirudi baada ya kutumia muda mrefu zaidi ya Profesa Lipumba, akijikita katika kueleza kilio cha muda mrefu cha kutaka Serikali ifungue macho na kuchukua hatua ili rasilimali za nchi ziweze kusaidia Watanzania.

“Kuna siku moja nilikuwa , nikawaambia wazungu tumechoka kuitwa masikini. Huwezi ukawa masikini wakati una gesi ya ujazo wa 57 trilioni, na madini na kila kitu, halafu unaitwa masikini. Tumechoka,” alisema Cheyo.

“Wewe (Rais) umetusaidia kuondoka katika kuchoka huku. Asante sana Mheshimiwa Rais.”

Cheyo alitumia nafasi hiyo kumuomba Rais awaamini Watanzania kwa kuwa nchi ina watu wengi wenye akili.

“Tanzania ina watu wenye bongo, na ndio maana inaitwa Bongoland,” alisema huku akishangiliwa.

Hata hivyo aligeukia suala la siasa akitaka vyama visigeuze iviepuke vurugu.

“Nawaomba rafiki zangu ambao tuko katika vyama vya ushindani, hesbu tusigeuze mfumo huu wa vyama vingi kuwa kiwanda cha chuki,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Bariadi Mashariki.

“Mwalimu (Julius Nyerere) aliyefanya kila nguvu kuwaambia wana-CCM-- pamoja na asilimia 20 kusema tuwe na vyama vingi- tuwe na vyama vingi.

“Nia yake haikuwa kutengeneza kiwanda cha kutukanana, kiwanda cha chuki, kiwanda cha kukosa uzalendo. Vyama vya siasa tuwe kiungo cha Watanzania wote kushirikiana na uongozi ambao umechaguliwa kidemokrasia, kuongoza nchi yetu kwa sababu nchi hii itaendeshwa na sisi wote. Na wote tuna nafasi.”

Naye Profesa Lipumba alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais kwa kulipa kipa umbele suala la madini ambalo wamekuwa wakilipigia kelele.

“Sisi viongozi wa vyama vya siasa, hususan vyama vya upinzani, kwa muda mrefu, kwa miaka mingi, hasa kutokea mwaka 2000, tumepiga kelele sana kuhusu mikataba ya madini na namna maliasili zinavyoibiwa,” alisema.

Alisema itakuwa ajabu sasa wakianza kubeza juhudi hizo.

Hivi Ndivyo Rais Magufuli Alivyojibu Hoja za Zitto Bila ya Kumtaja

$
0
0

Hivi Ndivyo Rais Magufuli Alivyojibu Hoja za Zitto Bila ya Kumtaja
Kwa takriban miezi miwili, kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amekuwa akihoji ukimya wa Serikali katika kutangaza mapato na hata ilipotangaza, alisema takwimu zimepikwa, lakini jana alipata majibu ya hoja zake.

Rais John Magufuli alitumia hafla ya kutunuku wajumbe wa kamati mbili alizoziunda kuchunguza biashara na udhibiti wa madini, kutoa ufafanuzi kuhusu hali ya makusanyo ya mapato, jambo ambalo Zitto amekuwa akihoji katika mikutano na waandishi wa habari, mikutano ya chama chake na katika mitandao ya kijamii.

Baada ya Benki Kuu (BoT) kutotangaza ripoti ya hali ya kiuchumi kwa miezi miwili kwa kile ilichoeleza kuwa ni ugumu wa upatikanaji wa taarifa, na Mamlaka ya Mapato (TRA) nayo kusuasua kutangaza makusanyo kwa miezi kadhaa, Zitto alisema hali hiyo ilitokana na Serikali kukusanya fedha kidogona kwamba ilikuwa ikipika taarifa.

Katika hotuba yake jana, Rais Magufuli hakumtaja mtu anayepotosha takwimu za Serikali, lakini alihoji hoja anazozitoa na kutaka hatua zichukuliwe.

“Nafikiri kama sikumbuki vizuri, Sheria ya Takwimu ya 2015, kuna kifungu kinasema mtu anayebadilisha takwimu za Serikali anaweza kufungwa miaka miwili jela,” alisema Rais.

“Unakuta mtu anazungumza makusanyo yameshuka, wakati anajua si kweli. Watu wa namna hii wangekuwa wanapelekwa mahakamani waka-justify (wakathibitishe).”

Alisema kwa hesabu za kawaida, kama mapato yanashuka, Serikali haiwezi kusaini mkataba wa kujenga reli yenye thamani ya zaidi ya Sh7 trilioni na urefu wa kilomita zaidi ya 700.

