Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Polisi Wawili Wauawa kwa Kupigwa Risasi

$
0
0
Polisi Wawili Wauawa kwa Kupigwa Risasi
Polisi wawili waliokuwa kituo cha Polisi Kayole Nairobi wameuawa kwa kupigwa risasi na kisha wauaji kuondoka na bastola walizokuwa nazo

Maafisa polisi wenzake kutoka kambi ya polisi ya Kirima waliikuta miili yao barabarani asubuhi ya leo
Mafisa hao wametambuliwa kuwa ni Konstebo Linus Inima and James Gitahi.

Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga uchaguzi na eneo la Kayole huko Nairobi ni kati ya maeneo yaliyoathiriwa na vurugu hizo, ila haijajulikana kama mauaji ya polisi hao yanahusiana na uchaguzi

Inakuwaje Kuna Pato la Taifa Linakuwa Wakati Wananchi Wanalalamika Hali Mbaya Vyuma Vimekaza- Zitto Kabwe

$
0
0
Inakuwaje Kuna Pato la Taifa Linakuwa Wakati Wananchi Wanalalamika Hali Mbaya Vyuma Vimekaza- Zitto Kabwe
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Mh.Zitto Kabwe amesema kuwa wanasikia pato la taifa linakuwa na ni miongoni kati ya nchi 20 ambalo pato la taifa lina kuwa kwa kasi wakati anasikia malalamiko ya wananchi wanasema hali mbaya na vyuma vimekaza.

Zitto ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu Takwimu za pato la Taifa amesema kuwa ni wajibu wa mchumi kujiuliza inakuaje tuna pato la taifa linalokuwa yani miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi sana lakini wakati huo huo wananchi wanalia.

“Tunasikia pato la taifa linakuwa na ni miongoni kati ya nchi 20 ambalo pato la taifa linakuwa kwa kasi kuliko nchi zingine lakini wakati huo huo mnasikia malalamiko ya wananchi wanasema hali mbaya, vyuma vimekaza sasa ni wajibu wa mchumi kujiuliza inakuaje tuna pato la taifa linalokuwa yani miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi sana lakini wakati huo huo wananchi wanalia kwamba vyuma vimekaza kwamba hali ni mbaya,” amesema Zitto.

“Kwanini sasa miaka ya nyuma tulikuwa hatutazami na kwakweli hata tulipotazama safari hii tumekuta miaka ya nyuma hakuna shida yani mpaka mwezi Machi 2017 takwimu zilizokuwa zinatolewa na serikali na takwimu ambazo unazikokotoa kutokana na hali ya uchumi na kanuni za uchumi hazina utofauti zilikuwa sawa kabisa lakini takwimu za mwezi AprilI,Mei,June zimeonyesha tofauti kubwa sana na ndicho kilicho tuletea mashaka.”

Hivi Hapa Vikosi Vya Simba, Yanga Vitakavyoonyeshana Ubabe Leo

$
0
0
Hivi Hapa Vikosi Vya Simba, Yanga Vitakavyoonyeshana Ubabe Leo
Hivi ndivyo ikosi viwili vya watani wa jadi ambavyo vinatarajiwa kuonyeshana ubabe leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam

KIKOSI CHA YANGA:

