Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

IEBC: Matokeo ya Urais Nchini Kenya Kutangazwa Leo

$
0
0
IEBC: Matokeo ya Urais Nchini Kenya Kutangazwa Leo
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya imekubali kutoa fomu za matokeo ya vituo vya kupigia kura maarufu kama Fomu 34A.
Muungano wa upinzani ulikuwa umelalamikia kukosekana kwa fomu hizo na kusema ilikuwa vigumu kukagua matokeo yaliyokuwa yakipeperushwa katika mtandao wa tume hiyo.
Mwenyekiti wa tume hiyo Bw Wafula Chebukati amewaambia wanahabari kwamba meza maalum itatengwa katika kituo kikuu cha kujumlishia matokeo ukumbi wa Bomas, Nairobi kwa ajili ya maajenti wa vyama ambao wangependa kukagua fomu hizo.

Mgombea urais wa National Super Alliance (Nasa) Raila Odinga usiku wa kuamkia Jumatano alikuwa amesema tume hiyo inafuata utaratibu usiofaa kwa kutangaza matokeo bila fomu hizo.
Bw Chebukati hata hivyo amesema matokeo yanayopakiwa kwenye tovuti hiyo si rasmi, na kwamba matokeo rasmi yatatangazwa baada ya kupokelewa kwa Fomu 34A kutoka vituoni.
Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Ezra Chiloba amesema tume hiyo ilikuwa imepokea fomu kutoka vituo 28,000 kufikia leo asubuhi.

Bw Chebukati amesema tume hiyo pia imepokea habari kuhusu tuhuma za muungano huo wa upinzani kwamba mitambo yake ya uchaguzi ilidukuliwa.
Amesema tume haiwezi kupuuza tuhuma kama hizo na kwamba maafisa wake watafanya uchunguzi kubaini iwapo kuna ukweli wowote katika madai hayo.
Hata hivyo alieleza imani yake kwamba mfumo wa uchaguzi unaotumiwa na tume hiyo ni imara na kwamba ulitumiwa na shughuli zote za awali, na sasa "imesalia shughuli ya mwisho" ya kupeperusha na kutangaza matokeo ya kura.

Tume hiyo ina hadi siku saba baada ya kumalizika kwa upigaji kura jana kutangaza matokeo lakini Bw Chebukati amesema matangazo rasmi yatatangazwa punde yatakapokuwa tayari.
Kufikia sasa, matokeo ya awali kutoka vituo 39046 kati ya 40883 yanaonesha Rais Uhuru Kenyatta akiwa kifua mbele na kura 7,906,062 (54.35%) naye Bw Odinga akiwa wa pili na kura 6513303 (44.77%)

Rais Magufuli Asema Yupo Tayari Kubadirisha Sheria Kuwalinda Wanaotakiwa Kupitiwa na Bomoabomoa

$
0
0
Rais Magufuli Asema Yupo Tayari Kubadirisha Sheria Kuwalinda Wanaotakiwa Kupitiwa na Bomoabomoa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema yuko tayari kubadilisha sheria ili kuweza kuwalinda wanachi wanaotakiwa kupitiwa na bomoa bomoa mkoani Mwanza, kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege na miundo mbinu mingine.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akihutubia taifa kwenye sherehe za uzinduzi wa daraja la Furahisha la mkoani Mwanza, na kusema kwamba serikali yake haiko tayari kuona watu wakionewa , hivyo yuko tayari kuwalinda hata kwa kubadilisha sheria itakayowaruhusu wananchi hao waendelee kuishi hapo.
"Tuliwatazama watu wakajenga wakaweka 'Investment' zao, sasa leo tunawafukuza, tusubiri kwanza, inawezekana walifanya makosa lakini kwa sababu serikali yangu ina huruma nasema ndugu zangu msiwabomoleshe, yapo maeneo ambayo kwa kweli itabidi watu wahame, mfano wale wa uwanja wa ndege, kama kuna mahali pa kubadilisha sheria mimi nitazibadilisha ili kusudi baadhi ya wananchi waliojenga pale miaka 30 tuweze kuwalinda na kukaa pale na kuendesha maisha yao", amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli leo yupo mkoani Mwanza kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo pia licha ya uzinduzi wa daraja la Furahisha, anatarajiwa pia kuzindua kiwanda kimoja.

