Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Baba Mzazi wa Joti Amfunda Mwanae Tulia Kwenye Maisha Yako ya Ndoa Mimi Nina Vituko Kuliko Wewe

0
0
Baba Mzazi wa Joti Amfunda Mwanae Tulia Kwenye Maisha Yako ya Ndoa Mimi Nina Vituko Kuliko Wewe
Baba mazazi wa Joti amemtaka mwanaye kuwa mtulivu katika maisha yake ya ndoa huku akidai yeye alikuwa navituko hata mkuzidi mtoto wake huyo lakini aliamua kutulia ili kuendesha maisha yake. Mzee huyo amesema hayo wakati wa sherehe ya ndoa ya mtoto wake huyo iliyofanyikia Mlimani City Dar es salaam ambapo  pia amemtaka Joti kuomba msamaha pindi anapomkosea mke wake.


CUF Wagoma Maalim Seif Kupimwa Akili

0
0
CUF Wagoma Maalim Seif Kupimwa Akili
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, Ahmed Nassor Mazrui amesema Katibu Mkuu wa CUF hatopimwa akili na wale wanaosema Maalim Seif Shariff Hamadi akafanyiwe uchunguzi huo ni vyema wakaenda wao.

Mazrui alisema Maalim Seif hawezi kupimwa akili kwa kuwa yupo ngangari na ana akili timamu kwa kila anachokifanya; kwa maslahi ya chama na Wazanzibari kwa ujumla.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa wilaya ya Mjini wa chama hicho hapa Zanzibar juzi, Mazrui alisema Maalim Seif ni mwenye akili timamu na kutaka wote wanaotoa madai hayo ya kupima akili wapuuzwe.

Alisema kuonyesha katibu huyo ni mwenye akili timamu amekuwa akigombea nafasi ya urais ndani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 25 bila ya kuchoka, kutetereka wala kukata tamaa.

Alisema katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Maalim Seif ndiyo nguli wa siasa na kuwataka wafuasi wa chama hicho kutovunjika moyo kwani kiongozi wao huyo yupo makini na anaendelea kuidai haki ya Wazanzibari "iliyoporwa" Oktoba 25, 2015.

Matokeo ya awali ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa 2015 yalionyesha Maalim Seif alikuwa akiongoza katika kinyang'anyiro hicho ambacho waangalizi wa kimataifa, ikiwemo Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Ulaya na Marekani, walidai kilifanyika kwa haki na amani.

Hata hivyo, uchaguzi huo wa rais na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ulifutwa kwa Tume ya Uchaguzi (ZEC) kwa maelezo kuwa ulikuwa na kasoro nyingi za msingi, ikiwemo idadi ya kura katika baadhi ya vituo kuvuka jumla ya wakazi waliojiandikisha.

“Mwenye kusubiri hajutii," alisema Mazrui, "kwa hivyo (wanachama) vuteni subra".

"Mambo yapo, sisi watendaji wakuu tushajiandaa kuchukua serikali.”

Aliwataka wafuasi hao kutoyumba wala kurudi nyuma na badala yake kumuunga mkono Katibu Mkuu ambaye alidai anafanya kazi kubwa ya kudai na kutetea haki ya Wazanzibari.

“Niwaombe wafuasi wa CUF musirudi nyuma, atakayerudi nyuma atakuja kuchujwa kwa chujio na kuachwa nyuma.”

Aidha, Mazrui alisema licha ya migogoro na usaliti mkubwa unaofanywa na baadhi ya watu kwa chama hicho, bado CUF haijatetereka na ipo imara.

Alisema CUF inaendelea na vikao vyake kama kawaida na chama hicho kinasonga mbele licha ya kuwa hakina ruzuku kwa sasa.

Alisema chama hicho kinaendelea kupambana kwa kutumia njia sahihi bila ya kuwaangamiza wanachama wake kwani viongozi wa CUF wanafanya kila njia kusimamia haki na kudai mamlaka kamili ya Zanzibar.

Aidha, aliwataka wafuasi wa chama hicho kukosoana ndani ya vikao vya chama badala ya kusemana nje.