Pia alisema kwa Serikali ambayo haina mapato, haiwezi kununua ndege sita mpya kwa wakati mmoja.

“Wanazinunua kwa kubadilisha kwa dagaa? Au migebuka ya Kigoma?” alihoji Rais.

Pia alisema kwa Serikali ambayo haina fedha, haiwezi kufufua mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kama wa Stiegler’s Gorge ambao ukikamilika utakuwa unazalisha megawati 2,100, wakati uwezo wa sasa ni megawati 1,460.

Alisema kutokana na kuwa na fedha, Serikali imetangaza zabuni ya mradi huo na zaidi ya kampuni 79 zimejitokeza kuwania kupata zabuni hiyo.

“Zabuni za mradi huu zimeshatangazwa na fedha zimeshatengwa. Kama mapato yamepungua tungepata wapi fedha,” alihoji Rais Magufuli.

“Kama huna fedha na makusanyo hayapo, utatangaza tenda ya namna hiyo? Utakuja kuwalipa nini?” alihoji Rais.

Akiendelea kufafanua kwa mtindo wa maswali, Rais pia alisema Serikali isingeongeza bajeti ya afya wala kutekeleza mradi wa Umeme Vijijini (Rea), kujenga madaraja, barabara kutoka Kigoma hadi Nyakanazi na ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria kama isingekuwa na fedha.

“Kama fedha hakuna utawawekaje makandarasi wale kwenda kujenga barabara kwa kiwango cha lami?” alihoji.

“Kwa hiyo ninachotaka kusema Watanzania muwapuuze watu wa namna hiyo.”

Zitto, ambaye amewahi kuongoza Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), amekuwa akihoji makusanyo ya Serikali na mwishoni mwa wiki alisema ACT Wazalendo imemtaka aende kuwasilisha ripoti kwenye chama kuonyesha jinsi Serikali inavyopika taarifa kuhusu makusanyo na hali ya kiuchumi.

Mke wa Dkt Slaa Atajwa Kesi Kwenye Kesi Inayomkabili Lulu ya Kumuua Kanumba Bila Kukusudia

$
0
0
Mke wa Dkt Slaa Ahitajika Kesi ya Lulu Kumuua Kanumba Bila Kukusudia
Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, (Lulu) imeendelea leo katika mahakama kuu jijini Dar es salaam, ambapo upande wa utetezi umeshindwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwa kukosekana shahidi mwingine.

Shahidi huyo aliyetajwa kuwa ni mke wa aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, Bi. Jacqueline Mushumbusi ambaye yuko nje ya nchi, ushahidi wake umekataliwa kupokelewa na mahakama mpaka awepo mwenyewe au askari ambaye aliandika maelezo yake afike mahakamani kutoa ushahidi huo.

Hapo jana wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala aliiomba mahakama iruhusu kupokelewa kwa ushahidi utakaotumwa na Bi. Mushumbusi, lakini mahakama imekataa ombi hilo ikisema upande wa utetezi hauwezi kusoma ushahidi huo na kutoa uamuzi wake wa kutaka shahidi awepo mwenyewe au askari aliyeandika ushahidi huo.
Kesi hiyo imeghailishwa mpaka kesho Oktoba 25, ambapo inatarajiwa askari aliyeandika ushahidi wa Bi. Jacquline Mushumbusi, kuwasili mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake.

Mashabiki Wapewa Taadhari Mechi ya Simba, Yanga

$
0
0
Mashabiki Wapewa Taadhari Mechi ya Simba, Yanga
Kuelekea mechi ya  watani wa jadi Simba na Yanga, Jumamosi  hii, wachezaji waliowahi kuzichezea klabu hizo, wameelezea namna ambavyo mashabiki wanaweza kuumizwa na matokeo yatakayokinzana na matarajio yao.

Hiyo ni kutokana na timu hizo kushinda kwa idadi sawa ya mabao kabla ya mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi mnono dhidi ya Njombe Mji kwa mabao 4-0,huku Yanga wakishinda ugenini dhidi ya Stand United kwa mabao 4-0.

Sekilojo Chambua  ni staa wa zamani wa Yanga, alielezea kuwa ; "Hii kila timu kushinda mabao sawa haina maana inaweza kubadili chochote kwenye matokeo zaidi ya kuleta hamasa na mchezo kuwa na presha kubwa, ila ninaloliona ni huku kwa mashabiki ambao wanatambiana kuona kila mtu anaweza kuibuka mshindi, wajiandae kisaikolojia."