Watu 60 Watengwa Kutokana na Homa ya Tumbili Nigeria

$
0
0
Watu 60 Watengwa Kutokana na Homa ya Tumbili Nigeria
Watu 60 wametengwa katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kano, baada ya kukaribiana na watu wanakosiwa kuugua homa ya tumbili au monkeypox.

Kamishia wa afya katika jimbo la Kano, Kabul Gesto, alisema kwau moja ya dalili za ugonjwa huo iligunduliwa kwenye mgongwa lakini akasema kuwa ugonjwa huo huenda ukawa homa ya ndege.
"Hadi pale matokeo ya sampuni za damu yaliyotumwa kwenda mji mkuu Abuja yatakaporudishwa, hiki kitakuwa kisa cha kushukiwa," alisema wakati wa mahajIano na BBC.

Dr Getso anasema kuwa wagonjwa 11 katika majimbo 36 nchini Nigeria wameathirika na homa ya tumbuli.

Mamlaka za afya nchini Nigeria zimekuwa zikionya dhdi ya ulaji wa tumbili na nyama ya msituni wiki chache zilizopita.

Waziri wa afya Isaac Adewole anasema katika taarifa ya hivi punde kuwa licha ya tiba ya ugonjw ahuo kutujulikana hakuma wasi wasi kwa sababu homa hiyo siyo hatari.
Hata hivyo amewashauri watu kuchukua tahadhari ikiwemo kujiepusha na maeneo yenye misongamano.

Hivi Ndivyo Kijana Nangale Alivyodakwa Akijipanga Kwenda Kufanya Mauaji

$
0
0
Hivi Ndivyo Nangale Alivyodakwa Akijipanga Kwenda Kufanya Mauaji
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela Meatu Simiyu amekamatwa akijipanga kuelekea Moru ndani ya hifadhi ya Serengeti akiwa na malengo ya kwenda kufanya mauaji kwa wanyama aina ya Faru.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amethibitisha kukamatwa kijana huyo na kusema kuwa wamemkuta akiwa na risasi 356, magazine 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha.
Kufuatia kufanikisha kumkamata kijana huyo kabla ya kutekeleza ujangili Waziri Kigwangalla amesema kuwa wataendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za kiintelinjesia kuthibiti ujangili na kudai kuwa watahakikisha wanakamata majangili kabla ya hawajafanya ujangili.
"Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini" alisisitiza Kigwangalla

Mzazi Mwenzie na Joti Ampa Makavu Steve Nyerere 'Wewe ni Mkubwaa Jielewe Ufupi Usikufanye Ukajiona Bado Mdogo'

$
0
0
Mzazi Mwenzie na Joti Ampa Makavu Steve Nyerere 'Wewe  ni Mkubwaa Jielewe Ufupi Usikufanye Ukajiona Bado Mdogo'
Mwanamama aliyezaa na msanii wa vichekeshomaarufu kama Merisa Bushoke amemtolea povu Steve Nyerere baada ya kumpongeza Joti kwa kufanikisha kufunga ndoa .
Kupitia ukrasa wake wa instagram steve Nyerere alianza kwa kuandika hivi