1. Youthe Rostand

2. Juma Abdul

3. Gadiel Michael

4. Andrew Vicent

5. Kelvin Yondani

6. Papy Tshitshimbi

7. Pius Buswita

8. Raphael Daud

9. Obrey Chirwa

10. Ibrahim Ajibu

11. Geofrey Mwashiuya


KIKOSI CHA SIMBA
1. Aishi Manula

2. Erasto Nyoni

3. Mohamed Zimbwe (C)

4. Juuko Murshid

5. Method Mwanjale

6. Jonas Mkude

7. Shiza Kichuya

8. Muzamiru Yassin

9. John Bocco

10. Emmanuel Okwi

11. Haruna Niyonzima

RC Makonda Atoa Agizo kwa Jeshi la JWTZ Kujenga Daraja Lililosombwa na Maji Kawe

$
0
0
RC Makonda Atoa Agizo kwa Jeshi la JWTZ Kujenga Daraja Lililosombwa na  Maji Kawe
MKUU wa Mkoa wa Dar es Saalam, Paul Makonda, ametembelea daraja lililokatika Kawe, na kuwapa pole wananchi wa eneo hilo kutokana na athari na hasara walizozipata kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea jijini Dar.
Aidha Makonda amewasihi wananchi waishio maeneo hatarishi kuhama haraka iwezekanavyo, ili kunusuru maisha yao, wasinga’nga’nie kulinda Tv wakati maisha yao yako hatarini.
Katika hatua nyingine Makonda amewaagiza Jeshi la Wananchi Tanzania [JWTZ] Kujenga daraja la muda katika eneo hilo ili kupunguza usumbufu na kuwarahisishia wananchi waweze kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine, huku mamlaka inayohusika na barabara TAMROADS Wakiendelea na ujenzi wa muda mrefu.
Chanzo Global Publishers

Video: Jot Aumwaga Ukapela Afunga Ndoa Leo

$
0
0

Muigizaji wa vichekesho nchini kutoka kundi la Orijino Komedi, Joti ameuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake katika Kanisa Katoliki la Magomeni jijini Dar.
Chanzo Global Publishers

Lazima Mwakani Nipate Mtoto Mungu Akinijaalia- Gigy Money

$
0
0
Lazima Mwakani Nipate Mtoto Mungu Akinijaalia- Gigy Money
Msanii wa muziki na video vixen Bongo, Gigy Money amesema mwakani anatarajia kupata mtoto.

Gigy ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Papa’ ameiambia E Fm Radio kuwa hicho ni kitu ambacho yeye na mpenzi wake wameshakaa na kukijadili.

“Watengemee tu mwakani nitakuwa na mtoto Mungu akinisaidia, yaani hiyo ni lazima” amesema Gigy Money.

Katika hatua nyingine Gigy Money ameongeza kuwa huu ni mwaka wa tatu yupo na mpenzi wake hivyo ni muda sahihi kufanya hivyo.

Ni Wakati Hivi Vikundi vya Maombi Vipigwe Marufuku- Alberto Msando

$
0
0
Ni Wakati Hivi Vikundi vya Maombi Vipigwe Marufuku- Alberto Msando
Wakili Maarufu Alberto Msando amefunguka na kusema kuwa anatamani baadhi ya vikundi vinavyoanzishwa kwa ajili ya maombi vipigwe marufuku kwani watu waonzisha vikundi hivyo wanalenga kujitafutia pesa na huku wananchi wa hali ya chini wakizidi kuumia.

Msando amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram baada ya Nabii mmoja nchini Tanzania kuuandaa ibada ya maombi ya kuvunja laana ya kutembea kwa miguu huku akiwaahidi watu wote watakaofika kwenye misa hiyo watapata baraka na kupata magari na kusema magari yao yameshikiliwa na shetani baharini.
"Na kuna watu wataenda. Kuna watu wataamini masuala ya imani ni magumu sana ila kadri siku zinavyozidi kwenda haya mambo yanaongezeka. Hali ngumu ya maisha inasababisha baadhi ya watu kuamini kila kitu. Na wanaoanzisha hivi vikundi vya maombi wanafaidika sana. Ni wakati baadhi ya vikundi vipigwe marufuku" alisisitiza Msando

Tecno Yazindua Simu Mpya TECNO Phantom 8 Leo

$
0
0
Tecno Yazindua Simu Mpya TECNO Phantom 8 Leo
Kampuni kubwa ya simu za mkononi TECNO iliyopo chini ya TRANSSION HOLDINGS , imetambulisha rasmi simu yake mpya  katika harakati zake za kukuza soko katika nchi za Asia na Africa, TECNO Phantom 8 katika jiji la Dubai.

Matumizi ya smartphone yanakua kwa kasi katika maeneo ya nchi za kiafrika na za mashariki ya kati kwa kiasi cha milioni 123. 7 mpaka 2016 toka milioni 106.4 mwaka 2015.