Kwa upande wa Bitta John, nyota wa zamani wa Simba, alisema; "Labda kwa Yanga mchezaji tishio naona atakuwa Chirwa, lakini kikubwa makocha wanatakiwa kufanya kazi kubwa ya kuwajenga wachezaji wao kuwa makini wasije wakaingia kwa kuvimba kiasi kwamba wakasahau kazi yao mwisho wa siku wakavuruga mchezo."

Dodoma FC Itaamua Hatma ya Toto Africans Jumamosi

$
0
0
Dodoma FC Itaamua Hatma ya Toto Africans  Jumamosi
Pambano la wikiendi hii kati ya vinara wa Kundi C, Dodoma FC utaamua hatma ya Toto Africans kuweka hai au kuzika matumaini yake ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

Timu hizo zitakutana Jumamosi, huku Dodoma ikiongoza kundi na alama 15 wakati Toto Africans ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi tano tu baada ya kila timu kucheza mechi saba.

Iwapo Dodoma itaibuka na ushindi kwenye mechi hiyo itafikisha pointi 18 na hivyo kuhitaji ushindi katika mechi tatu tu za duru la pili ili Toto isiweze kuifikia.

Na kama ikitokea Alliance inayoshika nafasi ya pili ikaibuka na ushindi dhidi ya JKT Oljoro katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza, itatakiwa kupata ushindi katika mechi zake nne kati ya saba za mzunguko wa pili ili kuinyima rasmi Toto nafasi mbili za kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

Kama Dodoma FC itaifunga Toto na kisha kupata ushindi katika mechi tatu zijazo itakuwa na pointi 27, wakati Alliance ikiifunga Oljoro na kupata ushindi kwenye mechi nne zitakazofuata, itafikisha pointi 28 ambazo hazitoweza kufikiwa na Toto Africans hata kama itapata ushindi kwenye mechi zote saba za mzunguko wa pili.

"Pasi na shaka, mechi yetu dhidi ya Dodoma FC ndio nafasi ya mwisho kuona kama bado tunaweza kuwa na nafasi ya kupanda au ndio basi tena," alisema Kocha wa Toto, Almas Moshi.

Kocha huyo alidai kikubwa kinachowakwamisha ni hali mbaya ya kifedha ambayo inawafanya wakose maandalizi mazuri kabla ya mechi zao.

Nisha Awachana Wanaomkashifu Lulu

$
0
0
Nisha Awachana Wanaomkashifu Lulu
MSANII wa Filamu za Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amewaonya watu wanaompiga vijembe msanii mwenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa muigizaji, Steven Kanumba.

Nisha aliiambia Full Shangwe kuwa, kwa kipindi kigumu alichonacho Lulu si cha kumnanga bali cha kumpa faraja.

“Tangu kesi ya Lulu ianze upya kusikilizwa, kuna watu wamekuwa wakimkashifu kwa maneno ya ajabu, bila kujua kuwa hakuna ajuaye ya kesho. Ni vyema tukampa faraja rafiki yetu kwa kipindi kigumu alichonacho,”alisema Nisha.

Wivu wa Kimapenzi Wawaondoa Wasanii Hawa MJ Records, Nay wa Mitego Ahusishwa

$
0
0
Wivu wa Kimapenzi Wawaondoa Wasanii Hawa MJ Records, Nay wa Mitego Ahusishwa
Producer Daxo Chali ambaye anafanya kazi zake katika studio za MJ Records hapo juzi alitangaza kuacha kumsimami msanii Nini kupitia studio hiyo, lakini stori za sasa zinadai chanzo cha hilo ni wivu wa kimapenzi.

Daxo Chali alikuwa akiwasimamia Haitham na Nini ambaye inadaiwa kuwekwa pembeni. Hiyo juzi kupitia ukurasa wake wa Instagrama Daxo chali aliweka wazi hilo kwa kuandika;

Nimeamua Kuacha Kuwasimamia , Juhudi Zangu Zimewafikisha Hapo. So Yeyote Atakayeweza Kuwaendeleza Please Awasaidie. Nitafurahi Nikiona Wanaendelea Nakufanikiwa , 🙏🏽 Ni Wasanii Wazuri Sana Wakipata Mtu Akawapatia KuwaPanga. Mapungufu Yapo Kwa Kila Mtu

Muimbaji Haitham akizungumza na E-Newz ya EATV amesema chanzo cha hayo yote ni katika mtandao wa Instagram ambapo Daxo Chali anamiliki akaunti za wote wawili na kuangalia nini kinaendelea na alipokuta Nini anachati na fulani ambaye inadaiwa kuwa ni boyfriend wake, Daxo  hakuridhika na mazungumzo hayo ndipo alipochukua uamuzi huo.