 "Hii ni familia mpya ndugu yangu Joti ' hakuangalia ule usemi mama wa kambo si mtu mzuri ameangalia mapenzi na utu wa anayemuoa kwa watoto wake na familia yake si wamama wakambo wote wana roho mbaya apana, bali mazingira ya hiyo roho inawekwa na wewe baba kama huna misimamo ya familia yako kwa mwanamke mwenyewe mwenye kukupenda wewe  atapenda na watoto wako na familia yako. Joti jana ulilia ukumbini nikajiuliza kwanini ulilia  nikapewa jibu mtoto wako amepata mtoto bora  huo nao ni ujasiri  sana kuhakikisha  mama huyo mnayeingia naye  mkataba wa kidini anakuwa mama bora, tumekuwa watu wa kukalili unayezaa naye ndio mama bora  kumbe si kweli  Joti umetengua kauli Joti wewe ni shujaaaa,,,,," aliandika steve Nyerere

Baada ya posti hiyo ya Steve nyerere mwanamama huyo naye akajibu kupitia ukrasa wake wa Instagram ameandika hivi na kumtagi Steve Nyerere

"Naitaji kusema hivi huyu mtoto wangu na mm ndo niliemzaa haata mama awe chizi, tahila, mjinga ndo mama ake na hatokuja  kutokea yoyote  ukafananisha upendo wake  na mama yake  kwa hiyo sitaki  maneno na mtu  yeyote kama unataka kupongeza  kitu kizuri kilichoanyika  tumia maneno yasiyomuhusu mwanangu  nadhani umenielewa  na maana yako nini kuongea ulichoongea sijapenda wewe  ni mkubwaa jielewe ufupi usikufanye  ukajiona bado mdogo @stevenyerere2 @stevenyerere2"

Chadema Yamjibu Lazaro Nyarandu Yakubali Ombi Lake la Kuamia Chama Hicho

$
0
0
Chadema Yamjibu Lazaro Nyarandu Yakubali Ombi Lake la Kuamia Chama Hicho
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimejibu ombi la aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye leo amejiuzulu wadhifa huo na kukihama chama cha CCM na kuomba kujiunga CHADEMA.

Akiongea na mwandishi wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, amesema CHADEMA inamkaribisha mtu yeyote anayetaka kujiunga na chama hicho, kwani chama cha siasa ni watu.

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire Anashikiliwa na Polisi

$
0
0

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire Anashikiliwa na Polisi
 Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire anashikiliwa na Polisi huku ikidaiwa kuwa amri ya kukamatwa kwake ni agizo la mkuu wa mkoa huo, John Mongella.
Hayo yamesemwa na Mariam Lima ambaye ni katibu wa mitandao ya taasisi ya Alliance inayomilikiwa na Meya Bwire ambaye ameeleza kuwa kuwekwa kwake sentro ni kunatokana na agizo la mkuu wa mkoa.
Hata hivyo, Mongella amekana kuamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo anayeshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Jiji la Mwanza.
“Nimepata taarifa za meya kuwekwa mahabusu; mimi sihusiki na ninazifuatilia kujua kinachoendelea,” amesema Mongella leo Jumatatu Oktoba 30,2017.
Taarifa zinasema meya Bwire amekamatwa katika Uwanja wa Ndege Mwanza wakati wa mapokezi ya Rais John Magufuli ambaye ziko ziarani mkoani humo.
Lima amesema, “Tunafanya jitihada za kumwekea dhamana ingawa tunakabiliana na changamoto nyingi.”
Tangu Aprili, Bwire na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba wamekuwa katika mgogoro kila upande ukiutuhumu mwingine kuhujumu shughuli za maendeleo.