Mbivu Mbichi Leo Hatima ya Ubomoaji Mjengo wa Mchungaji Getrude Rwakatale

0
0
Mbivu Mbichi Leo Hatima ya Ubomoaji Mjengo wa Mchungaji Getrude Rwakatale
HATIMA ya ubomoaji wa nyumba ya kifahari ya Mchungaji wa kanisa la TAG Mikocheni, Getrude Rwakatare, inatarajiwa kuanza kujulikana leo wakati Naibu Waziri mpya wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Kangi Lugola atakapotoa ripoti.

Wiki iliyopita Lugola aliomba Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kumpatia taarifa ya kukwama mwaka jana kwa ubomoaji wa 'hekalu' hilo lililopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Rais John Magufuli alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Oktoba 7 ambapo miongoni mwa sura mpya ni Naibu Waziri Lugola ambaye amechukua nafasi ya Luhaga Mpina aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

"Taarifa tayari ipo ofisini kwangu (tayari) nitaipitia Jumatatu (leo)," alisema Lugola ambaye alikuwa kwenye ziara mikoani wakati akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki. "Umma unataka kujua, hivyo siyo jambo la kucheleweshwa."

"Niliagiza nipatiwe taarifa ya tangu (sakata) ilivyoanza ili nijue ugumu (wa kubomoa) umetokana na nini halafu nitakwenda kushauriana na waziri wangu kile kilichojiri katika hiyo taarifa."

Mwanasheria wa NEMC, Heche Suguta alithibitisha kutekeleza agizo la naibu waziri kwa kuwasilisha taarifa ya jengo hilo liliopo kwenye viwanja namba 2019 na 2020 ofisini kwake.

"Siwezi kuzungumza chochote lakini alichokitaka waziri wangu tulitekeleze kabla ya muda aliotupatia," alisema Suguta ambaye pia alikuwa msimamizi mkuu wa bomoabomoa hiyo. "Tayari tumefanya hivyo."

Mchungaji Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kwa kipindi cha pili, alihamia katika hekalu hilo Agosti 30, 2012 ambapo taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinasema waumini wa kanisa lake wapatao 300 walifika kushuhudia sherehe ya uzinduzi wa nyumba hiyo.

Nyumba hiyo ni moja kati ya 8,000 zilizokuwa zibomolewe mwishoni mwa mwaka 2015 katika operesheni maalum ya kuondoa makazi kwenye fukwe, kingo za mito, maeneo ya wazi na mabondeni.

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Wakala wa Misitu (TFS) iliweka alama ya X kwenye kuta za nyumba hiyo wakidai imo katika hifadhi ya Bahari ya Hindi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria, na kwamba pia imejengwa kwenye hifadhi ya mikoko.

Iliachwa baada ya mchungaji huyo kwenda mahakamani kufungua kesi ya kusimamisha zoezi hilo akipinga madai kuwa imejengwa ndani ya mita 60 kutoka fukwe ya bahari.

Aidha, mmiliki huyo alidai ujenzi wa nyumba hiyo ulishajadiliwa na kesi yake kuhukumiwa na Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi ambayo ilimuona Mch. Rwakatare hakuvunja taratibu zozote za ujenzi. Hukumu hiyo ilitolewa Mei 22, 2015.

Dk. Rwakatare, ambaye pia alikuwa mbunge wa viti maalumu kwenye Bunge lililopita, alipoteza nyumba nyingine nne zilizokuwa kwenye kiwanja namba 314 Mbezi Beach baada ya kubomolewa kwa tuhuma za kuvamia eneo hilo.

Hatimaye Mmoja wa Watoto Pacha Waliotenganishwa India Afungua Macho

0
0
Hatimaye Mmoja wa Watoto  Pacha Waliotenganishwa India Afungua Macho
Mmoja wa watoto pacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikana kwenye vichwa amefungua macho yake siku nne baada ya upasuaji wa kuwatenganisha nchini India.
Jaga, mwenye umri wa miaka miwili aliweza kuitikia ishara ndogo kama kusongesha mikono yake.

