Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live

Mwana FA Afunguka Kolabo ya Diamond na Morgan Heritage

0
0
Mwana FA Afunguka Kolabo ya Diamond na Morgan Heritage
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Mwana FA amesema kolabo ya Diamond na kundi la Morgan Heritage ni kitu kilichomvutia kwani amekuwa shabiki wa kundi hilo kwa zaidi ya miaka 10 sasa.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Upo Hapo?’, amekiambia kipindi cha Uhondo cha E Fm kuwa kusikia kolabo hiyo kumeongeza mapenzi yake ya kimuziki kwa kundi hilo.

“Morgan Heritage ni miongoni mwa watu niliwasikiliza sana kwa miaka mingi, kama 2005/2006, nawasikiliza mpaka leo kama miaka 10, nawajua mpaka kwa majina ile familia” amesema Mwana FA.

“Kwa hiyo niliposikia wamefanya na Mbongo ilinivutia na niliposikiliza ngoma ni nzuri, ipo tofauti kabisa hata Diamond siyo yule ambaye tumemzoea, kwa hiyo ngoma kali. Mimi love yangu kwa Morgan Heritage naona wameichukua moja kwa moja kwenye huu wimbo” ameongeza.

Morgan Heritage ni kundi linalofanya muziki wa reggae kutoka nchini Jamaica na Diamond ameweza kuwashirikisha katika ngoma yake inayokwenda kwa jina la Hallelujah.

Nape Aeleza Watu Wanaomkwaza na Kumuudhi Kwenye Mitandao ya Kijamii

0
0
Nape Aeleza Watu Wanaomkwaza na Kumuudhi Kwenye Mitandao ya Kijamii
Mbunge wa Mtama, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kusema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakimkazwa na kumuudhi kwenye mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wakitafsiri vibaya vitu vitu anavyoweka wakidai anamsema Rais.

Nape Nnauye alisema hayo wiki iliyopita alipoongea na mwandishi wa EATV na kusema baadhi ya watu wamekuwa wakichukua baadhi ya vitu anavyoweka kwenye mitandao yake ya jamii na kuanza kusambaza wakimtuhumu kuwa anamsema Rais kitu ambacho anadai si kweli.
Mbunge huyo wa Mtama amesema kitendo hicho cha watu kuchukua maneno yake na kuanza kusema anamzungumzia Rais ni kitu ambacho kimekuwa kikimuumiza sana siku hizi.
"Maana watu kila nifanyalo wanaona kama namsema Rais hili linaudhi na kuniumiza sana siku hizi" alisisitiza Nape Nnauy

Video: Ngoma Mpya ya Izzo B 'Mkemia Mkuu' Akimshirikisha Quick Rock

Ray Aonyesha Jeuri ya Pesa Amwaga Zawadi kwa Ajibu

0
0
Ray Aonyesha Jeuri ya Pesa Amwaga Zawadi kwa Ajibu
Msanii nguli wa filamu nchini Vicent Kigosi maarufu kama ‘Ray’, amewaongoza mashabiki wa Yanga SC kutoka kundi la ‘Yanga For Life’ kwenye mtandao wa WhatsApp kutoa zawadi kwa wachezaji wa timu hiyo.

Ray na wenzake wametoa zawadi ya fedha, viatu na ‘Shin Gard’, mchana wa leo kwa wachezaji watatu, waliofanya vizuri katika michezo ya Ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu.
Miongoni mwa wachezaji waliopata zawadi hizo ni mshambuliaji Ibrahim Ajib ambaye amepewa kiasi cha Tsh Milioni moja, baada ya kuibuka nyota wa mchezo kwenye mechi mbili za Kagera Sugar na Stand United.
Kiungo kutoka DRC Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye aliibuka nyota wa mchezo wa watani wa Jadi jumamosi iliyopita amepewa zawadi ya shilingi laki tano huku kipa Youthe Rostand, akipata shilingi laki mbili, viatu na ‘Shin Gard’.  Baada ya kukabidhi zawadi hizo Ray amesema nia ya kundi lao ni kuwapa hamasa wachezaji wao ili waweze kutetea ubingwa wao wa ligi na kutwaa mara ya nne mfululizo.