Maneno ya Lowasa Baada ya Nyarandu Kujiudhuru 'Tumelamba Dume'

$
0
0
Maneno ya Lowasa Baada ya Nyarandu Kujiudhuru 'Tumelamba Dume'
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua nyadhifa zote alizokuwa nazo CCM.
Akionyesha kuwa na furaha alipozungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”.
Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango.
Dakika chache tangu Nyalandu aombe kujiunga na Chadema, Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani.
“Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne.
“Nyalandu ni hazina, ni mbunge imara na ni mwanasiasa wa mfano,” alisema Lowassa, ambaye alijiunga na Chadema mwaka 2015 na kuwania urais kupitia muungano wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa).
Lowassa alimsifu Nyalandu kwa kuisaidia jamii na akatoa mfano jinsi alivyosaidia watoto watatu wa Shule ya Lucky Vincent waliokwenda kutibiwa Marekani baada ya kupata ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.
“Nyalandu ana contacts (anafaham watu wengi) nyingi na jumuiya ya kimataifa, ni bidhaa nzuri kuwanayo,” alisema Lowassa, ambaye katika uchaguzi wa urais alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 6,072,848 (asilimia 39.97) ikiwa ni rekodi ya kura nyingi kwa upinzani tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe mwaka 1992.

Kutana na Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed Kutoka Bagamoyo...Ana Dawa za Kurudisha Mapenzi na Zingine Nyingi

$
0
0
MIUJIZA YA SHARIFU SEIF MOHAMED KUTOKA BAGAMOYO.

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,
(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

USHAURI: kama unahitaji msaada ni  bora kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate  msaada kwa haraka.

Chadema Yamjibu Hivi Lazaro Nyalandu Kuhusu Kujiunga Chadema

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimejibu ombi la aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye leo amejiuzulu wadhifa huo na kukihama chama cha CCM na kuomba kujiunga CHADEMA.

Akiongea na mwandishi wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, amesema CHADEMA inamkaribisha mtu yeyote anayetaka kujiunga na chama hicho, kwani chama cha siasa ni watu

Serikali yamjibu Zitto Kabwe, yasema anapotosha kuhusu takwimu za pato la Taifa

$
0
0
Ukuaji wa pato halisi la taifa katika robo ya pili ya mwaka 2017 ulikuwa ni asilimia 7.8

Asilimia 5.7 ni ukuaji wa pato la taifa katika robo ya kwanza mwaka 2017 na sio robo ya pili

Kanuni aliyotumia Zitto Kabwe haikuweka uzito kwenye kipengele muhimu cha kasi ya mzunguko wa fedha

Kabwe Zitto amepotosha kwa kutumia fahirisi ya bei ya walaji(CPI)kukokotoa badala ya kutumia fahirisi ya pato la taifa(GDP deflator)
 
VIDEO:

Nape Nnauye Aikana Taarifa ya Kuwa Leo Ataongea na Waandishi wa Habari

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kuweka sawa kuwa siku ya kesho Oktoba 31, 2017 hatakuwa na mkutano wowote na vyombo vya habari na kusema kuwa watu wanatunga hizo taarifa.

Nape Nnauye ametoa kauli hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii na kuwataka watu waache kumzushia mambo wakiwa na lengo la kutafuta nafasi na vyeo serikalini.
"Acheni kupiga ramli juu ya kesho yangu!! Kisa mnatafuta vyeo na hamuwezi kutumia akili kufikiri! Sina 'press conference' kesho" aliandika Nape Nnauye

Leo mchana watu wasio na nia nzuri na Nape Nnauye walizusha taarifa kuwa kiongozi huyo siku ya kesho Jumanne atakuwa na mkutano na waandishi wa habari jambo ambalo yeye mwenyewe amelipinga na kusema watu wanazusha taarifa hizo kwa maslahi yao wenyewe.

Ushahidi wa Picha Kuwa Irene Uwoya Kweli Kaolewa na Dogo Janja Huu Hapa

$
0
0
Picha ya kwanza ya kuthibitisha harusi ya DOGO JANJA na IRENE UWOYA!! Babu Tale ameipost kwenye page yake ya Instagram kumkaribisha Uwoya kwenye familia ya TIPTOP. Nadhani mpaka hapo mdau wangu utakuwa umeamini kuwa wameoana kweli

Diamond Ataja Fedha Anazolipa Kwenye Kolabo za Marekani

$
0
0
Diamond amefunguka kuhusu fedha anazowalipa wasanii wa Marekani kwa ajili ya kufanya kolabo.