Watoto hao walizaliwa wakiwa wanatumia kwa pamoja mishiba na nyama za ubongo na upasuaji uliochukua saa 16 uliwatenganisha.
Watoto hao wote wako hali nzuri na madaktari wameridhishwa na vile wanavyoendelea hadi sasa,
Pacha hao wanaotokea kijiji kilicho mashariki mwa jimbo la Orissa nchin India, walishikana kwenye kichwa hali inayofahamika kama craniopagus.

Craniopagus hukumba mtoto mmoja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa na asilimia 50 ya wale wanaopatwa na hali hiyo hufariki saa 24 baada ya kuzaliwa.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Ametembelea Kiwanda cha Bidhaa za Urembo

0
0
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Ametembelea Kiwanda cha Bidhaa za Urembo
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametembelea kiwanda ya bidhaa za urembo mjini Pyongyan akiandamana na mke wake Ri Sol-ju na dada yake Kim Yo-jing.

Kuoneka hadharani kwa Kim Yo-jong, kunakuja muda mfupi baada ya kupandishwa cheo ndani serikali ya Korea Kaskazini.
Bidhaa za urembo kutoka nchi za kigeni zimekuwa adimu nchini Korea Kaskani kutokana na vikwazo.

Korea Kaskazini inaonekana kujenga sekta yake ya bidhaa za urembo ambapo bidhaa kama Bomhyanggi na Unhasu vimepata umaarufu.
Licha ya umaarufu wake wa kupigwa picha akiwa katika vituo vya kijeshi na maeneo ya kufanyia majiribio makombora, ziara ya Kim katika kiwanda cha bidhaa za urembo ni moja ya propaganda ya kuhalalisha utawake wake kwa watu wa Korea Kaskazini.

Ziara hiyo "ni ya kuonyesha kuwa Korea Kaskazini inaweza kuwatunza watu wake na kuleta maendeleo kwa kiwango sawa na cha China na Korea Kusini," mdadisi wa masuala ya Korea Kaskazini Ankit Panda aliiambia BBC.
"Licha ya sisi kujua kuwa sio ukweli, ni muhimu kwa utawaka huo kuonyesha watu wake kuwa unaweza kuwapa bidhaa wanazozihitaji,"

Wakati wa ziara hiyo , Kim alikisifu kiwanda hicho kwa kuzalisha bidha za kiwango cha kimataifa, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la KCNA.

Mtibwa Suga Yashindwa Kuonyesha Ubavu Wake kwa Singida United

0
0
Mtibwa Suga Yashindwa Kuonyesha Ubavu Wake kwa Singida United
Mechi tano za raundi ya nane ligi kuu soka Tanzania bara zimemalizika  huku Mtibwa Sugar ikishindwa kupaa kileleni baada ya kulazimishwa sare tasa na Singida United.

Mtibwa Sugar imelazimishwa sare hiyo kwenye uwanja wake wa nyumbani hivyo kushindwa kukaa kileleni baada ya kufikisha alama 16 na kulingana na timu za Simba, Yanga na Azam FC.
Mechi nyingine za jana ni ile kati ya Kagera Sugar dhidi ya Ndanda FC ambapo Kagera Sugar imepata ushindi wake wa kwanza baada ya mechi 7, ikishinda mabao 2-1. Lipuli FC imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC.

Njombe Mji ikiwa nyumbani imelazimishwa sare tasa na Stand United huku Majimaji ikitoka sare ya bao 1-1 na Mwadui FC. Kesho kutakuwa na mchezo mmoja wa kukamilisha raundi ya nane kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Ruvu Shooting.Nafasi tano za juu kwenye msimamo zinashikiliwa na Simba yenye alama 16 ikifuatiwa na Yanga SC, Mtibwa Sugar na Azam FC zenye alama 16 pia. Singida United wanashika nafasi ya tano wakiwa na alama 13. Nafasi tatu za chini zinashikiliwa na Majimaji FC, Ruvu Shooting na Stand United zenye alama 5.