Tanzia:Hussein Juma a.k.a Dj Juice Amefariki Dunia Usiku wa Kuamkia Leo

0
0
Tanzia:Hussein Juma a.k.a Dj Juice Amefariki Dunia Usiku wa Kuamkia Leo
Dj wa muda marefu na mkongwe katika tasnia ya muziki na Burudani Tanzania, Hussein Juma a.k.a Dj Juice amefariki Dunia usiku wa kuamkia tarehe 31 katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa rafiki yake wa karibu ambaye wameshiriki mara kadhaa katika kazi za pamoja, Dj Mackay alitoa taarifa za msiba huo kwa kutoa salamu za pole kwa familia ya ndugu jamaa na marafiki na kuongeza kuwa shughuli za mziko ya Dj Juice zitafanyika jioni ya siku ya jumanne(leo) mida ya saa 10 jioni katika Makaburi ya Ndungumbi, Magomeni Makuti jijini Dar es Salaam.

Simba Yakimbilia TFF Baada ya Kutolizishwa na Waamuzi Katika Mchezo na Watani Wao wa Jadi

0
0
Simba Yakimbilia TFF  Baada ya Kutolizishwa na Waamuzi Katika Mchezo na Watani Wao wa Jadi

Klabu ya soka ya Simba imeandika barua ya kueleza malalamiko yake ya kutoridhishwa na maamuzi ya waamuzi katika michezo yake ya Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2017/18.

Hilo limebainishwa na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara wakati akiongea na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya klabu ambapo amesema nakala za barua hiyo wamezipeleka TFF, Bodi ya ligi TPLB pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
“Tumeliandikia barua shirikisho tukieleza dhuruma tunayofanyiwa na waamuzi pia nakala nyingine tumetuma kwa waziri mwenye dhamana ya michezo kwasababu haturidhishwi na maamuzi kwenye mechi zetu”, amesema Manara.
Manara ameeleza matukio mbalimbali ambayo klabu yake inalalamika kuhujumiwa ikiwemo Penalti mbili walizonyimwa dhidi ya Mbao FC ambapo mshambuliaji John Bocco alichezewa rafu lakini mwamuzi hakuchukua hatua sitahiki.

Matukio mengine ambayo Manara ameonesha kuchukizwa nayo ni kunyimwa Penalti kwenye mchezo dhidi ya Yanga Jumamosi iliyopita ambapo mlinzi Kelvin Yondani aliudaka mpira wa adhabu ndogo lakini mwamuzi Elly Saasi hakutoa adhabu ya Penalti.
Kwa upande mwingine Manara amesema klabu ya Simba inaendelea na maandalizi ya mchezo wake wa ligi dhidi ya Mbeya City chini ya kocha mkuu Joseph Omog na msaidizi wake Juma Masoud. Mchezo huo utapigwa siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Wale Majizi Makubwa Waliokuwa CCM Wanakimbilia CHADEMA- Magufuli

0
0
Wale Majizi Makubwa Waliokuwa CCM  Wanakimbilia CHADEMA- Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

"Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele" alisisitiza Rais Magufuli

Je Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa..Jibu Lipo Hapa

0
0
JE,UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZAKIUME,KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA,KUFIKA KILELENI MAPEMA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA UA MAUMBILE MADOGO YA UUME?


Tatizo la kukosa au kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya kiume husababishwa namambo mengi kama,KISUKARI,NGIRI,CHANGO,TUMBO KUUNGURLUMA,MAUMIVU YA KIUNO,UNENE KUPITA KIASI,KUJICHUA(MASTER BLASHION)HOMON Hishindwa kufanya kazi inavyotakiwa nk.upungufu wa nguvu za kiume husababisha tendo la ndoa kutofanyika kwa kujiami nakwa usahihi nahivyo husababisha ndoa mahusiano mengi kuvunjika.BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI,1KUKOSA HAMU YA TENDOL LA NDOA 2 UUME KISIMAMA KWA KULEGEA 3 KUWAHI KUFIKA KILELENI 4 KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA WAKATI 5 KUCHOKA SANA BAADA YA ROUND YAKWANZA NAKUKINAI TENDO NDOA KABISA.TUMIA 3 POWER KWA TATIZO LA UKOSEFU(UPUNGUFU)WA NGUVU ZA KIUME NAHAMU YA TENDO LA NDOA.FINA HUBORESHA MAUMBILE YA KIUME KWA KUNENEPESHA KWA SAIZI UIPENDAYO HAIJARISHI UMRI.PIA KUNA DAWA ZA KURUDISHA MPENZI KWA MUDA MFUPI SANA NAZAKUPATA KAZI,KESI,KUDHULUMIWA,NK WASILIANA NA SHEIKH OMARY AKUTATULIE MATATIZO YAKO HATA KAMA UMEHANGAIKA SANA PASIPO MAFANIKIO UMEFANIKIWA LEO