Akiongea na Dizzim Online hit maker huyo wa Hallelujah amesema kuwa hakuna fedha yoyote ambayo amewahi kumlipa msanii yoyote wa nchi hiyo ambao tayari ameshafanya nao kolabo.

“Mimi sijawahi kulipa kolabo yoyote kwanza ya Marekani niliyowahi kufanya, sijawahi kulipa na ukichunguza kiundani kolabo zangu na Wamarekani siyo kitu ambacho ‘nimejishobokesha’ ni watu wenyewe ambao wanatokea kunikubali na kuupenda muziki ambao ninaufanya,” amesema Diamond.

Msanii huyo ameongeza, “Ndio maana unaona sometimes sipost naona kama sina haja ya kupost ikiwa wao wenyewe wanakuwa wanafurahi na wanapenda kupost kitu tunachokifanya. Sometimes naogopa kupost naonekana kama nitajishauwa, sitaki kuonekana hivyo, nataka nionekane pointi yangu kuuchukua muziki wa Tanzania kuupeleka mbali.”

Kauli ya Wema Sepetu Kuhusu Hali ya Tundu Lissu na Nyalandu Kuihama CCM

$
0
0
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa anajisikia furaha na amani kuona Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa anaendelea vyema kadili siku zinavyokwenda lakini pia amegusia sakata la Nyalandu kujitoa CCM.

Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa anakula chakula akiwa hospitali Nairobi na kusema anajisikia vizuri kuona shujaa wao anaendelea vizuri.

"Ni jambo jema kumuona shujaa wetu anaendelea vyema kweli Mungu ni mwema siku zote, lakini pia nikiwa mkubwa nitahitaji kuwa kama Lazaro Nyalandu" aliandika Wema Sepetu

Wema Sepetu ameweka ujumbe huu masaa kadhaa toka Lazaro Nyalandu alipotangaza kujivua uanachama wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuandika barua kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge wa Singida Kaskazini na kuomba kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Rais Magufuli Aeleza Sababu za Kutokugawa Milion 50 Alizoahidi Kwa Kila Kijiji

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ameeleza sababu zinazomfanya achelewe kutimiza ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji alizoziajidi wakati wa kampeni za kugombea urais kuwa ni kutokana na kuwepo kwa mambo mengi nchini yanayohitaji utekelezaji wa haraka.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika mkutano wa hadhara ikiwa ni moja ya vitu alivyopanga kuvifanya katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani hapo.

Ameeleza kuwa ameona ni sahihi kuanza na mambo ya muhimu zaidi kama vile miundombinu ya barabara, huduma za afya pamoja na elimu kabla ya kutoa fedha hizo ambazo aliziahidi katika iilani ya uchaguzi wa mwaka 2015.

“Halitokuwa jambo jema mimi kutoa milioni 50 kwa kila kijiji nchini wakati huduma mbalimbali kama vile elimu, afya na miundombinu ya barabara na usafirishaji haijakaa vizuri. lakini niwahakikishie kuwa hizo fedha zipo na zitakabidhiwa kwa kila kijiji kama nilivyosema,” alisema Rais Magufuli.

“Inabidi muwe watulivu wakati serikali ikishughulikia matatizo na changamoto zinazohitaji utatuzi wa haraka kabla hatujazitoa fedha hizo,” aliongeza Rais Magufuli.

Rais Magufuli alimtaka pia Mkuu wa mkoa wa mwanza kuhakikisha kuwa anachochea maendeleo ya viwanda na kupitia hivyo nchi itapata maendeleo.

“Viwanda vitatengeneza ajira nyingi kwa watanzania na vitaongeza mapato ya serikali. Mapato yakiongezeka serikali itaweza kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi,” Alisema Rais.