“Wakati Nini anachati na Boyfriend wake nafikiri Daxo aliona, siwezi kufahamu walikuwa wanachati nini au ulikuwaje lakini tu after hours Nini ananipigia simu ananiambia Kim page yangu imebadilishwa password, so yeye hakumuuliza chochote Daxo” amesema Haitham.

“Baada ya muda akaona kwenye bio zile detail za kumthibitishia yeye ni msanii wa MJ Records zimefutwa, baadaye Daxo ananitumia sms kuwa Nini siyo msanii wangu, nilipoulizwa akiniambia mahusiano ya Nini na Nay wa Mitego yanaharibu CV ya studio, Aseme ni nini anachokita lakini kusema ni mahusiano, no!, kwa sababu kila mtu ana haki ya kupenda” ameongeza.


Daxo Chali

Kwa upande wake Nay amesema jambo hilo halina ukweli wowote na kueleza kuwa jambo hilo haliingi akilini na inadhihirisha upuuzi uliopitiliza

“Sijalipenda kwa sababu nimehusihwa kwenye vitu ambavyo si vya msingi, unamhusisha mtu ambaye atafanya wewe uonekane ni mpuuzi. Nitoe tu ushauri kwa brother Master Jay aangalie MJ Records ni label kubwa kumkabidhi mtoto na kuanza kufanya ujinga, inachafua na inatia doa” amesema.

Nandy: Sina Kinyongo na Ray C

$
0
0
Nandy: Sina Kinyongo na Ray C
Msanii wa bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amefunguka kuwa hawezi kumchukia msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ kwa sababu ya kutofautiana kwao.

Nandy aliiambia Full Shangwe kuwa, pamoja na Ray C kumtolea povu kuwa asiwe anaimba nyimbo zake, lakini yeye hana kinyongo naye.

Rehema Chalamila ‘Ray C’.
“Sina kinyongo na dada yangu Ray C kwa kile kilichotokea, alichokiposti ni mtazamo wake, sina bifu, sina uhasama naye ,”alisema.

Ushirikiano EAC Wakinufaisha Chuo Kikuu cha Aga Khan

$
0
0
Ushirikiano EAC wakinufaisha Chuo Kikuu cha Aga Khan
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU), Profesa Joe Lugalla amesema ushirikiano wa kielimu unaoendelea katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umekifanya chuo hicho kunufaika kwenye masuala ya uongozi, ulinzi, dini na elimu.

Profesa Lugalla amesema hayo jana Jumatatu Oktoba 23,2017 katika mkutano wa pili wa mwaka wa kujadili masuala ya taaluma kwa walimu uliofanyika nchini Uganda.

Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Elimu ya Juu wa Uganda, John Muyingo ukiwa na kauli mbiu ya “Kufikiria upya taaluma kwa walimu.”

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne Oktoba 24,2017 na AKU imesema mkutano huo ni wa siku mbili.

Profesa Lugalla amesema AKU na Taasisi ya Kuendeleza Elimu Afrika Mashariki (IED-EA) zimejikita kutoa elimu bora na yenye manufaa kwa jamii. Amesema ushirikiano ni chachu ya kufikia malengo yao.

“Utoaji wa elimu ni sera ya kidunia inayohitaji ushirikishwaji na ushirikiano baina ya mataifa. Tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja si katika kutoa mawazo ya jinsi ya kufikiria upya taaluma kwa walimu bali katika utekelezaji wake,” amesema Profesa Lugalla ambaye pia ni Mkurugenzi wa IED-EA.

Waziri Muyingo amekipongeza Chuo Kikuu cha Aga Khan kwa uongozi imara katika masuala ya elimu na afya nchini Uganda.

Amesema ni muhimu kuifanya taaluma ya ualimu kuwa ya kipekee.

“Natambua jitihada za Serikali pekee hazitoshi katika kuboresha, kuvumbua na kubadilisha taaluma ya elimu katika nchi yetu. Jitihada za sekta binafsi na wadau wengine bado zinahitajika kwa kiasi kikubwa,” amesema Muyingo.