Pia sheikh omary anatibu busha bila opresheni,kisukari,ngiri,presha,vidonda vya tumbo,korodani kivimba nakuuma,na anatoa ndagu za utajiri kwa wanaohitaji utajiri bila masharti yoyote magumu.ANAPATIKANA DAR ES SALAAM NAUTALETEWA POPOTE ULIPO TIBA HII UKIWA HAUNA NANAFASI YAKUFIKA OFISINI,

PIGA SIMU NO 0767 14 53 57/0629 03 45 5

Video: Nisingekamatwa Ningeshangaa – Mh. Zitto Kabwe

0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT – Wazalendo baada ya kukamatwa na polisi na kuachiwa kwa dhamana amesema kuwa Rais alisema kuwa akamatwe na asingekamatwa angeshangaa: Tazama video hii Zitto Mh. akieleza

VIDEO:

Tundu Lissu Afunguka Kuhusu Lazaro Nyalandu

0
0
Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki(CCM), Lazaro Nyalandu kwa kupata ujasiri wa kuchukua hatua kubwa ambayo hata wabunge wengi waliopo ndani ya CCM wanashindwa kuichukua.

Lissu ambaye yuko kwenye matibabu jijini Nairobi  amempongeza Nyalandu kwa kuwa ni alikuwa mbunge jirani yake na kuwa ujasiri wa kufanya hivyo.

Mbali na kumpongeza Nyalandu pia Lissu amezungumzia  uchaguzi wa madiwani katika kata 43 akieleza kuwa kuwapa CCM kura katika kata hizo ni sawa na kukubaliana na yanayoendelea nchini.

“Kuwapa CCM kura sasa hivi ni sawa na kuwapa CCM mamlaka ya kutapanya mali zetu kama wanavyotaka,”amesema Lissu leo Jumanne akiwa jijini Nairobi.

RC Makonda Amjibu Mhe Nyalandu ‘Dira ya Mafisadi Ndio imepotea’ (Video)

0
0
Baada ya siku ya jana aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samwel Nyalandu kutangaza kukihama Chama Cha CCM kwa madai kimepoteza mwelekeo na kushindwa kuikosoa serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemjibu mwanasiasa huyo kwa kueleza baadhi ya mambo ambayo yamefanywa na serikali hiyo inayoongozwa na chama cha CCM. VIDEO:

Pesa za Fiesta Zamfanya Dogo Aslay Kununua Gari.....

0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Aslay Isihaka ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Natamba' amefunguka na kushukuru uongozi wake mpya kwa kufanikisha yeye kuweza kupata ndinga mpya aina ya BMW.

Aslay ambaye ndani ya muda mfupi ameweza kuachia nyimbo zaidi ya 10 na ngoma hizo nyingi kufanya vizuri na kupokelewa vyema na wananchi jambo ambalo limeweza kufungua milango kwa msanii huyo kuweza kupata show nyingi na mafanikio mbalimbali.

"Alhamdulillah Asantee Mungu kwa hiki ulichonipa naishukuru management yangu Chambusso na Mxcarter, nakupenda Mama yangu kokote ulipo kila hatua dua 'new car' Umma unaongea" alindika Aslay kupitia mtandao wake wa Facebook.

Aslay Isihaka kwa mara ya kwanza kuanza kumiliki gari yake alizawadiwa na uongozi wake wa kwanza wa Yamoto Band chini ya Mkubwa Fella katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake mwaka 2015.