Mbunge Zitto Kabwe Akamatwa na Polisi Asubuhi ya Leo

$
0
0

Mbunge Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi leo asubuhi akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na amepelekwa Kituo cha Polisi Chang'ombe.

Kwa Nini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo?

$
0
0
 KWA NINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE  MADOGO?


Matatizo haya yame kuwa yakiwaathiri watu wengi sana kisaikolijia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wenzao kwa kawaida mwanaume ana takiwa awe na uume kuanzia inch(6_8)  vinginevyo mtu huyo atakuwa na matatizo.

Zipo sababu nyingi zinazo sababisha tatizo hilo  baadhi ni upungufu wa  vichocheo (Hormones za Getrogen) Ambazo  mwanaume akisha balehe vichocheo hivi huchochea  ukuaji wa  uume, chango husababisha NEVA ambayo huathiri misuri ya uume.

Ngiri ambayo Huleta maumivu ya tumbo kuunguruma  na kujaa guess, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri , miguu kufa ganzi, maumivu ya kiuno,upigaji wa punyeto sababu hizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembaba na mara kwa mara hipelekea kupunguka kwa nguvu za kiume na ham ya tendo la ndoa hukosekana na kuisha kabisa

NSUMBU:__Ni dawa dawa inayo zalisha hormones za Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.

NZAGI :--Ni dawa bora ya kurudisha  nguvu za kiume na kukupa hamu ya kurudia tendo la ndoa mara dufu utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4)bila hamu kuisha (kuchoka) dawa hii ni tiba kamili kwa matatizo hayo. Dawa hii pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk(15_30)kwa tendo moja la ndoa dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji kuanzia miaka(18_90)wana ruhusiwa kuzitumia

Pia tunatibu KISUKARI, PRESHA, PUMU, MALARIA SUGU, MIMBA KUHARIBIKA(Chango)

POWER :__Ni dawa ya mitishamba inaongeza hips, (makalio), miguu, ina punguza maziwa (chuchu). Ina toa harufu mbaya sehem  za siri Nk. Pia anazo dawa za  mvuto wa mapenzi,biashara, kurudishwa kazini, kumuita aliye mbali kwa mda mfupi tu OSTADH JUMA ANAPATIKANA MALARIA ZAKHIEM SIMU:_0769-597778 au 0784-002216 au 0627457957 Wote mnakaribishwa

Wabunge Acheni Kuwashwa Washwa na Kufanya Mambo ya Umbea- Ndugai

$
0
0
Wabunge Acheni Kuwashwa Washwa na Kufanya Mambo ya Umbea- Ndugai
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kwamba hana taarifa za kujiuzulu kwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu , na wala hiyo barua bado haijamfikia, na kuita kitendo alichokifanya ni umbea.

Job Ndugai ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, na kusema kwamba Lazaro hakupaswa kutangaza hivyo kabla ya kuhakikisha barua imemfikia.
Pamoja na hayo Spika Ndugai amewataka wabunge wengine kuacha kuwashwa washwa na kufanya mambo ambayo ameyaita ni ya umbea.

Hivi Ndivyo Halima Mdee Alivyomtahadharisha Nyarandu 'Naamini Utakuwa Imara Kukabiliana na Changamoto Tunazokumbana Nazo'

$
0
0
Hivi Ndivyo Halima Mdee Alivyomtahadharisha Nyarandu 'Naamini Utakuwa Imara Kukabiliana na Changamoto Tunazokumbana Nazo'
Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam Halima Mdee amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini ndani ya chama chao huku akimtahadharisha  kuhusu changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa chama hicho.

 Halima Mdee ametumia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kumkaribisha Nyalandu ambaye leo ametangaza kujiuzulu nafasi zake za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na nafasi yake ya ubunge aliokuwa nao.
"Mhe. Nyalandu karibu sana CHADEMA. Naamini utakuwa imara kukabiliana na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabili taifa letu".
Mapema leo Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM litangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.

Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images