Hizi Hapa Faida na Maajabu Yanayotokana na Kunywa Maji ya Uvuguvugu Kila Asubuhi

0
0
Hizi Hapa Faida na Maajabu Yanayotokana na Kunywa Maji ya Uvuguvugu Kila Asubuhi
Inawezekana unatumia kikombe cha chai  au kikombe cha  kahawa kila siku asubuhi, wengi wao hutumia maji ya kawaida ili kuanza siku vizuri. Hivi vitu vimekuwa
ndio tabia ya kila siku , hata hivyo wachunguzi wanasema kunywa maji ya uvuguvugu  asubuhi wakati tumbo halina kitu unapata faida  za kiafya zaidi.

Madactari wanashauri kutumia maji ya uvuguvugu   yaliotiwa  liau au ndimu ili  kupunguza radical ndani ya mwili. Kutumia maji ya moto  inaongeza na kufungua utumbo ili kukufanya wewe upate haja kubwa kwa urahisi

Na hapa kuna faida 7  za vitu vinavyotokea katika mwili wako utakapoanza kutumia maji ya moto kila asubuhi.

1.Yanasaidia kuondoa Mikunjo.

Kunywa maji inakusaidia usizeeke mapema,hakuna mtu anaependa kuzeeka mapema.hata hivyo  sumu ndani ya mwili inaweza kukufanya uzeeke mapema. Wakati mwili wako unapotoa sumu  utapunguza magonjwa   na uzee. Maji ya  moto usaidia kuondoa sumu na yanasafisha kabisa. Zaidi sana  yanasaidia kurejesha cells za ngozi iwe inaonekana kuvutia na nyororo.

2.Huepusha maumivu.

Dawa ya nguvu  ya kutegemea kupunguza maumivu wakati wa hedhi ni maji ya moto, yanafanya misuli ya tumbo  irelax  na kupungua kwa maumivu. Maji ya moto husaidia mzunguko kapirali  na misuli katika mwili pia.

3.Yanasaidia kupunguza uzito.

Inawezekana unajaribu kupunguza uzito  na umesikia kuwa maji ya moto asubuhi yanaweza kuwa ni msaada mkubwa kwako. Hii ni kweli., maji ya moto yanaongeza joto la mwili, ambalo  linabadilisha ongezeko la  kiasi cha metabolic, kuongezeka kwa metabolic  mwili unakuwa na uwezo wa kuchoma carories siku nzima.

Kama ukianza na kunywa maji ya moto yenye limau. Utausaidia mwili wako kuvunja vunja mafuta  yalioko ndani.

4.Yanaboresha digestion.

Unapokunywa maji ya moto asubuhi unastimulate  digestion yako  na  kuusaidia mwili kuwa na digestion bora. Kunywa maji ya baridi ya ya kula chakula inaweza kusimamisha digestion yako, na mwili wako ukawa  na matatizo, maana maji yabaridi yana gandisha mafuta yalioko kwenye chakula na kufanya digestion iwe ngumu kwako. Ni bora ukatumia maji ya moto kuliko ya baridi.

5.Yanaboresha mzunguko wa damu mwilini.

Kunakuwa na mlimbikizo wa  mlolongo wa nervous na mlimbikizo wa mafuta mwilini , lakini unapotumia maji ya moto yanaenda kuondoa hio migandanizo. Hii process inaflash sumu yote  ndani ya mwili na kuufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri na kufanya misuli kupumzika.

6.Inasaidia Usivimbilwe.

Watu wengi wamekuwa wakivimbiwa na kujisikia vibaya kutwa nzima na hata kwenda kwa dactari kwa ajili ya matibabu, kuna wengine  husaidiwa kwa kupigwa   bomba ili kupata nafuu , hata kuanza kutumia dawa mbalimbali.

Ukianza kutumia maji ya moto asubuhi kabla ya kula kitu chochote utasaidia  movement  yote. Hutasikia kuvimbiwa wala kushindwa kupata haja kubwa. Utapata kwa raha mstarehe.