Mchezaji Mavugo Akalia Kuti Kavu Simba...Viongozi Hawana Imani nae

0
0
Viongozi wa Simba wameonyesha kutofurahishwa na uchezaji wa mshambuliaji wao Laudit Mavugo hasa kutokana na kushindwa kuonyesha juhudi uwanjani.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, viongozi wa Simba wamemtaka Mavugo kujituma na kama inashindikana basi wataachana nao.

"Viongozi hawajafurahishwa na Mavugo kwa kuwa hajaonyesha juhudi zozote katika mechi dhidi ya Simba.

"Unajua hata katika upangaji, awali kocha alionekana kama nafasi ya kuanza angempa Bocco. Lakini alibadili ikawa ni Mavugo," kilieleza chanzo.

"Viongozi wao hawana uwezo wa kumuingilia kocha lakini wanakerwa na namna Mavugo asivyoonyesha kama ana uchungu. Hivyo walitaka kama ameshindwa aende zake.

"Tayari kaelezwa kuwa lazima ajitume na acheze kuitumikia timu na kuisaidia kwa kuwa kama ilivyo kwa wengine anapata kila kinachotakiwa."

Install Application ya MCHAMBUZI Kwenye Simu yako Kusoma Habari na Matamko ya Wanasiasa Kila Siku

0
0
Maswala ya Siasa na Matamko ya kila siku ya Wanasiasa Hakikisha Umedownload App ya Mchambuzi Kwenye simu yako
Bonyeza HAPA

Kama we ni Mpenzi wa Habari za Siasa Usipitwe na Hii Application ya Mchambuzi..... 
Bonyeza HAPA Kudownload kwenye Simu yako

Kutana na Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed Kutoka Bagamoyo...Ana Dawa za Kurudisha Mapenzi na Zingine Nyingi

0
0

MIUJIZA YA SHARIFU SEIF MOHAMED KUTOKA BAGAMOYO.

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,
(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

USHAURI: kama unahitaji msaada ni  bora kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate  msaada kwa haraka.

Nay wa Mitego: Tunakibarua Kikubwa cha Kurudisha Muziki Wetu wa Bongo Fleva Kwenye Mstari

0
0
Nay wa Mitego: Tunakibarua Kikubwa cha Kurudisha Muziki Wetu wa Bongo Fleva Kwenye Mstari
Msanii Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa ndani ya miaka miwili au mitatu inayokuja anaona wazi muziki wa bongo fleva unakwenda kufa kama ambavyo tasnia ya filamu bongo ilivyokufa kwa kile anachodai wasanii wamekuwa wazembe na kutegemea kiki.

Nay wa Mitego amesema kuwa wasanii wengi wa bongo saizi wanategemea zaidi kiki kuliko kufanya muziki mzuri jambo ambalo anaona litafanya muziki wa bongo kufa muda si mrefu kama wasanii hao hawatachukua jukumu la kurudisha muziki kwenye mstari.

"Kusema kweli kuna kitu nakiona kwenye muziki wetu wa bongo fleva tunakibarua kikubwa cha kurudisha muziki kwenye mstari sababu saizi watu wanatengeneza kiki kubwa ila muziki mdogo, yaani kiki zimekuwa mbele muziki unasindikiza kiki miaka miwili mitatu ijayo naiona bongo fleva ikiwa imepotea kama bongo movie ambavyo imepotea kama tusipokuwa makini kuamua kufanya kazi kweli na kiki ziwe tu kusindikiza muziki, saizi watu wanatengeneza kiki hata hazielezeki wasanii tunajisahau tuamke, turudishe muziki wetu kwa sababu tunawalemaza hata mashabiki" alisema Nay wa Mitego