Xi Jinping: Kiongozi Mwenye Nguvu Zaidi Nchini China Tangu Kipindi cha Mao Zedong'

$
0
0
Xi Jinping: Kiongozi Mwenye Nguvu Zaidi Nchini China Tangu Kipindi cha Mao Zedong'
Chama cha Kikomunisti nchini China kimepiga kura kujumuisha falsafa zake Xi Jinping katika katiba na kumuinua hadi kifikia kiwango alichokuwa nacho mwanzilishi Mao Zedong.
Kura hiyo ya kuunga mkono kuandika fikra zake Xi Jinping, ilifanyika wakati wa kukamilika kwa mkutano mkuu wa chama cha Kikomunisti ambao ndio mkutano mkubwa zaidi wa kisiasa nchini China.

Hatua hiyo ni ishara kuwa wapinzani wake hawawezi kumpinga bila ya kitishia utawala wa chama cha Kikomunisti.
Mkutano huo wa Komunisti ulianza wiki iliyopita kwa hotuba ya saa tatu ya Bw. Xi. ambapo alielezea falsafa yake ya siasa za ujamaa.
Maafisa wa vyeo vya juu na vyombo vya habari vya serikali walianza kuzungumzia falsafa hiyo wakiitaja kuwa fikra zake Jinping, ishara kuwa Bw. Xi alikuwa ameimarisha ushawishi wake chamani.
Meli ya China inayobeba ndege za kijeshi yawasili Hong Kong
Watoto wa shule, wanafunzi wa vyuo vikuu na wafanyakazi katika makampuni ya serikali sasa wataungana na wanachama milioni 90 wa chama cha Kikomunisti, kusoma fikra zake Xi Jinping kuhusu kipindi kipya cha ujamaa.

Mabadiliko ya katiba yanamweka Xi Jinping (kushoto) kiwango sawa Mao Zedong (kulia)
Ikiwa kwanza alikuwa ni mwenyekiti Mao kuunganisha nchi ambayo ilikuwa imeharibiwa na vita na ya pili, ya China kutajirika nchini ya Deng Xiaoping, kipindi hiki kipya ni cha kujenga umoja zaidi na wakati huo huo kuifanya China kwa na nguvu nje.

Kuyajumuisha haya yote kwa jina la Xi Jinping kwenye katiba ya chama ina maana kuwa washindani hawawezi kupinga Xi, bila ya kutishia chama cha Kikomunisti.
Zaidi ya wajumbe 2,000 walitumia mkutano huo wa wiki nzima kuwachagua wakuu wa chama mikoani, magavana na wakuu wa mashirika yanayomilikiwa na serikali.

Je Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa..Jibu Lipo Hapa

$
0
0
JE,UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZAKIUME,KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA,KUFIKA KILELENI MAPEMA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA UA MAUMBILE MADOGO YA UUME?Tatizo la kukosa au kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya kiume husababishwa namambo mengi kama,KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURLUMA,MAUMIVU YA KIUNO,UNENE KUPITA KIASI,KUJICHUA(MASTER BLASHION)HOMON Hishindwa kufanya kazi inavyotakiwa nk.upungufu wa nguvu za kiume husababisha tendo la ndoa kutofanyika kwa kujiami nakwa usahihi nahivyo husababisha ndoa mahusiano mengi kuvunjika.BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI,1KUKOSA HAMU YA TENDOL LA NDOA 2 UUME KISIMAMA KWA KULEGEA 3 KUWAHI KUFIKA KILELENI 4 KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA WAKATI 5 KUCHOKA SANA BAADA YA ROUND YAKWANZA NAKUKINAI TENDO NDOA KABISA.TUMIA 3 POWER KWA TATIZO LA UKOSEFU(UPUNGUFU)WA NGUVU ZA KIUME NAHAMU YA TENDO LA NDOA.FINA HUBORESHA MAUMBILE YA KIUME KWA KUNENEPESHA KWA SAIZI UIPENDAYO HAIJARISHI UMRI.PIA KUNA DAWA ZA KURUDISHA MPENZI KWA MUDA MFUPI SANA NAZAKUPATA KAZI,KESI,KUDHULUMIWA,NK WASILIANA NA SHEIKH OMARY AKUTATULIE MATATIZO YAKO HATA KAMA UMEHANGAIKA SANA PASIPO MAFANIKIO UMEFANIKIWA LEO

Pia sheikh omary anatibu busha bila opresheni,kisukari,ngiri,presha,vidonda vya tumbo,korodani kivimba nakuuma,na anatoa ndagu za utajiri kwa wanaohitaji utajiri bila masharti yoyote magumu.ANAPATIKANA DAR ES SALAAM NAUTALETEWA POPOTE ULIPO TIBA HII UKIWA HAUNA NANAFASI YAKUFIKA OFISINI,

PIGA SIMU NO 0767 14 53 57/0629 03 45 50.
SHEIKH OMARY WHATSAP 0759030343.