7.Yanakufanya Upate Usingizi Vizuri.

Unapotumia maji ya moto  wakati wa chakula cha usiku, na kabla ya kwenda kulala, utaufanya mwili wako kurelax na  kulainisha nerves zako. Hii itakufanya ulale vizuri na kuwa na utashi mzuri kwa ajili ya kuamka asubuhi.

Tumeona  faida 7 za kushangaza   ambazo zinaweza kutokea katika mwili wako utakapoanza kutumia maji ya moto kila asubuhi na jioni . Anza sasa kutumia maji ya moto kila siku ili uone faida  nzuri  tulizosoma hapo juu kwa ajili ya manufaa yako .

Mimi nimeanza  kujaribi na nimeona kuna faida, anza na wewe leo.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumatatu


Kwa Nini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo?

0
0
KWA NINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE  MADOGO?


Matatizo haya yame kuwa yakiwaathiri watu wengi sana kisaikolijia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wenzao kwa kawaida mwanaume ana takiwa awe na uume kuanzia inch(6_8)  vinginevyo mtu huyo atakuwa na matatizo.

Zipo sababu nyingi zinazo sababisha tatizo hilo  baadhi ni upungufu wa  vichocheo (Hormones za Getrogen) Ambazo  mwanaume akisha balehe vichocheo hivi huchochea  ukuaji wa  uume, chango husababisha NEVA ambayo huathiri misuri ya uume.

Ngiri ambayo Huleta maumivu ya tumbo kuunguruma  na kujaa guess, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri , miguu kufa ganzi, maumivu ya kiuno,upigaji wa punyeto sababu hizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembaba na mara kwa mara hipelekea kupunguka kwa nguvu za kiume na ham ya tendo la ndoa hukosekana na kuisha kabisa

NSUMBU:__Ni dawa dawa inayo zalisha hormones za Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.

NZAGI :--Ni dawa bora ya kurudisha  nguvu za kiume na kukupa hamu ya kurudia tendo la ndoa mara dufu utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4)bila hamu kuisha (kuchoka) dawa hii ni tiba kamili kwa matatizo hayo. Dawa hii pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk(15_30)kwa tendo moja la ndoa dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji kuanzia miaka(18_90)wana ruhusiwa kuzitumia

Pia tunatibu KISUKARI, PRESHA, PUMU, MALARIA SUGU, MIMBA KUHARIBIKA(Chango)

POWER :__Ni dawa ya mitishamba inaongeza hips, (makalio), miguu, ina punguza maziwa (chuchu). Ina toa harufu mbaya sehem  za siri Nk. Pia anazo dawa za  mvuto wa mapenzi,biashara, kurudishwa kazini, kumuita aliye mbali kwa mda mfupi tu OSTADH JUMA ANAPATIKANA MALARIA ZAKHIEM SIMU:_0769-597778 au 0784-002216 au 0627457957 Wote mnakaribishwa

Diamond Afunguka Kuhusu Fedha Anazotumia Kufanya Kolabo na Wasanii wa Marekani

0
0
Diamond  Afunguka Kuhusu Fedha Anazotumia Kufanya Kolabo na Wasanii wa Marekani
Diamond amefunguka kuhusu fedha anazowalipa wasanii wa Marekani kwa ajili ya kufanya kolabo.

Akiongea na Dizzim Online hit maker huyo wa Hallelujah amesema kuwa hakuna fedha yoyote ambayo amewahi kumlipa msanii yoyote wa nchi hiyo ambao tayari ameshafanya nao kolabo.

“Mimi sijawahi kulipa kolabo yoyote kwanza ya Marekani niliyowahi kufanya, sijawahi kulipa na ukichunguza kiundani kolabo zangu na Wamarekani siyo kitu ambacho ‘nimejishobokesha’ ni watu wenyewe ambao wanatokea kunikubali na kuupenda muziki ambao ninaufanya,” amesema Diamond.