Hii Hapa Sababu ya Joshua Nassari, Kukata Rufaa

0
0
Hii Hapa Sababu ya Joshua Nassari, Kukata Rufaa
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari, amekata rufaa kupinga hatua ya kuenguliwa wagombea wake wawili waliopitishwa kugombea udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa marudio unaofanyika katika kata tano katika Jimbo la Arumeru Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari, Nassari amesema kuwa amesikitishwa na uamuzi uliofanywa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo kwani hawakuzingatia kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi.
Nasari amesema amekata rufaa Tume ya Uchaguzi kupitia Mkurugenzi wa Taifa wa Uchaguzi kufikisha malalamiko yao kwani kutenguliwa kwa wagombea wao kutokana na kutofuatwa taratibu ikiwemo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kuwatengua wagombea wakati hana sifa ya kufanya hivyo
"Mapingamizi yaliyowekwa hayakuwa na mashiko Wagombea wetu wameenguliwa kinyume cha sheria. Na suala hili la kuenguliwa limekuja baada ya majaribio ya utekaji, fedha kutumia washawishi wakiwa viongozi wa mila, vitisho vya uhai wao kushindikana," Nassari.
Hata hivyo Nassari amesema alilazimika kuwahifadhi wagombea hao nyumbani kwake ili kuwaepusha na madhila pamoja na mitego waliyokuwa wamewekewa.


Mamlaka ya Hali ya Hewa Yatoa Taadhali ya Kuwepo kwa Mvua Kubwa

0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Yatoa Taadhali ya Kuwepo kwa Mvua Kubwa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yatahadharisha kuwapo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es saalam, Pwani, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba

Keisha Atoa Maneno Haya Kuhusu Ndoa ya Irene Uwoya, Dogo Janja Ambayo Yamewachanganya Watu

0
0
Keisha Atoa Maneno Haya Kuhusu Ndoa ya Irene Uwoya, Dogo Janja Ambayo Yamewachanganya Watu
Gumzo jingine kuanzia weekend iliyopita ni taarifa za ndoa ya Msanii Dogo Janja ikidaiwa kwamba kamuoa Mwigizaji Irene Uwoya ambapo tayari wawili hao waliandika kwenye mitandao yao ya kijamii kuonyesha kwamba ni kweli wameoana.

Pamoja na hayo leo Msanii wa Bongofleva Keisha ambae alionekana kwenye picha ya pamoja siku ya tukio ameandika maneno ambayo yameonekana kuwachanganya watu baada ya kuonyesha kwamba ile ilikua ni video na itaachiwa hivi karibuni hivyo akawashukuru kina Dogo Janja kwa kuhudhuria.

Mshambuliaji Awaua Watu 8 kwa Kuwagonga kwa Gari New York

0
0
Mshambuliaji Awaua Watu 8 kwa Kuwagonga kwa Gari New York
Meya wa mji wa New York, Bill De Blasio, amearifu kwamba watu 8 wamefariki dunia na zaidi ya 12 wamejeruhiwa na gari iliyowagonga waendesha baiskeli mjini humo.
Bill amelielezea tukio hilo kuwa la ugaidi lililosababisha hofu mjini humo.
Kamishna wa polisi wa jiji wa New York, James O'Neill, amemuelezea mtu aliyewtekeleza tukio hilo kuwa ni kijana wa miaka 29 aliyekuwa anaendesha gari ndogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi.

Alisema gari hilo liliwagonga watembea kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na basi la shule.
Kwa upande wake bwana O'Neill, amesema kuwa dereva wa gari hilo alitoka ndani ya gari lake na kuanza kuandaa silaha mbili kwa ajili ya shambulizi na kabla ya hilo, polisi walimuwahi na kumpiga risasi zilizomjeruhii.
Marekani
Polisi mjini humo wametoa tamko kwamba wanalichukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi , Mtuhumiwa wa tukio hilo alichukuliwa na polisi kwa mahojiano zaidi ambao walithibitisha taarifa hizo katika kituo cha Lower Manhattan.

Vyombo vya habari nchini Marekani vimenukuu taarifa za polisi kuwa kijana huyo aliamua kuendesha gari hilo katika njia ya waendesha baisikeli iliyoko karibu na Mto Hudson eneo la Lower di za Swahili

Maboti yanayojulikana kama dhow huonekana katika pwani ya bahari ya Tanzania
Raia 2 wa Tanzania na 10 wa Iran wakamatwa kwa dawa za kulevya

Viewing all 104423 articles
Browse latest View live




Latest Images