“Hivi karibuni ripoti zinaonyesha kwa kiasi kampuni imeweza kupenya katika soko na kuleta ushindani  katika bara la Afrika na mashariki ya kati” Alisema makamu wa rais wa kampuni mama TRANSSION HOLDINGS, Arif Chowdhury. “Mipango yetu ni mwaka jana ilikua kukua zaidi kupitia mashariki ya kati hivyo kuzindua rasmi Phantom 8 jiijini Dubai ni hatua mojawapo katika kuendeleza mipango hii. Simu zetu zitaendelea kujikita katika kufuata mahitaji ya wateja zaidi”. Alimaliza Makamu wa raisi.

TECNO Mobile inaendelea kutoa bidhaa zenye ubora kwa wateja wake hasa barani Africa ambapo kampuni hiyo ina nafasi kubwa katika mauzo hasa kwa nchi kama Tanzania na Nigeria na nchi kadhaa kutokea mashariki ya kati.

Kwa zaidi ya miaka 11 TECNO imekua ikifanya kazi ya kuunganisha wananchi katika mawasiliano kupitia simu hasa kwa kuleta simu zenye ubora na bei inayoendana na watumiaji wake.

Simu hiyo iliyozinduliwa jijini Dubai imekua gumzo tangu tetesi zitoke kua inakuja sokoni imezinduliwa ikiwa na jina la Phantom 8  huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia kubwa hasa kwa upande wa kamera ikiwa na megapixel 20 mbele na kamera mbili nyuma6 GB RAM  na ROM ikiwa ni 64GB. Kwa upande wa dizaini simu inametengenezwa vizuri ikiwa na muundo wa mithili ya Almasi na kioo.

Phantom 8 kutarajiwa kufika mabara mengine pia duniani.

Phantom 8 inauwezo wa kuweka “simcard” aina ya “Nano/ Micro” na inauwezo wa kumud memory card ya hadi 2TB (Terra Bytes) na pia inauwezo wa 4G plus ambayo inakuwezesha kutumia simu yako ndani na Zaidi ya nchi 200.

Kwa wateja waliopo Tanzania wataweza kuagiza simu hii mpya katika maduka maalumu ya simu za TECNO ili kuweza kuipata inapoingia sokoni siku chache zijazo.

Phantom 8 iliyozinduliwa hivi karibuni iikiwa imesheheni na sifa za kipekee kama Kamera, Ubo na muonekano wa kipekee pamoja na kasi ya ajabu. Kamera ikiw ana uwezo wa 20 MP, pamoja na kamera pacha zenye uwezo wa 13Mp +12 Mp kamera za nyuma ikiambatana na uwezo wa kuvuta picha mara 10 zaidi ya kamera ya kawaida, Ina uwezo wa HDR,4 in 1 uwezo wa kungarisha picha,AF na mambo mengine mengi yenye kukuhahkishia kupata picha zilizo bora na zenye muonekano mzuri.



Marekani Yaitaka DR Congo Kufanya Uchaguzi 2018

$
0
0
Marekani Yaitaka DR Congo Kufanya Uchaguzi 2018
Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Nikki Haley, ameiambia Jamhuri ya kidemokrasi uya Congo kufanya uchaguzi uliocheleweshwa 2018.
Bi Haley alionya kuwa usaidizi wa Marekani kwa taifa hilo uko hatarini iwapo hatua hiyo haitatekelezwa.

''Uchaguzi lazima ufanyike 2018 la sivyo DR Congo isitarajie msaada wowote kutoka kwa Marekani na jamii ya kimataifa', aliripotiwa na chombo cha habari cha AFP akisema.
Alitoa matamshi hayo baada ya kukutana na Corneille Nangaa mkuu wa tume ya uchakuzi nchini humo.

Uchaguzi ulitarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2016, lakini tume hiyo ya uchaguzi ukauahairisha kufuatia ukosefu wa mipango na fedha.

Marekani imesema kuwa mbali na maswala mengine ya kutia wasiwasi ya usalama ni mgogoro unaeondelea katika jimbo la kati la Kasai.
Tume hiyo wiki mbili zilizopita ilitangaza kwamba tarahe ya karibu ambapo taifa hilo linaweza kuandaa uchaguzi ni mwezi Aprili 2019.
Maandamano ya upinzani yamefanyika katika maeneo mbali mbali nchini humo dhidi ya kuongezwa kwa muda wa kutawala wa rais Kabila.