Msanii huyo ameongeza, “Ndio maana unaona sometimes sipost naona kama sina haja ya kupost ikiwa wao wenyewe wanakuwa wanafurahi na wanapenda kupost kitu tunachokifanya. Sometimes naogopa kupost naonekana kama nitajishauwa, sitaki kuonekana hivyo, nataka nionekane pointi yangu kuuchukua muziki wa Tanzania kuupeleka mbali.”

Hivi Ndivyo Alivyojibu Baraka Da Prince Kuhusu Kufulia Baada ya Kutoka Katika Label ya RockStar4000

0
0
Hivi Ndivyo Alivyojibu Baraka Da Prince Kuhusu Kufulia Baada ya Kutoka Katika Label ya RockStar4000
Msanii wa muziki Bongo, Baraka The Prince amejibu tetesi za kuyumba kimaisha.

Tangu msanii huyo kuondoka katika label ya RockStar4000 kumekuwa na taarifa zinazodai msanii huyo kuyumba kiuchumi hadi kupelekea kuuza gari kitu ambacho amekikanusha.

“Sijawahi kufanya hivyo, kwanini niuze gari yangu sema hizi fununu, watu wanatengeneza mastori” amesema Barakah.

Barakah kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Sometime’ ikiwa ni ngoma ya pili kutoka chini ya label yake ‘Bana Music’ baada ya ile ya mwanzo ambayo ilikuwa ya Naj ‘Utanielewa’.

Rais Magufuli Ameondoka Dar Leo Kuelekea Mwanza Kwa Ziara ya Siku Mbili

0
0
Rais Magufuli Ameondoka Dar Leo Kuelekea Mwanza Kwa Ziara ya Siku Mbili
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo ameondoka Dar es salaam kuelekea Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Rais wa Jamhiuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa ma Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa na maafisa wengine wakati akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Oktoba 30, 2017 kuelekea Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Rais wa Wakurdi Nchini Iraq Massoud Ajiuzulu

0
0
Rais wa Wakurdi Nchini Iraq Massoud Ajiuzulu
Rais wa Wakurdi nchini Iraq Massoud Barzani amejiuzulu kufuatia mgogoro kati ya Wakurdi na utawala wa Iraq wa jimbo hilo kutaka kujitenga na kuwa huru.

Rais Massoud Barzani ameachia wadhifa huo wakati eneo hilo linapambana na serikali kufuatia uhuru wake.
Kupitia barua iliyosomwa kwa bunge la Kurdi, Bw. Barzani amesema kuwa hataomba kuongezwa muhula baada ya huu alionao ukiwa unatarajiwa kukamilika siku nne zinazokuja.
"Ninaomba bunge kukutana ili kujaza nafasi hiyo," alisema
Wakurdi walipiga kura mwezi uliopita kuitenga Kurdistan lakini Iraq inasema kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na sheria, kisha jeshi la Iraq likaanzisha oparesheni ya kuukomboa mji uliokuwa chini ya wakurdi wa Kirkuk na kuteka vituo vya mafuta vya mji huo.
Bwana Barzani amesema atasalia kuwa mpiganaji wa kurdi na atazidi kutetea mafanikio ya watu wa Kurdistan.
Bw Barzani aliingia ofisini mwaka 2005 baada ya kuhusika katika wajibu mkubwa wa kuunda eneo huru la Kurdistan lililo kaskazini mwa Iraq baada ya Saddam Hussen kuondolewa madarakani.

Rais Magufuli Amemuagiza Waziri Mbarawa Kupeleka Bilioni 9 Mwanza Katika Ujenzi wa Uwanja wa Ndege.

0
0
Rais Magufuli Amemuagiza Waziri Mbarawa Kupeleka Bilioni 9 Mwanza Katika Ujenzi wa Uwanja wa Ndege.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuamuagiza Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano profesa Makame Mbarawa kupeleka bilioni 9 Mwanza katika ujenzi wa Uwanja wa ndege.