Haji Manara: Ajibu ni Kiburudisho Ila Viburudisho Peleka Kwenye Minuso Tuna Okwi Mbadara ya Viburudisho

$
0
0
Haji Manara: Ajibu ni Kiburudisho Ila Viburudisho Peleka Kwenye Minuso Tuna Okwi Mbadara ya Viburudisho
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amefunguka na kuweka wazi kuwa ni kweli Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu Migomba kwa sasa ni kiburudisho tosha nchini lakini amemtosa kuwa mshambuliaji huyo huwezi kumfananisha na Okwi.

Haji Manara amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii na kusema ni kweli aliwahi kutamka hilo lakini ukweli unabakia pale pale kuwa kwa sasa Ajib bado huwezi kumfananisha na Okwi kwani wanatofauti kubwa ndiyo maana hata idadi ya magoli yao imekuwa kubwa kati yao.
"Ni kweli niliandika Ajibu ni kiburudisho zaid nchini kwa sasa, ila ninaendelea kukemea kashushwa na Mungu ndio imani yangu itakavyo. Kisha sisi tunataka ubingwa, viburudisho peleka kwenye minuso, ndio maana tuna Okwi kama mbadala wa viburudisho, goli nane kwa tano wapi na wapi" aliandika Manara
Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi kwa sasa ndiye anayeongoza kwenye Ligi Kuu Bara kwa kuwa na idadi kubwa ya magoli ambayo ni 8 akifuatiwa na mshambuliaji kutoka Yanga Ajib ambaye ana magoli 5 kwa mechi 7 walizocheza.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Jumamosi hii Oktoba 28, 2017 katika mzunguko wa nane wa

Mkuu wa Wilaya Azima Vurugu Awapiga Stop FFU Kuwasumbua Wananchi

$
0
0
Mkuu wa Wilaya Azima Vurugu Awapiga Stop FFU Kuwasumbua Wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewapiga marufuku askari wa kikosi cha FFU na kusema hataki kuwaona wakisumbua wananchi katika eneo la Ukonga Dar es Salaam na kutaka waliohusika wachukuliwe hatua kwa kitendo walichofanya kuwapiga wananchi.

Sophia Mjema amesema hayo alipowatembelea wananchi hao ambao wamelalamika kufanyiwa fujo na kupigwa na askari hao kwa siku mbili kutokana na askari mmoja kuuwawa na watu wasiojulikana, Mkuu wa Wilaya anasema kuwa askari hao walipaswa kufanya uchunguzi kujua ni watu gani walihusika kufanya mauaji ya askari huyo na si kwenda kufanya fujo na kuwapiga wananchi pasipokuwa na sababu.
"Kama kuna askari alipatikana ameshafariki utaratibu ulikuwa uchunguzi ufanyike ili waweze kujiridhisha baada ya hapo wale ambao wangetambulika ndiyo wangechukuliwa hatua lakini kwa hili halikubaliki, kwa hiyo nasema hivi askari wote waliohusika kufanya fujo na vurugu wachukuliwe hatua za kinidhamu na huku barabarani sitaki kuona FFU yoyote anasumbua wananchi" alisema Mjema

Aidha Mkuu wa Wilaya huyo ametaka wananchi ambao wameumizwa na askari hao kwa vipigo kwa siku mbili mfululizo waweze kujiorodhesha kwa majina ili wapatiwe matibabu na kusema wale ambao wamepoteza mali zao utaratibu utafanyika kuona nini kifanyike.

Mwamuzi Sasii Kuchezesha Pambano la Watani wa Jadi Jumamosi

$
0
0
Mwamuzi Sasii Kuchezesha Pambano la Watani wa Jadi Jumamosi
Mwamuzi Bora wa msimu uliopita, Elly Sasii ndiye aliyeteuliwa kuchezesha pambano la watani wa jadi nchini, Simba na Yanga litakalopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwamuzi huyo kijana ndiye atakayepuliza kipyenga katikati ya Uwanja wa Uhuru na kusaidiwa na washika vibendera Joseph Bulali na Sudi Lila, huku mezani akiwa mkongwe, Israel  Nkongo.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana katika pambano lao la kwanza la Ligi Kuu Bara msimu huu, linalokuwa la 99 kwa timu hizo kukutana katika ligi tangu mwaka 1965.