Bwana Kabila alitarajiwa kuachia madaraka mnao mwezi Disemba 2016 lakini katika makubaliano yaliofikiwa na viongizi wa kanisa katholiki, ilikubalika kwamba ataondoka afisini mwisho wa 2017.

Ni Kweli Mapenzi ya Wizi ni Matamu Kuliko Katika Ndoa Halali?

$
0
0
Ni Kweli Mapenzi ya Wizi ni Matamu Kuliko Katika Ndoa Halali?
Mapenzi ni kitu ambacho kinafanya wapenzi kufurahia wakiwa pamoja lakini kwa sasa kumekuwepo kwa kusalitiana katika mahusiano.

Imekuwa kama kawaida mwanamke/mwanaume kuwa na mchepuko huku tayari yupo kwenye ndoa yake.
Kwa nyakati za sasa uzinifu si kitu cha ajabu tena.Wahusika wanadai kufaidi uasherati kuliko tendo la ndoa.Kumekuwepo kuchokana kwa wawili walio katika ndoa na kufanya mmojawapo ajaribu kutafuta kuridhishwa nje ya ndoa.Jamii yahitaji kuelimishwa juu ya kuridhishana katika ndoa kwani itafikia mahali ndoa itakuwa ni ya jina tuu.

Tusaidiane katika Kushauriana  Unafikiri nini chanzo cha utamu wa mapenzi ya kuchepuka kuliko mapenzi ya ndoa halali?

Fahamu Madhara ya Kufanya Mapenzi Kipindi Mwanamke akiwa na Hedhi

$
0
0
Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana..Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si madhuri kwa afya ya wote wawili.Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi...Zifuatazo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati KE yupo katika siku zake{period}..

 MADHARA KWA MWANAUME.
1.Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.

 2.Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.

 3.Kuziba kwa njia ya mkojo.

 4.Utasa au ugumba.

 5.Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.

 6.Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.

MADHARA KWA MWANAMKE.
1.Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID( PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

 2.Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).

 3.Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.

 4.Utasa au Ugumba.

 5.Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.

 6.Athari mbaya ya kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe hamjali wala mpendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.Pia kuona kuwa mumewe ajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume anataka KU-DO.
NOTE
 Hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.

Je Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa..Jibu Lipo Hapa

$
0
0
JE,UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZAKIUME,KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA,KUFIKA KILELENI MAPEMA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA UA MAUMBILE MADOGO YA UUME?



Tatizo la kukosa au kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya kiume husababishwa namambo mengi kama,KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURLUMA,MAUMIVU YA KIUNO,UNENE KUPITA KIASI,KUJICHUA(MASTER BLASHION)HOMON Hishindwa kufanya kazi inavyotakiwa nk.upungufu wa nguvu za kiume husababisha tendo la ndoa kutofanyika kwa kujiami nakwa usahihi nahivyo husababisha ndoa mahusiano mengi kuvunjika.BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI,1KUKOSA HAMU YA TENDOL LA NDOA 2 UUME KISIMAMA KWA KULEGEA 3 KUWAHI KUFIKA KILELENI 4 KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA WAKATI 5 KUCHOKA SANA BAADA YA ROUND YAKWANZA NAKUKINAI TENDO NDOA KABISA.TUMIA 3 POWER KWA TATIZO LA UKOSEFU(UPUNGUFU)WA NGUVU ZA KIUME NAHAMU YA TENDO LA NDOA.FINA HUBORESHA MAUMBILE YA KIUME KWA KUNENEPESHA KWA SAIZI UIPENDAYO HAIJARISHI UMRI.PIA KUNA DAWA ZA KURUDISHA MPENZI KWA MUDA MFUPI SANA NAZAKUPATA KAZI,KESI,KUDHULUMIWA,NK WASILIANA NA SHEIKH OMARY AKUTATULIE MATATIZO YAKO HATA KAMA UMEHANGAIKA SANA PASIPO MAFANIKIO UMEFANIKIWA LEO