Rais Magufuli ameagiza hilo leo Oktoba 30, 2017 akiwa jijini Mwanza wilayani Ilemela katika uzinduzi wa daraja la waenda kwa miguu la Furahisha ambapo ametaka fedha zaidi ya bilioni 9 zipelekwe Mwanza katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ili uwe uwanja wa kimataifa.
"Nimesikia kuwa mkandarasi anadai zaidi ya bilioni tisa, sasa Waziri naagiza mwambie huyo mkandarasi kuwa wiki hii atapata hizo fedha zote bilioni tisa kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, nataka uwanja huu uwe uwanja wa kimataifa akamilishe uwanja huu kabla sijamaliza muda wangu, kwani asipokamilisha ndani ya muda huo hapo atalala lele, nataka wafanyabishara wa samaki wasiende nchi zingine kwa ajili ya kusafarisha samakai zao' alisisitiza Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli amesema serikali yake imekusudia kujenga meli kubwa itakayobeba watu 1200, na tani za kutosha na magari katika ziwa Victoria. 
Rais Magufuli yupo jijini Mwanza katika ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo ziara hiyo imelenga kuzindua daraja la Furahisha ambalo tayari limeshazinduliwa na baadaye atazindua kiwanda.

Zitto Kabwe Yamemfika Hapa Aitaka Chadema Kuunganisha Nguvu Ili Kuing'oa CCM

0
0
Zitto Kabwe Aitaka Chadema Kuunganisha Nguvu  Ili Kuing'oa CCM
Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amevitaka vyama vingine vya upinzani ikiwemo CHADEMA, kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanaing'oa CCM kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani.

Zitto Kabwe ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni za kuelekea uchaguzi huo, na kusema kwamba wamegundua iwapo wataunganisha nguvu na kuachiana baadhi ya kata, watafanikisha kukitoa chama cha CCM, na hatimaye kutimiza malengo yao ya kushikilia kata hizo.

"Iwapo vyama vyote vya upinzani vikituachia sisi kugombea kata za Kijichi tutaishinda CCM, na iwapo sisi tukiwaachia kata ya Mbweni wataishinda CCM, tunaomba wenzetu tuweke nguvu ya pamoja, tushinde Kijichi na Salanga, tumefanya utafiti tumeona tuna nafasi kubwa ya kushinda Kijichi, tuna nafasi kubwa ya kugawa kura na wenzetu Mbweni”, amesema Zitto kabwe

Zitto Kabwe ameendelea kusema kwamba ...”Tunawaambia wenzetu kupitia nyie, tuna adui mmoja tu CCM, tuache majivuno, ushirikiane, na sisi tumeonyesha 'good faith' tumewaachia Mbweni, tunawaomba wa-extend hiyo good faith, na wakihitaji maada tutawasaidia, ili kwenye kata zote zinazofanya uchaguzi Dar es salaam CCM ishindwe”.
Hivi karibuni kunatarajiwa kufanyika chaguzi ndogo ndogo za madiwani katika maeneo mbali mbali nchini, kwa mujibu wa sheria na katiba za nchi.

Lamar: Producer wa Bongo Tunatoza Gharama za Chini Kimuziki Wasanii Wanatakiwa Wasapoti Producer Wao

0
0
Lamar: Producer wa Bongo Tunatoza Gharama za Chini Kimuziki Afrika Kwa Hiyo Wasanii Wanatakiwa Wasapoti Producer Wao
Producer wa muziki kutoka studio za Fish Crab, Lamar amesema producer wa Bongo wanatoza gharama za chini zaidi katika kurekodi ukilinganisha na nchini nyingine Afrika.

Kutokana na hilo Lamar ameshauri kuwa ni vema kwa wasanii kutoa sapoti kwa producer wa Bongo na si vinginevyo.

“Soko letu katika producers sisi ndio ambao tunatoza gharama za chini kimuziki Afrika, ukienda South Africa watu wanachajiwa mpaka dola 5,000 kurekodi lakini sisi gharama za juu sidhani hata kama inafika milioni mbili/tatu” Lamar ameiambia Bongo5.

“Kwa hiyo wasanii wanatakiwa wasapoti producer wao, unakuta msanii anaweza kwenda South Africa akalipia labda dola 3,000 kufanya wimbo lakini huku hataki kulipia hela hiyo au anataka bure” ameongeza.