Sasii ndiye aliyechezesha pambano la Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga lililochezwa Agosti 20 kwenye Uwanja wa Taifa na Yanga kulala kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa suluhu.

Serikali ya Kenya Yawapa Wananchi Wake Mapumziko

$
0
0
Serikali ya Kenya Yawapa Wananchi Wake Mapumziko
Serikali ya Kenya  imetangaza kuwa siku ya Jumatano itakuwa ya mapumziko ili kuwapa wananchi muda wa kutosha kwa maandalizi ya uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika  Alhamisi ya Oktoba 26.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang'i ameweka notisi hiyo leo katika Gazeti la Serikali na kufahamisha kwamba Alhamisi ya Oktoba 26 itakuwa siku ya mapumziko pia.
Wakenya watakwenda kwenye vituo kuchagua kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi Mkuu wa muungano wa upinzani (Nasa) Raila Odinga ingawa alitangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo wa marudio siku chache zilizopita.
Hata hivyo Raila amewataka wafuasi wake kususia uchaguzi huo na kampeni zake kubwa kwa sasa ni kuhakikisha haufanyiki kwa madai Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeshindwa kutekeleza marekebisho muhimu ambayo amekuwa akitaka yafanyike tangu yalipobatilishwa matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.

Nipo Tayari Kuwajibika Endapo Rais Ataruhusu- Zitto Kabwe

$
0
0
Nipo Tayari Kuwajibika Endapo Rais Ataruhusu- Zitto Kabwe
Mbunge na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa yupo tayari kuwajibika kuhusu kinachodaiwa kupika taarifa za serikali endapo Rais Magufuli ataruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye mapato ya mwezi Julai na Agosti 2017.

Zitto Kabwe amesema kuwa wao wanatumia takwimu za serikali kuwaonyesha wananchi kuwa serikali yao inadanganya na haisemi ukweli wote na uhalisia wa uchumi na kuporomoka kwa mapato. Zitto Kabwe amedai kuwa kodi inayokusanywa na TRA nchini inaweza kulipa mishahara na kuhudumia Deni la Taifa tu na si vinginevyo.
"Kwanini Rais wetu hasemi kuwa tunakopa? Kukopa sio dhambi, kwanini aaminishe watu kuwa anatekeleza miradi kwa kuwa kodi zimeongezeka? Kama Rais anaamini kuwa mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye mapato ya Julai na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi kwa umma. Rais akifanya hivyo nitawajibika" alisema Zitto Kabwe.

Jana Rais John Pombe Magufuli alisema kuwa kuna watu wanapika taarifa za serikali na kusema uongo na kuvitaka vyombo vya usalama na  Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kuwashughulikia watu hao ikiwezekana wafungwe kabisaa

Lulu Atimua Mbio Mahakamani, Baba Mzazi wa Lulu Akimbizana na Waandishi wa Habari

$
0
0
Lulu Atimua Mbio Mahakamani, Baba Mzazi wa Lulu Akimbizana na Waandishi wa Habari
Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael (Lulu),leo baadaya kuwasili Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikiliza muendelezo wa kesi yake ya kuuwa bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Charles Kanumba. Hatimae Lulu amewakimbi waandishi wa habari waliokuwepo Mahakamani hapo huku baba ake mzazi aliwaambia waandishi wa habari kuwa hakuna kupiga picha.

Tukio hilo la Lulu kuwakimbia waandishi wa habari limetokea baada ya Shahidi wa pili upande wa utetezi ambaye ni mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbushi, ambaye ameshindwa kufika mahakamani hapo leo hii kwa ajili ya kutoa ushahidi wake kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa yupo nje ya nchi na hakuweza kupatikana moja kwa moja.

Baba Lulu amekimbizana na waandishi wa habari mpaka kwenye gari analolitumia mwanae na kukaa mbele ya gari kuwaambia waandishi waliokuwepo hivi “Leo picha hampigi tafadhali mwiza maekata kata watu na viroba hampigi picha mmechimbi chini huyu mnamfuata leo hampigi picha,” hayo ndio baadhi ya maneno yaliyosikika kwa baba Lulu.

Hata hivyo mashabiki wa msanii huyo walianza kuwalaumu waandishi wa habari, kwa kusema kuwa ” Kwanini mmetuondolea Lulu wetu ilibaki kidogo aanguke na angeanguka mngempiga picha mngetukoma,” hayo ni maneno ya baadhi ya mashabiki wa msanii huyo kwa waandishi wa habari.