Pia sheikh omary anatibu busha bila opresheni,kisukari,ngiri,presha,vidonda vya tumbo,korodani kivimba nakuuma,na anatoa ndagu za utajiri kwa wanaohitaji utajiri bila masharti yoyote magumu.ANAPATIKANA DAR ES SALAAM NAUTALETEWA POPOTE ULIPO TIBA HII UKIWA HAUNA NANAFASI YAKUFIKA OFISINI,

PIGA SIMU NO 0767 14 53 57/0629 03 45 5

VIDEO:Serikali imedanganya Pato la Taifa - Zitto Kabwe

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amefunguka na kuelezea namna ambavyo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyodanganya juu ya Takwimu za pato la Taifa.

Zitto Kabwe amesema kuwa katika uchambuzi na uchunguzi ambao wamefanya wamegundua kuwa Pato la Taifa la Tanzania lilisinyaa kati ya mwezi wa April na June 2017 tofauti na Taarifa ya Serikali iliyotolewa karibuni.
Mtazame hapa Zitto Kabwe akifafanua zaidi juu ya jambo hili.

Ndoa ya Irene Uwoya, Marufuku Kuingia na Simu Ukumbini.

$
0
0
Baada ya Irene Uwoya kufunga ndoa Jana japo bado mume aliyefunga Naye hajamuweka wazi rasmi japo kuna uvumi ni Dogo Janja. Kutokana na watu waliohudhuria sherehe Hiyo.

Jambo la kushangaza lililowaudhi waudhuriaji ni ile Hali ya kuzuia watu wasiingie na simu ukumbini na kukataza watu kupiga picha ukumbini na kulikuwa na mabaunsa Ambao walisimamia zoezi hili ipasavyo.

Simba na Yanga Watunishiana Misuli

$
0
0
Mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba ligi kuu soka Tanzania bara raundi ya nane umemalizika jioni hii kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaa kwa sare ya bao 1-1.

Simba ambao walikuwa wageni kwenye mchezo huo ndio walianza kutikisa nyavu za wenyeji wao Yanga kwa bao la Shiza Kichuya dakika ya 57 lililopatika baada ya Emanuel Okwi kugongeana vyema na Haruna Niyonzima kisha Kichuya kupachika bao hilo.

Yanga hawakutoka mchezoni baada ya bao hilo badala yake walifanya shambulizi la haraka haraka na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 60 kupitia kwa Obrey Chirwa ambaye aliitendea haki pasi ya Godfrey Mwashiuya iliyotokana na kazi nzuri ya Ibrahim Ajibu.

Baada ya hapo timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini hakuna timu ambayo ilifanikiwa kuongeza bao hivyo hadi mwisho wa mchezo timu hizo zimetoka sare ya 1-1, na kugawana alama moja moja.

Matokeo hayo sasa yanaiacha Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara VPL msimu wa 2017/18 ikiwa na alama 16 sawa na Yanga na Azam FC ambazo pia zina alama 16 zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga.

Yanga inabaki kwenye nafasi ya pili huku Azam FC ikisogea hadi nafasi ya tatu baada ya jana kushinda dhidi ya Mbeya City na kuongoza ligi kwa muda. Mtibwa Sugar inayo nafasi ya kuongoza ligi endapo itashinda mchezo wake wa kesho dhidi ya Singida United ambapo hadi sasa ina alama 15 hivyo itafikisha alama 18.

Goli la Kichuya limenunuliwa kwa Tsh. 500,000

$
0
0
Mashabiki wa Simba kundi la Simba Kwanza (SK) wamekabidhi shilingi 500,000 Shiza Kichuya baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ‘Man of the Match’ ikiwa ni kutokana na goli alilowafunga watani wao wa jadi mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Mashabiki hao wamemchagua Kichuya kuwa Man of the Match wakiwa wameridhishwa na kiwango alichokionesha kwenye mchezo huo.

Kichuya aliifungia Simba bao la kuongoza lakini baadae goli hilo lilisawazishwa na Obrey Chirwa na kulazimisha timu hizo za Kariakoo kugawana pointi.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo amesema, huo utakuwa ni utaratibu wao wa kila mechi kutoa zawadi ya pesa kwa mchezaji atakaefanya vizuri kwenye mechi.