Irene Uwoya Afunguka Kuhusu Kuolewa na Dogo Janja 'Nimeolewa na Mwanaume wa Ndoto Zangu'

0
0
Irene Uwoya Afunguka Kuhusu Kuolewa na Dogo Janja 'Nimeolewa na Mwanaume wa Ndoto Zangu
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi juu ya tetesi iliyopo mtaani kuhusu kuolewa na msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja na kusema ni kweli ameolewa na msanii huyo kwani ndiye mwanaume wa ndoto yake.

Irene Uwoya kupitia mtandao wake wa Instagram amethibitisha hilo na kusema kuwa anampenda sana msanii huyo na kudai huyo ndiye mwanaume wa ndoto yake hivyo anafurahi kuona wamefunga pingu ya maisha.
"Nimeolewa na mwanaume wa ndoto zangu, bado naendelea kulia na kutokwa na machozi ya kwa furaha. Dogo Janja nakupenda sana na nimefurahi kumaliza maisha yangu ya duniani nikiwa na wewe" aliandika Irene Uwoya.
Kufuatia ujumbe huu ni wazi kuwa Irene Uwoya atakuwa amejibu maswali ya watu wengi ambao walikuwa hawaelewi nini kinaendelea kufuatia tetesi kuwa watu hao wamefunga ndoa siku za karibuni.


Breaking News: Lazaro Nyalandu Amejiuzulu Nafasi Yake Ndani ya CCM na Kuomba Kuungana na Chadema

0
0
Breaking News: Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu Amejiuzulu Nafasi Yake Ndani ya CCM na Kuomba Kuungana na Chadema
Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lazaro Nyalandu amejiuzulu nafasi yake ndani ya CCM na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia (CCM) kwa kile alichodai hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini.

Taarifa ambayo ameitoa leo Nyalandu amesema kuwa ameamua kuachana na CCM na sasa anaomba kuungana na CHADEMA kama watapendezwa na yeye kujiunga huko.
Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.
halikadhalika, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa" aliandika Nyalandu
"Nimechukua uamuzi huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA" alisisitiza
Mbali na hilo amesema kwa sasa anafikiria kujiunga na CHADEMA kama watakuwa tayari
"Mimi naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.
Hivyo, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.
"nimemua kujiuzulu kiti Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa MUNGU kuwa Haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane ki sera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na TAIFA lililo imara na nchi yenye ADILI"

Video: Hivi Ndivyo Lazaro Nyarandu Alivyotangaza Kujiuzuru CCM na Kutangaza Nia ya Kuingia CHADEMA

0
0
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amejivua uanachama wa CCM na nyadhifa zake zote leo huku akitoa sababu za kukikacha chama hicho kuwa  haridhishwi na mwenendo wa siasa nchini.

Kwa uamuzi huo, Nyalandu, ambaye aliomba ridhaa ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi uliopita, amejivua ubunge na nafasi nyingine zote alizokuwa akishikilia ndani ya CCM, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa Halmashauri Kuu.

Maneno ya Zitto Baada ya Nyarandu Kujiuzulu ' Umeonyesha Uongozi, Unahitaji Roho Ngumu Kuwa CCM '

0
0
Maneno ya Zitto Baada ya Nyarandu Kujiuzulu ' Umeonyesha Uongozi, Unahitaji Roho Ngumu Kuwa CCM '
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumpongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Nyalandu ambaye leo Oktoba 30, 2017 amefanya maamuzi ya kuachana na CCM na kusema kiongozi huyo amefanya maamuzi sahihi.

Zitto Kabwe amesema kuwa kutokana na uchumi unavyoporomoka haki za watu zinavyovunjwa jambo alilofanya Nyalandu ni sawa na kuwa huko ndiyo kuonyesha uongozi.
"Lazaro Nyalandu, umeonyesha Uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na Uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu Sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na Kwa sababu sahihi. Kila la kheri|" aliandika Zitto Kabwe
Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki mbalimbali.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images