Mrembo huyo wa filamu anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba tukio linalodaiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka 2012.

FFU Watuliza Vurugu za Abiria wa Fast Jet Zaleta

$
0
0
FFU Watuliza Vurugu za Abiria wa Fast Jet  Zaleta
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU) leo wamelazimika kuingilia kati kutuliza vurugu zilizoazishwa na abiria 75 waliokosa usafiri wa ndege ya kampuni ya FastJet kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kutokana na hitilafu za kiufundi.

Abiria hao waliokaa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa nne kuanzia saa 3:00 asubuhi walipotakiwa kusafiri hadi saa 7:00 mchana, walianzisha vurugu kushinikiza kupatiwa usafiri.

Wakizungumza na Mwananchi uwanjani hapo kwa nyakati tofauti, abiria Rukia Mohamed, Juma Kisombi na Mamad Mohamed wamesema walilazimika kuushinikiza uongozi wa kampuni hiyo kuwapa maelezo ya kutosha baada ya ahadi ya kutakiwa kusubiri kidogo kutotekelezwa kwa zaidi ya saa tatu waliyosubiri uwanjani hapo.

“Nimefika Jumapili iliyopita na leo, nilitakiwa kurejea jijini Dar es Salaam na nilifika uwanjani kwa muda uliotakiwa lakini hadi sasa hakuna ndege na uongozi hautoi maelezo ya kueleweka,” alilalamika Rukia.

Akizungumzia kadhia hiyo, Meneja wa FastJet Mkoa wa Mwanza, Ezekiel Manyiga amesema ndege iliyotakiwa kusafirisha abiria hao haikufika kutoka jijini Dar es Salaam kutokana na kupata hitilafu ya kiufundi.

“Hata abiria waliotakiwa kusafiri kutoka Dar es Salaam kuja Mwanza hawajafika hadi sasa; tunafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kutatua tatizo hili,” amesema Manyiga

Ilipofika saa 7:00 mchana jana, uongozi wa kampuni hiyo ulifikia uamuzi wa kuwarejeshea nauli abiria waliokuwa tayari kupokea fedha zao ili kutafuta usafiri mwingine pamoja na Sh30, 000 ya kujikimu kwa kila abiria aliyekosa usafiri.

“Watakaokuwa tayari kusubiri ndege yetu watalazimika kusafiri kesho (Jumatano)  kwa sababu ndege tayari imejaa,” amesema Manyiga

Rapper Mkali wa Kike Bongo Rosa Ree Atoa Wimbo Mpya Unaoitwa Dow..Usikilize na Kudownload Hapa

$
0
0
Rapper Mkali wa Kike Bongo Rosa Ree Atoa Wimbo Mpya Unaoitwa Dow..Usikilize na Kudownload Hapa


Jeshi la Polisi Latoa Tamko Mauaji Askari Ukonga

$
0
0
Jeshi la Polisi Latoa Tamko Mauaji Askari Ukonga
Jeshi la Polisi Kanda Maalum jiini Dar es salaam, limesema linalaani vikali vitendo vya mauaji ya askari wake wa kikosi cha kutuliza ghasia Ukonga, yaliyotokea sikuchache zilizopita.

Taarifa hiyo imetolewa na  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ambapo pia amelaani vikali kitendo cha askari wa jeshi la polisi kuvamia wananchi na kuwapiga, akisema si jambo sahihi kwa askari kufanya hivyo na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
"Tunalaani vikali mauaji ya askari wa polisi wa FFU kikosi cha Ukonga, lakini sambamba na hilo jeshi la polisi linalaani vitendo vya kihuni vya wananchi kushambuliwa, kuna watu wahuni ambao wanasambaa usiku wanakamata wananchi, kuwapiga na kuwadhalilisha kina mama na wengine kujeruhiwa, hakuna askari wa jeshi la polisi aliyefundishwa anayeweza kuyafanya hayo yanayoelezwa kufanyika, na kama atabainika ni kweli ni askari, watakamatwa, watahojiwa na tutawashughulikia kijeshi na kama wahalifu wengine watafikishwa mahakamani", amesema Kamanda Mambosasa.
Kamanda Mambosasa ameendelea kwa kusema kwamba jeshi hilo linaendelea na upelezi dhidi ya watu waliomuwa askari wake Charles Yanga wa kikosi cha Ukonga, na watakapobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images