Ameahidi kuwa, mechi ijayo ya Simba (Mbeya City vs Simba November 5, 2017) watatoa kisasi cha shilingi 2,000,000.

Wachezaji Okwi na Ajibu Washindwa Kufurukuta Kama Ilivyodhaniwa

$
0
0
Mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba ligi kuu soka Tanzania bara raundi ya nane umemalizika jioni hii kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaa kwa sare ya bao 1-1.

Simba ambao walikuwa wageni kwenye mchezo huo ndio walianza kutikisa nyavu za wenyeji wao Yanga kwa bao la Shiza Kichuya dakika ya 57 lililopatika baada ya Emanuel Okwi kugongeana vyema na Haruna Niyonzima kisha Kichuya kupachika bao hilo.
Yanga hawakutoka mchezoni baada ya bao hilo badala yake walifanya shambulizi la haraka haraka na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 60 kupitia kwa Obrey Chirwa ambaye aliitendea haki pasi ya Godfrey Mwashiuya iliyotokana na kazi nzuri ya Ibrahim Ajibu.

Baada ya hapo timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini hakuna timu ambayo ilifanikiwa kuongeza bao hivyo hadi mwisho wa mchezo timu hizo zimetoka sare ya 1-1, na kugawana alama moja moja.
Matokeo hayo sasa yanaiacha Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara VPL msimu wa 2017/18 ikiwa na alama 16 sawa na Yanga na Azam FC ambazo pia zina alama 16 zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga.

Yanga inabaki kwenye nafasi ya pili huku Azam FC ikisogea hadi nafasi ya tatu baada ya jana kushinda dhidi ya Mbeya City na kuongoza ligi kwa muda. Mtibwa Sugar inayo nafasi ya kuongoza ligi endapo itashinda mchezo wake wa kesho dhidi ya Singida United ambapo hadi sasa ina alama 15 hivyo itafikisha alama 18.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumapili

Bifu ya FA,Lady Jaydee Imenisumbua Sana Ila Nilijua Ipo Siku Watamaliza Tofauti- AY

$
0
0
Bifu ya FA,Lady Jaydee Imenisumbua Sana Ila Nilijua Ipo Siku Watamaliza Tofauti- AY
Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva nchini AY amefunguka na kusema kuwa bifu kati ya msanii Mwana FA na Lady Jaydee yeye ilikuwa inamsumbua sana na kusema aliamini ipo siku wanaweza kumaliza tofauti zao.

AY amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kusema kuwa kwa kuwa yeye alikuwa ni rafiki wa wasanii hao wote hivyo ilikuwa inampa ugumu kuona watu hao wanashindwa kupiga hata stori.

Watu Milioni 3 Wamo Hatarini ya Kufaa Nja DRC

$
0
0
Watu Milioni 3 Wamo Hatarini ya Kufaa Nja DRC
Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni tatu wamo katika hatari ya kufa njaa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kiongozi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia mpango wa chakula Duniani- WFP, ametoa wito wa msaada wa dharura wa kimataifa, ili kumaliza matatizo ya baa la njaa, nchini DR Congo.

David Beasley, ambaye anafanya ziara yake ya kwanza kabisa, katika jimbo linalokumbwa na msukosuko wa mapigano na uasi la Kasai, ameiambia BBC kuwa, zaidi ya watu milioni tatu, wanakabiliwa na baa la njaa.

Anasema kwamba, timu ya wafanyikazi wake, wameshuhudia watoto ambao wanakabiliwa na matatizo ya utapia mlo, huku mamia kwa maelfu yao, wakiwa katika hatari ya kufa, katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo, ikiwa msaada hautawafikia.

Mapigano mabaya yalianza katika jimbo hilo la Kasai mwezi Agosti mwaka 2016, baada ya kiongozi mmoja wa kitamaduni kuuwawa, katika mapigano na wanajeshi wa kulinda amani.
Ghasia mpya imesababisha mauwaji ya watu elfu tatu na kuwafurusha zaidi ya watu milioni moja, wengi wao wakiwa ni watoto kutoka nyumbani kwao.
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images